Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 759 | 760 | (Page 761) | 762 | 763 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Mbunifu wa Mavazi Amina  Plummer Akitoa Mada kwenye Semiana ya Ujasiriamali kwa Wanawake wa Zanzibar yenye Lengo la Kuwafundisha Mbinu Mbalimbali za Biashara pamoja na Matumizi Sahihi ya Vipodozi Pendwa vya Luvtouch.

  Mbunifu wa mavazi Amina Plummer amewaasa wanawake wa zanzibar kujikita kwenye ujasiriamali kwa kuwa ndio njia pekee ya kumkomboa mwanamke.amesema ajira nyingi zimekuwa na ubaguzi na pili ni nafasi chache sana zinatolewa kwa wanawake hivyo basi wanawake hawana budi kujikomboa kwa njia ya ujasiriamali.mama amina alisema hayo wakati akitoa mada alipowatembelea wanawake wa zanzibar walioniufaika na mradi wa manjano dream makers ulio chini ya taasisi ya manjano foundation yaliomalizika kwenye hotel ya mtoni marine zanzibar.
  Mbunifu wa mavazi Amina Design akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser Pamoja wa Baadhi ya wasaidizi Kutoka Taasisi ya Manjano Foundation.

  Akieleza Zaidi Mama Amina Plummer Ambaye  ni Mbunifu wa Mavazi amewaomba wanawake wa Zanzibar Kupenda Ujasiriamali kwa Kuwa ni Kazi Pekee ambayo kadiri Unavyoifanya kwa Juhudi na Maarifa Pia  inasaidia Kuongezeka kwa Kipato cahako.Hivyo wakina mama wa Zanzibar hawana Budi Kuchangamkia nafasi hiyo ya kujifunza Ujasiriamali Kutoka Taasisi Ya Manjano Foundation .
  Washiriki wa Semina Hiyo kutoka  Visiwani Zanzibar wakisikiliza kwa Makini Mda zilizokuwa zikitolewa kwenye Mafunzo hayo.

  0 0  0 0

   Wafanyakazi wa Airtel wakifanya ukarabati bucha la kijana Hashim Mikidadi, kijana aliyewezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa Airtel fursa Tunakuwezesha, wakiongozwa na Asisa mauzo wa Airtel Aminata Keita (katikati) Mwishoni mwa wiki .Hashim ni kijana mjasiriamali  anayejihusisha na kuuza bucha la nyama lililopo standi ya mabasi Ngerengere mjini Morogoro. 
   Afisa mauzo wa Airtel Aminata Keita, akikarabati duka la kijana Hashim Mikidadi mkazi wa Ngerengere mjini Morogoro aliyewezeshwa na Airtel Kupitia mpango wake wa Airtel Fursa. Wafanyakazi wa Airtel walijitokeza kumsaidia kijana Hashim,  mjasiriamali  anayejihusisha na kuuza bucha la nyama kwa kukarabati duka lake  lililopo standi ya mabasi Ngerengere mjini Morogoro baada ya kubahatika kuwezeshwa na mpango huo wa Airtel Fursa kwa kupatiwa vitendea kazi mbali mbali na elimu ya mafuzo ya biashara ya ujasiriamali.
  Afisa mauzo wa Airtel Aminata Keita (kushoto) akiongea na kijana Hashim  mkazi wa Ngerengere mjini Morogoro aliyewezeshwa na Airtel Kupitia mpango wake wa Airtel Fursa walipoungana nae katika ukarabati wa bucha lake kabla ya kukabidhiwa vitendea kazi mwanzoni mwa wiki ijayo.


  Katika jitihada za kusaidia vijana wajasiriamali, wafanyakazi wa  Airtel wameungana na shirika lao kupitia mpango wake wa Airtel FURSA kuwafikia vijana mkoani Morogoro. Mwishoni mwa wiki hii wafanyakazi hao walijitokeza kumsaidia kijana Hashim Mikidadi, kijana mjasiriamali  anayejihusisha na kuuza bucha la nyama kwa kukarabati duka lake  lililopo standi ya mabasi Ngerengere mjini Morogoro..

  Akizungumza wakati wa zoezi la ukarabati wa bucha hilo Afisa mauzo wa Airtel, Aminata Keita alisema "Airtel tunajali sana jamii yetu inayotuzunguka hivyo tunaelewa changamoto nyingi ambazo vijana wamekuwa wakikutana nazo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira, ukosefu wa mtaji wa kuanzisha biashara zao na mambo mengine mengi. Msaada wetu kama wafanyakazi wa Airtel ni kuunga mkono mpango wa kampuni yetu ya kusaidia vijana hapa nchini ujulikanao kama Airtel Fursa  katika kusaidia vijana wetu kwa kuwaonyesha njia ili waweze kuinua jamii inayowazunguka na kufikia ndoto zao."

  "Leo tunafuraha kubwa kuona kwamba tumeweza kumfikia na kumuwezesha kijana huyu mjasiriamali aliyewezeshwa na Airtel FURSA, ambaye Airtel Fursa imebadilisha maisha yake kwa kukarabati paa la bucha lake, kutengeneza sakafu kwa kuweka tiles za kisasa, na matengenezo mengine mengi ambayo imeipa duka hilo mtazamo mpya kabisa . Mapema wiki ijayo Airtel FURSA itamalizia kwa kumuwekea vifaa vya kisasa  kabisa  vikiwemo vifaa vya  kukatia nyama, jokofu la kisasa la kuhifadhia nyama na vifaa vingine vnavyohitajika kwa kazi za bucha. Vifaa hivyo na gharama za utengenezaji vimegharimu kiasi cha sh. milioni 9, alisisitiza Aminata

  Wakati wa shughuli hiyo ya makabidhiano, wafanyakazi wa Airtel walijiunga na wakazi wa  Ngerengere ambao walijitokeza kumuunga mkono  Hashim kwa kuwa na nidhamu kwa jamii inayomzunguka na ni mfano wa kuigwa na vijana wenzie.

