Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 728 | 729 | (Page 730) | 731 | 732 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki  la Dar es salaam katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo January 1, 2016. Kardinali Pengo alilazwa hospitalini hapo jana jioni kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.PICHA NA IKULU


  0 0


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewapongeza Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu, mara baada ya kuapishwa Ikulu leo jijini Dar es Salaam.  

  MAJALIWAAmetoa pongezi hizo wakati Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu wakiwa wametia saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma mbele ya waandishi wa habari.

  Waziri Mkuu Majaliwa pia amewataka viongozi hao, kuwa waaminifu, kuwajibika na  kutoa taarifa ya utendaji kwa wananchi.

   Aidha, alisema kuwa, viongozi wengine watakao apa mbele ya Kamishna wa Tume ya Maadili ni pamoja na  Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri, ikiwa ni hatua ya Serikali kudhibiti na kufuatilia matumizi ya rasilimali fedha.

  “Wakuu wa Wilaya watahakikisha fedha zilizoenda katika Halmashauri zao lazima zitumike katika shughuli zilizokusudiwa” alisema Waziri Mkuu.

  Waziri Mkuu alitoa wito kwa watanzania kuendelea kuwa na imani na Serikali ya Awamu ya Tano, kwakuwa itatimiza ahadi zote ambazo Mheshimiwa Rais na Makamu wa Rais walizitoa wakati wa Kampeni.

  Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu hao, wameapishwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli, ambapo shughuli hiyo ilihudhuriwa pia na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Mke wa Mheshimiwa Rais mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi mbalimbali.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI
  S.L.P 3021
  1141O DAR ES SALAAM
  IJUMAA, JANUARI 1, 2016.

  0 0

  B1
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiongoza Matembezi ya wanamichezo katika Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa yaliyofanyika leo kwa kuwanzia Uwanja wa Tumbaku Mjini Unguja na kumalizia Uwanja wa Amaan Studium.[Picha zote na Ikulu.]
  B2
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiongoza Matembezi ya wanamichezo katika Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa yaliyofanyika leo kwa kuwanzia Uwanja wa Tumbaku Mjini Unguja na kumalizia Uwanja wa Amaan Studium.
  B3
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wanamichezo wa Vikundi mbali mbali kama ishara ya kuyapokea maandamano ya vikundi hivyo katika kilele cha Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
  B4
  Wamamichezo wa Vikundi vya mazoezi wakipita mbele ya jukwaa kubwa Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika kilele cha Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa yaliyofanyika leo ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.

  B5
  Wamamichezo wa Vikundi vya mazoezi wakipita mbele ya jukwaa kubwa Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika kilele cha matembezi ya Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa yaliyofanyika leo ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
  B6
  Wanakikundi cha Amakweli Fitness Club ya Welezo Grinada wakibeba bango la Chama cha Mchezo wa Maziezi ya Vuingo Zanzibar (ZABESA) linalosema “JIKINGE DHIDI YA MARADHI YA KISUKARI PRESHA NA SARATANI KWA KUFANYA MAZOEZI”wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipoyapokea matembezi ya Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
  B7
  Kikundi cha Mazoezi Mwera Fitness Club kikipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipoyapokea matembezi wakati wa Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
  B8
  Kikundi cha Mazoezi Chumbuni Studio kikipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipoyapokea matembezi wakati wa Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
  B9
  Kikundi cha Mazoezi kutoka Kisiwani Pemba kikipita mbele mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipoyapokea matembezi ya Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
  B10
  Kikundi kutoka Dar es Salaam ni miongoni mwa vikundi vilivyojumuika katika matembezi ya Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
  B11
  Kikundi kutoka Dar es Salaam ni miongoni mwa vikundi vilivyojumuika katika matembezi ya Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
  B12
  Miongoni mwa Vikundi vya Mazoezi hapa Mjini Unguja nacho kikionesha manjonjo ya aina ya mazoezi mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika kilele cha Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguj.

  0 0

  Bella d (80)Christian Bella akipagawisha mashabiki waliofika Dar Live kwenye shoo ya mkesha wa kuukaribisha mwaka mpya 2016.Bella d (81)Malaika Band wakifanya yao.Bella d (82)Mashabiki wakiserebukaBella d (83)Bella d (84)...wakichukua matukio muhimu ya shoo hiyo kwa simu za mkononi
  Bella d (85)Bella d (86)Bella d (87)Ni hatariBella d (88)Bella d (89)Bella akiwaongoza Malaika Band kutumbuiza ukumbini hapoBella d (93)Bella d (94)Bella d (95)Bella d (96)Bella d (97)...shoo si ikanoga sasaBella d (98)Bella d (99)Bella akitamba jukwaaniBella d (48)Bella d (52)Mashabiki wakinogewa na shoo ya Malaika BandBella d (55)Bella d (59)Bella d (65)Bella d (67)Bella d (68)Bella d (70)Bella d (73)Bella d (75)Bella d (76)Bella d (77)Bella na jukwaa, Bella na mashabikiBella d (81)Kama kawaida yao Malaika Band wakikinukisha jukwaaniBella d (82)Bella d (83)Mashabiki wakifuatilia shoo hiyobella (1)Shabiki akipanda jukwaani kucheza na Bella bella (2) Dada huyu akikata mauno wakati wa shoo hiyobella (7)bella (9)bella (10)bella (15) Shabiki na Bella jukwaanibella (16) Bella akiendelea kuwasha motobella (19)bella (20)Shabiki akimzawadia Bella bella (24) Zawadi zikimiminikabella (56)bella (57)Shoo ikibamba bella (58)bella (59) Shangwe za mwaka mpyabella (60)bella (61)bella (62)bella (63)bella (64) Mashabiki wakipanda jukwaanibella (65)bella (66)bella (67)bella (68) Shoo ikinogabella (69)Bella akicheza na mashabiki wakebella (71)bella (72)bella (73) Shoo ikinogabella (74) Bella na mashabiki jukwaanibella (75)Mashabiki wakizidi kupagwa.
  PICHA NA MUSA MATEJA/GPL

