Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

JAHAZI MODERN TAARAB KUUPAMBA MKESHA WA MEI MOSI NDANI YA DAR LIVE LEO


JOB ALERT : Sales Executive at POPOTE Media

Mgahawa wa KFC wazindua tawi lake jijini Dar leo.

$
0
0
 Pichani kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa KFC-Tanzania,Bwa.Simon Schaffer akizungumza na Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,kuhusiana na uzinduzi wa tawi lao jijini Dar,Tanzania.Bwa.Simon alisema kuwa wazo la kufungua mgahawa huo nchini Tanzania,ni wazo ambalo limechukua muda wa miaka 3 kutimiza,amesema kuwa KFC itahakikisha viambata vinavyotumika kuandaa vyakula vinapatikana kutoka kwa wasambazaji waliokidhi vigezo vya viwango na ubora,aidha alibainisha kuwa Wafanyakazi wa mgahawa huo (ambao kwa asilimia kubwa ni Watanzania),walipata mafundisho ya miezi 6 kwa malengo ya kuboresha uwezo wao katika kuhudumia wateja kwenye sekta ya vyakula.

"Nasubiri sana kwa hamu kuona jinsi Watanzania watakavyo furahia chakula na huduma za KFC,huduma zetu zimeandaliwa kwa kuzingatia jinsi ya kuwapa wateja huduma kwa haraka na ubora,tunafurahia sana kwa kuanza kuhudumia soko la Tanzania na kuleta huduma tofauti na iliyo bora zaidi",alisema Bwa.Simon.KFC ina migahawa zaidi ya 17,000 duniani historia yake ikianzia huko Kentuky nchini Marekani.
Mmoja wa Wafanyakazi wa mgahawa wa KFC,Faraja Kilongole akifafanua  jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani), namna walivyopata mafunzo jinsi ya kuwahudumia wateja kupitia mgahawa huo,ambao ndio mara ya kwanza kufunguliwa nchini Tanzania.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgahawa wa KFC,wakishangilia jambo mara baada kuzinduliwa rasmi na kuanza kuwa tayari kuanza kuwahudumia wateja mbalimbali watakaokuwa wakiwasili kwenye mgahawa huo.

Exim Bank to offer more job opportunities to fresh graduates

$
0
0

 The Exim Bank Tanzania Chief Executive Officer Dinesh Arora (centre) interviews Faraji Mussa (right) a third year Economics and Statistics student at the University of Dar es Salaam (UDSM) during the Career Fair held at the UDSM campus at the weekend. Looking on at the left is the Exim Bank Assistant Human Resource Manager Hetal Ramaiya. 
 The Exim Bank Tanzania Clock Tower Senior Branch Manager Agnes Kaganda explains a point to university graduates during the Career Fair held at the UDSM campus at the weekend.
 The Exim Bank Tanzania Chief Executive Officer Dinesh Arora (right) interviews Jacob Msokwa  (left) a 2012 Banking and Finance graduate at IFM during the Career Fair held at the UDSM campus at the weekend. Centre is the Exim Bank Assistant Human Resource Manager Hetal Ramaiya. 
 The Exim Bank Tanzania staff poses for a photo during the Career Fair held at the UDSM campus at the weekend.
The Exim Bank Tanzania Chief Executive Officer Dinesh Arora (second left) poses for a photo with university graduates during the Career Fair held at the UDSM campus at the weekend. Centre is the Exim Bank Assistant Human Resource Manager Hetal Ramaiya. 
========  ======= ========
Exim Bank to offer more job opportunities to fresh graduates.

EXIM Bank Tanzania is set to offer more job opportunities to fresh graduates from higher learning institutions across the country in the bank’s efforts to nurture youths into various managerial positions.

Speaking during the Career Day Fair held at the University of Dar es Salaam at the weekend, the Exim Bank Chief Executive Officer Dinesh Arora said higher learning institutions have a big potential to fill the human resource gaps in the banking and financial sector.

“With the establishment of the Exim Academy, our bank is now turning focus to fresh graduates and experience will no longer be an issue as the graduates will be offered the necessary on-hands training when they join us. “I have personally had interviews with some of the fresh graduates and I see a great potential. We will be able to select a number of them and bring them on board,” Arora said.

Earlier, the Exim Bank Clock Tower Branch Senior Manager Agnes Kaganda challenged the graduates to stay focused if they are to achieve their life time dreams. “You should stay focused in life. Do not let anyone drive you from your dreams because with determination, some day your dreams will become true,” She said.

The Career Day Fair’s Organising Committee Vice President Wendo Lendo however said the Career Fair offered opportunities for the graduates to network with various corporate companies.

“The Career Day Fair has proved to be so beneficial because the education system in Tanzania does not categorically help in nurturing careers. Over 20 companies have taken part today and believe next year’s event will be bigger and better,” Lwendo said.

