Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 742 | 743 | (Page 744) | 745 | 746 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Mwenyekiti wa Good News for All Ministry, Askofu Charles Gadi akizungumza na waaandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu mkutano wa maombi siku ya Jumatano ya tarehe 20 Januari mwaka huu katika eneo la Soko la Samaki Feri ili kuomba Mungu kuepusha ongezeko la joto nchini kushoto ni Katibu wa Good News For All Ministry Mchungaji Palemo Massawe.
   Picha na Beatrice Lyimo Maelezo

  Na Beatrice Lyimo- Maelezo
  MWENYEKITI wa Good News for All Ministry, Askofu Charles Gadi ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kumuomba Mungu dhidi ya hali ya hewa ya joto kali nchini.

  Askfou huyo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar e s Salaam mara baada ya Mamlaka ya hali ya hewa kuonyesha hali ya joto kufika nyuzi joto 35°C.

  Askofu Gadi ameongeza kuwa, wanatarajia kufanya mkutano wa maombi  siku ya Jumatano ya tarehe 20 Januari mwaka huu katika eneo la Soko la Samaki maarufu kama Feri ili kuomba Mungu  kuepusha ongezeko la joto nchini.

  “Joto limesambaa katika maeneo ya pwani hususani Dar es Salaam, Tanga, na visiwa vya Zanzibar, hivyo kwa hali hii tumeona tufanye mkutano wa maombi mafupi katika eneo la Soko la samaki la feri siku ya Jumatano kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 6 mchana,

  “Mungu amenipa nafasi ya kuomba dhidi ya majanga ya kimazingira kama haya hivyo tunawakaribisha watu wote wa Dar es Salaam tuje tumlilie Mungu kwa pamoja ili tuondokane na janga hili la joto na madhara ya Elnino” alifafanua Askofu Gadi.

  Kwa upande wake katibu wa Good News For All Ministry Mchungaji Palemo Massawe amewataka  Wananchi kuchukua hatua ili kujikinga dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu kwa kufanya usafi katika mazingira yanayowazunguka.

  Uongozi huo unaendelea na maombi ya kumuombea Rais John Pombe Magufuli kufanikiwa katika juhudi zake za kulikomboa nchi kiuchumi na kielimu.

  0 0


  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. 
  KUHUSU UPOTOSHWAJI WA TAARIFA ZILIZOANDIKWA NA GAZETI LA MWANAHALISI KUHUSIANA NA UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA  KIJITOUPELE


  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), inapenda kutaarifu Umma na Watanzania kwa ujumla kuwa Jimbo la Kijitoupele lililoko  Zanzibar ni miongoni mwa Majimbo hamsini(50) ambayo yalitegemewa kufanya uchaguzi mkuu tarehe 25, oktoba,2015. 

  Hata hivyo Jimbo hilo halikufanya uchaguzi wake wa Mbunge kutokana na hitilafu katika karatasi za kupigia kura badala Wapiga kura walishiriki katika kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano.


  Tume imefikia uamuzi wa kutoa ufafanuzi huu kutokana na taarifa iliyochapishwa na gazeti la MwanaHalisi toleo l Na.322 la Januari 18, 2016 katika ukurasa wake wa mbele likidai  “ NEC YAIBUA MAPYA” Habari hii si sahihi na inalenga kuupotosha umma na kuleta uchochezi miongoni mwa Wananchi.


  Kwa ujumla maelezo yote yaliyopo katika taarifa hiyo yanaeleza kwamba, Tume imeanzisha Jimbio jipya, kwa mujibu wa taarifa ya gazeti husika ni Jimbo la Kijitoupele – Zanzibar.


  Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda inasisitiza kuwa taarifa zilizotolewa na Gazeti la MwanaHALISI siyo za kweli, ni za uongo, uzushi, uzandiki na uchochezi. Kufuatia taarifa hiyo,Tume inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:

  •          Tarehe 13 Julai, 2015 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari ikionesha Orodha ya Majimbo yatakayofanya uchaguzi wa Mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na Jimbo la Kijitoupele lipo katika Orodha hiyo. Taarifa hii ipo katika tovuti ya Tume.

  •          Katika Taarifa hiyo, Tume ilieleza wazi kuwa Majimbo ya Zanzibar yataendelea kuwa hamsini (50), ingawaje Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imeongeza majimbo manne na kuwa Hamsini na Nne (54).

  •          Tulieza sababu ya kubaki na Majimbo hamsini (50) ni kutokana na matakwa ya Ibara ya 98 (1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo ili kuongeza idadi ya wabunge kutoka Zanzibar inahitaji theluthi mbili ya Wabunge kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya Wabunge kutoka Zanzibar kuunga mkono mabadiliko hayo.

  •          Tulieza kuwa, kipindi hicho Tume isingeweza kuandaa na kuwasilisha Muswada Bungeni kwa kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilikuwa linamaliza muda.


  •          Katika taarifa hiyo, ilifafanuliwa kuwa, ili kubaki na majimbo Hamsini (50), kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, majimbo manne yaliunganishwa kwa ajili ya Uchaguzi wa Wabuge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaotoka Zanzibar.

