Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

RED AVENUE PARTY RELOADED DESEMBA 26, 2015


Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akutana na Mwenyekiti wa Kamisheni wa Umoja wa Afrika na Waziri wa Mambo ya nje wa Libya

$
0
0
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya, Mheshimiwa Mohammed Al-Dairi aliyemtembelea na kufanya nae mazungumzo jijini Johannesburg pembezoni mwa Mkutano wa China na Afrika.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne na Mjumbe Maalum wa Umoja wa Afrika nchini Comoro Leo amekutana na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Africa, Mheshimiwa Dkt. Nkosazana Dlamini Zuma kuzungumzia hail ya siasa nchini Comoro. Katika Mkutano huo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliwasilisha taarifa ya ziara maalum aliyoifanya Comoro tarehe 1 Desemba, 2015.




TGDC NA KAMPUNI YA TOSHIBA WATILIANA SAINI MKATABA WA MAELEWANO (MOU) WA UTAFUTAJI WA NISHATI YA JOTOARDHI

$
0
0
Meneja Mkuu Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe (kushoto) pamoja na Mtaalamu Mkuu toka Kampuni ya TOSHIBA Bwana Kentaro Kurahara wakiweka saini Mkataba wa wa Maelewano (MOU) wa kufanya tafiti kwa pamoja zinahusu maeneo yenye viashiria ya upatikanaji wa nishati ya jotoardhi katika Ofisi za TGDC zilizopo Jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe (kushoto) pamoja na Mtaalamu Mkuu toka Kampuni ya TOSHIBA Bwana Kentaro Kurahara wakikabidhiana Mkataba wa Maelewano (MOU) wa kufanya tafiti kwa pamoja zinahusu maeneo yenye viashiria ya upatikanaji wa nishati ya jotoardhi katika Ofisi za TGDC zilizopo Jijini Dar es Salaam.

Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
 Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC) pamoja na Kampuni ya TOSHIBA ya nchini Japan zimetiliana saini Mkataba wa Maelewano wa kufanya tafiti kwa pamoja zinahusu maeneo yenye viashiria ya upatikanaji wa nishati ya jotoardhi.

 Utiaji saini wa mkataba huo umefanyika Desemba 4, 2015 Jijini Dar es Salaam katika Ofisi za TGDC ambapo hatua hiyo itaiwezesha TGDC kuweza kupata msaada wa kitaalam ambao utaliwezesha shirika hilo kuweza kuchimba ardhini kwa lengo la kupata mvuke utakaoweza kuzalisha umeme.

 Akiongea ofisini kwake, Meneja Mkuu wa TGDC, Mhandisi Boniface Njombe amesema kuwa kupitia Serikali ya Japan hususani Shirika la Maendeleo Japan (JICA), Kampuni ya TOSHIBA watasaidia kuomba ufadhili wa Serikali yao ili kuweza kuendeleza ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme pamoja na matumizi mengine yanayoendana na nishati hiyo.

 “Katika utafiti wa nishati ya jotoardhi tunahitaji watu wenye elimu na uzoefu na ujuzi wa kutosha, miongoni mwa makubaliano ndani ya mkataba huu tuliosaini leo ni wafanyakazi wetu kadhaa kuwapeleka nchini Japan kwenye vyuo vyao ili kuweza kupata mafunzo ya darasani na kutembelea maeneo ambayo Japan wana vituo vya jotoardhi ili wapate ujuzi wa kufanya kazi na Wajapan na kutuletea ujuzi huo hapa nchini”, alisema Njombe.

 Aidha, ameeleza kuwa kupitia ushirkiano huo na Serikali ya Awamu ya Tano Japan itaendelea kuisadia Tanzania katika kuendeleza nishati ya jotoardhi kwakuwa ni nishati yenye tija katika kutimiza ndoto za Tanzania kwa kuifanya kuwa nchi yenye kipato cha kati kufikia mwaka 2020.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, na Rais Mstaafu wa awamu ya Tano, Dkt. Jakaya Kikwete, wakiangalia moja ya Ndege ya Kivita ya mfano, wakati walipotembelea Mabanda ya maonesho ya Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, uliofanyika Jijini Johannesburg Afrika ya Kusini jana.  Dkt. Jakaya Kikwete alihudhuria mkutano huo kama Rais Mstaafu mwalikwa. Mkutano huo unamalizika leo Dec 5, 2015.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika ukumbi wa mkutano wakati akijiandaa kuhutubia kwenye Mkutano mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, unaomalizika leo jijini Johannesburg Afrika ya Kusini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Rutageruka Mulamula, kabla ya kuhutubia katika Mkutano mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, unaomalizika leo jijini Johannesburg Afrika ya Kusini. Picha na OMR

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akutana na Rais wa China, atunukiwa Heshima ya Companion Award na Commonwealth Partnership for Technological Management (CPTM), aongoza ujumbe wa AU Comoro

$
0
0
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Jakaya Mrisho Kikwete akibadilishana mawazo na Rais wa China, Mheshimiwa Xi Jinping pembezoni mwa Mkutano wa Africa na China unaofanyika Johannesburg , Afrika Kusini. Waliosimama pembeni ni Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Tanzania, Rais Thomas Boni Yayi wa Benin, Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.
----------------------------------
Taasisi ya Commonwealth Partnership for Technological Management (CPTM) inayojishughulisha na kukuza ushirikiano katika nyanja ya sayansi na teknolojia kwa nchi za Jumuiya ya Madola, imemtunuku Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, heshima ya Juu ya CPTM (Companion Award) kwa kutambua mchango wake katika kuhamasisha ukuaji wa matumizi ya sayansi na teknolojia ikiwemo matumizi ya huduma za fedha kwa njia ya simu. Rais Mstaafu Kikwete, alikabidhiwa Tuzo hiyo tarehe 1 Desemba, 2015. 
Taasisi hiyo yenye makao makuu yake London ndio inayoendesha Midahalo ya Kimataifa maarufu kama Smart Partnership Dialogue. Mkutano wa mwisho wa aina hiyo ulifanyika Dar es Salaam mwaka 2013 ukiwa Na kali mbiu ya "Kutumia Teknolojia Kuchochea Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii Barani Afrika". 
Rais  Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Cheti cha Kumtunuku Yeshima ya Juu ya CPTM (Companion Award). Aliyesimama kushoto kwa Rais Mstaafu ni Dkt. Tan Sri Omar, Mwenyekiti wa Bose ya Wakurugenzi wa CPTM na pembeni yake ni Dkt. Mihaela Smith, CEO wa CPTM. Tuzo hiyo imetolewa wakati wa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPTM ambao uliambatana na maadhimisho ya Miaka 20 ya Taasisi hiyo jijini London.Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa neno la shukurani baada ya kutunukiwa tuzo ya  heshima ya Juu ya CPTM (Companion Award) wakati wa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPTM ambao uliambatana na maadhimisho ya Miaka 20 ya Taasisi hiyo jijini London.

