Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 73 | 74 | (Page 75) | 76 | 77 | .... | 1904 | newer

  0 0
  Shomari kimbau akiwa na Cheka baada ya kumvisha ubingwa wa IBF Africa aliokuwa akiutetea.

  Bondia Fransic Cheka Kushoto akipambani na Thomas Mshali wakati wa mpambano wao uliofanyika katika sikukuu ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam Cheka alishinda kwaKNOCKOUT raundi ya kumi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
  Bondia Fransic Cheka Kushoto akimshambilia kwa makonde ya nguvu Thomas Mshali wakati wa mpambano wao uliofanyika katika sikukuu ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam Cheka alishinda kwa KNOCKOUT raundi ya kumi .
  Bondia Thomas Mashali kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransic Cheka katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam Cheka alishinda kwa KNOCKOUT.

  Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Yusuph Jibaba wakati wa mpambano wao uliofanyika mei mosi katika ukumbi wa PTA Saba saba Dar es salaam Star Boy alishinda kwa KNOCKOUT raundi ya nne Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
  Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Yusuph Jibaba wakati wa mpambano wao uliofanyika mei mosi katika ukumbi wa PTA Saba saba Dar es salaam Star Boy alishinda kwa KNOCKOUT raundi ya nne Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
  Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Yusuph Jibaba wakati wa mpambano wao uliofanyika mei mosi katika ukumbi wa PTA Saba saba Dar es salaam Star Boy alishinda kwa KNOCKOUTraundi ya nne Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
  Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' akishangilia ushindi uku akiwa amebebwa juu juu kama mkungu wa ndizi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
  Bondia Cosmas Cheka kushoto akipambana na Charles Mashali wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba siku ya mei mosi Cheka alishinda kwa ponti mpambano huo Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
  Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' akimsindikiza wakati wa kupigana bondia Ibrahimu Class 'King class Mawe wakati wa mpambano wake na amos mwamakula
  Bondia Amos Mwamakula kushoto na Ibrahimu Class 'King Class mawe' wakisubili matokeo ambapo class alishinda kwa point Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
  Kotoka kushoto ni Kocha wa mchezo wa ngumi Kimataifa Rajabu Mhamila 'Super D' mdau ambaye ajajulikana jina Mtaalishaji wa mpambano kati ya Fransic Cheka Vs Thomasi Mashali Adamu Tanaka 'Tunaluza' na MC wa mpambano huo COOL p
  Rashidi Mhamila 'Ngade akiwa amepozi na Bady Boy wakati wa onesho hilo

  0 0


  Tigo Tanzania, Aprili 29, 2013: Tigo Tanzania wamezindua ukurasa wake mpya wa Twitter wa  kuchati moja kwa moja , huduma ya kipekee na ya kwanza Tanzania , ambapo wapenzi wa Tigo Twitter wanaweza kuchati na mastaa wawapendao moja kwa moja kwa njia ya mtandao huo kwa muda wa saa nzima. Kwa kuanzia, mashabiki wa msanii maarufu wa Tanzania, Elias

  Barnaba, wamepewa fursa ya kuchati moja kwa moja na msanii huyo ikiwa ni pamoja na  kumuuliza maswali ambapo atayajibu papo hapo.

  Meneja Chapa wa Tigo Bw William Mpinga alisema wakati wa uzinduzi kuwa, “Tigo inajivunia kuwapa wapenzi wa Tigo Twitter jukwaa la kuonana na kuchati moja kwa moja na mastaa wawapendao kupitia ‘Twitter Celeb Live Chat’, ambapo wataweza kufurahia na kubadilishiana nao uzoefu wa maisha yao kwa ujumla; huduma maalumu ya kipekee kabisa na ya kwanza

  Tanzania kutoka Tigo! Kupitia Jukwaa hilo maalumu , Staa maarufu wa muziki wa kizazi kipya Barnaba ambaye ndiye staa wa kwanza kushriki katika jukwaa hilo, atapokea maswali moja kwa moja kutoka kwa mashabiki wake na kutoa majibu papo kwa papo, jambo ambalo mashabiki hawakuwahi kulifikiria kabla..”

