Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

RAIS MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kufanya nae mazungumzo  Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ikulu jijini Dar es Salaam.


NAPE AZUNGUMZIA KIKAO CHA WABUNGE WA CCM MJINI DODOMA

0
0

DAR, BAGAMOYO KUKOSA MAJI KWA SIKU MBILI

0
0

SHIRIKA LA Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), imetangaza kuwapo tatizo la upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo yote yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu chini ya jiji la Dar es salaam, pamoja na baadhi ya maeneo  ya mji wa Bagamoyo mkoani Pwani kutokana na mtambo huo kuzimwa kwa wastani wa saa 48 kuanzia siku ya Jumamosi 23/01/2016 hadi Jumapili 24/01/2016.

Taarifa ya kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na kaimu meneja uhusiano wa DAWASCO, Bi  Everlasting Lyaro, imeeleza kuwa sababu ya kuzimwa kwa mtambo huo, ni kuruhusu mkandarasi kuunganisha bomba jipya na bomba la zamani katika tanki la Maji wazo-Tegeta, zoezi ambalo linaashiria kukamilika kwa upanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini, hivyo kuondoa  tatizo la upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu chini.

“Tunaelekea kwenye hatua za mwisho za kupokea Maji mengi kutoka mtambo wa Ruvu Chini baada ya kazi ya upanuzi inayoelekea kukamilika mapema mwezi February mwaka huu, na kiasi cha Maji kitaongezeka kutoka wastani wa Lita Milioni 182,000 zinazozalishwa sasa hadi Lita Milioni 270,000. Hivyo kuzimwa kwa mtambo huu ni moja ya hatua za mwisho-mwisho katika ukamilishaji wa Mradi wa Ruvu Chini” alisema Lyaro

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, DAWASCO imetoa wito kwa wateja na wananchi wote kuhifadhi Maji ya kutosha na kuyatumia kwa matumizi muhimu ili kukidhi mahitaji husika kwa kipindi hicho chote.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa matengenezo hayo yatasababisha maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam kukosa Maji, pamoja na mji wa Bagamoyo vijiji vya Zinga, Kerege na Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani,  Mbezi Beach na Kawe.

Maeneo mengine ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya Rufaa Muhimbili, Buguruni, Chang’ombe na Keko

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MAREHEMU LETICIA NYERERE

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho  Kikwete nyumbani kwa Baba wa Taifa  Msasani Dar es salaam wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere aliyefariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa leo Januari 20, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere aliyefariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa leo Januari 20, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere aliyefariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa leo Januari 20, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa heshima zao za mwisho  wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere aliyefariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa leo Januari 20, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimfariji mume wa marehemu Bw. Madaraka Nyerere wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere aliyefariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa leo Januari 20, 2016. Kulia ni Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimfariji Mama Maria Nyerere wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere aliyefariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa leo Januari 20, 2016. Kulia ni Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere.

Article 6

0
0

UBA TANZANIA TRAINS IFM (INSTITUTE OF FINANCE MANAGEMENT) STUDENTS ON CUSTOMER SERVICE MANAGEMENT

0
0
uba 1
Service Quality Manager, Queen Odunga during the training session at IFM (Institute of Finance Management).
Saturday, 16 January 2016 UBA trained IFM students on customer service management. Taking on the session was the Service Quality Manager, Queen Odunga, who explained how to handle a difficult customer. And after the session, the students tried to create a situation where the customer is complaining and doesn’t want to listen to the CSO. This came out so well as the one who was acting as CSO resolved the situation and the one acting as the client was happy that his problem was solved.

One happy student commended the UBA Team for taking them through the session “This has been a great session that we cannot easily get from our daily lectures. We thank UBA team especially Madam Queen who has highlighted on the importance and tactics of how to handle a difficult customer”, She concluded.

Queen Odunga the Service Quality Manager thanked the IFM Management for giving UBA the platform to share the knowledge on Customer service. She also applauded the students being attentive. “I would like to thank the IFM Management for providing UBA Tanzania with this platform and I would also like to thank the students for attending in numbers and being attentive throughout the session, it was quite interactive”. She continued by advising the students to take heed of the knowledge they have achieved in this session as “customer service is very vital for any business as it leads to customer retention and business development”.

Other UBA team members present at the session were also able to interact with the students giving them advise on the dos and don’ts in the finance and banking industry at large.
uba 2
Some of the students present at the training take a group picture with UBA staff members.
uba 3
A student ask a question during the training session with UBA Team on customer service management.
uba 4
Some of the students present at the training take a group picture with UBA staff members.
uba 5
Some of the students present at the training.

