Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

MRAGHABISHI MAIMUNA SAIDI AGEUKA SHUJAA WA KIJIJI CHA MWIME KAHAMA

$
0
0
Na krantz mwantepele ,

Ziara niliyofanya katika Kijiji cha Mwime kata ya Mwendakulima wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga mwishoni wa mwezi Novemba mwaka huu ,ilinipa mwanga wa jinsi ambavyo wananchi wakiamua kuchukua hatua wanaweza kubadili mfumo mzima na kuweza kujiletea maendeleo katika Nyanja zote za maendeleo .Kijiji cha Mwime ambacho wananchi wengi wanajihusisha na biashara, uchimbaji wa madini na kilimo cha pamba na wapo katika eneo ambalo Barick Buzwagi wanafanya uchimbaji mkubwa wa dhahabu.
Ofisi za kijiji hicho cha Mwime kilichopo kata ya Mwendakulima wilayani Kahama

Mgogoro wa Maslahi wa wananchi wanaozunguka mgodi uliokuwa unamilikiwa na Barrick na sasa Accaccia uliopo wa Buzwagi kwenye wilaya ya Kahama katika kijiji cha Mwime kilichopo kata ya Mwendamkulima katika wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, Unaibua mashujaa wa kutetea haki na kudai uwajibikaji u wa viongozi katika kuendeleza utawala bora na maendeleo kwa ujumla lakini mwishoni inageuka kuonekana ni maadui wa maendeleo . 

Kwa muda wa miaka zaidi ya mitano sasa kijiji hiki kimekuwa katika pilikapilika za kuhakikisha wan-aendelea kunufaika na rasilimali yao ya madini ya dhahabu ambayo kwa sasa yanachimbwa na kampuni ya Accacia katika mgodi wa Buzwagi kupitia Makubaliano ya Nyongeza ya Mkataba yaliyosainiwa mwaka 2007.

Kwa mujibu wa kifungu 1.1 cha Makubaliano ya Nyongeza ya Mkataba baina ya Kampuni ya Madini ya Pangea kwa niaba ya Barrick na kijiji; kampuni itakuwa ikikilipa kijiji kiasi cha Tsh milioni 60/- kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitano baada ya uzalishaji kuanza na kisha pande mbili hizi zitakaa pamoja na kupitia kiwango hiki kwa kadri ya uzalishaji utakavyokuwa kwa nia ya kuboresha zaidi. Na uzalishaji wa dhahabu katika mgodi huu ulianza rasmi mwaka 2009.

Nikiwa ziarani wilaya ya Kahama nilitembelea kijiji hiki ambacho mwanzoni mwa mwaka 2007 wananchi wengi wa kijiji cha Mwime na maeneo ya karibu walijihusisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu kabla kampuni ya Pangea kuja kuchukua maeneo hayo kwa kuhodhi mashimo yaliyojulikana kwa majina ya Zanzibar na majimaji na kuwafanya wakazi hao kuondoka hapo kupisha uchimbaji wa kisasa.

Mategemeo ya wananchi kupata maendeleo makubwa baada ya kampuni ya Pangea kuanza uchimbaji huo wa kisasa yaliendelea kufifia kila uchwao baada ya makubaliano ya kulipwa kiasi cha milioni 60 kila mwaka kwa kipindi cha miaka kipindi cha miaka mitano cha uchimbaji wa madini kutotimizwa kwa wakati.Licha ya kutokuwa na uelekezi rasmi wa kiseheria wa makubaliano hayo lakini yaliwafanya wananchi wa mMwime kuendelea kuishi maisha magumu licha ya kuwa mgodi wa Buzwagi kuweza kufanya uchimbaji kwa muda mrefu.

Kuchelewa kwa malipo kama walivyokubaliana kulisababishwa pia na mapungufu ya uongozi wa kijiji kushindwa kufuatilia suala hilo kwa ukaribu.Sababu nyingine inayotajwa ni kwa Wanamwime wenyewe kushindwa kudai na kuwahimiza vi-ongozi wao kuchukua hatua kwa kufuatilia suala hilo.
Bi Maimuna akiwa na mjukuu wake katika duka lake analouza pembejeo za kilimo kwa wakazi wa kijiji cha Mwime 

Mraghabishi na mpambanaji wa haki za binadamu Bi Maimuna Saidi ambaye pia ni mwananchi wa kijiji hicho ambaye yeye na wenzake watano walichukua hatua ya kuanza kuhimiza ufuatiliaji wa pesa hizo kama walivyokubaliana na baada ya mazungumzo marefu na pia ushirikishaji wa wananchi wote wa kijiji kupitia mikutano ya kijiji waliweza kufanikisha upatikanaji wa ya million 300/ kama malipo ya mwaka 2009 – 2013 .
Mama maimuma saidi (Mwenye kilembo)akitoa maelezo jinsi gani walivyofanikisha kupatikana kwa maendeleo katika kijiji cha Mwime kutoka katika mgodi wa Buzwagi kwa baadhi ya waandishi wa habari na wataalamu wa mitandao ya kijamii niliombatana nao .

Hivyo Maimuna Said kupitia ufahamu aliopatiwa alimshawishi Diwani mara kwa mara kuweza kuchukua hatua zaidi, kwa kuwa yeye alikuwa na mamlaka zaidi.Na mwishowe kupitia harakati mbalimbali na ushirikishwaji wa wananchi wenzao walifanikiwa kupata kiasi hicho cha pesa.

Pesa hizo pia zilitumika kuboresha shughuli mbalimbali za maendeleo na huduma za kijamii kama ujenzi wa miundombinu ya umeme ,nyumba za manesi, nyumba ya kupumzikia wageni kama kitega uchumi lakini haya yote yalikuwa kama kipaumbele cha wananchi kufaidikapia kiasi kilichobaki kulipa baadhi ya fidia kwa wananchi waliotoa maeneo yao katika upanuzi wa barabara .
Moja ya nyumba zinazojengwa katika kijiji hiki cha Mwime kama moja ya matumizi ya pesa walizopata kutoka katika mgodi wa Buzwagi .

Huu mchakato wote usingeweza kufanikiwa kama Wanamwime wenyewe wasingesimama pamoja na kudai haki yao. Kwa hakika ili tupate tutakachotaka ni lazima tuchukue hatua za dhati pasipo kuchoka wala kukata tamaa huku tukishirikiana na viongozi wetu kwani kuna msemo unasema umoja ni nguvu utengano ni udhaifu kama dhana waliotumia wanaMwime wakafanikiwa katika harakati zao za kujiletea maendeleo kijijini hapo.

