Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

Airtel Tanzania yapanga upya muundo wa utendaji kuboresha huduma

$
0
0
Dar es Salaam Tanzania Februari 8 2016, Kampuni ya Simu za mkononi nchini Airtel Tanzania, leo imetangaza mkakati wake wa kuboresha muundo katika nafasi zote za utendaji kuwa bora zaidi na kuweka idadi sahihi ili  viwango vya kiutendaji  kuimarika na hatimae dhamira yake ya pkibiashara ya kutoa huduma na bidhaa bora za kimawasiliano nchini Tanzania kufikiwa.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano alisema “ Mkakati huu wa kuboresha upya mfumo wa utendaji  wa kampuni yetu ni sambamba kabisa na mfumo wetu wa maboresho uliowekwa na kampuni yetu ambao tunaamini baada ya muda mfupi utakuwa na mafanikio makubwa kwa wadau wote wakiwemo wafanyakazi na wateja wetu tunaowahudumia”

Singano akifafanua alisema “Maboresha haya tunayofanya yatawahusisha takribani wafanyakazi 55  kwa nafasi zao za utendandaji kutokuwepo au kuhamishiwa kwa wadau watakao toa huduma kwa kampuni yetu, mfumo ujulikanao kama “outsource model”,  watoa huduma tutakaowapa jukumu la kusimamia baadhi ya huduma zetu”
Airtel tangu kuanza kwa mkakati huu wa maboresho yake ya kiutendaji kwaajili ya kutimiza malengo ya kibiashara imejizatiti kwa kuweka miundombinu madhubuti kwa kuingia mikataba ya kiutendaji.
“Vilevile kama njia ya kushirikiana na wale watakao guswa na zoezi hili la marekebisho ya mfumo huu kipindi hiki cha  mpito, Airtel tayari imeingia mkataba na kampuni inayohusiana na huduma za rasilimaliwatu ili kutoa mafunzo na ushauri wa kutosha ya jinsi ya kutafuta na kuzipokea nafasi zingine zinazojitokeza, Malipo ya huduma hii kwa wote watakaohitaji yamegaramiwa na Airtel” alimaliza kwa kusema Bi, Singano   .


WAZIRI UMMY MWALIMU AWASHUKIA WANAOTOA HUDUMA ZA AFYA KINYUME CHA SHERIA

$
0
0
Na Beatrice Lyimo- Maelezo

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameyataka Mabaraza na Bodi za kitaalamu za masuala ya afya kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wataalam na vituo vinavyotoa huduma za afya kinyume cha Sheria.

Waziri Ummy ametoa agizo hilo alipokuwa akizindua Baraza la Optimetria, Baraza la wataalamu wa Radiolojia pamoja na Bodi ya Maabara binafsi leo jijini Dar es salaam.

Alisema kisheria Mabaraza na Bodi za Kitataalam ndivyo vyombo vinavyofuatilia ubora wa huduma za Afya pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuwaepuka watoa huduma batili wasiokuwa na utaalam na ujuzi wala kukidhi vigezo vya utoaji huduma vilivyowekwa kisheria. 

“Siku hizi kumekuwa na matumizi makubwa ya vyeti vya kugushi vikiwemo vya vituo vya kutolea huduma na wataalamu, watu wasio na taaluma wanatoa huduma kinyume na sheria hivyo Mabaraza na Bodi  mna mamlaka ya kuwachukulia hatua za kinidhamu,” Alisema Waziri Ummy.

Aidha, alisema kuwa Serikali haitasita kuyachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuvunja Bodi au Mabaraza yatakayoshindwa kutekeleza majukumu yaliyoainishwa katika sheria iliyohusika kuyaanzisha.

Aliyataka mabaraza hayo kuhakikisha kuwa yanatoa Elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na ufahamu kuhusu huduma bora za afya zitolewazo na wataalamu  husika.

“Wananchi wakielimishwa wataepuka  watoa huduma batili wasiokuwa na utaalamu na ujuzi hivyo mabaraza na Bodi vinapaswa kuhakikisha mambo haya hayatokei  kwani vinauwezo mkubwa wa kufuatilia masuala haya kwa mujibu wa Sheria”alifafanua Waziri Ummy.

Akizungumza kuhusu utendaji kazi wa wataalamu hao Waziri Ummy amewataka wataalamu hao kujiendeleza kielimu kwani utaalamu bila kuwa na ujuzi ni butu hivyo suala la elimu lipewe kipaumbele.

Mbali na hayo Waziri ameitaka Mabaraza na Bodi kuhakikisha wataalamu wote, vifaa na vitendanishi vinasajiliwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa.

TAMKO LA WIZARA YA AFYA KUHUSU KIPINDU PINDU

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka watendaji wa Serikali na Sekta ya Afya kuwajibika ipasavyo kwa  kutoa taarifa sahihi juu ya idadi ya wagonjwa wa kipindupindu nchini.

Akitoa tamko kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa kipindupindu nchini pamoja na tahadhari ya ugonjwa wa Zika leo jijini Dar es salaam Mhe. Ummy amesema kuwa watendaji watakaoficha taarifa za wagonjwa katika maeneo yao watawajibishwa.

“Mojawapo wa changamoto katika mapambano ya kudhibiti mlipuko huu wa kipindupindu ni utoaji wa idadi pungufu au kutotoa kabisa taarifa za wagonjwa wa kipindupindu hivyo kupelekea kutokuwa na mafanikio katika mikakati iliyowekwa” alisema Waziri Ummy

 Aidha, ametoa wito kwa sekta nyingine kushirikiana na Wizara kupambana na ugonjwa huo ili kukabiliana  na baadhi ya changamoto zinazowakabili watoa huduma za afya na elimu walioko katika maeneo mbalimbali nchini.