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliteuliwa na Mama Nkosamana Dlamini Zuma kuwa Mjumbe Maalum wa AU Comoro.  Mhe. Kikwete alikwenda Moroni, Comoro tarehe 30 Novemba, 2015 kufanya mikutano na wadau wa siasa kuhusu mgogoro wa kisiasa unaonukia nchini humo kuhusu mchakato wa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utakaofanyika April, 2016


MICHANGO YA WASAMARIA WEMA YAFANIKISHA DADA JOYCE WA MBEYA KUWASILI MUHIMBILI KWA MATIBABU

$
0
0
 Dada Joyce akiwa ameketi kwa utulivu kwenye siti yake ndani ya ndege
…………………………………………………………………………………………………………
Ndugu Wasamaria wema,
Tunapenda  kutumia fursa hii kuwapa updates kuhusu dada
Joyce Mwambepo, mkaazi wa Sinde jijini Mbeya mwenye umri wa miaka 27 ambaye anaishi  na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na mwanaye mwenye umri wa miaka 4.Kwa bahati
mbaya mwezi April mwaka jana dada huyu alipata ajali ya kugongwa na gari ambalo dereva wake hakusimama kumsaidia. 
 
Ila kwa msaada wa wasamaria wema alipelekwa hospitali ya
rufaa ya mkoa wa Mbeya ambako inasemekana alikaa kwa miezi mitatu bila kupata  matibabu kwa kukosa fedha. 
Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce amevunjika miguu yote miwili,hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa Mbeya baada ya kukosa pesa za matibabu.
 
Baada ya mwanahabari Deo Kakuru wa Mbeya kumgundua na kufanya juhudi za kutoa taarifa za dada Joyce katika mitandao mbalimbali, wasamaria wengi  wa ndani na nje ya nchi  wakaguswa na kuchangia. Mungu mkubwa, kiasi kilichopatikana (kiasi cha 3.2m/-) kimewezesha dada Joyce kupelekwa Dar es salaam toka Mbeya kwa ndege ya Fast Jet Alhamisi
iliyopita na moja kwa moja kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili na
kupokelewa katika kitengo cha MOI na kupatiwa kitanda katika wodi mpya
ijulikanayo kama Wodi ya Magufuli, ghorofa ya tatu chumba namba mbili.
Cha kufurahisha ni kwamba Joyce aliweza kukaa kwenye kiti cha kusukumwa na hata kwenye ndege aliketi kama kawaida, zoezi ambalo hata yeye anasema limemsaidia kwani kwa mara ya kwanza hivi sasa ganzi miguuni inapotea taratibu na ukimgusa anahisi mguso tofauti na ilivyokuwa awali.
 
Daktari bingwa ameshaonana naye na kumpa matumaini ya kupona, hasa sehemu ya chini ya uti wa mgongo wake ambao inasemekana una matatizo yaliyopelekea kubana  mishipa ya fahamu na kufanya miguu ipooze.
Zoezi linalosubiriwa kwa sasa ni kupatiwa vipimo vya MRI ili kubaini kiufasaha tatizo lake na hatimaye kupatiwa matibabu. Zoezi hili linatarajiwa kufanyika wakati wowote kuanzia sasa.
 
Mpiganaji Deo Kakuru amesharejea Mbeya na kijiti cha kumwangalia dada Joyce amekabidhiwa Ankal ambaye anaomba Wasamaria wema waendelee kumuombea na kumsaidia kwa hali na mali dada huyu ambaye ni yatima.
Kwa bahati njema Ankal alikutana na kuongea na Msamaria mwingine aitwaye Mama Rozi ambaye  anamuuguza mama yake mzazi aliyelazwa  wodi moja na dada Joyce. Msamaria huyu amekubali kumsaidia dada Joyce kwa chakula na pia kumsaidia usafi maana hapo kitandani hawezi kuondoka.
 
Mungu kweli ni mkubwa. Dada Joyce anatabasamu na kuongea vizuri tu. Anatoa shukurani sana kwa wote waliomsaidia na wanaoendelea kumsaidia. Anasema hana cha kuwalipa ila kusema ASANTE SANA na anamwomba Mola Muumba awazidishie pale patapopungua. Ameomba anayeweza kumtembelea atafurahi sana maana hana ndugu hapa Dar es salaam.Pia
anawashukuru sana madaktari waliomhudumia vyema katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya ambao amesema hatowasahau kwa msaada wao.
 Ankal amejitolea kuendelea kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce.
 
 Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba+255 754 271266 kwa jina la Ankal.
AU mratibu-mwenza  Deo Kakuru Msimu
Pia unaweza kuwasiliana moja kwa moja na dada Joyce kwa namba
 Mpiganaji Deo Kakuru akiwa na dada Joyce ndani ya FastJet wakitoka Mbeya keuelekea Dar es salaam .
 Mpiganaji Deo Kkuru akiwa na dada Joyce mara baada ya kuwasili  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam.
 Msamaria mwema Mama Rozi akimhudumia dada Joyce akiwa kitandani kwake Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa cha MOI katika wodi ijulikanayo kama Wodi ya Magufuli ghorofa ya tatu.
 Dada Joyce akiwa wodini Moi

WALIMU WA SKULI MBALI MBALI ZA WILAYA WAPATIWA MAFUNZO YA MICHEZO NA KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA (TOC) MJINI ZANZIBAR

$
0
0
Mkufunzi wa Mafunzo ya Walimu wa Michezo wa Skuli yaliyoandaliwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Suleiman Mahmoudu Jabiri akitowa maelezo kwa washiriki katika siku ya mwisho ya mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 01 mwenzi huu.Mkurugenzi wa Idara ya Elimu mbadala na Watu wazima Mashavu Fak akifunga mafunzo ya walimu wa michezo wa Skuli katika Skuli ya Elimu Mbadala Rahaaleo Mjini Zanzibar.Mkurugenzi wa Idara ya Elimu mbadala na Watu wazima Mashavu Faki akiwakabidhi vyeti washiriki wa mafunzo yaliyoandaliwa na Kamati ya TOC katika Ukumbi wa Elimu Mbadala Rahaleo Mjini Zanzibar.


Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar

Idara ya ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imeshauriwa kuwaandalia michezo nje ya nchi walimu wa michezo wa skuli kwa lengo la kujipatia taaluma zaidi na kukukuza mechezo nchini ,

Hayo yameelezwa huko Rahaleo katika Ukumbi wa Elimu Mbadala na Watu wazima na Mkurugenzi Idaraya hiyo Zanzibar Mashavu Faki wakati akifunga mafunzo yalioandaliwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) yaliyofunguliwa tarehe 1 mwezi huu.Amesema iwapo walimu wa michezo watapatiwa mafunzo zaidi nje ya nchi wataweza kuwasomesha wanafunzi wao wa skuli na kuinua sekta ya michezo Zanzibar.

Mkurugenzi Mashavu amesema katika mwaka 2013 kulifanywa utafiti wa kimchezo na kuonekana kuwa nchi zinazoimarisha michezo maskulini ndizo zinazofanya vizuri zaidi katika masomo yao.Aidha amesema michezo huimarisha afya, kujenga upendo, udugu na uzalendo katika jamii hivyo hakuna budi kuendelezwa kwa manufaa ya wanamichezo wenyewe na Taifa kwa jumla.

Sambmba na hayo Mkurugenzi huyo amewashauri waalimu waliopata mafunzo hayo kwa kushirikiana na Idara husika kuandaa mafunzo kila baada ya miezi mitatu.Nae mkufunzi wa mafunzo hayo Suleiman Mahamoud Jabir amewataka washiriki wa mafunzo hayo kujenga moyo wa kujitolea kwani katika kufundisha mara nyingi hujitokeza matatizo mengi.

Kwa upande wao waalimu waliopata mafuzo hayo Mussa Abdulrab na Arafa Talib Omar wamesema wamejifunza mambo mengi wasioyajua na kuahidi kuwa watayafanyia kazi.Mafunzo hayo ya siku tano ya walimu wa michezo wa skuli mbali mbali za Zanzibar yameandaliwa na Kamati Tanzania.

Rebeca Malope kutikisa Diamond Tamasha la Krismasi

$
0
0
MWIMBAJI nguli wa muziki  wa Injili barani Afrika, Rebecca Malope ambaye ni raia wa Afrika Kusini anatarajia kuongeza nguvu katika Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama muimbaji huyo atakuwa jukwaa moja na wenzake Sarah K wa Kenya  na Ephraim Sekeleti  wa Zambia ambao watafikisha shukrani za Watanzania baada ya kufanya uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu, uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.Msama alisema Kamati yake inaendelea na mchakato wa kufanikisha tamasha hilo ambalo ni muendelezo wa Tamasha la Amani lililofanyika Oktoba 4 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Aidha Msama alisema Watanzania walichukilie tamasha hilo kama sehemu ya kurudisha shukrani kwa Mungu baada ya kutupitisha katika kipindi kigumu cha uchaguzi Mkuu ambao ulifanyika kwa amani na utulivu ingawa kulikuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani.

Msama alisemAa waimbaji wa Tanzania watakaosindikiza tamasha hilo ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Joshua Mlelwa, Kwaya ya Wakorintho wapili huku kamati ikiendelea na mchakato wa kufanikisha tamasha hilo. 
“Tumejipanga vilivyo na tamasha la Krismasi, hivyo tujiandae kupiga goti la kumrudishia Mungu Shukrani baada ya uchaguzi Mkuu ambao ulikuwa na mguso wa aina yake kutoka kwa vijana walioonesha kutaka maendeleo kutoka kwa serikali,” alisema Msama.Naye mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha hilo, Khamis Pembe aliwahakikishia Watanzania watakaohudhuria tamasha hilo ulinzi wa uhakika kupiia Jeshi la Polisi.

WATUMISHI WAANDAMIZI SABA WA TANESCO WAFUKUZWA KAZI KWA TUHUMA MBALIMBALI

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Felschimi Mramba akizungumza na waandishi habari juu ya mikakati mbalimbali ya uzalishaji umeme katika mazungumzo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Uzalishaji na Huduma kwa Mteja), Mhandisi Sophia Mgonja, Kushoto ni Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uzalishaji Umeme, Nazir Kachwamba, kushoto kutoka kulia ni Meneja Uhusiano Adrian Severine.
Waandishi habari wakimisikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felschimi Mramba leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SHIRIKA la Umeme nchini (Tanesco) limewafukuzisha kazi watumishi waandamizi wa Tanesco upande wa maneja na wahasibu kutokana na ubadhirifu wa fedha katika utumishi wao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Felschimi Mramba amesema kuwa shirika halitaweza kuwaacha watendaji wakawa wanafanya kazi kwa rushwa wakati wanalipwa mishahara.

Amesema wataendelea kuchukua hatua kwa watendaji wote watakabainika kufanya udanganyifu au kutoa lugha zisifaa kwa wateja na wakati mwingine kuomba fedha kwa huduma ambazo ni haki ya mwananchi kupata.

Mramba amesema Tanesco imeongeza uzalishaji wa umeme unaotumia gesi megawati 300  sawa na asilimia 115  na kufanya kuwa na umeme wa uhakika huku miradi mingi ikiendelea kufanyika.

Amesema  wanatarajia kupata megawati 240 kutoka Kinyerezi namba mbili  wakati wowote  na kufanya shirika kuwa na umeme wa uhakika.

Aidha amesema wakati wa suala miundombinu likifanyiwa kazi wananchi wawe wavumilivu wa kukatika umeme katokana na kuboresha miundombinu hiyo.

