Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 753 | 754 | (Page 755) | 756 | 757 | .... | 1903 | newer

  0 0

  Katibu Mkuu wa wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na watoto, Dkt. Ulisubisya Mpoki akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Siku ya saratani, huadhimishwa duniani kote kila mwaka ifikapo tarehe 4 ya Mwezi februari. Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani mwaka huu ni ‘TUNAWEZA, NINAWEZA. KWA PAMOJA TUWAJIBIKE KUPUNGUZA JANGA LA SARATANI DUNIANI.” (We can, I can. How everyone, as a collective or as an individual can do their part to reduce the global burden of cancer). 
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road, Julius Mwaiselage akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na huduma za matibabu zinazotolewa na Taasisi ya Ocean Road.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na watoto, Dkt. Ulisubisya Mpoki leo jijini Dar es Salaam.Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.   Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii


  WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya Ocean Road pamoja na wadau mbalimbali kuadhimisha siku ya Saratani kuanzia kesho kwa kutoa elimu ya umuhimu wa kuzuia na kujikinga na madhara mbalimbali yatokanayo na maradhi ya Saratani ambayo hufanyika kila Februali 4 ya kila mwaka .

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Ulisubisya Mpoki amesema kuwa Saratani ni ugonjwa ambao unaathiri watu wa rika na jinsia zote; watoto, watu wazima, wake kwa waume.

  Amesema takwimu za Shirika la Kimataifa la Atomiki la Utafiti wa Saratani (IARC) na Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaelezea kwamba kila mwaka duniani kunatokea wagonjwa wapya wa saratani wanaokadiriwa kufikia milioni 14.1, kati ya hao, zaidi ya wagonjwa milioni 8.2 hufariki dunia kutokana na ugonjwa wa Saratani, hii husababishwa kwa wagonjwa kuchelewa kufikishwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. Vifo vya ugonjwa wa Saratani ni asilimia 13 ya vifo vyote vinavyotokea duniani (WHO).

  Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Saratani duniani mwaka huu ni ‘‘Tunaweza , Ninaweza.Kwa pamoja tuwajibike kupunguza janga la saratani duniani’’.


  Dk.Mpoki amesema kuwa hatua madhubuti za kinga, uchunguzi wa mapema na tiba stahiki hazitachukuliwa haraka, tatizo la Saratani litaongezeka na kufikia makadirio ya wagonjwa wapya milioni 24 ifikapo mwaka 2035, huku ongezeko kubwa likiwa katika ukanda wa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.


  Amesema tatizo la Saratani limekuwa likiongezeka na kukua, kila mwaka, Takribani wagonjwa wapya wapatao 44,000 hugundulika na saratani za aina mbalimbali nchini, hii ni sawa asilimia 10 tu (4,400) kati ya wagonjwa wote wanaofanikiwa kufika katika Taasisi ya Saratani Ocean Road ili kuweza kupata tiba. Kati ya hao wanaobahatika kufika katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (takribani asilimia 80) hufika wakiwa katika hatua za mwisho za ugonjwa (Hatua ya 3 na ya 4), hali ambayo hupunguza uwezekano wa wagonjwa kuweza kupona maradhi hayo.

  Dk.Mpoki kwa mujibu wa taarifa kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road hapa nchini zinaonyesha kwamba aina za Saratani zinaoongoza ni kama ifuatavyo:


  Kwa upande wa wanaume,Saratani ya Ngozi ,Saratani ya Koo, Saratani ya Tezi Dume, pamoja na Saratani ya Tezi,na wanawake ni Saratani ya Shingo ya Kizazi, Saratani ya Ngozi, Saratani ya Matiti, pamoja na Saratani ya Koo.

  Amesema ugonjwa wa Saratani umekuwa na vyanzo mbalimbali vinavyosababisha tatizo hili kukua kwa kasi hapa nchini na Duniani ambayo yamegawanyika katika sehemu tatu ambazo Virusi vinavyosababusha Saratani ya Shingo ya Kizazi, Bakteria vinavyosababusha Saratani ya Tumbo, Parasaiti vimelea vya kichocho vinavyosababisha Saratani ya Kibofu cha mkojo.

  Aidha amesema mtindo wa kimaisha wa Uvutaji wa sigara, kula vyakula ambavyo si mlo kamili na vyenye mafuta kwa wingi, kutokula matunda na mboga mboga, kunywa pombe kupita kiasi, matumizi ya dawa za kulevya na kutokufanya mazoezi,Mionzi ya Miale ya jua ambayo inaathiri ngozi hasa kwa walemavu wa ngozi,Urithi katika familia kwa mfano Saratani ya Matiti, na Utumbo.

  Amesema Saratani ni ugonjwa ambao huweza kuchukua muda mrefu mpaka kujitokeza (Miaka 10-20), hivyo wakati mwingine inakuwa ni vigumu sana kujua chanzo cha Saratani pale inapokuwa imejificha.

  Dk.Mpoki amesema mambo yanayoongeza uwezekano wa kupata magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza ikiwa ni pamoja na saratani ni ulaji usiofaa mafuta na sukari, uzito uliozidi, unene uliokithiri, kutofanya mazoezi, uvutaji wa sigara na bidhaa zitokanazo na tumbaku, na unywaji pombe kupita kiasi.

  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto inatumia maadhimisho haya kuwa sehemu ya uhamasishaji kwa jamii kama ilivyo kwenye nchi zote duniani. Aidha,Taasisi ya Saratani ya Ocean Road inahamisisha wananchi kujitokeza kwa wingi kuanzi Februali 3 mpaka 4 ili kufanyiwa uchunguzi Saratani zifuatazo, Uchunguzi wa Saratani ya Tezi Dume , Saratani ya Shingo ya Kizazi, Saratani ya Matiti na saratani ya ngozi kwa walemavu wa Ngozi. Uchunguzi huu utafanyika bure bila ya malipo yoyote.


  ‘‘Mwanzoni, wengi wetu hawajitambui ya kuwa wana ugonjwa huu. Wengine wanakuwa na dalili lakini hawachukui hatua mapema. Dalili kubwa ya ugonjwa wa Saratani ni uvimbe,ambao hauna maumivu mwanzoni, kupungua uzito, upungufu wa damu mwilini na dalili zingine kwa aina ya Saratani na sehemu ilipo mwilini’’.amesema Mpoki.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 3, 2016.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Manyovu, Albert Obama Ntabaliba kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari3, 2016.

  Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde akizungumza Bungeni Mjini Dodoma Februari 3, 2016.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kibaha Vijijini Hamoud Abuu Jumaa kwenye viwanja vya Bunge mJini Dodoma, Februari 3, 2016.

  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Abuu Jumaa (katikati) na Mbunge wa Bukoba Vijijini Jasson Rweikiza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 3, 2016.
   (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Jogoo akiwa katika harakati za kutafuta chakula mara baada ya kutahamaki huku akinaswa na Kamera yetu.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0

   ke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiweka saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, 
  Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
    Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisikiliza taarifa kutoka kwa Bw. Ojuku Mgedzi, Mkuu wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, 
  Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea taarifa kutoka kwa Bw. Ojuku Mgedzi, Mkuu wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, 
  Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akikabidhiwa taarifa Bw. Ojuku Mgedzi, Mkuu wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, 
  Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akioneshwa maeneo mbalimbali na Bw. Ojuku Mgedzi, Mkuu wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, 
  Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.

    Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na wagonjwa waliofika kupata huduma katika zahanati ya Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, 
  Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitembelea chumba cha kujifungulia cha zahanati ya Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, 
  Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana kwa furaha na wakaazi wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
   Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe Sophia Mjema akimkaribisha Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli kuhutubia wakaazi wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akihutubia wakaazi wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, 
  Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.

   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi mchele, unga na maharage Mzee Anthony Kingongoti Mwenyekiti wa wakaazi wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, 
  Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea shukurani kutoka kwa Mzee Anthony Kingongoti Mwenyekiti wakaazi wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, 

  Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru Mzee Anthony Kingongoti Mwenyekiti wakaazi wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, 
  Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
  PICHA NA IKULU

  Na Magreth Kinabo –MAELEZO
  MKE wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Janeth Magufuli ameziomba na kuzimahamasisha taasisi za Serikali na zisizo za Serikali kushirikiana na Serikali kutatua changamoto mbalimbali zinazozikabili Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu Wasiojiweza kijulikanacho kwa jina la Nunge,viwemo vingine.


  Aidha alisema vituo hivyo jumla vipo 17, katika maeneo mbalimbali nchini.

  Kauli hiyo imetolewa leo na Mama Magufuli wakati alipotembelea makazi hayo yaliyoko Kigamboni eneo la Vijibweni jijini Dares Salaam, ambapo alisema changamoto wanazokabiliana nazo amezisikia na na aliwaahidi kuwa atashirikiana na wadau wote kuzitafutia majibu yake.


  Mama Magufuli alizitaja baadhi ya changamoto hizo, ni kuwa uchakavu wa miundombinu, uhaba wa rasilimali fedha na watu, pamoja na maslahi duni ya watoa huduma, upungufu wa vitendea kazi na huduma za jamii, pamoja na uvamizi wa eneo la kituo.


  Aidha Mama Magufuli alimwomba Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema kulishughulikia taizo la uvamizi wa eneo hilo na kulitafutia ufumbuzi.


  “ Natumainni zawadi tuliyoileta ni ndogo na haiwezi kumaliza matatizo yote mliyonayo. Lakini ni matumaini yangu kuwa zawadi hii inaweza kuwa chachu ya kuhamsha hamasa ya watu na vikundi vingine kujitoa kusaidia watu wasiojiweza. Ni imani yangu kuwa endapo watu wote tutajitoa kwa dhati tutaweza kuwahudumia wazee na watu wasiojiweza na hivyo kuwapunguzia makali ya maisha . 


  Tukumbuke ‘kutoa ni moyo na si utajiri’ na kwamba “sisi sote ni wazee na walemavu watarajiwa”.
  Aliongeza kwamba ni dhahiri kuwa Serikali ina wajibu mkubwa katika kuhudumia wazee na watu wasiojiweza. Hata hivyo Serikali pekee haiwezi kumaliza matatizo yote yanayowakabili na wazee na watu wasiojiweza.


  Hivyo basi, sote kwa pamoja tunao wajibu wa kusaidia nguvu za Serikali katika kuwahudumia watu hao.


  “Na kwa kutambua hilo , mimi na wenzangu niliombatana nao tumeamua kutoa zawadi yetu ndogo kwenu. Zawadi hiyo inajumuisha vitu vifuatavyo mchele kilo 3000, unga kilo 3000 na maharage kilo 1200. Kulingana na idadi yenu niliyopewa kila mmoja atapewa kilo 25za mchele, kilo 25 za unga na kilo 10 za maharage.


  “Nawaombeni mniruhusu pia kuchukua nafasi hii kuwasilisha kwenu salamu nyingi kutoka kwa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ameniomba niwaarifu kuwa yupo pamoja nayi na kwamba Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha wazee na watu wasiojiweza wanapata huduma zote muhimu kwa kadri ya uwezo wake,” alisisitiza Mama Magufuli.


  Mama Magufuli aliongeza kwamba wazee na watu wasiojiweza wanahitaji upendo, kuthaminiwa nakusaidiwa.Hivyo kipimo kimojawapo cha kupima jamii iliyostaarabika na inayoheshimu misingi ya utu ni kuangalia namna inavyo wathamini wazee na watu wasiojiweza.


  Aliupongeza uongozi na watumishi wote wa kituo hicho na vituo vingine nchini kwa kazi kubwa wanayoifanya licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa.


  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke , Sophia Mjema alimtaka kila mwananchi kutambua kwamba bila wazee hakuna tutakachoweza kufanya hivyo ni muhimu kuwa enzi na kuwasaidia wazee walioko majumbani na mitaani.


  “ Tuwaenzi wazee na kuwasaidia pia hata wale walioko mitaani tuwashauri warudi majumbani ili Serikali iweze kuwaorozesha kwa kuwa si vizuri kukaa barabarani, Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Magufuli itahakikisha inawajali wazee,” alisema.


  Akizungumzia kuhusu watoto wa mitaani alisemani wajibu wa wazazi kuhakikisha wanawalea watoto wao vizuri ili wasikilimbile mitaani kwa kuwa watoto ni taifa la kesho.


  Naye Mwenyekiti wa wazee wa makazi hayo, Anthony Kikongoti alimshukuru Mama Magufuli kwa niaba ya wenzake, kwa kuanza ziara yake ya kwanza ya kutembelea kituo hicho ,ambapo alimwomba apeleke salamu zao kwa baba yao ambaye ni Rais Magufuli kuwa wanasema asante.
  “Huu ni mwaka wa wanyonge dini zote tumwombee kwa pamoja ili aweze kuendelea kupunguza makali ya maisha,” alisema.  Afisa Mfawidhi wa kituo hicho, Ojuku Mgedzi alisema wanahitaji bajeti ya kutosha ya kuendesha shughuli mbalimbali, watumishi 42 , wakiwemo walinzi, kwa kuwa waliopo sasa ni 29 na hawatoshi.

  Alisema eneo hilo lina hekari 50.8 na nusu ya eneo hilo limevamiwa.
  Mgedzi alisema kituo hicho kina idadi yawakazi 112, ambapo alimkabidhi Mama Magufuli orodha ya idadi ya watu hao.

  0 0


  0 0

   Jaji wa Mhakama Kuu ambae pia ni Mkuu wa Chuo cha Mahakama cha Lushoto Jaji Ferdinand Wambali, akisaini kitabu cha wangeni alipotembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF, katika Maonesho ya Wiki ya Sheria leo jijini Dar es Salaam. 
   Jaji wa Mhakama Kuu ambae pia ni Mkuu wa Chuo cha Mahakama cha Lushoto Jaji Ferdinand Wambali, akimuaga Ofisa mawasiliano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF) Luhende Singu, katika Maonesho ya Wiki ya Sheria leo jijini Dar es Salaam.
   Ofisa mawasiliano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF) Luhende Singu akitoa maelekezo kwa wananchi juu ya kujiunga na mkuko huo, katika Maonesho ya Wiki ya Sheria leo jijini Dar es Salaam.