“ Jukumu la kupambana na mlipuko wa ugonjwa huu si la Wizara ya Afya pekee  naomba sekta nyingine ikiwemo Maji, Miondombinu, Biashara Elimu na Mazingira tushirikiane kwa pamoja ili kuutokomeza ugonjwa huu” 

Mbali na hayo Mhe. Ummy ameeeleza kuwa takwimu za kuanzia tarehe 1 hadi 7 februari mwaka huu zinaonyesha kuwa idadi ya wagonjwa wa kipindupindu imepungua kutoka 459 ya wiki iliyoisha tarehe 31 Januari hadi 258 ambapo ni sawa na punguzo la asilimia 44%.

Hata hivyo Wizara imewatoa hofu wananchi na kuwakumbusha kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Homa ya Zika pamoja na magonjwa mengine yanayoenezwa na Mbu.

KAMATI KUU YAFANYA UTEUZI WA WAGOMBEA WATAKAOZIBA NAFASI ZILIZOACHWA WAZI CCM

$
0
0
Katibu wa Itikadi na Uenezi Mhe. Nape Nnauye akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM, Ofisi Ndogo Lumumba.

Jana tarehe 07/02/2016 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ilikuwa na kikao maalum cha siku moja mjini Dodoma. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Kikao hicho kilikuwa na kazi ya kuteua wagombea wa nafasi mbalimbali zilizo wazi za uongozi ndani ya CCM mikoani na wilayani ambazo uteuzi wake upo kwenye Mamlaka ya Vikao vya Chama Taifa.

Nafasi hizi wazi zimetokana na sababu mbalimbali zikiwemo vifo na baadhi ya viongozi kukihama Chama na kujiunga na vyama vingine. Hivyo, nafasi zilizofanyiwa uteuzi na wagombea wake ni kama ifuatavyo:-

I.     UENYEKITI WA CCM MKOA.
1.      ARUSHA 
(i)      Michael Lekule Laizer
(ii)     Emanuel Makongoro Lusenga
(iii)   John Pallangyo

2.   SHINYANGA
(i)      Hassan Ramadhani Mwendapole
(ii)     Mbala Kashinje Mlolwa
(iii)   Erasto Izengo Kwilasa


3.   SINGIDA
(i)    Hanje Narumba Barnabas
(ii)   Misanga Mohamed Hamis
(iii)  Mlata Martha Moses
(iv)  Kilimba Juma Hassan

  
II.     UJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA NEC

1.       NYAMAGANA

(i)    DR. Sillinus Elias Nyanda
(ii)   Jamal abdul Babu
(iii)  Kelebe Bandoma Lutelil
(iv)  Patrick Kambarage Nyabugongwe

2.       KAHAMA

(i)   Pili Yakanuka Izengo
(ii)  Paschal Ndibatyo Mayengo
(iii) Sweetbert Charles Nkuba

3.       MONDULI

(i)  Namelock Edward Sokoine

III.    UENYEKITI WA CCM WILAYA

1.       MONDULI

(i)  Loata Erasto Sanare

2.       SUMBAWANGA MJINI

(i)  Chami Slegried Mask
(ii) Godfrey Mwimanzi Mwikala


IV.     KATIBU WA UCHUMI NA FEDHA MKOA WA KILIMANJARO

(i)    Shadrack Amani
(ii)   Chata Madata Joseph
(iii)  Karia Ahmed Mahamoud

V.      KATIBU WA SIASA NA UENEZI MKOA WA ARUSHA

(i)   Semmy Rabson Kiondo
(ii)  Shaban Omari Mdoe
(iii) Veraikunda Zablon Urio


VI.     UENYEKITI WA UVCCM WA MKOA

1.   ARUSHA

(i)     Erick Edward
(ii)            Lengai Loy Thomas
(iii)          Mwanzani Omar

  2.   KILIMANJARO

(i)      Amaly T.Mathew
(ii)     Frank Lumisha Nkya
(iii)   Juma Rahibu Juma

2.   SHINYANGA
                (i)   Mabembela Joseph Elias
                (ii)  Mipanda kali Dalushi
                (iii) Ndasa Jeremiah Damian
                (iv) Shigela Reubeen Bernard

Ratiba ya chaguzi hizo itatolewa wiki hii mwishoni.

Kamati Kuu pia imepokea taarifa ya maandalizi ya uchaguzi wa marudio Zanzibar na kuridhishwa na maandalizi hayo na kuwatakia kila la kheri Wazanzibar katika Uchaguzi huo. 

Wakati huo huo, Kamati Kuu imetoa pole kwa Jeshi la Polisi nchini kufuatia vifo vya Askari Polisi watatu vilivyotokea tarehe 06/02/2016 mjini Singida kutokana na ajali wakati Askari hao wakitimiza wajibu wao kwenye maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM. Kamati Kuu inawapa pole wafiwa wote na kuwaombea majeruhi wote kupona haraka.


Imetolewa na:-


Nape Moses Nnauye
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
08/02/2016

NSSF YAZINDUA MPANGO WA AKIBA NA AFYA KWA WANAFUNZI WA VYUO.

$
0
0
 Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (kushoto) akimkabidhi mfano wa kadi ya uanchama wa NSSF, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Rajabu Mahumba wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa AKIBA na AFYA 'AAPLUS' kwa wanafunzi wa vyuo hafla hiyo ilifanyika Chuo Kikuu cha Dodoma, mwishoni mwa wiki.
 (Picha na Francis Dande)
 Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed akimkaribisha Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde kwenye uzinduzi wa Mpango wa Hifadhi ya Jamii kwa Wanafunzi 'AAPLUS', uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). 
 Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde akipeana mkono na Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa NSSF wa Akiba na Afya kwa Wanafunzi wa Vyuo, uliofanyika UDOM. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Mariam Ahmed.
 Baadhi ya maofisa wa NSSF wakifuatilia uzinduzi huo.