  0 0

  Na"George Binagi-GB Pazzo @BMG
  Mwenyekiti wa Waendesha Pikipiki (Bodaboda) Mkoa wa Mwanza Makoye Kayanda Bunoro anawatakia Waendesha Pikipiki wote nchini Kheri ya Mwaka Mpya 2016 huku akiwasihi kutimiza majukumu yao kwa kufuata sheria na taratibu za Usalama barabarani bila shuruti.

  "Tuache Mchezo na Vyombo vya Moto, Tuvae Elmenti, tusibebe mishkaki (zaidi ya abiria mmoja) tusiendeshe kwa mwendo kasi kwani ni hatari, tusitumie pombe tukiwa kazini huku tikiwapenda abiria na kujiepusha na vitendo vya uhalifu vya aina yoyote". Anasema Bunoro.

  Aidha Bunoro amewaomba radhi wale wote waliopata usumbufu kwa namna moja ama nyingine kutokana na kazi ya bodaboda na kwamba kusameheana ndilo jambo la msingi huku akiwakumbusha bodaboda  kujipanga katika majukumu yao ili kuendana na kasi ya Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli ya "Hapa Kazi Tu".
  Bonyeza HAPA Kusoma Zaidi

  0 0

  Binagi Media Group, Kwa Pamoja Tuijuze Jamii, inapenda kuwatakia Kheri ya Mwaka Mpya 2015 Watazamaji, Wasikilizaji na Wasomaji wake wote ndani na nje ya nchi ya Tanzania. 

  Mwaka 2016 uwe wa Mafanikio zaidi kwenu huku kila mmoja akijiweka karibu na uwepo wa Mwenyezi Mungu.Ahadi yetu ni kuendelea kukuletea Habari na Matukio mbalimbali kadri yanavyotufikia na kadri tunavyoyafikia. Hakika Binagi Media Group, Kwa Pamoja Tuijuze Jamii inawajali na Kuwathamini.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence S.Milanzi akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Naibu wakatibu wakuu  iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Jaji Meja Jenerali Projest A.Rwegasira akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na  Naibu wakatibu wakuuiliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora,Dkt.Laurian Ndumbaro akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na  Naibu wakatibu wakuuiliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya Waandishi mbalimbali wa Vyombo vya Habari wakifuatilia kwa umakini hafla ya kuwaapisha kwa Makatibu Wakuu na  Naibu wakatibu wakuuiliyofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,Amina H.Shaban akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Naibu wakatibu wakuu  iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje,Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa,Balozi Ramadhan  Muombwa Mwinyi akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Naibu wakatibu wakuu  iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Immaculate Peter Ngwale akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Naibu wakatibu wakuu  iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi,Profesa Simon S.Msanjila akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Naibu wakatibu wakuu  iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Profesa James Epifani Mdoe akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Naibu wakatibu wakuu  iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,James Dotto akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Naibu wakatibu wakuu  iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria,Amon Mpanju akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na  Naibu wakatibu wakuuiliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya Makatibu Wakuu na Naibu wakatibu wakuu  kabla ya kuapishwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli.
  Pichani kuliani ni Makamau wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Naibu wakatibu wakuu  Ikulu jijini Dar,wa tatu kulia ni Mke wa Rais,Mama Janeth Magufuli pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Bwa.George Masaju.
  Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa amembatana na  Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakiwasili kwenye hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu wao iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

  0 0
 • 01/02/16--00:25: UCHAMBUZI WA MAGAZETI LEO.

 • 0 0

  Miss Tanzania USA Aeesha Kamara akipata picha ya upendeleo alipofika kwenye mkesha wa mwka mpya ulioandaliwa na Jumuiya ya Watanzania DMV siku ya Alhamisi Desemba 31, 2016 Lanham, Maryalnd nchini Marekani. PICHA NA KILIMANJARO STUDIO
  Asha Hariz Kushoto) pamoja na mama wa mitindo Asya Idarous Khamsini wakipata picha ya pamoja na Miss Tanzania USA Pageant alipohudhuria mkesha wa mwaka mpya DMV.
  Aeesha Kamara katika picha ya pamoja na msanii Patience Ibembo wa Congo mwenye makzi yake Marekani kwa sasa ambaye zamani alikuamcheza show wa Koffi Olomide.
  Kutoka kushoto ni Patience Ibembo, Aeesha Kamara, Mama Winny Casey Mratibu wa Miss Tanzania USA na Rukia Malipula ambaye ni mama mzazi wa Aeesha Kamara.
  Aeesha Kamara akitangaza kalenda ya 2016 iliyotengenezwa na Miss Africa USA na pichga yake kutumika kwenye kalenda hiyo baada ya kuwashinda mamiss wengine wa Africa shindano lililofanyika New York Novemba 2015. 

