Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

LIGI KUU MZUNGUKO WA 17 KUENDELEA KESHO.

0
0
LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania bara mzunguko wa 17 unatarajiwa kuendelea kesho Jumatano kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja mbalimbali, huku kila timu ikisaka pointi tatu muhimu kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Kesho Jumatano, Simba SC watakua wenyeji wa maafande wa Mgambo Shooting kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, JKT Ruvu watawakaribisha Mbeya City katika uwanja wa kumbukumu ya Karume Ilala, huku Mtibwa Sugar wakicheza dhidi ya Toto Africans katika uwanja wa Manungu – Turiani.

Jijini Mbeya, Tanzania Prisons watakua wenyeji wa vinara wa ligi hiyo Young Africans katika uwanja wa Sokoine, Wana kimanumanu African Sports watacheza dhidi ya Mwadui FC uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku wakata miwa wa Kagera Sugar wakiwakaribisha Majimaji FC katika uwanja wa Kamabarage mjini Shinyanga.

Alhamisi ligi hiyo itaendelea kwa kuchezwa mchezo mmoja tu, Wagosi wa Kaya Coastal Union watawakaribisha Ndanda FC katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.


Michezo ya viporo ya Azam FC imepangiwa ratiba, mchezo dhidi ya Tanzania Prisons utachezwa Februari 24 uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, huku mchezo dhidi ya Stand United ukichezwa Machi 16 katika uwanja wa Azam Complex.

Fahamu mengi kutoka kwa Afisa mkuu kutoka bohari kuu ya dawa, akikufahamisha mambo mengi kuhusu matumizi ya dawa.

0
0

Matukio Bungeni leo.

0
0
 Naibu Spika Mhe.Dkt Tulia Ackson akiingia Bungeni tayari kuongoza Kikao cha 6 cha Mkutano wa pili wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
 Mhe. Balozi Dkt Augustine Maiga akuungia Bungeni tayari kwa kuapishwa.
  Naibu Spika Mhe.Dkt Tulia Ackson akimwapisha Mhe. Balozi Dkt Augustine Maiga.
 Naibu Spika Mhe.Dkt Tulia Ackson akiongoza Kikao cha 6 cha Mkutano wa pili wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.

 Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa,majaliwa akiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa SerikaliMhe.George Masaju wakati katika Kikao cha 6 cha Mkutano wa pili wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye akifatilia Kikao cha 6 cha Mkutano wa pili wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Prof Jumanne Maghembe akijibu hoja toka kwa Wabunge mbalimbali katika Kikao cha 6 cha Mkutano wa pili wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.January Makamba akijibu hoja toka kwa Wabunge mbalimbali katika Kikao cha 6 cha Mkutano wa pili wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
 Baadhi ya wageni wakifatilia Kikao cha 6 cha Mkutano wa pili wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.

Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO

NHIF YAKABIDHI MASHUKA 170 KWENYE ZAHANATI YA KIJIJI CHA ENGUSERO WILAYANI KITETO.

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Kanali Samuel Nzoka (kulia) akipokea moja kati ya mashuka 170 yaliyotolewa juzi na Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) wa mkoa wa Manyara, Isaya Shekifu (kushoto) kwenye uzinduzi wa uhamasishaji wa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF.

Na Woinde Shizza,Manyara.
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Manyara, umekabidhi mashuka 170 kwenye zahanati ya Kijiji cha Engusero na hospitali ya wilaya ya Kiteto kwa ajili ya kutumiwa kujifunika na wagonjwa wanaofika kulazwa.

Mashuka hayo yalikabidhiwa kwa mkuu wa wilaya hiyo Kanali Samuel Nzoka na meneja wa NHIF wa mkoa huo Isaya Shekifu, kwenye uzinduzi wa uhamasishaji wa kujiunga mfuko wa afya ya jamii (CHF) uliofanyika juzi kijiji cha Engusero.

Akizungumza wakati akipokea mashuka hayo Kanali Nzoka aliushukuru mfuko huo na kuzitaka kaya za eneo hilo kujiunga na CHF ili wajipatie matibabu kwa mwaka mzima kwani kaya moja yenye watu sita italipia sh10,000.

Alisema tatizo la ukosefu wa dawa kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitalini litamalizika, endapo kaya nyingi zikijiunga na CHF kwani serikali nayo itaweka mkono wake ili kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa.

Wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo Kanali Nzoka alijitolea sh20,000 kwa ajili ya kuzilipia kaya mbili za watu 12 wa kijiji cha Engusero na Dosidosi na kuungwa mkono na viongozi wanne wa wilaya hiyo waliojitolea sh10,000 kwa kila mmoja.

Kwa upande wake, Shekifu alisema mwanachama wa CHF atanufaika na huduma zote za afya za msingi za kinga na tiba zitolewazo katika zahanati, kituo cha afya na hospitali ikiwemo huduma za wagonjwa wa kutwa na kulazwa.