KITCHEN PARTY GALA ILIVOFANA MWISHONI MWA WIKEND.

picha tatu za sehemu ya jiji la Dar mapema leo.

ajali mbaya,eneo la mboga-chalinze,wengi wajeruhiwa vibaya

$
0
0

 BASI AINA YA COASTER LIKIWA LIMEHARIBIKA VIBAYA BAADA YA AJALI HIYO

 HIZI NDO NAMBA ZA GARI NDOGO ILIYOSABABISHA AJALI HIYO
 HUYU NI KONDA WA COASTER HIYO ALIYETEGUKA KIUNO
 MAJERUHI WAKIWAISHWA HOSPITALI
 HICHI NI KICHWA CHA LORI KILICHOGONGANA NA COASTER 
 HAWA NI VIBAKA WALIOKAMATWA WAKITAKA KUIBA VITU VYA ABIRIA
 KWA MBALI NI KONDA ALIYETEGUKA KIUNO,NA MAMA ALIYEKATIKA MGUU
 POLISI WAKIWA ENEO LA TUKIO
 HILI NDO JILA COASTER HIYO ILIYOPATA AJALI

WANAJESHI KUTOKA NCHINI NIGERIA WAITEMBELEA WIZARA YA HABARI

$
0
0
picha no.3
picha no.4picha no.5
  picha no.2
picha no.6
picha no.7picha no.8jpgpicha no.9
Wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria wakiwa katika picha ya pamoja  na wafanyakazi wa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati walipoitembelea wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam. Wanajeshi hao  kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu wako nchini kwa  ziara ya mafunzo ya siku tano.

Kigwangalla ajibu tuhuma za ufisadi kupitia misamaha ya kodi

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Nzega,
Taarifa kwa UMA
Bungeni, Dodoma, Mei 1, 2013.