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Benedict Liwenga-Maelezo.

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamis Kigwangala leo amemtembelea na kumjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Kadinali Polycarp Pengo aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

  Akiongelea kuhusu hali ya Kadinali Pengo, Mhe. Kigwangala alisema kuwa Kadinali Pengo yuko salama katika mikono ya madaktari wa taasisi hiyo na hali yake inaendelea vizuri ambapo ameweza kuongea nae ana kwa ana kiasi cha kuweza kukaa na kuongea.

  ‘’Manzoni alilazwa katika Hospitali ya TMJ iliyopo hapa jijini Dar es Salaam, lakini ikaonekana ni vema akiletwa hapa kwenye Hospitali yetu hii ya juu kabisa ya matibabu ya moyo (Tasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete), hivyo napenda kuwapa taarifa Watanzania kwamba yuko salama kabisa katika mikono ya madaktari wetu na hali yake inaendelea vizuri.’’

  Awali Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli akiongozana na Mkewe mama Janeth Magufuli walienda pia kumjulia hali Kadinali Pengo katika taasisi hiyo na kumtakia afya njema ili aweze kuendelea na shughuli zake za kiroho.

  Kadinali Pengo alifikishwa katika taasisi hiyo ya moyo kwa ajili ya kuchunguzwa afya yake ambapo afya yake kwa sasa imezidi kuimarika.

  0 0

   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Makatibu Wakuu pamoja na Manaibu Katibu Wakuu wakati akifungua Semina Elekezi kwa Makatibu hao Ikulu jijini Dar es Salaam leo January 2, 2015
   Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam.
   Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam.
   Watoa mada katika semina elekezi hiyo wakiwa ni pamoja na (toka kulia) Makatibu Wakuu Kiongozi wastaafu Balozi Dkt. Marten Lumbanga,  Balozi Charles Sanga, Katibu Mkuu Mstaafu Ofisi ya Rais - Utumishi - Mhe. George D. Yambesi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad na wengineo
   Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam.
   Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

  0 0

  id01

  Balozi Seif Ali Iddi akinukuu kifungu cha Katiba ya Zanzibar kinachomruhusu Dkt. Ali Muhamed Shein kuendelea kuiongoza Zanzibar mpaka atakapoapishwa Rais mwengine.
  id1
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu  maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 kufikia miaka 52 Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
  id2
  Baadhi ya Waandishi  wa habari waliohudhuria mkutano wa  Makamu wa Pili wa Rais w Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakifuatiliia mkutano huo uliofanyika  Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
  ……………………………………………………………………………………………….
  Na Khadija Khamis – Maelezo  
  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema kuwa Maadhimisho ya Shereha za Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar yapo kama kawaida na yanatarajiwa kuanza  rasmi tarehe 3.12.2016  kwa kazi za usafi  wa mazingira katika maeneo mbali mbali  ya makaazi pamoja na sehemu za kutolea huduma za kijamii kama vile Hospitali Sokoni  na maeneo mengine.

  Kauli hiyo imetolewa  na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
  Alisema ingawa zoezi  la usafi hufanyika kila tunapoanza maadhimisho ya  Sherehe za Mapinduzi  lakini kwa muda huu wananchi  wanapaswa kuchukuwa  juhudi maalum ili kuhakikisha kuwa maeneo yote yanakuwa safi   muda wote kwa vile  hivi sasa  nchi inakabiliwa  na tatizo kubwa la kuenea kwa maradhi ya kipindupindu.

  “Zoezi la usafi  wa mazingira litakuwa la lazima na kutaandaliwa utaratibu maalum kwa kila Mamlaka za Mikoa ,Wilaya Baraza la Manispaa Mabaraza ya Miji na Halmashauri za wilaya kuratibu zoezi  la usafi na viongozi Wakuu  wa Kitaifa wataungana nasi katika katika maeneo watakayopangiwa, “Alisisistiza.

  Amesema  mbali na usafi wa mazingira, katika maadhimisho ya mwaka huu kutakuwa na shughuli mbali mbali zikiwemo ujenzi wa Taifa ,uwekaji wa  mawe ya msingi  na ufunguzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na burudani na michezo na kilele cha maadhimisho hayo itakuwa siku ya Jumanne katika Kiwanja cha Amaani.

  “Kama  kawaida kila ifikapo tarehe 12 Januari ya kila mwaka nchi yetu huadhimisha sherehe za Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964,  kwa mwaka 2016 tutakuwa tunatimiza miaka 52 tangu viongozi na wazee wetu walivyokomboa nchi yetu,”  alisema Balozi  Seif Ali Iddi.

   Alikumbusha kuwa mafanikio na maendeleo  yaliyopatikana  Zanzibar  yanatokana   na imani na jitihada kubwa za viongozi ambao ni wanamapinduzi chini ya uongozi wa Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume aliyeweka msingi imara wa mashirikiano .Alisema siku ya kilele cha maadhimisho hayo  katika Uwanja wa Amaani  kutakuwa na Gwaride la  Vikosi  vya Ulinzina Usalama , Burudani ya Ngoma za Utamaduni  pamoja na Maandamano ya Wananchi wa Mikoa Mitano ya Zanzibar.

