Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

RAIS WA ZANZIBAR AWAANDALIA CHAKULA VIJANA WA HALAIKI

$
0
0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akisalimiana na viongozi mara alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo katika chakula maalum kwa Vijana walioshiriki Halaiki ya sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akisalimiana na viongozi mara alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo katika chakula maalum kwa Vijana walioshiriki Halaiki ya sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na viongozi wakiimba wimbo maalum alipokaribishwa na vijana wa halaiki chakula maalum kwa Vijana hao walioshiriki Halaiki ya sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar alipowaandalia katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Boara DKt.Mwinyihaji Makame Mwadini akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa viongozi na vijana wa halaiki walioshiriki katika sherehe za Mapinduzi ya mwaka 2016 kutimiza miaka 52 katika viwanja wa Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) na Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakitia chakula wakati wa hafla maalum ya chakula aliyowaandalia Vijana walioshiriki katika Halaiki ya sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar iliyofanyika leo katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja,
Baadhi ya Vijana walioshiriki katika halaiki ya maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakichukua Chakula katika hafla ya iliyoandaliwa kwa ajili yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo,
Baadhi ya Vijana walioshiriki katika halaiki ya maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakichukua Chakula katika hafla ya iliyoandaliwa kwa ajili yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo.
Baadhi ya Vijana walioshiriki Halaiki ya sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakiwa katika hafla ya chakula maalum iliyoandaliwa kwa ajili yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo.
Hawa ni miongoni mwa Vijana walioshiriki katika halaiki ya maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakiwa katika hafla ya chakula kilichondaliwa kwa ajili yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo
Baadhi ya Viongozi walioshiriki katika hafla ya chakula cha mchana alichokiaandaa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa Vijana wa halaiki walioshiriki katika sherehe za Mapinduzi ya mwaka 2016 kutimiza miaka 52 katika viwanja wa Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo.Picha na Ikulu.

JK AONGOZA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 39 YA CCM MKOANI SINGIDA

$
0
0
 Mwenyekiti wa CCM,Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt  Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wakazi wa Singida na vitongoji vyake ndani ya uwanja wa Namfua,wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM,mkoani Singida.Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi Mbalimbali wa Kitaifa,akiwemo Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli,Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan,Waziri Mkuu,Mh.Kasim Majaliwa.
 Baadhi ya Wananchi na wafuasi wa chama cha Mapinduzi (CCM) wakisikiliza hotuba iliyokuwa ikisomwa na Mwenyeki wa chama hicho,Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 39 tangu kuanzishwa kwake ndani ya uwanja wa Namfua leo mchana mkoani Singida.
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi waliokuwa wamekusanyika kwenye uwanja wa Namfua kushuhudia sherehe za maadhimisho ya miaka 39 ya CCM mapema leo mchana mkoani Singida
 Rais John Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
 Rais John Magufuli akimpongeza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa hotuba yake wakati wa maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa CCM Namfua, mjini Singida leo.
 Sehemu ya umati wa wananchi wakiwa katika maadhimisho hayo.
 Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameongozana na Rais Dkt John Pombe Magufuli wakishuka jukwaani kwa pamoja mara baada kuhitimisha shughuli za maadhimisho ya miaka 39 ya chama hicho mkoani Singida,nyuma ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluh Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi madawati 1000 kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Paraseko Kone kwenye maadhimisho ya kutimia miaka 39 ya CCM yaliyoadhimishwa leo Februari 06,2016 katika Uwanja wa Namfua Mkoani Singida. Kushoto Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Rais Dkt John Pombe Magufuli.


WAZIRI MKUU APANGA KUKUTANA NA VIONGOZI WA DINI

$
0
0
Waziri kuu, Kassim Majaliwa akiteta na Askofu Mkuu wa Pili wa EAGT, Dkt. Brown Abel Mwakipesile katika Ibada ya kumsimika Askofu huyo iliyofanyika kwenye kanisa la EAGT Mlimwa West Mjini Dodoma Februari 7, 2016.

……………………………………………
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ataitisha kikao cha viongozi wa dini zote hivi kar ibuni ili wapange na kuainisha ni mambo gani ambayo wanaweza kutoa ushauri kwa Serikali na kupata njia bora ya kuwahudumia Watanzania.

Ametoa ahadi hiyo leo mchana (Jumapili, Februari 7, 2016) wakati akizungumza na mamia ya waumini walioshiriki ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa Pili wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Askofu Dk. Brown Abel Mwakipesile iliyofanyika kwenye kanisa la EAGT la Mlimwa West nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Waziri Mkuu Majaliwa ambaye alihudhuria ibada hiyo kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli alisema: “Hivi karibuni nitaitisha kikao cha viongozi wa dini zote kitakachojumuisha Maaskofu Wakuu, Masheikh na baadhi ya wachungaji ili tukae na kubaini ni nini kifanyike ili kuisadia Serikali namna nzuri ya kuboresha maisha ya Watanzania.”

Akijibu risala iliyosomwa na Katibu Mkuu wa kanisa hilo, Dk. Leonard Mwizarubi, Waziri Mkuu alisema Serikali imeanza kufanya mapitio ambayo yatawawezesha Watanzania kupata huduma kwa urahisi.

“Katibu Mkuu pamoja na Baba Askofu Mkuu wamegusia suala la upandaji wa gharama za vifaa vya ujenzi pamoja na suala la makazi bora. Mwezi ujao tunaanza vikao vya Bunge vya kupitia bajeti ya Serikali, tutaliangalia hili kwa kumshirikisha Waziri wa Fedha… tutafanya mapitio katika hili ili mwananchi wa kawaida aweze kumudu maisha,” alisema huku akishangiliwa na waumini hao.

Aliwaomba viongozi wa kanisa hilo pamoja na waumini wake waendelee kuiombea nchi pamoja na viongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano kwani kazi ya kutumbua majipu waliyoianzisha ina mitihani mikubwa.

“Kutokana na maombi yenu kwa viongozi wakuu wa kitaifa nina imani Taifa hili litafika tunakotaka liende. Endeleeni kutuombea kwa sababu kazi ya kutumbua majipu ina mitihani mikubwa. Lakini pia napenda niwahakikishie kuwa Serikali hii itatumbua majipu hayo kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa. Hakuna mtu ambaye ataonewa,” alisisitiza Waziri Mkuu.

Kuhusu mgogoro wa kiwanja cha kanisa hilo kilichopo eneo la Ipagala, Waziri Mkuu aliahidi kulishughulikia suala lao kesho asubuhi kabla hajaondoka kurejea Dar es Salaam. “Kesho asubuhi nitamuita Mkurugenzi Mkuu wa CDA na kumtaka anipe taarifa sahihi kuhusu mgogoro huu. Najua suala hili liko mahakamani, lakini naamini Mkurugenzi anaweza kuwa kiungo kizuri kati ya wananchi waliojenga eneo hili pamoja na kanisa ambao mnamiliki kiwanja husika”.

“Kama atapata eneo jingine na kupima viwanja, kisha akawapatia hawa wananchi anaweza kuwa amesaidia kuondoa mgogoro huu. Wananchi walienda mahakamani huku wakijua eneo lenu limewekewa uzio, sasa wanagoma kutoka kwa sababu hawana mahali pa kwenda,” aliongeza.