  Kwa upande wake Hashim aliwashukuru sana Airtel kwa kuweza kumpatia  fursa hii kwani ni vijana wengi sana wanaohitaji msaada huu lakini leo hii nafasi hii imemdondokea yeye.“Bila kuwasahau nawashukuru sana wafanyakazi wa Airtel kwa kusaidia ukarabati wa bucha langu kwani mtazamo huu mpya  na vifaa vya kisasa utasaidia kuhamasisha wateja wangu na wale ambao hawakuwa wateja wangu.”.

  “Nilianza nikiwa sina kitu. Lakini leo Airtel imeinua maisha yangu na kuniwezesha kuwapatia ajira vijana wenzangu waliokuwa mtaani bila kazi. ".
  Airtel Fursa uwezeshaji ilizinduliwa mwezi Mei mwaka jana na ina tarehe kufikiwa vijana zaidi ya 3000 na mafunzo ya ujasiriamali na misaada ya biashara kwa karibu na 100 wajasiriamali bora vijana wote mmoja mmoja na katika vikundi vya vijana na hatimaye kukua kujenga fursa na jamii inayowazunguka. Katika msimu wa pili Airtel imeahidi kutumia zaidi ya sh. bilioni 1 katika mpango wa kuwawezesha vijana wa Tanzania kufikia uwezo wao katika ulimwengu wa biashara

  Airtel Fursa awamu ya kwanza ulianza mwaka jana mwezi wa tano na mpaka sasa umeshaweza kufikia vijana zaidi ya 3000 kwa kuwapatia mafunzo ya biashara ya ujasiriamali na wengine wapatao 100 wameweza kuwezeshwa kwa kupatiwa vitendea kazi vya kuendelezea biashara zao za ujasiriamali. Katika awamu ya pili Airtel Fursa imeahidi kutumia zaidi ya sh. bilioni 1 ukiwa na lengo la kuwawezesha vijana kwa kuwapatia mbinu mbalimbali za biashara na vifaa vitakavyowawezesha kukuza biashara zao.

  0 0

  WAFANYABIASHARA waasa kulipa kodi  kwa kuto kulipa kodi ni kinyume cha sheria kwani huleta kuleta msukumo kwa Mamlaka ya Mapato kukusanya wa mapato ya serikali ili fedha hizo zitumike kwa matumizi yaliyokusudiwa.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango wakati akizungumza na wafanyabiashara jijini Dar es Salaam leo.

  Pia amesema kuwa   wafanyabiashara wanatakiwa kushirikiana na serikali ya awamu ya tano katika ukusanyaji mapato ili kujenga mazingira bora ya wafanyabiashara.

  Mpango amewaomba wafanyabiashara kutumia mashine za EFD ili kuongeza mapamo ya serikali wanampango wa kununua Mashine za EFD ili kuwapa wananchi ambao hawajaanza kuzitumia kwaajili ya kukusanya mapato ya serikali.

   Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango akizungumza na wafanyabiashara leo katika ofisi za wizara ya Fesha jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi (TPSF), Salum Shamte.
  Kutoka kulia ni Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Ashantu Kijaji, katika ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile wakiwa kwenye mkutano wa waziri wa Fedha na Mipango leo jijini Dar es Salaam.
   Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi (TPSF), Salum Shamte akizungumza na wafanyabiashara  waliokusanyika leo katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam leo.


  Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi (TPSF), Felix Mosha  na Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) wakiwa kwenye mkutano wa wafanyabiashara leo jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya wafabiashara wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

  Mwakilishi wa sekta ya Kilimo Sinari Sinari akizungumzia kuhusiana na sekta ya Kilimo jijini Dar es Salaam leo. 
  Mkurugugenzi wa Bravo Logistics, Angelina Ngalula akizungumza na wafanyabiashara katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na usafilishaji wa mizigo kwa kutumia magari na jinsi adha ya usafari katika sekta ya usafirishaji hapa nchini.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0

   Gari iliyopata ajali kama ionekanavyo pichani
  Piki piki iliyopata ajali.

  Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa akiwemo mke wa waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda Mama Tunu Pinda baada ya gari walilokuwa wakisafiria kumgonga mwendesha pikipiki wakati akikatisha barabara katika eneo la Mkundi barabara ya Morogoro Dodoma manispaa ya Morogoro. 

  Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane mchana katika eneo la Mkundi ikihusisha gari lenye namba za usajili STK 9242 gari la mke wa waziri mstaafu Mizengo Pinda likitokea Dodoma kwenda jijini Dar-es-Salaam  na pikipiki

  Majeruhi wengine wa ajali hiyo ni dereva wa gari hilo Bw Anjelo Mwisa, mlinzi wa mke wa waziri mkuu mstaafu Gaudensi Tembo na kijana wa familia ya Mama Tunu Pinda Bwana Gilbert Sampa.

  Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro Dr Rita Liamuya amesema hali ya mke wa waziri mkuu mstaafu na majeruhi wengine zinaendelea vizuri na kueleza kuwa  majeruhi hao wanatarajia kuhamishiwa jijini Dar-es-Salaam kwa matibabu zaidi.

  0 0  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

  Simu: 255-22-2114512, 2116898
  E-mail: press@ikulu.go.tz
  Tovuti : www.ikulu.go.tz              

  Faksi: 255-22-2113425  OFISI YA RAIS,
        IKULU,
   1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
  11400 DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
   

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za pole Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Tunu Pinda aliyepatwa na ajali ya gari, iliyotokea jana tarehe 08 Februai, 2016 akiwa safarini kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam.


  Ajali hiyo imetokea katika eneo la Mkundi lililopo katika Manispaa ya Morogoro ambapo gari aliyokuwa akisafiria Mama Tunu Pinda, ilipinduka baada ya kumgonga mwendesha pikipiki aliyeingia ghafla barabarani.