Alitaja huduma nyingine ambazo zitatolewa kwa mwaka mmoja kwa kuchangia sh10,000 ni vipimo vya maabara, upasuaji kulingana na utaratibu uliowekwa na halmashauri husika na wanachama kupata huduma bora ya afya.

“Pia watapata huduma ya upasuaji kulingana na utaratibu uliowekwa na Halmashauri zinazoendesha mifuko hii zinapata mapato ya tele kwa tele kutoka serikalini ambayo yatatumika kuboresha huduma za afya,” alisema.

Ofisa uratibu na matokeo wa CHF, Nicholaus Mwangomo alisema mpango huo ulianzishwa kwa sheria namba moja ya mwaka 2001 sura ya 409 ya sheria ya Tanzania toleo la 2002 wa kaya au familia kuchangia gharama za matibabu kabla ya kuugua.


Mwangomo alisema sababu za kuanzishwa CHF ni kuiwezesha jamii kumiliki huduma za afya zinazowahusu katika maeneo wanayoishi, kuchangia huduma za afya kwa wananchi na kuboresha huduma za matibabu kwa utaratibu rahisi.

JENGO LA GHOROFA 16 LILILOPO MTAA WA INDRA GHANDI JIJINI DAR LINAANDALIWA KWAAJILI YA KUBOMOLEWA.

0
0
 Alama zinazotoa tahadhali kwa watumiaji wa barabara hii wakiwa wakiwa wamewekewa tahadhali kwaajili ya kuvunjwa kwa gharofa la Ghorofa 16 lililopo mtaa wa Indra Ghandi jijini Dar es Salaam.
Mafundi wakiwatoa vyuma kupisha ubomoaji wa jengo la ghorofa 16 lililopo katika mtaa wa Indra Ghandi jijini Dar es Salaam. 
Jengo la Ghorofa 16 linaloandaliwa kwaajili ya kubomoa.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

Serikali kuongeza ajira

0
0
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Suleiman Jafo akijibu maswali toka kwa  wabunge katika kikao cha 6 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO

(Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO)
 
Serikali katika mwaka wa fedha 2016/2017 imepanga kuongeza ajira kwa vijana ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana wengi wa kitanzania kwa kuongeza ajira na kuwezesha wengine kujiajiri kupitia mifuko ya uwezeshaji toka Halmashauri za Wilaya nchini.
 
Akijibu swali la Mhe.Mgumba Tebweta Omary Mbunge wa Morogoro Kusini (CCM) lenye sehemu a na b lililouliza Serikali itaanza lini kuwawezesha vijana wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki  kifedha ili waweze kujiajiri na kuondokana na tatizo la ajira na umaskini ,Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe  Suleiman Jafo amesema vijana katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Kusini Mashariki wamekuwa wakiwezeshwa kiuchumi kupitia fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambapo kila Halmashauri hupaswa kutenga asilimia 5 ya mapato yake ya ndani kila mwaka kwa ajili ya vijana.
 
Mhe  Suleiman Jafo ameongeza kuwa katika Bajeti ya mwaka 2014/2015,Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ilifanikiwa kutoa Shillingi Millioni 10.3 kwa vikundi vya vijana 19 kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali za kiuchumi na katika Bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016 vikundi vya vijana vilitengewa Shilllingi Millioni 87.5 ili kuviwezesha kiuchumi kwa kujiajiri.
 
“ Katika kutatua changamoto zilizopo kwa vijana tunawawezesha  kifedha ili kujiajiri ili kumekuwa na tatizo la fedha kuchelewa kufika kwa walengwa ila Serikali kupitia Wizara yangu tunalifanyia kazi ili fedha zifike kwa wakati na tumetenga Shillingi Millioni 50 kwa kila kijijikwa ajili ya kuwezesha vijana walioko katika vikundi mbalimbali mfano SACCOS ili waweze kujiajiri na kujikwamua kiuchumi kwa kujiondoa katika hali ya umaskini”
 
“ Napenda kuwaomba wabunge tusaidiane sababu wao  wanahusika katika kamati za fedha za Halmashauri za Wilaya, waende wakasimamie hizo fedha kwa ajili ya kuwezesha vijana  zitoke na ziwasaidie walengwa” Alisema Mhe Jafo.
 
Aidha Mhe  Suleiman Jafo amesema kuwa Serikali imetenga Shillingi Billioni 233 kwa ajiri ya kuajiri vijana wapya takribani 71,408 kati ya hao watumishi wapya wa Afya wanatarajiwa kuwa takribani 10,871 na Waalimu 40,000 kwa nchi nzima ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana wanaomaliza vyuo mbalimbali nchini.
 
Serikali kupitia Halmashauri za Wilaya imejipanga katika kuwawezesha vijana katika maeneo yao kujikwamua kiuchumi kwa kujiajiri na kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Serikali itaboresha zaidi mifuko ya kuwezesha vijana katika Halmashauri za Wilaya kwa kununua vifaa zaidi vya kujifunza stadi mbalimbali za kazi zitakazowezesha vijana wengi zaidi kuwa na ujuzi utakaowasaidia kujipatia kipato na kujikwamua kiuchumi.

