Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 727 | 728 | (Page 729) | 730 | 731 | .... | 1904 | newer

  0 0

  Mchungaji Kiongozi wa Jimbo la Tarime Samweli Nyageswa akiwafungisha ndoa Bi.Mariam Baraka Binagi (wa pili kulia) wa Rebu Tarime, Mara pamoja na Mwalimu Godfrey Godwin Kihengu (wa pili kushoto) wa Nyansurura Tarime, Mara ikiwa ni katika ibada iliyofanyika jana Desemba 30,2015 katika Kanisa Anglikana Buhemba Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
  Picha na BMG (Binagi Media Group)
  Mchungaji Kiongozi wa Jimbo la Tarime Samweli Nyageswa akimkabidhi bwana harusi cheti cha ndoa
  Mchungaji Kiongozi wa Jimbo la Tarime Samweli Nyageswa akimkabidhi bibi harusi cheti cha ndoa
  Maharusi wakionyesha vyeti vyao vya ndoa.

  Bi.Mariam Baraka Binagi (Kushoto) akiwa pamoja na bwana harusi Godfrey Godwin Kihengu.
  Bibi harusi akimlisha keki bwana harusi
  Maharusi wakinyweshana Shampeni
  Maharusi Wakiwa katika picha ya pamoja na Wachungaji
  Maharusi Wakiwa katika picha ya pamoja na Wazazi wake akiwemo mama yake mzazi pembeni ya bibi harusi
  Maharusi Wakiwa katika picha ya pamoja na Wazazi wake
  Maharusi wakiwa pamoja na Wakwe zake
  Maharusi wakiwa katika picha ya pamoja na wadogo zao
  Bibi harusi akiingia Ukumbini siku ya Sendoff iliyofanyika juzi Desemba 29,2015
  Kushoto ni bi harusi akiwa ukumbini siku ya Sendoff iliyofanyika juzi Desemba 29,2015
  Bi.Mariam Baraka Binagi (Kulia) akiwa pamoja na bwana harusi Godfrey Godwin Kihengu (Kushoto)
  Kaka wa bibi harusi ambae pia ndie mmiliki wa BMG (Kushoto) akiwa pamoja na Mama Mzazi wa bibi harusi
  Kaka wa bibi harusi ambae pia ndie mmiliki wa BMG (Kulia) akiwa pamoja na dada wa bibi harusi
  "Tunawatakiwa Maisha Mema na Yenye Fanaka katika ndoa yenu na Mola azidi kuibariki"

  0 0

  Na Krantz Mwantepele .Kahama


  Wanawake ni nguzo muhimu sana katika uchumi wa watanzania wengi. Mwanamke ana ushawishi mkubwa na hasa pale anapoamua kuwa chachu ya maendeleo. Na hasa anapowezeshwa kufanya hivyo.


  Katika kufanikisha hili waraghbishi wameamua kutoa mafunzo ya uraghbishi kwa makundi mengine ya jamii. Mojawapo ya kundi hilo ni la wanawake. Waraghbishi wapya toka katika kijiji cha Nyandekwa, kati ya hao wapo 9 ambao ni wanawake.

  Mmoja wao ni Anna Alphonce, Mwenyekiti wa kitongoji cha Busolo, katika kijiji cha Nyandekwa. Akielezea jinsi alivyoanza uraghbishi alisema:
  “Mi niliona kuna kikundi wanakaaga humu karibu kila jioni. Na kila nilipokuwa napita jirani na hapa naona watu wamejaa, basi nikapenda namimi nijiunge nao na hasa baada ya kujua nini wanafanya. Na hapo ndipo nilipoanza uraghbishi,”
  Anna Alphonce (katikati) ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Busolo akifafanua jambo wakati akielezea uraghbishi anaofanya .


  Akiwa kama mwenyekiti mwanamke wa kitongoji aliweza kutumia nafasi yake kufanya uraghbishi kwa anaowaongoza. Kwa kuwa kilikuwa ni kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu, aliitisha mikutano kwenye kitongoji chake kwa lengo la kutoa hamasa ya wananchi kujitokeza kwa wingi. Kwa nafasi yake aliweza kuyafikia makundi ya wazee, vijana na wanawake. Ingawa kati ya hawa wanawake ndio walikuwa washiriki wazuri.

  “Msisitizo kwenye mikutano yangu ilikuwa ni kupiga kura kwa amani. Niliwasihi Vijana wetu wasiwe chanzo cha vurugu na badala yake wawe walinzi na kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika mazingira ya utulivu,”

  Haya ni maelezo ya mwenyekiti huyo akielezea jinsi alivyotumia nafasi yake kwenye kufanya hamasa ya amani. Akaongeza,
  “Kwangu mimi haya ni mafanikio kwa sababu kweli uchaguzi umefanyika kwa amani katika kitongoji change.” 


  Mraghabishi mwingine ni Matrida Peter toka katika kijiji cha Nyandekwa, yeye uraghbishi wake alifundishwa na Elizabeth Ngaljalina toka kijiji hicho hicho. Baada ya kufundishwa yeye alichoamua kufanya uraghbishi kwa vijana wa kijiji cha Nyandekwa pamoja na wale waliokuwa mashuleni pia.

