Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 726 | 727 | (Page 728) | 729 | 730 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akisaini kitabu cha wageni baada ya kufika katika Tume ya Mipango. Kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji Bi. Florence Mwanri.

    Baadhi ya wafanyakazi wa Tume ya Mipango wakimpokea Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipowatembelea kwa lengo la kuwaaga.
   Mmoja ya watumishi wa Tume ya Mipango Bw. Mohamed Ally akiongea mawili matatu na waziri mara baada ya mkutano kuisha.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Tume ya Mipango wakimpokea Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipowatembelea kwa lengo la kuwaaga.
   Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiongea na watumishi wa Tume ya Mipango alipowatembelea kwa kusudi la kuwaaga.
   Kaimu Katibu Mtendaji Bi. Florence Mwanri akimsikiliza kwa makini Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.
   
  WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango ameiagiza Tume ya Mipango kufanya utafiti kuhusu mapato ya Serikali na namna ya kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato.

  Amesema Tume ya Mipango kama chombo cha ushauri kwa Serikali kuhusu mipango na uchumi wa nchi, ni lazima ifanye utafiti juu ya ufanisi wa ukusanyaji wa mapato na kuongeza vyanzo wa kukusanya mapato ya Serikali ili kuiwezesha Serikali kuwahudumia wananchi wake.

  “Serikali isipokusanya kodi kwa ufanisi haiwezi kuwahudumia wananchi hivyo, ni lazima kodi ikusanywe ipasavyo ili kuiwezesha kujiendesha” alisema.

  Dkt Mpango aliyasema hayo alipokutana na wafanyakazi wa Tume ya Mipango kwa lengo la kuwaaga baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.

  Waziri wa Fedha amesema mianya yote ya ukwepaji kodi ni lazima izibwe ili kuiwezesha Serikali kukusanya mapato ya kutosha suala ambalo litairahisishia utoaji wa huduma za msingi kwa wananchi.

  Amesema Serikali haiwezi kutegemea kila kitu kutoka kwa wafadhili wakati nchi ina rasilimali za kutosha hivyo.Dkt. Mpango amesema Tume ya Mipango ni lazima iongoze nchi kuelekea katika uchumi wa viwanda ambavyo vitafanya pato la taifa kuongezeka na kutoa ajira kwa wananchi.

  “Sisi kama wataalamu tunatakiwa kuiongoza nchi katika kufikia kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 jambo ambalo linawezekana” alisema.Waziri pia amesema ni lazima tujenge uchumi imara na madhubuti utakaowezesha kupunguza umaskini miongoni mwa wananchi.

  “Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuboresha ufanisi na utendaji wa Serikali kwa ujumla hivyo ninyi kama wataalamu mna mchango mkubwa katika kutimiza hilo” alisema.

  Tume ya Mipango ni chombo mahususi cha fikra rejea na ushauri kwa serikali kuhusu sera na mikakati ya maendeleo, kiuchumi na kijamii ambao unaambatana na ufuatiliaji na utathmini wa mwenendo wa uchumi nchini.

  Aliwataka wafanyakazi wa Tume ya Mipango kufanyakazi kwa bidii, maarifa na weledi mkubwa ili kuimarisha utendaji Serikalini.

  0 0

  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(kushoto) akiongea na Mchezaji wa Timu ya TP Mazembe Mbwana Samatta(kulia) leo jijini Dar es salaam.Mbwana amemtembelea waziri Nape ofisini kwake na kuomba baraka za wizara katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika anayechezea ligi za ndani na pia kumpa habari njema za yeye kutegemea kujiunga na timu ya Ubelgiji ya Genk.
  Waziri wa Habari,Utamaduni,sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(katikati)akiongea na waandishi wa Habari na kuwaomba watanzania kumwombea Mbwana Samatta ili ashinde katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika anayechezea ligi za ndani kwani ni jambo la Taifa zima.Mhe Nape pia alimhakikishia kuwa Serikali ipo nyuma yake na ipo katika mkakati wa kuifanya michezo kuwa Shughuli Rasmi kwani itawafaidisha wanamichezo na Serikali kwa kupata kodi. 

  Mchezaji wa TP Mazembe Mbwana Samatta(wa kwanza kushoto)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) sababu za yeye kumtembelea Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika ofisi ya Wizara hiyo.Mbwana alisema kuwa amemtembelea waziri uyo kwa ajili ya kumfahamisha kuwa yumo katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika anayechezea ligi za ndani na hivyo kuomba baraka za Wizara.Pia kumpongeza Mhe. Nape kwa kuchaguliwa kuwa waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.Mbwana anategemea kujiunga na klabu ya Mpira ya Genk ya Ubelgiji kwa mkataba wa miaka minne.
  Picha na Daudi Manongi-WHUSM.

  0 0

  Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu Baraza hilo lilivyofanikiwa kutatua migogoro kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya Ujenzi nchini.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho leo Jijini Dar es salaam kuhusu Baraza hilo lilivyofanikiwa kutatua migogoro kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya Ujenzi nchini.


  Frank Mvungi- Maelezo

  Baraza la Taifa la Ujenzi limepokea migogoro 41 na kufanikiwa kuitafutia ufumbuzi katika kipindi cha mwaka 2015 kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya Ujenzi nchini.

  Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.

  Akizungumzia majukumu ya Baraza hilo katika kutatua Migogoro inayojitokeza katika Sekta hiyo, Mhandisi Chamuriho amebainisha kuwa migogogoro iliyojitokeza imekuwa ikitegemea Ukubwa wa mradi, Hali ya eneo la mradi, Ubora wa kazi, uelewa wa vipengele mbalimbali vya mkataba katika mradi husika na moja ya pande zinazohusika kukatisha mkataba.

  Kakika kukabiliana na migogoro hiyo, Baraza hilo limekuwa likitumia njia mbalimbali ikiwemo kutoa ushauri wa kitaalamu kwa pande zinazohusika katika mradi, kuwakutanisha wadau chini ya Baraza, kuweka wahusika chini ya aliyetatua mgogoro husika.

  Akifafanua, Mhandisi Dkt. Chamuriho amebainisha kuwa Baraza hilo limekuwa likitumia njia hizo kutatua Migogoro katika sekta hiyo pale inaposhindikana wahusika wanaweza kwenda mahakamani kama hatua ya mwisho katika kutatua mgogoro husika.

  Pia alitoa wito kwa watanzania wote hasa wadau wa Sekta ya Ujenzi kuwa na uelewa mzuri wa jinsi ya kutekeleza miradi ya ujenzi kwa kuzingatia Sheria na kanuni ili kuepuka Migogoro.

  Baraza la Taifa la Ujenzi ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria ya Bunge namba 20 ya mwaka 1987 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2008.(National Construction Council Act, CAP 162,R.E.2008) ambapo Baraza lilianza kufanya kazi tarehe 17 August 1981.


  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akizungumza  na washiriki  wa Mafunzo ya awali kwa Watumishi wa Mkataba wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi(hawapo pichani),wakati alipofungua mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengea uwezo watumishi wapya, katika ukumbi wa mikutano wizarani hapo,jijini Dar es Salaam.Kulia ni  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Numbilya Mpolo.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mbarak Abdulwakil akizungumza  na washiriki  wa Mafunzo ya awali kwa Watumishi wa Mkataba wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi wakati alipofungua mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengea uwezo watumishi wapya, katika ukumbi wa mikutano wa wizara, jijini Dar es Salaam.Kulia ni  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Numbilya Mpolo, kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa  Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa .

  Washiriki wa Mafunzo ya awali kwa Watumishi wa Mkataba wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil(hayupo pichani), wakati alipofungua mafunzo hayo katika ukumbi wa mikutano wizarani hapo,jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa  Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa, akizungumza na washiriki wa Mafunzo ya awali kwa Watumishi wa Mkataba wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi(hawapo pichani),kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Utawala na Usimamizi wa Idara ya Wakimbizi, Deusdedit Masusu.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil(watatu kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo ya awali kwa Watumishi wa Mkataba wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, muda mfupi baada ya kufungua mafunzo hayo katika ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam wanne kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa  Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa na wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi  wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Numbilya Mpolo .(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,MOHA).Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  OFISI YA RAIS


  Anuani ya Simu “TAMISEMI” DODOMA
  Simu Na: (026) 2322848, 2321607, 
                              2322853, 2322420,
  Nukushi: (026) 2322116,  2322146.
                               2321013,      
  Barua pepe:ps@poralg.go.tz

  Tawala za Mikoa
  na Serikali za Mitaa,
  S. L. P. 1923,                          DODOMA.
    

