Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46329 articles
Browse latest View live

BEI YA MADAFU LEO


WAGONJWA WA KIPINDUPINDU KWA MIKOA YA ARUSHA NA MWANZA WAFIKIA 171

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
TAKWIMU za Ugonjwa wa Kipindupindu zinaonesha kupanda kwa mikoa ya Mwanza na Arusha kwa kuwa na wagonjwa 171, kutoka wagonjwa wa mwanzo 105.

Katika mkoani Arusha maambukizi yameongezeka kutoka wagonjwa 60 hadi kufikia wangonjwa 111 huku mkoa wa Mwanza maambukizi mapya kutoka wagonjwa 45 hadi 60.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla amesema kasi ya maambukizi ya ugonjwa kwa wiki iliyopita imepungua katika mikoa ya Mbeya na Tanga huku mikoa ya Dar es Salaam na Lindi ikiwa haina taarifa za maambukizi mapya ya wagonjwa wa kipindupindu.

Kigwangalla amesema kuwa katika mikoa ambayo haijakuwa na taarifa za wagonjwa wapya wa kipindupindu wizara imetaka wadau wa mikoa hiyo kuendelea kwa jitihada walizozifanya katika kudhibiti ugonjwa huo.

Kigwangala amesema ugonjwa wa kipindupindu tangu kuanza kulipotiwa hapa nchini watu 202 wamefariki dunia.

 Aidha amewataka madiwani na viongozi wa kisiasa kuhamasisha usafi wa mazingira na kushindwa kufanya hivyo wanahatarisha nafasi zao.

WAKATI HUOHUO.
Na Magret Kinabo wa Maelezo anaripoti.

SERIKALI imezitaka kila halimashauri nchini kuhakikisha kuwa inatenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya damu ili kuwezesha wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo kuipata na kuepusha kupoteza maisha ya watu hususan wakina mamawajazwazito na watu waliathirika na ajali.

Aidha Serikali imesema damu hutolewa bure, hivyo  mtu yoyote atakayeuziwa damu ataoe taarifa kwa Mkuu wa Mkoa,  Mkuu wa Wilaya  au wizarani ili wahusika waeze kuchukuliwa hatua. Hivyo Watanzania wasikubali kutoa rushwa kwa ajili ya kupata  damu.

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi  Kingwangala katika ziara aliyoifanya leo katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu  zilizopo jijini Dares Salaam.

Awali akitembelea ofisi hizo, Dkt Kingwangala  alielezwa na Dkt . Avelina Mgasa kwamba changamoto zilizopo katika upatikanaji wa damu nchini ni halimshauri kutenga bajeti za kutosha kwa ajili ya huduma hiyo.

“ Mganga Mkuu au Mkurugenzi ambaye hatawajibika kuhakikisha damu inakuwepo katika vituo vya kutolea huduma ataripotiwa kwa mamlaka zilizomteua ili ziweze kumchukulia hatua,” alisema Dkt. Kingwangala.

Dkt. Kingwangala aliitaka mifumo ya bima nchini kuhakikisha iligharamia mifuko ya kuhifadhi damu na reagent(vitenganishi) kwa wagonjwa waowalipia huduma za afya  ili kuweza kusiadi changamoto inayoikabili ofisi hiyo.

Aidha Dkt. Kingwangala aliitaka ofisi hiyo kuwa na mfumo wa kieletroniki wa kuwatambua watu wanaochangia damu, kutoa taarifa jinsi damu zao zilivyookoa miasha ya wagonjwa   na kuwapa motisha ili waweze kuwa wachangiaji endelevu.

SERIKALI YANUNUA MASHINE MPYA YA CT-SCAN KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI YENYE UWEZO WA HALI YA JUU

$
0
0



Na Magreth Kinabo –MAELEZO.

Serikali imenunua mashine  mpya ya CT-Scan yenye thamani ya  takriban dola  za Marekani milioni 1.7  yenye uwezo wa hali ya juu kwa ajili ya kutoa huduma za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali  katika Hospitali  ya Taifa ya Muhimbili(MNH) iliyopo jijini Dar es Salaam.

 Ununuzi wa mashine hiyo, umefanyika kufuatia agizo la Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoifanya hivi karibuni ambapo aliutaka uongozi wa hospitali hiyo kuboresha huduma zake na kuhakikisha vifaa tiba na dawa   vinapatikana ili kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora za afya.

 Hayo yamegundulika leo baada ya Naibu  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi  Kingwangala aliyoifanya leo katika hospitali hiyo, ambapo alitembea Idara ya  Magonjwa ya Dharura,Idara ya Mionzi,  sehemu  mpya ya wagonjwa waliopo chini ya ungalizi maalum(ICU), ambayo inafanyiwa ukarabati na wodi mojawapo. Naibu  Waziri akitembelea katika Idara ya Mionzi ambapo  alijionea mashine za MRI na CT –Scan zinavyofanyakazi.

 Akizungumzia kuhusu mashine ya CT-Scan Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dkt. Flora Lwakatare alisema mashine hiyo , iliyotengenezwa na kampuni ya  Siemens  mpya imefungwa siku mbili zilizopita na imeshaanza kufanya majaribio  kwa wagonjwa 26  tangu ilipofungwa.

 Dkt. Flora aliongeza kwamba mashine hiyo iko moja tu nchini na katika nchi za Afrika Mashariki nchi nyingine iliyonunua mashine hiyo ni Kenya katika Hospitali ya Aghakhan.
“ Mashine hii inatoa huduma za hali ya juu kwa magonjwa ya moyo, ubongo tumbo kifua na inauwezo wa kupima kifua na tumbo kwa sekunde sita,” alisema. Akizungumzia kuhusu mashine hiyo Naibu Waziri huyo, alisema imenunuliwa kwa fedha za Serikali wala sio mkopo.“Tunatarajia kununua mashine hii katika hospitali ya Dodoma na Mwanza,” alisema Waziri Kingwangala.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa MNH, Profesa Laurence   Maseru alisema mashine hiyo ina sahani 128 mara 2 ikilinganishwa na iliyokuwepo ambayo ilikuwa inatumia  sahani sita. Kwa upande wa mashine ya MRI ambayo tangu ilipofanyiwa matengenezo makubwa Novemba 26, mwaka jana  hadi sasa imesha hudumia wagonjwa 560.

 Dkt. Kingwangala  alitembea katika Idara  cha huduma za dharura na kuangalia jinsi huduma zinavyotolewa, ambapo alielezwa na  Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura Dkt. Juma Mfinaga alisema ambayo huhudumia wastani wa wagonjwa 300 hadi 400 kwa siku ambacho kinafanya kazi kwa kutumia mfumo maalum wa kompyuta bila kutumia karatasi. Naibu Waziri huyo, mbali na kupongeza maboresho yaliyofanyika na huduma nzuri, alitoa maagizo kwa uongozi wa hospitali hiyo kuboresha huduma za  zilinazotolewa hospitalini kuwa za kitaifa zaidi.