  Akielezea jinsi ambavyo anafanya uraghbishi kwa vijana, Matrida anasema,

  “Nafundisha makuzi ya ujana ili kuweza kutimiza ndoto zao. Kwanza nawaelewesha kuhusu mabadiliko ya miili yao hasa wanapoingia hatua ya kubalehe na kuvunja ungo. Hii inawasaidia jinsi ya kujikinga na maambuzi ya virusi vya ukimwi.”

  Uraghbishi wake hauishii kwa vijana walio nje ya shule, hivyo alikwenda kumtembelea ili aweze kupata fursa ya kutoa elimu hiyo hasa kwa wanafunzi ya shule ya msingi. Walengwa wakubwa wakiwa ni wanafunzi wa kuanzia darasa la nne mpaka la saba. Akielezea rika la watoto hao, Matrida anasema:

  “Watoto wa siku hizi wana maumbo makubwa, hivyo hao wa darasa la nne mpaka la saba sio wadogo kiumbo na wengi ndio wapo kwenye huo umri. Wanahitaji mwongozo manake makuzi siku hizi yameachwa kwa wazazi na wao mda mwingine wanaona aibu kuongea nao,”

  Matokeo ya uraghbishi huu wa mwanamama Matrida ni kuongeza kwa watoto wenye uelewa wa mipango ya uzazi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi. Kwani maambukizi katika wilaya ya Kahama yapo juu kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini.

  Uraghbishi una maana tofauti tofauti kwa wanawake hawa wa kijiji cha Nyandekwa, kama anavyoelezea Mariam Stephano aliyeanza uraghbishi mwezi Septemba 2015:

  “Uraghbishi kwangu mimi ni kutetea haki za vijana na mabinti, na sio tu kutetea bali kujua na falsafa yake ya jinsi ya kutenda ili kufanikisha lengo hilo ninaloliangalia kama  ndio jukumu langu,”

  Wakati Suzan Stephano yeye analinganisha uraghbishi na haki za kikatiba. Huku akisisitiza umuhimu wa kuthaminiwa kwa mwanamke katika kijiji chao na taifa kwa ujumla. Na yeye pia anakiri kwa uraghbishi ni falsafa ya jinsi ya kutenda.


  Waraghbishi wanawake toka katika kijiji cha Nyandekwa wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kitongoji cha Busola akielezea uraghbishi wake katika ngazi ya kitongoji

  Mraghbishi mwingine ni Mwenyekiti wa kitongoji cha Bujika, Adam Joseph yeye alijiunga na uraghbishi mwezi Septemba 2015, kwa kutumia nafasi yake uwenyekiti alitambulisha uraghbishi kwenye kitongoji chake.


  “Cha kwanza nilichofanya ni kuongea na mtendaji wa kijiji na kukubaliana tunahitaji kufanya hamasa kwa vijana ili wawe wanafika katika mikutano ya vijiji. Hivyo nikaanza kupita kwenye vijiwe na kuwahamasisha vijana waweze kufika mikutanoni. Na tuliwalenga vijana wote wa kike na wa kiume,” anaelezea Adam.


  Vijana walimwambia mwenyekiti wao kwamba wao hawasikilizwagi wakija kwenye mikutano na hivyo hawaoni umuhimu wa kuja kwenye mikutano ya vijiji. Majibu haya yalimpelekea mwenyekiti kuitisha mkutano uliowausisha vijana na wazee kwa pamoja.


  “Nimeshaitisha mikutano miwili, muamko bado si mkubwa sana kwani bado vijana hawaoni umuhimu wa kushiriki mikutano hii. Lakini hili halinikatishi tamaa najua hapa ni mwanzo tu,” anaelezea Adam.  Kwa hakika hizi ni harakati za kweli katika kumwezesha mwanamke na jamii kwa ujumla. Waraghbishi kwa pamoja wanakili kwamba uraghbishi ni falsafa ya kutenda. Swali la msingi kwetu sote, je na sisi tunatenda na kama ndio tunatumia falsafa gani.                                     CHANZO; MWANAHARAKATI MZALENDO

  0 0

  Wachezaji wa Timu ya JKU wakisalimiana na Wachezaji wa Timu ya KVZ kabla ya kuaza mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya JKU imeshinda 2--0.
  Mchezo uliochezwa jioni mabao ya JKU yamefungwa katika kipindi cha kwanza na katika dakika ya 8 mshambuliaji wa Timu ya JKU Mbarouk Chande ameipatia bao timu yake katika dakika ya nane ya mchezo huo kipindi cha kwanza na Bao la ushindi la JKU limepatikana katika kipindi hicho cha kwanza katika dakika ya 35 ya mchezo huo lililofungwa na mshambuliaji wake Nassor  Mattar.
  Kocha Mkuu wa Timu ya KVZ King akifuatilia mchezo huo wakati timu yake ikiwa nyuma kwa mabao 2--0 
  Beki wa timu ya KVZ Juma Abdalla, akijiandaa kumzuiya mshambuliaji wa Timu ya JKU mwenye mpira Nassorv Mattar, wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar. 
  Mshambuliaji wa Timu ya JKU Mbarouk Chande(kulia) akimpita beki wa Timu ya KVZ Emill Wiliam  

  Mshambuliaji wa Timu ya JKU Mbarouk Chande, akimiliki mpira huku beki wa timu ya KVZ Emill William akijiandaa kumzuiya.  
  Mshambuliaji wa Timu ya JKU Mohammed Abdalla akimpiga chenga golikipa wa timu ya KVZ Yakub Bakari. hatimai mpira huo na kutoka nje ya uwanja. 