Aliongeza kuwa wanaotaka kufanya kazi na Tanesco kwa kupata nguzo lazima wazalishe nguzo zenye ubora wa kuweza kuhimili kwa muda mrefu bila kuanguka kuanguka.

VODACOM YAENDELEA KUNOGESHA SWAHILI FASHION WEEK

$
0
0
 Mwanamitindo akipita mbele ya watazamaji katika onesho la Swahili Fashion Week lililomalizika jana katika hoteli ya Sea Cliff, akiwa amevalia mavazi ya lebo ya Kibout ya mbunifu wa hapa nchini, onesho hilo limedhaminiwa na Kampuni ya simu ya Vodacom.
 Mbunifu wa mavazi wa lebo la Kibout Evamary Sospeter de Block akipita mbele ya watazamaji jana baada ya kuonesha mavazi yake katiak oneso la Swahili Fashion Week lililomalizika jana katika hoteli ya Sea Cliff chini ya udhamini wa kampuni ya simu ya Vodacom.
 Wanamitindo wakionesha vazi kutoka lebo ya Jina Langu Ni wakati wa onesho la mavazi la Swahili Fashion Week lililomalizika jana chini ya udhamini wa kampuni ya simu ya Vodacom.
 Wanamitindo wakionesha vazi la mbunifu wa mavazi Kiarasheba katika siku ya pili ya onesho la siku tatu la Swahili Fashion lililomalizika jana chini ya Udhamini wa kampuni ya simu ya Vodacom.
 Wanamitindo wakionesha mavazi ya lebo ya PSJ Couture katika siku ya pili ya onesho la mavazi la Swahili Fashion Week lililofanyika katika hoteli ya Sea Cliff chini ya udhamini wa kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania.

Wabunifu wa mavazi wanaomiliki lebo ya Bobbins & Sief wakipita baada ya kuonesha mavazi yao katika onesho la Swahili Fashion Week lililomalizika jana likiwa limedhaminiwa na kampuni ya simu ya Vodacom.

TAASISI YA SEKTA BINAFSI, BOT, BENKI YA DUNIA WAJADILI MFUMO WA MIRADI YA PPP.

$
0
0
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk Gideon Kaunda akihojiwa na waandishi wa habari katika hafla ya ufungaji wa mkutano wa siku mbili kuhusu ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya ubia kati ya sekta binafsi na ya umma (PPP), iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ulioandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), ikishirikiana  na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Benki ya Dunia.
 Mtaalamu wa uchumi kutoka Benki ya Dunia, Jeffrey Delmon (kulia) akizungumza na washiriki wa mkutano wa siku mbili kuhusu ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya ubia kati ya sekta binafsi na ya umma (PPP), uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kuandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), ikishirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Benki ya Dunia.
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk Gideon Kaunda (kulia) akizungumza katika hafla ya ufungaji wa mkutano wa siku mbili kuhusu ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya ubia kati ya sekta binafsi na ya umma (PPP), uliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ulioandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), ikishirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Benki ya Dunia. Kushoto ni Kamisha wa PPP kutoka Wizara ya Fedha, Dk. Francis Mhilu. 

 Kamishna wa Sera ya Ushirikiano wa Sekta Binafsi ya Umma (PPP) kutoka Wizara ya Fedha, Dk. Francis Mhilu (kulia) akiagana na Mtaalamu wa uchumi kutoka Benki ya Dunia, Jeffrey Delmon baada ya kumalizika kwamkutano wa siku mbili kuhusu ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya ubia sekta binafsi na ya umma (PPP), uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki uliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), ikishirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Benki ya Dunia. Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk Gideon Kaunda.
 Mmoja wa washiriki kutoka Benki ya Maendeleo, George Wandwalo (kushoto) akiuliza swali.
  Baadhi ya washiriki.
 Washiriki wakipiga picha ya kumbukumbu mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo uliokuwa ukijadili ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya ubia kati ya sekta binafsi na ya umma (PPP), uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 

WENYEVITI WA CCM MIKOA WAPONGEZA RAIS DK. JOHN MAGUFULI KWA KASI YAKE

$
0
0
 Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ramadhan Madabida akizungumza na waandishi wa habari (hayupo pichani) juu ya kazi inayofanywa na Rais Dk. John Magufuli leo jijini Dar es Salaam.
 Waandishi wa habari wakimfatilia Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ,Ramadhan Madabida leo jijni Dar es Salaam

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WENYEVITI wa Mikoa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamesema kuwa kasi ya Rais Dk. John Joseph Pombe Magufuli kwa kuwachukulia hatua watendaji wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao, wanapongeza kwa kufanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ,Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Wawenyeviti wa Mikoa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida amesema kuwa wenyeviti wanapongeza kwa hatua hizo ambazo amezifanya Rais Dk. John Magufuli.

Amesema watu walikuwa wanatoa huduma isiyo bora kwa wananchi hivyo kila mtu kwa nafasi yake afanye kazi yake kwa mujibu wa sharia

Madabida amesema kwa kasi hiyo wako tayari na maamzi yeyote ambayo anaweza kuyatoa kwa viongozi wa CCM ambao hawakuweza kufuata utaratibu.

Aidha amesema wananchi waunge juhudi ambazo Rais John Joseph Magufuli anafanya katika kuweza kila mtu aweze kuwajibika ipasavyo kuwahudumia wananchi wake.


Ameongeza kuwa Wenyeviti wataendelea kuwa pamoja na Rais katika majumu yake ya kuhakikisha nchi inakuwa na watendaji wanaojituma na kila nyakati ina dhana yake.

SPANISH CULINARY WEEKEND YA SIKU TATU YAZINDULIWA JIJINI DAR.

$
0
0
Balozi wa Hispania hapa nchini, H.E Felix Costaldes akizungumza wakati wa uzinduzi wa Spanish Culinary week ambayo imezinduliwa Ijumaa usiku  katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Habari Beach jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Balozi wa Hispania hapa nchini, H.E Felix Costaldes akikata keki kuashiria uzinduzi wa Spanish Culinary week iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Watumbuizaji wakitumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa  Spanish Culinary week jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya washiriki wakiwa katika picha ya pamoja  mara baada ya kuzindua  Spanish Culinary week jijini Dar es Salaam.

