Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 755 | 756 | (Page 757) | 758 | 759 | .... | 1904 | newer

  0 0

   Kijiko cha Kampuni ya Udalali ya Mem Auctioneers and General Brokers Ltd kikibomoa nyumba za makazi ya watu na biashara zilizojengwa katika eneo la Kampuni ya Dar es Salaam Cold Makers Ltd lililopo Shekilango Sinza jijini Dar es Salaam leo asubuhi.   Kijiko kikibomowa moja ya baa zilizokuwepo eneo hilo jirani na Baa ya Rego iliyopo Sinza jijini Dar.
   Wananchi, wamiliki wa nyumba na mabaa katika eneo wakiwa wamepigwa butwaa

   Hapa ni kupiga picha eneo la tukio na huzuni tupu.

   Kijiko kikibomoa nyumba ya ghorofa katika eneo hilo.
   Askari Polisi na mgambo wakiwa eneo la tukio kuimarisha ulinzi.
  Kontena likiondolewa katika eneo hilo inadaiwa mmiliki wa kontenta hilo aliuziwa eneo hilo miezi ya hivi karibuni kwa sh.milioni 400. hakika ni hasara kubwa.


  Na Dotto Mwaibale

  KAMPUNI ya Udalali ya Mem Auctioneers and General Brokers Ltd imebomoa nyumba za makazi ya watu na biashara zilizojengwa katika eneo la Kampuni ya Dar es Salaam Cold Makers Ltd lililopo Shekilango Zinza jijini Dar es Salaam.
  Uvunjaji wa nyumba hizo uliofanyika Dar es Salaam leo ambao ulisimamiwa na jeshi la polisi na mgambo uliwaanja mdomo wazi na wasijue cha kufanya wamiliki wa nyumba hizo na wafanyabiashara wa nyama choma ya nguruwe ambao wengi wao walishindwa kuondoa mali zao na kujikuta wakiingia hasara kubwa.
  Akizungumza na wanahabari eneo la tukio Meneja wa Biashara wa kampuni hiyo ya udalali, Elieza Mbwambo alisema wamebomoa nyumba hilo kwa agizo la mahakama baada ya mteja wao Dar es Salaam Cold Makers kushinda kesi ya msingi iliyofunguliwa na mtu aliyetajwa kwa jina la Ondolo Chacha aliyekuwa akidai eneo hilo ni lake.
  Mbwambo alisema kuwa eneo hilo lililokuwa linadaiwa kuwa ni mali ya Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kampuni hiyo lilikuwa na mgogoro tangu mwaka 1993 kati ya wamiliki halali na wavamizi ambayo ilikuwa ikisikilizwa kwa nyakati tofauti ambapo mmiliki wake halali alikuwa akishinda lakini watu wanaodaiwa wavamizi wakawa wanaweka pingamizi hadi aliposhinda tena hivi karibuni.
  "Baada ya mmiliki halali kushinda kesi hiyo mahakama ilitupa kibali cha kuwaondoa wavamizi ambao tumekuja kwaondoa baada ya kuwapa notisi lakini mfungua kesi hakuweza kuwapa notisi hiyo jambo lililoleta changamoto ya kwa watu waliokuwa wakitumia eneo hilo kushindwa kuokoa vitu vyao" alisema Mbwambo.
  Mbwambo alisema mteja wao kwa zaidi ya miaka 20 alishindwa kutumia eneo hilo kwa shughuli zake za uzalishaji mali kutokana na mgogoro.
  Mmoja wa wafanyabiashara katika eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la James alisema yeye alipangishwa katika eneo hilo kwa kulipa sh.milioni 20 hivyo ameingia hasara kubwa ya ujenzi wa mabanda na vitu vilivyokuwemo ambapo amepoteza zaidi ya sh.milioni 70.
  Mfanyabiashara huyo alisema eneo hilo walikuwa wakipangishwa na watu waliouziwa na mtu aliyedai ni lake na miezi michache iliyopita kuna mzee mmoja aliuziwa sehemu ya barabara na kutoa sh.milioni 400 na kujikuta akiingia katika hasara kubwa.
  "Tuta watafuta waliotuuzia maeneo katika eneo hilo na kutupangisha ili waweze kuturudishia fedha zetu" alisema James.

  0 0

  John Pambalu ambae ni diwani wa Kata ya Butimba (Chadema) akiwasilisha mchango wake katika kikao cha baraza la madiwani Jijini Mwanza.

  Na:George Binagi-GB Pazzo
  Madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Jijini Mwanza, wamemlalamikia Mstahiki Meya wa Jiji hilo kwa madai ya kuliongoza kibabe baraza la Madiwani.

  Wakizungumza baada ya kikao cha baraza la Madiwani kilichoketi hii leo, Madiwani hao wamelalamikia kitendo cha kuzuiliwa kujadili taarifa ya Kamati ya fedha iliyowasilisha katika kikao hicho kwa madai kwamba jukumu la baraza hilo ni kupitisha taarifa hiyo na si kuijadili.


  Samwel Range ambae ni diwani wa Kata ya Pamba pamoja na John Pambalu ambae ni diwani wa Kata ya Butimba (Wote Chadema), wamesema wamesikitishwa kuona kanuni za vikao zikivunjwa huku madiwani wakinyimwa fursa ya kujadili taarifa ya kamati ya fedha iliyowasilishwa.


  “Tumeshuhudia utawala wa kibabe ukianza katika halmashauri yetu huku mhe.Mwenyekiti wa kikao (Meya) pamoja na Mkurugenzi wake wakiamua kutofuata kanuni na kuamua kufuata matakwa yao binafsi. Tumeletewa taarifa ya kamati ya fedha, wakati wa kujadili tunaambiwa hakuna sababu ya kuijadili isipokuwa kuipitia na kuiidhinisha taarifa hiyo, kitu ambacho madiwani wa Chadema na Upinzani tunakilalamikia”. Alisema Pambalu.


  Nae Samwel Range amesema “Kamati ya fedha haina mamlaka ya kuidhinisha chochote ndani ya halmashauri ya Jiji la Mwanza. Inapaswa ilete taarifa yake na kuileta katika baraza la Madiwani ambapo sisi tunauwepo wa kuikubali au kuikataa”.


  Hata hivyo malalamiko hayo yamepingwa na James Bwire ambae ndie Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza na diwani wa Kata ya Mahina (CCM), ambapo amefafanua kwamba malalamiko ya madiwani wa Chadema hayana msingi wowote ikizingatiwa kwamba taarifa iliyowasilishwa na kamati ya fedha iliishajadiliwa ndani ya kamati hivyo hakukuwa na umuhimu wa kuijadili tena ndani ya baraza la madiwani bali kuipokea na kuipitisha.


  Baraza la Madiwani Jijini Mwanza linaundwa na Madiwani 24 na linaongozwa na Chama cha Mapinduzi CCM kwa upande wa Mstahiki Meya pamoja na Naibu Meya ambapo kuna Madiwani 19 kutoka CCM huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kikiwa na Madiwani Watano.  Kutokana na Uwiano huyo, Madiwani wa Chadema wanalalamika kuburuzwa katika baraza hilo kutokana na uchache wao, madai ambayo hata hivyo yanapingwa na Madiwani kutoka CCM ambao wanasema suala lolote lenye maslahi kwa umma linapewa nafasi sawa ndani ya baraza hilo bila kujadi itikadi za vyama vya siasa. 
  Kushoto ni Naibu Meya Jiji la Mwanza, Katikati ni Mstahiki Meya na Kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza
  Waheshimiwa Madiwani Jijini Mwanza.

  Waheshimiwa Madiwani Jijini Mwanza
  Watendaji wa Idara mbalimbali Jijini Mwanza.

  0 0

   Jaji Mkuu wa  Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwahutubia viongozi, mabalozi na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Sheria.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo kuhusu utendaji wa Mahakama na Utoaji wa Haki kwa wananchi kwa wakati kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria. Mhe. Rais alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na viongozi na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama ya Tanzania leo wakati wa kilele cha Siku ya Sheria nchini.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa dini na baadhi ya wakuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania wakati wa kilele cha Siku ya Sheria.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mawakili.
  Jaji Mkuu wa Kenya Dkt. Willy Mutunga (kulia) akimkabidhi zawadi ya kumbukumbu kutoka nchini Kenya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo jijini Dar es salaam. Jaji Mkuu wa Kenya alikua miongoni mwa wageni mashuhuri walioalikwa na Mahakama ya Tanzania kuhudhuria maadhimisho ya Siku ya Sheria.
  Wageni mbalimbali waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Sheria wakifurahia Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli aliyokua akiitoa leo jijini Dar es salaam.


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokewa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman leo jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini. Rais, Dkt. John Magufuli alikua mgeni rasmi. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria leo jijini Dar es salaam.
   Wimbo wa Taifa ukipigwa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya      Sheria. Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.     Dkt. John Pombe Magufuli (Kulia) akiwa na Jaji Mkuu wa                               Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman 
  Baadhi ya Viongozi waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya Sheria wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa. Kutoka kulia ni Jaji Mkuu wa Kenya Dkt. Willy Mutunga, Jaji Kiongozi wa Tanzania Mhe. Shaaban Lila (katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Mecki Sadiki.

  Baadhi ya Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama  nchini na wadau muhimu wa Mahakama waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya Sheria wakitoa heshima zao wakati wimbo wa Taifa ukipigwa.
  Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Charles Rwechungura akitoa salam na ujumbe wa Chama hicho wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria leo jijini Dar es salaam.
  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kulia) akifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa na viongozi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga.

