Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo afanya ziara TBC na BASATA.

0
0
nap1
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiangalia moja ya kazi za wasanii katika kiwanda cha kutengenezea batiki alipotembelea ofisi za Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) leo hii jijini Dar es Salaam.
nap2
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi Lilian Beleko (kulia) akimkaribisha kwa furaha waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye wizarani hapo leo hii jijini Dar es Salaam.
nap4
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye(kushoto) akiongea na menejimenti ya shirika la Utangazaji Tanzania-TBC(hawapo pichani) wakati alipotembelea makao makuu ya shirika hilo ili kujua changamoto walizonazo na jinsi gani atawasaidia kama waziri mwenye dhamana.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo afanya ziara TSN

0
0
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akifuatilia maelezo namna gazeti linavyotengenezwa kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi za Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wachapishaji wa magazeti ya HabariLeo, Dailynews na Spoti Leo,  leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO Bw. Assah Mwambene na Mhariri Mtendaji wa TSN Bw. Gabriel Nderumaki(katikati).
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akisoma gazeti lenye kurasa za matangazo alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi za Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wachapishaji wa magazeti ya HabariLeo, Dailynews na Spoti Leo,  leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa TSN Bw. Gabriel Nderumaki.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akiwa katika ziara ya kiakzi katika ofisi za Kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN) wachapishaji wa magazeti ya HabariLeo, Dailynews na Spoti Leo,  leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mhariri Mtendaji wa TSN Bw. Gabriel Nderumaki na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO Bw. Assah Mwambene.



Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa TSN  wachapishaji wa magazeti ya HabariLeo, Dailynews na Spoti Leo,alipofanya ziara ya kikazi ofini hapo  leo jijini Dar es Salaam.

 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza na uongozi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wachapishaji wa magazeti ya HabariLeo, Dailynews na Spoti Leo, alipofanya ziara katika ofisi zao leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanayakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wachapishaji wa magazeti ya HabariLeo, Dailynews na Spoti Leo,wakifuatilia mazungumzo ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi za kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akifuatilia maelezo namna gazeti linavyotengenezwa kutoka kwa Mkuu wa Press wa TSN Bw.Patrick Eusebio (aliyekaa)alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi za Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wachapishaji wa magazeti ya HabariLeo, Dailynews na Spoti Leo,  leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO Bw. Assah Mwambene na Mhariri Mtendaji wa TSN Bw. Gabriel Nderumaki.



Picha na Frank Shija,WHVUM.

DKT KIGWANGALA AFANYA ZIARA ZA KUSHTUKIZA KITUO CHA FOREPLAN CLINIC KINACHOMILIKIWA NA DKT. MWAKA

0
0

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akipokelewa na mmoja wa wauguzi wa kituo hicho ambapo jina lake halikupatikana kwa haraka baada ya mkurugenzi wa kituo hicho Dk. Mwaka Juma Mwaka kutokuwepo kwenye kituo chake cha Foreplan Clinic kilichopo Ilala Bungoni, jijini Dar es Salaam.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya wananchi waliofika kupata matibabu katika kituo cha Foreplan Clinic kuhusu huduma zitolewazo katika kituo hicho kinachomilikiwa na Dk. Mwaka Juma Mwaka..
Masaidizi wa Dk. Mwaka, Bi Teddy L. Mbuya akimtolea ufafanuzi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala kuhusu huduma zitolewazo katika kituo cha Foreplan Clinic mara baada ya kuanza kukagua kituo hicho kinachotoa Tiba .
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akikikagua kifaa kinachotumika kufanyia vipimo kwenye kituo cha Foreplan Clinic wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho leo jioni siku ya jumatatu.
Hiki ndicho kifaa kinachotumika kupimia wagonjwa kwenye maabara ya kituo hicho cha Tiba Mnadala.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akiwauliza maswali wasaidizi wa kituo hicho wakiongozwa na Bi Teddy L. Mbuya mara baada ya kukuta hari ya sintofahamu katika kituo hicho.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akikagua moja ya dawa zinazotolewa kwa wangonjwa wanaokuja kutibiwa kwatika kituohicho cha tiba Mbadala.
Bi. Rozaria Antoni ambaye ni muhudumu wa dawa akikaa kimya baada ya kuulizwa maswali na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala na kukosa la kujibu.

Hizi ni dawa za asili zinazouzwa katika kituo hicho cha afya.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akimpa maelekezo Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asilia na mbadala Dk.Paul Mhame kutoka wizara ya Afya na Ustawi wa jamii.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akiwasili katika kituo cha Foreplan Clinic kinachotoa tiba mbadala kilichopo Ilala Bungoni, jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho leo jumatatu kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asilia na tiba Mbadala Dk.Paul Mhame kutoka wizara ya Afya na Ustawi wa jamii.(Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog)

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala leo majira ya jioni amefanyaziara ya kushtukiza katika kituo kinachotoa tiba mbadala cha Foreplan Clinic kinachomilikiwa na Dk. Mwaka Juma Mwaka kilichopo Ilala Bungoni na kujionea hali halisi ya kituo hicho. Mara baada ya kufika alianza kufanya ukaguzi kuanzia sehemu ya Mapokezi mpaka kwenye vyumba vya matabibu lakini katika vyumba vyote hakuna daktari aliyekuwa anatoa huduma.