YAMOTO BENDI WAINGIA TUZO ZA KORA

$
0
0
Waimbaji wa yamoto bendi wakiwa katika picha ya pamoja.

Na Mwandishi Mwetu
WAKATI jana wakiendelea kutoa burudani katika mji wa Washington DC, Bendi ya Yamoto, imeingia katika kuwania tuzo za Kora 2016, ikiingia katika kipengele cha Most Promising Male Artist Of Africa.

Mkurugenzi wa bendi hiyo Said Fella, alisema kwanza anamshukuru Mungu vijana wake juzi usiku walikuwa na onesho lao la pili lililofanyika Washington DC na kuweza kufanya vizuri, lakini la pili kuingia katik tuzo za Kora. 

Fella ambaye ni diwani wa Kata ya Kilungule alisema ni kitu kikubwa sana kwake kwa bendi yake kuingia katika tuzo za Kimataifa.

Alisema kuingiaa kwa vijana wake katika tuzo hizo ni kitu kikubwa sana na kinazidi kuipandisha bendi yake ambayo sasa ipo nchini Marekani kwa ziara ya maonesho maalum.

"Ni kitu kikubwa sana kinazidi kutupandisha kutoka sehemu moja kwenda kwingine, tunaamini mwenyezi Mungu atatusimamia tuweze kupata kwa mashabiki wetu kuliona hili na kutuunga mkono katika kupiga kura"alisema Fella. 

Kwa upande wa ziara ya bendi yake nchini Marekani alisema vijana hao watafanya onesho la mwisho Desemba 12, katika mji wa Houston na baadae kurejea nchini kwa kazi zao nyingine. 

Alisema katika onesho la juzi walifanya onesho zuri la aina yake na katika mji wa Washington na kuudhuliwa na mashabiki wengi wa muziki. 

"Onesho letu la juzi lilikuwa zuri sana na limezidi kuongeza hamasa kwa vijana wazidi kujituma na kufanya viuri zaidi katika kuhakikisha wanapata mihaliko kama hii ya kuja nchini kama hizi ambazo nazo tumekuwa na mashabiki wetu"alisema Fella.

PPF YAIBUKA KIDEDE KATIKA UTUNZAJI BORA WA HESABU ZAKE, YATWAA TUZO YA WA HESABU UPANDE WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

$
0
0


Na K-Vis Media/Khalfan Said.
MFUKO wa Pensheni wa PPF, umeibuka kidedea kwa kutwaa tuzo ya uwasilishaji bora wa hesabu zake katika kipindi cha mwaka 2014.

Katika hafla ya kutoa tuzo kwa taasisi za serikali na za watu binafsi, Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu, NBAA, imetoa tuzo hizo kwa makampuni na taasisi mbalimbali nchini, ambapo kwa upande wa kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, PPF ndiyo iliibuka ya kwanza ambapo Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko huo, Bw. Martin Mmari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Bw. William Erio, alipokea tuzo hiyo kutoka kwa mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Khamis Mwinyimvua. Pichani Bw. Mmari akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Khamisi Mwinyimvua. 
(Picha na K-Vis Media/Khalfan Said)
Bw. Khamisi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na umuhimu wa kuwasilisha taarifa sahihi za hesabu.
Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. Martin Mmari, (katikati), akiwa amekamata tuzo wakati wa kupiga picha na baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko huo kwenye hafla ya kutolewa tuzo ya taasisi iliyowasilisha taarifa za mahesabu za mwaka 2014 kwa kuzingatia taratibu na kanuni za mahesabu kwenye kituo cha mikutano cha Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu NBAA, huko Bunju nje kidoto ya jiji la Dar es Salaam, Desemba 5, 2015. PPF ilishika nafasi ya kwanza katika kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Tuzo hizo hutolewa na NBAA
Bw. Mamri (wapili kulia), akigongesha glasi na mmoja wa waalikwa wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wawakilishi wa PPF katika hafla hiyo.

JUMUIYA YA KIMATAIFA YAOMBWA KUSAIDIA HUDUMA KAMBI YA NYARUGUSU

$
0
0
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) na ujumbe wake aliombatana nao Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (wa pili kushoto) pamoja na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (kushoto) kabla ya kuelekea kambi ya Nyarugusu walipita ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita kumsalimia pamoja na kusaini kitabu cha wageni. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

Na Mwandishi Wetu, Kigoma
JUMUIYA ya Kimataifa imekumbushwa kuisaidia Tanzania katika kuhudumia wakimbizi kutoka Burundi na Kongo ambao wanaishi katika kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma.

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakati akizungumza na waandishi wa habari mara tu baada ya kukamilisha ziara yake mkoani Kigoma.

Alisema kwamba serikali ya Tanzania kwa miaka mingi imekuwa na moyo wa huruma wa kusaidia majirani zake kwa kuhifadhi wakimbizi na kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kuona hilo na kusaidia Tanzania kufanikisha hifadhi ya wakimbizi.

Alisema Umoja wa Mataifa umekuwa ukishuhudia namna ambavyo serikali ya Tanzania inahudumia wakimbizi na kuridhika na hata pale ilipowapatia haki za kuwa Watanzania kwa kuwapa uraia na pia kusaidia kuwarejesha makwao wakati hali ilipokuwa njema.

Hata hivyo amesema kwa sasa hali ya Burundi na Kongo si njema na hivyo Watanzania kupata tena kazi yakuhifadhi wakimbizi.

Alisema Tanzania kwa huruma yake imetoa ardhi zaidi ili kupunguza msongamano katika kambi ya Nyarugusu na kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kusaidia kukamilisha makazi hayo mapema kabla ya mvua za masika ili wananchi hao waweze kuishi kwa amani.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita akimsikiliza kwa makini Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake kabla ya kuelekea kambi ya Wakimbizi Nyarugusu.

Alisema kambi ya Nyarugusu ni ya tatu kwa ukubwa duniani na inahifadhi zaidi ya wakimbizi 150,000 wakiwemo watoto na wanawake na wanahitaji huduma za shule, afya, maji na mengine.

Aidha wanahitaji nishati na hali hiyo haiwezi kuwezeshwa na serikali ya Tanzania pekee kwani watakuwa wakielemewa na huruma yake na moyo wa upendo kwa majirani zake.

