Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI OMBENI SEFUE AKUTANA NA BALOZI WA CANADA NCHINI MHE ALEXANDRE LEVEQUE LEO

$
0
0

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) katika mazungumzo na Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe Alexandre Leveque aliyemtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo asubuhi. Balozi Leveque aliongozana na Mkurugenzi Mwandamizi na Mkuu wa Ushirikiano wa Canadian International Development Agency (CIDA), Bi Patricia McCullagh. Wa pili kushoto ni Balozi Dorah Msechu, Mkurugenzi katika Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa anayeshughulikia kurugenzi ya Nchi za Ulaya na Amerika, akifuatiwa na  ofisa dawati Bi Upendo Mwasha. Picha na Ikulu.

mtu mmoja ajirusha chini toka ghorofa ya 9 Concord hotel,kariakoo jijini dar.

$
0
0

Muda si mrefu huyu kaka kajirusha toka ghorofa ya 9 concord hotel kariakoo akaangukia kwenye hiyo taxi dah chanzo hata hakijulikani kapatwa na nn ni mfanya biashara anaitwa Shirima kakimbizwa hosp. Tunafwatilia kwa hundani na habari kamili itawajia hanzo. bofya hapa.

Zoezi la 2 na Freddy Macha

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL APOKEA VIFAA VYA MICHEZO KWA AJILI YA VIJANA WA HARAIKI WA MBIO ZA MWENGE KUTOKA BENKI YA NMB

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea sehemu ya vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh. Milioni 35, kwa ajili ya vijana wa Haraiki ya Mbio za Mwenge utakaowashwa Visiwani Pemba Mei 6, mwaka huu, kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa Benki ya NMB, Domina Feruzi, wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, jana Mei 2, 2013. Kushoto ni Meneja wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa benki hiyo, Elieza Msuya.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wageni wake kutoka Benki ya NMB, baada ya makabidhiano ya vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh. milioni 35 kwa ajili ya vijana wa Haraiki wa mbio za Mwenge unaotarajia kuwashwa Mei 6, mwaka huu Visiwani Pemba.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa Benki ya NMB, Domina Feruzi (wa pili kulia) Meneja wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa benki hiyo, Elieza Msuya (kulia) Ofisa Mahusiano wa benki hiyo, Doris Kilale (wa pili kushoto) na Huruma Mwaihomba, Ofisa Mahusiano wa benki hiyo, baada ya makabidhiano hayo.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Habari waalikwa kwenye sherehe ya upambaji maharusi Mei tano

$
0
0

NAIBU Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuki,(pili kulia). ametoa ufadhili kwa Kundi la Waandishi wa Habari wanaojishughulisha na ujasiriamali (Habari Group) kushiriki katika sherehe za kutimiza miaka kumi ya upambaji maharusi ya kampuni ya Maznat.

Kairuki ambaye pia ni mlezi wa Habari Group alitoa nafasi hiyo ya pekee kwa waandishi hao kuhudhuria sherehe hizo zitakazofanyika Mei 5 mwaka huu, Diamond Jubilee ambapo pamoja na mambo mengine itasaidia kujenga mtandao na kujifunza mambo mbalimbali katika tasnia ya ujasiriamali.

Mwenyekiti wa Habari Group, Mwanamkasi Jumbe alisema wanamshukuru kiongozi huyo, ambaye amekuwa ni msaada mkubwa kwa kikundi hicho.

Aliongeza kuwa tangu kikundi hicho kizinduliwe rasmi Machi 8 mwaka huu, wamekuwa wakipata msaada mkubwa wa ushauri na usimamizi wa karibu kutoka kwa Angellah, na kwamba ni kiongozi anayejua majukumu yake.

"Kwa sasa tunaandaa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanachama na hayo tunaanda chini ya msaada mkubwa wa Mheshimiwa Kairuki. Kuachana na mambo mengine, ni kiongozi mwenye msaada wa kipekee kwa jamii yote,"aliongeza Mwanamkazi.

Wanachama wa Habari Group kila mtu kwa nafasi yake alishukuru kwa ufadhili huo, na kwamba watatumia nafasi hiyo vizuri kwa ajili ya kutimiza ndoto zao za kujikwamua kiuchumi kutoka katika hali ngumu ya kimaisha.

"Kwa kuwa Habari Group pia inaanda shughuli mbalimbali, itakuwa ni fursa ya pekee kujifunza jinsi wenzetu wanavyofanya, changamoto na mafanikio, ili nasi kwa nafasi zetu tufikie malengo tuliyojiwekea,"aliongeza Katibu Msaidizi, Asha Bani.

Sherehe hiyo ya Maznat itahudhuria na wajasiliamali wa aina zote wakiwemo wa mapambo, urembo, washehereshaji katika matukio mbalimbali na wabunifu wa mitindo. 
 

mvua zetu za jijini dar atha yake ndio kama hivi..!

$
0
0
   

Balozi Dr. Sezibera afungua kongamano la siku mbili katika kuadhimisha Siku Uhuru vyombo vya Habari jijini Arusha.

$
0
0
Na. Mahmoud Ahmad Arusha.

Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Dr. Richard Sezibera leo amefungua rasmi kongamano la waandishi wa Habari Tanzania pamoja nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki katika kuadhimisha ya siku ya uhuru wa vyombo vya Habari Duniani uliobeba kauli mbiu “USALAMA NA MAZINGIRA BORA YA KUFANYIA KAZI KWA WAANDISHI WA HABARI NA WAARIRI AFRIKA YA MASHARIKI”

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kaongamano hilo la waandishi wa habari liliofanyika jijini Arusha katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Naura springs amesema kuwa kongamano hili la vyombo vya Habari pamoja na wamiliki lina umuhimu kwa sababu litaifanya jamii pamoja na serikali kujua nini umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari katika maendeleo ya nchi na jamii yote.

Amesema kuwa uhuru wa vyombo vya habari kwa kiasi kikubwa unajikita katika uhuru wa kutoa maoni na pamoja na uhuru wa kutoa habari hivyo katika kuelewa hilo vyombo vya habari vinatakiwa viwe vinafanya kazi zake pasipo kutegemea upande wowote ili kisije kuchochea au kuvunja amani ya nchi kama ilivyotokea miaka ya nyuma kwa nchini Rwanda na Burundi.

Aidha amesema kuwa kuna changamoto kubwa sana zinazozikumba vyombo vya habari hususani vyombo vya kijamii ambapo wanakuwa na mazingira magumu ya kutafuta habari na kufanya wakati mwingine waandishi kuwa katika mazingira hatarishi kwa maisha yao pamoja na hali mbaya ya kiuchumi inayopelekea kutoweza kufanya kazi kuendana na mabadiliko ya sayansi na Teknolojia ikiwepo kujiingiza katika mawasiliano ya mkongo wa kitaifa.

