Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli amhamisha Naibu Katibu Mkuu Sheria na Katiba kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu Utumishi na Utawala bora


JAJI MKUU OTHUMAN CHANDE ATOA SIKU SABA KWA MAHAKIMU 508 WATOE MAELEZO KWANINI WASIFUNGULIWE MASHITAKA KWA KUFANYA KAZI CHINI YA KIWANGO

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo mchana , kuhusu utendaji wa mahakimu wa mahakama za hakimu mkazi, mahakama za wilaya na mahakama za mwanzo ambapo alitoa siku saba kwa mahakimu 508 watoe maelezo kwani ni wasifunguliwe mashitaka ya nidhamu na kuwajibishwa kwa kufanya kazi chini ya kiwango. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omari Mallungu na kulia ni Jaji Kiongozi wa Tanzania, Shaban Omari Lila. Jaji Chande alitoa kauli hiyo kwenye maonyesho ya wiki ya Sheria yanayoendelea viwanja vya Mnazi Mmoja. 
Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande, akikaribishwa kutembea mabanda mbalimbali kwenye maonesho hayo.
Mkurugenzi Msaidizi Ukaguzi na Maadili Mahakama ya Tanzania, Warsha Ng'humbu (kushoto), akimuelekeza jambo Balbina Mrosso (kulia), kutoka Babati mkoani Manyara aliyetembelea banda la Idara ya Malalamiko kuomba msaada wa kisheria katika maonyesho hayo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande, akisoma moja ya daftari katika banda la Idara ya Malalamiko kwenye maonyesho hayo. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Malalamiko Mahakama ya Tanzania, Happiness Ndesamburo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande (kulia), akielekezwa jambo katika banda la Divisheni ya Biashara katika maonesho hayo. 




Na Dotto Mwaibale


JAJI Mkuu wa Tanzania Othuman Chande ametoa siku saba kwa mahakimu 508 watoe maelezo ni kwanini wasifunguliwe mashtaka ya nidhamu na kuwajibishwa, baada ya kufanya kazi chini ya kiwango.

Jaji Chande ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Mnanzi Mmoja jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Sheria.

Alisema kiwango cha kesi kwa kila Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya ni 250, ambapo Mahakimu Wakazi 121 kwenye mahakama hizo wameamua kesi chini ya 100 mwaka jana.


Alibainisha kuwa kiwango cha kwa kila Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ni 260, ambapo mahakimu Wakazi na Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo 387 wameamua kesi chini ya 100 mwaka jana.


"Ukiondoa wale ambao wameajiriwa karibuni, wanaofanya kazi kwenye mahakama za mwanzo zisizokua na mashauri mengi au waliyokwenda masomoni kati kati ya mwaka au likizo za ujauzito hawatahusika katika sakata la kujieleza.

"Majaji Wafawidhi nimewaagiza wachambue na kuanisha mahakimu wote walioshindwa kufikia kiwango cha kesi walizopaswa kuamua kesi 250 na kesi 260 kwa mwaka jana na kuwataka watoe maelezo ndani ya siku saba kwa nini wasichukuliwe hatua," alisema Jaji Chande

Jaji Chande alitoa muda wa kukamilika kwa mchakato huo, ambapo walizitaka idara husika ndani ya siku 21 kila kitu kiwe kimekamilika ili ijulikane ni hatua gani wanachukuliwe.

Mahakama haikubali hakimu ambaye anabembeleza kesi. Hakimu hatakiwi kufanya hivyo anatakiwa asikilize kesi hizo naazimalize. Haiwezekani katika mahakama moja hakimu mmoja anamaliza kesi 800 mwingine anamalizia chini ya 100 hilo halitakubalika kutokana na kasi ambayo tunayo," alisema


Jaji Chande alisema mahakimu hao watapelekwa katika kamati zao kwa hatua ya kujieleza. Kazi kuu ya kamati hizo ni kupeleleza, kuchunguza na kushughulikia mashtaka yote ya nidhamu ya mahakimu.

"Mahakimu wote walioshindwa kufikia malengo ya mwaka la kesi na kushindwa kutoan sababu za kuridhisha kwa nini wameamua idadi ndogo ya kesi kuliko walivyopaswa, ambapo itashughulikiwa haraka na Kamati za Maadili za Mahyakimu kwa mujibu wa sheria na taratibu za haki," alisema

Hata hivyo, Jaji Chande alitoa pongezi kwa mahakimu ambao wamevuka kiwango, ambapo mahakimu 14 wameamua zaidi ya kesi 700 kwa mwaka jana na mahakimu wengine wamesikiliza kesi 915,789 na 778.

Alisema mkakati wao ni kuanza kesi sifuri mwaka unapoanza, kwa sababu kuna baadhi ya mahakama za mwanzo zimekuwa zikimaliza kesi na kuanza mwaka upya.

Jaji Chande alisema Januari 1, 2015 mahakama za mwanzo zilianza na kesi 34,126 na mwaka huu Januari 1 zilianza na kesi 20,431. Kiwango cha kumaliza kesi ukilinganisha na idadi ya kesi zilizosajiliwa 2015 nni zaidi ya asilimia 100. Mahakama ya Mkuranga asilimia 141, Rufiji asilimia 121 na Bukoba Mjini asilimia 224.


JAJI MKUU OTHUMAN CHANDE ATOA SIKU SABA KWA MAHAKIMU 508 WATOE MAELEZO KWANINI WASIFUNGULIWE MASHITAKA KWA KUFANYA KAZI CHINI YA KIWANGO.

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo mchana , kuhusu utendaji wa mahakimu wa mahakama za hakimu mkazi, mahakama za wilaya na mahakama za mwanzo ambapo alitoa siku saba kwa mahakimu 508 watoe maelezo kwani ni wasifunguliwe mashitaka ya nidhamu na kuwajibishwa kwa kufanya kazi chini ya kiwango. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omari Mallungu na kulia ni Jaji Kiongozi wa Tanzania, Shaban Omari Lila. Jaji Chande alitoa kauli hiyo kwenye maonyesho ya wiki ya Sheria yanayoendelea viwanja vya Mnazi Mmoja.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande, akikaribishwa kutembea mabanda mbalimbali kwenye maonesho hayo.
Mkurugenzi Msaidizi Ukaguzi na Maadili Mahakama ya Tanzania, Warsha Ng'humbu (kushoto), akimuelekeza jambo Balbina Mrosso (kulia), kutoka Babati mkoani Manyara aliyetembelea banda la Idara ya Malalamiko kuomba msaada wa kisheria katika maonyesho hayo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande, akisoma moja ya daftari katika banda la Idara ya Malalamiko kwenye maonyesho hayo. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Malalamiko Mahakama ya Tanzania, Happiness Ndesamburo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande (kulia), akielekezwa jambo katika banda la Divisheni ya Biashara katika maonesho hayo. 

