Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 756 | 757 | (Page 758) | 759 | 760 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles John Mwijage akijibu hija mbalimbali toka kwa wabunge katika kikao cha 9 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.Picha na Raymond Mushumbuai MAELEZO.

  Shillingi Billioni 60 zinategemea kutumika kufufua kiwanda ya matairi cha General Tyres kilichopo Jijini Arusha ambacho kimesharudi mikononi mwa Serikali, na fedha hizo zitatumila kurekebisha mitambo ya umeme ya kiwanda hicho na kupata mitambo mipya itakayoendana na teknolojia ya utengenezaji wa matairi duniani.

  Akijibu swali la Mhe. Joshua Nassari Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) lililouliza ni lini serikali itafufua kiwanda cha matairi cha General Tyres kilichopo Jijini Arusha kwani ni tegemeo kwa ajira kwa wananchi wa Jijini la Arusha,Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles John Mwijage amesema kiwanda hicho kimesharudi mikononi mwa Serikali na wako mbioni kukifufua ili kianze kufanya kazi ya kuzalisha matairi nchini.

  “ Tumeanzisha viwanda nchi ili kuzalisha bidhaa na kutoa ajira kwa watanzania na sio kuwatesa wananchi kwa kukosa ajira au kuagiza bidhaa ambazo tunaweza kuzalisha hapa hapa nchini, hivyo basi Serikali kupitia Wizara yangu tutatenga fedha kwa ajili ya kufufua kiwanda hiki ili kianze kufanya kazi mara moja”

  “ Sio tu tutafufua kiwanda cha General Tyres pekee bali tunafatilia viwanda vyote ambavyo vimekiuka sheria na kanuni kwa kutoviendeleza viwanda hivyo ili kuvirudisha mikononi mwa Serikali au kuwatafuta wawekezaji wengine watakaoweza kuviendesha viwanda hivyo” Alisema Mhe. Mwijage.

  Aidha Mhe. Charles John Mwijage amesema ni kweli makampuni mengi yaliyobinafsishwa hayakufanya vizuri katika uendeshaji wake ukiacha mifano ya makampuni machache yanayofanya vizuri yakiwemo Tanzania Breweries Limited (TBL),Morogoro Polyester 21st Century na Tanzania Cigarette Company Limited (TCC), hivyo Wizara yangu ikishirikiana na Msajili wa Hazina juu ya Viwanda ilifanya tathmini iliyoonesha kuwa mashirika mengi yaliyobinafsishwa hawakutekeleza mikataba ya mauziano kikamilifu.

  Ameongeza kuwa lengo ni kuhakikisha makampuni yote haya yanazalisha kwa tija ili tupate bidhaa,kodi ya Serikali na ajira kwa wananchi wa Tanzania ili kutimiza adhma ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuli ya kuwa na Tanzania yenye viwanda kwa maendeleo ya taifa.

  Serikali kupitia Wizara yetu inaboresha mazingira ya uwekezaji hali itakayowajengea imani kwa wawekezaji na kupelekea kupanua zaidi shughuli zao za kibiashara na pia kuendeleza mpango wa Viwanda vidogo na vya kati unaoshirikisha SIDO na Halmashauri za Wilaya na Mikoa ili kuanzisha Viwanda vya Mkoa vya kuongeza thamani ya bidhaa za Kilimo,Uvuvi na ufugaji kupitia njia hii ajira nyingi zitaongezeka na kupunguza tatizo la ajira nchini.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora(wa pili kushoto) akisikiliza maelekezo kutoka kwa Meneja Mradi bw. Xiong Hazbin (Kushoto) na kulia ni Mkurugenzi wa TEHAMA Eng. Peter Philip katika ziara ya kutembelea kituo mahiri cha taifa cha kutunzia kumbukumbu kilichopo kijitonyama jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora(kushoto) akimsikiliza maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wizara hiyo Eng. Peter Philip kuhusu mitambo ya kupozea umeme iliyoko katika kituo mahiri cha taifa cha kutunzia kumbukumbu kilichopo kijitonyama jijini Dar es Salaam.
  Mitambo ya kupozea umeme iliyopo katika kituo mahiri cha taifa cha kutunzia kumbukumbu kijitonyama jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora(kulia) akiongozana na Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wizara hiyo Eng. Peter Philip na baadhi ya maaafisa wa Wizara wakati wa ziara ya kukagua kituo mahiri cha taifa cha kutunzia kumbukumbu kilichopo kijitonyama jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora(kushoto) akipewa maelezo ya namna hali ya usalama inavyozibitiwa katika kituo mahiri cha taifa cha kutunzia kumbukumbu kilichopo kijitonyama jijini Dar es Salaam kutoka kwa Mkurugenzi wa TEHAMA Eng. Peter Philip .
  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora(kushoto) akionyeshwa mitungi ya kuzimia moto Salaam kutoka kwa Mkurugenzi wa TEHAMA Eng. Peter Philip alipofanya ziara yake ya kutembelea kituo mahiri cha taifa cha kutunzia kumbukumbu kilichopo kijitonyama jijini Dar es .
  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora(kushoto) akionyeshwa sehemu ya chumba cha kuhifadhia Jenereta kilichopo katika kituo mahiri cha taifa cha kutunzia kumbukumbu kijitonyama jijini Dar es Salaam ,kutoka kwa Mkurugenzi wa TEHAMA Eng. Peter Philip .(Picha na Lorietha Laurence-Maelezo)