 Alitolea  mfano  huduma kulipa kwa kuongeza vitanda na matumizi ya choo kimoja kila chumba ili kuweza kuvutia wateja. “Sisi tunaweza kufanya biashara kwa kuboresha huduma za kulipa ili zimpendeze na kuvutia wateja. Na fedha zitakazopatikana zitatumika kununua dawa , vifaa tiba na kuwapatia wafanyakazi motisha, alisema.Aliutaka uongozi huo pia kuhakikisha inawalipa wafanyakazi fedha za  malipo ya ziada kwa wakati ifikapo tarehe 25 ya mwezi unaofuata,kutumia mfumo wa kompyuta sehemu zote, kupunguza msongamno wa wagonjwa na kuwa wabunifu.

DKT. MAYUNGA AKABIDHI OFISI LEO JIJINI DAR.

$
0
0
 Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Sellasie Mayunga akikabidhi ofisi mbele ya waandishi wa habari leo katika Makao Makuu ya Wizara, Dar es Salaam ambapo amemshauri Naibu Katibu Mkuu mpya DKT. Moses Kusiluka kushughulikia kwa ukaribu suala la mpaka wa Kimataifa wa eneo la Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi kutokana na jambo hilo kuwa na maslahi makubwa ya Taifa.

Pia, amemsahuri Naibu huyo kutoa kipaumbele kwa ujenzi wa kituo cha kupokea picha za anga (Satellite receiving station) kilichopangwa kujengwa nchini mkoani Dodoma ambapo pamoja na faida zingine kitarahisisha utoaji wa hati za hakimiliki za ardhi kimila.

Serikali yaendelea kuimarisha ukaguzi wa Ndani Wizara na Taasisi za Serikali

$
0
0
Mkuu wa Ukaguzi wa ndani toka Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Mohamed Mtonga akiwaeleza waandishi wa Habari kuhusu miongozo mbalimbali iliyolewa na Serikali ikiwa ni moja ya hatua za kuimarisha vitengo vya ukaguzi wa ndani katika Wizara na Taasisi za Serikali kote nchini ili kuongeza tija,kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara Hiyo Bi. Ingiahedi Mduma na kushoto ni Kaimu Mkaguzi mkuu wa ndani bW. Chotto Sendo.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya fedha na Mipango uliofanyika leo jijini Dar es salaam ukilenga kuelimisha umma juu ya namna Serikali inavyochukua hatua katika kuimarisha vitengo vya ukaguzi wa ndani ikiwemo kuvipatia vifaa vya kisasa ili viweze kutimiza majukumu yake kwa ufanisi.

NHIF YATAMBUA UMUHIMU WA WATOA HUDUMA ZA AFYA.

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeipongeza Manispaa ya Ilala kwa kutoa huduma bora za afya kwa wanachama wa mfuko huo.

Akizungumza na waandishi wa habari, katika ufunguzi wa mkutano wa watoa huduma wa afya uliofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Masoko,Elimu kwa Umma na Utafiti Othuman Rehani (Pichani)amesema kwamba Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unatambua mchango mkubwa unaotolewa na watoa huduma za afya kwa wanachama wao.

“Utoaji wetu wa huduma za afya za kijamii kwa wanachama wetu umekua ukitegemea Hospitali za Umma na Binafsi”alisema Rehani.

Mkurugenzi Othuman Rehani aliongeza kuwa NHIF wanaamini kwamba, ushirikiano na watoa huduma utasaidia Serikali yetu ya awamu ya tano kufikia lengo lake la kutoa huduma bora.

Aidha Rehani ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa Bima ya Afya mwaka 2001 yakiwemo; kupanuka kwa upatikanaji wa huduma kwa kuongezeka kwa vituo vya kutolea tiba vilivyosajiliwa na mfuko,usajili wa maduka ya dawa yalioongeza upatikanaji wa dawa hadi vijijini,utoaji wa mikopo ya madawa na vifaa tiba ili kuimarisha utoaji wa huduma za afya pia kuongezwa kwa vitita vya mafao kwa wanufaika waliokua wakiongezeka mwaka hadi mwaka.

Katika mkutano huo wadau mbalimbali wa afya waliohudhuria ni pamoja na Mganga Mkuu wa Wilaya,Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,Meneja Mfawidhi wa Mkoa wa Ilala na Wakurugenzi wa Hospital za Rufaa.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umetimiza miaka 14 toka ulipoanzishwa na kuanza utekelezaji wake mwaka 2001 ikiwa na watoa huduma za afya wale wa hospitali za Umma na Binafsi waliokamilisha usajili wao katika Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Wazee na Watoto.

TRL NA RAHCO WAAGIZWA KUKARABATI RELI NDANI YA SIKU 3!

$
0
0
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mbarawa  amezitaka Menejimenti za  Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na Kampuni Hodhi ya Reli Rahco kufanya kila linalowezekana kuondoa athari za mafuriko ya mvua zilizoikumba eneo la stesheni za  Kilosa na Mzaganza ambako reli imekatika.

Mhe Waziri ameutaka uongozi huo kutumia ujuzi wao wote na wahandisi na mafundi wake  kurejesha tuta la reli katika hali ya kawaida ili huduma ziweze kuanza ndani ya siku 3 zijazo.

Aidha aliwataka Viongozi na wananchi wa eneo hilo la Mzaganza na Kidete kuzingatia kilimo chenye tija ambacho kitazuia mmong’onyoko wa ardhi ambao unafanya mafuriko yatokee killa mwaka. Eneo la zaidi ya kilomita 2 la tuta la reli  limekumbwa na mmong’onyoka (wash away) na hivyo kulazimisha kusitisha huduma za reli tokea Januari 1, 2016.

Waziri Mbarawa akifuatana na Maafisa Waandamizi wa Wizara yake na wale kutoka TRL na Rahco alifika eneo hilo asubuhi jana Januari 3 , 29016 kukagua uharibifu huo unaosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi lakini pia na shughuliza kibinadamu  ambazo hazizingatia kilimo cha kisasa.

Wakati taarifa hii inaandaliwa uongozi wa Rahco tayari umeshaanza kufanya mchakato wa ununuzi wa vifaa maalum vinavyohitajiwa na TRL ili kuikamilisha kazi ya ukarabati  wa eneo hilo kama ilivyoagizwa na Mheshimiwa Profesa Mbarawa.

