Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 764 | 765 | (Page 766) | 767 | 768 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin (kushoto) akikabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kwa maktaba kuu ya Zanzibar kwa Mkurugenzi wa Huduma za Maktaba Zanzibar, Bi Sichana Haji Foum (kulia). Wanaotazama ni kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Bwana Abdallah Mzee na upande wa 1.    kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Huduma za Maktaba Zanzibar, Suleiman Yahya.

  Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin (kushoto) akikabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kwa maktaba kuu ya Zanzibar kwa Mkurugenzi wa Huduma za Maktaba Zanzibar, Bi Sichana Haji Foum.
  Mkurugenzi wa Huduma za Maktaba Zanzibar, Bi Sichana Haji Foum (kulia) akiwaonyesha baadhi ya vitabu vya Maktaba Kuu ya Zanzibar, Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Bwana Abdallah Mzee (katikati) baada ya kampuni ya Zantel kukabidhi msaada wa shilingi milioni 10 kwa ajili ya ununuzi wa vitabu vya maktaba kuu ya Zanzibar.

    Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi msaada wa shilingi milioni 10 kwa maktaba kuu ya Zanzibar. kushoto Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Abdalla Mzee. 
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Bwana Abdallah Mzee akiishukuru kampuni ya Zantel baada ya kupokea msaada wa shilingi milioni 10 kwa ajili ya ununuzi wa vitabu vya maktaba kuu ya Zanzibar. kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin

  Mkurugenzi wa Huduma za Maktaba Zanzibar, Bi Sichana Haji Foum (kulia) akiwaonyesha baadhi ya vitabu vya Maktaba Kuu ya Zanzibar, Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Bwana Abdallah Mzee (katikati) baada ya kampuni ya Zantel kukabidhi msaada wa shilingi milioni 10 kwa ajili ya ununuzi wa vitabu vya maktaba kuu ya Zanzibar.

  Mkurugenzi wa Huduma za Maktaba Zanzibar, Bi Sichana Haji Foum (kulia) akiwaonyesha baadhi ya vitabu vya Maktaba Kuu ya Zanzibar, Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Bwana Abdallah Mzee (katikati) baada ya kampuni ya Zantel kukabidhi msaada wa shilingi milioni 10 kwa ajili ya ununuzi wa vitabu vya maktaba kuu ya Zanzibar.

  Mkurugenzi wa Huduma za Maktaba Zanzibar, Bi Sichana Haji Foum (kulia) akiwaonyesha baadhi ya Komputa za Maktaba Kuu ya Zanzibar, Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin, wakati wa kutembela maktaba hiyo baada ya hafla ya kukabidhi msaada wa shilingi milioni 10 kwa ajili ya ununuzi wa vitabu vya maktaba kuu ya Zanzibar.

  Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot
  Zanzinews.com. 

  0 0

  Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla amefanya ziara, Februari 12, 2016 katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Nyanda za juu kusini- Mbeya, na kutoa maagizo mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa mashine CT-Scan ndani ya siku 60 huku akibainisha kuwa endapo watazembea basi watawachukulia hatua kali na kuwajibishwa watendaji na uongozi wa Hospitali hiyo.

  Dk. Kigwangalla alifika hospitalini hapo majira ya saa tisa alasiri na kutembelea idara mbalimbali za hospitali hiyo kuona jinsi ya ufanyaji kazi ambapo ndipo alipobaini ukosefu wa mashine hiyo ya CT-Scan pamoja na vifaa vingine muhimu ambavyo alibainisha kuwa hata uongozi wa Hospitali hiyo walikuwa na uwezo wa kuvinunua bila kutegemea Serikali.

  Baadhi ya idara ambazo, Dk. Kingwangalla alitembelea ni pamoja na kitengo cha kutolea huduma kwa wagonjwa (OPD), Kitengo cha upasuaji, wodi ya upasuaji, duka la dawa la hospitali hiyo, wodi ya wanawake, wodi ya wanaume, watoto na kitengo cha Maabara ambapo kisha alipata kuongea na wafanyakazi pamoja na uongozi mzima wa Hospitali.

  Dk.Kigwangalla alitoa wasaha mwingi kusikiliza kero za wafanyakazi hao kuongea lile linalowakabili bila kuogopa ili aweze kujua matatizo na changamoto zinazowakabili.

  "Hospitali kubwa kama hii hapa Mbeya na wataalam wote mlionao mnashindwa kufanya biashara!, Mnategemea tu Serikali? lini mtakuwa na CT-scan kwa upande wenu? wakati mnaingiza Milioni 500 kwa mwezi?" alihoji Dk. Kigwangalla.Dk.Kigwangalla aliwaambia uongozi wa hospitali hiyo ina fursa na uwezo wa kufanya jambo kubwa kwani pia ina uwezo hata wa kukopa fedha kutoka mashirika ya bima ya afya.

  Aidha, Dk Kigwangalla amewataka uongozi wa Hospitali hiyo kuwa wabunifu katika uendeshaji wao ikiwemo kutengeneza jengo la kisasa la matibabu ya kulipia, kujenga nyumba za wafanyakazi ambapo amewapa mikakati hiyo imeanza na pindi atakaporejea tena hospitali hiyo.

  Imeandaliwa na Andrew Chale, modewjiblog, Mbeya
  Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akisisitiza suala la Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Nyanda za juu kusini- Mbeya kununua mashine ya CT-scan ndani ya siku 60, huku akiahidi kuwachukulia hatua kali ya kuwawajibisha watendaji watakaozembea katika hilo.
  Baadhi ya wafanyakazi na madaktari wa hospitali hiyo wakifuatilia mkutano huo wakati Naibu Waziri Dk.Kigwangalla (hayupo pichani) wakati wa alipofanya ziara Februari 12,2016. Wafanyakazi hao waliweza kutoa maoni yao mbalimbali ikiwemo suala la motisha na uboreshaji wa mishahara pamoja na ukosefu wa vitendea kazi ikiwemo kitengo cha maabara.
  Mmoja wa madaktari wa hospitali hiyo ya rufaa Mbeya akiuliza akitoa maoni yake kwa Naibu Waziri Dk.Kigwangalla.
  Kaimu Mkurugenzi wa hospitali ya Kanda ya rufaa Mbeya, Thomas Isidori akitoa fursa kwa Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla (kulia) kuzungumza na wafanyakazi katika mkutano wake huo. 
  Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipita katika moja ya maeneo ya hospitali hiyo ya Kanda ya rufaa Mbeya sambamba na wenyeji wake...

  Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akitazama moja ya kipimo cha mgonjwa ambacho hata hivyo ilieleza kuwa kilipimwa nje ya Hospitali hiyo na kuletwa hapo ambapo alipotaka kujua kwa nini imekuwa hivyo kwa hospitali kubwa kama hiyo alielezwa kuwa hawana mashine ya CT-Scan ndipo alipoutaka uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha mashine hiyo inapatikana ndani ya siku 60 kuanzia hiyo Februari 12.

  Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipata maelezo ya moja ya mashine ndani ya maabara ya hospitali hiyo ya Kanda ya rufaa Mbeya. Hata hivyo ameelezwa mashine hiyo ni ya zamani sana hivyo ufanisi wake ni mdogo huku wakimweleza kuwa inatakiwa wapatiwe mpya ilikuendana na kasi.

  Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akimjulia hali Mtoto Edger Emmanuel (2) anayepatiwa matibabu ya mguu wake katika wodi hiyo ya watoto kitengo cha upasuaji.

  Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla na Kaimu Mkurugenzi, Thomas Isidori wakimjulia hali Mzee Lazaro Mwakapunga aliyelazwa hospitalini hapo.

  Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipatiwa maelezo namna ya mfuko wa malipo wa ki-elektroniki unaotumiwa hospitalini hapo na Kaimu Mkurugenzi, Thomas Isidori. Hospiatli hiyo inatumia mfumo huo ambapo imeweza kufanikiwa katika ukusanyaji wake wa mapato.

  Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akipokelewa na Katibu wa Hospitali hiyo, Maryam Msalale wakati wa kuwasili katika ziara hiyo. (Picha zote na Andrew Chale, modewjiblog, Mbeya).

  0 0

  Dk. Deo Mtasiwa Naibu Katibu Mkuu wa Afya TAMISEMI akizungumza katika mkutano wa Afya Moja ulioshirikisha wadau mbalimbali wa Afya ya Mifugo, Binadamu na Mimea kutoka katika vyuo mbalimbali hapa nchini.(Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog).
  Mhadhiri na mtafiti mtoa huduma katika chuo kikuu cha Sokoine, Profesa Robson Mdogera akisoma risala mbele ya mgeni rasmi kuhusu mafanikio pamoja na changamoto wanazozipata kwenye mango wa Afya Moja wanapotaka kufanya kazi kwa pamoja kati ya madaktari wa afya ya mifugo, binadamu pamoja na aafya ya Mazingira.
  Dk. Kitua kutoka SACIDS akizungumza jambo wakati wa mkutano wa Wataalamu wa Afya kutoka vyuo mbalimbali hapa nchi ili kujadili nikwa jinsi gani wanaweza kushirikiana katika kufanya kazi bila kuangalia kuegemea upande wowote wa Afya.DSC_0017DSC_0008Profesa Mamuya kutoka MUHAS akiwasilisha mada kwenye mkutano uliowashirikisha wataalamu mbalimbali wa afya ya mifugo, binadamu pamoja na afya ya mazigira uliofanyika Bagamoyo.
  DSC_0023Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine kitengo cha Tiba ya Afya ya Jamii Dk. Helena Ngowi akiwasilisha mada mbele wataalamu mbalimbali wa Afya kutoka kwenye vyoa vya hapa nchini waliokuwa wanajidilini kwa jinsi gani wanaweza kushirikiana katika kufanya kazi.
  DSC_0038Profesa Rudovick Kazwala kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) akichangia mada kwenye mkutano wa wadau wa Afya moja uliowashirikisha wataalamu mbalimbali wa Afya kutoka vyuo mbalimbali vya Tanzania.
  DSC_0044Mhadhiri na mtafiti mtoa huduma katika Chuo Kikuu cha Sokoine, Profesa Robson Mdogera akizungumza jambo walipokuwa wanajadili mpango kazi wa pamoja ili kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kufanya bila kubagua upande wowote.
  DSC_0134Profesa Mark Rweyemamu akizungumza jambo wakati wa kuwasilisha mpango kazi wao ili kuweza kuutumia kwa pamoja na kuachana na mpango wa kila kundi.
  Makundi ya wataalamu mbalimbali wa Afya Moja wakijadili pamoja na kubuni mpango utakaowasaidia wataalamu wa Afya ya Mifugo, Binadamu pamoja na Mazingira kufanya kazi kwa pamoja yaani Afya Moja.
  DSC_0205Profesa Rudovick Kazwala akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasimi aliyefika kufunga mkutano huo.
  DSC_0211Picha ya pamoja.

  Taasisi za SACIDS na  OHCEA wameandaa mkutano uliowakutanisha wataalamu mbalimbali wenye ujuzi tofauti wa Afya hasa Afya ya Mifugo, Afya ya Binadamu pamoja na Afya ya Mazingira kutoka kwenye vyuo mbalimbali vya hapa Tanzania.
  Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuweza kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kufanya kazi kwa pamoja bila kubagua upande wowote ili kutatua tatizo lililokuwepo kwa miaka mingi hapa nchini Tanzania hasa pale yanapotokea magonjwa yanayowapata mifugo pamoja na binadamu.
  Mgeni rasmi aliyefika katika mkutano huo alikuwa Dk. Deo Mtasiwa ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Afya TAMISEMI ambaye alisema kuwa serikali iko pamoja na wataalamu wa Afya ya Mifugo, Afya ya Binadamu pamoja na Afya ya Mimea.
  Pia amesema mpango ulioandaliwa na wataalamu hao wa afya wa kufanya kazi kwa pamoja utachukuliwa na serikali ili kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kuutumia ili ikitokea ugonjwa kwa mifugo kwenda kwa binadamu iwe ni rahisi kutatua tatizo hilo.
  "Magonjwa ya kuambukia yanayotoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu yanaleta changamoto kubwa sana lakini kwa sababu umekuwepo mpango wa Afya mmoja basi utatusaidia na pia tutawatumia wataalamu bila kuangalia yuko kundi gani," alisema Naibu Katibu Mkuu
  Pia alisistiza kuwa umoja wao ndio mafanikio yao kwani wasipoungana na kufanya kazi kwa pamoja itakuwa ni vigumu kufikia yale malengo waliyojiwekea. "Napenda kuona mnatoa elimu katika jamii kuhusu magonjwa ya kuambukizwa ambayo yanatoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu ili kuweza kunusuru maisha ya wananchi walio wengi.
  Pia alisema serikali iko tayari kuwasaidia kwa pale watakapohitaji msaada wao kwa sababu afya ni kitu cha msingi kwa wanyama pamoja na binadamu na kuongeza atashirikiana bega kwa bega na wizara kama vile Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na Wizara ya Kilimo na Ufugaji ili kuweza kufikisha kile walichomtuma kama mtendaji wa serikali.
  Pia ameshukuru taasisi zilizofanikisha mkutano huo ambazo ni OHCEA na SACIDS zimetengeneza mipango mizuri kwa wataalamu wa afya na kuwaleta karibu kwa ajili ya kushirikiana.
  Akizungumza Profesa Robson Mdogera ambaye ni mhadhiri na mtafiti mtoa huduma katika Chuo Kikuu cha Sokoine amesema mkutano huu umekuja wakati muhafaka kwani kumekuwepo tatizo kubwa la kutoshirikiana katika hali zote.
  “Huu mpango waliokuja nao wa Afya moja unaweza kuleta mafanikio makubwa maana kuna viwatilifu vinavyowekwa kwenye mifugo au mazao ili kukinga magonjwa hivyo kunapelekea viwatilifu hivyo kuliwa na binadamu bila kujua na kupeleka adhari kubwa katika mwili wa binadamu. Hivyo kunahitaji kuwa na ushirikiano katika nyanja zote za afya ili kuweza kutatua tatizo pale tu linapotokea,” alisema Prof. Mdogera.

  0 0

  Dk. Mahadev, mshauri mwandamizi wa radiotherapia kutoka Hospitali za Apollo.