Akizungumza na wagonjwa waliokuwa wakisubilia tiba alisema kuna waliofika katika kituo hicho ili kutibiwa lakini kituo hicho hakina uwezo wa kuwahudumia wagonjwa hao. Na kuwataka wagonjwa hao waende kwenye hospitali ili wapate matibabu yanayoendana na magonjwa wanayoumwa.

Akizungumza msaidizi wa Dk. Mwaka, Bi Teddy L. Mbuya alisema yeye hawezi kusema kuhusu kituo hicho maana yeye sio msemaji mkuu bali alimwomba Naibu waziri kufanya ukaguzi katika kituo hicho pamoja na kuwaliza maswali wahusika mbalimbali wa vitengo vya ktuo hicho.

Baada ya ukaguzi wa kituo hicho Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala amemwagiza Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asilia na mbadala Dk.Paul Mhame ndani ya wiki moja kufanya ukaguzi kwa kituo cha Dk. Mwaka na aletewe taarifa iliyokamilika kuhusu taaruma yeke pamoja na washirika wake na pia dawa anazozitumia kama ni rafiki kwa wananchi wanaotumia dwa hizo pamoja na kufanya ukaguzi wa vituo vyote vinavyotoa tiba mbadala na tiba asilia kama Dk. Ndodi, Dk. Rahabu nk. ili kuwabaini wanaowalaghai wananchi.

Pia amesema Dk Mwaka Juma Mwaka amekuwa akijitangaza kupitia vyombo mbalimbali hapa nchini ambavyo ni kosa la kutangaza kama unafanya kazi za tiba tabibu.

Alisema madaktari wana miiko na katika miiko hiyo ambayo inatumika na mojawapo ikiwa ni kutojitangaza. Naibu waziri aliendelea kusema kuwa Dk. Mwaka amekuwa akijiita Dokta na amekuwa akichambua mwili wa binadamu kama vile ameusomea udakitari wakati sheria ya tiba asilia na tiba mbadala hairuhusu watu wa tibaAsilia na Tiba Mbadala kutumia maneno ya tiba ya kisasa.

Pia Naibu Waziri amamtaka Dk. Mwaka Juma Mwaka kufika wizarani kesho saa mbili asubuhi akiwa na nyaraka zake zote zinazohusu utoaji wa huduma ya Tiba Mbadala kwani amekuwa akijiita majina ya tiba za kisasa na pia kutibu kwa njia ya kisasa badala ya kutibu kwa njia ya Asilia au Tabibu.

WAZIRI KITWANGA, NAIBU WAZIRI WA USALAMA WA RAIA WA CHINA WASAINI HATI YA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO

0
0
mbo1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) na Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang wakisaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika masuala mbalimbali ya Ulinzi na Usalama wa Raia kati ya Wizara hizo mbili, katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
mbo2
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto), wakibadilishana Hati za Makubaliano ya Ushirikiano waliosaini na Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang, katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
mbo4
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang, mara baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya Wizara hizo mbili. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.

mbo5
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wa pili kushoto), akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang (kulia), kabla ya kusaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya Wizara hizo mbili. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu, Mbarak Abdulwakil. Picha na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
mbo6
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (watano kulia-mstari wa mbele),  Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang (watano kushoto-mstari wa mbele), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (watatu kulia-mstari wa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Mawaziri hao kumaliza kusaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya wizara hizo mbili. Tukio hilo lilifanya katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
mbo3
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto), akimpa zawadi ya kinyago Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang, mara baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya wizara hizo mbili. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.

TAMASHA LA MITIKISIKO 2015 LAACHA HISTORIA MKOANI IRINGA

0
0

Msaani maarufu wa bongofleva, Linex akifanya vitu vyake katika uwanja wa Mlandege mjini Iringa juzi kwenye tamasha la muziki (Mtikisiko) lililoandaliwa na redio Ebony FM ya mjini Iringa kwa udhamini wa kampuni ya simu za mkononi Tigo. Tamasha hilo hufanyika kila mwaka katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Msaani maarufu wa Hip hop,Darasa akifanya vitu vyake katika uwanja wa Mlandege mjini Iringa juzi kwenye tamasha la muziki (Mtikisiko) lililoandaliwa na redio Ebony FM ya mjini Iringa kwa udhamini wa kampuni ya simu za mkononi Tigo. Tamasha hilo hufanyika kila mwaka katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini
Umati wa wananchi wa Iringa waliojitokeza katika uwanja wa Mlandege mjini Iringa juzi kwenye tamasha la muziki (Mtikisiko) lililoandaliwa na redio Ebony FM ya mjini Iringa kwa udhamini wa kampuni ya simu za mkononi Tigo. Tamasha hilo hufanyika kila mwaka katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini .
Msaani maarufu wa Hip hop, Roma Mkatoliki akifanya vitu vyake katika uwanja wa Mlandege mjini Iringa juzi kwenye tamasha la muziki (Mtikisiko) lililoandaliwa na redio Ebony FM ya mjini Iringa kwa udhamini wa kampuni ya simu za mkononi Tigo. Tamasha hilo hufanyika kila mwaka katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini

MSHINDI WA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015 CAROLINE CHELELE, AKABIDHIWA RASMI ZAWADI ZA VIFAA VYA KILIMO

