Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

Dj Bon Love alivyokonga nyoyo za mashabiki wa burudani katika usiku wa Heart & Soul

0
0
Mkali wa magoma hapa nchini na nje, Dj Bon Love akifanya yake katika Usiku wa Heart & Soul uliofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye kiota kinachobamba zaidi hapa mjini cha Raphsody, ndani ya Jengo la Viva Towers katikati ya Jiji la Dar. Dj Bon Love na maDJ wengine wakali hukutana pamoja kwenye kiota hicho ili kukonga nyoyo za wapenda Burudani kutoka maeneo mbalimbali.Usiku huo uliwezeswa kwa Udhanimi Mkubwa wa Kilaji ya Heineken.
Baadhi ya Wadua wa Burudani wakiwepo DJ. Venture na Mwanalibeneke Haki Ngowi wakiwakilisha katika Usiku wa Heart & Soul.
 
Mmoja wa maDJ wanaopiga katika Usiku wa Heart & Soul akifanya mambo yake.
Furaha pindi wadau wanapokutana.
 Mdau Othman Michuzi (kulia) na marafiki wengine nao hawakutaka kukutukipwa ya Usiku wa Heart & Soul ndani ya kiota pendwa cha Raphsody, Jengo la Viva Towers katikati ya Jiji la Dar.

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii na Jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri , leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Katiba na Sheria, Harrison Mwakyembe katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Ashantu Kijaji katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha  Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Lameck Nchemba katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimwapisha waziri wa Sera, Bunge, Kazi ,Vijana,Ajira na Walemavu, Dkt. Abdallah Possi katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri, na manaibu Waziri leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII.JINSIA, WATOTO NA WAZEE AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KATIKA HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR LEO.

0
0
Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Khamis Kigwangala akielekea katika hospitali ya Amana leo jijini Dar es Salaa mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli.
        Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na            Watoto, Khamis Kigwangala akizungumza na wauguzi aliowakuta katika          hospitali ya Amana leo alipotembelea katika hospitali hiyo jijini Dar es                                                                                      Salaam.

Mhe. Anjela Kairuki Aanza Kazi rasmi Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora

0
0
ang3
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora Bw. Tixon Nzunda (aliyesimama) akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (wa kwanza kutoka kulia) kuongea na watendaji wa ofisi yake baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
ang4
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb) (kulia) akizungumza na watendaji wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora mara baada kufika ofisini kwake kuanza kazi leo Jumamosi.
anj1
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb) (wa pili kutoka kushoto) akiwasili ofisini na kulakiwa na watendaji wa ofisi yake mara baada ya kuapishwa. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Bw. Tixon Nzunda.
ang2
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb) akiweka saini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili rasmi katika ofisi yake leo Jumamosi.


…………………………………………………………………………….
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (MB) ameanza kazi rasmi Leo Jumamosi Desemba 12/2015 mara baada ya kuapishwa Ikulu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.  John Pombe Magufuli.

Mhe. Kairuki akiongea na watendaji wa Wizara yake alielekeza masuala ya kiutumishi ikiwamo  kusimamia nidhamu ya kazi ni jambo la msingi  hivyo kutumia daftari la mahudhurio  peke yake haitoshi.“Tutumie Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kubaini Watumishi wanaoiba muda wa kazi wa Serikali” Mhe. Kairuki alisisitiza na kusema kazi lazima zitekelezwe  kwa kiwango cha juu.

Mhe. Waziri Kairuki alisema suala la kufanya kazi kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali ni muhimu kwa kuwaelekeza watendaji wa Wizara yake kushirikiana na Wakala ya Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kubaini taarifa za watumishi wanaofariki ili wafutwe katika orodha ya malipo.Mhe. Waziri Kairuki alisema ushirikiano katika kazi ni jambo la msingi ili kushauriana katika kutatua changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa masuala mbalimbali ya kiutumishi na kuondoa malalamiko.

Awali, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Bw. Tixon Nzunda akimkaribisha Mh. Waziri Kairuki kuongea na watendaji wa Wizara alisema waajiri wote nchini walishaelekezwa kufanya kazi ya kusafisha takwimu zisizohitaji katika Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara Serikalini (HCMIS).

Bw. Nzunda alisema Watumishi wote wenye takwimu chafu (takwimu zisizohitajika) katika mfumo wa HCMIS watafutwa baada ya kukamilika kwa zoezi hilo ifikapo mwisho wa mwezi Desemba 2015 na endapo kutakua na mwajiri atakayekua na takwimu chafu atawajibika kwa kushindwa kutekeleza agizo hilo.

Zaidi ya Vijana 400 Wahitimu Mafunzo ya ZIMAMOTO na Uokoaji

Updates za dada Joyce Richard Mwambepo wa mbeya aliyelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuvunjika miguu ajalini

0
0
Ankal akiwa wodini kumtembelea dada Joyce 
 Dada Joyce alipowasili Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wiki iliyopita

Dada Joyce akiwa wodini MOI

Ndugu Wasamaria Wema,
Tunapenda kutumia fursa hii kuwashirikisha tena habari ya kusikitisha kuhusu dada Joyce Rishard Mwambepo (pichani akiwa na mwanaye wa miaka 4, na miguu yake iliyopooza) mkaazi wa Sinde jijini Mbeya. Dada huyu mwenye umri wa miaka 27 anaishi na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na huyo mwanaye wa miaka 4.
Kwa bahati mbaya mwezi April mwaka jana wa 2014 dada huyu alipata ajali ya kugongwa na gari ambayo dereva hakusimama kumsaidia. Ila kwa msaada wa wasamaria wema alipelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa  Mbeya ambako alikaa kwa miezi mitatu bila kupata matibabu, kwa kukosekana nyenzo pamoja na pesa  za kumfanyia uchunguzi.
Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce amevunjika miguu yote miwili,  hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa tena Mbeya baada ya kukosa pesa  za vipimo na matibabu.
Hadi  Msamaria mwema na Mpiganaji Deo Kakuru anakutana naye dada huyu alikuwa amelala nyumbani kwa bibi yake ambaye ni mlezi wake tangu akiwa na miaka minne baada ya wazazi wake wote wawili kufariki dunia. 
Hawezi kukaa wala kusimama na anajisaidia hapo hapo kitandani kwa msaada wa mwanaye huyp na bibi yake.  Inasikitisha.
Hivyo Deo Kakuru, kwa msaada mkuwa wa michango ya Wasamaria Wema,  amefanikiwa kumsafirisha dada Joyce kwa Fast Jet kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya  hadi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha MOI jijini Dar es salaam ambako alipokelewa na kulazwa katika jengo jipya liitwalo Wodi ya Magufuli ghorofa ya tatu wodi namba 2.
--------------------------------------
UPDATES:
Baada ya Deo Kakuru kuweka mitandaoni tatizo la dad Joyce, Wasamaria Wema kadhaa wakajitokeza kumsaidia.  Hatuna uhakika kwamba wote wangependa majina yao yawekwe hadharani, Ila tunapenda hadi sasa kukiri upokeaji wa Tshs:
1. 505,000/-
2. 50,000/-
3.100,270/-
4. 10,000/-
5. 100,000/-
6. 500,000/- (ahadi ya uhakika)
7. 500,000/- (Michuzi Media Group)
7. 800,000/-  (Kulipia gharama za vipimo vya CT Scan Regency Hospital mgonjwa atapofikishwa Dar es salaam).