MWANASAIKOLOJIA ANTI SADAKA AWAFUNDA WANAWAKE WA JIJI LA MWANZA

0
0
Mwanasaikolojia Anti Sadaka akitoa Mada kwenye Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Mwanza yanayoendesha na  Taasisi ya Manjano foundation yanaoendelea kwenye ukumbi wa Rocky city Jijini Mwanza.

Mwanasaikolojia Anti Sadaka amewafunda wanawake wa Mkoa wa Mwanza wanaoshiriki mafunzo ya ujasiriamali ya kujikita katika biashara ya Vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yanaendeshwa  na wataalamu kutoka taasisi ya Manjano  Foundation  yanayoendelea Jijini Mwanza kwa wiki nzima. Anti Sadaka amewataka wanawake hao kujitambua kwa lengo la kufikia malengo yao waliojiwekea. Akieleza zaidi katika semina hiyo amewataka wanawake hao kujitambua wao ni nani  wana nafasi gani kwenye jamii inayowazunguka, kufanya kazi kwa bidii na kudumisha nidhamu yao kwa kila wakifanyacho kwa lengo la kufikia malengo yao.
Semina hiyo inawanufaisha wanawake wa Mwanza kwa lengo la kuwaongezea kipato na pia kuweza kujiajiri ili kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira. Baada ya washiriki kupata mafunzo ya biashara na urembo watapatiwa  MIKOPO kutoka Taasisi ya Manjano  Foundation  kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. 
Wanawake wa Mkoa wa Mwanza wakifuatilia kwa amkini Mada zilizokuwa zinaendeshwa   kwenye Mafunzo hayo.
Pia amewaasa wanawake walioshiriki mafunzo hayo mkoani Mwanza kuchangamkia FURSA zinazowazunguka mapema iwezekanavyo. Alisisitiza umuhimu wa usafi wao binafsi na mazingira yao ya kazi kupewa kipao mbele kwa sababu usafi humlinda mteja asipate breakout ya ngozi yake na kuridhika na huduma yake yaani "Smart You & Environment."
 
Mwanasaikolojia Anti Sadaka Akiwa katika Picha ya Pamoja na wanawake wa Mkoa wa Mwanza waliojitokeza  kwenye Mafunzo ya Ujasiriamali  yanayoendeshwa  na Taasisi ya Manjano Foundation.
Washiriki wa mafunzo hayo  wameushukuru uongozi wa Taasisi ya Manjano  Foundation kwa kuwakumbuka na kuwaletea Mradi huo jijini Mwanza. Wakieleza zaidi wamesema kwa muda mrefu wamekuwa na hamu ya kujua zaidi kuhusu matumizi sahihi ya vipodozi lakini walikosa elimu hiyo ya kuwa Makeup Artists.

AIRTEL YAZINDUA DUKA KARIAKOO MSIMBAZI

0
0
Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba, akikata utepe wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Airtel Express lililopo Kariakoo mtaa wa msimbazi, Dar es Salaam, akishuhudia ni wakala mkuu wa Airtel kutoka Celnet, Bwana Kalpesh Bandar.
Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba (katikati), akiangalia simu aina ya Bravo Z10 wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Airtel Express lililopo kariakoo mtaa wa msimbazi, Dar es Salaam. Akitoa maelezo kuhusu simu hiyo ni Afisa mauzo wa Airtel , Meshack Joseph (kwanza kulia) , akishuhudia kulia ni Meneja Mauzo wa Airtel, James Moilo.
Afisa mauzo wa Airtel , Meshack Joseph (kwanza kulia) akitoa maelezo kuhusu simu mbalimbali za smartphone zinazopatikana katika duka jipya la Airtel Express Kariakoo wakati wa uzinduzi wa duka hilo jipya lililopo Kariakoo mtaa wa msimbazi, Dar es Salaam. Pichani ni Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba (katikati) akiwa na wateja pamoja na wafanyakazi wa Airtel

Airtel Tanzania imezindua duka la Airtel Xpress mtaa wa msimbazi, Kariakoo Dar es Salaam ikiwa ni moja ya mipango yake ya kusogeza huduma zake karibu zaidi na wateja wake.

Kuzinduliwa kwa duka la kariakoo Airtel Xpress inaongeza idadi ya maduka kuongezeka kufatia uzinduzi wa dula jipya la kisasa lililoko Morocco Dar es salaam ulifanyika wiki iliyopita.

Katika uzinduzi wa duka la Airtel XPress kariakoo mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba alisema, kufunguliwa kwa duka la Airtel Xpress kariakoo itawawezesha wateja wa Airtel na wafanya biashara wa Kariakoo, Ilala, Magomeni kupata huduma zetu kwa ukaribu zaidi kama kujipatia simu za kisasa na kwa bei nafuu. Tunaimani kufunguliwa kwa duka hili hapa kutatasaidia kupata huduma kwa uharaka na ubora zaidi.