Akizingumza na waandishi wa Habari aliofuatana nao Waziri Mbarawa alisema uharibifu huo wa eneo la Kilosa , Kidete, Godegode na Gulwe muda wake  umeifika upatiwe ufumbuzi wa kudumu. Ameahidi muda sio mrefu  kuitisha  kikao cha wataalamu ili kutafakari kwa kina kadhia hiyo ambayo sasa inaonesha kuwa kaburi la mapato ya Serikali linapatiwa ufumbuzi wa kudumu. “ Haiwezekani vichwa vyote hivi Wizarani , Rahco, TRL, Sumatra vishindwe kuja na jibu” Alisisitiza Waziri.

Wakati huo huo Uongozi wa TRL umewaomba radhi wateja wake na wananchi kwa ujumla kwa usumbufu wa kukosekana huduma muhimu wanayoitegemea. Aidha umewahakikishia kuwa TRL ikiishirikiana na Serikali na tasisi zake husika inafanya jitihada za dhati  kurekibisha eneo lililoathiriwa na mafuriko na kwamba wawe na subira na muda sio mrefu huduma za reli zitarejea kama kawaida.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Elias Mshana.

Dar es Salaam,
Januari 04, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE SAMIA AWASILI MKOANI GEITA KUANZA ZIARA LEO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Geita Mhe. Fatma Mwassa alipowasili Uwanja wa Ndege wa GGM Geita leo Januari 04,2016 kwa ajili ya kuanza ziara ya siku mbili  ya kukagua  na kuzindua miradi ya maendeleo Mkoani humo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na akina mama wa UWT Geita alipowasili Uwanja wa ndege wa GGM Geita Leo Januari 04, 2016 kwa ajili ya kuanza ziara ya siku mbili ya kukagua na kuzindua mirdeleo Mkoani humo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya wawekezaji wa Mgodi wa GGM Mkoani  Geita alipowasili Uwanja wa ndege wa GGM Geita Leo Januari 04, 2016 kwa ajili ya kuanza ziara ya siku mbili ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo Mkoani humo. (Picha na OMR).


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA NFRA NA UJENZI WA OFISI YA MKURUGENZI PERAMIHO

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mahindi yaliyohifadhiwa nje ya majengo ya maghala ya  Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA mjini Songea  akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Ruvuma Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mahindi yaliyohifadhiwa nje ya majengo ya maghala ya  Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA mjini Songea  akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Ruvuma Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mahindi yaliyohifadhiwa nje ya majengo ya maghala ya  Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA mjini Songea  akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Ruvuma Januari 4, 2016.  
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Jego la Halmashauri ya Wilaya ya Peramiho akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Januari 4, 2015.  
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Maposele wilayani  Peramiho baada ya kukagua ujenzi wa  jingo la Ofisi ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma  Januari 4, 2016. (PIcha na Ofisi a Waziri Mkuu
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungungua tawi la Benki ya Posta la Songea akiwa katika ziara ya mkoa wa  Ruvuma Januari 4, 2016. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Uratibu, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama .
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akitazama kadi ya akaunti yake ya Benki ya Posta Tanzania aliyokabidhiwa  baada ya kuifungua alipokuwa akifungua tawi la Benki hiyo la Songea Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassi Majaliwa akiagana na watuMishi wa Benki ya Posta, Tawi la Songea baada ya kufungua tawi lao Januari 4, 2016. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Rukwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
(Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akivalishwa vazi la jadi la  Wangoni baada ya kuwasili kwenye   kwenye kijiji cha Maposele  na kukagua ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Peramiho Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikabidhiwa  ngao silaha  na mzee Daniel Gama  baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Maposele  na kukagua ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Peramiho Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikabidhiwa silaha za jadi na mzee Daniel Gama  baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Maposele  na kukagua ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Peramiho Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma ya mila ya kabila la Wangoni wakati alipowasili    kwenye kijiji cha Maposele  na kukagua ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Peramiho Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA WAGENI MBALIMBALI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Profesa Mussa Juma Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Profesa Mussa Juma Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuber Ally Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuber Ally, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MheshimiwaDkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Mkurugenzi wa Mashtaka DPP Bw. Biswalo Eutropius Mganga Ikulu jijini Dar es Salaam. 


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Alhaji Abdallah Bulembo aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Alhaji Abdallah Bulembo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Picha zote na IKULU.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA TAWI JIPYA LA BENKI YA POSTA MJINI SONGEA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassi Majaliwa, (wapili kulia), waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu, (sera, uratibu, na watu wenye ulemavu), Bi. Jenista Mhagama, na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Bw. Sabasaba Moshingi, (wakwanza kushoto) wakikata utepe kuashiria kufunguliwa kwa tawi jipya la benki hiyo mjini Songea leo Januari 4, 2015. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akitazama kadi ya akaunti yake ya Benki ya Posta Tanzania aliyokabidhiwa  baada ya kuifungua alipokuwa akifungua tawi la Benki hiyo la Songea Januari 4, 2016
 Waziri Mkuu akiagana na watuishi wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, baada ya kufungua tawi la benki hiyo mjini Songea Januari 4, 2016. Watatu kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bw. Sabasaba Moshingi, na wapili kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa benki hiyo Bi.Mystica Mapunda Ngongi
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Bw. Sabasaba Moshingi, akimkabidhi zawadi ya saa ya ukutani yenye nembo ya TPB, Waziri Mkuu Kassim majaliwa, baada ya waziri Mkuu  kufungua tawi jipya la benki hiyo mjini Songea leo Januari 4, 2016. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Bw. Said Mwambungu

WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU AKAGUA KAMBI YA KIPINDUPINDU YA NYANKUMBU MKOANI GEITA

$
0
0
Wananchi wa Mkoa wa Geita wameaswa kufuata kanuni za usafi wa mazingira ili kudhibiti maumbukizi ya ugonjwa wa kipindupindu,Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu mara baada ya kutembelea kambi ya kipindupindu iliyopo kwenye kituo cha afya cha Nyankumbu,mkoani hapamli1
Waziri Ummy akivaa vifaa maalum vya kujikinga na kipindupindu kabla ya kuingia kwenye kambi hiyo,kulia ni Mganga mfawidhi wa Kituo hicho Josephat Msafiri.(Picha Zote na Catherine Sungura WAMJW-GEITA)
mli2 
  Waziri Ummy akivua vifaa hivyo mara baada ya kutoka kuwasalimia wagonjwa wa kipindupindu waliolazwa kwenye kambi hiyo,wagonjwa waliopo hadi leo mchana ni wagonjwa wanne mli3 
  Waziri huyo akiongea na mmoja wa wagonjwa wa kipindupindu waliolazwa kwenye kambi hiyo mli4 
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasalimia wagonjwa wa kipindupindu(hawapo pichani)kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dkt.Joseph Kisala mli5 
  Baadhi ya wagonjwa wa kipindupindu waliolazwa kwenye kambi ya kituo cha afya cha Nyankumbu

NEWS ALERT:MWIGULU NCHEMBA ATIMUA VIGOGO WALIOKULA BILION 5.7 ZA UJENZI WA MACHINJIO YA KISASA RUVU

$
0
0
Wakati Taifa na Mataifa yakiendelea kutoa pongezi zao kwa serikali ya Rais.J.P.Magufuli kwa speed yake ya kuchapa kazi,Mawaziri wake pia wameendelea kuonesha namna walivyodhamiria kusimamia shughuli za maendeleo ya Nchi yetu.