  "Ningependa kuwaarifu wateja wetu wote na wale wapenzi wetu wa Tigo Twitter kuwa hii ni mojawapo ya huduma bora kabisa za burudani za kuchati moja kwa moja ambapo nyingine nyingi za aina hii ziko njiani! Hii ni fursa ya pekee ya kufurahia maisha na ninatoa wito kwa

  wote kuijunga na mtandao wa Tigo Twitter na kuungana nasi ili kufuarahia mambo mazuri yanayofanywa na kuwezeshwa na mtandao wa Tigo. “ alifafanua zaidi Bw. Mpinga. Hivi karibuni, Tigo Tanzania ilipata tuzo ya utambuzi ya dunia kwa kuwa kampuni pekee

  inayowasilaina na wateja wao moja kwa moja kupitia kurasa za mtandao mbalimbali ya kijamii kama Facebook. Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la SocialBakers mnamo

  tarehe 7, Februari 2013, ikijumuisha chapa kumi bora za kijamii duniani kwenye mtandao wa wa Facebook katika robo ya mwisho wa mwaka 2012. Huduma ya kuchati moja kwa moja na mastaa mbalimbali ni njia ya kipekee ya Tigo kuwaunganisha, na kuwafanya wateja wetu

  wapendwa kujumuika kwa pamoja kupitia majukwaa mbalimbali ya habari ya kijamii ambayo wanayapenda. Kushiriki katika huduma hii ya kuchati moja kwa moja unahitaji kuungana na Tigo Tanzania kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, kisha tumia #OngeanaTigoCeleb na weka Tigo using @Tigo_Tz @jina la celeb Kama haujaiunga na mtandao wa Twitter, tafadhali tumia hatua rahisi zifuatazo ili kuweza unufaika huduma hii bomba ya Tigo:

  Andika @Tigo_Tz kwenye search kisha bofya
  • Utatokea ukurasa wa Tigo. Bonyeza kwenye follow.
  Baada ya hapo rudi kwenye ukurasa wako wa Twitter na utaweza kuziona Tweet za Tigo na celeb

  0 0


     Ney, Mauture, Roma, Madee, na Fid Q kupamba jukwaa la Airtel yatosha BURE.

  Katika mfululizo wa matamasha ya Airtel Yatosha yanayoendelea mikoa mbalimbali nchini , Kampuni  ya Airtel  mwishoni mwa wiki hii itatoa burudani pamoja na utambulisho wa huduma ya Airtel Yatosha kwa wakazi wa temeke , jijini Dar es salaam katika viwanja vya Mbagala Zakhem siku ya Jumamosi na Jumapili ya tarehe 4 na 5 mwenzi May 2013.

  Tamasha la Airtel yatosha litapambwa na waimbaji mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wakiwemo , Sir Juma Nature akiwa na kundi la wanaume halisi, Madii akiwa na kundi zima la tiptop connection,  pamoja na wakali wa hipop  Fid Q , Roma Mkatoliki na Ney wa mitego.

  Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando amesema, tumefanya matamsha ya Airtel yatosha katika mikoa mbalimbali nchini lengo hasa likiwa ni kutoa elimu kuhusu huduma zetu ikiwemo Airtel yatosha na kuwaunganisha watanzania katika mtandao wa mawasiliano bora na bei nafuu wa Airtel,

  Na mwishoni mwa wiki hii tunawafikia wateja na wakazi mkoa wa Dar es salaamawa na kuwapa  nafasi ya kusajili namba zao, kujiunga na huduma ya Airtel yatosha,  Airtel Money na  internet ya kasi ya 3.75G, kupata elimu kuhusu huduma na ofa mbalimbali za Airtel na kuunganishwa na mtandao wa Airtel kwa wale wateja wapya.

  Kiingilio ni  BURE, Njoo na kitambulisho chako upate kuunganishwa na huduma zetu na kupata burudani kutoka kwa wasanii mahiri wa kizazi kipya Aliongeza Mmbando.

  Kujiunga na huduma ya Airtel Yatosha mteja anatakia kupiga *149*99#  na kuunganisha moja kwa moja kwenye orodha ya huduma hii na kuchagua kifurushi anachokipenda na kuweza kujipatia dakika za maongezi, ujumbe mfupi na kifurushi cha internet.

  0 0

   Maandamano ya Wafanyakazi yakiongozwa na bendi wakati wakipita mbele ya mgeni Rasmi,Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Ally N. Rufunga jana katika uwanja wa Jamhuri Wilayani Kahama sherehe hizo zilipofanyika kimkoa.

   Burudani za ngoma za asili za kisukuma na nyimbo za taarabu kutoka kwa walimu zilifanikisha vilivyo.
   Mwenyekiti wa TUICO Mkoa wa Shinyanga Bw.Fue Mrindoko akimkaribisha Mhe.Ali N. Rufunga kuzungumza na wafanyakazi waliofurika katika kiwanja cha Jamhuri mjini Kahama.
  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Ally Rufunga jana katika uwanja wa Jamhuri Wilayani Kahama sherehe siku ya wafanyakazi duniani mei mosi.
  Picha na Magdalena Nkulu, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya pamoja na viongozi wengine wa chama na Serikali pamoja na wadau mbali mbalimbali na wafanyakazi wakiimba wimbo wa wafanyakazi maarufu kama "Solidarity Forever" Katika viwanja vya sabasaba mjini Namanyere Wilayani Nkasi zilipofanyika sherehe hizo kimkoa jana. Kauli mbiu ya sherehe hizo za Mei Mosi mwaka huu ni "KATIBA MPYA IZINGATIE USAWA NA HAKI KWA TABAKA LWA WAFANYAKAZI" 
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Iddi Hassan Kimanta wakiangalia maonesho mbalimbali yaliyokuwa yakifanywa na wafanyakazi wa sekta mbalimbali katika kufanikisha sherehe za Mei Mosi Wilayani Nkasi zilizofanyika huko kimkoa jana. 

