Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 754 | 755 | (Page 756) | 757 | 758 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Kiembe Samaki Mh.Ibrahim Raza nje ya jengo la Bunge  mjini Dodoma hapo jana.Mh Raza amempongeza Mh Kassim Majaliwa kwa uchapaji wake kazi na pia amemtaka kuendelea na kasi yao kubwa ya kutumbua majipu kuhakikisha nchi yetu inapanda kiuchumi na pia kuirudisha nchi katika mstari wa kuheshimu sheria za nchi na misingi yake.


  0 0

  SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
  MAELEZO KUHUSU MRADI WA UMEME MBOPO TEGETA

  DAR ES SALAAM.

  Februari 2, 2016 kwenye blogi hii kuna mteja wetu kutoka Wilaya ya Kitanesco Tegeta alilamikia Shirika kuchelewesha  Mradi wa kupeleka umeme eneo la Mbopo.


  UKWELI NI KWAMBA: Mradi wa kupeleka umeme Mbopo unagharama ya Tsh.236,396,581.73, na umegarimiwa na Shirika la Umeme  Tanzania (TANESCO) kwa asilimia 100.


  UKUBWA WA MRADI: Mradi wa kupeleka umeme Mbopo unagharama ya Tsh.236,396,581.73, na unagharamiwa na Shirika la umeme  Tanzania kwa ailimia 100. Mradi unahusisha;


  1. Ujenzi wa laini ya msongo wa kilovolti 33  yenye urefu wa kilomita 8 na nguzo 93

  2. Transfoma kubwa ya kusambaza umeme (100kva 33/0.4/0.23kv-01)

  3. Nguzo 62 za umeme wa msongo mdogo ya njia tatu yenye urefu wa kilomita 3.
  KAZI ILIYOFANYIKA MPAKA SASA:

  1. Nguzo zote 93 zimeshasimamishwa

  2. Waya zimevutwa kwa urefu wa kilomita 2 kutoka Mbopo zahanati hadi Pangaboy Bar.


  SABABU ZA KUCHELEWA KWA MRADI:

  1. Mradi huu umechelewa kukamilika kutokana utaratibu wa manunuzi ya baadhi ya vifaa vya ujenzi kwenye mradi. 

  2. Kukosekana kwa Njia ya kupitisha umeme (way leave) wakati wa zoezi la kusimamisha nguzo lilipoanza.
  AHADI KWA WANANCHI:

  Baada ya kupatikana kwa vifaa hivyo, Shirika linategemea kuanza tena utekelezaji wa Mradi huu Jumatatu Februari 08, 2016 na kukamilika Februari 26, 2016.


  MIRADI MINGINE MUHIMU:

  Pamoja na mradi huu, mkoa pia una miradi ambayo linategemea kujengwa kwa mwaka huu 2016. Taratibu za kuwapata wankandarasi zinaendelea.

  1. Mradi wa kupeleka umeme Block 8 Mbweni Mpiji,

  2. Mradi wa kupeleka umeme Block 7 Mbeni Mpiji,

  3. Mradi wa kupelekea umeme Mbweni Teta,

  4. Mradi wa umeme Mabwe pande Kikwete Vision,

  5. Mradi wa kupeleka Umeme Kisauke


  Uongozi unaendelea kusisitiza kwa wateja wake kuwa Mipango mizuri na inayotekelezeka ya kuwapatia watanzania umeme wa uhakika ipo na inaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.
    
  Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano,

  TANESCO Makao Makuu.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Ujumbe kutoka Olam Tanzania Limited wakati ujumbe huo ulipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Februari 04, 2016.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Olam Tanzania Limited wakati ujumbe huo ulipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Februari 04, 2016.

  (Picha na OMR)

  0 0

   Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
  Jaji Mkuu wa Kenya Mhe. Dkt. Willy Mutunga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuipongeza Mahakama ya Tanzania kwa utendaji wake wa kusikiliza  na kuamua mashauri mengi yanayopelekwa mahakamani. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman na Kulia ni Jaji Kiongozi Mhe. Shaan Lila.

  Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
  JAJI Mkuu wa Kenya Mhe. Dkt. Willy Mutunga ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa utendaji wake wa kusikiliza  na kuamua mashauri mengi yaliyopelekwa mahakamani kwa mwaka wa sheria uliopita wa 2015 na kutoa wito kwa watendaji wa Mahakama ya Tanzania kuendelea kufanya vizuri licha ya changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.

  Jaji Mkuu wa Kenya ametoa pongezi hizo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mara baada ya kukutana na kuongea na Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani Tanzania kufuatia mwaliko alioupata wa kuhudhuria maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yatakayofanyika Februari 4 mwaka huu.

  Mhe. Dkt. Mutunga amesema kuwa  nchi ya Kenya mpaka sasa ina mashauri yapatayo 300,000 ambayo bado hayajaamuliwa na kuongeza kuwa asilimia 5 ya wananchi wa Kenya ndio hupeleka mashauri yao Mahakamani huku asilimia 95 iliyobaki wakitafuta ufumbuzi wa kesi zao nje ya Mahakama.

  “Ni kweli Tanzania mnafanya vizuri katika katika kusikiliza mashauri kwa haraka, asilimia 95 ya Wakenya hutafuta ufumbuzi wa kesi zao kwa viongozi wa kidini na Kimila kutokana na baadhi yao kukosa fedha za kutosha za kufuatilia na kugharamia kesi zao” Amesema.

  Ameongeza kuwa Mahakama ya Kenya kwa mwaka huu 2016 imejipangia malengo ya kuhakikisha kuwa inasuluhisha mashauri yote ndani ya mwaka mmoja ili kuongeza ufanisi na imani kwa wananchi.

  Ameeleza kuwa Tanzania ina jambo la kujifunza kutoka Kenya kufuatia mageuzi ya Katiba iliyoyafanya mwaka 2010 hususan kwenye baadhi ya maeneo ikiwemo na nafasi ya Mahakama kwenye Katiba Mpya ambayo Tanzania inaendelea na mchakato wake.