“Airtel tumejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja wetu zaidi ya milioni 10 nchi nzima. Kipaumbele chetu ni kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma kiurahisi zaidi na kwa ufanisi wakati wote na hili limejidhihirisha leo kwa kufungua duka la Airtel Xpress”, aliongezea Adriana

Baadhi ya huduma zitakazotolewa kwenye duka la Kariakoo ni pamoja na Airtel Money, kusajili laini, huduma za internet na huduma zetu nyinginezo.

Pamoja na duka jipya lililozinduliwa kariakoo pia Airtel inamaduka sehemu mbalimbali katika mkoa wa Dar es Salaam kama Airtel Morroco, Mlimani City, J Mall, Buguruni Airtel inatarajia kufungua maduka zaidi ifikapo Juni 2016 yatakayotoa huduma sambamba na mawakala wake Zaidi ya 80,000 nchi nzima.

TPC yaagizwa kukusanya mapato kwa njia ya kielektroniki

0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

 WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO

                                                    
 ZIARA YA KATIBU MKUU (MAWASILIANO) YA KUTEMBELEA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora alifanya ziara ya kutembelea Shirika la Posta Tanzania ili kufahamu utendaji kazi na utekelezaji wa majukumu ya Shirika. Katika ziara hiyo Prof. Kamuzora aliambatana na Naibu Katibu Mkuu wake Dkt. Maria Sasabo na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Shirika hilo. 

Katika ziara hiyo Prof. Kamuzora alimuagiza Kaimu Posta Masta Kuu wa Shirika la Posta Tanzania Ndugu   Fortunatus Kapinga kuhakikisha kuwa ukusanyaji wa mapato yote ya Shirika la Posta Tanzania (TPC) nchi nzima yanafanyika kwa kutumia njia ya elektroniki ambapo alisema kuwa, “Shirika liboreshe mifumo yake ya kielektroniki ili kupunguza mianya ya wizi na upotevu wa fedha za Shirika na kufanikisha ongezeko la ukusanyaji wa mapato ya Serikali”. Prof. Kamuzora aliongeza kuwa Shirika la Posta Tanzania liendane na mabadiliko ili liende kuwahudumia wananchi wa sasa na wa vizazi vijavyo. Shirika ni la kipekee na lina nafasi nzuri ya kutoa huduma kwa wananchi kama ambavyo Shirika kama hili linafanya kazi nzuri  kwenye nchi ya China na Brazil. 

Aidha, Prof. Kamuzora aliwaagiza Viongozi wa wasimamizi wa Shirika la Posta Tanzania kutumia Sheria, Kanuni na taratibu za kuwasimamia wafanyakazi na kuwachukulia hatua kali na za kinidhamu watumishi wazembe; wasiotimiza majukumu yao; wasio waaminifu na wabadhirifu. Aliongeza kuwa watendaji wafanye kazi na kusimamia Shirika kwa kuwekeana malengo kama inavyojulikana kisheria kwa kutumia Mfumo wa wa Wazi wa Upimaji Utendaji Kazi (OPRAS). 

Alisisitiza kuwa, “Sheria zilizopo zinatosha kumsimamisha mtumishi kazi kwa makosa na hatimaye kumfukuza kazi kwa kuwa watumishi wazembe na wasio waadilifu wanawafanya wananchi wawe na mtazamo hasi na Serikali yao”. Prof. Kamuzora alisema kuwa wateja wanahitaji huduma nzuri; ya uhakika na kufikishiwa vifurushi, barua, vipeto na bidhaa nyingine kwa wakati.

Aliwaagiza viongozi wa Shirika kuangalia uwezekano wa kupunguza gharama za uendeshaji ili kuendesha Shirika kwa tija na faida. Prof. Kamuzora alisema, “Uchumi wa nchi hauwezi kukua wala kwenda popote bila kufanya kazi kwa tija. Alivitaka vyama vya wafanyakazi visiwatetee watumishi wazembe na vishirikiane na Serikali kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Shirika na watumie mtandao mpana wa Shirika uliopo nchi nzima na kuangalia fursa zilizopo ili kufikisha huduma kwa wateja. 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia Mawasiliano ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wake Dkt. Maria Sasabo aliagiza kuwa, “Shirika lijipange haraka na kuongeza kasi ya utendaji kazi ya kuwahudumia wateja wake na wananchi ili kuweza kuendana na Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli”. 