  Makamo wa Pili  Balozi Seif Ali Iddi alisema kuwa sherehe hizo zitahudhuriwa na Viongozi mbali mbali  wa Serikali na vyama vya siasa kutoka Zanzibar na  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .Amewataka  wananchi kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mpinduzi ya Zanzibar na amewahakikishia  Serikali imejipanga kikamilifu kuona kunakuwa na hali ya utulivu na usalama mkubwa katika maeneo yote ya Zanzibar wakati  wa maadhimisho hayo.

  0 0

  Mlimbwende akipita mbele ya mashabiki wa mitindo kuoka kwa gwiji la mitindo Tanzania mama Asya Idarous Khamsini aliponogesha mkesha wa mwaka mpya 2016 uliofanyika Lahnam, Maryaland nchini Marekani. PICHA NA KILIMANJARO STUDIO
  Mlimbwende akipita mbele ya mashabiki.
  Ni vivazi vya mama wa mitindo Asya Idarous Khamisni.
  Mtoto manshallah akiwa ndani ya vazi la mama wa mitindo Asya Idarous Khamsini.
  Mlimbwende akipita mbele ya mashabiki wa vivazi.
  Ilikua ni vivazi kwa kwenda mbele.
  Kijana akijitanashati na kivazi cha Asya Idarous Khamsini.
  Gwiji la mitindo na walimbwende wake.
  Kwa picha zaidi bofya HAPA

  0 0


  0 0

  Hapa ndipo kileleni na Mwonekano wa Irente 
   Hii ni Miamba mikubwa iliyopo Irente na moja ya kivutio kikubwa katika eneo hili kwa upande kwa Kushoto.
  Eneo hili wakazi wa Irente wanaliita Pango ambapo watu wengi wanapenda kupigia picha
  Hii ni njia ya kuelekea Pangoni 
  Ukiwa Juu ndani ya Pango utaona hivi 
  Mmoja wa walinzi akiandika akiwakatia risiti wageni mbalimbali waliotembelea eneo hilo.
   Mmoja wa wandishi wa Blogs za Mikoa Fredy Tony akiwa amefika kujionea eneo hilo.

  Watu wengi wamekuwa na utaratibu wa kukalili kuwa wanapoambiwa kwenda kufanya utalii basi mawazo yanahamia katika hifadhi za taifa au Fukwe za Bahari, wakati kuna utalii wa kupanda milima,utalii wa uwindaji utalii wa picha, utalii wa kiutamaduni,Utalii wa Ikolojia,utalii wa fukwe,Michezo ya kwenye maji, utalii wa mali kale,utalii wa mikutano,utalii wa matibabu,utalii wa mashambani na utalii wa jiji.

  Irente View Point inapatikana katika kijiji cha Irente kilichopo wilayani lushoto mkoani Tanga, eneo hili liligunduliwa na wazee wa kale ambao walikuwa wakifika hapo kwa ajili ya kuomba na kufanya matambiko na wengine walikuwa wakifika katika eneo hilo kwaajili ya kufanya ibada hasa wakati wa sikukuu za Christmas

  Eneo hili lina urefu wa Mita 1500 kutoka usawa wa Bahari , ukiwa juu unaweza kuona maeneo mbalimbali vizuri bila usumbufu wowote, pia watalii wengi wamekuwa wakifika eneo hilo kutokana na hali ya hewa kuwa nzuri, kuona Mandhari nzuri hasa wakati wa asubuhi na jioni.

  Jinsi ya kufikia ikiwa unatokea upande wowote, fika hadi Mombo, panda daladala Tsh 3,000 mpaka Lushoto mjini baada ya hapo unaweza panda Boda boda Tsh 3,000 au ukachukua Tax Tsh 10,000 , kiingilio ni Tsh 2,000. 

  (meandaliwa na Fredy A. Njeje  0 0

   Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akisaidia kupuliza dawa ya kuuwa wadudu katika moja ya nyumba kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Alhamisi ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.

  Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akisaidia kupuliza dawa ya kuuwa wadudu katika moja ya nyumba kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
  Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akisaidia kupuliza dawa ya kuuwa wadudu katika moja ya nyumba kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Alhamisi ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akisaidia kupuliza dawa ya kuuwa wadudu katika moja ya nyumba kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Alhamisi ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.IMG_0144
  Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akizungumza na mmoja wa wazee (jina lake halikupatikana) kabla ya kumpigia dawa ya kuua wadudu nyumbani kwake wakati alipotembelea makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
  IMG_0174
  Dada yake Hoyce Temu, Bi. Edith akishiriki kuondoa vyakula vyombo ili kuruhusu zoezi la upigaji wa dawa ya kuulia wadudu kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
  Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akigawa chakula kwa watoto katika makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza iliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Alhamisi ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
  Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akigawa chakula kwa watoto katika makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza iliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.Kwa matukio zaidi bofya hapa  IMG_9916IMG_9920
  Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (wa pili kushoto) akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (katikati) kushoto Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye ( wa pili kulia), Katibu wa Kamati ya Miss Tanzania Bosco Majaliwa (kulia) pamoja na mpiga picha wa kipindi cha Mimi na Tanzania, Geofrey Magawa a.k.a KIM (kushoto) wakiwasili Desemba 31, 2015 kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam. 