Mapema, akitoa hotuba yake, Askofu Mkuu Dk. Mwakipesile alisema kanisa litaendelea kuiombea Serikali ya awamu ya tano ili nchi idumu katika amani na utulivu.Aligusia eneo la kanisa lililopo kiwanja na 34, kitalu ‘E’, Ipagala East, Dodoma, ambalo ujenzi wa shule yake umesimama kutokana na mgogoro baina yao na wananchi waliovamia eneo lao kwa kujenga nyumba za kuishi licha ya kuwa eneo hilo lilikwishawekewa uzio.

“Kama kanisa tumeshindwa kukamilisha ujenzi wa shule kwa sababu wananchi hao walifungua kesi mahakamani kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa. Tunaomba uamuzi wa kesi hii uharakishwe,” alisema huku akishangiliwa.Alisema kanisa hilo lina majengo 4,670 nchini kote na viwanja 420 ambavyo ni vya kujenga makanisa na vituo vya kutoa huduma mbalimbali za kijamii.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa kanisa hilo, Dk. Mwizarubi alisema katika risala yake kwamba wanaiomba Serikali ifikirie kushusha bei ya vifaa vya ujenzi ili wananchi waweze kuwa na nyumba bora za kuishi.

“Maisha bora maana yake ni kuwa na nyumba bora. Tunaiomba Serikali yako ipunguze bei ya vifaa vya ujenzi ili Watanzania waweze kuwa na makazi bora,” alisema huku akishangiliwa.

JK AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU MAALUM MJINI DODOMA

$
0
0

Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Ku Maalum ya CCM, leo, CHamwino mkoani Dodoma. Picha na Bashir Nkoromo)
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma leo, kulia ni Mjumbe wa Kamati Kuu Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk John Pombe Magufuli na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASHIRIKI IBADA YA KUMSIMIKA ASKOFU MKUU WA PILI WA EAGT, DKT MWAKIPESILE

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa Pili wa EAGT, Dkt. Brown Abel Mwakipesile iliyofanyika kwenye Kanisa la EAGT Mlimwa West mjini Dodoma Februari 7, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya picha Askofu Mkuu wa Pili wa EAGT, Dkt. Brown Abel Mwakipesilie zawadi ya picha yenye maadishi ya neon la Mungu katika Ibada ya kumsimika Askofu huyo iliyofanyika kwenye kanisa la EAGT Mlimwa West mjini Dodoma Februari 7, 2016.
Waziri kuu, Kassim Majaliwa akiteta na Askofu Mkuu wa Pili wa EAGT, Dkt. Brown Abel Mwakipesile katika Ibada ya kumsimika Askofu huyo iliyofanyika kwenye kanisa la EAGT Mlimwa West Mjini Dodoma Februari 7, 2016.
Baadhi ya Waumini wa EAGT wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika Ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa Pili wa EAGT, Dkt Brown Abel Mwakilpesile kwenye kanisa la EAGT Mlimwa West mjini Dodoma Feb 7, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

ZAWADI DOTTO AIBUKA MSHINDI WA MASHINDANO YA URIMBWENDE YA "MISS ALBINISM 2016".

$
0
0
Mrimbwende Zawadi Dotto (Pichani) ameibuka kidedea katika Mashindano ya Miss Albinism Kanda ya Ziwa yaliyofanyika usiku wa Kuamkia leo Jijini Mwanza.

Miss Zawadi mwenye umri wa miaka 17 (mwanafunzi) ameibuka mshiki katika Mashindano hayo ambayo ni maalumu kwa ajili ya Watu wenye ulemavu wa ngozi kwa ajili kuonyesha umahiri wao katika tasnia ya urimbwene hii ikiwa pia ni ishara ya kwamba watu wenye ulemavu wa ngozi wanaweza kushiriki katika shughuli na mashindano mbalimbali.

Mashindano hayo yanaandaliwa na Taasisi ya kusaidia Watu wanaoishi katika Mazingira hatarishi iitwayo SAVE VUNERABLE FOUNDATION ya Jijini Dar es Salaam.Mratibu wa Shirika hilo Alexander Exaud Mutowo ametanabaisha kwamba, baada ya mashindano hayo kukamilika kwa kanda zote nchini, Washindi wa Kanda hizo watashindanishwa Jijini Dar es salaam ili kumpata Mshindi wa Kitaifa wa MISS ALBINISM 2016.
Wshiriki Saba wa Miss Albinism 2016 Kanda ya Ziwa na umri wao katika mabano ambapo kutoka Kushoto ni Hajra Sadru (22), Antonia Mathias William (17), Furaha Edward John (17), Pendo Faustine (15), Zabibu Abdallah (18), Zawadi Dotto (17) pamoja na Asteria Christopher.

Katikati ni Mshindi wa Kwanza, Kulia Mshindi wa Pili na Kushoto Mshindi wa Tatu
Kampuni ya Visimbuzi (Ving'amuzi) ya StarTimes ilikuwa miongoni mwa makampuni yaliyosaidia kufanikisha mashindano hayo. Mwenye Kinasa sauti ni Erick Makonya ambae ni Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Kanda ya Ziwa akitaja zawadi zilizotolewa kwa washindi na Kampuni hiyo ambapo Mshindi wa Kwanza amejinyakulia Simu ya StarTimes aina ya Solar5, Mshindi wa Pili simu aina ya P40 StarTimes na Mshindi wa tatu amejishindia simu aina ya B27 zote zikiwa ni android kutoka StarTimes.
Baadhi ya Wageni waalikwa wakiongozwa na Marcella Mayala ambae ni Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana (wa tatu kushoto) ambae alimwakilisha wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ambae alikuwa Mgeni Rasmi, wakiwa katika picha ya Pamoja na washindi.
Washiriki walioingia Nne bora ambapo kutoka kushoto Hajra Sadru, Furaha Edward, Zabibu Abdallah na Zawadi Dotto

Baada ya Mtifuano mkali hatimae majaji wakatangaza washini. Furaha Edward mshindi wa tatu (Kushoto), Hajru Sadru mshindi wa pili (katikati) na Zawadi Dotto akaibuka kuwa mshindi wa Kwanza (aliepiga magoti).

Mshindi wa Miss Albinism Kanda ya Ziwa akivikwa taji lake. Wa pili kulia ni Jalia Mtani ambae alikuwa Jaji Mkuu akitajana Majina ya washindi. Pembeni ni Mshereheshaji Emmanuel Shalali kutoka Sahara Media Group.
Mshindi wa Miss Albinism Kanda ya Ziwa akivikwa taji lake. Wa pili kulia ni Jalia Mtani ambae alikuwa Jaji Mkuu akitajana Majina ya washindi. Pembeni ni Mshereheshaji Emmanuel Shalali kutoka Sahara Media Group.
Alexander Exaud Mutowo ambae ni Mratibu wa Shirika la VUNERABLE FOUNDATION lililoandaa mashindano hayo akizungumza wakati wa mashindano hayo, ambapo amewasihi wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi ikiwemo kuunga mkono juhudi za shirika hilo kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jiko katika katika kituo cha kuwahifadhi watu wenye ulemavu wa ngozi Buhangija kilichopo Mkoani Shinyanga.
Fredy Samwel Kaula ambae ni Mwenyekiti wa Shirika la VUNERABLE FOUNDATION akizungumza katika Mashindano hayo
Alfredy Kapole ambae ni Mwenyekiti wa Tanzania Albinism Sociaty TAS akizungumza wakati wa mashindano hayo
Mwenye kinasa sauti ni Marcella Mayala ambae ni Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana (wa tatu kushoto) ambae alimwakilisha wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ambae alikuwa Mgeni Rasmi, akifungua mashindano hayo. 