Dkt. Maria Sasabo aliongeza kuwa Shirika la Posta lipo nchi nyingi duniani na bado linahitajika hivyo ni muhimu kujipanga kuendana na mahitaji ya sasa ya wateja na Shirika libadilishe utaratibu wa utendaji kazi na kuondoa urasimu ili kuweza kuwahudumia wateja. Dkt. Maria Sasabo aliwaagiza viongozi wa Shirika wafanye tathmini na kuangalia namna bora ya kujiendesha ikiwemo kupitia upya muundo na majukumu ya Shirika.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia Mawasiliano Prof. Kamuzora aliuagiza uongozi wa Shirika la Posta Tanzania kuongeza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa kuwa na huduma za ziada za kisasa zinazoendana na mahitaji ya wateja kwa kutumia biashara mtandao kusafirisha na kufanikisha usambazaji wa huduma na bidhaa za wateja kama vile uagizaji wa magari; vitabu na bidhaa nyingine kwa kushirikiana na kampuni kubwa duniani kama vile Alibaba, Amazon na eBay.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

NEWS ALERT: JPM AMSIMAMISHA KAZI KAMISHNA MKUU WA UHAMIAJI NA KAMISHNA WA UHAMIAJI ANAYESHUGHULIKIA UTAWALA NA FEDHA.

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Bwana Sylvester Ambokile na Kamishna wa Uhamiaji anayeshughulikia Utawala na fedha Bwana Piniel Mgonja   ili kupisha uchunguzi, kufuatia dosari alizozibaini Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Charles Kitwanga alipotembelea Idara ya Uhamiaji hivi karibuni.

RAIS DKT.MAGUFULI AMTEUA KIKWETE KUWA MKUU WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.

0
0

AHUKUMIWA MIAKA 19 JELA KWA KUIBA MBUZI MKOANI MBEYA

0
0
Na Ezekiel Kamanga,,Mbozi.

MAHAKAMA ya mwanzo vwawa mjini wilayani Mbozi mkoani Mbeya imemuhukumu Patrick Moses(19) mkazi wa Ilembo  kutumikia jela miaka mitano baada ya kukiri kosa la kuiba Mbuzi mmoja mwenye thamanai ya Sh 85,000 mali ya Bahati Mtafya.


Akisoma hukumu hiyo hakimu wa mahakama hiyo,lazima Mwaijega alisema kutokana kifungu cha sheria 268 na mshitakiwa kukiri kosa hivyo mahakama imeamuru mshitakiwa kutumikia kifungo hicho ili iwe fundisho kwake na kwa wengine wenye nia ya kutenda kosa kama hilo.

Mshitakiwa alipopewa nafasi ya kujitetea aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwani anategemewa na familia yake,hata hivyo hakimu Mwaijega amesema kifungo hicho cha miaka mitano amepunguziwa pia kwa kuwa ni kosa lake la kwanza na kwamba.

Awali imeelezwa mahakamani na  mwendesha mashitaka wa polisi Hamis Mohamed kuwa January 20,mwaka huu saa 11 jioni  mshitakiwa alivamia nyumbani kwa Bahati Mtafya (38) na kuiba mbuzi mmoja mwenye thamani ya Sh. 85,000 huku akijua kufanya vyo ni kosa kisheria namba 229 sura ya 16 kanuni ya adhabu.

Aidha mwendesha mashitaka huyo aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa wale wenye nia ya kutendakosa kama hilo kutokana na wimbi kubwa la vijana kujikita katika wizi na kuacha kufanya kazi halali.

Katika hatua nyingine mshitakiwa huyo alipandishwa kizimbani hapo kujibu tuhuma ya wizi wa kuku 23 wenye thamani ya Sh laki 4 mali ya Evance Mwakenja mkazi wa Ilembo Vwawa 

Imeelezwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa polisi Hamis Mohamed kuwa tukio hilo lilitokea januari 20 mwaka huu saa 8 usiku ambapo mshitakiwa aliiba kuku 23 wenye dhamani ya Sh.laki 4 mali ya Evance Mwakenja huku akijua kufanya hivyo nikosa kisheria.

Hata hivyo mshitakiwa alikana shitaka linalomkabili na hakimuwa mahakama hiyo Chirstina Mlwilo amesema shauli hilo litaanza kusikilizwa Januari 27 mwaka huu,pia hakimu huyo amesema dhamana kwa mshitakiwa ipo wazi kwa ahadi ya Sh.laki 4 pamoja na kuwa na  wadhamini wawili wenye vitambulisho vya mpiga kura. 

 Hata hivyo mshitakiwa ameludiswa maabusu kwa kushindwa kutimiza masharti  la dhamana pamoja na kuanza kutumikia kifungo cha miaka mitano ya wizi wa mbuzi.