Hii leo,Mh:Mwigulu Nchemba mwenye dhamana ya Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi amefanya ziara ya siku moja kwenye ranchi ya Taifa ya Ruvu kukagua ujenzi wa majengo ya machinjio ya kisasa ulioanza mwaka 2010.

Katika hali ya kusikitisha na kulazimu kuchukua hatua za kinidhamu,Mwigulu Nchemba amekutana na ubadhilifu wa Bilioni 5.7 ambazo zilitolewa kwaajili ya ujenzi wa jengo hilo,Fedha hizo zilizokuwa zimelengwa kuwezesha ujenzi wa machinjio hayo ya kisasa hazijafanya kazi kama ilivyokusidiwa.

Waziri huyo wa kilimo amekuta mradi huo umetelekezwa tangu mwaka 2010 bila kuendelezwa,Sababu za kutelekezwa kwa mradi huo zikidaiwa kuwa ni kutofautiana kwa mkandarasi na bodi ya NARCO(kampuni ya usimamizi wa ranchi za Taifa) hazikukubalika na Mh:Mwigulu Nchemba ambaye baada ya kusikiliza kwa makini ufafanuzi wa kutoka kwa viongozi wa ranchi hiyo aliamua ifuatavyo.

Kwanza,Mwigulu Nchemba amewatimua wakurugenzi wote wa bodi ya NARCO yenye dhamana ya kusimamia ranchi za Taifa kwa kushinda kukamilisha ujenzi wa mradi huo.Mbali na kushindwa,bodi hiyo imeutelekeza mradi huo na hivi sasa inapendekeza kujengwa kwa mradi mwingine kama huo ndani ya eneo hilohilo la ranchi ya ruvu.

Pili,Mwigulu Nchemba amesitisha utumishi wa Mkurugenzi mkuu wa ranchi za Tiafa kwa kushindwa kuchukua hatua za kusimamia ujenzi wa mradi huo hadi kukamilika kwake.

Pia,waziri huyo wa kilimo ameagiza kupitia vyombo vya sheria,wahusika wote walioshiriki ama kwa makusudi au kwa njia yoyote kuhujumu mradi huo usifanikiwe wanachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo.

Mwisho,Nchemba amewaagiza wataalam wa wizara yake kuhakikisha ndani ya siku 7 wanampelekea ripoti ya thamani ya jengo lililokwisha kujengwa na fedha zinazotakiwa kumalizia ujenzi wa jengo hilo.

Sambamba na hatua hizo,Mwigulu ametoa rai kwa watumishi wote wa umma kuwa mstari wa mbele kusimamia kwa ufanisi na uzalendo miradi yote ya maendeleo ya nchi yetu,Mbali na hapo,serikali ya Magufuli haitakuwa tayari kuona mali ya umma inachezewa na kuibiwa wakati kuna watanzania wanaweza kusimamia mali hizo na kuziendeleza.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi akiwasili kwenye mradi uliodumaa wa Ujenzi wa machinjio ya kisasa wa ranchi ya Ruvu mapema hii leo.Sehemu ya jingo lililobaki kama Gofu mara baada ya kutelekezwa na Uongozi wa Bodi ya ranchi za Taifa(NARCO)Mwigulu Nchemba akishangaa namna mali hii ya Umma ilivyotekelezwa.Mwigulu Nchemba akiwa na Mbunge wa Chalinze Mh.Ridhiwani wakisikiliza kwa makini sababu zilizopekea jingo hilo kutelekezwa.Anayetoa maelezo wa mwisho kushoto ni msimamizi wa ranchi hiyo Ngd.Bwire.Mwigulu Nchemba akiendelea kupewa maelezo ya kina kuhusu ubadhilifu uliojitokeza kwenye ujenzi huu.Mh.Ridhiwani kikwete Mbunge wa Chalinze akitoa malalamiko yake kwa Waziri.Mwigulu Nchemba kuhusu kukosekana kwa mahusiano mazuri kati ya wamiliki wa ranchi na wananchi wanaozunguka ranchi ya Ruvu.Mwigulu Nchemba akidadisi utunzaji wa maji ya Mifugo inayopatikana ndani ya ranchi ya Ruvu.Picha/maelezo na Festo Sanga Jr.

Pam D Ft Mesen Selekta – Popo lipopo (Official Video)

WATANZANIA MSIKUBALI KUTOZWA RUSHWA KWA AJILI YA DAMU, TOA TAARIFA KWA NESI, DAKTARI ATAKAYETOZA DAMU!- DK. KIGWANGALA

$
0
0
IMG_0681
Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma akitoa maelezo ya namna wanavyoendesha shughuli zao kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kigwangalla aliyefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo, Januari 4, 2016. (Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
IMG_0770
Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma akimwonyesha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla moja ya damu ambayo ni maalum kwa wamama wajawazito wakati wa kujifungua zilizohifadhiwa kwenye jokofu katika mabara hiyo.
IMG_0760
Mmoja wa watumishi katika maabara ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama (ambaye jina lake halipatikana) akiendelea kutekeleza majukumu yake kama alivyokutwa na mpiga picha wetu.

Na Modewjiblog, Team.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza watanzania wote wasikubali kutozwa rushwa kwa ajili ya damu salama na baadala yake kwa mtu atakayefanya hivyo watamchukulia hatua kali.

Kauli hiyo imetolewa mapema Januari 4 (jana) na Naibu huyo wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Kingwangalla alipofanya ziara katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dares Salaam.

Dk. Kigwangalla amefafanua kuwa, kwa watu wote ikiwemo Nesi, Daktari ama mtaalamu wa afya, atakayemtoza mtu damu, atachukuliwa hatua kali ikiwemo kufukuzwa kazi.“Kwa watanzania wote, msikubali kutoa rushwa kwa ajili ya damu. Na kama itatokea Nesi ama Daktari ama nani, anakuambia ulipie ili upate damu!. Kwa sababu kuna uhaba wa damu kwa sasa.. Ripoti kwa Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa ama Daktari Mkuu husika ama fika Wizara ya afya moja kwa moja na kuna namba tutaitoa kwa watanzania wote mtupatie ripoti.


