Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 733 | 734 | (Page 735) | 736 | 737 | .... | 1903 | newer

  0 0

   Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa akionesha kwa  waandishi wa Habari  picha rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli,kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO  Bw. Raphael Hokororo.picha hiyo inauzwa sh. 15,000/- tu.
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akionesha kwa msisitizo  Picha rasmi  ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli wakati wa mkutano na Vyombo vya habari leo Jijini Dar es salaam.

  Na Zainabu Hamis, Globu ya Jamii.

  PICHA Rasmi ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuri imetoka leo Januari 8, 2015 katika Ofisi ya Idara ya Habari  (MAELEZO) Dar es Salaam.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kaimu Mkurugenzi  wa Idara ya Habari (MAELEZO) Zamaradi Kawawa, amesema kuwa Picha hiyo ya Rais Magufuri  kwa kila moja itauzwa kwa sh15000 ya kitanzania bila ya kuwekwa frem,huku picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere  itauzwa kwa  sh 5000.

  Aidha Zamaradi amesema kuwa Nakala za picha hizo zinapatikana Idara ya Habari Maelezo  na Ofisi za Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini  (GPSA).

  Picha hiyo ya Rais pamoja na ya  Baba wa Taifa zinatakiwa kutundikwa katika ofisi zote za Serikali,Taasisi za Umma,Mashirika na Ofisi Binafsi.

  Aidha Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo Raphael Hokororo amesema picha ya Rais Magufuri imewahi kutoka mapema sana kuliko picha za Waheshimiwa waliopita na kusema  kuwa hairuhusiwi kukopi wala kunakili picha hiyo.

  Serikali inatoa onyo kwa wale wote wanaosambaza picha isiyo rasmi pamoja na Serikali kusitisha matumizi ya picha hiyo na wale wote wanaotengeneza picha ukubwa usio rasmi, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.Kwani Idara ya Habari Maelezo ndiyo yenye Haki miliki ya picha hiyo.

  0 0

  Picha maktaba ikionyesha wananchi jamii  ya kimasai wakiwa wanacheza mpira

  Na woinde shizza,Arusha
  Chama cha soka wilaya  ya Mondoli (MODFA),kinatarajia kufanya uchaguzi Mkuu Mwezi wa pili mwaka huu (2016), ili kupata uongozi kwa nafasi nane zinazowaniwa ili kupata uongozi utakao kiendesha chama hicho kwa miaka mitatu.

  Katibu Mkuu wa Chama cha soka wilayani humo Twaha Kibayasi, alisema kuwa taratibu kamilihazija kamilika japo mambo yanaenda vizuri na nafasi nane ndizo zinazowaniwa katika uchaguzi huo.

  Nafasi zitakazo waniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Muweka Hazina, Mjumbe wa mkutano Mkuu, Mwakilishi wa Vilabu na Wajumbe watatu wa kamati tendaji.

  “Zoezi la uchukuajiwa wa fomu bado halijaanza na pindi taratibu zitakapo kamilika tutawatangazia lasmi ikiwa pamoja na ada ya kila nafasi itakayo tangazwa, cha msingi ni kuwaomba wajitokeze na wawe tayari kugombea nafasi hizo” alisema  Kibayasi

  Kwa mujibu wa katiba ya MODFA mtanzania yeyote mwenye Sifa zitakazo ainishwa ikiwa pamoja na elimu ya sekondari na kuendelea anafaa kugombea nafasi yoyote.

  “Sio sifa hizo pekee Pia asiyewahi kushitakiwa kwa kosa lolote na kufungwa na awe mpenda michezo ndio sifa mojawapo itakayoangaliwa maana watu wanapenda kuleta siasa kwenye michezo na mwisho kuhalibu soka” aliongeza kusema Kibayasi.

  Kibayasi alisema kuwa mara baada ya mwaka mpya Kamati tendaji ya MODFA inatarajia kukaa pamoja na kujadili mambo mbalimbali ikiwepo juu ya kuandaa ligi ya Wilaya hiyo inayo suasua ili kupata bingwa atakaye iwakilisha Monduri katika Ligi ya Mkoa wa Arusha inayotarajia kuanza mapema mwezi januari.

  Uchaguzi huo umehairishwa zaidi ya mara mbili kutokana na sababu mabali mbali ikiwemo watu kutojitokeza kugombea nafasi zilizotangazwa, uchaguzi huo ulitarajiwa kufanyika mwezi wa tano mwaka uliopita (2015).

  Kibayasi Aliongeza kuwa kwa sasa wasipojitokeza watafanya uchaguzi kwa nafasi ambazo zitapata wagombea na pia wataandaa uchaguzi mdogo hadi wajaze nafasi zote kulingana na taratibu na sheria za MODFA

  0 0


  Z1

  Waziri wa Uwezeshaji, ustawi wa Jamii,Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Zainab Omar Mohammed akiweka Jiwe la Msingi la Mradi wa kuchuja Maji Chumvi kuwa Maji matamu huko katika Kijiji cha Michamvi wilaya ya Kusini Unguja.Aliyevaa kanzu ni Katibu mkuu Wizara ya Ardhi, Makaazi,Maji na Nishati Ally Khalil Mirza.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
  ……………………………………………………………………………….
  Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
  Jumla ya Wananchi 1,572 wa Vijiji vya Michamvi Pingwe na Michamvi Kae wanatarajiwa kupata Maji safi na salama baada ya kukamilika kwa Mradi wa kuchuja Maji Chunvi kuwa Maji matamu.

  Kukamilika kwa mradi huo kutawapunguzia Kero wananchi wa Vijiji vya Michamvi ambao kwa miaka mingi wamekumbwa na tatizo hilo bila ya msaada wowote.Hayo yameelezwa na Waziri wa Uwezeshaji, ustawi wa Jamii,Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Zainab Omar Mohammed wakati akiweka Jiwe la Msingi la Mradi huo huko Michamvi wilaya ya Kusini Unguja.

  Amesema uwekaji wa Jiwe la Msingi wa Mradi huo na kupata maji matamu ambayo yatawasaidia wananchi hao ni moja kati ya jitihada zinazofanywa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa lengo la kuwaondoshea shida ya upatikanaji wa maji wananchi wake.“Malengo makubwa ya jitihada hizo ni kuwaondoshea kero Wananchi ya kukosekana kwa huduma hiyo ya maji safi ili waweze kushughulikia zaidi kazi za uzalishaji mali na maendeleo kwa lengo kuimarisha kipato chao” amesema Waziri Zainab.


