Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live

PROF.ELISANTE AWATAKA WAMILIKI WA RADIO KUFUATA SHERIA NA KANUNI ZA UENDESHAJI NA KUANDAA VIPINDI VINAVYOELIMISHA JAMII

0
0
Na Lorietha Laurence-Maelezo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amewataka wamiliki  wa radio kuhakikisha kuwa wanafuata  sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji pamoja  na kuandaa vipindi vyenye maudhui yanayoelimisha na kujenga jamii. 


Aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari  katika  maadhimisho ya siku ya radio yaliyoratibiwa  na shirika la UNESCO katika kutambua umuhimu  wa radio za jamii.


“Ikiwa wamiliki wa redio watazingatia  kutoa maudhui sahihi kwa jamii basi jamii husika itakuwa imejengwa katika msingi ulioimara na dhabiti  kwa ajili ya kuleta maendeleo na maelewano,” alisema Prof. Gabriel


Prof.Gabriel aliongeza kuwa Serikali ipo tayari kushirikiana na wadau katika kuhakikisha kuwa sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji zinazotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) zinafuatwa ili kuepuka msuguano baina ya wamiliki wa radio na serikali.


Vilevile alibainisha kuwa radio ni chombo muhimu sana kwa kuwa kinawafikia watu wengi kutokana na kukua kwa teknolojia ambapo watu wanaweza kusikiliza radio popote wanapokuwa kwa kutumia simu zao za mkononi, tofauti na vyombo vingine vya habari.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Bi. Eda Sanga  anaeleza kuwa kwa sasa vipindi vingi vya radio  vina maudhui hafifu tofauti na zamani.


“Maudhui ni kitu muhimu sana kwa kuwa kupitia maudhui watu wanapata taarifa na kuelimika lakini zama hizi vipindi vingi vina maudhui ya muziki zaidi kuliko kuelimisha umma” alisema Bi. Sanga.Bi.Sanga amewataka  waandaji wa vipindi kujikita zaidi katika kuandaa vipindi vyenye maudhui muhimu kwa kufanya utafiti wa kina na kuangalia matokeo ya vipindi kwa jamii husika.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar  es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa habari  katika kuadhimisha  siku ya radio duniani iliyoratibiwa na shirika la UNESCO  leo jijini Dar  es Salaam .(Picha na Lorietha Laurence-Maelezo)

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Masauni Atembelea Makao Makuu ya Polisi Zanzibar Kujitambulisha

0
0
KAMISHNA wa Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Masauni alipofanya ziara katika Jeshi hilo Zanzibar kujionea Utendaji wake akiwa katika ziara ya kujitambulisha.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Hamad Yussuf Masauni akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake Zanzibar kujitambulisha kwa Maofisa wa Jeshi la Polisi Zanzibar.kushoto Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame, mkutano huo umefanyika Makao Makuu ya Polisi Kilimani Zanzibar.kabla ya kuaza ziara yake kujionea utendaji wa Jeshi hilo Zanzibar.
Makamanda wa Jeshi la Polisi Zanzibar wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani alipofika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar kwa kujitambulisha. 

Makamanda wa Jeshi la Polisi Zanzibar wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani alipofika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar kwa kujitambulisha. 

Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame akijibu maswali aliyoulizwa na waandishi wa habari wakati wa mkutano wao na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Mhe Hamad Yussuf Masauni. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Hamad Yussuf Masauni, akiwa na Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame, wakitoka katika jengo la Makao Makuu ya Polisi Ziwani kwa kuaza ziara yake baada ya mazungumzo na Maofisa hao.
Imetayarishwa na OthmanMapara.

TAMKO LA TASWA KUHUSU KUPIGWA KWA MWANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO NA MCHEZAJI WA SIMBA

0
0

Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA), kimestushwa na kitendo cha mchezaji wa Simba kudaiwa kumpiga mwandishi  kwa masikitiko makubwa kitendo cha wa  habari za michezo la gazeti la Mwananchi, Mwanahiba Richard.


Tumeongea na Mwandishi mwenyewe kujua ukweli, tumemtafuta kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Mika Nyange naye kutaka kufahamu hali ya upelelezi ilipofikia lakini kufanyika haraka kwa uchunguzi ili  haki ya kila mtu ipatikane.


Lakini tumeweza kuzungumza na upande wa pili, kwa viongozi wa Simba kujua kama nao wao wamebaini kosa la mchezaji huyo.Mwenyekiti wa Simba,Evans Aveva ameahidi kutoa ushirikiano na kuomba tusubiri uchunguzi wa Polisi ndipo upatikane ukweli wa jambo ili.


Sisi kama TASWA tunalaani tukio ili na tumekuwa tukikemea sana vitendo hivi kwa kupiga waandishi, lakini kumekuwa hakuna jitihada zozotew ambazo polisi inalichukua kwa wahusika na badala yake madai kama haya yanapotea.


Kwa kuwa jeshi la polisi limeahidi kutoa ufafanuzi wa upelelezi wa tukio ili haraka iwezekanavyo, naomba waandishi wenzangu pamoja na muathirika wa tukio ili, tuvute subira ili haki ichukue mkondo wake ili sheria ifanye kazi yake.