  0 0

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya maradhi ya saratani Zanzibar Dkt. Msafiri Marijani akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ya Jumuiya hiyo Mpendae ikiwa ni maadhimisho ya siku ya saratani duniani, kushotoni kwake ni Mkurugenzi wa Utumishi na uendeshaji Wizaraya ya Afya,
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Jumuiya ya maradhi ya saratani Zanzibar kwenye maadhimisho ya siku ya saratani Zanzibar.
  Mkurugenzi wa Utumishi na uendeshaji Wizaraya ya Afya Zanzibar ndugu Omar Mwinyi Kondo akizungumza na waandishi katika maadhimisho ya siku ya saratani duniani yaliyofanyika Ofisi ya Jumuiya Mpendae, (kulia)
  Picha ya pamoja ya mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya saratani duniani ndugu Omar Mwinyi Kondo (kati) mwenye suti na baadhi ya viongozi na waandishi wa habari waliohudhuria.
  PICHA NA MAKAME MSHENGA/MAELEZO ZANZIBAR

  ……………………………………………………………………………

  RAMADHANI ALI/MAELEZO ZANZIBAR 
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya maradhi ya Saratani Zanzibar Dkt. Msafiri Marijani ameitanabahisha jamii kwamba maradhi ya saratani yamekuwa janga linalosumbua dunia nzima kwa sasa na kila mmoja anawajibu wa kusaidia katika kukabiliana na maradhi hayo sugu.
  Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ya Jumuiya hiyo Mpendae nje kidogo ya Mjini Zanzibar, ikiwa ni maadhimisho ya siku ya saratani duniani, Dkt. Marijani amesema mtu anaweza kujikinga na maradhi hayo iwapo hatua za mapema zitachukuliwa.Amezitaja hatua zinazopaswa kuchukuliwa na wananchi katika kukabiliana na saratani kuwa ni kujenga mwamko wa kuchunguza afya mara kwa mara ili kugundua mapema iwapo mtu anazo dalili za maradhi hayo.

  Amesema hatua nyengine ni kuacha kutumia bidhaa zinazotokana na tumbaku, ulevi wa kupindukia, kupunguza matumizi ya mafuta kwenye chakula, kutumia zaidi vyakula vya matunda na mbogamboga na kujenga tabia ya kufanya mazoezi kila siku.Dkt. marijani amewakumbusha wananchi kuwa saratani ni uvimbe mpya kwenye mwili na baada ya muda mfupi huzalisha chembechembe zinazosababisha athari kubwa na kama haikuwahiwa mapema inasababisha donda kubwa na kuwa halitibiki tena.

  “Saratani inaweza kuzuilika iwapo itawahiwa mapema, tuongezeni nguvu kukabiliana nayo vyenginevyo inaweza kuathiri wananchi wengi kwani gharama ya matibabu yake ni kubwa na wagonjwa wengi hushindwa na kupoteza maisha,” alisisitiza Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.
  Amesema saratani ya matiti na shingo ya kizazi ndizo zinaongoza kwa wanawake Zanzibar na saratani ya tenzi dume inaongoza kwa upande wa wanaume.

  Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya maradhi ya Saratani Zanzibar, ambae ni Daktari bingwa wa uchunguzi wa saratani, amewaeleza waandishi wa habari kwamba mpaka hivi sasa hakuna takwimu rasmi za wagonjwa wa maradhi hayo Zanzibar lakini Hospitali ya Ocean Road ya Dar es salaam imekuwa ikipokea wagonjwa 1,000 kila mwaka kutoka Zanzibar mbali na wagonwa wengine wanaopelekwa nje ya nchi na wanaobakia majumbani kupatiwa dawa mbadala.
  Amesema kutokana na kadhia hiyo mwaka 2013 ilianzishwa Jumuiya ya kupambana na saratani Zanzibar ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa jamii juu ya njia za kujikinga na kuishauri serikali njia zinazofaa kupunguza ongezeko la maradhi hayo.
  Ameitaka Serikali kuongeza wataalamu na dawa za kupunguza maumivu katika hospitali kuu ya Mnazimmoja na hospitali nyengine za Zanzibar kwani zimekuwa hazitoshi.
  Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Utumishi na Uendeshaji Wizara ya Afya Ndugu Omar Mwinyi Kondo amewapongeza wanachama wa Jumuiya hiyo kwa juhudi kubwa wanayochukua kuelimisha jamii kujikinga na saratani.

  Amewahakikishia viongozi wa Jumuiya hiyo kwamba Serikali itaanzisha utaratibu rasmi wa kuwasajili wagonjwa wa saratani na kuongeza huduma za matibabu Hospitali kuu ya Mnazimmoja hasa dawa za kupunguza maumivu na wataalamu.

  ujumbe wa mwaka huu katika siku ya saratani duniani ni mimi na wewe tunaweza kujikinga na saratani.
  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

  0 0


  0 0


  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Hamad Yussuf Massauni akijibu hoja mbalimbali kuoka kwa Wabunge mbalimbali katika kikao cha 9 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.

  ……………………………

  Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

  Serikali kupitia Jeshi la Polisi imekua ikifanya operesheni maalum za mara kwa mara za kukamata waganga wa jadi wanaopiga ramli chonganishi ambazo ni kichocheo kikubwa cha ukatili dhidi ya walemavu wa ngozi nchini.

  Akijibu swali la Mhe.Mgeni Jadi Kadika Mbunge wa Viti Maaalum(CUF) lililouliza Serikali ina mpango gani wa kuwalinda na kuhakikisha usalama wa maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Hamad Yussuf Massauni amesema Serikali imeanzisha vituo vya kuwahudumia watu wenye ulemavu wa ngozi ambavyo vimesaidia kuimarisha ulinzi ikiwa ni pamoja na Polisi kuwatumia Polisi Jamii kutoa elimu kwa umma juu ya madhara ya vitendo vya kikatili vya mauaji na kujeruhi vinavyofanywa na baadhi ya watu kwa msukumo wa imani potofu za ushirikina.

