Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

WATUMISHI WA KADA ZA AFYA NCHINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUFUATA MAADILI NA VIAPO VYA TAALUMA ZAO

$
0
0
IMG-20160105-WA0026
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akimjulia hali mama aliyejifungua kwenye wodi ya wazazi hospitali teule ya rufaa ya mkoa wa Geita.(Picha Zote na Catherine Sungura WAMJW-GEITA).
IMG-20160105-WA0030
Wauguzi wa wodi ya akinamama katika hospitali teule ya mkoa wa Geita.
IMG-20160105-WA0029
Tabibu wa kituo cha afya Nyankumbu, Abdallah Kiroboto akimsikiliza Waziri Ummy mara alipoingia kwenye chumba cha kutolea huduma, pembeni ni mama aliyefika kituoni hapo na watoto wake kupata matibabu.
IMG-20160105-WA0031
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwlimu akisalimiana na wagonjwa kwenye kituo cha afya Nyankumbu mkoani Geita alipotembelea kituo hicho.
IMG-20160105-WA0028
Wagonjwa waliofika hospitalini hapo wakisubiri huduma kwenye hospitali hiyo.
IMG-20160105-WA0027
Mganga mfawidhi wa hospitali teule ya mkoa wa Geita, Dkt. Adam Sijaona (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu mara baada ya kutembelea hospitali hiyo.

mapokezi ya Katibu Mkuu Mpya Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano katika sekta ya Mawasiliano Prof. Faustine Kamuzora

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano upande wa sekta ya Mawasiliano Prof Faustine Kamuzora wa pili kulia akipokea nyaraka wakati wa makabidhiano ya ofisi kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Dkt Yamungu Kayandabila wa kwanza kutoka kulia.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano katika sekta ya Mawasiliano Mary Sassabo kulia wakati akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Faustine Kamuzora ( hayupo pichani) na kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na rasilimali watu Bi Selina Lyimo.
 Baadhi ya Watumishi  wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano katika Sekta ya Mawasiliano wakimsikiliza Katibu Mkuu wao  mpya Prof. Faustine Kamuzora hayupo pichani. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano katika sekta ya Mawasiliano Prof. Faustine Kamuzora akizungumza na manajimenti ya sekta ya Mawasiliano (hawapo pichani).

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROF. SOSPETER MUHONGO AKUTANA NA KAMPUNI YA MTIBWA SUGAR ESTATES LTD

$
0
0
 Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo (mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na kampuni ya Mtibwa Sugar Estates Ltd.   Profesa Muhongo aliitaka kampuni hiyo  kuwekeza kwenye uzalishaji wa umeme ili kukidhi mahitaji yake zaidi.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini -  Madini,  Prof. James Mdoe (kushoto) na Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini – Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Palangyo (kulia) wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtibwa Sugar Estates Ltd, Nassor Seif (hayupo pichani)
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mtibwa Sugar Estates Ltd, Nassor Seif akielezea shughuli zinazofanywa na kampuni ya Mtibwa Sugar Estate Ltd.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba akisisitiza jambo katika kikao hicho.

RAIS MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABALOZI WA UMOJA WA JAMHURI YA KOREA, UMOJA WA ULAYA NA PALESTINA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea Hati za Utambulisho za Mhe. Song Geum-young, Balozi wa Jamhuri ya Korea Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 5, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Mhe. Song Geum-young, Balozi wa Jamhuri ya Korea Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 5, 2016 baada ya kupokea hati zake za utambulisho
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Mhe. Song Geum-young, Balozi wa Jamhuri ya Korea Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 5, 2016 baada ya kupokea hati zake za utambulisho
 Balozi wa Jamhuri ya Korea Mhe. Song Geum-young  na Maafisa wa Ikulu na wa Wizara ya Mambo za nje wakisimama wakati nyimbo za Taifa zikipigwa
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) hapa nchini Mhe. Roeland Van de Greer  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 5, 2016

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Balozi wa Jumuiya ya Ulaya hapa nchini Mhe. Roeland Van de Greer  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 5, 2016 baada ya kupokea hati zake za utambulisho
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Balozi wa Jumuiya ya Ulaya hapa nchini Mhe. Roeland Van de Greer  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 5, 2016 baada ya kupokea hati zake za utambulisho
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Balozi wa Jumuiya ya Ulaya hapa nchini Mhe. Roeland Van de Greer  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 5, 2016 baada ya kupokea hati zake za utambulisho
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Palestina hapa nchini Mhe. Hazem M. Shabat Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 5, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli baada ya kupokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Palestina hapa nchini Mhe. Hazem M. Shabat alifanya naye mazungumzo  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 5, 2016.PICHA NA IKULU

DKT. MWAKYEMBE ATEMBELEA OFISI YA MKURUGENZI WA MASHTAKA (DPP)

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt, Harrison Mwakyembe (kulia) akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Sheria ikiwemo majumuisho ya ziara yake aliyoifanya hivi karibuni. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Sifuni Mchome pamoja na Naibu Katibu Mkuu wake Bwana Amon Mpanju, leo 5 Januari, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa mashtaka Biswalo Mganga akieleza mbele ya Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Harrison Mwakyembe (kushoto) pamoja na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) moja ya kazi walizozifanya ikiwemo kuwashataki waliopatikana na hatia ya madawa ya kulevya pamoja na uchomaji wa moto madawa hayo yaliyokamatwa kwa mwaka uliopita wa 2015 wakati walipokutana na Waandishi wa Habari leo 5 Januari, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa toka Waziri wa Katiba na Sheria pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka (hawapo pichani) leo 5 Januari, 2016 Jijini Dar es Salaam.