  Ameongeza kuwa eneo la Michamvi ni moja kati ya maeneo yanayokabiliwa na upatikanaji wa maji safi na salama na kwamba baada ya muda mfupi wananchi wataondokana na kero hiyo.

  Akitoa taarifa juu ya Mradi huo Naibu Katibu mkuu Wizara ya Ardhi, Makaazi,Maji na Nishati Mustafa Jumbe amesema Mradi umetekelezwa na kugharamiwa kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Kampuni ya UST kutoka Ujerumani ambapo jumla ya Shilingi Millioni 475 za Kitanzania zinatarajiwa kutumika.

  Amefafanua kuwa Kampuni ya UST imechangia Milioni 395 ambapo kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi kwa kushirikiana na Wananchi wamechagia Millioni 80.Jumbe amezitaja kazi zitakazofanyika kuwa ni pamoja na uchimbaji wa kisima,utiaji wa pampu,ujenzi wa kibanda cha kuwekea mitambo na ununuzi wa mitambo ya kusafishia maji chumvi kuwa matamu.

  Akitoa nasaha Mkuu wa Wilaya ya Kusini Jabir Khamis Makame amewaomba wananchi wa Michamvi kuuenzi Mradi huo ili uweze kuwaletea matunda yaliyokusudiwa.

  Uwekaji wa Jiwe la Msingi Mradi wa Kuchuja maji Chumvi kuwa Maji matamu ni moja ya matunda ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo lengo lake ni kuwakombo Wananchi na Umasikini ikiwemo kuwaletea maji safi na salama katika maeneo yao.

  0 0

  M1
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na balozi Namibia nchini, Mhe. Japhet Isaack ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Januari 8, 2016 kuaga.
  M2
  Waziri Mkuu, Kassim Mjaliwa akimkabidhi  Balozi wa Namibia nchini aliyemaliza muda wake, Mhe. Japhet Isaack  zawadi ya ramamni ya  Tanzania iliyochongwa kwenye mti wa mpingo  ili aendelee kuikumbuka Tanzania  atakapoondoka. alozi alikwendaofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Januari 8, 2016 kuaga.
  M3
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akimkabidhi Balozi wa Tanzania  nchini, Japhet Isaack zawadi ya  kinyago cha pundamilia  ili atakapoondoka  nchini abaki na kumbukumbu  ya  wanyamapori ambao nimuhimu kwa utalii hapa nchini. Balozi huyo alikwenda Ofisini kw Waziri Mkuu jijini Dares salaam Januari 8, 2016 kuaga.
  M4
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na balozi wa  Finland nchini Tanzania Mhe. Pekka   Hukka  kabla ya mazungumzo yao ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Januari 8, 2016.
  M6
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza  na balozi wa  Finland nchini Mhe. Pekka   Hukka  kabla ya mazungumzo yao ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Januari 8, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Na woinde shizza,Arusha

  Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Arusha (ARBA), Kipo katika hatua za mwisho kufanya uchaguzi Mkuu mapema mwezi huu uongozi utakao kiongoza chama hicho kwa muda wa Miaka Mitatu.

  Mwenyekiti wa chama cha Mchezo wa Kikapu Mkoa wa Arusha (ARBA) Barick Kilimba alisema kuwa nafasi kuu mbili zitagombewa ikiwa pamoja na nafasi ya Mwenyekiti Mkuu, na Msaidizi wake, Katibu Mkuu na Makamu wake.

  “Nilikuwa naongoza huku nacheza hivyo ilikuwa inaniwia vigumu sana wakati mwingine, katika kutoa maamuzi nilikuwa naogopa kuonekana napendelea Timu yangu, hivyo nimeamua niweke uongozi pembeni nibaki kuwa mchezaji pekee”

  “Shida ilikuwa hakuna watu wa kuongoza nafasi hizi lakini tumewashawishi wale wachezaji wakongwe waje washike madaraka ili watuongoze na kutuonesha wao walikuwa Wanafanyaje kipindi wao wanacheza” Alisema Kilimba.

  Aliongeza kuwa wanatarajia kufanya kikao cha viongozi wote Waliokuwa madarakani kwa sasa ili kupanga tarehe maalumu ya kufanya uchaguzi huo, ikiwa pamoja na kutangaza sifa za wagombea.

  Pia ARBA Wanatarajia kuendesha Bonanza la mchezo huo kwa kushirikisha timu zote zinazopatikana Mkoani hapa pamoja na mikoa ya Jirani ikiwa na Lengo kupanua na kutangaza Mchezo huo katika ukanda wa Kusini.

  Kilimba alisema kutoshirikiana baina ya viongozi ndio sababu kubwa ya Mchezo huo kufifia Mkoani hapa, kwa iongozi wengi kukwepa majukumu yao na kuwa Bize na mambo yao Binafsi.

  Hata hivyo alikiri ARBA kukabiliwa na ukata kitu ambacho kilisababisha kushindwa kushiriki mashindano ya Kitaifa yaliyokuwa yanafanyika Mkoani Dodoma mwezi Disemba mwaka uliopita, licha ya kukiandaa kikosi.

  0 0

   8c7900c1-d38a-4cc1-b96b-ca65c5aba350

  Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiongea na wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa kikao cha wafanyakazi kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  8fb4d08e-7a55-447b-b1fb-d18e2f201465
  Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akimkabidhi cheti cha mfanyakazi mmoja wa wafanyakazi wa  Wizara hiyo.
  1a611ab0-ea30-4644-ac9a-ce4a2bab8595
  Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye kushoto  akiongea  na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kulia Prof. Elisante Ole Gabriel kulia wakati wa mkutano wa wafanyakazi uliofanyika Dar es Salaam leo, katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo  Bw. Leornard Thadeo.
  e5ca5b00-7e55-43ab-bbc3-69c63cbc0326
  Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo mara baada ya mkutano na wafanyakazi hao.
  (Picha na Benjamin Sawe-WHSUM)
  …………..
  Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es  Salam
   
  Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Nape  Nnauye amempongeza mchezaji wa mpira wa miguu wa Taifa  Star Mbwana Samatta  baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa soka Afrika 2016 kwa wachezaji wanaocheza soka Barani Afrika.iliyotolewa  nchini Nigeria.