  (Na. Jacquiline Mrisho/Aron Msigwa - Dar es salaam)

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Mahakimu na Majaji wa Mahakama ya Tanzania kufanya kazi kwa kuzingatia weledi wa taaluma ya Sheria katika kushughulikia mashauri  yanayopelekwa Mahakamani.

  Aidha amewataka Majaji na Mahakimu kutoa hukumu za mashauri  yanayowasilishwa Mahakamani kwa haraka ili kuwasidia wananchi wanaotafuta haki.

  Akizungumza na mamia ya wageni kutoka ndani na nje ya nchi waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya sheria, Dkt. Magufuli amewataka Majaji na Mahakimu hao kutanguliza Uzalendo na maslahi ya taifa mbele pindi wanapotoa maamuzi ya mashauri yaliyoko Mahakamani.

   Mhe. Rais amemtaka Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  kuchukua hatua kwa watendaji wa Mahakama wanaokiuka maadili kwa kufanya vitendo vinavyochafua taswira ya Mahakama mbele ya macho ya jamii.

  Aidha, Katika hotuba yake Mhe. Rais amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuijengea uwezo wa kifedha Mahakama ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.


  Kwa taarifa zaidi fuatilia hotuba yake kwa njia ya sauti hapo chini


  0 0

  Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi.Costancia Gabusa (katikati) akichangia mada wakati wa kikao cha kupitia Filamu ya “DADA” kilichofanyika katika ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania leo jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimejumuhisha wajumbe kutoka Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu, Jeshi la Polisi, Wizara ya Afya na Maendeleo ya jinsia, wazee na watoto na TCRA.Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo na kushoto ni Afisa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Fredrick Mgaza.
  Katibu Mtendaji waBodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo akielezea jambo wakatika wa kikao kazi kwa ajili ya mapitio ya Filamu ya “DADA” iliyowasilishwa ofisini kwake kwa ajili ya ukaguzi leo jijini Dar es Salam.Kushoto ni Mtengenezaji na Mmiliki wa Filamu hiyo Bi. Christina Mroni.
  Wajumbe wa kikao cha mapitio ya Filamu ya “DADA” wakifuatilia Filamu hiyo leo jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (mwenye gauni la kitenge) akiwa na baadhi ya Wajumbe wa kikao cha mapitio ya Filamu ya “DADA” wakifuatilia Filamu hiyo leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Muongozaji wa na Mmiliki wa Filamu hiyo Bi. Christina Mroni.

  Picha na Frank Shija,WHUSM

  0 0

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akisoma hotuba yake kabla ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Mahakama katika Siku ya Sheria Duniani katika uwanja wa Mahakama mtaa wa Chimala eneo la Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 4, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Mahakama katika Siku ya Sheria Duniani katika uwanja wa Mahakama mtaa wa Chimala eneo la Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 4, 2016. 
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA


  Mkuu wa TAKUKURU (M) Ilala,

  S.L.P 6420, Kinondoni

  Simu : (022)2861088 Nukushi 2150047 

  Barua pepe: rbcilala@pccb.go.tz

  Ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Ilala imemkamata afisa wa ofisi ya uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam kwa tuhuma ya kuomba shilingi milioni 1 na kupokea Shilingi laki 5 kutoka kwa mfanyabiashara mwenye asili ya Kisomali mnamo tarehe 4 Februari, 2016.

  Bw.Kiangwike Ngumba mwenye cheo cha afisa mkaguzi wa uhamiaji alikamatwa baada TAKUKURU kupokea taarifa kutoka kwa Bw.Bille Mohamed kuwa mtuhumiwa na maafisa wengine walifika katika eneo lake la biashara na kuchukua hati ya kusafiria ya ndugu yake kwa madai kuwa wanakwenda kuifanyia ukaguzi. Hata hivyo, baadaye afisa huyo alimtaka mtoa taarifa kutoa kiasi cha shilingi milioni moja kama sharti la kurejesha hati hiyo.

  Uchunguzi wa tuhuma hii unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwafuatilia na kuwachunguza maafisa wengine waliohusika ili wafikishwe mahakamani. Afisa huyo na wenzake wanakabiliwa na tuhuma ya kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007. 

  Tunatoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza kuripoti vitendo au viashiria vyovyote vya rushwa dhidi ya watumishi wasio waadilifu katika ofisi za TAKUKURU ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

  IMETOLEWA NA RAPHAEL MBWAMBO- MKUU WA TAKUKURU MKOA WA ILALA 05/2/2016 


  0 0


  Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule (Kushoto), akizungumza na Mkurugenzi wa Mashariki mwa Afrika wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Uhalifu, Bw. Jose Vila De-Castillo, alipotembelea Ubalozini, jijini Nairobi, jana. Bw. De-Castillo aliomba Ubalozi uwe kiungo kati ya Taasisi yake na Serikali ya Tanzania. 

  Taasisi hiyo inaendesha mpango wa miaka mitano wa udhibiti wa rushwa, mitandao ya uhalifu, biashara na matumizi ya madawa ya kulevya, ujangili na biashara ya binadamu kwa nchi za Tanzania, Burundi,Comoro, 
  Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Madagascar, Mauritius, Rwanda, Seychelles na Somalia. Kulia ni Ofisa wa Ubalozi, Bw. Mussa Haji.

  0 0

  VIDEO ya Lupeza ya msanii wa kizazi kipya, Ali kiba ambaye pia ni 

  balozi wa WILD AID Afrika yazinduliwa jijini Dar es Salaam leo ikiwa wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya nchi walijitokeza kwa 
   wingi katika kumuunga mkono msanii na  balozi wa WILD AID Afrika, 

  katika uzinduzi wa video yake hiyo.

  Video hiyo iliyofanyiwa nchini marekani imezinduliwa katika Hoteli ya
  Slipway jiji Dar es Salaam huku kiba akiwataka watanzania na walimwengu
  kuachana na kujihusisha na ujangili wa kuuwa wanyama pori.


  Baadhi ya wasanii waliojitokeza ni AT,  MwanaFA, Aika, Nahreel,
  Vanessa, Jux,  Joh Makini, Wema Sepetu, Baraka Da Prince na wengine
  wengi.
   Msanii na  balozi wa WILD AID Afrika, Ali Saleh ‘Ali Kiba’ akizungumza na wadau mbalimbali  (hawapo pichani) juu ya  uzinduzi wa video yake mpya ya Lupeza jijini Dar es Salaam.

   Wadu mbalimbali wakimsikiliza  Msanii na  balozi wa WILD AID Afrika,Ali Saleh ‘Ali Kiba’katika uzinduzi wa video yake mpya ya Lupeza.jana jijini Dar es Salaam.

   Msanii na  balozi wa WILD AID Afrika,Ali Saleh ‘Ali Kiba’akiwakabidhi CD wasanii mbalimbali na wanau wa muziki mara baada ya uzinduzi huo.  0 0  0 0

   Mkuu wa Itifaki na Mawasiliano wa Jiji la Dar es Salaam Gaston Makwembe, akizungumza na wandishi wa habari (hawapo picha)  leo jijini Dar es Salaam, juu ya mradi wa kuboresha jiji unagharimu sh.milioni 500 ambao unatarajia kuanza Julai Mwaka huu,kulia ni Mkuu wa Idara ya Udhibiti Taka Protus Membe. 
  Wandishi wahaba habari wakimsikiriza Mkuu wa Itifaki na Mawasiliano wa Jiji la Dar es Salaam Gaston Makwembe.
  (Picha na Emmanue Massaka wa Globul ya Jamii)

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  HALMASHAURI ya Jijin la Dar es Salaam kutengeneza jiji katika ubora (Smart Area) ikiwamo kuondoa biashara zisizo rasmi katikati ya jiji.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo,Mkuu wa Itifaki na Mawasiliano wa Jiji, Gaston Makwembe amesema kuwa mradi huo wa kuboresha jiji unagharimu sh.milioni 500 ambao unatarajia kuanza Julai Mwaka huu.

  Makwembe amesema katika uboreshaji huo utakwenda sambasamba na uondoaji wa ombaomba katika ya jiji la Dar es Salaam.

  Maeneo yatakayoguswa ni barabara ya Kawawa kutoka makutano ya Kawawa na Karume hadi makutano ya Kawawa na Ali Hassan Mwinyi ,Makutano ya Mandela na Pungu pamoja maeneo ya mjini na Uwanja wa Ndege.


  Makwembe amesema katika uboreshaji huo ni pamoja na uzuiaji wa Pikipiki,bajaji,Maguta pamoja na gari zinazozidi tani 10 kuingia katikati ya jiji.

  0 0

  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akiongea na Ujumbe kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa(hawapo pichani). Ujumbe huo wa Washiriki wa Mafunzo wametembelea Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika ziara yao ya Mafunzo kuhusu Uendeshaji wa shughuli za Magereza hapa nchini.
  Wakufunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati yao na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani). Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Bregedia Jenerali, Jairos Mwaseba.
  Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kwa Washiriki wa Mafunzo kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa walipotembelea Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga kwa ziara yao ya Mafunzo(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Mwandamizi wa Magereza, Augustine Mboje.
  Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo kutoka chuo cha Ulinzi wa Taifa wakimwangalia mmoja wa wafungwa ambaye amepatiwa ujuzi gerezani wa kukata vitambaa vya nguo tayari kwa kushona nguo za wafungwa wliopo magerezani kama anavyoonekana katika picha katika Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Bregedia Jenerali, Jairos Mwaseba alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam akiwa pamoja na Washiriki wa Mafunzo katika chuo hicho cha Ulinzi wa Taifa(hawapo pichani) leo Februari 5, 2016(kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.

  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akisalimiana na Mkufunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa ambaye ni raia kutoka China(katikati) ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Bregedia Jenerali, Jairos Mwaseba alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam akiwa pamoja na Washiriki wa Mafunzo katika chuo hicho cha Ulinzi wa Taifa(hawapo pichani) leo Februari 5, 2016.

