Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 762 | 763 | (Page 764) | 765 | 766 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Bi Flora Mathias Kutoka Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkulima mdogo akitoa majumuisho kutoka kipengele cha namna ya kudhibiti Bajeti za Serikali kutoka katika mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2016/2017 ukurasa wa 14-20, picha ya juu ni wanakundi wakiwa wanajadili swala hilo. Picha ya juu ni baadhi ya mama Shujaa wa chakula ambao wanatoka katika Kampeni ya Grow inayoendeshwa na Oxfam Tanzania pamoja na wadai wengine wa kilimo
  Mzee Namagono Hassan Kutoka kikundi namba moja akitoa maelezo kutoka katika mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2016/2017 kutoka ukurasa wa 6-9  unaoelezea mambo muhimu katika mwongozo wa Bajeti 2016/17
   Datius Pastory Inshansha ambaye ni Mwanaharakati na Mkulima mdogo mdogo akiwasilisha kundi lake la Tano ambao walikuwa wanajadili ukurasa wa 20-23 kutoka katika mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2016/2017 inayozungumzia maelekezo mahsusi kwa sekretarieti za mikoa na mamlaka ya serikali za mitaa.
  Bwana Adam Simwinga akitoa maelezo kutoka kundi namba mbili ambao walikuwa wachambua mpango wa bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2016/2017 ukurasa wa 9-15 kipengele cha Maelekezo ya Maandalizi ya bajeti
   Bi. Kidani Mhenga kutoka kikundi namba tatu ambao walikuwa wanajadili ukurasa wa 3-5 mapitio ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti za Serikali kuoka katika mpango wa bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2016/2017
  Baadhi ya wakulima, wafugaji na wavuvi wakiendelea namjadala 

  Picha na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa

  MwongozowaMpangonaBajetikwamwaka2016/17umeandaliwakwa kuzingatiaKifunguNa.21chaSheria yaBajetiNa.11yaMwaka2015.Aidha, Mwongozowa MpangonaBajetiwa Mwaka2016/17 umejikita katika kujenga Taifa lenyeuchumiwa viwandakamailivyoainishwa kwenyeMpangowa Maendeleowa Taifa  wa  mwaka  2016/17  pamoja  na  Mpango  Elekezi  wa  Miaka  15


  Warsha hiyo ambayo imeandaliwa  na ushirikino wa mashirika matano ambayo ni  Oxfam, Policy Forum, ANASAF, Action Aid na TGNP zaidi ikiwa ni kuwaleta pamoja wakulima hao wadogowadogo  katika kupitia mwongozo na kuujadili kwa ukaribu pamoja na kuuchambua kwa kina zaidi.


  Wakati akitoa majumuisho kutoka ukurasa wa 14-20 Bi Flora Mathias Kutoka Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkulima mdogo ameomba Mkulima ameiunga mkono hoja ya mwanamke kuthaminiwa na kupata nafasi ya kuuza Bidhaa zake, kupewa nafasi ya kujitambua na kumiliki Ardhi, huku akiulalamikia mwongozo huo wa bajeti elekezi kutoweka wazi kuhusu mfuko wa wanawake katika kusaidia uzalishaji na kuomba bajeti inayokuja izingatie hilo.


  Mzee Namagono Hassan kutoka kundi la wakulima ametoa  maelezo kutoka ukurasa wa 6-9  kuhusu mambo muhimu katika mwongozo wa Bajeti 2016/17, kuwa pamoja na kuanzishwa kwa Benki ya wanawake, isitazame tuu wanawake wa mjini bali na  vijijini kwani wao ndio wazalishaji zaidi wa Chakula kuliko waishio mijini.  Kwa upande wake Datius Pastory Inshansha Mwanaharakati na Mkulima mdogo ukurasa wa 20-23 amepitia ukurasa 23-24 unaotoa maelekezo mahsusi kwa sekretarieti za mikoa na mamlaka ya serikali za mitaa na kushauri kuwepo uwazi wa mapato na matumizi ya Serikali za Mitaa, pia Bajeti ielekezwe zaidi vijijini kulipo mjini na kudhibiti fedha za uvuvi,kilimo na ufugaji zisiishie kwa watu wachache bali wahusika kwa ujumla.


  Maelezo mengine yametolewa na Bwana Adam Simwinga kuhusu ukurasa wa 9-15 kipengele cha Maelekezo ya Maandalizi ya bajeti kwamba amegundua hakuna mkakati wa kuongeza mapato kupitia simu, mkakati wa msamaha wa kodi, hivyo wameshauri kilimo kiwe ni sehemu ya eneo wezeshi na malighali katika viwanda nchini Tanzania na katika mpango wa maendeleo na kuongeza kuwa asilimia 30% hazijitoshelezi kukuza sekta ya kilimo nchini.


  Wanaharakati hao wameishauri serikali kutowasahau katika kuwawezesha mikopo ili kukuza sekta zao kimaendeleo huku wakilalamika wakulima  kutoshirikishwa kikamilifu.


  “Tunaomba mkopo wa Magari ya wabunge upungue kutoka Mil 90 hadi Mil 20 ili zile mil 70 zitumike katika shughuli zingine za maendeleo ikiwemo na kilimo na pia kuwe na viwanda vidogo vidogo katika mikoa mbalimbali mfano kiwanda cha Machungwa” aliongeza Bi. Kidani Mhenga wanajadili ukurasa wa 3-5 mapitio ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti


  0 0
 • 02/11/16--04:44: TAARIFA KWA UMMA
 • JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO  Simu: 022 2126826

  Nukushi: 022 2126834

  Baruapepe: km@habari.go.tz

   

  Jengo la PSPF Golden Jubilee Tower

  Ghorofa ya Nane,

  S. L. P. 8031,

  7  Mtaa wa Ohio,

  11481 DAR ES SALAAM.


   
                                                

  TAARIFA KWA UMMA


  DAWATI LA TAARIFA.


  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inapenda kuwafahamisha wananchi kwamba  imeanzisha Dawati la Taarifa linatoa  fursa kwa jamii kupata Taarifa mbalimbali za Wizara kwa kupiga Simu namba zifuatazo: +255222122771na +255222122772 ama kutuma ujumbe wa maneno kupitia barua pepe(email): dawati.taarifa@habari.go.tz Na utapatiwa majibu sahihi kwa wakati.

  Pia unaweza kufika katika ofisi za Wizara ambapo Dawati la Taarifa linapatikana Ofisi za Idara ya Habari Maelezo mtaa wa Samora ili kuweza kupata taarifa zaidi kuhusu huduma na namna unavyoweza kupata huduma zinazotolewa na Wizara.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini:


  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo


  0 0

  Makalbi ya mtaro wa kupitishia maji kutoka katika viwanja vya mpira mnazi mmoja yakitandikwa, na kulia ni mabomba ya mtaro huo ya zamani yaliokuwa yakitoa huduma hiyo ya kupitisha maji kutoka katika uwanja huo. 
  Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe.Luhaga Mpina akiangalia ujenzi huo wakati wa ziara yake kutembelea miradi huo. 
  Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe.Luhaga Mpina akiangalia ujenzi huo wakati wa ziara yake kutembelea miradi huo. 