  Na Rabi Hume, Modewjiblog
  Miss Tanzania wa mwaka 1999, Hoyce Temu amemaliza mwaka 2015 kwa kutembelea kituo Nunge ambacho ni makazi ya wazee na walemavu wasiojiweza kilichopo Vijibweni, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

  Hoyce ambaye amekuwa akisaidia watu wa aina mbalimbali wenye matatizo ikiwa ni kama moja ya kazi wanazofanya mamiss kwa jamii pia kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania ambacho kimekuwa kikisaidia watu mbalimbali na katika halfa hiyo aliongozana na watu wake wa karibu ikiwepo kamati ya Miss Tanzania.

  Katika halfa hiyo iliyodhaminiwa na Malaika Beach, Hoyce baada ya kuwasili kituoni hapo yeye na timu nzima aliyoongozana nayo walifanya shughuli za kijamii katika kituo hicho ikiwa ni pamoja na kufanya usafi katika makazi ya wazee na walemavu wasiojiweza waliopo kituoni kwa kupulizia dawa za kuulia wadudu katika nyumba zao, kugawa dawa za mbu, maji, juice na biskuti na baadae wakapata chakula cha pamoja na wazee na walemavu wasiojiweza.

  Akizungumzia halfa hiyo ya kufunga mwaka, Hoyce Temu alisema kumekuwepo na kusahaulika kwa makundi ya watu wasiojiweza na jinsi muda unavyokwenda wanazidi kusahaulika na jamii inayowazunguka.Alisema yeye kama Miss Tanzania ana wajibu wa kujitoa kuwasaidia watu wa aina hiyo na amekuwa akifanya maeneo mengi kwa kujumuika nao kwa kuwapa msaada na kuwafariji kwani nao wana thamani kama binadamu wengine.

  "Kadri inavyokwenda kumalizika karne ya 21 kunazidi kuongezeka kwa makundi ya wasiojiweza na mimi kama Miss Tanzania nimeamua kujitoa kwa kusaidia makundi haya kwani ni wajibu wetu na tukumbuke na sisi tunaelekea huko," alisema Hoyce.

  Aidha Hoyce alitoa ushauri kwa mamiss wenzake kuwa wanatakiwa kuisaidia jamii kwa kutumia fursa walizonazo mbele ya jamii kwa kutoa misaada kwa makundi ya aina mbalimbali.
  Alisema kazi ya kusaidia jamii siyo ya serikali pekee na wao kama mamiss na watu wenye uwezo kwa ujumla wana wajibu wa kusaidia na sio kutazama mijini pekee kutokana na kundi kubwa la wasiojiweza kuwa vijijini.

  "Sio swala la serikali pekee ... ukichaguliwa kuwa mrembo unakuwa na malengo ambayo umeyaweka hivyo watumie umaarufu, sura zao na sauti kufikia watu wa aina mbalimbali ambao wanahitaji msaada, " Na sio wazee pekee, 65% ya nchi yetu ni vijana na 20% wanajihusisha na kutumia madawa ya aina mbalimbali hivyo wanaweza kuwatembelea na kutoa elimu juu ya athari za utumiaji wa madawa hayo," alisema Hoyce.
  IMG_9931
  Mdau Matukio Chuma na Dada yake Hoyce Temu, Bi. Edith wakifurahi jambo wakati walipowasili kwenye kituo cha Nunge.
  Nae Mkurugenzi wa Lino International Agency, ambayo ndiyo waandaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashimu Lundenga alimtaja Hoyce kama Miss bora kuwahi kutokea tangu walipoanzisha shindano la Miss Tanzania mwaka 1994.

  Alisema mamiss wengi wamekuwa wakiisaidia jamii lakini Hoyce amekuwa akijitoa zaidi kuliko wengine na kufanya shindano hilo kuonekana kuwa na faida mbele ya jamii.
  "Naomba niseme ukweli Hoyce anatakiwa kuwa mfano wa kuigwa haijawahi kutokea miss aliyejitoa kusaidia jamii kama yeye na wapo wengine wanasaidia ila Hoyce amekuwa mstari wa mbele kwa hilo tunampongeza na tunamwomba azidi kuwa hivyo," alisema Lundenga.

  Kwa upande wa Afisa Mfawidhi wa kituo cha Nunge, Ojuku Mgedzi amemshukuru Hoyce kwa upendo amekuwa nao kwa kituo hicho ambacho awali aliwahi kukitembelea 2006 akiwa na marehemu Amina Chifupa na kumtaka kuzidi kuwa na moyo huo kwa jamii inayomzunguka.
  Mgedzi pia alizungumzia changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na kutokuwepo kwa uzio hivyo kutokuwa na hali ya usalama, kuvamiwa kwa eneo hilo na wananchi ambalo lina hekali 50.8 na tayari asilimia 50 imevamiwa na tayari taarifa ipo wizarani na wanashughulikia na zingine ndogo ndogo Hoyce akiahidi kuwasaidia.

