Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 705 | 706 | (Page 707) | 708 | 709 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Watendaji Wakuu wa ofisi zilizo chini yake katika kikao cha kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika ofisini kwake.

  Na Lilian Lundo-Maelezo
  OFISI ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma imeanza rasmi kutekeleza Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa Umma nchini ambao ulizinduliwa Agosti Mosi mwaka huu.

  Akiongea na vyombo vya habari leo, Katibu Mkuu Hab Mkwizu amesema utekelezaji huo umeanza rasmi Disemba, 2015 ambapo kila mtumishi wa Umma ataweka saini ya kiapo kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na mazingira ya Taasisi husika.

  “Utaratibu wa Utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa Umma umetolewa kupitia waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma Na. 2 wa mwaka 2015 kuhusu utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu kwa viongozi, watumishi wa Umma na sekta binafsi wa tarehe 1 Agosti, 2015.” Alisema Mkwizu.

  Mkwizu aliongezea kwa kusema, uanzishwaji wa Ahadi ya Uadilifu ni muendelezo wa uundwaji wa vyombo vya kusimamia maadili baada ya ongezeko kubwa la ubadhirifu, utoro sehemu za kazi na kushuka kwa nidhamu katika kipindi cha miaka ya themanini na tisini.

  Alivitaja vyombo vingine ambavyo vilianzishwa kusimamia ahadi na uadilifu kuwa ni Sekretariate ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

  Mkwizu alivitaja vipengele ambavyo mtoa ahadi anatakiwa kuvitamka ni, kuwa mzalendo wa nchi yake na kutii Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kuhudumia Umma na watumishi wenzake kwa heshima, kutimiza wajibu wa kutoa huduma bora kwa umma, kutoa huduma bora kwa usawa kwa watu wote na kutofanya ubaguzi wa dini, siasa, kabila, udugu, ukanda, jinsia, urafiki au hali ya mtu.

  Vipengele vingine ni kutumia rasilimali za Umma kwa manufaa ya Umma, kutotoa siri za Serikali au mteja kwa watu wasiohusika isipokuwa kwa maslahi ya Umma, kufanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juu, kutoomba kushawishi, kutoa wala kupokea rushwa na kutotumia madaraka kwa manufaa binafsi ya ndugu, rafiki au jamaa.


  Aidha, Mkwizu ametoa wito kwa waajiri wote kuhakikisha kuwa utekelezaji wa Ahadi na Uadilifu unakamilika ifikapo tarehe 31/12/2015 na kuwasilisha Ofisi ya Rais – UTUMISHI kabla ya tarehe 25/02/2016 na utekelezaji wake kuwa kila ifikapo Juni 30 ya kila mwaka. Fomu za Ahadi ya Uadilifu zinapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais – UTUMISHI yenye anwani www.utumishi.go.tz.

  0 0


   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu uchaguzi wa wabunge unaotarajiwa kufanyika Tarehe 13/12/2015 katika jimbo Handeni na Arusha Mjini, (kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura Bw.Clarence Nanyaro kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
   Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva(ambaye hayupo katika picha) leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waaandishi wa habari kuhusu taratibu zitakazo tumika katika uchaguzi wa wabunge katika jimbo la Arusha na Handeni.

  0 0

   Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Efm Radio, Denis Ssebo akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya wasanii zaidi ya 50 wa Bongo Movie akiwamo Steve Nyerere, Wema Sepetu na Vicent Kigosi (Rey) wataungana na kituo cha redio cha EFM na Benki ya DTB kufanya usafi Desema 9 mwaka huu. Usafi huo utaanzia katika barabara ya Morocco hadi Magomeni, mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkuu wa Bidhaa na Masoko wa benki ya Diamond Trust Bank (DTB), Sylvester Bahati.
   Mkuu wa Bidhaa na Masoko wa benki ya Diamond Trust Bank (DTB), Sylvester Bahati akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya usafi ni nguzo moja wapo katika benki hiyo na si kwa ajili ya agizo la Rais John magufuli bali ni zoezi endelevu, kulia ni Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Efm Radio, Denis Ssebo.
  Wandishi wa habari wakimsikiliza Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Efm Radio, Denis Ssebo, mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam
  Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii.

   WASANII  wa 
  Bongo Movie zaidi ya 50 akiwamo Steve Nyerere, Wema Sepetu na Vicent Kigosi (Rey) wataungana na kituo cha redio cha EFM na Benki ya DTB kufanya usafi Disemba 9 mwaka huu.

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa EFM, Denis Ssebo, amesema usafi huo utaanzia katika barabara ya Morocco hadi Magomeni.

  Ssebo amesema katika usafi huo EFM, DTB pamoja na wasanii hao watashirikiana na viongozi mbalimbali walioko madarakani pamoja na wakazi wa Kinondoni chini ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.

  Kauli mbiu ya siku hoyo isemayo ‘Naona aibu kuishi na uchafu’ huku tukiunga kauli mbiu ya kinondoni ‘Usafi uanze na mimi’ endapo kila mmoja atatambua umuhimu wa usafi wake, mazingira yake tutaweza kwa pamoja kulimaliza tatizo la uchafu nchini,”amesema Ssebo. 


  Kwa upande wake mwakilishi wa DTB Silvesta Bahati alisema usafi ni nguzo moja wapo katika benki hiyo na si kwa ajili ya agizo la Rais John magufuli bali ni zoezi endelevu.

  0 0

   Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete akiongozana na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli , Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana Kinana kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015.
    Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015.
   Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipigiwa saluti na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana Kinana kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015.

  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana Kinana.
   Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim. wengine ni Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa, Makamu wa Rais Mhe samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana Kinana kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015.
  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015
  PICHA NA IKULU.


  0 0

   Askari wakipita karibu na kiwanda cha urafiki jijini Dar es Salaam huku wakiwaangalia kwa makini wafanyakazi wa kiwanda hicho waliomo katika mgomo wakidai manejimenti yakiwanda hicho kiasi cha shilingi Bilioni 9.

  Bidhaa zinazouzwa katika moja ya eneo la kiwanda cha urafiki yaliyokodishwa na uongozi wa menejimenti ya kiwanda hicho unaolalamikiwa na wafanyakazi kwamba wanajipatia mapato kwenye maeneo ya kiwanda hicho huku wao wakiwalipa kiduchu.
   Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha urafiki wakiwa kwenye geti la kuingilia kiwandani hapo wakimngoja Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ili kuzungumza nao.

  Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Paul Makonda, akiwasili na msafara wake kiwandani hapo kwa ajili ya kuzungumza na wafanyakazi walio katika mgomo. 
  Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Paul Makonda akizungumza na wafanyakazi wa Kiwanda cha Urafiki leo jijini Dar es Salaam.
  Wafanyakazi wa kiwanda cha Urafiki wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.

  0 0


  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akitoa nasaa zake kwa Vijana wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kujitolea katika taasisi mbalimbali hapa nchini Tanzania wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea Duniani ambapo Tanzania yamefanyika jijini Dar. (Picha zote na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog).
  Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo akitoa historia ya kujitolea pamoja na kuwasisitiza vijana kuwa na moyo wa kujitolea katika jamii ili kutengeneza msingi mzuri wa chini.
  Mmoja wa vijana wanaojitolea Fatma Mohammed akieleza changamoto anazozipata kama mtoto wa kike kwa kipindi chake chone anapokuwa anajitolea kwenye mashirika mbalimbali.
  Kikundi kutoka kwa vijana wanaojitolea wakitoa burudani.
  Mkuu wa DFID Tanzania, Vel Gnanendran akitoa hamasa kwa vijana wanaojitolea wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea.
  Vijana wakifuatilia kwa makini kinachozungumzwa kutoka meza kuu wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea.
  Ofisa Mtendaji wa VSO, Dk Philip Goodwin akizungumza kambo wakati wa maadhimisho ya siuku ya kujitolea yaliyofanyika jijini Dar
  Baadhi ya vijana waliohitimu masomo ya Elimu ya Juu wakitoa ufafanuzi kuhusu changamoto za ajira wanazokutana nazo mara baada ya kuhitimu vyuo hadi kupelekea kufanyakazi za kujitolea ili kuweza kufanikisha malengo yao waliyojiwekea.DSC_0115
  Vijana wanaojishughulisha na shughuli za kujitolea katika taasisi mbalimbali hapa nchini Tanzania wakiwa wameshika baadhi ya malengo 17 ya maendeleo endelevu 17.
  Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na Vijana wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kujitolea katika taasisi mbalimbali hapa nchini Tanzania. 