Nawasalimu kwa heshima na taadhima.
Napenda kutumia fursa hii kutoa taarifa kwa wanahabari na umma kwa ujumla kufuatia habari iliyotoka leo mapema asubuhi kwenye gazeti la Sauti ya watu Tanzania Daima, toleo Na.3071 na kuzua mjadala mkubwa na mzito kwenye jamii pamoja na kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na hadhi, heshima na uadilifu wangu kwenye jamii nikiwa kama kiongozi wa umma. Niwape pole wale wote walioguswa na kushughulishwa na jambo hili, haswa familia yangu, ndugu, marafiki na wananchi wa Nzega; ambao siku zote wanaamini sana katika uadilifu wangu na namna ninavyosimamia misingi ya haki, sheria na uzalendo.
Nimesikitishwa sana na habari  hii hususan kwa kuwa ilichapishwa bila kunipa fursa ya kueleza kwa mapana uhusika wangu. Niwapongeze gazeti la Nipashe kwa kupuuza uzushi huu mara baada ya kunipigia na kueleza upande wangu wa hadithi.
Kumekuwa na wimbi kubwa la baadhi ya watu kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuandika habari za uongo kwa maslahi maovu ya kuwachafua wanasiasa na watu wengine. Watanzania sote tubadilike na tukatae tabia za kutumika vibaya namna hii, maana ni hatari kwa ustawi wa weledi, na kwa umoja na mshkamano wa kitaifa. Ukishaandika jambo ambalo litamchafua mwenziyo, hata kama utamsafisha kiasi gani ni wazi hautokuwa na uhakika kuwa utawafikia wale wale waliosoma zile za jana za kumchafua – hivyo ni jambo la kawaida kabisa kuanza kwanza kwa kuwa na uhakika kabisa na habari kabla ya kuiandika.
Mfano mwaka 2010 tu mara baada ya kuteuliwa nilizushiwa kashfa ya uongo kabisa inayohusiana na Uraia wangu na gazeti moja maarufu la kila siku na mengine yakaweka kwenye ukurasa wa mbele kabisa kwamba Kigwangalla ni Mrundi; hawakusema ni mrundi wa wapi, toka lini ama kivipi, walisema ni mrundi tu! Basi hata kusema shaka yao inaanzia wapi hawakusema. Kwa kuwa vyombo vya dola vilinisafisha na kupelekea kushinda mapingamizi yote yaliyowekwa na washindani wangu kisiasa, niliamua kudharau na kusema yatapita tu na yatasahaulika.
Pia gazeti lingine likaandika kwamba kampuni ya Kigwangalla ni miongoni mwa makampuni yaliyowahi kufaidika na ‘stimulus package’ baada ya mdororo wa uchumi mwaka 2008. Gazeti hata halikutaja kampuni ya Kigwangalla ni ipi, inaitwaje, Kigwangalla ana hisa kiasi gani, anaendesha kampuni hiyo ama la, na kampuni hiyo imepewa sh ngapi kutoka benki kuu, na je imepewa pesa hizo kwa nyaraka zipi na zenye namba gani? Na je pesa hizo imepewa kihalali ama imepitia mlango wa nyuma? Kama imezipata pesa hizo kinyume na utaratibu, basi kuna ushahidi gani! Kwa kuwa yalikuwa mambo ya uongo na uzushi niliamua kudharau na kuacha kama ilivyo.
Gazeti lingine la kila siku liliwahi tena kuandika ‘Kigwangalla atajwa kufadhili mgomo wa madaktari’ na liliweka hadithi hii kwenye ukurasa wake wa mbele kabisa. Halikusema amefadhili sh ngapi? Amempa nani? Zimeenda kufanya nini fedha hizo? Kwa kuwa lilikuwa ni jambo la uongo, pia nilidharau na kuacha lipite. Mwaka jana Novemba pia gazeti lingine liliandika habari na kuweka picha yangu na ya Ndg. Hussein Bashe, na katikati yetu picha ya bastola, na kusema ‘Kigwangalla na Bashe na vita ya bastola Nzega’, na humo ndani kueleza kuwa Kigwangalla na Bashe wanyoosheana bastola wakati wakirudisha fomu za kugombea ujumbe wa NEC. Na kuna mengine mengi: yale ya rushwa ya vitumbua n.k.
Yote haya kwa ujumla wake yalikuwa ni mambo ya uongo na yasiyo na chembe ya ukweli hata kidogo. Mara zote nimekuwa nikiyadharau na kuongea na wahariri wa vyombo husika vya habari kwa namna inayoashiria urafiki na weledi wa kushirikiana na kufanya kazi pamoja na si vinginevyo; ushauri ambao niliupata mwaka 2009 kutoka kwa moja ya wanasheria wa kampuni yangu (wa kampuni ya Marando, Mnyele & Co. Advocates), wakili nguli Mzee Mabere Nyaucho Marando, ambaye alisema ‘wasamehe tu hawa gazeti la Sauti Huru maana ni vema kujenga marafiki wengi zaidi na media kwa kuwa wewe ni kijana, kuliko kujenga maadui – na niliwasamehe bila gharama yoyote ile’. 
Mzee Marando hakukosea, ila ukweli ni kwamba ukifanya hivyo utaona patatulia kwa muda na baada ya hapo pataibuka tena jambo lingine la ukurasa wa mbele linaloandikwa bila ukweli wowote ule! Imekuwa wimbo wa kawaida kwenye baadhi ya media houses! Kufanya kazi kwa maslahi ya watu fulani ama chama fulani, misingi ya weledi ya uandishi haipo! Cha muhimu ni maelekezo ama utashi wa anayetoa chochote.  
Jambo moja kubwa nililojifunza kutokana na yote haya ni kwamba, jambo likiishaandikwa kwenye media halifutiki kwenye bongo za watu, hata muda ukipita namna gani! Leo hii kila siku haya mambo yamekuwa yakirudiwa rudiwa kwenye mitandao ya kijamii hata baada ya kuyatolea ufafanuzi wa kina. Nimefika mahali nimeona niachane na passive ways za kushughulika na media ili kuweka sawa kumbukumbu zangu mbele ya umma wa watanzania.

