Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI YASHTUSHWA NA KASI YA DAWASCO.

$
0
0
 Mkurugenzi wa Rasilimali watu w Shirika la Maji safi na Maji taka Dar es Salaam,DAWASCO,Bi,Joy Chidosa akifanya utamburisho katika kikao hicho.
Baadhi ya Mameneja wa vitengo mbalimbali katika Shirika la Maji safi na Maji taka jijini Dar es Salaam DAWASCO ,wakiwa katika kikao hicho.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Dawasco wakionekana wenye nyuso za furaha wakati wa kikao hicho.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maji safi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO) Mhakndisi Cypian Luhemeja akiongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Mbogo Mfutakamba ,wakielekea katika kikao cha Unongozi na wafanyakazi wa DAWASCO kilichofanyika makao makuu y a shirika hilo. 

Afisa Mtendaji mkuu wa DAWASCO,Mhandisi Cyprian Luhemeja akifurahia jambo na katibu mkuu wa wizara ya maji na umwagiliai Mhandisi ,Mbogo Mfutakamba. 
Afisa Mtendaji mkuu wa DAWASCO,Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza wakati wa kikao cha wafanyakazi kilicho fanyika makao makuu ya ofisi za Dawasco.
 Baadhi ya wafanyakazi wa DAWASCO. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagliaji,Mhandisi Mbogo Mfutakamba akizungumza na wafanyakazi wa DAWASCO wakati wa kikao kilichofanyika makao makuu ya shirika hilo . 
 Mwakilishi wa wafanyakazi wa DAWASCO,Abdalah Jongo akiongea kwa niaba yao wakati wa kikao hicho. 
Baadhi ya wafanyakazi wa DAWASCO wakiliombea dua shirika hilo ili liweze kutimiza malengo yake ya kutoa huduma ya maji safi na maji taka kwa usalama kwa wakazi wa miji ya Dar es Salaam,Kibaha na Bagamoyo.



Imeandaliwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini aliyekuwa jijini Dar es Salaam.


WIZARA ya maji na umwagiliaji, imesema inaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mipango ya usambazaji wa huduma za maji, inayofanywa na shirika la majisafi na majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) na kutoa rai kwa watumishi wa shirika hilo kushirikiana ili kufikia malengo ya utoaji wa huduma kwa wananchi.

Hayo yalisemwa jana na katibu mkuu wa wizara hiyo mhandisi Mbogo Futakamba, alipokuwa akiwahutubia wafanyakazi wa DAWASCO, katika makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam.

Mhandisi Futakamba, alisema kasi ya utoaji wa huduma bora za maji kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, imepunguza malalamiko mengi ya wananchi, na kwamba serikali imeanza kupata matumaini makubwa na kujenga imani kwa shirika hilo kwa kufanikisha malengo makuu ya usambazaji wa huduma hiyo kwa wananchi.

Aidha alisema kwa kiwango kikubwa wizara ya maji na umwagiliaji kwa sasa inajivunia kwa kazi nzuri iliyofanywa na shirika hilo, hasa kwa kuzingatia kuwa DAWASCO ndio jicho la wizara kutokana na wingi wa wananchi wanaohitaji huduma za maji zinazosambazwa na shirika hilo.

“Nimeona jitihada zenu, nimependa jinsi mnavyofanya kazi kama timu, naomba muwe na uaminifu mkubwa sana katika kazi, kuweni wawajibikaji ili wananchi wapate huduma ya maji”, alisema mhandisi Futakamba.

Katika hatua nyingine katibu mkuu huyo alipongeza juhudi kubwa zilizofanywa na shirika hilo za kupunguza kiwango cha upotevu wa maji pamoja na kudhibiti wizi wa maji, ambavyo vimekuwa kikwazo kinachochochea malalamiko ya wananchi kwa shirika hilo.

Awali akitoa taarifa ya shirika hilo, afisa mtendaji mkuu wa DAWASCO, mhandisi Cyprian Luhemeja, alisema shirika hilo limefanikiwa kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji, baada ya kuongeza uzalishaji kutoka mita za ujazo 7,834,234 hadi mita za ujazo 8,421,370 kati ya mwezi Mei hadi Novemba 2015.

Alizitaja sababu za mafanikio ya ongezeko la kiwango cha maji ni pamoja na udhibiti wa upotevu wa maji katika bomba kubwa, kufanya matengenezo ya tahadhari, maboresho ya maslahi ya wafanyakazi na kuboreshwa kwa kitengo cha upotevu wa maji.

Mhandisi Luhemeja alibainisha kuwa DAWASCO, imefanikiwa kufunga dira katika maungio ya maji, kuziba maeneo yanayovujisha maji kwa wakati, kupambana na wezi wa maji, kuhakiki ufanisi wa dira za maji, kusajili maboza ya wauzaji maji na kuboresha usomaji wa dira, ambavyo viliwezesha kupunguza kiwango cha maji yanayopotea kutoka asilimia 62 hadi 45, kati ya mwezi Mei mpaka Novemba 2015.

Aliongeza kuwa mafanikio ya utekelezaji wa mipango ya uboreshaji wa huduma za maji yaliwezesha shirika hilo la DAWASCO, kuongeza makusanyo ya mapato kutoka shilingi bilioni 2.9 hadi kufikia bilioni 6.2 kati ya mwezi Mei hadi Novemba 2015.

Wakati huo huo shirika hilo limeanza kutekeleza agizo la serikali linaloitaka DAWASCO, kuongeza idadi ya wateja wake hadi kufikia milioni moja, katika jiji la Dar es Salaam, miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani, hadi kufikia mwezi Juni 2016.

Katika utekelezaji wa agizo hilo DAWASCO iko katika utekelezaji wa Maagizo ya serikali ya kuhakikisha wananchi waishio katika Jiji la Dar s salaam, Miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani Pwani wanaunganishiwa Maji ifikapo Julai 2016. Katika kutekeleza agizo hilo Dawasco imejipanga katika awamu kuu NNE (4)

1. Awamu ya kwanza itawahusu wateja wote walioko katika maeneo ambayo kwa sasa yanapata maji na kuna miundo mbinu ya mabomba karibu.

2. Awamu ya Pili itahusu maeneo ambayo yamepitiwa na mabomba makubwa ya Maji jirani lakini wananchi wake hawana maji kwa sababu ya kukosekana kwa miundo mbinu ya usambazaji.



3. Awamu ya Tatu itahusisha maeneo yote yaliyopitiwa na mradi maarufu wa Mabomba ya Kichina, Maunganisho katika awamu hii yataanza baada ya kukamilika kwa Miradi ya Ruvu Chini na Ruvu Juu,


4. Awamu ya Nne itaanza katika maeneo yote ambayo kwa sasa hakuna miundo mbinu ya Maji na yako mbali kutoka katika mabomba makubwa .

