Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

Benki ya Exim yakabidhi gari kwa mshindi wa kampeni yake ya akaunti ya malengo

$
0
0
Meneja Bidhaa wa Benki ya Exim Tanzania, Bw Aloyse Maro (kushoto) akikabidhi mfano wa ufunguo wa gari kwa Meneja Mahusiano Msaidizi wa benki hiyo Bi. Naomi Sanga (katikati) ambaye alimuwakilisha mshindi mkuu wa kampeni ya akaunti ya malengo ya benki hiyo aliyejishindia gari aina ya Toyota IST kwenye hafla fupi ya makabidhiani iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Anaeshuhudia ni Meneja Masoko wa Benki hiyo Bw Abdulrahman Nkondo.

Benki ya EximTanzania imekabidhi zawadi kuukwamshindi wa kampeni ya akaunti ya malengo baada ya kuendesha droo yake ya mwisho na kubwa chini ya usimamizi wa Bodi ya taifa ya michezo ya kubahatisha (GBT) jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.

Bi. Naomi Sanga ambaye ni Meneja Mahusiano Msaidizi  wa benki hiyo alikabidhiwa funguo za gari aina ya Toyota IST kwa niaba ya mshindi katika hafla fupi ya makabidhiano iliyoandaliwa na benki hiyo na kufanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia ushindi huo wa mteja wao huyo Bi. Sanga alielezea furaha yake na kusema kuwa mpango wa Benki ya Exim wa kuwazawadia wateja wake unaonyesha shukrani za benki hiyo katika kutambua uaminifu na mchango wa wateja wao.

"Mshindi wetu ameupokea ushindi huu kwa furaha kubwa japo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake alishindwa kujumuika nasi leo. Ubora wa bidhaa za Benki ya Exim, huduma bora kwa watejanaviwango vinavyovutia vya riba vinavyotolewa katika akaunti hii ya malengo vinathibitishadhamiraya benki hiikatika kukidhi mahitaji yawateja wao,” alisema.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Meneja bidhaa wa Benki ya Exim, Aloyse Maro, aliwapongeza washindi waliojizolea zawadi mbalimbali katika kipindi chote cha kampeni hiyo huku akiwashukuru wateja waliojitokeza kushiriki katika droo hiyo.Kwa mujibu wa Bw. Maro, sambamba na zawadi hizo kampeni hiyo iliambatana na utoaji wa riba nzuri zaidi kwa wateja wanaofungua akaunti hiyo ya malengo.Alisema lengo la benki yake ilikuwa kuhamasisha utamaduni wa kujiwekea akiba miongoni mwa Watanzania.

“Hii ni moja ya njia za benki hii kukuza utamaduni wa kuweka akiba hapa nchini ili kuongeza tija katika maendeleo ya taifa,” alibainisha.

ONGEZENI IDADI YA WATUMIAJI MAJI DAR – PROF MBARAWA

$
0
0
Mh. Prof. Mbarawa akiongea na menejimenti ya Dawasco na Dawassa kwenye ukumbi wa Dawasco gerezani,mwishoni mwa wiki jijini Dar.(picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii) .
Mh. Prof. Makame Mbarawa akisaini kitabu cha wageni akiwa na Naibu waziri,Injinia Isack Kamwelwe (kushoto), pamoja na katibu mkuu na naibu katibu mkuu wa wizara ya maji (kulia) katika ofisi ya afisa mtendaji mkuu wa Dawasco. 
 Waziri wa maji mh. Prof. Makame Mbarawa akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Dawasco mapema leo alipotembelea makao makuu ya ofisi hizo
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Injinia Cyprian Luhemeja akiwa na waziri wa maji Prof. Makame Mbarawa mara tu baada ya kuwasili katika ofisi hizo


Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (Dawasco) limetakiwa kuongeza idadi ya wananchi wanaopata Maji jijini Dar es salaam kutoka wateja 148,000 waliopo sasa hadi wateja milioni 1 ifikapo Juni  2016.

Akiongea na Menejimenti ya Dawasco na Dawasa ikiwa ni siku moja tangu kuchaguliwa kwake Waziri wa Maji Mh. Prof Makame Mbarawa alizitaka Taasisi hizo kuweka mkakati wa lazima utakao hakikisha wateja milioni wanaunganishwa kwenye mtandao wa Majisafi na salama kwa wakazi wote jijini.

“Tumekuja kutekeleza ahadi ya Rais Magufuli aliyoitoa bungeni kuhusu Maji. Aliahidi Serikali ya awamu ya tano pamoja na mambo mengine watahakikisha wana mtua Mama ndoo kichwani” alisema Mh Waziri.

Aliongeza kuwa lazima taasisi hizi mbili zijue wajibu wake kwa wananchi na kutekeleza ahadi ya Rais ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa kutafuta Maji na hata wakiyapata gharama zisiwe juu, ameitaka Dawasco kuhakikisha inawahimiza wateja wake wote na taasisi za serikali kulipia Ankara za Maji kwa wakati.