Imeandaliwa na MWANAHARAKATI MZALENDO BLOG

Fella Akabidhi Kombe kwa Mshidi Mpinga Cup Temeke.

$
0
0
Mashindano ya mpinga cup.fainali zake zimemalizika leo kati ya oxford ya majimatitu na gussepe f.c.ya mzambarauni matokeo gusepe wameshinda kwa 4 kwa 2 kwa gusepe penati zimefungwa na Kassim, Gomea, Mrisho Chodo na Aguero. 
 
Kwa upande wa oxford walioshinda ni Hamza Mpili na Rajabu. Mikwaju miwili ilidakwa na golikipa wa gusepe ndg Haji machelazi waliokosa penati hizo ni Julius, Chikaka na selemani deko, mshindi wa kwanza amejinyakulia Ng'ombe Mshindi wa pili oxford ameshinda Mbuzi na mshindi wa tatu Kazembe boys wamechukua Jezi pea moja. mgeni rasmi diwani wa kilungule, Mh Said Fella ambaye alikabidhi zawadi hizo kwa washindi wote katika mchezo ambao ulimalizika jana katika viwanja vya Maji matitu.

RC KILIMANJARO AWASIFU WAANDAAJI WA BONANZA LA MADESHO DAY

$
0
0
Timu ya Ushrika wakijandaa kuvuta kamba katika bonanza la kumbukumbu ya Mwenyekiti wa kwanza wa klabu ya Moshi veterani Marehemu Madesho Moye. 
Timu za Maveterani wa KIA na Kitambi noma ya Arusha wakioneshana kazi katika kuvuta kamba. 
Mashindano ya Mbio za mita 100 pia zilikuwa kivutio hapa ,Salvatory Mtanange akionesha uwezo wa kukimbia mita 100 ambapo alifanikiwa kushinda. 
Mwamuzi maarufu wa mchezo wa kukimbiza kuku nchini akiingia uwanjani kwa ajili ya mchezo huo.
Kikosi cha timu ya Ushirika Veterani. 
Kikosi cha wachezaji wa timu ya Kitambi noma. 
Wachezaji wa timu ya Moshi eterani wakiongozwa na nahodha wao mpya aliyesajiliwa katika kipindi hiki cha dirisha dogo,Amosi Makala ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro wakinyoosha kabla ya kuanza mpambano. 
Amosi Makala akijaribu kutaka kupita walinzi wa timu ya Ushirika Veterani. 
 Amosi Makala akijiandaa kupiga mpira wa adhabu . 
Baadhi ya Mashabiki wa timu mbalimbali za maveterani zilizoshiriki Bonanza la kumbukumbu ya Mwanzilishi wa klabu ya Moshi Veterani,Marehemu Madesho Moye. 
Mshambiliaji wa klabu ya Ushirika Veterani Tumaini Masue akijaribu kutafuta njia za kutaka kumpita mlinzi wa timu ya Kitambi noma. 
Masue akijaribu kuzuia mara baada ya kushindwa kupita . 
 Bonanza la Kumbukumbu ya Madesho lilienda sanjari na sherehe ya kupokea Kipaimara cha mtoto wake Qareen Madesho ambaye aliongozana na familia yake hadi katika viwanja vya Moshi Club ambako Bonanza hilo lilifanyika.
Mke wa Marehemu Madesho,Shufaa Madesho alikuwepo uwanjani hapo kufuatilia Bonanza hilo. 
Mke wa Marehemu Madesho ,Shufaa Madesho akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Amosi Makala ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika Bonanza hilo wakifuatilia mchezo. 
Zawadi zikatolewa kwa mchezaji Cunbert Ngambira wa timu ya Maveterani wa KIA baada ya kushinda mbio za Mita 100 kwa wenye umri wa miaka 30-40. 
 Zawadi zikatolewa kwa mshindi wa mbio za Mita 100 Salatory Mtanange wa Moshi veterani kwa wakimbiaji wenye umri kati ya miaka 40 na 50. 
 Mshindi wa pili kwa upande wa mpira wa Miguu timu ya Ushirika Veterani ,wakakabidhiwa kikombe,nahodha wa timu hiyo Erick akapokea kwa niaba ya timu. 
Washindi wa pili timu ya Maveterani ya Best Maridadi ,wakakabidhiwa kikombe ,kikapokelewa na Ismail . 
Washindi wa kwanza kwa upande wa mpira wa miguu timu ya Maveteran wa njia panda ya Ulaya KIA,wakakabidhiwa kikombe na mgeni rasmi ,Amosi Makala.
KIA wakifurahia kikombe chao cha kwanza tangu kuanzishwa kwa timu hiyo. 
Mgeni rasmi katika Bonanza hilo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Amosi Makala akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi. 
Mke wa Marehemu Madesho akizungumza katika Bonanza hilo. 
Baadhi ya ndugu waliofika katika Bonanza hilo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini

MRADI WA VIJANA WAMFURAHISHA MRATIBU WA UN NCHINI

$
0
0
IMG_6443
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akikata kuzindua eneo la heka 3 la kituo cha mafunzo kwa vitendo kwa ajili ya kuwaanda vijana katika kilimo na ufugaji kuku (Youth incubation resource centre) ambalo limetolewa na manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Nyakitonto Youth For Development Tanzania kwa faida ya vijana Kigoma kujikwamua kiuchumi.
IMG_6445
IMG_6450
IMG_6466
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akipata maelezo ya eneo la ndani litakalotumika kwa vitendo katika kilimo na ufugaji kwa vijana wa Kigoma ili waweze kujikwamua kiuchumi.
IMG_6094
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Issa Machibya akiongozana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez mara tu baada ya kumpokea alipowasili ofisini kwake akiwa ameongozana na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan, pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (hawapo pichani).


Na Mwandishi wetu, Kigoma
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ameelezea kufurahishwa kwake na uwapo wa mradi wa kusaidia vijana wa kitanzania kujifunza ujasirimali na kujitegemea.
Akizungumza katika shughuli za uzalishaji mali za vijana wa Shirika lisilo la kiserikali la Nyakitonto Youth Development Tanzania la mjini Kigoma alisema kwamba shughuli wanazofanya vijana hao zinamsisimua sana.

“Tunafurahi sana mimi na wenzangu kutembelea mradi huu unaofadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ambao unachochea ujasirimali miongoni mwa vijana. Sote tunajua kwamba vijana wengi wa Kitanzania wanaume kwa wanawake wameelimika lakini hawana ajira rasmi. Na suala la ujasiriamali ni kitu ambachio mtu anaweza kujifunza, na ujasiriamali unatoa fursa kwa vijana kujiunga katika kundi la wafanyakazi kwa kujiajiri wenyewe.