  •          Majimbo yaliyounganishwa ni:

  1.         Jimbo la Bububu liliunganishwa na Jimbo la Mtoni, likaitwa jimbo la Bububu

  2.         Jimbo la Mwera liliunganishwa na Mto pepo likaitwa jimbo la Mwera

  3.         Jimbo la Kiembesamaki liliunganishwa na Chukwani likaitwa jimbo la Kiembesamaki

  4.         Jimbo la Pangawe liliunganishwa Kijitoupele likaitwa Kijitoupele

  •          Kwa mantiki hiyo Jimbo la Kijitoupele ni mojawapo ya Majimbo hayo (50) ambayo Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilisimamia na kuratibu Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge.

  •          Tarehe 28 Oktoba, 2015 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitoa taarifa kwa Umma kuwa, ilishapokea Matokeo ya Kura za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa kutoka Majimbo yote ya Zanzibar na siyo “siyo Matokeo ya Ubunge”


  •          Tarehe 19 Desemba, 2015 Tume ilitoa orodha ya Majimbo ambayo hayajafanya Uchaguzi wa Wabunge tarehe 25 Oktoba, 2015 kutokana na hililafu mbalimbali, mojawapo ya majimbo hayo nane (8), jimbo la Kijitoupele - Zanzibar ni miongoni.

  Ni vema wananchi wakafahamu kwamba, Tume ya Taifa ya Uchaguzi haianzishi na haijaanzisha Jimbo jipya la Uchaguzi baada ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015.

  Hii inaonesha ni kiasi gani Mhariri wa Gazeti la MwanaHALISI alivyodhamiria kuupotosha Umma kwani katika Makala/Taarifa hiyo hiyo ambayo anadai hakuna Jimbo la Kijitoupele (Unguja); anaeleza kuwa tarehe 25 Oktoba 2015 wapiga Kura wa Jimbo la Kijitoupele walikosa fursa ya kumchagua Mbunge. Amemtaja Mhariri wa Gazeti la MwanaHALISI kuwa ni Wapiga Kura wa Jimbo la Kijitoupele, ambalo anadai eti Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeliibua miezi mitatu baada ya Uchaguzi.  Huu ni uongo na upotoshwaji wa makusudi kabisa.


  Tume inapenda wananchi waelewe kuwa, hata kabla Tume ya Uchaguzi haijafuta matokeo wa Zanzibar, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilikuwa imesha tangaza kuahirisha Uchaguzi katika Majimbo nane (8) likiwemo la Kijitoupele kwa sababu za Vifo vya Wagombea na hitilafu mbalimbali. 


  Jimbo la Kijitoupele la Zanzibar ni miongoni mwa majimbo nane (8) ambayo yaliahirishwa kufanya uchaguzi wa Wabunge tarehe 25 Oktoba, 2015, ambapo majimbo sita (6) ambayo ni Lushoto, Ulanga Mashariki, Masasi Mjini, Ludewa, Handeni Mjini na Arusha Mjini yaliahirishwa kutokana na vifo vya wagombea na majimbo mawili (2) ya Kijitoupele - Zanzibar na Jimbo la Lulindi – Masasi yaliahirishwa kutokana na hitilafu mbalimbali.


  Hoja nyingine iliyotolewa na gazeti hilo ilihusu uteuzi wa Uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalum. Ifahamike kwamba katika maamuzi yake kuhusiana na viti maalum, Tume imezingatia matakwa ya Ibara ya 78 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inayoeleza kuwa, ili chama kilichoshiriki Uchaguzi Mkuu kipate Viti Maalum ni lazima kiwe kimepata angalau asilimia tano (5%) ya Kura zote halali za Ubunge.  Hivyo, Viti Maalum vilivyobaki haviwezi kugawanywa hadi hapo Jimbo la Kijitoupele litakapofanya Uchaguzi katika tarehe ambayo itaitangazwa  na Tume hapo baadaye.


  Mhariri wa Gazeti la MwanaHALISI alipaswa kufanya uchunguzi na uchambuzi wa kina kuhusu habari aliyoiachapisha ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Viongozi wa Tume ya Uchaguzi  ili wapate ufafanuzi wa Majimbo ya Uchaguzi na siyo kutoa Taarifa za uongo, uchochezi na upotoshaji kama walivyofanya.


  Mhariri wa Gazeti la MwanaHALISI atambue uandishi wa habari ni zaidi ya kushika kalamu na kuandika, unahusisha uwezo wa kutafuta habari pande zote mbili ili kupata mizania ya habari anayoiandika, kufanya utafiti, kujiridhisha pasipo shaka kuwa habari anayoitoa ni sahihi.


  Kwa kuwa Mhariri wa Gazeti la MwanaHALISI alikusudia kuupotosha umma kwa sababu anazozifahamu yeye mwenyewe kwa kutoa Taarifa zisizo sahihi, za uongo na uchochezi Tume ya Taifa ya Uchaguzi inamtaka Mhariri wa MwanaHALISI KUIOMBA RADHI TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI, UKURASA WA MBELE  WA TOLEO LIJALO KAMA ALIVYOFANYA KATIKA GAZETI HILO.