  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akimsikiliza Mhandisi wa Baraza la Manispa Zanzibar Ndg Mzee Khamis Juma akitowa maelezo ya kitaalumu ya Ujenzi wa Mtaro wa maji machafu wakati wa mvua kunyesha   
  Mhandisi wa Baraza la Manispa Zanzibar Mzee Khamis Juma akizungumza wakati wa ziara ya Mhe Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina wakati alipofika kutembelea mradi wa ujunzi huo katika uwanja wa mnazi mmoja Zanzibar, kuondosha tatizo wa maji katika uwanja huo unaokuwa kero kutumika kwa kiwanja hicho kipindi cha mvua na kuingia maji ya bahari. 
  Mradi wa Ujenzi wa Mtaro wa maji katika uwanja wa mpira wa mnazi mmoja unaoendelea na ujenzi wa mtaro huo.
  Mradi wa Ujenzi wa Mtaro wa maji katika uwanja wa mpira wa mnazi mmoja unaoendelea na ujenzi wa mtaro huo.
  Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe.Luhaga Mpina akizungumza wakati alipofika katika mradi wa Ujenzi wa Mtaro wa Maji katika Viwanja vya Mnazi Mmoja akiwa katika ziara yake kisiwani Zanzibar. na kumalizia Kisiwani Pemba kutembelea Miradi ya Mazingira kisiwani humo. 
  Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe.Luhaga Mpina akizungumza wakati alipofika katika mradi wa Ujenzi wa Mtaro wa Maji katika Viwanja vya Mnazi Mmoja akiwa katika ziara yake kisiwani Zanzibar. na kumalizia Kisiwani Pemba kutembelea Miradi ya Mazingira kisiwani humo. 
  Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akiwa katika ziara yake kutembelea Jimbo la Jangombe kujionea athari za mazingira inazozikabili Jimbo hilo kwa kutokea kwa kuzama kwa nyumba katika mwaka 1998 na baadhi ya nyumba nyengine kupata athari.
  Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akiwa katika ziara yake kutembelea Jimbo la Jangombe kujionea athari za mazingira inazozikabili Jimbo hilo kwa kutokea kwa kuzama kwa nyumba katika mwaka 1998 na baadhi ya nyumba nyengine kupata athari.
  Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akiwa katika ziara yake kutembelea Jimbo la Jangombe kujionea athari za mazingira inazozikabili Jimbo hilo kwa kutokea kwa kuzama kwa nyumba katika mwaka 1998 na baadhi ya nyumba nyengine kupata athari.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akiwa katika ziara yake Jimbo la Jangombe Zanzibar.kushoto Meya wa Baraza la Manispa Zanzibar Mhe. Khatib Abdurahan Khatib na Mkurugenzi  Mazingira Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Ndg Juma Bakari Alawi.
  Sheha wa Shehia ya Jangombe Ndg Khamis Ahmada Salum akitowa maelezo kwa Mhe Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe Luhaga Mpina wakati wa ziara yake katika Jimbo hilo.
  Mhe Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akisalimiana na Wazee wa Jimbo la Jangombe wakati wa ziara yake katika Jimbo hilo akiwa Zanzibar. 
  Eneo lilikozama Nyumba katika mtaa wa Jangombe Mshelishelini mwaka 1998 ambapo amefika Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina wakati wa ziara yake Zanzibar kutembelea Miradi ya Mazingira na ya Muungano ilioko Zanzibar.,
  Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akiwa katika eneo iklikoza nyumba hiyo Jangombe wakati wa ziara yake Zanzibar.
  Mwananchi wa Jangombe Nyumba yao ilididimika katika eneo hilo wakati wa Mvua za masika katika mwaka 1998 Ndg Salum Ibrahim Mgaza akitowa ushuhuda wa kuzama kwa nyumba yao kwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira wakati wa ziara yake katika jimbo hilo na kufika katika eneo hilo ilikozama nyumba hiyo katika mwaka 1998 na kubaki kiwanja hadi sasa. 


  Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akimsikiliza Sheha wa Jangombe wakati wa ziara yake katika Jimbo hilo kuangaria athari za Mazingira zinazolikabili Jimbo hilo akiwa katika eneo lililotokea shimo wakati wa mvua za mashika na kuleta athari katika eneo hilo.  


  Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akimsikiliza Sheha wa Jangombe wakati wa ziara yake katika Jimbo hilo kuangaria athari za Mazingira zinazolikabili Jimbo hilo akiwa katika eneo lililotokea shimo wakati wa mvua za mashika na kuleta athari katika eneo hilo.  
  Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Ndg Juma Bakari Alawi akitowa maelezo kuhusiana na hali ya Mazingira katika eneo la Jangombe ambolo linakumbwa na ujaaji wa maji ya mvua na kujitokeza kudidimia kwa ardhi ya eneo hilo, wakati wa Ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina, katika Jimbo la Jangombe kuangalia Miradi ya Maendeleo inayosimamiwa na Muungano Zanzibar.
  Imetayarishwa na Othman Mapara.

  0 0

  *Aibukia kitengo cha mita za kupimia mafuta Kurasini
  *Akuta mafundi wakizitengeneza, akuta zimejaa kutu
  *Ataka barua ya maelezo ifikapo saa 11 leo jioni


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara ya ghafla kwenye kitengo cha upimaji mafuta bandarini (Oil Flow Metres) na kukuta zimejaa kutu baada ya kutelekezwa kwa miaka zaidi ya mitano. Pia alitembelea mita za kupimia mafuta zinazoendelea kujengwa Kigamboni.

  Aidha, Waziri Mkuu amempa saa nne tu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo nchini (WMA), Bi. Magdalena Chuwa aandike barua ya kujieleza ni kwa nini aliamua kufunga mita hizo zisitumike kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita na amletee barua hiyo ofisini kwake ifikapo saa 11 leo jioni.

  “Nataka unieleze ni kwa nini ulitoa maelekezo ya kufunga mita hizo, na kwa nini jana uliamua kubadili uamuzi huo? Ni kwa nini umeamua kuchukua maamuzi haya baada ya kupokea ujumbe wa simu ya mkononi (sms) wakati mita zimekaa bila kufanya kazi kwa miaka mitano? Ni kwa nini umeamua kufanyia kazi ujumbe wa sms wakati unajua Serikali inafanya kazi kwa maandishi rasmi?” alisema Waziri Mkuu.

  “Umesema mlikuwa mnatumia utaratibu wa kupima kwa kijiti. Huu hauna uhakika na huwezi kutegemea taarifa ya mtu mwingine au kuingia kwenye meli ya mtu na kuanza kuchukua vipimo hadi ujiridhishe. Nataka kujua ni kwa nini mlikuwa na utaratibu wa ku-bypass mafuta ili yasipite kwenye mita za kupimia mafuta? Ni kwa nini umetoa amri zianze kutengenezwa jana na siyo mwaka 2012 au 2013?” alihoji Waziri Mkuu.