    Na Mwandishi wetu
  KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel wamewataka vijana kuwa na moyo wa ujasirimali kwa kuelewa umuhimu wa kujitolea.Ole Gabriel alitoa wito huo mwishoni mwa juma wakati akizungumza na vijana kwenye siku ya kujitolea (International Volunteers Day) iliyoadhimishwa kitaifa nchini Ijumaa badala ya Jumamosi.Alisema kwa kuwa na moyo wa kujitolea vijana wataongeza hamasa na kuthaminiwa na jamii kwani watakuwa wanatatua matatizo yao. 

    Pamoja na kutoa wito huo pia amewataka vijana ifikapo desemba 9 wajitokeze kwa wingi katika kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli ya kujitolea kufanya usafi.Alisema jamii ina matatizo mengi katika sekta ya elimu, hifadhi ya mazingira na ujenzi huku ikiwa na wahitimu wa vyuoni wengi wanaoweza kujitolea kubadili mazingira na kuchukua nafasi ya kufundisha wanafunzi wanaokosa walimu. 
    Aidha alisema kwa kujitolea katika kazi hizo vijana watakuwa wanajenga pia uzoefu na utaalamu unaotakiwa katika ajira mbalimbali zikiwemo za kujiajiri. 

    Alisema kitendo cha kukaa kimya wakati wamemaliza masomo na mafunzo yao bila kutumia ujuzi wao kwa jamii wakisubiri kuajiriwa hakuwasaidii kuwanoa na pia kuwajenga katika moyo wa kujitolea kujenga taifa.Pamoja na kuwataka vijana kujitoa katika kazi za ujenzi wa taifa kwa ajili ya kujenga uzoefu na pia kujinoa kitaalamu amewataka wananchi kuthamini vijana hao kwa kuwasaidia kufanikisha kujitoa kwao kwa taifa katika shughuli mbalimbali. 

    Aidha alisema katika mstari huo huo ni vyema wanafunzi wanapotaka mafunzo kwa vitendo kuhakikishiwa mazoezi hayo ili wawe watu wenye manufaa katika jamii.Katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utalii na kushirikisha mashirika ya kujitolea yaliyopo nchini vijana wameelezwa maana na umuhimu wa kujitolea.

   Ofisa Mtendaji wa VSO, Dk Philip Goodwin aliwataka vijana wasitangulize fedha katika kujitolea kwao kwani kwa kufanya hivyo hawataweza kujipatia hamasa inayoambatana na umuhimu wa kujitolea.Aidha alisema kwamba kwa sasa vijana wana sauti kuliko zamani na hivyo upo umuhimu mkubwa wa kutambua kwamba wao ndio chachu ya maendeleo na wasipofanyia kazi hawataweza kuleta mabadiliko yanayotakiwa. 

    Alihimiza kuwapo kwa moyo wa kujitolea wakati wote kwa kuwa ndio jibu la maendeleo yao ambayo anaamini kwamba hayahitaji fedha.Alisema alishawahi kukueleza jambo nchini Ethiopia wakati vijana wanasema kwamba wana mradi lakini hawawezi kuutekeleza kwa sababu hawana fedha.Aliwaambia vijana hao kwamba wanaweza kuutekeleza mradi huo kwa kuwa wao ndio nguvu kazi na wana akili. 

    Naye Mkuu wa DFID Tanzania, Vel Gnanendran aliwapongeza vijana kwa kufanya vyema katika kuhudumia jamii na kusema shughuli za kujitolea ni sehemu ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza duniani kote.Alisema ni kutokana na moyo wa kujitolea Tanzania inaweza kuhifadhi wakimbizi kutoka maeneo mengine kama Burundi na kusema anaheshimu sana maamuzi hayo.Anasema inafaa vijana wakajitolea kuhakikisha kwamba maeneo yaow anayoishi yanakuwa na nisati inayojali mazingira na hilo linawezekana kutokana na uwapo wa teknolojia na vijana kuwa na uwezo wa kutenda. 

    Naye Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini Awa Dabo akitoa salamu za Umoja wa Mataifa katika siku ya kujitolea duniani alisema kwamba hali ya baadae ya dunia inategemea vijana na kusema wao ndio chachu lazima waione hali ya sasa na kujikita kuleta mabadiliko yenye tija.Tanzania yenye vijana milioni 16.2 wanaweza kuleta mabadiliko makubwa kama watajitolea kufanikisha mipango mingi ambayo ipo katika jamii. 
    Washiriki wa hafla hiyo katika michango yao walitaka vijana kubadili mitazamo ili watambua kwamba mabadiliko katika mambo mbalimbali inawezekana kwa kushiriki katika shughuli za kujitolea ili kujenga uzoefu na uitaalamu wa kitu wanachokishughulikia.Aidha wametakiwa kuachana na nadharia kwamba kila kitu lazima apatiwe fedha.Vijana hao pia walitaka kuwepo na mfumo wa shughuli za kujitolea ili ionekane kwamba hata serikali inatambua uwapo kwa aina hiyo ya utendaji. 
    Sherehe hizo kubwa za siku ya kimataifa ya kujitolea ya Umoja wa Mataifa imelenga kuleta ushawishi wa kujitolea miongoni mwa vijana kwa ajili ya kutengeneza mahusiano, kukuza utaalamu na pia kujenga uzoefu.Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo alisema shughuli zakujitolea za Umoja wa Mataifa zilianza nchini tangu mwaka 1974 wakati Umoja wa Mataifa ulipozindua rasmi program hiyo.Kundi la watu wanaojitolea lipo katika miradi mbalimbali ya kiserikali na binafsi yenye lengo la kusaidia wananchi kukabiliana na umaskini, utunzaji wa mazingira na mapambano dhidi ya magonjwa ya UKIMWI.Aidha UN na serikali ya Tanzania kwa sasa inafanya taratibu ya kuragibisha kujitolea na pia kutoa nafasi hiyo katika sekta mbalimbali.

  0 0


  Mwenyekiti wa Bodi ya Wataalamu wa Manunuzi na Ugavi nchini(PSPTB)Dk Hellen Bandiho akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Wataalamu unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa AICC jijini Arusha na kusisitiza miiko ya uadilifu katika manunuzi ya umma na sekta binafsi.
  Mjumbe wa Bodi ya Wataalamu wa Manunuzi na Ugavi nchini(PSPTB)Ahmed Kilima akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Wataalamu unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa AICC jijini Arusha.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Manunuzi nchini(PSPTB)Dk Clemence Tesha akizungumza jambo na wajumbe wa mkutano wa mwaka wa Wataalamu wa taaluma ya Manunuzi na Ugavi unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa AICC jijini Arusha na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka mikoa mbalimbali nchini na wageni kutoka nchi jirani.
  Wajumbe wakiwa kwenye ukumbi wa Simba
  Wajumbe wa mkutano ambao ni wana taaluma ya Manunuzi na Ugavi wakifatilia mada kwenye mkutano huo leo.


  Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa Manunuzi na Ugavi wakifatilia mada kwenye mkutano huo leo.
  Wajumbe wa mkutano wa mwaka wa PSPTB

  Mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB,Dk Charles Kimei(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa fani Manunuzi na Ugavi nchini baada ya kufungua mkutano wa mwaka ambao amesisitiza umuhimu wa kufanya manunuzi sahihi yenye lengo la kuokoa fedha za umma.
  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Dila Africa, Jumba Dickson, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ufugaji wa sungura unaweza ukawasaidia wakulima katika kujiongezea kipato kwa mbali na kuuza nyama yake lakini pia wana uwezo wa kuuza kinyesi, mkojo pamoja na ngozi yake,katika ziara ya mafunzo kuhusu mradi huo katika eneo la Kivungwi kata ya Vigwaza, Mkoa wa Pwani.
    Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Dila Africa, Jumba Dickson,akiwaonesha waandishi moja ya sungura wanaopatikana katika shamba hilo, kulia ni Mjasiriamali na mfugaji wa sungura hao, Gladness Nyange, katika ziara ya mafunzo kuhusu mradi huo katika eneo la Kivungwi kata ya Vigwaza, Mkoa wa Pwani.
   Sehemu ya mabanda ya kufugia Sungura hao.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Dila Africa, Jumba akifafanu jambo kwa Wandishi wa habari  katika ziara ya mafunzo  kuhusu mradi  huo  katika eneo la Kivungwi kata ya Vigwaza, Mkoa wa Pwani.
   Picha na Emmanuel Massaka waGlobu ya jamii

  WATANZANIA wameshauriwa kujihusisha na ufugaji wa sungura ili waweze kujiongezea kipato kutokana na mnyama huyo kuwa na faida nyingi.


  Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Dila Africa, Jumba Dickson wakati akizungumza na waandishi wa habari waliokuwa katika ziara ya mafunzo kuhusu mradi huo jana katika eneo la Kivungwi kata ya Vigwaza, Mkoani Pwani.

  Dickson alisema, ufugaji wa sungura unaweza utawanufaisha wakulima katika kujiongezea kipato  mbali na kuuza nyama yake wana uwezo wa kuuza kinyesi, mkojo pamoja na ngozi yake

  “Tunawafundisha wakulima jinsi ya kufuga sungura ili waweze kunufaika, lakini wanaweza kujiuliza ni wapi wanaweza kuwauza wakishafikia hatua ya kuuzwa, sisi tunawapa soko kwa hiyo kikubwa kwa mkulima ni kufuga tu,” Dickson alisema.

  Alisema kampuni yake ina mashamba ya sungura hivyo wanapoingia mkataba na wakulima wanaohitaji kufuga wanakubaliana mambo mbalimbali ikiwemo kuwatafutia masoko ambapo wao wenyewe wananunua sungura hao. 

  Alisema mbali na faida ya kuuza nyama yake lakini pia wanaweza kuuza kinyesi, mkojo pamoja na ngozi yake.                                                                                  

  Naye Mjasiriamali na mfugaji wa sungura hao, Gladness Nyange alisema, kuna umuhimu wa kinamama  kutumia fursa ya ufugaji sungura ili kumudu kuwasomesha watoto wao badala ya kuwategemea waume zao.

  Alisema licha ya kuwa sungura hao wanahitaji uangalizi wa hali ya juu katika kuwafuga lakini amekuwa akihakikisha kuwa waishi katika mazingira mazuri ili waweze kumpa faida.

  “Huu ufugaji kwa kuwa ni mpya watu, wengi wanaweza kujiuliza inakuwaje au masoko watapata wapi...lakini mimi nilipoanza kufuga niliingia mkataba na hii kampuni na wao walinipa masoko ina maana kwa kila sungura wa kilo nne nauza kwa Sh 40,000,” Nyange alisema.

  Nyange alishauri wajasiriamali na hasa wanawake kujiingiza katika ufugaji huo ili waweze kufanya mambo yao mbalimbali bila kuwategemea akinababa ambao wakati mwingine wanakuwa na majukumu memgi.

  0 0

  MS1Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kinondoni jijjini Dar es salaam wakati akitambulisha ujio wa mwimbaji wa muziki wa injili Rebecca Malope kutoka Nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya kutumbuiza kwenye tamasha la Kushukuru linalotarajiwa kufanyika Desemba 25 kwenye uukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam , kulia ni Mratibu Tamasha la Kushukuru masuala ya usalama Bw. Hamisi Pembe.
  MS2 
  Mratibu Tamasja la Kushukuru masuala ya usalama Bw. Hamisi Pembe akifafanua jambo kuhusu usalama wa mashabiki wa muziki wa injili pamoja na mali zao wakati wa tamasha hilo, kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama.

  MWIMBAJI nguli wa muziki  wa Injili barani Afrika, Rebecca Malope ambaye ni raia wa Afrika Kusini anatarajia kuongeza nguvu katika Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama muimbaji huyo atakuwa jukwaa moja na wenzake Sarah K wa Kenya  na Ephraim Sekeleti  wa Zambia ambao watafikisha shukrani za Watanzania baada ya kufanya uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu, uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

  Msama alisema Kamati yake inaendelea na mchakato wa kufanikisha tamasha hilo ambalo ni muendelezo wa Tamasha la Amani lililofanyika Oktoba 4 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Aidha Msama alisema Watanzania walichukilie tamasha hilo kama sehemu ya kurudisha shukrani kwa Mungu baada ya kutupitisha katika kipindi kigumu cha uchaguzi Mkuu ambao ulifanyika kwa amani na utulivu ingawa kulikuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani.


  Msama alisema waimbaji wa Tanzania watakaosindikiza tamasha hilo ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Joshua Mlelwa, Kwaya ya Wakorintho wapili huku kamati ikiendelea na mchakato wa kufanikisha tamasha hilo.

  “Tumejipanga vilivyo na tamasha la Krismasi, hivyo tujiandae kupiga goti la kumrudishia Mungu Shukrani baada ya uchaguzi Mkuu ambao ulikuwa na mguso wa aina yake kutoka kwa vijana walioonesha kutaka maendeleo kutoka kwa serikali,” alisema Msama.Naye mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha hilo, Khamis Pembe aliwahakikishia Watanzania watakaohudhuria tamasha hilo ulinzi wa uhakika kupiia Jeshi la Polisi.

  0 0  kom5 
  Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo na Balozi mdogo wa China wakibadilishana hati za makabidhiano ya msaada wa dawa zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 500 katika sherehe zilizofanyika Bohari Kuu ya Madawa Maruhubi.
  kom6 
  Balozi mdogo wa China akimkabidhi Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo sehemu ya Dawa zilizotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kupitia Jimbo la Jiangsu (kati) Naibu Mkurugenzi Mkuu ambae pia ni Kamishna wa Afya na Uzazi wa Mpango wa Jimbo hilo Hong Hao. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.​
  kom1 
  Balozi mdogo wa China aliyepo Zanzibar Xie Yunliang akitoa maelezo wakati wa sherehe ya kukabidhi msaada wa dawa zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 500 zilizotolewa na  Jimbo la Jiangsu kwa ajili ya Wananchi wa Zanzibar. Sherehe hiyo ilifanyika Bohari Kuu ya Madawa  Maruhubi Mjini Zanzibar. na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
  kom2 
  Baadhi ya Madaktari wa China na waalikwa wakifuatilia sherehe ya makabidhiano ya msaada wa dawa  mbali mbali za binaadamu katika sherehe iliyofanyika Bohari Kuu ya Madawa Maruhubi.
  kom3 
  Kamishna wa Afya na Uzazi wa Mpango ambae pia ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Jimbo la Jiangsu Hong Hao akizungumza wakati wa makabidhiano ya dawa zenye thamani ya shilingi milioni 500 (kulia) Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabiti Kombo.
  kom4 
  Balozi mdogo wa China aliyepo Zanzibar Xie Yunliang na Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo wakitia saini makabidhiano ya dawa hizo zilizotolewa na Jimbo la Jiangsu.


  0 0

  index 
   Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu(kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es  Salaam kuhusu utekeleza wa Ahadi ya Uadilifu kwa Watumishi wa Umma nchini ambao ulizinduliwa Agosti Mosi mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Bw. Charles Senkondo
  Picha na Magreth Kinabo – (MAELEZO).
  ………………………………………………………………………………………………..
  Na Lilian Lundo-Maelezo
  Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma imeanza rasmi kutekeleza Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa Umma nchini ambao ulizinduliwa Agosti Mosi mwaka huu.
   
  Akiongea na vyombo vya habari leo, Katibu Mkuu Hab Mkwizu amesema utekelezaji huo umeanza rasmi Disemba, 2015 ambapo kila mtumishi wa Umma ataweka saini  ya kiapo  kwa kuzingatia  taratibu zilizowekwa na  mazingira ya Taasisi husika.
   
  “Utaratibu wa Utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa Umma umetolewa kupitia waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma  Na. 2 wa mwaka 2015 kuhusu utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu kwa viongozi, watumishi wa Umma na sekta binafsi wa tarehe 1 Agosti, 2015.” Alisema Mkwizu.
   
  Mkwizu aliongezea kwa kusema, uanzishwaji wa Ahadi ya Uadilifu  ni muendelezo wa uundwaji wa vyombo vya kusimamia maadili baada ya ongezeko kubwa la ubadhirifu, utoro sehemu za kazi na kushuka kwa nidhamu katika kipindi cha miaka ya themanini na tisini.
  Alivitaja vyombo vingine ambavyo vilianzishwa kusimamia ahadi na uadilifu kuwa ni Sekretariate ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
   
  Mkwizu alivitaja vipengele ambavyo mtoa ahadi anatakiwa kuvitamka ni, kuwa mzalendo wa nchi yake na kutii Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kuhudumia Umma na watumishi wenzake kwa heshima, kutimiza wajibu wa kutoa huduma bora kwa umma, kutoa huduma bora kwa usawa kwa watu wote na kutofanya ubaguzi wa dini, siasa, kabila, udugu, ukanda, jinsia, urafiki au hali ya mtu.
   