JAJI Mkuu wa Tanzania Othuman Chande ametoa siku saba kwa mahakimu 508 watoe maelezo ni kwanini wasifunguliwe mashtaka ya nidhamu na kuwajibishwa, baada ya kufanya kazi chini ya kiwango.

Jaji Chande ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Mnanzi Mmoja jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Sheria.

Alisema kiwango cha kesi kwa kila Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya ni 250, ambapo Mahakimu Wakazi 121 kwenye mahakama hizo wameamua kesi chini ya 100 mwaka jana.

Alibainisha kuwa kiwango cha kwa kila Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ni 260, ambapo mahakimu Wakazi na Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo 387 wameamua kesi chini ya 100 mwaka jana.


"Ukiondoa wale ambao wameajiriwa karibuni, wanaofanya kazi kwenye mahakama za mwanzo zisizokua na mashauri mengi au waliyokwenda masomoni kati kati ya mwaka au likizo za ujauzito hawatahusika katika sakata la kujieleza.

"Majaji Wafawidhi nimewaagiza wachambue na kuanisha mahakimu wote walioshindwa kufikia kiwango cha kesi walizopaswa kuamua kesi 250 na kesi 260 kwa mwaka jana na kuwataka watoe maelezo ndani ya siku saba kwa nini wasichukuliwe hatua," alisema Jaji Chande

Jaji Chande alitoa muda wa kukamilika kwa mchakato huo, ambapo walizitaka idara husika ndani ya siku 21 kila kitu kiwe kimekamilika ili ijulikane ni hatua gani wanachukuliwe.

"Mahakama haikubali hakimu ambaye anabembeleza kesi. Hakimu hatakiwi kufanya hivyo anatakiwa asikilize kesi hizo naazimalize. Haiwezekani katika mahakama moja hakimu mmoja anamaliza kesi 800 mwingine anamalizia chini ya 100 hilo halitakubalika kutokana na kasi ambayo tunayo," alisema

Jaji Chande alisema mahakimu hao watapelekwa katika kamati zao kwa hatua ya kujieleza. Kazi kuu ya kamati hizo ni kupeleleza, kuchunguza na kushughulikia mashtaka yote ya nidhamu ya mahakimu.

"Mahakimu wote walioshindwa kufikia malengo ya mwaka la kesi na kushindwa kutoan sababu za kuridhisha kwa nini wameamua idadi ndogo ya kesi kuliko walivyopaswa, ambapo itashughulikiwa haraka na Kamati za Maadili za Mahyakimu kwa mujibu wa sheria na taratibu za haki," alisema

Hata hivyo, Jaji Chande alitoa pongezi kwa mahakimu ambao wamevuka kiwango, ambapo mahakimu 14 wameamua zaidi ya kesi 700 kwa mwaka jana na mahakimu wengine wamesikiliza kesi 915,789 na 778.

Alisema mkakati wao ni kuanza kesi sifuri mwaka unapoanza, kwa sababu kuna baadhi ya mahakama za mwanzo zimekuwa zikimaliza kesi na kuanza mwaka upya.

Jaji Chande alisema Januari 1, 2015 mahakama za mwanzo zilianza na kesi 34,126 na mwaka huu Januari 1 zilianza na kesi 20,431. Kiwango cha kumaliza kesi ukilinganisha na idadi ya kesi zilizosajiliwa 2015 nni zaidi ya asilimia 100. Mahakama ya Mkuranga asilimia 141, Rufiji asilimia 121 na Bukoba Mjini asilimia 224.

RAIS DKT. MAGUFULI AMHAMISHA NAIBU KATIBU MKUU KATIBA NA SHERIA KWENDA UTUMISHI NA UTAWALA BORA

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemhamisha Bi. Suzan Paul Mlawi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Manejimenti ya utumishi wa umma na Utawala Bora.


Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imeeleza kuwa uhamisho huo umeanzia tarehe 26 Januari, 2016.


Taarifa hiyo imeeleza kuwa pamoja na shughuli nyingine za Unaibu Katibu Mkuu, Bi. Suzan Paul Mlawi, atashughulikia eneo la Utawala Bora.

Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria iliyoachwa wazi, haitajazwa kwa sasa.


Gerson Msigwa,

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.

Dar es salaam.


01 Februari, 2016.

Walemavu: Msama anajitambua

$
0
0
BAADHI ya walemavu hapa nchini  wametoa wito kwa Watanzania wengine kujitambua kuhusu Mungu na mikakati mbalimbali ya kimaendeleo katika jamii ikiwa ni kuelekea Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Machi 27 jijini Mwanza.

Akizungumza jana kwa niaba ya Esperance Wetewabo ambaye ni mlemavu wa mikono na mguu, mchungaji wa Godfrey Rubanzibwa 'Punda  wa Yesu' alisema jamii inatakiwa kujitambua kuhusu Mungu kama alivyo Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama anavyotekeleza majukumu yake katika muziki huo.

Punda wa Yesu alisema Msama amejitambua ndio maana anashirikisha kada mbalimbali katika jamii kuelekea Tamasha la Pasaka ambalo lina mafunzo mengi kwa jamii.

Punda wa Yesu alisema katika tamasha lake Msama anashirikisha waimbaji chipukizi, walemavu na wengineo ambao wanabeba dhana ya tamasha hilo ambalo dhamira yake ni kumuimbia na kumtukuza Mungu.
"Msama anajitambua waimbaji chipukizi na viongozi wa dini mbalimbali wanaohudhuria tamasha hilo, ivyo wengine nao waige mfano huo," alisema Punda wa Yesu.

Naye Honoratha Michael alitoa wito kwa Watanzania kujiandaa vilivyo na tamasha la Pasaka ambako pia alitoa wito kwa jamii kujitokeza kuwasaidia walemavu kama anavyofanya Msama.

Honoratha aliumia fursa hiyo kuwapa usia Watanzania wote wakiwemo walemavu kuiga mfano wa Msama ambaye anatekeleza majukumu hayo.

Serikali yapanga kufanya matumizi yenye tija

$
0
0
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Serikali katika mwaka wa fedha 2016/2017 imejipanga kufanya matumizi yeneye tija kwa kuelekeza bajeti kubwa kwenye mambo muhimu hasa sekta zenye za kutoa huduma na zile zenye kuleta maendeleo ya nchi moja kwa moja.
 