Meza Kuu.
Wanafunzi.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa NSSF wa Akiba na Afya kwa Wanafunzi wa Vyuo.
Baadhi ya waafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde.  
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed.
Mshauri wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dick Manongi akizungumza katika uzinduzi huo. 
 Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mpango wa NSSF wa Akiba na Afya kwa Wanafunzi wa Vyuo uliofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma. 
 Wakifuatilia uzinduzi huo.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma akitoa mada wakati wa uzinduzi wa mpango wa Akiba na Afya 'AAPLUS' kwa wanafunzi wa vyuo.
Mwanafunzi wa UDOM, Mishi Jumanne akiuliza swali kuhusu uanachama wa NSSF.
 Wanafunzi wakipimwa afya katika viwanja vya chuo cha UDOM.
 Dk. Leilah Manga wa Kituo cha Afya Chuo Kikuu cha Dodoma akipima mapigo ya moyo ya mwanafunzi wa UDOM, Hoza Ernest 
Wanafunzi wakijaza fomu za kujiunga na NSSF.
 Ofisa Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Issa Salim (kulia) akitoa maelekezo kwa wanafunzi wa UDOM waliojiunga na NSSF.
Ofisa Mwandamizi Idara ya Matekelezo, Abubakar Soud (katikati) akiwaelekeza namna ya kujaza fomu ya kujiunga na NSSF, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakati wa uzinduzi wa mpango wa Akiba na Afya 'AAPLUS' kwa wanafunzi wa vyuo uliofanyika katika chuo hicho, mwishoni mwa wiki.

Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (katikat) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa NSSF pamoja na baadhi ya wanafunzi wa UDOM.
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde akiagana na Ofisa Matekelezo Mwandamizi wa NSSF, Abdul Mzee.

KAMATI KUU YAFANYA UTEUZI WA WAGOMBEA WATAKAOZIBA NAFASI ZILIZOACHWA WAZI CCM

WADAU MBALI MBALI WAJIZOLEA ZAWADI ZA WAFANYE WATABASAMU

$
0
0
Marafiki mbalimbali wa Programu ya Wafanye Watabasamu, hivi karibuni wamejitwalia zawadi za michoro ya ukutani iliyochorwa na Mchora vibonzo maarufu ambaye pia ni Mratibu wa programu hiyo, Nathan Mpangala aka Kijasti, baada ya kuposti mara nyingi kwenye mitandao ya kijamii bango lililokuwa likihamasisha watu kujitokeza kwa wingi kwenye onesho la michoro lililoandaliwa na Nafasi Art Space ya jijini Dar es Salaam, wiki iliyopita. Pichani Mpangala aliyevaa suruali ya rangi ya Wekundu wa Msimbazi, akimkabidhi zawadi Mjasiriamali, Bi. Joyce Athanas huku wakishuhudiwa na marafiki mbalimbali hivi karibuni. Wengine Waliojitwalia zawadi hizo (hawapo pichani) ni Jesca Haule, Kanuni Midundo, Linah Mrimia, Orest Kawau wa Magic Fm na Othman Michuzi wa Michuzi Blog.
Mchoraji nguli nchini, Komredi Lute Mwakisopile (mwenye kifriji), akidakishwa zawadi yake toka kwa Mratibu wa Wafanye Watabasamu, Nathan Mpangala.
Mratibu wa Wafanye Watabasamu, Nathan Mpangala (anayekaribia paa), akimzawadia mchoro wa kupamba ukutani Meneja mafunzo, motisha na mawasiliano wa Vodacom, Bi. Belinda Wera.
Mjasiriamali Bi. Nana Mzobora wa Dar es Salaam akijitwalia yake.
Meneja masoko wa Nafasi Art Space, Kelvin Kyando akidaka ya kwake. 

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATOA TAARIFA YA MFUMUKO WA BEI LEO

$
0
0
Mkurugenzi wa Sensa za Jamii na Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephrahim Kwesigabo akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa bei mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira Bi. Ruth Minja.(Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo)
Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Ruth Minja akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa bei mapema hii leo jjijjini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi wa Sensa za Jamii na Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephrahim Kwesigabo.
Mkurugenzi wa Sensa za Jamii na Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephrahim Kwesigabo akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa beimapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira Bi. Ruth Minja.


Na; Frank Shija, MAELEZO

Matumizi ya kaya kwenye biadhaa za vyakula imepungua hadi asilimia 38.5 mwaka 2011/12 kutoka asilimia 47.8 ya mwaka 2007.ambapo kwa ujumla wake mfumuko wa Bei umepungu

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Takwimu za jamii na Sensa ya Watu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Ephraim Kwesigabo alipokuwa akizunguza na waandishi wa habari kuhusu mfumuko wa bei leo jijini Dar es Salaam.

Kwesigabo alisema kuwa kutokana na mwenendo huo kunaashiria kupungua kwa umasikini wa kipato kwenye kaya kwa kuelekeza matumizi mengine bidhaa zisizo za vyakula kama usafiri, mawasiliano, makazi, maji na nishati.

“Matokeo yanaonyesha kwamba mizania ya matumizi ya kaya kwenye bidhaa za vyakula imepungua hadi asilimia 38.5 mwaka 2011/12 kutoka asilimia 47.8 mwaka 2007” Alisema Kwesigabo.

Aliongeza kuwa makundi mengi mengine yaliyoonyesha kuwa na mizania mikubwa ya matumizi ya kaya mwaka 2011/12 kuwa ni pamoja na Usafi asilimia 12.5 kutoka asilimia 9.5 mwaka 2007, Makazi Maji na Nishati asilimia 11.6 kutoka asilimia 9.2 mwaka 2007 na Mavazi na Viatu asilimia 8.3 kutoka asilimia 6.7 mwaka 2007.

Aidha kumekuwa na ongezeko la Zaidi ya mara mbili ya matumizi ya kaya kwenye kundi la Mawasiliano asilimia 5.6 ikilinganishwa na asilimia 2.1 ya mwaka 2007

Kwa upande wake Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bibi. Ruth Minja amevitaja baadhi ya vigezo muhimu vinavyotumika kupata Fahirisi za Bei zinzoonyesha uhalisia wa matumizi ya kaya binafsi kuwa ni pamoja na mizania katikia bidhaa na huduma muhimu ikiwemo Vyakula, afya, Usafiri ,Maji na Nishati.