Gharama ya kuunganishiwa huduma ya Majisafi ni Tsh 200,000 kwa wateja wadogo (Domestic Customers)na Tsh 400,000 kwa wateja wakubwa (Corporate Customers).

NAIBU WAZIRI MASAUNI AWAONYA WANAOCHAFUA SERIKALI KUHUSIANA NA OPERESHENI KAMATA WAHAMIAJI HARAMU.

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni akizungumza na wananchi wa Visiwani Zanzniabr waliokuwa wakisubiri husduma katika ofisi za Uhamijia  alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kujionea shughuli za kiutendaji  zilizoko Kilimani Zanznibar.

 Naibu wAZiri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni akisikiliza maelezo ya hatua za maombi ya hati za kusariria  kutoka kwa afisa wa udhibiti wa hati za kusafiria katika ofisi za Uhamiaji Zanzibar alipofanya ziara ya kikazi kwa ajili ya kujione shughuli mbalimbali za kiutendaji .

 Naibu WaZiri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni (kushoto) akiongozana na Kamishna wa Uhamijai Zanznibar , Johari Sururu (Kulia) kuelekea katika chumba cha kuhiofadhi kumbumbuku za waombaji hati za kusafiria. Naibu huyo alitembelea ofisi hizo kwa ajili ya kujionea shughuli za kiutendaji  katika ofisi hizo
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni akikagua jarada lenye kuonyesha kumbukumbu za waombaji wa hati za kusafiria kutoka katika familia yake, aliyesimama ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzniabr Johari Sururu akifatiwa na Naibu Kamishna wa Utawala na fedha. Masauni alifanya ziara hiyo ya kikazi kwa ajili ya kujionea shighuli mbalimbali za kiutendaji.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni akizungumza na watendaji wakuu wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar alikofanya ziara ya kikazi kwa ajili ya kujionea shughuli za kiutendaji. Waziri huyo ametoa onyo kwa maafisa wote wanaotumia zoezi la kukamata wahamiaji haramu kinyume na agizo la serikali kuwa watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Kamishna wa Idara ya Uhamiaji zanzibar, Johari Sururu akitoa taarifa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni aliyefanya ziara ya kikazi kwa ajili ya kujionea shughuli za kiutendaji katika ofisi za Uhamiaji zilizopo eneo la Kilimani Zanznibar.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi akisalimiana na Naibu Kamishna wa uhamiaji Haji Hamza wakati alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi za Uhamiaji Zanzibar zilizopo katika eneo la Kilimanim, kulia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Sururu.
 Naibu Waziri wa Mmambo ya Ndani ya Nnchi Hamad Masauni akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Kamishina Mkuu wa Uhamiaji Zanzibar alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kujionea shughuli za kiutendaji katika ofisi hizo zilizoko Kilimani Zanznibar.
(IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO MAMBO YA NDANI YA NCHI).

WANACHI WASHAURIWA KUTUMIA KITUO CHA KURATIBU MATUKIO YA SUMU

$
0
0
Mratibu wa Kituo cha kuratibu matukio ya sumu nchini toka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw. Yohana Goshashy akiwaeleza waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam. kuhusu umuhimu wa kituo hicho hapa nchini ikiwemo kuwakinga na madhara ya sumu kwa kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya kemikali mbalimbali.kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Frank Mvungi.

(PICHA NA BENEDICT LIWENGA- MAELEZO).

Na Jovina Bujulu –Maelezo
SERIKALI imewataka wananchi kutumia kituo cha kuratibu matukio ya sumu wapatapo madhara yatokanayo na Sumu kote nchini.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Kituo hicho kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw. Yohana Goshashy wakati wa mkutano na Vyombo vya habari leo Jijini Dar es salaam.

“kwa sasa matukio mengi yanayotolewataarifa kituoni hapo ni dawa za kulevywa na dawa za kuulia wadudu waharibifu kwenye mimea(viuatilifu)” Alisema Ndudu Goshashy.

Akizungumzia majukumu ya kituo hicho Ndugu Goshashy alisema kuwa ni pamoja na kutoa taarifa za matukio ya sumu, kuzuia ajali za kemikali na kuratibu matukio ya Sumu, uchunguzi na utambuzi wa sumu mbalimbali na kufanyatafiti mbalimbali zinazohusiana na kemikali na sumu.

Aidha Ndugu Goshashy alisema kuwa kituo hicho kina wajibu wa kuzitahadharisha mamlaka husika juu ya uwepo wa viashiria vya athari za sumu ili hayua stahiki ziweze kuchukuliwa kuzui athari hizo.

“Taarida za tahadharizinaweza kusaidia kuweka mfumo wa udhibiti na usimamiaji wa kemikali na sumu kuweka alama ya utambulisho au kuiondoa bidhaa sokoni” alisema Ndugu Goshashy.

Akizungumiza utoaji waelimu kwa umma kuhusu huduma zitolewazo na kituo hicho Ndugu Goshashy alisema kwamba wanaelimisha kuputia vyombo vya habari, kutoa namba za simu na kuchapisha vipeperushi na kuisambaza.

“Tunatoa ushauri kuhusiana na dawa za kulevya, jinsi ya kuyaepuka na kushauri aina sahihi za vifumbua sumu” aliongeza Ndugu Goshashy.

Aidha ndugu Goshashy aliwashauri wananchi kuepuka madhara yanayoweza kutokea na kutoa taarifa za matukio mbalimbali kama kula, kunywa au kuvuta.
Mratibu wa Kituo cha kuratibu matukio ya sumu nchini toka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw. Yohana Goshashy akiwalezea waandishi wa Habari kuhusu kuanzishwa kwa kituo cha KuratibuMatukio ya sumu hapa nchini ambacho ni sehemu ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.Baadhi ya waandishi wa Habariw akifuatilia mkutano wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Vyombo vya Habari uliofanyika leo Jijini Dar es salaam leo.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI

$
0
0
DSC_0063
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari leo. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini, Dkt. Rufaro Chatora.

Taarifa kwa umma, kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa kipindupindu hapa nchini ni kama ifuatavyo; Tangu ugonjwa huu uanze, jumla ya watu 13,491 wameugua Kipindupindu, na kati yao jumla ya watu 205 wameshafariki kwa ugonjwa huu.

Katika kipindi cha wiki iliyoanza tarehe 04 hadi 10 Januari 2016, kumekuwa na jumla ya wagonjwa 615 walioripotiwa nchini kote na vifo vitatu (3). Mikoa ambayo bado imeripoti kuwa na ugonjwa huu ndani ya wiki moja iliyopita ni 11 kati ya 21 iliyokuwa imeripoti ugonjwa hapa nchini. Mikoa hiyo ni pamoja na Morogoro, Arusha, Singida, Manyara, Pwani, Dodoma, Geita, Mara, Tanga, Mwanza na Simiyu. Kati ya hiyo, mikoa inayoongoza kwa kuripoti idadi kubwa ya wagonjwa wapya ndani ya wiki moja iliyopita ni pamoja na Morogoro (Manispaa ya Morogoro 87, Halmashauri ya Morogoro 66), ukifuatiwa na Arusha (Arusha Manispaa 50), Singida (Iramba 40) na Manispaa ya Dodoma ( 33).

