Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 760 | 761 | (Page 762) | 763 | 764 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kulia), akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale (wa tatu kulia), huku Meneja wa TANROADS mkoa wa Dar es Salaam Eng. Julius Ndyamukama akifatatilia maelezo hayo.
  Muonekano wa Barabara ya Tankibovu-Goba inayojengwa kwa kiwango cha Lami kama ilivyokutwa leo mchana.
  Muonekano wa daraja la kinyerezi lenye urefu wa mita 40 ambao ujenzi wake umekamilika
  Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Dar es Salaam Eng. Julius Ndyamukama akitoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Kimara – Baruti – Msewe – Chuo Kikuu yenye urefu wa Km 2.6.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akifafanua hatua za Serikali za kuhakikisha ujenzi wa barabara za mzunguko jijini Dar es Salaam unakamilika mwezi juni mwaka huu.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema ujenzi wa barabara za mzunguko (ring roads) zenye lengo la kupunguza msongamano wa magari katikati ya jiji la Dar es Salaam utakamilika baadae Mwezi Juni mwaka huu.

  Amesema kufuatia Serikali kuanza kulipa madeni ya makandarasi amewataka makandarasi wote kurudi kazini ili kufikia lengo la Serikali la kukamilisha barabara hizo mwezi juni sambamba na ulipaji wa madeni yote.

  “Tunawaomba wale wenye nyumba pembeni mwa barabara za mzunguko ambao wapo kwenye orodha ya kulipwa fidia waondoke maeneo hayo ili kuruhusu kazi ya ujenzi wa barabara kuendelea”, amefafanua Waziri Prof. Mbarawa.

  Waziri Prof. Mbarawa amekagua barabara za Tankibovu – Goba (km9), Goba – Mbezi Mwisho (Km7), Kimara Baruti – Msewe – Chuo Kikuu (km2.6), Mbezi Mwisho – Malambamawili – Kifuru – Kinyerezi (km14), na Tabata Dampo – Kigogo (km1.6).

  Barabara hizo zenye urefu wa Km 27.2 zimejengwa kwa gharama ya takriban sh. bilioni 56.3 ikiwa ni gharama za ujenzi na fidia ambazo zote zinalipwa na fedha za mfuko wa barabara.

  Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale amewataka madereva kulinda barabara hizo kwa kutoegesha magari katika maeneo yasiyoruhusiwa na kukemea vitendo vya uchimbaji mchanga pembeni mwa madaraja.

  Waziri Prof. Mbarawa pia amekagua ujenzi wa daraja la Kinyerezi lenye urefu wa mita 40 lililojengwa kwa gharama ya sh. Bilioni 2.3 ambao ujenzi wake umekamilika.

  Barabara za mzunguko jijini Dar es Salaam zinajengwa kwa kiwango cha lami ili kuvutia magari mengi kutumia barabara hizo na kupunguza msongamano katikati ya jiji ambapo hadi sasa Km 27 zimekamilika na Km 28 zinaedelea kujengwa.

  0 0

  Kushoto ni Afisa Elimu wa Shule za Msingi wilaya ya Arumeru Tumsifu Mushi akikabidhi tuzo za Walimu Bora kwa mshindi wa Kwanza Maganga Lorry wa shule ya msingi Mbaaseny ,katikati niMkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tomorrow (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.
  Afisa Elimu wa Shule za Msingi wilaya ya Arumeru Tumsifu Mushi akizungumza katika utoaji wa tuzo za Walimu Bora ,,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.Picha na Ferdinand Shayo
  Kushoto ni Afisa Elimu wa Shule za Msingi wilaya ya Arumeru Tumsifu Mushi akikabidhi tuzo za Walimu Bora kwa mshindi wa 5 Mwalimu Clara Ernest wa shule ya Msingi Tuvaila , katikati niMkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tomorrow (TFFT)N,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo naMzawadi mbalimbali.
  washindi wa tuzo za walimu bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tommorrow (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.
  washindi wa tuzo za walimu bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tommorrow (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.
  Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tommorrow (TFFT) ,Melissa Queyquen akizungumza na walimu katika Halfa ya Utoaji tuzo za walimu bora kwa walimu wa shule za msingi wilaya ya Meru zilizofanyika jana ,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.
  washindi wa tuzo za walimu bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tommorrow (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.Picha na Ferdinand Shayo

  ……………………………………
  Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog ,Arusha.

  Serikali imetakiwa kuboresha mazingira bora ya walimu ili kukuza na kuboresha kiwango
  cha elimu nchini kwani walimu ni kiungo muhimu katika elimu ambacho kinapaswa
  kupewa kipaumbele kwenye kutimiza azma ya serikali kutoa elimu bora kwa
  Watanzania.
  Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tomorrow (TFFT) ,Melissa
  Queyquen ameyasema hayo jana wakati wa utoaji wa tuzo za walimu bora wa shule
  za msingi za serikali kwa kutambua mchango wa walimu katika maendeleo ya elimu
  nchini na ustawi bora wa jamii .

  Melisa alisema kuwa maendeleo ya taifa lolote lile yanategemea ubora wa elimu
  waliyonayo watu wake hivyo ni vyema serikali inapofikiria kuboresha elimu
  ifikirie kuboresha mazingira ya walimu kuanzia kitaaluma wanapoandaliwa kwenda
  kufundisha ,vifaa vya kufindishia pamoja na stahiki zao.