0
0
Mshindi wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula Msimu wa nne Bi. Caroline Chelele aliyekaa kwenye Pawatila akifurahia zawadi zake, Muda mfupi baada ya kukabidhiwa.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombelo Bw. Yahya Naiya (wa pili kushoto) aliye muwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilombelo akikata utepe kuashiria tukio la kumkabidhi zawadi rasmi mama shujaa wa chakula msimu wa nne 2015 Bi. Caroline Chelele, wa kwanza kushoto ni Mercy Minja Kaimu mkurugenzi wa wa mji wa Ifakara, wa tatu kutoka kulia ni Mama Shujaa wa Chakula Bi. Caroline Chelele na Mbunge wa Jimbo la Kilombelo Mh. Peter Lijuakali
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombelo Bw. Yahya Naiya (wa pili kushoto) aliye muwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilombelo akimpongeza Mama shujaa wa chakula 2015 baada ya kukabidhiwa zawadi ya vifaa vya kilimo vyenye thamani ya Tsh Milioni Ishirini(20,000,000)
 Vifaa  vya kilimo ambavyo alikabidhiwa  mama Shujaa wa Chakula Msimu wa nne 2015, ikiwa ni Pawatila na Mashine ya kumwagilia na Shamba lenye Hekta 7 ambalo halipo pichani.
 Mshindi wa Shindano la Mama shujaa wa chakula linalo endeshwa na Oxfam kupitia Programu yake ya Grow Bi Caroline Chelele akitoa neno la Shukurani baada ya kukabidhiwa zawadi.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombelo Bw. Yahya Naiya (wa pili kushoto) aliye muwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilombelo, akitoa neno la shukurani kwa Shirika la Oxfam kwa jinsi wanavyo wajali na kuwawezesha wakulima wadogo wadogo.
Mbunge wa Kilombelo Mh. Peter Lijuakali akimpa pongezi mama shujaa wa Chakula 2015 kwa kuleta ushindi mkubwa wilayani hapo na kuwasihi akinamama wengine wajitokeze kushiriki kipindi ambacho nafasi inatokea tena na kurudisha ushindi huko.
Meneja wa Ushawishi na utetezi kutoka Oxfam Eluka Kibona akielezea kwa undani kuhusiana na shindano la Mama shujaa wa Chakula.
Mtaalam wa Kilimo hai kutoka SOAM wa tatu kutoka kushoto akitoa maelezo ya namna ya kutengeneza mbolea asiyo na kemikali yoyote kwa kutumia Majani,Magugu, Majivu,Maji na Udongo
Baadhi ya wanakijiji wakifanya kazi kwa vitendo kwa kusombelea nyasi kavu pamoja na magugu kwa ajili ya kutengeneza Biwi
Shamba darasa la utayarishaji wa Biwi likiwa linaendelea 
Baadhi ya wanakijiji ambapo mama Shujaa wa Chakula alipokabidhiwa zawadi zake, wakifuatilia kwa makini shamba Darasa
 Mshindi wa shindano la Mama Shujaa wa chakula 2015 msimu wa nne Bi. Caroline chelele (Kulia) akimkabidhi zawadi Kaimu Mkurugenzi wa Mji wa Ifakara Bi. Mercy Minja kwa niaba ya Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombelo
 Bi.Caroline chelele akikabidhi zawadi yake ya Kigoda kwa Shirika la Oxfam, kutoka kushoto ni Narsis Silvesti, Eluka Kibona na wa kwanza kulia ni Suhaila Thawer wote kutoka Oxfam Tanzania
 Mama Shujaa wa chakula akikabidhi zawadi ya Picha kwa Shirika la Oxfam
 Watalam wa Kilimo hai kutoka SOAM wakimkabidhi vipeperushi vinavyozungumzia kilimo hai Mama Shujaa wa Chakula 2015 Bi. Caroline Chelele
 Baadhi ya wananchi waliokuwa katika sherehe hizo za kukabidhiwa zawadi mama shujaa wa Chakula.
Picha ya pamoja ya viongozi wa Wilaya ya Kilombelo, Shirika la Oxfam na Mshindi wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula Msimu wa nne 2015 Bi.Caroline Chelele
 ………………………………………………………………………………………………. 
Mshindi  wa shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015, Linaloendeshwa na Shirika la Oxfam kupitia program yake ya Grow msimu wa nne Caroline Chelele amekabidhiwa zawadi ya vifaa vya kilimo vyenye thamani ya kiasi cha shilingi Millioni 20, nyumbani kwake kata ya Ifakara mkoani Morogoro.
 
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo ya zawadi  Mkoani Morogoro wilayani Kilombero kata ya Ifakara,Meneja Ushawishi na Utetezi kutoka Shirika la Oxfam,Eluka Kibona alisema zawadi hiyo ni moja ya utekelezaji wa shindano hilo kwa mshindi aliyeshinda shindano hilo la Mama shujaa wa Chakula 2015.
 
Alisema shirika lao linatoa takribani Milioni 20 kwa mshindi ambapo mshindi  anatakiwakuchagua zawadi ya vifaa vya kilimo ili kuweza kumuwezesha zaidi. Kibona alisema Mshindi huyo alikabidhiwa Pawatila kwa ajili ya kubebea Mazao,vifaa vya umuagiliaji pamoja na Shamba lenye Ekali 7. 
 