  Maonesho ya wafanyakazi wa Serikali na Sekta binafsi kwa vitendo ilinogesha sherehe hizo.
  Maandamano ya wafanyakazi na mabango yenye jumbe mbalimbali ilikuwa sehemu ya maadhimisho hayo. Kauli Mbiu ya sherehe hizo kitaifa ilikuwa "KATIBA MPYA IZINGATIE USAWA NA HAKI KWA TABAKA LWA WAFANYAKAZI" 
  Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson Mashala wakiangalia maonesho mbalimbali yaliyokuwa yakifanywa na wafanyakazi wa sekta mbalimbali katika kufanikisha sherehe za Mei Mosi Wilayani Nkasi zilizofanyika huko kimkoa jana. 
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akitetea jambo na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi iliyofanyika kimkoa Wilayani humo jana. 
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi cheti na zawadi mmoja ya wafanyakazi bora wa mwaka 2012/2013 katika Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Elvira Malema ambaye Sekretari wa Mkuu  huyo wa Mkoa jana katika uwanja wa sabasaba Mjini Namanyere Wilayani Nkasi. Anayeshuhudia kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Iddi Hassan Kimanta.
  Michezo mbali mbali ya mpira wa miguu na netiboli pia ilifanyika ikiwa ni kuhamasisha michezo kwa wafanyakazi kwa ajili ya kuboresha afya zao kazini na kazi zao kwa ujumla. Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akitoa salam za Mei Mosi kwa wachezaji wa timu za Veteran Sumbawanga na Namanyere Nkasi kabla ya kuanza kwa mpambano, timu hizo zilitoa sare 1-1. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Iddi Hassan Kimanta. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo baada ya kulifungua rasmi leo. Picha na OMR.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia washiriki wa Kongamano la siku mbili la Sayansi ya Tiba, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili,(MUHAS) wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo leo Mei 2, 2013 katika Ukumbi wa Kunduchi Beach Hotel, lililoandaliwa na Chuo hicho.  
   Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia, kwenye Ufunguzi wa Kongamano la siku mbili la Sayansi ya Tiba, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS) leo

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya madokta wa Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili, wakati alipowasili Ukumbi wa Kunduchi Beach Hoteli leo Mei 2, 2013 kwa ajili kufungua Kongamanao la siku mbili la Sayansi ya Tiba, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS). Picha na OMR.


  0 0


  Benki ya Barclays Tanzania jijini- Dar Es Salaam imetangaza udhamini wa shillingi za kitanzania milioni 61 (TZS 61,000,000) kusaidia klabu ya Baylor Tanzania iliyoundwa kwa vijana wa umri wa kati wanaoiishi na virusi vya ukimwi na sehemu ya Chuo cha Utabibu cha Baylor cha Mfuko wa Watoto Tanzania (Baylor-Tanzania), asasi hiyo isiyo ya kiserikali, iliyosajiliwa chini ya muungano kati ya serikali ya Tanzania, USAID na Chuo cha Utabibu cha Baylor.

  Baylor – Tanzaniahufanya kazi Kanda ya Ziwa na Nyanda za juu Kusini, katika kituo cha kliniki ya watoto (Children’s Clinical Centers of Excellence (COEs)) kilichopo Mwanza (kilichojengwa kwa msaada wa Bristol Myers Squibb Fundation) na Mbeya (kilichojengwa kwa msaada wa mfuko wa Abbott). 

  Baylor Tanzania ni sehemu ya mtandao ulioenea Afrika: asasi hii anzilishi ya kimataifa ya kushughuikia masuala ya ukimwi wa watoto  (Baylor International Pediatric AIDS Initiative (BIPAI)), huendesha vituo vya kliniki za watoto na kliniki nyinginezo katika nchi kumi na mbili za jangwa la Sahara Afrika na vile vile Romania, na inajishughulisha na kutoa huduma za kinga ya afya ya mtoto, kimsingi HIV, kifua kikuu, malaria, ukosefu wa lishe na sababu za kawaida zinazosababisha magonjwa ya watoto. Watoto zaidi ya laki moja (100,000) na watu wazima wameshazipokea huduma za BIPAI tangu mwaka 1996, na kukifanya kuwa chuo kikuu kikubwa duniani kinachojihusisha na maendeleo ya afya ya mtoto.


  Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo, Bi. Tunu Kavishe, Mkuu wa mawasiliano na Huduma za jamii  wa Barclays Tanzania amesema, “Benki ya Barclays hujali umuhimu wa uraia kwa umakini na kutambua hilo kama ufunguo wetu wa kibiashara. 

  Tunapendezwa kufanya kazi pamoja na klabu ya vijana ya Baylor kuwapa nguvu vijana walioathirika na virusi vya ukimwi (HIV) na kuwa na uelewa chanya, kukuza mioyo yao na kuendeleza umuhimu wao kamili katika kupata ujuzi wa maisha, uzoefu mbalimbali, umuhimu wa utu uzima wa kuigwa na kazi maalumu, mwishowe kuwaongoza kukuza maendeleo yao ya kikliniki na kiakili katika muendelezo wa kuelekea utu uzima”.


   Mkurugenzi wa mradi kutoka Chuo cha Utabibu cha Baylor ambae hufanya kazi pamoja na vijana wa klabu Dk. Lumumba Mwita alisema “kuwapa kinga madhubuti ya virusi vya ukimwi vijana wanaopevuka huhitaji msaada mkubwa wa kijamii kutoka katika familia, vijana wenye umri sawa na wao na watu wazima wa mfano - kuwashawishi tiba halisia, kuwa wawazi, lishe bora na tabia nyingine za kiafya. 

  Vijana wanaoishi na virusi vya ukimwi (HIV) wana mahitaji yaomahususi lakini mahitaji hayo maranyingi hayafikiwi kwa sababu mbalimbali zikiwemo zile za kinga na mipango ya misaada ambayo mara nyingi hujengwa kwa watu wazima na kwa afya za watoto. Klabu ya Baylor hutoa elimu ya jinsi gani ya kuishi na virusi vya ukimwi na huwaaminisha  walengwa kwamba kuna maisha ya kuishi dhidi ya virusi vya ukimwi.

  Pia huwa ni sehemu ya kupata uhakiki, umri kamili wa kuanza mapenzi na maelezo ya afya ya uzazi, ujuzi wa maisha ukiwemo uongozi na maendeleo, utoaji maamuzi, kupambanua ujuzi, mawasiliano, miradi inayozalisha kipato cha ziada na mengine mengi. Aliongezea “tungependa kutanguliza shukrani zetu za dhati kwa  Benki ya Barclays Tanzania kwa kutambua umuhimu wa kufanya kazi na Baylor na kutusaidia katika fedha za kuendelea kujiendesha na kuwapatia ujuzi sahihi vijana”.


  Baylor Tanzaniahivi sasa husaidia Klabu Wanachama za Vijana zaidi ya mia sita (600) Kanda ya Ziwa na Nyanda za juu Kusini – namba hii inatarajiwa kuongezeka kadri watoto wanaoishi na virusi vya ukimwi kutambuliwa, kuandikishwa katika tiba na kuishi katika umri huo na zaidi. 

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Hai,Mh.Novatus Makunga akipokea msaada wa mbegu  za mahidi ya muda mfupi wa wananchi wa Hai hivi karibuni,uliotolewa na kampuni ya SEEDCO,kufuatia na baadhi ya wakazi wa Wilaya hiyo mashamba yao kukubwa na mafuriko na kupelekea uharibifu  mkubwa wa mazao yao.

  0 0

   Diwani wa kata ya Bulyanhulu wilayani Kahama Bw.Joseph Makoba akimkabidhi vitabu mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kakola  A, Bi.Joyce Lwanji kutoka kampuni ya simu za mikononi Tigo. Jumla ya vitabu elfu moja vilitolewa na kampuni ya Tigo katika  kuchangia elimu kwenye shule hiyo, kulia ni meneja wa Tigo kanda ya ziwa Bw. Joseph Mutalemwa.
   Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kakola A wilayani Kahama, Bi.Joyce Lwanji akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wake mara baada ya kupokea vitabu toka kampuni ya simu za mikononi Tigo jumla ya vitabu elfu moja vilitolewa na kampuini hiyo.
  Diwani wa kata ya Bulyanhulu wilayani Kahama Bw.Joseph Makoba akimkabidhi vitabu mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kakola  B, Bw.Raphael Kirega kutoka kampuni ya simu za mikononi Tigo. Jumla ya vitabu elfu moja vilitolewa na kampuni ya Tigo  katika  kuchangia elimu kwenye shule hiyo, kulia ni meneja wa Tigo kanda ya ziwa Bw. Joseph Mutalemwa.