  Mshambuliaji wa Timu ya KVZ Masoud Abdalla mwenye jezi ya kijani akimpita mchezaji wa timu ya JKU  Mbarouk Chande. 
  Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot
  Zanzinews.com.

  0 0

  Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (katikati) akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuwatafuta washindi wa droo ya nne ya promosheni ya "Jaza Mafuta na Ushinde" inayowawezesha wateja wake kujipatia lita 40 za mafuta kwa kila mshindi wa droo hiyo kila wiki. Kulia ni Mkaguzi wa michezo ya kubahatisha nchini, Bakari Maggid, na kushoto ni Meneja wa Fedha wa Kampuni ya mafuta ya GAPCO Tanzania, Michael Chobu.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitangaza Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu Ikulu jijini Dar es Salaam jioni ya leo December 30, 2015. Kushoto ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, na kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakisikiliza kwa makini.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijiandaa kumkabidhi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue orodha ya Makatibu na Manaibu Katibu Wakuu aliowateua huku Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akishuhudia.PICHA NA IKULU


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa makatibu wakuu na manaibu Katibu wakuu katika Wizara mbalimbali.
  Walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
  1. Katibu Mkuu Kiongozi
  Balozi - Ombeni Sefue
  1. Katibu Mkuu Ikulu
  Peter Ilomo
  1. Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
  Dkt. Laurian Ndumbaro

  1. Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
  Mhandisi Mussa Iyombe (Katibu Mkuu)
  Dkt. Deo  Mtasiwa (Naibu Katibu Mkuu - Afya)
  Bernard Makali (Naibu Katibu Mkuu - Elimu)

  1. Ofisi ya Makamu wa Rais
              Mbaraka A. Wakili ( Katibu Mkuu)
              Mhandisi Ngosi Mwihava (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu)
  Erick Shitindi (Katibu Mkuu Kazi na Ajira)
  Mussa Uledi (Katibu Mkuu Bunge)
  Dkt. Hamis Mwinyimvua (Katibu Mkuu - Sera)

  1. Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
  Dkt. Frolence Turuka (Katibu Mkuu - Kilimo)
  Dkt. Mashingo (Katibu Mkuu Mifugo)
  Dkt. Budeba (Katibu Mkuu - Uvuvi)

  1. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
  Mhandisi Joseph. Nyamuhanga (Katibu Mkuu - Ujenzi)
  Dkt. Leonard M. Chamuliho (Katibu Mkuu - Uchukuzi)
  Profesa Faustine R. Kamuzora (Katibu Mkuu - Mawasiliano)
  Mary Sassabo (Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano)

  1. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
  Dkt. Yamungu Kayandabira (Katibu Mkuu)
  Dkt. Moses Kusiluka (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Maliasili na Utalii
  Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi (Katibu Mkuu)
  Anjelina Madete (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
  Dkt. Adelhem James Meru (Katibu Mkuu - Viwanda)
  Profesa Adolf F. Mkenda (Katibu Mkuu - Biashara na Uwekezaji)
  Mhandisi Joel Malongo (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
  Maimuna Tarishi (Katibu Mkuu)
  Profesa Simon S. Msanjila (Naibu Katibu Mkuu)
  Dkt. Leonard Akwilapo (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
  Dkt. Mpoki Ulisubisya (Katibu Mkuu - Afya)
  Sihaba Nkinga (Katibu Mkuu - Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto)

  1.  Wizara ya Habari, Utamaduni,  Sanaa na Michezo
  Profesa Elisante Ole Gabriel Mollel (Katibu Mkuu)
  Nuru Halfan Mrisho (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Maji na Umwagiliaji
  Mhandisi Mbogo Futakamba (Katibu Mkuu)
  Mhandisi Kalobero Emmanuel (Naibu Katibu Mkuu)

  1.  Wizara ya Nishati na Madini
  Profesa Justus W. Ntalikwa (Katibu Mkuu)
  Profesa James Epifani Mdoe (Naibu Katibu Mkuu)
  Dkt. Paulina Pallangyo (Naibu Katibu Mkuu)

  1.  Wizara ya Katiba na Sheria
  Profesa Sifuni Mchome (Katibu Mkuu)
  Suzan Paul Mlawi (Naibu Katibu Mkuu)
  Amon Mpanju (Naibu Katibu Mkuu)

  1.  Wizara ya Mambo ya Ndani
  Jaji Meja Jenerali Projest A. Rwegasira (Katibu Mkuu)
  Balozi Hassan Simba Yahaya (Naibu Katibu Mkuu)