   Madaktari wakiendelea na kutoa huduma za vipimo vya (Bp) na Sukari bure kwa wananchi waleotembelea banda la (NHIF) leo jijini Dar es Salaam.
  Wananchi wakiwakiwa katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF) katika Maonesho ya Wiki ya Sheria leo jijini Dar es Salaam.

  Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya jamii

  0 0

    Mkuu wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba (kushoto) ,akifafanua jambo kwa baadhi ya wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha kitengo cha IT,wakati walipofanya ziara ya kimafunzo katika duka jipya la Airtel Expo katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam .
   Afisa mauzo wa Airtel Juma Hassan (katikati) ,akifafanua jambo kwa baadhi ya wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha kitengo cha IT,wakati walipofanya ziara ya kimafunzo katika duka jipya la Airtel Expo katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam.
   Wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha kitengo cha IT wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba (katikati) na baadhi ya wafanyakazi wa Airtel wakati walipofanya ziara ya kimafunzo katika duka jipya la Airtel Expo katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam.
  Wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha kitengo cha IT wakimsikiliza afisa masoko wa Airtel Tanzania Prosper Mwanda ( kulia) wakati walipofanya ziara ya kimafunzo katika duka jipya la Airtel Expo na kuweza kutembelea baadhi ya sehemu za katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam.

  -Wanafunzi wa IT wa chuo IFM wahimizwa kushirikiana na Airtel 

  WANACHUO kutoka chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) kitengo cha IT , wamefanya ziara ya mafunzo kwenye duka la kisasa la Airtel Expo lililopo katika ofisi kuu za Airtel mtaa wa morroco Dar es salam ikiwa ni mwendelezo wa kutanua wigo wa kutoa huduma zenye ubora za kibunifu kwa wateja wake.

  Wanachuo hao waliweza kujifunza mambo mengi juu ya kampuni hiyo inavyofanya kazi kuanzia huduma zake hadi bidhaa zinazouzwa na kampuni hiyo. Ikiwemo Modem iliyozinduliwa hivi karibuni maarufu kama modem ya maajabu Wingle Modem inayouweza kutumika na zaidi ya watu 10 kwa wakati mmoja, Simu za Kisasa za gharama nafuu na zenye OFA nzuri 

  Wanafunzi hao pia wamejionea jinsi duka la Airtel Expo linavyohudumia wateja wengi kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu ya kidigitali.

  Mkurugenzi wa Airtel huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba amewapongeza wanafunzi hao kwa dhamira yao ya kutaka kujifunza katika ulimwengu wa technolojia na kuwakaribisha wengine kuhudhuria' 

  tumefarijika sana kuona wanafunzi toka vyuo vya ndani ya nchi yetu kama nyie IFM mnafunga safari na kuja kushuhudia hili, hongereni sana tunawakaribisha wote sio tu wanafunzi bali kila mpenda maendeleo ya technolojia kutembelea duka hili la kisasa na kujionea au kushauriana na Airtel kufanya mambo mengi bora zaidi ya ulimwengu wa mawasiliano" alisema Bi Lyamba.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya PanAfrican Energy David K. Roberts (kulia) akimuelezea jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa wakati wa ziara yake huko Songosongo katika visima vya gesi asilia.
   Ni katika ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa katika visiwa vya Songosongo.

   PanAfrican Energy Operational SH Engineer, Onestus Mujemula akielezea jambo kwa wana habari katika ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini huko Songosongo kwenye visima vya gesi, kutoka kushoto ni PanAfrican Energy Country Chairman Patrick Rutabanzibwa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa na CSR Manager Andrew Kashangaki (wakwanza kulia)

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa akipata maelezo ya mradi kutoka PanAfrican Energy Operational SH Engineer Onestus Mujemula kuhusu mradi wa uchimbaji gesi asilia katika visima vinne uliomalizika kwa kutumia mtambo wa kisasa wa “RIG”
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa akiongea na wana habari wakati wa ziara yake ya kikazi katika visiwa vya Songosongo.

  0 0

  Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird aliyetembelea Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo, Katikati ni Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Kisekta wa Benki ya Dunia Bw. Waleed Maliki. 
  Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga (katikati) akimfafanulia jambo Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird (kushoto) alipotembelea banda la maonesho la Idara ya Malalamiko na Maadili la Mahakama katika viwanja vya Mnazi Mmmoja leo. 
  Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga (kushoto) akionesha ugeni kutoka Benki ya Dunia nchini Tanzania michoro ya majengo mapya ya Mahakama yanayoendelea kujengwa katika maeneo mbalimbali nchini . Kutoka kulia ni Bw. Larbi George Addo kutoka Benki ya Dunia akifuatiwa na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird (wa pili kutoka kulia) na Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Kisekta wa Benki hiyo Bw. Waleed Maliki. 
  Afisa Magereza kutoka Jeshi la Magereza jijini Dar es salaam, Rose Odemba (kulia) akitoa Ufafanuzi kwa Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird (katikati) na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga (kulia) kuhusu Utaratibu wa kuwaachia wafungwa kwa masharti baada ya kutumikia 1/3 ya vifungo vyao magerezani (PAROLE) walipotembelea banda la Maonesho la Jeshi la Magereza katika viwanja vya Mnazi mmoja leo. 
  Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Mahakama ya Tanzania Bi. Wanyanda Philip Kutta akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird (kulia) alipotembelea Maonesho ya Wiki ya Sheria leo jijini Dar es salaam. 
  Baadhi ya Wananchi waliotembelea mabanda ya maonesho ya Wiki ya Sheria nchini katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam wakiendelea kupatiwa msaada wa kisheria katika masuala mbalimbali. 
  Baadhi ya Wananchi waliotembelea mabanda ya maonesho ya Wiki ya Sheria nchini katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam wakiendelea kupatiwa msaada wa kisheria katika masuala mbalimbali. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha DC wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha,Fidelis Lumato akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani,kulia ni Mwenyekiti wa halmashauri,Noah Sapuk
  Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Arusha DC,Noah Sapuk akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani.
  Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Arusha DC wakifatilia mijadala kwenye kikao hicho.
  Baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo wakiwa kwenye kikao kujibu hoja mbalimbali kutoka kwa madiwani.
  Baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo wakiwa kwenye kikao kujibu hoja mbalimbali kutoka kwa madiwani.
  Diwani wa Viti Maalumu katika halmashauri ya Arusha DC,Nuru Ndossy akichangia hoja.
  Diwani wa Kata ya Mateves ,Julius Mollel akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.


  0 0

  Jaji Mkuu wa Kenya Mhe. Dkt. Willy Mutunga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuipongeza Mahakama ya Tanzania kwa utendaji wake wa kusikiliza na kuamua mashauri mengi yanayopelekwa mahakamani. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman na Kulia ni Jaji Kiongozi Mhe. Shaan Lila.
  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akizungumzia ujio wa Jaji Mkuu wa Kenya.

  ……………………………………………………
  Na. Aron Msigwa –MAELEZO.