Kongamano la mwaka huu limeratibiwa na MISSA TANZANIA kwa kushirikiana na EAJA, Mfuko wa vyombo vya Habari Tanzania ( TMF), Muungano wa club za wandishi wa habari (TPC), Umoja wa Mataifa Tawi la Tanzania, Baraza la Habari Tanzania (MCA), Wamiliki wa Vyombo vya habari Nchini (MOAT) pamoj na kituo cha habari kwa wananchi TCIB na kudhaminiwa na Shirika la UNESCO.
Picha juu na chini baadhi ya washiriki wakifuatilia kongamano hilo sanjari na hotuba ya mgeni rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulongo akitoa salamu za Serikali wakati wa kongomano la siku mbili katika kuadhimisha siku Uhuru wa vyombo vya habari lililofanyika leo jijini Arusha.
Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen akitoa Ujumbe wa Pamoja wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Irina Bokovas kuhusiana na Siku ya Uhuru wa Habari Duniani ulioenda sambamba na Kongamano la Uhuru wa vyombo vya Habari katika nchini za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha.
Picha juu na chini ni Meza kuu na washiriki wa Kongamano la Uhuru wa Habari Duniani wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka aliyekuwa mwandishi wa habari na Mwenyekiti wa Iringa Press Club Marehemu Daudi Mwangosi aliyeuwawa mkoani Iringa wakati akitimiza majukumu yake ya kazi ya kila siku.
Mkurugenzi wa Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene (kushoto) akiwa na wadau pamoja na Balozi wa Sweden nchini Mh. Lennarth HJELMAKER (kulia) aliyeambata na mkewe katika kongamano hilo.
Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi Bi. Itika Mwangosi akiwa na mtoto wa mwisho wa marehemu katika Kongamano hilo.

Washiriki wa kongamano la siku mbili la Uhuru wa Habari Duniani wakijiandikisha kabla ya kuanza rasmi kwa mkutano wa Siku mbili katika kuadhimisha Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani linalofanyika jijini Arusha katika Hoteli ya Naura Springs.
Mgeni rasmi katika siku ya Uhuru wa Habari Duniani Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Dr. Richard Sezibera akiwasili na kusalimiana na viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulongo katika Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha kufungua Kongomano la siku mbili la Uhuru wa vyombo vya habari kwa wahariri na waandishi wa habari na wadau mbalimbali wa habari
Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen akisalimiana na Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi Dr. Richard Sezibera mara baada ya kuwasili katika Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha kufungua Kongamano la siku mbili la wahariri na wanahabari pamoja na wadau wa habari katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ulimwenguni.
Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Dr. Richard Sezibera (katikati) akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulongo (kushoto) pamoja na Katibu Mtendaji wa MOAT Bw. Henry Muhanika wakiingia ndani ya ukumbi wa mkutano wa Kilimanjaro katika Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha.
MC katika Kongamano la Uhuru wa Vyombo vya habari ulimwenguni Usia Nkoma kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akitambulisha meza kuu ya wageni katika kongamano hilo.
Meza Kuu ikiongozwa na Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi Dr. Richard Sezibera (wa pili kulia) na Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen (wa tatu kushoto).
Picha juu na chini Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi Dr. Richard Sezibera akihutubia na kufungua Kongamano la Siku Mbili linaloenda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani.
Pichani ni mmoja wa washiriki akionyesha bango lililokuwa na tukio la kuuwawa kwa Mwandishi wa Daudi Mwangosi ambalo limeandikwa" HABARI NI MUHIMU KATIKA UJENZI WA TAIFA, UKIMUUA MWANDISHI WA HABARI UMEUA DEMOKRASIA, HAKI NA MAENDELEO YA NCHI YAKO".
Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Dr. Richard Sezibera akikabidhi hundi ya Shilingi Milioni 5 kwa Mjane wa Marehemu Daudi Mwangosi Bi. Itika Mwangosi iliyotolewa na Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) kumsaidia kuendesha maisha yake.
Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Dr. Richard Sezibera na Mwenyekiti wa UTPC Tanzania Bw. Abubakari Karsani (kulia) kwa pamoja wakimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi Milioni 5 Mjane wa Marehemu Daudi Mwangosi Bi. Itika Mwangosi.
Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Dr. Richard Sezibera akizungumza na mtoto wa mwisho wa Marehemu Daudi Mwangosi mara baada ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 5 kwa mjane wa marehemu.
Mwenyekiti wa UNCG Yusuph Al Amin kutoka UNESCO akifuatilia mada mbalimbali wakati wa kongamano hilo la Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani.
Mama Rahma wa Ofisi za Unesco Tanzania na Usia Nkhoma wa UNIC Dar.
Msanii wa kughani mashairi Mrisho Mpoto akitoa ujumbe wa waandishi wa habari kwenye siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari mbele ya mgeni rasmi na viongozi mbalimbali wa mashirika ya umoja wa mataifa na Serikali.
Mgeni rasmi akimfungua plasta mdomoni mmoja wa wasanii wa Band ya Mrisho Mpoto kama ishara ya kuwapa uhuru waandishi wa habari kuzungumza kilio chao mbele ya mgeni rasmi kama ujumbe wa siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani.
Wasanii wa Mrisho Mpoto wakiimba kwa hisia kali kuelezea madhila wayapatayo waandishi wa habari wawapo kazini ikiwemo usalama wao katika kazi zao za kila siku.
Mzee Kassim Mapili akiongoza Band ya Mrisho Mpoto kutoa burudani mara baada ya kongamano hilo kufunguliwa.
Mkurugenzi wa Habari-Maelezo Bw.Assah Mwambene (kushoto) akisalimiana na Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi Dr. Richard Sezibera.
Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi Dr. Richard Sezibera akiteta jambo na Balozi wa Sweden nchini Mh. Lennarth HJELMAKER nje ya ukumbi wa mikutano wa Kilamanjaro katika Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha.
Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi Dr. Richard Sezibera akiagana na Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen ambao ndio wafadhili wa Kongamano hilo.
Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi Stella Vuzo (katikati) akiagana na Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi Dr. Richard Sezibera mara baada ya kuzindua Kongomano la wahariri wa vyombo vya habari pamoja na waandishi ikiwa ni mwendelezo wa sherehe za Siku ya kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya habari ulimwenguni.
Maveretans wa Tasnia ya Habari wakiwa na Mkurugenzi wa Misa Tan Tumaini Mwailege ( wa tatu kushoto) na Wa kwanza Kushoto ni Mama Eda Sanga, Mama Rosemary Haji wa UNESCO, Leila Shekha na Theophil Makunga wakifurahi baada ya kukutana katika Kongamano hilo.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wakongwe katika tasnia ya Habari walioshiriki katika Kongamano hilo.

