Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 732 | 733 | (Page 734) | 735 | 736 | .... | 1904 | newer

  0 0


  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

  Simu: 255-22-2114512, 2116898
  E-mail: press@ikulu.go.tz
  Tovuti : www.ikulu.go.tz              

  Faksi: 255-22-2113425  OFISI YA RAIS,
        IKULU,
   1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
  11400 DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
   

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa Nchini IGP Ernest Mangu kufuatia kifo cha msaidizi wake Inspekta - Gerald Ryoba aliyepoteza maisha katika ajali ya kusombwa na mafuriko ya maji wakati akikatiza katika eneo la Kibaigwa, Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.

  Katika ajali hiyo iliyotokea 03 Januari, 2016 Inspekta Ryoba akiwa na Mkewe na watoto wake wawili, pamoja na watu wengine wawili walikua wakisafiri kutoka Geita kuja Jijini Dar es salaam na walipofika katika eneo la Bwawani gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji na wote sita kupoteza maisha.

  Rais Magufuli amempa pole nyingi Mkuu wa Jeshi la Polisi kwa msiba huo mkubwa, na amemuomba amfikishie salamu za pole kwa familia ya Marehemu Ryoba na kueleza kwamba anaungana nayo katika kipindi hiki kigumu.

  "Nimesikitishwa sana na tukio hili la kuondokewa na msadizi wako pamoja na familia yake, ni tukio linalotia uchungu mkubwa" amesema Mheshimiwa Rais.Aidha, Rais Magufuli amemuomba Mwenyezi Mungu awape nguvu na uvumilivu wafiwa wote, na aziweke roho za marehemu mahali pema peponi Amina.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam
  06 Januari, 2016

  0 0

   kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka Tanzania (TRA) (Katikati) Alphayo Kidata akisisitiza jambo wakati alipofanya mazungumzo na waandishi wa habari kuhusu taarifa za ukusanyaji wa mapato wa kila mwezi Kushoto ni Kaimu Kamishna wa Forodha Jocktan Kyamuhanga na kulia  ni Kaimu Kamishna wa Kodi za Ndani Yusufu Salum .
   Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka Tanzania (TRA) (Katikati) Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa za ukusanyaji wa mapato wa kila mwezi.Picha Na raymond Mushumbusi MAELEZO
   

  Jumla ya shilingi trilioni 1.4 imekusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kipindi cha mwezi Desemba mwaka uliopita wa 2015.

  Kiasi hicho ni sawa na ongezeko la wastani wa shilingi  bilioni 490 kwa mwezi ukulinganisha na wastani wa makusanyo ya kuanzia Julai hadi Novemba ambapo ,TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi bilioni 900 kwa mwezi.

  Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Kamishna Mamlaka ya Mapato  Tanzania (TRA) Alphayo Kidata wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kutoa taarifa kwa umma juu ya ukusanyaji wa kodi nchini.

  Ameongeza kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai mwaka jana hadi kufikia Desemba mwaka huo TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi trilioni 6.4 ambayo ilikuwa ni sawa na asilimia 95.5 ya lengo la kukusanya trilioni 6.5 katika kipindi hicho.

  Kaimu Kamishna huyo ametaja sababu za kuongeza kwa makusanyo ya kodi kuwa ni pamoja na kuziba mianya ya upotevu wa mapato na kuweka mifumo mizuri ya ufuatiliaji ili kumrahisishia mlipa kodi kulipa kodi anayostahili bila usumbufu.

  Kidata amesema kuwa katika kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya tano ya kuongeza mapato Mamlaka hiyo itasimamia kwa ukaribu ukusanyaji wa mapato na kuwabana wote wenye nia ya kukwepa na hatimaye kuwafikisha katika vyombo vya sheria watakaobainika wamekwepa kodi.
  Katika hatua nyingine Kaimu Kamishina Mkuu wa TRA huyo amesema jumla ya shillingi billioni 11.8zimekusanywa kutoka kwa wafanyabiashara walioondosha makasha katika Bandari Kavu kinyume na taratibu za forodha.

  Amesema kuwa makusanyo hayo yanajumuisha shilingi bilioni 5.3 kuoka kwa Kampuni na wafanyabiashara 19 ambao wamemaliza kulipa kodi za makasha yao na wengine 19 ambao wamelipa sehemu ya kodi ya makasha yao

  Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO
  Dar es Salaam
  6.1.2016


  0 0

  MWANDISHI wa habari wa magazetila Uhuru,Mzalendo na Burudani mkoani Arusha Shaaban Mdoe amejitokeza kuwania nafasi ya ukatibu wenezi wa CCMmkoa wa Arusha katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika mnamo Januari 28mwaka huu ili kuziba nafasi zilizo wazi kutokana na sababu mbalimbali.