  0 0


  *WATANZANIA NA WAKENYA WAINGIA NUSU FAINALI*
                                                                

   Jana usiku timu kutoka Kenya na Tanzania ziliwakilisha vizuzi  Afrika mashariki katika sehemu ya saba ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™. Timu ya Kenya ilifanikiwa kuzishinda timu nyingine na kufikia hatua ya mwisho ya ukuta wa pesa wa Guinness. Kenneth kamau na Wills Ogutu wote kutoka Nairobi wamefuzu nusu fainali pamoja na watanzania Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad ambao walipata nafasi ya pili jana usiku. 


  Timu hizi mbili kutoka Kenya na Tanzania sasa zina nafasi ya kuwakilisha Afrika mashariki na kushinda hadi dola za kimarekani 250,000 pamoja na kuvikwa taji la ushindi wa Pan-African, watakapoendelea hatua z juu zaidi. Timu hizi zitahitaji kujiandaa vizuri zaidi na kujiamini ili kufanya vizuri katika hatua ya nusu fainali.


  Timu zingine nne zitakutana katika robo fainali ijayo ili kuwania nafasi ya kuingia nusu fainali ya mashindano ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE.


  Usikose kuangalia robo fainali za Pan-African kupitia televisheni za ITV na Clouds TV ambapo timu za Africa Mashariki zinapokutana na timu na timu zingine kutoka Afrika Magharibi huku ukiburudika na kinywaji cha GUINNESS.


  Hakikisha kuufwatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali.

  -www.facebook.com/guinnesstanzania


  GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol.  Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku.  Tafadhali kunywa kistaarabu - Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.  0 0

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Bwa.Steve Gannon akionesha kizibo cha bia aina ya Serengeti Premium Lager chenye malekezo namna ya kujishindai zawadi mbalimbali,mbele ya wanahabari na baadhi ya washindi wa bahati nasibu waliowahi kujinyakulia zawadi mbalimbali kupitia promosheni ya bia hiyo.Pichani kati ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,Ephraim Mafulu wakiwa sambamba na mmoja washindi aitwaye Rahma,aliyewahi kujishindia piki piki kupitia promosheni za kinywaji hicho cha Serengeti Premium Lager.
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Bwa.Steve Gannon akionesha namna ya kutuma ujume wa promosheni ya WINDA NA USHINDE kwa kutuma ujumbe kupitia namba iliyowekwa maalum kwa promosheni hiyo,mbele ya wanahabari na baadhi ya washindi wa bahati nasibu waliowahi kujinyakulia zawadi mbalimbali kupitia promosheni ya bia hiyo.Pichani kati ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,Ephraim Mafulu wakiwa sambamba na mmoja washindi aitwaye Rahma,aliyewahi kujishindia piki piki kupitia promosheni za kinywaji hicho cha Serengeti Premium Lager.
   Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,Ephraim Mafulu “Kampeni na promosheni zetu zinalenga haswa kuwashukuru na kuwanufaisha wateja wetu,Winda na Ushinde itabadilisha maisha ya watu wengi.  Bia hii inatambua umoja na ushirikiano uliopo baina yetu na hivyo basi, tunazindua promosheni ambazo zawadi zake ni utoaji wa kweli na kuwafanya wateja wetu kujisikia kwamba wanadhaminiwa kwa njia moja au nyingine.,”alisemaBw. Mafuru.
   Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,Ephraim Mafulu akifafanua zaidi kuhusiana na promosheni hiyo ya WINDA NA USHINDE iliyozinduliwa leo ndani ya kiwanda cha kampuni hiyo,Temeke jijini Dar na kuhudhuriwa na  Mkurugenzi mkuu (Group Managing Director) Bw.Charles Ireland na Mkurugenzi mkuu wa Masoko na Ubunifu (Group marketing and Innovation Director) Ms. Debra Mallowah.Shoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,Bwa.Steve Gannon.
  Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye uzindu wa promosheni hiyo mapema leo,wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa SBL,Bwa.Steve Gannon alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu promosheni hiyo pia na pia kuwashukuru wateja wao wote ambao wamekuwa na wanaendelea kuwa nao.
  KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAZINDUA PROMOSHENI YA ‘WINDA NA USHINDE’  Kampuni ya bia ya Serengeti katika juhudi zake za kutambua na kuthamini wateja wake, leo imezindua promosheni ambayo inaendana na kampeni yake kuu inayoendelea ya TUPO PAMOJA.  Tupo Pamoja ni kampeni inayotambua wateja na kusherehekea nao pamoja.
  Mteja anaweza kujishindia kuanzia shilingi elfu kumi hadi million moja na pia anaweza kujipatia bia ya bure papo hapo.  Kampeni hii inatarajiwa kuendeshwa kwa miezi mitatu ijayo.
  Katika promosheni hii ya winda na ushinde, mteja atakaponunua bia ya  Serengeti ataweza kupata maelezo chini ya kizibo kama ilivyokuwa katika kampeni iliyopita ya vumbua hazi na chini ya kizibo.   Atapata namba maalum ambayo atatuma kwa njia ya sms kwa namba maalum na papo hapo atapata ujumbe utakaomjulisha ameshinda kiasi gani au kama amejipatia bia ya bure.   
  Kama kawaida ili kuhakikisha ushindi huu ni waukweli na uhakika, promosheni hii itasimamiwa na bodi ya Bahati nasibu, kampuni maahiri ya PWC na itaendeshwa na Push Mobile.
  Akiwakaribisha wageni na waandishi wa habari katika hafla fupi ya kuzindua promosheni hii ya Winda na Ushinde iliyofanyika katika kiwanda cha kampuni hiyo kilichopo Dar Es Salaam, Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Ephraim Mafuru alisema kwamba bia ya Serengeti lager ni bia inayojali na kuwatambua wateja wake kwa kiasi kikubwa. 
  “Kampeni na promosheni zetu zinalenga haswa kuwashukuru na kuwanufaisha wateja wetu,Winda na Ushinde itabadilisha maisha ya watu wengi.  Bia hii inatambua umoja na ushirikiano uliopo baina yetu na hivyo basi, tunazindua promosheni ambazo zawadi zake ni utoaji wa kweli na kuwafanya wateja wetu kujisikia kwamba wanadhaminiwa kwa njia moja au nyingine.,”alisemaBw. Mafuru.
  Uzinduzi wa promosheni hii pia ulihudhuri wa na Mkurugenzi mkuu (Group Managing Director) Bw.Charles Ireland na Mkurugenzi mkuu wa Masoko na Ubunifu (Group marketing and Innovation Director) Ms. Debra Mallowah.
  Wengine waliohudhuria ni Maofisa kutoka bodi ya Bahati Nasibu, maofisawa PWC na Push Mobile.  Pia kutoa walihudhuria washindi waliowahi kushinda zawadi mbalimbali katika promoshen za nyuma.