  Waziri Mkuu alisema mita hizo za Kurasini zilinunuliwa na Serikali kwa gharama za dola za marekani milioni 1.2 (wakati huo) na haiwezekani kuacha kuzitumia wakati watu wanachezea mifumo na kuongeza mianya ya kupoteza mapato kwa Serikali. Ameagiza mita hizo zianze kufanya kazi mara moja.

  Wazir Mkuu alisema matumizi ya mita hizo yaliafikiwa na Serikali baada ya kubaini upotevu mkubwa wa kodi kwenye mafuta yanayoingizwa nchini na baada ya kuona hakuna tija ya kuendelea na ukadiriaji au kupokea taarifa za waagizaji peke yao.

  Waziri Mkuu ambaye aliwasili Kurasini leo saaa 4: 30 asubuhi (Alhamisi, Februari 11, 2016) kwenye kitengo hicho kilichopo Kurasini (Kurasini Oil Jetty), alikagua mita hizo na kisha kwenda kukagua meli iliyokuwa ikishusha mafuta bila kutumia mita hiyo ya kupima mafuta yanayopokelewa kwa sababu mafundi walikuwa bado wanaendelea na ukarabati.

  Akiwa Kurasini, Waziri Mkuu alielezwa na Bibi Chuwa kwamba mita hizo zilianza kufanyiwa ukarabati jana na leo asubuhi moja imekamilika ambayo ni ya kupokelea mafuta ya petroli. Ya dizeli ilikuwa inafunguliwa na mafundi na kukutwa imejaa kutu sababu ya kutotumika kwa muda mrefu.

  “Hii ya dizeli imefunguliwa leo na ile ya mafuta ya kula, haijawahi kufanya kazi tangu ilipofungwa mwaka 2011,” alielezwa Waziri Mkuu na Kaimu Mkurugenzi wa Bandari, Eng. Aloyce Matei.

  Alipoulizwa ni kwa nini aliamua kuzifungia mita hizo ziisifanye kazi, Bi. Chuwa alijibu kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kupokea malalamiko kwamba zinawapunja wateja. Hata hivyo, hakufafanua ni wateja gani au wa aina gani.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa, ametembelea na kukagua mita mpya za kupimia mafuta ambazo zinajengwa Kigamboni. Mita hizo zimegharimu dola za marekani milioni 6 (sawa na sh. bilioni 12.96/- za sasa).

  Akiwa hapo, Waziri Mkuu alielezwa kwamba ujenzi huo ambao ulianza miezi nane iliyopita, unatarajiwa kukamilika ifikapo katikati ya mwezi Machi, 2016. “Tunajitahidi kazi hii ikamilike ifikapo katikati ya mwezi ujao,” alisema Eng. John Bura, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya BQ Contractors Ltd ambayo inasimamia ujenzi wa mita hizo.

  Vilevile, Waziri Mkuu alitembelea sehemu ya kuchukulia mafuta yanayotoka bandarini (TPA Manfold) iliyoko Kigamboni na kukagua mitambo ya kusambazia mafuta kwenye matenki ya mafuta ya kampuni ya TIPER yaliyoko Kigamboni yanayomilikiwa kwa ubia bainaya Serikali na kampuni ya Oryx Energies.

  Katika ziara hiyo ilibainika kuwa Kampuni ya TIPER imejiunganishia bomba la moja kwa moja kutoka kwenye bomba kubwa la mafuta linalotoka bandarini hali iliyomlazimu Waziri Mkuu kuagiza kwamba bomba hilo litolewe kwenye maungio hayo ndani ya mwezi mmoja.

  “Natoa mwezi mmoja hili bomba liondolewe kwenye mfumo huu na kama yapo mabomba mengine pia yaondolewe,” alisema huku akionyesha karatasi iliyokuwa mfukoni kwake yenye mchoro unaobainisha kuwa kuna bomba jingine la inchi 10 limeungwa kinyemela kwenye bomba kuu.

  “Kila mmoja anapaswa aje kuchukua pale kwenye manfold ili tujue nani kachukua nini. Msajili wa Hazina hili ni eneo lako na wewe unamiliki TIPER kwa asilimia 50, hebu simamia hili. Ninyi TPA leteni mapendekezo yenu Serikalini ili tuone tunaweza kudhibiti vipi vitendo kama hivi,” alisema Waziri Mkuu.

  Pia alimtaka Msajili wa Hazina, Bw. Lawrence Mafuru awasiliane na Mwanasheria Mkuu ili waangalie upya mkataba na umiliki wa matenki hayo uwe chini ya Serikali kwa asilimia 100 ili mafuta yanayoagizwa na Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (Petroleum Bulk Procurement Agency) yaweze kuhifadhiwa huko.

  Mapema, Waziri Mkuu ambaye alifuatana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, alikagua eneo la manfold ya Mamlaka ya Bandari iliyopo Kigamboni na kukuta ni kampuni nne tu zenye matenki Kigamboni ambazo zinachukua mafuta yao hapo.

  Kampuni hizo ni HASS, WORLD OIL, LAKE OIL na MOIL. TIPER haikutaka kufuata mfumo huo licha ya kuwa nafasi ya kufanya hivyo ipo. Kampuni nyingine zenye matenki yake nchi kavu, zinachukulia mafuta kwenye manfold ya Kurasini.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM.
  ALHAMISI, FEBRUARI 11, 2016.

  0 0

   
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Mhandisi, Aloys Mtei (kulia) kuhusu  mabomba yanayotawanya mafuta kwenda kwenye matangi makubwa ya makampuni mbalimbali kwenye eneo la Kigambo jini Dar es salaam Februari 11, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo ambalo mafuta hufunguliwa na kufungwa ili kwenda kwenye matangi ya kuhifadhia mafuta ya makampuni mbalimbali yanayoagiza mafuta toka nje ya nchi wakati alipokwenda enero la Kigamboni jijini Dar es salaam kuonamianya inayotumika kukwepa kodi za mafuta yanayoagizwa nje ya nchikupitia bandari ya Dar es salaamFebruari 11, 2016.  
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitaka maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo na Mizani, Bibi Magdalena Chuwa (kulia) kuhusu sababu zilizomfanya azuie matumizi ya flow Meter katika kuhakiki kiwango cha mafuta yanayoingia nchini kupitia bandari ya Dar es salaam wakati alipofanya ziara kwenye badari hiyo Februari11, 2016. katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Raymound Mushi. 

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyeshwa na kamimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamla ya bandari Tanzania, Mhandisi Aloys Mtei eneo zinakotia nanga meli kubwa zinazoleta mafuta nchini kupitia bandari ya Dar es salaam Februari 11, 2016. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo lenye mabomba yanayotumika kupitisha mafuta kutoka kwenye meli  kupitia bandari ya Dar es slaam wkatia lipofanya ziara ya kukagua miundombinu yenye mianya ya ukwepaji kodi hasa kwenye mafuta yanayoingia nchini Februari 11, 2016.  
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Ujezi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa (kulia) wikimsikiliza Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari Tanzania,Mhandisi, Aloys Mtei wakati alipotoa maelezo kuhusu uingizaji wa mafuta kutoka nje ya nchi kupitia bandari ya Dar es salaam Februari 11, 2016.Mheshimiwa majaliwa alikuwa katika ziara ya kukagua miundombinu yenye mianya ya ukwepaji kodi kwenye mafuta yanayoingia nchini kupitia bandadari hiyo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Flow Meter eneo la Kigamboni jijini Dar es salaam Februari 11, 2016. Mtambo huo utatumika kupima wingi wamafuta yanayotoka kwenye meli na kuingizwa hapa nchini. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymound Mushi.
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetuma salamu za rambirambi kwa familia ya mwandishi wa habari za michezo nchini Hamis Dambaya kufuatia kufiwa na mkewe, mwanae pamoja mama mkwe wake.