  0 0

  Dinah Somba Samanyi ambae ni Katibu wazWazazi (CCM) Mkoani Mwanza.

  ………………………………………
  Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
  Ikiwa hii leo ni Maadhimisho ya Miaka 39 tangu kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM, Wanachama wake wametakiwa kutulia ndani ya Chama hicho badala ya kujitoa katika chama jambo ambalo huwafanya baadae kujutia.Kauli hiyo imetolewa Mkoani Mwanza na Katibu wa Wazazi wa Chama hicho Ndg.Dinah Somba Samanyi, wakati akizungumza na BMG, kuhusiana na maadhimisho ya miaka 39 ya CCM mwaka huu 2016.

  Samanyi ametanabaisha kwamba, mwaka huu ikiwa ni miaka 39 tangu CCM kuasisiwa February 05,1977 ikiwa ni baada ya Muungano wa wa vyama viwili vya ASP kutoka Zanzibar na TANU kutoka Tanganyika, ni vyema wanachama wake wakawa waadilifu na kuepukana na tabia zisizo za kimaadili ambazo ni pamoja na kujitoa ndani ya chama hicho kama ambavyo baadhi yao wameshuhudiwa wakifanya jambo ambalo hata hivyo huwafanya baadae kulijutia.

  Kuhusu maadhimisho amesema “Chama kimejipanga vizuri katika kuadhimisha Siku hii na tangu kuzinduliwa Kitaifa kwa sherehe za maadhimisho haya kule Zanzibar, kumekuwa na shughuli mbalimbali zinazolenga kuimarisha uhai wa chama pamoja na kushiriki shughuli tofauti tofauti za kijamii”.

  Samanyi amebainisha “Katika Mkoani Mwanza kila Wilaya imepewa fursa ya kuandaa shughuli mbalimbali kwa ajili ya maadhimisho haya. Jumuiya mbalimbali ikiwemo Jumuiya ya Wazazi zimeshiriki shughuli tofauti tofauti kama vile kutembelea mashuleni, kufanya usafi wa mazingira pamoja na kutembelea wagonjwa Mahospitalini”.

  Nao baadhi ya makada wa vyama vya siasa Mkoani Mwanza wametoa maoni yao kuhusiana na miaka 39 ya CCM kikiwa ni chama kinachoongoza Serikali, ambapo Kada wa CCM Sarah Ramadhan anasema anasema kuwa miaka 39 ya chama hicho, taifa limepiga hatua kubwa kimaendeleo ikilinganishwa na miaka iliyopita huku Amos Joseph ambae ni Kada ya Chadema akisema kuwa miaka 39 ya uongozi wa CCM taifa limeshindwa kutatua changamoto za kimaendeleo ikizingatiwa kwamba maendeleo yaliyopatikana hayaendani na raslimali za asili zilizopo nchini.

  Pengine Maoni ya Makada hao ni fursa nyingine ya kuiwezesha CCM kuzidi kuwatumikia vyema Watanzania ili miaka 40 ijayo mwakani kusiwepo na utofauti wa kimtizamo pindi makada wa vyama vya siasa watakapokuwa wakitoa tena maoni yao.

  Kitaifa Sherehe za Miaka 39 ya Kuasisiwa Chama cha Mapinduzi CCM kwa mwaka huu, zilizinduliwa Visiwani Zanzibar na Dkt.Ali Mohamed Shein ambae ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa na kilele chake kinahitimishwa Mjini Singida katika Uwanja wa Namfua ambapo zitahitimishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.

  0 0
 • 02/05/16--07:13: Article 17
 • HOTUBA YA MHE. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUHITIMISHA SHUGHULI ZA MKUTANO WA PILI WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  TAREHE 5 FEBRUARI, 2016  I:       UTANGULIZI
  (a)                Masuala ya Jumla

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  1.            Kwanza nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kutujalia afya njema na uwezo katika kutenda yote yaliyo mema. Tumekuwepo hapa kwa takriban siku 11 katika shughuli za Mkutano wa Pili wa Bunge lako Tukufu. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutufikisha salama siku ya leo.

  2.            Tumekutana hapa tukiwa tumeshuhudia uundwaji wa Serikali unaoendelea ambapo Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya uteuzi wa Baraza jipya la Mawaziri ambao ni Waheshimiwa Wabunge wenzetu. Niruhusu nitumie nafasi hii ya awali kuwapongeza Mawaziri na Naibu Mawaziri wote ambao wameteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali katika Serikali ya Awamu ya Tano.

  (b)        Chaguzi Mbalimbali  

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  3.            Katika Mkutano huu, tumeweza kufanya Chaguzi za Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge. Vilevile, tumefanya chaguzi za Wenyeviti wa Bunge letu na Wajumbe wa kutuwakilisha katika Taasisi mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa. Kwa vile orodha ni ndefu, napenda nitumie nafasi hii kuwapongeza kwa dhati kabisa na kwa ujumla wao wote waliogombea nafasi hizo na kushinda. Ni matarajio yangu kwamba tutatumia nafasi hizo vizuri katika kuleta ushirikiano, mshikamano na kufanya kazi pamoja kama Wawakilishi wa Wananchi na kutekeleza majukumu yetu kama Wabunge ndani ya Bunge hili.

  (c)                Maafa na Ajali

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  4.            Tarehe 27 Januari, 2016 wakati Bunge lako Tukufu likiendelea na Vikao, Waheshimiwa Wabunge walipewa taarifa ya kusikitisha ya kuzama kwa Kivuko cha Kilombero, ambapo katika tukio hilo watu walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa. Aidha, mali za abiria zimepotea. Wakati huo huo, mvua zinazoendelea kunyesha nchini katika baadhi ya maeneo zimesababisha mafuriko, vifo, uharibifu wa mali ikiwemo mazao na miundombinu. Katika baadhi ya maeneo, mvua hizi zimesababisha njaa na athari nyingine kwa jamii.

  5.            Pamoja na maafa ya mvua na mafuriko, wapo wananchi waliofariki na wengine kupata ulemavu katika ajali mbalimbali za vyombo vya usafiri. Nitumie fursa hii kuwapa pole wote waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki katika matukio yote hayo. Aidha, napenda kuwatakia afya njema wote waliopata majeraha. Kwa wale wote waliopoteza maisha tunawaombea Roho zao zilale mahali pema peponi - Amina.

  6.            Kuhusu uharibifu wa miundombinu, tunazo taarifa za uharibifu mkubwa wa Miundombinu katika maeneo kadhaa. Napenda kulihakikishia Bunge lako Tukufu kwamba Serikali itafanya kila liwezekanalo kurekebisha miundo mbinu ya barabara iliyoharibika. Tunatambua gharama kubwa inayohitajika, lakini ni wajibu wetu kama Serikali kuhakikisha Wananchi wanapata huduma muhimu hasa za mawasiliano kati ya eneo moja na jingine.

  (d)       Maswali

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  7.            Leo tunahitimisha Mkutano wetu wa Pili wa Bunge tukiwa tumefanya shughuli mbalimbali ndani ya Bunge letu. Katika Mkutano wetu, Waheshimiwa Wabunge wamepata fursa ya kuuliza maswali ya kawaida na yale ya papo papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Jumla ya maswali 115 ya msingi na 307 ya nyongeza yaliulizwa na Waheshimiwa Wabunge na kujibiwa na Serikali.

  (e)        Mjadala wa Hotuba ya Rais

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  8.            Katika Mkutano huu moja ya agenda iliyochukua nafasi kubwa ni Hoja ya Serikali ya kujadili Hotuba ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Maufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hoja hiyo tuliihitimisha vizuri na kwa mafanikio makubwa. Kazi kubwa iliyoko mbele yetu ni kutekeleza yale tuliyokusudia kama wajibu wetu. Napenda kuwapongeza tena Waheshimiwa Wabunge wote kwa kushiriki katika mjadala wa Hotuba hiyo vizuri. Nichukue tena nafasi hii kuliahidi Bunge lako Tukufu kwamba michango ya Waheshimiwa Wabunge na maoni yao yatazingatiwa kwa utekelezaji.

  II: MPANGO WA TAIFA WA MAENDELEO

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  9.            Katika Mkutano huu wa Bunge, Waheshimiwa Wabunge wamepata fursa ya kujadili na kuidhinisha Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali katika mwaka wa Fedha 2016/2017. Vilevile, Bunge limejadili na kutoa maoni na ushauri katika mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika mwaka wa Fedha, 2016/2017. Kipekee, naomba nimshukuru Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango(Mb) na Naibu wake Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (Mb.) pamoja na Waheshimiwa Mawaziri wa Wizara za Kisekta kwa ufafanuzi mzuri walioutoa wakati wa kuhitimisha hoja hii. Aidha, napenda kutumia fursa hii kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge wote kwa michango yao mizuri, maoni na ushauri ambao Serikali itauzingatia katika kukamilisha maandalizi ya Mpango na Bajeti ya mwaka 2016/2017.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  10.         Naomba nami uniruhusu nitoe maelezo mafupi ya msisitizo katika maeneo machache yaliyopata michango mingi kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge waliochangia hoja ya Serikali ya mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo. Waheshimiwa Wabunge wengi wamesisitiza kuhusu umuhimu wa Serikali kuongeza uwajibikaji katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kuimarisha udhibiti wa matumizi ya Serikali. Aidha, Waheshimiwa Wabunge wameishauri pia Serikali kuweka kipaumbele cha ujenzi wa Reli mpya ya Kati, kujenga uchumi wa Viwanda, kuanza na kusimamia ujenzi na Mitambo ya kuchakata gesi asilia (LNG) na Kiwanda cha Mbolea Mkoani Lindi, kuongeza kasi ya usambazaji wa umeme Vijijini, ujenzi wa Bandari Mtwara, kutatua changamoto zinazowakabili Wakulima na Wafugaji pamoja na Wachimbaji Madini.