  Akizungumzia mageuzi hayo ambayo tayari Kenya imeyafanya kufuatia kuwepo kwa Katiba mpya Mhe. Mutunga amesema kuwa ni pamoja kupungua kwa madaraka ya Rais katika kuteua Majaji, na nafasi za Majaji kutangazwa na watu kupeleka maombi na sifa zao kujadiliwa ambapo wananchi huruhusiwa kutoa maoni kwa Tume ya Mahakama ya Kenya kuhusu majaji hao kabla ya kuapishwa.

  Aidha, ameeleza kuwa Watanzania wana kila sababu ya kujivunia umoja na mshikamano uliopo ambao umesababishwa na waasisi wa taifa hilo huku akibainisha kuwa majadiliano na upatikanaji wa Katiba Mpya utafanywa na Watanzania wenyewe kwa kuwa Watanzania ni walimu na mfano wa kuigwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akizungumzia ujio wa Jaji Mkuu wa Kenya amesema kuwa Mahakama ya Tanzania imenufaika na ujio wake kwa kuwa iko kwenye maadhimisho ya Wiki ya Sheria ambayo huwakutanisha wadau mbalimbali wa sharia kujadili changamoto na mafanikio ya Sekta ya Sheria nchini.

  Amesema kuwa kufuatia ziara ya Jaji Mkuu wa Kenya Mahakama ya Tanzania imejifunza masuala mbalimbali ambayo ni muhimu katika ufanisi wa shughuli zake ikiwemo Maslahi ya Watumishi wa Mahakama, Jukumu la Mahakama kutafsiri Katiba kwa kuangalia historian a uchumi pia kuazima baadhi ya hukumu zilizotolewa nchini Kenya kama ushauri.

  Aidha, amebainisha kuwa Mahakama ya Tanzania inao wajibu wa kuendelea kuongeza uwazi katika upatikanaji wa watendaji wake wenye nia ya kuwatumikia wananchi na kuboresha njia za kuwapata majaji.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha DC wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha,Fidelis Lumato akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani,kulia ni Mwenyekiti wa halmashauri, Noah Sapuk.
  Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Arusha DC,Noah Sapuk akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani. 
  Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Arusha DC wakifatilia mijadala kwenye kikao hicho. 
  Baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo wakiwa kwenye kikao kujibu hoja mbalimbali kutoka kwa madiwani. 
  Baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo wakiwa kwenye kikao kujibu hoja mbalimbali kutoka kwa madiwani. 
  Diwani wa Viti Maalumu katika halmashauri ya Arusha DC,Nuru Ndossy akichangia hoja. 
  Diwani wa Kata ya Mateves ,Julius Mollel akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.


  0 0

   Afisa Mradi wa KFW kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya
  Afya (NHIF),Francis Mbwana akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo
  kwa watoa huduma wa Afya ya Mama na Mtoto kutoka katika vituo
  mbalimbali vya Afya mkoani Tanga iliyofanyika ukumbi wa mkuu wa mkoa.

   watoa huduma za afya ya mama na mtoto kutoka
  katika vituo mbalimbali vya afya mkoani Tanga wakati wa ufunguzi wa
  mafunzo kwa watoa huduma wa Afya ya Mama na Mtoto,uliofanyika kwenye
  ukumbi wa mkuu wa mkoa Tanga. 
  Kaimu Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
  Mkoani Tanga,Dinna Mlwilo akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa
  mafunzo kwa watoa huduma wa Afya ya Mama na Mtoto,uliofanyika kwenye
  ukumbi wa mkuu wa mkoa Tanga.

  MFUKO wa bima ya afya kupitia mradi wake wa KFW umeanza kutoa elimu
  kwa wahudumu wa afya ya mama na mtoto namna ya kutumia mitandao ya
  simu kuwasilisha taarifa za afya mama mjamzito na mtoto mchanga.

  Hatua hiyo inalengo la kuhakikisha wanapunguza ikiwemo na kuzuia kwa
  kiasi kikubwa changamoto ya vifo vya wajawazito pamoja na watoto wa
  changa nchini kote.

  Hayo yamebainishwa na Afisa Mradi wa KFW mkoa wa Tanga Francis Mbwana 
  wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wahudumu wa afya ya mama na mtoto 
  kutoka katika vituo mbalimbali vya afya mkoani hapa.

  Alisema kuwa utaratibu huo wa kutumia teknolojia ya simu katika
  kusajili na kufuatilia hali za afya za mama wajawazito na watoto
  zitasaidi kupata taarifa za maendeleo ya afya zao mapema tofauti na
  sasa.

  “Kupitia mradi huu wa KFW muda mwingi fomu za wanachama wapya zilikuwa 
  zinachelewa kutufikia ,huku wakati mwingine mjamzito anakuwa katika 
  hali ya hatari tunashindwa kumfuatilia kwa wakati lakini kupiti njia
  ya simu tutaweza kufanya malipo na ufuatiliaji kwa haraka”alibainisha
  Mbwana.

  Aliongeza kuwa lengo la mradi ni kuhakikisha wajawazito wote nchini
  wanapata fursa ya kujiunga na huduma hiyo hususani maeneo ya vijijini
  ili kuhakikisha wanapata fursa ya kufaidika na mradi huo.

  Nae mmoja wa Wauguzi wa afya Ester Kimweri alisema kuwa toka KFW ianze miaka miatau iliyopita mahudhurio ya wajawazito yamekuwa yakiongezeka kila siku tofauti na hapo awali.

  “Mpango wa KFW umesaidia wajawazito wengi kuona umuhimu wa
  kujifunguali katika vituo vya afya,zahanati na hospitali tofauti na
  hapo awali mahudhurio yalikuwa ni madogo”alisema Kimweri.