Hivyo ndiyo kusema jumla ya Tshs. 2,565,270/-  tayari zilikusanywa kumsaidia dada yetu huyu anayeteseka. Kwa niaba ya mgonjwa tunashukuru sana kwa msaada huo, hana cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa Mola mzidishiwe pale mlipopungukiwa. KUTOA NI MOYO.

Aidha, kwa kiasi kilichopatikana tayari dada Joyce ameshafanyiwa vipimo vya MRI  Alhamisi  iliyopita na hivi sasa yanasubiriwa majibu siku ya Jumatatu ambapo baadaye Jopo la Madaktari Bingwa litaka na kuamua nini kifanyike kimatibabu. Tunashukuru madaktari na watumishi wote wa MOI kwa kuhitimisha hilo, nasi tunaendelea kuwaomba waendelee na huduma hiyo hadi dada Joyce atapopata matibabu.

Vile vile tunamshukuru sana Msamaria Mwema Mama Rozi aliyejitolea kumhudumia dada Joyce pale wodini ambako mama yake mzazi amelazwa na ana matatizo karibu sawa na ya dada yetu. Bila kuchoka mama Rozi amekuwa akimletea chakula na vinywaji dada Joyce kila siku na kumfanyia huduma za usafi kila siku. Ubarikiwe sana Mama Rozi.

Shukurani pia ziwaendee wasamaria wema wengine pamoja na wadau ambao baada ya kuguswa na matatizo ya dada Joyce wamekuwa wakimtembelea hapo wodini na kumfariji. Asanteni sana.

Wito wetu tunaomba tuendelee kumsaidia kwa hali na mali dada Joyce kwani mara baada ya majibu ya vipimo yatapotoka Jumatatu, ni dhahiri kutakuwa na mahitaji zaidi katika matibabu yake. 

Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal anaendelea kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce akiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Kitengo cha MOI. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba+255 754 271266 kwa jina la Ankal.

Mratibu mwenza Deo Kakuru naye anaendelea kusaidia kwa kumtunza bibi yake Joyce na mwanae mwenye umri wa miaka 4 huko Mbeya.
Deo Kakuru Msimu
Msamaria mwema



WAZIRI WA AFYA NA NAIBU WAKE WAFANYA ZIARA ZA KUSHTUKIZA KATIKA HOSPITALI YA MWANANYAMALA NA AMANA

0
0
IMG_8404
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akizungumza na baadhi ya wananchi kuhusu upatikanaji wa huduma wanazopata hospitalini hapo ambao wengi wao hawajaridhishwa na utendaji wa wahudumu wa zamu wa siku hiyo.
IMG_8408
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akizungumza na mmoja wa Daktari (ambaye hakutaka sura yake iyonekane) kuhusu utaratibu wa utoaji huduma kwa wagonjwa wanaosubiri huduma hizo.
IMG_8425
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akimuulizia Kiongozi wa zamu katika ofisi za mapokezi ya hospitali hiyo.
IMG_8433
Muuguzi Kiongozi wa Hospitali ya rufaa ya Amana, Bupe Mwakalenge akijibu maswali ya Mheshimiwa Naibu Waziri kuhusu kutokuwepo kwa baadhi ya Madaktari katika baadhi ya vitengo.
IMG_8475
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akitazama moja ya cheti cha mgonjwa aliyekuwa akilalamika kusubiri kwa muda mrefu bila kupatiwa huduma.
IMG_8498
Mwanasayansi wa Maabara ya Hospitali ya rufaa ya Amana, Jabir Mukhsin (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Dkt. Hamis Kigwangala kuhusu ubovu wa mashine inayotumika kufanya vipimo mbalimbali (MS4S) ikiwemo mzunguko wa damu mwilini ambayo kwa sasa imeharibika na kubakiwa na mashine moja ambayo ufanyaji wake wa kazi unachukua muda mrefu kutoa majibu sahihi.

IMG_8517
MS4S Mashine ambayo imeharibika.
IMG_8525
Mmoja wa wagonjwa waliokuwepo wakisubiri huduma ya kipimo cha MS4S akimwelezea Mh. Naibu Waziri kuhusu kutokufanyika kwa kipimo hicho licha ya kuwa hospitali wamepokea malipo yake ya kufanyiwa kipimo hicho.
IMG_8542
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akionekana kushangwazwa na jambo fulani wakati akiendelea na ziara yake hospitalini hapo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Gideon Malabeja.
IMG_8550
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akiwa nje ya chumba cha Ultra-sound ambacho kimefungwa kufuli licha ya maelezo ya Muuguzi Kiongozi wa Hospitali hiyo Bi. Mwakalenge kuwa mashine hiyo ni nzima na haina tatizo lolote.
IMG_8590
Muuguzi Kiongozi wa wagonjwa wa nje, Francis Itima akimwelezea Mheshimiwa kuhusu changamoto ya upungufu wa vitanda katika wodi ya wakina mama waliojifungua.
IMG_8599
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akikagua wodi ya watoto ambayo aliridhishwa na hali iliyopo katika wodi hiyo.
IMG_8611
Mfamasia wa zamu katika hospitali ya Amana, Anna Kajiru akimpa maelezo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala kuhusu upungufu wa dawa uliopo katika duka hilo la dawa hospitalini hapo.
IMG_8614
Baadhi ya wananchi wakipatiwa huduma ya dawa katika duka la dawa lililopo hospitalini hapo.
IMG_8667
Pichani juu na chini ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akitoa mrejesho kwa waandishi wa habari kuhusu ziara yake ya kushtukiza, matatizo yanayoikabili hospitali hiyo na hatua ambayo wizara itachukua.
IMG_8379
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akiwasili katika Hospitali ya rufaa ya Amana iliyopo Ilala, Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza baada ya sherehe za kuapishwa.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

Na Rabi Hume, Modewjiblog
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala ikiwa ni masaa machache tangu kutoka kuapishwa na Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Waziri wa Wizara hiyo.

Mhe. Ummy aliwasili katika hospitali ya Mwananyamala, majira ya saa 8 mchana na kuanza kuzungumza na wananchi mbalimbali waliokuwa wamekaa eneo la hospitali hiyo kuhusu matatizo yanayowakabili pindi wanapofika hospitali hapo kupatiwa huduma ambao wengi wao walionekana kutoridhishwa na huduma wanazopatiwa wanazozihitaji.

Mmoja wa wananchi ambao alielezea kwa masikitiko yaliyomkuta pindi alipofika hospitalini hapo ni, Bi. Khadija Meso ambaye alisema kuwa walikuwa na siku tatu tangu wamefika hospitalini hapo ambapo walikuwa wamempeleka mtoto wao ambae alikuwa anaumwa lakini alikuwa hapatiwi huduma hali imeyopelekea kupoteza maisha kwa mtoto huyo.Mwingine aliyezungumza aliyejitambulisha kwa jina la Mama Madohoro alisema kuwa anashangazwa na hospitali ya rufaa kuwatoza wazee pesa licha ya sera ya afya kusema wazee na watoto chini ya miaka 5 kupatiwa bure huduma za kiafya.

Alisema kuwa alimpeleka hospitalini hapo ndugu yake mwenye umri wa miaka 90 ambae alikuwa akihitajika kulipia vipimo vilivyo na gharama kubwa huku vya gharama ndogo akipatiwa bure na kutokana na uwezo mdogo wa kifedha alionao ukapelekea kupoteza maisha yake kwa mgonjwa huyo.