  Jaji Mkuu wa Kenya Mhe. Dkt. Willy Mutunga ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa utendaji wake wa kusikiliza na kuamua mashauri mengi yaliyopelekwa mahakamani kwa mwaka wa sheria uliopita wa 2015 na kutoa wito kwa watendaji wa Mahakama ya Tanzania kuendelea kufanya vizuri licha ya changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.

  Jaji Mkuu wa Kenya ametoa pongezi hizo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mara baada ya kukutana na kuongea na Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani Tanzania kufuatia mwaliko alioupata wa kuhudhuria maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yatakayofanyika Februari 4 mwaka huu.

  Mhe. Dkt. Mutunga amesema kuwa nchi ya Kenya mpaka sasa ina mashauri yapatayo 300,000 ambayo bado hayajaamuliwa na kuongeza kuwa asilimia 5 ya wananchi wa Kenya ndio hupeleka mashauri yao Mahakamani huku asilimia 95 iliyobaki wakitafuta ufumbuzi wa kesi zao nje ya Mahakama.

  “Ni kweli Tanzania mnafanya vizuri katika katika kusikiliza mashauri kwa haraka, asilimia 95 ya Wakenya hutafuta ufumbuzi wa kesi zao kwa viongozi wa kidini na Kimila kutokana na baadhi yao kukosa fedha za kutosha za kufuatilia na kugharamia kesi zao” Amesema.

  Ameongeza kuwa Mahakama ya Kenya kwa mwaka huu 2016 imejipangia malengo ya kuhakikisha kuwa inasuluhisha mashauri yote ndani ya mwaka mmoja ili kuongeza ufanisi na imani kwa wananchi.

  Ameeleza kuwa Tanzania ina jambo la kujifunza kutoka Kenya kufuatia mageuzi ya Katiba iliyoyafanya mwaka 2010 hususan kwenye baadhi ya maeneo ikiwemo na nafasi ya Mahakama kwenye Katiba Mpya ambayo Tanzania inaendelea na mchakato wake.

  Akizungumzia mageuzi hayo ambayo tayari Kenya imeyafanya kufuatia kuwepo kwa Katiba mpya Mhe. Mutunga amesema kuwa ni pamoja kupungua kwa madaraka ya Rais katika kuteua Majaji, na nafasi za Majaji kutangazwa na watu kupeleka maombi na sifa zao kujadiliwa ambapo wananchi huruhusiwa kutoa maoni kwa Tume ya Mahakama ya Kenya kuhusu majaji hao kabla ya kuapishwa.

  Aidha, ameeleza kuwa Watanzania wana kila sababu ya kujivunia umoja na mshikamano uliopo ambao umesababishwa na waasisi wa taifa hilo huku akibainisha kuwa majadiliano na upatikanaji wa Katiba Mpya utafanywa na Watanzania wenyewe kwa kuwa Watanzania ni walimu na mfano wa kuigwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akizungumzia ujio wa Jaji Mkuu wa Kenya amesema kuwa Mahakama ya Tanzania imenufaika na ujio wake kwa kuwa iko kwenye maadhimisho ya Wiki ya Sheria ambayo huwakutanisha wadau mbalimbali wa sharia kujadili changamoto na mafanikio ya Sekta ya Sheria nchini.

  Amesema kuwa kufuatia ziara ya Jaji Mkuu wa Kenya Mahakama ya Tanzania imejifunza masuala mbalimbali ambayo ni muhimu katika ufanisi wa shughuli zake ikiwemo Maslahi ya Watumishi wa Mahakama, Jukumu la Mahakama kutafsiri Katiba kwa kuangalia historian a uchumi pia kuazima baadhi ya hukumu zilizotolewa nchini Kenya kama ushauri.

  Aidha, amebainisha kuwa Mahakama ya Tanzania inao wajibu wa kuendelea kuongeza uwazi katika upatikanaji wa watendaji wake wenye nia ya kuwatumikia wananchi na kuboresha njia za kuwapata majaji.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Uongozi wa Benki ya CRDB ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Dkt. Charles Kimei wakati Uongozi huo ulipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Februari 03,2016 kwa lengo la kumuelezea kuhusu Banki hiyo itakavyoweza kusaidia wajasiriamali wadogo wadogo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Benki ya CRDB ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Dkt. Charles Kimei wakati Uongozi huo ulipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Februari 03,2016 kwa lengo la kumuelezea kuhusu Banki hiyo itakavyoweza kusaidia wajasiriamali wadogo wadogo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Uongozi wa Benki ya Posta Tanzania wakati Uongozi huo ulipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Februari 03,2016 kwa lengo la kumuelezea kuhusu Banki hiyo itakavyoweza kusaidia wajasiriamali wadogo wadogo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Benki ya Posta Tanzania wakati Uongozi huo ulipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Februari 03,2016 kwa lengo la kumuelezea kuhusu Banki hiyo itakavyoweza kusaidia wajasiriamali wadogo wadogo.(Picha na OMR)

  0 0

  Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Kairuki, Prof. Keto Mshigeni akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu maadhimisho ya 17 ya kumbukumbu ya Prof. Hubert Kairuki yatakayofanyika kuanzia Februari 4. Kushoto ni Ofisa Habari wa chuo hicho, Abraham Mwalugeni.
  Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu la Kairuki (KHEN), Dk. Muganyizi Kairuki, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu maadhimisho ya 17 ya kumbukumbu ya Prof. Hubert Kairuki yatakayofanyika Februari 4. Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Kairuki, Prof. Keto Mshigeni na Ofisa Habari wa chuo hicho, Abraham Mwalugeni. 
  …………………………………
  Katika kuadhimisha miaka 17 ya kumbukuzi ya mwaasisi wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert kairuki kuanzia tarehe 4 hadi 6 Feb ambayo itakuwa ni siku ya kilele.Mh Dr Salmin
  Ahmed Salim ambaye pia ndio mkuu wa chuo hicho atazindua jengo la utafiti na mafunzo ya Uyoga lililopo huko Boko katika eneo la chuo hicho.

  Sambamba na uzinduzi huo pia shughuli nyingine katika kumbukizo hizo itakuwa ni pamoja na muhadhara kuhusu Uyoga utakaotolewa na Profesa Keto Mshigeni ambaye ndiye makamu mkuu wa chuo hicho na mwanasayansi aliyebobea katika tafiti za uyoga.

  Pia hospital ya Kairuki it ataendesha zoezi maalum la upimaji na matibabu ya macho bila ya malipo kwa siku mbili mfululizo. Pia patakuwepo matembezi ya hiara kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya saratani ya kizazi.

  Aidha wanafunzi wa zamani wa chuo hicho waliopo Mwanza na mikoa ya kanda ya ziwa wataadhimisha kumbukizo hizo kwa kufanya zoezi la kupima afya bure kwa wakazi wa huko.