DC KINONDONI, PAUL MAKONDA APOKEA SARUJI MIFUKO 1640 KUTOKA KWA WADAU WA MAENDELEO KWA AJILI YA UJENZI WA SHULE ZA SEKONDARY

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Duma, Areeq Amran Mohamed (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda mfuko mmoja wa saruji kati ya 640 aliyoitoa kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Shule za Sekondari za wilaya hiyo Dar es Salaam leo asubuhi. Katika makabidhiano hayo Makonda alipokea mifuko 500 ya saruji kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo na Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk.Alex Malasusa aliyetoa mifuko 500.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo (kulia), akimkabidhi saruji hiyo DC Makonda.
Lori lilibeba saruji hiyo likiwa eneo la tukio.
DC Makonda na wageni wake wakiwa eneo la tukio kabla ya makabidhiano ya saruji hiyo.
Mhe. Bulembo akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada huo.
Wanahabari wakizungumza na watoa msaada huo.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO PROFESA MBARAWA AMTEUA MASANJA KUNGU KADOGOSA KUWA KAIMU MKURUGENZI MKUU WA TRL.

0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemteua Bwana Masanja Kungu Kadogosa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), ambako anakwenda kuchukua nafasi ya Mhandisi Elias Mshana ambaye anastaafu hivi karibuni.

Kabla ya Uteuzi huo Bwana Masanja Kadogosa alikuwa Mkurugenzi Idara ya Mikopo Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB). Uteuzi huo unaanza mara moja.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
02 Februari, 2016.

Serikali kuimarisha miundombinu kuboresha Utalii nchini.

0
0
Serikali imejipanga kuimarisha miundombinu inayoelekea kwenye mbuga za wanyama na vituo vingine vya utalii nchini ili kuboresha utalii wa ndani na wa nje ya nchi kwa kujenga barabara ili kuwezesha watalii kufika kwa urahisi katika sehemu za vivutio vya kiutalii.
 
Akijibu swali la Mhe.Risala Said Kabongo Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) lililoulizwa serikali ina mikakati gani kuboresha miundombinu ya barabara, malazi na viwanja vya ndege katika hifadhi, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Ramo Makani amesema jitihada zimefanya na zinaendelea kufanywa ili kuboresha na kuimarisha barabara mbalimbali zinazoelekea katika hifadhi mbalimbali nchini kwa kiwango cha lami ili kuongeza wigo wa watalii kutembelea maeneo hayo kwa urahisi.
 
Amezitaja barabara ambazo zilizoko kwenye mpango wa kuziboreshwa ili kurahisisha watalii kuyafikia maeneo hayo kuwa ni barabara ya Sumbawanga-kasanga, barabara ya Kigoma kuelekea kusini hadi Kalya na Mwese.
 
“Sio tutaboresha barabara tu ila tunaviangalia pia viwanja vya ndege vinavyotumika kwa kuviimarisha na kuviboresha viwanja vya ndege vya Songwe,Kigoma na Mpanda ambavyo vitasaidia kufikika kwa urahisi maeneo ya vivutiio”
 
“ Tunaendelea kuvutia wawekezaji binafsi kutoa huduma mbalimbali za watalii kama malazi na mpka sasa  tumetoa vibali 11 kwa wawekezaji kuwekeza katika malazi yaani Hoteli za kitalii katika Hifadhi za Ruaha,Mikumi,katavi na Mahale  na uwekezaji huo uko katika hatua za utekelezaji” Alisema Mhe. Ramo Makani.
 
Wizara kwa kushirikiana an Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Shirika la USAID inaandaa mikakati ya kuendeleza na kuutangaza utalii kwenye maeneo mbalimbali na kuboresha miundombimu ili kuwezesha watalii kufikia vivutio kiurahisi.

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA OFISI NDOGO YA CCM LUMUMBA LEO.

0
0
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye Ofisi ndogo ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam leo Februari 02, 2016 wakati Makamu wa Rais alipotembelea katika Ofisi hiyo.

 (Picha na OMR)

kiteto yakabidhiwa mashuka 170

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Kanali Samuel Nzoka (kulia) akipokea moja kati ya mashuka 170 yaliyotolewa juzi na Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) wa mkoa wa Manyara, Isaya Shekifu (kushoto) kwenye uzinduzi wa uhamasishaji wa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF.

Na Woinde Shizza,Manyara

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Manyara, umekabidhi mashuka 170 kwenye zahanati ya Kijiji cha Engusero na hospitali ya wilaya ya Kiteto kwa ajili ya kutumiwa kujifunika na wagonjwa wanaofika kulazwa.

Mashuka hayo yalikabidhiwa kwa mkuu wa wilaya hiyo Kanali Samuel Nzoka na meneja wa NHIF wa mkoa huo Isaya Shekifu, kwenye uzinduzi wa uhamasishaji wa kujiunga mfuko wa afya ya jamii (CHF) uliofanyika juzi kijiji cha Engusero.