Taswa itaendelea kulinda heshma ya mwandishi wa habari za michezo na isingepeda kuona mwandishi anaonewa na kudhalilishwa wakati akifanya majukumu yake.Kwa upande wetu napenda kutoa shukrani kwa nahodha wa Simba, Mussa Hassan Mgosi na kocha wa timu hiyo Jackson Mayanja kwa ushirikiano walioonesha katika tukio hilo na wamedhihilisha uwezo wa kuwaongoza wenzao.

TASWA itakuwa inafuatilia suala ili kwa karibu zaidi.Tupo katika kuhakikisha waandishi anafuata taratibu, sheria za taaluma ya habari.Jambo ambalo Mwanahiba amelifanya kwa kumlinda source wake hadi kupata kipigo .

Juma Pinto

Mwenyekiti TASWA

12.02.2016



WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI ATEMBELEA WILAYA ZA WANGING’OMBE NA MAKAMBAKO

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Assumpter Mshama akizungumza mbele ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Wanging’ombe (WINGISA), Philemon Luhanjo.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akiwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Mwenyekiti wa Bodi ya WINGISA, Philemon Luhanjo, Meneja WINGISA, Inj. Najib Asumbwile (mwisho kulia) na Mkurugenzi Msaidizi wa Maji Vijijini, Inj. Jackson Mutazamba (mwisho kushoto) pamoja na wafanyakazi wa WINGISA.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akitembelea chanzo cha maji cha Fukulwa, Wilaya ya Makambako.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akiwa na Mbunge wa Jimbo la Makambako, Deo Sanga na Mkuu wa Wilaya ya Makambako, Sarah Dumba wakiwa kwenye eneo la ujenzi la Bwawa la Tagamenda, Wilaya ya Makambako.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akizungumza na wananchi wa Manga, Wilaya ya Makambako.
………………………
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge leo ametembelea Wilaya za Wanging’ombe na Makambako mkoani Njombe na kujionea hali ya utekelezaji wa miradi ya maji kulingana na ahadi ya Mhe. Rais, John Magufuli katika kampeni zake za urais.Aidha, ziara yake hiyo imelenga kuhakikisha kuwa miradi inayosuasua inatekelezwa na kuisha kwa wakati ili kutatua kero ya maji kwa wananchi kulingana na Sera ya Maji ya Mwaka 2002, kutimiza lengo la ifikapo mwaka 2025 wananchi wote mijini na vijijini wawe wanapata maji kwa asilimia mia.


Vilevile, Inj. Lwenge alifika kwenye Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Wanging’ombe (WINGISA) kujionea utendaji wa mamlaka hiyo na kuzungumza na wafanyakazi wake kwa nia ya kuboresha utendaji wake.

WAZIRI MWAKYEMBE ATEMBELEWA NA BALOZI JAAP WA UHOLANZI.

0
0
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe (kushoto) akiongea na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Bw. Jaap Frederiks alipomtembelea ofisini kwake leo 12/2/2016 jijini Dar Es Salaam kwa mazungumzo.

Waziri Mwakyembe alimwelezea balozi huyo shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara na balozi Jaap aliahidi kushirikiana na Tanzania kwenye masuala ya kisheria ya kimataifa.

Katibu Mkuu TUCTA asifia Sheria za Kazi

0
0


Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Nicholas Mgaya akiongea na Wajumbe wa Kikao cha Tathmini ya Utendaji kazi wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi wakati wa Ufunguzi wa Kikao hicho leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Ulimwenguni kwa nchi za Tanzania, Kenya, Burundi, Rwanda na Uganda Bi. Mary Kawar akichangia mada wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Tathmini ya Utendaji Kazi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Masuala ya Walemavu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi akiongea na Wajumbe wa Kikao cha Tathmini ya Utendaji kazi wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi wakati wa Ufunguzi wa Kikao hicho leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Mhe. Shaaban Lila akichangia mada wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Tathmini ya Utendaji Kazi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa Kikao cha Tathmini ya Utendaji kazi wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi wakifuatilia uwasilishwaji wa mada toka kwa viongozi mbalimbali wakati wa Ufunguzi wa Kikao hicho kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI MHANDISI STELLA MANYANYA AFANYA ZIARA KATIKA MAMLAKA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI (VETA) MAKAO MAKUU, CHANG`OMBE JIJINI DAR ES SALAAM.

0
0
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na wafanyakazi wa VETA Makao Makuu (hawapo pichani) alipofanya ziara katika mamlaka hiyo Changombe jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA Geofrey Sabuni na kulia ni Wakurugenzi wa Wizara hiyo walioongozana na Naibu waziri.
Meneja Uhusiano wa VETA Sitta Peter akitoa maoni yake wakati wa mazungumzo kati ya Naibu Waziri na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo.
Wafanyakazi wa VETA Makao Makuu wakimsikiliza Naibu Waziri Mhandisi Stella Manyanya wakati wa ziara hiyo.

Mkurugenzi wa Mafunzo wa VETA Leah Lukindo akitoa wasilisho wakati Naibu waziri alipokutana na Menejimenti ya Mamlaka hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA Geofrey Sabuni akimkaribisha Naibu Waziri Mhandisi Stella Manyanya kuzungumza na wafanyakazi wa VETA Makao Makuu wakati Naibu waziri alipofanya ziara katika Mamlaka hiyo.