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. George Simbachawene amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kuwasimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Dodoma Bw. Elias N. Kamara na  Bibi Donatila D. Vedasto (Afisa Biashara) kuanzia leo tarehe 30/12/2015 kwa kosa la kusababisha urasimu katika utoaji wa leseni za biashara.

  Kutokana na hali hiyo Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kumuondoa kwenye nafasi yake Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa na Msaidizi wake na nafasi zao kukaimishwa kwa watu wengine ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizotolewa dhidi yao.

  Agizo hili limetolewa na Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara ambayo yalionyesha kuwepo kwa mazingira ya rushwa.

  Katika uchunguzi ambao umefanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imegundulika kuwa kulikuwa na maombi ya leseni 750 ambayo yalikuwa hayajashughulikiwa bila sababu za msingi na hali hiyo ilipelekea kuikosesha  Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kiasi cha shilingi Milioni 75.

  Aidha, Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI ameagiza Mamlaka za Serikali kote nchini kuhakikisha wanatoa leseni za biashara bila urasimu wowote na muombaji apate leseni ndani ya siku 2 au 3 anapoomba leseni.

  Mhe. Simbachawene ametoa agizo kwa Maafisa biashara wote nchini kuacha urasimu katika kutoa leseni na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

  Imetolewa na:
  Rebecca Kwandu
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  30 Desemba, 2015

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Ally Simba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na makampuni ya simu  za mkononi ya Tigo, Airtel, Halotel na Zantel na Smart kwa kuto kukidhi vigenzo. Pia amesema kuwa Makampuni hayo yamepigwa faini ya shilingi milioni 25 kwa mamlaka ya mawasiliano Tanzania kabla ya Januari 29 mwakani.
  Mwanasheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Elizabeth Zagi akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Ally Simba jijini Dar es Salaam leo.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  JAMHURI YA YA MUUNGANO YA TANZANIA
  MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  HATUA ZA KISHERIA NA KIUDHIBITI KWA MAKAMPUNI YA SIMU YALIYOSHINDWA KULINDA WATEJA WAKE KITEKNOLOJIA NA KISHERIA KUHAKIKISHA USALAMA WA MAWASILIANO YAO

  1. Katika shughuili zake za udhibiti wa huduma za mawasiliano nchini, Mamlaka ya Mawasilaino Tanzania imepokea malalamiko kutoka kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano dhidi ya kuwepo mazingira yasiyo salama katika huduma za mawasiliano na hivyo kusababisha kufanyika kwa vitendo vya utapeli unaofanywa kwa kutuma jumbe za udanganyifu na kulaghai, hivyo kusababisha watu kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.

   Kwa mfano kupokea ujumbe kutoka namba unayoifahamu ukikuagiza utume fedha au ujumbe wa kashfa au matusi wakati hautoki kwa mhusika mwenye namba. Mamlaka imepokea malalamiko mengi kutoka kwa wateja na malalamiko mengine hupelekwa Polisi. Kwa miezi miwili tu, matukio 42 yameripotiwa Polisi pamoja na TCRA ambayo tukio moja tu linakuwa na ulaghai wa takribani milioni 25 peke yake.

  2. Tarehe 16 Oktoba, 2015 Mamlaka iliwakumbusha watoa huduma za simu nchini juu ya wajibu wao kuchukua hatua za kusheria na kitaalamu ili kulinda watumiaji dhidi ya utumaji wa jumbe za kilaghai na kuchukua hatua mara moja kuzuia mitandao yao kutumika kutuma jumbe za udanganyifu na kulaghai. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Mamlaka tarehe 16 Desemba, 2015 Mamlaka ilibaini kuwa  kampuni za Benson Informatics Limited (inayojulikana kama Smart), MIC Tanzania Limited (inayojulikana kama Tigo), Airtel Tanzania Limited, Viettel Tanzania Limited (inayojulikana kama Halotel) and Zanzibar Telecom Limited inayojulikana kama Zantel) zimeshindwa, zimepuuzia na zimekataa kufuata maagizo ya Mamlaka kuchukua hatua mara moja kuzuia mitandao yao kutumika kutuma jumbe za kilaghai kinyume na Kanuni Na.8(a) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2011 [the Electronic and Postal Communications (Computer Emergency Response Team) Regulations, 2011].

  3. Tarehe 18 Disemba, 2015 Mamlaka iliwaamuru watoa huduma za mawasiliano waliotajwa hapo juu kufika mbele ya Mamlaka na kujieleza kwa nini hatua za kisheria zisichukuliwe dhidi yao kwa kuvunja sheria na kanuni ya 8(a) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielectroniki na Postal ya Mwaka 2011 [the Electronic and Postal Communications (Computer Emergency Response Team) Regulations, 2011] kwa kushindwa kuweka mazingira salama kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano.

  4. Watoa huduma walifika na kutoa maelezo ya utetezi kati ya tarehe 21 na 23 Desemba, 2015.

  5. Baada ya kuwasikiliza na kutilia maanani utetezi wa watoa huduma na kwa mujibu wa uchunguzi na majaribio uliofanywa na Mamlaka, Mamlaka imejiridhisha kuwa mitandao ya watoa huduma waliotajwa hapo juu haikuwa salama na kuwa watoa huduma hao walishindwa kufuata maelekezo ya Mamlaka juu ya kuweka mazingira salama katika huduma wanazotoa. Hivyo Mamlaka imejiridhisha kuwa watoa huduma wamekiuka matakwa ya Kanuni ya 8(a) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielectroniki na Postal ya mwaka 2011 (The Electronic and Postal Communications (Computer Emergency Response Team) Regulations, 2011) inayowataka watoa huduma kuweka mazingira ya mitandao salama kwa kuchukua hatua za kusheria na kitaalamu ili kulinda watumiaji dhidi ya uhalifu ikiwa ni pamoja na utumaji wa jumbe za kilaghai kupitia mitandao yao.

  6. Kwa mujibu wa Kifungu cha 17 cha Jedwali la Pili katika Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, Sura ya 306 ya Sheria za Nchi, kinachoipa Mamlaka uwezo wa kutoa adhabu kwa Wenye Leseni dhidi ya uvunjifu wa Sheria, Kanuni na Masharti ya Leseni, Mamlaka ya Mawasiliano imetoa:

  A. Onyo kali kwa Kampuni za:
  (i) Benson Informatics Limited (inayojulikana kama Smart),
  (ii)  MIC Tanzania Limited (inayojulikana kama Tigo),
  (iii)  Airtel Tanzania Limited,
  (iv)  Viettel Tanzania Limited (inayojulikana kama Halotel), na 
  (v) Zanzibar Telecom Limited (inayojulikana kama Zantel). 

  kwa kushindwa kutimiza matakwa ya Kanuni ya 8(a) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Postal ya mwaka 2011  [the Electronic and Postal Communications (Computer Emergency Response Team) Regulations, 2011] kwa kushindwa kuweza mazingira salama kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano.

  B. Imeamuru Kila Kampuni husika:
  (i)   Kuhakikisha kuwa, kuanzia siku ya kutolewa kwa amri hii, inaweka mazingira salama katika mtandao wake yatakayozuia utumaji wa jumbe za kilaghai (yaani ‘spoofed messages’) na matishio mengine ya kiusalama;
  (ii)   Kulipa faini ya Shilingi za Kitanzania Milioni Ishirini na Tano (Shs 25,000,000.00) kwa Mamlaka ya Mawasiliano kabla ya tarehe 29 Januari, 2016; na
  (iii) Endapo Makamuni haya yatashindwa kutimiza amri Na.2 hapo juu, Mamlaka itachukua hatua zaidi za kisheria na kiudhibiti dhidi ya Kampuni ya Simu husika.

  7. Aidha, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inapeda kuchukua fursa hii kuwatahadharisha wananchi kuwa makini na jumbe za kuwataka kutuma fedha bila ya kuwa na uhakika. Inashauriwa kuhakiki ujumbe husika kwa kupiga simu na kuongea na mhusika kabla ya kufanya maamuzi ya kutuma fedha hata kama namba inayotumika unaijua. Vilevile wawe makini wanapopokea jumbe zinazoonesha zinatoka kwa mtu fulani wanayemjua kumbe ni matapeli wanaotumia ulaghai kwa njia hii ya “spoofing”.