DK. KIGWANGALLA AFANYA ZIARA MUHIMBILI NA KUKAGUA MASHINE ZA CT-SCAN NA MRI, AFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI

$
0
0
IMG_0900
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akipata maelezo ya mashine mpya ya CT Scan iliyonunuliwa hivi karibu na Serikali kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru.
IMG_0903
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru (kushoto) akitoa maelezo ya uwezo mashine mpya ya CT-Scan iliyonunuliwa na Serikali hivi karibuni ambayo hadi kufikia Januari 4, 2016 ikiwa na muda wa siku tatu tangu kuanza kutumika hospitalini hapo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla.
IMG_0910
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru baada ya kuona mabadiliko makubwa katika hospitali hiyo tangu alipokaimu kiti hicho wakati wa zaiara ya kushtukiza katika chumba kilichofungwa mashine mpya ya CT-Scan iliyonunuliwa na Serikali hivi karibu na inauwezo mkubwa wa kufanya kipimo kwa sekunde 6 na kutoa majibu. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Flora Rwakatare.
IMG_0924
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiwa kwenye dirisha la malipo ya matibabu hospitalini hapo wakati wa ziara ya kushtukiza aliyoifanya, Januari 4, 2016.
IMG_0930
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla aliyetembelea kitengo chake, Januari 4, 2016. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru.
IMG_0932
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Dk. Hamisi Kingwangalla akiendelea kupewa maelezo ya namna wananchi wanavyohudumiwa katika kitengo hicho na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga.
IMG_0935
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinangaakitoa maelezo ya ubao maalum unaowaongoza madaktari na wagonjwa wanaohudumiwa katika kitengo hicho kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Dk. Hamisi Kingwangalla.

IMG_0950
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Dk. Hamisi Kingwangalla akikagua wodi mpya ya wagonjwa mahututi (ICU) ambayo ipo kwenye hatua za mwisho kukamilika. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru akimtembeza Mh. Naibu Waziri kwenye wodi hiyo.

IMG_0873
Baadhi ya watumishi katika kitengo cha vipimo cha MRI wakiandaa kitanda kwa ajili ya kumpokea mgonjwa wa kipimo cha MRI (hayupo pichani) kama walivyokutwa na mpiga picha wa wetu.
IMG_0876
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akipata taarifa ya idadi ya wagonjwa waliofanyiwa vipimo tangu mashine hiyo ipone kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Flora Rwakatare (kulia).
IMG_0886
Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Flora Rwakatare akizungumza jambo na waandishi wa habari katika chumba cha vipimo vya MRI wakati wa ziara ya kushtukiza iliyofanywa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla, Januari 4, 2016.
IMG_0891
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiwa ndani ya chumba cha vipimo vya MRI katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ya jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza, Januari 4, 2016.
IMG_0951
IMG_0833
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiwasili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipofanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo, Januari 4, 2016.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

IMG_0836
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akitoka katika ofisi ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo.
IMG_0857
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru (kushoto). Katikati ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga.
IMG_0861
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru (kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga (kulia) kuelekea kwenye chumba cha vipimo vya CT Scan pamoja na MRI alipofanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo, Januari 4, 2016.

Na Rabi Hume, Modewjiblog
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla amefanya ziara, Januari 4, 2016 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kutembelea idara mbalimbali za hospitali hiyo kuona jinsi ya ufanyaji kazi.
Baadhi ya idara ambazo, Dk. Kingwangalla alitembelea ni pamoja na Kitengo cha dharura, Chumba cha wagonjwa Mahututi (ICU), wodi ya Mwaisela, duka la dawa la MSD na kukagua ufanyaji wa kazi wa mashine ya CT-Scan na MRI.

Akizungumzia ziara hiyo mara baada ya kutembelea Hospitalini hapo, Dk. Kigwangalla ameeleza kuwa ili kuweza kuona hali ya utendaji wa kazi iliyopo katika hospitali hiyo ya taifa tangu ambapo Rais, Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kushtukiza na kutokuridhishwa na utendaji kazi wa hospitali hiyo hali iliyopelekea kuivunja bodi iliyokuwa ikisimamia hospitali.

Dk. Kingwangalla alisema amefurahishwa na utoaji wa huduma katika upimaji kwa kutumia mashine ya CT-Scan na MRI ambazo awali wakati wanaingia madarakani hazikuwa katika hali nzuri ya ufanyaji wa kazi na kuwataka watumishi wa hospitali hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuifanya hospitali hiyo kuonekana yenye hadhi ya kuwa hospitali ya taifa.

Alisema limekuwa jambo ambalo linasikitisha kuona huduma zinazopatikana katika hospitali ya taifa zinashindwa na huduma zinazotolewa katika hospitali za watu binafsi na akilinganisha huduma za kulipia vitanda zinazotolewa Muhimbili kuwa hazina viwango vya juu ambavyo vinaweza kuwashawishi wananchi wenye uwezo kuacha kwenda hospitali binafsi na kwenda hospitalini hapo.

“Ni jambo la kushangaza hospitali za watu binafsi zinakuwa na watu wengi kuliko hapa na wakati sisi tuna madaktari bingwa zaidi ya 500 hapa Muhimbili lakini hizo hospitali zao hazina hata daktari mmoja bingwa lakini na huduma zinazopatikana katika madaraja ya juu zinatakiwa kuboreshwa,
“Kama tunaweza kuwa na huduma nzuri katika first class (daraja la kwanza) tunaweza kuwavuta wananchi wengi waje hapa na waache kwenda hospitali binafsi, wanatakiwa kutengwa madaraja ya juu ambayo huduma zake zinakuwa zimeboreshwa sio mtu anakuwa daraja la kwanza alafu bado anachangia choo na wengine au anaelala nae hapewi kitanda,” alisema Mhe. Kingwangalla.

Aidha Mhe. Dkt.Kingwangalla aliwatupia lawama Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa jinsi wanavyopanga madaraja ya hospitali na kuilinganisha Muhimbili na hospitali zingine za watu binafsi kuwa jambo hilo siyo sahihi kwa kuiweka hospitali ya taifa sawa na hospitali za watu binafsi.

“NHIF wanaweka sehemu moja hospitali ya taifa na hospitali binafsi hili haliwezekani walinganishe huduma zilizopo hospitali ya taifa na zile zingine, nina mpango wa kuwatembelea hivi karibuni nitazungumza nao,” alisema Kingwangalla.

Aidha Mhe. Naibu Waziri aliupongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa kuongeza vitanda katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) ambayo awali ilikuwa na vitanda sita hali ambayo ilikuwa ikiwashangaza wananchi wengi kutokana na kuwepo kwa vitanda zaidi ya 1350 katika hospitali hiyo na hivyo kuongezeka kwa vitanda katika wodi hiyo kutasaidia upatikanaji wa wa huduma bora kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kupata huduma.