WAZIRI WA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO MHE. UMMY MWALIMU ATEMBELEWA NA MABALOZI WA SWITZERLAND NA KOREA OFISINI KWAKE.

0
0
 Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akizungumza na Balozi wa Korea Nchini Tanzania (Song, Geum-Young) wa kwanza kushoto akiwa na Katibu wake Songwon Shin wa pili kushoto. 
 Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na Barozi wa Switzerland Nchini Tanzania, Florence Tinguely Mattli wa kwanza kushoto akiwa na Mkuu wa Sekta ya Afya ya Ubalozi wa Switzerland, Thomas Teuscher wa pili kushoto.
Balozi wa Korea Nchini Tanzania, Song, Geum-Young akizungumza na Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, wa pili kushoto ni Katibu wake Songwon Shin.

ETHAD YAFUNGUA SEHEMU YA MAPUMZIKO KATIKA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA CHA ABU DHABI.

0
0
Mnamo Mei mwaka huu, shirika la ndege la la Etihad linategemea kufungua sehemu mpya ya mapumziko katika stesheni ya tatu ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi kwa ajili ya wageni wake wa “Daraja la Kwanza”, wasafiri wenye kadi maalum za Platinum za Etihad, wasafiri wenye kadi maalum za Platinum kutoka washirika wa Etihad na wale watakaotumia huduma ya “Makazi” iliyopo katika ndege zake aina ya Airbus A380. Etihad imewekeza sana katika kutimiza lengo hili kwa ajili ya wageni wake wa hadhi ya juu wanaopenda huduma zenye viwango bora zaidi.

Peter Baumgartner, Afisa Mkuu wa Biashara, alisema: “Huduma hii itakuwa kito katika taji letu hapa Abu Dhabi, ni nafasi nzuri kuonesha umahiri wetu kwenye ubunifu na uvumbuzi. Ni muhimu kwetu kuhakikisha msafiri anapata huduma bora kwanzia uwanjani hadi angani mpaka anaposhuka. Tuna imani huduma na bidhaa tutakazotoa nje ya ndege zitajizolea umaarufu kama za ndani ya ndege na tunategemea wateja watafurahia yote tunayowaandalia.”


Sehemu hii ya mapumziko itapambwa kwa mtindo wa Kiarabu na itaendana na umaridadi na umahiri uliozoeleka na kuhusishwa na jina la Etihad. Sehemu hii itaonesha uzoefu na ustadi wa Etihad na jinsi walivyojikita katika kuleta huduma yenye ukamilifu, kuanzia angani hadi ardhini.

MHE. KAIRUKI AITAKA TASAF KUONDOA KERO YA UMASIKINI KWA WANANCHI.

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga akiwatambulisha watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akisisitiza uwajibikaji kwa watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akiagana na viongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) mara baada ya kumaliza ziara ya kikazi aliyoifanya Makao Makuu ya TASAF mapema leo. 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) ameuagiza Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ili kusaidia jitihada za serikali za kuwaondolea wananchi kero ya umaskini.

Mhe. Kairuki amesema TASAF inayo dhima kubwa ya kuhakikisha kuwa huduma inazozitoa kwa wananchi zinakwenda sambamba na misingi ya uadilifu na utawala bora ili hadhi ya mfuko huo iendelee kuwa kubwa. 

Waziri Kairuki ameyasema hayo alipotembelea Makao Makuu ya TASAF jijini Dar es salaam ambako alizungumza na watumishi wa mfuko huo ikiwa ni mwendelezo wa ziara za kikazi katika taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora ambayo amepewa dhamana ya kuisimamia baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John P. Magufuli.

“Ninawasisitiza muhakikishe kuwa, walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wananufaika vilivyo na fedha zinazotolewa ili hatimaye waweze kuondokana na umaskini” alisema Kairuki.

Aidha, Mhe. Kairuki ameuagiza uongozi wa TASAF kuweka utaratibu utakaowezesha ukaguzi wa mara kwa mara wa walengwa wa Mpango huo nchini kote ili kuhakikisha kuwa watu wasiostahili wanaondolewa kwenye utaratibu wa ruzuku na kupunguza malalamiko yasiyokuwa ya lazima.

Mhe. Kairuki ameonya vikali dhidi ya uwezekano wa kuweko matumizi mabaya ya fedha kwa kutoa ruzuku kwa watu wenye uwezo jambo ambalo amesema halipaswi kufumbiwa macho na pale itakapobainika wahusika wachukuliwe hatua za kuwaondoa kwenye Mpango na kisha kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Katika hatua nyingine, Waziri Kairuki ameuagiza uongozi wa TASAF kutoa mapendekezo ndani ya siku 30 ya namna ya kukabiliana na malalamiko yanayoelekezwa kwa watendaji wa ngazi za vijiji,kata,na hata wilaya ambao wamekiuka taratibu za kuwabaini na kuwaorodhesha walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini ili hatua zichukuliwe haraka iwezekanavyo.

Awali akitoa maelezo kwa Waziri, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga amesema Mfuko umefanikiwa kuandikisha zaidi ya walengwa Milioni 1.1 ambao wanaendelea kupata ruzuku na kuwa hadi kufikia mwezi Januari 2016 zaidi ya shilingi Bilioni 204 zimetolewa kwa walengwa ambapo matokeo chanya yameanza kuonekana hususani katika Nyanja za elimu, afya na makazi.