Akizungumza wakati akipokea mashuka hayo Kanali Nzoka aliushukuru mfuko huo na kuzitaka kaya za eneo hilo kujiunga na CHF ili wajipatie matibabu kwa mwaka mzima kwani kaya moja yenye watu sita italipia sh10,000.

Alisema tatizo la ukosefu wa dawa kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitalini litamalizika, endapo kaya nyingi zikijiunga na CHF kwani serikali nayo itaweka mkono wake ili kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa.

Wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo Kanali Nzoka alijitolea sh20,000 kwa ajili ya kuzilipia kaya mbili za watu 12 wa kijiji cha Engusero na Dosidosi na kuungwa mkono na viongozi wanne wa wilaya hiyo waliojitolea sh10,000 kwa kila mmoja.

Kwa upande wake, Shekifu alisema mwanachama wa CHF atanufaika na huduma zote za afya za msingi za kinga na tiba zitolewazo katika zahanati, kituo cha afya na hospitali ikiwemo huduma za wagonjwa wa kutwa na kulazwa.

Alitaja huduma nyingine ambazo zitatolewa kwa mwaka mmoja kwa kuchangia sh10,000 ni vipimo vya maabara, upasuaji kulingana na utaratibu uliowekwa na halmashauri husika na wanachama kupata huduma bora ya afya.

“Pia watapata huduma ya upasuaji kulingana na utaratibu uliowekwa na Halmashauri zinazoendesha mifuko hii zinapata mapato ya tele kwa tele kutoka serikalini ambayo yatatumika kuboresha huduma za afya,” alisema.

Ofisa uratibu na matokeo wa CHF, Nicholaus Mwangomo alisema mpango huo ulianzishwa kwa sheria namba moja ya mwaka 2001 sura ya 409 ya sheria ya Tanzania toleo la 2002 wa kaya au familia kuchangia gharama za matibabu kabla ya kuugua.

Mwangomo alisema sababu za kuanzishwa CHF ni kuiwezesha jamii kumiliki huduma za afya zinazowahusu katika maeneo wanayoishi, kuchangia huduma za afya kwa wananchi na kuboresha huduma za matibabu kwa utaratibu rahisi.

MANISPAA YA ILEMELA YAWEKA MSIMAMO WAKE DHIDI YA WAFANYABIASHARA WA HOTEL NA NYUMBA ZA KULALA WAGENI.

0
0
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Wanga akitoa ufafanuzi kwa Wanahabari juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni.
Kikao juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni kikielendelea.
Afisa biashara Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza akitoa ufafanuzi juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni.
Hawa Waziri ambae ni Mwanasheria wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza akitoa ufafanuzi kwa wanahabari juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni.
Cyprian Oyier ambae ni mmoja wa wafanyabiashara wa hotel Manispaa ya Ilemela akiwasilisha hoja zake katika kikao juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni.
Lemmy Muganyizi Mboyelwa ambae ni mmoja wa wamiliki wa nyumba ya kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela akiwasilisha hoja zake katika kikao juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni.

Wafanyabiashara wa Hotel na Nyumba za Kulala Wageni katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, Wametakiwa kufanya biashara zao kwa mjibu wa kanuni na sheria za biashara zao ikiwemo kulipa ushuru na kodi mbalimbali kama ilivyoidhinishwa na Serikali.

Kauli hiyo imetolewa hii leo na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Wanga, katika Kikao cha Viongozi wa Manispaa ya Ilemela na Wafanyabiashara hao, juu ya Ufafanuzi wa Sheria ya Kodi ya Malazi, ambayo imeanza kukusanywa kwenye Hotel pamoja na nyumba zote za kulala wageni.

“Kama una wajibu wa kulipa kodi Majengo, leseni ya biashara, mabango, ushuru wa malazi, ushuru wa huduma na kodi nyingine zote zilizo kisheria, ni vyema ukalipa bila kushurutishwa. Kutokufanya hivyo utatufanya twende kwenye ule mkono mwingine ambao tusingependa sana kuutumia ambao ni kushurutishana”. Amesema Wanga. 

Hata hivyo licha ya agizo hilo, Wafanyabiashara katika Manispaa hiyo wameiomba Serikali kuwapunguzia mzigo wa Kodi walionao kwa kuwa hivi sasa wanakabiriwa na mzigo mkubwa wa kodi pamoja na Ushuru jambo ambalo wamesema ni tofauti na ahadi ya kuondoa kero ya kodi mbalimbali aliyoitoa Mhe.Rais John Pombe Magufuli wakati wa Kampeni zake.

“Kodi zimekuwa nyingi sana kwa sisi wafanyabiashara wa Hotel na Guest Houses (nyumba za kulala wageni), kwa mfano kodi ya majengo, leseni ya biashara, ardhi, mabango na nyinginezo. Yaani nyumba moja inakuwa na kodi zaidi ya 11 sasa itafika sehemu tutashindwa kufanya biashara. Sisi tuko tayari kulipa kodi ya majengo, ardhi na leseni hivyo serikali iangalie namna ya kutusaidia”. Alisema Nuru Ramadhan ambae ni mmoja wa wamiliki wa nyumba ya kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela na kuungwa mkono na wenzake.