Akiwasilisha mwongozo wa kuandaa mapango na bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Phillip Mpango amesema mwongozo wa  mpango na bajeti umezingatia mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/2017 pamoja na kuzingatia sera za uchumi na hadi sasa sera za bajeti kwa  mwaka 2016/2017 zinaonesha jumla ya shilling trillion 22.9 zinatarajiwa kukusanywa na kutumika katika kipindi hiki.
 
“ Kati ya mapato hayo,serikali inalenga kukusanya mapato ya kodi ya jumla ya shillingi trillion 14.1 sawa na ongezeko la asilimia 14.1 ikilinganishwa na makadirio ya mwaka 20015/2016, na kwa mapato yasisiyo ya kodi na mapato kutoka vyanzo vya Halmashauri ni shilling trillion 1.1.
 
“ katika mwaka wa fedha 2016/2017,Serikali tunatarajia kukusanya jumla ya shilling trilllioni 14.1 kutoka kwenye vyanzo vya kodi ,sawa na asilimia 13.2 ya pato la taifa hii ni sawa na ongezeko la asilimia 14 ukilinganisha na matarajio ya kukusanya jumla ya shilling trillion 12.3 kwa mwaka wa fedha 2015/2016” Alisema Mhe. Mpango.
 
Mhe Philip Mpango amesema mapato yote yatakusanywa na Wizara ya Fedha na Mipango, hivyo basi maafisa,Masuuli,wa Wizara,idara za serikali,Wakala,Taasisi,Sekretarieti za Mikoa, na Mamlaka za Serikali za Mitaa watatakiwa kuwasilisha mapato yote yatakayokusanywa na kuwasilisha kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali na yatagawiwa kulingana na bajeti iliyoidhinishwa.
Aidha amesema Serikali itahakikisha Mashirika ya Umma yaliyoundwa kwa lengo la kujiendesha kibiashara yanajiendesha kwa faida bila ya kutegemea ruzuku ya Serikali, na ameyataja baadhi ya mashirika hayo kuwa ni  Shirika la Umeme(TANESCO),Shirika la Reli ya Tanzania Zambia (TAZARA), Shirika la Reli ya Kati (TRL), Shirika la Ndege (ATCL),Wakala wa Vipimo (WMA), Bodi ya Mazao, na mashirika mengine.
 
Serikali itahakikisha kuwa inahimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuelekeza matumizi kwenye maeneo yenye tija kwa manufaa ya watanzania wote.

BALOZI WA SWEDEN AMTEMBELEA SPIKA OFISINI KWAKE

$
0
0
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akiwa katika picha ya pmoja na Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnitt na Maafisa wengine wa Ubalozi wa Sweden na wa Bunge
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akiaagana na Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnitt mara baada ya kuzungumza anye ofisini kwake. Kulia ni Afisa wa Ubalozi wa Sweden Bw. Ludvig Bontell.
Katibu wa Jukwaa la Wahariri Bw Neville Meena akifafanua jambo kwa Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah wakati alipomtembele Ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo. Kuli kwa Spika ni Naibu Katibu wa Bunge-Shughuli za Bunge Bw. John Joel.Wengine katika picha ni Viongozi wa Jukwaa la Wahiri na Maafisa wa Bunge.(Picha na Ofisi ya Bunge)
Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnitt akisaini kitabu cha Wageni alipomtembelea leo ofisini kwake tarehe 01 Febuari, 2016 Mjini Dodoma. Kulia kwake ni Afisa wa Ubalozi wa Sweden Bw. Ludvig Bontell.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnittaliyemtembelea leo Ofisni kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akifanunua jambo wakati akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnitt. Wengine katika picha ni maafisa wa Ubalozi wa Sweden na Wabunge.

BENKI YA CRDB YAWATOA HOFU WANANCHI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu serikali kuhamishia akaunti zote za mapato Benki Kuu. Kulia ni Mkurugenzi wa Hazina wa Benki ya CRDB, Alex Ngusaru na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa (kushoto) akizungumza katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa (kushoto), Mkurugenzi wa Hazina wa Benki ya CRDB, Alex Ngusaru na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya CRDB, Philip Alfred wakiwa katika mkutano huo.

SIKU moja baada ya Serikali kutangaza kuchukua hatua za kupunguza riba za mabenki kwa wananchi kwa kuagiza akaunti za mashirika na taasisi zake katika mabenki ya kibiashara zifungwe na kuhamisha fedha zilizopo katika akaunti hizo kwenda Benki Kuu ya Tanzania (BoT), benki ya CRDB imeunga mkono hatua hiyo.

Pia benki hiyo imewataka wananchi wasiwe na hofu juu ya mpango huo, kutokana na hofu iliyojengeka kwamba kuna hatari benki za kibiashara kufilisika nchini.Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei alisema uamuzi uliofanywa na Serikali utasaidia kukuza uchumi pamoja na kutambua fedha zake mahali zilipo.

Alisema Serikali ina haki na nia njema kwa kutaka akaunti hizo zifunguliwe BoT kwa kuwa zimekuwa zikifunguliwa kwenye mabenki makubwa ya kibiashara, huku baadhi ya Wakala wa ukusanyaji wa fedha wakishindwa kuzifikisha serikali kama inavyotakiwa.

Pia alieleza kuwa mfumo huo hauna utofauti na awali kwani utofauti utakuwepo kutokana na mashirika na taasisi kufungua akaunti BoT, ambapo lengo kubwa ni walaka wa Hazina kulenga kuboresha mapato ya serikali ammbayo yanaweza kutumiwa kwa namna mbalimbali.

“Mfumo huu…utakuwa hauna tofauti na ilivyo sasa kwa kuwa fedha zitakazokuwa zikiingizwa kwenye akaunti hizo ni zile zilizokuwa zikiingizwa kwenye benki awali, ili kupunguza kiwango cha riba,”alisema.

Pia alisema hofu nyingine inayojengeka kwa wananchi inatokana na mfumo huo kutotumiwa kwa muda mrefu na BoT, licha ya kuwa kuna baadhi ya nchi inatumia mfumo huo na hakuna madhara yoyote.

“Hivyo tunafikiri maamuzi hayo hayana athari zozote kwani nchi mbalimbali zimekuwa zikitumia mfumo huo ikiwemo Uganda, Rwanda na Kenya ila kwa kwetu unaonekana mgeni kutokana na kutotumika kwa muda mrefu,”alisema.