  Kama wasipofanya hivyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi italichukulia Gazeti la MwanaHALISI hatua za Kisheria.


  Imetolewa na
  Kailima,R.K

  MKURUGENZI WA UCHAGUZI.

  0 0


  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiambatana pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al – Sumait wakiingia kwenye uwanja kwa ajili ya Mahfali ya 15 ya chuo hicho hapo Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Kulia ya Balozi Seif ambae alimuwakilisha Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein kwenye Mahafali hayo ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Hicho Dr. Abdulrahman Al - Muhailan na kushoto ya Balozi Seif ni Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho Profesa Hamed Rashid Hikmany.


   Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al – Sumait wakiingia kwa maandamano kwenye uwanja kwa ajili ya kupewa stashahada zao.
    Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al – Sumait, Dr. Abdulrahman Al – Muhailan akitoa salamu kwenye mahafali ya 15 ya chuo hicho hapo chukwani.
    
   Balozi Seif kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Shein akimkabidhi zawadi mwanafunzi Bora wa Daraja la kwanza katika Fani ya Kiarabu na Dini Kijana Nuru Ally Nassor Muhanna.
   Balozi Seif Ali Iddi akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu hicho Dr. Abdulrahman Al – Muhailan kwenye mahafali ya 15 ya chuo hicho hapo chukwani.
   Seif pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu hicho Dr. Abdulrahman Al – Muhailan wakifurahia jambo mara baada ya kumalizika kwa mahfali ya 15 ya wahitimu 686 wa chuo hicho. Aliyepo kati kati yao ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamuhuni.

   Balozi Seif akiagana na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kubmu ya Dr. Abdulrahman Al – Sumait, Dr. Abdulrahman Al – Muhailan hapo Chukwani.Wa kwanza kulia anayeshuhudia maagano hayo ni Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho Profesa Hamed Rashid Hikmany.


  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein alisema Vyuo Vikuu Nchini licha ya kuendelea kutoa taaluma kwa vijana wa elimu ya juu lakini bado vina wajibu na jukumu kubwa la kuhakikisha wasomi wake wanatumia vipaji vyao katika kufanya tafiti kwenye maeneo mbali mbali.

  Alisema tafiti hizo zinaweza kuwa na mchango mkubwa kwa wasomi wachanga wanaoanza kupata taaluma kwenye Vyuo hivyo sambamba na kuliwezesha Taifa kupiga hatua za haraka za Maendeleo.

  Dr. Ali Moh’d Shein alitoa kauli hiyo wakati wa mahafali ya 15 ya Wahitimu 686 wa digrii ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al - Sumait kiliopo Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamuwa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

  Alisema kuimarika kwa eneo la utafiti kutatoa fursa kwa wananchi mbali ya kupata elimu katika kiwango cha juu lakini pia watapata mbinu na maarifa ya kukabiliana na changamoto zilizowakabili maisha yao ya kila siku.

  Rais wa Zanzibar alisema mchango mkubwa unaotolewa na Vyuo vikuu hapa Nchini hasa vile vyuo vikuu Binafsi umesaidia ongezeko kubwa la Walimu wa skuli mbali mbali za Sekondari hapa Visiwani.

  Mapema Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al Sumait Chukwani Profesa Hamed Rashid Hikmany alisema kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wa chuo hicho mwaka huu kimeongezeka mara dufu kutokana na mikakati mizuri iliyowekwa na Uongozi wa Chuo hicho.

  Profesa Hikmany alisema malengo ya uongozi wa chuo hicho kwa sasa ni kuimarisha zaidi utoaji wa wanafunzi wenye kiwango bora zaidi utakaokidhi mahitaji ya taaluma kimataifa.

  Akitoa salamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al - Sumait, Dr. Abdulrahman Al - Muhailan alisema Uongozi wa Chuo hicho utaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha Sekta ya Elimu.

  Dr. Al - Muhailan alisema hatua hii inalenga kuimarisha uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya Wananchi wa Zanzibar na Kuweit kupitia sekta za mendeleo na ustawi wa jamii ambazo tayari zimeshaleta mafanikio makubwa kwa pande hizo mbili rafiki.