  Katika salamu hizo, TFF imempa pole Dambaya kwa msibu huo mzito uliomfika na kusema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini, Shirikisho liko pamoja nao katika kipindi hichi kigumu cha maombelzo ya misiba hiyo.


  Mkewe Hamis Dambaya, mwanane na mama mkwe wake wamefariki katika ajali ya bus la Simba Mtoto iliyotokea leo asubuhi katikati ya eneo na Muheza na Hale wakati wakiwa safarini kuelekea jijini Dar es salaam wakitokea mkoani Tanga.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mama Mwantumu Mahiza, kufuatia vifo vya watu 11 waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani iliyosababishwa na Basi la Kampuni ya Simbamtoto kugongana uso kwa uso na Lori lililobeba mchanga katika eneo la Pandamlima, Wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga.


  Ajali hiyo imetokeo leo tarehe 11 Februari, 2016 majira ya saa 1:15 asubuhi katika eneo hilo lenye mteremko, ambapo basi la Kampuni ya Simbamtoto lilikuwa likisafiri kutoka Tanga kwenda Dar es Salaam na Lori lililokuwa limebeba mchanga, lilikuwa likielekea kiwanda cha Saruji cha Tanga.

  Rais Magufuli amewapa pole Ndugu, Jamaa na Marafiki wote waliofikwa na msiba huo na amewataka kuwa wavumilivu na wastahimilivu katika kipindi hiki kigumu.


  "Nimepokea taarifa ya vifo hivi kwa mshituko mkubwa, na kupitia kwako Mkuu wa Mkoa wa Tanga, napenda kuwapa pole nyingi wote waliofikwa na msiba huu mkubwa na naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo" alisema Rais Magufuli.


  Dkt. Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, na amewapa pole majeruhi wote 21 walioumia katika ajali hii.

  Aidha, Rais Magufuli amewakumbusha watumiaji wote wa barabara hususani madereva wa vyombo vya moto, kuwa makini watumiapo barabara kwa kuzingatia sheria zote zinazosimamia usalama barabarani ili kuepusha ajali.


  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

  Dar es salaam.


  11 Februari, 2016.

  0 0

  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) akimsikiliza kwa makini Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Didas Entertainment Bibi. Khadija Seif (Dida) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.Kampuni hiyo inajishughulisha na udhamini wa wasanii nchini.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni inayojishughulisha na uandaaji wa Filamu ya Didas Entertainment Bibi. Khadija Seif (Dida) (akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni hiyo wakiwa katika ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania leo jijini Dar es Salaam.

  Na: Frank Shija
  SERIKALI imepongezwa kwa namna inavyotoa ushirikiano na kusaidia wasanii na wadau wa tasnia ya Filamu hapa nchini.

  Pongezi hizo zimetolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Didas Entertainment Bibi. Khadija Seif (Dida) alipotembelea ofisi za Bodi ya Filamu leo jijini Dar es Salaam.

  Dida amesema kuwa kama mdau wa Filamu anaishukuru na kuipongeza Serikali namna ambavyo inathamini na kutambua mchango wa wadau wa tasnia hiyo hapa nchini.

  “ Naishukuru Serikali kwa namna ambavyo imekuwa ikitoa ushirikiano kwetu sisi wadau wa tasnia ya filamu hapa nchini” Alisema Dida.

  Aidha Dida amesema kuwa kupitia Kampuni yake ya Didas Entertainment yenye ofisi zake jijini London ipo katika uaandaaji wa Filamu mbili ambazo ni “Dida” na “Black Belt” zitakazo tengenezewa hapahapa nchini. 

  Nakuongeza kuwa filamu hizo zitakuwa shirikishwa baadhi ya wasnii kutoka Nigeria na zitakapo kamilika Filamu ya Black Belt inatarajiwa kuzinduliwa katika nchini nne tofauti ambazo ni Uingereza, Nigeria, Ghana na Tanzania

  Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesma kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa tasnia Filamu wandani na njje ya nchi ili kutanua wigo wa tasnia hiyo kukua kwa kasi.

  Fissoo ametoa wito kwa wadau wa Filamu kuja kuwekeza katika tasnia Filamu hapa nchini ili kutanua wigo wa filamu za Kitanzania 


  Didas Entertaiment imekuwa msaada mkubwa kwa tasnia za Filamu na Muziki ambapo mpaka sasa imewezesha takribani wasanii 30 kupata maonyesho nchini Uingereza, na imefanikiwa kutengeneza Filamu moja ya “Mateso yangu Ughaibuni”ambayo inafanya vyema katika soko.Kampuni hii imefungua milango kwa wasanii wa Filamu ili kutanua wigo wa Filamu za Kitanzania.

  0 0  Na Jacquiline Mrisho-Maelezo.

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kukamata bidhaa za magendo kwenye maeneo mbalimbali yaUkanda wa wa Bahari ya Hindi, Ziwa Viktoria na mipaka mingineyo nchini.

  Taarifa hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA) Bw. Richard Kayombo wakati akifanya mahojiano na Mwandishi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kuhusu juhudi za operesheni ya kutokomeza bidhaa za magendo nchini.

  Bw. Kayombo ameeleza kuwa, katika Mkoa wa Lindi TRA imefanikiwa kukamatamashua katika bandari ya Lindi ambayo ilisheheni bidhaa za magendo zenye thamani ya shilingi 159,361,046.

  Ameongeza kuwa katika operesheni hiyo, TRA imefanikiwa kukusanya kodi ya jumla ya shilingi 10,500,678 kutoka katika bidhaa zilizokuwa katika nyaraka za forodha (manifest) ambapo pia inategemea kukusanya kodi ya shilingi 19,529,500 kutoka katika bidhaa ambazo zilikuwa katika nyaraka za forodha lakini thamani yake ilikuwa chini ya beo halisi.

  Akitaja bidhaa hizo za magendo zilizokamatwa katika mashua hiyo ni mifuko 3,725 ya sukari yenye thamani ya shilingi 127,070,562, betri katoni 50, mchele mifuko 3,087, mafuta ya kula madumu 80, majokofu manne ya mtumba, baiskeli za mitumbo nne pamoja na katoni 20 za hamira.

  ‘’Mashua hiyo ilikamatwa katika bandari ya Lindi tarehe Mosi Februari, 2016 baada ya wasamaria wema kutoa taarifa ya kuwepo bidhaa za magendo ndani ya mashua hiyo ambapo upakuaji wa shehena hiyo ulianza mara moja’’, alisema Kayombo.