JAMIIMOJABLOG

RIPOTI YA TATHMINI YA MAZINGIRA YA KISHERIA KATIKA MWITIKIO WA UKIMWI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA ZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar (ZAC), Dk.Ali Ali (katikati), Kaimu Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Jumanne Issango (kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP), Titus Osundina wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi wa ripoti ya tahmini ya mazingira ya kisheria katika mwitikio wa ukimwi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliofanyika Makao Makuu ya Tacaids Dar es Salaam leo asubuhi.
 Viongozi hao wakiwaonesha wageni waalikwa na wadau mbalimbali ripoti hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tacaids, Elizabeth Kaganda na kilia ni Dk.Bwijo Bwijo kutoka UNDP.
 Naibu Mkurugenzi Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP), Titus Osundina, akihutubia wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar (ZAC), Dk.Ali Ali (kushoto), Kaimu Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Jumanne Issango (katikati) wakimpongeza Naibu Mkurugenzi Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP), Titus Osundina baada ya kuhutubia.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Uzinduzi ukiendelea.
Wadau wakiwa katika uzinduzi huo.
Picha ya pamoja na viongozi.
Wasanii wa Hisia Threatel Group kutoka Sandali Temeke jijini Dar es Salaam wakionesha igizo linalohusu ukimwi katika uzinduzi huo.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-

HUDUMA YA TRENI YA JIJI HAITOKUWEPO JIONI LEO JANUARI 22, 2016!

0
0



Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusitishwa huduma ya treni ya jiji maarufu kama Treni ya Mwakyembe awamu ya jioni ya leo Januari 22, 2016.

Taarifa imefafanua kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na mabehewa yake matano ya treni hiyo kupata ajali ya kuacha njia mara baada ya kuondoka kituo cha Kamata.wakati wa huduma ya asubuhi ikitokea Ubungo Maziwa.


Kwa sasa mabehewa hayo yanafanyiwa ukaguzi ili yaweze kurekebishwa kasoro ndogondogo tayari kwa kuendelea na huduma siku ya Jumatatu ijayo. Januari 25, 2016. Huduma ya treni ya jiji hutolewa kwa siku 5 kwa wiki ambapo ni kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, isipokuwa kwa siku za Jumamosi, Jumapili na sikukuu za Kitaifa.

Atakayesoma taarifa hii amuarifu mwenziye.


Uongozi wa TRL unasikitika kwa usumbufu utakaojitokeza.


Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya :

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,

Mhandisi Elias Mshana,

Dar es Salaam,


Januari 22, 2016.

Dkt. Mahiga azindua kitabu cha Dkt. Salim Ahmed Salim

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb), mwenye tai ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Dkt. Salim Ahmed Salim (Salim Ahmed Salim: Son of Afica), kitabu kinachozungumzia historia iliyotukuka ya Dkt. Salim ndani ya Tanzania, Afrika na Duniani kwa ujumla, wakiwa wameshikilia kitabu hicho baada ya kuzinduliwa rasmi tarehe 21-01-2016, katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.
Waziri Mahiga akimpongeza Dkt. Salim, muda mfupi baada ya kuzindua kitabu chake.
Waziri Mahiga akikata utepe, kama ishara ya kuzindua kitabu hicho.
Hivi ndivyo uso wa kitabu hicho unavyoonekana.
Dkt. Salim Ahmed Salim (kulia), na Mwakilishi wa Kituo cha Kutatua Migogoro Barani Afrika, (Centre for Humanitarian Dialogue-CHD), Bw. Mohamed Omary wakionyesha Fremu yenye Mashairi ya kumsifu Dkt. Salim, huku Waziri Mahiga akishuhudia tukio hilo.
Mhariri wa kitabu hicho, Dkt. Jackkie Cilliers akizungumza katika hafla hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb), ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Dkt. Salim Ahmed Salim (Salim Ahmed Salim: Son of Afica),akimzungumzia historia iliyotukuka ya Dkt. Salim Ahmed Salim, kabla ya uzinduzi wa kitabu hicho.
Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini, Mhe. Thami Mseleku (kushoto) akiwa pamoja na Balozi wa Malawi hapa nchini, Mhe. Eugene Segore Kayihura nao wakifuatilia uzinduzi wa kitabu hicho.
Dkt. Salim Ahmed Salim, akitoa maneno ya Shukrani kwa heshima aliyopewa kwa Mwandishi wa kitabu hicho lakini kwa wadau wote waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wa kitabu chake.Aliyekua Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (Katikati), akiwa na wageni mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho.
Mwanasheria nguli, Profesa Issa Shivji, akitoa muhtasari kitabu hicho kwa wadau mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo.
Muongozaji wa shughuli hiyo, Bw. Hamza Kasongo akiendelea na kazi yake.
Waziri Mahiga akifurahia jambo na Dkt. Salim.
Aliyekua Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akisalimiana na baadhi ya wageni waliohudhuria hafla hiyo.Dkt. Salim akizungumza jambo wakati wa hafla hiyo.Mgeni Rasmi, Waziri Augustine Mahiga akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuzindua kitabu cha Dkt. Salim katika hafla iliyofanyika tarehe 21-01-2016 katika hoteli ya New Africa jijini Dar es Salim. PICHA NA REUBEN MCHOME.