Ya ukweli: ni kweli kwamba ninamiliki hisa kwenye kampuni ya Emergent Africa Ltd. Nina hisa 40% na mke wangu Dr. Bayoum Kigwangalla anamiliki hisa 11%. Sijihusishi na kuendesha biashara hii kama mtendaji wa kila siku – kampuni ina watumishi wake sehemu mbalimbali. Ni kweli kwamba kampuni ina mradi wa kujenga chuo cha afya Nzega (International Institute for Health Tabora), eneo la uchama, na ni kweli imepewa orodha ndefu ya vitu ilivyosamehewa kodi na serikali kwa kuwa ni vitu/vifaa vya mtaji (deemed capital goods). Ni kweli kwamba kampuni imewahi kuingiza nchini kontena moja lenye vifaa vichache sana katika vinavyotajwa kwenye habari ile, na vingi kati ya hivyo vipo aidha kwenye stoo ya kampuni iliyopo Nzega ama ya Dar es salaam, Kigamboni. Kwa kuwa vipo, wanahabari wanakaribishwa kwenda kuvitazama vitu hivi kama wanapenda.
Ya uongo: Si kweli kwamba nina hisa 78% na mke wangu Dr. Bayoum Kigwangalla ana hisa 22% - ni uongo. Si kweli kwamba kampuni imeagiza vitu na kuvipitisha bandarini na forodhani kwa msamaha kwa nia ya kuuza na hivyo kuiibia serikali kwa njia ya kukwepa kodi. Si kweli kwamba kampuni ya Emergent Africa Ltd imeingiza vifaa vyote ambavyo imepewa msamaha, kama habari inavyotaka kuwaaminisha waTanzania. Sijawahi kuuza bidhaa zozote zile za kampuni hii zilizoingizwa nchini kwa njia ya msamaha wa kodi. Kampuni ya Emergent Africa Ltd haina mradi wa kuuza tiles na hivyo haijawahi kufanya biashara hiyo.  
Ingekuwa ni dhambi kubwa kama kweli ningekuwa naviuza vifaa hivi bila kuvilipia kodi. Na kama ningekuwa sina mradi genuine wa ujenzi wa chuo na labda nimetumia vibaya nafasi yangu ya ubunge kujipatia msamaha ili kurahisisha biashara zangu basi ningeanza kwa kuuza cement (ambayo ni bidhaa inayokimbia sana sokoni na kampuni yangu imepewa msamaha wa karibu tani 5000 – lakini sijawahi kuutumia msamaha huu kununua hata mfuko mmoja wa cement!).
Ama ningeingiza mabati/vigae vya kuezekea (ambavyo pia vinakimbia sana sokoni kwa kuwa watu wengi wanajenga – lakini sijaingiza hata kigae kimoja!), ama ningeingiza malori 4, Nissan Navara pick up 4, Mitsubishi Canter 2, Landcruiser Hardtop 4( ambazo zinatumika sana kwenye utalii na hata kwenye barabara za vumbi) kwa msamaha – lakini sijaingiza hata gari moja kati ya haya, kinyume na habari hii ya Tanzania Daima inavyotaka kuuaminisha umma! 
Kuonesha uadilifu nitaeleza hapa mfano mmoja kwamba mnamo Novemba mwaka jana nilinunua gari moja SUV aina ya Nissan Patrol (T934 CDB) na nimeilipia kodi zote bila msamaha japokuwa ningeweza kutumia msamaha wa kodi kununua na kuingiza moja ya magari yaliyopo kwenye msamaha huu wa kampuni ambayo mimi ni major shareholder. Pia nina ujenzi wa nyumba ya kuishi Nzega, Tabora na Dar es salaam katika hatua mbalimbali: ningeweza kutumia msamaha huu wa kodi wa kampuni yangu ili kujipatia unafuu kwenye manunuzi ya vifaa mbalimbali vya ujenzi kama cement, vigae ama mabati, lakini sijawahi kufanya hivyo hata siku moja!
Kuwa na hisa kwenye kampuni inayofanya biashara halali siyo dhambi. Kupata msamaha wa kodi siyo dhambi. Dhambi ingekuwa kuviuza baada ya kupata msamaha. Kama kuna mtu anaamini kuwa kuna vifaa vimeuzwa na kampuni yangu, kati ya hivi vilivyoingizwa nchini kwa msamaha, anakaribishwa kuleta uthibitisho wa nyaraka za mauzo (cash sale receipts, tax invoice ya mauzo, pay-in slip ya benki ya malipo, delivery note, ama receipt yoyote ile ya kampuni hii inayoashiria kuwa mauzo yamefanyika) ili niweze kufuatilia kujua ni nani aliyeuza na kwa nini alifanya hivyo ili niweze kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yake ikiwa ni pamoja na kumpeleka mbele ya vyombo vya sheria.
Msamaha wa vifaa hivi ni kwa ajili ya Ujenzi wa Chuo Cha Afya Nzega (kitakachoitwa International Institute for Health Tabora), ambacho nilikianza kwa fedha zangu mpaka pale kilipofikia na sasa tunasubiria majibu ya benki ya maombi yetu ya mkopo ndipo tuendelee. Na msamaha huo upo na hautotumika kwa mambo mengine ya binafsi kama nilivyoeleza hapo juu kwenye ununuzi wa gari langu binafsi la kutembelea na ujenzi wa nyumba yangu binafsi ya kuishi Nzega, Tabora ama Dar es salaam (ambako ninajenga).
Watanzania tuache kushabikia uongo. Kufanya hivyo kunaziba mianya ya ukweli kutamalaki. Tuache kutazama mambo kwa macho ya wivu, husda na majungu. Tusimame kwenye misingi ya ukweli daima. Nchi hii itaendelezwa na watu wenye kuchukua maamuzi thabiti na hatua za maksudi za kuleta mabadiliko – kama miradi ya namna hii (ya chuo cha afya Nzega kule!). 
Nchi yetu bado ina watu waaminifu na waadilifu na tunaamini tutafanikiwa kuwadhibiti walio waovu. Hata siku moja kweli haijawahi kushindwa vita na uongo. Si kila mtu aliyeko kwenye uongozi ndani ya CCM basi ni fisadi, watu wazuri na wasafi wapo pia. Tusimuangalie kila mtu kwa sura ya ‘ufisadi’ na ‘ubadhirifu’ tu! Tuaminiane jamani. Tusifedheheshane na kukatishana tamaa. Safari kuelekea mapinduzi ya maisha ya watanzania kiuchumi na kijamii bado ni ndefu lakini tutafika. Tufanyeni kazi.
Taarifa hii nimeiandika na kuitoa mimi mwenyewe, Hamisi Andrea Kigwangalla, M.D., Mbunge, Jimbo la Nzega. (simu yangu ya kiganjani ni 0782636963 na email yangu ni hkigwangalla@gmail.com, website: www.hamisikigwangalla.com )   

Hotel ya DoubleTree by Hilton Tanzania watoa msaada wa taa 200 kwa shule za Msingi Songea- Ruvuma.