Bwana Mwamanga amesema licha ya changamoto zilizopo hususani katika upatikanaye wa fedha za kukidhi idadi kubwa ya walengwa ,Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF )umeendelea kufanya juhudi za kutafuta fedha kutoka kwa wadau wa maendeleo na kuiomba serikali kuona namna inavyoweza kuunga jitihada hizo ili hatimaye vita dhidi ya umaskini iweze kufanikiwa .




Kuhusu Mpango wa kunusuru kaya maskini, Bw. Mwamanga amesema walengwa wa Mpango huu wamehamasika kwa kiwango kikubwa huku wengi wao wakionyesha uwezo katika kufuata masharti na taratibu za Mpango hivyo suala la upatikanaji wa fedha kwa uhakika lina umuhimu mkubwa ili kutowavunja moyo walengwa hao.

WATANZANIA WAMETAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA TAMASHA LA AMSHA MAMA TANZANIA.

0
0
WATANZANIA wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika Tamasha la ‘Amsha Mama Tanzania’ linalotarajiwa kufanyika Machi 5 katika uwanja wa Mwembeyanga Temeke jijini Dar es Salaam .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Kampuni ya Candy record yenye makao Mkuu yake nchini Kenya ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo Joe Kariuki amesema wameamua kuleta tamasha nchini ili kuwapa fursa akina mama wa Tanzania kujiinua kiuchumi .

“ Akina mama mjitokeze kwa wingi katika tamasha hili mahususi kwenu kwa kuwa mtapata fursa mbalimbali na mtaweza kupata mambo mbalimbali ikiwemo elimu” .Alisema Kariuki.

Kwa upande wake balozi wa Amsha Mama nchini Khalid Ramadhani (Tundaman), amewaomba wakinamama wachangamkie fursa kwani watajifunza mambo mengi 

“Nawaomba Mama zangu mjitokeze kwa wingi kwani tumepata bahati ya pekee ya kupendelewa kuletewa tamasha nchini kwani ni adimu kutokea,” .alisema Tundaman.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika pia katika uwanja wa Ranchi ya Kedong uliopo jiji la Naivasha nchini Kenya marchi 25-27 huku likitarajia kukutanisha akinamama kutoka nchi zote za Afrika .

Aidha kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii kama vile Juma Kassim ‘’Juma Nature’’, Khadija Kopa, Roma Mkatoliki, Young Killer, Msagasumu, Man fungo,Sharo mwamba,Q-Chief,Mr Blue,Snura,Tundaman,na Ally Choki.

Tamasha la Amsha Mama linatarajiwa kukutanisha akinamama mbalimbali kwa lengo la kujifunza kuhusu kujikwamua kiuchumi kwani wao ndio chachu ya mafanikio.


Alisema wamejipanga kuwapa radha tofauti watoto wa temeke na majirani zake ,hasa kwa akina mama kupata fursa ya kujielewa na kujitambua hasa katika kuendeleza familia zao.

WAZIRI ANNASTAZIA WAMBURA ATEMBELEA TFF.

0
0
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura akipokeza zawadi ya jezi ya timu ya Taifa ya Tanzania kutoka kwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji , Said Mohamed.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wamburaakizungumza na viongozi na wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake "Twiga stars" leo alipotembelea TFF.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura leo ametembela ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kupata kujionea shughuli mbalimbali zinazondeshwa na shirikiso hilo.

Akiongea na viongozi na wachezaji wa timu ya Taifa ya Wanawake “Twiga Stars” waliopo kambini kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake dhidi ya Zimbambwe, Wambura amesema Serikali itashirikiana na TFF kuhakikisha timu inapata ushindi katika mchezo huo wa awali utakaochezwa Machi 4, 2016.

Wambura amewataka wachezaji wa Twiga Stars kuwa na nidhamu ndani na nje ya uwanja, kujituma na kuiipenda kazi yao hiyo ambayo kwa sasa ni ajira itakayoweza kuwasaidia kuendesha maisha yao.

Aidha Wambura amesema anaamini kuwa Twiga Stara bado wana nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo unaowakbalili, na kuwaomba kupambana zaidi kuhakikisha inapanda na kushinda nafasi ya kwanza Afrika katika soka la wanawake.


Pia amesema wizara yake inashugulikia maombi ya TFF kuiomba wizara ya TAMISEMI ikasimishe mchezo wa mpira wa miguu katika mashindano ya UMITASHUMITA na UMISSETA yaweze kusimamiwa na TFF kwani wao ndio wenye utaalamu wa mchezo huu.

