Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 71 | 72 | (Page 73) | 74 | 75 | .... | 1898 | newer

  0 0

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipongezana na Balozi wa China nchini Tanzania, Lu Youqing, baada ya kuzindua rasmi Taasisi ya 'Confucius' ya Chuo Kikuu cha Dodoma, ambayo ni maalumu kwa ajili ya kufundishia Lugha na Tamaduni za Kichina. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 28, 2013 Chuo Kikuu cha Dodoma
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma, Prof. Idris Kikula, wakati akitembele kukagua majengo ya Taasisi ya 'Confucius' ya Chuo Kikuu cha Dodoma, ambayo ni maalumu kwa ajili ya kufundishia Lugha na Tamaduni za Kichina, baada ya uzinduzi wa Taasisi hiyo uliofanyika leo Aprili 28, 2013 Chuo Kikuu cha 
  Dodoma.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kuhusu Lugha na Tamaduni za Kichina, kutoka kwa Mkuu wa Taasisi ya 'Confucius', Zheng Xueyu, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi hiyo ya Chuo Kikuu cha Dodoma, ambayo ni maalumu kwa ajili ya kufundishia Lugha na Tamaduni za Kichina. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 28, 2013 Chuo Kikuu cha Dodoma.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia michoro ya picha zinazochorwa na wanafunzi wa Taasisi ya Confucius inayotoa elimu ya Lugha na Tamaduni za Kichina, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi hiyo ya Chuo Kikuu cha Dodoma. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 28, 2013 Chuo Kikuu cha Dodoma

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua ujenzi wa Chuo cha Afya cha UDOM.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya 'Confucius' ya Chuo Kikuu cha Dodoma, ambayo ni maalumu kwa ajili ya kufundishia Lugha na Tamaduni za Kichina. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 28, 2013 Chuo Kikuu cha Dodoma

   Picha ya pamoja
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha kuhitimu mafunzo ya Lugha ya Kichina, mmoja kati ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Jamillah Dauda, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya 'Confucius' ya Chuo Kikuu cha Dodoma, ambayo ni maalumu kwa ajili ya kufundishia Lugha na Tamaduni za Kichina. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 28, 2013 Chuo Kikuu cha Dodoma. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma, Prof. Idrs Kikula.

  0 0


  5
  Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo la Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama, wakati wa kusherekea Sherehe za miaka 46 ya Muungano zilizofanyika mwishoni mwa wikend katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.  IMG_1357
  Mkurugenzi Mkuu wa Exim Bank Antony Grant (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama, wakati wa kusherekea Sherehe za miaka 46 ya Muungano zilizofanyika mwishoni mwa wikend katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Amani Risasi Maulanga.

  0 0

   Mmiliki wa Kampuni ya McDonald Live Line Technology, McDonald Mwakamele (kulia) akiwaonesha maofisa kutoka Kampuni ya Umeme ya Kenya (KPCL), vifaa mbalimbali vinavyotumika kutengeneza umeme bila kuuzima walipotembelea chuo cha kampuni hiyo, mwanzoni mwa wiki, wilayani Mvomero, Morogoro. Kenya iko mbioni kuingia mkataba na kampuni hiyo kwa ajili ya mafundi wao kufundishwa teknolojia hiyo ya kisasa. Kutoka kushoto ni maofisa wa KPCL, Meneja Uendeshaji, Noah Ogano, Peter Waweru na Mhandisi Charles Mwaura ambaye ni Naibu Meneja Huduma za Kawaida.
   Mwakamele akiwaonesha maofisa wa KPCL, baadhi ya vifaa vinavyotumika katika kazi hiyo. 
   Mwakamele akiwaonesha maofisa wa KPCL kifaa kinachotumika kubebea nguzo.
   Mwakamele akiwaonesha gari maalumu linalotumika kumpeleka fundi kutengeneza nyaya na vikombe juu ya nguzo. 
   Mwakamele akionesha jinsi ya kutengeneza vikombe vya umeme
   Mwakamele akiwa juu ya nguzo akionesha jinsi ya kutengeneza umeme bila kuukata.
   Naibu Meneja wa KPCL, Mhandisi Charles Mwaura akikabidhiwa na Mwakamele mavazi maalumu ya kazi yasiyopisha umeme.
   Mhandisi Mwaura wa KPCL, akivishwa na Mwakamele moja ya mavazi hayo
  Mhandisi Mwaura akimshukuru Mwakamele.(PICHA ZOTE KAMANDA WA MATUKIO BLOG)


  Na Mwandishi Wetu, Morogoro

  UONGOZI wa Shirika la Umeme nchini Kenya(KPLC), umesema kuwa unaangalia namna ya kuingia makubaliano ya wataalamu wake kuja nchini Tanzania ili kujifunza kutumia teknolojia ya kufanya matengenezo ya umeme bila kuukata.
   