  Katika salamu hizo alizozituma kupitia kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko taarifa za kutokea kwa ajali hiyo na amemuombea Mama Pinda na Majeruhi wengine kupona haraka.


  "Kupitia kwako Mheshimiwa Waziri Mkuu Pinda, naomba unifikishie pole nyingi kwa mkeo Mama Pinda kwa kuumia katika ajali hii, na namuomba Mwenyezi Mungu awaponye majeruhi wote ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku"alisema Rais Magufuli.


  Mama Tunu Pinda anaendelea kupata matibabu Jijini Dar es salaam, na hali yake inaendelea vizuri.  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

  Dodoma

  09 Februari, 2016

  0 0

  Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru (katikati), akikata tepe kikiwa ni ishara ya uzinduzi wa huduma za kifedha kwenye tawi la Benki ya Posta Babati mkoani Manyara leo Februari 9, 2016. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi, na kushoto ni Menyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPB, Profesa Lettice Rutashobya


  Msajili wa hazina, Lawrence Mafuru (wapili kushoto), akimpa zawadi mmoja wa wateja wa Benki ya Posta tawi la Babati, Theofil Muhale Tsaghayo baada ya kufungua rasmi huduma za kibenki katika tawi la Babati, mkoaniManyara Februari 9, 2016. kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo Prof. Lettice Rutashobya.

  Na Mwandishi wa K-VIS MEDIA, Babati


  Benki ya Posta Tanzania (TPB) imezindua huduma za Kibenki kwa kufungua tawi lake jipya kwenye mji wa Babati mkoani Manyara. Akizungumza kwenye uzinduzi huo Februari 9, 2016, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPB, Lettice Rutashobya alisema tawi lililokuwepo hapo awali halikuweza kutosheleza mahitaji ya wakazi wa Mji wa Babati na vitongoji vyake kutokana na udogo wake.

  ‘’Tawi hili limefunguliwa ili kutimiza dhamira ya Benki yetu ya kupeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wateja wake, na sasa Tawi hili litatoa huduma bora na za kisasa ikiwemo ile ya ATM kwa wafanyabiashara, wafanyakazi na wananchi kwa ujumla katika wilaya hii ya Babati”, aliwahakikishia Profesa Rutashobya.

  Profesa Rutashobya aliwashukuru wateja wa TPB wa Wilaya ya Babati na vitongoji vyake kwa kutumia huduma wa TPB wa Wilaya ya Babati na vitongoji vyake kwa kutumia huduma za Benki hiyo kwa wingi, na kulifanya tawi hilo kuwa ni mojawapo ya matawi yanayofanya vizuri kifaida.

  Naye Msajili wa Hazina, Lawrence N. Mafuru, ambaye ndiye aliyezindua huduma za kibenki za tawi hilo, aliipongeza Benki ya Posta kwa kuleta maendeleo ya kuninua maisha ya Mtanzania ya hali ya chini kwa kuongeza huduma za kibenki karibu na jamii hiyo, na kwa kubuni huduma mbalimbali hususan za mikopo, zenye lengo la kumuinua kimapata mwananchi wa chini.

  Msajili huyo wa Hazina, alitumia nafasi hiyo kuwasisitiza wakazi wa Babati kuchangamkia fursa zinazotolewa na Benki ya Posta, kwa kufungua akaunti na kwenda kuomba mikopo ambayo oinatolewa kwa riba nafuu na benki hiyo.

  Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi amesema uamuzi wa kujenga tawi hilo ambalo linatoa huduma zote zinapatikana kwenye matawi mengine ya Benki ya Posta Tanzania nchi nzima.

  “Azma ya Benki ya Posta, ni kuwafikia na kutoa huduma za kibenki kwa wananchi wote (financial Inclusion), alisema Moshingi.