Nae Othaman Rwambo alimuomba Mhe. Waziri kuwa ajaribu kuzungumza na wauguzi wa hospitali hiyo kutokana na kutoa majibu machafu kwa wagonjwa wanaofika katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
IMG_8386
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akikagua vyumba vya madaktari baada ya kuona mlundikano wa wagonjwa wakisubiri huduma.
Alisema kuwa kasi ya rais wa awamu ya tano ni kufanya kazi na wao kama watumishi wa umma wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kuwahudumia watanzania na kuwataka watumishi hao kuweka uzalendo mbele kuliko maslahi binafsi.
Akiwajibu wananchi hao pamoja na kuelezea sababu ya ziara yake, Mhe. Ummy Mwalimu alisema kuwa amefika hospitalini hapo ili kujua changamoto zinazowakabili wananchi lakini pia kujifunza ni kitu gani ambacho wananchi wanahitaji kuboreshewa katika sekta ya afya.
Alisema kuwa matatizo aliyoyakuta ni changamoto kwake na wizara yake na watakaa kama wizara kuona ni jinsi gani wanaweza kutatua matatizo yanayojitokeza katika hospitali hiyo na kuutaka uongozi wa hospitali hiyo kumaliza matatizo yaliyo ndani ya uwezo wao ndani ya siku 3.
“Mambo ambayo nimeyakuta hapa ni kujifunza na kuona ni hali gani wanakumbana nayo wananchi wanapokuja kupata huduma za kiafya lakini pia kwangu ni changamoto lakini kwa kasi aliyonayo rais wetu wa awamu ya tano hatuna budi na sisi kuwa na kasi hiyo na mimi napenda kuwaambia wananchi wanaopata huduma katika hospitali hii tutatatua matatizo yanayowakabili,
“Nimeupa uongozi wa hospitali kazi ya kumaliza matatizo yaliyopo wanayoweza kuyamaliza kama neti kwenye wodi kama ile ya wajawazito, na hata mambo ya feni kwenye wodi za wanaume na mengine tutakaa kama wizara kuyajadili tuone jinsi gani tutayamaliza,” alisema Mhe. Ummy.
IMG_8392
Mh. Naibu Waziri, Dkt. Hamis Kigwangala akiingia katika chumba cha X-Ray kuangalia utendaji wa kazi unavyoendelea.
Aidha Mhe. Waziri alisema siku ya Jumatano wanatarajia kutambulisha namba ambayo wananchi watakuwa wanaitumia kutoa taarifa wizarani kuhusu kero wanazokutana nazo hospitalini wanapokwenda kupata huduma za matibabu.
Nae Naibu Waziri wa Wizara hiyo ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala amefanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya rufaa ya Amana na kukuta baadhi ya huduma za afya katika hospitali hiyo zikiwa zimesimama kwa sababu mbalimbali.
Baadhi ya matatizo ambayo amekutana nayo hospitalini hapo ni pamoja na kutokuwepo kwa mtoa huduma katika chumba cha Utra Sound, Ubovu wa mashine ya kuchunguza matatizo yaliyopo mwilini (MS4S) na kubakia moja ikifanya kazi ambayo inachukua muda mrefu kutoa majibu.
Matatizo mengine ambayo amekutana nayo ni uchache wa vitanda, kutokupatikana kwa dawa katika duka la hospitali huku maduka ya nje ya hospitali zikipatikana na kutokuwepo kwa baadhi ya watumishi ofisini kukiwa ni muda wa kazi.
IMG_8395
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akizungumza na mtoa huduma katika chumba cha X-Ray ambapo aliridhishwa na utoaji huduma wa mtumishi huyo.
Akizungumzia matatizo hayo alisema kuwa kuna uzembe umekuwa ukifanyika kwa baadhi ya watumishi hali inayofanya hospitali hiyo kuwa na wagonjwa wengi bila kupatiwa huduma na badala yake wanawapa rufaa kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Tunachotaka ni kuona wananchi wanapata huduma, nimefika hapa nakuta hata chumba cha Utra Sound anaehusika hayupo na hata wagonjwa wakija hawatapata huduma na kinachofata hapo wanampeleka Muhimbili ndiyo maana Muhimbili imejaa wagonjwa kumbe sababu ni uzembe uliopo huku kwenye hospitali za rufaa,” alisema Dkt. Kingwangala.

Aidha Mhe. Naibu Waziri ameuagiza uongozi wa hospitali hiyo kufika wizarani siku ya jumatatu saa 10 jioni ili kupewa maelekezo jinsi ya kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi na kwenda sawa na kasi ya rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye anahitaji kuona serikali yake ikifanya kazi kwa kuhudumia wananchi.
IMG_8691

WAZIRI UMMY MWALIMU NA NAIBU WAKE DK. KIGWANGALA WARIPOTI WIZARANI KWAO TAYARI KWA KAZI

0
0
IMG_8324
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiongozana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando (kulia) kuelekea ofisini kwake.
IMG_8325
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa wizara hiyo.
IMG_8329
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wageni ofisini kwake huku Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando akishuhudia tukio hilo.
IMG_8346
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akiwasili katika wizara ya hiyo moja kwa moja akitokea Ikulu baada ya kula kiapo.
IMG_8347
Pichani juu na chini ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa wizara hiyo.
IMG_8350
IMG_8354
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akimkaribisha Naibu wake Dkt. Hamis Kigwangala ofisini kwake.

IMG_8356
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando (kulia) akisalimiana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala ofisini kwa Mh. Ummy Mwalimu.
IMG_8359
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mh. Ummy Mwalimu.
IMG_8374
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando akitoa taarifa ya maendeleo ya Wizara kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu na Naibu wake Dkt. Hamis Kigwangala. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Gideon Malabeja.
IMG_8317
Gari la Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu likiwasili Makao Makuu ya wizara hiyo na kupokelewa kwa saluti mara tu baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli katika sherehe zilizofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
IMG_8321
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando mara tu baada ya kumalizika kwa tukio la kuapishwa.


Mfanyakazi wa Global, Haruni Sanchawa aagwa Dar, kuzikwa Serengeti-Mara

0
0
MWANDISHI wa habari wa Global Publishers Ltd, Haruni Sanchawa, aliyefariki dunia Desemba 9 mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar, ameagwa leo nyumbani kwa mjomba wake Kitunda jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea Mugumu-Serengeti, mkoani Mara, ambapo atazikwa kijiji cha Lemungololi.

Sanchawa alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya tumbo, alifariki saa chache baada kuhamishiwa katika hospitali hiyo baada ya kupewa rufaa kutoka Hospitali ya Amana alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa.

"MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU HARUNI SANCHAWA MAHALI PEMA PEPONI - AMEN"
DSC_0941Marehemu Haruni Sanchawa enzi za uhai wake.1.Mke wa Marehemu, Adelina Haruni Sancha akiuagwa mwili pamoja na wanaye wawili.Mke wa Marehemu, Adelina Haruni Sancha akiuagwa mwili pamoja na wanaye wawili.2.Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (wa kwanza mbele ) akiwa na huzuni msibani hapo.Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (wa kwanza mbele ) akiwa na huzuni msibani hapo.3.Waombolezaji wakiwa msibani.Waombolezaji wakiwa msibani.4.Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigiongo (wa pili kulia) akiomboleza msibani hapo.Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigiongo (wa pili kulia) na wafanyakazi wa Global wakiomboleza msibani hapo.6.Baadhi ya wafanyakazi wa Global Publishers waomboleza.Baadhi ya wafanyakazi wa Global Publishers wakiomboleza.
7.Huzuni ikiwa imetanda msibani hapo.Huzuni ikiwa imetanda msibani hapo.8.Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Haruni Sanchawa likishushwa Nyumbani kwa Mjombake Kitunda Dar kwa ajili ya kuagwa.Jeneza lenye mwili wa marehemu Haruni Sanchawa likishushwa Nyumbani kwa Mjomba wake Kitunda Dar kwa ajili ya kuagwa.9.Jeneza lenye mwili.Jeneza lenye mwili.10.Mchungaji wa Kanisa la Asebuliz of God, Benedict B.Salikiwa akitoa abada fupi y kumuombea marehemu.Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God, Benedict B. Salikiwa akiongoza ibada fupi ya kumuombea marehemu.11.Mhariri Mwandamizi wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambul akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Kampuni ya Global Publishers.Mhariri Mwandamizi wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Kampuni ya Global Publishers.12.Wafanyakzi wa Global, Bahati Haule na Hadija Mngwai wakipita mbele ya jeneza kuuaga mwili.Waombolezaji wakiaga mwili wa marehemu.13.Ndugu na jamaa wakiuaga mwili wa marehemu Sanchawa.Ndugu na jamaa wakiuaga mwili wa marehemu Sanchawa.14. Mwandishi wa Habari Imelda Mtema (wakwanza mbele) akiwa na huzuni wakati wa kuuaga mwili wa mpendwa wao.Wafanyakazi wa Global wakiuaga mwili wa mpendwa wao.15.Mwandishi wa Habari,Gladnes Malya akisaidiwa na wafanya kazi wenzake mara baada ya kushindwa kuuaga mwili wa Sanchawa.Mwandishi wa Habari,Gladnes Malya akisaidiwa na wafanya kazi wenzake mara baada ya kushindwa kuuaga mwili wa Sanchawa.17.Mhariri Mwandamizi, Walusanga Ndaki (mwenye fulana ya Uwazi) akitoa heshima za mwisho.Mhariri Mwandamizi, Walusanga Ndaki (mwenye fulana nyeupe) akitoa heshima za mwisho. 19.,Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo akitoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa Sanchawa.Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo akitoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa Sanchawa.20.Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Richard Manyota akiongoza wafanyakzi wa Global kuuaga mwili wa Sanchawa.Mhariri Kiongozi wa Gazeti la Championi, Saleh Ally (mbele mwenye miwani) na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Richard Manyota (mwenye fulana nyeusi) wakiauaga mwili wa Sanchawa.21.Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa, Osca Ndauka akitia heshim a za mwisho.Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa, Oscar Ndauka akiuaga mwili wa marehemu.F.Mkurugenzi wa Global Publishers, Lydia James (mbele) akipita kuuga mwili wa marehemu Sanchawa.Mkurugenzi wa Global Publishers, Lydia James (mbele) akipita kuuga mwili wa marehemu Sanchawa.DSC_0656A.Jeneza lililobeba mwili likiingizwa kwenye gari tayari kuelekea Serengeti Mkoani Mara.DSC_0654Mwili wa Marehemu ukipandishwa kwenye gari kwa ajili ya safari kwenda Mugumu, Serengeti mkoani Mara kwa Mazishi. 

Mbunge wa Jimbo la Chumbuni aanza Kutekeleza Ahadi Zake kwa Wananchi wa Jimbo la Chumbuni kwa Ujenzi wa Ukuta Kituo cha Afya Chumbuni

0
0
Mhe Mbunge AMJAD akichimba msingi wa ujenzi wa ukuta wa kituo hicho cha Afya Chumbuni Zanzibar.
Mhe Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Pondeza AMJAD akishgiriki katika ujenzi wa taifa wa uchimbaji wa msingi wa kituo cha Afya Chumbuni ikiwa ni ahadi yake ya kujenga ukuta huo kukiweka katika mazingira mazuri kituo hicho cha Afya Chumbuni kwa ajili ya kutowa huduma bora.  

Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar na Kamanda wa Vijana Jimbo la Chumbuni Mhe. Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwahutubia Vijana wa UVCCM Tawi la Chumbuni wakati wa Ziara ya Katibu Mkuu wa Vijana Mhe Shaka Hamdu Shaka kutembelea Jumuiya za Vijama katika Majimbo ya Zanzibar.
Vijana wa CCM wakimsikiliza Mbunge wao wakati wa mkutano ziara ya Katibu Mkuu wa UVCCM Tanzania Mhe Shaka Hamdu Shaka,mkutanom huo wa Vijana umefanyika tawi la CCM Chumbuni Karakana
Mbunge wa Chumbuni Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwa na Katibu Mkuu wa Vijana CCM TanZania Mhe Shaka Hamdu Shaka wakielekea katika ujenzi wa Taifa wa kuchimba msingi wa ukuta wa Kituo cha Afya cha Chumbuni ikiwa ni moja ya ahadi za Mbunge kukiimarisha Kituo hicho kwa kuaza ujenzi wa Ukuta ikiwa nin hatua za mwazo za kukiimarishas kituo hicho kutoa huduma bora kwa wananchi wa jimbo la chumbuni na jirani zao.

WADAU WAPONGEZA FILAMU MPYA YA "GOING BONGO"

0
0

Rais wa Shirikisho la Filamu Simon Mwakifamba akiongea na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi filamu ya ‘Going Bongo’ uliofanyika katika ukumbi wa cimema wa Cinemax jana Ijumaa jijini Dar es salaam

WADAU mbalimbali waliofika kwenye onyesho la kwanza la filamu ya Mtanzania anayeishi nchini Marekani wametoa sifa kemkema kuhusu filamu hiyo inayokwenda kwa jina la ‘Going Bongo’ na wamewataka wasanii wa hapa nchini waige mfano wake.

Wakizungumza baada ya kutoka kuaitazama ndani ya ukumbi wa cimema wa Cinemax Ijumaa usiku mkongwe katika filamu Ibrahimu Banane almaarufu kwa jina la ‘Mzee Katembo’ alisema kwamba mtunzi wa filamu hiyo amewashtua wasanii wa hapa nyumbani na Afrika Mashariki kwa ujumla.

“Ametushtua sisi kwamba tutunge filamu na kuzicheza katika kiwango cha kimataifa na tuchukue muda mrefu ili kuweza kutunga na kurekodi filamu zetu kama tunataka kulikamata soko hilo na kujitangaza kwa ujumla endapo tu tutafuata nyayo za mtunzi wake Ernest Napoleon.” alisema Katembo.

Alisema m ameiangalia filamu hiyo inayokwenda kwa jina la ‘Going Bongo’ ni nzuri kila muigizaji amesimama katika nafasi yake na kuuvaa uhusika vilivyo na endapo wasanii wa hapa nyumbani watataka kutengeneza filamu nzuri wasiogope kuingia gharama kama jinsi filamu hiyo inavyoonesha muandaaji alivyoingia gharama kwamba aimerekodiwa katika nchi mbili tofauti.

“Hapa nyumbani sisi tumezoea kuona kwamba msanii anafyatua filamu mbili ndani ya mwezi mmoja jambo ambalo hupunguza ubunifu kwani ni vigumu kichwa kimoja kuweza kutoa kitu kizuri ndani ya mwezi mmoja” alisema Katembo.

Msemaji wa Waigizaji nchini Massoud Kaftani aliimwagia sifa filamu hiyo na kusema kwamba wamepata somo kutoka kwa Ernest hivyo wanashukuru pia kwa kupata nafasi ya kuishuhudia filamu hiyo na kuahidi wkamba watafanyia kazi changamoto mbalimbali zilizo ndani ya tasnia ya filamu na maigizo nchini.