  “Bila Walimu Bora hakuna Elimu Bora ,Tumeamua
  kuwatia moyo wa walimu kwa kutoa tuzo hizi na vyeti vya kutambua mchango wao
  ,washindi ni 10 mshindi wa kwanza amepatiwa cheti na shilingi la kitano,na
  washindi wengine tumewapatia vyeti na fedha taslimu” Alisema Melisa

  Afisa Elimu wa Shule za Msingi Wilaya ya Meru Tumsifu Mushi
  amewataka walimu kufanya kazi ya ualimu kwa moyo na kwa kujituma huku
  wakitambua kuwa wana wajibu mkubwa wa kuandaa wataalamu watakaoisaidia jamii,taifa
  na duni jukumu ambalo ni nyeti linapaswa kubebwa kwa uzito unaostahili.

  Kwa upande wao walimu waliopewa tuzo hizo Rose Salim wa shule ya Msingi Uraki na Ekaeli
  Newasha wa Shule ya msingi Kimundo wamesema kuwa kundi la walimu limekua
  likisahaulika mchango wake katika jamii hivyo tuzo hizo Zimeamsha ari na hamasa ya kufanya kazi kwa bidii.

  “Kazi ya ualimu unapaswa uwe unapenda watoto unapenda kuwasaidia waweze kufika mbali kitaaluma ,binafsi nimefanya kazi hii kwa miaka mingi na ninaipenda sana” Alisema Mwalimu Rose Salim

  0 0

  Balozi wa Cuba nchini, Copez Tomo, akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akirekodi mambo muhimu kwenye 'diary' yake wakati wa mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini, Copez Tomo aliyemtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Uturuki nchini, Bi. Yasemin Fralp akifurahi jambo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu alipomtembelea ofisini kwake na kufanya naye mazungumzo yenye lengo la kuboresha mahusiano baina ya Tanzania na Uturuki.

  0 0

  MWIMBAJI nguli wa nyimbo za Injili hapa nchini, Upendo Nkone pia amethibitisha kushiriki Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Machi mwaka huu katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

  Akizungumza jana, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi, Alex Msama Nkone ameungana na wenzake waliothibitisha kushiriki tamasha hilo, Rose Muhando na Bonny Mwaitege waliothibitisha wiki iliyopita.

  Msama alisema hivi sasa kamati yake inaendelea na mchakato wa maandalizi ya tamasha hilo ambalo linatarajia kuanzia Geita (Machi 26), Mwanza (Machi 27) na Kahama (Machi 28).

  "Tunaendelea na mchakato wa kufanikisha Tamasha la Pasaka 2016 ambalo litakuwa ni la aina yake kwa sababu linatarajia kutoa ujumbe wa neno la Mungu kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa hasa mauaji ya walemavu wa ngozi 'albino'," alisema Msama.

  Aidha Msama alisema Tamasha la Pasaka lina malengo ya kufanikisha kuwasaidia wenye uhitaji maalum ambao ni pamoja na yatima, walemavu na yatima ambao husaidiwa kupitia tamasha hilo.

  Msama alitumia fursa hiyo kuwataka wakazi wa mikoa ya Kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi kwa lengo la kufanikisha matakwa ya wenyer uhitaji maalum.

  0 0

  Kutokana na Wasichana wengi walio Mashuleni kulazimika kukosa Masomo yao katika Kipindi cha hedhi, Mwanaharakati wa Kutetea haki za Wanawake na Wasichana nchini Khadija Liganga, amelazimika kuanzisha kampeni ya kukusanya pedi 3,000 ndani ya mwezi huu ili kuwasaidia wahitaji.


  Akizungumza jana katika Kipindi cha Passion Break Fast kinachorushwa na Radio Passion Fm ya Jijini Mwanza, Liganga alibainisha kwamba ameamua kukusanya pedi hizo kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuziwasilisha katika Shule 10 za Msingi na Sekondari zilizo katika Mikoa ya Mwanza na Mara hii ikiwa ni maalumu kwa ajili ya wasichana wanafunzi ambao hawana uwezo wa kumudu kununua pedi hizo.


  “Tarehe Moja mwezi wa Kwanza mwaka huu, wanawake tulikutana Jijini Mwanza chini ya mpango tuliouita Women Round Table kwa ajili ya kupanga mikakati mbalimbali ya kimaendeleo kwa mwaka huu 2016. Moja ya mikakati niliyoipanga ni pamoja kuanzisha mradi uitwao Binti Box ambao umelenga kusaidia uchangiaji na upatikanaji wa pedi kwa ajili ya wanafunzi wenye uhitaji mashuleni pamoja na kuwapa elimu ya namna ya kujiweka katika hali ya usafi wawapo katika kipindi cha hedhi”. Alisema Liganga na kuongeza kuwa mpango huo utakuwa endelevu.


  Kumekuwepo na tatizo la wanafunzi wasichana katika maeneo mbalimbali nchini kukosa masomo yao katika kipindi cha hedhi huku baadhi yao wakilazimika kuacha shule kutokana na aibu wanayokumbana nayo wawapo shuleni hii ikiwa ni kutokana na kukosa elimu ya kutosha pindi waingiapo katika kipindi cha hedhi.


  Unaweza kuungana na mwanaharaki huyo kwa kuchangia pedi ambapo anapatikana kwa nambari 0713 093 801 hiyo ikiwa ni kwa wale walio mbali na Jijini Mwanza ama waweza kutembelea ofisi za Dida Vitenge Wear zilizopo Nganza Sekondari barabara ya kwenda Chuo Kikuu cha SAUT jirani na ghorofa upande wa kushoto hapo.