  Vilevile, kuweka mikakati thabiti ya utekelezaji wa Miradi ya Sekta za Elimu, Afya, Maji na huduma kwa wenye Ulemavu na pia kuzingatia utawala bora. Serikali inatambua kuwa maeneo haya ni muhimu sana katika kujenga uchumi imara na endelevu na pia kuondoa umasikini. Hivyo, itazingatia sana ushauri huu mzuri uliotolewa na Waheshimiwa Wabunge.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  11.         Naomba nitumie fursa hii kumpongoeza Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli kwa umahiri mkubwa na umakini aliouonesha ikiwa ni mwanzo mzuri wa kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano. Mheshimiwa Rais ameonesha kasi kubwa na dhamira ya dhati ya kuwatumikia Watanzania katika kujenga uchumi imara, unaokuwa na endelevu. Waheshimiwa Wabunge wengi watakubaliana nami kwamba Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi chake cha mwanzo cha siku 100, imeonesha dhahiri nia ya dhati ya kuhakikisha kwamba makusanyo ya mapato yetu yanaongezeka. Jitihada hizo za kuongeza makusanyo ya mapato ya Serikali zimefafanuliwa vizuri kwenye Hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango. Serikali itaendelea na mikakati yake ya kuongeza Mapato yake na kudhibiti mianya ya kukwepa kodi. Ni matumaini yangu kuwa Waheshimiwa Wabunge, Wafanyabiashara na Wananchi wote wataunga mkono dhamira hiyo njema ya Serikali.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  12.         Kuhusu matumizi, tayari Serikali imeanza kuchukua hatua thabiti za kudhibiti matumizi yasiyo na tija katika Wizara, Idara za Serikali zinazojitegemea na Taasisi zote za Umma pamoja Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Lengo la hatua zinazochukuliwa ni kuhakikisha kwamba Serikali inasimamia kwa umakini matumizi ya fedha za Umma ili zitumike ipasavyo kwa malengo yaliyokusudiwa. Hatua hizi zitaimarishwa zaidi katika mwaka ujao wa fedha.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  13.         Kama nilivyoeleza awali hoja nyingi za msingi zilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge kuhusu Mpango wa Taifa, zimefafanuliwa vizuri na Waheshimiwa Mawaziri wa Kisekta na Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango. Naomba niwaahidi kuwa tutazizingatia katika mchakato wa maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017, kwa kadri itakavyowezekana. Waheshimiwa Wabunge watashirikishwa kikamilifu katika mchakato huo kupitia Kamati mbalimbali za Bunge. Serikali itafarijika sana kupata maoni na ushauri zaidi ili tuweze kuboresha mipango yetu ya muda mfupi na muda mrefu.


  III:  SEKTA YA KILIMO
  Uzalishaji wa Mazao ya Chakula 2014/2015 na Upatikaji wa Chakula 2015/2016
  Mheshimiwa Naibu Spika,
  14.     Hali ya chakula kwa mwaka 2015/2016 katika maeneo mengi ya nchi imeendelea kuwa ya kuridhisha kufuatia mavuno mazuri yaliyopatikana msimu wa kilimo wa 2014/2015. Takwimu za Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi zinaonesha kuwa albaki kutoka msimu uliopita nchi ilikuwa na ziada ya chakula licha ya kuwepo kwa maeneo machache ambayo hayakuwa na chakula.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  14.     Kutokana na uzalishaji wa mazao ya chakula kwa msimu wa 2014/2015 kuwa Tani milioni 15.5 na mahitaji ya chakula kwa mwaka 2015/2016 kuwa Tani milioni 12.9 hivyo nchi imejitosheleza kwa chakula kwa ziada ya Tani milioni 2.5 sawa na asilimia 120. Napenda kuwahakikishia Watanzania kuwa Serikali itaendelea kuhudumia maeneo yote yenye uhaba wa chakula.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  15.     Pamoja na Taifa kuwa na ziada ya asilimia 120 ya chakula, tathmini ya hali ya chakula nchini inaonesha kuwa kuna Halmashauri 69 katika mikoa 18 nchini yenye maeneo yenye dalili za upungufu wa chakula. Maeneo hayo yapo katika Mikoa ya Dodoma, Shinyanga, Lindi, Singida, Tabora, Arusha, Geita, Kilimanjaro, Manyara, Mara, Tanga, Simiyu, Mwanza, Morogoro, Iringa, Njombe, Mtwara, na Pwani.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  16.     Ili kukabiliana na hali ya uhaba wa chakula katika maeneo hayo, Serikali inaendelea kutoa chakula katika maeneo hayo ambapo jumla ya Tani 23,871.6 za chakula zilitengwa kwa ajili hiyo. Hadi kufikia tarehe 17 Januari, 2016, jumla ya Tani 11,860.8 zilikuwa zimechukuliwa toka Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwenda kwenye Halmashauri za Wilaya zenye upungufu wa chakula kwa ajili ya usambazaji. Natoa wito kwa Halmashauri ambazo hazijachukua mgao wao kufanya hivyo mara moja ili Wananchi katika maeneo hayo wasizidi kuathirika.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  17. Sambamba na utoaji wa chakula cha msaada, Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) inaendelea kutoa mahindi katika maghala ya Songea na Sumbawanga kwa ajili ya kuuzwa kwa wafanyabishara wa nafaka walioidhinishwa na mikoa yenye uhaba wa Chakula. Lengo ni kuongeza upatikanaji wa chakula na kukabiliana na kasi ya kupanda kwa bei ya vyakula katika maeneo hayo. Chini ya utaratibu huo, vibali vimeshatolewa kwa wafanyabiashara wa Mikoa 17, vya kununua jumla ya Tani 77,166. Hadi kufikia tarehe 18 Januari, 2016 jumla ya Tani 56,817.5 kati ya Tani 64,817.3 zilizokuwa zimelipiwa kutoka NFRA tayari zilikuwa zimechukuliwa.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  18. Ili kuongeza na kuimarisha uhakika na usalama wa chakula hapa nchini, Serikali imelenga kujenga maghala 275 kwa awamu katika sehemu zenye uzalishaji mkubwa wa zao la mahindi ambapo hadi sasa jumla ya maghala 125 yanaendelea kujengwa na kukarabatiwa katika maeneo hayo. Aidha, Serikali kwa kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) inaendelea kujenga maghala ya kimkakati kwa ajili ya kuhifadhi akiba ya Taifa. Kwa sasa ghala moja lenye uwezo wa kuhifadhi Tani 5,000 limeshajengwa Wilayani Mbozi Mkoani Mbeya. Aidha, Serikali imepata mkopo wenye masharti nafuu kutoka Serikali ya Poland ambao utawezesha kujenga vihenge vya kisasa (silos) vyenye uwezo wa kuhifadhi Tani 160,000 na maghala yenye uwezo wa kuhifadhi Tani 90,000.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  19.     Pamoja na hatua zinazochukuliwa na Serikali, ninawataka viongozi wa Mikoa, Wilaya na atendaji katika Halmashauri zote Nchini kuwahamasisha Wananchi kutumia vizuri mvua zinazonyesha nchini kote kulima kwa bidii ili kuweza kuvuna na kujiwekea akiba ya chakula cha kutosha kwa ajili ya kaya zao wakati wote wa mwaka. Aidha, wawahamasishe wafanyabiashara na wadau wengine kusaidia Serikali kuchukua chakula kutoka maeneo yenye ziada na kupeleka katika maeneo yenye upungufu. Ni imani yangu kwamba tukizingatia maelekezo haya pamoja na juhudi za Serikali zilizooneshwa, tatizo la uhaba wa chakula nchini litapungua, kama siyo kumalizika kabisa.

  IV:  MIFUGO:

  Hatua zilizochukulwa na Serikali katika Kushughulikia Migogoro ya Wakulima na Wafugaji;
  Mheshimiwa Naibu Spika,
  20.     Migogoro ya ardhi hapa nchini ina sura nne; migogoro kati ya Wakulima na Wafugaji, mgogoro kati ya Wananchi na Wawekezaji; migogoro kati ya Wananchi na Serikali na migogoro kati ya Mamlaka moja na Mamlaka nyingine ndani ya Serikali. Migogoro hii imeenea nchi nzima kutokana na sababu mbalimbali ikiwepo kuongezeka kwa matumizi ya rasilimali ya ardhi.