Aidha, mikoa iliyokuwa na maambukizi lakini kwa muda wa wiki moja iliyopita hakukuwa na mgonjwa yoyote wa kipindupindu ni pamoja na Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma, Kagera, Lindi. Vile vile mkoa wa Dar es Salaam ambako ndiko ugonjwa ulianzia na kudumu kwa muda wa miezi minne (4) haujaripoti mgonjwa wa kipindupindu kuanzia tarehe 22/12/2015.
Mikoa ambayo ilikwisha kuwa na ugonjwa huo lakini hapajakuwepo na wagonjwa wowote kwa muda wa zaidi ya miezi miwili iliyopita ni pamoja na Shinyanga, Kilimanjaro na Iringa. Pia mikoa ambayo haijawahi kutoa taarifa ya ugonjwa wa kindupindu tangu mlipuko huu uanze hapa nchini ni Njombe, Ruvuma na Mtwara.

Bado Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, inaendelea kusisitiza kuwa, ili kudhibiti ugonjwa huo na kuokoa vifo vinavyotokana na ugonjwa huu, wananchi wanasisitizwa kunywa maji yaliyo safi na salama, kuepuka kula chakula kilichoandaliwa katika mazingira yasiyo safi na salama, kunawa mikono kwa sabuni na maji safi
yanayotiririka:-
-kabla na baada ya kula
- baada ya kutoka chooni
-baada ya kumnawisha mtoto aliyejisaidia
-baada ya kumhudumia mgonjwa
Aidha, jamii inaaswa kutumia vyoo wakati wote na kutokujisaidia ovyo katika vyanzo vya maji vya mito, maziwa na mabwawa.Hivyo, Mamlaka za Mikoa na Halmashauri pamoja na watendaji wake kote nchini zinaagizwa kuendeleza juhudi za kuzuia kusambaa kwa mlipuko pamoja na kuchukua hatua stahiki za tahadhari kwa kusimamia utekelezaji wa yafuatayo:
*Ushirikishwaji wa viongozi ngazi mbali mbali, hasa ngazi za Halmashauri kwa kushirikisha madiwani na viongozi wa kata, vijiji, na mitaa.

*Mamlaka husika kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama ikiwa ni pamoja na uwekaji wa dawa ya klorini kwenye maji na kupima usalama wa maji mara kwa mara.*Upatikanaji wa dawa za kutibu maji (Water Guard, Aqua Tabs) katika maeneo ya mlipuko.*Juhudi kubwa ziongezwe kuhakikisha upatikanaji na matumizi ya vyoo bora kwa kila kaya.
*Uelimishwaji wa Baba na Mama Lishe, na wauzaji wengine wa vyakula kuhusu kanuni za afya.

*Kusimamia utekelezwaji wa Sheria ya Afya ya Mazingira na Sheria ndogo ndogo (By-Laws).
*Uhamasishaji wa Wananchi wanaopata ugonjwa kuwahi kutumia maji ya chumvi chumvi (ORS) na kuripoti mapema katika vituo vya huduma.
*Uboreshwaji wa vituo vya kutolea huduma za afya.
Hitimisho
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, inawashukuru wadau wote wanaoshirikiana na Serikali katika harakati za kupambana na ugonjwa huu. Aidha, Wizara inaipongeza mikoa ambayo ilikuwa na ugonjwa na sasa umetoweka au kupungua kwa kiasi kikubwa na pia kuikumbusha mikoa ambayo bado haijaathirika kuchukua hatua za tahadhari za kuzuia ili isipate mgonjwa yeyote wa Kipindupindu.

WABUNGE 15 WATEULIWA KUWA WAJUMBE WA KAMATI YA KANUNI ZA BUNGE.

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 
BUNGE LA TANZANIA


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA WABUNGE
KWENYE KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE.
Katibu wa Bunge anatoa taarifa kwa umma kwamba:
(a) Kwa mujibu wa Kanuni ya 116 (3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Aprili, 2013, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano amepewa mamlaka ya kuteua Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge kwa namna ambayo itawezesha kila Mbunge kuwekwa kwenye Kamati mojawapo. Katika kufanya uteuzi huo, Spika huzingatia vigezo mbalimbali vilivyoainishwa katika Kanuni ya 116 (5);

(b) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Mhe. Job Yustino Ndugai (MB), ametekeleza mamlaka yake ya uteuzi kwa mujibu wa Kanuni tajwa hapo juu, kwa kuwateua kwanza Wabunge Kumi na Tano (15) kuwa Wajumbe wa Kamati ya Kanuni za Bunge. Kamati hiyo imeundwa na kutangazwa kabla ya Kamati zingine ili ifanye marekebisho ya Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge kuhusu majukumu ya Kamati zingine za Bunge kwa kuyashabihisha na majukumu ya Serikali kwa kuzingatia Muundo wa Baraza la Mawaziri lililopo sasa. Lengo kuu ni kuleta urahisi, ufanisi na tija kwa Bunge katika kuisimamia na kuishauri Serikali; 

(c) Kwa msingi huo, Kamati ya Kanuni za Kudumu za Bunge, ambayo Spika ndiye Mwenyekiti wake na Naibu Spika ni Makamu Mwenyekiti, Kiongozi wa Upinzani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao ni Wajumbe kwa nyadhifa zao itakutana katika Ofisi ya Bunge, Dar es Salaam siku ya Ijumaa tarehe 15 Januari, 2016 saa tano kamili asubuhi katika Ukumbi wa Spika. Wajumbe wengine ni: -
(i) Mhe. Makame Kassim Makame, MB. - Jimbo la Mwera;

(ii) Mhe. Tundu Antipas Mughwai Lissu, MB. - Jimbo la Singida Mashariki;

(iii) Mhe. Jasson Samson Rweikiza, MB. - Jimbo la Bukoba Vijijini;

(iv) Mhe. Ally Saleh Ally, MB. - Jimbo la Malindi; 

(v) Mhe. Magdalena Hamis Sakaya, MB. - Jimbo la Kaliua;

(vi) Mhe. Salome Wycliff Makamba, MB. - Viti Maalum;

(vii) Mhe. Dkt. Jasmine Tiisekwa Bunga, MB. - Viti Maalum;

(viii) Mhe. Zainab Athman Katimba, MB. - Viti Maalum;

(ix) Mhe. Balozi Adadi Mohamed Rajab, MB. - Jimbo la Muheza;

(x)Mhe. Dkt. Charles John Tizeba, MB. - Jimbo la Buchosa; na

(xi) Mhe. Kangi Alphaxard Lugola, MB. - Jimbo la Mwibara.