“Dunia ikumbuke wema wa watanzania kwa miaka yote hii, na isaidie kuweka sawa hali ya kambi hiyo ili huduma zote muhimu za wananchi zipatikane” alisema mratibu huyo.

Akizungumza kuhusu wajibu wa Umoja wa Mataifa, alisema mashirika yake yamekuwa yakishirikiana na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kwamba wanatoa huduma kwa wakimbizi hao na kutaka wadau duniani kusaidia mashirika hayo na serikali ya Tanzania kufanikisha mahitaji muhimu kwa wakimbizi hao hadi hali itakapokuwa shwari katika nchi zao na kurejea kuishi makwao.

Tanzania imetoa maeneo matatu zaidi ya kupunguza msongamano katika kambi ya Nyarugusu na maeneo hayo yanahitaji huduma za msingi kama barabara, maji, vituo vya afya na shule.

Katika ziara hiyo ambayo aliambatana na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan, pamoja na kukagua maendeleo ya kambi ya Nyarugusu pia walikagua miradi inayofadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani ILO na ile ya Shirika la Mpango wa idadi watu duniani UNFPA.

ILO Kigoma inaendesha mafunzo ya ujasirimali kwa vijana kwa lengo la kuwawezesha kujiajiri wenyewe na kuhudumia familia zao kwa kuziwezesha kupata huduma bora za elimu na afya kutokana na kipato chao.
Katika msafara huo walikuwepo maafisa kutoka Shirika la linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) ofisi ya Kasulu mkoani Kigoma (walioipa mgongo kamera).

Alisema kwamba amefurahishwa na mradi huo ambao unawawezesha vijana kutambua fursa mbalimbali zilizopo na kuzitumia vyema kufanikisha maendeleo ya familia zao.

“Naona uwezekano wa vijana hawa kujiajiri na kuziwezesha familia zao kuondokana na tatizo la kipato.. elimu hii inaweza kutanzua mambo mengi na kuondoa changamoto nyingine zinazoambatana na kukosa kipato” alisema mratibu huyo.

Mkoa wa Kigoma una mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa yakifanya kazi mbalimbali za maendeleo na za kutoa huduma za kibinadamu kwa wakimbizi.

Mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa yanayotekeleza miradi mbalimbali mkoani Kigoma ni pamoja na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Shirika la Afya Duniani ( WHO), Shirika la Mpango wa Uzazi (UNFPA), Shirika la Kazi la Kimataifa ( ILO), Shirika la Kuhudumia Watoto ( UNICEF), Shirika la Kuhudumia Wahamiaji ( IOM), Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika la maendeleo (UNDP).

Akizungumza Afisa anayeshughulikia Ustawi na Usalama UNHCR, Kasulu, Bi. Zenobia Mushi, alisema shirika lake litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania na ya mkoa wa Kigoma katika kuhudumia wakimbizi kwa kuhakikisha kwamba mahitaji yao ya msingi yanapatikana.

Naye Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu Issa Machibya alishukuru Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kuwa tayari kusaidia mkoa wake.

“ Tunashukuru kwa mambo yanayofanywa na Umoja wa Mataifa katika dhima nzima ya ushirikiano katika kuhakikisha kwamba pengo la maskini na matajiri linazibwa na umaskini unaondolewa katika mkoa wa Kigoma.”
 

Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan akipiga picha kwenye bango linaloonyesha Serikali zinazofadhili misaada kwa Wakimbizi nchini Tanzania lililopo katika ofisi za UNHCR Kasulu.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita akizungumza kuhusu hali ya kambi ya Nyarugusu alisema kwamba hali ya kambi si nzuri na wakati msimu wa masika ukikaribia ni vyema Jumuiya ya Kimataifa ikaharakisha kukamilisha miundombinu ili kupunguza msongamano Nyarugusu.

Serikali imetoa maeneo mengine ya Nduta yaliyoko Kibondo na na Ntendeli, Kakonko kwa ajili ya kupunguza uwingi wa watu katika kambi hiyo.

DC huyo pia alisema kwamba kuna uharibifu mkubwa wa mazingira na lazima wadau wote washirikiane kuhakikisha kwamba mazingira yanaboreshwa pamoja na kupokea wakimbizi na kuwapa makazi.

Alisema kambi hiyo ilipangwa kuwa na watu elfu 50 kwa miaka ya 1996 lakini sasa inaweka wakimbizi wengi zaidi.

Aidha alisema kwamba pamoja na kupokea wakimbizi hao, inaonekana baadhi yao wameingia kufanya uhalifu na kuomba wakimbizi kushirikiana na polisi kuwataja wahalifu hao ili wadhibitiwe.
Kuwepo kwa kundi kubwa la wakimbizi kunasababisha uharibifu wa mazingira kama inavyoonekana pichani wakimbizi wakitoka kukata kuni kwenye misitu iliyopo karibu na kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Aidha katika mazungumzo ya shukurani kwa namna serikali ya Kigoma inavyotoa ushirikiano kwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika miradi ya maendeleo na misaada kwa wananchi na kwa wakimbizi, Mwakilishi wa Shirika la mpango wa idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem alisema kwamba kumekuwepo na mafanikio mengi kutokana na ushirikiano huo.

Alisema anachokiona yeye anaona hali ya baadae ya taifa la Tanzania kuwa bora zaidi kutokana na kuwapo kwa ushirikiano mzuri kati ya serikali, mashirika ya umma na kundi kubwa la vijana ambalo kwa sasa linapokea elimu mbalimbali kwa manufaa yao na ya baadae.

“Taifa la Tanzania nusu yake ni vijana na sehemu kubwa ni chini yake, taifa hili lina hali njema kabisa ya siku za usoni kutokana na ushirikiano wenye lengo la kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na wengi” alisema Kanem.

Anasema kwa kuangalia program zilizopo zinazotekelezwa kwa pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa na serikali anaona mafanikio ya mafunzo ya ujasiriamali na pia elimu inayotolewa kwa watu kwa malengo ya kufanikisha maendeleo.
Alisema UNFPA imefurahishwa sana namna mafunzo yanavyoendeshwa kwa vijana mafunzo ambayo yanaleta mshikamano wa pekee katika kufanikisha ustawi wa jamii na taifa kwa jumla.