  0 0


  0 0

  Balozi wa Uswisi nchini, Florence Tinguely Mattli akitoa neno la ufunguzi katika mdahalo huru kuhusu ajira kwa vijana.
  Washiriki wa mdahalo wakiwa katika makundi kujadili mada zilizotolewa.

  ……………………

  Katika kuadhimisha miaka 50 ya mahusiano na ushirikiano baina ya Uswisi na Tanzania, ubalozi wa Uswisi nchini umefanya mdahalo wa wazi kuhusu ajira kwa vijana ulioshirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ili kubadilishana mawazo jinsi wao wanavyofanya ili kupambana na tatizo la ajira.

  Mdahalo huo ambao ulifanyika katika hoteli ya Coral Beach, jijini Dar es Salaam ulijadili mambo mbalimbali ambayo yanasababisha kuwepo kwa ajira chache lakini pia uwezo wa vijana wa kuingia katika soko la ushindani la ajira.

  Aidha mdahalo huo uliweza kujadili kuhusu changamoto iliyopo ya ajira kwa vijana na kuependekeza njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kukabiliana na tatizo hilo ambalo linaonekana kukua kwa jinsi siku zinavyokwenda.

  Wakizungumza na Mo Dewji Blog baada ya kumalizika kwa mdahalo huo wadau mbalimbali ambalo walihudhuria walisema kuwa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana linaanzia katika aina ya sera ambazo serikali inazitumia katika sekta ya elimu kushindwa kufanya kazi katika soko la ajira la sasa.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze alisema kuwa ili serikali kupunguza tatizo la ajira kwa vijana inatakiwa kuhakikisha inaimarisha uchumi wa nchi lakini ambao unatoa nafasi za ajira zaidi.

  Alisema mbali na kuimarisha uchumi pia inatakiwa kuwatengenezea wananchi wake mazingira mazuri ambayo yatawashawishi kujiajiri bila kutegemea ajira ya serikali au makampuni binafsi ambayo kwa sasa ndiyo yanaonekana kutoa nafasi nyingi za ajira.

  “Vijana wengi kwa sasa wakimaliza vyuo wanajiajiri na hata kama wanauza barabarani korosho huko nako ni kujiajiri … serikali inatakiwa kuimarisha uchumi wa nchi na sio kukuza tu lakini ukue na utoe fursa za ajira kwa wazawa,” alisema Eyakuze.

  Aidha aliwataka vijana kuacha tabia ya kutegemea ajira za serikali na sekta binafsi kwani ushindani katika soko la ajira ni mkubwa na kama wanakuwa hawajajiandaa kwa kiasi kinachohitajika sasa katika soko la ajira basi inaweza kuwa ngumu kwao kupata nafasi.

  Nae Amabalis Batamula kutoka Femina alisema sera ambazo zinatumika nchini hazitekelezwi kama zinavyopangwa na serikali na pia hazina faida kwa soko la ajira la sasa kutokana na kubadilika kwa jinsi miaka inavyozidi kwenda.

  Alisema ni jambo la ajabu baadhi ya sera za elimu ni kuendelea kutumika hadi sasa licha ya soko la ajira kubadilika na hivyo kuhitaji sera mpya ambazo zinakwenda na wakati lakini pia kuwashauri vijana wanaohitimu kuacha kuishi kwa mazoea na badala yake wawe wakijiajiri ili kuepuka tatizo la ukosefu wa ajira.

  Katika taarifa ambayo imetolewa na Shirika la Kazi Duniani (ILO), inaonyesha kuwa zaidi ya vijana 800,000 humaliza chuo kila mwaka na wanaokadiriwa kupata ajira rasmi ni 40,000 pekee hivyo kuonyesha ni jinsi gani kuna upungufu mkubwa wa ajira nchini.

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiongea na wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii.
  Nibu Waziri Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) akiwa katika mkutano wa wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii. Kushoto ni Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alfayo Kidata.
  Makamu Mwenyekiti wa TPSF Salum Shamte (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na wafanyabiashara nchini kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii. Katikati ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile.
  Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt Reginald Mengi (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Godfrey Simbeye (kulia) wakiwa katika mkutano wa wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii.
  Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii.
  Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii.

  (Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

  …………………………………

  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

  Serikali imesema dhamira yake ya kujenga uchumi wa viwanda nchini imejengwa kupitia maeneo ya vipaumbele ambayo yataanza kutekelezwa katika bajeti ijayo ya mwaka wa fedha 2016/2017 kwa kutumia malighafi zipatikana nchini ikiwemo mzao ya misitu, kilimo, uvuvi na madini ili kuwahudumia wananchi.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipokuwa akiongea na wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam.

  Dkt. Mpango aliyaeleza maeneo hayo ya vipaumbele ambayo yataanza kutekelezwa katika bajeti hiyo ni pamoja na kuvirudisha viwanda vilivyobinafsishwa na kutafuta wabia ambao wanaweza kufanyakazi iliyodhamiriwa.

  Maeneo mengine ni miradi mikubwa ya kielelezo ambalo wataalam wanalifanyiakazi ili kuweza kupata matokeo makubwa, akitolea mfano Dkt. Mpango alisemas kuwa yapo maeneo maalum ya kibiashara yakiwemo Bagamoyo, Kigoma na Mtwara kutokana na maliasili iliyopo hapo.

  Zaidi ya hayo, Dkt. Mpango aliongeza kuwa ujenzi wa kiwanda cha chuma kwa kutumia malighafi inayozalishwa kwa kutumia chuma kutoka Liganga na Mchuchuma itakuwa ni msingi wa viwanda mama ikizingatiwa “Hakuna ujenzi usiohitaji chuma”.