(d) Spika atakamilisha uteuzi wa Wajumbe katika Kamati zingine za Bunge kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Pili wa Bunge tarehe 26 Januari, 2016, Mjini Dodoma ili kutoa fursa kwa Kamati zote kuchagua Viongozi wake na kuandaa Mpango Kazi kwa mwaka 2016/17; na

(e) Wabunge wote wanatangaziwa kuwa wawe wamefika Dodoma tarehe 20 Januari, 2016 tayari kwa kuanza kwa Kamati za Bunge na Mkutano wa Bunge, isipokuwa Kamati ya Wabunge (Caucus) wote wa Chama cha Mapinduzi wanatakiwa kuwa Mjini Dodoma tarehe 17 Januari, 2016 kwa Mkutano wao.

Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,
Ofisi ya Bunge,
S. L. P. 9133,
DAR ES SALAAM.
11 Januari, 2016.

Pam D azindua Video yake ya Popo Lipopo Maisha Basement

$
0
0
PAM D (70)PAM D (71)Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini, Pamela Daffa akiwaburudisha mashabiki waliojitokeza kwenye uzinduzi wa video yake ya Popo Lipopo ndani ya Maisha Basement usiku wa kuamkia leo.
PAM D (72)PAM D (73)Pam D akifanya yake na Mesen Selekta.
PAM D (74)PAM D (75)Pam D (mwenye kipaza sauti) akichana freestyle mbele ya mashabiki wake.
PAM D (64)Madensa wa Pam D wakiendelea kufanya yao.
PAM D (69)Pam D akicheza na Madensa wake.PAM D (50)Msanii na Mtayarishaji wa muziki wa Bongo Fleva, Mensen Selekta akifanya yake.
PAM D (53)
PAM D (49)...Mashabiki wakiendelea kujiachia.
PAM D (38)PAM D (59)...Wakiendelea kujiachia.
Usiku wa kuamkia leo, staa wa muziki wa Bongo Fleva, Pamela Daffa 'Pam D' kwa kushirikiana na mtayarishaji na mwanamuziki hatari Bongo, Mesen Selekta walikinukisha vya kutosha ndani ya Ukumbi wa Maisha Basement uliopo Kijitonyama jijini Dar.

Usiku huo uliotawaliwa na redcarpet ya hatari ambapo mashabiki kibao walipata nafasi ya kupiga picha na Pam sambamba na kuzungumza naye mawili-matatu, ulianza kwa kwa Mesen kupanda na kundi zima la Team Selekta ambapo alipopanda Mesen aliwapagawisha vilivyo na ngoma zake zote kali kama vile Kanyaboya, Sweetlove, Team Selekta pamoja na wimbo wake mpya wa Love Me.

Shangwe zilizidi pale walipopanda madensa wa PAm D kwa sarakasi kibao na madoido ambapo Pam alitokelezea na kuanza kuvurumusha nyimbo zake zote kali kuanzia Nimempata kisha akamalizia na Popo Lipopo ambapo mashabiki walipata fursa ya kuuona kwa mara nyingine live ukumbini hapo.
(PICHA: MUSA MATEJA/GPL)

ZIARA YA MKURUGENZI WA MAUZO NA MASOKO WA NHC LINDI, MTWARA NA RUVUMA

$
0
0
Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Lindi Patrick Mussa Kamendu akimpa taarifa ya hali ya mauzo na masoko na utekelezaji wa miradi ya shirika la nyumba la taifa katika mkoa wake kwa Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa katika ziara ya NHC mkoa wa Lindi kufuatilia utekelezaji wa miradi hiyo mikoani.
Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Lindi Patrick Mussa Kamendu akiongozana na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa kwenye mradi wa nyumba za gharama nafuu Mtanda Lindi, katika ziara ya NHC mkoa wa Lindi kufuatilia utekelezaji wa miradi hiyo mikoani.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa akishuhudia jambo katika mojawapo ya nyumba za gharama nafuu za Mtanda, Lindi kwenye mradi wa nyumba za gharama nafuu Mtanda Lindi.
Nyumba za gharama nafuu za NHC Mtanda, Lindi linavyoonekana katika picha.
Nyumba za gharama nafuu za Mtanda, Lindi linavyoonekana katika picha.
Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Lindi Patrick Mussa Kamendu akimweleza jambo Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa kwenye ziara ya mradi wa nyumba za gharama nafuu Mtanda Lindi.
Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Mtwara, Joseph John akimpa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya shirika la nyumba la taifa katika mkoa wake kwa Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa katika ziara ya NHC mkoa wa Mtwara kufuatilia utekelezaji wa miradi hiyo mikoani.
Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Mtwara, Joseph John akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa kwenye mradi wa nyumba za makazi Shangani Mtwara, katika ziara ya NHC mkoa wa Mtwara kufuatilia utekelezaji wa miradi hiyo mikoani.
Nyumba za makazi za Rahaleo Mtwara zinavyoonekana katika picha hivi sasa.
Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Mtwara, Joseph John akimweleza jambo Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa kwenye ziara ya mradi wa nyumba za gharama nafuu Napupa, Masasi.
Nyumba za gharama nafuu NHC Napupa, Masasi, Mtwara zinavyoonekana kwa sasa.
Nyumba za gharama nafuu NHC Mkuzo Songea zinavyoonekana kwa sasa.
Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Ruvuma, Saidi Bungara akiongozana na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa kwenye ziara ya mradi wa nyumba za gharama nafuu Mkuzo, Songea.
Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Ruvuma, Saidi Bungara akimwelekeza jambo Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa kwenye ziara ya mradi wa nyumba za gharama nafuu Mkuzo, Songea.

Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Ruvuma, Saidi Bungara akiongozana na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa kwenye ziara ya mradi wa nyumba za gharama nafuu Mkuzo, Songea.

KIWIA AONDOA KESI YA KUPINGA MATOKEO YA UBUNGE JIMBO LA ILEMELA BAADA YA KUSHINDWA KULIPA GHARAMA ZA MAHAKAMA.

$
0
0

Mutabanzi Julius Lugaziya ambae ni Mwanasheria Mwandamizi aliekuwa akimtetea Angelina Mabula akihojiwa na Wanahabari nje ya Mahakama
Mutabanzi Julius Lugaziya ambae ni Mwanasheria Mwandamizi aliekuwa akimtetea Angelina Mabula akihojiwa na Wanahabari nje ya Mahakama
Katibu wa Mbunge wa Ilemela Kheri James (mwenye miwani) akiwa katika mahojiano na wanahabari nje ya Mahakama.

Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imetupilia mbali kesi ya Kupinga Matokeo ya ubunge katika Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza, iliyofunguliwa na aliekuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Haighness Kiwia.