  Nae mmoja wa washiriki aliyeongozana na Hoyce, Tausi Mwenda alisema kuwa amejifunza mambo mengi kupitia halfa hiyo aliyoifanya Hoyce na kuwashauri watu wa aina mbalimbali kuwa na moyo wa kujitoa kusaidia jamii kama anavyofanya Hoyce.
  happy-new-year-2016-6
  Baadhi ya wadau waliombatana na Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (hayupo pichani) akiwemo Bi. Tausi Mwenda Mke wa aliyekuwa Meya wa Kinondoni, Yusuph Mwenda, (katikati) wakifurahi jambo walipowasili kwenye kituo cha Nunge, makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
  Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akisalimiana na mmoja wa wazee wenye ulemavu uliotokana na ugonjwa wa ukoma, Mganga Shija (66), wakati alipotembelea makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam juzi (Alhamisi) ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
  Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akimkumbatia rafiki yake wa siku nyingi mmoja wa wazee wenye ulemavu uliotokana na ugonjwa wa ukoma, Mganga Shija (66), wakati alipotembelea makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
  IMG_9942
  Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiendelea kufurahi na rafiki yake wa siku nyingi mmoja wa wazee wenye ulemavu uliotokana na ugonjwa wa ukoma, Mganga Shija (66), wakati alipotembelea makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
  IMG_9946
  Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akitazama jicho la upande wa kulia linalomsumbua mzee Mganga Shija (66), ambaye aliomba kusaidiwa matibabu CCBRT wakati alipotembelea makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
  IMG_9967
  Afisa Mfawidhi wa kituo cha Nunge, Ojuku Mgedzi (kushoto) akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya kituo hicho kwa Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu aliyeambatana na Kamati ya Miss Tanzania kwenye ziara hiyo.
  IMG_9974
  Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga akizungumza jambo na Afisa Mfawidhi wa kituo cha Nunge, Ojuku Mgedzi.
  IMG_0017
  Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiserebuka na mmoja wa wazee wanaoishi kwenye makazi ya Nunge kituoni hapo.
  IMG_0119
  Bi. Edith (kulia) ambaye ni Dada wa Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiteta jambo Bi. Tausi Mwenda mke wa aliyekuwa Meya wa Kinondoni, Yusuph Mwenda kabla ya kuelekea kwenye zoezi la upigaji wa dawa.
  IMG_0135
  Baadhi ya nyumbani za makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
  Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) na Tausi Mwenda (kushoto) wakichanganya dawa ya kuulia wadudu tayari kwa kupulizwa katika nyumba kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Alhamisi ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
  Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) na Tausi Mwenda (kushoto) wakichanganya dawa ya kuulia wadudu tayari kwa kupulizwa katika nyumba kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
  Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) na Tausi Mwenda (kushoto) wakichanganya dawa ya kuulia wadudu tayari kwa kupulizwa katika nyumba kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Alhamisi ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.


  0 0

  Mwigulu Nchemba akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh:Simbachawene wakikagua eneo la machinjio ya Vingunguti kabla ya kuzungumza na wadau wa eneo hilo pamoja na uongozi wake.
  Mh:Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na Mh:Simbachawene wakielekea kuzungumza na wananchi wanaotumia Machinjio ya vingunguti.
  Mawaziri kutoka kulia ni Naibu waziri wa Afya Mh:Kigwangallah,Wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Segerea Mh:Bonah,Watatu kutoka kulia ni Mh:Simbachawene na wa mwisho kushoto ni Mh:Mwigulu Nchemba wakijadiliana jambo.
  Mkutano ukiendelea wa kutoa majawabu kuhusu changamoto za Machinjioya Vingunguti.
  Mh:Simbachawene akiwaagiza watumishi wote wa Machinjio ya Vingunguti kuripoti ofisini kwake Jumanne wakiwa na mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.
  Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi(Wadau) wa machinjio ya Vingunguti kuhusu hatua za kinidhamu alizozichukua kwa Mkuu wa mnada wa pugu inakotoka mifugo kabla ya kufika Machinjio ya Vingunguti kwa upotevu wa mamilioni ya shilingi ya kodi za serikali.
  Mawaziri wakiagana na wananchi mara baada ya mkutano wa kutatua kero zao za Machinjio kumalizika.
  Furaha ya Wananchi mara baada ya kutatuliwa kero zao kwa hatua za awali,wananchi wanasukuma gari la Mh:Mwigulu Nchemba kama ishara ya kukubali hatua alizochukua.
  Mh:Mwigulu Nchemba akiwa ameambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mh:Simbachawene wakiwasili kwenye eneo la machinjio ya Vingunguti kwaajili ya kutoa majawabu kutokana na kero mbalimbali zinazowakabili wadau wa machinjio hayo.


   ……………………………………………………………………………………………………………………………………….
  Ile kauli ya HAPA KAZI TU imeendelea kutumika vizuri kwa mawaziri wa Mh:Rais John  Pombe Magufuli mara baada ya tukio la mawaziri watatu kufika eneo la Machinjio ya Vingunguti kwaajili ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wanaotumia eneo hilo kwa shughuli za kuchinja mifugo.

  Awali,Mh.Mwigulu Nchemba alifanya ziara ya kushitukiza usiku wa tar 01/01/2016 katika machinjio hayo na kukutana na madudu ya kutafunwa kwa fedha za ushuru unaokusanywa kwenye mifugo,lakini pia hali ya mazingira ya kutoridhisha ya Machinjio hayo.

  Hii leo mapema majira ya saa 3:asubuhi,Mwigulu Nchemba anarejea tena kwenye machinjio hayo akiwa ameongozana na mawaziri wawili ambao ni Mh:Simbachawene(TAMISEMI) na Mh:Kigwangallah(AFYA) ambao wote wanagushwa na machinjio hayo.