  0 0

  Na Beatrice Lyimo-Maelezo
  OFISI ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imewataka waajiri wote nchini kuhakikisha watumishi wao wanapata Fomu ya wazi ya Mapitio na Upimaji Utendaji Kazi( OPRAS) wa utekelezaji bila usumbufu.

  Kwa mujibu wa taarifa kutoka kitengo cha mawasiliano cha Ofisi hiyo imeeleza kuwa, kuna baadhi ya Taasisi za Umma watumishi wanaelekezwa kununua fomu za OPRAS kutoka kwa watu binafsi, kitendo ambacho ni kinyume cha Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.

  Fomu za OPRAS haziuzwi hivyo watumishi hawatakiwi kuzinunua, endapo mtumishi atashawishiwa au kulazimishwa kununua fomu hizi atoe taarifa Dawati la Malalamiko Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora ili hatua stahiki zichukuliwe, imefafanua taarifa hiyo.

  Pia Fomu hizo zinapatikana katika Tovuti ya Ofisi ya Rais-Menejiment ya Utumishi wa Umma yenye anwani ya www.utumishi.go.tz, hivyo waajiri wanaelezwa kutembelea tovuti hiyo.

  Aidha, Serikali ilianzisha matumizi ya mfumo wa wazi wa mapitio na Tathimini ya Utendaji Kazi OPRAS mwezi Julai mwaka 2004 kupitia waraka wa Utumishi Na.2 wa mwaka 2004 na kufuta mfumo wa zamani wa kupima utendaji kazi wa mtumishi kwa njia ya siri.


  Mabadiliko ya kutathimini UtendajI kazi wa Watumishi wa Umma kwa uwazi yanakwenda sambamba na Sera ya Menejiment na Ajira katika Utumishi wa Umma ya mwaka 1998 kama ilivyorekebishwa mwaka 2008 na kusisitiza uwekaji wa mifumo ya Menejimenti ya utendaji bora wa kazi inayojali matokeo.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(wapili kushoto) Balozi wa Vodacom Tanzania, Nasibu Abdul (Diamond Platinum) Kaimu Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Rosalynn Mworia(kulia) na Zarina Hassan(kushoto)wakionesha mabango yenye ujumbe wa jinsi ya kujiunga na Promosheni ya “Ongea Deilee”, wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo leo jijini Dar es Salaam, Itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi wakiongea jumla ya dakika 10 Vodacom kwenda Vodacom.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao( kushoto) na Zarina Hassan(Kulia) wakionyeshwa tangazo la promosheni ya”Ongea Deilee” kwenye simu lililofanywa na msaanii wa muziki wakizazi kipya Abdul Nasibu”Diamond Platinum”( katikati) wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo leo jijini Dar es Salaam, Promosheni hiyo itawawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi wakiongea jumla ya dakika 10 Vodacom kwenda Vodacom.
    Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(kushoto) akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa promosheni ya”Ongea Deilee” Itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi wakiongea jumla ya dakika 10 Vodacom kwenda Vodacom leo jijini Dar es Salaam,anayeshuhudia kulia ni Balozi wa Vodacom Tanzania,Nasibu Abdul (Diamond Platinum)
   Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(wapili kushoto) akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa promosheni ya”Ongea Deilee” Itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi waongeapo jumla ya dakika 10 Vodaocom kwenda Vodacom, leo jijini Dar es Salaam,wengine katika picha kutoka kushoto,Zarina Hassan, Balozi wa Vodacom,Nasibu Abdul (Diamond Platinum) Kaimu Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni hiyo,Rosalynn Mworia.


  SASA ni wakati wa watanzania kuongea, ambapo kuanzia leo wateja wa Vodacom, mtandao unaongoza nchini wataweza kuongea bure kwa saa nzima!


  Kupitia ofa yake maalum kwa wateja ya Ongea Bure Deilee, itakayokuwa ya miezi mitatu mfululizo, wateja wa Vodacom wataweza kuongea kwa muda wa saa moja bure kila siku.

  Ili kujiunga na ofa hii ambayo haijawahi kutokea nchini, mteja anachotakiwa kufanya ni kuongea kwa dakika 10 kila siku kwa viwango ya malipo vya kawaida na hapo hapo atapata ofa ya kuongea kwa muda wa saa moja bure.

  Ofa hii ya Ongea Bure Deilee pia imemuhusisha mwanamuziki nguli wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Diamond Platnumz, ambaye moja ya kibao chake kinachotamba ni ‘Number One’, ambao pia ni mwito wa simu maarufu kwa watumiaji wa mtandao wa Vodacom.

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa ofa hii, Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania Bw. Ian Ferrao amesema “Ongea Bure Deilee ni ofa ya aina yake kutolewa kwa wateja wa Vodacom popote walipo nchini. Ofa hii imebuniwa kubadilisha maisha ya wateja wetu walio wengi na kuendelea kuyafanya kuwa murua!”

  Aliendelea kusema kuwa Vodacom Tanzania imedhamiria kuendelea kuvuka kile ambacho wateja wake wanakitarajia, kwa kuwaunganisha kwa viwango nafuu ambavyo wanazoweza kuvimudu, lengo kubwa likiwa ni kuweza kuwainua kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

  Ofa hii itatolewa kwa wateja milioni moja wa kwanza watakaojiunga kila siku kupitia ujumbe mfupi wa maneno ambapo watakuwa huru kuongea wakati wowote watakao, iwe usiku au mchana, ili mradi watakaowasiliana nao ni watumiaji wa mtandao wa Vodacom.

  “Huu ni mwendelezo wa kampeni yetu ya Maisha ni Murua ambayo jitihada zetu katika kuwaletea wateja ofa za kipekee na ambapo kupitia ubunifu wa kutumia mtandao, tunawezesha maisha ya wateja wetu wote nchini kuwa murua. Kama ambavyo tunasema siku zote, tutaendelea toa huduma zinazowawezesha wateja wetu kuwasiliana kwa urahisi na wapendwa wao na hata katika shughuli zao za uzalishaji mfululizo,” aliongeza Ferrao.