$
0
0

Waziri wa Mazingira Dk. Terezya Huvisa ambaye ni Rais wa Mawaziri wa Mazingira Barani Afrika akiipongeza Hoteli ya DoubleTree by Hilton kwa kuona umuhimu wa elimu kwa kukabidhi taa mia mbili kwa Shule za Msingi zilizopo manispaa ya Songea mkoani Ruvuma , Shule zilizopewa msaada huo ni Shule ya msingi Mletele, Mwanamonga, Liumbu na Namang'ula , Taa hizi zinazotumia Nishati ya jua pia ni rafiki wa mazingira. " Taa hizi zitawasaidia kuepeuka kutumia vibatari na mishumaa muda wa kujisomea kwa sababu ni hatari kwani vimekuwa vikisababisha majanga ya kuungua kwa watoto wengi nchini ".
Mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Joesph Joseph Mkirikiti alie kaa katikati na kutoka kulia kwake ni Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli za DoubletTree by Hilton Tanzania Bw. Judd Helman na alie kaa kushoto ni mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata wakati wa hafula ya kukabidhi msaada wa taa zinazotumia nishati ya jua.
Mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Joseph Joseph mkirikiti akiteta jambo na mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata (kushoto) juu ya matumizi ya taa zinazotumia nishati ya Jua ambazo pia ni rafiki wa mazingira kwa Wanafunzi wa darasa la Saba. Kulia ni Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli za DoubletTree by Hilton Tanzania Bw. Judd Helman.
Toka kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata akiwa ameshikilia taa na wakatikati ni mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Joseph Joseph mkirikiti akiwa ameshikilia taa na wa mwisho ni Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli ya DoubletTree by Hilton Bw. Judd helman.
Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli ya DoubletTree by Hilton Bw. Judd helman akimkabidhi moja ya taa inayotumia nishati ya Jua mwanafunzi wa Shule ya Msingi Liumbu iliyopo ndani ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma .
Waziri wa Mazingira Dk. Terezya Huvisa ambaye ni Rais wa Mawaziri wa Mazingira Barani Afrika hapa ni umati wa wanafunzi (Viongozi wa leo) kila mmoja akitaka ampe mkono wa pongezi baada ya kumalizikla hafla ya kukabidhi taa za nishati ya jua kwa shule nne za manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Wanafunzi toka katika shule nne za msingi Mletele, Mwanamonga, Liumbu na Namang'ula na wakifatilia kwa makini hutuba iliyokuwa ikitolewa kabla ya kukabidhiwa taa zinazotumia Nishati ya jua ambazo zimetolewa na Hoteli ya DoubleTree by Hilton.

Wanafunzi hao wameishukuru Hoteli hiyo na kusema taa hizo zitawasaidia kujisomea hata kipindi ambacho Umeme umekatika majumbani hivyo kuongeza uwezo wao kielimu na kupunguza matumizi ya kununua mafuta ya taa kwa ajili ya kusomea

Naye Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata amesema "tumeamua kufanya kampeni hii ambayo ni endelevu tutakuwa tukigawa taa 200 za mezani zenye kutumia nishati ya jua kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa shule tofauti kila mwezi, lengo likiwa nikuwafanya wawe na ufahamu zaidi juu ya chanzo kingine cha umeme ambacho ni rafiki wa mazingira vile vile tunaomba wahisani wengine nao wajitokeze".
Picha na habari kwa hisani ya www.demashonews.blogspot.com