  Uamuzi huo unatokana na kile ambacho uongozi huo umeeleza wananchi wa Kenya wamechoshwa na tabia ya kukatiwa umeme wakati yanapofanyika matengenezo wakati wa kubadili nguzo au vikombe  na sasa wameamua kutafuta dawa ya tatizo hilo.

  Wakizungumzia wiki hii mkoani Morogoro walipotembelea kampuni pekee Afrika Mashariki na Kati inayoweza kutengeneza umeme bila kuukata ya McDonald Liveline Technology, walisema wamefurahishwa na teknolojia hiyo na imebaki kwao kuamua ni wataalamu wangapi wajifunze kwa maslahi ya nchi yao.

  Walisema kuwa wamefika mkoani hapa kwa sababu tu ya kuridhishwa na utendaji kazi wa kampuni ya McDonald Liveline Technology na kwamba wakiwa nchi jirani wana haki ya kupata utaalamu huo na ndio maana wamefunga safari ili kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Donald Mwakamele.

  Akizungumza zaidi akiwa katika eneo ambalo Kampuni ya McDonald imefunga mitambo yake kwa ajili ya kutoa mafunzo 'Liveline' Meneja wa Operesheni na Huduma wa KPLC Noah Omondi, alisema kuwa Tanzania imepata bahati ya kuwa na mtaalamu huyo na wao watamtumia kwa ajili ya kufanikisha malengo ya nchi yao ya kutokata umeme ovyo wakati wa matengenezo.

  Omondi aliyekuwa ameambatana na Mwalimu wa matengenezo ya mtandao wa ugavi wa umeme Peter Waweru na Meneja msaidizi wa huduma na matengenezo wa mkoa wa Nairobi Charles Mwaura alisema kuwa kikubwa ambacho wao wanakitazama sasa ni kutafuta ufumbuzi wa umeme nchini mwao na kwamba hawatarudi nyuma.

  Akizungumza zaidi kuhusu kampuni yake Mwakamele alisema teknolojia hiyo ni muhimu kwa nchi mbalimbali na kwamba kuifahamu kwake teknolojia hiyo ameweza kufanya kazi katika mataifa makubwa duniani ikiwemo Marekani na nchi nyingine za Afrika.

  Alisema hakuna sababu ya kukata umeme wakati unapoamua kutengeneza kwani teknolojia ambayo inaweza kutumika kufanya matengenezo bila kukata umeme ipo na kwake inapatikana muda wote.

  Aliongeza kukata umeme wakati wa matengenezo ni kusababisha hasara ambayo inaweza kuepukika kwa kutumia teknolojia ambayo yeye anaifahamu na anaifundisha.

  "Hakuna sababu ya kukata umeme,  njia mbadala ipo ambayo unaweza kuitumia kwa kufanya matengenezo bila kuukata.Tunaifanya teknolojia hii katika nchi mbalimbali.Nipo tayari kuifanya popote na wakati wowote ninapohitajika,"alisema Mwakamele.

  Alisisitiza endapo teknolojia hiyo ya matengenezo bila kukata umeme itatumika, Tanzania itaweza kuokoa fedha na muda ambavyo vimekuwa vikipotea kila umeme unapokatwa kwa ajili ya matengenezo kama ya kubadilisha nguzo au kukata miti iliyo karibu na nyaya za umeme.

  Hata hivyo alisema anaguswa na uzalendo wa nchi yake, na ndio maana kila mara amekuwa akiwataka watalaamu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kufika chuoni kwake kujifunza teknolojia hiyo ambayo ni muhimu katika kipindi hiki kwa maslahi ya taifa.

  0 0

  Lady Jaydee
  Katika mwaka huu wa 2013, inatimia miaka 13 tangu nianze  kazi ya muziki.

  Nashukuru MUNGU tuko pamoja na pia nashukuru umma wa Tanzania kwa kuendelea kusupport muziki wa Tanzania na kunipa nguvu mimi kama msanii.  Nashukuru vyombo vyote vya habari vinavyoshiriki kikamilifu kukuza na kulinda sanaa ya muziki Tanzania bila kujali maslahi binafsi.

  Tumeandaa sherehe kubwa na nzuri ya miaka 13 ya LADY JAYDEE katika muziki.  Na mdhamini mkuu kwa upande wa media ni East Africa TV.

  Sherehe ya miaka 13 ya Lady JayDee katika muziki itaambatana na uzinduzi wa album yangu ya sita inayokwenda kwa jina la 'NOTHING BUT THE TRUTH' ambayo ina jumla ya nyimbo 10.  Katika sherehe hizo pia kutakuwa na show ya nyimbo zote bora za JayDee nikishirikiana na baadhi ya wasanii wenzangu hapa nchini.