Awali akitoa taarifa mbele ya Mhe. Dkt. Kingwangalla, Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali hiyo, Dkt. Flora Rwakatare alisema tangu kuanza kwa kutumika kwa mashine ya MRI mwishoni kwa mwezi Novemba mwaka jana jumla ya wagonjwa 560 wamefanyiwa vipimo katika mashine hiyo na ndani ya siku tatu amabazo wamefunga mashine mpya ya CT-Scan wameshawapima wagonjwa 26.

Alisema kufungwa kwa mashine ya CT-Scan kunaonekana kuwepo kwa matumaini mapya kwa watanzania kutokana na kasi ya ufanyaji kazi kwa mashine hiyo ambayo imetengenezwa na kampuni ya Siemens ambayo inauwezo wa kupima kifua na tumbo kwa sekunde 6.

“Mashine ya CT-Scan ambayo imefungwa ina ubora mkubwa na ni ya pili kwa ukubwa Afrika Mashariki na kwasasa tunategemea kufanya kazi kwa ubora zaidi kutokana na ukubwa iliyonayo na inaweza kufanya kazi kwa kasi tofauti na ile iliyokuwa ikitumika awali,” alisema Dkt. Flora.

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru alisema awali hawakuwa wakifanya visingizo ili wasifanye kazi lakini ni hali halisi iliyokuwepo kuwa mashine iliyokuwepo awali ilikuwa na matatizo lakini kufanikisha kufungwa kwa mashine mpya ambayo imeigharimu serikali Dola za Kimarekani Milioni 1.7 ambapo ni zaidi ya Milioni 400 za kitanzania kutawapa wao motisha ya kufanya kazi kwa kutumia kifaa cha kisasa na chenye kufanya kazi kwa haraka.

NAIBU WAZIRI MASAUNI ATEMBELEA UHAMIAJI, AAGIZA MAKAMPUNI YENYE KUAJIRI WAGENI YACHUNGUZWE

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (kulia) akimsalimia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile wakati alipowasili Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Masauni aliiagiza Idara hiyo kuchunguza Makapuni yanayotoa ajira kwa wageni ambapo ajira hizo wangepewa Watanzania wenye sifa na kupunguza tatizo la ajira nchini.. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (kulia) akiwasalimia wananchi wanaosubiri kupata huduma ya Hati za Kusafiria katika Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake kwa Viongozi Wakuu wa Idara hiyo, Naibu Waziri Masauni aliiagiza Idara hiyo kuchunguza Makapuni yanayotoa ajira kwa wageni ambapo ajira hizo wangepewa Watanzania wenye sifa na kupunguza tatizo la ajira nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Afisa Uhamiaji anayeshughulika na uchapaji wa Hati za Kusafiria, Amir Hassan (kushoto), akitoa maelezo ya jinsi wanavyozichapisha Hati za Kusafiria, kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (katikati aliyevaa tai) ambaye alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao chake na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Wakwanza kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile, na Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha),  Piniel Mgonja. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Kamishna wa Idara ya Uhamiaji (Utawala na Fedha), Piniel Mgonja akitoa taarifa fupi ya utendaji wa Idara hiyo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (katikati) wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (wanne kushoto), Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile (wanne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji. Naibu Waziri Masauni alifanya ziara ya kikazi katika idara hiyo kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na idara hiyo. Hata hivyo, katika hotuba yake, aliiagiza idara hiyo kuchunguza Makapuni yanayotoa ajira kwa wageni ambapo ajira hizo wangepewa Watanzania wenye sifa na kupunguza tatizo la ajira nchini .
 Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

BALOZI SEIF ALI IDDI AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA KITUO CHA TIBA NA MAREKEBISHO YA TABIA KWA VIJANA.

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifunua pazia kuashiria kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Tiba na marekebisho ya Tabia kwa Vijana wanaoacha Dawa za kulevya hapo Kidimni, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unaguja.
 Balozi Seif pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dr. Omar Dadi Shajak wa kwanza kutoka kulia na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dr. Idriss Muslim Hijja nyuma yake wakifurahia na kupiga kofi mara tu baada ya Balozi Seif kuweka jiwe la msingi la Kituo cha Tiba na marekebisho ya Tabia kwa Vijana hapo Kidimni.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dr. Shajak wa pili kutoka kushoto akimpatia maelezo Balozi Seif wa kwanza kutoka kushoto jinsi ya ujenzi wa kituo cha Tiba na marekebisho ya Tabia kwa Vijana utakavyoendelea hapo Kidimni.Wa Pili kutoka kulia ni Mkandarasi wa ujenzi huo kutoka Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Zanzibar Nd. Mbwana Bakari juma.



 Baadhi ya wananchi walioshiriki hafla ya uwekaji wa Jiwe la msingi la Kituo cha Tiba na marekebisho ya Tabia kwa Vijana wanaoacha Dawa za kulevya hapo Kidimni Wilaya ya Kati.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dr. Omar Dadi Shajak akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa Kituo cha Tiba na marekebisho ya Tabia kwa Vijana hapo Kidimni Wilaya ya Kati.

Balozi Seif akizungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la Kituo cha Tiba na marekebisho ya Tabia kwa Vijana ikiwa ni shamra shamra za kutimia miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Picha na – OMPR – ZNZ.

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema wakati umefika sasa katika kuona Wananchi wanalazimika ipasavyo kutoa mashirikiano ili kusaidia kufanikisha ile azma ya Serikali Kuu ya kupambana na biashara na matumizi ya dawa za kulevya Nchini.

Amesema kuwa kukosekana ushirikiano katika kutoa ushahidi Mahakamani dhidi ya watu wanaotuhumiwa kuhusika na dawa za kulevya ambako kunawahusu zaidi Wananchi walio karibu na wahusika hao inapelekea kufutwa kwa kesi na hivyo kudumaza juhudi za Serikali katika vita dhidi ya matumizi ya dawa hizo.

Balozi Seif Ali Iddi amesema hayo baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Tiba na marekebisho ya Tabia kwa Vijana wanaoacha Dawa za kulevya hapo Kidimni, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unaguja ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za kutimia Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 1964.