  Na Mwandishi wetu,
  Matibabu ya kawaida ya saratani huwa yanahusisha upasuaji, radiotherapia na kemotherapia. Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa kwenye tiba kwa njia hizo mbili. Katika hatua za mwanzo, saratani huwa ni ugonjwa unaotibika kwa dozi moja mahususi lakini saratani iliyosambaa au kukomaa inahitaji dozi zaidi ya moja katika kuitibu. Radiotherapia, ni tiba iliyopo katika mfumo maalumu unaoleta matokeo katika mwili mzima.

  Dk. Mahadev , mshauri mwandamizi wa tiba ya uvimbe kwa mionzi kutoka hospitali za Apollo anaeleza kwamba radiotherapia inahusisha chembe chembe ndogo za mionzi ya gamma au X-rays katika kutibu saratani na hata matatizo ambayo sio ya saratani pia. Mionzi hii imegawanyika katika ile mionzi ya mbali (external radiotherapy) ambayo chanzo cha mionzi kinakuwa mbali na mwili na ile mionzi ya karibu ambayo mionzi inawekwa karibu ili kuchoma sehemu yenye uvimbe peke yake.

  Mionzi ya karibu ni aina nzuri ya kutibu saratani ila kwa uvimbe unaoonekana kirahisi na unaofikika. Hivyo saratani iliyopo mdomoni, saratani ya tezi dume, saratani ya kizazi zote zinaweza kutibiwa kwa mionzi ya karibu peke yake. Faida kubwa ya mionzi ya karibu ukilinganisha na mionzi ya mbali ni kwamba mionzi ya karibu inahusisha uponyaji ndani ya muda mfupi (siku 3-5) wakati mionzi ya mbali inachukua hadi wiki 7 hadi 8. Uvimbe wowote uliokomaa unahitaji mionzi ya mbali.

  Lengo kubwa la matumizi ya radiotherapia ni kuchoma sehemu pekee yenye uvimbe na kuepuka kuchoma sehemu nyingine za pembeni katika mwili. Mionzi ya mbali inahistoria ndefu kutoka enzi za cobalt kwenda kwenye hali ya teknolojia ya juu ya kutoa tiba ya mionzi kwa moduli ya hali ya juu (IMRT), mionzi kwa kuongozwa na picha (IGRT), upasuaji kwa njia ya sterio (SRS) na njia ya sterio kwa mionzi mwilini (SBRT). Mashine yenye program maalumu kwa ajili ya upasuaji (Cyberknife robotic radiosurgery ) ni njia bora zaidi katika kufanya SRS na SBRT, aliongeza Dk. Mahadev  kuwa teknolojia hizi zinapatikana katika hospitali za Apollo.

  Umuhimu pekee wa kutumia mashine yenye program maalumu kwa ajili ya upasuaji ni kukata milimeta sahihi na uponyaji katika siku chache. Ni tiba ya mgonjwa bila kulazwa na hahihitaji nusu kaputi katika kufanyika. Hivyo saratani ya mapafu na tezi dume inaweza kutibika ndani ya siku 3 hadi 5, wakati muda wake kawaida huchukua wiki 7-8 kwa uangalizi wa karibu. Mashine yenye program maalumu kwa ajili ya upasuaji ni muhimu katika kutibu uvimbe, ambao hauwezekani kufanyiwa operesheni kwa sababu ya eneo ilipo aidha katika ubongo au uti wa mgongo. Inatumika kutibu magonjwa kama meningiomas, uvimbe katika pituitary, mishipa ya ateri iliyodhofika (AVM) na madhara kutokana na saratani katika ubongo, mapafu na ini.

  Dk. Mahadev  anaelezea njia bora ya kutumia radiotherapia ni kwa protoni. Faida kubwa ya protoni ukilinganisha na njia ya kawaida ni katika kutoa mionzi kwa umakini zaidi hasa kuchoma sehemu yenye uvimbe peke yake. Hiyo inapelekea matokeo mazuri na madhaifu machache. Kutokana na kutokuwa na dozi zaidi katika kutibu uvimbe, ni vyema kudhibiti uvimbe ukiwa katika hatua za mwanzo ambapo huwa tunaogopaga madhara ya kutumia mionzi. Matumizi ya protoni ni mapinduzi katika tiba ya saratani. Saratani ya kichwa na shingo, mapafu na tezi dume huwa zinatibika kirahisi kabisa kwa mionzi hii ya protoni.

  Baadhi ya saratani zinazotibika kwa upasuaji, inaweza kutibika kirahisi kwa radiotherapia tu. Ikiwa hatua ya mwanzo, saratani ya mdomoni, mfumo wa chakula, tezi dume, zaweza tibiwa kwa mionzi peke yake. Faida katika kutibu aina hizi za saratani ni kuwa zipo sehemu zinazofikika. Mgonjwa anaweza kuwa na ogani inayofanya kazi vizuri hivyo kuona ubora wa maisha. Saratani nyingi zilizokomaa huwa zinahitaji kwa pamoja upasuaji, radiotherapia na kemotherapia katika kuitibu ambazo zote zinapatikana katika teknolojia ya juu kutoka hospitali za Apollo.

  Tumetoka kwenye enzi za kufanya operesheni kubwa na kuingia kwenye utunzaji wa ogani zetu kwa msaada wa teknolojia ya mionzi bora na dawa mpya na bora za tiba kwa kemotherapia. Kwa mfano saratani ya matiti ndio saratani inayoongoza kwa wanawake duniani. Hapo kabla, titi lote lilikuwa linakatwa. Ila kwa sasa wagonjwa wengi wanabaki na matiti yao salama kwa upasuaji mdogo tu unaofanywa.

  Tiba hiyo ndogo katika tiba inawasaidia wanawake kuwa na saikolojia chanya inayowafanya wapone haraka pia. Kichwa na shingo, mfumo wa chakula, saratani ya tezi dume na sehemu nyingine ambazo huwa kutokuondoa ogani ni kitu cha muhimu katika tiba.
  Radiotherapia ni mbadaka zuri kuepuka upasuaji au kemotherapia katika kupambana na saratani. Mabadiliko makubwa katika teknolojia na matumizi ya kompyuta yamewezesha utoaji bora wa huduma ya tiba ya mionzi kwa madhara kidogo sana.  Kuhusu Hospitali ya Apollo

  Hospitali za Apollo ni za kwanza katika eneo Asia Pacific kutoa huduma za upasuaji kwa kutumia mfumo huu wa Robot, ambayo ni aina ya upasuaji isiyokuwa na madhara. Taasisi ya upasuaji kutumia Robot iliyopo hospitalini hapo wamejitoa kipekee katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa.

  Taasisi ina wataalamu waliobobea kwenye mafunzo ya upasuaji, upendo katika utoaji wa huduma vifaa vya matibabu vya kisasa vinavyolenga kutoa uzoefu bora kwa mgonjwa. Vifaa hivyo ni pamoja na vifaa Robot ya Da Vinci inayotumika katika upasuaji.

  Mfumo huu wa upasuaji hutumika katika teknolojia ya upasuaji wa magonjwa yanayohusiana na mfumo wa mkojo (Urology), magonjwa ya wanawake (Gynaecology), moyo, utumbo, na magonjwa ya watoto na matatizo ya uti wa mgongo.