“Tunajua kwamba kupitia shughuli zinazofadhiliwa na ILO katika ngazi ya jamii na kwa kufuata maelekezo ya serikalai za mtaa vijana wanaanzisha biashara mbalimbali binafsi au na jamii. Kiwanda cha kutengeneza sabuni ni mfano mzuri sana. Tunaona kwamba mradi huu unawaongezea kipato na hivyo kuweza kusaidia familia zao na kupeleka watoto shuleni na kuboresha lishe . Kwa ufupi mradi kama huu unasaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazokabili kaya maskini Kigoma” alisema Rodriguez.

ILO Kigoma inaendesha mafunzo ya ujasirimali kwa vijana kwa lengo la kuwawezesha kujiajiri wenyewe na kuhudumia familia zao kwa kuziwezesha kupata huduma bora za elimu na afya kutokana na kipato chao.
IMG_6098
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Issa Machibya (kushoto) akibadilishana 'Business card' na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem.
Alisema kwamba amefurahishwa na mradi huo ambao unawawezesha vijana kutambua fursa mbalimbali zilizopo na kuzitumia vyema kufanikisha maendeleo ya familia zao.
Aidha alisisitiza haja ya jumuiya ya kimataifa kuusaidia mkoa Kigoma katika nyanja mbalimbali za kiuchumi hasa katika eneo la ajira kwa vijana kutokana na ukarimu wa wakazi wa mkoa huo katika kuwapokea na kuwahudumia wakimbizi kutoka nchi za maziwa makuu kwa upendo.
Rodriguez alisema pamoja na ombi hilo Mratibu huyo wa shughuli za kimataifa ambaye ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) alisema wao kama UN wakifanyakazi pamoja wataendelea kutoa misaada kwa wakimbizi hasa uanzishaji wa miradi ya kiuchumi kwa vijana na wanawake.
Kwa upande wake Mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa mataifa la Idadi ya watu (UNPFA), Dkt. Natalia Kanem alisema kuwa kupatiwa mitaji na kuanzisha vikundi vya uzalishaji kwa vijana na wanawake kunasaidia kuongeza ajira lakini pia kusaidia kupunguza ongezeko kubwa la idadi ya watu bila mpangilio.
Katika risala yao kwa uongozi huo wa Umoja wa Mataifa vijana kutoka Nyakitonto Youth Development Tanzania wamesema kuwa misaada iliyotolewa kwao imewasaidia kupata ujuzi na kuanzisha miradi ya uzalishaji mali ikiwa ni sehemu ya kujiajiri na kujiongezea kipato ili waweze kuendesha maisha yao bila utegemezi.
IMG_6105
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Issa Machibya akitoa taarifa ya mkoa wake kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na ujumbe ofisini kwa Mkuu huyo wa mkoa.
Hata hivyo vijana hao katika risala yao iliyosomwa na Meneja miradi wa shirika hilo, Anjelina Gulanywa walisema kuwa pamoja na mafanikio hayo wanakabiliwa na changamoto utaalam mdogo, mitaji na vitendea kazi vya kisasa ili kufanya shughuli zao kuwa na mafanikio zaidi.
Naye Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu, Issa Machibya alieleza kuridhishwa kwake na juhudi za Umoja wa Mataifa katika kusaidia miradi mbalimbali mikoani mwake ambayo inasadia wananchi kukabiliana na umaskini.
Mkoa wa Kigoma una mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa yakifanya kazi mbalimbali za maendeleo na za kutoa huduma za kibinadamu kwa wakimbizi.
Mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa yanayotekeleza miradi mbalimbali mkoani Kigoma ni pamoja na Shirika la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR),Shirika la Afya Duniani ( WHO), Shirika la Mpango wa Idadi ya watu (UNFPA) ,Shirika la kazi la Kimataifa ( ILO), Shirika la Kuhudumia watoto( UNICEF), Shirika la Kuhudumia wahamiaji ( IOM), Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika la maendeleo (UNDP).
IMG_6134
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akielezea dhumuni la safari yake katika mkoa wa Kigoma kwa Mkuu wa mkoa huo, Kanali Mstaafu, Issa Machibya.
IMG_6123
Afisa Mawasiliano wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) nchini, Magnus Minja akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana yenye lengo la kuwawezesha kujiajiri wenyewe na kuhudumai familia zao kwa kuziwezesha kupata huduma bora za elimu na afya kutokana na kipato chao unaofadhiliwa na shirika hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu, Issa Machibya.
IMG_6147
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwasilisha Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (Sustainable Development Golas-SDGs) kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Issa Machibya. Kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem.
IMG_6152
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akikabidhi zawadi ya Khanga ya 'miaka 60 ya UNFPA Tanzania', kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanal Mstaafu, Issa Machibya, huku Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem akishuhudia tukio hilo.
IMG_6156
Malengo ya maendeleo endelevu sasa yamewafikia Kigoma. Pichani ni Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu, Issa Machibya na baadhi ya wakurugenzi katika ofisi ya mkuu huyo wa mkoa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Umoja wa Mataifa Dar es Salaam na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
IMG_6161
IMG_6172
IMG_6164
Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu, Issa Machibya akiagana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyemtembelea ofisini kwake kabla ya kuelekea kambi ya wakimbizi Nyarugusu.
KUELEKEA KWENYE UKAGUZI WA MRADI WA VIJANA UNAORATIBIWA NA ILO........
IMG_6198
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem wakisikiliza taarifa ya waratibu wa mradi wa Vijana unaoratibiwa Shirika la Nyakitonto Youth Development Tanzania la mjini Kigoma (NYDT) na kufadhiliwa na ILO katika kuwawezeshaji vijana masuala ya ujasiriamali.
IMG_6216
Meneja miradi wa shirika hilo, Anjelina Gulanywa, Angelina Guranywa akitoa taarifa kwa Mkuu wa UN Tanzania (hayupo pichani) na ugeni wake alioambatana nao.
IMG_6230
Malengo ya maendeleo endelevu sasa yamewafikia Shirika lisilo la kiserikali la Nyakitonto Youth For Development Tanzania mkoani Kigoma.
IMG_6242
Baadhi ya vijana walionufaika na mradi wa ILO wa kuwezesha vijana kuwa wajasiriamali kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali.
IMG_6250
Mratibu wa Shirika lisilo la kiserikali la Nyakitonto for Youth Development Tanzania, Joel Nyakitonto, akitoa maelezo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez jinsi utengenezaji wa sabuni kutokana mafuta ya mbegu za Mchikichi walipotembelea kiwanda cha Sabuni kilichopo tarafa ya Katubuka ambacho kinamilikiwa na kijana Diocres Dionizi (hayupo pichani) ambaye ni mmoja kati ya vijana 30 aliyenufaika na mafunzo ya Anzisha Biashara Yako (ABIYA) yaliyotolewa na taasisi hiyo kwa ufadhili wa Shirika la Kazi nchini (ILO).
IMG_6281
Wafanyakazi wa kiwanda hicho wakikusanya mbegu kwa ajili ya kukamuliwa kwenye mashine maalum.
IMG_6283
Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan akimtwisha ndoo ya mbegu za Mchikichi zinazokamuliwa na kupatikana mafuta yanayotengenezea sabuni za magadi mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi.
IMG_6291
Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem akimsaidia kujaza mbegu za Mchikichi mmoja wa wafanyakazi kiwandani hapo kwa ajili kuzichuja na kupata mafuta yanayotengenezea sabuni za magadi.
IMG_6307
Mwanamke aliyebeba mtoto wake mgongo huku akiwa amejitwishandoo yenye mbegu za Mchikichi kuelekea ndani ya kiwanda cha kusaga mbegu hizo zinazotoa mafuta yanayotumika kutengeneza sabuni za magadi kiwandani hapo.
IMG_6310
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akivaa koti maalum kwa ajili ya kuingia kiwanda kujionea jinsi kijana huyo anayotengeneza sabuni za magadi zinazotokana mafuta ya mchikichi. Kushoto mmiliki wa kiwanda hicho kijana Diocres Dionizi aliyenufaika na mafunzo ya ABIYA yaliyofadhiliwa na ILO.
IMG_6327
Mfanyakazi wa kiwanda hicho kitengo cha ufungashaji bidhaa, Eric Mwesiga (27) akimwelekeza Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (kushoto) namna wanavyopakia sabuni hizo kwenye mifuko maalum tayari kuingia sokoni.
IMG_6345
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem wakishuhudia maandalizi ya utengenezaji wa sabuni kiwandani hapo.
IMG_6353
Maandalizi yakianza kwa kumimina mafuta yaliyotokana na mbegu za mchikichi.
IMG_6395
Kijana Diocres Dionizi aliyenufaika na mafunzo ya ABIYA yaliyofadhiliwa na ILO akisaidiana na mfanyakazi wake Erick Mwesiga kumwaga mchanganyiko huo kwenye chombo maalum huku Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akishuhudia tukio hilo.
IMG_6398
Erick Mwesiga akichanganya rangi kwenye mchanganyiko ambao unakaa siku tatu mpaka kukauka na kupatikana sabuni za magadi.
IMG_6410
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem katika picha ya pamoja na Baba mzazi wa kijana Diocres Dionizi ambaye ni mjasiriamali wa sabuni.
IMG_6424
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwasili kuzindua eneo la heka 3 la rasilimali na kuwaanda vijana (Youth incubation centre) ambalo limetolewa na manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Nyakitonto Youth For Development Tanzania wanaojihusisha na kutoa mafunzo mbalimbali ya masuala ya ujasiriamali ikiwemo kuanzisha biashara.