  Vipengele vingine ni kutumia rasilimali za Umma kwa manufaa ya Umma, kutotoa siri za Serikali au mteja kwa watu wasiohusika isipokuwa kwa maslahi ya Umma, kufanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juu, kutoomba kushawishi, kutoa wala kupokea rushwa na kutotumia madaraka kwa manufaa binafsi ya ndugu, rafiki au jamaa.
   
  Aidha, Mkwizu ametoa wito kwa waajiri wote kuhakikisha kuwa utekelezaji wa Ahadi na Uadilifu unakamilika  ifikapo tarehe 31/12/2015 na kuwasilisha Ofisi ya Rais – UTUMISHI kabla ya tarehe 25/02/2016 na utekelezaji wake kuwa kila ifikapo Juni 30 ya kila mwaka. Fomu za Ahadi ya Uadilifu zinapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais – UTUMISHI yenye anwani www.utumishi.go.tz.

  0 0

  TC3 
  Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu matumizi ya mashine mpya ya X-ray ya digitali.  Dk Lwakatare amesema mashine hiyo ina uwezo wa kupiga picha na kutumwa nje ya nchi kwa ajili ya ushauri wa kitaalamu zaidi. Mashine hiyo haihitaji chumba cha kusafishia picha wala dawa za kusafishia.
  TC4 
  Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akitoa maelezo kuhusu idadi ya wagonjwa waliopata huduma ya kipimo cha CT Scan baada ya mashine hiyo kukamilika.
  TC1 
  Pichani ni misaada ya shuka 200, neti 150 na Televisheni nne ikipokelewa leo  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
  TC2 
  Pichani ni misaada ya shuka 200, neti 150 na Televisheni nne ikipokelewa leo  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
  ………………………………………………………………………………
  Hospitali ya Taifa  Muhimbili (MNH) imepata mashine mpya na ya kisasa ya Digital X-ray ambayo wataalamu wake hawatalazimika kutumia filamu kusafisha picha kama ilivyozoeleka katika  mashine za kawaida.
   
  Mashine hiyo imegharimu Dola 200,000 za Marekani ambazo zimetolewa na serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii  ambayo ina uwezo wa kusafirisha picha nje ya nchi ili kupata ushauri wa kitaalamu.
   
  Akilelezea kuhusu maendeleo ya mashine ya MRI na CT-SCAN  , Mkuu wa Idara ya Mionzi wa MNH,  Dk Florah  Lwakatare amesema matengenezo ya mashine hizo  yamekamilika na kwamba hadi sasa wagonjwa 148 wamepimwa  kwa kutumia mashine ya MRI , wakati wagonjwa 304 wamepimwa kwa kutumia CT-SCAN . 
   
  Katika hatua nyingine Hospitali ya Taifa Muhimbili leo imepokea msaada wa mashuka 200, vyandarua 150 ,  Televisheni nne , Decoder 4 pamoja  na Tv Stand 4.
   
  Akikabidhi msaada huo ambao umetolewa na Kampuni ya Mr. Uk Electronics Limited ya Dar essalaam, mwakilishi wa kampuni hiyo    John Solomon   ametoa wito kwa jamii kuwa na moyo wakujitolea na kushirikiana na serikali katika kuboresha huduma mbalimbali za jamii ikiwemo  huduma za afya .

  0 0

  dr1 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd,Abeid Juma Ali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba,kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar,hafla ya kiapo  ilifanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,{Picha na Ikulu}
  dr2 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd,Ali Khamis Juma  kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha kabla alikuwa Naibu katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar,hafla ya kiapo hicho ilifanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,{Picha na Ikulu}
  dr3 
  Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba Nd,Abeid Juma Alina Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Nd,Ali Khamis Juma leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.{Picha na Ikulu}
  dr4 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu mpya wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba Nd,Abeid Juma Ali (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Nd,Ali Khamis Juma (kulia) baada ya kuwaapisha kushika nyadhifa hizo leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.{Picha na Ikulu}

  0 0


  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akitoa nasaa zake kwa Vijana wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kujitolea katika taasisi mbalimbali hapa nchini Tanzania wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea Duniani ambapo Tanzania yamefanyika jijini Dar. (Picha zote na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog).
  Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo akitoa historia ya kujitolea pamoja na kuwasisitiza vijana kuwa na moyo wa kujitolea katika jamii ili kutengeneza msingi mzuri wa chini.
  Mmoja wa vijana wanaojitolea Fatma Mohammed akieleza changamoto anazozipata kama mtoto wa kike kwa kipindi chake chone anapokuwa anajitolea kwenye mashirika mbalimbali.
  Kikundi kutoka kwa vijana wanaojitolea wakitoa burudani.
  Mkuu wa DFID Tanzania, Vel Gnanendran akitoa hamasa kwa vijana wanaojitolea wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea.
  Vijana wakifuatilia kwa makini kinachozungumzwa kutoka meza kuu wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea.
  Ofisa Mtendaji wa VSO, Dk Philip Goodwin akizungumza kambo wakati wa maadhimisho ya siuku ya kujitolea yaliyofanyika jijini Dar
  Baadhi ya vijana waliohitimu masomo ya Elimu ya Juu wakitoa ufafanuzi kuhusu changamoto za ajira wanazokutana nazo mara baada ya kuhitimu vyuo hadi kupelekea kufanyakazi za kujitolea ili kuweza kufanikisha malengo yao waliyojiwekea.DSC_0115
  Vijana wanaojishughulisha na shughuli za kujitolea katika taasisi mbalimbali hapa nchini Tanzania wakiwa wameshika baadhi ya malengo 17 ya maendeleo endelevu 17.
  Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na Vijana wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kujitolea katika taasisi mbalimbali hapa nchini Tanzania. 

    Na Mwandishi wetu
  KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel wamewataka vijana kuwa na moyo wa ujasirimali kwa kuelewa umuhimu wa kujitolea.Ole Gabriel alitoa wito huo mwishoni mwa juma wakati akizungumza na vijana kwenye siku ya kujitolea (International Volunteers Day) iliyoadhimishwa kitaifa nchini Ijumaa badala ya Jumamosi.Alisema kwa kuwa na moyo wa kujitolea vijana wataongeza hamasa na kuthaminiwa na jamii kwani watakuwa wanatatua matatizo yao. 

    Pamoja na kutoa wito huo pia amewataka vijana ifikapo desemba 9 wajitokeze kwa wingi katika kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli ya kujitolea kufanya usafi.Alisema jamii ina matatizo mengi katika sekta ya elimu, hifadhi ya mazingira na ujenzi huku ikiwa na wahitimu wa vyuoni wengi wanaoweza kujitolea kubadili mazingira na kuchukua nafasi ya kufundisha wanafunzi wanaokosa walimu. 
    Aidha alisema kwa kujitolea katika kazi hizo vijana watakuwa wanajenga pia uzoefu na utaalamu unaotakiwa katika ajira mbalimbali zikiwemo za kujiajiri. 

    Alisema kitendo cha kukaa kimya wakati wamemaliza masomo na mafunzo yao bila kutumia ujuzi wao kwa jamii wakisubiri kuajiriwa hakuwasaidii kuwanoa na pia kuwajenga katika moyo wa kujitolea kujenga taifa.Pamoja na kuwataka vijana kujitoa katika kazi za ujenzi wa taifa kwa ajili ya kujenga uzoefu na pia kujinoa kitaalamu amewataka wananchi kuthamini vijana hao kwa kuwasaidia kufanikisha kujitoa kwao kwa taifa katika shughuli mbalimbali. 

    Aidha alisema katika mstari huo huo ni vyema wanafunzi wanapotaka mafunzo kwa vitendo kuhakikishiwa mazoezi hayo ili wawe watu wenye manufaa katika jamii.Katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utalii na kushirikisha mashirika ya kujitolea yaliyopo nchini vijana wameelezwa maana na umuhimu wa kujitolea.

   Ofisa Mtendaji wa VSO, Dk Philip Goodwin aliwataka vijana wasitangulize fedha katika kujitolea kwao kwani kwa kufanya hivyo hawataweza kujipatia hamasa inayoambatana na umuhimu wa kujitolea.Aidha alisema kwamba kwa sasa vijana wana sauti kuliko zamani na hivyo upo umuhimu mkubwa wa kutambua kwamba wao ndio chachu ya maendeleo na wasipofanyia kazi hawataweza kuleta mabadiliko yanayotakiwa. 