  0 0

  Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Innocent Mungy, akizungumza na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na kutambua Simu Feki na kudhibiti uingiaji wa Simu hizo Tanzania na kueleza mwisho wa matumizi wa simu hizo Nchini Tanzania ni Juni 2016. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilima Zanzibar na kuwashirikisha waandishi wa Vyombo mbali mbali vilioko Zanzibar. 
  Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano TCRA Thadayo Ringo, akizungumza na waandishi wa habari jinsi ya kutambua Simu feki wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar, Amesema utambuzi wa kujua simu yako kama ni orijinali unaweza kupiga namba kuaza na Nyota Reli 06 Reli . *# 06# na utapata ujumbe wa Simu yako kwa Mfano zitakuja tarakimu 15 mfano IMEI 12456789067654 Na Kupiga 15090 Ujumbe wa kukuelewesha kama ni simu yako orijino. kwa mfano kama huu Sony Mobile Communications AB -SONY C5555 - Xperia. huu ni mfano wa kujua simu orijino.
  Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Thadayo Ringo akionesha mfano wa simu orijino kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
  Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo wa TCRA uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
  Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo wa TCRA uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
  Waandishi wakifuatilia mafunzo hayo kwa vitendo kuangalia somu zao kama ni orijino baada ya kupata elimu hiyo ya kujua simu feki na orijino wakati wa mkutano huo na Maofisa wa TCRA uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya zanzibar ocean view kilimani zanzibar. kwa kuingiza namba waliopewa.
  Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya TCRA Innocent Mungy, akitowa maelezo kwa waandishi wa habari baada ya kuangalia simu zao baada ya kuingiza namba hizo na kugunduwa kuwa ziko salama na siyo feki. kwa bahati nzuri takribani waandishi wote simu zao orijino.
  Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji Huduma za Maweasiliano Thadayo Ringo akimsomea ujumbe mmoja wa waandishi wa habari aliyehudhuria mkutano huo baada ya kuweka namba hizo na kuja ujumbe wa suimu siyo feki.
  Mdau wa habari Farouk Karim akiuliza swali wakati wa mkutano huo kuhusiana na uingiaji wa simu za kutoka ulaya nyingi huwa na lock wakati wa mkutano huo.
  Mwandishi Amour Mussa akiuliza kuhusu TCRA inachukua hatua gani endapo simu ikiibiwa.
  Ndg Issa Yussuf akuliza jinsi ya utaratibu wa kuwafikia Wananchi wa Vijiji na zoezi hilo la ungunduzi wa simu feki na kuweza kuepuka na hasara hii, wakati ikifika tarehe hiyo ya mwisho wa matumizi ya simu hizo feki. 
  Naibu Mkurugenzi Thadayo Ringo akifafanua na kujibu maswali yalioulizwa wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na matumizi ya Simu feki kufikia mwisho wake wa matumizi Tanzania.
  Meneja Mawasiliano TCRA Innocent Mungy akifafanua jambo wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na kusitishwa kwa matumizi ya simu feki ifikapo mwezi juni 2016. 
  Kaimu Meneja Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Zanzibar TCRA Ndg Seif S Waziri akizungumza wakati wa mkutano huo na kutowa neno la shukrani kwa waandishi wa habari kuhudhuria mkutano huo wa kutowa elimu ya simu feki kwa Wananchi wa Zanzibar na Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar 


  Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo wa mafunzo ya kutambua simu feki na Orijino uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.


  Imetayarishwa na Othman Mapara.Blogspot.


  Zanzinews.com.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe George Simbachawene akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) kuhusu kuanzishwa kwa Mkoa mpya waSongwe na Wilaya sita mpya 

  (Na Raymond Mushumbusi-maelezo)
   
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuli ameidhinisha kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Songwe na wilaya nyingine mpya nchini.
   
  Akitoa tamko hilo kwa niaba ya Rais Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe George Simbachawene amesema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imempa Mamlaka Rais ya kugawa Nchi kwa kadri ambavyo atakapoona inafaa.
   
  Mhe George Simachawene amesema kutokana na mamlaka hayo aliyopewa Rais jumla ya Wilaya sita na Mkoa mmoja wa Songwe umeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Mkoa mpya wa Songwe umeanzishwa kutoka Mkoa wa Mbeya.
   
  Amezitaja Wilaya mpya zilizoanzishwa kuwa ni Wilaya ya Songwe Mkoa wa Songwe,Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es salaam, Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam, Wilaya ya Mlanyi Mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi.
   

  “ Nichukue fursa hii kuwaagiza Wakuu wa Mikoa wote ambao Wilaya mpya zimeanzishwa kufanya maandalizi rasmi ili Mkoa na Wilaya hizo ziweze kuanza kufanya kazi,aidha mkazo uwekwe kwenye upatikanaji wa Ofisi na huduma zote muhimu kupatikana kwa urahisi katika Mkoa naWilaya hizo mpya” Alisema Mhe Simbachawene.

  0 0

  Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez akizungumza na waandishi wa habari na wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika Hoteli ya Hyatt Regence Kilimanjaro Dar es Salaam jana.
  Wadau mbalimbali na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
  Hapa kila mgeni mualikwa akiwa busy na simu yake kwenye uzinduzi huo.
  Ni kama wanasema 'tumependeza sana ngoja tujipige picha'.
  Wanahabari wakifurahia jambo kwenye uzinduzi huo.
  Hapa ni furaha tupu kwa wanahabari.
  Washereheshaji katika uzinduzi huo, Taji Lihundi na mwenzake wakifanya vitu vyao.
  Burudani ikiendelea.

  Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez (katikati), akiwa na viongozi wenzake katika uzinduzi huo.
  Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez (katikati), akiwa na washereheshaji wa uzinduzi huo.
  Makofi yakipigwa kufurahia uzinduzi huo.
  Wanahabari mabloggers wakiwa katika picha ya pamoja na msanii Lucas Muhuvile 'Joti'.


  Na Dotto Mwaibale


  KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Tigo, imetangaza huduma ya bure ya WhatsAap kwa watumiaji wa huduma hiyo.


  Akizungumza Dar es Salaam jana katika uzinduzi huo,Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez amesema kuwa wateja waote wa tigo wanaotumia vifurushi vya intaneti vya kampuni hiyo kwa wiki na mwezi watapata huduma ya whatsaap bure.


  Alisema kuwa ni mara ya kwanza kwa kampuni ya simu kitoa ofa ya bure ya mtandao huo wa jamii nchini pia kampuni ya tigo ina wateja zaidi ya milioni 10.


  "Unajua huduma ya whatsaap ambayo ni maarufu kwenye kutumia ujumbe kwa njia ya simu inawatumiaji zaidi ya milioni nane nchini tanzania na duniani inatumiwa na watu wapatao milioni 900,pia huduma hiyo inasaidia watumiaji kubadilishana habari ,ujumbe,video na miito ya sauti"alisema Gutierrez


  Alisema kuwa kuanzia sasa na kuendelea kwa wateja wote wa tigo wanaonunua vifurushi vyetu vya wiki au mwezi watakuwa na fursa ya kufurahia whatsaap bure.

  Aliongeza kuwa huduma ni kwa watumiaji wa smartphone na kupata huduma bure ya whatsaap kwa wateja tigo imejikita katika kuboresha mabadiliko kwenye maisha ya kidigitali.

  0 0

  Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani akijibu hoja toka kwa Wabunge mbalimbali katika cha 7 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO

  (Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO )

  Serikali katika mwaka wa fedha 2015/2016 ilitenga Shillingi million 300 kwa ajili matengenezo na ujenzi wa Barabara ya Kitosi- Wampembe katika Wilaya ya  Nkasi Mkoa wa Rukwa kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) ili kufanya Barabara hiyo iweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka.