  IMETOLEWA NA

  Dkt. Ally Y. Simba
  MKURUGENZI MKUU
  30 Disemba, 2015

  0 0

  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura akipewa maelekezo na Naibu Mkurugenzi wa maswala ya utangazaji wa Televisheni wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Frederick Ntobi mara baada ya kutembelea chumba cha maswala ya mawasiliano hasa ya Televisheni  leo jijini Dar es Salaam.
  Naibu Mkurugenzi wa maswala ya Posta wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Haruni Lemanya akizungumza na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) leo jijini Dar es Salaa mara baada ya Naibu waziri kutembelea katika ofisi ya Maswala ya Posta katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
   Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) WA kitengo cha TTMS, Mhandisi Gabriel Mruma akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura kutembelea katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.  

  Baadhi ya Kazi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) kwa upande wa mitandao ya Simu za mkononi na maswala ya Miamala ya Pesa katika mitandao ya simu kilichopo katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura akizungumza na wafanyakazi pamoja na wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya waandishi wa habari na wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura jijini Dar es Salaam leo.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0

  Ndugu zangu, Kwa niaba ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania kupitia kwenu wanahabari ninaomba nitoe salam za mwaka za Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF.

  Awali ya yote tumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ametulinda kwa mwaka mzima na kupitia Baraka zake tumeweza kuwa na nguvu, uwezo na hekima za kutimiza majukumu yetu mbalimbali katika kipindi hiki cha mwaka 2015. Tuzidi kumuomba atuvushe salama mwaka 2015.

  Ninaomba nichukue fursa hii kuwapongeza Watanzania wenzangu kwa kukamilisha mchakato wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Ninampongeza Mh. Dr John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hongera sana Mama Samia Suluhu kwa kuwa Makamu wa Rais na hongera kwa mwanamichezo mwenzetu Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa kwa kushinda ubunge jimbo la Ruangwa na kwa uteuzi wa kuwa Waziri wetu Mkuu. 

  Hongera za kipekee kwa Mheshimiwa Nape Nnauye kwa uteuzi wa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na hongera pia kwa Mama Anastasia Wambura kwa kuteuliwa kuwa naibu waziri wa wizara hii muhimu kwa mustakabali wa afya na ajira kwa vijana na utangazaji wa jina la Nchi yetu ya Tanzania nje ya mipaka ya nchi. Ninashukuru Mh. Waziri Nnauye majuzi alinipatia fursa ya kuwa mmoja wa viongozi wa kwanza wa vyama vya Kitaifa vya michezo ya kukutana naye na kujitambulisha rasmi kwake, ahsante sana.

  Ndugu zangu, Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania lipo kwa ajili ya kuendeleza na kusimamia mpira wa miguu Tanzania. Tunafanya hivyo kwa niaba ya Watanzania wote wapenzi wa mpira wa miguu. Kwa kutambua uzito na umuhimu wa jukumu hili ndio maana wakati wote TFF inafanya jitihada za dhati kuhakikisha timu zetu za Taifa zinafanya vizuri. 

  Kwa sasa tunazo timu za Taifa kumi ambazo ni za soka la ufukweni wanawake na wanaume, umri chini ya miaka 17 wanawake na wanaume, umri chini ya miaka 20 wanawake na wanaume, umri chini ya miaka 23 wanawake na wanaume na mbili za wakubwa za wanawake na wanaume. Katika kuingiza timu kwenye mashindano ya kimataifa tumekuwa tukizingatia vigezo kadhaa lakini kikubwa ikiwa ni utayari wa timu kushiriki mashindano na uwezo wa kugharamia mchezo wenyewe. 

  Kwa wastani gharama za kushiriki mkondo mmoja wa mechi ya Kimataifa kwa kucheza nyumbani na ugenini ni takribani shilingi million mia moja (USD 50,000.-), hii inajumuisha gharama za kambi, usafiri kwenda ugenini, posho, nauli na posho za waamuzi na kamisaa, malazi ya waamuzi na kamisaa nk. Kwa kuwa timu yenye udhamini kwa sasa ni timu ya Taifa wanaume tuu hivyo TFF imekuwa inabeba yenyewe gharama nyingine zote kwa timu zote zilizobakia. Imani yetu ni kuwa mwaka 2016 utashuhudia ufadhili unapatikana kwa timu zetu nyingine za Taifa.

  Ninaomba sasa nichukue fursa hii kuzungumzia maeneo kadhaa ambayo yamehusu mpira wetu na taasisi yetu kwa mwaka 2015:

  1. Timu ya Taifa ya wanaume “Taifa Stars”
  Baada ya timu yetu ya Taifa, Taifa Stars kutofanya vizuri katika michuano ya COSAFA huko Afrika Kusini mwezi Mei mwaka huu na baadae kufuatia kufanya vibaya katika mchezo wa kwanza katika mtoano wa mashindano ya CHAN, Kamati ya Utendaji ya TFF ilichukua maamuzi ya kusimamisha ajira ya kocha wa kigeni Martin Nooj na badala yake kuingia mkataba na makocha wazawa Boniface Charles Mkwasa akisaidiana na Hemed Morocco. 

  Tangu walimu hawa wamechukua timu ya Taifa Stars tumefungwa mechi mbili tuu za mashindano dhidi ya Algeria na Malawi ugenini, tumetoka sare na Uganda ugenini, tumetoka sare na Nigeria na Algeria nyumbani na kuwafunga Malawi nyumbani. 

  Aidha timu ya Kilimanjaro Stars chini ya kocha Abdalla Kibadeni na msaidizi wake Juma Mgunda katika mashindano ya CECAFA Challenge katika mechi nne ilizocheza Ethiopia haikufungwa hata mechi moja kwa muda wa mchezo (Open Play) ingawa ilitolewa kwa penati tano tano katika hatua ya nusu fainali. Katika mashindano hayo Taifa Stars ilishinda mechi mbili na kutoka sare mbili. Kipindi chote ambacho tumekuwa na makocha hawa wazawa kiwango cha Tanzania FIFA kimekuwa kikipanda mara zote.

  Tunawapongeza sana makocha wetu hawa na benchi zima la ufundi. Kwa sasa tunajiandaa na mechi mbali mbali za kufuzu kucheza fainali za Afrika Afcon 2017 nchini Gabon. Mechi hizi ni dhidi ya Tchad tarehe 25/03/2016 ugenini Ndjadema na mechi ya marudiano siku tatu baadae hapa Dar es Salaam tarehe 28/03/2015. 

  Imani yetu ni kuwa timu yetu itaendeleza wimbi la ushindi. Katika kujiandaa na mchezo wetu dhidi ya Nigeria, Taifa Stars iliweka kambi nchini Uturuki na pia timu iliweka kambi Afrika Kusini kujiandaa na mechi dhidi ya Algeria. Kambi hizi zimesaidia sana kuimarisha timu yetu kabla ya mechi hizi kubwa mbili. Katika kujiandaa na mechi dhidi ya Tchadi mwezi Machi mwakani ratiba ya ligi kuu ikiruhusu timu itaweka kambi pia nje ya nchi.

  2. Timu ya Taifa Wanawake “Twiga Stars”.

  Timu yetu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars chini ya kocha Rogasian Kaijage ilifanikiwa kuiondoa Zambia na hivyo kufuzu fainali za michezo ya Afrika Kusini Kongo Brazaville. Katika fainali hizi Tanzania ilifungwa na Ivory Coast na Nigeria na kutoka sare na Congo, hivyo kutolewa kaika hatua za makundi. Tunaamini uzoefu uliopatikana katika mashindano hayo utaimarisha timu na kufanya Twiga Stars iweze kushiriki fainali ya Afrika ya mpira wa wanawake nchini Cameroon mwaka 2016.

  Hatua ya awali Tanzania itapambana na Zimbabwe mwezi Machi 2016 na mshindi wa michezo huo atacheza hatua ya pili dhidi ya mshindi kati ya Namibia na Zambia.