  1.  Wizara ya Fedha na Mipango
  Dkt. Silvacius Likwelile (Katibu Mkuu)
  Dorothy Mwanyika (Naibu Katibu Mkuu)
  James Dotto (Naibu Katibu Mkuu)
  Amina Hamis Shaban (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
  Dkt. Aziz Mlima (Katibu Mkuu)
  Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi ( Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
  2. Job D. Masima (Katibu Mkuu 
  3. Immaculate Peter Ngwale (Naibu Katibu Mkuu
  Makatibu wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wote ambao hawajatajwa katika orodha hii watapangiwa kazi nyingine.
  Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Eliakimu Maswi kuwa Kaimu Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na ametengua uteuzi wa Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Lusekelo Mwaseba, ambaye atapangiwa kazi nyingine

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  30 Desemba, 2015

  0 0

   Msanii Tekno Miles (wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla iliyomtambulisha rasmi kwa waandishi wa habari iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Msanii huyo anatarajiwa kuburudisha katika Tamasha la mwisho la “Grown and Sexy, the Gold finale” litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite katika mkesha wa mwaka mpya ambapo pia atafunga rasmi mfululizo wa matamasha hayo ya Grown And Sexy tokea kuanzishwa kwake.
  Dj rasmi wa msanii Jay Z wa Marekani al maarufu kama “Young Guru” akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ya kumtambulisha rasmi Msanii Tekno Miles (Katikati) ambaye anatarajiwa kuburudisha katika Tamasha la mwisho la “Grown and Sexy, the Gold finale” litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite katika mkesha wa mwaka mpya. Dj huyo atasimamia vilivyo kazi yake katika shughuli nzima ya Tamasha hilo. 
  Meneja Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija (Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Msanii Tekno Miles (wa kwanza kushoto) na Dj rasmi wa msanii Jay Z wa Marekani al maarufu kama “Young Guru” wakati wa hafla iliyomtambulisha Msanii Tekno Miles kwa waandishi wa habari iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Msanii huyo anatarajiwa kuburudisha katika Tamasha la mwisho la “Grown and Sexy, the Gold finale” litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite katika mkesha wa mwaka mpya ambapo pia atafunga rasmi mfululizo wa matamasha hayo ya Grown And Sexy tokea kuanzishwa kwake. 


  Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa umakini mkutano wa kumtambulisha Msanii maarufu Tekno Miles kutoka Nigeria uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ambaye anatarajiwa kutumbuiza katika mkesha wa Tamasha la Grown and Sexy the Gold finale litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite jijini Dar es salaam.  Maandalizi ya Tamasha maarufu la Johnnie Walker “Grown and Sexy The Gold finale” kwa ajili ya kuuaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya yanaendelea vizuri ambapo kwa mujibu wa waandaaji wa Tamasha hilo, “Capital events” kupitia wadhamini wao “Johnnie Walker” chapa maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti wamemleta Msanii Tekno Miles kutoka Nigeria kutumbuiza laivu katika Tamasha hilo ambalo litakua la mwisho kabisa katika historia ya matamasha ya Grown and Sexy nchini Tanzania.

  Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam,Meneja chapa wa pombe kali SBL Shomari Shija alisema, “Tumeamua kulidhamini Tamasha hili kama njia mojawapo ya kujumuika na kufurahi kwa pamoja na wateja wetu wa chapa za Johnnie Walker katika kuuaga rasmi mwaka huu wa 2015.

  Bw. Shija aliongeza kuwa katika Tamasha la mwaka huu ambalo ni la mwisho katika historia ya mfululizo wa matamasha ya Grown and Sexy waliona ni vema kumleta msanii maarufu toka Nigeria “Tekno Miles” ambaye aliwasili jana usiku mida ya saa nane akitokea Nigeria tayari kwa kulipamba Tamasha hilo. Msanii huyo ambaye anatamba na vibao mbalimbali kwenye anga ya muziki hivi sasa kama Shoki, Duro na Wash atatumbuiza laivu kwenye Tamasha hilo ambalo litafanyika siku ya mkesha wa mwaka mpya katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga, Msasani karibu na Best Bite.

  Sambamba na uwepo wa msanii huyo wengine wataopamba Tamasha hilo ni Dj Maarufu “Young Guru” ambaye ni Dj rasmi wa msanii Jay Z toka Marekani ambaye ataisimamia shoo hiyo vilivyo pamoja na malkia wa uswazi mwanadada “Shaa” kisura wa Tamasha hilo ambaye atasherehesha shughuli nzima katika usiku wa tukio.

  Kwa upande wake Msanii Tekno alisema anafurahia kusherekea mkesha wa mwaka mpya akiwa Tanzania na kuahidi kuporomosha burudani ya nguvu kwa mashabiki wake watakaojitokeza kushuhudia Tamasha hilo la kufunga mwaka.  Naye Mwakilishi wa Capital events waandaaji wa Tamasha hilo Bw. Justin Massawe alisema “Tunawakaribisha wapenzi wote wa burudani na chapa ya Johnnie Walker kujitokeza kwa wingi kushuhudia Tamasha letu la mwisho la Grown & Sexy na kuahidi kuwa litakuwa la kufana zaidi kwani wamejipanga kutoa burudani ya nguvu na kuwafurahisha mashabiki mbalimbali.