  Mdoe ambaye amewahi kuwamjumbe wa baraza la vijana wilaya ya Arusha na mjumbe wa kamati mbalimbali zamaadhimisho ya sherehe mbalimbali za chama amesema amejitokeza kuwania nafasihiyo kutokana na msukumo wa fani yake,uzoefu katika chama na kazi mbalimbali zachama kupitia taaluma yake ya habari.

  Akizungumza na gazeti hilialisema kutokana na nia yake hiyo
  kesho(leo)atachukua fomu ya kuwania nafasihiyo katika ofisi kuu ya CCM
  mkoa wa Arusha ambapo pia atapata nafasi ya kuelezamikakati yake pindi
  jina lake litakaporejeshwa na vikao mbalimbali vya chama.

  Alisema sasa wakati umefikawa chama kupata viongozi wake katika baadhi
  ya nafasi kulingana na taalumakwakua ni jambo la muhimu taalumu
  kuzingatiwa katika kushika nyadhfa hizokwakua itasaidia katika
  utendaji kazi wake na kuleta mafanikio.

  Alisema kupitia taalumayake ya habari ameweza kufanya mambo mengi
  ikiwemo kuwaunganisha waandishi wahabari na vyombo mbalimbali wa mkoa
  wa Arusha katika kukitangaza chama jamboambalo anaamini pindi
  atakapopewa ridhaa hiyo ataifanya kazi hiyo zaidi ya palealipofikia.
  Mdoe anaeongozwa na kaulimbiu yake kuwa “Mshale unarudi porini”
  akimaanisha nafasi ya uenezi inahitajitaaluma ya habari,mahusiano na
  utendaji kazi wa kazi hiyo wakati wote na sikuwa na taaluma pekee bila
  kuifanyia kazi.

  “unajua ile dhana ya zamaniya uenezi kuwa ni ya kupanda jukwaani na
  kutambulisha wageni imepitwa na wakatikinachohitajika kwasasa ni
  kupata kiongozi wa nafasi hii mwenye kutenda kazihiyo kila wakati
  kwani mimi ni mwandishi sizuiwi na kazi nyingine hivyo nikiwa
  katikaziara za kujenga chama pia niko katika ajira yangu”alisema
  Mdoe.

  Mbali na mdoe wenginewaliotajwa kuwania nafasi hiyo ni pamoja na
  aliyewahi kuwa mwenyekiti waChadema Monduli Amani Silanga,aliyekuwa
  katibu wa siasa na uenezi wilaya yaArusha Semi Kiondo na Ally Rajabu.
  Nafasi hiyo ya ueneziiliachwa wazi na Isack Joseph aliyejiunga Chadema
  ambapo chaguzi huo mdogo pia piaunajumuisha nafasi ya mwenyekiti wa
  CCM mkoa kufuatia aliyekuwa mwenyekitiOnesmo Nangole kukihama chama.

  Pia uchaguzi huo utafanyikakatika kiti cha uenyekiti wilaya ya Monduli
  kufuatia aliyekuwa mwenyekitikujiunga Chadema,mchumi na mjumbe wa
  halmashauri kuu ya taifa(NEC) wa wilaya hiyo kufuatia aliyekuwa Mnec
  Edward Lowasa kuhamia Chadema

  0 0
 • 01/06/16--03:13: Article 7
 • Ubunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari akimsalimia moja wa watoto
  wanaouguzwa katika Hospitali ya Tengeru ,katika ziara yake alipofika
  kusikiliza matatizo yanawakumba wagonjwa haswa wakina mama waliolazwa katika hospitali ya tengeru alipofanya ziara ya ghafla hospitalin
  Ubunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari akimsalimia moja wa watoto
  wanaouguzwa katika Hospitali ya Tengeru ,katika ziara yake alipofika
  kusikiliza matatizo yanawakumba wagonjwa haswa wakina mama waliolazwa katika hospitali ya tengeru alipofanya ziara ya ghafla hospitalin
  Ubunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari Akisikiliza kero za wagonjwa
  wanaoitibiwa katika Hospitali ya Tengeru ,katika ziara yake alipofika
  kusikiliza matatizo yanawakumba wagonjwa haswa wakina mama waliolazwa katika hospitali ya tengeru alipofanya ziara ya ghafla hospitalin hapo

  0 0

  MICHUANO ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mzunguko wa tatu inatarajiwa kuendelea Januari 12 na wikiendi ya Januari 23-27 kwa timu 32 kuchuana kuwania kufuzu kwa hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

  Timu 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom zimeingia moja kwa moja mzunguko wa tatu ambapo sasa zinajumuika na timu 16 zilizofuzu kutoka raundi ya pili yenye timu kutoka ligi daraja la kwanza na ligi daraja la pili.