  Sherehe zitafanyika Ijumaa tarehe 31 May 2013.

  Nawakaribisha wote tufurahi pamoja

  Na Mungu Awabariki


  0 0
  0 0


   Mama ambaye jina lake halikupatikana mara moja akipita kwenye maji yaliyopoteza mwelekeo baada ya mto kufurika maji kutokana na mvua zinazonyesha wilayani Makete eneo la joshoni wilayani hapa.
  Afadhali kidogo ya mama huyu kavaa rain boot huku mkongojo ukimsaidia kukatisha kwenye maji kuelekea kwenye daraja 
   Mto huo ukiwa umefurika maji kupita kiasi
  Huu ni msitu wa chuo cha VETA Makete ambao umewekwa kibao cha onyo, lakini kina mama hao huenda msituni humo kuokota kuni na kupita hapa licha ya onyo hilo 
  Miti katika msitu wa VETA Makete ukiwa umepuruniwa hali inayoshawishi kina mama hao kwenda kuokota kuni.Picha zote na Mdau Edwin Moshi

  0 0


  Miza Othman-Maelezo Zanzibar.
  Imeelezwa kuwa iwapo Wahitimu waliopata Mafunzo ya Ujasiriamali watakuwa na umoja na mashirikiano katika kufanya biashara zao kutawawezesha kuondokana na umasikini wa kipato.
  Haho yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Kazi na Ajira, Ameiri Ali Ameiri alipokuwa akifunga mafunzo ya ujasiriamali yaliyofanyika katika Skuli ya Msingi Magogoni Mkoa wa Mjini Magharibi.
  Amesema Wananchi wengi wamekuwa wakipata mafunzo ya Ujasiriamali lakini kinachokosekana ni ushirikiano mdogo miongoni mwao jambo ambalo huwarudhisha nyuma kimaendeleo.
  Ameongeza kuwa kupata elimu ya Ujasiriamali humuezesha mwananchi kujua namna bora ya kuyakabili maisha kupitia elimu aliyopata na kujikomboa na umasikini.
  ‘’Nakuombeni sana Elimu mliyopata ya ujasiriamali muitumie vizuri na mushirikiane vya kutosha katika kufanya biashara zenu ili mabailiko yaonekane kwa haraka hapa Magogoni” Alisema Ameiri Ali Ameiri.  
  Kwa upande wake Mkufunzi  wa Ujasiriamali kutoka Kazi nje nje  Abubakari Hussein Talib amesema lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuwawezesha Wajasiriamali kubuni Miradi tofauti ya kibiashara ili kujiletea maendeleo katika shehia yao na maisha yao kwa ujumla.
  Aliwataka Wahitimu hao kubuni mawazo mapya ya kibiashara ambayo yatawafanya kujiongezea kipato na kubadili maisha yao kulingana na Mitaji yao. ‘’Kubuni wazo zuri la kibiashara ni kuleta maendeleo na kuipamba biashara ni kupata wateja waliobora katika biashara yako’’. Alisema Abubakari Hussein.
  Diwani wa Shehia ya Magogoni  Moh’d Suleiman Rajabu amesema Wananchi wanapaswa kupatiwa  mafunzo ya ujasiriamali yatakayowawezesha kujiajiri wenyewe ili kuepukana na dhana ya kuitegemea Serikalini katika ajira.
  Mafunzo  hayo ya Ujasiriamali kwa wananchi hao yamefadhiliwa na Mbunge wa jimbo la Magogoni Hamad Ali Hamad kwa kushirikiana na Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wananchi kiuchumi kwa lengo la kuwakomboa wananchi kiuchumi.
  IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

  0 0


   Wakala wa Uuzaji kinywaji cha asili cha Kibuku kinachozalishwa na Kiwanda cha Dar Brew, Samwel Marwa akinywa kinywaji hicho wakati wa semina ya siku moja ya kuboresha biashara ya kinywaji hicho mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Double View, Sinza, Dar es Salaam. Marwa anamiliki baa iitwayo Samwel Saccos iliyopo Nyantira, Jimbo la Ukonga.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG).
   Baadhi ya mawakala wakifaidi kinywaji hicho