Katika kesi hiyo ambayo ni namba mbili ya mwaka 2015 iliyofunguliwa Novemba 25 mwaka jana, Kiwia alikuwa akipinga ushindi wa mbunge wa Jimbo la Ilemela Angelina Mabula kupitia Chama cha Mapinduzi CCM kutokana na madai ambayo ni pamoja na kuendesha kampeni za ubaguzi wa kikabila sanjari na kupata kura ambazo hazikuendana na idadi ya wapiga kura walioandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura. 

Kesi hiyo imefutwa baada ya Kiwia kupitia kwa mwanasheria wake Paul Kipeja kuiomba Mahakama kufuta kesi hiyo kwa madai ya kwamba mteja wake ameshindwa kulipia gharama za Mahakama ambazo ni Shilingi Milioni 10 na kwamba washtakiwa walikuwa ni Angelina Mabula pamoja na Mwanasheria wa Serikali ambapo gharama ya kufungua kesi hiyo kwa kila mlalamikiwa ilikuwa ni shilingi Milioni Tano.



Kufuatia ombi hilo, Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Eugenia Gerald Rujwauka alitoa maamuzi ya kuifuta kesi hiyo kama ambavyo mlalamikaji alivyoomba.

Baada ya kesi hiyo kufutwa, Mutabanzi Julius Lugaziya ambae ni Mwanasheria Mwandamizi aliekuwa akimtetea mlalamikiwa, amebainisha kuwa baada ya maamuzi hayo anatarajia kukutana na mteja wake ili kujadiliana hatua za kuchukua na huenda akafungua kesi ya madai dhidi ya Kiwia kutokana na kufungua kesi na kisha kuiondoa mwenyewe na hivyo kumuingiza mteja wake katika gharama zisizo za lazima.


Ifahamike kwamba Angelina Mabula pamoja na Highness Kiwia hawakuhudhuria Mahakamani hapo na hakukuwa na wafuasi wengi wa vyama vya siasa kama ilivyozoeleka ambapo nje ya Mahakama hiyo, Agrey Laban ambae ni Katibu wa Kiwia ameilalamikia Mahakama kutokana na kushindwa kupunguza gharama za kesi hiyo jambo ambalo limepelekea haki kupotea.






Wakati hali ikiwa hivyo, Kheri James ambae ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Angelina Mabula, amepongeza maamuzi ya kesi hiyo kufutwa na kuongeza kuwa hatua hiyo inatoa wigo wa mbunge huyo kuwatumikia wananchi.

Akiwa ofisini kwake, Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akapata fursa ya kuzungumzia Maamuzi ya Mahakama juu ya kesi hiyo ambapo amempongeza Mabula kwa uvumilivu wake kwa kuwa kiongozi akiwa na kesi Mahakamani anakosa uimara wa kuwatumikia wananchi.

Katika uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25 mwaka jana, Angelina Mabula (CCM) aliibuka mbunge wa Jimbo la Ilemela kwa kupata ushindi wa kura 85,425 na hivyo kumshinda mpinzani wake wakaribu kutoka Chadema Highness Kiwia aliekuwa akitetea jimbo hilo ambae alipata kura 61,679.

WanaCCM wakieleza namna walivyopokea maamuzi ya Mahakama.
WanaCCM wakieleza namna walivyopokea maamuzi ya Mahakama
WanaCCM wakieleza namna walivyopokea maamuzi ya Mahakama
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akieleza namna alivyopokea maamuzi ya Mahakama.
Agrey Laban ambae ni Katibu wa Highness Kiwia akizungumza na Wanahabari nje ya Mahakama.

WAZIRI MAKAME MBARAWA AFANYA ZIARA kitengo cha huduma ya Makontena Bandarini (TICTS)

$
0
0
RA1
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Profesa Makame Mbarawa akipokea taarifa ya Utendaji kutoka kwa Mkurugenzi wa Biashara na Maendeleo wa kitengo cha huduma ya Makontena Bandarini (TICTS) Bw.Donald Talawa mara alipofanya ziara ya kukagua utendaji wa kitengo hicho Jijini Dar es salaam.
RA2
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Viongozi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) na TICTS ambapo amehimiza kuhusu hutoaji wa huduma kwa haraka ili kuongeza ukusanyaji wa mapato,Kulia ni Hebel Mhanga na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bwana Aloyce Matei.
RA3
Mtaalamu wa Uratibu wa huduma za upakuaji wa TICTS akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Mbarawa (Wa tatu kushoto) jinsi ya mfumo wa kupokea na kupakua Makontena unavyfanya kazi.
RA4
Wafanyakazi wa TICTS wakiendelea na utekelezaji wa majukumu yao ya kupokea na kuruhusu makontena.

MKURUGENZI WA MAUZO NA MASOKO WA NHC AFANYA ZIARA LINDI, MTWARA NA RUVUMA

$
0
0
 
 Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Lindi Patrick Mussa Kamendu akimpa taarifa ya hali ya mauzo na masoko na utekelezaji wa miradi ya shirika la nyumba la taifa katika mkoa wake kwa Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa katika ziara ya NHC mkoa wa Lindi kufuatilia utekelezaji wa miradi hiyo mikoani.
Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Lindi Patrick Mussa Kamendu akiongozana na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa kwenye mradi wa nyumba za gharama nafuu Mtanda Lindi, katika ziara ya NHC mkoa wa Lindi kufuatilia utekelezaji wa miradi hiyo mikoani.
 Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa akishuhudia jambo katika mojawapo ya nyumba za gharama nafuu za Mtanda, Lindi kwenye mradi wa nyumba za gharama nafuu Mtanda Lindi.
 Nyumba za gharama nafuu za NHC Mtanda, Lindi linavyoonekana katika picha.

  Nyumba za gharama nafuu za Mtanda, Lindi linavyoonekana katika picha.
Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Lindi Patrick Mussa Kamendu akimweleza jambo Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa kwenye ziara ya mradi wa nyumba za gharama nafuu Mtanda Lindi.

  Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Mtwara, Joseph John akimpa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya shirika la nyumba la taifa katika mkoa wake kwa Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa katika ziara ya NHC mkoa wa Mtwara kufuatilia utekelezaji wa miradi hiyo mikoani.
 Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Mtwara, Joseph John akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa kwenye mradi wa nyumba za makazi Shangani Mtwara, katika ziara ya NHC mkoa wa Mtwara kufuatilia utekelezaji wa miradi hiyo mikoani.
 Nyumba za makazi za Rahaleo Mtwara zinavyoonekana katika picha hivi sasa.
 Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Mtwara, Joseph John akimweleza jambo Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa kwenye ziara ya mradi wa nyumba za gharama nafuu Napupa, Masasi.
Nyumba za gharama nafuu NHC Napupa, Masasi, Mtwara zinavyoonekana kwa sasa.
 Nyumba za gharama nafuu NHC Mkuzo Songea zinavyoonekana kwa sasa.
Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Ruvuma, Saidi Bungara akiongozana na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa kwenye ziara ya mradi wa nyumba za gharama nafuu Mkuzo, Songea.
 Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Ruvuma, Saidi Bungara akimwelekeza jambo Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa kwenye ziara ya mradi wa nyumba za gharama nafuu Mkuzo, Songea.
Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Ruvuma, Saidi Bungara akiongozana na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa kwenye ziara ya mradi wa nyumba za gharama nafuu Mkuzo, Songea.