  Mara baada ya kusikiliza kero na maoni ya pande zote mbili,Mawaziri hao waliamua kuchua hatua zifuatazo kwa wahusika.Mwigulu Nchemba ameagiza Mkuu wa mnada na watumishi waliokuwa zamu tar 24/12/2015 na tar 01/01/2016 watafute kazi nyingine kuanzia sasa,Vilevile wahakikishe jumatatu wanafika ofisi ya Katibu Mkuu wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi.

  Pili,Mwigulu Nchemba ameagiza kuanzia sasa amesitisha ukusanyaji wa ushuru kwenye eneo la mnada wa pugu,badala ya hapo makusanyo yote yatafanyika eneo la machinjio la Vingunguti kwa kutumia mashine za kielektroniki za EFD.

  Tatu,Mwigulu Nchemba ameagiza wananchi(wadau) kuanzia leo waanze kutumia eneo lililokuwa limetengwa kwaajili ya kutunzia nyama,Eneo hilo awali lilisitishwa bila sababu maalum na umeme ukakatwa.
  Mwigulu Nchemba ameagiza umeme urudishwe hii leo na wananchi waanze kutumia eneo hilo.

  Wakati huohuo,Waziri wa TAMISEMI Mh:Simbachawene ameagiza watumishi wote wa machinjio hayo kujitathimini na kufika Jumanne waripoti ofisini kwake wakiwa na mkurugenzi kwaajili ya hatua Zaidi.
  Simbachawene ameenda mbali Zaidi kwa kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha fedha zinazokusanywa kwenye machinjio hayo zinatumika haraka kujenga miundombinu ya eneo hilo ilikuendana na wingi wa watu wanaotumia machinjio hayo.

  Kwa upande wa Afya,Naibu waziri wa Afya Mh.Kingwangallah ameagiza daktari wa machinjio hayo Ndg.Juma aache kutoa huduma eneo hilo hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo,Pia upimaji wa afya kwa wanaotumia machinjio hayo uwe wa bure na Uongozi wa machinjio utenge ofisi maalu ya kupima watu hao.

  Picha/Maelezo na Festo Sanga

  0 0

  Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa Chira Kata ya Kenyamanyoro katika Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara wakishiriki zoezi la ukarabati mdogo wa barabara ya Muturu (Remaghinga) iliyopo Mtaa wa Buguti Kata ya Rebu ambayo inayotegemewa na Wakazi Kata zote mbili za Kenyamanyori na Rebu hatika halmashauri hiyo.
   
  Zoezi hilo limefanyika leo Januari 02,2016 ambapo wananchi hao walikuwa wakifanya ukarabati wa kujaza moramu katika maeneo yaliyochimbika kutokana na maji ya mvua pamoja na kuchimba mitaro kwa ajili ya kupitisha maji wakati wa mvua.
   
  “Hii barabara ni kama imesahaulika na Halmashauri ingawaje ni mhimu sana kwani tegemeo kwa wananchi pamoja na shughuli mbalimbali kama vile ujenzi kwa kuwa hapo ng’ambo kuna shughuli za uchimbaji wa mawe hivyo malori huwa yanapita hapa kwa ajili ya kwenda kufuata mawe hayo kwa ajili ya ujenzi katika maeneo mbalimbali ya mji”. Alibainisha mmoja wa wananchi hao na kuongeza kuwa imekuwa kawaida yao kufanya ukarabati wa aina hiyo pindi barabara hiyo inapoharibika.
   
  Hatua ya Wananchi hao inapaswa kuigwa na wanajamii wengine pamoja na viongozi wenye dhamana ya kuwasimamia katika masuala ya maendeleo wakiwemo watendaji na wenyeviti wa serikali za mitaa kwani maendeleo yanapatikana haraka zaidi ikiwa wanajamii watashiriki ipasavyo katika shughuli zao za kimaendeleo badala ya kuishia kulalamika mitaani.
  Na:George Binagi-GB Pazzo @Binagi Media Group
  Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa Chira katika Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara wakishiriki zoezi la ukarabati mdogo wa barabara ya Muturu (Remaghinga) inayotegemewa na Wakati Kata za Kenyamanyori na Rebu hatika halmashauri hiyo.
  Hii ndiyo dhana halisi ya Maendeleo
  Wanajamii wajiwekee utaratibu wa kutatua kero mbalimbali za kimaendelo katika maeneo/mitaa yao
  Wanajamii wajiwekee utaratibu wa kutatua kero mbalimbali za kimaendelo katika maeneo/mitaa yao
  Maendeleo yanaanza na kila mmoja katika jamii
  Kulalamika mitaani si suluhisho la utatuzi wa kero mbalimbali katika jamii
  George Binagi-GB Pazzo ambae ni Mwanahabari na Mmiliki wa Mtandao wa Binagi Media Group (Mwenye jembe) nae alishiriki zoezi hilo
  George Binagi-GB Pazzo ambae ni Mwanahabari na Mmiliki wa Mtandao wa Binagi Media Group (Mwenye jembe) nae alishiriki zoezi hilo
  Barabara ya Muturu (Remaghinga) ni tegemeo kwa wananchi wa kila rika wakiwemo watoto 
  Hakika barabara hii imeharibika sana na inahitaji ushirikiano zaidi ili kuweza kurejea katika hali nzuri
  Picha hii inaonesha baadhi ya makazi ya watu wanaotegemea barabara hiyo ya Muturu (Remaghinga) ambapo imepigwa kutoka ng’ambo ya pili inakoelekea barabara hiyo.