Wimbo mpya wa BELLE 9 - BURGER MOVIE SELFIE

$
0
0
Huu ni wimbo mpya wa Belle 9 uliotoka Jumatatu Dec.7.2015. Audio imetengenezwa na Tiddy Hotter, na video pia imetopka na imefanyika Morogoro na producer aitwaye GQ ambaye pia ni wa Morogoro.

Mtaa Kwa Mtaa ya Michuzi tv na Changamoto ya vibaka jijini Mbeya

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MABALOZI WA MALAWI NA SWEDEN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Balozi wa Malawi hapa nchini Mhe. Hawa Ndilowe Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 8, 2015.
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Malawi hapa nchini Mhe. Hawa Ndilowe Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 8, 2015.
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimsindikiza na Balozi wa Malawi hapa nchini Mhe. Hawa Ndilowe baada ya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 8, 2015.

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipokea barua za salamu toka na Balozi wa Sweden hapa nchini Mhe. Katarina Rangnitt alipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 8, 2015.

VODACOM FOUNDATION YANOGESHA UZINDUZI WA MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO LEO

$
0
0
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni A.C.P Camillus Wambura(kushoto)akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia alipowasili ofisini kwake akiwa kama Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto leo katika viwanja vya Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Askari polisi na wanafunzi wa Shule ya Msingi Oysterbay na Mbuyuni wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe maalum wakati wa maandamano ya amani ya uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto leo katika viwanja vya polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo ulidhaminiwa na Vodacom Foundation.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Oysterbay na Mbuyuni wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe maalum wakati wa maandamano ya amani ya uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto leo katika viwanja vya polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo ulidhaminiwa na Vodacom Foundation.
 Askari wa jeshi la polisi kikosi maalum cha Kurasini jijini Dar es Salaam akiongoza maandamano ya amani ya uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto leo katika viwanja vya polisi Oysterbay.Uzinduzi huo ulidhaminiwa na Vodacom Foundation.

  Baadhi ya Askari polisi na wanafunzi wa Shule ya Msingi Oysterbay wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe maalum wakati wa maandamano ya amani ya uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto leo katika viwanja vya polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo ulidhaminiwa na Vodacom Foundation.
 Askari wa jeshi la polisi kikosi maalum cha kutuliza ghasia(FFU)cha jijini Dar es Salaam akiongoza maandamano ya amani ya uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto leo katika viwanja vya polisi Oysterbay.Uzinduzi huo ulidhaminiwa na Vodacom Foundation.
 Kamishina Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni A.C.P Emanuel J. Mley akiongea na wageni waalikwa waliofika katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto leo katika viwanja vya polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam,Kulia kwake ni Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia.Uzinduzi huo ulidhaminiwa na Vodacom Foundation.
 Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto,Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia akiongea na wageni waalikwa waliofika katika uzinduzi huo leo katika viwanja vya Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam,Kushoto kwake ni Kamishina Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni A.C.P Emanuel J. Mley.Uzinduzi huo ulidhaminiwa na Vodacom Foundation.
 Mkuu wa Dawati la Jinsia la Polisi Chuo kikuu cha Dar es Salaam,S.P Leah Mbunda(kushoto)akiteta jambo na Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto,Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia(kulia) wakati wa maadhimisho hayo,katika ni Mkaguzi msaidizi wa Polisi anayeshughulikia Dawati la Jinsia katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam,A/INSP Prisca Komba.

Kamishina Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni A.C.P Emanuel J. Mley(kulia)akijadiliana jambo na Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto,Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia,Wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika leo katika viwanja vya Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na Vodacom Foundation.