Aidha alifurahi kuona kwamba wanawake wanashiriki katika kutoa elimu hivyo kuingiza sauti katika mafanikio ya jamii na uongezaji wa uelewa miongoni mwa jamii.

Mratibu huyo Mkazi wa UN Tanzania, Alvaro Rodriguez na timu yake wamerejea Dar es Salaam baada ya ziara ndefu kuangalia miradi ya Umoja wa Mataifa inavyoleta tija na ufanisi wa maisha katika jamii.

Mratibu huyo alitembelea mikoa ya Manyara, Singida, Tabora na Kigoma.

Katika ziara yake alioneshwa kufurahishwa na miradi hiyo inavyobadili jamii husika na kusema kwamba umoja huo utaendelea kufadhili miradi ya maendeleo nchini Tanzania.
 
Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile (kulia) akielezea changamoto mbalimbali zinazowakabili kambini hapo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) na ujumbe wake aliombatana nao Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (wa pili kushoto) pamoja na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (kushoto) kabla ya kutembelea makazi ya wakimbizi hao.

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (kulia) na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan wakirekodi mambo muhimu wakati wa kupokea taarifa ya maendeleo ya kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu kutoka kwa Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile (hayupo pichani).
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem akizungumza jambo kwenye mkutano wa kupokea taarifa ya kambi hiyo.
Kutoka kushoto ni Afisa mahusiano wa UNHCR, Ofisi ya Kasulu, Agnes Mwangoka, Mshauri na Mtaalum wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Hoyce Temu, Mwandishi wa Habari, Prosper Kwigize pamoja na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan wakielekea kwenye kambi za Wakimbizi baada ya kupokea taarifa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem wakikagua ndani ya mahema wanakoishi Wakimbizi wapya wanaoendelea kuwasili katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem wakiuliza jambo kwa Ofisa Mtafiti Mshirikishi wa ofisi za UNHCR, Kasulu, Mariam Khokhar walipotembelea ndani ya mahema wanakoishi Wakimbizi wapya wanaoendelea kuwasili katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile.
Eneo la mahema ya kulalia familia za Wakimbizi wapya wanaoendelea kuwasili katika kambi ya Nyarugusu.
Mmoja wa Wakimbizi akiwa na mwanae nje ya chumba chake na mwanae katika kambi ya Nyarugusu.
Kuni zikitumika kupikia chungu cha Maharage kambini hapo.
Mtoto ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi akikoleza moto ulioonekana kufifia wakati akijiandalia chakula chake cha mchana kama alivyonaswa na kamera yetu. 
Moja ya familia ya Wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu wakiangalia msafara wa Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini uliotembelea kambini hapo mwishoni mwa juma.
Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan akipozi na moja ya familia katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisalimiana na Rais wa kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, Bi. Abilola Angelique wakati wa ziara yake ya kutembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETINI

$
0
0
SIMU.TV:  Kutokuwapo mawaziri kumeokoa mabilioni. TRA yaibana Bakwata msamaha wa kodi. Waliotorosha makontena hadharani,
SIMU.TV:  Moto wa rais Magufuli waichoma TANESCO. Mawakili watano kutetea ubunge wa Kubenea. Majipu miradi ya barabara; https://youtu.be/6BVQqblZyp4
SIMU.TV:  Wenyeviti CCM wampa tano rais Magufuli. Gesi yaleta mapinduzi makubwa ya umeme. Makonda aibua ufisadi bil.2.2; https://youtu.be/mtHOZI856-o  
SIMU.TV:  Wazee wa kazi YANGA wavamia Tanga. Kiongera, Kiiza wawekewa ulinzi. Azam yaiwaza Simba. Mbeya City yanasa watatu; https://youtu.be/NZKuOo2CggA 
SIMU.TV:  Magufuli, Manji hapatoshi CCM. Vigogo 7 TANESCO wazolewa, ni kasi ya utumbuaji majipu. Pata habari za kina katika magazeti ya leo; https://youtu.be/twaGmgKG1_k

MAHAFALI YA KWANZA YA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI (MoCU)

$
0
0
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) Pius Msekwa akitunuku Shahada ,Stashahada na Astashahada kwa wahitimu wa Chuo hicho wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho. 
Wahitimu wa kozi mbalimbali waliohitimu katika Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi,(MoCU) 
Miongoni mwa wageni waalikwa alikuwepo pia Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael. 
Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika (MoCU) Profesa Faustine Bee akizungumza wakati wa sherehe za mahafali ya kwanza ya Chuo hicho yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Chuo hicho. 
Miongoni mwa wahitimu walikuwepo pia Mbunge wa viti maalum,Sharry Raymond pamoja na Mkuu wa wilaya ya Mwanga ,Shaibu Ndemanga. 
Baadhi ya wakufunzi katika chuo hicho. 
Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro ,Severine Kahitwa (Kulia) akiteta jambo na Meneja wa benki ya NMB ,tawi la Mandela mjini Moshi ,Emanuel Kashusho wakatiwa mahafali ya kwanza katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi. 
Kaimu Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo (Utawala na Fedha) Ndayizera Manta (Kushoto) akiwa na Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) Profesa Gerald Monera wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo kikuu cha Ushirika Moshi. 
Muongozaji wa sherehe ya mahafali hayo Cyril Komba akitoa muongozo wa shughuli hiyo iliyofanyika viwanja ya Chuo kikuu cha Ushirika Moshi. 
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Pius Msekwa akitoka katika viwanja vya Ushirika mara baada ya kumalizika kwa sherehe ya mahafali ya kwanza ya chuo hicho. 
Baadhi ya wakufunzi wa Chuo hicho,Profesa Wakuru Magigi (kulia ) wakiwa na Mkuu wa Shule ya Polisi zamani Chuo cha Polisi Moshi,Matanga Mbushi . 
Mkuu wa wilaya ya Ilala,Raymond Mushi (kushoto) akiwa na mmmoja wa wakufunzi katika chuo hicho Dkt Kaleshu ,wakipozi katika picha ya pamoja na Mbunge wa Viti maalum CCM ,Sharry Raymond.
Picha zaote na  Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini (0755659929). 