  3. Udhamini na michuano mipya.
  Kwa kipindi hiki cha mwaka 2015 tumefanikiwa katika maeneo yafuatayo:
  3.1 Kufufua Kombe la Shirikisho Azam Sports Federation Cup.
  Kwa kushirikiana na mdhamini Azam Sports Kombe la Shirikisho limefufuliwa na kuboreshwa. Kwa mwaka huu tumeanza na timu 64 ambazo ni za ligi kuu (16), Ligi daraja la kwanza FDL (24) na Ligi daraja la pili SDL (24). Ili kupanua uwigo wa ushiriki wa Mikoa yote kwa misimu ya usoni timu mabingwa wa mikoa (RCL) nazo zitashirikishwa katika mashindano haya ili kila mkoa wa Tanzania upate fursa ya kushiriki katika mashindano haya. Fainali itachezwa mwezi Mei na bingwa wa Kombe hili ataiwakilisha Tanzania katika kombe la Shirikisho la Afrika CAF Confederation Cup.

  3.2 Udhamini Ligi daraja la kwanza.
  Tumefanikiwa kupata wadhamini wawili kwa ligi daraja la kwanza FDL. Tumempata STARTIMES ambayo ni mdhamini mkuu wa ligi na pia kampuni ya Television ya Sahara Media kupitia STAR TV imepewa haki za kuonyesha mechi hizi moja kwa moja. Haya ni mafanikio makubwa kwa ligi ya daraja la kwanza. Tunaishukuru kampuni ya Geita Gold kwa kuidhamini timu ya daraja la kwanza ya Geita Gold Sport na tunazidi kutoa wito kwa washirika wengine wazidi kujitokeza kudhamini timu zetu.

  3.3 Mkataba wa Vodacom na Ligi Kuu.
  Kampuni ya Vodacom baada ya mazungumzo marefu tuliafikiana na kutuliana saini ya mkataba mwingine wa miaka mitatu wa udhamini wa ligi kuu wenye ongezeko la thamani ya udhamini kwa asilimia 40%. Jitihada zimefanyika kuvutia wadhamini wengine nao waje waongeze udhamini kwa ligi kuu. Tunaishukuru kampuni ya ACACIA ambayo imejitolea kuidhamini klabu ya ligi kuu ya Stand United haya ni mafanikio makubwa kwa ligi yetu na tunazidi kuvipa moyo vilabu vizidi kupata wadhamini zaidi. 

  Tunayashukuru sana makampuni yote ambayo yamejitokeza kudhamini vilabu mbali mbali na tunazidi kutoa wito kwa makampuni mengine yajitokeze kutoa udhamini ikiwa ni sehemu ya kutangaza biashara na kukuza jina la chapa zao.

  3.4 Udhamini tarajiwa.
  Tunatarajia kupata wadhamini kwa ajili ya Ligi Kuu ya vilabu vya wanawake (Women Premier League) pamoja na ligi kya vilabu vya ligi kuu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 (U-20).

  Jambo hili likifanikiwa matumaini yetu ni kuwa tutaanzisha ligi mpya mbili mwaka 2016, Ligi ya vilabu vya wanawake (Women Premier League) na ligi ya vilabu vya ligi kuu ya vijana umri chini ya miaka 20 (U-20). Mechi hizi nazo zitakuwa zinaonyeshwa moja kwa moja kwenye television.

  Kwa matarajio haya sasa ni vyema uongozi wa kila mkoa kufanya jitihada za kuhakikisha vilabu vya mpira vya wanawake vinaanzishwa ili tuweze kuwa na ligi ya ushindani.

  Ninaomba nichukue fursa hii kuwashukuru washirika wetu wote, ambao kama sio kujitolea kwa haya mafanikio tusingeweza kuyafikia/kuyapata.

  Ahsante Kampuni ya Bia Tanzania kwa kupitia bia ya Kilimanjaro Lager.

  Ahsante Vodacom.
  Ahsante Azam Tv kwa kupitia channel ya Azam Sports HD.

  Ahsante Startimes Media kwa kupitia king’amuzi cha STARTIMES.

  Ahsante Sahara Media kwa kupitia Star Tv.
  Ahsante AIRTEL kwa kutuletea Airtel Raising Star kwa mara nyingine mwaka huu.

  Ahsante Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF.
  4. Soka la Vijana.
  4.1 Fainali za Afrika za vijana umri chini ya miaka 17 (U-17) mwaka 2017 Madagascar.
  Kikosi chetu cha Taifa cha vijana chini ya umri wa miaka 17 (U-17) kinachojiandaa na hatua za mtoano mwezi Juni, 2016 ilikuwa kifanye ziara ya kimichezo katika nchi za Rwanda, Uganda na Kenya, lengo ilikuwa kuwapatia vijana hao uzoefu wa Kimataifa. Wakati tayari kikosi kimejiandaa na kukabidhiwa bendera, akaunti za TFF zilifungiwa na mamlaka za mapato TRA na hivyo safari kuvunjika kwa ukosefu wa fedha. Mpango mkakati ni kuwa mwezi Aprili, 2016 timu hii itaweka kambi nje ya nchi ili kujiandaa na hatua ya mtoano (qualifiers).

  4.2 Fainali za Afrika U-17 mwaka 2019.
  Maandalizi ya fainali hizi ambazo Tanzania itakuwa mwenyeji yanaendelea vizuri vikao na Wizara tayari vimeanza kwa ajili ya kufanya maandalizi muhimu ya awali ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo. Pia maandalizi ya timu itakayoshiriki fainali hizi yameanza kwa vijana umri chini ya miaka 13 (U-13) kujumuishwa pamoja katika shule ya Alliance jijini Mwanza. Imani yetu ni kuwa Tanzania tutafanikiwa kuandaa mashindano mazuri mwaka 2019 na pia kunyakua kombe hili.

  4.3 Vituo vya mikoa vya kukuza na kuendeleza vipaji.
  Azma ya TFF ni kuhakikisha kuwa kila chama cha mpira wa miguu cha mkoa kinakuwa na kituo mama cha kukuza na kuendeleza vipaji vya mpira. Mkataba wa mfano (template) umekwisha pelekwa katika kila mkoa ili vyama vya mkoa ambavyo havina vituo vyake basi viingie mkataba wa ushirikiano na kituo kimoja kwa lengo la kukifanya kiwe kituo mama cha mkoa. Kupitia vituo hivi TFF itaweza kuratibu shughuli za maendeleo ya mpira wa vijana katika mikoa yetu, kuongeza nguvu kwa kuvipatia vifaa na walimu. Mipira 5,000 ya 3 na 4 ya ukubwa (size), koni 3,000, beeps 2,000 tayari vimeagizwa toka nje ya nchi kwa kutumia vyanzo vya fedha vya TFF yenyewe bila kuomba msaada kutoka popote kwa ajili ya kuendeleza program hii. Tayari kila mkoa una mwalimu angalau mmoja aliyefanya kozi ya FIFA ya ukocha wa vijana isipokuwa mikoa miwili tu ya Manyara na Njombe, jitihada zitafanyika nao wapate walimu stahiki. 

  Hivyo mtaji wa kutosha tunao wa kuanzisha vituo hivi. Pindi vituo hivi vikiimarika yataanzishwa mashindano ya kiumri (age categories) baina ya vituo hivi kuanzia ngazi ya mkoa, kanda na hatimaye Taifa. Ninatoa wito kwa viongozi wenzangu wa mikoa tujizatiti tuweke nguvu katika uwanzishwaji na uendelezaji wa vituo hivi ambavyo vitakuwa chachu kuu ya kutoa wachezaji wa Taifa wa kike na wakiume. Baada ya mazungumzo haya nitawakabidhi viongozi wa vyama vya mpira vya mkoa wa Manyara na Dar es Salaam mpira mmoja mmoja ikiwa ni ishara ya kuanzishwa rasmi kwa program hii ya kitaifa.

  5. Kozi mbalimbali.
  Kwa kushirikiana na CAF na FIFA Shirikisho letu limeandaa, kuratibu na kutoa kozi mbali mbali za waamuzi na makocha katika ngazi mbalimbali. Jitihada kubwa zimefanyika kuhakikisha mikoa iliyokuwa na hazina ndogo ya makocha na waamuzi inapewa fursa ya kuratibu kozi hizi. Tunashukuru viongozi wote wa mikoa na wilaya ambao tumeshirikiana nao kutimiza azma hii. Juhudi zinaendelea ili tuweze kupata makocha, waamuzi, madaktari wa michezo na watawala zaidi. Ninaomba tuwape moyo wakina mama wazidi kujitokeza kwa wingi kufanya kozi hizi maana wao ndio nguzo kuu ya kuendeleza mpira wa wanawake nchini mwetu. Ninatoa rai kwa waajiri, hasa wakurugenzi wa Halmashauri ambao ni waajiri wa walimu wanaofundisha mpira mashuleni, wazidi kutupatia ushirikiano kwa kutoa ruhusa kwa waajiriwa wao pindi wanapoomba kuhudhuria kozi mbalimbali zitolewazo na TFF.