Mtu atakayekutoza damu, wewe tuambie, huyo tutamfukuza kazi moja kwa moja, hatuwezi kuendekeza watu wa namna hii... Serikali inaingia gharama kubwa kukusanya damu kwa watu, Kuna watu wanajitolea damu zao bure. Leo wewe nesi ama mganga ukauze damu, hilo jambo hatutakubali hata kidogo kwa hiyo natoa rai kwa watanzaia hiyo damu ni bure na haiuzwi na usikubali kuuziwa damu hata kidogo.” Ameeleza hilo Dk. Kigwangalla.

Awali katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla ameipongeza Ofisi ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama kwa kazi wanayofanya na ubunifu waliofikia wa kuhusisha Halmshauri katika ukusanyaji wa damu huku wao wakisimamia kudhibiti viwango vya damu ya matumizi kwa watanzania huku akitumia wasaha huo kutoa maelekezo ya kuboresha mfumo wa motisha kwa wanaochangia damu salama ambapo kwa wachangiaji damu kuingizwa kwenye mfumo wa kieletroniki wa kuwatambua watu wanaochangia damu, kutoa taarifa jinsi damu zao zilivyookoa miasha ya wagonjwa na kuwapa motisha ili waweze kuwa wachangiaji endelevu.

“Motisha sio soda na maji kwa wanaochangia damu. Motisha ni hata kupewa taarifa kwamba damu yake imesaidia kuokoa maisha ya mwanadamu mwenzake aliyekuwa anaumwa ugonjwa fulani, hii ni motisha kubwa sana kuliko hata pesa, ama soda ama maji yanayotolewa anapochangia damu.

Lakini kama imeshajitokeza mtu kuwa na tabia ya kuchangia damu, huyu sio wa kumpoteza, maana yake kuna uwezekano mkubwa wa akarudi tena kuchangia damu, mtu huyu ni lazima kuwe na mfumo wa kielekrioniki wa komputa wa kumtakia salamu, taarifa na anakuwa kwenye database yenu.

“Mnatakiwa muwe na mfumo wa kumpa taarifa pindi damu yake imetumika, ikiwemo kumueleza kuwa damu yako imemsaidia Mama mjamzito aliyejifungua na kutokwa damu nyingi, na mtu huyo akipata taarifa hiyo ni motisha tosha hivyo ni lazima muwe na huo mfumo kutoa motisha zaidi.
IMG_0689
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla na msafara wake wakishuka ngazi kuelekea kukagua idara mbalimbali katika ofisi hizo, Januari 4, 2016.

Awali akielezwa na Meneja wa kanda ya Mashariki katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Eveline Mgassa kwamba changamoto zilizopo katika upatikanaji wa damu nchini ni halimshauri kutenga bajeti za kutosha kwa ajili ya huduma hiyo, Kwa hatua hiyo, Dk. Kigwangalla ameziagiza Halmshauri zote nchini kuhakikisha zinatenga bajeti za kutosha ilikusapoti mpango wa damu salama.
Katika hilo Dk. Kigwangalla ameapa kuwashughulikia wale wote watakaozembea na kuwachukulia hatua kali Ma DMO, Wakurugenzi na kushtakiwa kwa mamlaka zilizopo na kufukuzwa kazi.

“Naziagiza Halmashauri zote kuhakikisha zinatenga bajeti za kusapoti mpango wa ukusanyaji damu salama. Na Halmashauri zitakazoshindwa, DMO na Mkurugenzi wake tutahakikisha tunawashtaki kwa mamlaka zilizowateua ili uteuzi wao ukome mara moja. Maana hatuwezi kuacha akinamama wajawazito wapoteze damu wakati wa kujifungua, watu wanaopata ajali wapoteze maisha kwa sababu ya watu hawataki kutimiza wajibu wao.

Hilo haliwezi kukubalika, Mfumo wa hali ya damu kwa Tanzania kwa sasa unatisha. Kwa sasa nchi inakiwango cha chini mno, tokea wafadhili wajiondoe katika hili. Ni lazima tuwe makini sana maana leo mzima kesho umepata ajali, umepasuka mfupa wa kwenye paja damu nyingi zimemwagika unahitaji damu!!

Kwa upande wa watu wote wanaopata damu salama nchini, huduma hiyo wanazipata bure kwani damu hizo ni za Serikali, Hata hivyo mifuko na vitu vinavyotumika kuhifadhia damu hiyo vina gharama kubwa.

“Damu inatolewa bure na serikali. Mtambue kuwa, vifaa vya kutunzia damu hii ni gharama kubwa. Hivyo mifuko mashirika ya Bima, na mashirika mengine kuanzia leo kutazama namna ya kulipa gharama za vifaa vya utunziaji damu hizo. Damu ni bure, lakini mfuko ule wa kutunzia ile damu ni gharama kubwa sana na hata vifaa vya kupimia damu ile nayo ni gharama kubwa hivyo walipie kwa kila damu watakayochukua.” Alieleza Dk. Kigwangalla.
IMG_0703
Meneja wa kanda ya Mashariki Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Eveline Mgassa (mwenye miwani) akielezea utaratibu wa ukusanyaji wa damu unavyofanyika kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla aliyefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo, Januari 4, 2016 jijini Dar.
IMG_0690
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla (aliyeipa mgongo kamera) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma ya namna wanavyopokea watu wanaofikia kuchangia damu kwa hiari na kuhifadhiwa kwenye benki hiyo yaTaifa ya Damu Salama, alipofanya ziara ya kushtukiza, Januari 4, 2016 katika ofisi hizo.
IMG_0725
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akitoa mkono wa pongezi kwa wananchi walioonyesha uzalendo kwa kufika katika ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Januari 4, 2016 na kuchangia damu kwa hiari yao ambapo mmoja kati yao alisema hii ni mara yake ya nne na ni utararibu aliojiwekea.
IMG_0729
IMG_0743
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akisalimiana na kumpongeza mmoja wa wananchi (jina lake halikuweza kupatikana) aliyefika kuchangia damu kwa hiari, Januari 4, 2016 katika makao makuu ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama.
IMG_0764
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akiwa ndani ya maabara ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi hizo, Januari 4, 2015 jijini Dar es Salaam.
IMG_0774
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akisaini vitabu vya wageni nje ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Januari 4, 2016 wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo.
IMG_0826
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya ziara ya kushtukiza na kuzungikia vitengo mbalimbali katika ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama jijini Dar es Salaam.

MBUNGE WA AFRIKA MASHARIKI NDELAKINDO KESSY AWAKUMBUKA WATOTO KATIKA KUUANZA MWAKA 2016.