  Nnauye ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano na watumishi wa Wizara wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo leo jijini Dar es salaam.Amesema tuzo hiyo imemjengea heshima na kuleta sifa kwa Mbwana Samatta mwenyewe, wanasoka hapa nchini na Tanzania kwa ujumla katika medali ya Soka Kimataifa.Nnauye amewataka wachezaji wengine kufuata nyayo za mchezaji huyo kwa kuongeza juhudi, nidhamu katika michezo na watambue kuwa mchezo wa mpira wa miguu ni kazi kama zilivyo kazi nyingine.

  Akifafanua zaidi Nnauye alibainisha kuwa kilichomfikisha  Samatta hapo ni kujitambua na kujituma  katika ajira yake.Samatta ameibuka mshindi wa Tuzo ya Mchezaji bora wa mwaka kwa wachezaji wanaocheza ligi ya Barani Afrika kwa kupata alama 127 dhidi ya Robert Kidiaba aliyepata alama 88 na Baghdad Bounedjah alama 63.

  0 0


  Mkufunzi wa Masuala ya Majanga wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Christopher Marwa (kulia) akimuonyesha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (aliyevaa tai), gari la Uokozi ambalo lina vifaa mbalimbali vya uokozi. Waziri Kitwanga alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, na baadaye kujifunza kazi mbalimbali za jeshi hilo katika Kituo cha Zimamoto Kanda ya Ilala, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga aliliagiza Jeshi hilo kumchukulia hatua kali za kisheria kwa yeyote atakaye kiuka kulipisha gari la Zimamoto na Uokoaji wakati linaenda katika tukio lolote la uokoaji pamoja na kuzima moto. Pia aliitaka Jeshi hilo kuongeza kasi ya kukusanya mapato katika vyanzo vyake mbalimbali. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara yake katika Kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kanda ya Ilala, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake kwa waandishi hao wa habari, Waziri Kitwanga aliliagiza Jeshi hilo kumchukulia hatua kali za kisheria kwa mtu yeyote atakaye kiuka kulipisha gari la Zimamoto na Uokoaji wakati linaenda katika tukio lolote la uokoaji pamoja na kuzima moto. Pia aliitaka Jeshi hilo kuongeza kasi ya kukusanya mapato katika vyanzo vyake mbalimbali.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha (kushoto) akitoa taarifa ya utendaji wa Jeshi lake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga aliliagiza Jeshi hilo kumchukulia hatua kali za kisheria kwa yeyote atakaye kiuka kulipisha gari la Zimamoto na Uokoaji wakati linaenda katika tukio lolote la uokoaji pamoja na kuzima moto. Pia aliitaka Jeshi hilo kuongeza kasi ya kukusanya mapato katika vyanzo vyake mbalimbali.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiongozwa na Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha (kulia kwa Waziri) wakati Waziri huyo alipofanya ziara Makao Makuu ya Jeshi hilo, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam leo. Katika ziara hiyo, Waziri Kitwanga aliliagiza Jeshi hilo kumchukulia hatua kali za kisheria kwa yeyote atakaye kiuka kulipisha gari la Zimamoto na Uokoaji wakati linaenda katika tukio lolote la uokoaji pamoja na kuzima moto. Pia aliitaka Jeshi hilo kuongeza kasi ya kukusanya mapato katika vyanzo vyake mbalimbali.

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akiondoka Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mara baada ya kuzungumza na Makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiongozwa na Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha (kulia). Katika hotuba yake kwa viongozi hao wa jeshi, Waziri Kitwanga aliliagiza Jeshi hilo kumchukulia hatua kali za kisheria kwa yeyote atakaye kiuka kulipisha gari la Zimamoto na Uokoaji wakati linaenda katika tukio lolote la uokoaji pamoja na kuzima moto. Pia aliitaka Jeshi hilo kuongeza kasi ya kukusanya mapato katika vyanzo vyake mbalimbali.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimsalimia Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha wakati alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Katika ziara hiyo, Waziri Kitwanga aliliagiza Jeshi hilo kumchukulia hatua kali za kisheria kwa yeyote atakaye kiuka kulipisha gari la Zimamoto na Uokoaji wakati linaenda katika tukio lolote la uokoaji pamoja na kuzima moto. Pia aliitaka Jeshi hilo kuongeza kasi ya kukusanya mapato katika vyanzo vyake mbalimbali.

  0 0

  MHAN1
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF bwana Michael Mhando  na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Erio wakitia saini makubaliano yatakayowawezesha wajasiliamali wanaonufaika na fao la hiari la PPF kupata huduma za bima ya afya kupitia mpango wa kikoa
  Mpaka sasa fao la hiari la PPF lina wanachama 12, 000 ambao hivi karibuni wataanza kunufaika na mafao yatolewayo na NHIF baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeanza kutoa huduma za matibabu kwa wanachama wa VIKUNDI vya WAJASILIAMALI VILIVYOSAJILIWA ambapo kila mmoja anachangia shilingi 76,800 kwa mwaka na kupata matibabu katika hospitali zaidi ya 6000 zilizosajiliwa na NHIF nchi nzima.

  0 0

  Khadija Hassan who is 13 years old has been missing since Monday 4th January 2016 , she was last seen at KEKO Mwanga. If you see her immediately call 0657697217 or 0719 537 565 Naomba utusaidie kusambaza ujumbe huu: Mtoto was dereva wetu aitwa Khadija Hassan anaye umri 13 amepotea tangia Jumatatu tarehe 4 January 2016. Mwisho alionekana eneo la KEKO Mwanga. Ukimuona tafadhali utupigie Simu 0657697217 or 0719 537 565
  Sarina Murji's photo.

  0 0

  M2
  Waziri Mkuu, Kassim Mjaliwa akimkabidhi  Balozi wa Namibia nchini aliyemaliza muda wake, Mhe. Japhet Isaack  zawadi ya ramamni ya  Tanzania iliyochongwa kwenye mti wa mpingo  ili aendelee kuikumbuka Tanzania  atakapoondoka. alozi alikwendaofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Januari 8, 2016 kuaga.