Aliongeza kuwa ili kupata matokeo ya mfumuko wa Bei kumekuwa na mtindo wa kufanya marejeo baada ya kila miaka mitano ambapo marejeo ya mwisho yalifanyika mwaka 2007 na kuonyesha matumizi makubwa ya kaya yalikuwa kwenye bidhaa za vyakula zikiwa na asilimia 47.8 ya matumizi yote yakifuatiwa na usafiri asilimia 9.5 huku matumizi madogo zaidi yalikuwa ni huduma za afya kwa asilimia 0.9.

Takwimu hizi zimekuwa zikitolewa kwa mujibu wa sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 na zimekuwa zikisaidia katika kupima na kuboresha sera za kifedha na mipango ya kiuchumi ya kuthibiti mfumuko wa bei, kukadiria pato la Taifa,kuboresha mishahara ya wafanyakazi na mafao ya wafanyakazi waliostaafu.

MKUTANO WA WADAU WA UWEZESHAJI KUFANYIKA KESHO FEBRUARI 9 MWAKA HUU.

$
0
0
BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

 MKUTANO WA WADAU WA UWEZESHAJI UTAKAOFANYIKA TAREHE 9/02/2016.
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) lilianzishwa mwaka 2005 kwa Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (Sheria na. 16 ya Mwaka 2004) chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Baraza ni chombo cha juu kitaifa cha kuratibu, kusimamia, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004.
Katika kutekeleza Sera ya Taifa ya Uwezeshaji, Baraza limeshaandaa Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Mwongozo wake unaohusisha sekta zote nchini.

 Ili kufanikisha utekelezaji wa mkakati huo, Baraza limeandaa Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambao ni muundo rasmi katika kutekeleza Mkakati wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi. Mkutano huu ni sehemu ya Uratibu na utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji ambao unahusisha wadau mbali mbali ambao ni Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Mamlaka za Serikali za Mitaa, mashirika yasiyo ya kiserikali na sekta binafsi.

Mkutano huu wa Wadau wa Uwezeshaji utafunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Majaliwa Kassim Majaliwa (MB), tarehe 9/02/2016 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere.

MAJUKUMU YA BARAZA
                     i.        Kuandaa Mpango Mkakati wa Kisekta na kuhamasisha matumizi ya rasilimali kwa shughuli za uwezeshaji wananchi;
                    ii.        Kuhamasisha na kuhimiza uwekaji wa akiba, uwekezaji na ushirikishwaji makini wa wananchi kwenye shughuli za kiuchumi;
                   iii.        Kusimamia, kuongoza na kubaini vyanzo vya fedha kwa ajili ya Mfuko wa udhamini mikopo ya uwezeshaji ;
                   iv.        Kuwezesha na kuratibu mafunzo ya ujasiriamali kwa vikundi mbalimbali vya wananchi kutegemeana na mahitaji na changamoto zinazowakabili;
MALENGO YA MKUTANO WA WADAU WA UWEZESHAJI
  1. Kukutanisha wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kutoka sekta za umma na binafsi hapa nchini,
  2. Kujadili taarifa ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi;
  3. Kutambua  juhudi za wadau wanaotekeleza Sera ya Taifa ya Uwezeshaji;
  4. Kujaidili changamoto na kuibua mbinu bora za utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi;
  5. Kuhamasisha juhudi mbali mbali za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi,
MATARAJIO
Kupitia Mkutano huu wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Baraza lina matarajio yafuatayo;
i.        Kuanza rasmi kwa  Dawati la Uwezeshaji na Ushiriki wa Wananchi kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa, Wizara na Idara katika kufuatilia masuala ya Uwezeshaji, kuandaa taarifa na kuwasilisha katika kamati husika kwa maafikiano na kuwasilisha katika Baraza la Taifa la Uwezeshaji;
ii.        Taasisi za umma na binafsi kuwahudumia wananchi kwa ufanisi bila upendeleo pale wanapohitaji kuwezeshwa kupitia huduma wanazozitoa katika utendaji wao wa kila siku;
iii.        Kuratibu majukumu ya Uwezeshaji kwa kuzingatia uwajibikaji, uadilifu, uaminifu na kujali;
iv.        Kuchochea hamasa na kuhakikisha kuwa wananchi wanapewa upendeleo wa pekee kwa watoa huduma mbalimbali katika zabuni na miradi mikubwa katika maeneo yao pale wanapokidhi vigezo na masharti ya zabuni husika.
v.        Kila kiongozi kuhakisha kuwa rasilimali zilizotengwa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuwezeshaji wananchi kiuchumi zinaelekezwa katika miradi hiyo na kutumika kwa kuzingatia thamani ya pesa na miradi yenyewe;
Baraza linapenda kuwashukuru wadhamini wa Mkutano huu ambao ni (Mradi wa Ushindani wa Sekta Binafsi (Private Sector Competitiveness Project), World Vision Tanzania, Benki ya Maendeleo ya TIB (TIB Development Bank), Benki ya Posta, Benki ya CRDB, UTT Microfinance, Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma (PSPF), Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Serikali za Mitaa (LAPF), Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF) na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

KIDOGO CHA UCHANGIAJI DAMU CHA MBAGALA RANGI TATU JIJINI DAR CHAZINDULIWA LEO.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadic akizungumza leo katika uzinduzi wa Kituo cha Damu salama kilichopo Mbagara Rangitatu jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadic akikata utepe kuzindua kituo cha uchangiaji Damu salama cha Mbagala langitatu jijini Dar es Salaam leo.
Wananchi wakijitolea damu katika kituo cha Rangi tatu jijini Dar es Salaam leo.
MPANGO wa Taifa wa damu salama nchini ulio chini ya wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia, wazee na watoto  leo wamezindua kituo kidogo cha uchangiaji damu kilichopo Mbagala Rangi tatu. Uzinduzi huu unaambatana na uzinduzi wa vituo vingine vya afya vilivyopo wilaya zote za mkoa wa Dar es salaam kama vile Amana, Mwananyama, Sinza, Vijibweni na Mbweni.