Amesema ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza itaendeleza ushirikiano na Shirika la VUNERABLE FOUNDATION kwa ajili ya kupata wadau wa kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi.

Dickson Kiringo a.k.a Mr.White ambae ni Msanii chipukizi wa Muziki wa Kizazi kipya akitoa burudani. Msanii Barnaba Boy aliahidi kumsaidia Mr.White ili arekodi nyimbo mbili katika studio yake ikiwa ni bure kabisa.
Msanii Barnaba Boy akitoa burudani katika shindano la Miss Albinism 2016 Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza.
Majaji ambapo kutoka Kushoto ni Jaji Angelina Chuma, Jaji Mkuu Jalia Mtani na Jaji Lilian Lambo
Wa pili kulia ni Alfredy Kapole ambae ni Mwenyekiti wa Tanzania Albinism Sociaty TAS pamoja na wadu wengine wakifuatilia mashindano hayo

Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo wa BINAGI MEDIA GROUP

PPF WAKABIDHIWA RASMI JENGO JIPYA LA KISASA WALILOJENGA JIJINI ARUSHA LENYE THAMANI YA BILIONI 32.5

$
0
0
Kiongozi Mkuu wa mfuko wa PPF (Director General) William Erio (kushoto) akipokea michoro ya jengo jipya la PPF Jijini Arusha kutoka kwa Mbunifu na Msimamizi Mkuu wa mradi wa ujenzi wa jengo hilo, Arch. Dudley Mawalla (kulia) kutoka kampuni ya MD Consultancy Ltd ya Dar es Salaam, katika hafla fupi ya makabidhiano rasmi ya jengo kutoka kwa mkadarasi wa kichina CREJ (EA) Ltd. Anayeshuhudia Katikati ni Injinia wa Miradi ya PPF, Injinia Marko Kapinga.
DG William Erio (pichani juu) ameisifu timu yote iliyoshiriki kufanikisha kukamilika kwa mradi huo katika ubora uliotakiwa na katika bajeti iliyopangwa mwaka 2012 bila kuongezeka pesa yoyote, kuanzia kitengo cha miradi ya PPF makao makuu, wabunifu na wasimamizi, mamlaka za Jiji, idara nyingine za Serikali na wakandarasi wenyewe. 

Jengo hilo maalumu kwa shughuli za ofisi na biashara lenye ghorofa 10 sambamba na eneo la basmenet yenye uwezo wa kupaki magari 168, lina thamani ya shilingi bilioni 32.5. Limejengwa eneo la Corridor, Kitalu Na. 15 Barabara ya zamani ya Old Moshi Jijini Arusha. lina huduma zote muhimu kwa majengo ya kisasa zikiwemo 'lifti' za kutosha, majenereta makubwa, mataki ya maji na mafuta ya jenerato, mfumo wa kukabiliana na moto na bila kusahau camera 90 za usalama na eneo kubwa la kuegesha magari ndani ya jengo.

Kwa mujibu wa Mbunifu na Msimamizi Mkuu wa mradi huo wa kisasa, Arch Mawala, ujenzi wa jengo hilo ulianza rasmi Agosti 2 mwaka 2018 ukitarajiwa kukamilika miezi 104 baadae na ulikamilika rasmi (practica completion) mwishoni mwa mwezi Disemba mwakaa jana. Hata hivyo imewachukua miaka miwili na miezi 3 kuweza kukamilisha kila kitu katika ubora wa kiwango cha juu, ambapo miezi hiyo mitatu ni ya ngongeza ya muda kutokana na sababu ambazo hazikuweza kuzuilika. 
Sehemu ya muonekano wa mbele wa jengo
Mpaka kufikia kukabidhiwa kwake hii leo, tayari ukaguzi wa mamlaka za Jiji na Usalama wa Majengo umeshakamilika na ruhusa ya matumizi kutolewa. Tayari jengo hilo limeshapata wapangaji watatu ambao wapo kwenye jengo tayari zikiwemo benki za TIB na FBNB, huku asilimia 21 ya wapangaji wengine wakiwa wamekwisha saini mikataba na PPF na wapangaji wengine 24 wakiwa katika mazungumzo.

Aidha kwa maelezo ya Mratibu wa PPF Kanda ya Kasakazini, Bw Onesmo Rushahi, Ofisi za Kanda ambazo kwa sasa ziko maeneo ya Kaloleni Jijini hapa zitahamishiwa katika Jengo hili jipya, huku mkakati wa PPF ukiwa ni kuhakikisha baada ya mwaka mmoja jengo hilo liwe limefanikiwa kupata wapangaji maeneo yote kwa shughuli za ofisi na biashara. 

Mkandarasi Mkuu ni kampuni ya CRJE (EA) Ltd akisaidiwa na wakandarasi wengine kwa huduma za jengo kama vile ICT na Usalama - SSTL Group Ltd, Lifti - S.E.C (EA) Ltd, AC - M.A.K Enginering Co. Ltd, Mfumo wa maji safi na maji taka - Jandu Plumbers Ltd, na Umeme ni Central Electrical International Ltd. Pia kulikuwa na mamlaka za kiserikali kama wasimamizi wa usalama makazini OSHA, Idara ya maji Asurha - AUWSA, NAESCO, Halmashauri ya Jiji na Bodi za Ukaguzi kama AQRB na CRB.

Injinia Marko Kapinga, Meneja wa Utekelezaji wa Miradi ya PPF akikagua makabrasha yaliyokabidhiwa na mkandrasi kama michoro halisi ya namna jengo lilivyo kwa sasa
Kiongozi mkuu wa Kampuni ya CRJE (EA) Ltd, Bw Hu Bo (kulia) ambaye kamapuni yake ndio ilikuwa mkandarasi mkuu wa mradi akikabidhi funguo kwa Director General wa PPF Bw William Erio kama ishara ya makabdihiano ramsi ya jengo la PPF Plaza la Jijini Arusha hii leo. Kwa mbali anashuhudia Meneja wa jengo hilo kutoka PPF Bw..
Meneja wa PPF Kanda ya Kaskazini Bw Onesmo Ruhasha (kulia) akishuhudia makabidhiano rasmi ya jengo jipya la PPF Plaza la Jijini Arusha hii leo
Meneja wa PPF Uwekezaji Bw Selestine Some (kushoto) akimkabidhi ufungua kama ishara ya kuhamishia usimamizi wa jengo la PPF Plaza kwa Menenja Rasilimali, Bw Selemani Kituli wa PPF Kanda ya Kaskazini



Msimamizi Mkuu wa kazi zote za ujenzi kwa upande wa mkandarasi, kampuni ya CRJE, Bw Zhang Cuishan akitoa neno la shukrani katika hafla hiyo. 

Director General wa PPF Bw William Erio kulia pamoja na mkuu wa uwekezaji (PPF's Director of Investiment) Bw Steven Alfred 





DG William Erio katika picha ya pamoja mbeye ya sehemu kuu ya kuingilia kwenye jengo akiwa na timu ya wakandarasi, wasimamizi wabunifu wa mradi pamoja na wataalamu kutoka PPF Dar es Salaam.





Msanifu wa jengo na msimamizi mkuu wa mradi kutoka kampuni ya MD Consultancy Ltd, Arch Dudley Mawalla akiongoza ujumbe wa DG William Erio kufanya ziara ya ameneo mabalimabli ya jengo kabla ya makabidhiano rasmi.

