  Kayombo kaongeza kuwa kwa upande wa jijini la Dar es Salaam, TRA kwa kushirikiana na Kikosi cha doria cha Jeshi la Wanamaji wameweza kukamata Jahazi lenye jina la ‘Takbiri’ lenye usajili wa namba Z-875 likiwa limesheheni lita 19,700 za dizeli ambapo thamani yake bado haijapatikana kwakuwa imepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya Uchunguzi zaidi.

  Aidha, majahazi mengine matatu yamekamatwa katika eneo la Kigombe mkoani Tanga ambayo yalikuwa na bidhaa za magendo yenye thamani ya shilingi 99, 682, 273, 48 ambamo ndani kulikuwa na magunia ya sukari, mchele, mafuta ya kula, matairi ya magari, nyaya za kuzuia mbu, jokofu, jiko la umeme, rangi za kupuliza, betri na biskuti ambapo majahazi hayo yalitaifishwa baada ya wahusika kujitosa ndani ya maji na kutoroka.

  Aidha, TRA kwa kushirkiana na Jeshi la Polisi metoa wito kwa umma kuwa inafanya doria saa 24 kila siku katika maeneo yote yaliyoshamiri upitishaji wa bidhaa za magendo ambapo imeunda Kanda Maalum katika maeneo ya Mbweni, Msasani, Kunduchi pamoja na Kigamboni.

  0 0


  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala akizungumza wakati wa kikao cha bodi ya barabara kilichoketi katika ukumbi wa ofisi ya RC .

  Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi, Exaud Mamuya akichangia katika kikao hicho.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.


  Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho ambacho hutangulia kabla ya kikao cha Ushauri cha Mkoa (RCC).
  Waziri wa Maliasili na Utalii ,Pro Jumanne Mghembe ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mwanga akichangia hoja katika kikao hicho.
  Mkuu wa wilaya ya Mwanga ,Shaibu Ndemanga akifuatilia michango iliyokuwa ikitolewa katika kikao hicho.
  Mkuu wa Wilaya ya Rombo ,Lembris Kipuyo akifutilia michango ya hho .oja mbalimbali katika kikao hicho.
  Mkuu wa Wilaya ya Moshi Novatus Makunga akifuatilia michango katika kikao hicho.
  Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Kilimanjaro,Mwita Rubirya akizungumza wakati wa kikao cha Bodi ya barabara .
  Mkuu wa Wilaya ya Same,Herman Kapufi akifuatilia michango katika kikao hicho.
  Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akifuatilia michango katika kikao hicho.
  Mkuu wa wilaya ya Siha,Dkt Charles Mlingwa akifuatilia michango katika kikao hicho.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Same ,Christopher Ilila akichangia katika kikao hicho.
  Mkuu wa wilaya ya Same ,Herman Kapufi akichangia katika kikao hicho.
  Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akichangia katika kikao hicho.
  Mkuu wa wilaya ya Siha,Dkt Charles Mlingwa akichangia katika kikao hicho.

  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kulia) akimsikiliza Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Bw. Song, Geum-young alipomtembelea ofisini kwake mapema leo.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia) akizungumza na Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Bw. Song, Geum-young alipomtembelea ofisini kwake mapema leo.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia) akizungumza na Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Bw. Song, Geum-young alipomtembelea ofisini kwake mapema leo.

  0 0

   Jengo jipya la hosteli ya wasichana la Chuo cha Madini Dodoma (MRI) ambalo ujenzi wake umekamilika hivi karibuni.
   Bwalo la wanafunzi wa Chuo cha Madini Dodoma baada ya kukarabatiwa na kupanuliwa.

   Mkuu wa Chuo cha Madini cha Dodoma, Mhandisi Oforo Ngowi (wa pili kutoka kulia) akifafanua jambo wakati wa ukaguzi wa bwalo la wanafunzi. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Nishati na Madini, Caroline Musika akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo chaTehama, Wizara ya Nishati na Madini, Francis Fungameza. Wa kwanza kulia ni Mshauri Mwelekezi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PSM Architects Ltd, Peter Matinde.

   Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Nishati na Madini, Caroline Musika akikabidhiwa funguo za jengo la hosteli la Chuo cha MRI na Mkandarasi  aliyejenga jengo hilo kutoka kampuni ya Chichi Engineering Construction Ltd, Shaibu Katindi. Wanaoshuhudia ni Msanifu Majengo wa SMMRP, Arch. Joseph Ringo (kulia), Mkuu wa Chuo cha MRI, Mhandisi Oforo Ngowi (kushoto kwa Mkandarasi), Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini na washauri waliosimamia ujenzi wa jengo hilo. 

   Mkuu wa Chuo cha Madini cha Dodoma, Mhandisi Oforo Ngowi (wa pili kutoka kulia) akifafanua jambo wakati wa ukaguzi wa bwalo la wanafunzi. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Nishati na Madini, Caroline Musika akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo chaTehama, Wizara ya Nishati na Madini, Francis Fungameza. Wa kwanza kulia ni Mshauri Mwelekezi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PSM Architects Ltd, Peter Matinde.

   Mkandarasi kutoka kampuni ya Chichi Engineering Construction Ltd, Shaibu Katindi (kulia) akielezea jambo kabla ya kuanza kwa ukaguzi wa jengo la hosteli. Wengine katika picha ni wakaguzi pamoja na washauri waliosimamia ujenzi wa jengo hilo.

   Msanifu Majengo wa SMMRP, Joseph Ringo (mwenye shati jeupe) akifafanua jambo katika kikao na Mkuu wa Chuo cha Madini cha Dodoma, Mhandisi Oforo Ngowi (mbele katikati) mara baada ya kuwasili chuoni hapo. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama, Wizara ya Nishati na Madini, Francis Fungameza na kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Nishati na Madini, Caroline Musika.


   Mshauri Mwelekezi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PSM Architects Ltd, Peter Matinde (kulia) akielezea jambo mara baada ya kufanyika kwa ukaguzi wa jengo la hosteli la MRI. Sambamba nae ni Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini na  Mkandarasi.

   Moja ya chumba cha jengo lililokabidhiwa la hosteli ya wasichana ya Chuo cha Madini (MRI) Dodoma. 

   Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Nishati na Madini, Caroline Musika (kushoto) akiendelea na ukaguzi katika moja ya chumba katika jengo la hosteli. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama, Wizara ya Nishati na Madini, Francis Fungameza.


   Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Nishati na Madini, Caroline Musika (kulia) akiwa sambamba na Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mkandarasi pamoja na baadhi ya washauri waliosimamia ujenzi wakimsikiliza Mshauri Mwelekezi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PSM Architects Ltd, Peter Matinde (hayupo pichani) wakati wa ukaguzi wa jengo la hosteli.

  JENGO LA HOSTELI CHUO CHA MADINI LAKAMILIKA

  Wizara ya Nishati na Madini imepokea jengo la hosteli ya wasichana ya Chuo cha Madini cha Dodoma (MRI) kutoka kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Chichi Engineering Construction Limited katika makabidhiano yaliyofanywa hivi karibuni, mkoani Dodoma mara baada ya ujenzi kukamilika.