   Mkurugenzi wa Bia za Asili za Kampuni ya Bia Tanzania, Kirowi Suma akitoa maelezo kwa baadhi ya mawakala jinsi ya kuboresha biashara ya kinywaji cha Kibuku. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
   Baadhi ya mawakala wakinywa Kibuku na Bia baada ya semina kumalizika.                                                      Mawakala wakipata mlo
                               Sasa ni wakati wa msosi na hatimaye kushushia na Kibuku na Bia. 
   Mkurugenzi wa Bia za Asili za Kampuni ya Bia Tanzania, Kirowi Suma (katikati), akimsikiliza Meneja Mipango na Fedha wa Kiwanda cha Dar Brew, Andrew Asalile (kulia) walipokuwa wakijadiliana jambo wakati wa semina hiyo. Kushoto ni Sichilima Kazonda ambaye ni Meneja wa Operesheni. 
   Kibuku na bia zinayweka pamoja
                                                                    Makreti ya Kibuku
                              Mmoja wa mawakala akimimina Kibuku kwenye glasi tayari kwa kunywa.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli ya Double View, Venance Msaky akinywa Kibuku baada ya semina ya kuboresha biashara ya kinywaji kumalizika  mwishoni mwa wiki kwenye hoteli hiyo. Kulia ni Reginald Mosha ambaye ni Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Dar Brew kinachonunuliwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)Machi 15, mwaka huu. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Hussam A'ala, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam jana Aprili 28, 2013. Picha na OMR
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Hussam A'ala, wakati akimkaribisha ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam jana Aprili 28, 2013 alipofika kwa ajili ya mazungumzo. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Hussam A'ala, na ujumbe wake wakati alipofika Ofisini kwa Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo, jana Aprili 28, 2013.

  0 0


   Mshauri wa Maswala ya afya wa Kampuni BG Tanzania Dk John Wijnberg (Kulia) akikabidhi msaada wa regulator na oxygen administration blocks kwa Mratibu tiba wa Hospitali ya Mwananyamala Dk Delila Moshi(kushoto) na Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Kariamel John jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 

  =======  =======  =========

   BG TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA MALARIA DUNIANI KWA KUIFIKIA JAMII NA WAAJIRIWA

  Katika kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani mwishoni mwa wiki, BG Tanzania iliandaa matukio mbali mbali Dar es Salaam na kwingineko Tanzania. Hii ilikuwa ni pamoja na kuisaidia hospitali ya Mwananyamala; mafunzo kwa waajiriwa kuhusu uzuiaji wa malaria; kuchangia vyadarua kwa waajiriwa na wenye mikataba; na mafunzo kuhusu malaria. Mafunzo haya yalijumuisha maelekezo ya  kivitendo kuhusu namna ya kutumia vifaa vya kupima ugonjwa huo kwa haraka.

  Dr. John Wijnberg, mshauri wa kiafya wa BG, alieleza jinsi kampuni hiyo inavyotia bidii katika jitihada za kupambana na malaria. “Usalama ni wa muhimu katika mafanikio ya operesheni zetu, ambazo zinategemea pakubwa rasilimalikazi  yenye afya, ari na iliyo katika hali nzuri. BG Tanzania inachukulia malaria kama mojawapo ya majanga makubwa dhidi ya afya kwa rasilimali yake ya thamani zaidi, waajiriwa, na familia zao,” alisema Dr Wijnberg.

  “Kwa mantiki hiyo, BG Tanzania imebuni mpango mathubuti wa kusimamia malaria ndani ya rasilimali za BG Tanzania kwa ajili ya kushughulikia maeneo yote muhimu ya kuthibiti malaria, na imeweka lengo lake la kiafya la mwaka kuwa ni uwepo wa matukio sifuri ya malaria,” aliedelea kusema.

  BG Tanzania hivi karibuni iliungana na mradi wa malaria wa United Against  Malaria wa Chuo Kikuu cha John Hopkins, na sasa tumekuwa kampuni yenye furaha iliyo salama dhidi ya malaria. Kuwa kampuni salama dhidi ya malaria, inajumuisha kusimamia mihimili minne ambayo kampuni zilizo salama dhidi ya malaria zinatakiwa kufanyia kazi ambazo ni: elimu, ulinzi, utetezi na kutambulika/uwazi. Kwa kufuata hatua stahiki, kampuni inapunguza hatari ya malaria kwa wafanyakazi wake wote, familia zao na jamii ya karibu.

  Kama mojwapo ya jitihada hizi na kwa ajili ya siku ya malaria duniani, Dr. Wijnberg alitoa maelezo kuhusu uelewa wake juu ya kutibu malaria kwa manesi waajiriwa  waliopo mstari wa mbele katika wodi ya masuala ya watoto katika Hospitali ya Mwananyamala. Wakati wa kazi hii BG ilichangia vifaa viwili vya uthibiti na vile vya kumpa mtu hewa ya oxigen pamoja na kusaidia kununua mitungi mipya miwili ya hewa ya oksijen. Vifaa hivi ni muhimu kwani tiba ya oxijen ni nyeti sana katika kuwatibu wagonjwa walio katika hali mbaya.

  Baadaye siku hiyo, Dr.  Wijnberg aliongoza mafunzo ya kujenga uelewa kwa waajiriwa wa BG Tanzania katika makao yake makuu yaliyopo Masaki,   Dar es Salaam. Mafunzo ya aina hiyo pia yalifanyika kwa makandarasi wa BG Tanzania mchana huo.