  Akijibu swali la Mhe.Desdelius John Mipata Mbunge wa Nkasi Kusini (CCM) liliouliza ni lini Serikali itaitikia kilio hiki cha wananchi wanaopata shida kwa Barabara hizo kutopitika katika kipindi chote cha mwaka,Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani amesema Serikali kupitia Wizara yake imesikia kilio cha wananchi wa Wilaya ya Nkasi na inaendelea kutoa fedha za matengenezo ya Barabara ya Kitosi-wampembe.

  “ Kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Serikali ilitoa jumla ya Shillimgi Millioni 500 ili kufanya matengenezo ya Barabara ya Kitosi-Wampembe ili ziweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka” Alisema Mhe Ngonyani.

  Aidha ,katika kipindi cha mwaka wa fedha 2014/2015 Serikali ilitenga jumla ya Shillingi Millioni 45 na Shillingi Millioni 60 zimetengwa katika mwaka wa fedha 2015/2016 kwa ajili ya matengenezo ya aina mbalimbali ya barabara ya Nkana-Kala kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ili kuhakikisha inapitika kwa kipindi chote cha mwaka.


  Ukarabati wa barabara ya Kitosi-Wampembe yenye urefu wa kilomita 67 na Barabara ya Nkana –kala yenye urefu wa kilometa 68 uko chini ya Mfuko wa Barabara ikisimamiwa na Wakala wa Barabara (TANROADS)  na Barabara zote hizi ziko chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ambayo inawajibika kuwezesha Barabara zinapitika kwa kipindi chote cha mwaka.

  0 0  Mwanasaikolojia Anti Sadaka amewafunda wanawake wa Zanzibar wanaoshiriki mafunzo ya ujasiriamali ya kujikita katika biashara ya Vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yanaendeshwa na wataalamu kutoka taasisi ya Manjano Foundation na Zanzibar Chamber of Commerce yanayoendelea Zanzibar kwa wiki nzima. Anti Sadaka amewataka wanawake hao kujitambua kwa lengo la kufikia malengo yao waliojiwekea. 

  Akieleza zaidi katika semina hiyo amewataka wanawake hao kujitambua wao ni nani wana nafasi gani kwenye jamii inayowazunguka, kufanya kazi kwa bidii na kudumisha nidhamu yao kwa kila wakifanyacho kwa lengo la kufikia malengo yao.Pia amewaasa wanawake walioshiriki mafunzo hayo mjini Zanzibar kuchangamkia FURSA zinazowazunguka. 

  Semina hiyo inawanufaisha wanawake wa Zanzibar kwa lengo la kuwaongezea kipato na pia kuweza kujiajiri ili kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira. 

  Anti Sadaka amewashauri wanawake wasiache kujifunza na kujibweteka baada ya mafunzo haya kuisha isipokuwa wawe makini kutafuta elimu zaidi ya kujiongezea ujuzi katika kazi zao.

  0 0

    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na  Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Vicent Kone mara baada kuwasili mkoani humo jioni ya leo,tayari kwa kuanza maandalizi ya shamra shamra za maadhimisho ya chama cha Mapinduzi (CCM) kutimiza miaka 39 Kitaifa mkoani Singida.Sherehe hizo zitakazofanyika Februari 6 2016 zinatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho.
  Ndugu Kinana akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Said Amanzi baada ya kuwasili Singida leo,kulia kwake ni MKuu wa Mkoa wa Singida  Dk.Parseko Vicent Kone  
   Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Vicent Kone sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Singida Said Amanzi wakiwa na wageni wao ,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye mara baada kupokelewa jioni ya leo mjini humo
   Mwenyeki wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Singida Bi.Diana Chilolo  samba na Mkuu wa Mkoa Dk.Parseko Vicent Kone wakiwakaribisha wageni wao jioni ya leo mkoani humo.
  Baadhi ya Wafuasi wa chama cha CCM wakijimwaya mwaya mara baada ya kuwapokea wageni wao waliowasili jioni ya leo mkoani humo.
  Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukiwasili mkoani Singida jioni ya leo kwa ajili ya maandalizi ya shamra shamra za maadhimisho ya chama cha Mapinduzi (CCM) kutimiza miaka 39 Kitaifa mkoani Singida,ambapo sherehe hizo ambazo zitahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho zinatarajiwa kurindima Februari 6 2016 katika uwanja wa Namfua.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya wafuasi wa chama hicho waliofika kumlaki mara baada ya kuwasili mkoani humo jioni ya leo,tayari kwa kuanza maandalizi ya shamra shamra za maadhimisho ya chama cha Mapinduzi (CCM) kutimiza miaka 39 Kitaifa mkoani Singida.Sherehe hizo zitakazofanyika Februari 6 2016 zinatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya wafuasi wa chama hicho waliofika kuwalaki mara baada ya kuwasili mkoani humo jioni ya leo,tayari kwa kuanza maandalizi ya shamra shamra za maadhimisho ya chama cha Mapinduzi (CCM) kutimiza miaka 39 Kitaifa mkoani Singida.Sherehe hizo zitakazofanyika Februari 6 2016 zinatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho.
   Mwenye wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Singida Bi.Diana Chilolo akimlaki Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Ndugu Nape Nnauye mara baada ya kuwasili mkoani humo akiwa ameambatana Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana tayari kwa maandalizi ya maadhimisho ya chama hicho kutimiza miaka 39,ambapo kilele chake itakuwa Februari 6 ndani uwanja wa Namfua.

  0 0

  Hizi ni miongoni mwa baiskeli 104 zilizotolewa na Shirika la Kitanzania lisilo la kiserikali AGPAHI (Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI zilizotolewa katika mkoa wa Shinyanga.Shirika hilo limetoa baiskeli 104 katika halmashauri nne za wilaya mkoa wa Shinyanga,ambazo ni halmashauri ya mji Kahama,halmashauri ya Msalala,Ushetu na manispaa ya Shinyanga. 