  Jumamosi, Januari 12, Majimaji itacheza dhidi ya JKT Mlale uwanja wa Majimaji mjini Songea, Januari 23 Pamba v Toto Africans uwanja wa CCM Kirumba, Ndanda FC v Mshikamano Nagwanda Sijaona Mtara, huku Burkinafaso wakiwakaribisha Simba SC katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

  Januari 24, Young Africans watacheza dhidi ya Friends Rangers uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Njombe Mji v Tanzania Prisons uwanja wa Amani Makambako, mjini Shinyanga Stand United watachuana dhidi ya Mwadui FC.

  Mechi zingine ni Kagera Sugar v Rhino Rangers, Panone v Madini, Mtibwa Sugar v Abajalo, Lipuli/Kurugenzi v JKT Ruvu, Ashanti United v Azam FC, Africa Sports v Coastal Union, Geita Gold v Mgambo Shooting, Singida United v Mvuvuma na Wenda v Mbeya City.

  Timu 15 zilizofuzu hatua ya tatu kutoka raundi ya pili ni Ashanti United, Friends Rangers, Panone, Geita Gold, Pamba, Mvuvuma, Burkinafaso, Rhino Rangers, Madini FC, JKT Mlale, Mshikamano FC, Njombe Mji, Wenda FC, Singida United, Abajalo huku mchezo mmoja kati ya Lipuli dhidi ya Kurugenzi ukichezwa leo hii kusaka timu ya kufuzu raundi ya tatu.


  Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) ataiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) mwaka 2017.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano) Mh. January Makamba (Kushoto) akifurahia jambo na Balozi wa Norway nchini Bi. Hanne-Marie Kaarstad. Balozi huyo na ujumbe wake walimtembelea Mh. Waziri leo Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli kwa lengo la kujadili juu ya kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na Finland katika nyanja za Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira. 
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano) Mh. January Makamba (Kushoto) akiongea na Balozi wa Finland nchini Bw. Pekke Hukka. Balozi huyo na ujumbe wake walimtembelea Mh. Waziri leo Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli kwa lengo la kujadili juu ya kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na Finland katika nyanja za Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira. 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano) Mh. January Makamba (Kushoto) akiongea na Balozi wa Norway nchini Bi. Hanne-Marie Kaarstad. Balozi huyo na ujumbe wake walimtembelea Mh. Waziri leo Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli kwa lengo la kujadili juu ya kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na Finland katika nyanja za Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira.

  0 0

   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Yussuf Masauni akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hatua zinazochukuliwa na Wizara kudhibiti wageni wanaoishi nchini na kufanya kazi kinyume na sheria. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam.
  Afisa Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Johannes Msumule akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Yussuf Masauni alizungumzia hatua zinazochukuliwa na Wizara kudhibiti wageni wanaoishi na kufanya kazi nchini kinyume na sheria. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam.

  Sehemu ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Yussuf Masauni, wakati wa mkutano wa kuzungumzia hatua zinazochukuliwa na Wizara kudhibiti wageni wanaoishi nchini na kufanya kazi kinyume na sheria. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam.
  (PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI).

  0 0

  WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Africommerce International Limited, Elisante Muro na kuzungumzia fursa mbalimbali za uwekezaji nchini hususan katika sekta ya Nishati.

  Muro alimtembelea Waziri Muhongo na kueleza nia ya Kampuni yake kuwekeza kwenye mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirishia mafuta kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza na vilevile uwekezaji kwenye mradi wa ujenzi wa nguzo za umeme za zege. 
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Africommerce International Limited, Elisante Muro wakati wa kikao cha kujadili fursa za uwekezaji.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Africommerce International Limited, Elisante Muro (hayupo pichani) ambaye alimtembelea Waziri huyo kuzungumzia fursa za uwekezaji kwenye sekta ya nishati nchini. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu- Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu- Madini, Profesa James Mdoe.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza jambo wakati wa kikao na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Africommerce International Limited, Elisante Muro (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kujadili fursa za uwekezaji. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu- Madini, Profesa James Mdoe na wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu- Nishati, Dkt. Mhandisi, Juliana Pallangyo.

  0 0


  ISO 9001:2008 CERTIFIED
  TAARIFA KWA UMMA
  Kumekuwa na upotoshwaji kuhusu zoezi la ufuatiliaji wa matumizi ya misamaha ya kodi inayosimamiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa wafanyabiashara, wawekezaji, Taasisi za Dini na Taasisi zisizo za kiserikali kwa maelezo kwamba TRA inazilenga baadhi ya Taasisi.