Pia Dk.Kimei kuwa kutokana na uwepo wa mfumo huo benki za kibiashara zitawakopesha zaidi sekta binafsi, ikiwa tofauti na malalamiko ya mwanzo kwamba Serikali inapata manufaa kutokana na kukopeshwa zaidi.

“Hii itasaidia hata wananchi wa kiwango cha chini kuchukua mikopo kutokana na riba kuwa ndogo, ambapo hata wananchi wa chini wataweza kuchukua mkopo, ikiwa tofauti na awali wananchi wanashindwa kuchukua mikopo kutokana na riba kuonekaa kuwa juu zaidi ya asilimia 10,”alisema.

Mbali na hilo, pia Kimei alisema endapo riba ikiwa inapungua itasaidia kukuza uchumi kutokana na wananchi wengi wa hali ya chini kuchukua mikopo.

Wanafunzi waliowahi kusoma miaka ya 80 katika Shule ya Sekondari ya Hegongo wakutana

$
0
0
 Wanafunzi waliowahi kusoma miaka ya 80 katika Shule ya Sekondari ya Hegongo, Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga, wakicheza muziki wakati wa hafla yao ya kukumbukana iliyofanyika kwenye Mgahawa wa City Sports Lounge, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Martine Jengo (kulia) na Mzee Hassan wakiserebuka
 Mmiliki wa TSN Group, Farouq Baghoza (kulia), ambaye pia alisoma katika shule hiyo, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kumbukumbu.
 Mmiliki TSN Group,  Farouq Baghoza (kulia) akiwa na wanafunzi aliosoma nao katika shule ya Hegongo,  Mkurugenzi wa Mgahawa wa City Sports Lounge, Benny Kisaka (kushoto) pamoja na Gerald Yambi ambaye ni mwanachama maarufu Kundi la  Friends of Simba. Baghoza aliwahi pia kuwa Mwenyekiti wa Saidia Taifa Stars Ishinde.
 Mwanafunzi Edwin Pemba (kushoto) akiwa na Mwalimu John Sebo (katikati) aliyewahi fundisha katika Shule ye Sekondari ya Hegongo.

UTT AMIS YATOA ELIMU YA UWEKEZAJI WA PAMOJA KWA WABUNGE

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa UTT AMIS Dk. Charles Kibola (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Idara ya Masoko ya Kampuni hiyo kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma, mwishoni mwa wiki.
Ofisa Masoko Mwandamizi wa UTT AMIS, Martha Mashiku (katikati) akitoa elimu juu ya Uwekezaji wa Pamoja kutoka Kampuni ya UTT AMIS. 
Baadhi ya wabunge na wafanyakazi wa bunge wakipata elimu juu ya Uwekezaji wa Pamoja kutoka Kampuni ya UTT AMIS.

RAIS MHE. DKT MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JAJI DAMIAN LUBUVA

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Bw. Ramadhan Kailima.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU. 


MPANGO WA KUSAIDIA KAYA MASIKINI WANUFAISHA KAYA MILIONI 1.1 NCHINI

$
0
0
Mpango wa Kijamii wa Uzalishaji Salama ili kusaidia kaya masikini kupambana na umasikini (PSSN) umefanikiwa kuwa na matokeo mazuri kwa kusaidia kaya Milioni 1.1 nchini na kusaidia juhudi za serikali kupambana na umasikini.

Hayo yamefahamika wakati washirika wa maendeleo ambao ni Umoja wa Mataifa, Benki Kuu ya Dunia, Serikali ya Uingereza kupitia kitengo cha Maendeleo ya Kimataifa, Irish Aid, USAID, Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Sweden (SIDA) walipotembelea miradi ya maendeleo katika wilaya za Unguja, Chamwino, Babati, Sumbawanga (Manispaa na Wilaya), Singida na Hanang kwa kipindi cha siku tatu kuanzia Januari, 19 hadi 22.
Bi. Kazijya Kila ambaye ni mmoja wa wanufaikaji wa fedha akitoa ushuhuda kuhusu mradi wake wa chakula ulivyowezeshwa na TASAF ambapo hadi hivi sasa anatengeneza faida ya Shilingi 7000 kwa siku na kabla ya kuwezeshwa alikuwa akikaa nyumbani na mama yake bila kuingiza kipato chochote.

Katika Mpango huo ambao utekelezwaji wake unasimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) unafanyika Tanzania Bara na Tanzania visiwani ukiwa na lengo la kuzisaidia kaya masikini pesa za matumizi ili kukidhi mahitaji ya kupata chakula pamoja na kuwawezesha kusaidia watoto wao kupata elimu jambo ambalo linaonekana kuzaa matunda kwa maeneo mengi ikiwepo Tanzania visiwani.

Serikali ya Tanzania imekuwa ikisaidia na washirika wa maendeleo ili kupunguza umaskini uliokithiri kwa wananchi wake na mwaka 2013 iliweka mpango wa kusaidia kaya masikini 275,000 kwa kipindi cha miaka mitano na tangu ianzishe mpango huo ilifanikiwa kusaidia kaya 275,000 kwa mwaka 2013 pekee katika wilaya nane nchini.
Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Jamii kutoka Benki ya Dunia, Bw. Muderis Abdulahi Mohamed (kushoto) na Msimamizi wa mpango wa PSSN, Bw. Ramadhani Madari wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu kwa wanufaikaji wa fedha hizo.

Na mpaka kufikia sasa mpango huo umeshatoa malipo mara 12 na jumla ya kaya masikini milioni 1.1 zimeshafaidika na mpango huo ikiwa ni kwa wilaya 161 na vijiji 9789 nchini.

Malengo ya serikali ya Tanzania na mashirika ya kimataifa ni kuhakikisha kufikia mwaka 2030 kunakuwa hakuna masikini hivyo ni wajibu wa kila nchi kuhakikisha inawasaidia wananchi wake ili wajijengee uwezo wa kujitegemea na kuondoka katika janga la umasikini.
Asilimia kubwa ya wanufaikaji wa mpango huo ni wanawake, kama wanavyoonekana pichani.
Mkurugenzi wa Huduma za jamii kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Amadeus Kamagenge akizungumza na wanufaikaji wa mpango wa TASAF (hawapo pichani).
Mkurugenzi wa Huduma za jamii kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Amadeus Kamagenge (kushoto) akifurahi jambo na Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Jamii kutoka Benki ya Dunia, Bw. Muderis Abdulahi Mohamed.
Timu ya TASAF na wadau wa maendeleo wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri katika mkutano huo.
Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Jamii kutoka Benki ya Dunia, Bw. Muderis Abdulahi Mohamed na Aine Mushi wa UN/NRA.
Bi Jabo Omari Othman akiwa kwenye shamba lake alilonunua kutokana na fedha za TASAF visiwani Unguja.