  6. Bodi ya Ligi na Vilabu.
  Utendaji katika bodi yetu umeimarishwa kwa kutoa ajira kwa mtendaji mkuu Ndugu Boniface Wambura. Mipango ya kuimarisha sekretariet ya Bodi ikiwa ni pamoja na kupata nafasi kubwa zaidi ya kufanyia kazi iko mbioni. Matarajio yetu ni kuwa chombo hiki kikiweza kuimarika kitakuwa ni chachu ya kuandaa ligi zilizo bora zaidi na zenye ushindani.

  Pamoja na jitihada za kutafuta wadhamini wa mashindano mbalimbali yanayohusisha vilabu, jitihada pia zinaendelea kufanyika kuhakikisha vilabu vyetu vinaimarisha utawala bora. Kufuatia CAF na FIFA kuanzisha utaratibu wa kutoa leseni kwa vilabu (Club Licencing) jitihada sasa zinafanyika kuhakikisha vilabu vinaelimishwa kwa kina juu ya mahitaji ya leseni hizi. Katika utaratibu wa leseni za vilabu, vilabu vyetu sasa vitalazimika kuwa na ofisi, watendaji wa kuajiriwa, kuwa na maeneo ya kufanyia mazoezi, kuwa na program ya maendeleo ya vijana, kuajiri walimu wenye sifa n.k. Tunaamini utaratibu wa leseni za vilabu ukitekelezwa ipasavyo uendeshaji wa vilabu vyetu utaboreshwa na hivyo kuongeza tija kwa vilabu vyetu.

  7. Tiketi za Eletroniki.
  Kutokana na matatizo yaliyojitokeza matumizi ya tiketi za eletroniki yalisimamishwa na mmiliki wa uwanja wa Taifa ambaye ni Serikali. Baada ya mazungumzo na mtoa huduma ambaye ni Benki ya CRDB ilikubaliwa atafutwe mshauri mwelekezi (Consultant) kwa kupitia mfumo mzima ili kubaini matatizo na baadae kutoa ushauri wa namna ya kuboresha mfumo huo. Tenda ya kumpata mshauri huyu ilikwishatangazwa na kinachofuatia ni TFF kwa kushirikiana na CRDB kuteua mshauri huyo. Imani yetu ni kuwa kazi ya mshauri ikikamilika basi mwongozo utapatikana ili utekelezaji wa uboreshaji wa mfumo ukamilike na matumizi ya tiketi za eletroniki yaweze kuendelea.

  8. Mfuko wa Maendeleo ya Mpira (Football Development Fund).
  Baada ya mfuko huu kuanzishwa kikatiba katika mkutano mkuu uliopita, kamati ya utendaji ya TFF iliteua wajumbe wa kamisheni ya uendeshaji wa mfuko huu chini ya Mwenyekiti Ndugu Tido Mhando na Mtendaji Mkuu Henry Tandau. Mfuko huu tayari umefanikiwa kupata ofisi yake na shughuli zake zitaanza punde baada ya kuwekewa vitendea kazi. Lengo la mfuko huu kama ilivyoanishwa ni kuwa chanzo kikuu cha kupata rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya mpira wa miguu nchini mwetu. Ninaomba tuwaunge mkono na kuwapa ushirikiano watendaji wa mfuko huu huku tukitambua kuwa maendeleo ya mpira yanahitaji rasilimali nyingi.

  9. Kufungiwa akaunti za TFF.
  Kutokana na madeni ambayo yamekuwa kwenye mafaili ya mamlaka ya mapato kwa kipindi karibia miaka mitano iliyopita, mamlaka ya mapato nchini TRA iliamua kuzifungia akaunti zetu na pesa yote kuhamishiwa Benki kuu. Mazungumzo yanaendelea kati ya TFF, Mamlaka ya mapato na Wizara husika ili fedha hizi ziweze kurudishwa. Tunaushukuru uongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambao wametusaidia kutuongoza namna ya kukabiliana na changamoto hii.

  OMBI KWA SERIKALI.
  Duniani kote, iwe katika nchi tajiri au maskini, michezo huendelezwa kwa ushirikiano wa karibu kati ya Serikali na taasisi zinazoendesha shughuli za michezo husika. Tunaiomba serikali tuzidi kushirikiana kwa karibu katika kuandaa timu zetu za Taifa, kuboresha miundo mbinu ya kuchezea mpira, kusaidia upatikanaji wa vifaa vya michezo kwa gharama nafuu, kuto fursa kwa waajiriwa wake, hasa walimu, wafanye kozi mbalimbali za ukocha na uamuzi. TFF itafarikika sana iwapo itapewa fursa na Serikali ya kuratibu na kusimamia mpira wa miguu katika mashindano ya Taifa ya shule za msingi (UMITASHUMTA) na Sekondari (UMISSETA). Tunaamini TFF ikipewa fursa hiyo itaongeza uweledi katika usimamizi wa mashindano hayo na kuhakikisha vipaji vinaibuliwa kila mwaka kuliko ilivyo sasa.

  Ndugu zangu, wakati tunauaga mwaka 2015 na kuelekea kuingia mwaka 2016 ninaomba nimalizie kwa kutoa wito kwa wadau wote wa mpira wa miguu Tanzania tuzidi kushirikiana, penye makosa tukosoane japo kwa staha na penye kuhitaji ushauri tushauriane.

  Imani yetu ni kuwa mwaka 2016 utakuwa ni mwaka wa mafanikio kwa mpira wetu.
  Mungu Ibariki Tanzania.

  Mungu Ibariki Afrika.
  Ahsanteni,

  Jamal Malinzi
  Rais wa TFF

  Dar es Salaam.

  30 Desemba, 2015.

  0 0

    
  STATE HOUSE ZANZIBAR

  OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

  PRESS RELEASE

    Zanzibar                                                                 30.12.2015
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo ametembelea miradi ya Maendeleo ukiwemo mradi wa gati mpya pamoja na mradi wa maji safi na salama huko Wilaya ndogo Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja na kueleza kuwa ahadi zake zina lengo la kuwasaidia wananchi na kuwaletea maendeleo endelevu.


  Akizungumza na wananchi mara baada ya kutembelea miradi hiyo Dk. Shein alisema kuwa amefurahishwa kwa kiasi kikubwa na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo ambayo itakuwa ni mkombozi mkubwa katika kuwaletea maendeleo sambamba na kuimarisha huduma za kijamii.


  Dk. Shein alisema kuwa  ujenzi wa gati mpya   umejengwa kwa kitaalamu zaidi kwani gati hiyo itahilimi vishindo vya vyombo vyote kwani juhudi hizo zote ni kwa ajili ya usafiri wa uhakika wa wananchi wa kisiwa cha Tumbatu pamoja na bidhaa zao hasa ikizingatiwa kuwa wananchi hao wa Tumbatu wao wenyewe ndio waliokuwa mafundi chini ya usimamizi wa Shirika la Bandari.


  Katika maelezo yake  Dk. Shein alisema kuwa ujenzi huo wa gati ni miongoni mwa maendeleo makubwa yaliokusudiwa kwa ajili ya wananachi wa Tumbatu ambapo kabla ya kuwepo kwa gati hiyo wananchi hao walikuwa wakipata usumbufu mkubwa.


  Akieleza kuhusu mradi mpya wa maji safi  na salama, Dk. Shein alisema kuwa kutokana na kuwa maji ni uhai na hakuna maisha ya mwanaadamu bila ya kuwepo kwa huduma ya maji ndipo Serikali ikaona haja ya kuwaongeza huduma hiyo wananchi wa Tumbatu kwa kuanzisha mradi huo mpya wa maji.


  Dk. Shein alisema kuwa lengo na madhumuni ya mradi huo ni kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi wa Tumbatu hivyo aliwataka wananchi hao kuutunza mradi huo ili uwasaidie zaidi wao na vizazi vyao vijavyo.


  Aidha, Dk. Shein aliwaahidi wananchi wa Tumbatu kuwa matangi kwa ajili ya maji yatajengwa  kisiwani humo na Serikali kwani uwezo huo inayo.