  Kwa upande wake, Diamond Platinumz, ambaye sasa ni balozi wa Vodacom alisema “Ninayo furaha kuwa sehemu ya kampeni hii kabambe kutoka Vodacom. Nilipopata taarifa kwa mara ya kwanza kuhusu ofa hii nilipata mshtuko na kusema dah, Vodacom imeleta tena bonge la ofa, kwa hakika ofa hii itaniunganisha na washabiki wangu, marafiki, familia na wafanyabiashara wengine”.

  Aliongeza “Nitawaelezea washabiki wangu, familia na marafiki jinsi wanavyoweza kufanya maisha yao kuwa murua kupitia kampeni hii mpya kutoka Vodacom. Wanachotakiwa kufanya ili kujiunga na kufurahia ofa ya Ongea Bure Deilee ni rahisi tu, yaani ni kupiga simu *149*01#.

  0 0

   Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya Wilaya Monduli, ambaye pia ni Mkuu wa wilaya hiyo, Francis Nyamiti akiongoza kikao cha kamati hiyo kujadili urejeshaji hali katika shule ya sekondari Edward Lowasa iliyopata maafa ya moto,, (wa kwanza kushoto) ni Mkurugenzi wa Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya, tarehe 4 Februari, 2016. 
   Mkurugenzi wa Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya, (wakwanza kushoto) pamoja na wajumbe wa Kamati ya maafa wilaya Monduli wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Mkuu wa wilaya hiyo, Francis Nyamiti (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kamati hiyo kujadili urejeshaji hali katika shule ya sekondari Edward Lowasa iliyopata maafa ya moto tarehe 4 Februari, 2016. 

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Wilaya ya Monduli, ambaye pia ni Mkuu wa wilaya hiyo, Francis Nyamiti (Mbele wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo mara baada ya kikao cha kamati hiyo kujadili urejeshaji hali katika shule ya sekondari Edward Lowasa iliyopata maafa ya moto, (Mbele wa pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya, tarehe 4 Februari, 2016. 
  (Picha zote na Ofsi ya Waziri Mkuu).

  Na. Mwandishi maalum.
  Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu maafa imezitaka Kamati za Maafa za Mikoa, Wilaya na Vijiji zote nchini kufanya tathmini zenye uhalisia wa athari za maafa yanapotokea wakati wanapokuwa wanatekeleza jukumu hilo ambalo husaidia kuainisha hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika Kuzuia/Kupunguza, Kujiandaa, Kukabili na Kurejesha hali baada ya maafa kutokea. 

  Akiongea wakati alipokutana na Kamati ya maafa ya Wilaya ya Monduli Tarehe 4 Februari 2016, Mkurugenzi wa Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya amebainisha kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imekuwa inapokea maombi ya misaada ya maafa ambayo tathmini zake huwa zimefanywa na Kamati za maafa ikiwa na aidha thamani kubwa au idadi kubwa kulingana na hali halisi ya athari ya maafa. 

  “Ofisi ya Waziri Mkuu idara ya uratibu maafa inalojukumu la kuratibu shughuli za maafa katika hali ya kujiandaa, kuzuia, kukabili na kurudisha hali ya kawaida pindi maafa yanapotokea. Katika ngazi ya wilaya maafa yakiwashinda kuyakabili huomba msaada katika ngazi ya mkoa halikadhalika mkoa ukishindwa huomba msaada katika ngazi ya kitaifa. Mfano mzuri ni maombi ya chakula cha msaada tumekuwa tunapokea maombi ya maefu ya tani lakini wataalamu wetu wakifanya tathmini ya kujiridhisha maombi hayo huwa mamia ya tani na wananchi huridhika” amesema Brig. Jen. Msuya 

  Msuya aliongeza kuwa kamati hazinabudi kuelewa kuwa nchi yetu inakumbwa na majanaga ya asili na yale ambayo husababishwa na wanadamu ambapo kimsingi serikali inalojukumu la kuzuia au kupunguza athari za maafa hayo. Hivyo uongezaji wa thamani na idadi ya mahitaji ya misaada ya maafa hufanya waathirika wengine kutopata misaada kwa wakati pamoja na iliyopungufu kwa kuwa serikali huanza kutafuta rasilimali za ziada ili kuweza kukabili na kurejesha hali ya maafa husika. 

  “Kamati ya maafa ya wilaya hii imefanya tathimini kwa uhalisia kwa maafa ya moto yaliyotokea shule ya sekondari ya Edward Lowasa, uhalisia wa tathimini hii umewezesha Kamati ya wilaya kuweza kumudu kurejesha hali ya shule hii kwa kuwa hakuna uongezaji wa thamani wala idadi. Tukifanya hivi kwa kamati zote nchini katika ngazi zote tutaweza kuwa na menejimenti nzuri ya maafa nchini”, alisisitiza Brig. Jen. Msuya. 

  Awali akiongea katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Monduli Franicis Nyamiti alifafanua kuwa mara baaada ya maafa ya moto kutokea katika shule ya sekondari Edward Lowasa, kamati ya maafa imekutana ili kuweza kujadili urejeshaji hali wa shule hiyo ambapo taarifa ya tathimini ya athari ya maafa iliyofanywa na Kamati ya Wilaya ndiyo iliyokuwa inawaongoza katika utekelezaji. 

  “Ni dhahiri kuwa taarifa ya tathimini ikiwa na uhalisia mara nyingi idadi na thamani mnaweza kuimudu kwa kushirikiana na wadau wa maafa. Sisi tumewashirikisha wadau hao ambao tayariwamejitokeza kutupatia magodoro yote 72 yaliyoungua, mansanduku ya wanafunzi hao pamoja na mchanga wa ujenzi. .”alisisitiza Nyamiti.