  Jumla ya wanafunzi 686 wa fani za Sayansi, Sanaa, Lugha ya Kiswahili, Kiarabu mfunzo ya Dini ya Kislamu wamehitimu mafunzo yao na kukabidhiwa stashahada ya kwanza.
  Othman Khamis Ame
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

  19/1/2016.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh:Abbas Kandoro akizungumza na Waandishi wa Habari hawapo Pichani nje ya Ukumbi wa Mkapa uliopo Sokomatola Jijini Mbeya katika Semina ya Wadau wa Elimu wa Mkoa wa Mbeya na Mkowa wa Katavi ambao wamekutana leo kuzungumzia juu ya Mbinu ambazo wanazitumia Mkoa wa Katavi kufanikiwa kufaulisha Wanafunzi kwa Asilimia kubwa kulinganisha na Mkowa wa Mbeya na Mikoa mingine.
  Kutoka Kushoto ni Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya Ndugu,Charles Mwakalila na Afisa Elimu Mkoa wa Katavi Ndugu,Helenest Hinju akizungumza na Wadau wa Elimu Mkowa wa Mbeya na Katavi hawapo Pichani katika Semina ya Wadau wa Elimu iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya.
  Baadhi ya Wadau wa Elimu Mkowa wa Mbeya na Katavi wakisikiliza kwa makini Semina hiyo ya siku mbili juu ya Mbinu za Ongezeko la ufauru kwa Dalasa la Saba Mkoa wa Mbeya.
  PICHA NA MR.PENGO GLOBU YA JAMII MBEYA.

  0 0

  Hali ya kiwanja cha Jangwani wakati mvua ikiendelea kunyesha jijini Dar es Salaam hii leo ikiwa mvua imenyesha kuanzia usiku hadi asubuhi.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mhe. Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) ambaye ni mgeni rasmi wa mkutano huo, akiongea na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa NEC (hawapo pichani) leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam kuhusu masuala ya maadili na na ufanisi kazini.
  Mkurugenzi wa Uchaguzi, Bwana Ramadhani Kailima akiongea na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa NEC (hawapo pichani) leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam kuhusu masuala ya maadili na na ufanisi kazini kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza 
  Mkurugenzi wa Uchaguzi, Bwana Ramadhani Kailima wakazi akizungumza katika ukumbi wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
  (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO).


  · Awataka kuzingatia maadili na Kanuni za Utawala bora na maadili katika utendaji kazi,
  · Awataka kuepukana na rushwa na kushinda vishawishi vya rushwa.

  MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mhe. Jaji Mstaafu Damian Lubuva amewataka Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa NEC kuboresha mazingira ya kazi na kuongeza ufanisi ikiwemo kuzingatia maadili na kanuni za Utawala Bora na kuepukana na rushwa.

  Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dar es Salaam wakati alipofungua Mkutano wa Kumi na Mbili wa Baraza la Wafanyakazi na kuongea na Wajumbe wa Tume hiyo pamoja na Wajumbe wengine wa TUGHE ngazi ya Taifa na Matawi.

  Jaji Lubuva amesema kuwa, Mabaraza ya Wafanyakazi yameundwa Kisheria kwa madhumuni ya kuishauri Serikali katika ngazi ya Taasisi ili kusimamia rasilimali pamoja na utekelezaji wa majukumu ya Taasisi husika, hivyo kufanyika kwa mkutano huo ni moja ya chachu ya kuboresha mazingira ya kazi na kuongeza ufanisi na tija katika Taasisi hiyo.

  Akizungumzia kuhusu masuala ya rushwa, Jaji Lubuva ameeleza kuwa, moja ya jukumu la NEC ni kuimarisha na kukuza demokrasia na Utawala Bora, hivyo watumishi wa Tume hiyo hawanabudi kuzingatia maadili na kanuni za utawala bora na maadili katika utendaji wa kazi zao pamoja na kuepukana na vitendo vya rushwa na vishawishi vyake.

  ‘’Nimeambiwa kuwa, katika kikao hiki mtajadili kuhusu mada mbalimbali kama vile Taratibu za Utendaji kazi Serikalini, masuala ya uanzishaji SACCOS, Utekelezaji wa Bajeti na miradi ya Maendeleo, Ukimwi, Bima ya Afya na masuala ya Madawa ya kulevya, niwaombe kujadili mada hizo kwa kina na busara huku mkitambua kuwa matokeo ya majadiliano yenu ni kwa ajili ya maslahi ya Taasisi yetu na Taifa kwa ujumla’’, alisema Lubuva.

  Kwa upande mwingine, Jaji Lubuva amewataka wajumbe wa Baraza hilo kujadili masuala ya afya kwa Wafanyakazi hususani suala la ugonjwa waUkimwi katika sehemu ya kazi ambapo aliwaasa kila mfanyakazi kujikinga dhidi ya janga hilo kwa kulinda afya yake na ya familia yake ili Taifa liweze kunufaika na nguvu kazi iliyopo.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Ramadhani Kailima ameitaka jamii kuondokana na dhana potofu dhidi ya Tume hiyo kuwa mara baada ya Uchaguzi Mkuu na chaguzi ndogo zilizofanyika Tume hiyo imekuwa haina kazi ya kufanya mpaka uchaguzi mwingine kwa kufafanua kuwa, Tume hiyo ina majukumu mengi hata baada ya uchaguzi ikiwemo Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, Uandaaji na Uratibu wa Kura za Maoni ya Katiba Inayopendekezwa, Uratibu wa Marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi.