  0 0


  0 0  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  IDARA YA HABARI - MAELEZO
  TAARIFA KWA UMMA


  Serikali imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa iliyotolewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu  (THRDC) na kusambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuhusu siku 100 za utawala wa Rais Magufuli kuwa zimekandamiza Uhuru wa Habari nchini kwa kulifuta  Gazeti la Mawio.

  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inasisisitiza kwamba hatua iliyochukuliwa dhidi ya gazeti la Mawio ni Sahihi na lilistahili adhabu hiyo. Aidha, taratibu zote za kulifuta Gazeti hilo zilifuatwa ikiwa ni pamoja na Mhariri  Mtendaji wa Gazeti hilo kupewa nafasi ya kujitetea.

  Hatua ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRCD) kutaka kujenga taswira kwamba Gazeti la MAWIO lilionewa na kwamba halikupewa nafasi ya kujieleza na kujitetea si sahihi na ni kuupotosha umma.

  Serikali inazitaka taasisi zinazo jishughulisha na Utetezi wa Haki za Binadamu kuacha kufanya tafsiri potofu kwa Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976 na Sheria nyingine za nchi. Hakuna Uhuru usio na Mipaka na Staha.

   Serikali inautaarifu Umma kuwa hatua ya kutunga Sheria ya Huduma za Habari (Media Service Bill) na Haki ya kupata tarifa inaendelea vizuri na Wizara zinaendelea kupokea maoni ya kuboresha Miswaada hiyo.

  Muswaada wa Haki ya Kupata Taarifa unasimaiwa na Wizara ya Katiba na Sheria, Muswaada huo unawahusu watu wote. Muswaada wa Huduma za Habari ni mahsusi kwa Wadau wote wa tasnia ya Habari.

  Serikali inatoa wito kwa wadau wote wa sekta ya habari kuchangia kuboresha miswaada hiyo. Aidha, inawataka Wanahabari wawe mstari wa mbele katika kuchangia uboreshaji wa Muswaada wa Huduma za Habari  badala ya kuwaachia wanataaluma nyingine kutoa maoni na maelekezo katika muswaada huo.

  Serikali inawakumbusha wananchi kwamba Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 itaendelea kutumika mpaka pale Sheria mpya itakapopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Katika hatua nyingine Serikali inapenda kuwataarifu wananchi kuwa suala la urushaji wa matangazo ya “live” kupitia  Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) lilisha tolewa ufafanuzi na Viongozi Wakuu wa Serikali. Hivyo mjadala huo ulihitimishwa.

   IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI (MAELEZO)
  13/FEBRUARI/2016.

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe, Ummy Mwalimu akitoa shukurani za dhati kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli mbele ya Mufti Mkuu wa Tanzania pamoja na baadhi ya Viongozi waliohudhuria mkutano wakati siku ya kuruhusiwa kurejea nyumbani kwa Mufti huyo, leo Jijini Dar es Salaam.
  Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally (Kushoto) akitoa shukurani za mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe, Ummy Mwalimu pamoja na baadhi ya Viongozi waliohudhuria mkutano wakati siku ya kuruhusiwa kurejea nyumbani kwa Mufti huyo, leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Suleiman Lolila.
  Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Suleiman Lolila akisoma taarifa ya shukurani toka kwa Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally mara baada ya kupata matibabu na kuruhusiwa kurejea nyumbani toka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili-Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete leo Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Vyama vya Siasa, Viongozi wa Taasisi mbalimbali, Masheikh, Madaktari pamoja na Waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano Hospitalini hapo wakifuatilia taarifa toka kwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally (hayupo pichani) leo katika Ukumbi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo Jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Benedict Liwenga)


  Mufti Mkuu wa Tanzania asifia huduma bora za Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.


  Na Benedict Liwenga-Maelezo.

  MUFTI Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally amepongeza huduma bora alizopatiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Kitengo cha Taasisi ya Moyo cha Jakaya Mrisho Kikwete mara bada ya kupata ruhusa ya kurejea nyumbani.

  Pongezi hizo amezitoa leo Jijini Dar es Salaam mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Viongozi wengine wa Serikali, Viongozi wa Vyama vya Siasa, Viongozi wa Taasisi mbalimbali, Masheikh, Madaktari pamoja na Waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano Hospitalini hapo.

  Mufti Zubeiry ameeleza kuwa, yeye pamoja na Familia yake pamoja na Baraza la Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) wanatoa shukurani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli kwa msaada wa kumwezesha kupata matibabu hospitalini hapo pamoja na watu wengine waliofanikisha matibabu hayo kwa namna moja au nyingine.

  Amesema kuwa Hospitali hiyo ina Mabingwa wazuri waliobobea wenye uwezo na endapo wakitumika vizuri hali ya huduma ya afya hospitalini hapo itavutia kama zile zilizoko nje ya nchi, pia ameiomba Serikali kuona umuhimu wa kuangalia suala la Madakati, vitendea kazi, pamoja na Wauguzi hospitalini hapo ili huduma bora zizidi kutolewa.‘’Namuomba Rais wetu kuitazama Hospitali hii chini ya Wizara ya Afya pamoja na mabingwa wetu tulionao kwani hapa ni gereji ya binadamu hivyo panapaswa kuangaliwa kwa makini’’, alisema Mufti Zubeiry.

  Katika hatua nyimngine, Mufti Zubeiry amewashukuru Marais Wastaafu wa Serikali ya Tanzania akiwemo Mhe. Benjamin William Mkapa pamoja na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufika kumfariji kipindi yuko mgonjwa.‘’Pia ninawashukuru Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na familia yake, Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Naibu Spika Turia Ackson kwa moyo wao wa kuja kunifariji’’, alisema Mufti.

  Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ameeleza kuwa, kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, John Pombe Joseph Magufuli amezipokea shukurani hizo toka kwa Mufti Mkuu wa Tanzania kwa kupona na kuruhusiwa hospitalini hapo na pia amewashukuru Madaktari bingwa na Wauguzi wote walioshiriki katika kumtibu Mufti huyo.

  ‘’Mmetupa changamoto sisi ya kutaka kufanya vizuri zaidi, ni matarajio yetu sisi kama Serikali kuona viongozi wote wa Tanzania akiwemo Mufti Mkuu na wengine wanatibiwa katika Hospitali yetu ya Taifa ya Muhimbili, hivyo mmetusaidia sana kutuma ujumbe kwa Watanzania kuwa tunaweza kutumia hospitali zetu katika kuwatibu viongozi wetu nchini’’, alisema Mhe. Ummy.

  Almeongeza kuwa, Wizara ya Afya itaendelea kujitahidi kuboresha huduma za afya hospitalini hapo, ikiwemo suala la Wataalamu, vifaa vya tiba pamoja na kuongeza hamasa kwa Watanzania ya kutibiwa hospitalini hapo kwakuwa Mufti pamoja na baadhi ya na viongozi wengine ambao wamewahi kutibiwa hospitalini hapo wameonyesha moyo wa kuboresha zaidi huduma hospitalini hapo.