Viituo hivi vimejengwa kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali ambao ni Hospitali ya CCBRT, Hospital ya Mbweni Mission MDH, Umoja wa wamiliki hospital binafsi (APHTA) NA Halmashauri za temeke Ilala na Kindondoni.  Vilevile  Mpango wa Taifa wa Damu salama unawapongeza wachangia damu kwa hiari ambao  wamekuwa wakichangia damu mara kwa mara ili kuokoa maisha ya wahitaji tangu kampeni hii ilipoa nza rasmi tarehe 3 februari 2016.

Maisha ya watu wengi yanaokolewa kila mwaka nchini kwa kuongezewa damu . Nchini Tanzania kinamama wengi na watoto hupoteza maisha kwa kukosa damu. Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha  kuwa nchini Tanzania takriban wanawake 432 kati ya vizazi hai 100,000 hufa kila mwaka kutokana na uzazi na asilimia 80 ya hivyo vifo husababishwa na ukosefu wa damu. Hivyo ufunguzi wa vituo hivi utasaidia kuondoa tatizo la uhaba wa damu na hatimaye kutokomeza tatizo la vifo vinavyotokana na kukosa damu.

Katika mkoa wa Dare s Salaam mahitaji ya damu ni makubwa , kwa mwezi tunahitaji chupa 4000 lakini zinazopatikana ni chupa 2000 tu ambayo ni nusu ya mahitaji. Kuna wakati mahitaji haya yanakuwa makubwa zaidi na hivyo upungufu huongezeka kufikia asilimia 70, hali ambayo ni hatari kwa maisha ya binadamu.

Damu ni uhai na haipatikani kwa njia yeyote ile isipokuwa  kwa kuchangiwa na binadamu wenzetu . Uchangiaji damu ni zoezi endelevu na la kudumu kwakuwa damu huhifadhiwa kwa muda wa siku 35 tu tangu inatolewa . Kutokana na uhifadhi wa damu kuwa ni wa muda mfupi ndio maana inasisitizwa umuhimu wa watu kuchangia damu walau mara mbili kwa mwaka.




  











WAZIRI MBARAWA AWATAKA AIR TANZANIA KUANZA KUFANYA KAZI.

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa,akisisitiza jambo kwa Menejimenti ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), alipokutana nao kabla ya kuongea na Wafanyakazi.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (mwenye koti la kaki), akisisitiza jambo kwa Wafanyakazi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL),alipokutana nao jijini Dar es Salaam.
 Rubani Lilla Borri wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa Wafanyakazi wa Shirika hilo na Waziri Prof. Mbarawa, uliofanyika  katika ofisi za Shirika hilo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akiagana na Wafanyakazi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), mara baada ya kuongea nao Ofisini Hapo.

SERIKALI imezungumzia umuhimu wa kulifufua upya Shirika la Ndege nchini Air Tanzania (ATC) kwa kulinunulia ndege mpya na kulipa mtaji ili lifanye kazi kibiashara na kutengeneza faida kama ilivyokusudiwa awali.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (Pichani)ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na menejimenti na wafanyakazi wa Shirika hilo alipolitembelea jijini Dar es Salaam leo.


“Tutawekeza kwenye Air Tanzania ili kuongeza fursa za kiuchumi na kuvutia wasafiri wengi kufika nchini moja kwa moja na kuvutia sekta ya utalii”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.


Waziri Prof. Mbarawa amewataka wafanyakazi wa Shirika hilo ambao sio waadilifu na wavivu kuondoka mara moja ili kupisha wafanyakazi wabunifu na wenye mawazo ya kibiashara kuendesha shirika hilo kwa faida.


“Tunataka watu watakaolitoa shirika hili kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa kuliwezesha kiuchumi na kujitegemea ili kushindana na mashirika mengine ya ndege katika biashara“, amesisitiza Prof. Mbarawa.


Prof. Mbarawa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli yuko tayari kununua ndege mpya ili kulifufua shirika hili hivyo amewataka wafanyakazi hao kuwa na mtazamo chanya wa kufanya biashara ili kuiletea taifa tija.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ATC Bw. Johnson Mfinanga amemwambia Waziri Prof. Mbarawa kuwa kwa sasa shirika hilo lipo katika hali mbaya kiuchumi na hivyo kuhitaji nguvu ya Serikali kulikwamua ili litoe huduma inayoshahili.


Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amesisitiza kuwa Serikali itaangalia upya taratibu za ajira katika shirika hilo na watakaobainika kuajiriwa kinyume cha taratibu watafukuzwa kazi mara moja.


“Tutanataka watu waadilifu, wabunifu na wenye sifa stahiki ili wafanye kazi kwa maslahi ya shirika na taifa kwa ujumla”, amefafanua Waziri Mbarawa.


Shirika la Ndege nchini ATC toka mwaka 2009 limekuwa likijiendesha kwa hasara na Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kulifufua shirika hilo ili lifanye kazi kwa faida na kuboresha usafiri wa anga ndani na nje ya nchi na hivyo kuvutia wasafiri wengi kuja nchini moja kwa moja.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

MATUMIZI YA BIDHAA YA VYAKULA YAMEPUNGUA -NBS

$
0
0
 Mkurugenzi wa Sensa za Jamii na Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephrahim Kwesigabo akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa bei mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira Bi. Ruth Minja.

Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Ruth Minja akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa bei mapema hii leo jjijjini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi wa Sensa za Jamii na Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephrahim Kwesigabo.