  Pamoja na hayo, Dk. Shein aliwataka wananchi wa Tumbatu kuwapuuza wale wote watakaobeza miradi hiyo kwani hulka hizo ni miongoni mwa hulka za baadhi ya wanaadamu na kusisitiza kuwa mwanaadamu yeyote anaepata neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni vizuri akashukuru.


  Dk. Shein pia, alitumia fursa hiyo kuwapongeza wananchi wa Tumbatu kwa kushiriki vyema katika ujenzi wa miradi hiyo na kuwaadi kuwa Serikali yao itaendelea kuwaunga mkono katika kuwapelekea miradi ya maendeleo.


  Akitoa shukurani kwa wazee wa Tumbatu, Dk. Shein alipokea ombi lao la kutaka kuimarishiwa zaidi kituo chao cha Polisi kwa lengo la kuongezewa ulinzi wanachi hao pamoja na mali zao huku akiwaahidi kuwa juhudi zitachukuliwa na Serikali katika kukiimarisha zaidi kisiwa cha Tumbatu kwa kujenga barabara pamoja na taa maalum za muangaza wa jua kwa mashirikiano ya pamoja Serikali na uongozi wa Jimbo hilo.


  Nae Mwakilishi wa Jimbo la Tumbatu Mhe. Haji Omar Kheir alitoa pongezi kwa Dk. Shein kwa juhudi zake za makusudi za kuhakikisha wananchi wa Tumbatu wanapata huduma bora maendeleo zikiwemo huduma za afya, maji safi na salama,umeme, elimu ujenzi wa gati na huduma nyenginezo.


  Aidha, Mwakilishi huyo wa Tumbatu ambaye pia, ni Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ alitoa pongezi kwa Wizara ya  Miundombinu na Mawasiliano pamoja na Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati kwa kutekeleza kwa vitendo Ilani ya CCM.


  Mapema Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Zanzibar Abdalla Juma alimueleza Dk. Shein kuwa ujenzi wa gati hiyo mpya ni kutekeleza agizo la Serikali na kusema kuwa kwa upande wa Tumbatu umekamilika na kilichobaki ni mambo madogo madogo huku akieleza kuwa kwa upande wa gati ya Mkokotoni ujenzi wake unatarajiwa kuanza mapema mwaka ujao.


  Mkurugenzi Juma alisema kuwa ujenzi wa gati hiyo mpya kwa upande wa Tumbatu ambayo tayari imeshaanza kutumika hadi kumaliza kwake utagharimu Shilingi 374 ambapo kwa upande wa gati ya Mkokotoni ambayo tayari michoro yake ipo, itagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni moja na wakati wowote tenda yake itatangazwa.


  Alisema kuwa kwa upande wa gati ya Tumbatu ni kwa ajili ya vyombo yote vidogo vidogo vikiwemo vile vya kienyeji ambapo pia, limejengwa eneo maalum kwa ajili ya mizigo na kwa upande wa Mkokotoni bandari hiyo mpya itatumiwa na hata boti kubwa.


  Nae Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dk. Mustafa Ali Garu kwa upande wake alisema kuwa mradi huo mpya wa maji safi na salama kisiwani unaotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar umeshaanza kutoa huduma huku akieleza kuwa mchango mkubwa umetolewa na wananchi wa Tumbatu, Mwakilishi wa pamoja na Washirika wa Maendeleo wakiwemo Ubalozi wa Marekani na Iran.


  Garu alisema kuwa mradi huo unatarajiwa kuwa na visima vitatu ambapo tayari hivi sasa kisima kimoja kimeshaanza kazi kilichochimbwa huko Donge Kipange na vyengine vinaendelea na kueleza kuwa kukamilika kwa visima hivyo na kuunganishwa kwake kutaondosha kabisa upatikanaji wa maji kwa mgao kama ilivyo hivi sasa na badala yake yatapatikana kwa muda wote wa masaa 24.


  Garu alisema kuwa Mradi huo unatekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia ZAWA ikiwa ni pamoja na kulaza mabomba baharini na  uchimbaji visima na kueleza kuwa gharama za Mradi huo ni T. Shilingi Bilioni moja na nusu na kwa hivi sasa tayari Shilingi milioni 700 zimeshatumika.


  Nao wazee wa Tumbatu walitoa pongezi kwa Dk. Shein kwa juhudi za makususdi anazozichukuwa za kuwapelekea maendeleo wananchi wa kisiwa hicho sambamba na kutekeleza kwa vitendo ahadi anazowaahidi.


  Sambamba na hayo, Wazee hao walimueleza Dk. Shein kuwasaidia kukiimarisha kituo chao cha polisi kwa lengo la kuimarisha hali ya usalama katika kisiwa chao.  
  Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

  Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

   E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk  0 0

  SPIKA WA BUNGE, JOB NDUGAI AMEREJEA LEO KUTOKA INDIA ALIKOKUWA KWA AJILI YA MATIBABU. AWASHUKURU WATANZANIA KWA MAOMBI YAO. AELEZEA HALI YAKE KUWA NI IMARA KABISA.
   Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akilakiwa na Naibu Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson mara baada ya kuwasili katika uwanja Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nchini India alikokuwa kwa ajili ya matibabu.
   Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akilakiwa na Naibu Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson mara baada ya kuwasili katika uwanja Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nchini India alikokuwa kwa ajili ya matibabu.
    Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Naibu Waziri wa Nishai na Madini Mhe. Medard Kalemani mara baada ya kuwasili katika uwanja Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nchini India alikokuwa kwa ajili ya matibabu. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambula na aliyeko kulia ni Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah.

   Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai na Mkewe wakisalimiana na Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah mara baada ya kuwasili katika uwanja Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nchini India alikokuwa kwa matibabu.

   Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akifafanua jambo kwa Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai mara baada ya kumpokea katika uwanja Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nchini India alikokuwa kwa ajili ya matibabu. Katikati ni Naibu Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson.

  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khadija Bakari Juma akitoa ufafanuzi kwa Wadau waliohudhuria hafla ya Utiaji Saini wa Mikataba miwili ya Ujenzi baina ya Wizara yake na Makandarasi kutoka M/S. Hamphrey Construction Limited ya Arusha na Mindset Teches (T) ya Dar es Salaam Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Wizara ya Elimu Zanzibar.
   Wadau mbalimbali waliohudhuria katika sherehe za kutiliana saini mikataba hiyo.
    Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khadija Bakar Juma na Mkandarasi wa Kampuni ya M/s.Humphrey Construction Limited ya Arusha wakitiliana saini Mkataba wa kupanua Taasisi ya Maendeleo ya Utalii iliopo Maruhubi.
   Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Khadija Bakar Juma na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi M/s. Humphrey Construction Limited ya Arusha wakibadilishana Mikataba baada ya kutiliana saini.

   Mkandarasi wa Kampuni ya M/s. Mindset Techies (T) Limited ya Dar es Salaam Thabit Kombi akitia saini Mkataba wa Ujenzi wa Kupanua Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume katika ukumbi wa Wizara ya Elimu Zanzibar.
   Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Khadija Bakar Juma na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi M/s. Mindset Techies (T) Limited ya Dar es Salaam Thabit Kombi wakibadilishana Mikataba baada ya kutiliana saini.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya habari Utamaduni Na Michezo Zanzibar Issa Mlingot Ali akizungumza na Wadau waliohudhuria katika Mkutano huo.

  PICHA NA ABDALLA OMAR ( HABARI- MAELEZO ZANZIBAR)

  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (wa pili kulia) akizungumza na watumishi wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto) akimsikiliza Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Claudia Mpangala alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto) akiwahimiza watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma kuwajibika alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akitazama nyaraka inayoandaliwa kutunzwa katika nakala laini (soft copy) alipoitembelea Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa mapema leo.


  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kulia) akitazama moja ya kifaa cha kutunzia kumbukumbu alipoitembelea Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa mapema leo.

  0 0

  Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (katikati), akizungumza na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge wakielekea kukagua mitambo ya kusafisha na kusafirisha maji Wami, katika Halmashauri ya Mji wa Chalinze, mkoani Pwani leo.
  Rais Jakaya Kikwete na Lwenge wakiangalia mitambo ya kusafisha maji
  Wakiwa katika picha ya pamoja
  Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete , akizungumza na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge (kushoto kwake) wakielekea kukagua mitambo ya kusafisha na kusafirisha maji Wami, katika Halmashauri ya Mji wa Chalinze, mkoani Pwani leo.Wa pili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete.
  Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akionesha kitu walipotembelea mitambo ya maji Wami
  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge katika mitambo hiyo.