  0 0


  Chief Executive Officer, (CEO), with UTT-Project and Infrastructure Development PLC, Dr.Gration Kamugisha, (First-R), speaks during a joint news conference prior to the first annual general meeting of UTT promoted companies at Julius Nyerere International Convention Centre in Dar es Salaam Saturday February 14, 2016. Other sister companies include UTT-AMIS, and UTT-Microfinance. Others from left to right is UTT Microfinance’s CEO James Washima, UTT-AMIS’ CEO, Dr. Hamis Kibola, ane Finance Management Officer from the Office of Treasury Registrar, Edgar Rugaimukamu. (Photos:K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

  Chief Executive Officer with UTT-AMIS, Dr. Hamis Kibola, display the reports of UTT-PID, and UTT-Microfinance, during a joint news conference prior to the first annual general meeting of UTT-Promoted companies at Julius Nyerere International Convention Centre in Dar es Salaam, Saturday February 14, 2016
  UTT-PID's Acting Board Chairperson, Elipina Mlaki, walk- through the meeting agenda
   Participant reads UTT-PID's  annual report for the year ended 30th June 2014.
   Cross section of participants
   Close follow-up
   Chairman of the Boardof Directors of UTT-Microfinance, Ambassador Fadhili Mbaga, chair the session
   Chairman of UTT-AMIS, Professor Joseph Kuzilwa, speaks during the opening session of the meeting
   Chief Executive Officer with UTT-PID, Dr. Gration Kamugisha, speaks during a news conference prior to the AGM
   UTT-PID Head of Lega Unit, Tuzo Mpiluka, (L), in tet-atet with the acting Head of Corporate Affairs, Eugenia Simon
   Head of Procurement Management Unit, of UTT-PID,  Milton Shango, (L), in tet-atet with the Head of Legal Unit of UTT-PID, Tuzo Mpiluka
   Finance Management Officer from the Office of Treasury Registrar, Edgar Rugaimukamu, speaks on behalf of Treasure Registrar,
   UTT-PID's Director, Chairperson of Investment Committee, Janet Mmari makes his opinions
   Chief Operations Officer of UTT-AMIS, Simon Migangala, explains on the issues raised by participants towards his company's  report
   Chief Executive Officer with TUT-Microfinance, James Washima, peruses before taking the floor.
   UTT-PID's CEO, Dr. Gration Kamugisha addresses the audience
   Chief Executive Officer with TUT-Microfinance, James Washima,(L), speaks
   Cross section of senior staff
  UTT-PID's Head of Operations, Alexsandar Nikolik (L), and UTT-PID Senior Officer, listen attentively to the speeches

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Meck Sadik wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee tayari kwa kuongea na wazee wa mkoa wa Dar es salaam leo ambapo mkutano huo pia ulihudhuriwa na Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.

  Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amehudhuria katika mkutano huo ambapo alionekana mtu mwenye kufurahia hotuba hiyo, Kamera ya Fullshangwe ilimnasa askofu huyo maarufu kwa matamshi yake ya "Wakale Malimao" akiwa na tabasam kubwa akionekana kufurahia kuhudhuria kwake katika mkutano huo.

  Mwanzo wakati alipofika ukumbini hapo alikuta ratiba inaendelea hivyo ilibidi akae viti vya nyuma lakini Shekh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhadi Mussa Salim alimpigia simu na kumwambia aende mbele akakae pamoja na viongozi wenzake wa dini na ndipo alipoenda kukaa eneo hilo.(PICHA NA JOHN BUKUKU- FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
  Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ukiwasili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo wakati alipoongea na wazee wa mkoa wa Dar es salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Wazee wa mkoa wa Dar es salaam mzee Hemed Mkali kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa wa dar es salaam Mh. Raymond Mushi na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhan Madabida.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa wazee wa mkoa wa Dar es salaam wa zamani Mzee Idd Simba, Kulia ni mfanyabiashara Abdullah Mohamed.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa na Mke wa Rais Mama Janet Magufuli wakiwa meza kuu pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dar es salaam.
  Baadhi ya mawaziri wa wizara mbalimbali katika serikali ya awamu ya tano wakiwa katika mkutano huo.
  Baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristo na ya Kiislamu wanaounda kamati ya Amani wakiwa katika mkutano huo
  Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima hakubaki nyuma na yeye amehudhuria katika mkutano huo na hapa akionekana mwenye furaha na bashasha kama alivyonaswa na kamera yetu.
  Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akiwa amekaa pamoja na viongozi wenzake wa dini katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam wakati Rais Dk. John Pombe Magufuli alipozungumza na wazee wa mkoa wa Dar es salaam.
  Baadhi ya wazee wa Dar es salaam wakitambulishwa katika mkutano huo.
  Baadhi ya mawaziri waliohudhuria katika mkutano huo kutoka kulia ni Mh. Profesa Sospeter Muhongo, Dk. Abdallah Posi, Nape Nnauye, Januari Makamba na Ummy Mwalimu.
  Baadhi ya wazee wakifuatilia kwa makini wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia mkutano huo


  Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu akisalimia wazee katika mkutano huo.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimia wazee katika mkutano huo.
  Mwenyekiti wa Wazee wa mkoa wa Dar es alaam Mzee Hemed Mkali akihutubia katika mkutano huo na kumkaribisha Rais Dk. John Pombe Magufuli ili kuwahutubia wazee hao.
  Wazee hawa wakionekana kuhamasika na hotuba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli.
  Rais Dk. John Pombe Magufuli akihutubia katika mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo.

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametembelea hospitali ya Taifa Muhimbili kukagua utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kuwataka watumishi wa wizara hiyo waliokuwa wakilitumia jengo la Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto kuhamisha ofisi zao na kuliacha kwa ajili ya matumizi ya wodi ya wazazi.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo katika hospitali hiyo, Waziri Ummy amesema kuwa mpaka kufikia kesho tayari jengo hilo litakuwa limeanza kutumika kwa kuwa watafanya kazi ya kuhamisha makabrasha ya watumishi hao usiku kucha kuhakikisha agizo la Rais John Magufuli linatekelezwa mara moja.
  FSA_6533

  Picha mbalimbali zinaonesha Waziri Ummy Mwalimu akikagua utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli pamoja na watumishi na vibarua wakihamisha nyaraka na makabrasha mbalimbali kutoka kwenye jengo lililokuwa likitumiwa kama ofisi na watumishi wa wizara hiyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.

  ????????????????????????????????????

  FSA_6540
  ????????????????????????????????????