  0 0

  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo  nyumbani kwa Waziri wa zamani, Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na Mweka Hazina wa Taifa wa CCM wa zamani, Marehemu Alfred Tandau, aliyefariki dunia juzi jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alikokuwa  amelazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya tumbo. 
   Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezi  nyumbani kwa Waziri wa zamani, Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na Mweka Hazina wa Taifa wa CCM wa zamani, Marehemu Alfred Tandau, aliyefariki dunia juzi jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alikokuwa  amelazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya tumbo. 
   Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma KLikwete wakiwafariji wafiwa nyumbani kwa Waziri wa zamani, Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na Mweka Hazina wa Taifa wa CCM wa zamani, Marehemu Alfred Tandau, aliyefariki dunia juzi jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alikokuwa  amelazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya tumbo. 
   Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwet akiwa na watoto wa marehemu Alfred Tandau. Kulia kwake ni Bw. Henry Tandau na kushoto kwake ni Bw Julius Tandau. Hapo  nyumbani kwa marehemu aliyekuwa  Waziri wa zamani, Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na Mweka Hazina wa Taifa wa CCM wa zamani, Marehemu Alfred Tandau, aliyefariki dunia juzi jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alikokuwa  amelazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya tumbo. 
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, na Mama Salma Kikwete, wakitambulishwa kwa watoto wa Waziri wa zamani, Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na Mweka Hazina wa Taifa wa CCM wa zamani, Marehemu Alfred Tandau nyumbani kwa marehemu Magomeni jijini Dar es salaam walipofika kufariji wafiwa
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa ameongozana na mke wake Mama Salma Kikwete, wakipokelwewa  nyumbani kwa Waziri wa zamani, Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na Mweka Hazina wa Taifa wa CCM wa zamani, Marehemu Alfred Tandau, aliyefariki dunia juzi jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alikokuwa  amelazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya tumbo. PICHA NA IKULU

  0 0

  Wafanyakazi wilayani Makete wakiandamana kutoka ofisi za halmashauri ya wilaya kuelekea kwenye viwanja vya mabehewani kwenye sherehe za mei mosi 2013
  Wafanyakazi wakiingia katika viwanja vya mabehewani kwa maandamano

   Mwakilishi wa wafanyakazi akisoma risala kwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Mei Mosi
  Msomaji risala akimkabidhi risala mgeni rasmi
   Mtumishi kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya ya Makete Bw. Sanga akipewa zawadi ya ufanyakazi bora na mgeni rasmi
   Katibu tawala wilaya ya Makete Joseph Chota ambaye pia ni mgeni rasmi akisoma hotuba kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro kwenye sherehe za Mei Mosi wilaya ya Makete
   Kutoka kushoto ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Francis Chaula, diwani wa kata ya Iwawa Benjamin Mahenge na katibu wa CCM wilaya ya Makete, Miraji Mtaturu wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi
  Baadhi ya wafanyakazi wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi(Picha zote na mdauEdwin Moshi).