Dalbit Petrolem yamwaga msaada wodi ya watoto MOI

0
0
Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohammed Bakari (katikati) akikata utepe kuashiria kupokea msaada wa vitanda 27 na magodoro yake kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa vichwa na mgongo wazi,vilivyotolewa na Kampuni ya mafuta ya Dalbit Tanzania,hafla hiyo ilifanyika katika wodi ya watoto hao katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.Wengine katika picha Mkurugenzi Mkuu wa Dalbit Tanzania,Margaret Mbaka(kulia) na Mkurugenzi wa huduma za wauguzi wa Hospitali hiyo Flora Kimaro.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya mafuta ya Dalbit Tanzania,Margaret Mbaka( kulia) akimfafanulia jambo Mganga Mkuu wa Serikali Prof.Mohammad Bakari juu ya msaada wa vitanda 27 na magodoro yake kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa vichwa na mgongo wazi,vilivyotolewa na Kampuni hiyo wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada huo iliyofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa huduma za wauguzi wa Hospitali hiyo Flora Kimaro.
Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Patrick Mvungi na Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni ya mafuta ya Dalbit Tanzania, Anthony Kagiri,wakibandika stika kwenye vitanda na vifaa mbalimbali vilivyotolewa msaada na kampuni hiyo kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa vichwa vikubwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili vyenye thamani ya shilingi Milioni16/-

Rais Dkt Magufuli akiwasalimia wananchi jijini Arusha wakati akielekea wilayani MOnduli kikazi

0
0
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wa Arusha Mjini wakati akipita Barabarani kuelekea Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli ambako pamoja na mambo mengine kesho tarehe 23 Januari, anatarajiwa kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kundi la 57/15.
Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt Magufuli akiwasikiliza wananchi kwa makini alipopita maeneno ya Sanawali kuwasalimia wakati akielekea Wilayani Monduli.
Baadhi ya Wananchi wa Maeneo ya Sanawali wakishangilia ujio wa Rais John Pombe Joseph Magufuli,alipokuwa akielekea Wilayani Monduli mapema leo asubuhi.
Rais Magufuli akiwa amevalia sare za kijeshi amesimamishwa na kuwasalimu wananchi katika maeneo ya SANAWALI, TEKNIKO, NGARENALO, MBAUDA, MAJENGO na KISONGO



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


Simu: 255-22-2114512, 2116898

E-mail: press@ikulu.go.tz

Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,

      IKULU,

 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  

11400 DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameonya kuwa wilaya ama Mkoa wowote ambao utakumbwa na njaa, itakua ni kipimo tosha cha kuonesha kuwa Mkuu wa Mkoa ama Mkuu wa wilaya husika hafai kuendelea na wadhifa huo.


Rais Magufuli ametoa onyo hilo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti aliposimamishwa na wananchi wa Arusha Mjini akiwa njiani kuelekea Monduli ambako amefunga za "Zoezi Onesha Uwezo Medani" lililoandaliwa na kutekelezwa na kamandi ya Jeshi la nchi kavu ambalo ni sehemu ya jeshi la wananchi wa Tanzania.


Amesema kwa kuwa mvua zinaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi, Viongozi wa Wilaya na Mikoa wana wajibu wa kuwahamasisha wananchi kuzalisha mazao ya chakula ili wasikumbwe na njaa.


Rais Magufuli ameendelea kuwasihi wananchi wa Arusha Mjini kuwa uchaguzi umekwisha na kwamba kilichobaki sasa ni kazi huku akiwahimiza kufanya kazi za uzalishaji mali ikiwemo kilimo.


"Naomba ndugu zangu mniombee, na ninapenda kuwahakikishia kuwa sitawaangusha. Yote niliyoahidi nitayatekeleza bila kubagua nawaombeni mnipe muda na muwe wavumilivu"alisisitiza Rais Magufuli.


Amerejea kauli zake alizozitoa jana alipoingia mkoani Arusha kuwa atendelea kuwashughulikia wezi, mafisadi na watendaji wote wa serikali ambao wamekua wakijineemesha kwa kufuja mali ya umma kupitia kampeni yake ya "Kutumbua Majipu" na amewaomba watanzania wote waendelee kumuombea ili atumbue majipu yote hadi yaishe.