MKUTANO WA 25 WA WADAU NA WANACHAMA WA PPF WAMALIZIKA LEO JIJINI DAR

0
0
 Mgeni rasmi katika Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Jenista Mhagama akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mkutano huo Meneja wa Rasilimali watu na Utawala wa Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam (DIT), Sebastian Ndahani Inoshi, mara baara ya kufunga Mkutano huo leo Februari 12, 2016, kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam . Wanaoshuhudia toka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Hifadhi ya Jamii nchini (SSRA), Irene Isaka, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya SSRA, Juma Muhimbi. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI - MMG.
 Mgeni rasmi katika Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Jenista Mhagama akitoa hotuba yake ya kufunga mkutano huo, uliofanyika kwa siku mbili kuanzia jana February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Washriki wa mkutano huo na Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini hotuba fupi ya kufunga mkutano huo iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Jenista Mhagama, uliofanyika kwa siku mbili kuanzia jana February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah akiwakaribisha watoa mada mbalimbali katika Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, uliofanyika kwa mbili, na kufungwa rasmi leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Jenista Mhagama.
Sehemu ya Meza kuu ikifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kikao cha pili cha Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, unaoendelea kwa siku ya pili, Mkurugenzi Mstaafu wa PPF, Naftali Nsemwa akifafanua jambo kwenye mkutano huo.
Baadhi ya viongozi Waandamizi wa mfuko wa PPF wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye mkutano huo uliowakutanisha Wadau mbalimbali, uliofanyika kwa siku mbili kuanzia jana February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Mdau Mkubwa wa mifuko ya jamii,Mkurugenzi Mstaafu wa PPF, David Mataka akizungumza kwenye Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, unaoendelea kwa siku ya pili,mkutano huo uliowakutanisha Wadau mbalimbali, unaofanyika kwa siku mbili kuanzia jana February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Masha Mshomba akizungumza mbele ya Washiriki wa mkutano huo (hawapo pichani) namna ya mfuko huo unavyoweza kutoa huduma kwa jamii na shughuli zake mbalimbali kwa jamii.
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo akiuliza swali Meza kuu kuhusiana na shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko wa PPF hasa kwa huduma yao ya Fao la uzazi
Baadhi ya Washiriki wakifuatilia Mkutano huo.
Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", uliowakutanisha Wadau mbalimbali, ukiendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.

TAARIFA YA SIKU 100 ZA KWANZA ZA SERIKALI YA AWAMU YA TANO YA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI

0
0
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akitoa taarifa ya siku 100 za kwanza za Serikali ya awamu ya tano.

TAARIFA YA SIKU 100 ZA KWANZA ZA SERIKALI YA

AWAMU YA TANO ILIYOTOLEWA NA

BALOZI OMBENI Y. SEFUE, KATIBU MKUU KIONGOZI,

IKULU, TAREHE 12 FEBRUARI, 2016

__________________________



Utangulizi


Serikali ya awamu ya Tano imetimiza siku 100 tangu iingie madarakani tarehe 5 Novemba, 2015. Japo siku 100 ni chache sana kufanya tathmini ya kina, zinatosha kuonesha muelekeo wa serikali na kupata kionjo cha uthabiti wa dhamira yake ya kutekeleza ahadi zake kwa wananchi.


            Kumekuwa na shauku kubwa ya wananchi kujua kilichofanywa na Serikali hii katika siku zake 100 za mwanzo. Ni shauku ya haki ambayo sisi katika Serikali hii lazima tujaribu tuwezavyo kuikidhi. Ndio maana kuanzia juzi Mawaziri mbalimbali wanazungumzia mafanikio katika hizo siku 100, kila mmoja akienda kwa undani kwenye sekta yake. Nawaomba wananchi wafuatilie kwa karibu yale ambayo Mawaziri hawa wanayatolea taarifa kwenu ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji wao kwa wananchi.


            Mimi pia, kwa nafasi yangu ya Katibu Mkuu Kiongozi, ambaye ni Katibu wa Baraza la Mawaziri na Mkuu wa Utumishi wa Umma, nimepokea maswali mengi ya waandishi wa habari na wananchi wengine kuhusu siku 100 za kwanza za uongozi wa Rais, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Maeneo yanayohusu sekta mbalimbali yatazungumzwa na Mawaziri wanaohusika. Lakini nimeona baadhi ya maswali yanaweza kujibiwa tu na ofisi hii, yaani Ikulu.



            Nimeyaweka maswali hayo katika makundi matano na nitayazungumzia kwa ujumla:


·       Yapo maswali yanayohusu uongozi wa Rais wetu;


·       Yapo maswali yanayohusu sifa binafsi za Rais wetu;


·       Yapo maswali yanayohusu utendaji wake;


·       Yapo maswali yanayohusu mahusiano yake na sekta binafsi kwenye utawala wake; na


·       Yapo maswali yanayohusu mwelekeo wake kwenye mambo ya nje na diplomasia ya Tanzania.



Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano Ukoje?


            Wahenga walisema, “Nyota njema huonekana asubuhi.” Naam! Katika siku 100 za kwanza, Rais Magufuli amethibitisha kwa uwazi zaidi kuwa yeye ni kiongozi bora na wa kupigiwa mfano. Taarifa tunazoletewa na wananchi ni kuwa kwa kauli, matendo na dhamira yake, wananchi wengi wamemwelewa, wamemkubali na wanamwamini. Katika hizi siku 100, Rais amewathibitishia Watanzania kuwa yeye ni kiongozi, mwenye sifa muhimu za uongozi. Sifa hizo ni pamoja na:


·       Kiongozi bora lazima awe na dira, maono na malengo kuhusu anakotaka Taifa liende. Katika siku 100 za kwanza Rais Magufuli amedhihirisha kuwa ana sifa hiyo.