“Huu ni muendelezo wa shindano la mama shujaa wa Chakula kukabidhi zawadi kwa ajili ya kuwainua wakulima wadogo wadogo kuonekana na Serikali kama wao wanamchango mkubwa kwa jamii
kutokana na Chakula wanacholima ndicho kinacholisha taifa,”alisema Kibona . Aliongeza shindano hilo lipo chini ya Kampeni ya GROW yenye lengo la kuwainua wakulima wadogo wanaokumbana na changamoto mbalimbali katika kilimo.
 
Kwa Upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero , Yahya Naniya aliishukuru shirika hilo kwa hatua ya kuwathamini na kuwapigania wakulima wadogo ambao asilimia kubwa kati yao ni wanawake.Alisema
kupitia shindano hilo linaweza kuongeza Chachu kwa wakulima kufanya
shughuli za kilimo kwa kasi na kuongeza wigo mpana wa kupata mazao mengi kutokana na Mashirika mbalimbali kuwawezesha.
 
Naye Mshindi wa Shindano hilo 2015,Caroline Chelele alisema  atahakikisha zawadi hizo anazifanyia kazi ipasavyo itakayomuwezesha kumuongezea mazao mengi zaidi. Aliomba Serikali pamoja na mashirika mbalimbali kuendelea kuasidia wakulima wadogo na kuhakikisha nao
wanathaminiwa kama wakulima wakubwa.

Dkt. Ashatu Kijaji akutana na watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango

0
0
Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akiongea na watendaji wa Wizara na Taasisi alipokutana nao katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango.  Akizungumza na uongozi wa Wizara na Taasisi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji aliwaasa viongozi kutekeleza majukumu waliyokabidhiwa na kuhakikisha bajeti ya Serikali inalenga vipaumbele vinavyogusa wananchi katika kutekeleza ahadi ya Serikali.
Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akijadiliana na watendaji wa Wizara na Taasisi kuhusu masuala mbalimbali ya Wizara pamoja na Taasisi zilizo chini ya Wizara.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji kabla ya kuanza majadiliano na watendaji wa Wizara na Taasisi.

MAWAZIRI WAKABIDHIWA OFISI

0
0

mah1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano Mh. January Makamba akipokea nyaraka za Ofisi wakati akikabidhiwa Ofisi na Waziri aliyemaliza muda wake Dk. Binilith Mahenge Ofisini Mtaa wa Luthuli Dar es Salaam.
mah2
Naibu Waziri   Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano Mh. Luhaga Mpina akikabidhiwa nyaraka za Ofisi na Naibu Waziri aliyemaliza muda wake Mh. Stephen Masele . Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini jijini Dar es Salaam
mah3
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais akiwa Bwana Sazi Salula akiwa katika picha ya pamoja na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano Mh. January Makamba na Waziri aliyemaliza muda wake Dkt. Binilith Mahenge mara baada ya makabidhiano ya Ofisi.

Article 19

0
0



UNCDF YATOA BILIONI 2.4/- KUSAIDIA MIRADI 6 YA MIUNDOMBINU

0
0

Mkurugenzi wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini Tanzania, Peter Malika akizungumza na wageni waalikwa wakati wa makabidhiano ya misaada kwa miradi ya maendeleo iliyodhaminiwa na UNCDF Tanzania.
Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba akisoma hotuba yake wakati wa kukabidhi hundi kwa mashirika binafsi na ya umma kwa ajili ya kuendeleza miradi ya maendeleo.
Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba (katikati) akimkabidhi hundi bilioni moja na milioni sabini (1,070,000,000) Mkurugenzi wa Mji wa Kibaha, Bi. Jennifa C. Omolo (kulia) na kushoto ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini Tanzania, Peter Malika.DSC_0211
Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Bw. Jeshi Godfrey Lupembe (kushoto) akikabidhiwa hundi ya shilingi milioni mia tano na tisa (509,000,000/=) na Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini Tanzania, Peter Malika.
Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini Tanzania, Peter Malika wakiwakabidhi masisita hundi ya milioni miamoja na saba (107,000,000/=) wa kwanza kulia ni Msimamizi wa Mradi wa Umeme wa Lupali, Sister Imakulata Mlowe na Sister Helga Silinu ambaye ni fundi umeme katika mradi wa Lupali.
Mkuu wa wilaya ya Ileje , Mh. Rosemary Senyamule (kulia) akipokea hundi ya milioni mia mbili na milioni ishirini na sita (226,000,000/=) kutoka kwa UNCDF iliyotolewa na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini Tanzania, Peter Malika.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiendelea kufuatilia kwa makini kinachozungumzwa na baadhi ya viongozi.
Mkurugenzi wa Mji wa Kibaha, Bi. Jenifa C. Omolo akitoa neno la shukrani kwa niaba ya sekta za umma na sekta binafsi zilizopata msaada huo ili kuendeleza miradi ya maendeleo hapa nchini.
Picha ya pamoja.

Na Mwandishi wetu 
  MFUKO wa Maendeleo ya Mtaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) umetoa msaada wa shilingi bilioni 2.4 kama kianzio cha mtaji kwa waandaaji wa miradi kutoka sekta binafsi na umma. Katika hafla iliyofanyika leo na kufunguliwa na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Kagyabukama Kiliba hawala sita zilikabidhiwa wawakilishi wa waendeshaji katika miradi iliyotawanyika sehemu mbalimbali nchini. 