Aidha amewahimiza Dawasa kuboresha mtandao wa Majitaka ili kuwafikia wateja wengi zaidi wanaohitaji huduma hiyo ya Majitaka na kuepusha usumbufu kwa wananchi unaotokana na Majitaka hayo kuendelea kumwagika ovyo katika mitaa mingi ya jiji.“Hakikisheni mnaboresha mfumo wote wa Majitaka, uendane na mahitaji ya sasa ya jiji ili kuwapunguzia wananchi kupata kero mbalimbali zinazotokana na uchavu wa miundombinu ya Majitaka” alisema Mh.Mbarawa.

AIRTEL FURSA YAENDELEA KUBORESHA MAISHA YA MKULIMA WA MBOGAMBOGA

$
0
0
 Meneja masoko wa kampuni ya Airtel kanda ya Ziwa, Emmanuel Raphael (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na kijana Innocent  Aloyce baada ya kumkabidhi  zawadi ya Toyo, alipomtembelea katika shamba lake
mkoani Mwanza wilaya ya Misungwi ambaye ni miongoni mwa vijana waliowezeshwa na  mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” kwa nyanja mbalimbali miezi sita iliyopita.
 Meneja masoko wa kampuni ya Airtel kanda ya Ziwa, Emmanuel  Raphael (kushoto) akimwangalia  kijana Innocent  Aloyce baada ya kumtembelea katika shamba lake mkoani Mwanza wilaya ya Misungwi ambaye ni
miongoni mwa vijana waliowezeshwa na  mpango wa Airtel Fursa  “Tunakuwezesha” kwa nyanja mbalimbali miezi sita iliyopita.
Meneja masoko wa kampuni ya Airtel kanda ya Ziwa, Emmanuel  Raphael (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na kijana Innocent  Aloyce baada ya kumkabidhi  zawadi ya Toyo, alipomtembelea katika shamba lake
mkoani Mwanza wilaya ya Misungwi ambaye ni miongoni mwa vijana waliowezeshwa na  mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” kwa nyanja mbalimbali miezi sita iliyopita huku akishuhudiwa na ndugu na wafanyakazi  wa Airtel.      
    
Jijini Mwanza  Wilaya ya Misungwi, kampuni ya Airtel kupitia mradi  wake wa *Airtel  Fursa Tunakuwezesha imefurahishwa na juhudi zilizoonyeshwa na kijana   Innocent Aloyce mkaazi wa kijiji cha Mwalogwabagole ambaye ameonyesha   mafanikio katika shughuli zake za ulimaji mbogamboga na nyanya  tangu    kupatiwa  mashine ya kuvuta maji kwa ajili ya umwagiliaji pamoja na jembe  la plau miezi mitatu iliopita.

Airtel kupitia mradi wake wa Airtel Fursa Tunakuwezesha, umeendelea
kuwawezesha zaidi vijana  uliowashika mkono,  wanaozidi kuonyesha mafanikio katika kuboresha shughuli zao mbalimbali za kijasiriamali.Ikiwa na lengo la   kuwakwamua vijana kiuchumi na kujiajiri wao wenjewe ili kuondokana na   tatizo la ukosefu wa ajira .

Akielezea changamoto za usafirishaji wa mazao yake  mjasiliamali huyu
ameeleza tofauti anayoiona mara baada ya kukabidhiwa chombo cha
usafirishaji mazao kutoka kampuni ya simu  ya mkononi ya Airtel
walipomtembelea shambani kwake mwishoni mwa wiki hii na kuona maendeleo  yake ya shughuli zake za ulimaji.

Katika kukabidhi pikipiki kwa ajili ya usafirishaji mazao kwa  Innocent,
meneja masoko wa kampuni ya Airtel kanda ya Ziwa, Emmanuel Raphael
amewataka vijana kuiga mfano unaaonyeshwa na Innocent.

Aliongeza kwa kusema “vijana inabidi waachane na dhamira ya kutaka kukaa tu   vijiweni na kusubiri watafutiwe ajira. Ni juhu di zao wao wenyewe ndio    zitakazoweza kuwakomboa na kupata maendeleo kama alivyoweza kufanikiwa  Innocent.

Kufuatia kushikwa kwake mkono na Airtel leo hii  Innocent meweza
kubadilisha maisha yake na familia yake. Hiyo nawahimiza vijana wasikate
tamaa na kujitokeza kwa wingi kwa kuchangamkia fursa hii na nyingine nyingi  
zinazowazunguka”, .

HII NDIYO PICHA RASMI YA MHE. WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI AWAAGIZA WAKUU WA IDARA KUANDAA TAARIFA ZA IDARA ZAO.

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi akizungumza na wakuu Idara katika wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi alipokutana nao leo alipokaribishwa kwa mara ya kwanza katika wizara  hiyo, tangu achaguliwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kuwa Waziri wa wizara, na kuwaagiza wakuu wa idara katika wizara hiyo kutoa taaarifa za idara zao ifikapo jumatatu ya wiki ijayo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi akipokea ripoti ya wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Katibu mkuu wa wizara yaWizara wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Alphayo Kidata. Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula. 
Naibu Waziri wa Wizara Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akipokea ripoti ya wizara ya Ardhi, nyumba na Maendeleo makazi leo walipokutana na wakuu wa idara mbalimbali leo jijini Dar es Salaam. katikati ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi.
Naibu Waziri wa Wizara Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akizungumza na wakuu wa Idara wa wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam, akizungumzia kuhusiana na wawekezaji ambao watakua hawajaendeleza ardhi ambayo walichukua kwa aajili ya uwekezaji na ardhi hiyo kurudishwa kwa wananchi. Kutoka Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara ya Ardhi Nymba na Maendeleo ya Makazi, Alphayo Midata, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi  na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Ardhi, Nymba na Maendeleo ya Makazi, Selassie Mayunga.
Baadhi ya waandishi wa habari pamoja na wakuu wa Idara za wizara ya Ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