  0 0


  0 0


  Mkufunzi wa Warembo wa Redd's Miss Kibaha Rehema Uzuwiya akizungumza na warembo hawo wakati wa mazoezi yao yanayo endelea katika ukumbi wa Vijana Kinondoni.

  Warembo wa Redd's miss kibaha wakiwa katika pozi wakati wa mazoezi yao.

  Warembo watakao wania taji la Redd's Miss Kibaha wakiwa katika pozi wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika ukumbi wa vijana Kinondoni Dar es salaam picha nawww.burudan.blogspot.com

  0 0

  Ndugu zangu,

  ” Maisha yetu huanza kuisha siku tunapoanza kunyamaza kwenye mambo yenye maana”- Martin Luther King Jr.

  Leo Mei 3 ni Siku ya Uhuru wa Vyombo Vya Habari  Duniani. Hapa Afrika Mashariki, siku hii inaazimishwa kule Arusha kwa Kongamano lililoandaliwa na Mfuko wa  Ruzuku kwa Vyombo Vya Habari ( TMF).

  Macho na masikio yetu yanaelekezwa Arusha. Maana, kule Arusha kunatarajiwa kuzinduliwa kwa Itifaki ya Vyombo Vya habari.  Ndio, kuna  Azimio la Arusha linakuja, lakini hili linawahusu Wanahabari. Na kauli mbiu ya Siku hii ya Vyombo Vya Habari ni ” Mazingira  Mazuri na Salama ya Kufanyia Kazi Kwa Wanahabari wa Afrika Mashariki”.

  Ni ukweli, kuwa mwanahabari hawezi kuwa huru kwenye mazingira mabaya na yasiyo salama ya kufanyia kazi. Lakini, kuna maswali ya kujiuliza na kutafakari kwa kina. Ni  natumaini yetu walio kule Arusha wataifanya kazi hii ya kufikiri. Wafanye hivyo  ili Azimio watakalotoka nalo Arusha liwe lenye maana kwa wanahabari na umma unaowatumikia.Na mwanahabari anapokuwa hana uhuru wa kiuchumi kimsingi anawekwa kwenye mazingira mabaya na yasiyo salama ya kufanyia kazi.

  Hakika, Media ni mhimili muhimu sana katika nchi yeyote inayotaka kupiga hatua za kweli za maendeleo. Hata hivyo, katika nchi zetu hizi, media imefanywa kuwa adui wa watawala na hivyo basi, wakati mwingine kumekuwa na mahusiano ya uhasama, kuviziana  na kuwindana.

  Na kwa umma, media nayo ina sehemu yake ya lawama pale inaposhiriki kubomoa badala ya kujenga misingi ya Utaifa na Ujenzi wa Taifa Huru lenye nguvu za kiuchumi. Ni pale, inaponyamaza kwenye mambo ya maana na kushabikia yasiyo na maana, yenye kupotosha na kusababisha chuki na migongano katika jamii. Mathalan, udini, ukabila na mambo ya  abrakadabra kama vile ndoto za Babu wa Loliondo na Kikombe chake.

  Na hakika hili huchagizwa pale Media inapoingiliwa na wanasiasa, wafanyabiashara na hata baadhi ya viongozi wa dini. Ni matokeo ya Media kukosa uhuru wa kiuchumi. Ni wakati sasa wa vyombo vya habari na wanahabari kwa ujumla wake, kudai haki za kuwa na trade unions zake zenye meno. Kudai pia haki ya kupewa ruzuku na Serikali inayotokana na kodi za wananchi ili vyombo hivyo viweze kujijengea uwezo zaidi katika kuitumikia jamii. Media ya nchi haiwezi kuishi kwa kutegemea ruzuku inayotokana na walipa kodi wa Ulaya na Marekani. Ni fedheha pia.
  Ndugu zangu,

  Mengine tunayoyashuhudia siku hizi  ni  kwa baadhi ya vyombo vya habari  kushabikia mambo yasiyo na maana na kunyamazia yale ya msingi. Hii ni hatari kwa mustakabali wa nchi zetu hizi.

  Na tusije kusahau kuwa umma bado una imani kubwa kwa media. Hivyo, kuna umuhimu wa kuzingatia maadili.  Inahusu virtue, kwa maana ya maadili na kutenda yalo ya haki. Kutenda yalo mema. Mtu mwenye maadili mema utamwamini, ndivyo pia wasemavyo Waingereza; a virtuous person  is someone you can trust.