  Katika suala la ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha Kimataifa, Dkt. Mpango alisema kuwa mradi huo ni muhimu kwa lengo la kusukuma mbele sekta ya usafirishaji ndani na nje ya nchi ikwemo nchi za Rwanda, Burundi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na mataifa mengine.

  Mafanikio ya ujenzi wa viwanda nchini yanawezekana kwa kwa kuwa Serikali imedhamiria kushirikiana na serkta binafsi kwa kuwa maendeleo ya viwanda yanapaswa kuendana na maendeleo ya watu kwa kuwapatia ajira, elimu inayoendana na mahitaji ya viwanda ili maisha ya wananchi yawe bora zaidi.

  Aidha, ili kujenga uwezo wa kuwa na viwanda nchini, Serikali imejipanga kukusanya kodi ambayo ndiyo msingi wa kuwa na uchumi imara utakaosaidia nchi kujiendesha ambapo wafanyabiashara wote nchini wanapaswa kujisajili na kupewa namba ya usajili (TIN) huduma ambayo inapatikana nchi nzima kupitia ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

  Katika mkutana huo, Dkt. Mpango amewaasa wafanyabiashara kutunza kumbukumbu za biashara yao ili kuwa na kumbukumbu ambazo zinatoa taarifa sahihi na kuhimiza wafanyabiashara wenye mashine za kielekroniki (EFD) waendelee kuzitumia wanapouza bidhaa zao na kuwaptia risiti wateja wao, kwa wale wasio na mashine hizo, Serikali inaendelea kutekeleza agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli la kuwapatia mashine hizo.

  Vile vile, Dkt. Mpango ametoa namba za simu za ofisi za TRA kitengo cha Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi ambapo wananchi wanaweza kuwasiliana moja kwa moja na Idara ya Mambo ya Ndani TRA juu ya maadili ya watumishi wa mamlaka hiyo nchi nzima kwa namba 0689122515 na kutuma ujumbe mfupi kwa namba 0689122516.

  Aidha, Dkt. Mpango amewaonya wafanyabiashara ambao sio waaminifu waache kufanyabiashara za magendo ambapo ameainisha baadhi ya maeneo yanayotumiwa ni pamoja na mwambao wa bahari ya Hindi maeneo ya Mbweni, ziwa Victoria na ziwa Tanganyika.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati na Sera TPSF Felix Mosha amesema kuwa Sekta binafsi itaendelea kushirikiana na Serikali katika mpango wa kukuza uchumi wa nchi na kumhakikishia Waziri wa Fedha na Mipango kuwa watatimiza wajibu wao wa kulipa kodi na kuhamasisha wafanyabiashara wote nchini wanakwenda pamoja na Sera ya “Hapa Kazi Tu”.

  0 0

  NA K-VIS MEDIA Na Mashirikaya Habari

  HILARY Clincton, (Pichani juu), ambaye anaomba kuteuliwa na chama chake cha Democrat, kuwania kiti cha rais wa Marekani kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini humo, ameshindwa kwenye mchujo wa uteuzi katika jimbo la New Hamshire.

  Pia Mgombea wa chama cha Republican, “mbaguzi” Donald Trump, ameshinda kwenye mchujo wa uteuzi katika jimbo hilo la New Hamshire uliofanyika sambamba Jumanne usiku.

  Seneta wa Vermont Bernie Sanders, ndiye aliyemshinda Hillary Clinton, huku Trump, tajiri mkubwa kutokaNew York, na ambaye amekuwa akiwashutumu wageni hususan Waislamu kuwa wanaleta “shobo” nchini humo yeye amewabwaga mahasimu wake wa karibu Gavana wa Ohio, John Kasich aliyeshika nafasi ya pili, Gavana wa Florida, Jeb Bush, Seneta wa Texas, Ted Cruz na Seneta wa Florida, Marco Rubio.

  Trump na Seneta Sanders wote wawili wamekuwa wakiwataka watu wapige kura dhidi ya watu ambao tayari wamekuwa kwenye mfumo wa utawala wa nchi hiyo.

  Clinton ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mamboya Nje wa Marekani kwenye utawala wa sasa wa Obama, tayari amempongeza Bw Sanders, lakini akasema ataendelea kupigania kila kura kwenye kinyang’anyiro hicho cha kumtafuta mgombea urais wa chama cha Democratic.
  Seneta Bernie Sanders (kushoto) na Tajiri Donald Trump

  0 0

  Mabondia Fransic Miyeyusho kushoto na Nassibu Ramadhani wakitambulisha mpambano wao utakaopigwa siku ya sikukuu ya pasaka katika uwanja wa ndani wa taifa katikati ni kiongozi wa ngumi Antony Rutta.
  Kiongozi wa mchezo wa masumbwi nchini Antony Rutta katikati akiwainua mikono juu kuwatambulisha mabondia Fransic Miyeyusho kushoto na Nassibu Ramadhani mbele ya waandishi wa habari Dar es salaam jana kwa ajili ya kutambulisha mpambano wao wa pasaka katiku uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
  Mabondia Fransic Miyeyusho kushoto na Nassibu Ramadhani wakitunishiana misuli mbele ya waandishi wa habari katikati ni kiongozi Antony Ruta wa pili kushoto ni Dei Miyeyusho na mwingine ni kocha Cristopher Mzazi wakati wa kutangaza mpambano wa mabondia hawo siku ya Pasaka .