  “Ningependa kuwashukuru wadhamini wetu mbalimbali katika kipindi chote cha mfululizo wa matamasha haya tokea yalipoanzishwa rasmi kwa ushirikiano mzuri ambao wametupatia hadi hii leo tunapofunga rasmi tamasha hili la mwisho la Grown and Sexy the Gold finale.”

  Bw. Justin hakusita pia kuwashukuru Johnnie Walker kwa kuhakikisha wanakamilisha mikataba yote ya kumleta msanii Tekno Miles pamoja na Dj Young Guru hapa nchini na kwa kuhakikisha kwamba tamasha la mwisho linakamilika kwa mafanikio” makubwa zaidi.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akifanya mazungumzo na Balozi wa Qatar Mhe. Abdullah Jassim Almaadadi alipofika Wizarani kwa ajili ya kumpongeza kwa kuteuliwa katika wadhifa wake mpya na pia kumhakikishia ushirikiano kati ya Tanzania na Qatar. Mazungumzo hayo yalifanyika tarehe 30 Desemba, 2015. 
  Balozi Al maadadi naye akizungumza huku Mhe. Mahiga akimsikiliza. 
   Mazungumzo yakiendelea 
   Waziri Mahiga akiagana na Balozi Al Maadadi mara baada ya kumaliza mazungumzo. 
  .......Mkutano na Balozi wa Kuwait nchini 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Augustine Mahiga (kulia) akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Nassem Ibrahim Al Najib, alipokuja kumtembelea Wizarani na kufanya mazungumzo naye kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Kuwait na pia kumpongeza. 
  Balozi Mahiga akiagana na Balozi wa Kuwait mara baada ya kumaliza mazungumzo naye. 
  Picha na Reginald Philip

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

                                                    WIZARA YA MAMBO YA NDANI

                                                       JESHI LA POLISI TANZANIA

   
                                                                                              31/12/2015
  TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI

  KUHUSU TAHADHARI KATIKA MKESHA WA MWAKA MPYA    


  Tunapoelekea kumaliza mwaka 2015 na kuukaribisha  mwaka mpya wa  2016, wananchi hutumia muda huo kwenda  katika nyumba za ibada ama kusherekea katika maeneo mbalimbali ya starehe, ambapo uzoefu unaonyesha kuwa baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo  vinavyohatarisha usalama wa raia mali zao.


  Jeshi la Polisi nchini, limejipanga vizuri katika mikoa yote kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha kwamba vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyojitokeza  hususani katika kipindi hiki cha kuelekea mkesha wa mwaka mpya vinadhibitiwa. Ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine yote ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.


  Aidha,  Jeshi la Polisi linatoa tahadhari kwa wananchi wote kuwa makini na kuchukua hatua stahiki za haraka kwa kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu katika maeneo yao ya makazi ama maeneo ya biashara. Simu za polisi endapo mwananchi atakuwa na taarifa ni 111 au 112.


   Pia,  Jeshi la Polisi linawatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani na hasa kwa madereva wa magari na pikipiki, kuepuka kujaza watu kupita kiasi, kwenda mwendo kasi, kutumia vilevi pamoja na kupiga honi hovyo.


  Vilevile, wananchi kuacha tabia ya kuchoma matairi barabani pamoja na kupiga mafataki. Aidha, yeyote atakayefanya vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.


  Nawatakieni watanzania wote kheri ya mwaka mpya.

  Imetolewa na:

  Advera John Bulimba-SSP

  Msemaji wa Jeshi la Polisi.


  Makao Makuu ya Polisi.         


  0 0
 • 12/31/15--03:33: Taarifa ya Utapeli


 • 0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru Initiative for Policy & Education(UIPE), Isack Dornad akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
  Baadhi ya waandishi wa  habari wakimsikiliza 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru Initiative for Policy & Education(UIPE), Isack Dornad  jijini Dar es Salaam leo. 
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  Na Zainabu Hamis, Globu ya Jamii
  TANZANIA ni miongoni mwa nchi 100 Duniani zilizo huru Kiuchumi, pia imeshika nafasi ya 82 ya Uhuru wa Kiuchumi Dunia kwa mwaka huu.

   Nafasi hiyo imetolewa na Umoja wa Shirika lisilo la Kiserikali lijulikanao kama Mtandao wa Uhuru wa Kiuchumi kutoka nchini Canada.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru Initiative for Policy & Education(UIPE), Isack Dornad amesema kuwa,Tanzania imepanda nafasi kumi katika ripoti ya mwaka huu kutoka nafasi ya 92 katika ripoti ya 2014 hadi kushika nafasi ya 82 katika ripoti ya 2015 na kushika nafasi ya tatu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Amezitaja nchi mbalimbali zilizoongoza katika nafasi 10 bora ambazo ni Hong Kong, Singapore, New Zealand, Switzerland, United Arab Emirates, Mauritius, Jordan, Ireland, Canada, Uingereza na Chile.

   Pia amezitaja nchi zilizo shika mkia kuwa ni nchi ya Angola, Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Zimbabwe, Algeria, Argentina, Syria, Chad, Libya, Jamuhuri ya Kongo na Venezuela.