  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekuaana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Namibia ambaye anamaliza muda wake, Bwana Japhet Isaack.

  Akizungumza na Balozi  Isaack leo ,ofisini kwake ,Magogoni jijini Dar es salaa, Waziri Mkuu ameshukuru Balozi huyo na  kumumwomba  waendeleze uhusiano mwema   ulipo baina ya nchi hizi mbili ambao ulianza tangu enzi za kugombania uhuru ili  kusaidia kukuza uchumi wa nchi hizi mbili.

  “Namibia ni  nchi yenye uchumi uanaokua haraka, na mmefanikia katika baadhi ya sekta , hivyo ningependa  Tanzania ijufunze kutoka kwenu hasa katika sekta za Utalii, Afya, na Elimu,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

  Pia, alitumia fursa hiyo kuwakaribisha  raia wa Namibia kuja kuwekeza nchini  katika maeneo mbalimbali ikiwemo  viwanda  na kuendeleza maeneo ya ukanda maalum ya uwekezaji (EPZ) ili kuongeza thamani ya mazao pamoja na kutatua tatizo la ajira nchini.

  Kwa upande wake,  Balozi  Isaack  amesema kwa kipindi alichokaa Tanzania amejifunza mengi, na amefurahishwa  ambavyo Waziri Mkuu pamoja Serikali kwa ujumla  inavyofanyakazi kwa kasi na kwa mafanikio makubwa.

  “Hongera, ninafurahishwa na unavyofanya kazi  hongera sana”, alisema Balozi Isack. Pia, amefurahi sana kipindi chote alichokaa Tanzania kwani kimekuwa na matukio mengi yenye kumbukumbu  nzuri kwake.

  Balozi Isack   ameomba mahusiano ya nchi hizi mbili yaendelezwe ili zishirikiane zaidi katika masuala mbalimbali ya kukuza uchumi.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S. L. P 3021,
  11410 DAR ES SALAAM
  IJUMAA, JANUARI 8, 2016.

  0 0  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  OFISI YA MAKAMU WA RAIS
  TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU ZOEZI LA KUHAMISHA WAKAZI WA MABONDENI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM

  Utangulizi

  Nchi yetu ina kingo za mito na mabonde na maeneo mengi hatarishi ambamo watu wanaishi kinyume cha sheria, huku wakiharibu mazingira na kuhatarisha maisha yao.  Kutokana na uhaba wa makazi, hali ni mbaya zaidi katika mabonde ya Jiji la Dar es Salaam, hasa bonde la Mto Msimbazi.
  Serikali za awamu zote, zimekuwa zikifanya jitihada za kuwaondoa wakazi wa maeneo ya mabondeni wanaoishi katika maeneo hayo kinyume cha sheria lakini mafanikio yamekuwa si ya kuridhisha. 

  Serikali ya Awamu ya Tano, ambayo moja ya misingi yake mikuu ni utii wa sheria za nchi, imeanza jitihada za kuwaondoa wakazi hawa. Tuliamua kuanza na Bonde la Mto Msimbazi kwasababu ndiko kwenye watu wengi na athari kubwa.Sababu zetu kuu za kufanya zoezi hili ni kusafisha mabonde na mito katika jiji la Dar es Salaam na mazingira yanayozunguka ni:-

  1. Kunusuru maisha ya wananchi wanaoishi katika mazingira hatarishi. Eneo la Bonde la Mto Msimbazi lilitangazwa kuwa ni eneo hatarishi kuishi binadamu tangu mwaka 1949 na baadaye 1979.

  1. Kupanua uwezo wa mito ya Dar es Salaam ili kupitisha maji ya mvua kwa kasi kubwa, hivyo kupunguza uwezekano wa kutokea mafuriko na maafa wakati wa mvua nyingi;
  2. Kuzuia milipuko ya magonjwa, hasa ya kipindupindu, hasa wakati wa mvua;

  1. Kuzuia eneo hilo kuendelea kutumika kama maficho ya wahalifu na uhalifu;

  1.  Kutoa nafasi kwa Serikali kuandaa na kuendeleza eneo hilo kwa mujibu wa sheria za nchi na mipango miji;
  Utaratibu wa Zoezi

  Kabla ya nyumba kubomolewa, taasisi hizi zinashirikiana kuhakiki iwapo nyumba anayokaa mkazi ina nyaraka za umiliki na vibali vya ujenzi na iwapo nyaraka hizo zina uhalali wowote. Nyumba ambazo zimethibitika kuwepo katika maeneo yasiyostahili ndio zinawekwa alama X kuashiria kwamba wakazi wanapaswa kuhama au kubomoa. Baada ya hapo, mkazi hupewa muda wa kubomoa na kuhama mwenyewe. 

  Kutokana na utaratibu huu, sehemu kubwa ya nyumba zinazobomolewa ni zile ambazo watu wamekwishaamua kubomoa wenyewe. Baada ya hapo, alama huwekwa kuonyesha mpaka wa bonde. Katika zoezi hili, imebainika kwamba sehemu kubwa ya wakazi wa maeneo ya mabondeni ni wapangaji huku wamiliki wakikaa sehemu nyingine salama. Serikali pia imeweka Dawati la Malalamiko katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.


  Tathmini ya Zoezi

  Jana, terehe 7 Januari 2016, Mawaziri watatu (Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI; na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais; pamoja na Naibu Waziri wa  Maliasili na Utalii), walifanya mkutano wa kutathmini zoezi la kuhamisha wakazi wa mabondeni katika Jiji la Dar es Salaam.  