  Akizungumza kwa niaba ya Meneja Mradi wa  Usimamizi  Endelevu wa  Rasilimali Madini (SMMRP), Mhandisi Idrisa Yahya, wakati wa makabidhiano hayo Msanifu Majengo (Architect) wa SMMRP, Joseph Ringo alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi huo kutapunguza uhaba wa nafasi za malazi kwa wanafunzi hususan wa kike katika chuo hicho.

  Aidha, alisema kulingana na takwimu za MRI inaonyesha kila mwaka usaili wa wanafunzi unaongezeka na kwa kuwa chuo hicho hakina hosteli za kutosha, inawalazimu wanafunzi wengi kupanga vyumba nje ya chuo jambo ambalo alisema si jema kwa wanafunzi hao.
  “Kila mwaka wanafunzi wanaongezeka, kwahiyo kupitia jengo hili jipya la hosteli ya wasichana nina imani changamoto ya malazi kwao itakuwa imetatuliwa,” alisema.

  Katika makabidhiano hayo, ilielezwa kuwa jengo hilo la hosteli linao uwezo wa kuchukua jumla ya wanafunzi 88.Aidha, mbali na jengo hilo la hosteli, makabidhiano hayo pia yalihusisha bwalo la wanafunzi ambalo likikuwa limekarabatiwa kwa kupanulia pamoja na ofisi ya Mkuu wa Chuo.

  Ringo alieleza kuwa, makabidhiano hayo yanakamilisha Awamu ya Kwanza ya Mradi wa SMMRP kwa chuo hicho na kuongeza kuwa matarajio ya baadaye ni kujenga miundombinu zaidi ili kukidhi mahitaji ya chuo hicho.“Mahitaji ya chuo kuhusiana na majengo ni makubwa kuliko haya yaliyojengwa,” alisema.

  Akizungumzia mikakati ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya mradi wa SMMRP (Additional Financing), Msanifu Ringo alisema hatua zote za kuanza utekelezaji zimeanza.

  “Matarajio yetu ni kuwa malengo yaliyopangwa yatafikiwa kwa muda uliopangwa. Mradi huu umebeba dhima kubwa ya kuhakikisha Watanzania wananufaika zaidi na sekta  ya Madini," alisema.

  Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho cha Madini, Mhandisi Oforo Ngowi, alisema mradi huo wa ukarabati na ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa Chuo, bwalo la wanafunzi na hosteli unao umuhimu wa kipekee katika kuboresha miundombinu pamoja na kuleta maendeleo endelevu ya chuo hicho.

  “Huu ni ukombozi mkubwa sana kwa wanafunzi waliokuwa wanahangaika kutafuta malazi nje ya chuo. Kilichobaki hapa ni kusoma tu”, alisema.
  Mradi huo wa Chuo cha Madini uliokabidhiwa umefadhiliwa na Benki ya Dunia chini ya usimamizi wa SMMRP na ulianza Julai, 2014 na kukamilika mwaka huu 2016 na ilielezwa kwamba umegharimu takriban milioni 997.

  Aidha jengo hilo la hosteli limebuniwa na kampuni ya ubunifu Majengo ya PSM Architects Ltd kwa kushirikiana na Howard Humphreys (T) Ltd na Mas-Q Associates Ltd.
  Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazotekeleza miradi mbalimbali ya sekta ya madini chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia.  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitaka maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo na Mizani, Bibi Magdalena Chuwa (kulia) kuhusu sababu zilizomfanya azuie matumizi ya flow Meter katika kuhakiki kiwango cha mafuta yanayoingia nchini kupitia bandari ya Dar es salaam wakati alipofanya ziara kwenye badari hiyo Februari11, 2016. 

  SERIKALI imeamua kuwasimamisha kazi watendaji wawili kutoka Wakala wa Vipimo nchini (WMA) kuanzia leo ili kupisha uchunguzi wa upotevu wa mafuta bandarini kutokana na zuio la kufunga kwa mita kwa zaidi ya miaka mitano.

  Waliosimamishwa kazi ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo nchini (WMA), Bi. Magdalena Chuwa na Meneja Vipimo Kitengo cha Bandari, Bi. Bernadina Mwijarubi. Bi. Mwijarubi ndiye anashughulikia kitengo cha mafuta bandarini.

  Akitangaza uamuzi huo kwenye kikao cha Makatibu Wakuu kilichofanyika leo (Ijumaa, Februari 12, 2016) ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Adelhelm Meru awaandikie barua za kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi huo.

  “Katibu Mkuu Viwanda, waandikie barua za kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi. Katika kipindi hiki hawatatakiwa kusafiri kwenda popote hadi uchunguzi utakapokamilika. Pia utafute mtu wa kukaimu nafasi hiyo ili kazi ziendelee,” alisema.

  Waziri Mkuu pia amesema ofisi yake itawaandikia barua ofisi ya TAKUKURU na polisi ili wafuatilie suala hilo mara moja na ikithibitika kuwa walihusika hatua rasmi zitachukuliwa na itathibitika hawakuhusika basi watarudishwa.

  Waziri Mkuu pia aliagiza mfumo wa upimaji mafuta kwa kutumia flow meters uendelee kutumika na ule upimaji wa kukadiria uache kutumiwa mara moja.

  Jana (Alhamisi, Februari 11, 2016) Waziri Mkuu alifanya ziara kukagua flow meters za zamani zilizopo Kurasini (Kurasini Oil Jetty) na kisha akatembelea na kukagua flow meters mpya ambazo zinajengwa Kigamboni. Mita hizo zimegharimu dola za marekani milioni 6 (sawa na sh. bilioni 12.96/- za sasa).

  Pia Waziri Mkuu alitembelea sehemu ya kuchukulia mafuta yanayotoka bandarini (TPA Manfold) iliyoko Kigamboni na kukagua mitambo ya kusambazia mafuta kwenye matenki ya mafuta ya kampuni ya TIPER yaliyoko Kigamboni yanayomilikiwa kwa ubia baina ya Serikali na kampuni ya Oryx Energies.

  Katika ziara hiyo ilibainika kuwa Kampuni ya TIPER imejiunganishia bomba la moja kwa moja kutoka kwenye bomba kubwa la mafuta linalotoka bandarini hali iliyomlazimu Waziri Mkuu kuagiza kwamba bomba hilo litolewe kwenye maungio hayo ndani ya mwezi mmoja.

  “Jana niliagiza kuwa bomba hilo ling’olewe. Nimetoa mwezi mmoja ili kurekebisha mfumo huo. Simamieni vizuri na kuhakikisha kuwa na wao pia wanarudi kwenye manfold kama ilivyo kwa wengine,” alisema Waziri Mkuu.

   
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM.
  IJUMAA, FEBRUARI 12, 2016.

  0 0
 • 02/12/16--02:23: Article 20


 • 0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa JOWIKA KASUNGA amewataka waalimu Wilayani Mufindi kujiepusha na masuala ya ulevi, uwasherati sanjari na maneno ya ovyo ili wawe mfano bora kwa wanafunzi wanaowafundisha kwa shabaha ya kuimarisha nidham jambo ambalo litachangia kuongeza ufaulu wilani humo.