  Pamoja na hawala hizo za bilioni 2.4 imo pia shilingi bilioni 1.6 kwa ajili ya miradi yenye mwelekeo wa kibiashara inayoandaliwa na mamlaka za serikali za mitaa nchini Tanzania. Miradi iliyopewa kianzio cha mtaji ni pamoja na halmashauri ya mji wa Kibaha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha basi na soko la kisasa, halmashauri ya manispaa ya Moshi kwa ajili ya kituo cha kisasa cha mabasi cha biashara na manispaa ya Ileje kwa ajili ya ujenzi wa mnara wa redio kwa kushirikiana na sekta binafsi. 

  Mradi mwingine ni wa uzalishaji wa umemejua (mtandao wa vijijini) unaotekelezwa wilaya ya Korogwe na kampuni binafsi ya Ensol, mradi binafsi wa uzalishaji umeme kwa maji unaoendeshwa na wanawake wa wilaya ya njombe vijijini na mradi mdogo binafsi wa uzalishaji umeme wa Maguta uliopo wilayani Kilolo. Akizungumza kumkaribisha mgeni rasmi kutoa hundi hizo, Mkuu wa UNCDF nchini Tanzania Peter Malika alisema msaada uliotolewa umelenga kuonesha mafanikio ya program ya mradi wa fedha za nahalia (LFI) wa UNCDF katika kusaidia waandaaji wanaojishughulisha na miradi inayotoa mchango katika maendeleo ya uchumi ya maeneo husika. 

  “Licha ya kuongezeka kwa upatikanaji wa mtaji wa uwekezaji kutoka vyanzo vya umma na binafsi kwa ajili ya miundombinu, ni kiasi kidogo sana kinachofikia miundombinu ambayo inaunda uti wa mgongo wa michakato ya uchumi. LFI ilibuniwa ili kushughulikia changamoto hizi na uliundwa ili kuonyesha kwamba miradi ya miundombinu ambayo inapewa kipaumbele na serikali za mitaa na jamii inaweza kuvutia fedha endapo matatizo ya soko la mtaji yaliyopo yatashughulikiwa” alisema Malika. 

  Aidha Malika alisema katika mwaka huu timu ya LFI ilitoa msaada wa kiufundi wa kulenga na kianzio cha mtaji kwa zaidi ya miradi 30,tisa kati ya hiyo ikiwa katika hatua za juu na kwa hiyo kuwa tayari kupokea uwekezaji ikiwemo miradi tisa iliyotunukiwa msaada jana. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2012 LFI-T imesaidia zaidi ya miradi ya maendeleo ya mahalia 30 nchini Tanzania katika hatua mbalimbali tangu uwekaji mipango hadi kuwa tayari kupokea uwekezaji kwa kufanyakazi kwa karibu na Tamisemi na taasisi za fedha. 

  Aidha LFI-T inasaidia miradi katika mikoa 18 iliyo katika sekta mbalimbali ikiwamo ya usindikaji mazao ya kilimo, tabia nchi, nishati salama na uzalishaji wa bidhaa za viwandani. Naye Naibu Katibu Mkuu Kiliba akizungumza na hadhara kabla ya kutunuku hawala hizo sita alisifu kazi ya ubunifu iliyofanywa na UNCDF katika utoaji fedha kwa maendeleo ya jamii na kusema hiyo ndiyo njia sahihi ya kusababisha maendeleo. Pia aliwapongeza waanzishaji wa miradi walipookea kianzia cha mtaji wa uwekezaji kutoka UNCDF na kuwatakia mafanikio mema huku akisema kwamba serikali ya Tanzania inakaribisha uendelezwaji wa program ya LFI-Tanzania. 

  Kiliba alisema kwamba wizara yake imeanzisha kitengo maalumu cha kuhakikisha kwamba miradi ya ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi katika halmashauri inafanikiwa.Mmoja wa wakurugenzi wa halmashauri waliopewa mtaji huo wa kianzio, Jenifa Omolo kutoka halmashauri ya mjui wa Kibaha alishukuru UNCDF kwa kufanikisha halmashauri ya Kibaha kuwa na soko la kisasa na kituo cha basi cha kisasa. 

  AlisemaUNCDF na Tamisemi wamekuwa mstari wa mbele katika kuwezesha kutekelezwa kwa wazo hilo kuanzia mwanzo hadi sasa wanapopata mtaji huo. Alihimiza halmashauri nyingine nchini kupata msaada wa kiufundi kwa mawazo yao kutoka UNCDF ili kuwa na uwezo wa kusimamia maendeleo ya umma na jamii.

  “Hatuna soko katika mji wetu, kuna magenge tu na tuna kituo kidogo tu cha mabasi ambacho hakikidhi mahitaji- hizi zimekuwa changamoto kubwa kwetu kwa zaidi ya miaka kumi. Mji wetu unakua na sasa tunahitaji kuwa na miundombinu ya kisasa” alisema Omolo na kuongeza kuwa mji wa Kibaha una wajibu wa kutoa huduma bora na kwamba miundombinu mipya na ya kisasa itasaidia kuongeza mapato kwa mji huo.

Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Waziri wa Nchi wa Mambo ya Nje wa Japan

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) (kulia) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Nchi wa Mambo ya Nje wa Japan yaliyofanyika katika Ofisi ya Wizara hiyo leo.
Walioshuhudia mazungumzo hayo kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Mbelwa Kairuki, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi, Mindi Kasiga na Katibu wa Waziri, Bw. Thobias Makoba.
Maofisa kutoka Serikali ya Japan.



FURSA KWA WANAWAKE WA KITANZANIA.NJOO UJIAJIRI MWENYEWE,JIKOMBOE SASA

0
0
 
Wanawake wa Kitanzania  Miliki Biashara yako sasa.Njoo upate elimu ya Biashara kisha Ujiajiri na kukuza Kipato chako mwenyewewe.Jiandikishe kuwa mshiriki wa Manjano Dream-makers na kuingia katika Tasnia ya Vipodozi nchini kwa kujiongezea kipato kupitia kipodozi pendwa cha LuvTouch Manjano. 
Washiriki watakaochaguliwa watapata mafunzo yenye ueledi wa biashara na ujasiriamali pamoja na jinsi ya kupamba, yaani Professional Makeup-up artist BURE! Application deadline ni tarehe 24 December 2015! LuvTouch Manjano ni kipodozi cha kwanza kuzinduliwa nchini Tanzania (Makeup line) na imependwa na wanawake wengi nchini. Jiongezee kipato kwa kuwa mmoja wa washiriki kwa kuweza kuuza bidhaa zako katika eneo unaloishi huku ukiwa mtaalam vile vile wa kuwapamba wateja wako katika ubora wa uhakika. 
Tuma maombi yako kwa kujaza form iliyoandikwa ‘Participant Form’ kwenye tovuti ya Manjano Foundation www.manjanofoundation.org au leta maombi yako kwa mkono katika ofisi zetu za Manjano Foundation zilizopo Kijitonyama, jengo la Millennium Towers gorofa ya kwanza.Mafunzo haya yatatolewa kwa wanawake 30 kwa mikoa mitano (jumla wanawake 150) tu katika maeneo na tarehe zifuatazo;

MANJANO DREAM-MAKERS TRAINING TIMETABLE

1. Dar es Salaam – Tarehe: January 4 - 8, 2016

2. Mwanza – Tarehe: January 18 - 22, 2016

3. Zanzibar – Tarehe: February 1 – 5, 2016

4. Kilimanjaro – Tarehe: February 15 - 19, 2016

5. Dodoma – Tarehe: March 7 – 11, 2016 
Apply now to become a LuvTouch Manjano representative and enjoy financial independence! Sign up now by filling the form titled ‘Participant Form’ at our website http://www.manjanofoundation.org 







@luvtouchmanjano  

@shearillusionsafrica 

Kwa Maelezo Zaidi Tembelea Manjano Foundation

WAZIRI MKUU, MAJALIWA AITISHA KIKAO CHA KAZI CHA BARAZA LA MAWAZIRI LEO

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mawaziri na Naibu Mawaziri katika kikao cha kwanza cha kazi cha Baraza la Mawaziri alichokiitisha Ofisini kwake jijini Dar es salaam Desemba 15, 2015.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama wakati alipomkaribisha kuzungumza katika kikao cha kwanza cha baraza la kazi la Mwaziri, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Desemba 15,2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MKUU WA MKOA WA DODOMA AFUNGUA MASHINDANO YA TUSA

0
0
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mh. Chiku Gallawa akisalimia na wachezaji wa timu ya Zanzibar Univestity wakati wa ufunguzi wa mashindano ya shirikirisho la vyuo vikuu Tanzania (TUSA) yatakayojumuisha michezo mbalimbali ambayo yanafanyika Katika chuo kikuu cha Dodoma.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mh. Chiku Gallawa akizungumza wakati akifungua mashindano ya shirikirisho la vyuo vikuu Tanzania (TUSA) yatakayojumuisha michezo mbalimbali ambayo yanafanyika Katika chuo kikuu cha Dodoma.
washiriki mbalimbali wa mashindano ya shirikirisho la vyuo vikuu Tanzania (TUSA) yatakayojumuisha michezo mbalimbali ambayo yanafanyika Katika chuo kikuu cha Dodoma.

MBUNGE WA JIMBO LA UBUNGO, SAID KUBENEA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO.

0
0
 Mbunge wa jimbo Ubungo,(Chadema) Saed Kubenea amefikishwa mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam mapema hii leo akielekea katika  chumba cha kusomewa shtaka la kutoa lugha chafu dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
 Mbunge wa jimbo Ubungo,(Chadema) Said Kubenea akiwa na wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo, leo mara baada ya kusomewa shitaka lililokuwa likimkabiri katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo. 
 Mbunge wa jimbo Ubungo,(Chadema) Saed Kubenea akizungumza na waandishi wa habari katika mahakama ya kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Hata hivyo, Kubenea amekana kufanya kitendo hicho na kesi yake imehairishwa hadi Desema 29, mwaka huu.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

MAHAKAMA KUU YATOA DHAMANA KWA WATUHUMIWA WATATU WA UHUJUMU UCHUMI WA TRA

0
0
Mshitakiwa namba moja katika kesi ya kuhujumu uchumi, aliyekuwa naibu wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Tiagi Masamaki (Kulia) akiwa na wenzake Mahakama Kuuu Tanzania wakikabiliwa na shtaka la makosa ya jinai na uhujumu uchumi.