  MABONDIA Fransic Miyeyusho na Nassibu Ramadhani wamesaini mkataba wa makubaliano wa kuzipiga siku ya sikukuu ya Pasaka katika uwanja wa ndani wa taifa jijini Dar es salaam

  akizungumzia mpambano uho mratibu wa mabambano hayo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa amewasainisha mabondia hawo kwa kuwa viwango vyao vipo juu sana katika kipindi hiki na ndio mpambano utakaokuwa kama ndio mkali wa kufungua mwaka 2016

  aliongeza kwa kusema mbali na mpambano uho siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo mabondia mbalimbali watazipiga siku ya pasaka

  Mohamed Matumla atavaana na Cosmas Cheka wakati mabondia Mada Maugo atavaana na Abdalla Pazi katika mpambano wa nani zaidi kati yao pia bondia Vicent Mbilinyi atavaana na Mwinyi Mzengela na Pius Kazaula wa Morogoro atamenyana na Seba Temba

  Super D amewataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi kuja kwa wingi kushudia mpambano uho ambao utakuwa na msisimko wa aina yake vilevile wamepanga kuanza ngumi hizo mapema ili wapenzi wawai kurudi majumbani kwa na kujumuika na familia zao katika sikukuu hiyo hivyo ameomba mashabiki kufika mapema ili ngumi nazo zianze kwa wakati na kumalizika kwa wakati.


  0 0
 • 02/10/16--02:40: Article 13
 • LIST OF CLEARING & FORWARDING AGENTS SUSPENDED FROM SERVICE AT TPA EFFECTIVELY FROM 09th FEBRUARY 2016.

  S/N
  COMPANY NAMES:

  1. 21st Century Freight Forwarders
  2. Aristepro Investment Co. Ltd
  3. Ace Exim
  4. Ally Vay C & F Agency
  5. A & D Holdings Ltd
  6 A & G Holdings Ltd
  7.ACW Investment Ltd
  8.Afro Centre (T) Ltd
  9.Allmol trading
  10.Amico Trading Ltd
  11.Avow Holding (T) Ltd
  12.Afritel Systems Ltd
  13.Afrovision International Co. Ltd
  14.Arusha Cargo Clearing & Forwarding Ltd
  15.Arusha Freight Transport Agency
  16.Bakhresa Food Products Ltd
  17.Boston Forwarders Ltd
  18.Babylon Freight Ltd
  19.Beam Tanzania Ltd
  20.Best Ocean Air Ltd
  21.Break Through Holdings Ltd
  22.Business Service Promotion Ltd
  23.B & J Co. Ltd
  24.BNM Co. Ltd
  25.Boneste General Enterprises Ltd
  26.Blue Light Investment Ltd
  27.BN Metro ( E.A) Ltd
  28.Cad Mulungu Co. Ltd
  29.Capital Cargo Removers Ltd
  30.Cargo Stars Ltd
  31.Car Freight Station ICDV
  32.Clear Services Tanzania Ltd
  33.Clampek (T) Ltd
  34.Classic Choices Investment Ltd
  35.Continetal Reliable Clearing Ltd
  36.Conanza Express Ltd
  37.Cos Africa Logistics Ltd
  38.Cosmos Haulage Co. Ltd
  39.Chissel C & F Ltd
  40.Cusna Investment Ltd
  41.Daffor Enterprises Ltd
  42.Dynamic Freight Forwarders Ltd
  43.Datar & Co. Ltd
  44.Dar Es Salaam Global Access Ltd
  45.Dar Coast Enterprises Ltd
  46.Denilo Freight Ltd
  47.Destination Tanzania Cargo Logistics
  48.Divine Cargo Services Ltd
  49.Dow Elef Ltd
  50.Dolusi (T) Ltd