Airtel yatangaza mshindi wa million 50 wa promosheni ya Amka millionea

$
0
0

 Mwandishi wa Clouds TV Austin Bayadi ( wakwanza kushoto) akibonyesha kitufe cha komputa wakati wa droo kubwa ya mwisho ya kumtafuta mshindi wa shilingi million 50 wa promosheni ya Amka millionea ambapo bwana Layakal Akbar Thawer mkazi wa Dar es salaam aliibuka mshindi wa promotion hiyo. Wakishuhudia ni meneja uhusiano wa Airtel  Jackson Mmbando(aliyekaa katikati) akifatiwa na mwakilishi wa bodi ya michezo ya Bahati Nasibu Emmanuel Ndaki akifatiwa na Afisa masoko wa Airtel  Khalila Mbowe.
 Meneja Uhusiano wa Airtel  Jackson Mmbando(katikati) na Afisa masoko wa Airtel  Khalila Mbowe kwa pamoja wakionyesha droo ya kumtafuta mshindi wa millioni 50 wa Amka millionea inavyotafuta mshindi wakati wa droo hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel Moroco na kushuhudiwa na Waandishi wa habari, akishuhudia kulia ni mwakilishi wa bodi ya michezo ya Bahati Nasibu Emmanuel Ndaki
Meneja Uhusiano wa Airtel  Jackson Mmbando(aliyekaa katikati) akiongea na wandishi wa habari (hapo pichani) wakati wa droo kubwa ya mwisho ya kumtafuta mshindi wa shilingi million 50 wa promosheni ya Amka millionea ambapo bwana Layakal Akbar Thawer mkazi wa Dar es salaam aliibuka mshindi wa promosheni hiyo.  Kushoto ni mshindi wa million 15  wa promosheni ya Amka milionea bwana Juma Ibrahim Hiza mkazi wa Dar es Saalam na kulia ni  mshindi mwingine wa shilingi milioni 15 Bwana  Adnan Ayub Khan mfanyabiashara  Simiyu.


===============  =======  =========
Airtel yatangaza mshindi wa million 50 wa promosheni ya Amka millionea

·         Zaidi ya washindi 1458 wazawadiwa pesa taslimu zenye thamaniya shilingi million 626 Hadi mwisho wa promosheni hii.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imechezesha droo ya mwisho ya promosheni ya Amka millionea na kumzawadia mshindi  wa droo hiyo kitita cha shilingi million 50.

Droo hiyo kubwa na ya mwisho ilifanyika katika makao makuu ya Airtel morocco na kushuhudia na waandishi wa habari ambapo mkazi wa Kariakoo Dar es Salaam  Bwana Layakal Akbar Thawer  mwenye umri wa 60  mafanyabiashara wa duka la rangi aliibuka kuwa mshindi wa millioni 50 na kutangazwa rasmi kuwa mshindi.

Akiongea wakati wa droo hiyo, Mkuu wa kitengo cha Masoko wa Airtel Levi Nyakundi alisema,  Mpaka sasa Airtel kwa kupitia promosheni ya Amka millionea imewazawadia watanzania na wateja wengi nchini. leo tunashuhudia bwana Akbar akiibuka kuwa mshindi wa pesa taslimu shilingi million 50 kupitia promosheni hii ya Amka millionea na Airtel. 

Hii inathibitisha thamira yetu ya kutuoa huduma bora na bei nafuu huku tukiendelea kuwazawadia watanzania na wateja wetu kwa kupitia promosheni mbalimbali ikiwemo hii ya Amka millionea Tunaahiidi kuendelea kuboresha huduma zetu na kuhakikisha tunawafikia watanzania wengi zaidi,  mpaka sasa kwa kupitia huduma ya Airtel yatosha wengi wamepata unafuu wa gharama za mawasiliano na kuwezeshwa kupiga simu kwenda mitandao yote nchini na kushuhudia kuwa kweli Airtel yatosha. 

Tunaamini kwa kuendelea kuongeza ubunifu katika huduma zetu na  kuwazawadia wateja wetu kwa kupitia promosheni mbalimbali pamoja na huduma bora zikiwemo za kibenki kupitia Airtel money na huduma ya internet ya kasi zaidi ya 3.75G wateja wataendelea kupata suluhusho la mawasiliano na za kimtandao zilizo bora , za uhakika na gharama nafuu aliongeza Nyakundi.

Akiongea kwa njia ya simu mshindi wa shilling million 50 bwana Layakal Akbar Thawer alisema “ mimi nimekuwa mteja wa Airtel kwa miaka 7 sasa na nafurahia huduma zao, napenda kuwambia watanzania washiriki promosheni hizi nao wananafasi ya kuibuka washindi. 

Promosheni ya  Amka milionea ilizinduliwa rasmi mwenzi December mwaka jana na kuongezewa muda wake mwenzi machi mwaka huu, mpaka sasa wateja zaidi ya1458 na pesa taslimu zenye thamani ya zaidi ya shilingi  million 626 zimezawadiwa kwa washindi walioibuka kutoka katika mikoa mbalimbali nchini.

Mshindi mwingine wa shilingi million 50 alipatikana na kuzawadia mwenzi watatu naye ni Mwalimu wa shule ya msingi na mkazi wa manyara kiteto bwana Grayson Safieli Kabora , huku washindi wa shilingi million 15 wakiwa ni pamoja na  Juma Ibrahim Hamza  umri wa miaka 30 na mkazi wa kawe  Dar es Saalam na Adrian Ayub khan umri wa miaka 25 mfanyabiashara Simiyu

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WASHIKADAU WA SMART PARTNESHIP LEO IKULU

RAIS KIKWETE AMPOKEA RAIS WA SERIKALI YA MPITO YA MADAGASCAR ALIETUA DAR JIONI HII

$
0
0
Rais Dkt . Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Rais wa Serikali ya Mpito ya Madagascar Mhe. Andry Rajoelina aliyewasili jioni ya leo Ijumaa Mei 3, 2013 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili hapa nchini,katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.PICHA NA IKULU

FASHION WEEK ZANZIBAR GEARS UP FOR FIRST EDITION

$
0
0



First-ever event celebrating local and locally inspired fashion design in Zanzibar set to premiere.