  Taarifa ya Ofisi ya habari na mwasiliano kwa umma ya Halmashauri ya wilaya ya Mufindi kwa vyombo vya habari, imebainisha kuwa, Mkuu huyo wa Wlaya ameyasema hayo kwenye kikao maalum cha tadhimini na kutunuku zawadi kwa shule zilizofanya vizuri zaidi kwenye mitihani ya kumaliza elimu ya msingi iliyofanyika mapema mwaka jana ambapo Wilaya ya Mufindi ilipanda kwa aslimia 11 na kushika nafasi ya pili Kimkoa.

  Kasunga ambaye pia ni mwalimu kitaaluma ameongeza kuwa, waalimu wanawajibu wa kulinda hadhi ya uwalimu katika jamii na kuacha vitendo vinavyo dhalilisha tasnia yao kisha akasisitiza kuwa taaluma ya uwalimu itabaki kuwa wito na kufafanua kuwa dhana ya uwalimu ni kama kazi nyingine ituike tu wakati wa kudai maslai bora ya walimu na si kuilinganisha na taaluma nyingine.

  Kwa pande wao baadhi ya waalimu wakuu wa shule za msingi zilizofanya vizuri zaidi na kupandisha ufaulu kutoka aslimia 68. 2 mwaka 2014 mpaka asilimia 80. 3-9 mwalimu JACKSON MKOLA wa shule ya msingi HOLO na Mwalimu EVER MWANJESI shule ya msingi Mjimwema wamesema ushirikiano na na kufanya kazi kwa kujituma ndio chachu ya mafanikio hayo.

  0 0

   Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa,Dominician Mkama(kushoto) na Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino cha jijini Mwanza,Padri Leons Maziku(kulia)pamoja na wanafunzi wa Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino cha jijini Mwanza wakiwaonesha waandishi wa habari(hawapo pichani)baadhi ya vifaa vya michezo,Vilivyotolewa na Vodacom Tanzania kwa ajili ya mashindano ya ligi ya Vyuo vikuu itakayoanza kutimua vumbi jijini humo hivi karibuni.
   Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa,Dominician Mkama(kushoto) akimkabidhi tisheti Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino cha jijini Mwanza,Padri Leons Maziku(kulia)na vifaa mbalimbali vya michezo,Vilivyotolewa msaada na Vodacom Tanzania kwa ajili ya mashindano ya ligi ya Vyuo vikuu itakayotimua vumbi jijini humo hivi karibuni.
   Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino jijini Mwanza,Padri Leons Maziku(kulia)akimfafanulia jambo Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa,Dominician Mkama(kushoto)baada ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali vya michezo chuoni hapo kwa ajili ya mashindano ya ligi ya Vyuo vikuu itakayotimua vumbi hivi karibuni jijini humo.

  Na Mwandishi wetu-Mwanza
  LIGI ya Vyuo Vikuu kutimua vumbi jijini Mwanza
  Ligi ya Vyuo vikuu vilivyopo mjini Mwanza itaanza kutimua vumbi jijini humo hivi karibuni ikiwa ni mkakati wa kuibua vipaji vya wanamichezo wasomi uliobuniwa na Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustine (SAUT) kampasi ya Mwanza.

  Kuanza kwa ligi hiyo kulitangazwa jana na Padre Leons Maziku, Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino Padri Leons Maziku, ambaye pia ni mratibu wa michezo katika Chuo hicho katika hafla ya kupokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.

  “Nashukuru Vodacom kwa kutuunga mkono katika kuendeleza michezo na napenda kuwatangazia wadau wote na wapenda soka kwa ujumla kuwa ligi hii ambayo ina lengo la kuendeleza michezo maandalizi yake yanaendelea na itafanyika katika Chuo hiki cha SAUT na itaanza katika siku za hivi karibuni”.Alisema.

  Akikabidhi msaada wa vifaa hivyo, Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa Dominician Mkama, alisema kuwa Vodacom inayo furaha katika kushiriki kudhamini michezo hiyo ya wasomi kwa kuwa moja ya mkakati wake ni kuendeleza michezo na Sanaa nchini.

  “Vodacom Tanzania tayari tunatambua kuwa sanaa na michezo inaweza kuinua hali ya maisha ya vijana kwa kupunguza tatizo la ajira ndio maana tulipopata ombi la kudhamini mashindano haya tulilifanyia kazi kwa haraka na tunaendelea na mkakati wa kudhamini michezo nchini ikiwemo Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania na mashindano ya kudansi yanayojulikana kama”Dance 100%”.

  Aliwataka vijana popote walipo nchini kuchangamkia fursa za michezo na utamaduni kwa kuwa ni eneo ambalo bado lina nafasi ya kutoa ajira na kuinua maisha yao kama ambavyo tumeshuhudia wachezaji wa michezo mbalimbali na wasanii wana maisha mazuri kutokana na kazi hizi.


  “Baadhi ya sanaa na michezo kama vile kucheza dansi,kuimba nyimbo,kucheza mpira wa miguu,kucheza tenesi,kucheza mpira wa mikono,riadha,mpira wa pete,bila kusahau tasnia ya filamu ambayo wasanii wengi waTanzania wamekuwa na mwamko nayo hivi sasa ni ajira tosha kwa vijana ikifanywa kwa umakini na wadau kuwawezesha washiriki na serikali inaweza kupata mapato kupitia fani hizi”Alisema Mkama.

  0 0
 • 02/12/16--02:38: Article 17


 • 0 0


  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo wa ‘Shika Adabu Yako’ ulioimbwa na Msanii Nay wa Mitego kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili, kashfa, uchochezi, kudhalilisha watu na kuhatarisha amani na utengamano miongoni mwa wasanii na jamii kwa ujumla.


  Sambamba na kuufungia wimbo huo, BASATA litampa karipio kali Msanii huyo na kumwagiza kuacha mara moja kujihusisha kwa namna yoyote na tabia ya kuutangaza wimbo au kuusemea katika vyombo vya habari vinginevyo hatua kali zaidi na za kisheria zitachukuliwa.


  Ieleweke kwamba kwa mujibu wa kifungu cha 4 (1) (j) cha sheria ya BASATA namba 23 ya mwaka 1984, Baraza limepwa mamlaka ya kuratibu na kufuatilia mienendo ya mtu yeyote anayehusika na kazi za Sanaa na kuhakikisha linalinda maadili ya kitaifa miongoni mwa Wasanii wanapokuwa jukwaani au wanapobuni kazi yoyote ya Sanaa.


  Aidha, kifungu cha 4 (2) cha sheria hii kinalipa Baraza nguvu ya kisheria kufanya jambo lolote lile kuliwezesha kufanya majukumu yake kwa faida na ustawi wataifa.Baraza la Sanaa la Taifa limekuwa likipokea simu za maswali na malalamiko kadhaa kutoka kwa waandishi wa habari na wadau wa Sanaa ambao kwa njia moja ama nyingine wameguswa na kuchukizwa na kazi hiyo ambayo si tu inadhalilisha tasnia ya Sanaa bali inawafanya watu makini kuanza kuhoji hadhi ya msanii, weledi na taaluma ya Sanaa kwa ujumla.