Msafara ukitembelea eneo la kuegeshea magari chini ya jengo la PPF Plaza. Jumla ya magari 168 yanaweza kuegeshwa katika maeneo mbalimbali yaliyotengwa ndani ya jengo.








Msimamizi Mradi mkaazi kwa niaba ya PPF, Injinia Norbert Nselu akitoa maelezo kwa Bw William Erio namna gari zinavyoweza ingia basement na kuegeshwa.








Director General William Erio akipata maelezo ya mfumo wa usalama wa kieletronic wa jengo namna unavyofanya kazi kutoka kwa mataalamu wa maswala ya usalama na mawasialiani ya kielectronic kutoka kampuni ya SSTL Ld, Bw Athumani Pongwe ndani ya chumba cha usalama. Jumla ya kamera 90 za usalama zimeunganishwa na taarifa zake kuletwa kwenye chumba hiki.








wakiangalia moja ya viambaza vya dani ya jengo.








Hapa DG William Erio na wataalamu wengine wakifurahia utani wa wake





Meeneja wa PPF Kaskazini Bw Onesmo Ruhasha, kulia na Director General wa PPF wakijadiliana jambo wakati wa kutembelea maeeneo ya jengo. 








Baadhi ya watumishi wa PPF Kanda ya kaskazini wakiangalia moja ya maneo ambayo ni maalumu kwa wapangaji kufanya biashara ama kuweka ofisi za shughuli zao.








msimamizi mkaazi kwa niaba ya PPF, Injinia Norbert Nselu akimfafanulia DG Erio hatua kwa hatua namna ujenzi ulivyoanza mkapa kukamilika kwake.








Director General wa PPF akiangalia madhari ya Jiji la Arusha kutokea ghorofa ya nane katika moja ya baraza za jengo la PPF Plaza lililokamilika na kukabidhiwa hii leo. Pamoja nae ni Msanifu wa jengo na Msimamizi Mkuu wa Mradi Arch. D Mawalla









Bw Selemani Kituli (property manager wa PPF) na Bw Selestine Some, Meneja Uwekezaji wakifahamishana jambo katika hafla fupi ya makabidhiano ya jengo la PPF Plaza kutoka kwa Mkandarasi Mkuu CRJE (EA) Ltd 






Sehemu ya timu ya washauri wasimamizi wa mradi kwa maswala ya gharama, uimara na huduma (Project Costs, Structural Strength na Building Services Engineering) 












Msimamizi mradi mkaazi (Clerk of Works) kwa naiab ya PPF, Injinia Norbert Nselu akifafanua jambo katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano kwa Director General wa PPF haonekani pichani.









Mkuu wa Kampuni ya CRJE (EA) Ltd, kampuni ya kichina ambayo ndiyo ilikuwa mkandarasi mkuu wa mradi uliokamilika wa jengo la PPF Plaza la Jijini Arusha akitoa salamu zake katika hafla fupi ya makabidhiano ya jengo hilo








Director General wa PPF Bw William Erio akisalimiana na Bw Habib O Kiango, mmoja wa watumishi wa ofisi ya PPF Kanda ya Kaskazini iliyoko Kaloleni Jijini Arusha. 





Director General wa PPF, Bw William Erio akisalimiana na Bi Getrude Haule, ambaye pia ni mmoja wa watumishi wa ofisi ya PPF Kanda ya Kaskazini iliyoko Kaloleni Jijini Arusha katika hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la PPF Jijini hapa. Anayeshuhudia ni Bi Grace Estomih, mtumishi pia wa PPF Kanda ya Kaskazini ofisi ya Arusha. 








DG William Erio akitaniana na wafanyakazi wa taasisi anayoisimamia ofisi ya Kanda ya Kaskazini, Arusha hii leo








Director General wa PPF, Bw William Erio akisalimiana na Bw Fortunatus Woiso, ambaye pia ni mmoja wa watumishi wa ofisi ya PPF Kanda ya Kaskazini iliyoko Kaloleni Jijini Arusha katika hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la PPF Jijini hapa.








Mbunifu/msanifu mkuu na msimamizi mkuu wa mradi wa jengo la PPF Plaza la Jijini Arusha, Arch. Dudley Mawalla akizungumza na wataalamu washauri wa masuala ya gharama za ujenzi ambao walisimamia fedha zote za mradi kwenda kwa wakandarasi na kuandaa bajeti yake, QS Mrosso (kushoto) kutoka kampuni ya Cost Consult Ltd ya Jijini Dar es Salaam.

PICHA&MAELEZO : TUMAINIEL SERIA, ARUSHA

WAZIRI MBARAWA AWATAKA MAKANDARASI KURUDI KAZINI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kulia) akimsikiliza Mbunge wa Mvomero Sadick Murad (kushoto) wakati akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa barabara ya Magole-Turiani yenye urefu wa Km 48.6. Katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Edwin Ngonyani.
Sehemu ya juu ya daraja la Diwale lenye urefu wa mita 75 likiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake kama linavyoonekana.
Mbunge wa Mvomero Sadick Murad akimwongoza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa pili kulia) kuelekea katika daraja la Diwale, wa tatu kulia ni Meneja wa TANROADS mkoa wa Morogoro Eng. Dorothy Mtenga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akizungumza na wananchi wa Turiani kuhusu kukamilika kwa ujenzi wa Darajala Diwale.
Muonekano wa Daraja la Diwale linalounganisha wilaya ya Mvomero na Kilindi.
Mafundi wanaotengeneza vichwa vya treni katika karakana kuu ya TRL, Mkoani Morogoro.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa mkandarasi Sanayejenga.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawsiliaano Prof.Makame Mbarawa (Wa pili kushoto), akitoa maelekezo kwa Meneja bishara wa kampuni ya Malaysia inayojenga vichwa vya treni Srinivasan Rajmohan (Wa kwanza kulia) kuhusu kufanya kazi hiyo kwa haraka ( Wa pili kushoto) ni katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi Eng.Leonard Chamuriho na (Wapili kulia) ni Naibu Waziri Eng.Edwin Ngonyani.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa akizungumza na Wafanyakazi wa TRL (Hawapo pichani), Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Ucukuzi na Mawasiliano Eng.Wdwin Ngonyani, akifuatiwa na Kaimu Meneja wa TRL Morogoro Eng.Yusto Goima na Meneja TANROADS Morogoro Eng.Dorothy Mtenga.
Wafanyakazi wa karakana kuu ya Reli Mkoani Morogoro wakimsiliza Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa (Hayupo pichani), akiwapa muongozo wa kufanya kazi.
……………….

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewataka Makandarasi waliosimamisha kazi za ujenzi wa barabara nchini kuendelea na ujenzi baada ya Serikali kuanza kuwalipa madai yao.Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Magole-Turiani yenye urefu wa kilomita 48.6 Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro, Prof. Mbarawa amesema tayari Serikali imeshalipa makandarasi mbalimbali nchini shilingi bilioni 400 na itaendelea kufanya hivyo ili kumaliza madeni yao kwa haraka.
“Hakikisheni mnarejea kazini na kuwapa mikataba ya ajira wafanyakazi wenu katika kipindi cha wiki mbili kuanzia sasa ili ujenzi wa barabara na madaraja ukamilike kwa mujibu wa mkataba na hivyo kuondoa usumbufu kwa watumiaji wa barabara hii”, amesema Prof Mbarawa.