The  all-new Fashion Week Zanzibar will take over Zanzibar in a celebration of local fashion and unique East African design. The new initiative is dedicated to showcasing fashion created in or inspired by the beautiful island of Zanzibar, Tanzania. 

The island’s homegrown fashion industry has been developing in exciting new ways in recent years. One-of-a-kind designs pulling from the varied influences of Zanzibari culture and island life, mixed with the brightly coloured patterns of kanga and kitenge, create a strong sense of place and culture in the local fashion industry.  

The event is founded and organized by photographer and filmmaker Javed Jafferji, internationally renowned designer Farouque Abdela, and budding photographer Adnan Abbas. “We decided to celebrate Zanzibar’s up-and-coming fashion and create a festival dedicated to our one-of-a-kind fashion flavor,” says Jafferji. “The decision was made on the spur of the moment and the whirlwind hasn’t stopped since.” 

 “We hope to encourage the local fashion industry and empower young designers,” says Abdela. As a part of the community, organizers say the event will continue to grow and shape the potential of this promising industry in Zanzibar’s future. 

For up-to-the-minute information and updates, please visitwww.fashionweekzanzibar.com or on Face book see the following link 


BIG DAY FOR IBF, GHAHA, NIGERIA AND AFRICA

$
0
0

IBF/AFRICA – SATURDAY 04 MAY, 2013 – DAR ES SALAAM, TANZANIA Ghanaian fighting machine and BEIJING 2008 Olympiad Issa Samir becomes the first ever Ghanaian “IBF Youth Champion of the World” after stopping the Georgianhandsomely true man Robison Omsarashvili 1 minute 29 seconds in round 3 at the Accra National Sports Stadium last night.
 Cheered on by thousands of Ghanaians who thronged the stadium from all walks of life, Samir lured the handsomely Georgian to his much anticipated “killer punches”. He peppered him with his telling jabs while dancing like a butter fly (Muhammad Ali’s style) as thousands of Ghanaians in attendance including several ministers and Nigerian Ambassador to Ghana cheered him throughout the rumble.
 Every punch that BEIJING 2008 Olympiad Samir threw was calculated to do damage to the handsomely Georgian and it became obvious that his team had the perfect game plan.  Charming the Georgian with his telling jabs so as to lure him to his WEB, Samir’s fighting speed and power was awesome in that Robison could hardly see his punches coming.
 As the Ghanaians kept counting when he was administering his lethal punches tearing the handsomely Georgian, Samir’s huge right drove straight to Robison’s jaw and sent him crashing on the canvas with the sound of the falling tree! It was all over even before referee May Mensah Akakpo of Ghana started counting!
 In another epic rumble of the evening, Princess Helen Joseph of Nigeria became the Champion of the “IBF Intercontinental Featherweight Female Title” after humiliating the beautiful Mariana Gulyas from Hungary in the shortest fight in history.  As thousands of boxing fans (many from Nigerian community in Ghana and other who arrived by hired busses from Nigeria, including their Ambassadot to Ghana ) cheered her, Helen's brinkmanship of the game proved her rightful Princess role on the mantles of the IBF Intercontinental Featherweight division after stopping te beautful Hungarian 23 seconds in round one.          
 AND! The man who is touted as the next Sugar Ray Leonard in the making Albert Mensah proved his prowess in boxing as a professional sport after beating his “arch-rival” and boatful Ben Odamettey. It was really drama as groups from each camp danced and beating their drums as the bout progressed on.
 Mensah’s articulated style and strength became obvious as the rumble progressed to Odamattey’s anguish as if he wanted to teach “the Bad Boy on the Block” a lesson or two! The two made the stadium live with drums and dance from their camps but as it is always said in boxing, it was Albert Mensah who had the “last laugh” after becoming the “IBF Continental Africa Jr. Welterweight” champion by TKOed Odametey  in round 7. Years from now as they judge his performance, historians would begin at this stage when he assumed his mantles as the “IBF Continental Africa Jr. Welterweight” champion!
 Thumb up to both GoldenMike Boxing Promotions Syndicate, Ghana and Nigeria for the excellent rumble. This put the Ghana way ahead of others in the continent as it consolidates its role as the “boxing powerhouse”.
 Harrah to IBF as it continue its “top dog” position in boxing as a professional sport. Indeed, African professional boxing has “come of age”.

RAIS ANDRY RAJOELINA WA MADAGASCAR ATUA DAR KWA MAJADILIANO NA RAIS KIKWETE MEI 3, 2013

RAIS ANDRY RAJOELINA KATIKA ZIARA YA KIKAZI NCHINI TANZANIA

$
0
0

PICHA NA IKULU.
ra2
Rais wa Serikali ya Mpito ya Madagascar Mheshimiwa Andry Rajoelina amewasili mjini Dar Es Salaam jana jioni  , Ijumaa Mei 3, 2013 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. 
Amepokelewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere mjini Dar Es Salaam na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. 

Viongozi hao wanatarajiwa kufanya  mazungumzo baadaye leo Ikulu, Dar Es salaam.
Rais Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi yaa Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Anakutana na Rais Rajoelina kwa mara ya tatu sasa, mara ya kwanza ikiwa ni mwezi Desemba mwaka jana, na baadaye mwezi Januari  mwaka huu.

Rais Kikwete alipokutana mara ya mwsho na Rais huyo wa serikali ya mpito ya Madagascar alifanikiwa kumshawishi akubaliane na mapendekezo ya nchi za SADC kuwa asigombee kwenye uchaguzi mkuu utaofanyika mwaka huu kama njia ya kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini humo.