  Aidha Dornad ametaja vikwazo mbalimbali vinavyo sababisha Tanzania kuwa nyuma kiuhuru wa uchumi kuwa ni pamoja na Ulazimishwajia wa kuchangia huduma za kiserikali, Mikataba ya Ajira Kima cha chini cha Mishahara, Kumiliki akaunti za benki za fedha za nje, Viwango vya juu kwenye kodi za mishahara na vipato, malipo ya ziada, hongo na upendeleo.

  0 0


  SERIKALI imesema kuwa haina mpango wakujenga nyumba za kuwapa Wananchi bure kutokana na gharama ambazo Serikali inagharamia katika ujenzi nyumba hizo.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula (Pichani)wakati alipotembelea Shirika la Nyumba la Taifa(NHC).

  Angeline amesema kuwa shirika la nyumba la Taifa linajenga nyumba kwaajili ya kuuzwa pamoja na kupangisha na si kuwapa wanchi bure.

  Amesema kuwa gharama ya kujenga nyumba hizo inakuja katika maandalizi ya ujenzi ikiwa ni pamoja na kuandaa miundombinu kama Barabara, Maji pamoja na Umeme.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC), Nehemia Mchechu amesema shirika hilo tayari limejenga nyumba za kutosha katika miji mikubwa kama Dar es Salaam, Arusha na Mwanza.

  Pia amesema katika nyumba za mikoani shirika hilo limeuza nyumba hizo kwa 40% hadi 50% huku akisisitiza zaidi kuendelea na Kampeni ya (Nyumba yangu, Maisha yangu) ili wananchi wawezi kumudu gharama za nyumba hizo.

  0 0

   Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa. Joyce Ndalichako, akitembezwa katika maeneo ya ofisi za Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) jijini Dar es salaam jana na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dk.Primus Nkwera. Waziri huyo alikuwa katika ziara ya kutembelea taasisi za elimu zilizochini ya wizara yake.
   Na Mpigapicha wetu.
   Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako (kushoto), akisisitiza jambo, alipokuwa akizungumza na wafanykazi wa Baraza la Taifa la Elimu na Ufundi (NACTE) jana alipotembelea makao makuu ya baraza hilo lililopo jijini Dar es Salaam jana,wapili toka kushoto ni na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dk.Primus Nkwera.
   Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako,akimsikiliza kwa makini Vincent Jacob, mtalamu wa mtandao wa udhibiti wa utoajia wa vyeti vya satifiketi na Diploma wa Baraza la Taifa la Elimu na ufundi (NACTE). Waziri alifanya ziara ya kutembelea makao makuu ya baraza hilo jijini Dar es Salaam jana,Watatu kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dk.Primus Nkwera.

  Waziri wa Elimu Sayansi,Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kuzungumza na wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Elimu na ufundi (NACTE) jijini Dar es salaam jana.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


  KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.


  Kesho Ijumaa 01 Januari, 2016 Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wataapishwa rasmi katika Ukumbi wa Ikulu, uliopo lango kuu litazamalo baharini kuanzia saa nne asubuhi.


  Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wote ambao wataapishwa na wale ambao walishaapishwa wanapaswa kuhudhuria katika tukio hili, ili mara baada ya kiapo kukamilika washiriki zoezi la kutia saini Hati ya Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma (Integrity Pledge).  


  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema zoezi la kutia saini hizo, litafanyika kwa uwazi mbele ya vyombo vya habari.

  Aidha, Balozi Sefue amefafanua kuwa hata kama wapo baadhi ya Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu ambao walishasaini Hati hizo, watapaswa kusaini upya mbele ya vyombo vya habari.

  Tukio hili pia litarushwa ‘live’ kupitia luninga.


  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi Mawasiliano, IKULU


  31 Desemba, 2015.

  0 0

  MERY MICHAEL LASWAI anatangaza kuibiwa kwa Wallet ikiwa na  Nyaraka (Document) nyingi pamoja na Vitambulisho, Leseni ya Uderava, Kadi za Benki na Kadi ya Mpiga kura vyote vikiwa na jina la  MERY MICHAEL LASWAI.

  Vitu hivyo aliibiwa akiwa maeneo ya Boko jijini Dar es Salaam
   atakayeviona mahari popote pale tunaomba apige simu namba 0754441165 na 0688045999.
   SHUKRANI.

  0 0

  Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri akitoa ufafanuzi kwa Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kushoto) kuhusu utendaji wa Wakala hiyo leo wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Angella Kairuki katika Ofisi za Wakala hiyo leo jijini Dar es salaam.
  Mkurugenzi wa Uratibu wa Miundombinu ya TEHAMA wa Wakala ya Serikali Mtandao Bw. Benjamin Dotto akitoa ufafanuzi kwa Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kulia) kuhusu kituo cha ufuatiliaji mifumo ya mawasiliano Serikalini leo jijini Dar es salaam.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri akitoa ufafanuzi kwa Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kulia) kuhusu kituo cha ufuatiliaji mifumo ya mawasiliano Serikalini leo jijini Dar es salaam. 
  Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kushoto) akipokewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri leo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dar es salaam.
  Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (katikati) akiwasili Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao kwa ziara ya kikazi leo jijini Dar es salaam.