   “Kuwa katika usalama dhidi ya malaria, kunadhihirisha jithada za BG Tanzania za kusaidia jithada zote za kupambana na ugonjwa huo ndani ya kampuni,” Dr. Wijnber alieleza

  Kwingineko nchini, BG Tanzania ilifanya mazungumzo ya kujenga uelewa na ikagawa vyandaru vilivyotibiwa kwa dawa za wadudu kwa waajiriwa na makandarasi katika sehemu zao za kazi Mtwara pamoja na wafanyakazi wanaofanya kazi baharini katika vituo vya uchimbaji mafuta.


  0 0


   Wananchi mbalimbali wa mkoani mwanza walijitokeza na kujiuga na Airtel

  ili waweze kutumia huduma za Airtel Yatosha

   Msanii Hiphop anaeshabikiwa kwa wingi Ney wa Mitego,akikamua wakati tamasha maalum 
  la uzinduzi wa AIRTEL YATOSHA mkoani mwanza katika viwanja vya 

  Furahisha


   Msanii Chipukizi aliyeonyesha kipaji cha hali ya juu kwa kughani

  mashairi yenye mvuto kwa miondoko ya HIPHOP wa mkoani Mwanza maarufu 
  kwa jina la Dogo D alifanya burudani kali katika tamasha maalum la 
  Airtel yatosha mkoani Mwanza katika viwanja vya Furahisha

    Wananchi mbalimbali wa mkoani mwanza walijitokeza na kujiuga na Airtel

  ili waweze kutumia huduma za Airtel Yatosha.

   Msaniii wa Miondoko ya Hip Hop ROMA Mkatoliki akitoa burudani kwa
  maelfu ya wakazi wa Mwanza waliofurika katika viwanja vya Furahisha
  Mkoani humo kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha
  uliofanyika mwishoni mwa wiki kwa siku mbili mfululizo.
  ==========  =============  ===========
  WASANII BONGO FLEVA WAFUNIKA KAMPENI YA AIRTEL YATOSHA JIJINI MWANZA


  WASANII wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva)  wamefunika kwa kutoa
  burudani ya nguvu kwenye kampeni inayoendeshwa na Kampuni ya Airtel
  nchini ya airtel yatosha  na kuwapa raha maelfu ya wapenzi wa muziki
  huo waliofurika katika  viwanja vya wazi vya Furahisha Jijini Mwanza.  Kampeni hiyo ya siku mbili iliyofanyika katika viwanja hivyo na
  kushuhudia na maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Mwanza kupata ushuhuda wa
  Airtel yatosha kwa kununua laini za simu za mkononi za Kampuni hiyo na
  jinsi ya kutumia huduma ya Internet, kuongea kwa kujiunga na kupata
  dakika nyingi za muda wa maongezi kwenda mitandao mingine kwa bei
  nafuu zaidi kwa laini moja tu ya Airtel.  Wasanii wa Bongo Fleva waliotoa burudani na kuwaacha hoi maelfu ya
  wananchi waliofurika kupitia vibao vyao vinavyotamba kwenye vituo
  mbalimbali vya redio na televisheni hapa nchini ni pamoja na Juma
  Khasim ‘Nature’ na kundi lake la wanaume halisi, Roma Mkatoliki, Madee
  na Ney wa Mitego.  Maelfu ya wananchi walioshuhudia kampeni hiyo waliweza pia kushuhudia
  vipaji vya uimbaji kutoka kwa vijana walioshindanishwa na
  waliojitokeza kucheza muziki wa Bongo fleva katika viwanja hivyo na
  kupata zawadi ya laini na fulana (T-shirt) za Kampuni ya Airtel
  zilizotolewa kwa washindi waliopatikana.  “Wananchi wengi wamekuja hapa kupata burudani kutoka kwa wasanii
  mbalimbali wa muziki wa Bongo fleva kama ulivyojionea lakini pia wengi
  kwa sasa wanatumia mtandao wa Airtel ikiwemo huduma hii ya Airtel
  yatosha pamoja na kununua laini na kupatiwa maelezo ya jinsi ya
  kutumia huduma hii”alisema msanii Ney wa Mitego.