KNCU 1984 YAJUMUIKA NA WAFANYAKAZI WENGINE MOSHI KUSHEREKEA MEIMOSI

$
0
0
 Wafanyakazi tawi la TCCCo, kiwanda cha kukoboa Kahawa wakiwa ktk maandamano.
 Wanyama waliokaushwa, kutoka Wizara ya Malia Asili na Utalii.
Jonia Bwakea, Afisa Habari wa KNCU, akikabidhi zawadi ya Kahawa inayokaangwa na kufungashwa na KNCU kwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh.Leonidas Gama wakati wa sherehe za siku ya Mei Mosi zilizofanyika ndani uwannja wa Chuo cha Ushirika Moshi.
 Sheli inayotembea, ukiishiwa mafuta popote ulipo mjini Moshi, huna haja ya kukimbia sheli na kidumu, unapiga simu namba 
Wadau wa zao la Kahawa TaCRI nao walikuwepo kwenye maandamano.
 Moja ya kivutio kutoka kutoka Wizara ya Utalii na Maliasili.
Bajaji iliyotengenezwa kama ndege, kuonesha kazi zinazofanywa na kiwanja cha kimataifa cha ndege cha KIA (Kilimanjaro International Airpot)
Msururu wa Mgari ukipita kwenye kikuta shoto maarufu mjini Moshi kama cha Cocacola.
 wafanyakazi wa Tanesco, Mjini Moshi, wakiungana na wenzao wa KNCU kusherekea Mei Mosi.  
 Chama cha wafanyakazi wa mashamba TPAW , wajiandaa kuanaza maadanamano.
wafanyakazi wakijipanga kuanza maandamano
 Maandamano ya Mei Mosi Mjini Moshi yakianzia Makao makuu ya KNCU.

Balozi seif Ali Idd awataka vijana wa zanzibar kujenga utamaduni wa ujasiriamali na kujiajiri.

$
0
0

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewataka vijana wa Zanzibar  wabadilike na kujenga Utamaduni wa Ujasiriamali na wawe tayari kujiajiri kupitia vyama vya ushirika vya uzalishaji mali pamoja na kuanzishsa SACCOS ili kupata mitaji yenye unafuu.

Balozi Seif ameeleza hayo katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za Wafanyakazi Duniani (Mei mosi) zilizofanyika katika Kiwanja cha Amaan na kuwashirikisha Wafanyakazi wa Mawizara, Maidara na Mashirika ya Serikali pamoja na taasisi binafsi baada ya kuyapokea maadamano ya wafanyakazi hao.

Amesema pamoja na Serikali kuchukua juhudi kubwa ya kupunguza tatizao la ukosefu wa ajira  kutoka asilimia saba mwaka 2007 hadi asilimia nne mwaka 2010 bado tatizo la ajira ni changamoto kubwa Zanzibar kama lilivyo nchi nyingi Duniani.

Hata hivyo Makamu wa pili wa Rais ameahidi  kwamba Serikali itaendelea kufanya kila juhudi kupunguza ukosefu wa ajira nchini ili vijana waweze kuishi kwa amani.

“La muhimu vijana wetu waache tabia ya kuchagua kazi.  Kazi ni kazi mradi inakupatia riziki yako kwa njia ya halali, ” amesisitiza Balozi Seif Ali Iddi.

Ameviagiza Vyama vya Wafanyakazi kusaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kwa njia ya kutoa elimu itakayowasaidia kukabiliana na ushindani wa soko la ajira la sekta binafsi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki

Amesema uzoefu unaonyesha kwamba vijana wengi  wamekosa Utamaduni wa kufanyakazi katika sekta binafsi, matokeo yake huacha kazi baada ya kipindi kifupi cha kuajiriwa na nafasi zao kuchukuliwa na vijana kutoka nchi jirani.

Makamu wa pili wa Rais pia amevitaka vyuo vikuu nchini kuangalia mahitaji ya ajira yaliyokuwepo nchini kwa kuandaa mitaala na mafunzo yatakayowasaidia vijana kuajiriwa kwa urahisi.

“Vyuo vyetu vikuu nchini navyo vinanafasi kubwa ya kusaidia kupunguza tatizo la ajira kwa kuandaa mitaala yao ya kufundishia na mafunzo mengine kwa mujibu wa mahitaji yaliyopo kama vinavyofanya vvyuo vikuu vyengine vingi  Duniani, ”  alifahamisha Makamu wa pili wa Rais.
 
Blozi Seif amewahakikishia  wafanyakazi kwamba Serikali itaendelea kuchukua hatua mbali mbali za kuboresha maslahi yao ili kuhakikisha yanalingana na kazi wanazofanya na kwa upande wao amewataka kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kukuza tija  huku wakijua kwamba haki na wajibu ni watoto pacha.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mwakilishi wa Shirika la kazi duniani (ILO) Bibi Hopholang Phororo ameishauri Serikali kuendelea kuwajengea wafanyakazi mazingira bora ya kazi ikiwemo kulinda afya na haki zao.

Ameahidi kuwa Shirika hilo liko tayari kuendelea kuunga mkono  katika kusaidia juhudi za Serikali ili kuhakikisha wafanyakazi wako salama wakiwa kazini.

Katibu Mkuu wa ZATUC Maalim Khamis Mwinyi Muhammed ameelezea kuridhishwa na mafanikio makubwa  katika awamu ya saba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwa karibu sana na Shirikisho hilo na kutekeleza kanuni na sheria za kazi.