MADEREVA DALADALA JIJINI MWANZA WATISHIA KUGOMA IKIWA MAJIPU YA TAX BUBU HAYATATUMBULIWA.

$
0
0
Ridhione Senga (wa pili kushoto) ambae ni Mwenyekiti wa Madereva wa Daladala wanaofanya shughuli zao katika barabara ya Bugarika-Mzunguko Jijini Mwanza, jana akilalamikia suala la uwepo wa tax bubu linalowasumbua katika shughuli zao.

Alisema licha ya madereva wa tax bubu wanaobeba abiria kama daladala katika eneo wanalofanyia kazi hususani kubeba abiria wanaoenda na kutoka katika hospitali ya Rufaa ya Bugando kuzuiliwa, bado madereva hao wa tax bubu wameendelea na biashara hiyo kama kawaida.

Senga alibainisha kwamba hatua hiyo inawaweka katika wakati mgumu katika kutimiza majukumu yao kutokana na kupata hasara kila kukicha ambapo amesema ikiwa itaendelea wataitisha mgomo ili kushinikiza kilio chao kufanyiwa kazi.

"Sisi tunalipa mapato, lakini jambo la ajabu hawa madereva wa tax bubu ambao hawana leseni ya kubeba abiria wamekuwa ndio wanafanya kazi ya daladala licha ya kupigwa marufuku katika kikao tulichokaa ijumaa iliyopita baina ya Sumatra, halmashauri ya Jiji, Polisi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza pamoja na wawakilishi wengine bila kuwasahau viongozi wa daladala na tax. Kama hali hii itaendelea tutafanya mgomo hapa na hakuna huduma yoyote ya kubeba abiria itakayotolewa".Alisema Senga.

Ramadhan Idd ambae ni Kaimu Mwenyekiti wa Madereva wa daladala za Bugarika-Muzunguko Jijini Mwanza aliunga mkono hoja ya mwenyekiti huyo na kusema kuwa ikiwa mamlaka husika zitashindwa kutatua suala la tax bubu katika eneo hilo, wao watachukua hatua ya kusitisha huduma ya usafirishaji katika barabara hiyo ya Bugarika-Buzuruga.

"Hizi tax bubu tunasikia ni za wakubwa na ndiyo maana hawa madereva wanaoziendesha wana jeuri mno. Sisi tunasema haya ni majipu na tunawaomba viongozi wengine wakubwa akiwemo Mhe.Magufuli, waangalie huku Jijini Mwanza maana kuna majipu makubwa ya kutumbua".Alisema Athuman Bin Malick ambae ni mmoja wa madereva wa daladala za Bugarika-Mzunguko Jijini Mwanza.

Kaptaini Michael Rogers ambae ni Afisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoani Mwanza, ameshauri suala hilo kutatuliwa na jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kuwa ndilo lenye jukumu la kukamata vyombo vya usafiri vinavyofanya kazi kwa kukiuka sheria na taratibu zilizoweka na mamlaka husika ikiwemo halmashauri ya Jiji Mwanza ambayo ndiyo inasimamia taratibu la utendaji kazi wa tax.

Juhudi za kuwatafuta madereva wa tax hizo zinazodaiwa kufanya kazi kinyume cha sheria (tax bubu) bado zinaendelea ili kujua kuzungumzia malalamiko yanayowakabiri.
Ramadhan Idd ambae ni Kaimu Mwenyekiti wa Madereva wa daladala za Bugarika-Muzunguko akitoa malalamiko yake.
Athuman Bin Malick ambae ni mmoja wa madereva wa daladala za Bugarika-Mzunguko Jijini Mwanza.
Kulia ni Kaptaini Michael Rogers ambae ni Afisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoani Mwanza akitoa ufafanuzi wake.Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo

Benki ya Exim yatangaza kupata ongezeko la faida ya asilimia 46

$
0
0
Afisa Mkuu wa Fedha wa benki ya Exim Tanzania Bw. Selemani Ponda (katikati) akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati akitoa taarifa ya mapato ya benki hiyo katika kipindi cha mwaka uliopita. Wengine ni NaibuAfisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Bw. Issa Hamisi (kulia) na Mkaguzi Mkuu wa ndani wa hesabu za benki hiyo Bw. George Binde


BENKI ya Exim Tanzania imetangaza kupata faida ya sh. bilioni 35.3 (kabla ya kodi) kwa mwaka ulioipita 2015, sawa na ongezeko la faida kwa asilimia 46 ikilinganishwa na mwaka 2014 hatua iliyochagizwa  na ufanisi wa benki hiyo katika usimamizi mizania.

 “Kwa kuangalia hali halisi ya changamoto mbalimbali katika masuala ya kifedha ikiwemo masuala ya riba sambamba na kuporomoka kwa thamani ya shilingi kwa muda wote, mafanikio haya tunayaona kuwa ya kuridhisha,’’ alisema Afisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Bw Selemani Ponda alipokuwa akitoa ripoti  ya awali (kabla ya ukaguzi) ya benki hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

Alisema katika kipindi hicho faida kwenye riba ilikuwa kwa asilimia 28 na kufika sh. Bilioni 73 ikilinganishwa na kiasi cha sh. 57 kilichopatikana katika kipindi kama hicho kwa mwaka uliopita. Ongezeko hilo limechagizwa na mkazo wa benki hiyo katika amana za gharama nafuu, wingi wa matawi ya benki hiyo pamoja na usimamizi mzuri wa mizania.

Zaidi, tozo mbalimbali za huduma za kibenki katika kipindi cha mwaka ulioipita kiliongezeka kwa asilimia 25 hadi kufikia sh bilioni 50, kutoka sh bilioni 40 kilichopatikana mwaka uliopita.Ongezeko hilo pia lilichagizwa na  faida katika biashara ya kununua na kuuza fedha za kigeni pamoja na mapato mengine ya ada kutokana na ufanisi katika utoaji huduma kwa wateja wakubwa na wale wa kati.

Jumla ya mapato yatokanayo na uendeshaji yaliongezeka kwa asilimia 29 hadi kufikia sh. Bilioni 95 yakibebwa na ukuaji mkubwa kwenye ada pamoja na kamisheni ambayo ilikuwa asilimia 29 kutoka sh bilioni 24 hadi sh. Bilioni 31 kwa mujibu wa Bw Ponda huku akiongeza kuwa katika kipindi hicho gharama za uendeshaji wa benki hiyo zilikuwa kwa asilimia 20 na kufikia sh. Bilioni 80.