    Alihimiza kuwapo kwa moyo wa kujitolea wakati wote kwa kuwa ndio jibu la maendeleo yao ambayo anaamini kwamba hayahitaji fedha.Alisema alishawahi kukueleza jambo nchini Ethiopia wakati vijana wanasema kwamba wana mradi lakini hawawezi kuutekeleza kwa sababu hawana fedha.Aliwaambia vijana hao kwamba wanaweza kuutekeleza mradi huo kwa kuwa wao ndio nguvu kazi na wana akili. 

    Naye Mkuu wa DFID Tanzania, Vel Gnanendran aliwapongeza vijana kwa kufanya vyema katika kuhudumia jamii na kusema shughuli za kujitolea ni sehemu ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza duniani kote.Alisema ni kutokana na moyo wa kujitolea Tanzania inaweza kuhifadhi wakimbizi kutoka maeneo mengine kama Burundi na kusema anaheshimu sana maamuzi hayo.Anasema inafaa vijana wakajitolea kuhakikisha kwamba maeneo yaow anayoishi yanakuwa na nisati inayojali mazingira na hilo linawezekana kutokana na uwapo wa teknolojia na vijana kuwa na uwezo wa kutenda. 

    Naye Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini Awa Dabo akitoa salamu za Umoja wa Mataifa katika siku ya kujitolea duniani alisema kwamba hali ya baadae ya dunia inategemea vijana na kusema wao ndio chachu lazima waione hali ya sasa na kujikita kuleta mabadiliko yenye tija.Tanzania yenye vijana milioni 16.2 wanaweza kuleta mabadiliko makubwa kama watajitolea kufanikisha mipango mingi ambayo ipo katika jamii. 
    Washiriki wa hafla hiyo katika michango yao walitaka vijana kubadili mitazamo ili watambua kwamba mabadiliko katika mambo mbalimbali inawezekana kwa kushiriki katika shughuli za kujitolea ili kujenga uzoefu na uitaalamu wa kitu wanachokishughulikia.Aidha wametakiwa kuachana na nadharia kwamba kila kitu lazima apatiwe fedha.Vijana hao pia walitaka kuwepo na mfumo wa shughuli za kujitolea ili ionekane kwamba hata serikali inatambua uwapo kwa aina hiyo ya utendaji. 
    Sherehe hizo kubwa za siku ya kimataifa ya kujitolea ya Umoja wa Mataifa imelenga kuleta ushawishi wa kujitolea miongoni mwa vijana kwa ajili ya kutengeneza mahusiano, kukuza utaalamu na pia kujenga uzoefu.Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo alisema shughuli zakujitolea za Umoja wa Mataifa zilianza nchini tangu mwaka 1974 wakati Umoja wa Mataifa ulipozindua rasmi program hiyo.Kundi la watu wanaojitolea lipo katika miradi mbalimbali ya kiserikali na binafsi yenye lengo la kusaidia wananchi kukabiliana na umaskini, utunzaji wa mazingira na mapambano dhidi ya magonjwa ya UKIMWI.Aidha UN na serikali ya Tanzania kwa sasa inafanya taratibu ya kuragibisha kujitolea na pia kutoa nafasi hiyo katika sekta mbalimbali.

  0 0

  IMG_6503

  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) na ujumbe wake aliombatana nao Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (wa pili kushoto) pamoja na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (kushoto) kabla ya kuelekea kambi ya Nyarugusu walipita ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita kumsalimia pamoja na kusaini kitabu cha wageni. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
  IMG_6682
  Kuni zikitumika kupikia chungu cha Maharage kambini hapo.
  IMG_6703
  Mtoto ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi akikoleza moto ulioonekana kufifia wakati akijiandalia chakula chake cha mchana kama alivyonaswa na kamera yetu.
  IMG_6710
  Moja ya familia ya Wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu wakiangalia msafara wa Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini uliotembelea kambini hapo mwishoni mwa juma.


  Na Mwandishi Wetu, Kigoma
  JUMUIYA ya Kimataifa imekumbushwa kuisaidia Tanzania katika kuhudumia wakimbizi kutoka Burundi na Kongo ambao wanaishi katika kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma.
  Kauli hiyo imetolewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakati akizungumza na waandishi wa habari mara tu baada ya kukamilisha ziara yake mkoani Kigoma.

  Alisema kwamba serikali ya Tanzania kwa miaka mingi imekuwa na moyo wa huruma wa kusaidia majirani zake kwa kuhifadhi wakimbizi na kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kuona hilo na kusaidia Tanzania kufanikisha hifadhi ya wakimbizi.

  Alisema Umoja wa Mataifa umekuwa ukishuhudia namna ambavyo serikali ya Tanzania inahudumia wakimbizi na kuridhika na hata pale ilipowapatia haki za kuwa Watanzania kwa kuwapa uraia na pia kusaidia kuwarejesha makwao wakati hali ilipokuwa njema.Hata hivyo amesema kwa sasa hali ya Burundi na Kongo si njema na hivyo Watanzania kupata tena kazi yakuhifadhi wakimbizi.
  Alisema Tanzania kwa huruma yake imetoa ardhi zaidi ili kupunguza msongamano katika kambi ya Nyarugusu na kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kusaidia kukamilisha makazi hayo mapema kabla ya mvua za masika ili wananchi hao waweze kuishi kwa amani.
  IMG_6505
  Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita akimsikiliza kwa makini Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake kabla ya kuelekea kambi ya Wakimbizi Nyarugusu.

  Alisema kambi ya Nyarugusu ni ya tatu kwa ukubwa duniani na inahifadhi zaidi ya wakimbizi 150,000 wakiwemo watoto na wanawake na wanahitaji huduma za shule, afya, maji na mengine.
  Aidha wanahitaji nishati na hali hiyo haiwezi kuwezeshwa na serikali ya Tanzania pekee kwani watakuwa wakielemewa na huruma yake na moyo wa upendo kwa majirani zake.
  “Dunia ikumbuke wema wa watanzania kwa miaka yote hii, na isaidie kuweka sawa hali ya kambi hiyo ili huduma zote muhimu za wananchi zipatikane” alisema mratibu huyo.

  Akizungumza kuhusu wajibu wa Umoja wa Mataifa, alisema mashirika yake yamekuwa yakishirikiana na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kwamba wanatoa huduma kwa wakimbizi hao na kutaka wadau duniani kusaidia mashirika hayo na serikali ya Tanzania kufanikisha mahitaji muhimu kwa wakimbizi hao hadi hali itakapokuwa shwari katika nchi zao na kurejea kuishi makwao.
  Tanzania imetoa maeneo matatu zaidi ya kupunguza msongamano katika kambi ya Nyarugusu na maeneo hayo yanahitaji huduma za msingi kama barabara, maji, vituo vya afya na shule.

  Katika ziara hiyo ambayo aliambatana na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan, pamoja na kukagua maendeleo ya kambi ya Nyarugusu pia walikagua miradi inayofadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani ILO na ile ya Shirika la Mpango wa idadi watu duniani UNFPA.