Wakati huohuo Rais wa Shirikisho la Filamu Simon Mwakifamba aliongeza kwa kusema kuwa yeye binafsi amevutiwa na filamu hiyo kutokana na kuzingatiwa kwa vina na mpangilio mzuri, “hili ni jambo la kujivunia kama watanzania pia tunatoa wito kwa watanzania wengine wanao ishi nje ya nchi kujipanga na kuibua vipaji vyao kimataifa kama jinsi alivyotuonesha Ernest hivyo huko waliko nina imani na wao wameifuatilia filamu hii ya Going Bongo ilete chachu kwa watanzania wanaoishi ughaibuni na wa hapa nyumbani wote tujipange kwa pamoja katika kuikuza na kuiendeleza tasnia hii” alisema Mwakifamba.

Filamu hiyo ilishuhudiwa na wadau mbalimbali akiwamo Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ huku akiitoa maneno ya kuisifa gfilamu hiyo na kusema kuwa muandaaji ametoa somo kwa wasanii wahapa nchini.

Filamu hiyo inayokwenda kwa jina la ‘Going Bongo’ ilioneshwa kwa mara ya kwanza kwenye ukumbi wa sinema wa Century Cinemax uliopo Mlimani City, Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mashabiki wengi ambao wengi wao walikiri kuvutiwa nayo.

Filamu hiyo ambayo mpaka sasa imetwaa tunzo kadhaa, pamoja na tunzo ya Ziff ina maudhui ambayo yanonyesha maisha ya Daktari aliyejitolea kwenda kufanya huduma nchini Tanzania kwa muda wa mwezi mmoja huku mtunzi na muandishi pia aliyeisimamia katika kuitengeneza na kuigiza filamu hiyo ni Ernest Napoleon .

Filamu hii imerekodiwa majiji makubwa mawili ambayo ni Dar es Salaam na California Marekani, inaelezea sehemu ya maisha ya kweli aliyonayo Daktari mwenye asili ya nchini Ufaransa aliyeondoka Ulaya na kwenda kufanya kazi barani Afrika.


Kati ya tuzo ambazo filamu hii imeshinda ni pamoja na, Filamu Bora Afrika Mashiriki katika tamasha la Zanzibar International Film Festival (Ziff) na Filamu Bora ya Kimataifa katika tamasha la ‘Black Entertainment Fashion’, ‘Film and Television Awards’ (BEFTA)

KAMPUNI 15 ZASHINDWA KULIPA KODI ZA KONTENA 329 ZILIZOTOROSHWA KATIKA BANDARI KAVU YA AZAM

0
0
Kaimu Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Dk. Philip Mpango akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) juu ya hatua za ulipaji wa kodi iliyokwepwa katoka katika kontena 329 katika bandari Kavu ya Azam,leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakifatilia taarifa kwa Kaimu Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Dk. Philip Mpango leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

KAMPUNI 15 zimeshindwa kulipa kodi za kontena zilizotoroshwa katika bandari kavu ya Azam inayomilikiwa na Said Salim Bakhressa na kodi iliyokuwa imekwepwa kwa kampuni 43 ni zaidi ya Sh. Bilioni 12.

Kodi iliyolipwa ya Kontena 329 hadi jana ambayo ndio ilikuwa ulipaji wa hiari kwa ndani ya siku saba za Rais Dk. John Pombe Magufuli ni zaidi ya sh. bilioni 10 pekee.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Kamisha Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Dk. Philip Mpango amesema kuwa kampuni hizo zinatakiwa kulipa kodi hiyo kwani ulipaji wa hiari wa siku saba za Rais Dk. John Pombe Magufuli umeisha jana  hivyo hatua zitachukuliwa kuhakikisha wanalipa kodi hiyo ya Watanzania.

Mpango amesema kuwa kampuni 13 tu ndio zimeweza kumaliza kodi  yote iliyokuwa imekadiriwa na TRA kwenye Kontena 329 zilizotoroshwa katika Bandari Kavu ya Azam (ICD).

Amesema kampuni 15 zimelipa sehemu ya kodi na wanaendelea kuwadai licha ya kuisha kwa siku saba hivyo wanawajibu kulipa kodi iliyobaki katika Akaunti ya TRA iliyofunguliwa Benki Kuu (BoT) yenye namba 9921169 785.

Mpango amesema  kuwa wafanyabiashara ambao wameshindwa kulipa katika hicho hatua zitachukuliwa na wasubiri cha moto.
Amesema watumishi 36 wa TRA wanatuhumiwa kushiriki katika upotevu wa kodi kutokana na kontena 329  kuondoshwa bandarini kinyume cha taratibu za forodha na hivyo kusababisha serikali ikose mapato.

Mpango amesema kuwa TRA inawaomba wananchi taarifa juu mali za kifisadi na mwenendo mbaya wa baadhi ya watumishi wa mamlaka hiyo.

Amewataka watumishi kuwasilisha tamko za mali wanazomiliki pamoja na fedha zilizo katika benki na mwisho wa kufanuya hivyo ni Desemba 15 mwaka huu.

BONANZA LA UZAZI WA MPANGO KWA VIJANA LAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Mkurungezi Mkuu wa Marie Stopes Tanzania, Anil Tambay akizugumza na wananchi  (hawapo pichani)  kwenye bonanza la uzazi wa Mpango kwa vijana ambalo lilifanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mwembeyanga,Temeke jijini Dar.
 Mgeni rasmi Zukrah Mkwizu akizungumuza na wananchi (hawapo pichani) kuhusiana na suala zima la Uzazi wa Mpango,na kusisitiza kuwa uzazi wa mpangp ni silaha imara ambayo vijana wanaweza kuitumia kupangilia maisha yao na kujikinga dhidi ya utoaji mimba usio salama na kulinda ndoto zao dhidi ya mimba zisizotarajiwa.
 Balozi wa vijana wa Marie Stopes , Doreen Benne akifafanua jambo mbele ya wakazi wa mji wa Temeke na viunga vyake waliofika kwenye kwenye Bonanza la Uzazi wa Mpango kwa Vijana lililofanyika mwishoni mwa wiki ndani ya viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam.
 Mwanamuziki Barnabas Elias 'Barnaba akionesha umahili wake wa kulitawala jukwaa katika Bonanza la Uzazi wa Mpango kwa Vijana Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam
Sehemu Ya Wananchi Waliofika Katika Bonanza La Uzazi Wa Mpango Kwa Vijana wakifuatilia yaliyokuwa yakijili kwenye bonanza hilo ndani viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Jijini Dar Es Salaam
 (Picha na Emmanuel Massaka , Globu ya jamii).


 =======  =======  ========
Wanamuziki na Viongozi wa serikari ya Mkoa wanashirikiana na Marie Stppes Tanzania na zaidi ya Vijana 1,000 kutoka vikundi mbalimbali vya vijana kuhamasisha upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango, Mwembeyanga, Wilaya ya Temeke Leo.

Akiongea katika mkutano huu, Mkurungezi Mkuu wa Marie Stopes Tanzania, Anil Tambay amesema, “Hiki ni kizazi kikubwa zaidi cha vijana katika hisoria ya Tanzania, asilimia 54 ya Watanzania wapo chini ya umri wa Miaka 20. Mafanikio yao yanamaanisha mafanikio ya Tanzania na mategemeo ya uchumi Imara ambao kila mmoja wetu ataufurahia na kunufaika nao. Lakini wakati huo huo, maisha na matarjio ya vijana yanaharibiwa – au wakati mwingine yanaishia pabaya – kutokana na mimba zisizotarajiwa.”