NCHI ZA AFRIKA ZIWEKEZE NGUVU YA PAMOJA KUPAMBANA NA EBOLA

$
0
0
 Dokta Julius Julian Lutwan kutoka Uganda akitoa mada kwa wadau mbalimbali wa afya kutoka katika mashirika na taasisi mbalimbali za Afrika na Ulaya zinazoshughulikia masuala ya afya katika warsha ya siku mbili inayofanyika mkoani Arusha kujadili njia bora za kupambana na magonjwa ya mlipuko kama Ebola na mengineyo katika bara la Afrika na kwingineko dunia.
Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa mambo ya afya ya CORDS ya nchini Ufaransa Professa Nigel Lightfoot akitoa mada kwa wadau mbalimbali wa afya kutoka katika mashirika na taasisi mbalimbali za Afrika na Ulaya zinazoshughulikia masuala ya afya katika warsha ya siku mbili inayofanyika mkoani Arusha kujadili njia bora za kupambana na magonjwa ya mlipuko kama Ebola na mengineyo katika bara la Afrika na kwingineko duniani.

Na Mwandishi Wetu NCHI za kiafrika zimetakiwa kuweka nguvu ya pamoja kuhakikisha zinapata njia bora na za kudumu za kupambana na magonjwa ya mlipuko kama Ebola na kuachana na utegemezi wa misaada kutoka nchi wahisani. Dokta Andrew Kitua wa taasisi ya afya ya Ngalakeri ya Morogoro aliyasema hayo jana katika warsha ya siku mbili ya kujadili njia bora na za kudumu za kupambana na magonjwa ya mlipuko kama Ebola inayofanyika mkoani Arusha.

 Alisema kwakuwa bara la afrika ni miongoni mwa waathirika wa magonjwa hayo wadau husika katika sekta ya afya kwa pamoja na serikali za nchi husika hazina budi kuwekeza nguvu katika kutafuta suluhisho la magonjwa hayo. Alisema ingawa tayari kuna jitihada mbalimbali zinafanyika katika mapambano dhidi ya magonjwa hayo lakini bado kumeonekana kuna changamoto kubwa ya kukabiliana nayo katika maeneo yanayoathirika.

 “Waafrika tunahitajika kuweka nguvu ya pamoja katika kuhakikisha tunapata njia bora na za kudumu za kupambana na magonjwa ya mlipuko kama Ebola,” “Warsha yetu ya siku mbili inayoshirikisha wadau kutoka mashirika na taasisi mbalimbali za afya itajadili na kubadilishana uzoefu wa jinsi ya kupambana na magonjwa hayo na hatimaye kupata mikakati maalumu ya kuiwekea nguvu dhidi ya mapambano hayo,” alisema Dokta Kitua. Kwa upande wake Professa Julias Lutwan kutoka Uganda alisema nchi zote kwa pamoja bila kujali kama zimewahi kuathirika au la zinahitajika kujiweka tayari kukabiliana na magonjwa hayo. 

Alisema kwa afrika ukanda wa nchi za magharibi zinaonekana kupata athari hiyo kwa kiasi kikubwa unapolinganisha na ukanda wa mashiriki lakini bado kwa pamoja tunahitajika kujiweka sawa kwa tahadhari katika hilo. Kwa upande wa changamoto wanazokabiliana nazo katika tafiti wanazofanya kwa pamoja na mapambano ya jumla ya magonjwa hayo alisema mawasiliano na kada za chini katika maeneo ya vijijini ni miongoni mwa changamoto kubwa. 

Alisema kwa kuwatumia wataalamu mbalimbali wa mawasilino wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kurahisisha lugha ya mawasiliano ili jamii ya chini iweze kupata ufahamu wa jinsi ya kupambana na magonjwa husika. Warsha hii inayoshirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya afya kutoka barani afrika na ulaya imeandaliwa kwa pamoja na taasisi za afya za SACIDS na EAIDSNet na kufadhiliwa na taasisi ya afya ya CORDS ya nchini Ufaransa.

Filamu Nne Kutoka Proin Promotions zaingia kwenye kinyanganyiro cha Africa Magic Viewers Choice Awards 2016, wadau tunaomba tuzipigie kura zilete ushindi nyumbani

$
0
0
Proin Promotions Ltd imefanikiwa kuingiza filamu zake nne katika Shindano la Africa Magic Viewers Choice Awards 2016 (AMVCA 2016) katika vipengele viwili huku Filamu zote nne zikiingia katika Kipengele Kimoja cha BEST MOVIE - EAST AFRICA filamu zilizoingia katika kipengele hiko ni  MAPENZI YA MUNGU, KITENDAWALI, MPANGO MBAYA, DADDY’S WEDDING huku filamu ya KITENDAWILI ikiingia katika Kipengele kingine cha BEST INDIGENOUS LANGUAGE MOVIE/TV SERIES – SWAHILI.
Filamu zote nne zimeingia katika kipengele kimoja zikichuana zenyewe huku mbili zikitokea nchini nyingine.
 Tunawaomba watanzania kuweza kuzipigia kura filamu hizi ili kuweza kuibuka mshindi. Jinsi ya Kupiga kura fuata tovuti hii www.africamagic.tv
Washindi wa shindano hii wanatarajiwa kutangazwa Mwakani 2016 mwezi wa 3.