  51.Dolphin Sea And Air Ltd
  52.E-3 Freight Co. Ltd
  53.Eagle Tallons (T) Ltd
  54.Econ Consult & Trading Co. Ltd
  55.Eltex Investment Ltd
  56.Edams Holdings Ltd
  57.Efficient Freighters (T) Ltd
  58.Equity Agencies
  59.Expro Freight Services Ltd
  60.Evergreen General Logistics (T) Ltd
  61.Enterprises Logistics Ltd
  62.East African Fossils Fossils Ltd
  63.Fedrol Cargo Ltd
  64.Full Cargo Support Ltd
  65.Freight 24/7 Ltd
  66.Favre Freight Forwarders Ltd
  67.Freight Forwarders (T) Ltd
  68.Freedom Freight Forwarders Ltd
  69.Fifa & Flow Co. Ltd
  70.F.K. Farms & Co. Ltd
  71.First Choice Clearing & Forwarding Ltd
  72.Freight Works Ltd
  73.Frafza Freight Forwarders Ltd
  74.General Envirocare (T) Ltd
  75.General Shami Investment Co. Ltd
  76.Glory Freight Ltd
  77.Grand Movers Co. Ltd
  78.Gwiholoto Impex Ltd
  79.GS InterTrade Co. Ltd
  80.Hamymack Trading Co. Ltd
  81.Hadolin (T) Ltd
  82.Hasa  Customs Agency (T) Ltd
  83.Horizon Freight Forwarders Ltd
  84.Hodari Freight Ltd
  85.Hardmark Logistics Ltd
  86.HK Freight Forwarders Ltd
  87.Hotreef Trading Ltd
  88.Home Base Tanzania Ltd
  89.Ilemela Investment Ltd
  90.Impact Trading And Investment Co. Ltd
  91.Jambo Freight Ltd
  92.Jas Express Ltd
  93.Jamaap Co. Ltd
  94.Joe Ocean C & F Ltd
  95.Juhudi Clearing And Forwarding
  96.Juni Trust Freight Tz Ltd
  97.Kas Freight Ltd
  98.Kahe International Ltd
  99.Kassam freight Ltd
  100.Kiwaepa International Co. Ltd
  101.Khan's C & F Ltd
  102.Kams Trading Ltd
  103.Kings Freight (T) Ltd
  104.K & K Cargo Logistics
  105.K&K Company Ltd
  106.Kadengere Traders Ltd
  107.Korufreight (T) Ltd
  108.Lawia (T) Ltd
  109.Laz ltd
  110.Lesidi General Cargo Ltd
  111.Liberal International Ltd
  112.LCR Limited
  113.LDV Macro Investment Ltd
  114.Logistics Efficiency Co. Ltd
  115.Lesheti Trading Ltd
  116.Lichinga (T) Ltd
  117.Mambona freight Ltd
  118.Mamba Enterprises Ltd
  119.Maxima C & F Ltd
  120.Mwaya C & F
  121.Marine Air Freight Ltd
  122.Maritime Shipping Consultants
  123.Mechanised Cargo Systems
  124.METL
  125.Metrologic C &f F Ltd
  126.Minex Logistics Ltd
  127.Mpepa Traders Co. Ltd
  128.Mogo Forwarders Ltd
  129.Mokha Agency Co. Ltd
  130.Mwagy Investment Ltd
  131.Naito General Supplies Ltd
  132.Nal Business Co. Ltd
  133.Nemarts Limited
  134.Neighbour Trading Co . Ltd
  135.Ngaramau Contractors Ltd
  136.Nutricare (T) Ltd
  137.Nkira Trading Ltd
  138.NM Freight Ltd
  139.Overseas Hi-Tech Industrial Ltd
  140.Orbit Freight Ltd
  141.Pasiwa Cargo Ltd
  142.P & D Freight Forwarders Ltd
  143.Platinum Trading Co. Ltd
  144.Palm Swift Tz Ltd
  145.Quality Logistics Ltd
  146.Runner Co. Ltd
  147.Rungwe Trading Ltd
  148.Reindeer Investment Ltd
  149.Regent (T) Ltd
  150.Rukwi Holdings Ltd
  151.Royal Freight Ltd
  152.Ruma International Ltd
  153.R.H.G General Traders Ltd
  154.Sky Land Across Freight
  155.Sai C & F Ltd
  156.Shift Cargo Ltd
  157.Sachsen Spedition Ltd
  158.Sahara Desert Freighters
  159.Sahuse Services & Supplies Ltd
  160.Selwek & Solar Forwarders Ltd
  161.Sami Agency Ltd
  162.Sahe C & F Ltd
  163.Sangare Express Ltd
  164.Sea Bridge Co. Ltd
  165.Sea Air Forwarders Ltd
  166.Sea Africa Cargo Freight Ltd
  167.Scol (T) Ltd
  168.Shakura Trading Services
  169.Space Land Logistics
  170.Senkondos Import & Export Ltd
  171.Smith Freight Forwarders Ltd
  172.Sino Logistics Ltd
  173.Scanland Shipping Consultants Ltd
  174.SpacelandLogistics Ltd
  175.Sachsen Spedition Ltd
  176.Swiftways International Ltd
  177.Stepio Freight Ltd
  178.Switch Trade Ltd
  179.Sun Fresh Co .Ltd
  180.StarVision International Ltd
  181.Tanga Cargo & Trust Ltd
  182.Trade Waves Investment Co. Ltd
  183.Transit Ltd
  184.Trident Clearing Ltd
  185.Team Freight
  186.Trans Net Freighters
  187.Three way Shipping Service Ltd
  188.Trans Pack Tanzania Ltd
  189.Trans African Forwarders Ltd
  190.TransBarriers Freight Ltd
  191.Transit Ltd
  192.Tripple D
  193.Twende Freight Forwarders Ltd
  194.Ujiji C & F Ltd
  195.United Youth Shipping Co. Ltd
  196.United family Co. Ltd
  197.Uwanji General Tradersb Ltd
  198.Uprising C & F Ltd
  199.Upland Freight Ltd
  200.Vigu Trading Ltd
  201.Vamwe Investment Co. Ltd
  202.Viccom resources co ltd
  203.Way Logistics Ltd
  204.West Freight Forwarders
  205.Wings Wheels Co. Ltd
  206.Walmax Freight Forwarders Co. Ltd
  207.Xpress Maritime Agency Co. Ltd
  208.Zappex International Ltd
  209.Zaihuse C & F Ltd
  210.Zzoikos (T) Ltd

  F.J. Liundi
  For : Port Manager
  Dar es  Port.

  0 0

  Na. Lilian Lundo – Maelezo
   
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni ACP Christopher Fuime amewataka wananchi wa Mkoa wa Kinondoni kutoa malalamiko ya uhalifu vituo vya Polisi badala ya kulalamika  matukio ya uhalifu katika vyombo vya habari.

  Kamanda Fuime amesema hayo leo kwa njia ya simu mara baada ya baadhi ya wananchi kulalamika kwenye vyombo vya habari kwamba kuna ukabaji na uporaji unaofanyika  katika daraja la Manzese wakati wa usiku.

  “Hatuwezi kujua kama daraja hilo linatumiwa na vibaka kupora na kuwakaba kama wananchi hawajaripoti kwenye vituo vyetu juu ya uhalifu huo kwani hata tunapofanya doria hatujawai kukuta kundi la watu bali mtu mmoja mmoja ambao huwa ni wapita njia,” alisema Fuime.