  0 0

  Jeshi ni sehemu muhimu ya nchi na usalama wake. Kila mwaka nchi hutenga bajeti kwa ajili ya kuimarisha majeshi yake. Nchi nyingi duniani huchukua tahadhari za kiusalama kwa kuimarisha majeshi yake kulinganisha na nchi nyingine zinavyofanya. Nchi hizo hufanya hivyo kwa kumiliki idadi kubwa ya wanajeshi, kuboresha teknolojia ya kijeshi, kutoa mafunzo na kutengeneza propaganda za kidiplomasia ili kuwaogopesha maadui wao wa kiusalama. Ngoja tuangalie majeshi kumi (Top 10) hatari duniani kwa sasa na bajeti zake; PHIL SUSSMAN Japanese soldiers from the 22nd Infantry Regiment of the Japan Ground Self-Defense Force train in urban assault with American Soldiers from 1st Battalion, 17th Infantry Regiment, 5th Brigade Oct. 17, 2008 during a bilateral exercise at Fort Lewis' Leschi Town.
  Wanajeshi wa Japani.
  10: JAPAN Japan ilikuwa moja ya nchi vinara katika Vita ya Pili ya Dunia (WW2) iliyomalizika mwaka 1945. Cha kufurahisha, baada ya vita hiyo, Japan iliingia kwenye mkataba wa amani na kukubaliana kuwa na jeshi la kawaida lakini kufuatia kukua kwa Jeshi la China ndipo ikaanza kupanua tena jeshi lake ikiweka ngome za kijeshi kwenye visiwa vyake. Bajeti ya Jeshi la Japan imekuwa ikiongezeka kila mwaka hadi kufikia Dola za Kimarekani bilioni 49. Jeshi hilo lina zaidi ya wanajeshi 247,000 waliopo kazini na zaidi 60,000 wa akiba. Lina ndege za kivita zipatazo 1,595 na meli 131. KOREA KUSINI
  Wanajeshi wa Korea Kusini wakifanya mazoezi.
  9: KOREA KUSINI Korea Kusini wanashirikiana mpaka na Korea Kaskazini ambao nao wapo vizuri kijeshi. Ili kukabiliana na majeshi makubwa ya China and Japan, Korea Kusini imekuwa ikiongeza bajeti ya jeshi lake hadi kufikia dola bilioni 34. Lina wanajeshi waliopo kazini 640,000 na wengine wa akiba 2,900,000. Lina ndege kubwa za kivita 1,393 na meli za kijeshi 166.
  UTURIKI
  Wanajeshi wa Uturuki.
  8: UTURUKI Labda ni kwa sababu ya kushirikiana kupambana na kundi korofi la kigaidi la Islamic State linalotishia amani duniani ndiyo maana ni kubwa na linaogopeka zaidi. Limeongeza bajeti yake kwa 10% hadi kufikia dola bilioni 18. Lina wanajeshi wapatao 660,000 walioko kazini na wa akiba. Pia lina ndege za kivita 1,000 na silaha za nchi kavu 16,000 likiwa lina ushirikiano mkubwa na lile la Marekani.
  UJERUMANI
  Wanajeshi wa Ujerumani.
  7: UJERUMANI Miongoni mwa nchi zenye majeshi hatari duniani ni Ujerumani. Linatengewa bajeti ya dola bilioni 45, japokuwa linaonekana kushuka katika miaka ya hivi karibuni labda kwa sababu kizazi cha sasa nchini humo hakipendi mambo ya vita na watu wengi wanaogopa kujiunga na jeshi hilo. Lina wanajeshi 183,000 walioko kazini na 145,000 wa akiba likiwa na ndege za kivita 710 na silaha za nchi kavu zaidi ya 5,000.
  UFARANSA
  Wanajeshi wa Ufaransa.
  6: UFARANSA Katika miaka ya hivi karibuni, Ufaransa imepunguza bajeti ya jeshi lake hilo kwa 10%. Bajeti yake inafikia dola bilioni 43 kwa mwaka. Lina wanajeshi 220,000 waliopo kazini na 500,000 wa akiba. Pia lina ndege za kivita 1,000 na vifaa vya nchi kavu 9,000.
  UINGEREZA
  Waajeshi wa Uingereza.
  5: UINGEREZA Uingereza ni miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) ambao wapo kwenye mkakata wa kupunguza wanajeshi wake kwa 20%. Bajeti ya jeshi lake hatari ni dola bilioni 54 kwa mwaka likiwa na wanajeshi 205,000, ndege za kivita 908 na meli 66.
  INDIA
  Wananchi wa India wakiwa katika mazoezi.
  4: INDIA Jeshi lake lina jumla ya ‘wajeda’ milioni 3.5, wakiwemo milioni 1.325 waliopo kazini na wengine ni wa akiba. Lina magari ya kivita 16,000 na ndege 1,785 pamoja na silaha za nyuklia. Bajeti yake ni dola bilioni 46.
  CHINA
  Wanajeshi wa China.
  3: CHINA Bajeti ya Jeshi la China inafikia dola bilioni 126 likiwa na wanajeshi milioni 2.285 waliopo kazini na milioni 2.3 wa akiba. Ni moja ya majeshi makubwa kwa sasa duniani likiwa katika Tatu Bora. Lina vifaa vya kivita vya nchi kavu 25,000 na ndege 2,800. Pia lina silaha za nyuklia 300.
  URUSI
  Wanajeshi wa Urusi.
  2: URUSI Bajeti ya jeshi hatari la Urusi ni dola bilioni 76.6 ambayo inatarajiwa kuongezwa kwa 44%. Tangu alipoichukua Urusi, Rais Vladimir Putin mwaka 2000, nchi hiyo imekuwa moto wa kuotea mbali katika masuala ya kijeshi. Lina wanajeshi 766,000 waliopo kazini na milioni 2.5 wa akiba. Urusi inaongoza kwa silaha za kivita zikiwemo za nyuklia zipatazo 8,500Scouts with the 82nd Airborne Division’s 1st Brigade Combat Team fire on a line during a course in advanced rifle marksmanship March 21-24, 2011, at Fort Bragg, N.C. The weeklong course emphasized adapting to battlefield problems by knowing one’s tools and capabilities. (U.S. Army photo by Sgt. Michael J. MacLeod)
  Wanajeshi wa Marekani.\
  1: MAREKANI Jeshi kinara la Marekani linatengewa bajeti ya dola bilioni 612.5. Hakuna jeshi lenye bajeti kama hiyo duniani. Lina wanajeshi milioni 1.4 waliopo kazini na 800,000 wa akiba. Hawa jamaa ni wabaya kwa ndege, meli na manowari za kivita. Pia lina silaha za nyuklia 7,500. Kama ulikuwa hujui ndilo jeshi namba moja duniani tangu Vita ya Pili ya Dunia iliyomalizika mwaka 1945. Nchi kama Urusi na China zinangoja sana kwa jeshi la Marekani kutokana na kuwa na mbinu na teknolojia ya hali ya juu ya kijeshi. NB: Data kama hizi ni vigumu kuzipata kwa baadhi ya nchi za Afrika. Imeandaliwa na Sifael Paul kwa msaada wa mtandao.

  0 0

  DAMU2Maadhimisho ya miaka 6 ya utoaji wa Huduma ya Damu Hospitali ya Muhimbili Tarehe 25-27 Februari 2016 kuanzia Asubuhi mpaka Jioni.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imebuni na kuanza kutekeleza Sera ya Uwekezaji ili kufikia lengo la kuwawezesha wananchi kiuchumi. 

  “Taarifa zilizopo zinaonyesha ni asilimia 10 tu ya Watanzania ndio wanaomiliki uchumi wa nchi na sera hiyo ndiyo inatoa mwongozo wa jumla unaohakikisha kwamba wananchi wanapata fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo zitawawezesha kujenga na kufaidika na uchumi wa mchi yao,” alisema.