Profesa Mbarawa amemhakikishia mkandarasi China Civil Engineering Construction Corporation anayejenga barabara ya Magole-Turiani kuwa tayari serikali imeshamlipa zaidi ya kiasi cha dola za kimarekani zaidi ya laki 735 na Shilingi za kitanzania zaidi ya Milioni 795 hivyo ni wakati wa kukamilisha ujenzi huo hususan sehemu za madaraja kabla ya mvua za masika kuaanza.
Akizungumza katika ukaguzi huo Mbunge wa Mvomero Mhe. Sadick Murad ameiomba Serikali kumalizia daraja la Diwale lenye urefu wa mita 75 ili liweze kupitika.

Katika hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amekagua karakana ya ujenzi wa vichwa vya treni mjini Morogoro na kumtaka mkandarasi anayekarabati vichwa hivyo kufanya kazi hiyo kwa haraka na kutoa kazi nyingine kwa watanzania ili kuwajengea uwezo wa kazi hizo.

Amewataka wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Kufanya kazi kwa ubunifu, uadilifu na uwazi ili kufufua hadhi ya Shirika hilo ambalo ni muhimu kwa uchumi wa nchi hii.
Amesema takribani asilimia 96 ya mizigo inayoshushwa katika Bandari ya Dar es salaam husafirishwa kwa njia ya barabara hivyo ni jukumu la TRL kuhakikisha inapata mizigo ya kutosha ya kusafirisha ili kupunguza mizigo hiyo kusafirishwa na barabara lakini kufufua uchumi wa TRL na taifa kwa ujumla.

“Fanyeni kazi kwa bidii, uwazi na kwa kushirikiana ili kujenga Shirika la Reli la kisasa lenye uwezo wa kujitegemea acheni vitendo vya hujuma na migomo vinavyoweza kudhoofisha shirika hili”, amesisitiza Prof. Mbarawa.Naye Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amekemea vitendo wa wizi wa mafuta na kuhujumu Reli vinavyofanywa na watumishi wasio waaminifu na kuwataka kuwa wazalendo kwa nchi yao ili kuchochea kasi ya maendeleo.

Akizungumza katika hafla hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilino (Sekta ya Uchukuzi) Eng. Dkt. Leonard Chamuriho amewataka watumishi wa TRL Kuepuka migomo itakayoathiri utendaji wa Shirika hilo, kubuni mikakati ya kuwezesha shirika hilo kujiendesha kwa faida, kupambana na ubadhirifu wa mali na miundombinu na kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuleta tija inayokusudiwa.

Profesa Mbarawa alikuwa kwenye ziara ya kukagua utendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano ambapo amepata fursa ya kukagua ujenzi wa mizani ya kisasa ya Mikese na kituo cha mtandao wa mawasiliano ya simu vijijini ya Halotel unaosambazwa katika taasisi za Serikali ikiwemo Hospitali, Polisi, Mahakama na Shule hapa nchini.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilano

RAIS WA ZANZIBA AWAANDALIA CHAKULA VIKOSI VYA ULINZI ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akichukua chakula wakati wa hafla ya chakula maalum iliyofanyika leo katika viwanja vya mpira Makamo Makuu ya Polisi Ziwani Zanzibar kwa Vikosi vya ulinzi vilivyoshiriki sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar (katikati) Kamishna wa jeshi la Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makam
Maaskari wa vikozi vya ulinzi wakichukua chakula cha mchana kilichotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya katika viwanja vya mpira Makamo Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Unguja walioshiriki sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Maaskari wa vikozi vya ulinzi wakichukua chakula cha mchana kilichotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya katika viwanja vya mpira Makamo Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Unguja walioshiriki sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Askari wa Vikosi vya Ulinzi wakiwa katika hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya katika viwanja vya mpira Makamo Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Unguja kwa ushiriki wao katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Maaskari wa vikozi vya ulinzi wakijipanga kwa mstari wakati wa kuchukua chakula cha mchana kilichotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya mpira Makamo Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Unguja kwa ushiriki wao katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Askari wa Vikosi vya Ulinzi wakiwa katika hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya katika viwanja vya mpira Makamo Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Unguja kwa ushiriki wao katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)pamoja na viongozi wengine wakiitikia dua iliyoombwa baada ya chakula alichowaandalia askari wa vikosi vya ulinzi leo katika viwanja vya katika viwanja vya mpira Makamo Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Unguja kwa ushiriki wao katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana na Kamishna wa jeshi la Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame leo baada ya hafla ya chakula maalum ilichokiandaa kwa Vikosi vya ulinzi vilivyoshiriki sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya mpira Makamo Makuu ya Polisi Ziwani Zanzibar Mjini Unguja,Picha na Ikulu.]

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AOMBOLEZA VIFO VYA ASKARI WALIOFARIKI DUNIA SINGIDA

PROFESA KILLIAN WA CHUO CHA MKWAWA ASHINDA SAFARI KUTAZAMA BUNDESLIGA UJERUMANI NA STARTIMES

$
0
0
 Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo, akichezesha droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia).
 Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia) akiandika namba ya mshindi wa droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) na Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo.
 Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) akipiga namba ya simu ya mshindi aliyepatikana katika droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia).
 Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo akizungumza na mshindi kwa njia ya simu aliyepatikana wakati wa uchezeshwaji wa droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia).
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Chuo cha Ualimu cha Mkwawa cha mkoani Iringa ambacho ni chuo kishiriki cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Bernadeta Killian (50) amefanikiwa kuibuka mteja wa kwanza mwenye bahati kwa kujinyakulia tiketi ya kwenda Ujerumani kutazama mechi ya Bundesliga kutoka kwa kampuni ya StarTimes katika droo iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza kwa njia ya simu Profesa Killian baada ya kutangazwa kuwa ni mshindi amesema kuwa anayo furaha isiyoelezeka kupata taarifa hiyo ya ushindi ambao hakufikiria kama kuna ofa hiyo nzuri kwa wateja.

“Ninajisikia furaha kwa kutangazwa kuwa mshindi kwani sikutarajia kama wateja wa StarTimes tunaweza kupewa kubwa kiasi hiki ya kwenda Ujerumani kutazama mechi ‘Live’. Naweza kusema mwaka umeanza vizuri kwa kuonyesha dalili ya neema kama hii, ni fursa kubwa kwangu mimi kama mteja kwani kuna maelefu ya wateja ambao wangependa kupata fursa hii. 

Nawashukuru kwa hili kwani wameliendesha zoezi bila ya upendeleo na sisi wateja wao tunafurahi na kuwapongeza sana na tutandelea kuwaunga mkono.” Alieleza Profesa Killian

Mshindi huyo wa kwanza wa droo iliyopewa jina la ‘Pasua Anga na StarTimes’ alipatikana baada ya kujiunga na kifurushi cha Super ambacho ni shilingi 36,000/- katika dishi. Lakini pia mteja yoyote wa StarTimes anaweza kuibuka mshindi kwa kujiunga na kifurushi chochote kuanzia cha shilingi 5,000/- na kuendelea kwa upande wa ving’amuzi vya dishi na antenna. Na kwa wateja wapya pindi wajiungapo na huduma za kampuni hiyo wamekuwa wameunganishwa moja kwa moja na droo ya bahati nasibu.