NAPE AAHIDI KUTOA USHIRIKIANO KWA WANAHABARI NA WASHIKA DAU WAKE

$
0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na Wakurugenzi na Viongozi wa Idara mbali mbali walio chini ya Wizara yake ambapo aliwaambia kuwa atasimamia haki za wasanii zinapatikana na hatokuwa na huruma na wale wanaokwamisha au kudhulumu kazi za wasanii.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiwa ofisini kwake .
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Annastazia Wambura akiwasalimu Viongozi, Wakuu wa Idara kwenye kikao cha kwanza ambapo aliwataka kuzingatia kazi na kuzifanya kwa ufanisi.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na Wakurugenzi na Viongozi wa Idara mbali mbali walio chini ya Wizara yake .

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na Wakurugenzi na Viongozi wa Idara mbali mbali walio chini ya Wizara yake ambapo aliwaambia kuwa atashirikiana nao katika kufanikisha yale yatakayowezesha tasnia ya habari, michezo , utamaduni na sanaa na sanaa kukua.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

NAIBU WAZIRI WIZARA YA MALIASILI NA UTALII ENG. RAMO MATALA MAKANI AAZA KAZI RASMI LEO KATIKA OFISI YAKE MPYA MPINGO HOUSE

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Eng. Ramo Matala Makani 
(kushoto) akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru (katikati) ofisini kwake leo tarehe 14 Desemba 2015 baada ya kufika kwa mara ya kwanza toka kuteuliwa kwake na Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli kuwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo. 

Katika salam zake kwa uongozi na watumishi wa Wizara hiyo amewaomba ushirikiano wa dhati kwa kila mmoja kutekeleza majukumu yake kwa wakati ili kuleta maendeleo katika sekta ya Maliasili na Utalii nchini. Ameongeza kuwa yeye binafsi hawezi kuleta maajabu Wizarani hapo bila kupewa ushirikiano katika kazi. Pichani kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Ndugu Selestine Gesimba.   
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru (kulia) akitoa taarifa fupi ya muundo pamoja na shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Mhe. Naibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Ramo Matala Makani muda mfupi baada ya kuwasili katika ofisi yake mpya iliyopo Mpingo House Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Eng. Ramo Matala Makani 
(kushoto) akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru wakati akimpa taarifa fupi ya muundo wa Wizara hiyo leo tarehe 14 Desemba 2015 . (Picha na Hamza Temba wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii)

BALOZI WA IRAN AMTEMBELEA MZEE MWINYI NYUMBANI KWAKE

$
0
0
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kulia) akikabidhi Picha yake rasmi kwa Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mh. Mehdi Aghajafari, wakati alipomtembelea Nyumbani kwake, Mikocheni, Jijini Dar es salaam Disemba 14, 2015.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kulia) akikabidhi Picha kwa Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mh. Mehdi Aghajafari, inayoonyesha sehemu ya Utamaduni wa Tanzania, wakati alipomtembelea Nyumbani kwake, Mikocheni, Jijini Dar es salaam Disemba 14, 2015.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mh. Mehdi Aghajafari pamoja na Msaidizi wake mpya, Bw. Ali Bagheni. Balozi huyo alifika nyumbani kwa Mzee Mwinyi kwa kumtambulisha Msaidizi wake huyo Mpya, leo Disemba 14, 2015.

SHIVYAWATA WAPONGEZA UTEUZI WA DKT. ABDALLAH POSSY

$
0
0
SHIRIKISHO la Vyama vya Watu  wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA)  limempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph kwa kumteua Dkt Abdallah Possy kuwa Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, kazi, Ajira, Bunge, Vijana na Walemavu).

Dkt. Possy ambaye pia ni ambaye ni Mwalimu katika Chuo Kikuu cha Dodoma, ameteuliwa kuwa mbunge na Naibu Waziri katika Baraza la Mawaziri la Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Akizungumza  na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa shirikisho hilo Amon Mpanju  alisema wanaishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kutimiza ahadi yake ya kuwajali na kuwapa kipaumbele jamii ya watu wenye ulemavu kwa kuhamisha usimamizi wa masuala ya watu wenye ulemavu toka  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na kuyaweka chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa utekelezaji wenye tija chini ya Serikali yake.

“Ni Faraja kwetu Watanzania hususani sisi wenye ulemavu tumetengewa nafasi yetu maalum ndani ya Serikali.hatua ambayo itaifanya Serikali kutenga rasilimali za kutosha ili kuwezesha utekelezaji wa masuala yetu” alisema Mpanju.