  0 0

   Heri ya mwaka mpya. Nina furaha kuwafahamisha kuwa kitabu kipya, “Dokta John Pombe Magufuli: Safari ya Urais, Mafaniko na Changamoto katika Urais wake” sasa kinapatikana. Kitabu hiki ni mfululizo wa vitabu kadhaa ninavyotarajia kuvichapisha mwaka huu 2016. 
   
  Wakati kitabu hiki kikiingia sokoni, kitabu kingine kuhusu taaluluma ya Usalama wa Taifa kipo katika hatua za mwisho, na matarajio ni kukiingiza sokoni mwishoni mwa mwezi huu.
   
  Kitabu hiki cha Dokta Magufuli kina sura sita. Katika utangulizi, kitabu kinazungumzia mazingira ya uchaguzi mkuu uliopita, msisitizo ukiwa kwenye hali ya nchi ilivyokuwa kabla ya uchaguzi huo.
   
  Kadhalika, utangulizi huo unaelezea mabadiliko ya ghalfa ya kisiasa, hususan ndani ya CCM, yaliyojitokeza kufuatia jina la mwanasiasa aliyekuwa maarufu kuliko wote wakati huo, Edward Lowassa, kukatwa na chama hicho tawala wakati wa mchakato wa kupata mgombea wake wa kiti cha urais.
   
  Sura ya kwanza inamtambulisha Dokta Magufuli, kwa kuangalia historia fupi ya maisha yake. Sura ya pili inaeleza mchakato aliopitia Dkt Magufuli hadi kuibuka mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM. Sura hii inachambua kwa undani ushindani miongoni mwa makada zaidi ya 40 waliochukua fomu kuwania urais kupitia chama hicho.
   
  Sura ya tatu inaelezea fursa alizokuwa Dokta Magufuli na CCM kwa ujumla katika kipindi cha kampeni na uchaguzi mzima kwa ujumla. Sura hii inachambua uimara wa mwanasiasa huyo sambamba na turufu za kawaida za CCM katika kila uchaguzi. Kwa uapnde mwingine sura hiyo yaangalia pia mapungufu yaliyopelekea urahisi kwa Dokta Magufuli kumshinda mpinzani wake mkuu Lowassa, sambamba na mapungufu ya UKAWA yaliyoiwezesha CCM kushinda.
   
  Sura ya nne inajadili changamoto na vikwazo kwa Dokta Magufuli na CCM kwa ujumla wakati wa kampeni. Kadhalika, sura hii inazungumzia jinsi Lowassa na UKAWA walivyoshindwa kutumia changamoto hizo za wapinzani wao.
   
  Sura ya tano inajadili urais wa Dokta Magufuli tangu aingie Ikulu, wakati sura ya mwisho inajadili changamoto zinazoukabili urais wake na kutoa mapendekezo.
   
  Nimejitahidi kadri nilivyoweza kuandika kitabu hicho kama mtu niliyeufuatilia uchaguzi huo kwa karibu. Natambua kuna wanaoweza kuwa na hofu kuwa ‘niliisapoti CCM na Dokta Magufuli wakati wa kampeni, na kutoiunga mkono UKAWA na Lowassa.’ Naomba kuwatoa hofu kwani kitabu hiki ni si cha kiitikadi bali kwa ajili ya Watanzania wote bila kujali tofauti zao za kiitikadi.
   
  UTAKIPATAJE?
   
  Bei ya kitabu sasa ni Shilingi 4,000 tu. Ili kukipata, nunua kwa M-PESA namba 0744-313-200 jina JOHN ZABLON MPEFO au TIGO-PESA namba 0652-112-071 jina CHRISTINE JOHN MANONGI
   
  KARIBUNI SANA

  0 0

  Kundi la Mziki la Navy Kenzo Linaloundwa na Aika na Nahreel wametutoa kimasomaso Watanzania Baada ya Video yao ya Wimbo wa Game Walioshirikiana na Vanessa Mdee Kushika Namba Nne katika Chat ya Video 50 Bora za MTV Base Africa Zilizofanya Vizuri mwaka 2015..

  Diamond Platnumz na Wimbo wake wa Nana umeshika namba 5 Katika Chat hizo, Wimbo huo wa Nana Pia Umetengenezwa na Producer Nahreel Kitu kinachomfanya Aendelee kuwa Producer Bora zaidi Kuwahi kutokea Tanzania na East Africa kwa Ujumla,

  Mwimbaji Wizkid wa Naigeria Ameshika Namba 6.

  Pongezi ziende kwao @nahreel,@aikanavykenzo wanaounda Kundi la Navykenzo
  Pia Pongeze Kwa Diamond Platnumz kwa Kuwa Namba 5 Katika Chat Hiyo...

  Mwaka Huu Tegemea Mambo Makubwa Kutoka Kwao na The Industry Kwa Ujumla...

older | 1 | .... | 728 | 729 | (Page 730) | 731 | 732 | .... | 1898 | newer