“Ningependa kutoa wito kwa wateja wenzangu waendelee kujiunga kwani bado nafasi zimebaki kushindaniwa na zote zipo kwa ajili yao, hivyo wasilaze damu. Ninaahidi kuitumia fursa hii ipasavyo kwa kuenda kutazama wenzetu wa ulaya wanafanya nini kwa upande wa soka kwani kwa muda mrefu tumekuwa tukitazama kupitia kwenye luninga, pongezi tena kwa StarTimes kwa kuifanya ligi ya Bundesliga ionekane kupitia ving’amuzi vyake kwa gharama nafuu kabisa ambayo kila mtu anaweza kuimudu. Wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuipa ligi hiyo umaarufu nchini kwani sasa kwa kiasi kikubwa michezo yote inaonekana ‘Live’ na kufuatiliwa na watu wengi.” alihitimisha Mkuu huyo wa Chuo cha Ualimu Mkwawa

Naye kwa upande wake Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amebainisha kuwa, “Hii si mara ya kwanza sisi kuchezesha droo ya bahati nasibu kwa kuwazawadia wateja wetu ni zawadi mbalimbali, hivyo basi huu ni muendelezo tu wa ofa nyingi zinazoendelea kumiminwa kwa wateja wetu waaminifu. Safari hii wateja wetu tumeamua kuwazawadia safari itakayolipiwa gharama zote na kampuni kwenda Ujerumani kutazama ligi ya Bundesliga ambayo kwa Afrika ndio kampuni pekee yenye hakimiliki ya kuionyesha ‘Live’.”

“Makubaliano baina ya wamiliki wa ligi hiyo ya Ujerumani na kampuni ya StarTimes yaliingiwa kwa dhumuni kubwa la kuifanya ligi hiyo maarufu barani Afrika kama ligi zingine. Na ni kwa kupitia StarTimes pekee hilo linaweza kufanikiwa kutokana na wingi wa wateja wetu, ubora wa huduma na gharama nafuu ambazo mwananchi yoyote wa kipato cha chini anaweza kuzimudu,” alisema Bi. Hanif na kumalizia, “Hivyo basi nampongeza mshindi wa leo na nawasihi wateja wetu waendelee kujiunga nasi au walipie vifurushi vyao ili waingie kwenye droo ya bahati nasibu na kujishindia safari hii kubwa kwenda Ulaya kutazama mechi moja kwa moja pamoja na mashabiki wengine ulimwenguni.”

Akielezea machache kutokana na ushuhuda wake baada ya kupata fursa ya kutembelea ofisi za Bundesliga na kushuhudia mechi kadhaa nchini Ujerumani, Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda, ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli za michezo, amesema kuwa, “Bahati ya kupata safari ya kwenda Ujerumani ni fursa kubwa sana kwa wateja na ningependa waitumie vema. Kuna mengi tu ya kujifunza licha ya kufurahia safari hiyo. Wenzetu wamepiga hatua kubwa na tunayo mengi ya kujifunza kutoka kwao, hivyo nawasihi waitumie vemam ili waje kutuhadithia na sie huku.”

Zoezi zima la uchezeshwaji wa droo ya bahati nasibu ya kumpata mshindi ilichezeshwa kwa uwazi na haki mbele ya waandishi wa habari ikishuhudiwa na mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.

CHUO KIKUU CHA AFRICAN GRADUATE UNIVERSITY CHAFANYA MAHAFALI YAKE YA PILI NCHINI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Makamu Mkuu wa Chuo cha African Graduate University, Askofu Profesa Stephano Nzowa (kulia), akizungumza katika mahafali ya pili ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam juzi.Kushoto ni Mkuu wa chuo hicho, Profesa Timothy Kazembe kutoka nchini Zambia na mgeni rasmi wa mahafali hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), Dk. Fredrick Ringo.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), Dk. Fredrick Ringo, ambaye alikuwa mgeni rasmi akihutubia katika mahafali hayo.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Askofu Profesa Stephano Nzowa akimvika kofia Mwimbaji wa nyimbo za injili, Stella Joel wakati akimtunuku Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Mahusiano katika mahafali hayo. Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho kutoka nchini Zambia, Profesa Timothy Kazembe.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), Dk. Fredrick Ringo akimpongeza mwimbaji Stella Joel kwa kupata tuzo hiyo.
Wahitimu wa chuo hicho wakiwa wamejipanga tayari kwa kuingia ndani kuanza kwa shughuli mbalimbali za mahafali hayo.
Ndugu na jamaa na wageni waalikwa kwenye mahafali hayo.
Wahitimu hao wakishiriki kuimba wimbo wa taifa.
Mahafali yakiendelea.
Taswira katika ukumbi wa mahafali.
Waliotoa huduma katika mahafali hayo wakiwa katika pozi.
Waimbaji wa nyimbo za injili wakitoa burudani.


Na Dotto Mwaibale


WAHITIMU wa Chuo Kikuu cha African Graduate University katika ngazi mbalimbali wametakiwa kutumia elimu waliyopata kwa ajili ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Mwito huo ulitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), Dk. Fredrick Ringomgeni aliye kuwa mgeni rasmi katika mahafali ya pili ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam juzi.

"Nawaombeni sana elimu mliyopata itumieni kwa ajili ya kuinua maisha ya familia zetu, wananchi na taifa kwa ujumla na si vinginevyo" alisema Dk.Ringo.Makamu Mkuu wa chuo hicho Askofu Profesa Stephano Nzowa aliwata wahitimu hao kuendelea kujiendeleza kielimu hadi kufikia ngazi mbalimbali za juu.

Nzowa alisema watu wengi wamekuwa wakijiendeleza kielimu wakiwa na matumaini ya kuja kupata kazi nzuri jambo ambalo alisema ni bahati."Msisome kwa ajili ya kuja kupata kazi nzuri bali someni ili kujiongezea uelewa wa mambo mengi ambayo yatawasaidieni kuanzisha miradi mbalimbali ya kuwaingizia fedha" alisema Nzowa.

Profesa Nzowa alisema chuo hicho chenye makao makuu yake nchini Sieralaoni kipo katika nchi kadhaa barani Afrika na kwa Tanzania kinajengwa Wanging'ombe mkoani Njombe na kuwa mahafali hayo ni ya 25 na kwa hapa nchini ni ya pili.


Mkuu wa chuo hicho Profesa Timothy Kazembe kutoka nchini Zambia alisema lengo lao ni kufungua chuo hicho katika nchi mbalimbali duniani ili wanafunzi kujua mambo mbalimbali yakiwemo ya kijamii na ya mungu.


ZAIDI YA KAYA 60 KIWALALA NA MJIMWEMA ZIMEATHIRIKA NA MAFURIKO

$
0
0
Mafuriko Wilaya ya Lindi

Zaidi ya Kaya 60 za Vitongoji vya Kiwalawala na Mjimwema Kata ya Kitomanga Wilayani Lindi Zimeathiriwa na Mvua Zilizoambatana na Mafuriko Huku watu 94 wakifanikiwa Kuokolewa Kufuatia Jitihada za Halmashauri ya wilaya Ya Lindi kupeleka Boti kusaidia zoezi la Uokoaji.

Mvua hizo zilizonyesha Mwanzoni mwa wiki hii Tayari Maeneo mbalimbali ya wilaya Hiyo pamoja na Wilaya ya Kilwa kukosa sehemu za Kuishi huku jitihada za Kuokoa waliozungukwa na Maji zikiendelea.