Aidha Bwana Mpanju aliiomba Serikali kushughulikia changamoto zao ikiwa ni pamoja na kuifanyia marekebisho ya Sheria ya Haki za Watu wenye Walemavu ili iakisi muundo mpya wa uratibu na usimamizi wa masuala ya watu wenye ulemavu chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Mpanju alisema wameiomba Ofisi ya Waziri Wkuu kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Ofisi ya  Bunge Ikulu kuajiri wakalimani wa lugha ya alama ambao watakuwa watafanya tafsiri ya mijadala ya vikao vya Bunge, Hotuba za Rais na taarifa za habari na vipindi vyote muhimu vinavyotolewa kwa umma kupitia runinga.

Kwa mujibu wa Mpanju alisema Shivyawata pia limeiomba Serikali kuhakikisha kuwa vyuo vya ufundi vilivyo chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii ambavyo vilikuwa vinatoa ujuzi kwa watanzania wenye vinafufuliwa na vihamishiwe Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknoloia na Ufundi.

Mpanju aliwataka Watanzania wamuunge mkono Mh. Dr John Pombe Magufuli na Serikali ya awamu ya tano katika kuzishughulikia kero zinazoikabili nchi yetu na kikubwa kumuombea kwa mungu ili amtunze na kumwezesha kuyatimiza malengo yake.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA KADHI MKUU WA TANZANIA

$
0
0
0d766169-dd05-48f7-8eb5-58506ff0a6c4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Kadhi Mkuu wa Tanzania, Abdallah Mnyasi, ofisini kwake jijini Dar es salaam Desemba 14, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI WALETA MAAFA KATIKA KIJIJI CHA DIHINDA MVOMERO MKOANI MOROGORO

$
0
0
Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mwigulu Nchemba akiangalia Ng'ombe walio uwawa katika Mgogoro wa wakulima na Wafugaji uliotokea katika kijiji cha Dihinda kata ya Kanga wilayani Mvomero, katika tukio lililotokea Desemba 12 mwaka huu.

Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mwigulu Nchemba akiwa na Mkuu wa wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa wakiwajulia hali watu waliojeruhiwa katika mgogoro wa wakulima na wafugaji katika hospitali ya Teule wilayani humo,uliotokea katika kijiji cha Dihinda kata ya Kanga wilayani Mvomero Desemba 12 mwaka huu.
Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mwigulu Nchemba akizungumza na Mkuu wa wilaya Mvomero, Betty Mkwasa katika kijiji cha Dihinda kata ya Kanga wilayani Mvomero Desemba 12 mwaka huu, walipotembelea katika kijiji hicho na kuona madhara makubwa yaliyojitokeza katika mgogoro wa wakulima na wafugaji. Nchemba alimwagiza Mkuu wa wilaya Mvomero, Beth Mkwasa kuunda kamati ya Ulinzi na Usalama katika wilaya ya Mvomero ili kamati ihusike maeneo yote ya Nchi yetu ili kuhakikisha wanaimarisha ulinzi maeneo yote yenye migogoro, pia wahakikishe waliosababisha maafa wanakamatwa mara moja na kufikishwa kwenye vyombo vya sharia. 
Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mwigulu Nchemba akizungumza na wanachi wa kijiji cha Dihinda waliokusanyika katika eneo lililotokea mauaji ya wanyama na baadhi ya watu kujeruhiwa. 

"Natoa rai kwa Wananchi hususani wa jamii ya Wafugaji na Wakulima, kuwa hakuna ardhi au Mnyama mwenye thamani sawa na Maisha ya Mwanadamu yeyote yule, njia bora na salama ya kutatua migogoro hii inayohusisha wakuliama na wafugaji ni kufuata taratibu za kuonana na Uongozi wa Serikali wa eneo husika hatua kwa hatua, Nawaomba wananchi waache kujichukulia sheria mikononi, tunakwenda kuunda kamati za usuruhishi wa migogoro hii kwa kila kijiji zitakazohusisha pande zote mbili ili kubaini wavamizi wa maeneo na kuwachukulia hatua za kisheria." Alisema Nchemba. 

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN, AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MABALOZI, AMKARIBISHA WAZIRI WA OFISI YAKE JANUARY MAKAMBA.

$
0
0
DE1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Mhe. Jorge Luis Lopez, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 14, 2015 kwa mazungumzo.
DE2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na  Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Mhe. Jorge Luis Lopez, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Mhe Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 14, 2015 kwa mazungumzo. Picha na OMR
DE3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Yasemin Eralp, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 14, 2015 kwa mazungumzo. Picha na OMR
DE4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na  Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Yasemin Eralp, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Mhe Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 14, 2015 kwa mazungumzo. Picha na OMR
DE5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Januari Makamba, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 14, 2015 kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo. Picha na OMR
DE6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika mazungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Januari Makamba, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 14, 2015 kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo. Picha na OMR

DE8
DE9
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Januari Makamba, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Mhe Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 14, 2015 alipofika kujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo. Picha na