  Sheria ya Mamlaka ya Mapato Tanzania inaipa Mamlaka ya kusimamia, kukagua na kuhakiki mapato ya Serikali pamoja na kuzuia ukwepaji wa kodi wa aina yoyote ile ikiwemo matumizi mabaya ya misamaha ya kodi inayotolewa kwa mujibu wa Sheria.

  Kifungu cha 5 (3) cha Sheria ya TRA kinatoa mamlaka kwa TRA kufanya jambo lolote lenye tija na manufaa katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu yake kisheria.

  Kwa vile misamaha ya kodi inatolewa kwa mujibu wa Sheria zinazosimamiwa na TRA, ni wajibu wa Mamlaka kuhakiki kama bidhaa au huduma zilizosamehewa zinatumiwa na watu au Taasisi zinazostahiki misamaha hiyo au kwa miradi iliyokusudiwa.

  Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa za upotoshaji kwamba TRA imeilenga Taasisi moja ya kidini kwa kuiandikia barua ya kuomba vielelezo na ufafanuzi juu ya misamaha ya magari iliyopewa awali na kuonekana kana kwamba ni utaratibu mpya wa utoaji wa misamaha.

  Tungependa kufafanua kwamba TRA haibagui wala kulenga Taasisi yoyote bali inatekeleza wajibu wake wa kufuatilia misamaha iliyotolewa

  Katika kipindi cha Mwezi Oktoba hadi Desemba 2015 TRA iliwaandikia walipakodi 65 kupata vielelezo juu ya matumizi ya misamaha ya kodi walioipata na katika hao zimo Taasisi za kidini 39.

  Ukaguzi huu huisadia TRA kupata taarifa muhimu ili kuishauri Serikali namna bora ya kutoa misamaha kwa ajili ya kuleta tija na ufanisi uliokusudiwa ikiwemo kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu za jamii na kupunguza umaskini. Aidha taarifa za misamaha ya kodi zinaisadia TRA kubaini matumizi bora ya misamaha pamoja na mianya ya upotevu wa mapato kupitia misamaha hiyo ili TRA ichukue hatua zinazostahili pale inapobainika kuwa kuna ukwepaji na kuziba mianya hiyo.

  Zoezi hili ni endelevu hivyo tunaziomba Taasisi zote za kidini na mashirika yote yanayonufaika na misamaha ya kodi kuchukulia zoezi la ukaguzi wa misamaha hiyo kuwa ni utekelezaji wa sheria na wahusika wote ushirikiano kwa TRA pale wanapohitajika ili zoezi hilo lifanyike kwa ufasaha na kwa manufaa kwa wote.

  “Pamoja Tunajenga Taifa Letu

  A. J. Kidata

  KAIMU KAMISHNA MKUU.

  0 0

   
  Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

  Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) imesema itaendelea kupambana na wale wote watakaogundulika kwa wizi wa kazi za sanaa.

  Agizo hilo limetolewa na Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Alphayo Kidata alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari na kueleza kuwa wapo katika operesheni ya kukamata wezi wa kazi za sanaa .

  "Ipo  kamati ambayo inajumuisha wadau kama Bodi ya Filamu, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na COSOTA ikishirikiana na Jeshi la Polisi katika  kupambana na wizi wa kazi za wasanii unaokidhiri siku hadi siku' `Alisema Kaimu Kamishna Kidata.

  Serikali ipo makini kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania katika kukusanya mapato hasa kuongeza maeneo ya kukusanya mapato ikiwemo eneo la kazi za sanaa hivyo  Serikali haitakubali kuona inakosa mapato hayo na yoyote anayejua mtu au kikundi cha watu kinachofanya wizi wa kazi za sanaa atoe taarifa ofisi za TRA.

  0 0

   Balozi Seif Ali Iddi akizindua Mradi wa Maji safi na salama katika kisiwa cha Tumbatu ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
   Balozi Seif akimtwisha ndoo ya Maji Bibi Miza Ali Haji mara baada ya kuuzindua mradi wa maji safi na salama katika kisiwa cha Tumbatu kiliopo Mkoa wa Kaskazini Unguja.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Wananchi wa Kisiwa cha Tumbatu waliohudhuria uzinduzi wa maji safi na salama hapo katika eneo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya hiyo pembezoni mwa Bandari ya Tumbatu.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwasili katika Bandari ya Kisiwa cha Tumbatu na kupokewa na Katibu Tawala wa Wilaya Ndogo ya Tumbatu Nd. Khatib Habib Ali kwa ajili ya uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi na salama Kisiwani humo.