  Nyamiti alifafanua kuwa uhalisia wa tathmini ya athari za maafa hufanya urejeshaji hali kuwa kwa wakati kwani tayari mdau mwingine amaeshajitolea kubomoa mabaki ya jingo la bweni lililoungua tayari kwa kuanza ujenzi, aidha Mmiliki wa shule jirani ya Tumaini sekondari amejitolea bweni lake, vitanda na magondoro amabavyo wanafunzi hao watakuwa wanatumia wakati ujenzi ukikamilika.
  Shule ya Sekondari ya Edward Lowasa inao wanafunzi 700 ambapo wanafunzi 72 ndio walioathirika na maafa ya moto yaliyotokea tarehe 27 Januari, 2016 kwa kuungua bweni la wanafunzi hao. Aidha kutokana na maafa hayo hakuna mwanafunzi aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa . 

  0 0


  Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Mary Maziku (kushoto)akisoma taarifa ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana . 
  Wajumbe wa Kamati ya Siasa CCM mkoa wakisikiliza wakati Kaimu Katibu wa Mkoa Ndugu Mary Maziku akiwakilisha taarifa za maandalizi ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye ofisi za CCM mkoa wa Singida. 
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na kamati ya siasa ya CCM mkoa wa Singida mara baada ya kupokea taarifa za maandalizi ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi jengo la CCM mkoa wa Singida ikiwa sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM.

  PICHA NA MICHUZI JR-MMG-SINGIDA

  0 0

  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Kinondoni, tarehe 02/02/2016 imewafikisha washitakiwa wafuatao mahakamani:-Bw.Bryceson Kajigiri Mwangoma mwenye umri wa miaka 54, Bw.Abel Sebabil Slaa mwenye umri wa miaka 44 na Bw.Bernard Thomas Mkude mwenye umri wa miaka 42 kwa kuiibia Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni  Tsh.33,681,780.

  Washitakiwa hawa Bw.Mwangoma na Bw.Slaa wakiwa Maafisa watendaji wa Kata ya Kimara kwa vipindi tofauti, na Bw.Mkude akiwa Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Kimara Baruti walitenda makosa kinyume na kifungu cha 31, 22, 28 (1) 3 vya sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 pamoja na kifungu cha 258, 270 vya sheria ya Kanuni za Adhabu. Washitakiwa wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya na kujipatia manufaa kwa kufanya wizi wa fedha hizo zilizokua zimewekwa na Wananchi katika akaunti ya Urasimishaji Ardhi kata ya Kimara iliyopo benki ya Wananchi wa Dar – es- Salaam (DCB) tawi la Magomeni kwa ajili ya kupimiwa maeneo yao.

  Mshitakiwa wa kwanza Bw. Mwangoma akiwa mtendaji wa kata kwa kipindi cha tarehe 01/04/2011 hadi tarehe 30/11/2011 kwa kushirikiana na Mshitakiwa wa tatu Bw.Mkude ambaye ni mshitakiwa wa pili walitumia madaraka yao kwa kushirikiana  kuiba kiasi cha Tsh. 24,764,280. Bw. Slaa akiwa mtendaji kata kwa kipindi cha tarehe 01/06/2013 hadi tarehe 31/01/2014 kwa kushirikiana na Bw.Mkude waliiba kiasi cha Tsh. 8,917,500.

  Washitakiwa walifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni na kufunguliwa kesi namba 51/2016 inayosimamiwa na Mhe. Hakimu Mushi. Watuhumiwa wako nje kwa dhamana na kesi imepangwa kusikilizwa tena tarehe 16/02/2016.


  IMETOLEWA NA   MKUU WA TAKUKURU (M) KINONDONI
  BENN LINCOLIN
  04/02/2016

  0 0

  Mchekeshaji wa orijino Komedi alimaarufu kama MPOKI ametembelea kituo cha radio cha Efm 93.7 katika ofisi zao na kuonana na wakurugenzi pamoja na watangazaji wake kwa lengo la kubadilishana mawazo sambamba na kuona jinsi gani kituo hicho kinavyoendesha shughuli zake za utangazaji.
  Mchekeshaji wa orijino Komedi alimaarufu kama MPOKIakiteta jambo na mkurugenzi mkuu wa Efm radio Francis Siza leo asubuhi.
  Mchekeshaji wa orijino Komedi alimaarufu kama MPOKI Wakifurahia jambo huku wakiagana baada ya mazungumzo.
  Mchekeshaji wa orijino Komedi alimaarufu kama MPOKI akisalimiana na Meneja mkuu wa kituo hicho Bw. Geofrey Ndaula.
   Meneja mahusiano na Mawasiliano Bw. Dennis Ssebo akimkaribisha Mpoki ofisini kwake leo alipotembelewa na Mchekeshaji wa orijino Komedi alimaarufu kama MPOKI.
  Mhariri mkuu wa Efm Radio Scholastica Mazula akisalimiana na Mpoki alipofika katika chumba cha habari.
  Akiwa pamoja na watangaziji wa kipindi cha Sports HQ (kulia) Maulidi Kitenge na (kushoto) Ibrahimu Masoud (Maesro)
  Picha ya pamoja na mtangazaji wa kipindi cha UHONDO Dina Marios na Mchekeshaji wa orijino Komedi alimaarufu kama MPOKI.
   Ma producer wa Efm Radio katika picha ya pamoja na Mchekeshaji wa orijino Komedi alimaarufu kama MPOKI.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mjimkongwe Issa Said Makarani akizungumza na waandishi wa habari pichani hawapo juu ya kutumia njia moja ya kuingilia Mjimkongwe kuanzia tarehe 8/2/2016.
   Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Mkadam Khamis Mkadam akizungumzia namna Jeshi la Polisi lilivyojipanga kuhakikisha Wananchi wananchi wanafuata sheria zitakazowekwa na Mamlaka ya Mjimkongwe kuanzia Februari 8 mwaka huu.
    Mkurugenzi Mipango Miji Dokta Moh’d Juma akijibu maswali kutoka kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano wa kutoa taarifa ya njia moja ya kuingilia Mjimkongwe kuanzia Februari 8 mwaka huu.
   Mkurugenzi wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Aboud Hassan Serenge akielezea mashirikiano waliyonayo na Mamlaka ya Mjimkonge katika kuimarisha matumizi ya njia ya Mjimkongwe ifikapo tarehe 8/2/2016.
   Mwandishi wa Habari wa Coconut FM Tabia Makame akiuliza maswali kuhusu zoezi zima la utumiaji wa Njia hiyo na namna wananchi watakavyoepuka usumbufu katika Mjimkongwe.
  Picha na Abdalla Omar Habar-Maelezo Zanzibar.


  Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mji Mkongwe Issa Said Makarani akijibu masuala ya waandishi wa habari.

  Mwashungi Tahir Maelezo 4-2-2016.
  SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kuanzisha utaratibu wa kutumia njia ya upande mmoja kubwa ya kuingia Mji Mkongwe kuanzia tarehe nane mwezi huu ili kupunguza usumbufu unaowapata wageni na watumiaji wengine wa Mji huo.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mamlaka ya Mji Mkongwe Forodhani, Mkurugenzi Mkuu Issa Saidi Makarani amesema uwamuzi huo umefikiwa kutokana na ongezeko kubwa la vyombo vya moto linalohatarisha usalama wa mji huo ambao ni urithi wa kimataifa.

  Amesema mji wa Zanzibar umekuwa ukipokea watalii na wageni wengi na wakati wa matembezi yao wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa kutokana na kuongezeka vyombo hivyo.

  Ameongeza kuwa ongezeko hilo la magari pia limepelekea athari kubwa kwenye majengo kutokana na mtikisiko mkubwa wa magari yenye uzito mkubwa na kubomoa baadhi ya majengo ya mji.

  “Watumiaji wa Mji huu na wanaofika kila siku kwa shughuli zao za kimaisha wanapata usumbufu na kubwa zaidi wingi wa vyombo hivyo tayari vimesababisha athari ya baadhi ya majengo,”alisisitiza Mkurugenzi Makarani.

  Amesema njia kubwa ya ndani ya kuingilia Mji Mkongwe itaanzia Vuga kupitia Afrika House , Hoteli ya Serena , Wizara ya Ardhi , Makaazi, Maji na Nishati , Benki ya NBC , Jengo La zamani la Watoto Forodhani , njia ya Mizingani hadi kuishia lango kuu la kuingia bandarini Malindi.

  Amezitaja njia zitakazofungwa kuanzia tarehe nane kuwa ni ile inayoanzia jengo la Wizara ya zamani ya Mawasiliano na Uchukuzi kupitia Kiponda na kumalizikia Darajani, njia inayoingia Mkunazini na kumalizikia Skuli ya Sunni Madrassa na njia inyozunguka nyuma ya jengo la sinema ya zamani Majestic.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Mkadam Khamis amesaema lengo la kuweka zoezi hilo ni kuweka usalama kwa wenye magari na wanaokwenda kwa miguu.

  Amewaomba wananchi kuunga mkono zoezi hilo ambalo litaweka mji Mkongwe katika hadhi na ubora wake uliopelekea kuwa miongoni mwa Miji ya Urithi wa kimataifa duniani.

  Mkurugenzi wa Baraza la Manispaaa Aboud Hassan Serenge amewataka wananchi wanaoishi katika maeneo ya Mji Mkongwe kubadilika na kuanzisha utamaduni wa kuimarisha suala la usafi.

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa maabara katika shule ya Sekondari  ya Unyianga,kata ya Unyianga mkoani Singida.Shule hiyo mpya yenye madarasa manne ikiendelea kujengwa kwa nguvu za wanannchi.
  Sehemu ya jengo la ujenzi wa maabara ukiendelea kwa nguvu za Wananchi
  Badhi ya Wananchi waliokuwa wakishiriki ujenzi wa maabara hiyo,wakielekea kumsikiliza Katibu MKuu wa chama cha CCM Ndugu Kinana aliyefika katika shule hiyo ya sekondari ya Unyianga kushiriki ujenzi na kuwahimiza wananchi kushiriki kujenga maendeleo yao.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa akiongozwa na mwenye shamba la Mtama Bwa.Elisha Abdallah sambamba na Mbunge wa jimbo la Singida Mjini Mussa Ramadhani alipokwenda kushiriki palizi la mkulima huyo wa mfano katika kata ya Mtamaa,mkoani Singida
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pichani kati akisukuma jembe la Plau linalokokotwa na N'gombe (kama aonekanavyo pichani) ikiwa sehemu ya kushiriki palizi katika shamba  hilo la Mtama lenye ukubwa wa Ekari moja na nusu  lililopo katika kata ya Mtama mkoani humo.Ndugu Kinana na ujumbe wake yuko mkoani Singida kwenye maandalizi ya sherehe za kuadhimishwa miaka 39 ya CCM,zinazotarajiwa kufanyika Februari 6 katika uwanja wa Namfua mkoani humo.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akitoa ufafanuzi kwa Wajasiria Mali hao mara baada ya kusikiliza kero na malalamiko mbalimbali ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo,ili kuendana kasi ya Rais Dkt Joseph Magufuli ya kuwahimiza wananchi kufanya kazi kwa kujituma kupitia kauli yake ya Hapa kazi Tu.
   Katibu Mku wa CCM Ndugu Kinana akiwa katika ukumbi wa ofisi za chama mkoa akisikiliza kero na mambo mbalimbali ya Wananchi ikiwemo kuyafanyia kazi,Ndugu Kinana amekutana na wajasiriamali (Mama Lishe,Boda boda,Wauza Mitumba na Wafanyabiashara nyingine ndogo ndogo.