$
0
0

Mkurugenzi wa Mambo ya nje wa Chama cha NCCR-Mageuzi na Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki,Ndelakindo Kessy akizungumzia utaratibu ambao chama hicho umeuanzisha wa kusaidia watoto waishio katika mazingira magumu katika jimbo la Vunjo.

Baadhi ya watoto kutoka kata 16 za jimboo la Vunjo walioandaliwa sherehe ya kuukarbisha mwaka mpya wa 2016 na Chama cha NCCR-Mageuzi katika jimbo la Vunjo.
Mbunge wa Viti Maalum kupitia chama cha NCR-Mageuzi,Corona Kundi akizungumza na watoto

Baadhi ya watoto wlfika kwa ajili ya sherehe hiyo.
Mbunge w viti maalum kpitia NCCR-Mageuzi Eveline Lyimo akiongea na watoto.




Watoto wishio katika mazingira magumu wakifurahia wakati wa sherehe iliyoandaliwa na Mbunge wa jimbo l Vunjo,James Mbatia pamoja na mbunge wa afrika mashariki,Ndelakindo Kessy.


Mbunge Ndelkindo Kessy akiongea na watoto.












Watoto wakichukua Chakula .







Watoto wakila Chakula.

WIZARA YA MAJI YAMUAGA NAIBU KATIBU MKUU INJ. MWIHAVA, YAMKARIBISHA INJ. KALOBELO

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Inj. Emmanuel Kalobelo akipokea nyaraka  kama ishara ya kukabidhiwa rasmi ofisi kutoka kwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Inj. Ngossy Mwihava, wakishuhudiwa na Katibu Mkuu, Inj. Mbogo Futakamba.

Wizara ya Maji imemuaga rasmi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Inj. Ngossy Mwihava na kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu mpya, Inj. Emmanuel Kalobelo katika Makao Makuu ya Wizara hiyo Ubungo Maji jana.

 “Naomba ushirikiano wenu ili tuweze kufanikisha azma ya kuleta maendeleo kwenye Sekta ya Maji, na nasisitiza kufanya kazi kwa bidii na kujituma kwetu sote ili tulete faraja kwa wananchi”, alisema Naibu Katibu Mkuu, Inj. Emmanuel Kalobelo katika hafla fupi ya kutambulishwa na makabidhiano ya ofisi.
 Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Inj. Ngossy Mwihava akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Inj. Emmanuel Kalobelo ofisini kwake, kabla ya kumkabidhi ofisi.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Inj. Mbogo Futakamba (katikati), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Inj. Emmanuel Kalobelo (kushoto), aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Inj. Ngossy Mwihava (kulia) na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Gideon Manambo.
 Naibu Katibu Mkuu, Inj. Emmanuel Kalobelo akizungumza na Menejimenti ya Wizara ya Maji mara baada ya kutambulishwa.
 Menejimenti ya Wizara ya Maji ikimsikiliza Katibu Mkuu, Inj.  Mbogo Futakamba alipokuwa akizungumza.

WANASIASA WADAIWA KUKWAMISHA SHUGHULI ZA URAGHABISHI WILAYA YA SHINYANGA VIJIJINI

$
0
0
Mchungaji wa kanisa la Umoja wa Makanisa ya Ubatizo Lucas Machibya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu baadhi ya shughuli za uraghabishi katika kijiji cha Pandagichiza. 
Baadhi ya waraghabishi wa kijiji cha Pandagichiza wakiwa na waandishi wa habari za mtandaoni katika moja ya jengo la jiko la shule ya msingi Pandagichiza ambalo limetoakana na juhudi zao za uraghabishi 


Na Krantz Mwantepele ,Shinyanga 

Si mara nyingi viongozi wa kidini hujihusisha moja kwa moja na harakati za kisiasa ila wamekuwa mstari wa mbele kukemea matendo yanayofanywa na wanasiasa. Hawafanyi hivyo kwa bahati mbaya ila kutokana na nafasi yao katika jamii, hususani kuwaongoza waumini wao kwenda mbinguni. 

Hata hivyo, hii haimaanishi hakuna kabisa viongozi wa dini waioamua kujiingiza katika harakati za siasa ili kuleta maendeleo ya watu kwa haraka na ufanisi. Mchungaji Lucas Machibya ni mmoja kati ya viongozi wachache wa dini wanaoingia katika siasa. 

Huyu ni mchungaji wa kanisa la Umoja wa Makanisa ya Ubatizo lililopo katika kijiji cha Pandagichiza chenye wakazi wanaokadiriwa 2,481, idadi kubwa ikiwa ni ya wanawake wanaokadiriwa kufikia 1,476. Hiki ni moja ya vijiji vilivyopo wilaya ya Shinyanga Vijijini, jimbo la Solwa.

Machibya ni mmoja wa wachungaji waraghbishi toka mkoa wa Shinyanga ambao uraghbishi wao umepelekea wananchi kumchagua kuwa mwenyekiti wa kijiji. Kujibainisha kwake kama mtu mwenye uwezo wa kusimamia anachokiamini na kushawishi wananchi kutambua majukumu na haki zao na jinsi ya kuzidai vimekuwa nguzo yake kubwa ya kukubalika.

Kama walivyo wananchi wengi wa kijiji chake, yeye ni mkulima mdogo ambaye pia ni mwanachama wa Mtandao wa Wakulima Wadogo Tanzania (MVIWATA). Kupitia mwaliko wa mkulima mwenzake, Elizabeth Edward, Machibya amefanikiwa kupata maarifa ya uraghbishi na jinsi ya kufanya uraghbishi; uwezo wa kuwashawishi na kuwahusisha ama kuwachokoza watu ili waweze kujitambua na kutojiona wao ni wa jamii ya chini. 

Sifa iliyomfanya aalikwe kwenye mafunzo ya uraghbishi ni uwezo wake wa kuhoji mambo mbalimbali pasipo kukata tamaa kama anavyosema mwenyewe:

“Mimi ni mtu wa kuhoji vitu na si mtu wa kuridhika ama kukaa kimya n’napoona kuna jambo sijalielewa. Kwa kweli yale mafunzo yalinifanya kujiona mtu tofauti sana nikijilinganisha na nilivyokuwa awali. Nilijihisi tayari nimekuwa mtaalamu wa masuala ya uwajibikaji na utawala bora.”

Kwa kuwa wao ni wakulima, walianza uraghbishi wao kwa kutaka kujua nini kinaendelea kuhusu bei ya pamba. mchungaji Machibya anaeleza ilivyokuwa:
“Kule tulifundishwa jinsi ya kuuliza maswali. Na cha kwanza tulichotaka kujua ni kwa nini bei ya zao letu la pamba imeshuka sana. Hili tuliliuliza sisi sote, mimi na waraghbishi wengine.”