  Mkutano huo ulipokea ripoti ya timu ya wataalam wa Wizara mbalimbali, inayoongozwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, ambayo, pamoja na mambo mengine ilibainisha kwamba sehemu kubwa ya kubaini makazi yaliyojengwa kinyume cha Sheria katika Bonde la Mto Msimbazi imekamilika. Ripoti ilieleza kwamba, hadi sasa, wananchi katika nyumba 774  wamehama na nyumba hizo kubomolewa. Ilielezwa pia kwamba kabla ya mkazi kuombwa  kuhama, uhakiki kuhusu uhalali wa makazi anayoishi hufanywa. Kutokana na uhakiki huo, jumla ya wakazi 20 walikuwa na hati halali za makazi na wakazi 119 walikuwa na leseni za makazi za muda mfupi. Hawa watu hawakuhamishwa. Mawaziri walipokea maelezo kuhusu changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika zoezi hilo.  Baada ya tafakuri na mjadala, Mawaziri hao walitoka na msimamo ufuatao, kama uamuzi wa Serikali: -

  1.      Zoezi la kuwaondoa wananchi waishio katika bonde la Mto Msimbazi (eneo hatarishi) litaendelea kwa utaratibu ambao hautaleta mateso na usumbufu kwa wananchi;

  2.      Katika awamu hii, zoezi litajikita katika Bonde la Mto Msimbazi tu.

  3.      Kwa wakati huu, watakaohitajika kuhama ni wale tu ambao makazi yao yamo NDANI kabisa ya bonde, kwenye miteremko ya kuingia bondeni na kwenye KINGO za mto;

  4.      Wale watakaokuwa na nyaraka halali walizopewa na mamlaka za umma, zilizowamilikisha na kuwaruhusu kujenga katika bonde hilo, hawatahamishwa bila kupewa sehemu nyingine za kujenga. Na watumishi wa umma waliowamilikisha maeneo hayo watachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria;

  5.      Serikali, ndani ya siku tatu zijazo, itaanza zoezi la kuzoa kifusi na kusafisha maeneo ambapo ubomoaji umefanyika.

  6.      Serikali itaheshimu amri za mahakama kuhusu mapingamizi yaliyowekwa na baadhi ya wakazi wa mabondeni lakini pia itafuatilia kesi hizi ziishe haraka ili taratibu zinazofuatia zifanyike;

  7.       Serikali itawachukulia hatua za kinidhamu watumishi wake wanaoendesha zoezi hili kinyume na misingi ya sheria zinazotekelezwa, na kinyume na misingi ya haki na uwazi, ikiwemo wanaoweka alama za X zaidi ya mita zilizowekwa kisheria. Limeanzishwa dawati la malalamiko katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kupokea malalamiko au maswali kuhusu zoezi hili.


  8.      Nyumba na majengo ya miaka mingi, yaliyokuwepo miaka mingi kabla ya kutungwa kwa Sheria zinazotekelezwa kwa zoezi hili, hayatabomolewa isipokuwa tu pale maisha ya wakazi yapo hatarini. Wanaoishi katika makazi hayo watapewa miongozo ya hatua za kuhifadhi mazingira na kujiokoa na maafa;

  9.      Serikali haina dhamira ya kubomoa mahoteli makubwa ya siku nyingi yaliyo karibu na fukwe katika maeneo ya Masaki. Wamiliki wa mahoteli haya watapewa masharti na miongozo ya kuhifadhi mazingira kwa mujibu wa Sheria.


  10.    Serikali inaweka uratibu wa karibu zaidi miongoni mwa taasisi zake ili hatua za utekelezaji wa sheria za nchi zisiwe chanzo cha taharuki katika jamii.

  11.  Serikali haina dhamira ya kuwatesa wananchi wake kwa kuwalazimisha kuhama katika makazi yao bila sababu za msingi. Lakini pia Serikali haiwezi kuruhusu wananchi waendelee kukaa katika maeneo ambayo ikinyesha mvua kubwa maisha yao yapo hatarini. Itakumbukwa kwamba katika mafuriko ya mwaka 2011, wananchi 49 waishio mabondeni walipoteza maisha. Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Hali ya Hewa, mwaka huu zinatarajiwa kunyesha mvua kubwa kuliko zilizowahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni.

  12.  Serikali inafuatilia kwa karibu kwa mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya taarifa za wananchi wanaohitaji msaada maalum wa kibinadamu.

  Suala la Mchungaji Getrude Rwakatare

  Mkutano ulipokea taarifa kuhusu suala linaloongelewa sana la nyumba ya Mchungaji Rwakatare.  Ilielezwa kwamba Mchungaji Rwakatare amejenga nyumba yake pahali ambapo amezuia mtiririko wa mto kwa kujaza kifusi ili kupata eneo zaidi katika eneo la miti ya mikoko, kinyume kabisa na Sheria tatu muhimu.  Pia ilielezwa kwamba tangu wakati ujenzi unaanza jitihada za kumsimamisha zilifanyika na mamlaka za Serikali za Mitaa lakini ikashindikana kutokana na sababu mbalimbali. Pale Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira lilipoingilia kati na kutaka kuibomoa nyumba hiyo, Baraza lilishtakiwa mahakamani. Wakati kesi inataka kuanza kusikilizwa, mwanasheria mdogo wa Baraza, yeye mwenyewe bila kuagizwa wala kuwaarifu wakubwa zake, mnamo tarehe 11 Mei 2015, aliingia makubaliano na mawakili wa Mchungaji Rwakatare kwa niaba ya Baraza ya kuondoa kesi hiyo mahakamani na kukubali, kwa niaba ya Baraza, kutombughudhi kabisa Mchungaji Rwakatare.  Makubaliano hayo yalisajiliwa na Mahakama kama hukumu tarehe 13 Mei 2015. Mwanasheria huyo alificha makubaliano hayo kwa miezi mitano hadi Oktoba 2015, yalipogundulika na mtumishi mwingine wa Baraza. Mkutano ulielezwa kwamba Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, kwa kufuata taratibu zote, alishaagiza kufukuzwa kazi, kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa mwanasheria huyo. Mwanasheria huyo alifukuzwa kazi siku ya juzi tarehe 6 Januari 2016 na taarifa zake zimekwishafikishwa TAKUKURU. Vilevile, Ofisi ya Makamu wa Rais, iliiagiza Baraza kufungua shauri mahakamani la kuomba “makubaliano” kati yake na Mchungaji Rwakatare yawekwe pembeni kwasababu yalipatikana na njia ya udanganyifu. Shauri hilo lilifunguliwa tarehe 29 Disemba 2015.