·       Lakini dira bila mkakati ni ndoto. Kiongozi bora lazima awe na mikakati ya kutekeleza dira na maono yake, pamoja na kufikia malengo katika vipindi tofauti. Katika siku 100 za kwanza Rais Magufuli amedhihirisha anayo sifa hiyo.


·       Kiongozi bora lazima aheshimike na awe na mvuto wa kuwafanya wananchi wamwamini, na kumfuata. Katika siku 100 za kwanza za utawala wake, Rais amewafanya hata ambao hawakumpigia kura, wamwamini, wamwombee na kumfuata.


·       Kiongozi bora anagawa majukumu, na haogopi kufanya hivyo, lakini anafuatilia. Katika siku 100 za kwanza Rais Magufuli amethibitisha kuwa anayo sifa hiyo.


·       Kiongozi bora anajua na haogopi kuweka vipaumbele na mpangilio wake wa utekelezaji na kuvisimamia. Katika hizi siku 100 Rais Magufuli amethibitisha anayo sifa hiyo muhimu ya uongozi.


·       Kiongozi bora haogopi kufanya maamuzi magumu. Hakuna mwenye shaka kuwa katika hizi siku 100, Rais wetu amedhihirisha kwa kauli na kwa vitendo kuwa, anapotetea maslahi ya Taifa na wananchi, haogopi kufanya na kusimamia maamuzi magumu.


Rais ana Maono na Mikakati pevu ya kutimiza maono yake


Kama nilivyosema, sifa mojawapo ya kiongozi bora, ni kuwa na maono pevu na mikakati madhubuti inayote

ZANTEL YAIPA MAKTABA KUU 10 M/- KUNUNULIA VITABU

0
0
Na Salum Vuai-Zanzibar

KAMPUNI ya simu Zantel, imeendelea kuipa msukumo sekta ya elimu Zanzibar, mara hii ikitoa msaada wa shilingi milioni kumi kwa Shirika la Huduma za Maktaba Zanzibar kwa ajili ya kununulia vitabu na uendeshaji wa shughuli zake.

Akizungumza katika hafla iliyofanyika leo katika jengo la maktaba hiyo Maisara mjini Zanzibar, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Benoit Janin, amesema msaada huo unalenga kusaidia upatikanaji wa maarifa miongoni mwa jamii ya Wazanzibari.

Janin alisema, ni miongoni mwa majukumu na wajibu wa Zantel, kuhakikisha inatoa huduma bora na zenye ufanisi zinazokidhi mahitaji ya wakaazi wanaoishi mijini na vijijini na kurahisisha upatikanaji wa taarifa za elimu, habari, utamaduni na burudani.

“Upatikanaji wa maarifa kwa wanajamii ni jambo la muhimu na suluhisho la changamoto hii ni kuhakikisha tunatoa fursa sawa kwa kuwezesha kukua kwa maktaba za jamii,” alisema Janin.

Aidha alieleza kuwa, ni fahari kwa kampuni yao kusaidiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuchangia ukuaji na ustawi wa jamii.“Tunaamini kwamba kujifunza ni muhimu kwa maendeleo ya elimu kama moja maeneo ya shughuli zake za kusaidia jamii,” alieleza Ofisa huyo.

Akitoa shukurani zake kwa Zantel, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Abdalla Mzee, aliipongeza kampuni hiyo kwa mchango wao wa miaka mingi katika kukuza maendeleo ya elimu Zanzibar.

“Tunafarijika na mchango wa Zantel katika kusaidia maendeleo ya elimu nchini, na msaada huu uliotolewa leo kwa maktaba yetu kuu utasaidia kurahisisha upatikanaji wa vitabu na hivyo kuimarisha mazingira ya utoaji maarifa miongoni mwa Wazanzibari,” alieleza.

Hata hivyo, aliiomba kampuni hiyo kuangalia uwezekano wa kusaidia maeneo mengine ya kielimu yanayokabiliwa na changamoto kadhaa, ikiwemo kukamilisha ujenzi wa baadhi ya madarasa uliokwama, pamoja na madawati.

Mapema, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Huduma za Maktaba Zanzibar Sichana Mussa Foum, aliishukuru Zantel kwa msaada huo, akisema ni muhimu kwa wateja wa maktaba zake Unguja na Pemba. 

Alifahamisha kuwa, pamoja na jitihada za serikali kuziendeleza maktaba hizo, mchango wa taasisi nyengine unahitajika kutoana na ongezeko la wanafunzi na wananchi wanaohitaji huduma za maktaba.