Benki tanzu zilizopo nje nchini Djibouti na Comoro zimeendelea kufanya vizuri na kuchangia asilimia 4 ya faida tofauti na mwaka jana zilileta hasara kwa ujumla wao. Djibouti imefanya vizuri kulinganisha na mwaka uliopita kwa kupata faida ya Sh bilioni 1.2. “Tunategemea benki hizi tanzu kufanya vizuri zaidi mwaka 2016” aliongeza  mkuu huyo wa fedha.

Bw Ponda aliongeza kwamba katika kujiongezea mtaji wa biashara na ushirikishaji wa wawekezaji wote nchini (financial inclusion), benki hiyo hivi karibuni ilizindua uuzaji wa dhamana za muda mrefu (hati fungani) ambapo hadi uuzwaji wa hati hizo unafungwa rasmi Disemba 18 mwaka 2015 benki hiyo ilikuwa imefanikiwa kukusanya kiasi cha sh bilioni 19.7 kutokana na mauzo ya hati hizo tofauti na makadirio ya sh. Bilioni 10 iliyokuwa imejipangia kukusanya hapo awali. Benki ya Exim imekuwa taasisi ya kwanza kuzindua dhamana ya muda mrefu ikilenga wawekezaji wadogo, wakati na wakubwa.

“Pia ni katika mwaka uliopita tumezindua kituo chetu kipya cha  huduma  kwa wateja kwa njia ya mawasiliano ya simu ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha huduma zetu kupitia teknolojia ya mawasiliano,’’

“Exim tunaahidi kuendelea na muelekeo huu ulio sahihi kwetu na kwa wateja wetu  katika kutimiza malengo yetu. Ripoti hii inaonyesha kuwa mwaka uliopita ulikuwa na mafanikio makubwa na ya kujivunia,’’ alisema Bw Ponda huku akiwapongeza wafanyakazi na wadau wote waliochangia mafanikio hayo. 

HAPPY BIRTHDAY SALEH ALLY, MHARIRI KIONGOZI WA MAGAZETI YA CHAMPIONI

$
0
0

Leo ni siku ya kuzaliwa ya Saleh Ally, mchambuzi na mwandishi mkongwe wa michezo nchini Tanzania ambaye kwa sasa ni Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi yanayomilikiwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd na Mmiliki wa Blog  ya Saleh Jembe.


Saleh Ally amefanya mengi katika ulimwengu wa michezo na burudani ambapo amesharipoti michuano mbalimbali mikubwa ikiwemo Kombe la Dunia na pia amesafiri katika nchi nyingi za mabara tofauti akifanya kazi hiyo.

Kazi zake nyingi nzuri zimekuwa hamasa kwa waandishi wengi ambapo amekuwa kioo ‘role model’ kwa wengi wao. Tunamtakia kila la kheri katika maisha yake yote na Mungu ampe baraka nyingi.

Happy birthday Saleh Ally

WITO UMETOLEWA KWA WAMILIKI WA SILAHA KUHAKIKI SILAHA ZAO KWA WAKATI

$
0
0
Pichani :Kamanda Liberatus Sabas, alipokuwa akifunga Kampeni za ABIRIA PAZA SAUTI, Jijini Arusha, 


Na Vero Ignatus wa Wazalendo 25 Blog, Arusha.

Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limewataka watu wote wanaomiliki silaha kwa njia halali wafike kwenye kituo cha polisi kuhakiki silaha zao na kuzilipia kama inavyostahili na kwa kufuata utaratibu kama sheria inavyoagiza. 

Hayo ya mesemwa Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas, kwamba kila mwaka huwa kila mwenye silaha anafika polisi na silaha yake na vitabu vyake kwaajili ya kuihahiki na kuilipia kama inavyostahili ,na kama zipo tuhuma zozote kutokana na matumizi ya silaha, itasimamishwa kwaajili ya taratibu zingine na kunyang’anywa hadi hapo jeshi litakapojiridhisha kuwa silaha hiyo matumizi yake ni sahihi ama siyo sahihi Kamanda amesema utaratibu huu huwa unaratibiwa na makao makuu ya jeshi la polisi kwaajili ya kuhakiki silaha ,ikiwa ni pamoja na kulipia mapato ya serikali ,amewataka watu wanaomiliki silaha wafuate masharti yake kama inavyotakiwa, nawakumbuke sheria inambana kila mtu mara anapotenda kosa ,na kama mtu akiitumia ndivyosivyo atanyang’anywa silaha kwa kutumia sheria iliyowekwa. 

Ameongeza kuwa wapo watu ambao wamewatishia silaha wenzao,na wengine kesi zao zipo tayari na zingine zimefutiwa umiliki kwa mujibu wa sheria, amesema kimsingi kabla mtu hajakabidhiwa silaha ili amiliki, yapo masharti yakufuata na yapo kwenye kitabu kile cha leseni anachopewa wakati wa umiliki, amesema kuwa ukitoka nje ya hayo masharti huna sifa ya kumiliki silaha. 

Kamanda Sabas ametoa anagalizo kwa wamiliki wa silaha na kusema kuwu silaha ya moto siyo kama panga,silaha hiyo ukiifanyia kosa mara moja yaweza kuua mtu au watu hivyo amewataka kuwa makini sana katika ufuatiliaji wa umiliki, pamoja na namna zinavyotunzwa,amesema jeshi la polisi lipo makini kufuatilia kwa ukaribu wakithibitisha silaha haitunzwi kama inavyostahili utanyang’anywa.aidha amesema kwa wazee amabao umri wao umeenda nab ado wanamiliki silaha huwa wanaichukua na kuihifadhi . 

Amehitimisha kwa kusema kuwa kila , mtu amnayetaka kumiliki silaha, kamati za ulinzi na usalama kuanzia kwenye kata ,Wilaya, Mkoa wakamuidhinisha kuwa na silaha afuate masharti na kuitunza silaha isije ikaangukia kwenye mikono ya wahalifu wakaitumia isivyo halali sheria itafuata mkondo wake, Silaha huwa zinatakiwa kulipiwa kila mwaka kuanzia mwezi julai hadi septemba ukichelewa kulipia unapigwa penati kwa mujibu wa sheria.