  “Kwa takwimu halisi tulizonazo tangu mwaka 2006 mpaka 2015 jumla ya mauaji ya walemavu wa ngozi 43 yametokea na jumla ya watuhumiwa 133 walikamatwa kuhusika na vitendo hivyo na watuhumiwa 19 walihukumiwa adhabu ya kifo”

  “ Katika kupambana na vitendo hivi Jeshi la Polisi linakumbwa na changamoto mbalimbali zikiwemo uhaba wa askari katika kuhudumia wananchi ambapo kwa Tanzania askari mmoja anahudumia wananchi 1000 mpka 1500 ikiwa ni nje ya matakwa ya kimataifa ya askari mmoja kuhudumia wananchi 400 mpka 450 na uhaba wa magari kwa ajili ya doria mbalimbali ambapo takribani magari 387 yamegawanywa katika maeneo mbalimbali nchini ili bado tunaendelea kupambana na kutatua changamoto hizi kadri ya bajeti iyakavyoruhusu” Alisema Mhe.Massauni.

  Wizara kupitia Jeshi la Polisi ikishirikiana na Kamati za Ulinzi na Usalama za Vijiji,Kata,Wilaya, na Mikoa imeanzisha vikosikazi(TASK FORCES) hususani kwenye Mikoa na Wilaya zilizokithiri matukio ya ukatili dhidi ya walemavu wa ngozi ambapo Vikosikazi hivyo hukusanya taarifa za kiintelejensia na kuzifanyia kazi.

  0 0


  (Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO)
  …………………………………..
  Serikali imetoa tamko la kulaani kitendo kilichotokea nchini India kwa mwanafunzi wa kike wa kitanzania kuvuliwa nguo na kutembezwa barabarani ambapo Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje,Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na kimataifa imetoa tamko la kulaani suala hilo kwa kuitaka Serikali ya india kuchukua hatua.

  Akitoa tamko hilo Bungeni Mjini Dodoma Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Dkt Augustine Mahiga amesema ni kweli kwamba kuna mwanafunzi wa kike wa kitanzania alifanyiwa kitendo cha udhalilishaji nchini India kwa kuvuliwa nguo na kutembezwa barabarani suala ambalo lilizua mijadala mikubwa nchini kuhusu udhalilishaji huo.

  “Wizara yetu imezungumza na Balozi wa India nchini na kumweleza ni kwa jinsi gani watanzania wamefadhaika na kusononeshwa na kitendo alichofanyiwa mtanzania mwenzao huko India na Balozi alituhakikishia kwamba amewasiliana na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi yake na kusema Serikali ya India kwa kushirikiana na Jeshi la polisi nchini humo wamefanikisha kuwakamata wote waliohusika na kitendo hicho na kuwafikisha mahakamani kujibu mashataka hayo”

  “ Pia Serikali ya India imeahidi kutoa ulinzi kwa wanafunzi wa kitanzania na wenye asilia ya Afrika wanaosoma huko ili kuwalinda na kuwaepusha na vitendo hivyo vinavyofanya na raia ambao hawana nia njema kwa mahusiano mazuri ya kimataifa yaliyopo kati ya India na Tanzania”Alisema Mhe. Mahiga.

  Serikali ya Tanzania imekuwa na mahusiano mazuri na Serikali ya India kwa miaka mingi sasa na kutokana na kitendo hiki kilichotokea nchini India,Waziri wa Mambo ya Nje ya India amefatana na Balozi wa Tanzania nchini humo kwenda Mji wa Bangalo ili kuongea na wanafunzi wakitanzania na wale wenye asili ya Afrika wanaosoma huko ili kujenga mahusiano mazuri na wazawa ikiwa ni jitihada za kupunguza vitendo hivyo kutokea mara kwa mara.

  0 0

   Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipiga picha na mke wake Mama Salma Kikwete, leo, mbele ya nyumba alimoishi mjiini Singida mwaka 1975, wakati huo akiwa katibu Msaidizi wa  TANU  wilaya ya Singida mjini. Kikwete yupo mkoani Singida kwa ajili ya kuongoza Maadhimisho ya Miaka 39 ya CCM, ambayo kilele chake kitaifa ni leo. (Picha na Bashir Nkoromo).
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Singida leo, alipotembelea Ofisi hiyo, akiwa mkoani humo kwa ajili ya kuongoza Maadhimisho ya Miaka 39 ya CCM, ambayo kilele chake kitaifa ni leo. Kushoto ni Mama Salma Kikwete, na wengine ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Mbunge wa Mtama Nape NNauye na Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Singida Mary Maziku

  0 0

  Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukikatisha misitu na mabonde wakati ukielekea kata ya Mwangeza kijiji cha Kibampa ambako jamii hiyo inaishi. 
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia Sola zinazosukuma maji kwenye kisima cha mradi wa maji yanayotumika kwenye kijiji pamoja na shule ya msingi ya Munguli iliyopo wilaya ya Mkalama mkoani Singida.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya mradi wa maji wa kijiji cha Munguli kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Ndugu Christopher Ngubiagai.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ndani ya hosteli ya shule ya msingi Munguli ambayo wanasoma watoto wa Kihadzabe.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakulima wakati akiwa njiani kuelekea kata ya Mwangeza kijiji cha Kibampa.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakulima wakati akiwa njiani kuelekea kata ya Mwangeza kijiji cha Kibampa.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikaribishwa kijiji cha Kibampa na wakazi wa hapo amabao ni Wahadzabe.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akifurahia jambo na kijana wa kabila la Kihadzabe 

  Wahadzabe wakiwa kwenye kikao maalum kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakishiriki kupanda mihogo kwenye shamba ya la Wahadzabe kwenye kijiji cha Kibampa wilaya ya Mkalama.
  Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Ndugu Christopher Ngubiagai akimuelekeza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana namna Wahadzabe wanavyosaga mtama kwa kutumia jiwe. 


  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana leo ameweka historia ya kuwa kiongozi wa nne mkubwa wa Kitaifa kufika kwenye kijiji cha Munguli na Kibampa ambavyo wanaishi jamii ya Wahadzabe .Kijiji cha Munguli kilitembelewa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere, akifuatiwa na aliyekuwa Makamu wake Abdu Jumbe na Mama Sofia Kawawa.