  ‘’Sio kweli kwamba Tume ya Uchaguzi mara bada ya Uchaguzi Mkuu na chaguzi nyingine ndogo zilizofanyika kwamba ndo basi hatuna cha kufanya, Tume ina majukumu mengi hata baada ya uchaguzi kama vile Uratibu na Usimamizi wa Utungwaji wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Uundaji wa Mpango Mkakati wa Tume, Uandaaji wa Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa wateja, Usimamizi wa Ujenzi wa Jengo la Tume na Usimamizi wa chaguzi ndogo pale zinapojitokeza na Mrekebisho ya Muundo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi’’, alisema Kailima.


  Mkutano huo umefunguliwa leo ukiwahusisha Watumishi wa Taasisi toka NEC, Wajumbe wa TUGHE ngazi ya Taifa na Matawi ambao jumla yao ni 54.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitia saini kitabu cha kumbukumbu kufuatia kifo cha aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere alifariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa, wakati Makamu wa Rais alipofika Nyumbani kwa Marehemu Msasani Dar es salaam leo Januari 21, 2016.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Makamu wa Rais mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilal walipokutana Msasani Dar es salaam leo Januari 20, 2016 wakati wa kuaga Mwili wa aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere alifariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kulia na Rais mstaafu Dkt. Jakaya M Kikwete, wakizungumza walipokutana leo Januari 20, 2016 Msasani Dar es salaam kwenye shuhuli ya kuaga Mwili wa aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere alifariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitoa heshima za mwisho leo Januar 20,2016 wakati wa Mwili wa aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere alifariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa. 
  (Picha na OMR).

  0 0

  Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akiwaongoza wanahabari kupata chai maalum iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya pamoja na kufahamiana zaidi ikiwemo huduma na utendaji kazi kwa hapa nchini. 

  (Picha zote na Andrew Chale, modewjiblog).

  Baadhi ya wanahabari wakiwa katika shughuli hiyo maalum iliyoandaliwa kwa ajili yao na MultChoice Tanzania ambao ni wasambazaji wa ving'amuzi vya DSTV kwa Tanzania.
  Baadhi ya wanahabari wakipata Chai katika shughuli hiyo maalum iliyoandaliwa kwa ajili yao na MultChoice Tanzania ambao ni wasambazaji wa ving'amuzi vya DSTV kwa Tanzania.

  Watendaji wa Multchoice Tanzania wakitoa shukrani zao kwa wanahabari waliofika katika mwaliko maalum wa kuukaribisha mwaka pamoja na kufahamiana zaidi halfa iliyofanyika mapema asubuhi ya leo katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. 
  Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu (kulia) akiwa na Shumbana Walwa wa kampuni hiyo akipata picha ya kumbukumbu.


  Washindi watatu ambao ni wanahabari wakipata picha ya pamoja na zawaidi zao ambao wamejishindia ving'amuzi vya DStv na hofa za kifurushi cha mwezi mmoja pamoja na kufungiwa bure majumbani kwao.
  Wanahabari walioshinda vifurushi vya mwezi vya "Premium" wakipata picha ya pamoja na maafisa wa Multchoice Tanzania 
  Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu (kulia) akizungumza na wanahabari kuhusiana na siku hiyo maalum ya kukaribisha mwaka mpya pamoja na kuandaa chai maalum kwa wanahabari.
  Wanahabari wakibadilishana mawazo na Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo katika halfa hiyo makao ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  IMG_0652

  Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla.

  Na Rabi Hume, Modewjiblog
  Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameanzisha kikosi kazi cha watu 24 ambacho kitakuwa na kazi ya kutengeneza mpango mkakati wa kuwezesha kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).

  Katika taarifa ambayo imetolewa na Dkt. Kigwangala imeeleza kuwa kazi ya kuanzisha kikosi kazi hicho ni agizo kutoka kwa Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ambaye alimtaka aanzishe kikosi hicho ili washirikiane kuanzisha mpango mkakati wa kuwezesha kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii.

  “Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu alinipa kazi ya kuunda kikosi kazi maalum na kushirikiana nacho kutengeneza mpango mkakati wa kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF),” alisema Dkt. Kigwangalla.
  Dkt. Kigwangalla amewataja wajumbe wa kikosi kazi hicho kuwa ni Prof. Angwara Kiwara, Prof. Phares Mujinja, Dkt. Francis Frederick, Dkt. Heri Marwa, Dkt. Deogratius Pisa, Dkt. Amos Kahwa, Irenei Kiria, Semkae Kilonzo, Gemini Mtei, Dkt. Jehovaness Aikaeli na Obey Assey.

  Wengine ni Mathias Kabunduguru, Dkt. Dereck Chitama, Prof. Flora Kessy, Florence Mwanri, Athuman Rehani, Maximillian Mapunda, Bedason Shallanda, Daniel Ngowi, Beng' Issa, Edwin Mikongoti, Hussein Sengu, Dkt. Beatus Leon na Dkt. Pastory Sekule.Aidha Dkt. Kigwangalla amewashukuru wajumbe hao kwa kukubali kufanya kazi na wizara ya afya kupitia mpango mkakati wa kuwezesha kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii bila malipo yoyote.