  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Kodi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Denis Rugemalila akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mpango kazi wa utekelezaji wa mkakati wa utozaji faini kwa wamiliki waliobadili matumizi ya ardhi kinyume cha sheria. Kushoto ni Afisa Sheria Mwandamizi Bi. Martha Isaga.
  Afisa Sheria Mwandamizi Bi. Martha Isaga kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akitoa wito kwa wananchi kuzingatia sheria na kanuni ili kuwa na matumizi sahihi ya ardhi hivyo kuepusha migogoro. Kulia ni mkuu wa kitengo cha Kodi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Denis Rugemalila.

  ……………………………………
  Na Fatma Salum (MAELEZO)
  Serikali inatarajia kutekeleza zoezi la utozaji faini kwa wamiliki waliobadili matumizi ya ardhi kinyume cha sheria kwa kuzingatia Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999 na Sheria ya Mipango Miji namba 8 ya mwaka 2007.  Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Kodi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Denis Rugemalila wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mpango kazi wa utekelezaji wa zoezi hilo.

  Akifafanua kuhusu zoezi hilo Bw. Rugemalila amesema kuwa kuanzia Februari 8, 2016 Wizara ya Ardhi kwa kushirikiana na Halmashauri za Temeke, Kinondoni na Ilala itaanza operesheni jijini Dar es Salaam ya kukagua na kutoa adhabu ikiwemo kutozwa faini kwa waendelezaji wote waliobadili matumizi ya Ardhi na kuongeza majengo kinyume cha sheria.

  Aidha Bw. Rugemalila ameeleza kuwa licha ya tozo za faini hatua nyingine stahiki zitachukuliwa dhidi ya maendelezo ya ardhi ambayo yamefanyika bila vibali kama vile viwanda, vituo vya mafuta na shughuli nyingine zinazoathiri mazingira na kuleta kero kwa jamii.“Endapo kutabainika kuwepo kwa vibali vinavyotia mashaka, vitaainishwa ili vifanyiwe uhakiki kwa ajili ya kuchukua hatua stahiki dhidi ya wahusika.” Alisema Rugemalila.

  Sanjari na zoezi hilo pia wizara ya Ardhi inaendelea na zoezi la usambazaji wa hati za madai kwa wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi na watakaokaidi watafikishwa mahakamani pamoja na kushika mali zao, kufilisi au kufutiwa kwa miliki zao.“Tunawaomba wamiliki wote wa ardhi nchini kulipa kodi ya pango la ardhi na kutoa ushirikiano kwa maafisa wetu watakapokuwa wanapita kufanya ukaguzi” alisema Rugemalila.

  Serikali imeamua kuendesha zoezi la utozaji faini baada ya kubaini kuwa kuna baadhi ya waendelezaji wa ardhi wamekuwa wakibadili matumizi ya ardhi kiholela na kusababisha kero kwa umma, pia baadhi ya waendelezaji wanaongeza majengo tofauti na yale yaliyoidhinishwa kujengwa katika kiwanja husika.

  0 0


  Na. Jonas Kamaleki-MAELEZO.

  VYAMA vya Siasa nchini vimeaswa kuepukana na migogoro na kutumia vikao vyao katika kuendeleza shughuli zao za kisiasa.

  Hayo yamesemwa leo na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mhe. Jaji Francis Mutungi wakati akikabidhi Cheti cha Usajili wa muda kwa Chama kipya cha Maadili na Uwajibikaji (CM-TANZANIA).

  Aidha, Jaji Mutungi amevitaka Vyama vya siasa nchini kufanya siasa na sio uanaharakati kwaki kwa kufanya hivyo malengo yao yatatimia na kuifanya Tanzania kuwa na amani.‘’Msipende kukimbilia kwenye vyombo vya habari mnapokuwa na migogoro bali malizeni tofauti zenu ndani ya vikao vyenu kulingana na Katiba ya Vyama vyenu’’, alisema Jaji Mutungi.Aliongeza kuwa, Tanzania inapaswa kuwa na vyama vya siasa vinavyojitambua na vinavyojua wajibu wao katika kuleta maendeleo ya Taifa kwani siasa sio chuki wala uasama.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Maadili na Uwajibikaji (CM-TANZANIA) Bwana Laban Nkembo amesema kuwa, chama hicho kimeanzishwa kwa lengo la kuiweka Tanzania kimaadili na uwajibikaji kwa kuwa kinabeba mambo makubwa mawili yakiwemo Amani na Upendo. Ameongeza kuwa, chama chao sio cha Upinzani na kinaheshimu chama kilichopo madarakani hivyo, kinaahidi kushirikiana na Chama Tawala kuenzi mazuri yanayofanywa na chama hicho. ‘’Chama chetu sio cha upinzani, tunataka nchi nyingine duniani ziwe zinakuja kujifunza Tanzania kuhusu amani na maendeleo tulionayo’’, alisema Nkembo.

  Aidha, amebainisha kuwa, chama chao cha CM-TANZANIA kitatoa ajira za kudumu kwa Wanachama wake na hata kwa wale wasiokuwa wanachama ambapo kimeshaandaa Idara ya usimamizi mzuri wa huduma kwa jamii kama vile Wazee, Wajane, Walemavu pamoja na Yatima.

  CM-TANZANIA ni Chama cha 23 kupokea usajili baada ya Vyama vingine vya siasa 22 vyenye usajili wa kudumu.

  0 0

   Aliekuwa Mbunge wa Mchinga,Mudhihiri Mudhihiri Akizungumza na waandishi wa habari hawapo picha juu ya kitabu cha ‘‘Mwele Bin Taaban’’ ambacho kina ujumbe mbalimbali.leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Abdallah Makumbila aka Muhogo Mchungu. 
   .Mwana muziki Mrisho Mpoto akifafanua jambo kushoto ni Abdallah Makumbila aka Muhogo, leo jijini Dar es Salaam. 
  Waandishi wa habari wakimsikiliza Aliekuwa Mbunge wa Mchinga,Mudhihiri Mudhihiri, leo jijini Dar es Salaam. 
  (Picha na Emmanuel Massaka wa Globul ya Jamii).