MAJALIWA AMPOKEA WAZIRI JENISTA NA NAIBU MAWAZIRI MAVUNDE NA POSSI

$
0
0
si14
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama  (wapili kushoto), na Naibu Mawaziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Abdallah Possi  (wapili kulia)  na Anthony Mavunde (kulia) baada ya kuwakabidhi taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakati waliporipoti Ofisini kwa Waziri Mkuu kuanza kazi Desemba 14, 2015.
si15
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama (katikati), Naibu Mawaziri Dkt. Abdallah Possi (kulia) na Anthony Mavunde (wapili kulia)) baada ya mawaziri hao kuripoti  Ofisini kwake kuanza kazi Desemba 14, 2015. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt, Florence Turuka, Wanne kushoto ni katibu Mkuu Kazi na Ajira, Eric Shitindi na watatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Regina Kikula.
si16
Waziri Mkuu, Kassim majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama  (kushoto) na Naibu Mawaziri, Dkt. Abdallah Possi (Wapili kulia) na Anthony Mavunde (kulia) baada ya Waziri huyo na Manaibu wake  kuripoti Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam kuanza kazi Desemba  14, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

si2
Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama na Naibu Mawaziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Abdallah Possi na (wapili kushoto) na Anthony Mavunde (kushoto) wakisalimiana na Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu waliojitokeza kuwapokea na kuwakaribisha wakati walipoingia Ofisini  kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam kuanza kazi , Desemba  14, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
si3
Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama akipokea maua kutoka kwa mtumishi wa ofisi ya Waziri Mkuu, Numpe mwadumbya (kushoto) baada ya kuwasili ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam kuanza kazi Desemba 14, 2015. (Picha na Ofisi ya 
Waziri Mkuu)
si4
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama (wapili kushoto)  akishuhudia wakati Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde (wapili kulia ) na  Dkt. Abdallah Possi(kulia) wakipokea maua kutoka kwa Mtumishi wa Ofisi ya Waziri Tina Ambros (kushoto) baada ya kuwasili kwenye ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam kuanza kazi Desemba 14, 2015. (Picha na Ofisiya Waziri Mkuu)
si5
Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama na Naibu Mawaziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Abdallah Possi na (wapili kushoto) na Anthony Mavunde (kushoto) wakisalimiana na Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu waliojitokeza kuwapokea na kuwakaribisha wakati walipoingia Ofisini  kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam kuanza kazi , Desemba  14, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
si6
Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama na Naibu Mawaziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Abdallah Possi na (wapili kushoto) na Anthony Mavunde (kushoto) wakisalimiana na Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu waliojitokeza kuwapokea na kuwakaribisha wakati walipoingia Ofisini  kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam kuanza kazi , Desemba  14, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
si8
Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama na Naibu Mawaziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Abdallah Possi na (wapili kushoto) na Anthony Mavunde (kushoto) wakisalimiana na Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu waliojitokeza kuwapokea na kuwakaribisha wakati walipoingia Ofisini  kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam kuanza kazi , Desemba  14, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
si9
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 14, 2015 baada ya kuwasili ofisini kuanza kazi . Kushoto ni Naibu Waziri wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Abdallah Possi na kulia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
si10
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiteta na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Turuka (kabla ya kuwapokea Waziri na Naibu Mawaziri, Ofisini kwake jijini Dar es salaam, Desemba 14, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
si11
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama wakati aliporipoti Ofisini kwake jijini Dar es salaam kuanza kazi Desemba 14, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
si12
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde  wakati aliporipoti Ofisini kwake jijini Dar es salaam kuanza kazi Desemba 14, 2015. Katikati ni Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenisa Mhagama .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
si13
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt Abdallah Possi   wakati aliporipoti Ofisini kwake jijini Dar es salaam kuanza kazi Desemba 14, 2015. Wapili kushoto  ni Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenisa Mhagama  na kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Dkt.Kalemani awaagiza TANESCO kuongeza uzalishaiji wa umeme ifikapo mwishoni mwa Desemba 2015

$
0
0
Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (kushoto) akimsikiliza Naibu Mkurugenzi Mtendaji Tanesco Bw.Decklan Mhaiki alipokuwa akimwonyesha mradi wa Kinyerezi I mara baada ya kuwasili katika kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia gesi eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam

Meneja Mradi TANESCO Mhandisi Simon Jalima (wa pili kushoto) akimwonyesha  Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa pili kulia) moja ya mtambo unaopokea gesi kutoka mtwara na kuisambaza mpaka kituo cha Ubungo alipofanya ziara ya kuona maendeleo ya mradi huo leo katika eneo la mradi Kinyerezi jijini Dar es Salaam, wa kwanza kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Tanesco Bw. Decklan Mhaiki. 

 Meneja Mradi TANESCO Mhandisi Simon Jalima (wa pili kushoto) akimtembeza Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa pili kulia) kumwonyesha mitambo mbalimbali ya uzalishaji wa umeme uliyopo katika kituo hicho cha Kinyerezi I, jijini Dar es Salaam.

 Mmoja wa wataalamu wa kuendesha mitambo inayosambaza nishati ya umeme uliyozalishwa kwa kutumia gesi (Shift Supervisor) Bw. Mohamed Lanzi akimwonyesha Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa kwanza kulia) mtambo wa usambazaji wa umeme wa Morogoro unaotokea  Kinyerezi I namna wanavyouendesha.
 Meneja Mradi  wa Kinyerezi Extension kutoka Kampuni ya Sumitomo Japan Bw. Shoji Watanabe akimweleza  Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani ni kwa muda gani mradi huo utakamilika mara baada ya kupewa mkataba wa kuanza kazi hiyo, leo Kinyerezi jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa kwanza kulia) akitoa maagizo kwa Meneja Mradi  wa Kinyerezi Extension kutoka Kampuni ya Sumitomo Japan Bw. Shoji Watanabe (wa kwanza kushoto) alipokuwa akigua eneo la mradi huo leo Kinyerezi jijini Dar es Salaam, (wa pili kulia) ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Tanesco Bw. Decklan Mhaiki.
 