Hawakuishia hapo tu bali wakaanza pia kufuatilia mapato na matumizi ya fedha za kijiji toka kwa viongozi wao. Walifanya hivyo kwa kuwatembelea ofisini na kuomba kupatiwa taarifa hizo na pia walitaka kufanyika mikutano ya hadhara. Baada ya harakati hizo kushika kasi, iliwabidi waongeze watu wengine zaidi kwa kuwatembelea majumbani kwao na kuwaraghbisha.

“Mchungaji aliomba kunitembelea nyumbani na alipofika alinipatia elimu. Kimsingi, alitaka nijitambue kwa kujua wajibu na haki zangu. Alinitaka nisiogope kuuliza maswali kwenye mikutano kwa kuwa tuna uhuru wa kufanya hivyo. Nikajua kuwa nina wajibu kuuliza na kujua mapato ya fedha za kijiji na na matumizi yake kuwa hiyo ni haki yangu,” anaeleza Bw. Daudi Denis toka kijiji cha Pandagichiza.

Kufanikisha haya yote kumewajengea uaminifu mkubwa sana waraghbishi na baadhi yao wamekuwa wakishirikishwa katika vikao muhimu vya maendeleo na serikali yao ya kijiji. Baadhi yao wametokea kuaminika zaidi na jamii kiasi cha kuombwa wagombee nyadhifa mbalimbali za uongozi wa serikali na ndani ya vyama vya siasa kama ilivyokuwa kwa mchungaji Machibya.

Hivyo basi, waraghbishi wengi wanaojihusisha na siasa wamejikuta wakinasa katika mtego huu wa migogoro ya kimaslahi kati ya shughuli zao za uraghbishi na zile za kisiasa kwa kuchukiwa na baadhi ya watu wanaotofautiana kimlengo wa kisiasa na kuonekana wasaliti na watu wasiokuwa na misimamo.

Wakati mwingine wanachukiwa ikidhaniwa kuhoji kwao mara kwa mara ni njia ya kujitafutia mtaji wa kisiasa na si kuwatumikia wananchi na kuibua maovu kwa maslahi ya jamii nzima na kwamba uraghbishi unawanufaisha wao binafsi na vyama vyao tu.

Uraghbishi ulimuingiza mchungaji Machibya kwenye mgogoro mkubwa na walinzi wa jadi, Sungusungu. Katika maeneo mengi ya Kanda ya Ziwa walinzi hawa wamekuwa na nguvu kubwa na wakati mwingine wanaweza kutoa adhabu kali kwa yeyote anayebainika kutenda kosa. 

Tofauti hiyo na Sungusungu ilisababisha yeye na waraghbishi wengine sita kukamatwa na kutozwa faini ya shilingi laki tano na elfu sitini (560,000/=) kwa mpigo kwa kisingizio cha kuvuruga amani katika kijiji hicho. Hii ni kwa sababu tu walikuwa wanauliza maswali kuhusu mapato yanayotokana na faini na michango mingine toka kwa wanakijiji. 

Vitisho na maonyo ya uongozi viliwapunguza kasi baadhi ya waraghbishi na kuingiwa hofu kiwa wangefikishwa pabaya zaidi ya hapo. Ila mchungaji Machibya hakuishia hapo bali aliendelea na shughuli hizo kama kawaida. Baadaye aliteuliwa kuwa katibu wa mtandao wa waraghbishi na huko ndiko alikojizolea uaminifu na umaarufu zaidi baada ya kuanza kujihusisha na kuhoji mambo makubwa ya kiutawala na utendaji kijijini hapo. 

Hiyo ilimwongezea hamasa ya kuendelea kuwatumikia watu kwa kuongeza juhudi katika shughuli za uraghbishaji na kufikia hatua ya kuombwa na wananchi kugombea wadhifa kichama (siasa) na uongozi katika serikali ya kijiji. 

Na mwaka 2014 wakati wa mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa ukiendele, ndipo yeye alijikita kwa dhati kuomba nafasi ya kugombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kufanikiwa kuteuliwa kugombea. Akielezea ilivyokuwa, mchungaji Machibya anasema: 

“Wapinzani wangu walipojua kwamba mimi ndio nimepitishwa waliamua kujitoa katika vyama vyao na kuniunga mkono. Hii kwa sababu hawakuona sababu ya kupingana nami kwa kuwa wanafahamu uwezo na umakini wangu kiutendaji na kiuwajibikaji.”

Matokeo ya harakati hizo ni kwamba Mchungaji Machibya alichaguliwa kwa kishindo kuwa mwenyekiti wa kijiji na baadaye alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa wenyeviti wa wilaya nzima. Sanjari na nafasi mwenyekiti wa kijiji, aliendelea pia kushika nyadhifa nyingine ikiwamo kuwa mraghbishi kiongozi na mchungaji. 

Hizi ni nyadhifa nyingi zinazoambatana na majukumu mengi kwa mchungaji Machibya hivyo kujikuta kwenye mazingira magumu sana ya kutumikia nyadhifa zote. Lakini pia alipata upinzani mkali sana kutoka kwa viongozi wengine na hata wakati mwingine kushindwa kusimamia kwa pamoja majukumu yote. 

Huku ni mraghbishi na huku ni mwenyekiti wa kijiji. Hii haikuwa changamoto ndogo kwake. Akifafanua hilo, mchungaji Machibya anasema:

“Kwa sababu nilikuwa kiongozi wa waragbishi ilikuwa ni kama nayajua maswali kabla ya mtihani na wenzangu walikuwa wanashindwa kuhoji vizuri kwa kuwa mie ni kiongozi wao. Ndipo nikaamua kujitoa uongozi na kuwa mraghbishi wa kawaida, lakini sikuishia hapo nikajivua na majukumu ya uchungaji wa kanisa japo ni shughuli niliyoipenda sana na kuwa mzee wa kanisa kawaida.”

Kwa haraka haraka, unaweza kusema shughuli ya kuhoji mwenzio inafanana na kuhojiwa wewe binafsi. Mwanzoni alipata ugumu kidogo kwa sababu kila mwananchi alikuwa anategemea mabadiliko ya haraka wakati vitu vingine vilikuwa kimfumo zaidi. Hiyo ilimfanya achelewe kutoa majibu ya haraka. 

Na ili asiangukie kwenye dimbwi la lawama, alihakikisha anakuwa muwazi kwa wananchi na viongozi wake wa karibu katika kila jambo. 

Kuna mbinu kadhaa alizotumia ikiwa ni pamoja na kuteua viongozi wa halmashauli ya kijiji wanaoendana na falsafa yake ya uwazi na uwajibikaji na pia aliendelea kuwatumia waragbishi wenzake katika kuibua mambo pale alipohisi yanakwama.