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
MATUMIZI ya kaya kwenye bidhaa za vyakula imepungua hadi asilimia 38.5 mwaka 2011/2012 kutoka asilimia 47.8 ya mwaka 2007. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Takwimu za jamii na Sensa ya Watu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo amesema kuwa kutokana na hali hiyo kunaashiria kupungua kwa umasikini wa kipato kwenye kaya kwa kuelekeza matumizi mengine bidhaa zisizo za vyakula kama usafiri, mawasiliano, makazi, maji pamoja na nishati. 

Amesema matokeo yanaonyesha kwamba mizania ya matumizi ya kaya kwenye bidhaa za vyakula imepungua hadi asilimia 38.5 mwaka 2011/2012 kutoka asilimia 47.8 mwaka 2007.

Amesema kumekuwa na ongezeko la zaidi ya mara mbili ya matumizi ya kaya kwenye kundi la Mawasiliano asilimia 5.6 ikilinganishwa na asilimia 2.1 ya mwaka 2007. 

Nae Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ruth Minja amesema baadhi ya vigezo muhimu vinavyotumika kupata Fahirisi za bei zinzoonyesha uhalisia wa matumizi ya kaya binafsi kuwa ni pamoja na mizania katika bidhaa za huduma muhimu ikiwemo Vyakula, afya, Usafiri, Maji na Nishati. 

DKT MAHIGA AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI KUWAANDALIA MABALOZI MCHAPALO WA MWAKA MPYA (SHERRY PARTY) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akihutubia wakati akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika Mchapalo wa Mwaka Mpya kwa Mabalozi na Wawakilishi wa Taasisi mbalimbali za Kimtaifa maarufu kama "Sherry Party" Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu February 8, 2016
Mabalozi na Wawakilishi wa Taasisi mbalimbali za Kimtaifa wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akihutubia wakati akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika Mchapalo wa Mwaka Mpya maarufu kama "Sherry Party" Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu February 8, 2016 
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja Mabalozi na Wawakilishi wa Taasisi mbalimbali za Kimtaifa jijini Dar es Salaam leo.

MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI AMTEMBELEA MUFTI MKUU WA TANZANIA SHEIKH ABUBAKAR ZUBEIRY HOSPITALI MUHIMBILI.

$
0
0
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimjulia hali Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry aliyelazwa kwa matibabu katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Pamoja naye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mhe Ummy Mwalimu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Masaju pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa Mohamed Janabi leo Jumatatu February 8, 2016.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisindikizwa wakati wa kuondoka baada ya kumjulia hali Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry aliyelazwa kwa matibabu katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Pamoja naye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mhe Ummy Mwalimu na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa Mohamed Janabi leo Jumatatu February 8, 2016.

SHUKRANI YA FAMILIA YA GOGADI NA MBUGUNI.

$
0
0
SHUKRANI 
FAMILIA YA GOGADI NA MBUGUNI INATOA SHUKRANI ZA DHATI KWA WOTE WALIOSHIRIKI KATIKA KUTUFARIJI HADI MAZISHI YA BABA YETU MPENDWA MAREHEMU DEUSDEDIT GOGADI ALIYEFARIKI GHAFLA TAREHE 31 DECEMBER, KWA KUWA SIYO RAHISI KUMSHUKURU MMOJA MMOJA TUNAOMBA SHUKRANI ZETU ZIWAFIKIE WOTE.  

MKESHA WA KUOMWOMBEA MAREHEMU BABA YETU UTAFANYIKA NYUMBANI KWAKE KIJITONYAMA TAREHE 12 IJUMAA NA KUFUATIWA NA IBADA YA SHUKRANI KATIKA KANISA LA MWENGE ROMAN CATHOLIC TAREHE 13 SAA 12.30 ASUBUHI. RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA NA NURU YA DAIMA IMWANGAZE APUMZIKE KWA AMANI AMEN.

KAMUSOKO MCHEZAJI BORA MWEZI DISEMBA.

$
0
0
MCHEZAJI Thaban Kamusoko amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Disemba, 2015 baada ya kumshinda mchezaji mwenzake wa Yanga (Amissi Tambwe).

Kamusoko ameisaidia timu yake ya Yanga katika michezo iliyochezwa mwezi Disemba kwa kushiriki dakika zote katika michezo mitatu iliyochezwa mwezi wa Disemba.


Kwa kuchaguliwa kwake kuwa mchezaji bora wa wa mwezi Disemba, Kamusoko atakabidhiwa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni moja (1,000,000) kutoka kwa wadhamini wa ligi Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

TANZANIA KUENDELEZA UTAFITI WA BIOTEKNOLOJIA

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Uvuvi, Dk. Florens Turuka (kulia), akizungumza na watafiti wa kilimo Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akifungua mkutano wa nane wa mradi wa mahindi yanayostahimili ukame na kupambana na wadudu waharibifu wa Wema wa siku tatu wa watafiti kutoka nchi za Afrika wa kutathimini utendaji kazi wa Wema kwa mwaka uliopitaKushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Uharishaji wa Teknolojia za Kilimo (AATF), Dk. Denis Kyetere na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Hassan Mshinda.
Mkurugenzi wa Ushirikiano Mradi wa Wema, Kampuni ya Monsanto, Mark Edge (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Ofisa Mkuu wa Programu, Taasisi ya Bill and Melinda Gates Dk.Lawrence Kent (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
Meneja Mradi wa Wema, Shirika la Kimataifa la Uhaurishaji wa Teknolojia za Kilimo (AATF), Sylvester Oikeh akizungumza katika mkutano huo.
Mtafiti wa Mahindi, Shirika la Kimataifa la utafiti wa ngano na mahindi (CIMMYT), Yoseph Beyene akizungumza kwenye mkutano huo.
Meneja Mfumo na Uzalishaji wa Mbegu (AATF), Gospel Omanya akitoa mada katika mkutano huo.
Watafiti na washiriki wakiwa kwenye mkutano huo.
Watafiti na washiriki wakiwa kwenye mkutano huo.
Watafiti na washiriki wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Hapa ni kazi tu za utafiti.
Watafiti na washiriki wakiwa Busy na nyaraka.