Amesema suala la Dawa za kulevya hivi sasa limekuwa janga la Dunia kwa vile ni la muda mrefu na kuathiri watu wengi hasa Vijana. Hivyo udhibiti wa matumizi yake unahitaji maamuzi magumu ya Serikali pamoja na ushirikiano wa Kitaifa, Kikanda na Dunia kwa ujumla.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwanasihi walioanzisha nyumba hizo pamoja na Vijana wanaoishi kwenye nyumba hizo kujitahidi kutoshawishika kurudi nyuma kwa kujiingiza tena katika janga la matumizi ya dawa za kulevya.

Mapema akitoa Taarifa ya ujenzi wa Kituo hicho Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dr.Omar Dadi Shajak alisema ujenzi wa kituo hicho unagharimiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa zaidi ya Shilingi Bilioni Nne na Milioni Mia Mbili { 4,200,000,000/- } hadi kukamilika kwake.

Dr. Shajak alisema Kituo hicho cha aina yake ndani ya ukanda wa Mwambao wa Afrika Mashariki kitakuwa na uwezo wa kuhudumia Vijana wapato 200 wake kwa waume kwa wakati mmoja ambapo pamoja na mambo mengine kutakuwa na mafunzo ya kazi za amali, michezo na huduma nyengine za kurekebisha tabia.

Dr. Omar Dadi Shajak amewafahamisha kwamba Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar katika kukabiliana na wimbi la uingizaji, uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya tayari imeshaandaa zawadi kwa Mtu au Kikundi kitakachojitolea kutoa Taarifa ya kukamatwa kwa wahusika wa dawa za kulevya.

Ujenzi wa Kituo cha Tiba na marekebisho ya Tabia kwa Vijana wanaoacha Dawa za kulevya hapo Kidimni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja chenye eneo la ukubwa wa Eka Tatu kinajengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Al – Hilal General Trading Cooperation Limited chini ya Mkandarasi Mbwana Bakari Juma kutoka Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Zanzibar.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 5/1/2016.


NEWZ ALERT:WAZIRI WA MALIASILI PROF. JUMANNE MAGHEMBE AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI WA MIPANGO WA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (TFS) NA MAOFISA MISITU WA MIKOA YOTE NCHINI LEO

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza katika kikao na Idara ya Misitu na Nyuki pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu wa Wizara hiyo Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo tarehe 05 Januari, 2015. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Gaudence Milanzi.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza katika kikao na Idara ya Misitu na Nyuki pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu wa Wizara hiyo Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo tarehe 05 Januari, 2015.
 Kamu Mkurugenzi Idara ya Misitu na Nyuki Bi. Gladnes Mkamba (wa pili kulia) akiwasilisha taarifa ya Idara yake kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe wa (pili kushoto) katika kikao hicho.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Bw. Juma Mgoo (kulia) akiwasilisha taarifa ya ofisi yake kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kulia).  
 Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe.
 Sehemu ya wajumbe katika kikao hicho. 
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi (wa pili kulia) akizungumza katika kikao hicho.

...................................................................


Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Bw. Mohammed Kilongo na Maofisa wa Misitu wa Mikoa nchi nzima kupisha uchunguzi wa upotevu wa mapato ya Serikali.
Akizungumza leo na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya Wizara hiyo Dar es Salaam, Prof. Maghembe amesema agizo hilo limekuja kutokana na ubadhilifu unaofanywa na Maofisa wa ukusanyaji wa maduhuri ya Serikali yanayotokana na rasilimali za misitu katika Mikoa na Wilaya kwa kutowasilishwa katika mfuko Mkuu wa Serikali.
Ameagiza pia maofisa hao wote wanaokusanya maduhuri ya Serikali katika Wilaya watumie muda wa siku kumi kuanzia leo kuhakikisha maduhuri yote yaliyokusanywa yanapelekwa benki ikiwa ni pamoja na kukabidhi vitabu vya kukusanyia mapato kinyume cha hapo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
“Wale district forestry officers wote wapeleke vitabu vyao wanavyokusanyia maduhuri ya Serikali kwenye ofisi za Kanda, Naibu Katibu Mkuu tusaidie kuwasiliana na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali ifanye ukaguzi wa vitabu hivyo ndani ya siku kumi tuhakikishe fedha zinazotakiwa zinaingia kwenye mfuko wa Serikali, Mtu anakusanya fedha  ya Serikali toka mwaka 2004 mpaka leo hajapeleka benki ananeemesha hali yake ya nyumbani, hili hapana”. Alisisitiza Prof. Maghembe.
Kwa mujibu wa Waziri Maghembe Bw. Mohammed Kilongo ambaye Idara yake ndiyo inatoa vitabu kwa ajili ya kukusanya maduhuri ya Serikali katika Mikoa yote na Wilaya zote nchini analazimika kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi ambapo ukikamilika sheria itachukua mkondo wake bila uonevu wowote.  
Katika hatua nyingine Waziri huyo wa Maliasili na Utalii amewaagiza pia Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS) kutumia muda wa siku saba kurudi katika jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii maarufu kama Mpingo House ambalo walihama mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka jana na kwenda kupanga katika jengo la NSSF Mafao House lililopo Ilala.
“Wakati tunajenga nyumba hii hapa, tumejenga jengo hili ni kama jengo la misitu ndio maana linaitwa Mpingo House kwa maana ni jengo la Misitu, ninyi wenyewe mmejenga jengo kubwa hili mmemaliza mmehama, Naagiza jumatatu Desemba 11 muwe mmesharudi katika jengo hili, ghorofa ya tatu nikija kukagua niwakute, haiwezekani mueleze matatizo yote mliyonayo muhame nyumba ya Serikali mkapange jengo hapo jirani” Alisema Prof. Maghembe.
Katika hatua nyingine ya kuboresha uhifadhi wa Misitu nchini Waziri Maghembe ameiagiza Idara ya Misitu na Nyuki ya Wizara ya Maliasili kuhakikisha inajiimarisha katika lengo lake kuu la uhifadhi kwa kushirikiana na wadau wanaohusika kuhakikisha Mamlaka iliyolengwa ya Uhifadhi Misitu inakamilika.
“Tunataka tutoke kwenye Wakala wa Huduma za Misitu (Tanzania Forestry Services Agency) twende kwenye Mamlaka ya Uhifadhi wa Misitu (Tanzania Forestry Services Authority) ili tuweze kufanya vizuri zaidi kwenye eneo la uhifadhi na uendelezaji wa misitu nchini, Katibu Mkuu tunaomba pia usaidie kufanikisha hili” Alisema Prof Maghembe.
Aliongeza kuwa wakati wa kuundwa Mamlaka hiyo ni vizuri pia Idara ya Misitu na Nyuki ya Wizara ya Maliasili ikatenganishwa na kila moja kuwa Idara kamili kutokana na umuhimu wa kila sekta katika kujenga uchumi wa nchi kwa kutoa fursa ya kuboresha maeneo hayo na kuongeza pato la taifa.
Ameitaka pia Idara ya Misitu na nyuki kupitia Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kuhakikisha kuwa inaongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa kuziba mianya yote ya ubadhilifu pamoja na kuanzisha vyanzo vipya vya mapato na kuboresha vyanzo vilivyopo.
Akizungumzia mchango wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kwenye pato la taifa Mtendaji Mkuu, Bw. Juma Mgoo amesema katika mwaka huu wa fedha TFS imeweka makisio ya kukusanya Tsh. Bilioni 88 ambapo mpaka hivi sasa wameshakusanya zaidi ya asilimia 20 na makisio hayo.
Waziri Maghembe akizungumzia kuhusu uvamizi kwenye hifadhi za taifa na mapori ya akiba amewataka wananchi wote waliovamia maeneo ya hifadhi za taifa kwa ajili ya kuchunga mifugo waondoke ndani ya siku saba zijazo, na wale walivamia mapori ya akiba kwa shughuli za kilimo na ufugaji waondoke ndani ya miezi mitatu ijayo.
 "Serikali itawaondoa kwa nguvu wasipotekeleza agizo hili la kuondoka katika maeneo ya hifadhi za taifa na kwenye mapori ya akiba yaliyohifadhiwa” Alisisitiza Prof. Maghembe.
Akizungumzia kuhusu biashara ya Mkaa, Prof. Maghembe amewaagiza wataalamu wa Idara ya Misitu kusimamia biashara ya mkaa kwa kuzingatia taratibu na sheria ikiwa ni pamoja na kuzuia usafirishaji wa Mkaa nje ya nchi.
Ameongeza kuwa nishati ya Mkaa ni muhimu lakini Tanzania ina hifadhi kubwa ya makaa ya mawe ambapo ameitaka Idara ya Misitu kwa kushirikiana na wadau wengine kuona ni namna gani ya kuweza kutumia mbadala huo kwa kuzalisha makaa hayo ya mawe kwa matumizi ya kawaida ili kuokoa misitu nchini.  
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Gaudence Milanzi amesema kuwa maagizo yote yaliyotolewa na Waziri yatafanyiwa kazi kwakuwa lengo lake ni kuona dhamira ya msingi ya Serikali ya awamu ya tano inafikiwa ya kubana matumizi, kuongeza mapato ya Serikali na kuhifadhi maliasili za taifa ikiwemo misitu. 
(Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii - www.wizarayamaliasilinautalii.blogspot.com)

SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU MISAADA ILIYOKATALIWA

$
0
0
Na Magreth Kinabo –Maelezo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema misaada inayotolewa na watu mbalimbali kwa ajili ya kusaidia jamii ni lazima iwe imekidhi viwango vya ubora, hivyo haitakiwi kuangaliwa kwa vigezo vya dini, itikadi wala siasa.
 
 Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake baada kituo kimojwapo nchini kukataa misaada iliyotolewa na Mbunge wa Bukoba Mjini (Chadema), Wilfred Lwakatare wa Chama cha Wananchi(CUF), hivi karibuni.
 
 Dkt. Ulisubisya  alisema hivi karibuni gazeti moja la kila siku la hapa nchini liliripoti kwamba misaada iliyotolewa na Mbunge huyo, katika baadhi vituo afya Zahanati  kwa ajili ya wajawazito  kukataliwa.“Serikali ina sera ya kusaidia jamii hususan misaada inayotolewa  kwenye huduma za afya, ambayo inakidhi viwango vya ubora kulingana Sheria , kanuni na taratibu za Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA),” alisema Katibu Mkuu huyo.  
 
Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari kiliripoti kwamba baadhi ya wakuu wa vituo vya afya na zahanati katika Manispaa ya Bukoba, wamegoma kupokea misaada kwa ajili ya wajawazito uliotolewa na kwa madai ya kupewa maelekezo na Serikali.Dkt. Ulisubisya aliwataka watendaji wa afya wa vituo hivyo kuwa wasiangalie misaada hiyo kwa misingi ya dini, itikadi na kisiasa.
Hata hivyo Katibu Mkuu huyo aliwataka watu mbalimbali wenye lengo la kutoa misaada katika vituo vya afya kuhakikisha kwamba imekidhi viwango viliyowekwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).Katika hatua nyingine aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando alikabidhi ofisi hiyo kwa Katibu Mkuu huyo mpya.

KICHUPA KIPYA : KITA- I WANNA FLY (OFFICIAL MUSIC VIDEO)

Article 19

$
0
0
 Washiriki wa Mafunzo hayo wakisikiliza kwa Makini Mafunzo hayo..
Awamu ya Tatu ya Mafunzo ya Ujarisiamali kwa Mkoa wa Dar es salaam yameanza leo. Wanawake 35 wa jiji la Dar es salaam Watanufaika na mafunzo ya ujasiriamali kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yanayoendeshwa na mtaalamu wa mambo ya Biashara Bw Felix Maganjila na Shekha Nasser. Mafunzo haya yenye lengo la kumwezesha mwanamke wa Kitanzania kuondokana na tatizo la ukossefu wa ajira kwa kujikita katika kujiajiri ndani ya Tasnia ya Urembo
 Mafunzo haya yamegawanywa katika awamu mbili ili kumsaidia mjasiriamali wa kike kujikwamua. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya Biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika Mpangilio wa Biashara ikiwemo Matumizi sahihi ya Rasilimali Muda, Fedha, Muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na Biashara yake
 Awamu ya Pili mshiriki anafundishwa Matumizi sahihi ya Vipodozi kuendana na wakati, mfano office makeup, day, evening na namna ya kumpamba bi Harusi. Pia wanafundishwa namna bora ya kutumia Vipodozi vya LuvTouch Manjano kwa lengo ya kuwa kila mshiriki atakayehitimu mafunzo haya aweze kujiajiri na kujitegemea kwa kuendesha maisha yake ya kila siku kwa kuwapambamba watu wenye Shuguli Mbalimbali
 Pamoja na mafunzo, kila mshiriki anaunganishwana Mwanamke mmoja mwenye mafanikio katika biashara au uongozi katika jamii kwa Lengo la kumuongoza katika safari yake ya biashara kwa muda wa mwaka mzima. Baada ya Wanawake hawa kuhitimu Mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa Mikopo kwajili ya kuwawezesha Kuanzisha Biashara wakiwa chini ya Uangalizi Maalum wa taasisi hiyo kwa Lengo la Kuhakikisha kila Mhitimu wa Mafunzo haya anapiga hatua na kuweza Kujitegemea.