Hawa Waziri ambae ni Mwanasheria wa Manispaa ya Ilemela, amewasihi Wafanyabiashara hao kuwa tayari kulipa kodi zilizopo kisheria, ikiwemo Kodi ya Malazi huku wakiendelea kujenga hoja Serikalini ili Sheria hizo zifanyiwe marekebisho bungeni na hatimae kupunguzwa.

Awali Wafanyabiashara wa Hotel na Nyumba za Kulala Wageni, walikuwa wakilipa Kodi ya Malazi ambayo ni asilimia 20 ya mapato yanayotokana na malipo ya kila mteja, kabla ya kodi hiyo kusitishwa na Serikali ambapo hata hivyo imerejeshwa tena na Wafanyabiashara hao wanatakiwa kulipa kodi ya asilimia 10 ya mapato yanayotokana na mteja badala ya 20 kama ilivyokuwa awali.
Nuru Ramadhani ambae ni mmoja wa wamiliki wa nyumba ya kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela akiwasilisha hoja zake katika kikao juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni

Melikior Fundi Minsa ambae ni mmoja wa wamiliki wa nyumba ya kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela akiwasilisha hoja zake katika kikao juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni


Wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela wakiwa katika kikao cha ufafanuzi juu ya kuanza kutumika kwa kodi ya Malazi


Wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela wakiwa katika kikao cha ufafanuzi juu ya kuanza kutumika kwa kodi ya Malazi


Kushoto ni Stella Lwakatare ambae ni Afisa Biashara Mkuu katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza akifafanua jambo kwenye kikao cha Wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela juu ya kuanza kutumika kwa kodi ya Malazi.

Katikani ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Paul Wanga na Kulia ni Peter Revelian ambae ni Mwekahazina wa Manispaa ya Ilemela.


Watumishi wa idara mbalimbali katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.

Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo

TANZIA YA MFANYAKAZI WA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO, Marehemu Jovitha Dellan Tarmo.

0
0

MTUMISHI WA WIZARA YA HABARI AFARIKI  KWA AJALI YA GARI.


Kufuatia kifo cha Mfanyakazi wa  Bodi ya Filamu Tanzania Bwana Jovitha Dellan, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel ameitumia salamu za Rambirambi familia ya Mzee Dellan Tarmo kufuatia kifo kijana wao mpendwa kilichotokea juzi (tarehe 31.1.2016)kwa ajali ya gari mkoani Arusha.


“Pokea rambirambi zangu za dhati, sote kwa pamoja tumepoteza kijana  mchapakazi, hodari na aliyependa kushirikiana na wenzake katika kazi zake, hakika tutamkumbuka siku zote” Katibu Mkuu amesema.


Katibu Mkuu, Pia amemtumia salamu za pole kwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu(KBF) na Wafanyakazi wote wa Bodi ya  Filamu Tanzania.“Nimepokea taarifa za kifo cha Jovitha Dellan kwa huzuni kubwa, najua machungu na maumivu mliyonayo kwa kuondokewa na kiungo muhimu katika utendaji wenu, poleni sana,  niko nanyi katika msiba huu mzito kwenu”, amesema Katibu Mkuu huyo.

Katibu Mkuu amesema pamoja na kwamba kifo hakiepukiki, bado ni kitu ambacho kinashtua, kuhuzunisha na kuleta unyonge mkubwa kwa wafiwa katika jamii. “Naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu kumuombea kijana wetu Jovitha Dellan ili mwenyezi Mungu ampe mapumziko mema ya Milele” Mwenyezi Mungu awatie nguvu, awape uvumilivu na subira katika kipindi hiki”.

“Niko nanyi katika kipindi hiki kigumu kwa hali na mali, nawaomba msijisikie wapweke” Katibu Mkuu amesema na kuwatakia utulivu na amani katika kipindi hiki cha msiba mkubwa kwa familia.


Marehemu Jovitha Dellan  amefariki juzi tarehe 31 Januari, 2016 mkoani Arusha ambapo alikuwa njiani kurejea kazini jijini Dar es salaam.

          Marehemu Jovitha Dellan anatarajiwa kuzikwa wiki hii mkoani Manyara .

          Mungu ailaze Roho ya Marehemu Jovitha Dellan mahali Pema Peponi, Amina.


Imetolewa na:

Idara ya Habari(MAELEZO)

DSM.

2 Februari, 2016

 

WANANCHI WA JIMBO LA BUMBULI WAMPONGEZA WAZIRI MAKAMBA NI BAADA YA SERIKALI KUVUNJA MKATABA NA MWEKEZAJI WA KIWANDA CHA KUZALISHA CHAI MPONDE

0
0

NA RAISA SAIDI, BUMBULI.
SERIKALI ya Tanzania imevunja rasmi mkataba na mwekezaji
wakiwanda cha kuzalisha Chai cha Mponde kilichopo wilayani Bumbuli
Mkoani Tanga na kuamuru kitwaliwe na kianze kazi mara moja.