Watuhumiwa watatu wa uhujumu uchumi wakisindikizwa na Polisi wakitoka mahama kuu ya Tanzania  mara baada ya kupewa dhamana jijini Dar es Salaam leo.

MADIVA WA MWANZA WAJITOKEZA KWA WINGI KUFUNGA TAMASHA LA “TRUST DIVAS ONLY”

0
0
Shabiki wa Msanii Vanessa Mdee akiwa kwenye pozi la Red Carpet wakati wa Tamasha la “Trust Divas Only” ambalo lilifanyika katika hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo ambalo ni maalum kwa ajili ya akina dada ni mahususi kwa ajili ya utoaji elimu ya afya ya uzazi na maendeleo yao ya baadae.
Msanii wa Bongo fleva Vanessa Mdee, akipiga picha na baadhi ya mashabiki wake wakati wa Tamasha la “Divas only” ambalo ni mahusisi kwa ajili ya kuwaelimisha madiva mbalimbali kuhusu elimu ya afya ya uzazi. Tamasha hilo la mwisho lilifanyika katika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza baada ya kuzunguka katika majiji ya Dodoma na Mbeya katika wiki zilizopita.
Msanii wa Bongo fleva Vanessa Mdee akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa TRUST wakati wa Tamasha la “Divas only” ambalo ni mahusisi kwa ajili ya kuwaelimisha akina dada kuhusu elimu ya afya ya uzazi. Tamasha hilo lilifanyika katika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Wafanyakazi wa TRUST wanaohusika na mpango wa kuelimisha wasichana juu ya elimu ya uzazi wakiwa jukwaani tayari kwa kufungua Tamasha la “Divas Only” kwa kucheza muziki. Tamasha hilo lilifanyika katika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Madiva mbalimbali wakijiandikisha wakati wa ufunguzi wa Tamasha la “Divas Only”ambalo lilikuwa maalum kwa ajili ya kuwaelimisha akina dada juu ya afya ya uzazi na maendeleo yao ya baadae. Tamasha hilo ambalo lilipambwa vilivyo na burudani toka kwa Msanii Vanessa Mdee lilifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza.
Msanii wa Bongo fleva Vanessa Mdee akitumbuiza kwenye Tamasha la “Trust Divas Only” lililofanyika katika hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo ni maalum kwa ajili ya kina dada na limekua likitoa elimu juu ya afya ya uzazi na maendeleo ya baadae ya madiva hao tokea uzinduzi wa mfululizo wa matamasha hayo jijini Dodoma wiki mbili zilizopita.


TAMASHA la “Trust Divas only” limefunga pazia lake rasmi usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Malaika Beach resort uliopo pembezoni mwa ziwa Victoria jijini Mwanza. Wakazi na madiva wa mkoa huo walijitokeza kwa wingi kushuhudia Tamasha hilo la mwisho na la aina yake lakini kikubwa zaidi kupata elimu na hamasa juu ya uzazi wa mpango na mambo yanayowahusu wakina dada katika kupanga maendeleo yao ya baadae.

Aliyelipamba Tamasha hilo si mwingine bali ni diva wa nguvu na msanii wa kizazi kipya Vanessa Mdee ambaye tokea awali amekua akishirikiana na Trust katika mfululizo wa matamasha hayo yaliyoanza rasmi wiki mbili zilizopita jijini Dodoma.

Mara baada ya kupanda jukwaani na kuporomosha burudani ya nguvu Vanessa alionekana kushangiliwa kila kona na madiva hao waliokuwa wakiimba sambamba na msanii huyo ambae alifanikiwa kukata kiu ya madiva wengi wa mkoa huo waliojitokeza kwa wingi kushuhudia burudani yake.

Mfululizo wa matamasha hayo ya Trust ambayo ni chapa ya njia za kisasa za uzazi wa mpango zenye kuaminika pamoja na bidhaa na huduma za maisha na urembo zinazotengenezwa kwa ajili ya wanawake yamefikia tamati baada ya kuzunguka kwa muda wa wiki tatu kwenye miji mitatu tofauti ili kuhamasisha madiva mbalimbali wajipange kwa ajili ya mafanikio yao ya baadae. Trust ipo katika kumsaidia diva wakati wote wa safari hii.

“Ni furaha yangu kubwa kuwa tumeweza kukamilisha zoezi hili kwa ufanisi mkubwa tangu tulipozindua matamasha haya jijini Dodoma”… alisema Meneja Masoko wa Trust Sialouise Shayo.

Bi. Shayo aliongeza kuwa katika zoezi zima wamefanikiwa kuwafikia madiva lukuki katika mikoa yote mitatu waliyoitembelea ambapo kwa pamoja wameweza kufurahi, kuelimishana na kujifunza kutoka kwa wataalamu mambo mbalimbali zikiwemo njia nyingi bora za uzazi wa mpango kama njia ya kitanzi ambayo ni bora sana na ina ufanisi wa zaidi ya asilimia 99.9.