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA TUMBAKU MKOANI RUVUMA NA KUWASIMAMISHA KAZI VIONGOZI WA CHAMA CHA USHIRIKA CHA SONAMCU

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha kusindika  tumbaku  cha mkoani Ruvuma na kuwasimamisha kazi viongozi wa Chama Cha Kikuu Cha Ushirika cha SONAMCU.

Akizungumza  jana jioni(Jumanne, Januari 5, 2016), katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu Ndogo ya Songea, wakati alipokutana na wakulima wa zao la tumbaku wa Wilaya ya Namtumbo, Wananchama wa Vyama Vya Ushirika vya Mkoa wa Ruvuma, viongozi wa Mkoa pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini.

Waziri Mkuu amesema, Serikali ina dhamira ya kufufua kiwanda cha kusindika tumbaku cha SONAMCU, na lengo la kutembelea kiwanda hicho ni katika utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli la kufufua viwanda nchini.

Waziri Mkuu Majaliwa, ametembelea maeneno mbalimbali ya kiwanda hicho na kukagua mitambo iliyokua ikitumika kusindika tumbaku, kabla kiwanda hicho kuzimwa miaka kadhaa iliyopita  baada ya kukosa malighafi za kuendelea na uzalishaji.

Pia, amemtaka Afisa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bibi. Stela Lugongo kuandaa na kuwasilisha kwake mkakati wa kufufua kiwanda hicho cha kusindika tumbaku, na baadae kuwasimamisha kazi viongozi wote wa Chama Kikuu cha Ushirika cha SONAMCU waliohusika na tuhuma hizo na kutaka wafikishwe Mahakamani.

“Serikali imeazimia kufufua viwanda, hasa vile ambavyo havina wawekezaji vimebaki vyenyewe, Tunahitaji kujua namna ya kuvifufua”. Alisema Waziri Mkuu huku akishangiliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa pia, amesikiliza  na kujibu kero mbalimbali za wakulima wa tumbaku wa Mkoa huo, ambao walilalamikia  mfumo wa Vyama vya Ushirika na namna ambavyo vyama hivi vimekua vikiwaibia fedha zao  hadi kushindwa kuendelea kulima zao la tumbaku na kukosa masoko ya mazao yao.

Aidha, Waziri Mkuu amewasihi wakulima kuwa watulivu na kusubiri maamuzi ya Mahakama baada ya kuwa viongozi wa Chama cha Ushirika SONAMCU ambao wamehusika na wizi wa fedha za wakulima kiashi cha Shilingi milioni 800 kwa kipindi cha mwaka 2011 hadi 2014 tayari wamefikishwa Mahakamani na uchunguzi unaendelea. Pia, amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu kukutana na wakulima hao ili kupatia ufumbuzi matatizo yao.

Aidha, ametoa wito kwa wakulima kuendelea kulima zao la tumbaku kwa kuwa linaongeza pato la mtu mmoja mmoja, linasaidia kuchangia pato la Mkoa na kukua kwa uchumi wa nchi. Amewashauri wakulima kuunda  na kuviendesha Vyama Vya Ushirika kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

Waziri Mkuu amemaliza ziara yake mkoani Ruvuma, atafanya majumuisho ya ziara hiyo leo, kabla ya kuagana na viongozi wa Chama na Serikali na kurejea jijini Dar es Salaam.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMMATANO, JANUARI 6, 2016.

Waziri wa kilimo atua mkoani Iringa, akutana na wakulima wa Tumbaku

$
0
0
  mwi5
Waziri wa Kilimo Mifugo na Ushirika Mh. Mwigulu Nchemba  akipokelewa katika  ofisi ya Mkuu wa Iringa na kupokelewa na  Mkuu wa Mkoa Mh. Amina Masenza na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela.
mwi3
Waziri wa kilimo Mh Mwigulu Nchemba leo amesikiliza malalamiko ya wakulima wa Tumbaku na kuwahakikishia zao la tumbaku halitakufa kwani linaleta pato kwa taifa. Waziri wa kilimo Mh Mwigulu Nchemba leo amesikiliza malalamiko ya wakulima wa Tumbaku na kuwahakikishia zao la tumbaku halitakufa kwani linaleta pato kwa taifa. 

wakulima wamelalamika sana uchelewashwaji wa pembejeo, bei duni ikiwemo madaraja mengi ya mfano kuna madaraja zaidi 72 ya grade za tumbaku kitu ambacho wakulima wamesema inawaumiza sana kwenye bei. 
 
Pia wakulima wamelalamika ubadhirifu wa chama cha mtandao (Union) kiitwacho ITCOJE. Katika ziara hiyo Mh waziri aliambatana na Mrajisi wa vyama vya ushirika Dr. Rutabanzibwa na Mkurugenzi wa bodi ya Tumbaku Bwana Mushi. Mh. waziri ameagiza matatizo mengi yawe yametattuliwa kabla kikao cha bunge hakijaanza.
 
Mh. Mwigulu aliwasili kwanza ofisi ya Mkuu wa mkoa na kupokewa na Mkuu wa Mkoa Mh Amina Masenza na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela. Mh Masenza alimpa taarrifa fupi ya hali ya Kilimo katika mkoa wa IRINGA.
mwi4
Wajumbe mbalimbali wa mkutano huo wakiwa katika mkutano
mwi2
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Ushirika akisalimiana na wajumbe mbalimbali wa mkutano huo.