  Hata hivyo mara baada ya kuwachagua wajumbe wa kikosi kazi hicho tayari kimependekeza mapendekezo yao jinsi ya kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii ambayo ni kuipa nguvu kadi ya CHF ili itumike kwenye mfumo wa Afya mpaka ngazi ya Hospitali za Rufaa za Mikoa na vituo vya Jirani na kupandisha kiwango cha kuchangia CHF mpaka 30,000.

  Mapendekezo mengine ni kuweka bei za kukatisha tamaa watumiaji wa huduma za Afya bila kadi ya Bima ya Afya ama ya CHF na kuwahamasisha waamue kujiunga kuliko kulipa gharama za kila huduma watakayotumia, kuhamisha Mfuko wa fedha za CHF kutoka Halmashauri na kuupeleka NHIF ngazi ya mkoa lengo likiwa kumtenganisha mtoa huduma na mteja na kuweka 10,000 kuwa kiwango cha chini kwa bei za huduma za afya sehemu yoyote nchini kwa mtu asiye na kadi.

  Aidha mapendekezo yao yatatumika kama serikali itayaridhia na wao wametoa mapendekezo hayo kutokana na kutambua kuwa Watanzania wapo tayari kulipia huduma za afya kwa bima ilimradi wawe wanapatiwa huduma bora ambazo zitawaridhisha.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Hiiti Sillo akizungumza na waandishi wa habari juu ya uhamasishaji wa masuala ya Chakula Salama iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya waandis wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, hayupo pichani leo makao makuu ya TFDA jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa TFDA, Raymond Wigenge akizungumza na waandishi habari juu ya jamii kufuata taratibu za uandaji wa chakula ili kuweza kuwa salama kuepuka magonjwa yanayotokana viini vya vimelea vya magonjwa katika chakula iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
  WANANCHI wametakiwa kuangalia usalama wa chakula ili kuweza kuepuka vimelea vya viini vya magonjwa yanayotokana na kula chakula kisicho salama.

  Hayo ameyasema jana Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakulana Dawa (TFDA),Hiiti Sillo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya uhamasishaji masuala ya usalama wa Chakula, amesema kula chakula chenye usalama inafanya kuwa taifa la maendeleo kiuchumi.

  Amesema kuwa chakula ni muhimu kwa maisha ya binadamu kwa kula chakula ambacho hakijachafuliwa na viini vya magonjwa kama, kuhara,kipindupindu.

  Sillo amesema watu milioni 91 duniani wanaugua magonjwa kutokana na kula chakula kilichochafuliwa na viini vya vimelea magonjwa.

  Amesema TFDA licha kuwa na changamoto lakini wameweza kuwa na mafanikio kwa kuweka watendaji mipakani pamoja na viwanja vya ndege na bandari wa kufanya ukaguzi wavyakula vinavyoingia 

  Aidha amesema usalama chakula ni elimu endelevu hivyo kila mtu kwa nafasi yake ahakikishe anakula chakula salama ambacho hakina vimelea vinavyoweza kusababisha ugonjwa.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio akizungumza katika semina ya wadau wa gesi leo jijini Dar es Salaam.


  Mkurugenzi wa uzalishaji, uchakataji, usafirishaji na usambazaji kutoka TPDC, Dkt. Wellington Hudson akizungumza katika semina na wadau wa gesi leo jijini Dar es Salaam.

  KATIKA kutekeleza azma ya Serikali kuanzisha viwanda mbalimbali nchini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kushirikiana na Kampuni ya Ferostaal Industrial Project GmbH (wawekezaji kutoka Ujerumani) na washirika wake wameinigia makubaliano (Joint Venture) ya kutekeleza mradi wa mbolea. Mradi huu unalenga kuzalisha tani 3,850 za mbolea kwa siku na utatumia gesi kiasi cha futi za ujazo milioni 104 kwa siku. 

  Akizungumza na Madiwani wa Halmashauri ya Kilwa, Mkurugenzi wa uzalishaji, uchakataji, usafirishaji na usambazaji kutoka TPDC, Dkt. Wellington Hudson alisema ujenzi wa kiwanda hiki unalenga kuzalisha aina mbili za mbolea ambazo ni ammonia na urea na uwekezaji wake unatarajiwa kugharimu dola za marekani bilioni 1.9. Dkt. Hudson aliyasema haya wakati wa semina ya kujenga uelewa kwa Madiwani na viongozi wengine wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa juu ya miradi mbalimbali ya gesi asilia inayopangwa kutekelezwa katika Wilaya ya Kilwa na Mkoa wa Lindi kwa ujumla. 

  Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio akizungumza katika semina hiyo alisema mradi huu wa mbolea unatarajiwa kutoa ajira takribani 5000 za moja kwa moja, kufungua fursa zaidi za kutoa huduma na kuuza bidhaa kipindi cha ujenzi na hata kipindi cha kutekeleza mradi huu. Vile vile, mradi utaongeza pato kwa Halmashauri kwa uongeza uzalishaji wa gesi asilia na kuboresha huduma mbalimbali kama vile za afya, kiwanja cha ndege, bandari, huduma za afya na nyinginezo nyingi.