  Waziri Mkuu amesema maeneo yanayolengwa na sera hiyo ni yale yenye kuleta matokeo ya haraka na yanayogusa maisha ya wananchi hasa katika sekta za kilimo, ufugaji, uvuvi, misitu, ujenzi, biashara, utalii, madini, viwanda na usafirishaji.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Februari 7, 2016) wakati akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Kwanza wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi nchini uliofanyika kwenye ukumbi wa kituo cha kimataifa cha mikutano cha mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.

  Alisema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inalenga kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya uchumi wa nchi yetu inamilikiwa na Watanzania wenyewe. Waziri Mkuu pia alizindua Mwongozo wa Utekelezaji Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

  Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Walemavu, Bibi Jenista Mhagama alisema hadi sasa mikoa 20 imekwishatenga maeneo ya uwekezaji kwenye halamhashauri zake  na imeanza kuweka miundombinu ya kuvutia wawekezaji.

  Naye Mweyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Prof. Omari Issa alisema katika dunia ya sasa imebainika kuwa haina maana kumpatia mtu mkopo bila kumtafutia masoko au kumuunganisha wadau wa masoko. Kwa hiyo wamejipanga kuwasaidia Watanzania kwa kuwaunganisha na masoko.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM.
  JUMANNE, FEBRUARI 9, 2016.

  0 0

  Meneja Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha (Kushoto) akikabidhi vifaa mbalimbali vifaa vya mawasiliano na michezo vyenye thamani ya shilingi milioni nane kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC) Habel Chidawali, ili kufanikisha bonanza la wanahabari la kufunga mwaka 2015 lililopangwa kufanyika baadaye mwezi huu. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Dodoma. 
  Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC) Habel Chidawali, akitoa shukrani mara baada ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali vifaa vya mawasiliano na michezo vyenye thamani ya shilingi milioni nane na Meneja mawasiliano wa Tigo John Wanyancha ili kufanikisha bonanza la wanahabari la kufunga mwaka 2015 lililopangwa kufanyika baadaye mwezi huu wanaoshuhudia ni makamu mwenyekiti wa CPC Rachel Chibwete (kushoto) na katibu wa CPC bw .Bilison vedastus 

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Rais wa VICOBA, Devota Likokola (wapili kulia ) wakati alipotembelea banda la Benki ya Posta Tanzania katika Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi alioufungua kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha walimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016.   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kaipata maelezo kutoka kwa Bi Fatuma Kango kuhusu Msimbomilia au Barcode baada ya kufungua Mkutano wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es slaam Februari 9, 216.


   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafisi nchini, Reginald Mengi baada ya kufungua mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. 

  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  -Kupitia ujumbe wa simu za mkononi
  WASICHANA Nchini kuanzia leo wataanza kunufaika na kampeni maalumu ya kutumia ujumbe mfupi wa maneno kwa njia ya simu za mkononi kwa ajili ya kutoa elimu kwa wasichana kuhusiana na hedhi na jinsi ya kujistiri wanapokuwa kwenye kipindi hicho.

  Kampeni hiyo ambayo Taasisi ya Vodacom Foundation kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la T-MARC imewalenga wasichana wenye umri wa kuanzia miaka 18-40  wanaotumia simu za mkononi pia inahamasisha jamii kuacha kuonea aibu mijadala kuhusiana na changamoto za kipindi cha hedhi ambazo zinawakumba wasichana wengi na pia kutoa elimu ni jinsi gani ya kujistiri vizuri ili waendelee na majukumu yao ya kila siku.

  Vodacom Foundation imewezesha mradi huu kwa kutoa fursa ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno wenye thamani ya shilingi milioni 100 na utatekelezwa na Shirika la T-MARC Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya  PUSH Mobile kwa kipindi cha miezi sita.

  Ushirikiano wa Vodacom Foundation na T-MARC unaendelea kutekeleza mradi wa Hakuna Wasichoweza unaondelea katika mikoa ya Lindi a Mtwara ambao kwa kiasi kikubwa meanza kuonyesha mafanikio kwa kupunguza uoro wa wasichana mashuleni wanapokuwa katika vipindi vya hedhi.Mradi huu pia unatarajiwa kuwafikia wasichana  Zaidi ya 10,000 katika mikoa hiyo.

  Akiongea kuhusu mradi wakati wa uzinduzi,Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania Ian Ferrao,alisema Vodacom inajivunia kushirikiana na T-MARC kusaidia  afya za wanawake kwa kuwa moja ya dhamira ya kampuni ni kutumia ubunifu wa teknolojia kuboresha maisha ya watu kwenye jamii kama ambavyo imefana kutumia mtandao wake kutoa elimu ya afya na uzazi.

  Naye Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO Dk.Moshi Kimizi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa  kampeni hii alipongeza Vodacom Foundation na T-MARC kwa kuona umuhimu wa kuelimisha jamii kuhusiana na changamoto za hedhi ambazo zinachangia  wanawake kubaki nyuma.

  “Napenda kuungana na kauli mbiu ya kampeni hii,ambayo ni Hedhi sio ikwazo cha kupata elimu kwa wasichana na nawaomba watanzania wote waungane na mimi kuhakikisha kuwa wanashiriki katika kampeni hii kwa kutuma neon MSICHANA kwenda namba 15077 ili kupata taarifa sahihi kuhusiana masuala haya”.Alisema Dk.Kimizi.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la T-MARC,Diana Monica Kisaka ameshukuru Vodacom kwa kutoa msaada huu na kudai kuwa utasaidia wasichana wengi kupata elimu ya afya hususani kuhusiana na suala la hedhi na jinsi ya kukabiliana na changamoto zake pia utaweza kupata taarifa Zaidi kuhusiana na ukubwa wa tatizo hili ambalo liko nchini pote.
  Takwimu zilizopo juu ya tatizo hili kutokana na utafiti uliofanyika  mwaka 2010 zinabainisha kuwa wasichana wapatao 68,538 wamekatiza masomo yao kutokana na  changamoto za hedhi ambao ni asilimia 75 ya  wanafunzi watoro mashuleni.