Mchungaji Machibya anafahamu kwamba yeye kama kiongozi ana wajibu wa kuwa na uelewa wa mambo mbalimbali ikiwemo sheria na sera za nchi. Kwa kuelewa hilo, alipoanza kutafuta fursa za mafunzo ya uongozi na kukutana na mashirika mbalimbali yaliomwezesha kupata elimu. 

Hakuishia hapo bali aliendelea kujenga mizizi ya waraghbishi wengi zaidi na mpaka sasa amefanikiwa kuwajengea uwezo wenyeviti wenzake 40 kati ya 126 wa wilaya nzima, na bado anaendelea kutafuta maarifa mengine ili awape wenzake.

Kwa nafasi yake, anatafuta wadau na mashirika yenye ujuzi huo ili awezeshe wenyeviti wote kupata mafunzo kwani wengi wao wanatawala wananchi kimazoea tu. Hawana ufahamu wa namna nzuri ya kutekeleza majukumu yao.

Kwa misingi hiyo, mchungaji Machibya ameamua kutumia uraghbishi kama nyenzo ya kumuongezea ufanisi katika majukumu yake na si kutengeneza uadui na waragbishi kama ilivyo kwa viongozi wengi wa vyama na serikali. Kwa mfano huu, tunapata picha halisi ni kwa namna gani uragbishi ukichukuliwa kwa mtazamo chanya unakuwa nyenzo muhimu ya kuongeza chachu ya utawala bora katika serikali zetu za mitaa, kijiji na taifa kwa ujumla. Na kwa sasa, anapambana na mambo makuu matano ikiwa ni pamoja na mradi wa maji utakaomwezesha kukusanya kiasi cha shilingi 500,000. 

Pamoja na mapato mengine yanayokusanywa na Sungusungu pamoja na kuhamasisha kusomeshwaji kwa wingi kwa watoto wa kike. Na tayari hatua za makusudi za kuhakikisha kwamba malengo ya kuongeza mapato na hivyo kulipia watoto wa kike kuhudhuria shuleni zimeshachukuliwa. 

Hii ikiwa ni pamoja kupunguza adhabu kali za viboko, kuunda upya uongozi wa Sungusungu. Kwa upande wa mapato, wameweka mikakati ya wazi ya kuhakikisha mapato yanayopatikana yanasomwa mbele ya wananchi. Kwa upande wa shule, kila mzazi na jamii nzima imeandaliwa mikakati ya makusudi kuwawajibisha wale wote wanaoshindwa kuwapeleka watoto wa kike. Waraghbishi wamekuwa chachu kubwa katika uvumbuaji wa taarifa pamoja na uelimishaji pia.

Jambo la kwanza kwa kiongozi yeyote anayetaka mafanikio katika uongozi wake ni kutanguliza maslahi ya wananchi kwanza kabla ya maslahi binafsi au ya chama chake. Kinyume na hivyo anaweza kutia doa hata huo uraghbishi wake. Utu wa mtu hupimwa kwa matendo yake na hata mtazamo wa watu anaowaongoza. 

Viongozi wengi wanatumia uraghbishi kama nyenzo ya kujijengea umaarufu wakati wenyewe ni kama hulka ama tabia ya mtu kupenda haki na mambo yakiwa yanasonga. Kwa hiyo unaweza kukuta waraghbishi wengi sana kama matendo yako yatalenga kukomboa watu na si maslahi binafsi.

Jambo lingine ambalo alisisitiza ni kwamba hawa viongozi wawe na utamaduni wa kutafuta maarifa na si kusubiri fursa za kuletewa tu na wahisani. Kiongozi bora ni lazima aendane na mabadiliko ya kila siku na si kuongoza watu kwa mazoea. Binadamu wanabadilika kila siku, hivyo kuna umuhimu wa kuonesha tofauti kati ya kiongozi mraghbishi na wa kawaida. Hiyo itaibua mwamko mkubwa wa viongozi wengi kuwa waraghbishi.

Kiongozi asiyejua sheria na sera za nchi ni sawa na kipofu. Siri ya elimu na ufahamu ipo kwenye maandishi, mafunzoni na kwenye semina elekezi kwani bila kufanya hivyo utauchukia uraghbishi.

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA TAMISEMI

$
0
0


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA - TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb) kwa Mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 2(2) cha Amri ya kuanzisha Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), (The Executive Agencies) (The Dar Rapid Transit Agency) (Establishment) Order ) Tangazo la Serikali  namba 120 la 2007, amemteuaMhandisi Ronald Lwakatare kuwa Kaimu Mtendaji Mkuuwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es salaam (DART) kuanzia tarehe 04/01/2016.

Uteuzi huo unafuatia kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kwa aliyekuwa Mtendaji Mkuu Bibi Asteria L. Mlambo tarehe 23/12/2015. Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Ronald Lwakatare alikuwa Naibu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund Board) akishughulikia Ufuatiliaji na Tathmini. Mhandisi Lwakatare anatakiwa kuripoti na kuanza kazi mara moja.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Januari 05, 2016

Mhe. Kairuki akutana na watumishi wa ofisi yake

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angella Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa Ofisi yake (hawapo pichani) wakati wa kikao chake na watumishi hao kilichofanyika jana alasiri..
Katibu Mkuu mteule Ofisi ya Rais-Utumishi Dkt. Laurian Ndumbaro (kushoto) akipokea Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma (Standing Order) kutoka kwa aliyekuwa akishika nafasi hiyo Katibu Mkuu, Bw. HAB Mkwizu (kulia). Anayeshuhudia ni aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Tixon Nzunda. 
 Watumishi wa Ofisi ya Rais – Utumishi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angella Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Mhe. Waziri na watumishi wa ofisi hiyo kilichofanyika jana alasiri.
 Aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi, Bw. HAB Mkwizu akizungumza na Watumishi wa Ofisi ya Rais – Utumishi (hawapo pichani) wakati wa kikao cha Mhe. Waziri na watumishi wa ofisi hiyo kilichofanyika jana alasiri. 
 Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi, Bw. Tixon Nzunda akizungumza na Watumishi wa Ofisi ya Rais – Utumishi (hawapo pichani) wakati wa kikao cha Mhe. Waziri na watumishi wa ofisi hiyo kilichofanyika jana alasiri.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Dkt. Laurian Ndumbaro akizungumza na Watumishi wa Ofisi ya Rais – Utumishi (hawapo pichani) wakati wa kikao cha Mhe. Waziri na watumishi wa ofisi hiyo kilichofanyika jana alasiri.
Viewing all 46329 articles
Browse latest View live




Latest Images