Hata hivyo Maalim Khamis ameeleza masikitiko ya wafanyakazi wa Zanzibar kwa kutopandishwa viwango vya mishahara yao mwaka uliopita licha ya uchumi kuelezwa kuwa umekua.

NA RAMADHANI ALI / MAELEZO ZANZIBAR     
 1.5.2013 

rais kikwete aongoza maelfu ya watu sherehe za mei mosi jijini Mbeya leo.

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akishirikiana na viongozi wengine kuimba wimbo wa Solidarity Forever wakati wa maadhimisho ya Sikuukuu ya Wafanyakazi duniani iliyofanyika kitaifa mkoani Mbeya.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa TUCTA Philemon Mgaya,Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,Waziri wa Kazi na ajira Mhe.Gaudensia Kabaka, Kaimu Rais wa TUCTA Bibi Nortubunga Maskini, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Mh.Abdulrahman Kinana.

 Baadhi ya wafanyakazi wakishiriki katika maandamano  yaliyofanyika wakati wa maadhimisho ya Mei Mosi  katika Uwanja wa michezo  wa Sokoine mjini Mbeya.Kuona picha za mapokezi ya Rais Kikwete Mbeya BOFYA HAPA

dada lilian anatafuta mchumba.

$
0
0

 Naitwa dada Lilian naomba sana uniwekee tangazo langu kwenye blog yako ya kijamii. Tangazo langu ni kuwa natafuta mchumba, mchumba ninaemtafuta awe mstaarabu, mpole, mwenye hekima na busara. Asiyekuwa muhasherati, ambaye pia hajawahi kuoa wala hana mtoto. Pia awe anamfahamu Mungu na awe mkristo wa dhehebu lolote. Mwenye nia ya kuanzisha familia hivi karibuni maana nipo serious kwa swala hili.
Dunia ya sasa imeharibika sana pia kuna magonjwa mengi hivyo awe tayari kupima ukimwi.
 
Elimu iwe kuanzia chuo kikuu. Umri kuanzia miaka 36 na kuendelea.
Aliye tayari anaweza kuniandikia kwenye email address yangu:
 Natanguliza shukrani kaka yangu.

PICHA MBALI MBALI ZA KITCHEN PARTY GALA ILIVYOKUWA NDANI YA GOLDEN JUBELEE JIJINI DAR.

$
0
0
Mmoja wa waimbaji mahiri wa muziki wa taarabu nchini,Khadija Omari Kopa akitumbuiza mbele ya watazamaji waliofika kwenye hafla ya Kichen Party Gala iliyofanyika kwenye ukumbi wa Golden Jubelee jijini dar mwishoni mnamo tarehe 27 April. 
Mmoja wa Waratibu wa hafla hiyo,ambaye pia ni Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena kupitia Clouds FM,Dina Marios akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa mbalimbali.

Event ilifanyika tarehe 27 april 2013
Venue ilikuwa golden jubelee tower
Dress code ilikuwa rangi za bendera ya Tanzania na waliotokezea zaidi walizawadiwa.wasemaji Getrude Mungai wa Kenya,Aunty Sadaka,mama Victor Mburudishaji Khadija Kopa.

Mmoja wa watoa Mada kwenye hafla hiyo,Mama Sadaka akiendelea kuzungumza mambo mbalimbali yaliyohusu shughuli hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa.













WOSIA WANGU KAMA IKITOKEA NIMETANGULIA KUFA KABLA YA RUGE AU JOE KUSAGA-LADY JAY DEE.

$
0
0

 

Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.

Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.

Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.

Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.
Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.

Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.
Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.

Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.
Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.

Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.

Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.

Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame
Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.

Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai
Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.

Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge. 
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.

Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..

Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.
Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.

Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani??
Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??

Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.

Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma??
Roho gani hiyo??

Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu

JIDE

tannesco waibuka kinara bonanza la Sports Bar & Sports Xtra Day viwanja vya Lidaz club, jijini dar.

$
0
0

 Muwakilishi kutoka benki ya NMB akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya TANESCO,mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza katika  bonanza la soka la Mei Mosi lililojulikana kwa jina la Sports Bar & Sports Xtra Day,lililoratibiwa na Clouds Media Group na kufanyika kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.Bonaza hilo lilijumuisha makampuni 14 na yote yalichuana vikali kuhakikisha kila mmoja anajitahidi kushinda ili kulinda heshima.
Pichani kulia ni Meneja wa bia ya Castle Lager (TBL) kabula Nshimo akimkabidhi nahodha wa timu ya Fast Jet kikombe kwa kuibuka washindi wa pili katika bonanza la soka la Mei Mosi lililojulikana kwa jina la Sports Bar & Sports Xtra Day,lililoratibiwa na Clouds Media Group.
 Baadhi ya wachezaji  na washabiki wa timu ya Fast Jet wakishgalia kombe lao mara baada ya kunyakua nafasi ya washindi wa pili.
 Mchezaji wa timu ya Clouds Media Group,Ben Kinyaia akiwatoka wachezaji wa timu ya TBL
 Mchezaji wa timu ya TANESCO akimchomoka mchezaji wa timu ya Fast jet,wakati wa fainali yao iliyowakutanisha pamoja,ambapo timu ya TANESCO waliibuka kinara kwa kuifunga timu hiyo ya Fast Jet goli 1-0,na hatimaye kunyakua kombe la ushindi katika bonanza hilo lililofana kwa kiasi kikubwa.
Baada ya mpira wa miguu kuisha na kuwapata washindi,pia kulikuwepo na burudani iliyotolewa na bendi ya muziki wa dansi ya Skylight pamoja na wasanii mbalimbali kutoka THT.