  Jamii ya Wahadzabe inaishi kwa kutegemea uwindaji,kula matunda ya porini,mizizi ,wadudu na miti hata hivyo juhudi kubwa zimefanyika kuanza kuwafundisha kilimo, kuwapeleka watoto shule ,zaidi ya Wahadzabe 305 wanasoma kwenye shule ya msingi Munguli, pamoja na vijana zaidi ya 50 kupelekwa kujiunga na JKT.

  Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone kwa jitihada zake za kuwasaidia jamii ya Wahadzabe ikiwa pamoja na kuhakikisha wanapata elimu, wanajifunza kilimo lakini pia uamuzi wa kupima maeneo ya Wahadzabe ili wamiliki ardhi yao wenyewe.PICHA NA MICHUZI JR-MMG-SINGIDA
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akiwa kwenye nyumba maalum ya chifu wa wahadzabe pamoja na Mwenyekiti wa Wahadzabe Edward Mashimba na Mama Sarah Philipo.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakitoka kwenye nyumba ya Chifu wa Wahadzabe iliyopo kijiji cha Kibampa kata ya Mwangeza wilaya ya Mkalama mkoani Singida
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Kibampa ambako wakazi wake ni jamii ndogo yenye kaya 300 ya Wahadzabe,kushoto ni Mwenyekiti wa Wahadzabe Ndugu Edward Mashimba (kushoto) ambaye alikuwa akitafsiri kwa lugha ya Kihadzabe
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Kibampa ambako wakazi wake ni jamii ndogo yenye kaya 300 ya Wahadzabe,kushoto ni Mwenyekiti wa Wahadzabe Ndugu Edward Mashimba (kushoto) ambaye alikuwa akitafsiri kwa lugha ya Kihadzabe
  wakazi wa kijiji cha Kibampa ambaco wakazi wake ni jamii ndogo yenye kaya 300 ya Wahadzabe wakishangilia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia

  0 0


  0 0

  Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ukipita katika eneo la Msamvu mjini Morogoro kuelekea Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Msamvu mjini Morogoro wakati akiwa njiani kuelekea Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Wami dakawa mkoani Morogoro wakati akiwa njiani kuelekea Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa eneo la Magole mkoani Morogoro.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ukarabati unaondelea katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma eneo la Kibaigwa . sehemu ya barabara hiyo inakarabatiwa chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS.

  PICHA NA IKULU

  0 0

  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akilakiwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Singida leo, kaba ya kukutana na kuzungumza na wazee wa Singida Mjini. Kulia ni Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Mary Maziku.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akisubiri kuvalishwa skafu baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Singida leo. Kushoto ni Mama Salma Kikwete. na Kulia ni Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Singida Mary Maziku na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.
  Chipukizi wakimvalisha Skafu Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akienda katika Ofisi ya CCM mkoa wa Singida, akiwa na Mkewe Mama Salma Kikwete, Nape na Mary Maziku
  Kikwete akijadiliana jambo na Nape
  JK akiwasalimia wananchi
  JK akizungumza baada ya kupatiwa taarifa ya CCM Mkoa wa Singida. Kushoto ni Mary Maziku Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Singida
  Kina mama wakitumbuiza kwa ngoma kumlaki Kikwete Ofisi ya CCM mkoa wa Singida
  JK akisalimiana na mmoja wa wanachama wa CCM 
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akionyesha jengo lililokuwa Ofisi ya TANU mkoa wa Singida miaka ya 75 akiwa katibu msaidizi wa TANU wa wilaya

  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipiga picha na mke wake Mama Salma Kikwete, leo, mbele ya nyumba ambamoishi mjii Singida mwaka 1975, wakati huo akiwa katibu Msaidizi wa TANU wilaya ya Singida mjini. Kikwete yupo mkoani Singida kwa ajili ya kuongoza Maadhimisho ya Miaka 39 ya CCM, abayo kilele chake kitaifa ni kesho.
  JK akisalimiana na wazee alipowasili kuzungumza nao mjini Singida leo
  Na Richard Mwaikenda,Singida 

  MWENYEKITI CCM, Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amewaomba wazee kote nchini, kumuunga mkono Rais John Magufuli katika uongozi wake ili kumpa moyo wa kuwatumikia Watanzania.

  Alisema, kipindi ambacho Dk Magufuli ameingia madarakani hadi sasa ni mda mfupi, hivyo si vema kuanza kudodosa na kulaumu panapopwaya, badala yake Wazee na watanzania kwa jumla wazidi kumuunga mkono ili kumtia moyo wa kutekeleza yote aliyokusudia kuyafanya kwa manufaa ya taifa. 

  Kikwete alitoa ombi hilo alipokuwa akizungumza katika mkutano na wazee wa Mkoa wa Singida, ambapo alisema kuwa kuongoza bila ushauri wa wazee nchi inaweza kuyumba. "Kuongoza nchi bila wazee mambo hayaendi vizuri na ukikosa mzee kwenye jahazi wapiga makasia vijana wanaweza kuanza kuzozana na chombo kwenda mrama, lakini wakiwepo wazee watawaongoza vizuri na chombo/ nchi kwenda salama". Alisema Kikwete huku akishangilia na wazee. 

  Si Kila mzee ni mwasisi wa chama, kila mwenye mvi na mwasisi, wengine wameingia kwenye chama wazee. Alisisitiza kwamba ukitaka nchi itulie kamata wazee, lakini ukiongoza nchi kwa kutumia vijana pekee nchi inaweza kuyumba, na itafika mahali mtakosa mahali pa kushika. Alisema kuwa hata yeye kwa mara ya kwanza .alipokwenda kuomba ubunge jimboni kwake Bagamoyo, Pwani aliunda kamati ya wazee ambayo ilimsaidia sana. 