The African Best Player Mbwana Samatta visited Belgium Embassy today

$
0
0
SAM1
The African Best Player Mbwana Ally Samatta 2015/16 (for those who play local league in Africa) visited Belgium Embassy for courtesy call visit and obtaining the visa to join KRC Genki in Belgium. He is real focused, talented and determined Tanzanian soccer player. We wish him all the best in his new venture. Go go Samatta
SAM2SAM3

Tume ya Taifa ya Uchaguzi yapitia vipaumbele vyake bajeti ya mwaka 2016/2017

$
0
0
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani akitoa mada kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Ramadhan Kailima.
………….
Na Mwandishi-NEC
Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanza kupitia vipaumbele kwa ajili ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017.Katika kikao chake cha Menejimenti kilichofanyika leo Januari 11, 2016, baadhi ya vipaumbele vinavyoendelea kujadiliwa ni uhuishaji wa Sheria mbalimbali zinazosimamia masuala ya uchaguzi, Elimu ya Mpiga Kura, na ujenzi wa ofisi ya Tume.

Vipaumbele vingine vinavyojadiliwa ni pamoja na miongozo na mifumo ya ufuatiliaji na tathmini, mifumo ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na mifumo ya uendeshaji wa Uchaguzi.

Tume imeanza mandalizi haya ili kujipanga vema ili mwongozo wa Bajeti utakapotoka, Menejimenti ya NEC iwe imekamilisha hatua zote za awali na kusubiri kuwasilisha katika ngazi husika.

Huu ni utaratibu mpya ulioanzishwa na Tume ya Uchaguzi ili kuhakikisha masuala yote muhimu yanakuwepo katika uandaaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/2017.

Vikao hivi vya Menejimenti ya Tume ni vikao vya kawaida vinavyofanyika kila Jumatatu kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa kila Idara na kujipanga kwa utekelezaji wa wiki inayoanza. 

MRADI WA MAJI SAFI WAKAMILIKA KIJIJI CHA KINDUNI WILAYA KASKAZINI “B” UNGUJA WAKAMILIKA

$
0
0
????????????????????????????????????
Na Khadija Khamis –Maelezo 
Zaidi ya shilingi million 73 za Kitanzania zimetumika kwa ajili ya kufanikisha  mradi wa maji  safi na salama katika kijiji cha kinduni wilaya ya kaskazini B Unguja ambapo zaidi ya wananchi 5582 watafaidika na mradi huo.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Makaazi Maji na Nishati Ali Khalili Mirza ameeleza hayo mbele ya Waziri wa Kilimo na Maliasili Mhe.Dkt. Sira Ubwa Mamboya wakati wa  uzinduzi wa mradi wa maji  safi Kinduni ikiwa ni muendelezo wa shamrashamra za Sherehe ya Miaka 52 ya Mapinduzi Zanzibar .

Alisema fedha zilizotumika kwa kufanikisha mradi huo ni nyingi  hivyo iko haja kwa wananchi kuhakikisha wanalinda na kuenzi rasilimali hiyo ili iwe chachu ya kuleta maendeleo katika kijiji hicho na vijiji  vya karibu ambavyo vitafaidika na huduma  hiyo . Waziri wa Kilimo aliwataka wananchi wa vijiji hivyo  kujenga  mashirikiano katika kulinda na kutunza vianziao vya maji ili viweze kudumu kwa muda mrefu na kuondondosha  usumbufu wa tatizo hilo .

“Tone  moja la maji ni gharama  hivyo tunapaswa kuongeza ushirikiano  katika kulinda, kutunza na kudumisha rasilimali hiyo tuliopewa,“ Alisema Dkt. Sira .Hata hiyo Waziri Mamboya aliwataka wananchi kuchangia  huduma hiyo   ili kukabiliana na gharama ndogo ndogo za uchakavu wa vifaa   na kurahisisha kufanyiwa  matengenezo  haraka iwezekanavyo.

Aliwashukuru wahisani  ambao wameunga mkono juhudi za Serikali katika kufanikisha mradi huo wakiwemo  Raas Alkheima, Viongozi mbali mbali  na wananchi. Amezitaja Skuli zilizofanya vibaya  kitaifa kwa  kidato cha pili ni Mfurumatonga, Uzi, na Mchangani, skuli ya Chambani, Kandwi , Mwambe shamiani, Mfurumatonga, Chambani na Mahonda wamefanya vibaya darasa la sita na saba .Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali amesema katika mitihani hiyo kesi nne za udanganyifu zilijitokeza zote kwa wanafunzi wa darasa la  sita.

Aliwataja wanafunzi waliofanya vizuri zaidi  kidato cha pili ni Philip William Panduka kutoka Skuli ya Mikunguni, darasa la saba ni Farid Ali Hamad kutoka Ziwani na darasa la sita ni Seif Khamis Nassor kutoka Skuli ya Madungu ‘A’.

Waziri Shamhuna  amewataka wazazi na walezi wa wanafunzi ambao hawakufaulu mitihani hiyo kutovunjika moyo na badala yake amewashauri kuwapeleka vituo vya kujiendeleza. Waziri huyo wa Elimu ameahidi kufanya utafiti na kuzifuatilia skuli zilivyofanya vibaya ili kuweza kufahamu  tatizo  na kulitafutia  ufumbuzi unaofaa.

Mbwana Samatta akutana na Mufti Mkuu Sheikh Zuberi

$
0
0
 Mwanasoka Bora Afrika Ndg. Mbwana Samatta akikabidhiwa baadhi ya zawadi mbalimbali na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir katika ofisi kuu za Bakwata zilizopo Kinondoni Jijini Dar Es Salaam. 
Leo tarehe 11 January 2016, Mwanasoka Bora Afrika Ndg. Mbwana Samatta alimtembelea Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir katika ofisi kuu za Bakwata zilizopo Kinondoni Jijini Dar Es Salaam.

Mufti Mkuu mbali na kumpatia zawadi mbalimbali kwa ajili ya kumsaidia katika imani yake pia alipata nafasi ya kumuombea dua ya mafanikio zaidi huko aendako Ulaya na kumpa nasaha asisahau kumuomba Mwenyezi Mungu kila wakati na kufanya ibada muda wote atakaokuwa nje ya mazoezi. 