WASANII WATAKIWA KUKATAA RUSHWA KWENYE KAZI ZAO

$
0
0
 Msanii mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Star Mayunga Malini (Kulia) akiongea na wadau wa Sanaa (hawako pichani) mapema wiki hii kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA). Wengine katika picha ni Afisa Habari wa BASATA, Aristides Kwizela (Katikati) na Afisa Sanaa wa Baraza hilo Augustino Makame.
 Msanii Mayunga Malimi akiimba wimbo wake wa Nice Couple sambamba na mkongwe wa muziki wa dansi nchini Kassim Mapili kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa mapema wiki hii.
 Msanii mkongwe wa Sanaa za Maonesho Nkwama Ballanga akimpongeza Msanii Mayunga kwa juhudi zake na kujituma katika kazi anazofanya. Wadau wengi wa Sanaa waliohudhuria kwenye programu ya Jukwaa wiki hii walifurahishwa na juhudi binafsi za Msanii Mayunga.
Sehemu ya wadau wa Sanaa waliohudhuria programu ya Jukwaa la Sanaa wakimfuatilia kwa makini Msanii Mayunga.  


WASANII WATAKIWA KUKATAA RUSHWA KWENYE KAZI ZAO
Wasanii nchini wametakiwa kujituma na kutengeneza kazi za Sanaa zenye ubora na kuachana na dhana ya kutegemea rushwa na hongo katika kuyafikia mafanikio yao kisanaa.
Wito huo umetolewa mapema wiki hii na wadau wa Sanaa kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa ambayo huandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kufanyika kwa mwezi mara mbili siku ya Jumatatu kwenye ukumbi wa Baraza hilo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau hao walisema kwamba kumekuwa na wimbi la wasanii na mameneja wa wasanii kutegemea rushwa za fedha na wengine kufikia hatua kutoa rushwa za ngono ili kufanikiwa kisanaa hasa katika kuvishawishi vituo vya radio na televisheni kucheza nyimbo zao.
“Ukweli ni kuwa rushwa na hongo zinaendekezwa na wasanii walioshindwa. Msanii anayejitambua hawezi kutoa rushwa ili wimbo wake uchezwe. Lazima wasanii waachane na dhana hii potofu, waelewe kwamba kazi ya Sanaa iliyo bora itapendwa tu na kukubalika na jamii” alisema Nkwama Bhallanga ambaye ni Msanii wa Sanaa za Maonesho.
Kwa upande wake Katibu wa chama cha wachezesha disko (TDMA) Asanterrabi Mtaki alisema kuwa dhana kwamba wasanii lazima wahonge watangazaji au ma DJs ili nyimbo zao zichezwe ni potofu na ni chanzo cha kutangaza muziki au kazi za Sanaa zisizo bora na kuziacha zile zenye ubora.
“Kama wimbo wako ni mzuri kwa nini uhonge au utoe rushwa ili uchezwe? Hapa ndipo tatizo la kuendekeza kazi mbovu za Sanaa linapoanzia. Muziki wa wenye fedha na wanaohonga ndiyo unasikika, ule mzuri unaondaliwa na wasanii wasiyo na uwezo haupati nafasi” alisema Mtaki.
Alitoa wito kwa wasanii kufikiria njia mbadala za kutangaza nyimbo zao hasa kumbi za disko badala ya kutegemea vituo vya radio pekee.
Awali akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa, Msanii na mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Star Mayunga Malini alisema kuwa wasanii hawana budi kujituma, kutafuta fursa na kuzitumia ipasavyo hasa kwa kutumia muda mwingi kubuni kazi zenye ubora.
Aliongeza kuwa, wasanii hawana budi kuachana na dhana ya utegemezi na kutegemea fedha na hongo katika kupata mafanikio kwani kazi za Sanaa zikitengenezwa kwa ubora na kwa kuzingatia vigezo vyote zitapendwa na kutuzwa tu.

AIRTEL YAZIDI KUBORESHA VIFURUSHI VYA AIRTEL YATOSHA YAZIDI.

$
0
0
Meneja Masoko wa Airtel Bi Anethy Muga akionyesha moja ya tangazo la ongezeko la muda wa masaa ya vifurushi vya Airtel yatosha wakati wa kutangaza muda mpya wa kuisha kwa vifurushi vya Airtel yatosha kwa siku kuwa ni masaa 25. Yaani masaa 24 ya siku ongeza saa moja.

· Wateja wa Airtel waongezewa muda kufaidi zaidi katika vifurushi vya Airtel Yatosha

AIRTEL Tanzania imeendelea kutimiza dhamira yake ya kujali wateja wake kwa kuboresha vifurushi vyake vya huduma ya Airtel Yatosha hivyo kuvifanya kuwa bora, vya ushindani na gharama nafuu nchini.

Akiongea kuhusu kuboreshwa kwa huduma hiyo, Meneja Masoko wa Airtel Bi, Aneth Muga alisema "huduma yetu ya Airtel Yatosha inaendelea kukidhi mahitaji ya Wateja wetu kwani vifurushi tunavyotoa sasa vya Airtel Yatosha vya siku kwa shilingi 500 tumeongeza muda wake wa kutumika zaidi ukilinganisha na vifurushi vingine vinavyotolewa sokoni

Bi. Muga alisema sambamba na hili vifurushi vya Airtel Yatosha vinamuwezesha mteja kupiga simu kwenda mtandao wowote ule nchini wakati wowote masaa 25 yaani mteja anafaidika na vifurushi hivi kwa masaa 24 na 1 la nyongeza.

Kikubwa na kizuri zaidi bado pia mteja anapojiunga na vifurushi hivi anapata nafasi ya kuingia kwenye droo ya promosheni yetu kabambe ya Airtel Mkwanjika na kujishindia pesa taslimu hadi sh. Milioni moja"


Kujiunga na vifurushi mbalimbali vya Airtel yatosha mteja anatakiwa kupiga *149*99# na kisha kuchagua kifurushi kinachokithi mahitaji yake. Airtel yatosha inapatikana katika vifurushi vya siku, wiki au mwezi.

MPANGO WA TASAF AWAMU YA TATU KUBORESHWA.

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Angella Kairuk akijibu maswali toka kwa wabunge katika kikao cha 6 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
 Picha na raymond Mushumbusi MAELEZO.

(Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO)
SERIKALI imejipanga kuborsha zaidi mpango wa kunusuru Kaya masikini nchi ujulikanao kama TASAF kwa awamu ya tatu kwa kutengeneza miundombinu mizuri ya kutambua Kaya zinazolengwa na kuondoa malalamiko ya wananchi kuwa mpango huu umekuwa ni wa Kaya chache na fedha hizo utolewa kwa upendeleo.