PANAFRICAN ENERGY YATOA YAFADHILI UJENZI WA WODI YA ‘MAMA NGONJEA’ HOSPITALI YA WILAYA KINYONGA KILWA KIVINJE NA KUKARABATI WODI ZA UZAZI NA CHUMBA MAALUM CHA UANGALIZI WA AKINA MAMA

$
0
0

Meneja Uwajibikaji kwa jamii kutoka Kampuni ya PanAfrican Energy Andrew Kangashaki (kushoto ) na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Twalib Mbasha wakikabidhiana mkataba wa miradi ya ujenzi wa nyumba ya mama ngojea katika hospital ya Kinyonga na ukarabati wa wodi ya uzazi mara baada ya kumaliza kusaini mikataba hiyo katika hafla fupi iliyofanyika jana Kilwa Kivinje.

Meneja Uwajibikaji kwa jamii kutoka Kampuni ya PanAfrican Energy Andrew Kangashaki(wa tatu kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Twalib Mbasha (wa tatu kulia) wakisaini makubaliano ya miradi miwili ya ujenzi wa mama ngojea ‘maternity waiting home’ yaani nyumba maalum kwa kina mama wajawazito watakaokua wakisubiri kujifungua itakayojengwa katika hospitali ya Kinyonga – Kilwa Kivinje na kukarabati wodi ya uzazi na chumba maalum cha uangalizi wa akina mama mara tu baada ya kujifungua katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko. 

Huku wakishuhudiwa na Mwanasheria wa Wilaya Mh. Godfrey Makary (wapili kutoka kulia), Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Juma Abdalah Njwayo(wa pili kushoto), Mbunge wa jimbo la Kilwa Kaskazini kupitia chama cha CUF Mh. Vedasto Edgar Ngombale(wakwanza kushoto) pamoja na Mbunge wa Kilwa Kusini kupitia chama cha CUF Selemani Bungawa a.k.a Bwege(wakwanza kulia).
Mbunge wa Kilwa Kusini kupitia chama cha CUF Selemani Bungawa a.k.a Bwege(wapili kulia) akitoa neno la shukrani kwa Kampuni ya PanAfrican Energy kwa niaba ya wananchi wa Kilwa Kusini mara baada ya makabidhiano ya mkataba wa miradi itakayowanufaisha wananchi wa kilwa.
Wafadhili wa mradi wa ujenzi wa wodi ya wazazi Kampuni ya PanAfrican Energy pamoja wakiwaonesha wanahabari chumba cha uzazi katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko ambacho kipo katika mradi uliosainiwa kati ya wilaya ya Kilwa na kampuni hiyo. Hii ni katika kuunga jitihada za serikali za kuboresha huduma za afya.
Hali halisi ya mazingira ya wodi ya wagonjwa katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko, hii ni wodi ya wanaume. Kiyuo hichi cha afya kilijengwa mwaka 1952 enzi za ukoloni mpaka sasa hakijawahi kukarabatiwa.


Wakisaini makubaliano ya miradi ya ujenzi wa mama ngojea na ukarabati wa chumba cha uzazi na wodi maalum ya uangalizi wa kina mama mara tu baada ya kujifungua wilayani Kilwa ni Meneja Uwajibikaji kwa jamii kutoka Kampuni ya PanAfrican Energy Andrew Kangashaki(wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Twalib Mbasha (wa pili kulia) wanaowashuhudiwa ni Mwanasheria wa Wilaya ya Kilwa Mh. Godfrey Makary ( kulia), Mkuu wa Wilaya ya hiyo Juma Abdalah Njwayo (kushoto) jana katika hafla fupi iliyofanyika jana katika hospitali ya Kinyonga Kilwa Kivinje.
Wanahabari wakihakikisha wanapata habari sahihi kutoka kwa wahusika.
Wauguzi wa Hospitali ya Kinyonga Kilwa Kivinje wakishuhudia makabidhiano ya mkataba wa miradi ya ujenzi wa mama ngojea ‘maternity waiting home’ utakaofanyika katika hospitali yao na mradi mwingine wa ukarabati wa wodi ya uzazi utakaofanyika katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko. Hafla hiyo ilifanyika hospitalini hapo jana.PICHA NA MICHUZI JR-MICHUZI MEDIA GROUP.


========= ======= ====== ==========

PANAFRICAN ENERGY KUTOA TSH .335,142,142 KUFADHILI UJENZI WA WODI ZA AKINA MAMA WAJAWAZITO WANAOSUBIRI KUJIFUNGUA ‘MAMA NGONJEA’ YAANI MATERNITY WAITIING HOME, HOSPITALI YA WILAYA ,KINYONGA KILWA KIVINJE NA KUKARABATI WODI ZA UZAZI NA CHUMBA MAALUM CHA UANGALIZI WA AKINA MAMA MARA TU BAADA YA KUJIFUNGUA KITUO CHA AFYA CHA KILWA MASOKO.

Wakazi wa Kilwa wana haki ya kuendelea na kuwa na matumani baada ya kushuhudia makubaliano ya miradi mingine mikubwa katika eneo lao kati ya Kampuni ya PanAfrican Energy na Wilaya ya Kilwa. Moja ya miradi hiyo ni ujenzi wa wodi ya kupumnzikia wakina mama wakisubiri kujifungua katika Hospitali ya Kinyonga iliyopo Kilwa Kivinje, na mradi mwingine ni ujenzi wa wodi ya wazazi na chumba maalum cha uangalizi wa akina mama mara baada ya kujifungua katika Kituo cha afya cha Kilwa Masoko. 


Katika hospitali ya wilaya , PANAfrican Energy watafadhili ujenzi wa wodi ya kusubiria akina mama, yaani mama ngonjea (maternity waiting home,) ambayo ni sehemu wanaposubiri akina mama ambao wanaweza kuwa kwenye uzazi hatarishi. Hii ni njia kuu ya kuondoa tatizo la umbali mrefu kama kikwazo cha akina mama kujifungua salama ambapo hivi sasa wakina mama hushindwa kufika mapema hospitalini kutokana na kutokuwa na chumba maalum kwa ajili ya kusubiria huduma ya kujifungua. 

Kuwepo kwa wodi ya kupumnzikia akina mama hawa hapa Kinyonga ni manufaa tosha ukiangalia hali halisi ya mazingira na miundombinu ya Kilwa. Pamoja na na kupunguza vifo vya akina mama wajawazito kwani watakuwa karibu na hospitali, pia itapunguza gharama kwani mama huyu anaweza kuchukua usafiri wa kawaida na kwa utaratibu wake na kwenda kusubiria.