Rais Kikwete awali ya hapo aliweza pia kumshawishi  Rais wa zamani wa Madagascar Mhe Marc Ravalomanana  asigombee katika uchaguzi  mkuu huo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
03 Mei, 2013

NAOMBA MNICHAGUE KAMA MWANAMUZIKI BORA WA RAGGA /TANZANIA

$
0
0

Mambo vipi watu wangu naomba mnipe tough tunichagua kama mwanamuziki wa ragga nimefanyikisha kuingiza ngoma yangu ya PUSH DEM kwenye kinywang'anyilo cha KILIMANJARO MUSIC AWARD , nipigie kura yako kwa kutumia simu ya mkononi andika BW4 kisha tuma kwenda namba 15345 utakuwa umeniwezesha kushinda tuzo hiyo ahsante tusisahau kula vyakula vya asili kama vile ugali wa mtama na matunda matuna pamoja na mboga za majani 
one love wote

ngoma hii hapa ilioingia kwenye tuzo


BARCLAYS TANZANIA YATOA SHS. 61 MILLIONI KWA BAYLOR TANZANIA KUSAIDIA VIJANA WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI (HIV/AIDS)

$
0
0

Mkuu wa Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa Benki ya Barclays Tunu Kavishe,akikabidhi hundi ya Sh 61 Milioni kwa Mkurugenzi wa Mradi wa Chuo cha Utabibu  Baylor Dk Lumumba Mwita(kushoto)wakati wa makabidhiano yaliyofanyika  jijini Dar es Salaam jana,ambapo fedha hizo zitasaidia vijana wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.
===========  =======  =======


Benki ya Barclays Tanzania jijini- Dar Es Salaam imetangaza udhamini wa shillingi za kitanzania milioni 61 (TZS 61,000,000) kusaidia klabu ya Baylor Tanzania iliyoundwa kwa vijana wa umri wa kati wanaoiishi na virusi vya ukimwi na sehemu ya Chuo cha Utabibu cha Baylor cha Mfuko wa Watoto Tanzania (Baylor-Tanzania), asasi hiyo isiyo ya kiserikali, iliyosajiliwa chini ya muungano kati ya serikali ya Tanzania, USAID na Chuo cha Utabibu cha Baylor.


Baylor – Tanzaniahufanya kazi Kanda ya Ziwa na Nyanda za juu Kusini, katika kituo cha kliniki ya watoto (Children’s Clinical Centers of Excellence (COEs)) kilichopo Mwanza (kilichojengwa kwa msaada wa Bristol Myers Squibb Fundation) na Mbeya (kilichojengwa kwa msaada wa mfuko wa Abbott). Baylor Tanzania ni sehemu ya mtandao ulioenea Afrika: asasi hii anzilishi ya kimataifa ya kushughuikia masuala ya ukimwi wa watoto  (Baylor International Pediatric AIDS Initiative (BIPAI)), huendesha vituo vya kliniki za watoto na kliniki nyinginezo katika nchi kumi na mbili za jangwa la Sahara Afrika na vile vile Romania, na inajishughulisha na kutoa huduma za kinga ya afya ya mtoto, kimsingi HIV, kifua kikuu, malaria, ukosefu wa lishe na sababu za kawaida zinazosababisha magonjwa ya watoto. Watoto zaidi ya laki moja (100,000) na watu wazima wameshazipokea huduma za BIPAI tangu mwaka 1996, na kukifanya kuwa chuo kikuu kikubwa duniani kinachojihusisha na maendeleo ya afya ya mtoto.


Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo, Bi. Tunu Kavishe, Mkuu wa mawasiliano na Huduma za jamii  wa Barclays Tanzania amesema, “Benki ya Barclays hujali umuhimu wa uraia kwa umakini na kutambua hilo kama ufunguo wetu wa kibiashara. Tunapendezwa kufanya kazi pamoja na klabu ya vijana ya Baylor kuwapa nguvu vijana walioathirika na virusi vya ukimwi (HIV) na kuwa na uelewa chanya, kukuza mioyo yao na kuendeleza umuhimu wao kamili katika kupata ujuzi wa maisha, uzoefu mbalimbali, umuhimu wa utu uzima wa kuigwa na kazi maalumu, mwishowe kuwaongoza kukuza maendeleo yao ya kikliniki na kiakili katika muendelezo wa kuelekea utu uzima”.


 Mkurugenzi wa mradi kutoka Chuo cha Utabibu cha Baylor ambae hufanya kazi pamoja na vijana wa klabu Dk. Lumumba Mwita alisema “kuwapa kinga madhubuti ya virusi vya ukimwi vijana wanaopevuka huhitaji msaada mkubwa wa kijamii kutoka katika familia, vijana wenye umri sawa na wao na watu wazima wa mfano - kuwashawishi tiba halisia, kuwa wawazi, lishe bora na tabia nyingine za kiafya. Vijana wanaoishi na virusi vya ukimwi (HIV) wana mahitaji yaomahususi lakini mahitaji hayo maranyingi hayafikiwi kwa sababu mbalimbali zikiwemo zile za kinga na mipango ya misaada ambayo mara nyingi hujengwa kwa watu wazima na kwa afya za watoto.

 Klabu ya Baylor hutoa elimu ya jinsi gani ya kuishi na virusi vya ukimwi na huwaaminisha  walengwa kwamba kuna maisha ya kuishi dhidi ya virusi vya ukimwi. Pia huwa ni sehemu ya kupata uhakiki, umri kamili wa kuanza mapenzi na maelezo ya afya ya uzazi, ujuzi wa maisha ukiwemo uongozi na maendeleo, utoaji maamuzi, kupambanua ujuzi, mawasiliano, miradi inayozalisha kipato cha ziada na mengine mengi. Aliongezea “tungependa kutanguliza shukrani zetu za dhati kwa  Benki ya Barclays Tanzania kwa kutambua umuhimu wa kufanya kazi na Baylor na kutusaidia katika fedha za kuendelea kujiendesha na kuwapatia ujuzi sahihi vijana”.


Baylor Tanzaniahivi sasa husaidia Klabu Wanachama za Vijana zaidi ya mia sita (600) Kanda ya Ziwa na Nyanda za juu Kusini – namba hii inatarajiwa kuongezeka kadri watoto wanaoishi na virusi vya ukimwi kutambuliwa, kuandikishwa katika tiba na kuishi katika umri huo na zaidi.


DKT. MWINYI AZINDUA BODI MPYA YA NHIF

$
0
0
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Hamis Mdoe alipowasili kuindua Bodi mpya ya Wakurugenzi wa NHIF, leo kwenye Hoteli ya Courty Yard, Sea View, Dar es Salaam. Wengine ni Mwenyekiti mpya wabodi hiyo, Balozi Ali Mchumo (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba na Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Regina Kikoli.
 Wakurugenzi wa NHIF, wakipiga makofi wakati Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Mwinyi alipokuwa akiingia kuzindua bodi hiyo.
Dk. Mwinyi akihutubia wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo.Kulia ni Mwenyekiti wa bodi hiyo, Balozi Mchumo.
 Baadhi ya mameneja wa Mikoa wa NHIF, na maofisa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa bodi hiyo.
 Mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo, Balozi Mchumo (kushoto) akimshukuru Waziri, Dk. Mwinyi kwa kuzindua bodi hiyo.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Humba.
 Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba akitoa maelezo kuhusu utendaji wa mfuko huo,  Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Regina Kikoli
 Mwenyekiti mpya wa Bodi ya NHIF, Balozi Ali Mchumo akuhutubia wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi (wa nne kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya ya NHIF. Kutoka kushoto ni Mwanaidi Mtanda,Donnan Mmbando, Mwenyekiti Balozi Ali Mchumo, Mohammed  Hashim, Charles Kajege, Dk. Ali Mohammed na Naibu Katibu Mkuu wa wa wizara hiyo, Regina Kikoli.Waliosimama ni Mkurugenzi Mkuu, Emmanuel Humba (kulia na Naibu Mkurugenzi Mkuu, Hamis Mdoe.