  Semina hiyo ilihudhuriwa na Madiwani wote wa Wilaya ya Kilwa, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Kilwa, Wabunge, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mkurugenzi wa Wilaya na Wakurugenzi wengine wa Halmashauri na ililenga kujenga uhusiano na kuboresha mahusiano baina ya TPDC na Wilaya ya Kilwa. 

  Ugunduzi wa gesi asilia nchini umeendelea kufungua fursa zaidi za uwekezaji na kuendelea kukuza uchumi. Mpaka sasa tayari takribani asilimia 70% ya umeme unaotumika hapa nchini unazalishwa kwa gesi asilia. Kwa mujibu wa taarifa kutoka TPDC tayari viwanda vipatavyo 37 jijini Dar es Salaam vinatumia gesi asilia. 

  0 0

  naw1

  Wananchi wa Kata ya Nyengedi Lindi wakimsikiliza Mh. Nawanda DC wa Lindi akiwaelimisha umuhimu wa CHF katika kampeni ya uhamasishaji unaofanywa na NHIF kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya hiyo
  naw2
  Mkuu wa wilaya ya Lindi Mh. Yahya Nawanda akiwasikiliza akisikiliza kwa makini hoja za wana Nyengedi ili kupata mrejesho wa huduma za afya katika kata hiyo. wakati alipokuwa akiwaelimisha kuhusu umuhimu wa huduma za CHF katika kampeni ya uhamasishaji inayofanywa na NHIF kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya hiyo
  naw3
  Mkuu wa wilaya ya Lindi Mh. Yahya Nawanda akisisiztiza jambo wakati NHIF ilipozindua kampeni hizo katika wilaya ya Lindi mkoa wa Lindi kulia ni Mkuu wa mkoa huo Mh. Jordan Lugimbana na kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa na Eugine Mikongoti Mkurugenzi wa wa Huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Tanzania, NHIF
  naw4
  Wana Nyengedi wakipima ili kujua afya zao katika kampeni ya CHF.
  naw5
  Wanakijiji wa Nyengedi wakidunduliza fedha ili kufikisha mchango wa sh. 10,000 kwa kaya ili wajisajili na CHF baada ya kuhamasika.
  ............................................
  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kishirikiana na Halmashauri ya Lindi Vijijini wameendelea na kampeni ya uhamasishaji wa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii CHF katika kata ya Nyangedi.Katika uhamasishaji huo uliongizwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Nawanda kaya 70 zilijiunga papo hapo kwa kuchangia Shilingi 10,000 kwa kaya hivyo jumla ya Shilingi 700,000 zilikusanywa.

  Aidha Mh. Nawanda alimwagiza Mganga Mkuu wa Wilaya kuhakikisha hakuna upungufu wa dawa katika kituo hicho na endapo litatokea hilo wananchi wamjulishe mapema.Pia aliwakumbusha maagizo ya Mkuu wa Mkoa kwamba wasiojiunga na CHF watalipia Sh. 10,000 kwa matibabu kila wanapoenda kutibiwa kama hawaoni umuhimu wa kuchangia 10,000 kwa kaya kwa mwaka mzima na wakatibiwa kwa kadi. 

  Alimaliza kwa kuwahimiza watu kufanya kazi kwa bidii ili waweze kutimiza mahitaji yao kama afya kwani fursa za uzalishaji zipo.Uhamasishaji wa CHF unaendelea katika kata mbalimbali za Lindi katika wiki hìi na baada ya hapo katika Halmashauri mbalimbali nchini.

  0 0

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbawara (wapili kulia) akitoa maekekezo kwa Viongozi wa TTCL katika ziara yake Mkoani Mtwara juzi.     Wafanyakazi wa TTCL Mtwara katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Prof. Tolly Mbwette na Ofisa Mtendaji Mkuu wao, Dk. Kamugisha Kazaura. Ofisa Mtendaji Mkuu wao, Dk. Kamugisha Kazaura (wa kwanza kushoto) akizungumza kwenye ziara ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbawara mkoani Mtwara juzi. Mazungumzo kati ya Wafanyakazi wa TTCL Mtwara katika mkutano na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbawara alipofanya ziara yake.

   SERIKALI ipo katika hatua za mwisho za kuilipa kampuni ya Bharti Airtel ili kurejesha umiliki wa asilimia 100 katika Kampuni ya Simu Tanzania, TTCL. 

  Uamuzi huo unaotarajiwa kutekelezwa kabla ya mwisho wa mwezi huu utaiwezesha TTCL kurejesha hisa zake 35% zilizonunuliwa na Airel mwaka 2001 na kuifanya Bharti Airtel kuwa mbia mwenza katika Kampuni hiyo. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa ametangaza uamuzi huo Jumatatu hii Mkoani Mtwara alipotembelea Ofisi za TTCL Mkoa wa Mtwara, kukagua mitambo na miundo mbinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.