  Wazee ni sehemu ya matumaini ya chama na Serikali, panapokuwepo wazee hapaharibiki jambo. "Nawashukuru sana wazee endeleeni kukijenga chama na kuiunga mkono Serikali inayoongozwa sasa na Dk John Magufuli." Alisisitiza Kikwete na kuongeza kuwa, "Hata kwenye chama chetu tumeunda Baraza la Washauri la Wazee wasitaafu, ambapo wengi walipinga, hata hao wazee tuliowataka waunde baadhi yao walipinga, lakini mwisho walikubali kwa masharti kwamba wawe wanaitwa panapotokea jambo kubwa litakalohitaji ushauri wao." 

  Alisema mmoja wa viongozi aliyekuwa msitari wa mbele kuunda baraza hilo, alikuwa Rais msitaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ambaye alitoa ushauri wa kuitwa kutoa ushauri panapotokea jambo kubwa na kwamba hata wakitoa ushauri, viongozi waliopo madarakani wawe hiari kuukubali au kuukataa'. 

  Aliwataka wazee kuendelea kuiunga mkono serikali ya sasa ambayo kwa hivi sasa imetimiza muda mfupi wa miezi mitatu ambaye ni sawa na mtoto mdogo anayekua. Alisema kuwa Jambo kubwa ni kuwaunga mkono, kuliko kuwalaumu ama sivyo watavunjika moyo, ndani ya miaka mitano itakuwa hasara. watieni moyo ili wajiamini wahudumie vizuri zaidi ili nchi isonge mbele kimaendeleo.

  Kikwete alisisitiza kuwa hata yeye akitakiwa kwenda kutoa ushauri atakwenda, na akiwa na jambo la kushauri atakwenda pia, lakini aliwaasa kuwa si kila jambo wazee watake kwenda kutoa ushauri, itachelewesha mambo mengi. 

  JK akisalimiana na wazee alipowasili kwenye mkutano ambapo alizungumza na wazee wa mkoa wa Singida
  JK akiwasili katika mkutano na wazee wa Mkoa wa Sindiga leo
  Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungmza kabla ya kumkaribisha Mke wa Mwenyekiti wa CCM, Salma Kikwete kuzungumza na wazee wa Mkoa wa Singida
  Mama Salama Kikwete akizungumza katika mkutano huo
  Katibu wa Baraza la Wazee Mkoa wa Singida,Athuman Sima akisoma risala mbele ya Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete
  Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Singida, Juma Mudida akiapa mbele ya Jakaya Kikwete kuwa yupo tayari kupambana na mtu yeyote alatayepingana na utumbuaji wa majipu unaofanywa na Rais Magufuli
  Jakaya Kikwete akizungumza katika mkutano na wazee amabapo amewaomba kuunga mkono uongozi wa Rais John Magufuli ili nchi isonge mbele kimaendeleo.
  JK akiagana na mmoja wa wazee baada kumaliza kuzungumza nao
  JK akiagana na wazee baada ya kumaliza mkutano

  Baadhi ya wazee wakiondoka baada ya kuzungumza na JK mjini Singida leo

  0 0  Na Waandishi wa NEC, Mbeya

  Serikali imeombwa kuzifadhili Asasi za kiraia zinazotoa Elimu ya Mpiga kura ili ziweze kuwaelimisha wananchi kwa wakati umuhimu wa kupiga kura katika uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.

  Katika Uchaguzi Mkuu uliopita Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitoa vibali vya kutoa Elimu ya Mpiga kura kwa Asasi za kiraia 447 kutoka maeneo mbalimbali nchini lakini ni asasi chache zilizofanikiwa kupata fedha kutoka kwa wafadhili kwa ajili ya kutoa elimu hiyo.

  Wakizungumza kwenye Mkutano wa tathmini ya Elimu ya Mpiga Kura kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Asasi za Kiraia uliofanyika leo jijini Mbeya, wawakilishi wa Asasi hizo walisema Elimu ya Mpiga Kura inapaswa kutolewa mapema kwani katika Uchaguzi Mkuu uliopita asasi zilipata fedha kipindi kifupi kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu.

  Walisema kutokana na Asasi nyingi kutokupata fedha kutoka kwa wafadhili, Elimu ya Mpiga Kura haikuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi na hivyo kusababisha baadhi ya wananchi wengi kutojitokeza kupiga kura na kura nyingi kuharibika.

  Aidha, wajumbe hao pia wameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kusimamia na kuratibu Elimu ya Mpiga Kura ili iwe endelevu badala ya kusubiri kutoa Elimu hiyo katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu pekee.

  Naye Msimamizi wa Uchaguzi wa jiji la Mbeya Dkt. Samwel Lazaro amezitaka Asasi za kiraia kuhakikisha zinatoa elimu hiyo mpaka kwenye maeneo ya vijijini ambapo wananchi hawapati taarifa za kutosha ukilinganisha na maeneo ya mijini.

  Alisema Elimu hiyo ikitolewa kwa ufasaha itasaidia kupunguza idadi ya kura zinazoharibika na kuongeza idadi ya wananchi wanaojitokeza kupiga kura wakati wa uchaguzi Mkuu.

  Katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, jumla ya wananchi milioni 22,658,247 waliandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambapo kati ya hao, 15,596,110 sawa na asilimia 67 waliojiandikisha walijitokeza kupiga kura. Kura zilizoharibika au kukataliwa zilikuwa ni 402,248 sawa na asilimia 2.5.

  Mkutano wa Tathmini ya Elimu ya Mpiga Kura kati ya Tume na Asasi za Kiraia ulizishirikisha Asasi za kiraia zaidi ya 15 kutoka mikoa mitatu ya Mbeya, Rukwa na Katavi zilizopewa kibali na Tume ili kutoa elimu ya mpiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

  0 0


  H.E. Mama Salma Kikwete earlier today met with Ms. Natalie Gonnella – Platts and Toun Olateju who paid a visit to WAMA Foundation. Natalie works with First Ladies Initiative while Toun works with Pink Ribbon Red Ribbon at the George W. Bush Presidential Centre.