  Kuhusu Karakana ya Mradi wa Mabasi Yaendayo kwa Kasi (DART)

  Mkutano pia ulijulishwa kuhusu hoja inayozungumzwa kwamba wananchi wanaondolewa katika maeneo ya kuishi mabondeni lakini mradi wa DART umeachwa. Mkutano ulielezwa kwamba Sheria ya Mazingira (kifungu 57 (2)) inatoa nafasi ya kutolewa ruhusa kwa miradi/shughuli zenye maslahi ya taifa kufanyika katika maeneo ya mabondeni, na kwamba Waziri mwenye dhamana ya mazingira anaruhusiwa kutoa miongozo ya namna ya shughuli hizo zinavyoweza kufanyika bila kuathiri mazingira. Mradi wa DART ulipata kibali hicho na una mkataba na Baraza la Mazingira kuhusu hatua za hifadhi ya mazingira zinazopaswa kutekelezwa katika mradi huo.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA MAKAMU WA RAIS
  08.01.2016

  0 0


  Mr. Mbwana Aly Samatta-2nd from left receiving an Award as the African Player of the Year based in Africa during an event that took place in Abuja, Nigeria on 7th January, 2016 
  =======================

  The Tanzania Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation wishes to inform the world and all football fans that Mr. Mbwana Aly Samatta, the African Player of the Year based in Africa is a citizen of Tanzania and not of Botswana or Tunisia as was reported by NBC Sports.com and several other international media. 
   
  Mr. Samatta is one of the star players of the Tanzania national team (Taifa Stars) currently playing for TP Mazembe Club in the Congo DRC.
  The Tanzanian icon was announced by the Confederation of African Football (CAF) as the African Player of the Year based in Africa in an event that took place in Abuja, Nigeria on 07th January, 2016. Mr. Samatta becomes the first player from   East Africa to win the prestigious title.
  The Ministry takes this opportunity to thank Mr. Samatta for placing Tanzania on the international football stage and congratulate him for the victory well deserved.

  Issued by:
  Government Communication Unit
  Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation
  8th January, 2016
  0 0

   Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Ummy Mwalimu na Kushoto ni Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea, Damian Dallu.
  Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kupongeza jopo la Madaktari waliomhudumia katika Hospitali ya Mhimbili.
   Katika mkutano huo  Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo  alitoa zawadi za kadi za pongezi kwa baadhi ya madaktari mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
    Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Ummy Mwalimu akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Mrisho Kikwete iliyopo katika hospitali ya Taifa ya Mhimbili, Profesa Mohamed Janabi. 

   Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akiingia katika ukumbi wa mikutano katika kitengo cha Moyo cha Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete kilichopo katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili.
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee Mhe Ummy Mwalimu akimkaribisha Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ili aweze kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
   Kulia ni aliyekuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwashamu Askofu Titus Mdoe na Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea, Damian Dallu wakiwa katika mkutano wa Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mkutano wa Kitengo cha Moyo cha Jakaya Mrisho Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili.

  Katibu Mkuu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee,  Dkt. Mpoki Ulisobisya akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusiana na swali lililoulizwa na mwandhishi wa habari kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee haitoi ruhusa ya mtu yoyote kwenda kutibiwa nje ya nchi na ruhusa hiyo hutolewa na Madaktari wenyewe ambao walikua wanamtibia mgonjwa.

  Na Chalila Kibuda 
  wa Globu ya Jamii.

   Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amepongeza weledi wa huduma  za madaktari na huduma zinazotolewa katika Tasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

  Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ametoa pongezi hizo  jana  Ijumaa Januari 8, 2016 wakati akizungumza  na waandishi wa habari hospitalini hapo ambako alikuwa amelazwa kwa uchunguzi wa afya yake na matibabu. 

  Alisema kwamba awali yeye alikuwa anaogopa kutibiwa hapo kutokana na taarifa potofu zilizokuwa zinazotolewa kwenye vyombo vya habari juu ya  operesheni tata zilizowahi kufanyika katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, na kwamba  sasa ameridhika kuwa ni vinginevyo kwani Kitengo cha magonjwa ya moyo cha hospitali hiyo kimemdhihirishia kwamba kina uwezo mkubwa wa matibabu ya moyo kama ilivyo hospitali zingine popote pale duniani.

  Askofu Mkuu huyo wa Jimbo kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alilazwa katika taasisi hiyo ya moyo tangu Januari Mosi mwaka huu. Hali yake imeendelea kuimarika kila siku baada ya kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu hapo.
  Kwa upande wake  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali imeokoa kiasi cha shilingi bilioni nne ambazo zilikua zipotee kwa ajili ya kupeleka wagonjwa wa moyo kutibiwa  nje ya nchi.
  Aidha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Mrisho Kikwete iliyopo katika hospitali ya Taifa ya Mhimbili, Profesa Mohamed Janabi amesma kuwa Askofu Pengo ataruhusiwa mwisho wa juma hili kwa kuwa afya yake imeimarika.


  0 0

   Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nnape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya Wakuu wa Idara ya Habari Maelezo na Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari  mapema leo,alipokutana nao na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabiri tasnia hiyo,mkutano huo umefanyika kwenye moja ya ukumbi ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
    Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nnape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya Wakuu wa Idara ya Habari Maelezo na Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari 
   Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akiwakaribisha Wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,kwenye mkutano ulioitishwa na Waziri Nape kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali yanayoikabiri tasnia ya habari hapa nchini.Pichani kati ni Waziri Mh.Nape pamoja na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda.
  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda akitoa muongozo kwa Wahariri wa Vyombo vya habari (hawapo nchini) kuhusina na mkutano wao ulioitishwa na Waziri Nape kujadili mambo mbalimbali na changamoto zinazoikabiri tasnia hiyo kwa ujumla.
   Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa ukumbini humo.
   Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nnape Nnauye akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,kwenye mkutano uliohusu kujadili mambo mbalimbali zikiwemo changamoto zinazoikabiri tasnia ya habari hapa nchini.Pichani kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda na kushoto ni  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa .
   Mmoja wa Wahariri Kurwa Kaledia kutoka New Habari Hause akiomba ufafanuzi wa jambo kwa Mh Waziri Nape huku baadhi ya wahariri wakifuatilia kwa makini.
   Mmoja wa Wahariri Grace Hoka akifafanua jambo kwenye mkutano huo
   Baadhi ya Wahariri wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo
   Baadhi ya Wahariri juu pichani wakishiriki kuchangia mambo mbalimbali kwenye mkutano huo.
   Mmoja wa Wahariri akifafanua jambo kwenye mkutano huo
  Baadhi ya Wadau wakubwa wa habari pia walikuwepo kwenye mkutano huo