Kama wewe ni Diva wa Trust ama unataka kujua Trust inahusu nini, Tutafute kupitia ofisi zetu zinazopatikana Dodoma, Mbeya na Mwanza au kwa kupitia tovuti yetu (trustlife.co.tz) na ututembelee leo.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA KATIBU MKUU WA CCM LUMUMBA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha kwenye Makao Makuu ya Chama, Ofisi Ndogo CCM Lumumba,Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mhe.Majaliwa Kassim Majaliwa.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro nje ya Ofisi Ndogo,Lumumba katikati ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka wilaya ya Simanjiro Mhe. Christopher Ole Sendeka nje ya Ofisi Ndogo, CCM Lumumba.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha wageni cha Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

ENHANCE AUTO YAKABIDHI GARI KWA MSHINDI WA SHINDANO LA MATUMIZI BORA YA MITANDAO YA KIJAMII

0
0

Kamanda wa Kikosi Usalama barabarani, Mohamed Mpinga (kulia) akimkabidhi zawadi ya gari aina ya Toyota Sarf, mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Jackson Kapongo aliyeshinda kupitia mchezo wa Matumizi bora ya Mitandao ya Kijamii iliyoendeshwa na Kampuni ya Enhance Auto ya Jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq Butt.Picha na Father Kidevu Blog.

Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq Butt akionesha stika za kuhamasisha usalama barabarani ambazo pia zilizinduliwa na Kamanda Mpinga.

Meneja Mauzo Enhance Auto, Ayaka Kashida akionesha shindano jipya ambalo mshindi atajishindia Toyota Noah mpya.

Jackson Kapongo akiwa katika gari yake Toyota Sarf na pembeni yake ni Kamanda Mpinga.

Hii ndio gari jipya Toyota Sarf aliyo jishindia Kapongo. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA





Wageni mbalimbali waalikwa wakifuatilia tukio hilo.

Bahati na sibu ilichezeshwa na wateja kujishindia mipira .

Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq Butta akitoa maelezo ya bahati nasibu ya kushinda mipira.

Na Father Kidevu

MHITIMU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jackson Kapongo ameibuka mshindi na kukabidhiwa gari aina ya Toyota surf lenye thamani ya zaidi ya sh milioni 24 katika shindano lililochezeshwa na kampuni ya kuuza magari ya Enhance Auto.

Kapongo alikabidhiwa gari lake hilo na Kamanda wa Polisi Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga baada ya kushinda katika shindano lililoendeshwa na Enhance Auto likiwataka washiriki kuonesha ni namna gani wanaweza kutumia mitandao ya kijamii na kujiletea manufaa.

Akizungumza kampuni hiyo, Mpinga alisema imekuwa ikichezesha shindano hilo kila mwaka na kushirikisha nchi mbalimbali Afrika ambapo kwa mwaka jana mshindi alipatikana kutoka Zambia lakini kwa mwaka huu ameshinda mtanzania hivyo ni jambo la kujivunia.

Alisema mbali na kutoa zawadi lakini kampuni hizo za magari zinajukumu kubwa la kutoa mchango kwa usalama barabarani kwa kutoa elimu sambamba na kuuza magari yenye viwango vinavyokubalika ili kuepusha ajali zisizo za lazima.

"Natoa wito kwa kampuni zingine kuwekeza katika usalama barabarani na wasifikirie tu kuuza magari bali wahakikishe magari yanakuwa salama na wanaoendesha wanakuwa salama... tuagize magari yenye viwango mana ajali nyingi pia zinasababishwa na ubovu wa magari" alisema.

Mapema Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq Butt alisema shindano hilo mshiriki anatakiwa kushiriki kwa kuchagua mitandao yao ya kijamii kwa wingi zaidi na lilishirikisha nchi ambazo wanafanya nao biashara ikiwemo Botswana, Burundi, Jamhuri ya Kongo, Malawi, Msumbiji, Sudan ya Kusini, Uganda, Zambia, Zimbabwe na Tanzania.

Martha Mwaipaja, Jesca BM, Mwahangila kupanda jukwaa la Krismasi

0
0
WAIMBAJI nyota wa muziki wa Injili hapa nchini Martha Mwaipaja, Jesca BM na Christopher Mwahangila wanatarajia kupanda katika jukwaa la Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Waimbaji hao wanaungana na wenzao waliotangulia kuthibitisha kushiriki tamasha hilo ambalo lina mlengo wa kurudisha Shukrani kwa Mungu baada ya kufanikisha uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 kwa amani na utulivu.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama aliwataja wengine ambao watakuwa sambamba na wenzao siku hiyo ni pamoja na Sifael Mwabuka sambamba na Kwaya ya Yombo KKKT.

Msama alisema tamasha hilo linadhaminiwa na gazeti la Dira ya Mtanzania ambako alitoa wito kwa mashirika na kampuni mbalimbali kujitokeza ili kufanikisha tamasha hilo.

Aidha Msama aliwataja wengine waliothibitisha kupanda jukwaa la tamasha hilo ni pamoja na Rebeca Malope, Eiphraim Sekeleti, Solomon Mukubwa, Faustine Munishi, Upendo Nkone, Christina Shusho, Joshua Mlelwa na Kwaya ya Wakorintho Wapili.

Msama anaweka bayana kauli mbiu ya tamasha hilo ni Njooni wote tumsifu Mungu kwa pamoja, tumuinue Mungu kwa nyimbo na kucheza mbele yake.
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images