  0 0


  Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde akizungumza na wafanyakazi wa tigo baada ya kufanya ziara mapema leo katika makao makuu ya Tigo kijtonyama jijini Dar es laam
  Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na waandishi wa habari na wafanyakazi wa tigo baada ya kufanya ziara mapema leo katika makao makuu ya Tigo kijitonyama Dar es laam
  Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez , akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) katika mkutano alioshiriki pia Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde baada ya kufanya ziara katika makao makuu ya Tigo Kijtonyama jijini Dar es laam

  Dar es Salaam, 30th December 2015- Tigo Tanzania leo imepokea kwa furaha ugeni wa ghafla wa Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo yaliyoko Kijitonyana jijini Dar es Salaam.

  Mhe. Mavunde ambaye alikuwa ameongozana na waandishi wa habari na maofisa kutoka ofisi za uhamiaji alitinga ofisini hapo mnamo saa nne asubuhi ya Jumatano ya tarehe 30 Desemba na kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Bwana Diego Gutierrez pamoja na wafanyakazi wengine wa kampuni ya Tigo.

  Bwana Gutierrez alimtembeza Naibu Waziri kwenye idara mbalimbali za kampuni hiyo huku akitambulisha huduma zinazotolewa na kujibu maswali yaliyokuwa yakiulizwa na Mhe. Waziri.

  Kampuni ya Tigo imekuwa mstari wa mbele kwenye sekta ya mawasiliano kwa kutoa huduma na bidhaa zenye ubunifu na manufaa makubwa kwa jamii, hivyo kuchangia kwa kiasi kukubwa sana kuendeleza sekta hii muhimu kupitia njia mbali mbali kama kutoa ajira, kuchangia pato la taifa, kuchangia maendeleo ya jamii na kuwezesha watanzania wajiendeleze kiuchumi na kijamii kupitia mawasiliano ya bei nafuu.

  Bwana Gutierrez alisema kampuni ya Tigo imefurahishwa mno na ugeni huo huku akiongeza kuwa ugeni huo unadhihirisha kwamba serikali imeonesha kwamba inajali huduma zinazotolewa na mashirika ya sekta binafsi.

  Bwana Gutierrez alisema “Tutaendelea kushirikianana na serikali ya awamu ya tano kuhakikisha kuwa sekta ya mawasiliano inakua zaidi na inaleta mabadiliko lukuki kwenye maisha ya watanzania na nchi nzima kwa ujumla. Tigo imejikita kwenye kupanua wigo wa mawasiliano kuhakikisha kila mtanzania popote alipo anaweza kuwasiliana kwa bei nafuu, kupitia mtandao bora na wenye huduma zenye uhakika".

  Kuhusu kuitembelea Tigo, Mh. Mavunde alisema: "leo tumetembelea kampuni ya Tigo, kwa ajili ya kujitosheleza vipi kampuni hii inajali waajiri wake, na katika ziara hii tumebaini mambo kadha ambayo tungependa kampuni ya Tigo, ivifanyie kazi kwa mfano kwenye maswala ya afya na usalama, na pia tungependa kuona mikataba baina ya Tigo na watoa huduma wake, pia serikali ya awamu ya tano, ipo makini kuhakikisha sheria inafuatwa ili tuwe na jamii inayozingatia sheria"

  0 0

  ummy-msd 175
  Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitembelea moja ya ghala la kuhifadhia dawa iliyopo makao makuu ya MSD,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laureane Bwanakunu na watatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya MSD Prof.Idris Mtulia.
  ummy-msd 178
  Waziri Ummy akiuliza jambo kwa wafanyakazi wa bohari hiyo.
  ummy-msd 185
  Waziri huyo akiendelea na ukaguzi wa maghala hayo, kulia ni Mkurugenzi wa Ugavi Misanga Muja na kushoto ni mwenyekiti wa Bodi ya Bohari hiyo.
  ummy-msd 190
  Baadhi ya watumishi wakiendelea na kazi ya kuhakiki dawa kwenye moja ya ghala mojawapo.

  ummy-msd 191
  Waziri Ummy akielekea kwenye ujenzi wa jengo jipya linaloendelea kujengwa, ambapo linatarajiwa kumalizika kujengwa mwezi Juni, 2016 ,Kushoto ni Katibu mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Donnan Mmbando.
  ummy-msd 198
  Mkurugenzi wa MSD Bwanakunu akieleza dira,malengo na majukumu ya Bohari hiyo.
  ummy-msd 202
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiangalia dawa zilizowekwa nembo ya serikali (GoT) ambayo itasaidia udhibiti wa upotevu wa dawa nchini.
  ummy-msd 205
  Waziri huyo akionesha kopo la dawa la Bohari ya dawa.
  ummy-msd 220
  Waziri Ummy akimuonesha ukurasa wa ugawaji fedha za bohari Mwenyekiti wa Bodi ya Bohari ya dawa Prof.Idris Mtuliya.(Picha zote kwa Niaba ya Wizara ya Afya).

  Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametembelea Makao Makuu ya Bohari ya Dawa (MSD) na kuahidi kuwa balozi wa kuhakikisha deni la serikali linalipwa ili kuiwezesha MSD kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

  Waziri huyo ameeleza hayo baada ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu kueleza kuwa ukosefu wa fedha na deni la serikali ni changamoto kubwa inayoathiri utekelezaji mzuri wa majukumu ya MSD.Mbali na hilo, Waziri wa Afya amesema mbali na deni hilo, hata kiasi cha fedha kinachotengwa na serikali kwaajili ya hospitali, vituo vya afya na zahanati na kununua dawa hakitoshelezi mahitaji, hivyo lazima suala hilo lifanyiwe kazi mapema, huku akisisitiza hata kiasi hicho kidogo kinachopatikana kitumike vizuri.

  Katika hatua nyingine ameishauri Bohari ya Dawa kuanza utaratibu wa kununua dawa na vifaa tiba moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, kuhakikisha dawa muhimu zinapatikana wakati wote na kuiagiza MSD itangaze kwenye vyombo vya habari dawa zote ambazo zinapelekwa vituoni, zahanati na kwenye hospitali, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu ameeleza kuwa tayari MSD imeshaanza kubandika kwenye mbao za matangazo za hospitali orodha ya dawa inazofikisha.

  Waziri huyo ambaye alifuatana na Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Donald Mbando na watendaji wengine pia alitembelea maghala ya kuhifadhia dawa ya MSD, jengo la ofisi linalojengwa pamoja na kuwa na mkutano na menejimenti ya MSD, ambapo pamoja na mambo mengine ameipongeza MSD kwa hatua iliyofikia ya kuweka nembo ya GOT kwenye vidonge vyake ili kudhibiti upotevu wa dawa za serikali pamoja na kuanzisha maduka ya dawa Muhimbili, na mengine yanayotarajia kufunguliwa hivi karibuni mkoani Mbeya, Arusha na Mwanza.

  Waziri Ummy Mwalimu alihitimisha kwa kusema kuwa ajenda yake kuu ni upatikanaji wa dawa kwa wakati, kama rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alivyoaainisha, hivyo MSD itekeleze majukumu yake ipasavyo kwani mafanikio ya MSD ni mafanikio kwake pia.


  0 0

  Na Jacquiline Mrisho MAELEZO

  Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam limewatahadharisha wananchi kutokufanya fujo wakati wa  mkesha wa mwaka mpya kwa kuweka mikakati mikali kwa watakaokaidi amri hiyo.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova amepiga marufuku uchomaji wa matairi ya gari,  upigaji baruti, risasi za moto na fataki ambazo zaweza kusababisha madhara wakati wa mkesha wa mwaka mpya.

  “ Ni baraka zaidi kusherekea sherehe kama hizi kifamilia na sio vizuri kuingia mwaka mpya ukiwa mahabusu, huo ni mkosi” Alisema Kamishna Kova.

  Kamishna Suleiman Kova aliongeza kuwa watashirikiana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Jeshi la Zimamoto, kampuni binafsi za ulinzi, vikundi vya ulinzi shirikishi pamoja na kutumia ndege za Polisi kufanya doria ili kuhakikisha kuwa wanailinda amani na kudhibiti aina yoyote ya uhalifu utakaojitokeza.