 Waziri Dk. Hussein Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi pamoja na wakurugenzi wa NHIF.
 Waziri, Dk. Hussein Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mameneja wa NHIF wa mikoa.
 Waziri, Dk. Hussein Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mameneja wa NHIF wa mikoa.
Waziri, Dk. Hussein Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mameneja wa NHIF wa mikoa.
Dk.Mwinyi akibadilishana mawazo na Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo, Balozi Ali Mchumo (kushoto) pamoja na Mjumbe wa bodi hiyo, Mohammed Hashim.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Regina Kikoli 9kulia) akiagana na Balozi Ali Mchumo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG


Na Grace Michael.

WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi amesema ni wakati muafaka sasa kwa kuwa na chombo kimoja kitakachokabidhiwa jukumu la kusimamia bima ya afya kwa Watanzania badala ya kushughulikiwa na taasisi nyingi kama ilivyo hivi sasa.

Dk. Mwinyi ameyasema hayo Dar es Salaam leo wakati akizindua bodi mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambapo ameitaka bodi hiyo kuangalia uwezekano wa kuanzisha mjadala wa kuundwa kwa chombo kimoja kitakachosimamia huduma za bima ya afya ili kuwafikia watanzania wote katika utaratibu wa kuchangia kabla ya kuugua.

“Hadi sasa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeonesha mafanikio makubwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kusimamia huduma za afya hali inayonishawishi kuwa na chombo kimoja,” alisema Dk. Mwinyi.

Alisema kuwa Serikali inatambua wingi wa mifumo na taasisi zinazojihusisha na huduma za bima ya afya na lengo lililopo ni kuhuishwa ili kuimarisha mfumo wa uchangiaji wa huduma za afya ambapo kwa sasa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umekasimiwa mamlaka ya kuendesha Mfuko wa Afya ya Jamii utakaoangalia namna nzuri ya kupanua wigo.

Akizungumzia mchango wa NHIF katika uboreshaji wa huduma za matibabu vituoni, alisema kuwa pamoja na juhudi zinazofanywa na  Mfuko huo angependa kuona Mfuko ukijikita katika uwekezaji unaolenga uboreshaji wa huduma za afya na si vinginevyo, hivyo akaiagiza bodi mpya kuhakikisha inaagalia na kuurejea upya utaratibu wa mikopo ya vifaa tiba na ukarabati wa majengo ili watoa huduma wachangamkie zaidi fursa hiyo.



Dk. Mwinyi pia hakusita kuzungumzia mahusiano mazuri ya kazi baina ya bodi, menejimenti na watumishi wa Mfuko ambapo alisema kuwa Mfuko mpaka sasa umefanikiwa kwa kiwango kikubwa kujenga misingi bora ya uhusiano mwema wa kazi miongoni mwa watendaji wake ambao wamekuwa ni mfano wa kuigwa na taasisi zingine hivyo akasisitiza hali hiyo kuendelezwa ili kuongeza zaidi ufanisi wa utoaji huduma.

Naye Kaimu Mkuu wa Wizara ya Afya, Regina Kikuli aliiambia bodi hiyo kuwa jukumu walilokabidhiwa ni kubwa kwa kuwa linagusa moja kwa moja afya za wanachama na watanzania kwa ujumla hivyo ni vyema bodi ikaliona hilo na kuhakikisha inakuja na mbinu mpya za kuhakikisha inaimarisha na kuboresha Mfuko huo ili uweze kufikisha malengo yake ya kuwahudumia watanzania wote.

Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo, Balozi Ali Mchumo aliahidi kuwa kazi aliyokabidhiwa kwa kushirikiana na wajumbe wenzake wataifanya kwa uaminifu mkubwa na kwa kutumia uwezo wao wote ili kuhakikisha Mfuko huo unawasaidia watanzania wote.

Akitoa maelezo ya utangulizi Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Emanuel Humba alisema kuwa moja ya mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Mfuko kwa sasa ni watanzania wengi kutambua umuhimu wa bima ya afya hivyo Mfuko unafanya kila jitihada ya kuhakikisha inafikia watanzania wengi zaidi na kukabiliana na changamoto zote zilizopo ili lengo la afya bora kwa wote liweze kufikiwa.
Ciooo

mvua kubwa yaitikisa kyela

$
0
0

Na Edwin Moshi, Kyela 

WANANCHI  wa Tarafa ya Ntebela wilayani Kyela mkoani Mbeya wapo hatarini kukumbwa na baa la njaa sambamba na kukosa mahala pa kuishi kutokana na mazao yao pamoja na nyumba zao za kudumu kusombwa na mvua za mafuriko yaliyotokea  siku tatu mfululizo na kuleta maafa makubwa kwa wakazi wa Tarafa hiyo,

Kauli hiyo ilitolewa na Afisa mtendaji wa kata ya Makwale Tarafa ya Ntebela Evance Mwaipopo wakati akizungumza na mtandao huu ulipotembelea katika Tarafa hiyo mara baada ya kutokea mafuriko hayo,ambapo alidai kuwa mvua hizo za mafuliko zimeleta maafa makubwa kwa wakazi wa Kata hiyo na Tarafa kwa ujumla,

Alisema kuwa mvua hizo zilizoleta mafuliko yaliyosababisha baadahi ya mito ukiwema mto Lufilyo kuhama katika njia zake za asili na kupasua kuelekea katika makazi ya watu na kusababisha maafa makubwa ya kuharibu nyumba zaidi ya 200,na mazoa ya chakula ya muda mfupi kama mpunga,mihogo na viazi,na mazao ya muda mrefu kama michikichi,miembe na miti mingine ya matunda,ambayo yote imesombwa na maji,



Awali aliongeza kuwa kulitokea na mafuliko kama hayo yaliyoleta maafa ambapo yaliharibu mazao kama hayo pamoja na makaburi 30 na jengo la Kanisa  la Kiinjili la Kilutheri Tanzania pamoja na ofisi ya Kijiji cha Ngeleka one,ambavyo vyote vilisombwa na maji kufuatia mafuliko hayo,