Mwisho Mufti alimtakia mafanikio mema na kumuambia dua za watanzania wote zipo naye.

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA YAONGEZEKA TANZANIA

$
0
0
 Wakazi wa Arusha wakiwasikiliza waelimishaji wa magonjwa yasiyoambukiza kutoka Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukizwa (TANCDA)jana katika hospitali ya mkoa wa Mount Meru ambapo shughuli za upimaji wa magonjwa ya moyo,kisukari na saratani yalifanyika bure kwa wananchi wote.
Mtaalamu wa masuala ya Afya kutoka akipima mzunguko wa damu  Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukizwa (TANCDA)jana katika hospitali ya mkoa wa Mount Meru ambapo shughuli za upimaji wa magonjwa ya moyo,kisukari na saratani yalifanyika bure kwa wananchi wote

Na Woinde Shizza,Arusha
Kutokana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo magonjwa ya moyo ,kisukari na saratani ,Watanzania wameaswa kuzingatia lishe bora na mtindo bora wa maisha ili kuepuka magonjwa  hayo ambayo husababishwa na mtindo mbaya wa maisha pamoja unywaji pombe,uvutaji sigara na ulaji uisiofaa.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukizwa (TANCDA) ,Dokta Tatizo Waane alisema kuwa kumekua na ongezeko kubwa la watu wenye magonjwa  hao kitaifa ambapo ugonjwa wa moyo asilimia 26% ugonjwa wa kisukari umeongezeka kwa Asilimia  9.6.

Akizungumza katika zoezi la upimaji na utoaji elimu kwa wananchi juu ya magonjwa hayo ,Dr.Waane amesema kuwa magonjwa ya moyo yameongezeka kwa asilimia 10 hivyo Watanzania hawana budi kuangalia hali yao ya lishe na kuzingatia kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa yasiyo ya lazima.

"Watu wengi wamekua hawatilii maanani magonjwa yasiyoambukiza lakini yana athari kubwa kiafya na kwenye uchumi wa watu kwani hutumia muda mrefu na fedha nyingi kutibu" Alisema Dokta Waane

Mratibu wa zoezi la upimaji wa  magonjwa hayo kwa mkoa wa Arusha Dokta David Shungu  alisema kuwa wananchi wanapaswa kupatiwa elimu kwani magonjwa hayo yanaongoza kwa kusababisha vifo sawa na magonjwa yanayoambukiza.

Kwa upande wake Mkazi wa Arusha aliyejitokeza kupima afya yake na kupata ushauri Tunu Ndege alisema kuwa zoezi hilo litawasaidia wananchi wengi kujua afya zao na kuchukua hatua kulinda afya zao dhidi ya magonjwa ,pia ameshauri huduma hiyo ya upimaji iwafikie watu wa vijijini wanaoteseka na magonjwa bila kujua.

Alisema Mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza ya moyo,sukari na saratani yanapaswa kutiliwa mkazo kwa kutoa elimu na tiba kwa wananchi kwani magonjwa hayo hudumu kwa muda mrefu na kusababisha hasara ya kijamii na kiuchumi hata kupelekea vifo na ulemavu.


Airtel Fursa Msimu wa 2 wazinduliwa, kuendelea kuinua maisha ya watanzania wengi zaidi

$
0
0
 Naibu waziri  Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde ( wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw, Sunil Colaso,akifatiwa na Mshauri wa Airtel Fursa, Eng George Mulamula kwa pamoja wakionyesha bango kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Airtel Fursa msimu wa pili. Akishuhudia (kushoto) ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano Mallya.
 Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw, Sunil Colaso akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa 2. mradi unaowawezesha vijana kati ya miaka 18 hadi 24
kupata fursa za kuinua biashara zao, uliyozinduliwa Naibu waziri Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde  katika ofisi ya Airtel makao makuu Jijini Dar es saalam
 Naibu waziri  Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa 2 mradi unaowawezesha vijana kati ya miaka 18 hadi 24  kupata fursa za kuinua
biashara zao. Uzinduzi huo ulifanyika katika ofisi ya Airtel makao makuu Jijini Dar es saalam
 Kijana aliyewezesha kupitia mradi wa Airtel FURSA msimu wa 1, Mohamed Kigumi akipongezwa na  Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw, Sunil Colaso kwa kufanya vizuri katika biashara yake wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa mradi wa Airtel FURSA , mradi wenye lengo la kuwawezesha vijana kufikia malengo yao na kukuza biashara zao. Wakishuhudia (kushoto) ni Naibu waziri  Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde  akifatiwa na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano Mallya. (kulia) ni Mshauri wa Airtel Fursa, Eng George Mulamula
 Mshauri wa Airtel Fursa, Eng George Mulamula akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa pili
 Wageni waalikwa na waandishi wa habari wakifatilia uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa pili uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel Morocco jijini Dar es Saalam 


Naibu waziri  Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde  akiteta jambo na  Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano Mallya wakati wa uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa pili.
 

  *   zaidi ya shilingi billion 1 kusaidia  miradi ya kuwawezehsha vijana llings
 Kampuni ya simu ya mkononi
ya Airtel leo imezindua msimu wa pili wa mradi wake wa kuwawezesha
vijana ujulikanao kama "Airtel FURSA" kwa lengo kuendelea kudhihirisha
kutimiza dhamira yake kuendeleza huduma za kijamii nchini
Mradi wa "Airtel FURSA" ulizinduliwa Mei 2015, ukiwa na lengo la
kuwawezesha vijana kwa kuwapatia mbinu mbalimbali za biashara na vifaa
vitakavyowawezesha kukuza biashara zao

Msimu wa kwanza wa "Airtel FURSA"  umewawezesha vijana zaidi ya 2500
wenye umri kati ya miaka 18 hadi 24 kupata mafunzo ya biashara na
wengine 13 wafanyabiashara chipukizi wanaofanya vizuri zaidi kupokea
vifaa vilikvyowasaidi kuboresha biashara zao na kutengeneza fursa
zaidi kwa jamii inayowazunguka.

Akiongea wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw, Sunil
Colaso, alisisistiza dhamira ya kampuni yake  kuwawezesha vijana na
kutambua mchango walio nao katika kuendesha uchumi wa Tanzania
" Mradi huu wa "Airtel FURSA"   unadhihirisha dhamira yetu ya
kuwawezesha vijana wa kitanzania wenye malengo ya kuinua maisha yao na
kutimiza ndoto zao. Msimu wa kwanza wa "Airtel FURSA" umetoa matokeo
mazuri sana na  tumefanikiwa  kugusa maisha ya  maelfu ya vijana wengi
kutoka katika mikoa mbalimbali nchini,"

"Katika msimu huu wa pili tunawekeza takribani  shilingi  billion moja
ili  kuweza kufikia vijana wengi zaidi ambao wako tayari kutumia fursa
na vipaji vyao. Tutaendelea kuwapatia mafunzo ya kibiashara, misaada
ya vifaa na kuanzisha mfumo wakisasa wa mafunzo kupitia simu zao za
mkononi" alisema Colaso.