  0 0

  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akikabidhi hundi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Patrick Karangwa,ikishuhudiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa(katikati)
  Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea mgodi wa Bulyanhulu

  Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa Akiwa chini ya archi kilomita moja kutoka uso wa dunia akiwapongeza wafanyakazi wazawa katika mgodi wa Bulyanhulu kwa kufanya kazi ambazo zamani watanzania walikuwa hawawezi, kazi ya kufanya kazi kwa mitambo ya kisasa ya inayojulikana kama Jumbo na mashine zingine za teknolojia ya kisasa zinazotumika katika kuchimba dhahabu kwenye mgodi mkubwa wa dhahabu nchini Bulyanhulu.
  Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa Akiwa anatoka kwenye lifti kutokea chini ya ardhi baada ya kutembelea mgodi wa dhahabu chini ya ardhi.
  Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Vita Kawawa akizungumza wakati wa ziara yake katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ambapo amesisitiza kuwa kodi ya ushuru wa huduma iliyotolewa na Mgodi wa Bulyanhulu itumike vizuri kujenga miundombinu ambayo wananchi wataiona kwa macho.
  Afisa Maendeleo na Mahusiano wa mgodi wa Bulyahulu ,Sara Teri akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa,kushoto kwake ni Mshauri wa Mahusiano ya Kampuni ya Acacia na Serikali , Alex Lugendo.
  Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa (Kushoto) akielekea katika eneo la mgodi wa chini ya ardhi Bulyanhulu.
  Mkuu wa wilaya ya kahama Vita Kawawa na ujumbe wake pamoja na mshauri wa mahusiano ya kampuni na serikali wa Acacia aliyesimama katikati mwenye shati ya bluu Alex Lugendo wakiwa katika picha ya pamoja.
  Kaimu Meneja wa Uchimbaji katika Mgodi wa Bulyanhulu Salvatory Tesha
  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Bw.Graham Crew akifafanua jambo kwa mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa.
  Meneja wa Ufanisi wa Kampuni katika Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Elias Kasitila akimuonyesha ramani ya uchimbaji mkuu wa Wilaya ya Kahama na ujumbe wake


  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
  Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Vita Kawawa amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kuwa fedha zitumike vizuri katika miradi inayoonekana. 

  “sitaki masuala ya kusema unajua pesa tuliitumia katika kuweka kifusi barabarani na sasa mvua imekiosha, hapana, hilo litakuwa ni jipu linatakiwa kutumbuliwa, fedha hizi zitumike kujenga miradi inayoonekana kama vila vyumba vya madarasa, zahanati nakadhalika.”

  0 0

  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania, (TSSA), Meshack Bandawe, (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Februari 14, 2016. Pamoja na mambo mengine Bandawe alisema, mkutano wa mwaka wa Muungano wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Mamlaka za Usimamizi Sekta za Hifadhi za Jamii kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (ECASSA), utafanyika nchini kuanzia Februari 18 mwaka huu 2016. (Kushoto) ni Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Vincent Tiganya, na kulia ni mjumbe wa kamati ya waandaaji wa mkutano, Rehema Kabongo.

  NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

  TANZANIA itakuwa mwenyeji wa mkutano wa Muungano wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (Pensheni na afya), na Mamlaka za usimamizi wa sekta za hifadhi ya Jamii za nchi za Afrika Mashariki na Kati, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania, (TSSA), Meshack Bandawe Amesema.

  Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Februari 14, 2016 kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam, Bandawe alisema, mkutano huo utakuwa wa siku mbili na utaanza Februari 18 na kukamilika Februari 19 mwaka huu 2016.

  “Mkutano utafanyika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu (BoT) na utafunguliwa na Mh. Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.” Alisema Bandawe

  Alisema, madhumuni ya mkutano huo ambao hufanyika kila mwaka kwa mzunguko wan chi wanachama, ni kujadili sera zinazohusiana na sekta ya hifadhi ya jamii. “Washiriki hupokea mada zinazowasilishwa na wataalamu mbalimbali, kuzichambua na kuzijadili kabla ya kuweka maazimio kwa ajili ya kuboresha sekta ya hifadhi ya jamii katika nchi wanachama.

  Kwa mara ya kwanza mkutano kama huu ulifanyika jijini Mwanza na kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “Kuwiania sera za Kiuchumi, upatikanaji wa ajira na maendeleo ya sekta ya hifadhi ya jamii katika Afrika Mashariki na Kati”.
  Waandishi wakiwa kazini


  0 0

   Viongozi wa Shirika la Umeme Tanesco kutoka kushoto Naibu Mkurugenzi Mtendaji -Uwekezaji Mhandisi,Decklan Mhaiki,Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji-Usambazaji na Huduma kwa Wateja Mhandisi,Sophia Mgonja na Meneja Mafunzo Dorothy Migembe.
   Kiongozi wa JICA akizungumza na waandishi.
   Naibu Mkurugenzi Mtendaji -Uwekezaji Mhandisi,Decklan Mhaiki,akizungumza na waandishi.
   Naibu Mkurugenzi Mtendaji -Uwekezaji Mhandisi,Decklan Mhaiki,akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa viongozi wa JICA.
   Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji-Usambazaji na Huduma kwa Wateja Mhandisi,Sophia Mgonja,akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa viongozi wa JICA. 
   Sehemu ya viongozi wa JICA.
   Wafanyakazi wa Tanesco. 
   Viongozi wa Tanesco wakifuatilia jambo wakati wa mkutano.
  Viongozi wa Tanesco na JICA wakiwa katika picha ya pamoja.
   Viongozi wa JICA
   Viongozi wa JICA

   Viongozi wa TANESCO

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kulia) akipata maelezo ya namna mitambo ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) inavyofanya kazi kutoka kwa Mtaalamu wa Mitambo (Technician) Edward Lukungu (wa pili kushoto) wakati wa ziara ya kutembelea Shirika hilo jijini Mwanza.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) akipata taarifa ya utendaji wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) kutoka kwa Meneja Mkoa wa Mwanza Bw. Julius Chifungo (katikati) wakati alipotembelea ofisi za Shirika hilo jijini Mwanza. Kulia ni Meneja wa TTCL Mkoa wa Mwanza, Johnbosco Kalista.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiangalia moja ya mitambo ya mkongo wa taifa iliyopo Mkoani Mwanza
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa menejimenti ya TTCL na POSTA alipowatembelea jijini Mwanza.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na wafanyakazi (hawapo pichani) kuhusu kufanya kazi kwa uadiliafu na uwazi ili kusaidia mashirika hayo kusonga mbele.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa TTCL na POSTA mara baada ya kutembelea na kuona utendaji kazi wao, jijini Mwanza.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisalimiana na watumishi wa TTCL na Posta mkoani Mwanza.

  …………………………………………………………………………………………………………..

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewataka watendaji wa Shirika la Posta Tanzania na Kampuni ya simu ya (TTCL) kufanya kazi kwa weledi na mtazamo wa kibiashara ili kuyaongezea mapato mashirika hayo na hivyo kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanaoyotokea nchini.

  Akizungumza na wafanyakazi wa TTCL na POSTA mkoani Mwanza Prof. Mbarawa amesema kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano duniani biashara simu na posta hivi sasa ina ushindani mkubwa unaohitaji mtazamo mpana wa kibiashara ili kukidhi mahitaji ya soko.

  “Serikali inajitahidi kuisaidia TTCL na POSTA hivyo wekezeni vizuri kwenye data na uharaka wa utoaji huduma ili muweze kushindana kwenye soko na kukuza uchumi wa taasisi hizi muhimu kwa usitawi wa nchi”, amesema Prof Mbarawa.

  Prof. Mbarawa amezitaka menejimenti za POSTA na TTCL kufanya kazi kwa uwazi na uadilifu ili malengo na mikakati ya taasisi hizo yafahamike kwa wafanyakazi wote na kuwezesha kujipima kama wanafikia malengo yaliyokusudiwa.

  “Hakikisheni wafanyakazi wote wanaelewa malengo na mikakati ya tasisi zenu ili kazi ya kuyatekeleza ifanywe kwa umoja na ushirikiano”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

  Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amesisitiza umuhimu wa wafanyakazi kuwa wadilifu na kuepuka kuwa mawakala wa mashirika mengine na hivyo kuihujumu Serikali.