Akijibu swali la Mhe.Magdalena Hamisi Sakaya Mbunge wa Kaliua (CUF) lililouliza ni vigezo gani vinatumika kuondoa Kaya zilizopendekezwa kwenye mradi na kubakiza Kaya chache, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki amesema mpango wa kunusuru Kaya maskini hutambulishwa kijijini na wataalam kutoka Halmashauri husika kwa kusimamiwa na uongozi wa kijiji kisha kuweka vigezo vya Kaya maskini.

“ Wakusanya taarifa huchaguliwa kutoka miongoni mwa vijana wanaoishi kijijini hapo na kupitia nyumba kwa nyumba kuorodhesha Kaya ambazo zinakidhi vigezo vilivyoanishwa na mkutano wa Kijiji ila bado kuna malalamiko yanayotolewa kuwa Kaya maskini zinaachwa na kupewa Kaya nyingine ambazo sio maskini kwa kuliona tatizo hilo suala hili tunalifanyia uchunguzi na tunaomba watu watoe taarifa ikiwa wataona ukiukwaji wa uorodheshaji wa Kaya zitakazohusika na mpango huu ili hatua ziweze kuchukuliwa dhidi ya yoyote atakaye bainika kufanya hivyo”

“ Mpaka sasa kutokana malalamiko yaliyojitokeza katika kuorodhesha Kaya maskini zinazotakiwa kuwezeshwa na mpango huu tumewaajibisha watendaji toka Wilaya za Karagwe, Kagera na Kibondo, Kigoma na tuomba kupewa taarifa kwa sehemu yoyote ambapo kutatokea tatizo kama hili na tutachukua hatua mara moja kuokoa fedha zilizotakiwa kwenda kusaidia watu husika” Alisema Mhe Angella Kairuki.

Aidha Mhe. Angella Kairuki ameongeza kuwa kuna taarifa zinazoenezwa kuwa fedha za mpango wa TASAF Awamu ya Tatu ni fedha za freemasons, taarifa hizo sio za kweli kwani fedha hizi zizantolewa na Serikali ili kusaidia Kaya maskini ili ziweze kujikwamua kiuchumi kwa kuweza kupata Elimu Malazi na chakula bora.


TASAF ni mpango wa kunusuru Kaya maskini na imekuwa katika awamu tatu mpaka hadi sasa kwa ajili ya kuwezesha Kaya maskini kujikwamua kiuchumi.

WAZEE WAWILI WAUAWA KIKATILI MKOANI MBEYA KUTOKANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA.

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

“PRESS RELEASE” TAREHE 02.02.2016.
· WAZEE WAWILI WAMEUAWA KIKATILI WILAYANI KYELA MKOANI MBEYA KUTOKANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA.

· MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MAPAMBANO JIJINI MBEYA AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI.

· MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA GARI KUGONGANA NA PIKIPIKI.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:
WAZEE WAWILI WAKAZI WA KITONGOJI CHA BULINDA WILAYA YA KYELA MKOANI MBEYA WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. GENELI KAPWELA [65] NA 2. RAHABU BUNGULU [70] WALIUAWA KWA KUKATWA NA VITU VYENYE NCHA KALI SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO NA KISHA KUCHOMWA MOTO NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI.

MIILI YA MAREHEMU ILIKUTWA KATIKA NYUMBA WALIMOKUWA WAKIISHI MNAMO TAREHE 01.01.2016 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI HUKO KITONGOJI CHA BULINDA, KIJIJI/KATA YA MATEMA, TARAFA YA NTEMBELA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA.

KATIKA TUKIO HILO, GENELI KAPWELA ALIUAWA KWA KUTENGANISHWA KICHWA NA KIWILIWILI NA KUKATWA MKONO WA KUSHOTO NA VIUNGO HIVYO HADI SASA HAVIJULIKANI VILIPO NA RAHABU BUNGULU ALIUAWA KWA KUCHOMA NA KITU CHENYE NCHA KALI NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI.

INADAIWA KUWA, WANANCHI HAO WALIVAMIA NYUMBA WALIYOKUWA WAKIISHI MAREHEMU KISHA KUWAKATA NA VITU VYENYE NCHA KALI NA BAADA YA KUTEKELEZA MAUAJI HAYO, WATU HAO WALIANGUSHA NYUMBA WALIYOKUWA WAKIISHA AMBAYO ILIKUWA IMEJENGWA KWA MIANZI NA KISHA KUICHOMA MOTO.

CHANZO CHA TUKIO HILO NI IMANI ZA KISHIRIKINA KWANI MAREHEMU WALIKUWA WANATUHUMIWA KULETA UGONJWA WA KIPINDUPINDU KIJIJI HAPO KWA NJIA ZA KISHIRIKINA. WATU WAWILI WAMEKAMATWA KWA MAHOJIANO KUHUSIANA NA TUKIO HILO AMBAO NI 1. ALIKO MWAMTOBE [47] MKAZI WA MATEMA NA 2. ALISOLOMON MWAMTOBE [49] MKAZI WA KITONGOJI CHA BULINDA. 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA KATIKA JAMII.

KATIKA TUKIO LA PILI:
MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MAPAMBANO ILIYOPO JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FELISTA MWANSASU [12] AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.949 CVS AINA YA MITSUBISHI FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA NSAJIGWA ALISALA [39] MKAZI WA MBEYA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 01.01.2016 MAJIRA YA SAA 07:50 ASUBUHI HUKO MAENEO YA MAFIATI, KATA YA MUUNGNANO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA. 

CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA AMEKAMATWA, UPELELEZI UNAENDELEA.

KATIKA TUKIO LA TATU:
MWENDESHA PIKIPIKI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ASIFIWE MWANTOBE [25] MKAZI WA TUNDUMA MKOANI MBEYA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA PIKIPIKI ALIYOKUWA AKIENDESHA KUGONGANA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 975 CPS AINA YA TATA BUS LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA EMANNUEL ADAM [36] MKAZI WA MBEYA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 01.01.2016 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO MAPOROMOKO KATIKA BARABARA YA TUNDUMA/MBEYA, WILAYA MOMBA, MKOA WA MBEYA.

INADAIWA KUWA, MARA BAADA YA AJALI HIYO PIKIPIKI ALIYOKUWA AKIENDESHA MAREHEMU ILITOROSHWA NA WATU WASIOJULIKANA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA WA BASI AMEKAMATWA NA UPELELEZI UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA NA KUHESHIMU SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA KUWA MAKINI KATIKA MATUMIZI YA BARABARA HASA KWA KUFUATA SHERIA ZA BARABARANI.

Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images