  0 0

  ju1
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt. Mwinyihaji Makame akifungua pazia kuashiria ufunguzi wa jengo jipya la wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Kivunge, Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ikiwa ni miongoni mwa shamrashara za sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar. Alievaa miwani ni Naibu Waziri wa Afya Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na Daktari dhamana wa Hospitali ya Kivunge Tamim Hamad. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
  ju2
  Muonekano wa sehemu ya mbele ya jengo jipya la Wagonjwa wa nje wa Hospitali ya Kivunge, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
  ju3
  Meneja wa Mradi wa Kuimarisha Afya Zanzibar (HIPZ), ambao umetoa mchango mkubwa kufanikisha ujenzi huo, Bi. Pamela Allard akizungumza wakati wa shehere za ufunguzi wa jengo hilo.
  ju4
  Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akitoa maelezo ya ujenzi wa Jengo hilo na baadae kumkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt. Mwinyihaji Makame.
  ju5
  Baadhi ya Wawakilishi wa Mashirika Wahisani wakifuatilia ufunguzi wa Jengo hilo katika Hospitali ya Kivunge.
  ju6
  Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria ufunguzi wa jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Kivunge, Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakimskiliza Mgeni rasmi Dkt. Mwinyihaji Makame hayupo pichani. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
  ju7
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt. Mwinyihaji Makame akizungumza na wananchi kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wakati wa ufunguzi wa jengo la wagonjwa wa nje liliopo Hospitali ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  …………………………………………………………………………………………….
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa hatua za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba za kuimarisha huduma za afya za vijijini ni miongoni mwa utekelezaji wa shabaha ya Mapinduzi ya mwaka 1964 ya kuzifikisha huduma bora za afya hadi vijijini kwa nia ile ile ya waasisi wa Mapinduzi.

  Dk. Shein aliyasema hayo katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini, mara baada ya kulifungua jengo la wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Kivunge, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

  Katika hotuba hiyo, Dk. Shein alisema kuwa  huduma bora za afya kwa wananchi wote bila ya ubaguzi ni miongoni mwa malengo ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 ambapo Chama cha ASP kilichoongoza Mapinduzi hayo katika manifesto yake, kiliweka bayana azma yake ya kutoa huduma za afya bure bila ya ubaguzi wakati kitakaposhika hatamu za Serikali.

  Dk. Shein alisema kuwa jitihada kubwa zimefanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kipindi cha miaka 52 ya Mapinduzi katika kuimarisha huduma za afya kwa kutambua kwamba afya bora ni muhimu kwa wananchi ili waweze kuishi vyema katika kazi ya kuleta maendeleo ya nchi yao.

  Alisema kuwa mafanikio makubwa yamepatikana katika utekelezaji wa mipango na mikakati ya kuiendeleza sekta ya afya nchini kupitia vitengo na programu mbali mbali zinazoendeleshwa na Serikali kwa ushirkiano na Washirika wa Maendeleo.
  “Nyote ni mashahidi wa kuimarika kwa huduma za afya katika hospitali na vituo vytetu vyote va afya… Aidha, kuna ongezeko kubwa la vituo vya afya vya daraja mbali mbali kiasi kwamba hivi sasa wananchi wa Zanzibar hawawezi kwenda zaidi ya kilomita tano bila ya kukuta kituo cha afya”,alisema Dk. Shein.

  0 0


  Baadhi ya mitambo iliyotelekezwa kwenye Kiwanda cha kutengenezea Zana za Kilimo ZZK

  Mitambo ambayo ilikuwa ikitumika kutengenezea Zana za Kilimo katika kiwanda cha ZZK Iyunga jijini Mbeya ikiwa imetelekezwa

  Niranjan Bandi, aliyejitambulisha kuwa ndiye Mkurugenzi mkuu wa shughuli zinazoendelea katika kiwanda cha ZZK chini ya kampuni ya CMG akiwapa maelezo waandishi wa habari.
  Waandishi wakitoka katika kiwanda cha ZZK huku wakijiuliza maswali mbali mbali kutokana na walichokikuta ndani ya kiwanda hicho

  0 0

  Msafara wa magari uliokuwa umembeba Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika wa Wachezaji wa Ndani 2015, Mbwana Samata,ulionaswa na Camera ya Globu ya jamii maeneo ya Morocco jana jioni ukitokea hoteli ya Kempinsk baada ya kuzungumza na vyombo vya habari,Msafara huo akiwemo Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye ulipita maeneo kadhaa ya jiji la Dar na kukomea katika kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar,ambako alikutana na kupongezwa na Wadau mbalimbali wa tasnia ya Michezo.Mwanasoka huyo aliwasili juzi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam akitokea Abuja, Nigeria katika hafla ya utoaji tuzo kwa mwanamichezo bora.
  PICHA NA MICHUZI JR-MMG.
  Baadhi ya Waendesha Boda boda nao hawakuwa na hiyana kuunga mkono mafanikio ya Mbwana Samatta,ambayo yameiletea heshima kubwa nchi yetu.
  Msafara wa Mbwana Samatta ukikatiza maeneo ya Morocco
  Baadae akawasili viwanja vya Escape One akiwa ameambatana na Waziri Nape Nnauye tayari kwa kukamilisha ratiba nyingine,pia alipata selfie na washabiki wa soka kama uonavyo pichani
  Baadae akawasili viwanja vya Escape One akiwa ameambatana na Waziri Nape Nnauye tayari kwa kukamilisha ratiba nyingine,pia alipata selfie na washabiki wa soka kama uonavyo pichani
  Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kazini,huku Nyota wetu Mbwana Samatta akiwa amepozi na tuzo yake ya mchezaji bora wa Afrika.
  Samatta akipata picha ya pamoja na Waziri Mh.Nape Nnauye.
  Wadau wa Soka wakijadiiana jambo,wakati huo Samatta anafanya mahojiano ya hapa na pale na baadhi ya vyombo vya habari
  Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano) Mh. January Makamba sambamba na Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauyewakijumuika pamoja kwenye hafla fupi ya kumpongeza Mbwana Samatta ndani ya kiota cha maraha-Escape One Mikocheni jijini Dar
  Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano) Mh. January Makamba sambamba na Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh.Nape na wadau wengine wa soka wakijumuika kwa pamoja kumpongeza Samatta. PICHA NA MICHUZI JR-MMG.