  21.     Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa na Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi kwa kutumia Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ya mwaka 1999 na Sheria ya matumizi ya Ardhi Na. 6 ya mwaka 2007, hadi kufikia mwezi Juni 2015 jumla ya Vijiji 620 katika Wilaya 81 kwenye Mikoa22 zimeweza kutenga Hekta Milioni 1.9 kwa ajili ya Wafugaji. Wito wangu kwa Wananchi na Wadau wa Kilimo na Ufugaji nawaomba kutunza na kuendeleza maeneo haya ili yaweze kutumika kwa mujibu wa malengo yaliyopangwa.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  22.     Nitumie fursa hii pia kulijulisha Bunge lako Tukufu kuhusu hatua ambazo Serikali imechukua kukabiliana na migogoro ya Wakulima na Wafugaji iliyotokea katika Mikoa ya Morogoro (Wilaya za Mvomero na Kilombero) na Manyara (Wilaya ya Kiteto). Katika kushughulikia tatizo hili, Jumla ya Vijiji53 vimeainisha maeneo kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo Kilimo na Ufugaji. Aidha, jumla ya Mashamba Pori Manane (8) yameanishwa na orodha yake imewasilishwa kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua za kufutiwa hati miliki na hatimaye kufanya utaratibu wa kuyatumia kwa ufugaji. Ni matarajio yangu kuwa maeneo haya yatapunguza sana kwa kiasi kikubwa matatizo ya uhaba wa malisho hapa Nchini. Wito wangu niwatake Viongozi wa Vijiji kusimamia vizuri matumizi ya maeneo yatakayotolewa kwa ajili ya malisho ili tatizo hili la kukosa maeneo ya malisho lisijirudie tena.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  23.     Bado kuna mgogoro wa Wafugaji na Wakulima katika Bonde Oevu la Kilombero ambao umetafutiwa ufumbuzi kwa kuweka alama (branding) mifugo yote katika eneo hili ambapo jumla ya Mifugo 52,780 ilipata usajili wa Wilaya. Aidha, jumla ya Mifugo 24,586 imeondolewa katika eneo la Bonde la Kilombero. Kwa kuzingatia hatua zilizochukuliwa na Serikali Wananchi wanapaswa kufuata Sheria na kuhakikisha Mifugo hairudi tena katika maeneo yaliyokatazwa na kwamba maeneo haya yanahifadhiwa kwa mujibu wa Sheria.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  24.     Mgogoro wa Wafugaji na Wakulima katika maeneo ya Kiteto ni wa muda mrefu na kwa bahati mbaya sana umeleta madhara makubwa kwa maisha ya Wanadamu na uharibifu wa mali. Napenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kwamba Tume iliyoundwa na aliyekuwa Waziri Mkuu (Mstaafu) Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda ikiongozwa na Askofu Amos Mhagachi imekamilisha hatua muhimu ya kuleta maelewanao na maridhiano katika pande zilizoathirika na mgogoro huo. Kwa sasa hali imeendelea kuimarika na tunaendelea kufuatilia kuhakikisha inakuwa shwari kwa muda wote.  

  25.     Vilevile tarehe 29 Januari 2016 nimekutana na Viongozi wa Serikali, Halmashauri ya Wilaya na Chama kutoka Wilaya ya Kiteto hapa Dodoma ambapo nilipata fursa ya kupokea taarifa ya Tume niliyoitaja hivi punde. Nimeiagiza Tume kuendelea na hatua iliyobakia ili kurejesha utulivu na amani kwa wananchi wa Kiteto. Hata hivyo, nimepanga kufanya ziara Wilayani Kiteto katika siku chanche zijazo ili niweze kukutana na Wananchi walioathirika na mgogoro huu na ikiwa ni pamoja na kujionea hali halisi Wilayani Kiteto ili tuweze kutatua migogoro yote. Wito wangu kwa ndugu zangu wa Kiteto ni kuwaomba waendelee kuvumilia wakati jitihada za Serikali katika kutatua migogoro hiyo inaendelea.

  V:  UTEKELEZAJI WA ELIMU MSINGI BILA MALIPO

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  26.     Tangu Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli atoe maaelezo ya utekelezaji wa elimu ya msingi bila malipo, kumekuwa na umuhimu wa kutoa elimu na ufafanuzi zaidi juu ya utekelezaji wa agizo la elemu bila malipo kwa Watanzania kuanzia darasa la awali hadi Kidato cha Nne katika Shule za Umma. Hii ni hatua ya Serikali katika kuhakikisha uwepo wa fursa ya elimu bora kwa wote kwa kuwapunguzia mzigo wazazi na walezi kugharamia au kuchangia upatikanaji wa elimumsingi.

  Katika mpango huu, Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa mwanafunzi atasoma kuanzia darasa la awali hadi kidato cha Nne bila ya wazazi na walezi kulipa ada ya shule, gharama za mitihani na michango mbalimbali. Hata hivyo, yapo majukumu ambayo yataendelea kutekelezwa na wazazi na walezi wote ambayo ni pamoja na kununua sare za shule na michezo, madaftari, kalamu na chakula kwa wanafunzi wa shule za kutwa zilizojiwekea utaratibu huo. Maeneo mengine ni kulipia nauli ya kwenda na kurudi shule, na mahitaji mengine kama kununua godoro, shuka na vifaa vya usafi binafsi. Mzazi au mlezi anao wajibu wa kugharamia matibabu ya mtoto wake.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  27.     Napenda nitumie nafasi hii kuwaomba Waheshimiwa Wabunge wote tushirikiane katika juhudi za kuunga mkono uamuzi wa Serikali kuhusu elimu bila malipo. Aidha, nawaomba wote kwa ujumla wetu kushirikiana kuwaelimisha Wananchi wetu kuhusu utaratibu huu na wajibu wa kila mmoja wetu kama Mzazi/Mlezi, Serikali na jamii kuhusu utekelezaji wa zoezi hili. Nia yetu ni kuhakikisha kwamba Watanzania wanapata fursa ya kupata elimu bora kwa mtoto mwenye umri wa kwenda Shule na wote walioko katika Shule za Msingi na Sekondari. Napenda pia kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba kama tulivyokwisha sema suala la ada elekezi inafanyiwa kazi na ikikamilika Wananchi watajulishwa kuhusu utaratibu huo. Vikao vya pamoja baina ya Serikali na wadau vitaanza hivi karibuni.

  Mheshimiwa Naibu Spika;
  28.     Katika kutekeleza mpango huu, Serikali imetenga fedha shilingi Bilioni 131.4 kuanzia mwezi Disemba 2015 hadi Juni, 2016, kuhudumia wanafunzi wa bweni kwa chakula, kufidia gharama za ada za mitihani, ada ya shule na kutoa fedha za uendeshaji wa shule (Capitation Grants). Aidha, kupitia Waraka wa Elimu Na. 5 wa mwaka 2015, Serikali imefuta michango yote iliyokuwa inachangishwa shuleni kwa idhini ya Kamati na Bodi za Shule.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  29.     Tunatambua katika utekelezaji wa zoezi hili zipo changamoto zilizojitokeza. Kwa mfano, baadhi ya shule zenye wanafunzi wachache kupata fedha kidogo sana kwa kuwa ugawaji wa fedha unazingatia idadi ya wanafunzi. Lakini pia zipo changamoto katika kutoa chakula cha mchana kwa wanafunzi wa kutwa na uendeshaji wa Hosteli ambazo wazazi na walezi au jamii walikuwa wanachangia fedha za chakula. Serikali inaendelea kuzifanyia kazi changamoto hizo zilizojitokeza katika utekelezaji wa mpango huu ikiwemo uelewa wa jamii na wadau kuhusu mpango mzima kwa ujumla wake.

  VI: HUDUMA YA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  30.     Serikali imeendelea kutoa huduma ya mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kwa kuzingatia Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Namba 9 ya mwaka 2004 (Kama ilivyorekebishwa), Kanuni za Utoaji Mikopo za mwaka 2008, na Mwongozo wa utoaji Mikopo na Ruzuku kwa mwaka wa masomo 2015/2016. Hadi kufikia mwishoni mwa Januari 2016, Serikali ilikuwa imetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 207.9 kwa wanafunzi122,786 wa elimu ya juu, wakiwemo wanafunzi wa mwaka wa kwanza 53,850 ambao ni asilimia98.9 ya wanafunzi 55,254 walioomba mikopo hiyo.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  31.     Ili Taifa liendelee kuwa na wataalamu wa kutosha katika nyanja muhimu, Serikali itaendelea kutoa kipaumbele cha kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu wanaodahiliwa katika programu za kipaumbele ikiwemo Sayansi za Tiba, Ualimu wa Sayansi na Hesabu, Uhandisi wa Mafuta na Gesi, Uhandisi Umwagiliaji, Sayansi za Kilimo, Wanyama na Ardhi. Aidha, Serikali inaendelea kufanyia kazi mikakati ya kuimarisha urejeshaji wa mikopo pamoja na kuwa na vyanzo endelevu vya kupata fedha za kumudu ongezeko la wanafunzi wenye mahitaji ya mikopo.

  VII:  HALI YA USALAMA NCHINI

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  32.     Hali ya usalama katika Nchi yetu kwa ujumla ni shwari. Hata hivyo, katika  kipindi  hiki  nchi yetu  imekuwa ikikabiliana na changamoto ya ongezeko kubwa la Wakimbizi hususan katika Mkoa wa Kigoma. Kambi zetu zilizoko mikoa ya Kigoma, Katavi, Tabora na Tanga zinahifadhi wakimbizi wapatao 218,895 kutoka  mataifa  ya  Burundi (wakimbizi 156,377),  Congo-DRC (wakimbizi62,176), Somalia (wakimbizi 150) na Mataifa Mchanganyiko (wakimbizi 192) kutoka nchi za Rwanda, Uganda, Sudan ya Kusini na Ethiopia. Kwa ujumla, katika kipindi hiki wamepokelewa wakimbizi zaidi ya 122,267 kutoka Burundi. Aidha, hadi  kufikia tarehe 31 Desemba,  2015  kambi mpya ya wakimbizi ya Nduta  imepokea  wakimbizi 38,994 wengi  kati yao wamehamishiwa kutoka Kambi ya Nyarugusu na wachache wakiwa wameingia moja kwa moja kutokea Burundi.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  33.     Kufuatia ujio wa wimbi kubwa la wakimbizi toka Burundi kumejitokeza matukio ya uhalifu wa kutumia silaha za moto ndani na nje ya kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu. Aidha, kutokana  na upekuzi  na  ukaguzi  kwa wakimbizi unaofanywa kwa pamoja na vyombo vya dola sanjari na taarifa za ki-intelijensia imebainika kuwepo kwa askari waasi waliokimbia pamoja na raia wa kawaida ambao wanajaribu kuwashawishi vijana kujisajili ili kujiunga na vikundi vya waasi. Nitoe wito kwa wananchi na wakimbizi kushirikiana na vyombo vyetu vya usalama kwa kutoa taarifa za uhalifu, hususan umiliki haramu wa silaha za moto kwenye makambi na katika maeneo mbalimbali.