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akikabidhi sehemu ya msaada kwa baadhi ya watoto kutoka Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede kilichopo Buguruni Malapa cha jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa leo na Kampuni ya TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. 
  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akimkabidhi Mlezi wa Watoto na Vijana, Stella Mwambenja wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede kilichopo Buguruni Malapa cha jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya watoto wa kituo hicho.
  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhi sehemu ya msaada wa chakula kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016 kwa vituo vitatu vya watoto yatima Dar es Salaam. Kulia ni Mlezi wa Watoto na Vijana wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede, Stella Mwambenja. 
  Mmoja wa watoto kutoka Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede cha Buguruni Malapa Dar es Salaam akitoa shukrani kwa kampuni ya TTCL baada ya kukabidhiwa msaada huo na Kampuni ya TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. 
   Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) na Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Amanda Luhanga (kulia) wakipewa historia fupi ya Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge kwa Ofisa Mfawidhi, Ojuku Mgezi (katikati) kabla ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya. 
   Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Ofisa Mfawidhi wa Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge, Ojuku Mgezi (wa pili kushoto) msaada huo umetolewa leo na TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. Wengine ni viongozi na wawakilishi wa jumuiya ya Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge. 
  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Ofisa Mfawidhi wa Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge, Ojuku Mgezi (wa pili kushoto) msaada huo umetolewa leo na TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. Wengine ni viongozi na wawakilishi wa jumuiya ya Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge. 
  Sehemu ya makazi ya Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge 
  Sehemu ya msaada ukishushwa kwenye Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge. Msaada huo umetolewa leo na TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. Msaada huo umetolewa leo na TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. 
  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas  (kulia) akizungumza na watoto wa Kituo cha Kulelea Watoto Wanaoishi katika Mazingira Magumu cha Honoratha cha Temeke jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. 
   Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada Mlezi wa Kituo cha Kulelea Watoto Wanaoishi katika Mazingira Magumu cha Honoratha cha Temeke jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. TTCL imetoa msaada wa mifuko ya Unga, Sukari, Mchele, Maharage na Mafuta ya Kupikia kwa vituo vitatu tofauti vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu. 

  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (katikati) kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa Kituo cha Kulelea Watoto Wanaoishi katika Mazingira Magumu cha Temeke cha jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa leo na TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. 

  0 0

   Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Wiliam Lukuvi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, akihutubia kwenye Mkesha Mkubwa Kitaifa,Dua Maalum ya kuwaombea viongozi na Taifa uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
   Mchungaji Eden Godfrey akihubiri kwenye Mkesha Mkubwa Kitaifa, Dua maalum uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

   Viongozi wakiwa wameshikana mikono wakati wa maombi maalum kwa Taifa na Viongozi wake .
   Umati wa wakazi wa jiji la Dar es salaam waliojitokeza kwenye ibada maalum ya mkesha wa mwaka mpya uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru.
   Wananchi wakiwa kwenye maombi ya kuliombea Taifa Amani, na kuwaombea viongozi wake afya njema.
   Mwalimu Teddy Kwilasa akitoa maombi maalum kwa Taifa kwenye mkesha wa mwaka mpya.
   Wananchi wakiwa kwenye maombi mazito ya kuwaombea Viongozi wa Taifa letu
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (wa pili kulia) akiwa pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye pamoja na wake zao wakiupokea mwaka kwenye Mkesha Mkubwa Kitaifa, ambapo Taifa na Viongozi wake waliombewa.
   Sehemu ya Vijana waliojitokeza kwenye mkesha mkubwa uliofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akitoa salaam maalum za kuwataka wazazi kuwafundisha watoto wao umuhimu wa amani ya nchi wakati wa mkesha wa mkubwa kitaifa wa kuombea Taifa na Viongozi wake dua maalum.
   Bi. Christina Elias wa Aleluyah kwaya kutoka Tabata  akiimba kwa hisia kwenye mkesha mkubwa wa kitaifa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
   Viongozi wakiwa kwenye maombi maalum ambapo waliwakilisha Mawaziri wote nchini.
  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0

  Mhandisi Mohamed Millanga akiongoza msafara wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Prof. Makame Mbarawa kukagua ujenzi wa jengo la tatu la abiria (TBIII).
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Prof. Makame Mbarawa (katikati) akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa TBIII kutoka kwa mhandisi Mohamed Millanga (kulia).
    Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (aliyenyoosha mkono) akimpa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jingo la tatu la abiria, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Pro. Makame Mbarawa.
    Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (aliyenyoosha mkono) akimpa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jingo la tatu la abiria, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Pro. Makame Mbarawa.
    Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (aliyenyoosha mkono) akimpa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jingo la tatu la abiria, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Pro. Makame Mbarawa.
    Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (aliyenyoosha mkono) akimpa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jingo la tatu la abiria, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Pro. Makame Mbarawa.
   Waziri akiwa katika picha ya pamoja.
    Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (aliyenyoosha mkono) akimpa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jingo la tatu la abiria, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Pro. Makame Mbarawa.
  Waziri waWizara ya Ujenzi,. Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Prtof Makame Mbarawa akisaini kitabu cha wageni katika jingo la kikosi cha zimamoto cha kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).