  ILO Kigoma inaendesha mafunzo ya ujasirimali kwa vijana kwa lengo la kuwawezesha kujiajiri wenyewe na kuhudumia familia zao kwa kuziwezesha kupata huduma bora za elimu na afya kutokana na kipato chao.
  IMG_6515
  Katika msafara huo walikuwepo maafisa kutoka Shirika la linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) ofisi ya Kasulu mkoani Kigoma (walioipa mgongo kamera).
  Alisema kwamba amefurahishwa na mradi huo ambao unawawezesha vijana kutambua fursa mbalimbali zilizopo na kuzitumia vyema kufanikisha maendeleo ya familia zao.
  “Naona uwezekano wa vijana hawa kujiajiri na kuziwezesha familia zao kuondokana na tatizo la kipato.. elimu hii inaweza kutanzua mambo mengi na kuondoa changamoto nyingine zinazoambatana na kukosa kipato” alisema mratibu huyo.
  Mkoa wa Kigoma una mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa yakifanya kazi mbalimbali za maendeleo na za kutoa huduma za kibinadamu kwa wakimbizi.
  Mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa yanayotekeleza miradi mbalimbali mkoani Kigoma ni pamoja na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Shirika la Afya Duniani ( WHO), Shirika la Mpango wa Uzazi (UNFPA), Shirika la Kazi la Kimataifa ( ILO), Shirika la Kuhudumia Watoto ( UNICEF), Shirika la Kuhudumia Wahamiaji ( IOM), Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika la maendeleo (UNDP).
  Akizungumza Afisa anayeshughulikia Ustawi na Usalama UNHCR, Kasulu, Bi. Zenobia Mushi, alisema shirika lake litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania na ya mkoa wa Kigoma katika kuhudumia wakimbizi kwa kuhakikisha kwamba mahitaji yao ya msingi yanapatikana.
  Naye Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu Issa Machibya alishukuru Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kuwa tayari kusaidia mkoa wake.
  “ Tunashukuru kwa mambo yanayofanywa na Umoja wa Mataifa katika dhima nzima ya ushirikiano katika kuhakikisha kwamba pengo la maskini na matajiri linazibwa na umaskini unaondolewa katika mkoa wa Kigoma.”
  IMG_6520
  Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan akipiga picha kwenye bango linaloonyesha Serikali zinazofadhili misaada kwa Wakimbizi nchini Tanzania lililopo katika ofisi za UNHCR Kasulu.
  Naye Mkuu wa wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita akizungumza kuhusu hali ya kambi ya Nyarugusu alisema kwamba hali ya kambi si nzuri na wakati msimu wa masika ukikaribia ni vyema Jumuiya ya Kimataifa ikaharakisha kukamilisha miundombinu ili kupunguza msongamano Nyarugusu.
  Serikali imetoa maeneo mengine ya Nduta yaliyoko Kibondo na na Ntendeli, Kakonko kwa ajili ya kupunguza uwingi wa watu katika kambi hiyo.
  DC huyo pia alisema kwamba kuna uharibifu mkubwa wa mazingira na lazima wadau wote washirikiane kuhakikisha kwamba mazingira yanaboreshwa pamoja na kupokea wakimbizi na kuwapa makazi.
  Alisema kambi hiyo ilipangwa kuwa na watu elfu 50 kwa miaka ya 1996 lakini sasa inaweka wakimbizi wengi zaidi.
  Aidha alisema kwamba pamoja na kupokea wakimbizi hao, inaonekana baadhi yao wameingia kufanya uhalifu na kuomba wakimbizi kushirikiana na polisi kuwataja wahalifu hao ili wadhibitiwe.
  IMG_6551
  Kuwepo kwa kundi kubwa la wakimbizi kunasababisha uharibifu wa mazingira kama inavyoonekana pichani wakimbizi wakitoka kukata kuni kwenye misitu iliyopo karibu na kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
  Aidha katika mazungumzo ya shukurani kwa namna serikali ya Kigoma inavyotoa ushirikiano kwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika miradi ya maendeleo na misaada kwa wananchi na kwa wakimbizi, Mwakilishi wa Shirika la mpango wa idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem alisema kwamba kumekuwepo na mafanikio mengi kutokana na ushirikiano huo.
  Alisema anachokiona yeye anaona hali ya baadae ya taifa la Tanzania kuwa bora zaidi kutokana na kuwapo kwa ushirikiano mzuri kati ya serikali, mashirika ya umma na kundi kubwa la vijana ambalo kwa sasa linapokea elimu mbalimbali kwa manufaa yao na ya baadae.
  “Taifa la Tanzania nusu yake ni vijana na sehemu kubwa ni chini yake, taifa hili lina hali njema kabisa ya siku za usoni kutokana na ushirikiano wenye lengo la kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na wengi” alisema Kanem.
  Anasema kwa kuangalia program zilizopo zinazotekelezwa kwa pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa na serikali anaona mafanikio ya mafunzo ya ujasiriamali na pia elimu inayotolewa kwa watu kwa malengo ya kufanikisha maendeleo.
  IMG_7365
  Alisema UNFPA imefurahishwa sana namna mafunzo yanavyoendeshwa kwa vijana mafunzo ambayo yanaleta mshikamano wa pekee katika kufanikisha ustawi wa jamii na taifa kwa jumla.
  Aidha alifurahi kuona kwamba wanawake wanashiriki katika kutoa elimu hivyo kuingiza sauti katika mafanikio ya jamii na uongezaji wa uelewa miongoni mwa jamii.
  Mratibu huyo Mkazi wa UN Tanzania, Alvaro Rodriguez na timu yake wamerejea Dar es Salaam baada ya ziara ndefu kuangalia miradi ya Umoja wa Mataifa inavyoleta tija na ufanisi wa maisha katika jamii.
  Mratibu huyo alitembelea mikoa ya Manyara, Singida, Tabora na Kigoma.
  Katika ziara yake alioneshwa kufurahishwa na miradi hiyo inavyobadili jamii husika na kusema kwamba umoja huo utaendelea kufadhili miradi ya maendeleo nchini Tanzania.
  IMG_6558IMG_6601
  Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile (kulia) akielezea changamoto mbalimbali zinazowakabili kambini hapo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) na ujumbe wake aliombatana nao Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (wa pili kushoto) pamoja na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (kushoto) kabla ya kutembelea makazi ya wakimbizi hao.
  IMG_6608
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (kulia) na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan wakirekodi mambo muhimu wakati wa kupokea taarifa ya maendeleo ya kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu kutoka kwa Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile (hayupo pichani).
  IMG_6624
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem akizungumza jambo kwenye mkutano wa kupokea taarifa ya kambi hiyo.
  IMG_6632
  Kutoka kushoto ni Afisa mahusiano wa UNHCR, Ofisi ya Kasulu, Agnes Mwangoka, Mshauri na Mtaalum wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Hoyce Temu, Mwandishi wa Habari, Prosper Kwigize pamoja na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan wakielekea kwenye kambi za Wakimbizi baada ya kupokea taarifa.
  IMG_6664
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem wakikagua ndani ya mahema wanakoishi Wakimbizi wapya wanaoendelea kuwasili katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
  IMG_6668
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem wakiuliza jambo kwa Ofisa Mtafiti Mshirikishi wa ofisi za UNHCR, Kasulu, Mariam Khokhar walipotembelea ndani ya mahema wanakoishi Wakimbizi wapya wanaoendelea kuwasili katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile.
  IMG_6659
  Eneo la mahema ya kulalia familia za Wakimbizi wapya wanaoendelea kuwasili katika kambi ya Nyarugusu.
  IMG_6661
  Mmoja wa Wakimbizi akiwa na mwanae nje ya chumba chake na mwanae katika kambi ya Nyarugusu.

  IMG_6725
  Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan akipozi na moja ya familia katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu.
  IMG_6732
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisalimiana na Rais wa kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, Bi. Abilola Angelique wakati wa ziara yake ya kutembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.Kwa matukio zaidi ya picha bofya link hii

  0 0


  * Atengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu TPA

  * Amsimamisha kazi Katibu Mkuu Uchukuzi

  * Waziri Mkuu awasimamisha kazi watumishi wengine 13 wa bandari

  RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amevunja Bodi ya Mamlaka ya Bandari (TPA) na kutengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari, Prof. Joseph Msambichaka pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari, Bw. Awadhi Massawe.

  Dkt. Magufuli pia ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaban Mwinjaka kuanzia leo (Jumatatu, Desemba 7, 2015), na kwamba atapangiwa kazi nyingine.

  Akitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika leo ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hatua hizo zimechukuliwa kufuatia ziara mbili za kushtukiza alizozifanya katika mamlaka ya bandari Novemba 27 na Desemba 3, mwaka huu.

  Waziri Mkuu amesema Rais Magufuli amevunja bodi hiyo na kutengua uteuzi wa viongozi hao kutokana na utendaji mbovu wa muda mrefu wa Mamlaka ya Bandari na kwa kitendo cha viongozi hao kutochukua hatua kwenye vyanzo.

  Pia alisema Katibu Mkuu amesimamishwa kazi kwa sababu ya kutosimamia kwa makini mashirika mawili ya Bandari na Reli ambayo yako chini ya wizara yake ambako yeye mwenyewe alizuru Shirika la Reli (TRL) Desemba 3, 2015 na kukuta kuna ubadhirifu wa sh. bilioni 16.5/-.