  VIII:  MPANGO ENDELEVU WA USAFI WA MAZINGIRA NCHNI

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  34.     Mtakumbuka kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, aliamua maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru ya terehe 9 Desemba, 2015 yafanyike kwa kufanya usafi wa mazingira katika maeneo ya Umma na maeneo yanayowazunguka. Kwa ujumla Wananchi, Taasisi za Umma na Binafsi ziliitikia agizo hilo na kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo. Nichukue fursa hii kuwapongeza kwa dhati wananchi, taasisi za umma na binafsi wote kwa kushiriki katika zoezi hilo kikamilifu. Mlionesha moyo wa uzalendo na ari kwa nchi yenu. Nawapongeza sana!

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  35.     Usafi ni dhana muhimu katika kulinda afya za binadamu na kudhibiti magonjwa mbalimbali ya mlipuko ikiwemo kipindupindu. Ili kufanikisha lengo hili, kunahitajika juhudi za makusudi na za pamoja katika usimamizi wa sheria, kanuni na taratibu tulizojiwekea. Hivyo, Serikali imeamua kulifanya zoezi la usafi wa mazingira kuwa endelevu. Kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Serikali imetoa Waraka unaoelekeza kuwa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi iwe Siku Maalum ya kufanya Usafi wa Mazingira.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  36.     Napenda kuendelea kusisitiza katika kila ngazi yaani Viongozi na Wananchi kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha zoezi hili linakuwa endelevu. Aidha, napenda kuwahimiza Viongozi wa Mkoa, Wilaya na Halmashauri kusimamia usafi wa mazingira katika maeneo yao ya utawala zoezi ambalo litakuwa linafanyika kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi. Kila Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya nchini awe na mikakati ya kudumu ya usafi ikiwa ni pamoja kuhakikisha kuwa kuna sheria ndogo za usafi wa mazingira na zinatekelezwa ipasavyo. Aidha, Halmashauri zote nchini zihakikishe kuwa uchafu uliokusanywa katika maeneo mbalimbali unazolewa na kupelekwa katika maeneo mahususi ya dampo. Simamieni kikamilifu wakandarasi waliopewa zabuni hizo na kuona wanatimiza wajibu wao kikamilifu.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  37.     Kama tulivyoona Usafi wa mazingira ni jukumu la kila Mwananchi na linapaswa kuwa endelevu. Rai yangu kwa Watanzania wote ni kujenga tabia ya kuhakikisha kuwa mahali pa kazi na mazingira yanayowazunguka yanakuwa safi wakati wote. Kufanya hivyo, kutasaidia kuimarisha usafi wa mazingira na kuboresha afya. Hali kadhalika kupunguza mlipuko wa magonjwa yakiwemo kipindupindu.

  38.     Wito wangu kwa Wananchi ni kuona kuwa zoezi la usafi ni la kila mmoja wetu na kuepuka kuchafua mazingira kwa makusudi ikiwemo kuepuka tabia za kutupa taka hovyo wanapokuwa katika vyombo vya usafiri na pia kutofanya biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa ili kuzuia kutupwa taka hovyo. Wamiliki wa mabasi yanayofanya safari ndefu wanatakiwa waweke vifaa vya takataka. Yeyote atakayebainika kutupa takataka dirishani, atachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na mmiliki wa basi hilo.

  Watendaji wa Mitaa na Kata na Vijiji kutimiza wajibu wao wa kuhakikisha maeneo wanayoyasimamia yanakuwa katika hali ya usafi. Nitumie fursa hii kuwahimiza Wananchi, Taasisi na Jumuiya zote kuhakikisha wanaweka mazingira katika hali ya usafi na pia kushiriki katika siku ya usafi kama iliyopangwa na Serikali.

  IX:  UHUSIANO WA KIMATAIFA

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  39.     Nchi yetu imeendelea kuwa kivutio kikubwa katika mahusiano baina ya Nchi na Nchi, Jumuiya za Kikanda na Kimataifa. Hii inatokana na Viongozi wetu ambao wamekuwa katika mstari wa mbele kudumisha mahusiano yetu katika Medani za Kimataifa. Yapo mambo mengi yaliyofanyika na yanayo endelea kufanyika kama mwendelezo wa kudumisha ushirikiano katika Jumuia hizi za Kikanda na Kimataifa.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  40.     Kutokana na juhudi za Viongozi wetu kutangaza Nchi yetu Kimataifa, ni hivi karibuni tuMheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bwana Ban Ki-moon kuwa mmoja wa Wenyeviti wa jopo la ushauri la ngazi ya juu kuhusu Afya ya Mama na Mtoto Duniani (Every Woman, Every Child). Hii ni heshima kubwa kwa nchi yetu kwa kuwa itaiweka Tanzania kuwa miongoni mwa mataifa yenye kuheshimika duniani. Aidha, uteuzi huu ni chachu ambayo inaleta matumaini mapya katika kukabiliana na changamoto za afya ya mama na mtoto, hususan katika nchi zinazoendelea kama Tanzania. Nitumie fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa uteuzi huo. Tunamuombea heri na baraka tele katika kutekeleza jukumu hilo kubwa la Kimataifa kwa maendeleo ya watu wetu.

  X:  KUIMARISHA UTENDAJI SERIKALINI NA MAADILI

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  41.     Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi imedhamiria kurejesha nidhamu na maadili ya Watendaji wa Serikali na Watumishi wa Umma katika kutoa huduma mbalimbali kwa Wananchi kwenye maeneo mbalimbali. Katika kuhakikisha Watumishi wa Umma na Watanzania wote wanafanya kazi, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekuja na kauli mbiu ya “Hapa Kazi Tu”Tafsiri ya falsafa hii ni kuwataka Watanzania wote katika nafasi mbalimbali walizopo kufanya kazi kwa bidii na kujiepusha na vitendo vya uzembe, urasimu na kutenda kazi kwa mazoea.

  42.     Aidha, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 chini ya Ibara ya 22inaainisha kuwa, kila Mtu anayo haki ya kufanya kazi. Vilevile, Ibara ya 25 inafafanua kuwa kufanya kazi ndiyo njia pekee ya kumwezesha Mtanzania kupata utajiri na ndilo chimbuko la ustawi wa wananchi na ni kipimo cha utu.

  Wakati akihutubia Mkutano wa kwanza wa Bunge lako Tukufu, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, kwa maneno yake alisema, napenda kunukuu:-
  “Serikali nitakayounda, nataka iwe inawahudumia Wananchi kwa haraka na sio kuwasumbua sumbua na kuwazungusha. Natoa rai kwa Watumishi wa Serikali, hasa ambao ni wazembe na wavivu, kujiandaa. Wamevumiliwa kwa muda mrefu sasa basi. Kwa sababu Watumishi wa aina hiyo hawatavumiliwa katika Serikali nitakayoiongoza. Lugha za “Hiyo ni changamoto tutaishughulikia” au “Mchakato unaendelea”hazitavumiliwa katika Serikali ya Awamu ya Tano. Mimi nataka watu waKazi tu. Hatuwezi kulea watu ambao wanalipwa mishahara lakini hawafanyi kazi wanazotakiwa kufanya, au wamegeuza Ofisi za Umma kuwa ni mahala pa kuchuma bila kufanya kazi.” mwisho wa kunukuu.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  43.          Ili kutekeleza maneno ya Mheshimiwa Rais na kuhimiza matakwa ya Kikatiba, kila Mtanzania anapaswa kushiriki na kujituma kwa uaminifu katika kazi halali za uzalishaji mali. Aidha, kila Mwananchi anapaswa kuwa na nidhamu ya kazi na kuhakikisha anafikia malengo yaliyowekwa. Nitumie fursa hii pia kuwakumbusha Watumishi wa Umma kuwa wamepewa dhamana ya kuwahudumia Wananchi kwa niaba ya Serikali. Hivyo wanawajibika kuhakikisha wanawahudumia Wananchi kwa haki, weledi, uadilifu na kwa taaluma zao. Ni lazima wahakikishe kuwa wanatatua kero za Wananchi. Sio sahihi wananchi kuwasilisha kero zao kwa viongozi wa ngazi za kitaifa hasa wakati wa ziara ilhali viongozi wa mikoa na wilaya wapo katika maeneo hayo kwa wakati wote.

  44.          Tunatambua kuwa wapo Watumishi wanaotekeleza vyema majukumu yao. Lakini pia wapo Watumishi ambao hawazingatii maadili ya kazi zao na pia wanafanya kazi kwa uzembe. Serikali haitaacha kuchukua hatua za nidhamu kwa watumishi wote wasiozingatia kikamilifu sheria, kanuni na taratibu katika Utumishi wa Umma. Aidha, kwa kuzingatia maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Viongozi na Watumishi wote wa Umma lazima tufanye kazi kwa kuzingatia weledi na kujiamini. Kila mtu anapaswa kujitathmini kama dhamana aliyopewa anaitendea haki.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  45.         Huu sasa ni wakati wa kufanya mabadiliko ya dhati katika utendaji na uadilifu. Kwa maana hiyo napenda kusisitiza mambo yafuatayo kwamba:-
  (i)           Kila Kiongozi na Mamlaka ya nidhamu ni lazima kuwajibika kusimamia Utendaji na Maadili ya Kazi. Hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa wakati na kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi. TUSIONE HAYA HATA MARA MOJA, CHUKUENI HATUA.