  BASATA mara kadhaa limekuwa likikemea na kuchukua hatua kadhaa dhidi ya tabia hii chafu ambayo ilianza kujitokeza kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana wa 2015. Kukemea huku ni kwa msingi mmoja kwamba asili ya tasnia hii ya Sanaa ni kuelimisha jamii, kukosoa pale kunapokuwa na tatizo, kuburudisha na kujenga jamii yenye staha, umoja wa kitaifa, mshikamano na amani.


  Ni wazi wasanii wengi wanafanya kazi zao vizuri, kwa kubuni kazi zenye ubora, zenye kujenga jamii na zaidi zinazoburudisha rika zote kiasi cha kuzifanya zililetee heshima taifa. Kati ya hawa wengi, kuna wachache ambao wanaipaka matope tasnia ya Sanaa na kwa kiasi kikubwa wanaonesha wazi kutokuwa na nia njema.


  Kwa mantiki hii BASATA halitavumilia hawa ‘wasanii’ wachache ambao wanataka kuigeuza tasnia ya Sanaa na wasanii genge la wahuni, wasio na staha, wa kudharaulika  na waliojipanga kuibomoa jamii na kuharibu amani na utulivu uliopo nchini.


  BASATA linapenda kueleza yafuatayo:


  1.    Vyombo vya habari viwe vya kwanza kuchuja maudhui ya kazi yoyote ya Sanaa kabla ya kuingia kwenye mtego wa kuwa mawakala wa uharibifu wa jamii kupitia kucheza kazi chafu za Sanaa. BASATA lilishaziandikia radio zote kuzishauri kuwa na kamati za maudhui ya kazi za Sanaa lakini inashangaza baadhi ya vyombo vya habari vinakuwa vya kwanza kushabikia nyimbo hizo chafu na kuwapa muda mrefu wa mahojiano wasanii hao na baadaye kurudi BASATA kuhoji uhalali wa nyimbo husika. Hii si sawa hata kidogo.


  2.    Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli imejipanga kuwajengea mazingira bora ya utendaji Wasanii wote nchini kupitia kuboresha miundombinu ya Sera, Sheria na Kanuni. Hata hivyo, uwepo wa Wasanii kama hawa unafanya jamii kuhoji hadhi ya wasanii, nafasi yao katika jamii na kwa maana hiyo kukatisha tamaa juhudi za kuipa msukumo sekta hii maana wadau wakuu ambao ni wasanii wanaanza kuoneasha kuwa mawakala wa uharibifu wa jamii.


  3.    BASATA linawataka wasanii kujiuliza mara mbili kabla ya kubuni kazi zao za Sanaa. Wafikirie wazazi, ndugu, jamaa na marafiki zao watazipokeaje? Wavae nafasi ya wale wanaowatukana na kuwadhalilisha, Waelewe kwamba Sanaa si uwanja wa kutusi na kudhalilisha watu hata kidogo. Ikitokea wale wanaotukanwa na kudhalilishwa kughafilika Sanaa itakuwa uwanja wa vita. Hili halikubaliki.


  4.    Tunafahamu kuna wasanii wamekuwa wakifanya hivyo makusudi kutafuta ‘umaarufu uchwara’ ambao wanadhani utakuja kutokana na kuzungumziwa sana. Tunapenda kusema wazi kwamba umaarufu hauji kwa upuuzi wa namna hiyo unakuja kwa msanii mwenyewe kujiheshimu, kujituma, kubuni kazi bora na zenye kulifahamu vema soko la ndani na la kimataifa.

  SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI


  Godfrey L. Mngereza


  KATIBU MTENDAJI, BASATA


  0 0


  0 0

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. 

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akielezea jambo alipotembelewa na Uongozi wa TBL na Excutive Solution ambao ni wadhamini na waratibu wa Mbio za Kilimanjaro Marthon leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni  Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin na kushoto ni Mkurugenzi wa Masuala ya Ushirikiano Bibi. Georgia Mutagahywa.

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akifurahia jambo alipotembelewa na Uongozi wa TBL na Excutive Solution ambao ni wadhamini na waratibu wa Mbio za Kilimanjaro Marthon leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia kwa Waziri ni  Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin, Mkurugenzi wa Masuala ya Ushirikiano Bibi. Georgia Mutagahywa na Mkurugenzi Mkuu wa Excutive Solution na Mshauri wa Mahusiano wa TBL Bw. Aggrey Marealle.

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Excutive Solution na Mshauri wa Mahusiano wa TBL Bw. Aggrey Marealle NA Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group Bibi. Kushilla Thomas (wapili kutoka kulia).
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akikabidhiwa zawadi kutoka TBL kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin (kushoto) kupitia Bia yake ya Kilimanjaro Lageralipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group Bibi. Kushilla Thomas (wapili kutoka kulia) na Meneja Masuala ya Nje na Mawasiliano Bibi. Emma Oriyo.Picha Zote na: Frank Shija, WHUSM.


  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya Kilimanjaro Marathoni yatakayofanyika tarehe 28 Februari kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.


  Hayo yamebainisha na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Executive Solution ambayo ndio waratibu wa mbio hizo Bw. Aggrey Marealle walipotembelea ofisini kwa Waziri leo jijini Dar es Salaam.“Mbio za Kili Marathon zinatarajia kufanyika tarehe 28 mwezi huu katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ambapo mgeni rasmi atakuwa Mhe. Nape Moses Nnauye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo”. Alisema Marealle.

  Marealle alisemakuwa Mbio hizo  zitakuwa katika makundi manne ambayo ni mbio za Kilomita 42 ambazo ndiyo marathoni yenyewe inayothaminiwa na TBL kupitia bia ya Kilimanjaro,zingine ni Nusu Marathon za kilomita 21 zinazodhaminiwa na Tigo,mbio za kilomita 10 zinazowashirikisha walemavu wanaotumia Baiskeli za matairi matatu na Viti vya matairi zinazodhaminiwa na kampuni ya mafuta ya Gapco na mbio zinginge ni za kilomita 5 ambazo zinadhaminiwa na TBL kupitia kinywajji cha Grand Malt


  Aliongeza katika mbio hizo washindi kumi kila kundi watapewa zawadi ambapo mshindi wa kwanza kwa mwanaume na mwanamke katika mbio za kilomita 42 watapatiwa zawadi ya shilingi milioni nne kila mmoja.


  Aidha alisema kuwa zaidi ya washiriki 7000 wanakadiriwa kushiriki mbio hizo huku kati yao takribani washiriki 1000 watatoka nje ya nchi.

  Kilimanjaro Marathon inatimiza miaka 14 tokea kuanzishwa kwake ambapo waandaji wa mashindano hayo ni Kampuni ya Wild Frontiers ya Afrika Kusini na kuratibiwa na Executive Solutions Ltd ya Tanzania na mdhamini mkuu wa mbio hizo ni Kampuni ya Bia TBL kupitia Bia ya Kilimanjaro Lager.


older | 1 | .... | 762 | 763 | (Page 764) | 765 | 766 | .... | 1897 | newer