  Mbali na msaada huu,Vodacom Foundation imeishatumia Zaidi ya shilingi 378 katika mradi wa Hakuna Wasichoweza kati ya mwaka 2014-2015 ambao unaendelea katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
   Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Unesco,Dkt Moshi Kimizi(katikati)na Mkurugenzi mtendaji wa T-Marc Tanzania,Diana Kisaka(kushoto) wakimsikiliza Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation,Renatus Rwehimbiza(kulia) wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo(hawapo pichani)katika hafla ya Uzinduzi wa kampeni ya Ujumbe Mfupi(SMS) kwa Njia ya Simu za mkononi kupitia mradi wa”Hakuna wasichoweza”unaotoa elimu bora ya kujisitiri kwa wasichana wakati wa hedhi na Usafi kwa mtoto wa kike ambayo huwafanya wasichana kukosa masomo yao mara kwa mara.
   Mkurugenzi mtendaji wa T-Marc Tanzania,Diana Kisaka(kushoto)na Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation,Renatus Rwehimbiza(kulia) wakimshuhudia Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Unesco,Dkt Moshi Kimizi(katikati)akibofya kitufe cha kompyuta kuashiria Uzinduzi rasmi wa kampeni ya Ujumbe Mfupi(SMS) kwa Njia ya Simu za mkononi kupitia mradi wa”Hakuna wasichoweza”unaotoa elimu bora ya kujisitiri kwa wasichana wakati wa hedhi na Usafi kwa mtoto wa kike ambayo huwafanya wasichana kukosa masomo yao mara kwa mara.Hafla hiyo ilifanyika leo jijini Dar es Salaam. 
   Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Unesco,Dkt Moshi Kimizi(katikati)akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Push Mobile,Freddie Manento(wapili kushoto) wakati wa hafla ya Uzinduzi wa kampeni ya Ujumbe Mfupi(SMS) kwa Njia ya Simu za mkononi kupitia mradi wa”Hakuna wasichoweza”unaotoa elimu bora ya kujisitiri kwa wasichana wakati wa hedhi na Usafi kwa mtoto wa kike ambayo huwafanya wasichana kukosa masomo yao mara kwa mara,Wanaoshuhudia kushoto Mkurugenzi mtendaji wa T-Marc Tanzania,Diana Kisaka na  Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation,Renatus Rwehimbiza(kulia)
  Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu, Afya, wafanyakazi wa T-Marc Tanzania na Vodacom wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Uzinduzi wa kampeni ya Ujumbe Mfupi(SMS) kwa Njia ya Simu za mkononi kupitia mradi wa”Hakuna wasichoweza”unaotoa elimu bora ya kujisitiri kwa wasichana wakati wa hedhi na Usafi kwa mtoto wa kike ambayo huwafanya wasichana kukosa masomo yao mara kwa mara.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na wajumbe (hawapo pichani) wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba. Kulia ni Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA), Esaka Mugasa. Katika hotuba yake, Katibu Mkuu aliwataka watu wanaomiliki silaha nchini isivyo halali kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kabla ya operesheni ya kuwakamata haijaanza. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin Komba akizungumza na wajumbe (hawapo pichani) wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam, kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu ili aweze kuifungua warsha hiyo ya siku mbili. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA), Esaka Mugasa akizungumza na wajumbe (hawapo pichani) wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Watatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba. Katibu Mkuu katika hotuba yake ya ufunguzi wa warsha hiyo, aliwataka watu wanaomiliki silaha nchini isivyo halali kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kabla ya operesheni ya kuwakamata haijaanza. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kulia) akitoka katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam mara baada ya kufungua Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba, wapili kushoto ni Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi-Makao Makuu, Hezron Gyimbi na kulia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Yusuph Ilembo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na wajumbe wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Katibu Mkuu aliwataka watu wanaomiliki silaha nchini isivyo halali kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kabla ya operesheni ya kuwakamata haijaanza. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Sehemu ya wajumbe wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza na wajumbe hao katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam kabla ya kuwafungulia warsha yao ya siku mbili itakayojadili umasishaji wa Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha ya Mwaka 2015. Hata hivyo, katika hotuba yake, Katibu Mkuu aliwataka watu wanaomiliki silaha nchini isivyo halali kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kabla ya operesheni ya kuwakamata haijaanza. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati waliokaa), Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba (wapili kushoto waliokaa), Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi-Makao Makuu, Hezron Gyimbi (wapili kulia), Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Yusuph Ilembo (kulia) na kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA), Esaka Mugasa, wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi. Warsha hiyo ya siku mbili ilifunguliwa na Katibu Mkuu, Rwegasira katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
  WAZIRI wa Fedha na Mipango,Dk.Philip Mpango,Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe pamoja na Jaji Mkuu, Othman Chande wamekutana kwa ajili ya fedha ya Sh.bilioni 12.3 iliyotolewa na Rais John Pombe Magufuli juu ya uendelezaji wa miundombinu ya mahakama nchini pamoja na uendeshaji wa kesi mbalimbali.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Jaji Mkuu Othman Chande mbele ya mawaziri wa wawili, amesema fedha hiyon itakwenda katika maeneo ya utengenezaji wa miundombinu ya mahakama ili wanannchi waweze kupata haki katika vyombo vya sheria.

  Jaji Mkuu, Chande amesema kuwa michoro ipo tayari kwa ajili ya ujenzi wa mahakama za mwanzo na wilaya ambazo hazina pamoja na mikoa ambayo hazina mahakama kuu.

  Amesema adhima ya Rais Dk. John Pombe Magufuli ni kuhakikisha wananchi wanapata haki pale wanapotaka katika vyombo vya sheria isiwe kikwazo cha kukosekana kwa mahakama katika eneo husika.

  Nae Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema kuwa hundi iliyotolewa jana tayari fedha hiyo imeingizwa katika akaunti ya mahakama ziweze kuanza kazi yake iliyokusudiwa.