Akizungumza katika mkutano uliowajumuisha wadau wazao la
chai,Msajili wa Hazina Laurence Mafuru amesema kuwa kwa mamlaka
aliyopewa amevunja rasmi mkataba huo kwasababu Mwekezaji
aliyekuwepo kashindwa kutekeleza makubaliano yaliyoweka .

Mafuru alisema kuwa wamefikia uwamuzi huo kutokana na
kujiridhisha pamoja na kupitia mikataba walioingia na mwekezaji
huyo ndipo serikali imeamua ikirudishe kiwanda hicho mikononi
mwa Wizara ya Viwanda na Biashara ili utaratibu mpya wa
uendeshwaji wa kiwanda uanze huku Bodi ya Chai Tanzania
ukiendelea kukisimamia mpaka hapo serikali itakapotafuta mwekezaji
mwingine.

Mei mwaka 2013, wakulima wa chai waliitisha mkutano na kumwalika
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Januari Makamba na kueleza kutokuwa na
imani na mwekezaji na Chama cha Wakulima wa Chai cha Usambara (UTEGA) na kuamua kukifunga kiwanda licha ya Mbunge kuwasihi wasichukue uamuzi huo wa hasira.

Tangu wakati huo jitihada nyingi zimefanyika zikiongozwa na Mheshimiwa
Makamba kuhakikisha kwamba kiwanda kinafunguliwa na wakulima wanauza chai yao.

‘’ Tuliteseka kwa muda mrefu na leo Serikali imefanya uamuzi
wa kukirudisha kiwanda mikononi mwetu, Tunaishukuru Serikali kwa
kutusaidia sisi wananchi tulioteseka kwa muda mrefu ,” Alisema
Challes Ngovi ambaye ni mkulima wa chai Mponde.

Hata hivyo Mafuru alibainisha kuwa ucheleweshaji wa kukifungua
kiwanda hicho ulitokana na utaratibu uliokuwa ukifanywa na Serikali
na baada ya kujiridhisha ndipo ikaamua kumuandikia rasmi
barua Mwenyekiti wa Utega inayoonyesha kuvunjwa kwa mkataba huo
na kuamuru kiwanda kirudi Serikalini.

Kwa upande wake, Mbunge wa Bumbuli January Makamba alisema kwamba
kazi waliyomtuma wananchi ya kukirudisha kiwanda mikononi mwao
imekamilika ingawa imechukua muda mrefu.

Makamba ambaye pia ni Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
anayeshughuliokia Mazingira na Muungano alitumia nafasi hiyo
kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Magufuli kwa
kuingilia kati mgogoro huo ambao umedumu kwa zaidi miaka mitatu
na hatimae kuumaliza.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima wa Chai Usambara UTEGA
William Shelukindo aliilaumu serikali kutoka na uamuzi wake wa
kukitaifisha kiwanda hicho bila ya kutoa nafasi kwa mwekezaji kuweza
kujitetea kwani ni ameshindwa kuzalisha.

“Serikali katika hili imeshindwa kutupa nafasi ya kujitetea ili kuweza
kujua sababu za kushindwa kuzalisha ,lakini kwa sasa hatuna cha
kufanya zaidi ya kutekeleza matakwa yao”alisema Shelukindo.

Ambapo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza alisema kuwa siku 90 za kupeleka malalamiko na utetezi kwa seriklai zilishatangazwaa na
kumalizika kilichobaki ni utekelezaji wa kanuni na taratibu za
serikali kukichukuwa kiwanda na kuanza uzalishaji .

“Niwaombe wananchi hakikisheni mnazalisha zao hilo kwa wingi ili
kiwanda kiweze kufanyakazi na kuboresha uchumi wa kila mmoja
wenu,wilaya,mkoa na taifa kwa ujumla kwani Bumbuli mnategemea zao la
chai kwa kiasi kikubwa.

Wakati huo huo,Wananchi waishio maeneo mbalimbali katika Jimbo la
Bumbuli wilayani Lushoto mkoani Tanga wamempongeza Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira kwa
hatua ya kuwasaidia kuishawishi serikali kukipatia ufumbuzi mgogoro wa
kiwanda cha chai cha Mponde.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi, mmoja ya
wakulima hao,Swahiba Mbili alisema kuwa kufunguliwa utawasaidia
wananchi ambao walikuwa na changamoto ya mazao yao kuharibika shambani kupata soko la uhakika ambalo linaweza kuwainua kimaisha.

Swahiba alisema kuwa wao kama wakulima pamoja na kuishukuru serikali
kutwaa kiwanda lakini wanamshukuru Januari Makamba kwa sababu hakuweza kuwa mbali nao kwenye kipindi chote wakati kiwanda hicho kimefungwa na kuaidi kumpa ushirikiano katika kipindi cha kuwatumikia wananchi hao.