  Msaada huo umetolewa na Shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa Mfuko wa kusaidia watoto wenye VVU wa watu wa Uingereza (Children’s Investment Fund Foundation UK - CIFF) kwa lengo la kurahisisha kazi kwa watoa huduma ya afya kwa ngazi ya jamii ambao hufanya kazi na shirika hilo kuelimisha jamii kuhusu VVU na UKIMWI.Zoezi la kugawa baiskeli hizo limefanyika Februri 02,2016 na Februari 03,2016..Fuatilia hapa chini matukio katika picha 32 zilizoletwa na Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,ndugu Kadama Malunde Hapa ni katika ofisi ya mganga mkuu wa halmashauri ya mji Kahama mkoani Shinyanga,kulia ni kaimu mganga mkuu wa halmashauri ya mji Kahama Dkt Samwel Mwalutambi akiwa na Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Cecilia Yona akizungumzia kuhusu msaada huo wa baiskeli.Dkt Mwalutambi alilishukuru shirika hilo kwa kuona umuhimu wa kusaidia watoa huduma za afya kwa ngazi ya jamii na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuhudumia jamii. Kulia ni mwandishi wa habari kutoka Radio Kahama FM, bi Amina Mbwambo akizungumza na msimamizi wa kituo cha Huduma na Matunzo kwa watu wanaoishi na VVU kilichopo katika hospitali ya mji wa Kahama -Dkt John Malulu,ambaye pia alieleza kufurahishwa na shirika la AGPAHI kutoa baiskeli 25 kwa halmashauri hiyo. Kushoto ni ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Cecilia Yona akimweleza mganga mkuu wa wa halmashauri ya mji wa Kahama Dkt Bruno Minja kuhusu msaada wa baiskeli 84 katika wilaya ya Kahama zilizotolewa na shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa Mfuko wa kusaidia watoto wenye VVU wa watu wa Uingereza (Children’s Investment Fund Foundation UK - CIFF). Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Kahama Dkt Bruno Minja akizungumza wakati wa kupokea msaada wa baiskeli 84 katika wilaya ya Kahama,yaani baiskeli 25 Halmashauri ya Mji Kahama, Halmashauri ya Msalala 32 na Halmashauri ya Ushetu 27 kwa ajili ya watoa huduma ya afya ngazi ya jamii.Dkt Minja alisema watajihidi kadri iwezekanavyo kuhakikisha kuwa baiskeli hizo kutumika kwa kazi iliyokusudiwa ili kuwarahisishia kazi watoa huduma hiyo ambao hufanya kazi ya kutoa elimu ya VVU na UKIMWI kwa kujitolea Zoezi la kushusha baiskeli 25 kwa ajili ya watoa huduma ya afya ngazi ya jamii katika halmashauri ya mji Kahama likaanza Pichani ni baiskeli kwa ajili ya watoa huduma ya afya ngazi ya jamii katika halmashauri ya mji Kahama mkoani Shinyanga zilizotolewa na Shirika la Kitanzania lisilo la kiserikali AGPAHI (Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI kwa ufadhili wa Mfuko wa kusaidia watoto wenye VVU wa watu wa Uingereza (Children’s Investment Fund Foundation UK - CIFF). Watoa huduma ya afya ngazi ya jamii katika halmashauri ya mji Kahama mkoani Shinyanga wakikagua baiskeli hizo kabla wakati wa zoezi la makabidhiano Msimamizi wa kituo cha Huduma na Matunzo kwa watu wanaoishi na VVU kilichopo katika hospitali ya mji wa Kahama, Dkt John Malulu akikagua baiskeli,kulia kwake ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Cecilia Yona akitoa maelekezo ya kutunza baiskeli hizo ambapo alisema zitakuwa chini ya watoa huduma hao wa afya na watakuwa wanazitunza na baada ya mradi kumalizika zitakuwa zao lakini ambaye hatatumia kwa malengo yaliyokusudiwa atanyang'anywa na kupewa mwingine mwenye wito wa kufanya kazi Kila mmoja anakagua ya kwake Msimamizi wa kituo cha Huduma na Matunzo kwa watu wanaoishi na VVU kilichopo katika hospitali ya mji wa Kahama Dkt John Malulu akikagua moja ya baiskeli hizo Kulia ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Cecilia Yona akiwasainisha mkataba wa kupokea baiskeli watoa huduma ya afya ngazi ya jamii katika halmashauri ya mji Kahama,ambapo miongoni mwa masharti ya mktaba huo ni kutumia baiskeli hizo ajili ya kufuatilia wateja waliopotea katika huduma ya kupata dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (ARV’s) sambamba na kufuatilia watoto chini miaka miwili, wajawazito, wanaonyonyesha na watoto chini ya miaka 15,pia kusaidia jamii kupata elimu ya VVU na UKIMWI.