  Kwa upande wa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema kuwan fedha hiyo itasukuma ujenzi wa miundombinu ya mahakama ili wananchi waweze kupata haki.

  Amesema hatua za ujenzi wa Mahakama ya Wahujumu Uchumi na Wala Rushwa nao uko katika hatua nzuri lakini kwa fedha hiyo ni kwa ajili uboreshaji wa miundombinu ya mahakama.
   Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa kutimiza ahadi yake ya kuipatia Mahakama kiasi cha shilingi Bilioni 12.3 zitakazotumika  katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya Mahakama na ujenzi wa Mahakama mpya katika maeneo mbalimbali nchini. Kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto).
  Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kutoka kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusu Serikali kuendelea kushirikiana na Mahakama ya Tanzania ili kuwezesha ufanisi wa shughuli zake.

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo tarehe 09/02/2016 katika ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu ya Wizara hiyo kuzungungumzia tukio la hivi karibuni (tarehe 29 Januari 2016) la kushambuliwa kwa helkopta ya doria na kuuawa Rubani Rogers Gowel Raia wa Uingereza. Katikati ni Naibu Waziri Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani na Katibu Mkuu Wizara hiyo Maja Gen. Gaudence Milanzi. 
   Mkutano na Waandishi wa Habari ukiwa unaendelea.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, INSPEKTA Jenerali (IGP), Ernest Mangu, kulia akifafanua moja ya jambo katika Mkutano huo. Kulia ni Waziri wa  Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe.
   Baadhi ya viongozi kutoka Wizara ya Maliasili walioshiriki mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Bw. Herman Keraryo. 
  Waandishi wa habari wakichukua matukio ya mkutano huo na baadhi ya washiriki wakifuatilia.
  (Picha na Hamza Temba - Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Maliasili na Utalii)

  0 0

  Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba sambamba na Mbunge wa jimbo la Mvomero Mh Sadick Murad (mwenye shati ya drafti),ikiwemo na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Morogoro sambamba na wananchi wakishuhudia tukio la mgogoro wa Wakulima na Wafugaji,ambapo takribani mbuzi zaidi ya 70 wamekatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana,ambapo Waziri huyo ameahidi sheria na hatua za kudumu za tatizo hilo kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

  Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mwigulu Nchemba ametembelea Kijiji cha Kigurukwa mjini Morogoro kulikotokea mapigano ya Wakulima na Wafugaji yaliyosababisha kuuawa kwa mbuzi  na Kondoo zaidi ya 70.Waziri Mwigulu ameagiza Kamati ya Ulinzi ya Mkoa kuhakikisha wote waliohusika katikla tukio hilo wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

  Pia ameagiza kutekelezwa haraka hukumu ya mahakama iliyotolewa mwaka 2005 iliyoagiza kuwekwa kwa mipaka kati ya eneo la wafugaji na wakulima.

   Baadhi ya Mbuzi waliokatwa katwa na mapanga .
   Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba akiongozwa na wafugaji kabila la Wamasai kufuatia mgogoro wao na Wakulima na kupelekea uharibifu mkubwa wa kuuwawa kwa wanyama zikiwemo mbuzi zaidi ya 70.  

   Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba sambamba na Mbunge wa jimbo la Mvomero Mh Sadick Murad (mwenye shati la drafti),wakiwemo na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya ya Mvomero na wananchi mbalimbali wakishuhudia tukio la kuuwawa kwa mbuzi zaidi ya 70 wakiwa wamekatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana,ambapo Waziri huyo ameahidi sheria na hatua za kudumu za tatizo hilo kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.
   Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Mvomero katika kijiji cha Kigurukwa mkoani Morogoro kufuatia mgogoro mkubwa kuzuka kati ya Wakulima na wafugaji,ambapo inaelezwa kuwa katika tukio hilo mbuzi  na kandoo zaidi ya 70 wakiwa wamekatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana.Waziri Mwigulu Nchema ameahidi  kuwa sheria na hatua za kudumu za tatizo hilo kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

  0 0

  Shimo katika tuta la reli  eneo la Buguruni kwa Mnyamani  ambalo limesababishwa na mvua inayoendelea kunyesha hapa nchini ambapo ukarabati wa eneo hilo unaendelea ili kufanikisha usafiri kurejea hapo kesho.


  KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)
  Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusitishwa huduma ya treni ya jiji maarufu kama Treni ya Mwakyembe awamu ya jioni ya leo Februari 09, 2016. 

  Taarifa imefafanua kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na maji ya mvua kuchimba shimo kubwa katika tuta la reli karibu na stesheni ya Buguruni kwa Mnyamani.

  Uharibifu huo uligundulika leo asubuhi mara baada ya treni kupita eneo hilo ikielekea stesheni ya Dar es Salaam.wakati wa safari yake ya kwanza kutoka Kituo cha Ubungo Maziwa.

  Tayari mafundi wa TRL wako katika eneo la tukio wakiendelea na kazi ya ukarabati na kwamba inatarajiwa huduma hiyo itarejea tena hapo kesho kama kawaida.

  Atakayesoma taarifa hii amuarifu mwenziye.
  Uongozi wa TRL unasikitika kwa usumbufu utakaojitokeza.
  Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya :
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
  Nd Masanja Kungu Kadogosa
  Dar es Salaam,
  Februari 09, 2016.