  “Tarehe 3 Desemba mwaka huu nilifanya ziara ya kushtukiza pale TRL nikakuta wametumia visivyo sh. bilioni 13.5/- walizopewa na Serikali. Pia nilikuta wamekopa sh. bilioni 3/- kutoka benki ya TIB lakini nazo wamezitumia nje ya utaratibu. Fedha hizi zilikuwa ni za kusaidia kuboresha miradi ya shirika lakini wao wamezitumia visivyo. Uchunguzi bado unaendelea,” alisema Waziri Mkuu.

  Wakati huo huo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi kuanzia leo viongozi watano wa sekta zilizotoa ruhusa ya makontena kutoka ndani ya bandari pamoja na watumishi wanane wa bandari kavu ambao walihusika na ukwepaji kwa makontena 2,387.

  “Viongozi hawa hawakuwemo kwenye ripoti ya ukaguzi lakini ni wahusika wakuu. Hawa ndiyo waliotoa ruhusa ili makontena yaende kwenye ICDs. Nao ni aliyekuwa Meneja Mapato ambaye kwa sasa amehamishiwa Makao Makuu kitengo cha Fedha, Bw. Shaban Mngazija; aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Mkuu wa Bandari Kavu (ICD) – ambaye amehamishiwa Makao Makuu kwa Naibu Mkurugenzi Co-operate Services, Bw. Rajab Mdoe; Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Bw. Ibin Masoud; na Meneja Bandari Msaidizi – Fedha, Bi. Apolonia Mosha

  Pia amewasimamisha kazi wasimamizi wanane wa Bandari Kavu (ICDs) ambao ni Happygod Naftari, Juma Zaar, Steven Naftari Mtui, Titi Ligalwike, Lydia Prosper Kimaro, Mkango Alli, John Elisante na James Kimwomwa ambaye alihamishiwa Mwanza lakini kuanzia sasa anasimamishwa kazi huko huko aliko.

  “Bila wao kuidhinisha hakuna kontena linaweza kutoka au kwenda kokote. Watumishi wote hao wawe chini ya ulinzi na waisaidie polisi kupata taarifa hayo makontena ni ya nani na yana thamani gani,” Waziri Mkuu alisema.

  Waziri Mkuu Majaliwa aliwaeleza waandishi wa habari kwamba Desemba 3, mwaka huu aliamua kurudi tena bandarini kufuatilia na kuangalia hatua ya udhibiti wa upitishaji wa bidhaa mbalimbali kinyume cha utaratibu. “Ziara yangu ilinipitisha hatua zote za upitishaji mizigo ambazo pia kwa mujibu wa Taarifa ya Ukaguzi wa Ndani ya tarehe 30 Julai 2015, Mamlaka ya Bandari iligundulika kuwepo kwa mianya mingi ya ukwepaji kodi ikiwemo makotena 2,387 yaliyopitishwa kati ya Machi – Septemba 2014 kinyume cha utaratibu”.

  “Vitendo hivi vinaonyesha kuwa bandari yetu hupitisha makontena mengi bila ya kulipiwa kodi na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa. Serikali haitavumilia kuona watu wachache au kikundi chochote kilichojipanga kuhujumu mifumo au kuiibia Serikali kwa namna yoyote ile kwa manufaa ya wachache kwani bandari ni eneo muhimu ambalo likisimamiwa vizuri, linaweza kukusanya fedha nyingi na kuchangia Pato la Taifa,” alisema.

  Desemba 3, mwaka huu, Waziri Mkuu alimpa saa tatu tu Kaimu Meneja wa Bandari, Bw. Hebel Mhanga amletee ofisini majina ya watumishi wote waliohusika na ukwepaji kodi huo. Pia alimpa Meneja huyo wiki moja kuhakikisha kuwa mamlaka hiyo inabadilisha mfumo wa utozaji malipo kutoka kwenye billing system na badala yake kuweka mfumo wa malipo wa kielektroniki (e-payment). Mwisho wa kukamilisha zoezi hilo ni Desemba 11, 2015.


  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA WAZIRI MKUU,

  2 MTAA WA MAGOGONI,

  S. L. P. 3021,

  11410 DAR ES SALAAM

  JUMATATU, DESEMBA 7, 2015.

  0 0

  NA BASHIR YAKUB .
  BIASHARA  hufanywa kwa mitindo ya aina nyingi kutegemea na mahitaji ya wahusika. Unaweza kufanya biashara kwa mtindo wa kampuni, unaweza kufanya biashara kwa mtindo wa mtu binafsi, lakini pia unaweza kufanya biashara kwa mtindo wa shirika ( firm)/ubia. Mitindo hii yote inatofautiana kiutendaji, kifaida na kiuwajibikaji (liability). 

  Kuhusu kampuni tumeeleza mara nyingi faida zake, aina zake, masuala ya hisa, mpaka namna ya kuunda kampuni, ada zinazostahili na kila kitu. Pia yapo makala yaliyoeleza biashara binafsi hasara na faida zake. Leo katika makala haya tutapata kuona biashara ya shirika (firm)/ubia . Tukumbuke kuwa haya yote ni mazao ya sheria na hivyo huwa tunayatizama kwa mtazamo wa sheria.

  Sheria imeeleza kwa mapana kabisa aina zote hizi za biashara ili kuepusha migongano baina ya wahusika. Sura ya 345 ya sheria ya mikataba iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 ndiyo inayozungumzia shirika/ubia kama tutakavyoona.

  1.SHIRIKA/UBIA NI NINI.
  Shirika/Ubia ni uhusiano uliopo baina ya watu wanaofanya biashara ya faida kwa pamoja . Kwa hiyo ili ubia uwepo ni lazima watu wawili au zaidi waungane na waamue kufanya biashara kwa pamoja. Hii ni kwa mujibu kifungu cha 190 cha sheria ya mikataba. Kuungana huku ili kufanya biashara sio kuunda kampuni. 

  Ni kuungana ambako hakuhusishi kampuni lakini kunakotambulika kisheria. Muungano wa kufanya biashara kwa pamoja ndio ubia.
  Watu walioingia ubia kwa umoja wao wanaitwa shirika ( firm). Kwa hiyo shirika na ubia humaanisha kitu kimoja na ndio maana katika makala maneno haya yanatumika pamoja. Na jina wanalotumia wabia linaitwa jina la shirika ( firm name). 

  Mifano ni mingi ila mojawapo ni yale mashirika ya wanasheria yaitwayo law firm, au ya wahasibu yaitwayo accountant firm na mengine mengi. Lakini hata katika biashara za kawaida za uuzaji wa bidhaa na mengineyo nako ubia hufanyika.

  2. TOFAUTI YA SHIRIKA UBIA (PARTNERSHIP FIRM ) NA KAMPUNI (COMPANY).
  Tofauti ni nyingi ila hizi ni baadhi :
  ( a ) Katika shirika (firm) ikiwa kuna mkopo umekopwa na shirika kwa ajili ya biashara fulani basi wanashirika wote wanawajibika kwa deni hilo kila mtu mmoja mmoja kwa nafasi yake. Na ikiwa shirika litashindwa kulipa basi  mali binafsi za kila mmoja ya washirika zinaweza kukamatwa kulipia deni hilo. Hii haipo kwenye kampuni. KatIka kampuni haiwezi kutumika mali ya mtu binafsi mwanahisa kufidia deni ambalo kampuni imeshindwa kulipa hasa kama mali hiyo haikutumika kama rehani. Ni mali ya kampuni tu itakayotumika.

  ( b ) Shirika linaposababisha hasara kwa mtu mwingine ambaye sio mwanashirika kwa maana ya mtu wa tatu basi wanashirika(partners) wanawajibika kufidia hasara hiyo kwa michango yao. Hii ni tofauti na kwenye kampuni ambapo wenye kampuni hawawajibiki kufidia hasara iliyosababishwa na kampuni kwa mtu ambaye si mhusika katika kampuni hiyo. Kampuni kama kampuni ndiyo inayowajibika kufidia hasara hiyo na si wenye kampuni. Mali za kampuni ndizo zitakazotumika na kama hazipo hilo ni jambo jingine. Muhimu ni kuwa mali za wenye kampuni hazitaguswa.

  ( c ) Katika ubia hakuna mtu anaweza kualikwa kuwa mbia katika shirika bila ridhaa ya wabia wote. Kila mbia ni lazima aridhie ujio wa mbia mpya. Katika kampuni hasa makampuni ya umma (public company) haihitajiki ridhaa ya wana hisa wote ili mtu mpya akubaliwe kuwa mwanahisa. 