Akizindua rasmi mradi wa "Airtel FURSA" Naibu waziri  Wizara ya Kazi
Vijana na Ajira Anthony Mavunde aliwapongeza Airtel kwa kuanzisha  na
kuwekeza kwenye mradi huu mkubwa na kutoa wito kwa vijana kutumia
fursa hii ili kuboresha maisha yao. alisema Mh Mavunde
"Nchi yetu ya Tanzania imebarikiwa kwa kuwa na rasilimali,
zikiunganishwa pamoja na fulsa zinazoletwa na miradi kama hii ya
"Airtel FURSA" ni wazi vijana wenye malengo Dhahiri ya kujiendeleza
wataweza kuboresha maisha yao. Napenda kuwahasa vijana wetu kutumia
fursa hii na kufanya kazi kwa bidii:"

"Serikali chini ya Wizara yetu na itaendelea kushirikia Airtel na
kufanya kazi kwa pamoja huku ikiweka mazingira bora yatakayochochea
vijeza ana kupata fursa ili waweze kuchangia katika kuendeleza  uchumi
wa nchi" aliongeza Mavunde

"Airtel FURSA"  ni mradi endelevu unaowalenga vijana nchi nzima kwa
kuwapatia vifaa  ,mafunzo ya biashara na mafunzo mbalimbali kupitia
mtandao ili kufikia malengo yao. Kutuma maombi tuma ujumbe mfupi
kwenda namba 15626 ikiwa na taarifa zifatazo Jina, umri, aina ya
biashara unayoifanya, mahali na namba za simu. Unaweza pia kutuma
maombi yako kwa kupitia barua pepe ya
airtelfursa@tz.airtel.com<
mailto:airtelfursa@tz.airtel.com>. Or
tembelea tovuti yetu ya  www.airtel.com<http://www.airtel.com>  na
ujaze fomu yako ya maombi

CUBA YAENDELEA KUSAIDIA TANZANIA KUPAMBANA NA MALARIA

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini, Bwana Jorge Luis Lopez Tormo ambaye ameahidi kuendelea kusaidia Tanzania katika mapambano dhidi ya malaria.

Akizungumza na Balozi  Tormo leo ,ofisini kwake ,Magogoni jijini Dar es salaa, Waziri Mkuu amemshukuru Balozi huyo, kwa Serikali ya Cuba kuendelea kusaidia Tanzania katika  mapambano  dhidi malaria  kwa kusaidia ujenzi wa kiwanda cha  kwanza Afrika cha  viuadudu vya kuua viluwiluwi wa mbu wanaoeneza ugonjwa wa malaria kilichopo, Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani kinachosimamamiwa na Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC).

 “Nawashukuru sana kwa namna mnavyosaidia kupambana na malaria, kupitia mradi huo mkubwa Afrika ambao unalenga kumaliza ugonjwa wa malaria,unaosababisha idadi kubwa ya vifo katika nchi yetu.” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Pia, ametumia fursa hiyo kuwakaribisha  raia wa Cuba kuja kuwekeza nchini hasa   katika  teknolojia. Na ameahidi kuendeleza uhusiano mwema ulipo baina ya nchi hizi mbili.

Waziri  Mkuu ameendelea kwa kusema kuwa Cuba ni nchi  iliyoendelea katika biashara, viwanda na uwekezaji  na imefanikiwa  kutoa bure huduma za kijamii ikiwemo afya, hivyo Serikali ya Tanzania haina budi kujifunza kutoka kwao ili kutimiza azma yake ya kutoa bure huduma mbalimbali za kijamii kama ambavyo sasa  inatolewa elimu bure.

 Kwa upande wake, Balozi Tormo   amesema kuwa pamoja na Serikali ya Cuba kusaidia kutoa wataalamu katika kujenga kiwanda hicho cha   viuadudu vya kuua viluwiluwi wa mbu wanaoeneza ugonjwa wa malaria ambao utanufaisha pia nchi za jirani siku za usoni, wanapenda  kuendeleza ushirikiano na Tanzania katika kuzalisha wataalamu kupitia programu mbalimbali  ikiwemo afya na elimu. Mfano progamu inayoendelea ya kubadilishana  wataalamu katika kitivo cha madawa cha Chuo Kikuu Cha Zanzibari (SUZA).

“Tunaweza kuendeleza program za kujifunza lugha ya Kiswahili, kama hapo awali, hii ni njia nzuri na muhimu ya kuendeleza uhusiano wetu na watu kuelewa lugha zetu”, alisema Balozi Tormo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P 3021,
11410 DAR ES SALAAM
IJUMAA, JANUARI 11, 2016.

NGOMA AFRICA BAND AKA FFU INAWATAKIENI HERI YA MIAKA 52 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

$
0
0
 Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni inawatakieni heri ya kuazimisha miaka 52 ya  mapinduzi ya Zanzibar,Mapinduzi yaliyofanyika 12 January 1964 ambayo yaliwakomboa wananchi wanyonge wazanzibarwalikuwa chini ya utawala wa Kisultan,Mapinduzi hayo ya tarehe 12 January 1964yaliyomfanya Sultan kuikimbia Zanzibar na kusahau kiremba kitandani.
 
Mungu yabariki mapinduzi,Mungu wabariki Wanzibari na kuhudumisha amani na upendo daima,Mungu ibariki Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Tusherehekee Mapinduzi day burudani www.ngoma-africa.com.

RAIS DKT. MAGUFULI AWAFARIJI FAMILIA YA NYERERE.

$
0
0
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mama Maria Nyerere, Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na wanafamilia  alipokwenda nyumbani kwake Msasani kumfariji kufuatia kifo cha mkwe wake Marehemu Leticia Nyerere huko Maryland, Marekani. 
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimfariji  na Mama Maria Nyerere, Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,na wanafamilia  alipokwenda nyumbani kwake Msasani kumfariji kufuatia kifo cha mkwe wake Marehemu Leticia Nyerere huko Maryland, Marekani. 
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Mama Maria Nyerere, Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na wanafamilia alipokwenda nyumbani kwake Msasani kumfariji kufuatia kifo cha mkwe wake Marehemu Leticia Nyerere huko Maryland, Marekani.

RAIS MAGUFULI AMJULIA HALI WAZIRI MKUU MSTAAFU SUMAYE ALIYELAZWA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI LEO

$
0
0
  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Freredick Sumaye na Mama Esther Sumaye alipokwenda kumjulia hali katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Jumatatu Januari 11, 2016
su1:Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Freredick Sumaye alipokwenda kumjulia hali katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Jumatatu Januari 11, 2016
PICHA NA IKULU.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images