  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
  ALIYEKUWA Mbunge wa Mchinga,Mudhihil Mudhihil ametunga kitabu cha ‘‘Mwele Bin Taaban’’ ambacho kina ujumbe mbalimbali. 

  Mudhihil ametunga kitabu hicho kwa kushirikisha watu mahiri ikiwa lengo ya kukuza Kiswahili kuweza kutumika sehemu ya ajira. 

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mudhihil amesema kuwa kitabu hicho kinaweza kutumika katika mtaala wa shule za Sekondari kwa kudato cha tatu na sita na hadi vyuo vikuu. 

  Amesema kuwa katika Dibaji ya kitabu hicho ameandika Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Harrison Mwakyembe ambaye ana ujumbe wake katika kitabu hicho. 

  Mudhihiri amesema kuwa watanzania hawapendi kusoma na kuwataka kusoma kutafanya wajue vitu vingi na kujua nchi yao. 

  0 0

  Na Nyakongo Manyama
  Halmashauri ya Wilaya ya Butiama Mkoani Mara imesema imepata ufumbuzi wa changamoto ya wanafunzi wa darasa la kwanza na awali Shule ya Msingi Mwibagi wilayani waliokosa mahali pa kusomea kwa kuwagawa wanafunzi hao kwa awamu mbili.

  Hayo yamebainishwa leo (Alhamisi 04, Februari 2016), Afisa Elimu wa Wilaya hiyo, Hans Mgaya, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii, ambapo alikiri kuwepo kwa changamoto ya uhaba wa madarasa shuleni kutokana na ongezeko la wanafanuzi walioandikishwa kuanza darasa la kwanza mwaka huu, ambapo hata hivyo tayari wameshachukua hatua mbalimbali za kukabiliana na tatizo hilo.

  Aidha, Mgaya amesema kuwa jitihada za muda mfupi walizozifanya ni kuwagawa wanafunzi hao katika mikondo miwili ili waweze kubadilishana madarasa , mkondo mmoja utaingia asubuhi na mkondo mwingine mchana. 

  Kwa mujibu wa Mgaya alisema jitihada za muda mrefu ni kujenga shule nyingine mpya ili kusaidia kuchukua wanafunzi wengi kwa wakati mmoja, ujenzi wa shule hiyo ulishaanza kabla ya tamko la elimu bure na tupo katika hatua ya awali ya ujenzi wa msingi wa madarasa hayo alisema Mgaya.

  “wanafunzi walioandikishwa kujiunga na shule ya msingi kwa mwaka huu 2016 imeongezeka kwa kiasi kikubwa hivyo kusababisha idadi ya wanafunzi kuwa kubwa” alisema Mgaya.


  Idadi ya wanafunzi wa darasa la awali na la kwanza walioandikishwa kwa mwaka 2016 katika shule ya msingi Butiama kuanza masomo, ambapo hata hivyo zaidi ya wanafunzi 240 wa shule hiyo wanasomea katika chumba kimoja.

  0 0

  WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chawene ametembelea ofisi za Mfuko wa Pension wa LAPF mjini Dodoma Leo. Katika ziara hiyo mh. Waziri amepongeza jitihada za Mfuko kuongeza Wanachana kila mwaka pamoja na huduma bora zinazotolewa kwa wanachama hasa katika kulipa mapema madai ya wananchama.

  Akiongea na watumishi wa Mfuko wa LAPF amepongeza jitihada za watumishi kwa utendaji wao mzuri unaopelekea utendaji bora wa Mfuko. Mh. waziri amepongeza uwekezaji unaofanywa na LAPF katika kuhakikisha Mfuko unakuwa endelevu . 

  Pia ameahidi kushirikiana na Mfuko ili kuhakikisha unaendelea kufanya 
  vizuri zaidi.
  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chawene akisalimiana na kiongozi wa LAPF leo alipotembelea ofisi za Mfuko wa Pension wa LAPF mjini Dodoma.
   Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chawene akisaini kitabu cha wageni leo alipotembelea ofisi za Mfuko wa Pension wa LAPF mjini Dodoma.

  Wafanyakazi wa Mfuko wa Pension wa LAPF  wakimsikiliza Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chawene alipotembelea ofisi za Mfuko huo mjini Dodoma.
  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chawene akizungumza na wafanyakazi wa  Mfuko wa Pension wa LAPF alipotembelea ofisi za Mfuko huo leo mjini Dodoma. 

  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chaweneakizungumza na wafanyakazi wa mfuko huo leo alipotembelea ofisi za Mfuko wa Pension wa LAPF mjini Dodoma.

  0 0

   
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili mkoani Singida tayari kwa maadhimisho ya Miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM yanayotarajiwa kufanyika Februari 6 mwaka huu siku ya Jumamosi kwenye uwanja wa Namfua mkoani humo, Kauli Mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Kufanya Kazi”
   Mh Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa MKoa wa Singida Dk Parseko Kone
   Mh Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya,Ndugu Khamis Nguli.
   Mh Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa UWT mkoa,Mh Diana Chilolo mara baada ya kuwasili mkoani Singida jioni ya leo
  Rais Mstaafu,Mh Jakaya  Kikwete akiwapungia mkono wananchi
   Mke wa Rais Mstaaafu Mama Salma Kikwete  akipokelewa na baadhi ya wafuasi wa chama cha CCM mkoani humo mapema leo jioni
    Mwenyekiti wa CCM, Rais mstaafu Jakaya Kikwete akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) pamoja na Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye.shoto ni Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete
   Mwenyekiti wa CCM,Rais Mstaafu Dk Jakaya Kikwete akipata utambulisho kutoka kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Singida ,Mama Mary Maziku.
  Mwenyekiti wa CCM, Rais mstaafu Jakaya Kikwete akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Said Amanzi

older | 1 | .... | 754 | 755 | (Page 756) | 757 | 758 | .... | 1898 | newer