  (ii)          Wananchi wahudumiwe ipasavyo na kwa weledi, haki, uadilifu na heshima. Mambo haya yakizingatiwa hakuna mwananchi atakayesafiri kutoka kijijini, wilayani au mkoani kutafuta huduma Makao Makuu ya Wizara, Ofisi ya Waziri Mkuu au IKULU.

  (iii)        Madawati ya malalamiko yawepo katika Ofisi za Umma. Aidha, tayari maelekezo yametolewa ya Watumishi wa Umma wazingatie utaratibu wa kuvaa vitambulisho vyenye majina yao kwa urahisi wa wananchi kuwatambua wanapowahudumia. AGIZO HILI LITEKELEZWE.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  46.         Ni kweli kwamba, Mheshimiwa Rais ametumia dhana ya “kutumbua jipu” kama dawa ya kusimamia uwajibikaji hasa katika wale wenye dalili ya kukosa maadili ya Utumishi wa Umma. Tafsiri ya dhana hii ya “Kutumbua jipu” inalenga katika kuwarejesha Watumishi wa Umma na walioko Serikalini katika mstari mzuri wa utendaji. Nitoe wito kwa Waheshimiwa Wabunge wote kama tulivyo na kwa umoja wetu, tumuunge mkono Mheshimiwa Rais katika vita hii kubwa ya “Kutumbua Majipu”.  Tukiwa pamoja na kwa kushirikiana tutaweza kuibadilisha nchi yetu kuwa nchi ya maadili na yenye sifa ya juu katika utendaji wa Utumishi wa Umma.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  47.         Aidha, naomba nisisitize kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli inaongozwa na Katiba, Sheria, Kanuni na Taratibu za Nchi. Vilevile inaheshimu na kuthamini haki za Watumishi wa Umma wa ngazi zote na inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Watumishi wa Umma katika kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa. Kamwe, Serikali haitamwonea mtumishi yeyote wala kumnyanyasa endapo tu atakuwa anatenda yale yanayopasa. Lakini pia haitamvumilia mtumishi mzembe na asiyetimiza wajibu wake. Serikali itaendelea kuchukua hatua za kurejesha nidhamu kwa Watumishi wa Umma ili kuwezesha Nchi yetu kuwa na Utumishi wenye kuzingatia uadilifu na uliotukuka.

  XI:  HITIMISHO.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  48.         Uzoefu nilioupata katika muda mfupi tuliokaa pamoja hapa Bungeni, nimegundua kuwa tuna Waheshimiwa Wabunge mahiri waliobobea katika nyanja mbalimbali. Wapo wasomi wa ngazi zote, wazee kwa vijana ambao wana uzoefu na utaalam mkubwa. Ni imani yangu kuwa tutatumia utaalam na uwezo mkubwa tulionao katika kuijenga nchi yetu na kuwasaidia Watanzania kutoka hapa tulipo hadi hatua ya mbele katika kuleta maendeleo. Wananchi waliotuchagua wanatutegemea. Nawaomba tutangulize uzalendo katika kila jambo tufanyalo kwa manufaa ya Taifa letu na watu wake. Tufike mahali ambapo kwa elimu, busara na hekima tulizonazo kuacha kabisa ushabiki wa kisiasa badala yake tutizame mbele katika kuwaletea wananchi maendeleo.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  49.         Napenda kuhitimisha Hotuba yangu kwa kurejea tena nilivyosema hapo awali kwamba, baada ya kukamilika kwa Uchaguzi Mkuu kwa mafanikio makubwa, kazi kubwa iliyo mbele yetu ni kuijenga nchi yetu kwa umoja na mshikamano. Nawaomba tuweke maslahi ya Watanzania na Taifa letu mbele. Tudumishe amani na utulivu. Tupuuze sera zozote za kudhoofisha utaifa wetu kama Watanzania na kutugawa kwa misingi yoyote ile, iwe ya kikabila, imani za dini, rangi au kwa itikadi za kisiasa. Dhamira yetu sote iwe ni kukuza uchumi wa nchi yetu na kuondoa umaskini ili kuwaletea wananchi wetu maendeleo na maisha mazuri.

  50.         Ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa Tanzania inapiga hatua mbele. Tufanye kazi kwa bidii kuunga mkono kaulimbiu yetu ya “Hapa ni Kazi Tu”. Aidha tutumie juhudi, maarifa na ubunifu zaidi katika kila jambo. Mimi naamini kuwa kwa ushirikiano katika Bunge hili na wananchi kwa ujumla, tutaweza kutimiza matarajio ya wananchi waliotuchagua na matarajio ya Watanzania wote.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  51.         Naomba nitumie nafasi hii tena kuwashukuru wote waliosaidia kufanikisha mkutano huu. Nikushukuru wewe Naibu Spika, na Mheshimiwa Spika kwa kutuongoza vizuri na kwa weledi mkubwa. Kipekee niwashukuru Wenyeviti wa Bunge ambao wamekalia kiti kwa mara ya kwanza lakini kwa weledi mkubwa, Hongereni sana!!.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  52.        Nitumie nafasi hii kumshukuru Katibu wa Bunge na Wasaidizi wake wote kwa kazi nzuri ya kuhakikisha mkutano huu unakamilisha shughuli zake kama ilivyopangwa. Niwashukuru Wataalam wote wakiwemo Waandishi wa Habari kwa kazi nzuri waliyofanya kufanikisha Mkutano huu.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  53.        Nimalizie kwa kuwatakia wote safari njema mnaporejea kwenye maeneo yenu ya kazi na katika majimbo yenuNinaamini kwamba, Mwenyezi Mungu atatulinda na kutuweka salama sote kama tulivyo hadi kukutana tena katika Mkutano ujao.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  54.        Baada ya kusema hayo, naomba sasa kutoa Hoja kwamba, Bunge lako Tukufu liahirishwe hadi tarehe 19 Aprili,  2016 saa 3:00 asubuhi litakapokutana katika Mkutano wa Tatu kwenye Ukumbi huu hapa Dodoma.

  Mheshimiwa Naibu Spika,
  55.        Naomba kutoa Hoja.

  0 0

  (Na Raymomd Mushumbusi-Dodoma)

  Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni  Mhe Freeman Mbowe Mbunge wa Hai (CHADEMA) ametangaza rasmi Baraza la Mawaziri vivuli litakalosaidiana na Serikali katika kuendesha shughuli za kimaendeleo.

  Akitangaza Mawaziri hao vivuli  kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani amesema anawaomba Mawaziri wa Wizara husika kuwapa ushirikiano wale wote walioteuliwa kuwa Mawaziri vivuli katika Kambi ya Upinzani  ili kupeleka mbele gurudumu la maendeleo nchini.

  Waliotangazwa Katika Orodha hiyo ni Pamoja na Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora  Jaffar Michael, Manaibu wake ni Joseph Nkundi na Ruth Mollel, Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Ali Saleh Abdalla na Naibu wake ni Pauline Gekul, Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu Esther Bulaya na Manaibu ni Yusuph Makame na Maftah Abdalla, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi ina mawaziri wawili ambao ni Magdalena Sakaaya na Emmaculate Swari Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Inj. James Mbatia na Naibu Waziri Willy Kombucha.

  Aidha ameendelea kuwataja Mawaziri wengine kuwa ni Waziri wa Fedha na Mipango Halima Mdee  na Naibu Waziri ni David Silinde, Waziri wa Nishati na Madini  John Mnyika na Naibu Waziri ni John Heche, Waziri wa Katiba na Sheria  Tundu Lissu na Naibu Waziri Abdalla Mtolela, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Peter Msigwa na Naibu Waziri Riziki Shaghal, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  Juma Omari na Naibu Waziri Mwita Waitara, Waziri ya Mambo ya Ndani Godbless Lema  na Naibu Waziri Masoud Abdalla, Waziri ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wilfred Lwakatare na
  Naibu Waziri Salum Mgoso.

  Wengine walioteuliwa katika Baraza kivuli ni Waziri wa Maliasili na Utalii Esther Matiko na Naibu Waziri Cecilia Pareso, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Anthony Komu na Naibu Waziri Cecil Mwambe, Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi Suzan Lyimo Naibu Waziri Dkt. Ali Suleiman Yusuph, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel na Naibu Waziri Zubeda Sakul, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Joseph Mbilinyi na Naibu Waziri  Devotha Minja na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Hamidu Hassan na Naibu Waziri Peter Lijualikali.

  0 0

  tunda-man
  Msanii wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake mpya wa Mama Kijacho Khalid Ramadhani ‘Tundaman’. MSANII wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake mpya wa Mama Kijacho Khalid Ramadhani ‘Tundaman’’ hatimaye amepata dili la ubalozi wa kampeni ya kuhamasisha wanawake wa Africa kuhusiana na tamasha la wanawake liitwalo (AFWAB AMSHA MAMA2016). Joe Kariuki Blog pic
  Mkurugenzi Mtendaji wa ‘lebal’ ya Candy na Candy Records,Joe Kariuki.
  Tamasha hilo ambalo lilianza tangu mwishoni mwa Desemba mwaka jana, kunako Hoteli ya nyota tano ya The Tribe na vitongoji vya Nairobi, Kenya, mfanyabiashara mashuhuri na mwenye jina kubwa music , alifanya bonge la tamasha liliacha gumzo kwa kuvuta maelfu wa watu kutoka kila kona ya dunia. Mkurugenzi Mtendaji wa ‘lebal’ ya Candy na Candy Records, Joe Kariuki, aliratibu tamasha maridadi lililojulikana kama Amsha Mama, maalum kwa Wanawake wa Kiafrika, tamasha lililofanyika katika Hoteli ya kifahari ya Tribe, sehemu ambayo ni maarufu sana pia kwa wasanii kutoka Marekani, akiwemo Akon. 