Miradi hii miwili inaunga mkono jitihada za serikali za kuboresha huduma za afya nchini na imekuja muda muafaka ambapo serikali inachukua hatua kupunguza na kutokomeza kabisa vifo vya akina mama wajawazito na matatizo yanayotokana na ujauzito. Kutokana na utafiti uliofanywa mwaka 2009/10 nchini inaonesha kuwa wanawake 454 hufariki kwa kila 100,000, kila mwaka kutokana na matatizo yanayotokana na ujauzito.

Vifo vya akina mama wajawazito vinatokana na kutokwa damu nyingi wakati na baada ya kujifungua, utoaji mimba usio salama, shinikizo la damu, na kukosa uchungu wa kutosha au kukosa kabisa wakati muda wa kujifugua umefika .Uwepo mdogo wa sehemu za dharura na huduma kwa mtoto aliyezaliwa, ukosefu mkubwa wa watoa huduma za afya wenye ujuzi pamoja na mfumo duni wa rufaa, yote haya yanachangia kwa kiasi kikubwa vifo vya kina mama wajawazito.

Akiongea katika hafla ya kusaini makubaliano ya miradi hiyo leo kwa niaba ya Kampuni ya PanAfrican Energy, Meneja Uwajibikaji kwa jamii wa Kampuni ya PanAfrican Energy Bwana Andrew Kangashaki alisema, “Idadi ya vifo vya kina mama wajawazito imekua kubwa ya kutisha na tunataka kuwahakikishia wakazi wa kilwa kwamba ni kupitia miradi kama hii mabpo tunaweza kuwa sehemu ya kumaliza tatizo hili kwa pamoja.

Leo tena tunasaini makubaliano mengine na wilaya ya kilwa katika masuala ya afya; Tutafadhili miradi hii miwili yenye gharama ya Tshs 335,142,142. Moja ni nyumba ya kupumzikia kina mama wajawazito wanaosubiri kujifungua katika hospitali ya Kinyonga, Kilwa, ambayo itagharimu Tsh 220,292,430.00 huku wodi za wazazi katika kituo cha afya cha kilwa masoko kitagharimu Tsh 114,849,636.00.

Huu ni muendelezo wa kusapoti Nyanja za afya katika wilaya ya kilwa. Mwanzoni mwa mwaka huu kampuni ya PanAfrican Energy ilikamilisha ujenzi wa nyumba za wauguzi wa kituo cha affya cha Nangurukuru, ambacho hapo awali walikikarabati. Nyumba za wauguzi zilikabidhiwa mwezi Juni kwa mkuu wa wilaya ya Kilwa. 

“Lengo letu kuu ni kuchangia mafanikio ya kiuchumi na ya kijamii katika wilaya ambapo Kampuni inafanya kazi, kutambua na kuimarisha uhusiano usiotengeka kati ya ustawi wa biashara na ustawi wa jamii kwa kutimiza mahitaji yao. Tunawasikiliza wananchi wa Kilwa na kuyazingatia mahitaji yao kwa umaakini. “aliongeza, Bw.Andrew.

Naye Mkurugenzi wa wilaya ya kilwa Bw.Twalib Mbasha aliishukuru Kampuni ya PanAfrican Energy kwa jitihada kubwa wanazoendelea kuzifanya katika kuwawezesha wakazi wa kilwa. “Mmetuhakikishia kuwa mpo nasi, nyie ni washirika tunaweza kuwategemea katika Nyanja zinazogusa na kuhusu maisha yetu. 

Tunapenda kuwahakikishia kuwa tutakuwa pamoja katika kukamilisha miradi hii kuanzia mwanzo mpaka mwisho.” Alisema. Pamoja na wauguzi na wafanyakazi wa sekta ya afya wilaya ya Kilwa, pia walioshuhudia usainishaji wa makubaliano hayo ni Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Mhe. Juma Njwayo pamoja na wabunge wa Kilwa Mh.Vedasto Edgar Ngombale and Selemani Bungawa.

Mahojiano na DC Paul Makonda katika kipindi cha JUKWAA LANGU Dec 7 2015

$
0
0

Kipindi cha JUKWAA LANGU hukujia kila Jumatatu kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Marekani ya Mashariki kuijadili Tanzania ya sasa na ile tuitakayo
Katika kipindi hiki, tumeungana na Mhe Paul Makonda. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jiji Dar Es Salaam ambaye mbali na mambo mengine, ameeleza "ya moyoni" kuhusu tofauti iliyopo kati ya utendaji wa Rais wa awamu ya nne Mhe Jakaya Kikwete (aliyemteua katika wadhifa huo) na Rais wa sasa Dk John Magufuli. Kabla ya hapo aligusia namna alivyoteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya, na kwanini anaamini inastahili kuwepo namna nzuri zaidi ya kuteua watu katika nafasi kama yake.

Na kabla ya hayo yote, alizungumzia migogoro mbalimbali inayoendelea wilayani mwake kama wa kiwanda cha Urafiki, kubomolewa kwa nyumba za thamani, mgogoro wa Coco Beach nk.Na kama ilivyo desturi, akapokea maswali na ushauri toka kwa wasikilizaji wetu
KARIBU

CCM YAIPONGEZA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KWA KASI ILIYOANZA NAYO

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM),Ndugu  Abdulrahman O.Kinana(Pichani) akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais,Dkt.John Pombe Magufuli,Makamu wa Rais,Mhe.Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu,Mhe.Kassim Majaliwa kwa kasi nzuri waliyoanza nayo katika utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 8, 2015, katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiendelea kumsikiliza Ndugu Kinana alipokuwa akizungumza mbele yao mapema leo mchana jijini Dar.


Na Bakari Issa Madjeshi.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais,Dkt.John Pombe Magufuli,Makamu wa Rais,Mhe.Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu,Mhe.Kassim Majaliwa Kassim kwa kasi nzuri waliyoanza nayo katika utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho.

Kutokana na Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika Desemba 07,2015 jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM,Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,kikao hicho kilipokea taarifa juu ya utendaji wa Serikali katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020.

Akitoa pongezi hizo kwa niaba ya Chama,Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu  Abdulrahman O.Kinana amesema Kamati Kuu imeunga mkono hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuhakikisha Ilani ya Uchaguzi ya  Chama hicho kwa mwaka 2015-2020 inatekelezwa kwa ufanisi.
Pia,Kinana amesema Kamati Kuu ya Chama inapongeza na kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika kusimamia vyanzo vya mapato ya Serikali ikiwa ni kuhakikisha Mamlaka ya Mapato(TRA) na Mamlaka ya Bandari Nchini(TPA) zinasimamia ukusanyaji wa kodi za Serikali ipasavyo.