  Mama Salma Kikwete partnered with Mrs. Laura Bush, former First Lady of US to launch the First Ladies Initiative in Dar es Salaam three years ago. Mama Kikwete champions efforts to curb the spread and morbidities associated with breast and cervical cancers in Tanzania which is one of the key priorities of the Bush centre through Pink Ribbon Red Ribbon initiative.

  Speaking at the meeting, Mama Kikwete reiterated her commitment to continue supporting women and girls in the areas of education, health and economic empowerment. These are the three pillars that cannot be tackled separately if we wish to transform the lives of women in Tanzania, Said Mama Kikwete. WAMA understands and embraces this concept to the extent that they constitute part of the four strategic objectives of the organization.

  “I am look forward to continue working with Mrs. Laura Bush, Former US First Lady, President Bush and other colleagues at Bush Institute to increase awareness and expand treatment services for cervical and breast cancer. Having made significant investment in cervices, awareness becomes a very important strategy in mobilizing masses to come forward and utilize screening and treatment services for early signs. We are also keen to continue working with other partners to rollout vaccination to young girls” Mama Kikwete said.

  Mr. Daudi Nasib, WAMA Executive Secretary on his part explained WAMA’s in championing the national HPV vaccination program for young girls. He highlighted the progress made by the Government of Tanzania in introducing Human Papilloma Virus (HPV) for young Girls aged 9 to 13. The vaccination program was officially launched in Kilimanjaro Region by Mama Salma Kikwete, then First Lady and WAMA Chairperson, in 27th April 2014 during the National Immunization Week.

  “Since then the WAMA Chairperson has been doing advocacy all over the country in rolling out the vaccination program around the country. WAMA has mobilized resources to conduct mass screening and treatment campaigns for cervical and breast cancer in Tanzania” Mr. Nasib said

  Ms. Toun Olateju Manager, Country Programs of Pink Ribbon Red Ribbon expressed her great appreciation to WAMA Foundation Chairperson, Mama Salma Kikwete and staff for the excellent performance in implementing the Pink Ribbon Red Ribbon Initiative on Prevention and treatment of Cervical Cancer in Tanzania.

  “I would like to convey Mrs. Laura Bush greetings to Mama Salma Kikwete and WAMA Staff. They are all committed to this initiative and will continue collaborating with you to improve the health of women in Tanzania” Ms. Olateju said. 

  Ms. Natalie Gonnella, Manager First Ladies Initiative from George W. Bush Institute added that Mrs. Laura Bush is very active and eager to continue relationship with WAMA Chairperson. She informed mama Kikwete that the George W. Bush Institute and the International Center for Research on Women (ICRW) are now working on a research study on the role and influence of the First Ladies in improving their people’s lives. Since she is a great example of what the First Ladies could do to improve lives of the communities, they would like to engage her in this research”. Natalie told Mama Salma Kikwete.

  The Pink Ribbon Red Ribbon initiative was introduced in Tanzania in 2013 during the African First Ladies Summit, themed Investing in Women: Strengthening Africa that was held in Dar es Salaam from July 02-03, 2013. WAMA Foundation partners with Medical Women’s Association of Tanzania (MEWATA), T-MARC Tanzania, Tanzania Youth Alliance (TAYOA) and the Mbeya HIV/AIDS Network to implement the Pink Ribbon Red Ribbon Initiative in Tanzania.

  0 0

   Katibu Mku wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM,Rais Mstaafu wa awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete mapema leo asubuhi ndani ya uwanja wa Namfua, kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM mkoani Singida
   Mwenyekiti wa CCM,Rais Mstaafu wa awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete akiwapungia mkono Wananchi waliofika kushuhudia maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM  mapema leo asubuhi ndani ya uwanja wa Namfua, mkoani Singida.
   Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ukiwasili ndani ya uwanja wa Namfua mapema leo asubuhi kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM mkoani Singida
   Katibu Mku wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Rais Dkt John Pombe Magufuli mapema leo asubuhi ndani ya uwanja wa Namfua, kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM mkoani Singida
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akimkaribisha Rais Dkt John Pombe Magufuli mapema leo asubuhi ndani ya uwanja wa Namfua, kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM mkoani Singid,pichani kati ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana
   Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi alipokuwa akiwasilia mapema leo asubuhi ndani ya uwanja wa Namfua,mapema leo asubuhi ndani ya uwanja wa Namfua, kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM mkoani Singida
   Badhi ya Wananchi mbalimbali wakifuatilia yanayojiri ndani ya uwanja wa Namfua mkoani Singida hivi sasa. 

  PICHA NA MICHUZI JR-MMG-SINGIDA
  0 0


  Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Tamasha la Pasaka litakalofanyika  Mkoani Shinyanga Wilayani Kahama Machi 28 mwaka huu ambapo Tamasha la Pasaka mwaka huu halitafanyika jijini Dar es Salaam na baadala yake kufanyika mikoani. 

  Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama wakati akizungumza nao leo jijini Dar es Salaam.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  TAMASHA la Pasaka mwaka huu kufanyika Machi 28 Mkoani Shinyanga katika viwanja kahama wilaya ya Kahama, ambapo tamasha hilo limewapa kipaumbele waimbaji wa ndani ya nchi yetu.

  Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

  Msama amesema kuwa Kauli mbiu ya Tamasha la Pasaka mwaka huu ni "UMOJA NA UPENDO HUDUMISHA AMANI KATIKA NCHI YETU". ambayo itatawala katika tamasha hilo hapa nchini.

  Msama amesema kuwa Mwimbaji wa nyimbo za Injiri Bonfasi Mwaitege amethibisha kutumbuiza katika tamasha hilo pamoja na Mwimbaji wa nyimbo za Injiri Rose Mhando.