Na Anitha Jonas –MAELEZO
Tarehe 14/12/2015
Dar es Salaam.

Wizara ya Nishati na Madini imewaagiza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha uzalishaji wa umeme katika Mradi wa Kinyerezi I na Kinyerezi II unakamilika ifikapo mwezi Februari 2016  na kuanza kufanya uzalishaji ilikuongeza kiasi cha nishati ya  umeme kufikia zaidi ya Megawati 100.

Agizo hilo lilitolewa leo na Naibu Waziri, Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani alipofanya ziara yake katika kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya Gesi cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam,hii ni baada ya kuelezwa kuwa kituo hicho kwa sasa kinazalisha 70 Megawati za umeme ambaohautoshelezi kwa matumizi ya watanzania.

“Watanzania wamechoshwa na mgao wa umeme na wanaimani kubwa na uzalishaji wa kituo hiki cha kuzalisha umeme kwa kutumia gesi hivyo wanatarajia umeme wa uhakika katika kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji na kujipatia kipato”,alisema Dkt.Kalemani.

Hata hivyo Dkt. Kalemani aliwapongeza watendaji wa TANESCO na wakandarasi wanaosimamia uendeshaji wa mitambo hiyo ya uzalishaji huku akiwasihii waongeze jitihada za dhati kwani watanzania bado hawaridhishwi na kiasi cha umeme kinachozalishwa kwa sasa.

Kwa upande wa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Omari Chambo alisema kuna mradi mpya uitwao Kinyerezi Extension unakaribia kuanzishwa hivi karibuni ambao utazalisha Megawati 345 za umeme na kupitia mradi huu uzalishaji wa umeme utaongezeka kwa kiasi kubwa.

“Tutajitahidi kwa sasa umeme usikatike mara kwa mara na jitihada za kusafisha mitambo miwili ya phase I na Phase II inafanyika na itakapokamilika tunatarajia kuzalisha zaidi ya Megawati 140 za umeme na usafishaji wake unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu”,alisema Mhandisi Chambo.

Naye Naibu Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Bw.Decklan Mhaiki alisema mradi wa Kinyerezi Extension ambao utagharimu  jumla ya kiasi cha Dola Milioni 340 unatarajia kuanza hivi karibuni mara baada ya kukamilika kwa Mkataba na malipo ya 15% kwa mkandarasi.

Pamoja na hayo wizara ya Nishati na Madini imetoa angalizo kwa watendaji wote wanaozalisha umeme kwa kutumia maji walinde vyanzo vya maji na kuacha kutumia maji hayo kwa matumizi mengine kama ya kilimo.

Uzalishaji wa umeme kwa kutumia Nishati ya Gesi utasaidia kupunguza gharama za watumiaji wa umeme pamoja na kushusha gharama za uzalishaji.

NAIBU Waziri ofisi ya Rais, Tamisemi, Selemani Jaffo atoa siku 27 kwa wakurugenzi wa halmashauri nchini kuanza kutumia mfumo wa kielekroniki

$
0
0
 Naibu Waziri ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jaffo akishiriki zoezi la kuwapima uzito mmoja wa watoto waliokuwepo katika kituo cha Afya Bahi baada ya kufanya ziara ya kukagua utoaji Huduma za afya katika wilaya ya Bahi, Mkoani Dodoma.
 Naibu waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jaffo akizungumza na wagonjwa Mara baada ya kukagua wodi ya akina mama katika Kituo cha afya bahi.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jaffo akizungumza na watumishi na wakuu wa idara katika halmashauri ya wilaya ya bahi(hawapo pichani), kulia, ni Mkuu wa wilaya ya bahi Fransis Mwonga na kushoto ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Rachel Chuwa.
 .baadhi ya wakuu wa idara katika halmashauri ya bahi.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jaffo(mwenye tai nyekundu) akisikiliza maelezo kuhusu mradi wa maji wa mkakatika kutoka kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya bahi Rachel Chuwa. 
 
NAIBU Waziri ofisi ya Rais, Tamisemi, Selemani Jaffo ametoa siku 27 kwa wakurugenzi wa halmashauri nchini kuhakikisha wanakamilisha na kuanza kutumia mfumo wa kielekroniki wa ukusanyaji Mapato.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akizungumza na wafanyakazi na wakuu wa idara wa halmashauri hiyo kufuatia ziara ya kushtukiza ya kuangalia utendaji kazi wa watumishi wilaya hiyo.

Amesema mfumo huo ulitakiwa kuwepo katika halmashauri julai mwaka huu lakini hadi sasa inamsikitisha kuona kuna halmashauri hazijatekeleza suala hilo na kufanya kuendelea kuwepo kwa upotevu wa mapato na kutaka ifikapo januari 10 mwakani kukamilisha mfumo huo kwenye halmashauri zao.

Naibu huyo alisema kwa wilaya ya Bahi ilitakiwa kuwa ya mfano kwa kuweka mfumo huo lakini kutokana na uzembe na inawezekana umecheleweshwa ili kuendelea kufanya mianya ya watu kujipatia fedha.