Hata hivyo,Ndugu Kinana amesema pamoja na  kuunga mkono na kupongeza kasi waliyoanza nayo,Rais Magufuli,Makamu wa Rais na Waziri Mkuu,Kamati  Kuu inawataka viongozi wengine wote kuiga mfano huu mzuri na kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ipasavyo.

KAMANDA MPINGA AONYA WENYE MABASI KUONGEZA NAULI, AZINDUA HUDUMA FASTA FASTA KWA BODABODA

$
0
0
 Kamanda wa Polisi wa kikosi cha usalama Barabarani nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi, Mohammed Mpinga, akipata maelezo jinsi ya kujiunga na huduma mpya kwa abiria wa bodaboda inayopatikana kwa njia ya mtandao wa simu za mikononi ijulikanayo kwa jina la “Fasta Fasta Services”. Huduma hiyo umwezesha abiria kupata huduma ya usafiri huo kwa kufuatwa mahali alipo. Picha/Mpiga Picha wetu
Kamanda wa Polisi wa kikosi cha usalama Barabarani nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi, Mohammed Mpinga pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Fasta Fasta, Prasad Acharya wakizindua huduma mpya kwa abiria wa bodaboda inayopatikana kwa njia ya mtandao wa simu za mikononi ijulikanayo kwa jina la “Fasta Fasta Services”. Huduma hiyo umwezesha abiria kupata huduma ya usafiri huo kwa kufuatwa mahali alipo.

Na Mwandishi wetu.
KAMANDA wa Polisi wa kikosi cha usalama Barabarani nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi, Mohammed Mpinga ametoa onyo kwa wamiliki na mawakala wa usafiri wa mabasi yaendayo mikoani kutoongeza nauli kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka na wakibainika watachukulia hatua za kisheria pamoja na kufungwa jela.

Kamanda Mpinga alisema hayo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya kwa abiria wa bodaboda kwa njia ya mtandao wa simu ya mkononi ijulikanayo kwa jina la “Fasta Fasta Services” ambayo umwezesha abiria kupata huduma ya usafiri huo kwa kufuatwa mahali alipo.

Alisema kuwa imekuwa tabia ya wamiliki na mawakala wa usafiri wa mabasi yaendayo mikoani kuongeza nauli kinyume na sheria na taratibu zilizowekwa.

Alisema kuwa ili kuwabaini wanao kiuka sheria hiyo, wameweka askari kanzu vituo vyote vya mabasi yaendayo mikoani kwa lengo la kuwakamata wahusika.

“Tumejipanga nchi nzima kukomesha uhalifu huu, si kwa kituo cha mabasi cha Ubungo tu, bali nchi nzima, tumewapandikiza abiria ambao watakuwa na kazi ya kutoa taarifa za kuwakamata wahusika,” alisema Mpinga.

Aalifafanua kuwa mwaka jana, wamiliki na mawakala watano walifungwa jela kwa kosa kama hilo na mwaka huu wamedhamilia kuona kila mmiliki wa mabasi na mawakala wao wa ukatishaji tiketi wanashughulikia suala hilo.

Kuhusiana na huduma ya usafiri wa bodaboda ya Fasta Fasta, Kamanda Mpinga alisema kuwa huduma hiyo inawarahisishia madereva wa bodaboda kuweza kuongeza kipato, kuondoa uhalifu na usalama wa mali zao.

Alisema kuwa huduma hiyo itamwezesha dereva na abiria kujuana na hata tatizo linapotokea, ni rahisi kujua nani wa kumkamata kwa ajili ya masuala mengine ya kisheria.

“Huduma ina mwezesha abiria kupata usafiri mahala popote alipo, anatakiwa kujiunga kupitia simu yake ya mkoni kwa ‘kudownload application’ na kuzijua bodaboda zote zilizomo katika huduma hiyo na kutuma ujumbe mahali ulipo na unataka kwenda wapi, dereva wa bodaboda atakujibu na atakuja kukuchukua mahali ulipo na hata nauli italipa kwa umbali wa kilometa,” alifafanua Mpinga.

Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Fasta Fasta, Prasad Acharya alisema kuwa kwa kuanza wameanza kuzindua huduma hiyo Dar es Salaam na baada ya mwezi Februari mwakani, watapanua wigo kwa kuzindua huduma hiyo mikoani.Acharya alisema kuwa mbali na pikipiki, huduma hiyo pia itazinduliwa kwa bajaji na taksi katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

Tume ya Haki za Binaadamu yaandaa Mpango Endelevu kufikia malengo ya Millenia

$
0
0

hk1 
Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tume ya Haki za Binadamu Bi. Rehema Ntimizi akiongea na wadau hawapo pichani walioshiriki katika kongamano la kujadili malengo endelevu kufikia malengo ya Milenia jijini Dar es salaam leo.
hk2 
Mkurugenzi wa Tume ya Haki za Binadamu Bw. Francis Nzuki akiongea na waandishi wa habari katika kongamano la kujadili malengo endelevu kufikia malengo ya Milenia jijini Dar es salaam leo.
hk3 
Wadau kutoka sehemu mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja waliposhiriki kongamano la kujadili malengo endelevu kufikia malengo ya Milenia jijini Dar es salaam leo.
hk4 
Wadau kutoka sehemu mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja waliposhiriki kongamano la kujadili malengo endelevu kufikia malengo ya Milenia jijini Dar es salaam leo.