TIGO YATOA MSAADA WA MADAWATI 400 KWA SHULE ZA MSINGI MKOANI MOROGORO

0
0
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani Goodluck Charles akiongea na wananchi na wanafunzi waliohudhuria hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 400 katika shula za wilaya ya Morogoro vijijini.
Mwanafunzi wa darasa la sita kutoka shule ya msingi kibangile Radia Hamis akishukuru kwa msaada wa madawati kwa niaba ya wanafunzi wa shule hiyo kwa Mkurugenzi wa Tigo kanda ya pwani Goodluck Charles katika hafla ya kukabidhi madawati 400 kwa shula 10 za wilaya ya Morogoro vijijini.
Mbunge wa jimbo la Morogoro kusini Prosper Mbena akimshukuru Mkurugenzi wa tigo kanda ya pwani Goodluck Charles baada ya hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 400 yaliyotolewa na kampuni ya Tigo Tanzania kwa shule 10 za jimbo la morogoro kusini.
Mkurugenzi wa tigo kanda ya pwani Goodluck Charles akimkabidhi Afisa wa Elimu wilaya ya Morogoro vijijini Donald Pambe msaada wa madawati 400 katika shule 10 za wilaya hiyo hafla iliyofanyika katika shule ya msingi Kibangulile
Mkurugenzi wa Tigo, kanda ya Pwani Goodluck Charles(wa nyuma kushoto) na Afisa Uhusiano wa Tigo Halima Okash (mbele kushoto) wakikabidhi madawati 400 yaliyotolea na kampuni ya tigo Tanzania kwa shule kumi za wilaya ya Morogoro vijijini kwa mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mh Prosper Mbena (nyuma kulia) na Afisa Elimu wilaya hiyo Donald Pambe katika shule ya msingi Kibangile iliyopo kata ya Matombo.
…………………………………………………
Kampuni ya Tigo Tanzania imetoa msaada wa madawati 400 yenye thamani ya shilingi milioni 60 kwenye shule 10 za msingi katika mkoa wa Morogoro ikiwa ni mchango wa kampuni hiyo katika kuisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule za msingi nchini.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Shule ya Msingi Kibangile iliyopo Kitemu katika kata ya Matambo, Morogoro Kusini, Mkurugenzi wa Tigo wa Kanda ya Pwani Goodluck Charles mchango huo ni sehemu ya utekelzaji dhamira ya kampuni hiyo ya kuunga mkono shughuli mbalimbali za maendeleo nchini.

“Mchango huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tigo katika kusaidia utekelezaji wa miradi yenye tija kubwa kwa jamii. Tunaamini kwamba kupitia msaada huu, Tigo inatoa mchango wake katika kujenga viongozi wa
baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali wakiwamo madaktari, wahandisi na wengineo, “alisema Charles.

Charles alisema mwaka jana Tigo ilikabidhi msaada kama huo wa madawati katika shule za msingi katika mikoa ya
Shinyanga, Mbeya na Iringa na kuongeza kwamba kampuni hiyo itaendelea kutoa madawati zaidi sehemu mbalimbali nchini siku za zijazo.

Makabidhiano yalihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr Rajabu Rutengwe ambaye alisema madawati hayo 400 yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto katika Mkoa wa Mporogoro na kutoa wito kwa wadahu wengine kuunga mkono zoezi hilo.

“Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya Tigo kwa kuwa mdau muhimu kwetu katika jitihada zinazoendelea za kujaribu kupunguza tatizo la ukosefu wa madawati ya kutosha katika shule za msingi za mkoa wetu wa Morogoro. Ni Dhahiri kwamba msaada huu wa madawati 400 yatawawezesha mamia ya wanafunzi wetu kupata
sehemu za kukaa na hivyo kujipatia elimu zao katika mazingira bora Zaidi,” alisema Dr Rutengwe. 

MUONEKANO WA KITUO KIPYA CHA KUSUKUMA MAJI RUVU DARAJANI KIKIWA KIMEKAMILIKA

0
0
Muonekano wa kituo kipya cha kusukuma maji kilichopo eneo la Ruvu Darajani kikiwa kimekamilika ambapo kitakuwa kinasukuma maji kwenda katika mtambo wa Ruvu Juu.

Pampu moja ya kituo hicho inauwezo wa kusukuma maji lita milion 60 kwa siku kuna jumla ya pampu mpya tatu na pampu mbili zitakuwa zinafanya kazi kwa wakati mmoja.

ASYA IDAROUS KHAMSIN AFANYIWA MAHOJIANO BBC LONDON, LADY IN RED, RICH MAVOKO LEO PATAKUA HAPATOSHI

0
0
Mtangazaji idhaa ya Kiswahili BBC London Maryam akimfanyia mahajiano nguli wa mitindo Bi. Asya Idarous Khamsin jijini London siku ya Ijumaa Februari 12, 2016 mahojiano maalum kwa ajili ya Lady in Red itakayofanyika leo Jumamosi Februari 13, 2016 mjini humo. Onyesho hilo litakalo washirikisha wasanii mbalimbali wakiongozwa na msanii wa Bongo Flava Rich Mavoko litakua ni sehemu ya kusherehekea siku ya wapendanao ambayo mwaka huu imeangukia siku ya Jumapili.
Kulia ni ClubMalibu ambaye ndiye mwenyeji na mdhamini wa Lady in Red itakayofanyika leo jijini London akiwa katika picha ya pamoja na mtangazaji mahiri wa idhaa ya Kiswahili BBC London Bwn. Salim Kikeke.
Kutoka kushoto ni msanii wa Bongo Flava Rich Mavoko, Mgalula Fundikila, Salim Kikeke na mama wa mitindo Asya Idarous Khamsini walipokua mjengoni idhaa ya Kiswahili BBC London.
Mtangazaji wa idhaa ya Kiswahili BBC London Sakuma Kssim akiwa katika picha ya pamoja na nguli wa mitindo Bi. Asya Idarous Khamsin wakati mwanamitindo huyo alipokua mjengoni huko kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano.
Kutoka kushoto ni Saluma Kssim, Maryam, Aisha Yahya wakiwa katika picha ya pamoja mama nguli wa mitindo Asya Idarous Khamsini.