"Inawezekana mfumo unacheleweshwa kwa makusudi ili kufanya ile mianya ya ukusanyaji fedha kwa njia nyingine uendelee, naagiza hapa itakapofika tarehe 10 Mwezi wa kwanza nataka nipate taarifa hapa, mfumo unafanya kazi na ufungwe idara ya maliasili, afya ili mtu atakayelipa aone fedha inalipwa kwa utaratibu halali, watu wanakosa fedha kutokana na kuingia kwenye mifuko ya watu,"amesema

Amebainisha Mkurugenzi atakayeshindwa kutimiza hilo aandike barua kwa Katibu Mkuu tamisemi kwamba ameshindwa kutimiza uwepo wa mfumo huo.

"Inaonekana aigizo lilitoka lakini watu walishindwa kutimiza majukumu yao na kila Mkurugenzi atawajibika katika hili kwa kushiriki ufisadi wa kuikosesha halmashauri mapato, kila mtu ahakikishe mfumo unakamilika katika halmashauri yake na ukamilike idara zote,"amesema

Katika idara ya utumishi, Naibu huyo amesema kuna vijiji havijafanya mikutano yake tangu uchaguzi wa serikali za mitaa ufanyike Mwezi wa 12 mwaka jana.

Amesema mpaka sasa mwaka umeisha wananchi hawapati taarifa za mapato na matumizi katika vijiji vyao, hivyo maafisa utumishi wahakikishe wanatimiza wajibu wao kwa kuhakikisha kila kijiji kinafanya mkutano.

Kuhusu malalamiko ya wafanyakazi, Jaffo alisema kumekuwepo na malalamiko ya kupanda madaraja, kulipwa posho za likizo ambapo mwisho wa siku taarifa zile matokeo yake serikali inalaumiwa wakati wanaofanya ni wenyewe kwa wenyewe.

Amesema inawezekana wakuu wa idara husika wanajifanya miungu watu hawatimizi wajibu wao na hawataki kutimiza haki za wafanyakazi wa chini na kutupa malalamiko ya wenzao.

"Sitaki kusikia malalamiko ya watumishi, kuna malalamiko mengine yanaendana na rushwa, mimi nitakapopokea maswali kutoka kwa mbunge kuhusu malalamiko ya wafanyakazi maana yake wewe Mkurugenzi na wakuu wako wa idara hamtoshi,"amesema

RAIS MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA JAPAN NCHINI

$
0
0
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida aliyefika Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo. Katika Mazungumzo hayo Balozi Yoshida amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuiongoza Tanzania katika awamu hii ya tano na pia amezungumzia miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Japan hapa nchini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa Maofisa walioambatana na Balozi Yoshida Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Kalenda kutoka kwa Balozi wa Japan hapa  nchini Mheshimiwa Masaharu Yoshida mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kulia akiagana na Balozi wa Japan Nchini Mheshimiwa Masaharu Yoshida mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU. 

SHIVYAWATA WATAKA MAZINGIRA RAFIKI YA ELIMU KWA SERIKALI YA AWAMU YA TANO

$
0
0
 Mwenyekiti wa Taifa wa Shirikisho la Vyama Watu wenye Ulemavu Tanzania(SHIVYSWATA) Amon Anastaz Mpanju akizungumza na wandishi wa habari hawapo pichani juu ya kumpongeza  Rais   John Pombe Joseph Magufuli kwa kutimiza ahadi yake ya kuyajali  na kuyapa kipaumbele masuala ya watanzania wenye ulemavu kwa uteuzi wa Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi Vijana na Ajira  Dk.Abdallah Possy, kulia ni Mwekahazina Alias Masamaki
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa Shirikisho la Vyama Watu wenye Ulemavu Tanzania(SHIVYSWATA) Amon Anastaz Mpanju.(picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii).
 
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SHIRIKISHO la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (Shivyawata), limesema kuwa changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu nchini ni ukosefu wa mazingira rafiki  ya kupatia elimu kwa jamii hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Shivyawata , Amon Mpanju amesema kuwa kwa serikali ya awamu ya tano iweke mkazo katika mazingira ya watu wenye ulemavu ikiwemo na upataji wa habari kwa kundi la watu wasiosikia.

Mpanju amesema kuwa watu wenye ulemavu wamekuwa na sera lakini hajawahi kutekelezwa katika serikali zilizopita hivyo kwa serikali ya awamu ya tano  itekeleze sera kwa vitendo.

KAPUMZIKE KWA AMANI MPAMBANAJI MWENZETU DOTTO MZAVA.

$
0
0

BLOGGER chipukizi nchini Dotto Mzava, amefariki Dunia katika ajali ya barabarani Desemba 14, 2015 hapa jijini Dar es Salaam. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Bloggers Nchini, (TBN), ambao marehemu alikuwa ni mwanachama wake, Bw. Joackim Mushi amesema Dotto ambaye alikuwa akifanyia kazi Jamii Media (Wamiliki wa mtandao wa Jamii Forum, amefariki kwa ajali ya pikipiki ingawa haikuelezwa ajali hiyo imetokea maeneo gani hasa ya jiji la Dar es Salaam. 

Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina lake Lihimidiwe Amin.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images