WAZIRI WA MAMBO YA NJE AUGUSTINE MAHIGA ALA KIAPO CHA UBUNGE LEO

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki na Kikanda, Augustono Mahiga akiapa Bungeni mjini Dodoma Februari 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson akimwapisha Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki na Kikanda, Augustono Mahiga , Bungeni mjini Dodoma Februari 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SERIKALI ITAENDELEA KUWAFUNGIA MAGETI WATUMISHI

0
0

Na.Catherine Sungura-Nzega

Serikali haitokuwa tayari kuwaona watumishi wa umma wachache wakinufaika na kufaidi pesa za walipa kodi hususan wa kipatao cha chini na wale maskinini

Hayo yamesema wilayani hapa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kigwangwalla alipokuwa akiwahutubia wananchi wa wilaya hiyo

Dkt.Kigwangwalla alisema serikali ya awamu ya tano inawataka watumishi wote nchini kufanya kazi za kuwahudumia wananchi na kuacha uzembe kwani awamu hii haiwezi kuwavumilia watumishi wa namna hiyo.

“Serikali haitowav umilia watumishi wazembe,hivyo tutaendelea kuwafungia mageti na kuwashughulikia wale wazembe,tunataka watumishi wa umma wafanye kazi ya kuwahudumia wananchi kwa ufanisi,mtumishi akizembea tutamtumbua majipu,akichelewa tunamfungia geti na akiiba tunafilisi pamoja na kumpeleka jela,hii ndiyo serikali ya hapa kazi tu”

Aidha alisema serikali ya awamu ya tano inataka kero za wananchi zifanyiwe kazi na kutekeleza ahadi zote za ilani ya uchaguzi ya ccm zinatimizwa.

“hatutomuonea mtu,lakini tutafanyia kazi pale penye matatizo,tunataka Tanzania mpya ya mwaka 2015 inakua,hatutaki hadithi wala ahadi”

Hatahivyo aliwataka wazazi wote wenye watoto wenye umri wa kwenda shule kuwapeleka watoto wao kuanza masomo kwani elimu kwa sasa ni bure na hakuna michango yoyote.

“natoa wito kwa walimu wote wasitoze michango yeyote wala ushuru kwa wazazi wanaowapeleka kuwaandikisha watoto shule kwani shule zimepatiwa pesa za kuendeshea shule hizo.

Dkt. Kigwangwalla aliwakumbusha watumishi wa umma kujipanga na kama watagundulika ni majipu bali hawatosita kuwatumbua hadi kina kitoke,usaha na damu kutoka bila huruma.

MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA MAGARI MATATU KUGONGANA JIJINI MBEYA.

0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA.
· MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA MAGARI MATATU KUGONGANA JIJINI MBEYA.

· JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA RAIA WAWILI WA NCHINI ETHIOPIA KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

· JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 08 KWA MAKOSA MBALIMBALI.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA [DEREVA] WA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 321 CSV AINA YA TOYOTA COASTER AITWAYE LWIMIKO MWANSASU [36] MKAZI WA UYOLE ALIFARIKI DUNIA BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 877 CWE AINA YA SCANIA BASI MALI YA KAMPUNI YA SUPERSHEM LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA EMANUEL JOHN [42] MKAZI WA MWANZA KUGONGANA NA GARI HILO NA KISHA KULIGONGA GARI JINGINE LENYE NAMBA ZA T. 321 CSV AINA YA TOYOTA HIACE LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AMBAKISYE MBOMA [45] MKAZI WA AIRPORT.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 02.02.2016 MAJIRA YA SAA 06:30 ASUBUHI HUKO ENEO LA SOWETO, KATA YA ILOMBA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. 

CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI WA BASI HILO LILILOKUWA LINATOKA MBEYA KUELEKEA MWANZA. DEREVA AMEKAMATWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. UPELELEZI UNAENDELEA.

TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA 1. AYNO ASATA [21] NA 2. CHARU SUMESO [18] KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

WAHAMIAJI HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 02.02.2016 MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI HUKO ENEO LA MAJENGO, KATA YA NSALAGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI ZINAENDELEA.

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATANO 1. HAIDAN RODRICK [35] 2. JULIUS BUTEMELE [53] 3. VISENT MAPILE [29] 4. DOTO MWASHITETE [25] NA 5. JOSEPH BUTEMELE [40] WOTE WAKAZI WA ISANGAWANA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA WAKIWA WANAKUNYWA POMBE MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TANO [5].

WATUHUMIWA KWA PAMOJA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 02.02.2016 MAJIRA YA SAA 14:45 MCHANA HUKO KIJIJI NA KATA YA ISANGAWANA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. 

MTU MMOJA MKAZI WA IYULA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JUMANNE HAONGA [32] ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA KUMI [10]. 

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 02.02.2016 MAJIRA YA SAA 11:20 ASUBUHI HUKO KIJIJI, KATA NA TARAFA YA IYULA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. 