   DAR ES SALAAM, Tanzania


  WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh.Prof.  Makame Mbarawa ameagiza  watumishi wa Tassisi  zote  zinazotoa  huduma katika viwanja vya ndege  hapa nchini kuwajibika kwa Mameneja  wa Mamlaka  ya Viwanja vya Ndege  (TAA)  wanaosimamia  viwanja  ambavyo  watumishi hao wamepangiwa  kufanya  kazi.   Mh. Mbarawa ametoa agizo hilo jana wakati alipofanya ziara ya siku moja kwenye Makao Makuu  ya  TAA  ambapo  pamoja na mambo mengine  alikagua  ujenzi unaondelea wa jengo la tatu la abiria (TBIII), na  kituo cha Zimamoto na Uokoaji. Pia  alitembelea mradi  wa usimikaji wa vivuko vipya vya abiria (Passenger Boarding  Bridges) na  usimikaji wa mitambo mipya ya kufua umeme wa dharura (Standby Generators) iliyopo katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).  Akizungumza  na menejimenti ya TAA ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi  Suleiman S. Suleiman  katika Ofisi  za TAA  ikiwa ni sehemu ya majumuisho ya ziara yake, Prof. Mbarawa aliwapongeza TAA kwa kazi nzuri wanayoifanya hususan  katika uboreshaji wa muindombinu na kuhudumia wateja. Hata hivyo alisema pamoja na sifa hiyo nzuri, kuna haja kwa TAA kuwa mdhibiti wa taasisi nyingine zote  zinazofanyakazi katika viwanja vya  ndege hapa nchini kama njia ya  kuepuka kuchafua sifa nzuri ya viwanja hivyo na nchi kwa ujumla.

  “ Pamoja na kazi nzuri mnayoifanya,nadhani  wakati umefika sasa kwa taasisi zote zinazotoa huduma katika viwanja vya ndege hapa nchini  ziwe chini ya TAA”,  alisema  Prof. Mbarawa  huku akisisitiza umuhimu wa  taasisi hizo kufanya kazi  kwa kushirikiana  kama timu moja. 

   “Nyinyi ndio kioo katika jamii yetu, taasisi nyingine mfano uhamiaji wakachelewa kugonga mhuri kwenye hati za kusafiria, watu hawatambui kama ndio wao waliochelewesha na lawama watawatupia nyinyi,” alisisitiza Mh. Mbarawa na kuongeza kwamba anafanya utaratibu wa kuwasiliana na Wizara zote zinazohusiana  na taasisi hizo ili kupanga utaratibu muafaka.

  Mbali na idara ya uhamiaji,  taasisi nyingine zinazotoa huduma kwenye viwanja vya ndege ni pamoja na Idara ya maliasili,  afya, kilimo, mifugo, madini,  polisi na kitengo cha kuzuia madawa ya kulevya.  

  Mh. Mbarawa  pia  ameiagiza  TAA kubuni  mikakati  ya kuongeza ukusanyaji wa mapato zaidi ili iweze kujiendesha na pia ihakikishe kuwa inaepukana  na matumizi yasiyo ya lazima. Aliitaka watumishi wa TAA  kuzingatia uadilifu na weledi katika utendaji wao wa kazi na kuhudumia wateja  ikizingatiwa kuwa viwanja vya ndege ni kioo cha nchi.

  “Nisingependa taarifa za matukio mbalimbali yanayotokea kwenye viwanja niyasikie au kuyaona kwenye vyombo vya habari wakati mimi mwenyewe sijui, hivyo tujenge utamaduni wa kuwa waadilifu na tufanye kazi kwa kuzingatia weledi, tuepukane na matukio ya hovyo,” alisisitiza Mh. Mbarawa.

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi S.S.Suleiman alimhakikishia Waziri Mbarawa kutekeleza maagizo yake, likiwemo la kubuni mbinu mpya za mapato, na hata kuweka utaratibu wa kumpatia taarifa mbalimbali zinazotokea kwenye viwanja kabla hazijapelekwa sehemu nyingine yeyote, kwa ajili ya utekelezaji na kujenga uhusiano mzuri baina ya mamlaka na wizara kwa ujumla. 

  “Kuhusu mapato tunauhakika wakati wa jengo la tatu la abiria likifunguliwa yataongezeka, lakini tunaahidi kubuni mbinu nyingi zaidi, ili  tuwe na vyanzo vya uhakika vya mapato,” alisema Mhandishi Suleiman. Alisema kukamilika kwa jengo hilo kutaongeza idadi ya abiria watakaosafiri na ndege za ukubwa mbalimbali ikiwemo 380 Airbus yenye uwezo wa kubeba abiria 300.

  Awali Mh. Mbarawa alipotembelea ofisi za zimamoto zilizopo JNIA, alielezwa wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa na hususan  magari ya zimamoto ambayo mbali na kuhudumia viwanja vya ndege, wakati mwingine  kulazimika pia kusaidia  jamii endapo nyumba zao zinakumbwa na majanga ya  moto.
   
         Imetolewa na kitengo cha Habari na Mahusiano na Sheria TAA.

  0 0older | 1 | .... | 727 | 728 | (Page 729) | 730 | 731 | .... | 1904 | newer