‘’Ni kweli  wananchi wa tarafa hii wapo katika hatari ya kukubwa na baa la njaa kufuatia kukumbwa na maafa haya na wengine wakikosa makazi ya kudumu kutokana na nyumba zao kusombwa na maji,lakini taarifa za maafa haya tumezipeleka serikalini ili kujua namna watakavyo weza kuwasaidia waathirika hao’’alisema Mwaipopo,

Diwani  wa kata ya Makwale Alico Kasyupa kwa upande wake alisema kuwa mafuliko hayo yalianza kwenye kata yake ambapo aliwaamuru wakaza wa kata hiyo waliojenga pembezoni mwa mto huo kuyahama makazi hayo ambapo tayali zoezi hilo limefanyika huku wengine walilazimika kubomoa nyumba zao na kuzijenga katika maeneo ya mwinuko ili wasikumbwe na mafuliko hayo,

Alisema kuwa hivi sasa mvua hizo za mafuriko zimeendelea kuleta maafa makubwa katika kata zingine hususani Tarafa nzima ya Ntebela huku idadi ya waathirika ikiongezeka kutokana na nyumba zao kubomoka ikiwa ni pamoja na mazao ya chakula yaliyokuwa tayari yameanza kukomaa,huku huduma za usafiri kutoka Ipinda Matema zikisimama,

Aliongeza kuwa Serikali Wilayani Kyela imepata taarifa ya uwepo wa maafa hayo na inafanya juhudi za kujua namna ya kukabiliana na maafa hayo ikiwa ni pamoja na kuurudisha mto huo katika njia yake ya asili ili usiendelee kuleta maafa zaidi,

Wananchi wa Tarafa hiyo kwa upande wao wameilalamikia Halmashauri ya wilaya hiyo kwa kuwa wazito kulitafutia ufumbuzi suala hilo,huku wakiendelea kuteseka bila msaada kutoka katika Serikalini,na kwamba wameitaka Serikali wilayani hapa kuliangalia kwa jicho la tatu tatizo hilo ili kujua ni namna gani watawasaida wananchi waliokumbwa na maafa hayo,

Gala Dinner ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari duniani iliyoambatana na Uzinduzi wa Mfuko wa Mwangosi.

$
0
0

Mkurugenzi wa MISA-TAN Bw. Tumaini Mwailenge akizungumza na waalikwa kwenye Gala Dinner ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa habari Duniani iliyoenda sambamba na uzinduzi wa Mfuko wa Mwangosi utakao kuwa ukisaidia waandishi wa habari pindi wapatapo matatizo wakiwa kazini. Kushoto ni Mzee Kassim Mapili wa Mjomba waliosherehesha usiku huo kwa buradani ya aina yake.(Picha na Dewji Blog).
Mmoja wa waandishi wa siku nyingi kwenye tasnia ya habari ambaye pia ni Mwanaharakati wa kutetea haki za Wanawake Bi. Leila Sheikh akisoma wasifu wa Marehemu Daudi Mwangosi wakati wa hafla hiyo.

Mgeni rasmi kwenye Gala Dinner ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari duniani ulioenda sambamba na uzinduzi wa Kitabu kilichoandaliwa na Media Council Tanzania (MCT) pamoja na Kitabu cha Uhuru wa Vyombo vya Habari Kusini mwa Jangwa la Afrika Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akitoa salamu za Rais Kikwete za Pongezi kwa wanahabari Tanzania kwa kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari Duniani ambapo Serikali imeahidi kushirikiana na wanahabari bega kwa bega kwa mustakabali wa kuboresha tasnia hiyo.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akizindua Ripoti ya Habari hapa nchini ya mwaka 2012 iliyoandaliwa na Media Council of Tanzania (MCT) aliyeshika kitabu hicho ni Afisa Mipango Mwandamizi wa Taasisi ya Media Council of Tanzania (MCT) Bi. Alakok Mayombo na Mjumbe wa MCT Bw. Allan Lawa na MC wa Gala Dinner hiyo Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania Jane Mihanji.
Sasa imezinduliwa rasmi.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene, Mwenyekiti wa Misa-Tan Bw. Mohammed Tibanyendera na mwakilishi wa Ubalozi wa Ireland kwa pamoja wakizuindua Kitabu cha Uhuru wa Vyombo vya Habari Kusini mwa Jangwa la Afrika kilichandaliwa na MISA katika Gala Dinner ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akionyesha kitabu "SO THIS IS DEMOCRACY" mara baada ya kukizindua rasmi.



Baadhi ya Wanahabari walioshiriki kwenye Gala Dinner ya siku ya Uhuru wa Habari iliyoenda sambamba na Uzinduzi wa Mfuko wa Mwangosi kusaidia waandishi wa habari ambao wamepata matatizo wakiwa kazini.
Blogger Pamela Mollel (katikati) wa Jamii Blog ya jijini Arusha akibadilishana wanahabari wenzake Tonia Kasoni( kushoto) wa Radio 5 pamoja na Mhariri wa Sibuka TV wakati wa hafla hiyo.
Mjane wa Marehemu Daudi Mwangosi na mtoto wa mwisho wa marehemu wakati wa uzinduzi wa Mwangosi Fund utakaokuwa ukisaidia waandishi wa habari wanaopata majanga wakiwa kazini vile vile utaenda sambamba na Tuzo ya Mwandishi ambaye atakuwa amepata matatizo, misukosuko katika kutafuta habari za uchunguzi na Tuzo hiyo itakuwa ikitolewa kila mwaka Septemba 6 siku aliyokufa Daudi Mwangosi na mshindi wa Tuzo hizo atajinyakulia Milioni 10 zitakazotolewa na waendeshaji wa mfuko huu UTPC.
Mzee Kassim Mapili wa Mjomba Band akikung'uta gitaa wakati akipiga wimbo wa Mbaraka Mwishe" Njoo mjionee Morogoro"....wakati wa hafla ya kuchangisha fedha za mfuko wa Daudi Mwangosi zilizoenda sambamba na uzinduzi wa mfuko huo katika hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha.
Mmoja wa waandishi wa siku nyingi kwenye tasnia ya habari ambaye pia ni Mwanaharakati wa kutetea haki za Wanawake Bi. Leila Sheikh akiimba nyimbo za zamani pamoja na Mjomba Band inayoongozwa na Mzee Kassim Mapili na Mrisho Mpoto.
Bi. Leila Sheikh akisakata Rhumba la enzi hizo sambamba na Mzee Makwaiya Wakuhenga wakati Gala Dinner katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari Duniani kwenye Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha usiku wa kuamkia leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Abubakar Karsan.
Wanahabari kutoka Zanzibar nao walijumika na wenzao wa Bara kutoka nchini za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Gala Dinner.