  Fuime aliongezea kwa kusema, licha ya daraja hilo kutumika kuvushia watu lakini pia mara nyingi daraja hilo limetumika kama sehemu ya utalii kwa watanzania hasa kutoka mikoani, hivyo hupenda kupiga picha na hata kuangalia mji kutoka darajani.

  Aidha, Fuime amewataka wananchi kutoa taarifa haraka iwezekanavyo pale wanapofanyiwa uhalifu wa aina yoyote kwani inawapa urahisi Polisi kujua ni wapi pakuanzia kuliko kunyamaza kimya na kulalamika kwenye vyombo vya habari.

  0 0


  0 0

  Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia,Ufundi  na Mafunzo ya Ufundi,Eng. Stella Manyanya(kushoto)akimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwera(kulia)Wakati alipotembelea chumba cha maktaba ya kutunzia nyaraka alipofanya ziara maalumu ya kikazi,Makao makuu ya baraza hilo jijini Dar es Salaam.Wapili toka kushoto Mkurugenzi Msaidizi  wa Wizara hiyo Eng.Enock Kayani na  Mratibu wa maktaba ya Nacte, Clara Kihombo. 
   Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia,Ufundi  na Mafunzo ya Ufundi,Eng. Stella Manyanya(kushoto)akimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwera(kulia)Wakati alipotembelea chumba cha maktaba ya kutunzia nyaraka alipofanya ziara maalumu ya kikazi,Makao makuu ya baraza hilo jijini Dar es Salaam kujua maendeleo ya utendaji wa baraza hilo,katika Mratibu wa maktaba hiyo, Clara Kihombo.
    Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia,Ufundi  na Mafunzo ya Ufundi,Eng. Stella Manyanya akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara maalumu ya kikazi,Makao makuu ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) jijini Dar es Salaam kujionea maendeleo ya utendaji wa baraza hilo.
   Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia,Ufundi  na Mafunzo ya Ufundi,Eng. Stella Manyanya(katikati) akiteta jambo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwera(kulia)Wakati alipofanya ziara maalumu ya kikazi,Makao makuu ya baraza hilo jijini Dar es Salaam, kujionea maendeleo ya utendaji wa baraza hilo,kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi  wa Wizara hiyo Eng.Enock Kayani.

   Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia,Ufundi  na Mafunzo ya Ufundi,Eng. Stella Manyanya(wapili kulia)akimsikiliza Vicent Jacob Mtaalam wa Mtandao wa Udhibiti wa Utoaji wa vyeti vya Satifiketi na Diploma kwa Baraza la Taifa na Ufundi(Nacte) wakati alipofanya ziara maalumu ya kikazi,Makao makuu ya baraza hilo jijini Dar es Salaam, kujionea maendeleo ya utendaji wa baraza hilo.Watatu toka kulia Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwera.
   Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia,Ufundi  na Mafunzo ya Ufundi,Eng. Stella Manyanya(kushoto)akimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwera(kulia)Wakati alipotembelea chumba cha maktaba ya kutunzia nyaraka alipofanya ziara maalumu ya kikazi,Makao makuu ya baraza hilo jijini Dar es Salaam kujua maendeleo ya utendaji wa baraza hilo,Wapili kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi  Wizara hiyo Eng.Enock Kayani.

  0 0

  Mama wa mitindo Asya Idarous Khamsin na Rich Mavoko watua London kwa ajili ya maandalizi ya usiku wa lady in red London, Onesho  la mavazi kwa ajili ya Valentine, pia kutakuwa na burudani kutoka kwa Rich Mavoko na waimbaji kibao Dress code ni red and white.  Itakuwa ni usiku wa Tarehe 13/Feb/2016  Venue ni starlight suite London Tiket zinauzwa Na mlangoni zitakuwapo. Asya na Rich Mavoko wamealikwa na  CLUBMALIBU London. Yatakayo jili tutakujulisha endelea kuwa pamoja nasi.

  0 0

  Na Lorietha Laurence-Maelezo

  Serikali imebaini wizi wa  takribani  shilingi Milioni 700 katika Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kupitia kampuni ya Wakala wa ukatishaji tiketi ya Salama World Travel iliyopo visiwa vya Komoro.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ,Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa ameeleza kuwa wizi huo umefanywa kwa kushirikiana na wafanyakazi wa shirika hilo.

  “Kufuatia upotevu huo Serikali  imechukua hatua thabiti ikiwemo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa ATCL Bw.Steven Kasubi ili kupisha uchunguzi utakaofanywa na kikosi  cha polisi  kitengo cha usalama mtandaoni  ili kubaini mtandao mzima uliohusika  ” alisema Prof.Mbarawa.

  Aidha aliongeza kuwa kwa utaratibu wa kawaida wa  shirika hilo wakala anapewa ruhusa ya  kuuza tiketi za ndege kuanzia kiasi cha shilingi milioni 15 tu na pale anapomaliza mauzo anarudisha fedha kwa shirika na baadaye kupewa ruhusa tena.

  Prof.Mbarawa anasema kwa sasa wameanza na shirika la Ndege la Tanzania kwa kwa lengo la kulifufua kwa kununua ndege mpya na kuwa na wafanyakazi wachapakazi na waadilifu.

  “Siku mbili zilizopita nilifanikiwa kukutana na menejimenti ya ATCL na kubaini mapungufu mengi na hivyo kuamua kuyafanyia kazi kwa kuhakikisha shirika hii linarudi kutenda kazi kwa udhabiti kwa kuwashughuikia wale wote wanaoenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma” alisema Prof.Mbarawa.