  Hapa ni katika Zahanati ya Segese katika halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga..Pichani ni watoa huduma ya afya ngazi ya jamii kutoka maeneo mbalimbali ya halmashauri ya Msalala waliojitokeza kupokea msaada wa baiskeli ambapo katika halmashauri hiyo jumla ya baiskeli 32 zimetolewa na shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa Mfuko wa kusaidia watoto wenye VVU wa watu wa Uingereza (Children’s Investment Fund Foundation UK - CIFF),Pichani mbele kushoto ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Cecilia Yona akitoa maelekezo kuhusu msaada wa baiskeli hizo Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Cecilia Yona akisoma maelezo ya mktaba kati ya shirika la AGPAHI na watoa huduma ya afya ngazi ya jamii huku kila mmoja akiwa ameshikilia mktaba wake Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Cecilia Yona akizungumzia umuhimu wa kutumia vyema baiskeli hizo ili kuwarahisishia kazi ya kuwafikia wateja majumbani Baiskeli zilizokabidhiwa kwa watoa huduma ya afya ngazi ya jamii katika kituo cha Segese halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga Wa pili kushoto ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Cecilia Yona akiwaonesha watoa huduma kituo cha Segese baiskeli watakazozitumia kuwafikia wateja wa majumbani Kulia ni mtoa huduma ya afya ngazi ya jamii katika kituo cha Segese bwana Mwaje Dotto akitafakari jambo na Mviu mshauri kituo cha Segese bwana Kanzaga Fabian ambao kwa pamoja walieleza kufurahishwa na msaada huo kwani awali walikuwa wanatumia gharama kubwa kuwafikia wateja majumbani Hapa ni katika kituo cha afya cha Lunguya katika halmashauri ya wilaya ya Msalala ambapo watoa huduma ya afya ngazi ya jamii katika eneo hilo walipewa baiskeli kwa ajili ya kuwarahisishia kufanya kazi zao,pichani ni watoa huduma wakikagua baiskeli zao Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Cecilia Yona akiwasisitiza watoa huduma za afya ngazi ya jamii kuhakikisha kuwa wanawafuatilia wateja waliopotea katika huduma ya kutumia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI(ARV's) katika eneo la Lunguya ili warudi kwenye huduma badala ya kusubiri miili idhoofike ndiyo waanze kutumia dawa Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Cecilia Yona akiwa na muuguzi mkuu katika kituo cha afya cha Lunguya Pili Paulo wakati wa kukabidhi baiskeli kwa watoa huduma katika kituo hicho Kushoto ni Mwandishi wa habari wa Kahama Fm Amina Mbwambo akifanya mahojiano na muuguzi mkuu katika kituo cha afya cha Lunguya Pili Paulo,ambaye alieleza changamoto kubwa katika kituo hicho ni wateja kupotea kwa wateja kutokana na uwepo wa migodi ya madini katika eneo hilo Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Cecilia Yona akiwasisitiza watoa huduma katika kituo cha Lunguya kuendelea kuielimisha jamii kuhusu VVU na UKIMWI Kila mmoja akaondoka na ya kwake,kwa kuwa jukumu la kutunza ni kila aliyechukua,basi wengine wakaanza kujaza upepo baiskeli hizo ili waendelee na kazi ya kuelimisha jamii kuhusu VVU na UKIMWI Hapa ni katika ofisi za afya za manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga ambako zoezi la kukabidhi baiskeli 20 kwa watoa huduma katika manispaa hiyo limefanyika leo Februari 03,2016 likiongozwa na meneja Mradi kutoka AGPAHI mkoa wa Shinyanga Dkt Gastor Njau Kulia ni meneja Mradi kutoka AGPAHI mkoa wa Shinyanga Dkt Gastor Njau akisaini mikataba ya msaada wa baiskeli kwa watoa huduma ya afya ngazi ya jamii katika manispaa ya Shinyanga,kulia ni bi Dafrosa Chale Shiluka ambaye ni mratibu miradi kutoka AGPAHI Kulia ni meneja Mradi kutoka AGPAHI mkoa wa Shinyanga Dkt Gastor Njau akisaini mikataba ya msaada wa baiskeli kwa watoa huduma ya afya ngazi ya jamii katika manispaa ya Shinyanga,kulia ni bi Dafrosa Chale Shiluka ambaye ni mratibu miradi kutoka AGPAHI wakiwa katika ofisi ya mganga mkuu wa manispaa hiyo wakati wa zoezi la kugawa baiskeli 20 kwa watoa huduma ya afya ngazi ya jamii Meneja Mradi kutoka AGPAHI mkoa wa Shinyanga Dkt Gastor Njau akizungumza wakati wa kukabidhi baiskeli hizo 20,ambapo alitumia fursa hiyo kuwaomba watoa huduma hao wa afya kutumia baiskeli hiyo kuwafikia watoto wanaoishi na VVU waliopotea katika huduma ya tiba na jamii kwa ujumla kwani dhamira kubwa ya shirika hilo ni kuwahudumia wananchi Meneja Mradi kutoka AGPAHI mkoa wa Shinyanga Dkt Gastor Njau alisema baiskeli hizo zitakuwa mali ya watoa huduma hao ambao watakuwa wanazitengeza pindi zinapoharibika Dafrosa Chale Shiluka ambaye ni mratibu miradi kutoka AGPAHI akiwaongoza watoa huduma ya afya ngazi ya jamii katika manispaa ya Shinyanga kujaza mikataba wa makabidhiano ya baiskeli hizo Meneja Mradi kutoka AGPAHI mkoa wa Shinyanga Dkt Gastor Njau akijaribu kuendesha moja ya baiskeli hizo baada ya zoezi la makabidhiano kukamilika Watoa huduma za afya ngazi ya jamii katika manispaa ya Shinyanga wakiwa wameshikilia baiskeli zao-Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog Shinyanga ********* Shirika la Kitanzania lisilo la kiserikali AGPAHI (Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI limetoa msaada wa baiskeli 104 kwa watoa huduma ya elimu ya VVU na UKIMWI ngazi ya jamii katika halmashauri nne za wilaya mkoani Shinyanga. Zoezi la kugawa baiskeli hizo limefanyika jana na leo ambapo Halmashauri zilizopata msaada huo ni Halmashauri ya Mji Kahama iliyopata baiskeli 25, Halmashauri ya Msalala baiskeli 32, Halmashauri ya Ushetu 27 na Manispaa ya Shinyanga iliyopata baiskeli 20. Akizungumza wakati wa kukabidhi baiskeli hizo ,Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Cecilia Yona alisema msaada huo umetolewa na Shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa Mfuko wa kusaidia watoto wenye VVU wa watu wa Uingereza (Children’s Investment Fund Foundation UK - CIFF) ambao ni moja ya wafadhili wa shirika la AGPAHI “Mfuko huu wa CIFF unafadhili mradi wa kusaidia kuongeza usajili wa watoto waishio na VVU kupata huduma za tiba na matunzo, hivyo, lengo la ufadhili wa baiskeli hizi ni kurahisisha kazi kwa watoa huduma ya afya kwa ngazi ya jamii ambao hufanya kazi na shirika hili”, alisema Yona. “Matumaini yetu ni kwamba baiskeli hizi zitatumika kwa ajili ya kufuatilia wateja waliopotea katika huduma ya kupata dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (ARV’s),kufuatilia watoto chini miaka miwili, wajawazito, wanaonyonyesha na watoto chini ya miaka 15 wanaoishi na VVU pamoja na kuisaidia jamii kupata elimu ya VVU na UKIMWI", aliongeza Yona. Yona aliwataka watoa huduma wa afya waliopata baiskeli hizo kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa huku akiwasisiza juu ya umuhimu wa kufuatilia wateja waliopotea kwani taifa linapoteza nguvu kazi kutokana na baadhi ya watu waliopata maambukizi ya VVU kutozingatia masharti waliyopewa na wataalam wa afya ikiwemo kuacha kabisa kutumia dawa za ARV’s. "Bado kuna changamoto ya wateja wetu kuacha kutumia dawa hasa wanapoona miili yao ina nguvu lakini pindi tu miili ikianza kudhoofika hukimbilia hospitali,naomba jamii ibadilike,na kupitia baiskeli hizi mtawafikia wale wote waliopotea katika huduma",alieleza Yona. Naye Meneja mradi kutoka AGPAHI mkoa wa Shinyanga Dkt Gastor Njau alitumia fursa hiyo kuwataka watoa huduma ya afya majumbani kuwafikia watoto wenye maambukizi ya VVU kwani bado watoto wengi hawajafikiwa na kuamini kuwa baiskeli hizo watazitumia kuwafikia watoto walio wengi zaidi. Kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Kahama Dkt Samwel Mwalutambi mbali na kulishukuru shirika hilo kwa kuwajali watoa huduma ya afya majumbani aliwataka waliopata baiskeli hizo kuzitunza kama zao huku akiahidi uongozi wa wilaya kusimamia baiskeli hizo katika vituo vyao vya afya kwa maslahi ya jamii nzima. Naye Muuguzi mkuu katika Kituo cha afya Lunguya halmashauri ya Msalala Pili Paulo alisema miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo ni wateja wengi kukatisha huduma hali inayowawia ugumu kuwapata ili warudi katika huduma ya tiba kutokana na eneo lao kuzungukwa na migodi hivyo watu wanakuja na kuondoka katika eneo hilo. Msimamizi wa kituo cha Huduma na Matunzo kwa watu wanaoishi na VVU kilichopo katika hospitali ya mji wa Kahama, Dkt John Malulu alisema hivi sasa hali ya unyanyapaa kwa wagonjwa wa UKIMWI imepungua ukilinganisha na miaka iliyopita na kilichobaki sasa ni unyanyapaa wa watu binafsi kuogopa kupima afya zao ili kubaini kama wana maambukizi ya VVU au la. Kwa upande wao baadhi ya watoa huduma ya afya waliopata msaada huo, Stella Paul na Nobert Zephania walisema kabla ya kupata baiskeli walikuwa wanalazimika kutumia gharama zao kuwafikia wateja wao hivyo baiskeli hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuifikia jamii. AGPAHI ni shirika la kitanzania lisilo la kiserikali linalojishughulisha na shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI,kutoa huduma ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto,kutoa huduma ya uchunguzi na huduma za awali ya saratani ya shingo ya kizazi na kutoa huduma za afya ya uzazi na uzazi wa mpango. Na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga

older | 1 | .... | 753 | 754 | (Page 755) | 756 | 757 | .... | 1903 | newer