Mafuriko Wilaya ya Lindi

Lindiyetu.com ilifika katika Maeneo Jirani na kijiji Cha Mjimwema jirani na Kitongoji wanachoishi wafugaji na Kushuhudia zoezi la Uokoaji Likiendelea na Ilifanikiwa Kuongea na Baadhi ya waliookolewa ambapo walieleza Jinsi walivyokutwa na Maafa hayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Lindi Bi Oliva Vavunge akiongea na Lindiyetu.com wakati zoezi la Uokoaji likiendelea amewataka wananchi wote wanaoishi sehemu za mabondeni kuhama maramoja kwani Mvua hizo bado zinaendelea kunyesha kama ilivyotangazwa na mamlaka ya hali ya hewa nchini.
Mafuriko Wilaya ya Lindi
Diwani wa kata Ya Kitoanga alitoa ombi kwa Kitengo cha Maafa kutoa msaada wa haraka kwa wahanga hao.
Mafuriko Wilaya ya Lindi
Sambamba na Tukio Hilo Mkurugenzi Mtendaji pia amewataka wakazi wanaoishi katika Bonde la Mto Lukuledi Kuanza Kuondoka katika Bonde Hilo Ili kunusuru Maisha yao pamoja na Mali zao.
http://kickzacelebrity.blogspot.com/

WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI WATUNUKIWA TUZO ZA HESHIMA KUTOKA CHUO KIKUU AFRICAN GRADUATE UNIVERSITY CHA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Askofu Profesa Stephano Nzowa akimvika kofia Mwimbaji wa nyimbo za injili, Stella Joel wakati akimtunuku Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Mahusiano katika mahafali hayo. Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho kutoka nchini Zambia, Profesa Timothy Kazembe.
Hapa Stella Joel akipongezwa na ndugu yake.
Mkuu wa Chuo hicho kutoka nchini Zambia, Profesa Timothy Kazembe akimvika kofia Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Ado Novemba wakati akimtunuku tuzo ya heshima ya udaktari. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), Dk.Fredrick Ringo akimkabidhi tuzo hiyo.
Waimbaji wa nyimbo za injili, Stella Joel (kulia) ambaye ametunukiwa Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Mahusiano na mwenzake Upendo Mbila (kushoto), aliyetunukiwa Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Umma wakiteta jambo kwenye mahafali hayo ya pili ya Chuo cha African Graduate University yaliyofanyika Dar es Salaam juzi.
Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja.
Paul Mbila (kulia), akimvika taji mama yake Upendo Mbila ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za injili baada ya kutunukiwa tuzo Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Umma.


Na Dotto Mwaibale

Chuo Kikuu cha African Graduate University kimewatunuku tuzo za heshima za stashahada ya uzamili katika ngazi mbalimbali waimbaji wa nyimbo za injili nchini kutokana na mchango wao katika jamii.

Akizungumza wakati wa kukabidhi tuzo hizo kwa waimbaji hao katika mahafali ya pili ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam juzi Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Askofu Profesa Stephano Nzowa alisema ni jambo jema kuwakumbuka watu mbalimbali waliolifanyia taifa mambo mazuri.

"Chuo chetu kimeona ni vema kikawapa tuzo za heshima watu mbalimbali wakiwemo wanamuziki wa nyimbo za injili kwani kupitia uimbaji wao wameweza kutoa mafunzo kwa watu na wengine kuacha kutenda dhambi na kuamua kuokoka" alisema Profesa Nzowa.

Baadhi ya waimbaji wa nyimbo za injili waliotunukiwa tuzo hizo ni Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Ado Novemba ambaye alitunukiwa tuzo ya heshima ya udaktari, Stella Joel ambaye ametunukiwa Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Mahusiano na Upendo Mbila aliyetunukiwa Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Umma.


Akizungumza baada ya kupata tuzo hiyo Stella Joel alisema anamshukuru mungu kwa kumuwezesha kupata tuzo hiyo na kuwa imemtia nguvu kuendelea kufanya kazi ya mungu kupitia uimbaji.

Kwa upande wake Upendo Mbila alitoa shukurani zake kwa chuo hicho kwa kutambua mchango wa waimbaji wa nyimbo za injili kwa kuwapa tuzo hizo ambazo ni muhimu kwao.

PSPF YAZIDI KUJITANUA, WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WAZIDI KUMIMINIKA KWENYE MFUKO HUO KWA KUJIUNGA NA MPANGO WA PSS

$
0
0

 Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Msanii wa majigambo, Mrisho Mpoto, akitoa elimu juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSS, na umuhimu wa wanafunzi wa UDSM kujiunga na Mfuko huo kupitia Mpango wa uchangiaji wa hiari, PSS. Warsha hiyo iliyokusanya wanafunzi karibu 3,000 ilifanyika ukumbi wa Nkurumah wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani jijini Dar es Salaam, Februari 6, 2016

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said




WANAFUNZI wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani na wale wa Chuo Kikuu Cha Tumaini, kampasi ya Dar es Salaam, (TUDACO) wameendelea kuchangamkia “fursa” kwa kujiunga na Mfuko wa Pensehni wa PSPF, kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari, PSS



Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, UDSM, Kitapenda Ahadi na Makamu wake, Irine Deodatus Ishengoma, waliongoza mamia ya wanafunzi pale mlimani kwa kujaa fomu za kujiunga na Mfuko huo.


Hatua ya kujiunga na Mfuko huo ni baada ya semina iliyotolewa na Maafisa wa Mfuko huo, wakiongozwa na mabalozi wa PSPF, Mwanamitindo wa Kimataifa anayefanya kazi zake Ulaya na Marekani, Flaviana Matata, na Msanii maarufu wa hapa nchini, Mrisho Mpoto almaaruu kama “Mjomba”.


Akizungumzia huduma zitolewazo na Mfuko huo, Afisa wa Matekelezo (compliance), wa PSPF, Albert M.Feruzi na Hadji Jamadary, walisema, kuna uchangiaji wa mpango wa lazima, (mandatory scheme) na ule wa hiari Supplementary Scheme) na kuwataka wanafunzi hao ambao wengi wao ni wa mwaka wa mwisho, kuchangamkia fursa kwa kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari.


Nao mabalozi wa PSPF, waliwaeleza wanafunzi hao kuwa pindi wakijiunga na PSPF, hawatajutia uamuzi wao, kwani kuna watafaidika na mafao mbalimbali kama vile mkopo wa elimu, fao la uzazi, mkopo kwa muajiriwa mpya, mkopo wa nyumba na mkopo wa viwanja.


Chuo Kikuu ChaTumaini, tawi la Dar es Salaam, (TUDACO), ndio waliokuwa wakwanza kujiunga na Mfuko huo ikiwa ni wiki moja tu baada ya wanafunzi wenzao hapo hapo kuchukua uamuzi huo.