Watafiti wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi. 


Na Dotto Mwaibale

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Florens Turuka amesema Serikali ya Tanzania itaendeleza utafiti wa bioteknojia pamoja na kutekeleza mradi wa WEMA kwa hatua. Mradi huo unajishughulisha na utafiti wa mbegu za mahindi nchini.

Turuka ameyasema hayo kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo, wakati akifungua mkutano wa nane wa mradi wa mahindi yanayostahimili ukame na kupambana na wadudu waharibifu wa WEMA, leo asubuhi jijini Dar es salaam. Mkutano huo wasiku tatu umewaleta pamoja watafiti kutoka nchi za Afrika, kutathimini utendaji kazi wa mradi kwa mwaka uliopita.

Alisema awamu ya utafiti wa njia ya kawaida wa mahindi imekamilika na aina sita mpya za mahindi zimepatikana na kuwa hivi sasa kwa kufuata kanuni za usalama wa viumbe, itaanza utafiti wa mahindi kwa njia ya uhandisi jeni.

"Sera na kanuni zipo, tutafanya utafiti wa GMO na matokeo ya utafiti yatatoa mwongozo wa dira yetu ya kilimo" alisema Dk. Turuka.Katika hatua nyingine Dk. Turuka amewataka watafiti wa mbegu za mahindi nchini kuhakikisha mbegu bora walizozifanyia utafiti zinawafikia wakulima kwa wakati.

"Serikali inafurahishwa na mradi huu wa WEMA kwani unamsaidia mkulima kupata mbegu bora ambazo zinahimili ukame na haziwezi kushambuliwa na magonjwa" alisema Dk.Turuka.

Alisema kwa kutumia mbegu bora zilizotokana na utafiti huo mkulima anaweza kupata tani 8.5 za mahindi kwa ekari moja na kusisitiza kuwa mbegu hizo zisipo mfikia mkulima kwa wakati mradi huo utakuwa haujaisaidia serikali.

Dk. Turuka alisema serikali inaangalia kwa karibu sheria na kanuni za kuwapa uwanja mpana watafiti bila ya kuharibu mazingira na kuhatarisha maisha ya wananchi wakati wa kufanya tafiti zao.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk.Hassan Mshinda alisema tafiti hizo za mbegu zinatoa nafasi kwa wakulima kupata mbegu bora na kuwa utafiti huo uliofanywa kwa kushirikiana na watafiti kutoka nchi mbalimbali umeonesha mafanikio makubwa.

Mratibu wa mradi huo wa WEMA, Dk.Alois Kullaya alisema mradi huo ulianza mwaka 2008 na kuwa wamekuwa wakitumia mbinu za kisasa kupata mbegu bora.

Alisema Tanzania na nchi nyingine tayari zimepasisha mbegu 59 ambapo kwa hapa nchini zipo mbegu sita tu ambazo zinazalishwa.Aliongeza kuwa kwa nchi ya Afrika Kusini wao tayari wameidhinisha matumizi ya mbegu za GMO.

MKUTANO MKUU WA 25 WA MWAKA WA PPF KUFANYIKA JIJINI DAR FEB 11 NA 12,

$
0
0
Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar.

WADAU mbalimbali,Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wanatarajia kukutana kwenye Mkutano Mkuu wa 25 wa mwaka wa mfuko huo kwaajili ya kujadili mambo mbalimbali yakiwemo ya uendelezaji wa sekta ya uhifadhi ya jamii.

Akizungumza na mtandao huu,jijini Dar es Salaam leo mchana  wakati akitoa taarifa hiyo, Meneja Uhusiano PPF, Lulu Mengele alisema kuwa mkutano huo utafanyika Februari 11 na 12 mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini hapa,huku ukihudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema pamoja na kujadili uendelezaji huo pia watajadili mafanikio ya mfuko huo kwa mwaka mzima na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko, huku Kaulimbiu ya mkutano huo ikiwa ni 'Uendelezaji wa Sekta ya Hifadhi Jamii na Umuhimu wa kuzingatia Mabadiliko'.



"Mkutano huo utafanyika na wadau mbalimbali wakiwemo Wenyeviti na wajumbe wa bodi, maofisa watendaji wakuu, wakurugenzi, wakuu wa vitengo, vyama vya waajiri, ambapo baadhi ya Wanachama watapata fursa ya kutoa ushuhuda kuhusu huduma za mfuko wa PPF" alisema Lulu

Wakati huohuo, Mengele alizungumzia mfumo maalumu wa Wote Scheme ambao unazihusisha sekta zisiyo rasmi na ule mfumo wa ziada uliopo kwenye sekta iliyo rasmi.

Alifafanua lengo kuu la mfumo huo kuwa ni kukidhi mahitaji na kutambua mchango na ushiriki wa sekta isiyo rasmi kwenye uchumi na pia kutoa fursa mbalimbali kwa wafanyakazi waliopo kwenye sekta rasmi ili kuwawezesha kunufaika na mfumo huo kwa ajili ya kukuza shughuli mbalimbali za kiuchumi  na kijamii.

Kuhusu nani anastahili kujiunga , Mengele alisema kila mtu au kikundi chenye kipato na chenye mlengo wa  kiuchumi kilichopo kwenye sekta isiyo rasmi kama vile wakulima, wafugaji, wavuvi, mama lishe, waendesha bodaboda, wajasiriamali, wadogo, wasanii, wanamichezo wachimbaji madini wadogo.

Ambapo alisema kuwa jinsi ya kuchangia kiwango cha chini kwa mwezi ni sh.20,000 ambacho kinaweza kulipwa aidha moja kwa moja kwenye akaunti ya Mfuko wa Pensheni wa PPF au kwa njia ya M-Pesa, Airtel money na Tigo pesa.

NEC YASEMA ELIMU YA MPIGA KURA HAIKUWAFIKIA BAADHI YA WANANCHI NCHINI.