  Akizungumzia Kampeni hiyo Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Jackson
  Mmbando alisema kwamba tangu kuzinduliwa na kufanyika  katika mikoa
  sita hadi sasa hapa nchini kumekuwa na mapokeo na mafanikio makubwa
  kwa kuongeza wateja wanaotumia mtandao wa Airtel kupitia huduma zote.  Mfanyabiashara wa vituo vya kuuza mafuta Barnabas Mathayo wa Jijini
  Mwanza alitoa ushuhuda wa kukubali huduma inayotolewa na Airtel katika
  mahojiano maalumu alisema kwamba tangu kuanzishwa kampeni ya Airtel
  yatosha amekuwa akinunua kifurushi na kujiunga na kujipatia muda wa
  kutosha kufanya mawasiliano na ndugu, rafiki, wavuvi wanao nunua
  mafuta kwaajli ya boti zao pamoja na wafanyabiashara mbalimbali
  kupitia mitandao yote kwa bei ile ile.
  “Huu ni Mkoa wa sita sasa na kama mlivyoshuhudia wingi wa watu
  wanaokuja kushuhudia burudani na kupata maelezo ya jinsi ya kutumia
  mtandao huu kwa garama nafuu zaidi na ikizingatiwa Mkoa wa Mwanza ni
  moja ya mikoa inayojishugulisha na uvuvi, kilimo, ufugaji na
  wafanyabiashara kutoka ndani na nchi za maziwa makuu”alisema Meneja
  huyo.  “Hatukaangi laini ni moja tu yatosha zingine za nini na ukiangalia
  Mwanza ni Mkoa wa burudani, biashara, viwanda, kilimo, uvuvi na
  ufugaji hivyo wananchi wake hawana budi kutumia mtandao wa Airtel
  ambao umedhamiria kuwainua kiuchumi na kuletwa kwa kampeni hii
  itawasaidia kujifunza Airtel kuna nini ndani ya mtandao huu”alisema  Mbando aliongeza kuwa kampeni hiyo inaendelea katika Mikoa ningine na
  mwishoni mwa juma hili kampeni hiyo itahamia Jiji kubwa la Dar es
  salaam katika viwanja vya Zakhem na kutakuwa na burudani ya kukata na
  shoka kutoka kwa wasanii mbalimbali kutokana na wasanii wengi kuwa
  jijini humo na kutoa wito kwa wananchi kufika kushuhudia na kujifunza
  ndani ya mtandao wa Airtel kuna vitu gani na kwa gharama nafuuu.

  0 0


   Meneja mahusiano ya nje-Vodacom Tanzania,Salum Mwalimu akifafanua zaidi kuhusiana na udhamini wa kampuni hiyo kwenye tamasha la soka la kuadhimisha sikukuu ya Wafanyakazi nchini,ambapo timu kumi 14 zimepangwa kushiriki.Kulia ni Ofisa Udhamini na Matukio Bwa.Kaude Ibrahim,Mkuu wa Idara ya Michezo-Clouds Media Group Shaffih Dauda na mwisho kabisa kushoto ni Mwakilishi kutoka THT ambao pia watashiriki kutoa burudani kwa ujumla.

  Mkuu wa Idara ya Michezo-Clouds Media Group Shaffih Dauda (pili kulia) akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) mapema leo kwenye viwanja vya Lidaz Club kuhusiana na kufanyika kwa tamasha la soka la kuadhimisha sikukuu ya Wafanyakazi nchini,ambapo timu kumi 14 zimepangwa kushiriki. 
  =========  ======== ======

  Timu 14 kushiriki tamasha la Mei Mosi

  Tamasha la soka la kuadhimisha sikukuu ya wafanyakazi nchini litafanyika siku ya jumatano (Mei Mosi) kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini.
  Tamasha hilo lililoandaliwa na kampuni ya Butterfly Advertizing and Marketing kwa kushirikiana na Sports Extra and Sports Bar , litashirikisha jumla ya timu 14 za makampuni mbalimbali ya hapa jijini kwa mujibu wa mratibu wake, Shafii Dauda.
  Dauda alizitaja kampuni hizo kuwa ni Benki ya CRDB, NMB, Vodacom Tanzania, Clouds Media group, Infinity Communications, Tanzania Cigarette Company (TCC),  NSSF, TBL, Tanesco, National Housing Corporation (NHC), Simbanet, Fastjet, Umoja Water na  DHL.
  Alisema kuwa Vodacom Tanzania na NMB ndiyo wadhamini wakuu wa tamasha hilo lililopangwa kuanza saa 3.00 asubuhi na kupambwa na bendi ya Sky Light na Tanzania House of Talent (THT).
  Kwa mujibu wa Dauda, timu hizo zitagawanywa katika makundi manne na kucheza kwa mchezo wa ligi na mshindi wa kwanza na wa pili wa bonanza hilo watazawadiwa vikombe na timu nyingine shiriki zitapewa vyeti.
  Alisema kuwa sababu kubwa ya kuandaa bonanza hilo lililopangwa kumalizika saa 2.00 usiku ni kuwakusanya pamoja na kubadilishana mawazo wafanyakazi katika siku yao hiyo muhimu.
  Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni ya Vodacom, Salum Mwalimu  alisema kuwa sababu kubwa ya kudhamini na kushiriki katika bonanza hilo ni kuwapa zawadi wateja wao kwani wanaaminikuwa timu zote shiriki ni wateja wao.
  “Mbali ya kudhamini, sisi tutashiriki na timu yetu, tunataka kuwaonyesha kuwa hata soka nasi tunacheza, tunawataka mashabiki kufika kwa wingi kwani ni hakuna kiingilio,” alisema Mwalimu.