 Rais Magufuli amelazimika kuzungumza na wananchi wa Arusha Mjini waliokuwa wamekusanyika kwa maelfu kando kando mwa barabara na hivyo kujikuta akisimamishwa na wananchi wa Sanawali, Tekniko, Ngarenaro, Kona Ya Nairobi, Mbauda, Majengo Na Kisongo.


Akiwa katika eneo la Ngarenaro wananchi wamelalamikia vitendo vya rushwa vilivyokithiri katika mahakama ya mwanzo ya Maromboso na pia katika eneo la Kona ya Nairobi wananchi wamelalamikia kero za kelele na uchafu wa kiwanda kilichojengwa kandokando mwa barabara ambapo Rais Magufuli ameahidi kufanyia kazi kero hizo.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Arusha.


22 Januari, 2016.  

WATUMISHI NEC WAPONGEZWA KWA KUFANIKISHA UCHAGUZI MKUU 2015

0
0
Afisa Ufuatiliaji toka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Ambrose Manyanda akielezea mafao mbalimbali yanayotolewa na mfuko huo kwa watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) hawapo pichani, wakati wa kikao kazi kilichofanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
: Afisa Ushirika toka Manispaa ya Ilala Bi. Mihayo Malunde akielezea umuhimu wa Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuanzisha kikundi cha akiba na mikopo (SACCOS) wakati wa kikao kazi kilichofanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Ramadhan Kailima (aliyesimama) akiwakaribisha wajumbe na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi wakati Wajumbe hao na Mwenyekiti walipokwenda kuwashukuru na kuwapongeza watumishi wa tume hiyo kwa kuweza kufanikisha zoezi la uchaguzi kwa mafanikio makubwa.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akiongea na watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakati alipokwenda kuwashukuru na kuwapongeza watumishi wa tume hiyo kwa kuweza kufanikisha zoezi la uchaguzi kwa mafanikio makubwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Ramadhan Kailima (aliyesimama) akifurahia jambo na watumishi wa tume hiyo wakati Wajumbe na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi walipokwenda kuwashukuru na kuwapongeza watumishi wa tume hiyo kwa kuweza kufanikisha zoezi la uchaguzi kwa mafanikio makubwa.Picha zote na Eliphace Marwa -Maelezo

DK SHEIN ASHIRIKI KATIKA MAZISHI YA MAKAMU MWENYEKITI WA UWT KATIKA KIJIJI CHA KIANGA WILAYA YA MAGHARIBI B UNGUJA

0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, kushoto Baba Mazazi wa Marehemu Asha Bakari Makame Mzee Bakari Makame na Viongozi wengine wakiwa katika mazishi ya Marehemu Makamu Mwenyekiti wa UWT Zanzibar Asha Bakari Makame katika makaburi ya Kianga wakati wa mazishi hayo leo asubuhi.
VIJANAS wa Chama cha Mapinduzi wakiwa amebeba jeneza likiwa na Mwili wa Marehemu Asha Bakari Makame wakati wa maziko yake katika kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharibi B Unguja leo asubuhi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, na Viongozi wa Serikali wakishiriki katika Mazishi ya Marehemu Makamu Mwenyekiti wa UWT Zanzibar Asha Bakari Makame katika makaburi ya Kijiji cha Kianga nje kidogo ya Mji wa Unguja Wilaya Magharibi B.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwaka mchanga katika kaburi la marehemu Asha Bakari Makame.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Asha Bakari Makame.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Asha Bakari Makame.
MAKAMU wa Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Mohammed Gharib Bilal akiweka mchanga katika kaburi.
BABA Mzazi wa Marehemu Mzee Bakari Makame akiwaka mchanga katika kaburi la mwanawe baada kuzikwa katika makaburi ya Kianga Kijijini Wilaya ya Magharibi B Unguja.
WANANCHI wakihughuria mazishi ya Marehemu Makamu Mwenyekiti wa UWT Zanzibar Asha Bakari Makame katika makaburi ya Kianga Wilaya ya Magharibi B Unguja leo asubuhi.(Picha na Ikulu)