  Mzazi anapaswa kuwa a virtuous person, kiongozi wa kisiasa anapaswa kuwa a 

  virtuous person, kiongozi wa kidini anapaswa kuwa a virtuous person,  Mwandishi wa habari anapaswa kuwa a virtuous person. Vivyo hivyo kwa mwalimu.

  Ndugu zangu,
  Wanahabari wa Kenya kuelekea Uchaguzi Mkuu wao uliopita wameonyesha kuwa inawezekana, kwa Media kutanguliza maadili, kuachana na yasiyo na maana na kujielekeza kwenye yaliyo ya msingi na yenye kulinda Umoja na Utaifa wao.

  Na katika haya ya kushabikia yasiyo na maana, kuna wakati Julius Nyerere alitua Jomo Kenyatta Airport. Hapo aliongea na wanahabari. Ni miaka ile ya mwanzoni mwa Uongozi wa Rais Mwinyi baada ya Nyerere kung’atuka. Enzi za Mwinyi kuna mambo yaliyoonekana yana nafuu zaidi. Kukawa na minong’ono, kuwa  eti Julius Nyerere anamwonea wivu Mwinyi na ana mipango ya kumwondoa madarakani.

  Pale Jomo Kenyatta mwanahabari wa Kenya akamwuliza Nyerere: ” Mwalimu tunasikia unapanga njama za kumwondoa Mwinyi madarakani na hata Rais Moi wa hapa Kenya!”
  Julius Nyerere alijibu, ” Hivi wewe ukiambiwa mimi natembea na mama yako, utakimbilia kwenda kuandika habari hiyo?!”

  Naam, tunajifunza nini kwenye jibu hilo la Julius Nyerere?
  Kwamba kwenye falsafa tunaambiwa, kuwa unapoletewa jambo kuna matatu ya kuyaangalia na kuyazingatia: Udadisi wa uhalisia wa jambo lenyewe (Reasoning), Mantiki ( Logic) na Ulinganishi wa nadharia ( Metafisiki)

  Hivyo basi, unapokutana na mtu akakuambia kuwa alipokuwa akitembea  jana usiku, njiani alimwona mbwa akimtafuna mbwa mwenzake, basi, unachopaswa kufanya ni kutulia na kutafakari.

  Yumkini usiku huo mtu huyo alikuwa akitoka kwenye kilabu cha pombe, na kwenye ulevi wake, paka aliyemwona akigombana na paka mwenzake,  kwake ilikuwa ni mbwa anayemtafuna mbwa mwenzake!
  Happy Media Day!
  Maggid Mjengwa,
  Iringa.

  0754 678 252


  0 0

  Tamasha kubwa la kusifu na kuabudu linatarajia kufanyika leo katika ukumbi wa BCIC mbezi beach kuanzia saa 3 usiku hadi saa 12 alfajiri lenye lengo la kuliombea Taifa Amani, Upendo na uchumi. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mlezi wa Aflewo (Africa Let’s Worship) Askofu Fredy Kyara, alisema watanzania wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kwani hakuna kiingilio.

   Alisema kuwa, tamasha hilo litashirikisha kwaya mbalimbali kutoka makanisa 32 ya madhehebu tofauti katika kusifu na kuabudu. Askofu kyara alisema, tamasha hilo linafanyika kwa mara ya tatu tangia kuanzishwa hapa nchini mwaka 2011 na kuenea nchi zote za Afrika. “Tamasha hili limeboreshwa kwa kuongeza muiondombinu ya utendaji kazi, kwa kutanua wigo wa ushirikishwaji wa makanisa mengi,” alisema Kyara. 

   Aidha matasha mengine ya Aflewo, yanatarajia kufanyika nchi nzima kwa kufanyika kila mkoa, kwa mwaka huu litaanza kufanyika katika mikoa ya Mwanza, Moshi na Zanzibar na hatimaye Afrika yote.

  0 0

  HONGERA SANA KWA KUPIGA HATUA
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
 • 05/03/13--04:14: GARI INAUZWA


 •  
  1.MAKE: NISSAN X-TRAIL
  2.COLLOR: GRAY
  3.YEAR OF MANUFACTURE: 2002
  4.ENGINE CAPACITY: 1990
  5.FUEL: PETROL
  6:ADOMETER READING; 167537km
  7.TRANSMISSION: MANUAL
  8. CONDITION:NI NZURI SANA HAINA TATIZO LOLOTE IMETUMIKA NA MIMI MWENYEWE TANGU IJE TOKA JAPAN
  Kwa yeyote atakayeonyesha kuipenda tuwasiliane kwa simu number: 0712 00 66 61 inapatikana Dar es salaam

older | 1 | .... | 73 | 74 | (Page 75) | 76 | 77 | .... | 1904 | newer