  “kuna watu ndani ya TTCL na POSTA ambao ni wazembe, wavivu na wanao hujumu Serikali tutawaondoa mara moja, Ni vema kubaki na wafanyakazi wachache waadilifu kuliko wengi wasiotimiza maelngo yaliyokusudiwa”, amefafanua Waziri Prof. Mbarawa

  Naye Meneja wa TTCL mkoa wa Mwanza Bw. Johnbosco Kalista amemweleza Waziri Mbarawa kuwa wigo wa mtandao kutofikia walaji wengi, wateja kutolipa madeni kwa wakati na ulinzi na usalama wa miundombinu ya mawasiliano ni miongoni mwa changamoto zinazoikabili shirika hilo mkoani Mwanza.

  Kwa upande wake Meneja wa POSTA mkoa wa Mwanza, Bw. Julius Chifungo amebainisha kuwa uchakavu wa barabara, maslahi yasiyokidhi ya wafanyakazi na uchakavu wa majengo ni miongoni mwa vikwazo vinavyoathiri utendaji kazi wa shirika hilo mkoani Mwanza.

  Takribani masanduku elfu tisa yanasimamiwa na Shirika la Posta mkoani Mwanza katika ofisi zake kumi na moja na asilimia 96.8 hukodishwa na kuingizia shirika hilo faida, Wakati takriban wateja 45,041 wanahudumiwa na TTCL katika Mkoa wa Mwanza.

  0 0

  Mkurugenzi wa Woman Fund Tanzania Mama Mary Lusindi pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Imelda Lulu Urio kushoto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya(Mama Ardhi Alliance)wakizindua rasmi taasisi hiyo ambayo kazi yake kubwa ni kuwatetea wanawake katika masuala mbalimbali yanayohusu umiliki wa Ardhi, uzinduzi huo umefanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi za shirika la Tanzania Women Lawyers Association (TAWLA) Ilala jijininDar es salaam.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
  Mkurugenzi wa Woman Fund Tanzania Mama Mary Lusindi pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Imelda Lulu Urio kushoto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya(Mama Ardhi Alliance)wakikata utepe kama ishara ya kuzindua rasmi taasisi hiyo ambayo kazi yake kubwa ni kuwatetea wanawake katika masuala mbalimbali yanayohusu umiliki wa Ardhi.
  Mkurugenzi wa Woman Fund Tanzania Mama Mary Lusindi akionyesha huku Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Imelda Lulu Urio kushoto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya(Mama Ardhi Alliance) na wanachama wenzake wakifurahia mara baadea ya kuzindua rasmi taasisi hiyo ambayo kazi yake kubwa ni kuwatetea wanawake katika masuala mbalimbali yanayohusu umiliki wa Ardhi, Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA Tike Mwambipile.
  Mkurugenzi wa Woman Fund Tanzania Mama Mary Lusindi akimpongeza Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Imelda Lulu Urio kushoto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya(Mama Ardhi Alliance)mara baada ya kuizindua rasmi taasisi hiyo ambayo kazi yake kubwa ni kuwatetea wanawake katika masuala mbalimbali yanayohusu umiliki wa Ardhi
  Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Imelda Lulu Urio kushoto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya(Mama Ardhi Alliance) akisaini kulia ni Naemy Silayo Program Officer Gender And Children Unit wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)
  Mkurugenzi wa Woman Fund Tanzania Mama Mary Lusindi akizungumza jambo katika kikao hicho kutoka kulia ni Bi.Lilian Liundi kutoka TGNP na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA Bi. Tike Mwambipile.
  Jaquiline Waya Afisa Mipango wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo Afrika WILDAF akizungumza jambo katika mkutano huo kulia ni Loyce GondweOfisa wa Sheria katika shirika la Tanzania Media Women Association (TAMWA)
  Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Imelda Lulu Urio kushoto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya(Mama Ardhi Alliance) pamoja na baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakiendelea na majadiliano.
  Wajumbe wa Taasisi ya Mama Ardhi Alliance wakipitia nyaraka kabla ya kusainiwa na kuzindua taasisi hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA Tike Mwambipile akizungumza jambo katika kikao hicho 

  Mkutano ukiendelea

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiongea na viongozi wa COSOTA na wa Kampuni ya Copyright Management Eas t Africa kuhusu mfumo wa ukusanyaji wa mirahaba utakavyokuwa unafanya kazi. .(Picha na Benjamin Sawe- WHUSM)
  Mkuu wa uendeshaji wa Kampuni ya Copyright Management Eas t Africa Bw. Abdi Zagar aliesimama akimuelekeza Mhe. Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye jinsi mfumo wa ukusanyaji wa mirahaba utakavyokuwa unafanya kazi, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Copyright Management Eas t Africa Bw. Paul Matthysse .(Picha na Benjamin Sawe- WHUSM)
   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Copyright Management Eas t Africa Bw. Paul Matthysse kulia akimuelekeza Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye jinsi mfumo wa ukusanyaji wa mirahaba utakavyokuwa unafanya kazi.(Picha na Benjamin Sawe- WHUSM).

  0 0

  Jeshi la vijana Watafuta Njia (PFC) wakionesha programu maalum katika sherehe ya kumuaga Mch. Amosi Lutebekela (hayupo pichani) iliyofanyika katika kanisa la waadventista wasabato Manzese jana.
  Kwaya ya wasabato ya Mbiu wakikabidhi zawadi ya kwaya kwa Mch. Amosi Lutebekela na Mkewe kwenye sherehe ya kuwaaga iliyofanyika jana katika kanisa la wasabato Manzese.
  Kwaya ya Wasabato Ruvu kitonga wakimtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji wakati wa sherehe ya kumuaga Mch. Amosi Lutebekela iliyoandaliwa na kanisa la wasabato mtaa wa Manzese.
  Kwaya ya Angaza wakiimba wimbo maalum wa kumuaga Mch. Amosi Lutebekela kwenye sherehe ya kumuaga iliyoandaliwa na kanisa la wasabato mtaa wa Manzese.
  …………………………………….

  Na. Sarah Reuben

  Mkurugenzi wa Sauti ya Unabii, Uchapaji na Maeneo Mapya Mch. Amosi Lutebekela jana amekemea tabia mbaya ya baadhi ya waumini wa kanisa la waadventista wasabato wanaoshindwa kutimiza kiapo chao cha ndoa na kuanza kudai kuvunja ndoa kwa sababu zisizokubalika kibiblia.

  Akizungumza wakati wa ibada kuu katika kanisa la waadventista wasabato Manzese, jijini Dar es Salaam, Mch. Lutebekela alisema hivi karibuni idadi ya wanandoa ambao wanaomba kuvunja ndoa inaongezeka tena kwa sababu zisizokubalika kibiblia.

  “Mimi kama msajili wa ndoa nimekuwa nikishughulikia changamoto mbalimbali za wanandoa ambao wamekuwa wakiomba kuvunja ndoa kama suluhisho la migogoro yao. Ninakemea wanandoa wote wenye malengo ya kuvunja ndoa kinyume na utaratibu wa biblia. Tabia hiyo ikome mara moja kwa jina la Yesu, alisisitiza.