Asilimia 44 ya wanawake Tanzania – karibu nusu yao – hupata ujauzito wafrikiapo umri wa miaka 19. Huu huwa mwisho wa matarajio/ndoto ya kielimu na taaluma au utoaji mimba usio salama, ambao idadi yao inakadiliwa kuwa 1,500 kila mwaka kwa wanawake wanaoishi Tanzania – wengi wao wakiwa vijana wa kike.

“Vijana wa kiume wanaathirika pia” Aliongeza Mr Tambay, “Wengi wao hujikuta wanakuwa kin baba kabla hawajawa Tayari, hivyo hujikuta wanaachana na mipago ya kwenda chuoni au chuo kikuu ili waweze kutafuta fedha kwa ajili ya familia ambayo hawakuitarajia.”

Championi wengine wa upatikanaji wa huduma za Uzazi wa Mpango kwa vijana kwenye tukio hili ni Bambo, Barnaba, Haika, Mwasiti, Nahreel na Queen Darleen. Message inayotolewa ni kuwa,Uzazi wa Mpango ni silaha imara ambayo vijana wanaweza kuitumia kupangilia maisha yao – kujikinga dhidi ya utoaji mimba usio salama na kurinda ndoto zao dhidi ya mimba zisizotarajiwa.

“Leo tunawaambia vijana wachague Maisha mazuri kwa ajili yao” Alielezea Mr Tambay,“Natunawaomba watu wote wenye madaraka – Manesi, Walimu na Viongozi wa serikari – wasiwe vikwazo kwa upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpago kwa vijana badala yake wawaunge mkono na kwawashauri watumie kiuwajibikaji. Napenda kumalizia kwa kusema, nawashukuru vijana wote  waliofika hapa kushirikiana nasi. 

Maria Stopes ipo hapa kwa ajili yenu na kwa ajili ya kwaunga mkono kufanya maamuzi. Kama una ndoto, zilinde na jilinde kwa Uzazi wa Mpango.

Tume ya Mipango yatembelea Kiwanda cha Karatasi Mufindi

0
0
Magogo ambayo yanasagwa na kuwa vipande vidogo vidogo ambavyo vinasagwa na kuwa karatasi.
Vipande vidogo vidogo vya miti vikiwa katika mkanda (conveyer belt) wa kupeleka kwenye mashine ya kutengeneza karatasi.
Matius Makupa, Meneja wa Kiwanda cha Karatasi cha Mufundi akitoa maelezo juu ya utengenezaji wa karatasi kwa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo waliotembelea kiwandani hapo.

MAZOEZI YA VITENDO WAKATI WA KUHITIMISHA MAFUNZO YA AWALI KWA WAHITIMU WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI YALIYOFANYIKA CHUO CHA UONGOZI JKT KIMBIJI

0
0
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakionyesha jinsi ya kuzima moto wakati wa maonyesho ya kufunga mafunzo ya kozi ya awali ya Sajini na Askari wa Jeshi hilo,yaliyofanyika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji,jijini Dar es Salaam,mwishoni mwa wiki.
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakiwa wamebeba mfano wa majeruhi wa ajali, mara baada ya kumuokoa kutoka eneo la tukio wakati wa maonyesho ya kufunga mafunzo ya kozi ya awali ya Sajini na Askari wa Jeshi hilo,yaliyofanyika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji,jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

Wahitimu wakionyesha mafunzo ya karate waliyopata mara baada ya kuhitimu kozi ya awali ya Sajini na Askari wakati wa kufunga mafunzo hayo katika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji,jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.


ENHANCE AUTO YAKABIDHI GARI KWA MSHIBNDI WA SHINDANO LA MATUMIZI BORA YA MITANDAO YA KIJAMII

0
0

Kamanda wa Kikosi Usalama barabarani, Mohamed Mpinga (kulia) akimkabidhi zawadi ya gari aina ya Toyota Sarf, mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Jackson Kapongo aliyeshinda kupitia mchezo wa Matumizi bora ya Mitandao ya Kijamii iliyoendeshwa na Kampuni ya Enhance Auto ya Jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq Butt.Picha na Father Kidevu Blog.
Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq Butt akionesha stika za kuhamasisha usalama barabarani ambazo pia zilizinduliwa na Kamanda Mpinga.
Meneja Mauzo Enhance Auto, Ayaka Kashida akionesha shindano jipya ambalo mshindi atajishindia Toyota Noah mpya.
Jackson Kapongo akiwa katika gari yake Toyota Sarf na pembeni yake ni Kamanda Mpinga.

Hii ndio gari jipya Toyota Sarf aliyo jishindia Kapongo. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA






Wageni mbalimbali waalikwa wakifuatilia tukio hilo.

Bahati na sibu ilichezeshwa na wateja kujishindia mipira

Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq Butta akitoa maelezo ya bahati nasibu ya kushinda mipira.


**************








Na Father Kidevu

MHITIMU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jackson Kapongo ameibuka mshindi na kukabidhiwa gari aina ya Toyota surf lenye thamani ya zaidi ya sh milioni 24 katika shindano lililochezeshwa na kampuni ya kuuza magari ya Enhance Auto.

Kapongo alikabidhiwa gari lake hilo na Kamanda wa Polisi Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga baada ya kushinda katika shindano lililoendeshwa na Enhance Auto likiwataka washiriki kuonesha ni namna gani wanaweza kutumia mitandao ya kijamii na kujiletea manufaa.

Akizungumza kampuni hiyo, Mpinga alisema imekuwa ikichezesha shindano hilo kila mwaka na kushirikisha nchi mbalimbali Afrika ambapo kwa mwaka jana mshindi alipatikana kutoka Zambia lakini kwa mwaka huu ameshinda mtanzania hivyo ni jambo la kujivunia.

Alisema mbali na kutoa zawadi lakini kampuni hizo za magari zinajukumu kubwa la kutoa mchango kwa usalama barabarani kwa kutoa elimu sambamba na kuuza magari yenye viwango vinavyokubalika ili kuepusha ajali zisizo za lazima.

"Natoa wito kwa kampuni zingine kuwekeza katika usalama barabarani na wasifikirie tu kuuza magari bali wahakikishe magari yanakuwa salama na wanaoendesha wanakuwa salama... tuagize magari yenye viwango mana ajali nyingi pia zinasababishwa na ubovu wa magari" alisema.

Mapema Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq Butt alisema shindano hilo mshiriki anatakiwa kushiriki kwa kuchagua mitandao yao ya kijamii kwa wingi zaidi na lilishirikisha nchi ambazo wanafanya nao biashara ikiwemo Botswana, Burundi, Jamhuri ya Kongo, Malawi, Msumbiji, Sudan ya Kusini, Uganda, Zambia, Zimbabwe na Tanzania.
Hata hivyo alisema kwa kutambua umuhimu wa usalama barabarani kwa kushirikiana na jeshi la polisi kikosi cha Usalama Barabarani wameanzisha kampeni ya 'Endesha kwa Usalama' ambapo pia walikabidhi stika za magari lengo likiwa ni kujenga uhusiano na wateja wao.

Akizungumza zawadi hiyo, Kapongo aliishukuru kampuni hiyo na kuwataka vijana kutumia mitandao ya kijamii kwa faida na si kwa kujifunza mambo ambayo huharibu maadili ya jamii.