AIRTEL FURSA YATUA BUKOBA, YAONGEA NA VIJANA KUTOOGOPA VIKWAZO KATIKA UJASILIAMALI

$
0
0
 Mjasiliamali wa mjini Bukoba Adamu Hemed akipokea cheti kutoka kwa meneja biashara wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Mohamedi kabeke baada ya kuhudhuria mafunzo ya ujasiliamali yaliyoendeshwa na mradi wa Airtel FURSA kwa Zaidi ya vijana 200. kati ni Afisa ujasilimali wa VETA mjini bukoba Bw, Frabius Ngemela na Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando mwishoni mwa wiki hii mkoani Kagera.
 .Mkulima wa mboga mboga kutoka Bukoba mjini Agnetha Frenk akipokea cheti toka kwa meneja wa biashara Airtel BUkoba Mohamed kabeke baada ya kuhudhuria mafunzo ya ujasiliamali yaliyoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel mjini Bukoba kati ni Afisa ujasilimali wa VETA mjini bukoba Bw, Frabius Ngemela na anaefuata ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando. Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwa siku mmoja na kuhudhuriwa na vijana zaidi ya 200 mkoani Kagera.
Mkazi wa mtaa wa Nshambya mjini Bukoba Janath Shafi anayejishughulisha na biashara ya ufugaji wa mbuzi akipokea cheti toka kwa meneja wa biashara Airtel BUkoba Mohamed kabeke baada ya kuhudhuria mafunzo ya ujasiliamali kwa vijana yaliyandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Airtel mkoani Kagera. Cheti baada ya kuhudhuria mafunzo ya ujasiliamali yaliyoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Katikati ni mwalimu wa mambo ya ujasiliamali ambae pia ni Afisa ujasilimali wa VETA mjini bukoba Bw, Frabius Ngemela na anaefuata ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando. Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwa siku mmoja na kuhudhuriwa na vijana zaidi ya 200 mkoani Kagera.
 Kijana anayejishughulisha na ufugaji wa kuku kutoka Kijiji cha Katoka Wilaya ya Bukoba Vijijini Lucas Joseph akipokea cheti toka kwa meneja wa biashara Airtel BUkoba Mohamed kabeke baada ya kuhudhuria mafunzo ya ujasiliamali kwa vijana yaliyandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Airtel mkoani Kagera. Katikati ni mwalimu wa mambo ya ujasiliamali ambae pia ni Afisa ujasilimali wa VETA mjini bukoba Bw, Frabius Ngemela na anaefuata ni meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando. Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwa siku mmoja na kuhudhuriwa na vijana zaidi ya 200 mkoani kagera.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya ujasiliamali yaliyofanyika mjini Bukoba yaliondaliwa na kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa fursa tunakuwezesha. Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwa siku mmoja na kuhudhuriwa na vijana zaidi ya 200 mkoani kagera

· Bukoba zaidi ya wajasiliamali vijana 200 wanolewa na Airtel Fursa
KAMPUNI ya mawasiliano ya simu za mkononi airtel imewataka watanzania kuchangamkia fursa zilizopo kwa kufanya ujasiriamali kwa mtazamo mpana kwa lengo la kuondokana na umasikini au maisha duni yasiyo na kipato maalum.

Hayo yamesemwa na mwalimu wa mambo ya ujasiliamali ambae pia ni Afisa ujasilimali wa VETA mjini Bukoba Bw, Frabius Ngemela kwa zaidi ya wajasiliamali 200 waliohuduria semina ya ujasiliamali ya Airtel Fursa BUKOBA akiwataka vijana wajasiliamali kutumia ujuzi na maarifa katika kuboresha miradi yao kama njia mojawapo ya kukabiliana na suala la umasikini na kuwataka wajasiliamali hao kutokata tamaa ya maisha badala yake waongeze juhudi katika uzalishaji mali bila kuogopa vikwazo ili kujikomboa.

Airtel Fursa imekuja Bukoba leo kuwaambia msikate tamaa, nawafundisha leo kuvitambua vikwazo na msiviogope katika shughuli zenu, mkashirikiane na mradi wa Airtel Fursa ili kujikwamua.

Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alieleza “Airtel Fursa sio tu tunawasaidia vijana kuzitambua fursa pia tunawapatia mitaji na vitendea kazi muhimu ambavyo vimekua ni vikwazo vya kutimiza malengo yako ili uweze kuzalisha zaidi na kusaidia jamii zao.

“Hadi sasa tumeshazunguka mikoa zaidi ya 12 ndani ya miezi hii minne tukiwaeleza vijana jinsi wanavyoweza kukamata FURSA na kuwasaidia kupitia warsha kama hizi pia kuwapatia vitendeakuzalis kazi na vifaa mbalimbali waweze kuzalisha zaidi” alisema Mmbando.

wakiongea mara baada ya kupatiwa elimu ya ujasilimali baadhi ya wajasiliamali wadogo Peace Ruben MJASIRIAMALI, alisema licha ya kupatiwa elimu hiyo bado wanakabilina na changamoto mbalimbali ikiwemo mitaji ya kuendeshea biashara zao ambapo pia wametumia nafasi hiyo kuiomba kampuni ya airtel kwa kutumia mradio wao wa Airtel fursa kuwapatia mitaji itakayo wasaidia kuendesha biashara zao.

“Mi kazi yangu ni kufuma vitambaa na nguo za kuzuia baridi kwa watoto , wateja wangu wanapatikana kwa urahisi hapa bukoba na nje ya bukoba yaani hapo mpakani mwa Tanzania na Uganda lakini tatizo ni vitendea kazi vya kutosha ili kuongeza uzalishaji, ikiwa Airtel Fursa itanitoa nitafurahi sana” alieza Peace Ruben

TANZIA

$
0
0
FAMILIA ya Marehemu Mzee Anthony Kazimoto Ritte wa Kinondoni B DSM, wanasikitika kutangaza kifo cha mpendwa wao Apolito Anthony Ritte kilichotokea katika Hospitali ya Muhimbili saa sita usiku wa kuamkia tarehe 05/12/2015. Mazishi yatafanyika siku ya Jumatano tarehe  09/12/2015 katika makaburi ya Kinondoni.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live


Latest Images