Rais Kikwete azindua upya gazeti la Mfanyakazi

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizindua rasmi Gazeti la Mfanyakazi wakati wa kilele cha Sherehe ya Sikukuu ya Wafanyakazi,Mei mosi zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa michezo wa Sokoine mkoani Mbeya.kushoto ni Kaimu Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Bi.Nortiburga Maskini na kulia ni Katibu mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Ndugu Nicholaus Mgaya(picha na Freddy Maro)

JOIN NOW AT SILVA INSTITUTE OF BUSINESS AND MANAGEMENT

$
0
0
ABOUT SIBM
Silva Institute of Business and Management (SIBM) was the registered on 4th April 2013 under the Business Names (Registration) Act (Cap 213). CIBM is owned by BluWat Tanzania Limited (BW), a limited liability company incorporated in Tanzania under the Companies Act, 2002 vide Certificate of Incorporation number 86598 issued on 20th October 2011. BluWat Tanzania Limited has the Consultancy licence; it consults mainly in Management and Business Services.
Vision
To become a centre of excellence in knowledge and technological advancement in East Africa thereby providing lifelong learning and superlative quality education Mission To function as knowledge and technological centre by Continuously investing in the capacity building of the institute management, staff and infrastructure Building reputation in the quality of education offered to satisfy the needs of eventual employers of the graduates and to suit the social and economic development needs.

Conducting research and development studies that will enable the institute to become the most trusted centre in provision of professional advice in economics and business management.
PROGRAMS OFFERED.
Basic Technician Certificate In Procurement And Logistics Management 
(BTCPLM).

Basic Technician Certificate In Accoutancy (BTCA)
Basic Technician Certificate In Human Resource Management (BCHRM)
Basic Technician Certificate In Business Administration (BTCBA)
Front side.
REQUIREMENTS.

Qualified selected applicants will be informed by admission letters before course commencement. Each student will be required to have four (4) passport size photographs (colour) for processing of identity card and other official uses. 

Identity Cards will be available immediately after completing registration at the institute. All students will therefore be required to submit a satisfactory Medical Examination report from a recognized Health Facility dully filled, signed and stamped by a qualified Licensed or registered Medical Practitioner.

The Foundation course is open to form four leavers who were not able to secure at least three principal passes at level (D) hence ineligible to join Basic Technician certificate programme. Candidates for the Basic Technician courses should have attained certificate of secondary school education with a minimum of 3 passes at level (D) of the major subjects.

Candidates for the Technician courses should have attained a Basic Technician certificate from a recognised college. Candidates for the ordinary diploma courses should have completed advanced level education with at least two principal passes or a Technician certificate from a recognised college on the respective course.
Inside class room.
CONTACTS.

The college is located at Plot No 90, Block D, Kimbiji, Kijaka, Kigamboni in Temeke district. Administratively, Temeke is divided into three divisions namely Chang’ombe, Mbagala and Kigamboni. Kigamboni is situated in Dar-Es-Salaam, Tanzania and its geographical coordinates are 6° 49' 0" South, 39° 19' 0" East. According to various studies, the presence of unpolluted beaches, the redevelopment of Kigamboni will spearhead economic development and increase the national income.

The Principal,
Silva Institute of Business and Management,
P. O. Box 15805,

NSSF YANOGESHA TAMASHA LA MICHEZO LA MEI MOSI

$
0
0
Mshambuliaji wa timu ya DHL, Regan Kimaro akimtoka beki wa timu ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Gasper Tumbeza (kulia) katika mchezo wa tamasha la michezo la Mei  Mosi kwa Makampuni lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam. 

 Mshambuliaji wa timu ya NSSF, akiwa katika harakati za kufunga wakati wa tamasha la michezo la Mei Mosi kwa Makampuni.
Kikosi kamili cha timu ya NSSF kilichoshiriki tamasha la michezo la Mei Mosi kwa Makampuni na kufanyika katika viwanja vya Leaders Club jijijni Dar es Salaam.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images