Wakongwe katika tasnia ya habari hapa nchini akiwemo Mzee Salim Salim na Mzee Hamza Kasongo na wenzao wakibadilishana mawazo.

Usia Nkhoma wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na mwanahabari mwenzake wakifurahia jambo wakati wa hafla hiyo.

Mzee Hamza Kasongo akiendesha Harambee kwa wanahabari na wahariri kwa ajili ya kuchangisha mfuko wa Mwangosi utakaokuwa ukisaidia wanahabari pindi wapatapo matatizo kazini.
Stella Vuzo wa UNIC akitangaza ahadi yake binafsi ambapo ameahidi kutoa Dola 300 kuchangia Mfuko wa Mwangosi.
Mwenyekiti wa Misa-Tan Bw. Mohammed Tibanyendera akitoa ahadi yake binafsi ambapo ameahidi kuchangia Laki moja huku Misa-Tan imetoa ahadi ya Shilingi Milioni moja kuchangia mfuko wa Mwangosi uliozinduliwa rasmi usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha.
Mwakilishi kutoka BBC ambao nao pia waliguswa na kuchangia mfuko wa Mwangosi kiasi cha Shilingi Milioni Mbili.
Mwendeshaji wa Harambee hiyo Mzee Hamza Kasongo akitangaza kiasi cha fedha zilizokusanywa kwenye Harambee hiyo ambacho ni zaidi ya shilingi Milioni 19 wakati wa Gala Dinner ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari duniani.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akikabidhi fedha taslim shilingi laki 5 zilizokusanywa kwenye Harambee hiyo kwa Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya.

MWEYEKITI CWT MAKETE ATOFAUTIANA NA KATIBU WAKE

$
0
0

Mwenyekiti wa CWT Makete Mwl. Lutangilo Sanga (kulia) akizungumza na mwandishi wa habari hii

Na Edwin Moshi.

Ikiwa zimepita siku nne sasa tangu kufanyika sikukuu ya wafanyakazi, kumeibuka sintofahamu katika chama cha waalimu(CWT) wilaya ya Makete kutokana na kuwepo tuhuma kuwa baadhi ya waalimu waliuziwa fulana zilizotolewa na chama hicho taifa kwa ajili ya kusherehekea kinyume na makubaliano

Hii inatokana kuwepo baadhi ya waalimu kudai kuwa waliuziwa fulana hizo kwa shilingi 1,000/= kwa fulana moja tofauti na agizo la CWT makao makuu kuwa waalimu wote wapewe fulana za Mei mosi bure

Kutokana na minung’uniko iliyokuwa ikitolewa na watu wanaosadikika kuwa ni waalimu ambao hawakutaka kutaja majina yao, ripota wetu alilazimika kumfuata mwenyekiti wa chama cha waalimu wilaya ya Makete Bw. Lutangilo Sanga ambaye bila kumumunya maneno alimtwisha lawama katibu wa chama hicho wilaya ya Makete kuwa ndiye aliyepokea shilingi elfu moja moja za fulana hizo

Mwenyekiti huyo alisema amesikia tetesi hizo ambapo pia alipigiwa simu na baadhi ya waalimu ambao hakuwataja, ambao walimpa malalamiko yao kuwa wameuziwa fulana za Mei mosi licha ya kuwa na taarifa kuwa fulana hizo walitakiwa kupewa bure, jambo alilosema hakuwa na majibu nalo kwa kuwa katibu wake ndiye alikuwa akilishughulikia

Mwenyekiti huyo alikwenda mbali zaidi na kudai kuwa katibu wake amekuwa akifanya baadhi ya mambo bila kumshirikisha na ndiyo maana yeye anakosa majibu, lakini alipoulizwa na mwandishi wetu kuwa kama mwnyekiti amechukua hatua gani kama katibu wake hamshirikishi, hakuwa na jibu

“Mimi nifanyeje kama hanishirikishi na ndiyo maana yanatokea kama haya” alisema 

Mtandao huu ulilazimika kumfuata Katibu wa chama cha waalimu wilaya ya Makete aliyejitaja kwa jina moja la Kapinga na kushangazwa na taarifa hizo huku akisema kuwa hajauza hata fulana moja kwa waalimu na kama wapo waalimu waliouziwa fulana wakadai fedha zao

Katibu CWT Makete
“Ndugu mwandishi wa habari orodha ya waliopokea fulana za mei mosi hizi hapa, na hawa ndio wamepokea kutoka kwangu, mimi wakati nagawa fulana nilikuwa naonana na viongozi tu, kama ni mratibu elimu, ama mwakilishi yeyote namkabidhi fulana na kofia za kata ama shule yake, anasaini naondoka, kama orodha hii( huku akiionesha) ilivyo sasa huo uuzaji unatoka wapi” alisema Kapinga

Alisema kama kuna mwalimu yeyote ambaye ameuziwa fulana na katibu huyo ajitokeze hadharani, na yuko tayari kuwajibika kwa hilo kama ni kweli yeye amewuzia waalimu fulana, huku akisema yeye kama mtendaji mkuu wa chama hajapokea malalamiko yoyote ofisini kuhusu waalimu kuuziwa fulana

Ameongeza kwa kuwa yeye alikuwa akigawa fulana hizo kiujumla kulingana na idadi ya waalimu wa shule, inawezekana wapo baadhi ya waliozipokea halafu wakaenda kuziuza kwa waalimu, ambapo kosa si lake bali ni la aliyeuza ingawa anafahamu kuwa zinapaswa kutolewa bure, na aliyefanya hivyo anapaswa kurejesha fedha za mwalimu huyo na hatua nyingine zitafuata

Kuhusu tuhuma kuwa amekuwa akijiamulia mambo bila kumshirikisha mwenyekiti wake, katibu huyo alisema si kweli na badala yake asema yeye mwenyekiti ndiye amekuwa akijiamulia mambo mwenyewe ikiwemo kuitisha vikao ilihali muitishaji wa vikao ni katibu kama katiba ya chama inavyoelekeza

“Mfano mzuri ni hii barua hapa ameitisha kikao na amesaini, bila hata kunishirikisha ilihali mimi katibu ndiye muandaaji wa vikao kwa kushirikiana na yeye, sasa yeye kawaita wajumbe kwa barua hii na kufanya kikao, sasa hapo nani hamshirikishi mwenzie” alisema Kapinga
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images