  3. KANUNI KUU ZINAZOONGOZA SHIRIKA (FIRM).
  Kanuni kuu inayoongoza shirika ni makubaliano ya kimkataba. Kile mnachokubaliana kimkataba ndicho kinachotakiwa kutekelezwa. Kama hakuna makubaliano yoyote basi masharti yaliyo katika kifungu cha 194 cha sheria ya mikataba ndiyo yatakayotumika kama makubaliano yenu. Masharti hayo ni pamoja na kila mbia kuwa sehemu ya uongozi wa shirika, maamuzi kufanywa kwa kura za walio wengi, haki ya kukagua vitabu vya shughuli za shirika, kugawana faida kwa usawa, n.k.

  4. SHIRIKA (FIRM) HUSAJILIWA WAPI.
  Mashirika (firm) husajiliwa kwa msajili wa makampuni na biashara BRELA. Vipo vyeti maalum ambavyo hutolewa kwa ajili ya usajili baada ya ada ya usajili hulipwa. Katika makala nyingine tutaona kipi bora kibiashara kati ya shirika (firm) na kampuni ( company).

  MWANDISHI WA MAKALA HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA SERIKALI LA HABARI LEO KILA JUMANNE, GAZETI JAMHURI KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com

  0 0

  Walimbwende wakiwa tayari kufanya vitu vyao wakiwa na vivazi vya mwanamitindo nguli Asya Idarous Khamsini kwenye siku ya Mtanzania iliyofanyika siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 Seattle jimbo la Washington nchini Marekani.
  Mlimbwende akiwa kwenye kivazi kutoka kwa mwanamitindo nguli Asya Idarous Khamsini kwenye siku ya Mtanzania iliyofanyika siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 Seattle jimbo la Washington nchini Marekani.
  Kivazi chekundu kikiwa na riboni ya punda milia kikimfanya mlimbwende atabasamu jinsi gani alivyopendeza kivazi toka kwa mwanamitindo nguli Asya Idarous Khamsini kwenye siku ya Mtanzania iliyofanyika siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 Seattle jimbo la Washington nchini Marekani.
  Kivazi toka kwa mwanamitindo nguli Asya Idarous Khamsini kwenye siku ya Mtanzania iliyofanyika siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 Seattle jimbo la Washington nchini Marekani.


  0 0

  Waliokwepa kodi TRA walipa bil.8.6/-. Kigogo kiwanda cha Urafiki asimamishwa kazi. Chagonja ahamishiwa jeshi la  zimamotoSIMU.TV:  Majipu yaendelea kutumbuliwa, rais Magufuli atengua uteuzi wa vigogo. Salamu za Gwajima zamkera Dr.Slaa; https://youtu.be/S3V6HWW_o10

  SIMU.TV:  Bomoabomoa mpya yaliza mamia Dar.  Ada elekezi shule binafsi sasa ni kizungumkuti. Mkwasa aja ki vingine. Tata Africans yaandaa harambee kujikwamua. Yanga yawapotezea Wakenya , Waganda;https://youtu.be/Ft3zrHpz-Dc 

  0 0

  DSC00871
  Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Be Forward Geoffrey Mibaz akimkabidhi mshindi ambaye ni Mwalimu wa Shule ya St. Jude Mkoani Arusha aliyeambatana na familia yake,  Rasul Mngazija gari aina ya Toyota IST yenye thamani ya Sh. Milioni 12 katika promosheni ya jishindie IST iliyofanyika jana jijini Arusha iliyoendeshwa na kampuni ya uuzaji magari ya Be Forward Tawi la Tanzania
  DSC00877
  Muonekano wa Gari aina ya Toyota IST yenye thamani ya Sh. Milioni 12

  DSC00875
  Mshindi Rasul Mngazija akiwa na mkewe Hazina Msechu wakiwa na nyuso za furaha ndani ya gari aina ya IST walioshinda katika promosheni iliyokuwa ikiendeshwa na kampuni ya Be Forward Tanzania
  DSC00874
  Rasul Mngazi akiwa ndani ya gari akijaribu kuwasha huku akiwa na uso wa tabasamu
  DSC00854
  Afisa masoko kampuni ya Be Forward tawi la Arusha Gooluck Lyimo akiwa anamkabidhi mshindi documenti za gari ofisini kwao jijini Arusha jana mara baada ya kutembelea ofisi hizo

  DSC00850
  Meneja Masoko wa Kampuni ya Be Forward Geoffrey Mibaz akionyesha documenti za gari kwa waandishi wa habari pamoja na wadau waliofika jana katika promosheni hiyo ya Shinda Gari
  DSC00837
  Afisa Masoko Shufaa Kilango akiwa anatoa maelezo kwa ugeni uliotembelea ofisi zao jana jijini Arusha
  DSC00842
  Muonekano wa ndani wa ofisi za Be Forward jijini Arusha
  DSC00884
  Aliyeshika mfuko ni mkurugenzi wa jamiiblog Pamela Mollel akiwa na timu nzima ya Be Foward Arusha pamoja na mshindi wa gari IST akisindikizwa na familia yake
  DSC00887
  Familia ya Be Forward wakiwa katika picha ya pamoja na mshindi
  DSC00881
  Wafanyakazi wa Be Forward wakiwa katika nyuso za furahaaaa
  SAM_6844
  Rasul Mngazija akiongea katika halfa hiyo ambapo alisema kuwa “Sikutegemea kwanza kama ntakuwa mshindi kwani nilifika katika ofisi zao kwa ajili ya kuagiza gari nyingine,”
  SAM_6822
  Meneja Masoko wa Kampuni ya Be Forward Geoffrey Mibaz akiongea katika ofisi za Be Foward jijini Arusha

  SAM_6841
  Mwandishi wa habari  gazeti la Mwananchi na Citizen Musa Juma akiangalia zawadi alizopewa na kamapuni hyo
  SAM_6794
  Mshereheshaji wa halfa hiyo Akida ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha Radio 5 akifanya yake  katika ofisi za Be Forward jijini Arusha(Picha na 

  Pamela Mollel wa Jamiiblog Arusha)
  Mwalimu wa Shule ya St. Jude iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha Rasul Mngazija ameshinda gari aina ya Toyota IST yenye thamani ya Sh. Milioni 12 katika promosheni iliyofanyika jijini Arusha iliyoendeshwa na kampuni ya uuzaji magari ya Be Forward Tawi la Tanzania
  Akizungumza Mara baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo jana katika ofisi za kampuni hiyo Mwl. Mngazija aliyekuwa ameongozana na famlia yake kupokea zawadi hiyo aliishukuru BE Forward  kwa kumchagua kuwa mshndi katika promosheni hiyo.“Sikutegemea kwanza kama ntakuwa mshindi kwani nilifika katika ofisi zao kwa ajili ya kuagiza gari nyingine,”
  “Nikiwa hapo ndipo waliponijulisha pia kwamba kuna promosheni wanaendelea nayo kwa wateja wanaoagiza magari kupitia kwenye ofisi zao. Kwa hiyo nilijaza fomu na kuendelea kusubiria,”Mngazija aliendelea kusema kwamba kufanikiwa kuibuka mshindi wa zawadi hiyo gari kumemuongezea chachu ya kuhamasisha watu wengine zaidi kutumia huduma za kampuni hiyo kwa kuwa balozi wa Be Forward

  Kwa upande wake Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Be Forward Geoffrey Mibazalisema kwamba kampuni hiyo itaendelea kuwa karibu zaidi na jamii katika shughuli zake ikiwamo kurudisha sehemu ya faida inayopatikana.
  Alisma baada ya kufungua ofisi zao jijini Dar es Salaam sasa wamefungua katika jiji la Arusha lengo likiwa ni kuwasogezea huduma zaidi wananchi.Katika uzinduzi huo ulioambatana na kumkabidhi gari mshindi, Geofrey aliwataka watanzania na watu wengine wanaopanga kununua magari kutumia zaidi kampuni hiyo kwa ajili ya usalama wa fedha na mali zao.
  “Mtu yeyyote anayekuja kuagiza gari ofisini kwetu tunampa ushauri wa bure, wa aina gani ya gari anatakiwa kuagiza masuala ya kodi,”
  Pia aliongeza kuwa wanatoa huduma ya ushauri kwa wateja wao kabla ya kuagiza gari huku akiwataka wananchi kutumia kampuni hiyo kuagiza magari kwakuwa usalama upo wa kutosha ukilinganisha na wajanja wa mjini

older | 1 | .... | 705 | 706 | (Page 707) | 708 | 709 | .... | 1897 | newer