  Katika hotuba yake vilevile Mch. Lutebekela aliwataka vijana ambao hawajaingia katika ndoa kuzingatia sifa za kiroho zaidi badala ya kutegemea mivuto ya kimwili yaani sura nzuri na muonekano wa nje. “Ninapenda kuwaasa vijana wa kiume na wakike epukeni sana kutafuta wenzi wa maisha kwa kuangalia mivuto ya nje yaani sura na muonekano. Sura inachakaa lakini roho na tabia njema haitachakaa hata umri wenu ukisonga, alifafanua Mch. Lutebekela.

  Mch. Amosi Lutebekela aliyasema hayo katika sherehe ya kumuaga rasmi iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa Manzese baada ya kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa Sauti ya Unabii, Uchapaji na Injili katika maeneo mapya hivi karibuni. Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi, Mch. Lutebekela alikuwa mchungaji anayesimamia Mtaa wa Manzese.

  0 0

  Baadhi ya viongozi wa wilaya ya Hai,wakiwa katika kikao kidogo na Waziri Ndalichako.
  Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka (kushoto) akimueleza jambo Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi ,Prof Joyce Ndalichako aliyefanya kikao kidogo na watumishi wa Elimu katika halmashauri ya wilaya ya Hai.
  Waziri Prof Ndalichako akizungumza na viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia elimu katika halmashauri ya wilaya ya Hai.
  Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akimsikiliza kwa makini Prof Ndalichako.
  Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akiongozana na Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako alipofika ofisi ya mkuu huyo wa wilaya na kuzungumza mambo machache na Wakaguzi wa elimu na maofisa elimu wa wilaya ya Hai.
  Waziri Ndalichako akitia saini katika kitabu cha wageni ofisini kwa mkuu wa wilaya ya Hai.
  Waziri Prof Ndalichako akizungumza na kutoa maagizo mbalimbali kwa maofisa elimu na wakaguzi wa elimu katika wilaya ya Hai.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi.Amina Masenza akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Afya, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa kwanza waliokaa kushoto) wakati alipotembelea ofisini hapo. Wengine ni watendaji wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (waliokaa kulia).

  Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla mapema leo Februari 15, ametembelea kambi ya Wagonjwa wa Kipindupindu pamoja na wale waliokumbwa na mafuriko katika kijiji Mboliboli Kata Pawaga Wilayani Iringa ambapo hadi sasa kambi hiyo ina wagonjwa 40 huku zaidi ya wagonjwa 223 walilipotiwa kuugua tangu kipindupindu kimeanza katika eneo hilo.

  Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi.Amina Masenza wakati wa kutoa taarifa yake kwa Naibu Waziri Dk. Kigwangalla aliyetembea ya Mkuu wa mkoa huyo, alimweleza kuwa kati ya wagonjwa hao 223, wagonjwa 17 ni watoto walio na umri wa chini ya miaka 5, Mbali na hao hadi sasa yamesababisha kifo kimoja.

  Ugonjwa huo umeelezwa kuwa umewakumba kutokana na mvua zilizonyesha na kubomoa vyoo na kutapanya kinyesi hali iliyopelekea ugonjwa huo kusambaa Zaidi katika makazi ya wananchi hao.

  Hadi sasa eneo hilo limekumbwa na maji huku wananchi wakilazimika kuyakimbia makazi yao na hata kuzungukwa na maji karibu eneo kubwa na usafiri wa watoa huduma kuwa wa shida ikiwemo kutumia boti maalum ama chopa.

  Mkoa huo ulikumbwa na mvua mnamo Februari 3 hadi leo bado maji yameendelea kuzingira maeneo ya vijiji hivyo.

  Imeandaliwa na Andrew Chale, modewjiblog-Iringa.
  Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akitoa taarifa namna ya kamati yake ilivyopambana usiku na mchana na hatua waliofikia katika kuakikisha kipindupindu kinakwisha katika eneo hilo huku wakiendelea na jitihada za kupambana na mafuriko ikiwemo kuokoa wananchi waliobakia eneo hilo.
  Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla, akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa mara baada ya kumaliza kwa mazungumzo na taarifa fupi juu ya ugonjwa wa kipindupindu kwenye maeneo ya vijiji vya Mkoa huo ambapo hadi leo wamefikia jumla ya wagonjwa 40.
  Naibu Waziri wa Afya, Dk. Hamisi Kigwangalla pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela wakiwasili katika uwanja wa Ndege wa Nduli, Iringa tayari kwa kuelekea kupanda Chopa kuelekea kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko pamoja na ugonjwa wa kipindupindu.
  Wakielekea katika Chopa maalum ya jeshi la Polisi kwa ajili ya kuwafikia wananchi waliozingira na maji ya mafuriko pamoja na ugonjwa wa kipindupindu.
  Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipanda Chopa tayari kuelekea kwenye eneo lililokumbwa na mafuriko katika vijiji vya Mbolimboli, Pawaga, Mkoani Iringa. 

  (Picha zote na Andrew Chale, Iringa).

  0 0


  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na Athumani Hamisi alipomtembelea nyumbani kwake Sinza Madukani jijini Dar es Salaam.Athumani Hamisi alikuwa Mpigapicha Mkuu wa Magazeti ya Daily/Sunday News na Habari Leo, yanayomilikiwa na Serikali kupitia Shirika lake la Standard Newspaper, ambaye alipata ajali iliyomsababishia baadhi ya viungo vyake kutokufanya kazi.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza waandishi wa habari ambapo alisema Serikali itaendelea kumsaidia Athumani Hamisi na kutafuta suluhisho la kudumu.Athumani Hamisi alikuwa Mpigapicha Mkuu wa Magazeti ya Daily/Sunday News na Habari Leo, yanayomilikiwa na Serikali kupitia Shirika lake la Standard Newspaper, ambaye alipata ajali iliyomsababishia baadhi ya viungo vyake kutokufanyakazi


  Waziri wa Habari utamaduni Sanaa na michezo Nape Nauye ameahidi kutatua changamoto zinazomkabili aliyekuwa mpiga Picha na mwandishi mwandamizi Athumani Hamis. Wazir Nape ametoa kauli hiyo alipomtembelea nyumbani kwake , Sinza Dar es salaam akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Global Publisher Eric Shigongo.

  Waziri Nape ameamua kumtembelea Athmani kutokana na kutambua mchango wake kwenye tasnia ya habari ambapo aliitumikia kwa muda mrefu kabla ya kupata ulemavu. "Amefanya Kazi kubwa serikalini, sisi kama serikali tunao wajibu wa kumsaidia". "Nimechukua Yale yote ambayo yanachangamoto kwake na tunachukua uamuzi wa kumsaidia,"alisema Wazir Nape.

  Waziri Nape amempongeza Rais MstaafuJakaya Kikwete kwa kumsaidia Athmani katika kipindi chote cha uongozi wake na kwamba yeye kama Waziri mwenye dhamana kwa kushirikiana na wadau wengine wataendelea kutoa msaada kwa Athmani na familia yake.

  Pia Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ndugu Eric Shigongo ametoa wito kwa Watanzania kutoa msaada kwa moyo mmoja.

older | 1 | .... | 764 | 765 | (Page 766) | 767 | 768 | .... | 1897 | newer