  Picha na – OMPR – ZNZ.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar daima itaendelea kutekeleza kazi zote zilizoahidiwa na chama cha zamani cha Afro Shirazy Party { ASP } katika kuwajengea  ustawi bora Wananchi wake.

  Amesema  huduma za maji safi na salama ilikuwa ni miongoni mwa ahadi kubwa Nne zilizotolewa na ASP wakati ikiomba ridhaa ya kutaka kuviongoza Visiwa vya Zanzibar wakati ikipigania  kuwakomboa Wananchi wake.

  Akizindua mradi wa maji safi na salama uliopo Wilaya ndogo ya Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya kutimia miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 Balozi Seif Ali Iddi alisema SMZ inatambua  umuhimu wa maji kwa uhai na maendeleo ya Wananchi na ndio maana ikaamua kwa makusudi kutekeleza ahadi hizo.

  Alisema hali ya upatikanaji wa huduma za maji safi na salama ndani ya Zanzibar hasa Vijijini inatia moyo kutokana na jitihada kubwa zilizochukuliwa na Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } Wadau wa Maendeleo ndani na nje ya Nchi kwa kushirikiana katika kukabiliana na upungufu wa maji.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwakumbusha Wananchi  lazima wajenge tabia ya kushiriki kikamilifu katika uhifadhi wa vianzio vya maji kwa lengo la kulinda mazingira.

  Akitoa Taarifa ya Kitaalamu ya mradi wa maji safi na salama katika Kisiwa cha Tumbatu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Mkaazi, Maji na Nishati Zanzibar Nd. Ali Khalil Mirza alisema ujenzi wa mradi huo ulioanzia kwa hatua ya uchimbaji  wa visima viwili vyenye uwezo wa kuzalisha Maji Lita Laki 250,000  katika Vijiji vya Tingatinga na Pale ulienda sambamba  na ulazaji wa Mabomba  yenye  urefu wa Kilomita 8.25.

  Katibu Mkuu huyo wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati alifahamisha kwamba awamu ya kwanza ya mradi huo tayari imeshatumia zaidi ya shilingi Mia 636.7 Milioni wakati ile iliyobakia inatarajiwa kutumia shilingi Milioni 400.Mapema  akisoma  Risala ya Wananchi wa Kisiwa hicho Katibu Tawala wa Wilaya ndogo ya Tumbatu Ndugu Khatib Habib Ali alisema kukamilika kwa mradi huo wa maji safi na salama kutawapunguzia usumbufu wa kupata huduma hiyo hasa akina Mama.

  Nd. Khatib alisema Wananchi wa Shehia zote nne zilizomo ndani ya Kisiwa cha Tumbatu wanathamini juhudi kubwa za Viongozi wao ambazo ni kichocheo cha kasi katika kuelekea kwenye  Maendeleo.Aliuomba Uongozi pamoja na wahandisi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } kuhakikisha kwamba awamu ya Pili iliyobakia ya mradi huo inakamilika kwa wakati uliopangwa.

  Othman Khamis Ame
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula.

  Na:George Binagi.
  MBUNGE wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza Stanslaus Mabula (CCM, ameahidi kushughulikia suala la ujenzi wa maegesho ya magari makubwa ya mizigo nje ya jiji la Mwanza ili kuzuia magari hayo kuingia katikati ya jiji.

  Akizungumza ofisini kwake hii leo, Mabula amebainisha kuwa upo mpango wa kujenga maegesho hayo katika maeneo yaliyo nje ya Jiji la Mwanza, hatua ambayo itasaidia magari hayo kutoingia katikati ya Jiji na hivyo kuondoa malalamiko yaliyopo kutoka kwa madereva wa magari madogo ya mizigo wanaolalamikia uingiaji wa magari makubwa ya mizigo katikati ya jiji.

  Ameyataja maeneo yanayotarajiwa kujengwa maegesho hao kuwa ni Buhongwa pamoja na Igoma na kwamba baada ya ujenzi wake kukamilika, magari yote makubwa ya mizigo hayataruhusiwa kuingia katikati ya Jiji.

  Mabula ambae alikuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza katika uongozi uliomalizika mwaka jana, amebainisha kuwa utekelezaji wa ujenzi wa maegesho hayo unatarajiwa kufanyika kwa uharaka zaidi ambapo amewahimiza wawekezaji mbalimbali kujitokeza ili kushirikiana na halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa ajili ya kufanikisha ujenzi huo.

  Suala la magari makubwa kuingia katikati ya Jiji la Mwanza huku yakiwa na mizigo, linalalamikiwa na madereva wa magari madogo ya mizigo kwa kile wanachoeleza kuwa wanaingiliwa katika shughuli ambazo wao wangezifanya na hivyo kujiingia kipato ambapo wameiomba halmashauri ya Jiji la Mwanza kutoruhusu magari hayo kuingia katikati ya Jiji.
  Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula.

  Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula akiongea na wanahabari ofisini kwake.

  0 0

  Walimu (Msingi) wakishiriki mafunzo ya Kujenga Uwezo katika ufundishaji na ujifunzaji katika Mkoa wa Ruvuma. Mafunzo hayo yanawezeshwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

  MAMLAKA ya Elimu Tanzania kwa kushirikiana na  Wizara ya Elimu, Sayansi, na Teknolojia, na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imewezesha awamu ya pili ya Programu ya kujenga uwezo wa walimu na wanafunzi, kwa walimu mahiri (Msingi) wa masomo ya Hisabati, Kiswahili na Kiingereza  katika mikoa mitatu nchini; Songea, Katavi, na Singida.


  Lengo la mafunzo haya ni kuwawezesha walimu kuwatambua wanafunzi wenye uwezo mdogo kimasomo na kuwapatia mafunzo rekebishi; na kuwajengea uwezo ili wote wawe na uelewa unaolingana.


  Programu ya kujenga uwezo wa walimu na wanafunzi katika ufundishaji na ujifunzaji (Student Teaches Enrichment Program)  ni moja kati ya mikakati  9 iliyoibuliwa wakati wa maabara ya BRN katika sekta ya elimu ambao unatekelezwa kupitia mafunzo kwa walimu, na kufadhiliwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania.


  Awamu ya kwanza ya mafunzo haya ilihusisha  Halmashauri 40 ambapo jumla ya walimu 19,300 walipatiwa mafunzo kwa mwaka 2014/15. Hii ni awamu ya pili ya mafunzo haya ikihusisha halmashuri 60 ambapo jumla ya walimu mahiri 900 wanawezeshwa katika vituo 8 vilivyoteuliwa kuwa mwenyeji wa mafunzo haya, yanayolenga kuwafikia walimu 18,501 katika mwaka huu wa fedha 2015/2016.


  Mafunzo wezeshi kwa walimu wa sekondari wa masomo ya Kiingereza, Hisabati, Kiswahili, na Biology nayo yanaendelea kwa ufadhili wa Mamlaka ya Elimu Tanzania.

  0 0
 • 01/08/16--02:47: HONGERA KWA TUZO SAMATTA.
 • RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Jamal Malinzi amempongeza mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya TP Mazembe ya Congo DR (Pichani) kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani.
  Samatta ameshinda tuzo ya mchezaji bora kwa wachezaji wanaocheza Afrika baada ya kwashinda Robert Kidiaba (Congo DR) alieshika nafasi ya pili na Bounedjah Baghdad (Algeria) aliyeshika nafasi ya tatu.
  Kwa kushinda tuzo hiyo, Samatta amekua mchezaji wa kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki kushinda tuzo kubwa barani Afrika.
  Pamoja na kushinda tuzo hiyo, Samatta pia amejumuishwa katika kikosi bora cha wachezaji wa Afrika kwa mwaka 2015 sambamba na Robert Kidiaba (Congo DR), Sergie Aurier (Ivory Coast), Aymen Abdenmor (Tunisia), Mohamed Meftah (Algeria), Sadio Mane (Senegal), Yaya Toure (Ivory Coast), Yacine Ibrahim (Algeria), Andrew Ayew (Ghana), Mbwana Samatta (Tanzania), Pierre-Emercik Aubameyang (Gabon) na Baghdad Bounedjah (Algeria).
  Mshambuliaji Mbwana Samatta alieyambatana na Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine wanatarajia kuwasili nchini leo saa 8 usiku kwa shirika la ndege la Ethiopia.

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari Katika ukumbi wa Maendeleo ya Jamii, Jisia, wazee na watoto jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kuhamasisha wazazi au walezi kuwahamasisha waoto kujiunga na shule za Msingi na Sekondari kwa 2016.
  kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  akiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
   Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu jijini Dar es Salaam.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
  SERIKALI itawafungilia mashtaka na kuwapeleka mahakamani wazazi na walezi wote watakashindwa kutimiza wajibu wao wa kuwapeleka watoto shule ili kupata Elimu ya Msingi na Sekondari.

  Pia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ikishirikiana na Ofisi ya Rais- TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sayansi, Technologia, na Ufundi inawahamasisha wazazi au walezi kutimiza wajibu wao kuhakikisha kuwa watoto wenye umri wa kuanza shule za msingi na Sekondari kuanza kwa wakati.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

  Pia viongozi na watendaji wa mikoa na halmashauri,  maafisa Maendeleo ya jamii na watendaji wa kata wameaswa kusimamia na kutekeleza majukumu yao kwa kuhakikisha wanahamasisha jamii ipasavyo juu ya watoto kujiunga na darasa la kwanza na kidato cha kwanza kwa mwaka huu.