TAMASHA LA ‘AMSHA MAMA TANZANIA’ KUFANYIKA MACHI 5 KATIKA UWANJA WA MWEMBEYANGA TEMEKE JIJINI DAR

0
0
WATANZANIA  wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika Tamasha la ‘Amsha Mama Tanzania’ linalotarajiwa kufanyika Machi 5 katika uwanja wa Mwembeyanga Temeke  jijini  Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Kampuni ya  Candy record yenye makao Mkuu yake nchini Kenya ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo Joe Kariuki amesema wameamua kuleta tamasha nchini ili kuwapa fursa akina mama wa Tanzania kujiinua kiuchumi .“ Akina mama mjitokeze kwa wingi katika tamasha hili mahususi kwenu kwa kuwa  mtapata fursa mbalimbali na mtaweza kupata mambo mbalimbali ikiwemo elimu” .Alisema Kariuki.

Kwa upande wake balozi wa Amsha Mama nchini Khalid Ramadhani (Tundaman), amewaomba wakinamama wachangamkie fursa kwani watajifunza mambo mengi “Nawaomba Mama zangu mjitokeze kwa wingi kwani tumepata bahati ya pekee ya kupendelewa kuletewa tamasha nchini kwani ni adimu kutokea,” .alisema Tundaman.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika pia katika uwanja wa Ranchi ya Kedong uliopo jiji la Naivasha nchini Kenya marchi 25-27 huku likitarajia kukutanisha akinamama kutoka nchi zote za Afrika .

Aidha kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii kama vile Juma Kassim  ‘’Juma Nature’’, Khadija Kopa, Roma Mkatoliki, Young Killer, Msagasumu, Man fungo,Sharo mwamba,Q-Chief,Mr Blue,Snura,Tundaman,na Ally Choki.
Tamasha la Amsha Mama linatarajiwa kukutanisha akinamama mbalimbali kwa lengo la kujifunza kuhusu kujikwamua kiuchumi kwani wao ndio chachu ya mafanikio.

Alisema wamejipanga kuwapa  radha tofauti  watoto wa temeke na majirani zake ,hasa kwa akina mama kupata fursa ya kujielewa na kujitambua hasa katika kuendeleza familia zao.
Mwisho.

HATIMAYE VIFAA VYA KUMALIZIA UJENZI WA UWANJA WA KAITABA VYAWASILI HII LEO MJINI BUKOBA. UJENZI SASA KUMALIZIKA MWEZI HUU.

0
0
Magari yaliyowasili hii leo katika Uwanja wa Kaitaba yaliyoleta vifaa kwa ajili ya Umaliziaji wa Ujenzi wa Uwanja ambao ujenzi wake ulikuwa ukisua sua kutokana na kukwama kwa Vifaa hivyo Jijini Dar es salaam.
Mshauri wa ufundi Bwana Rutayunga Peregrinus akiteta jambo na waandishi wa habari(kulia) leo kwenye Uwanja wa Kaitaba juu ya Umaliziaji wa Uwanja huo muda mfupi baada ya Vifaa hivyo kuwasili hii leo. Picha Na Faustine Ruta wa bukobasports.com
Mshauri wa ufundi Bwana Rutayunga Peregrinus
Ndipo akafafanua kwamba Uwanja baada ya Vifaa kuwasili umaliziaji utaanza mara moja huku akisisitiza kwamba Mwezi huu wa februari kama mambo yaenda vyema utamalizika. Na Timu ya Kagera Sugar itamalizia michezo yake ya Msimu huu kwenye Uwanja huu. Pia Bukobasports imeweza kupata habari zaidi kuwa Rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi nae yupo Mjini hapa Bukoba akifuatilia Mradi huo wa Uwanja unavyoendelea na kesho Jumamosi atakutana na Viongozi wengine na kuteta nao na hatimae kukamilisha Ujenzi huo wa Uwanja Mwezi huu wa Februari.
Afisa utamaduni wa Mkoa wa Kagera Bw. Rugeiyamu nae alikuwepo katika Uwanja huo. Picha Na Faustine Ruta wa bukobasports.com.


Mesh rubber crumb
Junior Mwemezi wa Azam Tv akiteta jambo na Mshauri wa ufundi Bwana Rutayunga Peregrinus
Swala zima ni juu ya Umaliziaji wa Uwanja wa Kaitaba ndicho kilichokuwa kikisisitizwa leo baada ya Vifaa kuwasili.
Sehemu ya Uwanja huo kama unavyoonekana ukiwa ulishawekwa nyasi bandia
Sehemu ya Ukingo ambayo ukutanisha maji na kuyatoa nje kupitia kwenye bomba maalum.Junior Mwemezi wa Azam Tv na Fausti Ruta Taswira ya Uwanja wa Kaitaba ulivyo kwa sasa.Junior Mwemezi wa Azam Tv na Fausti Ruta wa bukobasports walipata muda wakapumzika japo kwa uchache katika Uwanja huo ambao unaelekea kumalizika ujenzi wake.
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live




Latest Images