   "Serikali imesikia kilio cha muda mrefu cha Watanzania na wadau wote wa TTCL kuhusu kuondoka kwa mbia mwenza Kampuni ya Bharti Airtel. Ubia huu wa TTCL na Bharti Airtel utahitimishwa Rasmi kabla ya mwisho wa mwezi huu. Tumefanya majadiliano ya kutosha, tumekubaliana kuwa Serikali iilipe Bharti Airtel sh bilioni 14.9 ili kurejesha hisa za 35% za TTCL na kuifanya Kampuni hii ya TTCL kuwa mali ya Umma kwa 100%. 

  Tutatumia fedha za Mapato ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kukamilisha utaratibu huu. Naiagiza Bodi na Menejimenti ya TTCL kufanya kazi kwa bidii na Ufanisi Mkubwa na kusimamia kikamilifu shughuki za TTCL ili kutimiza jukumu lake kwa Umma.

   Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Prof. Tolly Mbwette amesema, kukamilika kwa mchakato huu ni hatua muhimu sana kwa Uhai na ufanisi wa TTCL na kusisitiza kuwa, mpango wa mageuzi ya kibiashara wa kampuni hiyo sasa utatekelezeka kwa kasi kubwa baada ya hatua hii.

   Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura amesema, jitihada kubwa za TTCL sasa zitaelekezwa katika kuboresha huduma kwa kutumia fedha za ndani na Mikopo ya wadau wa kibiashara ili kuiwezesha kampuni kuendelea kuwa kiongozi katika utoaji wa huduma bora na nafuu katika soko la Mawasiliano nchini.

   Hivi karibuni, TTCL imezindua huduma za Mtandao wenye kasi zaidi wa 4G LTE na kuimarisha ubora wa huduma zake za data na sauti. Aidha, TTCL na Benki ya TIB zimeingia makubaliano ya mkopo wa fedha na dhamana za Benki utakaoiwezesha TTCL kupata fedha dola za Marekali milioni 329 ili kuingiza mitambo mipya ya kisasa itakayo boresha huduma zake ikiwa ni pamoja na kuanzisha huduma ya miamala ya fedha kwa njia ya mtandao.

  0 0

   Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Slivery Mgonza akimkabidhi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii (Bloggers-TBN) kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya wanachama wa TBN. Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Slivery Mgonza akimkabidhi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii (Bloggers-TBN) kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya wanachama wa TBN. Kushoto ni Ofisa wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa, Nicholaus Mwangomo. Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Slivery Mgonza akimkabidhi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii (Bloggers-TBN) kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya wanachama wa TBN. Kushoto ni Ofisa wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa, Nicholaus Mwangomo.
   Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Slivery Mgonza akimkabidhi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii (Bloggers-TBN) kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya wanachama wa TBN. Kushoto ni Ofisa wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa, Nicholaus Mwangomo. Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Slivery Mgonza akimkabidhi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii (Bloggers-TBN) kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya wanachama wa TBN.


  0 0

   Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akionesha umahiri wake wa kutumia Cherahani na kushona nguo za wafanyakazi wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kuvifahamu vitengo mbalimbali vya Ikulu jijini Dar es salaam Januari 20, 2016 
   Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kushona kwa ustadi wa hali ya juu
  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimalizia moja ya nguo za wafanyakazi wa Ikulu.

  0 0

  K1
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akielezwa jambo  na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakati wa mazungumzo yao  kwenye Ofisi Kuu ya CCM mjini DodomaJanuari 20, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  K2
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kwenye Ofisi Kuu ya CCM mjini DodomaJanuari 20, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  K3

  0 0


  0 0


  0 0  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
   

  Simu: 255-22-2114512, 2116898
  E-mail: press@ikulu.go.tz
  Tovuti : www.ikulu.go.tz              

  Faksi: 255-22-2113425

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa Mnyaa kufuatia kifo cha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Suleiman Said Suleiman aliyekufa maji jana tarehe 18 Januari, 2016 wakati akiogelea katika bahari ya Hindi.

  "Nimepokea kwa mshtuko mkubwa kifo cha Suleiman Said Suleiman na kupitia kwako Mheshimiwa Waziri, naomba kuungana na familia ya marehemu, wafanyakazi wa TAA, ndugu, jamaa na marafiki wote katika kuomboleza msiba huu mkubwa uliotokea" Amesema Dkt. Magufuli.
  Rais Magufuli amesema Taifa limepoteza mtu muhimu ambaye mchango wake ulikua bado unahitaji.

  Ameongeza kuwa Taifa linatambua mchango mkubwa alioutoa Marehemu Suleiman Said Suleiman katika uendelezaji wa viwanja vya ndege hapa nchini, na kwamba njia pekee ya kumuenzi ni kuendeleza yote mazuri aliyoyafanya.
  "Namuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu Suleiman Said Suleiman mahali pema peponi, Amina" Amemalizia Rais Magufuli

  Gerson Msigwa.
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam.
  19 Januari, 2016older | 1 | .... | 742 | 743 | (Page 744) | 745 | 746 | .... | 1896 | newer