  Aidha Kamishna Kova amesisitiza kuwa vituo vyote vya polisi vitakuwa wazi masaa 24 ili kuwawezesha wananchi kutoa taarifa haraka pindi wanapopata matatizo au wanapoona dalili zozote za uvunjifu wa amani pia amehakikisha kuwa fukwe zote za bahari na maeneo  yote yenye mikusanyiko yatalindwa.

  Katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka wa 2015 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limetoa rai kwa wananchi kushirikiana na Jeshi hilo katika kuzuia uhalifu kwa kutoa taarifa haraka pindi waonapo dalili za uvunjifu wa amani.

  0 0


  Sehemu ya Wakimbizi wa Kambi ya Nduta, Wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma wakimsikiliza Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza na wakimbizi hao. Majaliwa aliwaonya wakimbizi hiyo kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama katika kambi hiyo.
  Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Kambi ya Nduta, Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wakati alipofanya ziara katika kambi hiyo. Katika hotuba yakekwa wakimbizi wa kambi hiyo, Majaliwa aliwaonya wakimbizi hao kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama katika eneo waliohifadhiwa.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akimwagilia mti wa kumbukumbu alioupanda katika Kambi ya Nduta, Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wakati Waziri huyo alipoambatana na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa katika ziara katika kambi hiyo. Katika hotuba yake, Waziri Mkuu Majaliwa aliwaonya wakimbizi hao kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama katika eneo waliohifadhiwa.
  Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi ya Nduta, wilayani Kibondo, Fred Nsijile akitoa taarifa ya kambi yake kwa Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (kushoto). Katika taarifa hiyo Mkuu wa Kambi alisema kambi yake inakabiliwa na upungufu wa maji kutokana na idadi kubwa ya wakimbizi wanaoishi kambini humo.

  Hata hivyo katika hotuba yake, Waziri Mkuu Majaliwa alisema atalifanyia kazi tatizo hilo na pia aliwaonya wakimbizi katika kambi hiyo kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama katika eneo waliohifadhiwa. Wapili kushoto meza kuu ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima (watatu kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke.
  Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia) akiwafurahia wacheza ngoma ambao ni wakimbizi kutoka Burundi wakati walipokuwa wanamkaribisha katika Kambi ya Nduta, mkoani Kigoma kuzungumza na wakimbizi hao. Katika hotuba yake, Majaliwa aliwaonya wakimbizi hao kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama katika eneo waliohifadhiwa. Wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimkabidhi mkimbizi Cesiwa Angelani (kushoto) zawadi ya ndoo yenye vifaa vya kumuhudumia mtoto baada ya mzazi huyo kujifungua katika Hopsitali iliyopo katika ya Nyarugusu ambapo Wakimbizi wanahifadhiwa. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga.

  0 0

  ni4
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua mfereji wa maji kuangalia upatikanaji wa Maji Safi na Salama alipofanya ziara maalum ya kutembelea miradi ya maendeleo ya Wilaya Ndogo ya Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja leo,[Picha na Ikulu.] (30Disemba2015)
  ni5
  Wananchi na Wanachama wa CCM Jimbo la Tumbatu wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akiwasalimia mara alipofika kijiji cha Tumbatu Kichangani kuangalia maendeleo ya miradi ya Maendeleo katika kijiji hicho leo ikiwemo ujenzi wa Bandari na Maji Safi na Salama iliyofanikisha kwa nguvu za Serikali ya Mapinduzi na Wananchi,[Picha na Ikulu.](30Disemba2015)
  ni6
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa shukurani zake kwa  Wananchi wa Tumbatu Jimbo la Tumbatu waliofika katika mapokezi wakati alipofika Kijiji cha Tumbatu Kichangani Wilaya Ndigo Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja akiwa katika ziara maalum ya kutembelea miradi ya maendeleo ya Kisiwa hicho leo,[Picha na Ikulu.](30Disemba2015)

  ni1
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Tumbatu pamoja na Viongozi mbali mbali wakati alipofika Bandari ya Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja akiwa katika ziara maalum ya kutembelea miradi ya maendeleo ya Kisiwa hicho leo,[Picha na Ikulu.] (30Disemba2015)
  ni2
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo wakati alipokuwa akiangalia ramani ya Ujenzi wa Bandari ya Tumnbatu kutoka waMhandisi Mkuu wa Shirika la Bandari Mbarouk Hamadi Mbarouk wa Shirika la Bandari Zanzibar wakati alipofanya ziara maalum ya kutembelea maendeleo ya miradi ya maendeleo katika kisiwa cha Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja leo,[Picha na Ikulu.]  (30Disemba2015)
  ni3
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wananchi wa Tumbatu Jimbo la Tumbatu waliofika katika mapokezi wakati alipofika Bandari ya Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja akiwa katika ziara maalum ya kutembelea miradi ya maendeleo ya Kisiwa hicho leo,[Picha na Ikulu.] (30Disemba2015)

  ni7
  Mzee Hassan Khamis Haji akiwa miongoni mwa Wazee waliokuwa wakimpongeza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa jitihada zake za kuwatembelea wakati alipofika Kijiji cha Kichangani Wilaya Ndogo Tumbatu leo alipotembelea miradi ya maendeleo ikiwemo wa Maji safi na Salama na Ujenzi wa Bandari iliyojengwa na Mafundi wa Kijiji hicho kwa Usimamizi wa Shirika la Bandari Zanzibar,[Picha na Ikulu.] (30Disemba2015)
  ni8
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) akifuatana na Wananchi pia   Wanafunzi wa madrasa wakisoma Qaswida wakati walipomshindikiza akiwa katika ziara ya kuangalia maendeleo ya Miradi ya maendeleo ya Kijiji cha Kichangani Wilaya Ndogo Tumbatu leo ikiwemo Ujenzi wa Bandari na Maji Safi na Salama,[Picha na Ikulu]

  0 0

  Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (katikati) akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuwatafuta washindi wa droo ya nne ya promosheni ya "Jaza Mafuta na Ushinde" inayowawezesha wateja wake kujipatia lita 40 za mafuta kwa kila mshindi wa droo hiyo kila wiki. Kulia ni Mkaguzi wa michezo ya kubahatisha nchini, Bakari Maggid, na kushoto ni Meneja wa Fedha wa Kampuni ya mafuta ya GAPCO Tanzania, Michael Chobu.

  0 0

  Benki ya Exim Tanzania imetangaza kufunga mauzo ya dhamana yake ya muda mrefu (hati fungani) huku ikibainisha kuwa kiasi kilichopatikana kutokana na mauzo ya hati hizo kimezidi mara dufu (asilimia 195) ya malengo ya awali.
  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na benki hiyo jijini Dar es Salaam jana, uuzwaji wa dhamana hizo ulifungwa rasmi Disemba 18 mwaka huu huku benki hiyo ikifanikiwa kukusanya kiasi cha sh bilioni 19.7 kutokana na mauzo ya dhamana hiyo tofauti na makadilio ya sh. bilioni 10 iliyokuwa imejipangia kukusanya hapo awali.
  “Awali lengo letu lilikuwa ni kukusanya takribani kiasi cha bilioni 10 hadi bilioni 15. Tunashukuru kuona kwamba tulichokusanya ni karibu asilimia 200 ya malengo yetu ya awali na kiasi kilichopatakina kimetoka kwa wawekezaji mbalimbali kutoka kila kona ya nchi,’’ alibainisha, Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki hiyo, Bw. Selemani Ponda.
  Kupitia dhamana hiyo wawekezaji wanapatiwa uhakika wa kupata riba ya 14% kwa mwaka isiyokuwa na makato ya kodi,itakayolipwa kila baada ya miezi 6 kwa kipindi cha miaka 6 huku  ikiruhusu wawekezaji wenye kiasi cha kuanzia shilingi milioni moja.
  Akizungumzia zaidi mafanikio hayo Bw Ponda alisema yametoa fursa kwa watanzania kuwa sehemu ya ukuaji wa benki hiyo huku akiongeza;“Mafanikio haya yanaonyesha imani kubwa waliyonayo watanzania kwa benki ya Exim na zaidi wanavutiwa na ubunifu wa benki hii katika huduma za kifedha.,’’
  Bw Ponda alitumia fursa hiyo kuwashukuru baadhi ya wadau ikiwemo Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana nchini (CMSA), Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Wakala wa mauzo ya dhamana hiyo, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) pamoja na wawekezaji wote kwa kufanikisha mchakato mzima wa mauzo ya dhamana hiyo.

older | 1 | .... | 726 | 727 | (Page 728) | 729 | 730 | .... | 1898 | newer