MTU MMOJA MKAZI WA ILOLO WILAYA YA MBOZI MKOANI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DANIEL NZUNDA [30] ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA POMBE MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TANO [5].

MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 02.02.2016 MAJIRA YA SAA 13:40 MCHANA HUKO KIJIJI NA KATA YA ILOLO, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. 

WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI MARA BAADA YA UPELELEZI KUKAMILIKA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA WAGENI KUFUATA TARATIBU ZILIZOWEKWA ZA KUINGIA NCHINI ILI KUJIEPUSHA NA MATATIZO.

Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

TCRA YATOWA SEMINA KWA WAANDISHI WA HABARI KUGUNDUA SIMU FEKI ZANZIBAR.

0
0
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Innocent Mungy, akizungumza na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na kutambua Simu Feki na kudhibiti uingiaji wa Simu hizo Tanzania na kueleza mwisho wa matumizi wa simu hizo Nchini Tanzania ni Juni 2016. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilima Zanzibar na kuwashirikisha waandishi wa Vyombo mbali mbali vilioko Zanzibar. 
Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano  TCRA Thadayo Ringo, akizungumza na waandishi wa habari jinsi ya kutambua Simu feki wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar, Amesema utambuzi wa kujua simu yako kama ni orijinali  unaweza kupiga namba kuaza na Nyota Reli 06 Reli . *# 06#  na utapata ujumbe wa Simu yako kwa Mfano zitakuja tarakimu 15  mfano   IMEI 12456789067654  Na Kupiga 15090 Ujumbe wa kukuelewesha kama ni simu yako orijino. kwa mfano kama huu Sony Mobile Communications AB -SONY  C5555 - Xperia. huu ni mfano wa kujua simu orijino.
Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Thadayo Ringo akionesha mfano wa simu orijino kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo wa TCRA uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo wa TCRA uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Waandishi wakifuatilia mafunzo hayo kwa vitendo kuangalia somu zao kama ni orijino baada ya kupata elimu hiyo ya kujua simu feki na orijino wakati wa mkutano huo na Maofisa wa TCRA uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya zanzibar ocean view kilimani zanzibar. kwa kuingiza namba waliopewa.
Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya TCRA Innocent Mungy, akitowa maelezo kwa waandishi wa habari baada ya kuangalia simu zao baada ya kuingiza namba hizo na kugunduwa kuwa ziko salama na siyo feki. kwa bahati nzuri takribani waandishi wote simu zao orijino.
Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji Huduma za Maweasiliano Thadayo Ringo akimsomea ujumbe mmoja wa waandishi wa habari aliyehudhuria mkutano huo baada ya kuweka namba hizo na kuja ujumbe wa suimu siyo feki.
Mdau wa habari Farouk Karim akiuliza swali wakati wa mkutano huo kuhusiana na uingiaji wa simu za kutoka ulaya nyingi huwa na lock wakati wa mkutano huo.
Mwandishi Amour Mussa akiuliza kuhusu TCRA inachukua hatua gani endapo simu ikiibiwa.
Ndg Issa Yussuf akuliza jinsi ya utaratibu wa kuwafikia Wananchi wa Vijiji na zoezi hilo la ungunduzi wa simu feki na kuweza kuepuka na hasara hii, wakati ikifika tarehe hiyo ya mwisho wa matumizi ya simu hizo feki. 
Naibu Mkurugenzi Thadayo Ringo akifafanua na kujibu maswali yalioulizwa wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na matumizi ya Simu feki kufikia mwisho wake wa matumizi Tanzania.
Meneja Mawasiliano TCRA  Innocent Mungy  akifafanua jambo wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na kusitishwa kwa matumizi ya simu feki ifikapo mwezi juni 2016. 
Kaimu Meneja Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Zanzibar TCRA Ndg Seif  S Waziri akizungumza wakati wa mkutano huo na kutowa neno la shukrani kwa waandishi wa habari kuhudhuria mkutano huo wa kutowa elimu ya simu feki kwa Wananchi wa Zanzibar na Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar   



Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo wa mafunzo ya kutambua simu feki na Orijino uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Imetayarishwa na Othman Mapara.Blogspot.
Zanzinews.com. 

BEI YA MADAFU HII LEO.

0
0

MAFUNDI WAKIENDELEA NA UJENZI WA BARABARA YA MWENGE MOROCCO.

0
0
  Mafundi wakiendelea na ujenzi wa barabara ya Bagamoyo kipande cha kilometa 4.3 cha Mwenge – Morocco, leo jijini Dar es Salaam, ambayo ni kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Pombe  Joseph Magufuli.
 Scavertor kikichota undongo na kupakia katika magari kwenye barabara ya Mwenge hadi Morocco kwa kuongeza njia mbili za lami leo jijini Dar es Salaam.

Fundi akitoa maelekezo kwa mwendasha Scavertor katika barabara ya Mwenge hadi Morocco kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni matumizi ya Fedha za Uhuru zilizoagizwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kutengeneza Barabara hiyo.



(Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya jamii).
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images