  0 0

  Leticia Nyerere enzi ya uhai wake.

  Familia ya Leticia Nyerere ya Lanham, MD inasikitika kutangaza kifo cha mama Yao mpenzi kilichotokea tarehe 10 January 2016 nchini marekani. Mipango na utaratibu wa kusafirisha mwili inafanywa.
  Msiba upo 9004 brightlea court, Lanham MD 20706.
  Kama mila na desturi zetu tufike kuwafariji familia. Kwa maelezo zaidi wasiliana na :
  Margareth mageni 240 462 9138
  Emmanuel muganda 240 447 2801
  Ramadhani kamguna 202 459 3838


  Bwana ametoa, Bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe.

  0 0

  Mtaalamu wa masuala ya Afya kutoka akipima mzunguko wa damu Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukizwa (TANCDA)jana katika hospitali ya mkoa wa Mount Meru ambapo shughuli za upimaji wa magonjwa ya moyo,kisukari na saratani yalifanyika bure kwa wananchi wote.
  Wakazi wa Arusha wakiwasikiliza waelimishaji wa magonjwa yasiyoambukiza kutoka Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukizwa (TANCDA)jana katika hospitali ya mkoa wa Mount Meru ambapo shughuli za upimaji wa magonjwa ya moyo,kisukari na saratani yalifanyika bure kwa wananchi wote.

  Na Woinde Shizza,Arusha.
  Kutokana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo magonjwa ya moyo ,kisukari na saratani ,Watanzania wameaswa kuzingatia lishe bora na mtindo bora wa maisha ili kuepuka magonjwa hayo ambayo husababishwa na mtindo mbaya wa maisha pamoja unywaji pombe,uvutaji sigara na ulaji uisiofaa.

  Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukizwa (TANCDA) ,Dokta Tatizo Waane alisema kuwa kumekua na ongezeko kubwa la watu wenye magonjwa hao kitaifa ambapo ugonjwa wa moyo asilimia 26% ugonjwa wa kisukari umeongezeka kwa Asilimia 9.6.

  Akizungumza katika zoezi la upimaji na utoaji elimu kwa wananchi juu ya magonjwa hayo ,Dr.Waane amesema kuwa magonjwa ya moyo yameongezeka kwa asilimia 10 hivyo Watanzania hawana budi kuangalia hali yao ya lishe na kuzingatia kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa yasiyo ya lazima.

  "Watu wengi wamekua hawatilii maanani magonjwa yasiyoambukiza lakini yana athari kubwa kiafya na kwenye uchumi wa watu kwani hutumia muda mrefu na fedha nyingi kutibu" Alisema Dokta Waane.

  Mratibu wa zoezi la upimaji wa magonjwa hayo kwa mkoa wa Arusha Dokta David Shungu alisema kuwa wananchi wanapaswa kupatiwa elimu kwani magonjwa hayo yanaongoza kwa kusababisha vifo sawa na magonjwa yanayoambukiza.

  Kwa upande wake Mkazi wa Arusha aliyejitokeza kupima afya yake na kupata ushauri Tunu Ndege alisema kuwa zoezi hilo litawasaidia wananchi wengi kujua afya zao na kuchukua hatua kulinda afya zao dhidi ya magonjwa ,pia ameshauri huduma hiyo ya upimaji iwafikie watu wa vijijini wanaoteseka na magonjwa bila kujua.


  Alisema Mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza ya moyo,sukari na saratani yanapaswa kutiliwa mkazo kwa kutoa elimu na tiba kwa wananchi kwani magonjwa hayo hudumu kwa muda mrefu na kusababisha hasara ya kijamii na kiuchumi hata kupelekea vifo na ulemavu.

  0 0
 • 01/11/16--05:02: JK AMPONGEZA SAMATTA LEO
 • Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akiingia ukumbini na Nyota wa Soka Tanzania, aliyeshinda Tuzo ya mwanasoka Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa ndani, Mbwana Samatta, alipokutana na mchezaji huyo leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, kwa ajili ya kumpongeza kufuatia kutwaa tuzo hiyo.Picha zote na Bashir Nkoromo.
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akiwa ukumbini na Nyota wa Soka Tanzania, aliyeshinda Tuzo ya mwanasoka Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa ndani, Mbwana Samatta, alipokutana na mchezaji huyo leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, kwa ajili ya kumpongeza kufuatia kutwaa tuzo hiyo.
  Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye akimkaribisha Kikwete kuzungumza na waandishi wa habari, katika hafla hiyo ya kumpongeza Samatta. 
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Kikwete akizungumza na kumpongeza Nyota wa Soka Tanzania, aliyeshinda Tuzo ya mwanasoka Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa ndani, Mbwana Samatta (kushoto), alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kutana na mchezaji huyo leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, kwa ajili ya kumpongeza kufuatia kutwaa tuzo hiyo.Kulia ni Waziri Nape.
   Nyota wa Soka wa Tanzania, aliyeshinda Tuzo ya mwanasoka Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa ndani, Mbwana Samatta, akimkabidhi Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Kikwete, aliyokuwa akiitumia katika timu ya TP Mazeembe ya Congo DRC, katika hafla ya Kikwete iliyofanyika leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, kwa ajili yaRais huyo mstaafu kumpongeza kufuatia kutwaa tuzo hiyo.
  JK na Samatta wakitoka ukumbini.
  Samatta akiongozana na Kikwete kutoka ukumbini huku akiwa na tuzo yake.
  Samatta akiongozana na Kikwete kutoka ukumbini huku akiwa na tuzo yake.
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Kikwete na Waziri Nape wakirudi Ofisini baada ya kumsindikiza Samatta.
  Baadhi ya waandishi wa habari waliokuwepo kwenye hafla hiyo leo. 

  PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.

older | 1 | .... | 733 | 734 | (Page 735) | 736 | 737 | .... | 1903 | newer