Afisa Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Rahma Ngassa, (wakwanza kushoto), mhamasishaji, Anthony Luvanda, (wapili kushoto), Mabalozi wa PSPF, Flaviana Matata, (watatu kushoto) na Mrisho Mpoto, (wane kushoto) na Makamu wa Rais wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Irine Deodatus Ishengoma, wakifurahia jambo wakati wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na uongoz wa DARUSO kwa kushirikiana na Mfuko wa Pensehni wa PSPF, na kufanyika ukumbi wa Nkuruma wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mamia ya wanachuo walijiunga na Mfuko huo kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS)

Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani, wakijaza fomu za kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS), wakati wa semina ya siku moja iliyofanyika Ukumbi wa Nkrumah wa chuo hicho mwishoni mwa wiki.
 Afisa wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Gasper Lyimo, akigawa fomu za kujiunga na uanachama wa Mfuko huo, kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, ambao walijiunga na Mpango wa uchangiaji wa hiari, PSS
 Rais wa Serikali ya Wanafuzni wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, DARUSO,

NSSF YAZINDUA MPANGO WA AKIBA NA AFYA KWA WANAFUNZI WA VYUO

$
0
0
 Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (kushoto) akimkabidhi mfano wa kadi ya uanchama wa NSSF, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Rajabu Mahumba wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa AKIBA na AFYA 'AAPLUS' kwa wanafunzi wa vyuo hafla hiyo ilifanyika Chuo Kikuu cha Dodoma, mwishoni mwa wiki. (Picha na Francis Dande)
 Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed akimkaribisha Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde kwenye uzinduzi wa Mpango wa Hifadhi ya Jamii kwa Wanafunzi 'AAPLUS', uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). 
 Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde akipeana mkono na Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa NSSF wa Akiba na Afya kwa Wanafunzi wa Vyuo, uliofanyika UDOM. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Mariam Ahmed.
 Baadhi ya maofisa wa NSSF wakifuatilia uzinduzi huo.

Meza Kuu.
Wanafunzi.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa NSSF wa Akiba na Afya kwa Wanafunzi wa Vyuo.
Baadhi ya waafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde.  
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed.
Mshauri wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dick Manongi akizungumza katika uzinduzi huo. 
 Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mpango wa NSSF wa Akiba na Afya kwa Wanafunzi wa Vyuo uliofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma. 
 Wakifuatilia uzinduzi huo.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma akitoa mada wakati wa uzinduzi wa mpango wa Akiba na Afya 'AAPLUS' kwa wanafunzi wa vyuo.
Mwanafunzi wa UDOM, Mishi Jumanne akiuliza swali kuhusu uanachama wa NSSF.
 Wanafunzi wakipimwa afya katika viwanja vya chuo cha UDOM.
 Dk. Leilah Manga wa Kituo cha Afya Chuo Kikuu cha Dodoma akipima mapigo ya moyo ya mwanafunzi wa UDOM, Hoza Ernest 
Wanafunzi wakijaza fomu za kujiunga na NSSF.
 Ofisa Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Issa Salim (kulia) akitoa maelekezo kwa wanafunzi wa UDOM waliojiunga na NSSF.
Ofisa Mwandamizi Idara ya Matekelezo, Abubakar Soud (katikati) akiwaelekeza namna ya kujaza fomu ya kujiunga na NSSF, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakati wa uzinduzi wa mpango wa Akiba na Afya 'AAPLUS' kwa wanafunzi wa vyuo uliofanyika katika chuo hicho, mwishoni mwa wiki.

Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (katikat) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa NSSF pamoja na baadhi ya wanafunzi wa UDOM.
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde akiagana na Ofisa Matekelezo Mwandamizi wa NSSF, Abdul Mzee.

GARI ALTEZZA INAUZWA

$
0
0




Make : TOYOTA 
Model: ALTEZZA
Body type: SALOON (CLOSED TOP) 
Colour: SILVER
Year of manufucture:2000
Engine no:01GEAA1909
Engine capacity;1980
Fuel;PETROL

ANAEHITAJI PIGA SIMU 
+255755311477 0R +255754710458

NEW VIDEO : B-GWAY FT MESEN SELEKTA - MPERA MPERA

AHADI YA SH.BILIONI 12.3 YA RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI YA MAOMBI YA UENDESHAJI WA MAHAKAMA YATIMIA LEO.

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango (Katikati) akiwakabidhi Naibu waziri wa katiba na sheria, Amon Mpanju(kulia) na Mtendaji mkuu wa Mahakama Hussein Kattanga cheki ya shilingi Bilioni 12 na milioni mia tatu ikiwa ni kutimiza ahadi  ya Rais Dkt. John Pombe Josef Magufuli aliyoahidi siku alipokuwa mgeni rasmi siku ya Mahakama hapa nchini ikiwa ni siku tano tuu tangu siku ya kuahidi.
Waziri wa Fedha Mipango, Philip Mpango (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na kutimiza ahadi aliyoiahidi Rais  Dkt. John Pombe Josef Magufuli alipoahidi katika maadhimisho ya siku ya mahakama hapa nchini. Kulia ni Naibu waziri wa katiba na sheria, Amon Mpanju na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile. 
Mtendaji mkuu wa Mahakama Hussein Kattanga (kushoto)akimshukuru Rais  Dkt. John Pombe Josef Magufuli kwa kutimiza ahadi yake aliyoiahidi siku ya maadhimisho ya siku ya mahakama. kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

 Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
WIZARA ya Fedha na Mipango imetoa sh.bilioni 12.3 kwa ajili shughuli za mahakama ikiwa ni sehemu ya ahadi ya  Rais Dk. John Pombe Magufuli aliyoiahidi katika kilele cha maadhimisho ya  siku ya mahakama.


Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema fedha hiyo imetolewa kwa kutimiza ahadi ya Rais ya uendeshaji wa shughuli za mahakama.


Mpango amesema kuwa ahadi ya Rais ilikuwa ni ya siku tano ambazo zimetimia kwa kutoa hundi ya sh.bilioni 12.3 ambazo zitakwenda kufanya kazi iliyokusudiwa.


Amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango kutokana na ahadi hiyo imefanya kuweka wazi juu ya fedha hizo kwa waandishi wa habari.


Nae Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju amesema lengo ni kuongeza kasi kwa mashauri yaliyopo kuondoshwa  pamoja na waliokwepa kodi  yashughulilikiwe.


Ahadi ya Rais ilitolewa baada ya maombi ya Jaji Mkuu, Othman Chande katika maadhimisho ya  kuanza kwa mwaka wa mahakama kudai kuwa wana uhaba fedha za maendeleo  katika kuweza kuendesha shughuli za kimahakama.
Naibu waziri wa katiba na sheria, Amon Mpanju akisaini dafari la wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za wizara ya fedha na mipango jijini Dar es Salaam leo. 
Mtendaji mkuu wa Mahakama Hussein Kattanga (kushoto) akisaini kitabu cha wageni leo alipowasili katia ofisi za wizara ya fedha na mipango jijini Dar es Salaam leo.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA YAANZA KAZI RASMI – YAPOKEA TAARIFA YA UTENDAJI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akijitambulisha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kabla ya Kamati hiyo kuipokea taarifa ya Wizara hiyo katika kikao cha kwanza cha Kamati hiyo baada ya kuundwa na Bunge hivi karibuni. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Balozi Adadi Mohamed Rajabu anayefuatia ni Makamu wake, Kanali Masoud Khamis. Kulia kwa Masauni ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Mohamed Rajabu akizungumza jambo na Wajumbe wa Kamati yake pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kikao chao kwanza tangu Kamati hiyo iundwe na Bunge hivi karibuni. Wapili kulia mstari wa mbele ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni, na kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Kanali Masoud Khamis. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akitoa taarifa ya Wizara katika kikao cha kwanza cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. Kikao hicho kilichohudhuriwa na Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Maafisa wa Wizara, kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Balozi Adadi Mohamed Rajabu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni (hayupo pichani) alipokuwa anawasilisha taarifa ya Wizara kwa Kamati hiyo katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (katikati) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira wakiiweka sawa taarifa ya wizara yao kabla ya kuiwasilisha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Balozi Adadi Mohamed Rajabu. Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Watendaji wa Wizara walikutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya Ulinzi na Usalama. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images