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini NEC imebainisha kwamba, ukosefu wa elimu ya kutosha kwa Wapiga Kura, ulisababisha mapungufu mbalimbali kujitokeza katika uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25 Mwaka jana.


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Kailima Ramadhani (Pichani juu) aliyasema hayo jana Jijini Mwanza, katika Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.


Ramadhani alisema katika baadhi ya Kata nchini, kulitokea mapungufu kadhaa katika zoezi la kupiga kura ikiwemo Kura kuharibika kutokana na wapiga kura kuchora michoro na alaza zisizostahili katika karatasi ya kupigia kura huku baadhi yao wakiandika matusi katika karatasi hizo.


Hata hivyo Kailima alitanabaisha kwamba, zoezi la utoaji wa elimu kwa mpiga kura, lilishindwa kufanikiwa zaidi kutokana na baadhi ya Asasi za kiraia nchini kutoa elimu kinyume na mwongozi wa NEC, ambapo baadhi ya Asasi hizo zilikuwa zikitoa elimu ya mpiga kura kwa kuangazia zaidi matakwa ya wafadhiri wake.


Edwin Soko ambae ni mmoja wa Wadau kutoka Asasi zilizohudhuria katika Mkutano huo ambao umejumuisha Asasi mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa, amesema kuwa katika Uchaguzi wa Mwaka jana, Asasi nyingi hazikuweza kuyafikia maeneo mengi hususani vijijini kwa ajili ya Kutoa elimu ya Mpiga kura, hii ikiwa ni kutokana na ukosefu wa fedha ambapo wameishauri Serikali kuwa na utaratibu wa kutoa ruzuku kwa asasi hizo ili kutoa elimu hiyo katika chaguzi zijazo.


Kando ya Tathmini hiyo, Suala la Kuahirishwa kwa Uchaguzi Visiwani Zanzibar likajitokeza, ambapo Wanahabari walitaka kujua sababu za Uchaguzi huo kuahirishwa, na hapo ndipo Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka NEC akatumia tena fursa hiyo kufafanua kwamba Uchaguzi Visiwani Zanzibar uliahirishwa na Tume ya Uchaguzi Visiwani humo ZEC kutokana na tume hiyo kubaini kasoro kadhaa katika karatasi zake za wapiga kura, kasoro ambazo hata hivyo hazikujitokeza katika karatasi zilizokuwa zikisimamiwa na Tume ya Uchaguzi nchini NEC ikizingatiwa kwamba ZEC na NEC ni tume mbili tofauti zisizoingiliana katika majukumu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Kailima Ramadhani akifungua Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Kailima Ramadhani akizungumza na Wanahabari Jijini Mwanza nje ya Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Kailima Ramadhani akizungumza na Wanahabari Jijini Mwanza nje ya Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.
Wadau mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.

Wadau mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.
Wanahabari na Wadau mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.
Wadau mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.
Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Geita.
Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Kagera.
Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Mwanza.
Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Shinyanga.
Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Mara.
Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Simiyu.

MKUU WA WILAYA YA HAI,ANTHONY MTAKA ATEMBELEA KIWANDA CHA MAZIWA CHA KINA MAMA WA NRONGA WILAYANI HAI.

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akiongozana na Mchungaji wa Usharika wa Nronga,Jorome Kimaro ,kulia kwake ni katibu na meneja wa Chama cha Ushirika wa Maziwa cha Nronga Heln Ainea alipotembelea Chma hicho. 
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akiteta jambo na Katibu wa Chama cha Ushirika wa Maziwa cha Nronga Helen Ainea wakati wa mkutano mkuu wa 28 wa Ushirika huo uliofanyika katika kiwanda cha zamani cha maziwa cha ushirika huo. 
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akizungumza na wanachama wa chama cha Ushirika wa Maziwa cha Nronga wakati wa mkutano mkuu wa 28 wa Ushirika huo. 
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Ushirika wa Maziwa cha Nronga. 
Baba Mchungaji wa Usharika wa Nronga,Jorome Kimaro akitoa neno wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 28 wa Ushirika wa Maziwa wa Nronga. 
Baadhi ya wanachama. 
Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Maziwa cha Nronga wilayani Hai,Apansia Lema akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi katika mkutano wa 28 wa chama hicho. 
Baadhi ya wanachama wa chama cha Ushirika wa Maziwa cha Nronga wakimpongeza mgeni rasmi ,mkuu wa wilaya ya Hai,Athony Mtaka mara baada ya kutoa hotuba yake ikiwa ni pamoja na kushughulikia changamoto zinazoukabili ushirika huo papo hapo. 
Katibu na Meneja wa Ushirika wa Maziwa wa Nronga,Helen Ainea akimueleza jambo Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka alipotembelea kiwanda hicho. 
Kiwanda cha kwanza cha Ushirika wa Maziwa cha Nronga kilichopo Nronga-Machame wilayani Hai. 
Katibu na Meneja wa Ushirika wa Maziwa wa Nronga,Helen Ainea akimmuonesha Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka maeneo mbalimbali yanayotumika katika uandaaji wa maziwa katika kiwanda hicho. 
Katibu na Meneja wa Ushirika wa Maziwa wa Nronga,Helen Ainea akimueleza jambo Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka alipotembelea kiwanda hicho 
Mkuu wa wilaya ya Hai,Athony Mtaka akitizama bidhaa ya maziwa katika kiwanda cha Ushirika huo kilichopo Nronga -Machame. 
Bidhaa ya Maziwa ya Chama cha Ushirika cha Nronga . 
Kiwanda cha Maziwa cha Ushirika wa Maziwa cha Nronga wilayani Hai, 
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akizungumza jambo na Mwandishi wa habari James Paul alipotembelea kiwanda hicho. 
DC Mtaka akiangalia mja ya mtambo unaotumika katika uandaji wa Maziwa katika kiwanda cha Ushirika wa Maziwa wa Nronga. 
Sehemu ya mitambo hiyo.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. 
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images