  Vilevile aliongeza kuwa Serikali imemuagiza  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) kufanya uchunguzi kwa mawakala wengine wote wa Shirika hilo kubaini kama fedha za uuzaji wa tiketi hizo zinarudishwa kama inavyotakiwa.

   Prof.Mbarawa ametoa wito kwa wananchi kuachana na wizi kwa  njia ya mtandao kwa kuwa sheria ya mtandao iliyoanzishwa mwaka jana inatumika katika kuhakikisha kuwa watuhumiwa wanafikishwa katika mkondo wa sheria na kuchukuliwa hatua stahiki. 


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake leo kwa Wananchi katika sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar zilizofanyika katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja,(kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohammed Othman Chande,
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akionesha kitabu cha Sheria ya mwaka Zanzibar (ZANZIBAR YEARBOOKOF LAW) Volume 4 baada ya kukizindua rasmi leo katika sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja,(kulia)Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,(kushoto) naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Ali Abdalla,Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohammed Othman Chande.
  Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na wananchi katika sherehe za siku hii ya sheria.
  Baadhi ya majaji waliohudhuria katika sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake leo kwa Wananchi katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.

  Mwanasheria Mkuu zanzibar Said Hassan Saidi akitoa maelezo mafupi na kumkaribisha jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu wakati wa sherehe za kilele cha siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu (kulia) na Jiji Mkuu Tanzania Mohammmed Chande Othman wakati alipowasili viwanja vya Victoria Garden katika sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar.
  Kikundi cha sanaa na maigizo cha Blackroot walipotoa igizo lao leo katika sherehe zakilele cha siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ,{Picha na Ikulu.].

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho -MAELEZO


  Serikali kushirikiana na Benki ya Dunia inategemea kuanza ukarabati wa Miundo Mbinu mibovu hususani ya mitaro inayosababisha maafa wilayani Temeke kuanzia mwezi Mei mwaka huu.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Afisa Habari wa Wilaya ya Temeke Joyce Msumba alipokua akiongea Ofisini kwake kuhusu maafa yaliyotokea maeneo ya Sokota,Shule ya Sekondari ya Kibasila na Mtaa wa Butiama ambayo yalisababishwa na ubovu wa miundo mbinu hiyo.

  Hili limetokea baada ya uchunguzi uliofanyika jana ambapo Mhandisi wa Wilaya, Bwana Afya pamoja na Afisa Habari wa Wilaya walifika eneo la tukio na kuona hali halisi.

  ‘’Ni kweli maafa hayo yametokea na sababu hasa ni miundo mbinu ya mitaro ambayo ilielekezwa katika maeneo ya makazi ya watu,kwahiyo inapotokea mvua kubwa maji hayaendi yanapostahili na badala yake yanaingia katika nyumba za watu’’Alisema Msumba.

  Aliongeza kuwa ukarabati huo wa mitaro ni mradi ulio chini ya Dar es salaam Metropolitan Development Project (DMDP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

  Aidha, Joyce Msumba amesema kuwa endapo mvua kubwa zitanyesha kabla ya mradi kuanza watatumia njia ya kuyanyonya maji kwa pampu na kuyapeleka sehemu husika ili kuzuia maafa yasiendelee kutokea.

  Mradi huu unalenga kuhamisha njia za mitaro kutoka kwenye maeneo ya makazi na kuielekeza Bahari ya Hindi ili maji yanayopita katika mitaro hiyo yaende moja kwa moja baharini.

  0 0


  0 0

  Na Beatrice Lyimo-Maelezo

  Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshiba amekabidhi Gari la huduma ya dharura (AMBULANCE) kwa Kituo cha Uratibu wa Matukio ya Sumu nchini kilichopo chini ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

  Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es salaam kati ya Balozi huyo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu sambamba na kuzindua Cheti cha Ithibati cha kuitambulisha Maabara hiyo kimataifa. 

  Akizungumza mara baada ya kukabidhi gari hilo Balozi Yoshiba amesema kuwa Jumuiya ya Zimamoto ya nchini Japan imetoa magari 83 kwa Tanzania ikiwemo magari 10 ya huduma ya  dharura kwa nia njema na pia kukuza uhusiano wa kirafiki kati ya Tanzania na Nchi ya Japani.

  Amesema Jumuiya hiyo ilianza kutoa magari hayo tangu mwaka 2006 na kuahidi kuendeleza uhusiano huo wa kirafiki wenye manufaa kati ya Tanzania na Japani.

  Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa makabidhiano ya gari hilo yameleta hamasa kwa upande wa Wakala na Wadau wengine katika kukabiliana na matukio ya Sumu nchini.

  “Ili Taasisi iweze kufanya kazi kwa ufanisi uwepo wa miundo mbinu kama vifaa ikiwemo mitambo, vitendea kazi kama vile magari na majengo bora ni suala ambalo halina budi kupewa kipaumbele”alisema Waziri Ummy.

  Pia Waziri Ummy amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu na unyeti wa majukumu yanayotekelezwa na Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika kulinda afya, mazingira  na usalama kwa watu na hivyo kuleta utengemano katika jamii.

  Aidha, Waziri Ummy amezindua cheti cha Ithibati chenye namba ISO 1705:2005 kinachoitambulisha maabara ya Mkemia Mkuu kimataifa.

  Katika hatua nyingine Waziri huyo ametoa agizo kwa Wakala wa maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kutoa kipaumbele suala la Madaya ya Kulevya kwa kuwapima watoto haswa wa shule za msingi na sekondari ili kuweza kupambana na janga hilo.

older | 1 | .... | 760 | 761 | (Page 762) | 763 | 764 | .... | 1897 | newer