Lukuvi awarejeshea wananchi Shamba lililokuwa na mgogoro wa zaidi ya miaka kumi

$
0
0
luku1
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwarudishia wananchi shamba la Hekta 1,870 kutoka kwa Muwekezaji wa kampuni ya Export Trading Company kijiji cha Kapunga Wilayani Mbarali Mkoa wa Mbeya. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abasi Kandoro na Katikati ni Muwekezaji Mahesh Patel.
luku2
Wananchi wa Kapunga wakiwa katika mkutano ulioitishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati wa kuwatangazia urejeshwaji wa Hekta 1,870 kutoka kwa Muwekezaji.
luku3
Shamba la kapunga lililokuwa na Mgogoro wa zaidi ya Miaka kumi ambalo kwa sasa limerudishwa kwa wananchi kutoka kwa Muwekezaji.Picha na Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Ardhi.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundu Mhe. Eng Stella Manyanya afungua mafunzo ya walimu mahiri wa masomo ya Hisabati, Kiingereza na Kiswahili Ruvuma.

$
0
0
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Eng Stella Manyanya akizungumza na washiriki wa mafunzo ya Walimu Wawezeshaji wa masomo ya Hisabati, Kiingereza na Kiswahili kutoka shule za msingi katika Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma  na Halmashauri ya Ludewa Mkoa Njombe.
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Eng Stella Manyanya akishiriki katika darasa mojawapo la mafunzo ya Walimu Wawezeshaji wa masomo ya Hisabati, Kiingereza na Kiswahili kutoka shule za msingi katika Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma  na Halmashauri ya Ludewa Mkoani Njombe.

Afisa wa Kitengo cha Ufatiliaji cha Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Lawrence Sanga akitoa taarifa fupi juu ya mafunzo ya walimu wawezeshaji yanayoendelea kufanyika katika vituo Shule ya Sekondari ya Wasichana Songea, Shule Sekondari Mwangaza - Katavi na Shule ya Sekondari Mwenge - Singida
 Baadhi ya Washiriki wa mafunzo  ya Walimu Wawezeshaji wa Masomo ya Hisabati, Kiingereza na Kiswahili wakimsikiliza mgeni rasmi Mhe. Stella Manyanya Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya  hayo mkoani Ruvuma

SUMATRA yawaomba wananchi kupendekeza nauli za BRT

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya UDA Rapid Transit (UDA-RT), Bw. David Mgwassa akifafanua jambo wakati wa majadiliano ya wadau juu mapendekezo ya nauli zitakazotumika na mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) jijini Dar es Salaam jana.  Majadiliano hayo yanaendelea.
Wadau wa sekta ya usafiri wakiwa katika majadiliano ya mapendekezo ya nauli zitakazotumika baada ya kuanza kwa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) jana jijini Dar es Salaam.  Majadiliano ya mapendekezo hayo yaliyotolewa na kampuni ya UDA-RT bado yanaendelea. 


Mamlaka ya Udhibi wa Usafiri wa Majini na Nchi kavu (SUMATRA) jana imewaomba  wakazi wa Jiji la Dar es Salaam  kupendekeza kwa maandishi ya nauli zitakazotumika katika Mradi wa Mabasi ya Yaendayo Haraka (BRT) wa jijini Dar es Salaam.Huduma  katika kipindi cha mpito zimepangwa kuanza Januari 10, mwaka huu.

Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA,Bw. Gillird Ngewe, ametoa ombi hilo baada ya nauli zilizopendekezwa naKampuni ya UDA Rapid Transit (UDA-RT) kukataliwa na mkutano wa wadau wa usafiri uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini jana. UDA-RT itatoa huduma za kipindi cha mpito.

“Tumeletewa mapendekezo haya ya nauli na UDA-RT na wote tumeyajadili na wengi wetu tunahitaji yafanyiwe kazi zaidi.  Tuleteeni mapendekezo yenu. Na sisi tunawaondoa wasiwasi kuwa mapendekezo ya nauli na maoni yenu tutavifanyia kazi,” aliahidi Bw Ngewe.

Ameeleza kuwa  katika  kuamua suala la nauli SUMATRA haiwezi kuangalia tu mapendekezo ya waendeshaji wa mradi mabasi hayo, bali inazingatia pia maoni ya wadau, wananchi na hali halisi ya nchi, na kuahidi kwamba maoni na mapendekezo yote yatapewa uzito wakati wa kuamua nauli za kutumika.

“Sisi ni wadhibiti  maoni yenu yatafanyiwa kazi na endeleni kujenga utamaduni wa kushiriki majadiliano kama ilivyo hivi leo;   hii itasaidia mamlaka kufanya kazi zake kwa urahisi na kwa maslahi ya nchi”, amesisitiza Bw.Ngewe.

Amewahakikishia wananchi kuwa nauli zitakazopangwa ndizo tu zitakazotozwa na wenye mabasi na si vinginevyo.Bw Ngewe ametumia nafasi hiyo kuwataka wenye mabasi ya abiria kufuata sheria kwa kutoza nuali elekezi nchi nzima ili kujenga utamaduni wa kufanya biashara yenye maslahi kwa pande zote mbili.

Mkurugenzi Mkuu wa UDA-RT,Bw. David Mgwassa, amesifu mchango wa wadau na kuahidi kuutumia katika kupendekeza nauli zenye maslahi kwa pande zote mbili.

“Tunathamini maoni ya wadau na tunaomba pia mamlaka izingatie hali ya uendeshaji wa mabasi ili watumiaji na kampuni tuweze kufaidika na mradi mzima”, alisema,Bw. Mgwassa.

Awali kampuni yake ilipendekeza nauli ya 1,200/- kutoka Kimara hadi Kivukoni na 700/- kutoka Mbezi hadi Kimara Tsh. 700 na 1,400/- kwa njia za mrisho  wa nji kuu.  Mapendekezo yote yalikataliwa na wadau katika mkutano wa jana.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Wakaji la SUMATURA (SUMMATRA Consumers’ Council),Dkt. Oscar Kikoyo, ameitaka mamlaka hiyo kuzingatia maoni ya wadau na nauli zinazotumika sasa ndizo zitumiwe na mradi wa BRT  ili kuwapunguzia wananchi mzigo.Amesema nauli zitozwe kwa kilometa au ukanda na amepinga wazo la nauli ya aina moja kwa barabara nzima.

“Tunatambua kuwa huu ni uwekezaji mkubwa na kwa maoni umekuja kuboresha maisha ya wananchi. Kwa hiyo  nauli za mabasi hay zibaki ni hizi zilizopo”, amesema Dkt. Kikoyo.Wachangia wengine waliona nauli zilizopendekezwa na Kampuni ya UDA-RT ni kubwa mno.