   Aidha Msama amelishukuru  Balaza la Sanaa Tanzinia(BASATA) kwa kuruhusu kufanyika Tamasha la Pasaka wilayani Kahama pia amewaomba wananchi wajitokeze kwa wingi katika tamasha hilo mkoani humo.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akizungumza na Watendaji na Viongozi wa Serikali za Mitaa wa wilaya hiyo kwenye mkutano uliofanyika Dar es Salaam leo kuhusu jinsi ya kutatua na kukomesha kero za ardhi
  Watendaji na Viongozi wa Serikali za Mitaa wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo, Paul Makonda (hayupo pichani)

  Na Dotto Mwaibale

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ametoa siku 20 kwa Wenyeviti wote wa Serikali za Mitaa Manispaa hiyo kuwa na ramani ya mitaa ili kuyatambua maeneo ya wazi.Makonda amewataka watendaji wa Manispaa hiyo kwenda na kasi ya serikali ya kuwatendea haki wananchi katika kumaliza migogoro ya ardhi.

  Akizungumza Dar es Salaam leo mchana na Wenyeviti zaidi ya 100 wa Serikali za Mitaa ya9 Manispaa ya Kinondoni ,Makonda alisema baadhi ya watendaji wanatanguliza maslahi mbele kuliko mahitaji ya Wananchi na Taifa kwa ujumla.

  Alisema migogoro ya ardhi ni kero kila sehemu misibani, harusini na kwenye mazishi suala kubwa ni la ardhi na kuongeza kuwa mabaraza ya ardhi ya Kata hayana uhalali wa kuamua kesi hizo kwa kuwa baadhi yao hata uelewa wa masuala hayo hawana na yamekuwa yakiongeza matatizo.

  "Leo tumekutana hapa kwa sababu ya migogoro ya ardhi na kuanzia sasa ndani ya Wilaya ya Kinondoni nataka kurudisha heshima ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa nawaagiza kuanzia sasa mtu yeyote kutoka Wizarani,Manispaa au hata mwekezaji lazima apitie kwanza kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mitaa,"alisema.

  Alisema watendaji wengi Manispaa ndio chanzo cha migogoro ya ardhi kwa kutotimiza wajibu wao na wameshindwa kuonyesha dira ya kuwasaidia wananchi."Kibaya zaidi ili kujitengenezea mazingira ya ulaji wenyeviti hawashirikishwi katika hatua za awali wanahusika zaidi pale kunapotokea mgogoro,"alisema.

  Aliongeza kuwa "Sina hofu wala uoga wala sina sifa ya kupendwa wala kutafuta kupendwa hivyo nitahakikisha ninatumia Mamlaka niliyopewa kufanya migogoro hii ya ardhi Kinondoni na kuwa historia na nikitaka jambo huwa sishindwi"alisema.Alisema baada ya wenyeviti hao kupewa ramani atahakikisha anakutana na Wazi ri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wilium Lukuvi na maofisa wa ardhi."Hapo sasa watakaobainika kuhusika katika michezo michafu na kuchochea migogoro basi Waziri Lukuvi aondoke nao maana wameshindwa kazi"alisema

  Makonda aliwataka wenyeviti hao kuonesha maeneo ya wazi na yale yaliyovamiwa ili kuchukua hatua kwani wenye dhamana wapo ofisini huku wananchi wakiwa wanateseka na migogoro hiyo.Mkuu wa Idara ya Mipango Miji Manispaa ya Kinondoni Juliana Letara alisema Wenyeviti wote watapewa ramani za mitaa yao ndani ya wiki mbili kwa kuwa zipo kwenye kompyuta ofisini hivyo atawapatia ramani hizo.

  Alisema kutokana na migogoro mingi ya ardhi anapendekeza kufanyike mapendekezo ya mabadiliko ya sheria kwa kuwa kesi zote za mabaraza ya kata zinaigharimu serikali zaidi ya milioni tatu kwa siku.Alizitaja kesi hizo kuwa ni za ardhi ya hifadhi,ardhi ya kawaida na ile ya kimila 


  "Tulikopa benki ya TIB mkopo kwa ajili ya kupima Viwanja likiwemo eneo la Mabwepande lakini kila siku tunatozwa riba ya sh.milioni tatu jambo ambalo ni gumu na ipo siku litashindikana na ndio maana tunauza Kiwanja hadi milioni 20 na 30,"alisema. Baadhi ya wenyeviti wa Serikali za Mitaa ambao walipata nafasi ya kuzungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo walimtaka Makonda kuondoa majipu sugu katika Manispaa hiyo likiwemo la maofisa mipango miji.


  Alisema wako tayari kufanyazi na Makonda lakini sio wafanyakazi hao kitengo cha ardhi kwa kuwa wamekuwa chanzo cha migogoro mikubwa ya ardhi.  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh. Amos Makalla na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na usalama Mkoa wamekagua mpaka wa Tanzania na Kenya amekagua alama za mpaka (mawe) ameridhishwa na hali ya usalama wa mpaka na kuagiza kamati ya ulinzi na usalama wiilaya kuwa na mikutano ya ujirani mwema .Aidha Mkuu wa Mkoa ameshiriki kuteketeza mitambo 6 ya kutengeneza pombe haramu ya Gongo, lita 140 za gongo, pipa 33 za maloweko ya gongo  Pia amewataka wananchi kuacha unywaji na upikaji gongo.
  Baadhi ya mitambo ya kutengeneza pombe haramu ya Gongo,