  Ummy amesema kuwa maafisa wa maendeleo ya jamii za mikoa, Halmashauri na kata  zote hapa nchini watoe taarifa za utekelezaji wa jambo la watoto kwenda shule mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.

  Aidha  Serikali inatoa rai kwa wazazi na walezi kuhakikisha kuwa watoto wote wanaendelea na masomo ya shule ya Msingi na Sekondari vizuri na wahudhurie masomo yao kwa ufanisi, pia serikali haitegemei kuona utoro wa watoto mashuleni kutokana na sababu zinazoweza kuepukika.

  0 0

  SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu (TFF), limetuma salamu za rambirambi kwa kocha msaidizi wa Taifa Stars Hemed Suleiman “Morocco” kufutia kifo cha baba yake mzazi Suleiman Ally Hemed kilichotokea juzi kisiwani Zanzibar.
  Katika salamu hizo za rambirambi, TFF imewapa pole wafiwa, ndugu jamaa na marafiki na kusema wapo pamoja na familia ya marheemu katika kipindi hiki kigumu cha maombeloezo.
  Aidha TFF imetuma rambirambi (ubani) wa shilingi laki mbili (200,000) kwa familia ya kocha Hemed Moroco kufuatia kifo cha baba yake Suleiman Ally.
  Mazishi ya marehemu Suleiman Ally Hemed yamefanyika jana jioni mjini Zanzibar.

  0 0
 • 01/08/16--04:38: VITA DHIDI YA RUSHWA DUNIANI

 • 0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya Ndege Zanzibar Kepten  Saidi Iddi Ndumbugani, kuhusu aina ya Taa mbali mbali zilizofungwa kwa uongozaji wa Ndege wakati wa ikitua  katika  sherehe ya uzinduzi wa Taa za kuongozea Ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Pemba uliofanyika jana ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Katika barabara ya ndege katika uwanja wa ndege wa Karume Pemba zikiwa zinaonekana Taa hizo zikiwa tayari kufanya kazi inayohitajiwa kwa wakati,taahizo zilizinduliwa jana na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika  sherehe ya uzinduzi wa Taa za kuongozea Ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Pemba ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya Ngege Zanzibar Kepten  Saidi Iddi Ndumbugani, wakati alipofika kutembelea kuona  aina ya Taa mbali mbali zilizofungwa kwa uongozaji wa Ndege wakati wa ikitua  katika  sherehe ya uzinduzi wa Taa za kuongozea Ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Pemba uliofanyika jana ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Aina ya Taa zilizokuwa mwishoni mwa kiwanja cha ndege cha Karume Pemba zikiwa na Rangi ya Nyekundu na Buluu ambazo hutoa ishara kwa Kepteni anayeongoza Ndege ikitua,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Viongozi mbali mbali aliofuatana nao walijionea  taa hizo namna zilivyofungwa  katika utaratibu maalum wakati  uzinduzi wa Taa za kuongozea Ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Pemba uliofanyika jana ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

  Aina ya Taa zilizokuwa nje kabisa ya  kiwanja cha ndege cha Karume Pemba  ambazo hutoa ishara kwa Kepteni anayeongoza Ndege ikitua,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Viongozi mbali mbali aliofuatana nao walijionea  taa hizo namna zilivyofungwa  katika utaratibu maalum wakati  uzinduzi wa Taa za kuongozea Ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Pemba uliofanyika jana ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifungua pazia kama iskara ya Uzinduzi wa Taa za Kuongozea Ndege katika kiwanja cha Ndege cha Karume Pemba jana ikiwa ni katika sherehe za shamra shamra za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar (kushoto) Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi(GAVU).
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya Ngege Zanzibar Kepten  Saidi Iddi Ndumbugani, kuhusu majenereta yanayotoa umeme baada ya kuzindua rasmi  Taa za kuongozea Ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Pemba jana ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Wafanyakazi Mamlaka ya Viwanja vya Ndege na Wananchi wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi wakati alipkuwa akitoa hutuba yake ya uzinduzi wa Taa za kuongozea Ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Pemba jana ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Dk.Juma Malik Akili alipokuwa akitoa maelezo ya kitaalam kuhusu mradi wa uwekaji wa Taa  za kuongozea Ndege katika sherehe za uzinduzi wa Taa za Kuongozea Ndege katika kiwanja cha ndege cha Pemba jana ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi(GAVU) akitoa slamau za Wizara pamoja na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na wananchi katika sherehe za uzinduzi wa Taa za Kuongozea Ndege katika kiwanja cha ndege cha Pemba jana ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na wananchi katika sherehe za uzinduzi wa Taa za Kuongozea Ndege katika kiwanja cha ndege cha Pemba jana ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid na (kushoto) Naibu Waziri wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi(GAVU).
   [Picha na Ikulu.]