SERIKALI YAJA NA MIKAKATI MIPYA YA KUHAKIKISHA UTALII WA NDANI UNAKUA

0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii,Bi. Uzeeli Kiangi akisisitiza jambo wakati alipokuwa anamkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja. Generali. Gaudence Milanzi kufungua Mkutano Mkutano wa Kamati ya Uwezeshaji Utalii ( Tourism Facilitation Committee- TFC) uliofanyika leo Mpingo House jijini Dar es Salaam wa kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Utalii nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja. Generali. Gaudence Milanzi ( kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Bw. Deogratius Mdamu (kushoto) wakimsikiliza Mjumbe ( hayupo pichani ) wakati wa Mkutano wa Kamati ya Uwezeshaji Utalii ( Tourism Facilitation Committee- TFC) uliofanyika leo Mpingo House jijini Dar es Salaam akiwa anazungumzia changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Utalii nchini na kutoa ushauri ya namna kuuimarisha Utalii wa ndani ambao umekuwa bado ni changamoto kwa wananchi wengi kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini
Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Uwezeshaji Utalii ( Tourism Facilitation Committee- TFC) wakiwa wanajadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Utalii nchini kwa kutoa maoni, ushauri na ufumbuzi wa changamoto ikiwa na kuchangia mikakati mbalimbali itakayowezesha kusaidia kuhamasisha Utalii wa ndani.

Wakati nchi nyingi Afrika zikiwa zinafanya jitihada mbalimbali za kuimarisha Utalii wa ndani ambao umekuwa ndo wa uhakika katika kuiingizia nchi mapato hata pale majanga yanapotokea, Nayo Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeendelea kuhakikisha kuwa Utalii wa ndani unakua kwa kasi inayotarajiwa


Baadhi ya Majanga hayo yanayoathiri Sekta ya Utalii ni milipuko ya magonjwa kama Ebola, matukio ya Ugaidi Kenya na kushuka kwa Euro ya Ulaya dhidi ya Dola ya Marekani.

Hivyo Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wadau wa Utalii nchini wamepanga mikakati ya kuhakikisha kuwa Utalii wa ndani unakuwa tegemeo tofauti na sasa ambapo Watalii kutoka nje ndio wamekuwa wamekuwa wakitembelea hifadhi zetu kwa kiasi kikubwa.

Akizungumza kwenye Mkutano wa Kamati ya Uwezeshaji Utalii ijulikanayo kama Tourism Facilitation Committee ( TFC) uliofanyika leo Mpingo House jijini Dar esSalaam , Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili, Meja. Generali. Gaudence Milanzi na Utalii amesema maendeleo ya Utalii yanahitaji sana Utalii wa ndani kuimarika baadala ya kudhani kuwa vivutio vya utalii vilivyopo ni kwa ajili ya wageni kutoka nchi za nje.

Meja. Generali. Milanzi amesema Utalii ni sekta nyeti sana katika kuliingiza Taifa pesa za kigeni lakini hata hivyo ni sekta ambayo imekuwa inaathirika kwa haraka sana pindi majanga yanapotokea nchi jirani hivyo ni lazima jamii ijengewe utamaduni wa kutembelea vivutio vya Utalii ili kuweza kujihakikishia Watalii wa ndani wanakuwa wengi.

Baadhi ya mikakati iliyopendekezwa na Wajumbe wa kamati ya Uwezeshaji Utalii (TFC) ni kuwawezesha maafisa Utalii wa Halmashauri wanatengewa bajeti ya kutosha, wanajengewa uwezo kuhusu ya vivutio vya utalii vilivyopo kwenye maeneo yao pamoja na Idara ya Utalii kufungua ofisi kila kanda ili kuweza kutimiza majukumu yake ipasavyo.

Aidha,viwanja vya ndege vilivyopo nchini viimarishwe ikiwa pamoja na nchi kuwa ndege zake kama ilivyo kwa nchi jirani kama Kenya na Rwanda Awali , Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii,Bi. Uzeeli Kiangi alisema Mkutano wa TFC hutoa fursa za kuziibua na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Utalii hivyo Sekta Binafsi zinawajibu mkubwa wa kuhakikisha changamoto zinazoikabili sekta zinatafutiwa ufumbuzi Aliongeza kuwa Idara ya Utalii imekuwa ikishiriki katika maonesho mbalimbali ya kitaifa lengo likiwa ni kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya Utalii nchini.

Aidha, Prof Wineastor Anderson amesema sekta ya Utalii imekuwa inakua lakini si kwa kiwango cha kuridhisha hivyo jitihada za kutangaza utalii ndani na nje nchi upewe uzito unaostahili kwa kuiwezesha Bodi ya Taifa ya Utalii inatengewa bajeti ya kutosha.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya Utalii Tanzania ( TCT) Bw. Richard Rugimbana, amesema Utalii wa ndani ili uweze kukua suala la elimu linahitajika kutolewa ili kuweza kuibadilisha jamii ipende kutembelea vivutio vya Utalii.

Naye Kamanda wa Polisi Jk Ndaki anayeshghulikia dawati la Utalii ( Tourism Police Unit) amewahakikishia usalama wao watalii wa ndani na nje ya nchi kutembelea vivutio vya Utalii bila hofu yoyote kuwa Jeshi la Polisi nchini lipo macho muda wote.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images