  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa Balraza la Michezo Zanzibar BMZ akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi fedha kwa timu za JKU na Mafunzo za mchezo wao wa Kombe la CAF inayotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
  Meneja wa Makampuni ya Hoteli za Ocean View Zanzibar Jacob Makundi akizungumza na Waandishi wa habari na Viongozi na Wachezaji wa Timu za JKU na Mafunzo wakati wa kukabidhi fedha za ununuzi wa tiketi wa michuano hiyo inayoandaliwa na CAF Championc Leagua na Confederation Cup 2016. na kuahidi kutowa gharama zote za michezo hiyo. inayotarajiwa kufanyika tarehe 13-2-2016 na 14-2-2016 katika uwanja wa amaan Zanzibar.
  Viongozi wa Timu za JKU na Mafunzo wakimsikiliza Meneja wa Makampuni ya Zanzibar Ocean View Zanzibar akizungumza wakati wa hafla hiyo na kutoa ahadi kwa kilia Timun ikishinda mchezo wao huo wa awali itazawadiwa shilingin Milioni Tano kwa ushindi wowote ule,wakati wa hafla ya kukabidhi fedha za tiketi za mchezo huo Kampuni yake imenunua tiketi zote zenye thamani ya shilingi miliono tano kila moja na kutowa fursa kwa Wapenzi wa mchezo wa mpira Zanzibar kuona mapambano hayo bure bila ya kiingilio.
  Meneja wa Makampuni ya Hoteli ya Zanzibar Ocean View Zanzibar Jacob Makundi akimkabidhiwa Tiketi ya Mchezo wa JKU na Gaborone United Club na Kiongozi wa Timu ya JKU Khamis Mohammed, mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Kampuni ya Zanzibar Ocean View Imenunua tiketi hizo zote za mchezo huo na kutowa fursa kwa Wananchi na Wapenzi wa Michezo Zanzibar kujionea Michuano hiyo ya CAF kujionea bure. makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa hoteli hiyo Kilimani Zanzibar.
  Meneja wa Makampuni ya Hoteli ya Zanzibar Ocean View Zanzibar Jacob Makundi akimkabidhi Milioni tano fedha za mauzo ya Tiketi ya Mchezo wa JKU na Timu ya Gaborone United Club Kiongozi wa Timu ya JKU Khamis Mohammed, mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Kampuni ya Zanzibar Ocean View Imenunua tiketi hizo zote za mchezo huo na kutowa fursa kwa Wananchi na Wapenzi wa Michezo Zanzibar kujionea Michuano hiyo ya CAF kujionea bure. makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa hoteli hiyo Kilimani Zanzibar.
  Meneja wa Makampuni ya Hoteli ya Zanzibar Ocean View Zanzibar Jacob Makundi akimkabidhi Milioni tano fedha za mauzo ya Tiketi ya Mchezo wa Mafunzo na AS Vita Club ya Congo Kiongozi wa Timu hiyo Khamis Ali Machenga, mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Kampuni ya Zanzibar Ocean View Imenunua tiketi hizo zote za mchezo huo na kutowa fursa kwa Wananchi na Wapenzi wa Michezo Zanzibar kujionea Michuano hiyo ya CAF kujionea bure. makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa hoteli hiyo Kilimani Zanzibar.
  Meneja wa Makampuni ya Hoteli ya Zanzibar Ocean View Zanzibar Jacob Makundi akimkabidhi Milioni tano fedha za mauzo ya Tiketi ya Mchezo wa Mafunzo na AS Vita Club ya Congo Kiongozi wa Timu hiyo Khamis Ali Machenga, mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Kampuni ya Zanzibar Ocean View Imenunua tiketi hizo zote za mchezo huo na kutowa fursa kwa Wananchi na Wapenzi wa Michezo Zanzibar kujionea Michuano hiyo ya CAF kujionea bure. makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa hoteli hiyo Kilimani Zanzibar.
  Wachezaji wa Timu za JKU na Mafunzo wakiwa katika hafla hiyo katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
  Wachezaji wa Timu za JKU na Mafunzo wakiwa katika hafla hiyo katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
  Imetayarioshwa na OthmanMapara.Blogspot Zanzinews.com

  0 0

   
  Hii ni sehemu ya hotuba fupi ya Rais Dkt John Pombe Magufuli alipoitoa leo mchana mbele ya Wananchi wa Singida,alipoombwa awasalimie,kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM mkoani Singia

  " Leo sio siku yangu ya kutoa hutuba, leo ni siku ya bosi wangu, mheshimiwa Mmwenyekiti wetu wa chama cha mapinduzi, chama tawala ambapo sisi viongozi tunatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi. Lakini nataka nichukue nafasi hii chanya ambayo nimepewa niwashukuru wananchi wa Singida na watanzania kwa ujumla kwa kunipa kura nyingi na kuwa Rais wenu. 

  Napenda kukuthibitishia mwenyekiti wetu, mimi pamoja na serikali ninayoiongoza tutaendelea kukienzi chama cha mapinduzi na tutatekeleza ilani ya uchaguzi ili wananchi wote waweze kuondolewa kero zao.Kero zote zinazowakabili wananchi tutahakikisha tunazitafutia ufumbuzi wa haraka, lengo likiwa ni kufuta kabisa ndoto za wapinzani kushika dola.

   Na nitoe wito kwa watendaji wote wa serikali, watendaji wote wa serikali kuanzia juu mpaka chini, anaejijua ni mtendaji wa serikali ana jukumu moja tu la kutekeleza Ilani ya chama cha mapinduzi. 

  Asieweza atupishe pembeni, uwe mkuu wa wilaya, tekeleza ilani ya CCM, uwe katibu tarafa, wewe uko ndani ya CCM kwa sababu tunaoteua ni sisi, mimi ni Rais lakini ni Rais niliechaguliwa na chama cha mapinduzi. Kwa hio nitoe wito kwa watendaji wa serikali ambao wanapokuwa kule wanajifanya wao ni watendaji wa serikali, wajue serikali hii inaongozwa na Rais mwana CCM ambae yuko hapa kwa ajili ya kutekeleza. 

  Nilitaka hili niliweke wazi, tumedhamiria kufanya kazi na ninasema tutafanya kazi kwelikweli na ndio maana kauli yetu ni hapa kazi tu, lakini pia imeungwa mkono na chama changu na mheshimiwa mwenyekiti kwamba kazi ipo pale" .

older | 1 | .... | 756 | 757 | (Page 758) | 759 | 760 | .... | 1897 | newer