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS, IKULU

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salam za pongezi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na  Michezo Mhe. Nape Nnauye kufuatia mchezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu  Mbwana Ally Samatta kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza Barani Afrika; iliyotolewa katika mji wa Abuja nchini Nigeria jana usiku.


  Mhe. Rais Magufuli amemtaka Waziri Nape Nnauye amfikishie salam zake za pongezi kwa mchezaji huyo ambaye pia ni mchezaji wa kulipwa wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.


  Amesema tuzo hiyo imemjengea heshima na kuleta sifa kwa Mbwana Samatta mwenyewe, wanasoka hapa nchini na Tanzania kwa ujumla katika medali ya Soka Kimataifa.


  Aidha, Rais Magufuli amewasihi wachezaji wa soka wote na wadau wa mchezo huo kuongeza juhudi za kuundeleza mchezo huo ili upige hatua zaidi za kimaendeleo.


  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

  Dar es Salaam
  08 Januari, 2016.

  0 0

   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katika). Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Upande wa Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo na anayefuatia ni Naibu Katibu Mkuu Upande wa Madini, Profesa James Mdoe na Balonzi wa Uturuki Nchini Tanzania, Yasemin Eralp na Msaidizi wake.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na Balonzi wa Uturuki Nchini Tanzania, Yasemin Eralp wakati akisaini kitabu cha wageni.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Balonzi wa Uturuki Nchini Tanzania, Yasemin Eralp katika picha ya pamoja.  
  Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo katikati mbele akiwa katika kikao hicho.

  Na Rhoda James
  Serikali ya Uturuki imeomba kuwekeza katika sekta ya Nishati nchini hususani umeme ili kusaidia upatikanaji wa umeme wa kutosha na wa uhakika.

  Ombi hilo linafuatia kikao baina ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin Eralp kilichofanyika jijini Dar es Salaam, huku pia Balozi huyo akigusia uwekezaji katika sekta za Kilimo na Utalii.

  Vilevile, Balozi Eralp aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwakaribisha kuwekeza katika sekta ya umeme na pia alimshukuru Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kwa kuwa muwazi na kuufahamisha ujumbe huo kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo nchini kupitia sekta za nishati na madini.

  Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, alitumia nafasi hiyo kumweleza Balozi Eralp na ujumbe wake kuhusu fursa za uwekezaji kupitia vyanzo mbalimbali vya nishati ikiwemo Nishati Jadidifu, Gesi Asilia, Makaa ya Mawe ili kuzalisha umeme ikiwemo pia sekta ya madini.

  Prof. Muhongo pia alieleza kuhusu uwekezaji katika sekta ndogo za Mafuta na Gesi hususani katika Kitalu kilichopo upande wa Kusini Mashariki mpakani mwa Tanzania na Msumbiji, eneo ambalo Profesa Muhongo alieleza kuwa, Serikali inahitaji mwekezaji mbia.

  “Kipo Kitalu upande wa Kusini Mashariki mwa Tanzania na Msumbiji ambacho Serikali ya Tanzania inahitaji mwekezaji Mbia. Mnaweza kushirikiana na Shirika letu la Maendeleo ya Petroli Tanzania. (TPDC),” alisisitiza Profesa Muhongo.

  Pia, Profesa Muhongo alimweleza kuhusu maeneo mengine yanayohitaji uwekezaji   kuwa ni Malagarasi, Kakono na Ruhuji. “Lakini pia mnakaribishwa kuwekeza katika madini, tunayo madini ya aina nyingi nchini ikiwemo dhahabu,” alisema Profesa Muhongo.

  Vilevile, Waziri Muhongo alimweleza Balozi Eralp kuhusu kuisaidia Tanzania katika suala la elimu, hususani ufadhili wa masomo katika ngazi za Uzamivu na uzamili katika upande wa masomo ya Jiolojia, Mafuta, Gesi na maeneo mengine.

  Akijibu ombi hilo, Balozi alimweleza kuwa, “Uwezekano wa ufadhili wa masomo hayo upo na mara nyingi taratibu za kutuma maombi huanzia mwezi Aprili’,” alisema Balozi Eralp.

older | 1 | .... | 732 | 733 | (Page 734) | 735 | 736 | .... | 1904 | newer