  0 0

   The Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant (left) poses for a photo with Honorary Secretary Marian Cummins of the Royal Society of St. George, Tanzania Chapter (center), and renowned English standup comedian Dave Thompson ( right) during St George’s charity ball held in Dar es Salaam at the weekend. Proceeds from the event will support the Dogo Dogo orphanage centre in Dar es Salaam.
  The Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant (right) explains a point to the Rickshaw Travels Limited PR Manager Andrea Bardino (left) during St George’s charity ball held in Dar es Salaam at the weekend. Proceeds from the event will support the Dogo Dogo orphanage centre in Dar es Salaam.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Ujumbe wa Kampuni ya Zarubezhstry Joint Stock ya nchini Urusi, uliyoongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Bw. Renat Shigapov, walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Aprili 29, 2013, kwa mazungumzo. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa moja ya mfano wa ramani ya bandari wanazotengeneza katika nchi mbalimbali duniani, na Aleksandra Necheporenko, Naibu Kiongozi wa Idara ya Kimataifa ya Kampuni ya Zarubezhstry Joint Stock ya nchini Urusi baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Aprili 29, 2013. Picha na OMR

  0 0

  palikuwa hapatoshi ukumbini,ilikuwa ni shangwe kwa kila mgeni mwalikwa kwenye mnuso huo uliofana kwa kiasi kikubwa ndani ya moja uya ukumbi wa hotel ya Serena,jijini `dar

  0 0  Diwani wa kata ya Bulyanhulu Bw. Joseph Makoba akikata utepe kuzindua minara mipya ya kampuni ya simu za mkononi Tigo kata za Kakola na Segese wilayani Kahama mkoani Shinyanga, anayeshuhudia ni meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Bw. Joseph Mutalemwa.

  ==========  ========= ============
  Tigo Tanzania leo wanaendeleza mipango yao ya kuwekeza katika upanuzi wa mtandao wake katika Kata za Kakola na Segese wilayani Kahama Mkoani Shinyanga ili kuongeza kiwango cha ubora na upatikanaji wa mtandao huo nchini kote. 

  Upanuzi huo pia utakwenda sambamba na kujenga miundombinu mipya ya mawasiliano hasa katika maeneo ya vijijini, kuleta mawasiliano kwa maelfu ya watu. Minara mipya ya mawasiliano itajengwa nchi nzima ambapo mradi huo umeanzia katika mkoa wa Kigoma na kuendelea maeneo kama Mwanza, Tabora, Mara na Kagera.

  Akitangaza mradi huo, Meneja Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez alisema “Tigo Tanzania imeendelea kukua kwa kasi mwaka hadi mwaka. Bidhaa zetu za kipekee na huduma pamoja na kuongezeka kwa wateja ni ushahidi wa wazi kabisa wa kukua kwetu. 

  Uzinduzi wa minara hii mipya utawezesha kuwapatia wateja wetu bidhaa bora za kipekee zilizobuniwa katika ubora wa hali ya juu ili wateja wetu waweze kunufaika na huduma na bidhaa zenye kiwango cha hali ya juu kabisa kwa hatua mpya. Hii ndio dhamira yetu ambayo imetufanya tuendelee kuwa kampuni inayoongoza ya mtandao wa simu za mkononi Tanzania.”

  Tukiwa tayari na mtandao imara wa mawasiliano katika mikoa mingi ya Tanzania bara na Zanzibar, upanuzi huu wa mtandao wetu unalenga kuhakikisha kuwa mtandao wetu unapatikana katika mikoa mingi zaidi nchini. Itaboresha ubora wa mtandao katika maeneo ambayo tayari yana mtandao wa Tigo kuhakikisha mawasiliano yanaboreka zaidi na huduma za Intaneti zinapatikana vizuri zaidi na wakati huo huo kuhakikisha kuwa tunapeleka huduma za mtandao wa Tigo nje kidogo ya Tanzania, kuwawezesha wateja wapya kuungana na wenzao ulimwenguni na kuwa sehemu ya jamii kubwa ya mtandao wa mawasiliano ya simu.