  0 0

  Hatimaye Alikiba ametoa wimbo wake “Lupela” uliokuwa ukisubiriwa na mashabiki wake Afrika Mashariki kwa wiki kadhaa sasa. Wimbo huo ni sehemu ya kampeni ya “Ujangili Unatuumiza Sote” iliyozinduliwa mwaka jana na WildAid na African Wildlife Foundation mashirikia yanayofanya kazi pamoja barani Afrika na Asia kupunguza mahitaji ya bidhaa zitokanazo na wanyamapori na kuongeza uelewa wa janga la ujangili linaloikabili Afrika. Video ya wimbo huo imerekodiwa jijini Los Angeles Marekani ambapo Alikiba alikuwa mgeni rasmi kweye hafla maalum iliyoandaliwa na shirika la uhifadhi wanyamapori la kimataifa la WildAid. Chini ya kauli mbiu “Ujangili Unatuumiza Sote”, Alikiba amefanya kazi na WildAid kuongeza uelewa wa Watanzania kuhusu tatizo la ujangili wa tembo ambao wamechinjwa kwa maelfu miaka ya hivi karibuni kwa ajili ya meno yao.
  Katika uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Slipway jijini Dar es salaam, wageni mbalimbali na waandishi wa habari walipata fursa ya kuusikiliza wimbo na kuangalia video yake kwa mara ya kwanza. "Tunaona fahari sana kuwa na Alikiba kama Balozi wa WildaAid”, alisema Salome Gasabile Meneja wa WildAid Tanzania. “Katika mwaka mmoja uliopita, yeye na meneja wake Seven wamefanya kazi bila kuchoka kupinga ujangili wa tembo na tunaamini wimbo huu utakuwa na faida kubwa katika vita dhidi ya ujangili”. “Nina furaha kubwa kuwa sehemu ya mradi huu. Naamini kila mara watu wakisikiliza wimbo huu watakumbuka faida ya tembo kwa urithi na uchumi wa bara la Afrika. Wanaingiza pesa nyingi kupitia utalii na fedha hizo zinaweza kusaidia kuleta ajira, kujenga shule na hospitali kwenye jamii zinazozunguka hifadhi za taifa,” alisema Aleya Aleya Janell ambaye ameshiriki kwenye video ya wimbo huo kama Lupela.
  Asha Franklin, aliyeshiriki kama tembo wanaocheza muziki amefanya kazi na Rihanna na Ciara katika video mbalimbali amesema “Hii video ni nzuri kwani imechanganya burudani ya muziki na jambo zuri kwa jamii” Ushiriki wetu kama tembo wananocheza muziki ilikuwa ni ubunifu wa hali ya juu lakini pamoja na kwamba ni burudani bado unaweza kuona faida ya kubwa ya wimbo huu.” Video hiyo iliongozwa na Kevin Donovan, huku ikirekodiwa na kutengenezwa na muandaaji filamu maarufu wa Hollywood Brian Rumsey ikiwa ni mchango wake kwa kampeni hiyo. Oththan Burnside, ambaye ameishafanya kazi na wanamuziki wengi maarufu kama Rihanna na Sean Paul alihusika kuandaa wimbo huu na staili ya uchezaji wa tembo.
  “Tuufanye mwaka 2016 mwaka wa tembo – mwaka ambao hatimaye tutakumbuka kuwa hatimaye tuikomesha ujangii wa tembo na kuwapa tembo nafasi ya kuishi” alisema Burnside. “Tusaidie kuokoa maisha ya wanyama hawa wazuri,” alisema Burnside. Kwa mujibu wa shirika la WildAid wimbo huo hautatumika kibiashara na unapatikana bure kwa mashabiki kupakua au kusikiliza kweye mtandao wa www.yearoftheelephant.org Uzinduzi wa wimbo huo umeenda sambamba na kampeni ya #jointheherd inayofanyika kupiti mitandao ya kijamii ikiongozwa na wau maarufu mbalimbali wakiwemo muigizaji Lupita Nyong’o, Jackie Chan na Jacqueline Mengi ambao wanaendelea kuhamasisha watu kupitia www.yearofthelephant.org ambapo watu huweza kujitengenezea picha zao na kuzitumia kwenye mitandao ya jamii.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Michael Kagondela (kulia) akimuonesha Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi eneo ambalo mchezaji bora wa Afrika, Mbwana Samatta atapimiwa ekari tano na kukabidhiwa na mtandao huo kwa ajili ya kujenga chuo cha wanamichezo, Mkuranga mkoani Pwani. Picha na Mpiga picha Wetu.
  ……………………………………
  Na Mwandishi Wetu, Mkuranga

  MKURUGENZI wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi ameupongeza uongozi wa Mtandao wa wasanii Tanzania (SHIWATA)kumpatia uanachama wa heshima na kumzawadia ekari tano za eneo la ardhi mchezaji bora wa Afrika, Mbwana Samatta ili ajenge kituo cha kuendeleza michezo nchini.

  Akizungumza na Katibu Mkuu wa SHIWATA, Michael Kagondela katika kijiji cha Wasanii Mwanzega, Mkuranga juzi, Madadi ambaye pia ni mwanachama wa SHIWATA alisema huo ni motisha mzuri utakaowavutia wachezaji wengine kujibidiisha kuiga nyayo za Samatta.

  Alisema Samatta amefungua njia kwa wachezaji wengine ambao kuanzia sasa watajitahidi kuonesha vipaji vyao binafsi ambavyo matokeo yake vinageuka kuwa lulu katika sura ya Afrika na dunia.

  Naye Katibu Mkuu wa SHIWATA, Kagondela alisema mtandao huo unaomiliki ekari 300 kwa ajili ya kujenga makazi na viwanja vya burudani na kumbi za starehe inatarajia kupata wawekezaji kuwekeza katika fani mbalimbali za michezo.

  Alisema kutoka Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anna Wambura alipotembelea kijiji cha wasanii Mkuranga hivi karibuni ahadi zake za kuwapatia huduma za jamii za umeme, barabara na maji zimekuw2a kichocheo kwa wasanii kujenga nyumba zao kwa kasi.

  Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib alisema wameanza kutekeleza rai ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga aliyoitoa hivi karibuni akiwataka SHIWATA kuandaa tamasha kubwa mwaka huu litakalowakutanisha wasanii wa fani zote nchini.

older | 1 | .... | 759 | 760 | (Page 761) | 762 | 763 | .... | 1896 | newer