WANAFUNZI WA MLIMANI WATOA YA MOYONI KWA MHE.NAPE

0
0

Wahitimu TIA wameaswa kutumia mafunzo ya ujasiriamali kukabiliana na changamoto ya soko la ajira nchini.

0
0
TI5
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua akimkbidhi Mwanafunzi Cosmas Ephraim zawadi ya kufanya vizuri katika masomo yake ya  shahada ya Uhasibu wakati mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
TI6
Baadhi ya wahitimu wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakati wa mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
ti1
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua akitoa hotuba wakati mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
TI2
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Fedha na Mipango Prof. Isaya Jairo akimkaribisha Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua kutoa hotuba wakati mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
TI3
Afisa Mtendaji Mkuu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt. Joseph Kihanda akitoa taarifa fupi ya taasisi hiyo inayojumuisha pia idadi ya wahitimu 3,169 ambao kati yao wanawake ni 1,562 sawa na asilimia 49.3 na wanaume ni 1,607 sawa na asilimia 50.7 wakati mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
TI4
Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiwasili viwanja vya mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.


TI7
Baadhi ya wahitimu wakisiliza Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua akisoma tamko la kuwatunuku vyeti wahitimu hao wakati wa mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
TI8
TI9
TI10
Baadhi ya wahitimu washangilia kwa furaha baada ya kutunukiwa vyeti na Mgeni Rasmi ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakati wa mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
TI11TI12
Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua (katikati) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Fedha na Mipango Prof. Isaya Jairo (kushoto) wakiondoka eneo la mahafali mara baada ya kuatunuku vyeti wahitimu 3,169 wakati wa mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt. Joseph Kihanda
……………………………………………………………………………………………..
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Wahitimu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wameaswa kutumia mafunzo ya ujasiriamali waliyoyapata chuoni hapo katika kukabiliana na changamoto ya soko la ajira na kuelekeza mawazo yao katika kujiajiri badala ya kuajiriwa.Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakati mahafali ya 13 ya taasisi hiyo kwa Kampasi ya Dar es salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam

“Mafunzo ya ujasiriamali mliyoyapata yawe chachu ya ufanisi wenu katika kufanyakazi kwa bidii, uadilifu, ubunifu, umakini na weledi wa hali ya juu ili kujiletea maendeleo yenu wenyewe yenye na yenye tija kwa taifa”,“Msingi wa mafanikio na kuhifadhi ajira ni kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni, jiepusheni na vitendo vya rushwa na ubadhirifu mkitabua kuwa rushwa ni adui wa haki na maendeleo” alisisitiza Dkt. Mwinyimvua.

Mahafali hayo ya 13 yanajumuisha wahitimu kutoka fani za Uhasibu, Ununuzi na Ugavi, Usimamizi wa Biashara, Uongozi wa Rasilimali Watu, Masoko na Uhusianao wa Jamii na Uhasibu wa Fedha za Umma ambazo msingi wake ni kendesha uchumi wa taifa katika kusimamia mapato na matumizi ya fedha za umma kwa kutumia wataalamu mbalimbali ambao wengi wao ni tunda la Taasisi ya Uhasibu Tanzania.

Aidha, Dkt. Mwinyimvua aliwasihi wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata vema katika kuendeleza uchumi wa taifa, kuboresha maisha yao na jamii inayowazunguka pamoja na kupambana na kupambana na changamoto zinazolikabili taifa kwa kudhibiti ubadhirifu na matumizi yasiyo sahihi ya rasilimali za taifa.

Awali akitoa taarifa fupi kwa Mgeni Rasmi, Afisa Mtendaji Mkuu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt. Joseph Kihanda alisema kuwa wapo jumla ya wahitimu 3,169 kati yao wanawake ni 1,562 sawa na asilimia 49.3 na wanaume ni 1,607 sawa na asilimia 50.7.

Idadi hiyo inajumuisha wahitimu 441 kutoka kampasi ya Mtwara na wahitimu 2,728 kutoka kampasi ya Dar es salaam kwa ngazi ya cheti, stashahada, shahada na shahada ya uzamili.Dkt. Kihanda alisema kuwa kwa mwaka wa masomo 2014/2015 Taasisi ya Uhasibu Tanzania ina jumla ya wahitimu 6,949 kutoka kampasi za Dar es salaam, Mbeya, Singida, Mtwara, Mwanza na Kigoma.

Kati ya wahitimu hao idadi ya wanawake ni 3,458 ambao ni sawa na asilimia 49.8 na idadi ya wanaume ni 3,491  ambao ni sawa na asilimia 50.2, wahitimu kutoka kampasi ya Kigoma ni wa kwanza tangu taasisi hiyo ianzishwe mkoani humo.Dkt. Kihanda aliongeza taasisi bado inaendelea na zoezi la udahili kwa mwaka wa masomo 2015/1016 kwa ngazi ya shahada ya kwanza pamoja na wanafunzi katika ngazi ya cheti cha awali kwa awamu ya pili mwanzoni mwa mwaka 2016.

Taasisi hiyo inatarajia kudahili wanachuo wapatao 10,500 katika kampasi zake zote na kufanya idadi ya wanafunzi kuongezeka kutoka 12,899 ya sasa hadi 17,739.Kwa upande wake mwanafunzi Cosmas Ephraim alisema kuwa amefarijika kuhitimu masomo ya shahada ya Uhasibu mbayo ameahdi kuitumia elimu hiyo ili kutoa mchango wake katika kuendeleza taifa liweze kuwa na maendeleo yenye tija kiuchumi kwa Watanzania wote.

WAALIMU NCHINI WATAKIWA KUWAPA FURSA NA KUWAHAMASISHA WANAFUNZI KUSHIRIKI MICHEZO

0
0
 Washindi walishiriki  katika mashindano mbali mbali wakipewa zawadi na Mgeni Rasmi Leonard  Thadeo  mara baada ya kumaliza mashindano hayo
 Washindi walishiriki  katika mashindano mbali mbali wakipewa zawadi na Mgeni Rasmi Leonard  Thadeo  mara baada ya kumaliza mashindano hayoPicha zote na Miza Othman - Maelezo, Zanzibar
 Walimu walioshiriki mashindano ya michezo mbalimbali wakionyesha vipaji vyao katika mashindano yaliyofanyika viwanja vya nje Amani Mjini Zanzibar 
  Walimu walioshiriki mashindano ya michezo mbalimbali wakishindana kuvuta kamba
  Mkurugenzi  Idara ya Maendeleo ya Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Tanzania Leonard  Thadeo akitoa maneno ya shukurani wakati wa  kuwakabidhi  zawadi  washindi  wa  mashindano mbali mbali  ya Walimu kutoka Wilaya 3 Kaskazini, Mjini na Kusini huko katika viwanja vya nje Amani Mjini Zanzibar.


Na Rahma Khamis -Maelezo, Zanzibar 
Waalimu Nchini wametakiwa kuwapa fursa na kuwahamasisha wanafunzi wa Skuli mbalimbali kushiriki katika michezo ili kuwezesha kupata timu nzuri na kushiriki katika mashindano ya Kimataifa. 

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari Utamaduni Wasanii na Michezo Tanzania Leonaed Thadeo katika Uwanja wa Amani nje wakati alipokua akifunga Shamrashamra za Tamasha siku ya Walimu Duniani. 

Amesema nchini  Tanzania wananchi wengi hulalamika kwa kutofanya vizuri katika michezo kutokana na Waalimu kusahau wajibu wao wa kuwajenga wanafunzi wao kimichezo tangu wadogo wakati wapo Maskulini jambo ambalo linarejesha nyuma maendeleo ya michezo hiyo. 