Sampuli ya Vitambaa kwa ajili ya Vazi la Taifa

$
0
0


Vitambaa vya Kanga vilivyopendekezwa kwa ajili ya kutumika kama Vazi la Taifa.

Vitambaa aina ya Vitenge vilivyopendekezwa kwa ajili yaVazi la Taifa

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Halotel kufikisha mtandao kwa asilimia 95 ya watanzania hadi mwishoni mwa mwaka 2016

$
0
0
 Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya mawasiliano ya Halotel, Le Van Dai akizungumza na wanahabari katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo kuhusuiana na mtandao huo kutanua huduama zake hadi kufikia asimimia 95 ya watazanzania. Wanaoshuhudia ni Naibu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Emanuel Malyeta (kushoto), na kulia kwake ni  mwanasheria wa kampuni hiyo,Christopher Masai.
Naibu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Halotel, Emanuel Malyeta akifafanunua jambo kwa waandishi wa habari. Katikati ni Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya mawasiliano ya Halotel, Le Van Dai kulia kwake ni  mwanasheria wa kampuni hiyo,Christopher Masai.
Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya mawasiliano ya Halotel, Le Van Dai akimkabidhi zawadi mwandishi wa gazeti la the Guardian, Sylivester Domaso.

Dar es Salaam, 5/1/2016: Kampuni mpya ya simu za mikononi, Halotel, leo imetangaza mpango wake wa kufikisha mtandao wa simu kwa asilimia 95 ya watanzania hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Wakiongozwa na kauli mbiu yao ya Pamoja katika Ubora, wanalenga kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na simu ya mkononi pamoja na kupata huduma ya mtandao kwa kila sehemu ya Tanzania, ambapo mpaka sasa imeshaunganisha mtandao wa simu kwa zaidi ya vijiji 1500 ambavyo havikuwa vimeunganishwa na huduma ya mtandao awali.
Hadi sasa Halotel imeshawekeza zaidi ya dola bilioni 1 za kimarekani mpaka sasa kwa kutengeneza miundombinu na kuboresha mtandao wa mawasiliano, kampuni ya Halotel imefanikiwa kufikisha huduma za mtandao katika mikoa yote 26 nchini, pamoja na miji na vijiji, ikiwa ni zaidi ya asilimia 95% ya watanzania wote hivyo kuifanya kuwa kampuni yenye mtandao mkubwa zaidi nchini.

Akizungumzia mipango ya kampuni yake kwa mwaka 2016, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Halotel, bwana Le Van Dai amesema kampuni yake itaendelea kupeleka mtandao katika vijiji vingine 1500 katika mwaka 2016 na kuweka mkazo wa hali ya juu katika mrejesho kwa wateja pamoja na kuboresha mtandao, huduma kwa wateja, huduma kwa jamii hali itakayopelekea mapinduzi katika sekta ya mawasiliano nchini.
‘Kampuni yetu itashirikiana na watanzania katika kuhakikisha inaleta maendeleo kwa watanzania, kama ambavyo kauli mbiu yetu ilivyo, Pamoja katika Ubora, ndivyo ambavyo tutaendelea kuwekeza hapa nchini hali itakayopelekea kukua haraka kwa kampuni yetu’ alisema Bwana Dai.
Katika hatua nyingine Dai amewashukuru watanzania na serikali yao kwa mapokezi waliyoipa kampuni yao, na pia amewahakikishia kuwa Halotel itaendelea kufanya kazi kwa kuzingatia sheria za nchi na wataendelea kushirikiana nao katika kusukuma maendeleo ya nchi.
‘Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa waliotupa, na kuelekea mwaka 2016, kampuni yetu itaendelea kukuza ubunifu, zawadi pamoja na huduma nyingine kwa wateja wetu’ alisema Dai.
Kwa mwaka 2015 pekee, kampuni ya Halotel imelipa kodi ya zaidi ya dola milioni 27 za kimarekani, ambayo kati ya hiyo dola milioni 24 imetumika kulipa kodi uingizaji bidhaa na dola laki saba ni kodi inayohusuiana na rasrimali watu.
Dai amesema pia kampuni yake imetengeneza zaidi ya ajira 1,500 za moja kwa moja na zaidi ya 20,000 za ajira zisizo za moja kwa moja, akisisitiza kuwa kampuni yake itahakikisha inafata sheria za ajira za Tanzania.
Katika hatua nyingine, Dai alielezea masikitiko yake kwa matukio ya wizi na uporaji wa mitambo ya Halotel, akielezea kuwa zaidi ya matukio 52 yameripotiwa kuanzia mwezi wa kwanza hadi Disemba mwaka huu, ambapo imewasababishia hasara ya jumla ya shilingi milioni 393.Lengo la Halotel ni kuhakikisha kila mtanzania ana simu ya mkononi ili kubadilisha namna watanzania wanaishi na namna wanavyokuza na kujenga uchumi wao.
‘Kampuni yetu ina zaidi ya kilomita 18,000 za fibre optic, pamoja na zaidi ya minara 2500, hivyo kuifanya Halotel kuwa kampuni yenye mtandao mkubwa zaidi nchini, ambayo pia itatumika kuunganisha serikali za mitaa 150, hospitali 150, vituo vya polisi 150, ofisi za posta 65 na intaneti ya bure kwa shule zaidi ya 450’ alimaliza Dai.

BALOZI WA NORWAY NCHINI AMTEMBELEA WAZIRI NAPE OFISI KWAKE

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye kushoto akiongea na Balozi wa Norway nchini Tanzania Hanne-Marie Kaarstad wakati wa Kikao kilichofanyika Ofisini kwa Waziri,katika kikao hicho Norway iliahidi kuendelea kudumisha ushirikiano na Tanzania katika sekta ya utamaduni, Sanaa na Michezo. 
Balozi wa Norway nchini Tanzania Hanne-Marie Kaarstad kulia akiongea na  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye kushoto wakati wa Kikao kilichofanyika Ofisini kwa Waziri,katika kikao hicho Norway iliahidi kuendelea kudumisha ushirikiano na Tanzania katika sekta ya utamaduni, Sanaa na Michezo. (Picha na Benjamin Sawe-WHUSM).
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images