  “Tukiwa tunajiamini katika utoaji wa huduma bora za mawasiliano ya simu na nia ya kuendelea kusonga mbele zaidi kwa siku zijazo, tumeona umuhimu wa kupanua na kuboresha mtandao wetu. Uzinduzi wa minara hii mipya utatuwezesha kupanua huduma zetu za mawasiliano katika maeneo haya mapya, kwa wateja tulionao na tutakaokuwa nao kama tunavyodhamiria”

  Awali upanuzi wa mtandao wa Tigo vijijini ulianzia kata za wilayani Kasulu mkoani Kigoma

  Katika ripoti ya hivi karibuni ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ya robo mwaka ya mawasiliano ya mwezi Septemba 2012, idadi ya wateja wa Tigo iliongezeka kwa 20% kati ya mwezi Juni mwishoni 2012 na Septemba 30, 2012 ikiwa na wateja 630,000 walioripotiwa. Tukiwa na mikakati hii ya upanuzi, tunatarajia kukua zaidi kwa mwaka huu 2013.

  0 0  0 0


  Februari 6 mwaka huu nilipata bahati ya kukutana na kuongea na wake wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini. Ilikuwa ni nyumbani kwa Balozi wa Sudan.

  Kwenye mazungumzo yangu ( Pichani) niliongelea umuhimu wa Jumuiya hiyo ya wake wa Mabalozi kuendelea kuchangia elimu ya wasichana waliokatishwa masomo. 
  Kwamba ni haki kupata elimu na pia kumpa msichana nafasi ya pili katika maisha.

  Nikakumbushia historia ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu Jamii kwa kutolea mfano nchi ya Sweden. Kwamba kwa hapa nchini Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi vimetokana na urafiki wa kati ya Rais wa kwanza wa Tanzania, Julius Nyerere na Waziri Mkuu wa Sweden aliyeuawa, Olof Palme.

  Kwamba ni kutokana na ziara ya Julius Nyerere Sweden iliyopelekea avione Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi vya huko na kuamua kuiga mfano huo. Hapa nchini Vyuo hivyo vilianzishwa katikati ya miaka ya 70. Idadi ya vyuo hivyo kwa sasa ni 53.

  Niakaelezea pia umuhimu wa elimu na namna binadamu tunavyopata maarifa. Kwamba tunapata maarifa kutokana na milango mitatu; Uzoefu ( Fronesis) Shule ( Episteme) na Vipaji ( Tekne). Nilifafanua hayo kwa kutolea mifano hai.

  Na kwamba , wasichana hao wanaokatishwa masomo yao wengine kwa kubakwa na walimu wao nao wana uzoefu ambao, ukichanganywa na elimu ya darasani na vipaji vyao, wanaweza kwenda mbele kimaisha na kutoa mchango katika ujenzi wa nchi yao.

  Juzi, kupitia Shirika la Karibu Tanzania Association, wake hao wa Mabalozi wametoa mchango wa takribani shilingi milioni 4 kusaidia miradi ya kujitegemea ikiwamo ufugaji wa kuku wa kienyeji na bustani inayofanywa na wasichana hao kwenye Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi vya Njombe, Ilula na Ulembwe.

  Tunawashukuru kwa mchango huo, na kubwa kabisa, ni kwa wao kufikisha ujumbe, kuwa kuna umuhimu kwa wasichana waliokatishwa masomo kwa sababu ya uja uzito kupewa nafasi ya pili maishani.

  0 0


  FFU ughaibuni wanatoa salamu za heri ya MEI MOSI kwa dau wote

  Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa band" aka FFU yenye makao kule Ujerumani,inawatakiwa kila la heri na fanaka wadau wote katika kusherehekea siku kuu ya wafanyakazi duniani "Mei Mosi" (1st May).

  Pongezi kwa Wafanyakazi wa sekta zote kuanzia wachuuzi,akina mama nitilie, wafanyakazi viwandani,maofisini,mashambani,wapagazi,wakokota mikokoteni n.k, Kazi ni kazi !  Baada ya kazi tufurahie Mei Mosi kwa kupata burudani kamili ya muziki kama vile "Bongo Tambarare" na Supu ya mawe, n.k at FFU camp   click http://www.ngoma-africa.com au www.ngoma-africa.com

  0 0


  Kumekucha....Redds Miss Nyamagana 2013 mchakato umeanza...shindano kufanyika Jumamosi ya tarehe...11/05/2013 JB Belmont Hotel Mwanza..Show nzima Itasimamiwa na mchekeshaji Zembwela..huku burudani ikikamilishwa na Recho kutoka THT.....Warembo Zaidi ya 20 watapanda jukwani...wakiwa na hamu sio tu kulichukua taji la Miss Nyamagana lakini pia Taji la Miss Tanzania 2013/14. Tiketi zitauzwa mapema, wahi tiketi yako..kwani ni chache mno!! Karibu....

older | 1 | .... | 71 | 72 | (Page 73) | 74 | 75 | .... | 1898 | newer