Aidha amefahamisha kuwa iwapo jamii itashiriki katika michezo mbalimbali itaweza kujiepusha na mararadhi sambamba na kujenga afya hivyo zoezi hilo liwe endelevu kwani kufanya hivyo kutasaidia walimu kuwa imara kimichezo. 

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amewataka waalimu kutoa fursa kwa kushirikiana na Wizara huusika kwenda kusoma katika Chuo cha Maendeleo ya michezo Tanzania Bara ilikuongeza uwezo na idadi ya waalimu wa michezo. 

Kwa upande wake mwalimu Mussa Abdulrabi kutoka Wizara ya Elimu amesema lengo la kufanya tamasha hilo ni kuwafanya walimu kushiriki michezo mbalimbali na kuonesha vipaji vyao katika michezo hiyo. 
Amesema katika mwaka huu hakuna changamoto zilizojitokeza hivyo wanajiandaa mwakani ili wawe na uwezo wa kufanya vizuri zaidi katika tamasha lijalo . 

Sambamba na hayo mwalimu huyo ameaahidi kuwa watawashajiisha walimu wenzao kwenda kujiunga na Chuo cha Maendeleo ya Michezo ili kupata walimu wengi kwa ajili ya michezo kwani Serekali ina nia ya kuendeleza Michezo . 

Wakielezea furaha zao washindi katika Tamasha hil
o wameiomba Wizara kuangalia suala la michezo zaidi kwa kuandaliwa mafunzo maalum ili kuweza kushiriki katika mashindano mbalimbali. 
Katika shamrashamra hizo kumefanyika michezo ya ikiwemo kuvuta kamba, Mpira wa Mkono, mbio za Gunia pamoja na Mpira wa miguu kutoka katika Mikoa mitatu ya Zanzibar ikiwemo Mkoa Kusini Unguja , Kaskazini Unguja na Mkoa wa mjini Magharib ambapo Mkoa wa Kaskazini na Mjini ndio walioibuka washindi ikifuatiwa na Mkoa wa Kusini Unguja.

Maaskofu wafurahishwa Makamu wa Rais kukubali kuwa mgeni rasmi Tamasha la Krismasi

0
0
MAASKOFU wa madhehebu  mbalimbali wa Makanisa hapa Tanzania wamempongeza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kukubali kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo linalokwenda sambamba na Shukrani kwa Mungu baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 kwa amani na utulivu, uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Askofu wa Kanisa la KKKT, Dk Alex Malasusa anasema ni jambo jema kumshukuru Mungu baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika kwa amani na utulivu kiasi cha kumpata rais mchapakazi.

Amefurahishwa na kukubali kuwa mgeni rasmi kwa kuitikia wito wa ombi la madhehebu mengine ingawa yeye ni Muislamu kwani kufanya hivyo ni kuzidi kuvunja makundi ya udini ndani ya nchi yetu.Anasema ni  wakati wa kumshukuru Mungu baada ya  tukio kubwa la uchaguzi Mkuu ambako kabla yalifanyika maombi ya kumuomba Mungu kuwapitisha katika uchaguzi Mkuu ambao ulifanyika kwa amani na utulivu.     
  
Askofu Dk. Valentino Mokiwa wa Kanisa Anglican,  jimbo Kuu la Dar es Salaam, amempongeza Msama Promotions kwa kuandaa matamasha ya kumuimbia na kumtukuza  Mungu kupitia matamasha yake.Askofu Mokiwa anasema ni suala la kujivunia ikiwa ni mara ya kwanza kuwa na mgeni rasmi ambaye ni mwanamke wa kwanza nchini kuwa Makamu wa Rais na kitendo chake kinaonekana kuwa ni cha kizalendo.

 Anasema ni jambo la kumshukuru Mungu baada ya kufanikisha kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu hivyo amemtaka Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama kuendelea kujitolea kuandaa matamasha  kama hayo yenye tija kwa taifa.Naye  Askofu Mkuu wa jimbo la Mashariki la Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dk Lawrence Kametaanasema amefurahishwa  na  Makamu  wa  Rais, kuonesha uzalendo na kukubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo lenye lengo la kushukuru baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.


Anasema kuwa kitendo hicho cha Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan  kuwa Mgeni rasmi kimezidi kuiaminisha Dunia kuwa Tanzania ni ya amani na haina matabaka ya kidini na ukabila.Katibu Mkuu wa Makanisa ya Kipentekoste nchini, Askofu David Mwasota amesema kwamba Tanzania  imezaliwa upya kwa kutinga katika neema ambayo ilikuwa inatarajiwa na wengi.

Askofu Mwasota anasema  kuwa Rais Magufuli  hakukosea kumteua mama Samia kuwa makamu wa Rais  wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Askofu wa Kanisa la Wasabato, Warwa Marekana anasema wamefurahishwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassani kukubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha la Krismasi ambalo linakwenda sambamba na kushukuru Tanzania kupita kwenye uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25.

Marekana anasema kukubali kuwa mgeni rasmi inathibitisha kwamba tamasha hilo halina ubaguzi wa dini kwani Waislamu na Wakristo  Askofu  wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Telesphor Mkude amesema kuwa kama amani itakuwepo nchini ana amini serikali ya Awamu ya Tano chini ya John Pombe Magufuli kutakuwa na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo.

Amesema kuwa wao kama viongozi wa dini wanafurahishwa na jinsi kiongozi mwanamama shupavu tena muislamu kuamua kuabudu pamoja na wakristo katika  tamasha hilo la shukrani.

Hiyo ni nzuri na sisi kama viongozi wa dini tunaiunga mkono kampuni ya Msama Promotions kwa kutoa mwaliko kwa Makamu wa Rais hivyo tunaamini atakuwa chachu ya kuwahimiza wananchi wengine ambao sio wakristo kujumuika katika kutoa shukrani kwa mungu mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu.

Alisema, hata kama Magufuli atakuwa ni kiongozi bora kiasi gani lakini kama amani haitapatikana itakuwa ni kazi bure hivyo amewataka wananchi kuienzi amani iliyopo.Alisema amekuwa akifuatilia matamasha yanayoandaliwa na kampuni ya Msama Promotions, yamekuwa yakilenga katika jamii hivyo ni kitu  cha kushukuru kwa kampuni hiyo kuandaa matamsha kwa lengo la kuenzi amani.

Amesema angeomba hali hiyo iendelee hata mikoani  ili kuwafanya wananchi wa mikoani kuona umuhimu wa amani haiitajiki Dar es Salaam pekee.Amesema kuwa anashukuru kumaliza kwa uchaguzi mkuu kumalizika salama  na nchi imepoa baada ya kupatikana Rais ambaye anaonekaa kuwa na dhamira ya kweli katika kuhakikisha anaipelekea Tanzania katika uchumi wa kati.

Askofu Mkude amesema suala la amani ni muhimu na amewataka Maaskofu na Mapadri kuhakikisha wanahubiri amani wanapokuwa katika ibada zao.Askofu wa Kanisa la Menonite, Amos Mhagache amesema ni nafasi yetu kumshukuru Mungu kwa kutubariki kupita katika kipindi kigumu cha uchaguzi Mkuu.

Askofu Mhagache anasema kwamba Yesu Kristo ni mwokozi hasa sasa hivi ndio nchi Mungu aliyotupa katika kipindi hiki baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25.
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images