   Tamasha hilo ambalo lengo kubwa lililenga kuzungumzia bayana hali halisi ya maisha ya mwanamke wa Afrika kuhusu safari yake, mapigano yake kimaisha, mafanikio, biashara, ubunifu na ushindi wake katika maisha.   Kama mwanaume ambaye siku zote aliye karibu na moyo wa mwanamke ambaye alitaka kumtuza ama kumzawadia kwa hatua aliyofikia, kumtia moyo, kumhamasisha katika safari yake ya mafaniko katika jamii hii yenye mfumo dume barani Afrika.   Akizungumza katika event hiyo, Joe alisema: 

  "Kuwawezesha wanawake ni muongozo katika jamii, nami nataka kutumia ujuzi wangu na uzoefu nilionao kujenga jukwaa kwa ajili ya wanawake kukua biashara zao."  Washiriki wengi ambao ambao wengi wao walisafirishwa kutoka nchi za mbali kwa ajili ya kuhudhuria ‘event’ hiyo, waliunga mkono mawazo ya Joe, mfano Uganda na Italia. Lisa raia wa Italia alisema: "Dhana ya Amsha Mama ni ya kipekee. Naangalia wanawake wenye uwezo wa kuzalisha hila zitakazotumika huko Milan.

  "  Sophie kutoka Uganda, alisema: "Ninawezaje ku-miss hii! Kama mwenyekiti wa chama chetu cha wanawake 600 nataka kuhakikisha wanapata aina hii ya fursa kwa ajili ya kuonyesha bidhaa zao na kwa ajili ya kupata mtandao na wanawake wengine." Rundo la wanawake waliokuwa na hisia kama hizo, akiwemo mwingine kutoka Copenhagen, Denmark: "Tamasha haya ndiyo tunahitaji kwa ajili ya kukuza wanawake. Inaonyesha nguvu za wanawake na mipango yao." 

   Na katika hilo, Joe anaendeleza jitihada zake za si tu kumwezesha Mwanamke wa Afrika, bali pia kumuinua, kumtia moyo wake, kumpa mwangaza na kujihusisha kwake.   Hivyokwa sasa na ndiyo maana ameandaa maonyeshwa makubwa ya wanawake (AFWAB AMSHA MAMA 2016), yatakayofanyikia katika Uwanja wa Kedong ranch uliopo katika jiji la Naivasha nchini Kenya Machi 25-27 2016.

  0 0

  UNFPA, the United Nations Population Fund, is closely monitoring the outbreak of the Zika virus and warning about its potentially adverse effects on the health of women and babies, particularly in Latin America. We are also closely monitoring its possible spread to other regions.

  UNFPA will continue to lead efforts to promote widespread information about the virus and about voluntary family planning. Given reported cases of Zika virus transmission through sexual contact, the role of UNFPA as the world’s leading agency on reproductive and maternal health, and the biggest public sector supplier of family planning commodities, including condoms, is ever more pertinent.

  Women and girls should be able to make informed decisions about their reproductive health and family planning methods, and to protect themselves and their babies if they decide to be pregnant. UNFPA will continue to work with countries around the world to scale up access to information and to a wide range of voluntary family planning commodities so that women can make informed decisions and protect themselv

  0 0

  Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Vuga, Mjini Zanzibar, kuhusiana na maadhimisho ya wiki ya Sheria Zanzibar iliyoanza tarehe 5 mwezi huu.
  Rais wa Wanasheria Zanzibar Omar Saidi akitoa ufafanuzi kuhusu jumuiya hiyo inavyotoa huduma za kisheria kwa wananchi kwenye mkutano ulioitishwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar uliozungumzia wiki ya sheria Zanzibar.
  Baadhi ya Waandishi wa Habari walioshiriki mazungumzo ya Jaji Mkuu wa Zanzibar kuhusu wiki ya Sheria Zanzibar inayoanza tarehe 5 mwezi huu wakisikiliza kwa makini mazungumzo hayo.
  Hakimu anaeshughulikia kesi za watoto katika Mahakama ya Vuga Mjini Zanzibar Sabra Ali Mohd akielezea changamoto zinazoikabili kesi za watoto kwenye mkutano huo.PICHA NA ABDALLA OMAR-HABARI MAELEZO ZANZIBAR

  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu wa Benki ya Exim hiyo, Bw Frederick Kanga, akizungumza wakati wa semina maalumu ya kuzindua mpango maalum wa kutambua, kusimamia na kuwajengea uwezo wa kiutendaji wafanyakazi wake, iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.


  BENKI ya Exim Tanzania imezindua mpango maalum wa kutambua, kusimamia na kuwajengea uwezo wa kiutendaji wafanyakazi wake hasa wale wanaonyesha uwezo mkubwa katika kutimiza majukumu yao ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.
  Mpango huo unaofahamika kama ‘Talent Management Program’ umetajwa kuwekeza zaidi katika kuwajenga kiutendaji wafanyakazi hao ikiwa ni jitihada za benki hiyo kuandaa watendaji waandamizi wa benki hiyo kutoka ndani ya benki.
  Akizungumza kwenye semina maalumu ya kuzindua mpango huu iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu wa benki hiyo Bw Frederick Kanga alisema mpango huo unaoendeshwa kwa uwazi ulianzishwa mahususi  kubaini manufaa ambayo benki hiyo inayapata kutoka kwa wafanyakazi na zaidi kuyatumia manufaa hayo kujiendeleza na kuboresha huduma zake.
  “Kama benki tumebaini uwepo wa nguzo tatu muhimu katika ukuaji wetu ambazo ni pamoja na rasilimali watu ambayo ndio nguzo kuu, ikifuatiwa na teknolojia  na kisha michakato (processes).Ni kutokana na filosofia hiyo Exim tunaamini katika uwepo wa msingi imara unaojengwa na wafanyakazi wetu kuwa ndio chachu ya ukuaji na uendelezaji wa biashara yetu,’’ alisema.
  Alisema ili kufanikisha mpango huo, uongozi wa benki hiyo umebuni mchakato wa wazi katika utambuzi wa wafanyakazi watakaonufaika na mpango huo huku akibainisha kwamba tayari kamati maalumu imeundwa kusimamia zoezi hilo na hatimaye kuwapata walengwa.

  “Kwa kuanzia uongozi tayari umefanikiwa kupata orodha ya wafanyakazi 16 wenye sifa kunufaika na mpango huu kutoka matawi yote na tayari wamepewa wataalamu wa kuwasaidia kujijengea uwezo zaidi kwa usimamizi wa benki ikiwasimamia,’’ alisema.
  Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi walioteliwa kunufaika na mpango huo, Meneja Msaidizi wa Mipango, Maendeleo na Uendeshaji wa benki hiyo Bw Liberat Mtui alisema;“Ujio wa mpango huu kwa upande wetu wafanyakazi ni kama ngazi ya kutusaidia kufika kule tunapotaka kwa kuwa utatuwezesha kujijengea uwezo zaidi katika masuala ya kibenki,’’

  0 0

   KUKANUSHA UPOTOSHAJI DHIDI YANGU
  Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar
  Kumekuwa na upotoshwaji wa taarifa zinazosambaa juu ya aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF, na Mkuuwa Wilaya ya Wanging'ombe, Fredrick Wilfred Mwakalebela, ambapo baadhi ya vyombo vya habari kama Magazeti na mitandao ya kijamii vimekuwa viripoti tofauti.

  Akizungumza na mtandao huu, wa Sufianimafoto.com kwa njia ya simu, Mwakalebela alisema kuwa zimekuwepo taarifa za upotoshwaji dhidi yake baada ya kuibuka kesi ya mtuhumiwa aliyepandishwa Kizimbani mwenye jina linalofanana na lake mwenye jina la David John Mwakalebela (56).

  Aidha Mwakalebela alisema kuwa Mtuhumiwa huyo, aliyewahi kuichezea timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, na timu ya Taifa, wakati yeye akiwa ni Katibu Mkuu wa TFF, alipandishwa kizimbani yeye na aliyewahi kuwa Mr. Tanzania 2015, Muhammad Khalil (32) wakikabiliwa na mashitaka saba likiwemo la kuishi nchini bila kibali na kumsaidia Mshitakiwa kutoa taarifa za uongo.

  Kutokana na kufanana kwa majina hayo,kumekuwepo na sintofahamu na usumbufu mkubwa kwa Mhe. Mkuu wa Wilaya huyo ya Wanging'ombe huku ndugu, jamaa na marafiki wakihaha huku na huko na wengine wakimpigia simu kwa mshituko, jambo ambalo si la kweli.

  ''Zimeene taarifa potofu juu yangu zikielekeza tuhuma hizo dhidi yangu kwa makusudi au kwa kutofahamu jambo ambalo ni Hatari kwa Mimi binafsi, familia na marafiki kwa ujumla, nawaomba wahusika wawe wakifuatilia undani wa stori yenyewe ili kupata uhakika kabla ya kuanza kueneza uzushi na kuzua taflani,


  Aidha napenda kuwapa pole wanafamilia yangu, ndugu, jamaa na marafiki kwa usumbufu wote uliojitokeza kwao kutokana na sintofahamu hii na kusababisha kadhia dhidi yako". alisema Mwakalebela
  Mtuhumiwa David Mwakalebela, akiwasili Mahakamani,ambaye amefananishwa na Fredrick Mwakalebela.


older | 1 | .... | 755 | 756 | (Page 757) | 758 | 759 | .... | 1904 | newer