………………………………………………………………………………………..
Na Shamimu Nyaki¬¬-MaelezoDar es salaamKatika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu duniani ambayo ni tarehe10 Disemba mwaka huu,Tume ya haki za binadamu na Utawala bora leo imeandaa kongamano la siku moja kujadili Mpango wa Maendeleo Endelevu unaotarajia kuanza rasmi januari mwaka2016.
  Mgeni Rasmi katika kongamano hilo Bi Rehema Ntimizi kutoka Tume ya haki za binaadamu ameiomba jamii kushiriki kwa ukamilifu katika kuleta maendeleo yao wenyewe na taifa kwa ujumla kwa kuwa maendeleo yanaanza na watu wenyewe kwa kuhakikisha wanaondokana na umasikini,kuwa na afya bora ,pamoja na elimu na kutambua kuwa ni haki yao kuwa na uwelewa wa suala hilo.“Binadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa hivyo wote tuwajibike katika maendeleo”Alisema bi Ntimizi.
 Bi Rehema ameongeza kuwa dunia nzima kwa sasa inashirikisha makundi yote katika jamii katika kutoa maamuzi hasa yale yaliyosahaulika kama wanawake,wazee na watoto waishio vijijni hivyo wakati umefika sasa kwa kila mtu katika jamii kushiriki hatua zote za maendeleo.
 Akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano la kujadili mpango huo leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Tume ya haki za Binaadamu bw Francis Nzuki ameeleza kuwa lengo la kongamano hilo ni kujadili mpango huo wa maendeleo endelevu jinsi gani utaleta matokeo chanya katika kufikia malengo ya millenia ifikapo mwaka 2030.
 Ameongeza kuwa mpango huo umejikita katika malengo kumi na saba ambayo miongoni mwao ni kuondoa umaskini,kutoa Elimu bora, afya bora pamoja na maji safi kwa kila kundi lililopo katika jamii ambao ni vijana,wazee, wanawake, pamoja na watoto katika jamii ya Watanzania ili kuweza kufikia malengo ya millenia.
 Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa Tume itaanzisha utaratibu wa kutembelea hospitali za umma kuanzia ngazi ya mkoa hadi kijiji ili kuweza kubaini malalamiko na changamoto wanazopata wananchi ,lakini pia kutoa elimu jinsi watakavyoweza kusaidiwa na tume pale wanakutana na changamoto katika suala linalohusu haki na utu wao.
 Kauli mbiu katika kongamano hilo ni “Haki zetu uhuru wetu daima”.Aidha mshiriki kutoka shirika linalowahudumia wazee linaloitwa Helpage Intanational Fund Bw Joseph Mbasha amesema kuwa wazee wanapaswa kushirikishwa katika masuala yote ya maendeleo kwa kuwa nao ni binaadamu na wana uhuru wa kutoa mawazo na kupewa afya bora, kuondokana na umaskini lakini pia kumiliki ardhi.“Kila mmoja ashiriki katika maendeleo yake na Taifa kwa ujumla”Alieleza Mbasha.
 Kongamano hilo limehudhuriwa na wadau mbalimbali wa haki za binaadamu wakiwemo Haki Elimu,YUNA,Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP),Chuo kikuu cha Dar es salaam pamoja na Chuo cha Uhasibu.

SERIKALI YATOA UFAFANUSI KUHUSIANA NA KUADHIMISHA SIKU YA UHURU HAPO KESHO

U15 YAREJEA DAR

$
0
0
ZIARA ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) iliyoanzia kanda ya ziwa na kanda ya Magharibi kisha kuendelea katika nchi za Rwanda, Uganda na Kenya mwezi huu imesitishwa kutokana na kufungwa akaunti za Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).

Timu hiyo ya vijana iliondoka wiki iliyopita kuelekea jijin Mwanza, ambapo iliagwa na kukabidhiwa bendera ya Taifa na katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel, ilicheza mchezo mmoja wa kirafiki na timu ya Alliance kabla ya kuelekea mkoani Kigoma.

Ikiwa Kigoma U-15 ilicheza michezo miwili ya kirafiki na timu ya kombaini ya mkoa wa Kigoma U-15, jumapili ikacheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya Burundi U-17, na jana asubuhi kuanza safari ya kurejea jijini Dar essalaam.

Awali ziara ya timu hiyo ya U-15 ilikua iendelee katika mji wa Kigali kwa kucheza na U17 ya Rwanda, Kampala kucheza na Uganda U17, jijini Nairobi kwa kucheza na U17 ya Kenya na kumaliza ziara hiyo kwa kuchez ana U15 kombaini ya mkoa wa Arusha Disemba 23, na kurejea jijin Dar es salaam Disemba 24, 2015.

U-15 inajiandaa na michuano ya Viajana U17 kuwania kufuzu kwa Mataifa ya Afrika mwaka 2017 nchini Madagascar itakayoanza kutimua vumbi Juni 2016.

MFUMUKO WA BEI WA NOVEMBA UMEONGEZEKA KWA ASILIMIA 6.6

$
0
0
 Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Epharaim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari juu ya mfumuko wa bei kwa mwezi Novemba ambao umefikia asilimia 6.6 leo jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Meneja wa  Mfumuko wa Bei wa NBS , Ruth Minja.
 02.Waandishi wa habari wakifatilia taarifa kutoka Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu,Epharaim Kwesigabo  hayupo picha leo jijini Dar es Salaam 
(Picha na Chalila Kibuda wa Globu ya Jamii)
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Epharaim Kwesigabo jijini Dar es Salaam leo.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa  Novemba 2015 umeongezeka hadi asilimia 6.6 kutoka asilimia 6.3  ya Oktoba mwaka huu.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu,Epharaim Kwesigabo amesema kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Novemba.
 
Kwesigabo amesema mfumuko wa bei wa bidhaa ya za vyakula na vinywaji  Baridi  Novemba mwaka imeongezeka  kwa asilimia 11.2 kutoka asilimia 10.2 tofauti na mwezi uliopita.
 
Amesema kuongezeka kwa Mfumuko wa bei wa Novemba 2015  kumechangiwa na kuongezeka kwa baadhi ya bidhaa za vyakula kwa  kipindi cha mwezi uliopita zikilinganishwa na bei za Novemba mwaka jana.
 
Aliongeza kuwa mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoonesha kuongezeka Novemba 2015 ukilinganishwa na bei za Novemba 214  ni pamoja na mchele kwa asilimia 25.8, Mahindi asilimia 16.4, unga wa mahindi asilimia 12.0  nyama asilimia 8.7, Samaki asilimia 21.4, Mharagwe asilimia 14.5  Choroko asilimia 15.3 Mihogo asilimia 10.7  pamoja na viazi vitamu 23.4.
 
Kwesigabo amesema kuwa uwezo wa sh.100 katika kununua bidhaa na huduma umefikia sh.62.31 mwezi Novemba, 2015 kutoka Septemba 2010  ikilinganishwa na Sh. tofauti na Novemba mwaka jana sh.100 uwezo wake ulikuwa ni sh.62.82  ilivyokuwa Oktoba 2015.

Mfumuko wa bei  Afrika Mashariki,nchi ya Kenya  kwa Novemba imeongezeka kwa asilimia 7.32, kutoka asilimia 6.72 ya  Oktoba mwaka huu, Uganga imeongezeka hadi asilimia 9.1kutoka asimia 8.8 ya mwezi uliopita  hali hiyo inafanya nchi ya Uganda kuwa ya kwanza kwa kuongeza mfumuko wa bei.

NAPE AWAPA MAKATIBU KATA WA JIMBO LAKE PIKIPIKI

$
0
0

 Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye akimkabidhi Katibu wa kata ya Mtua Kilimahewa funguo ya pikipiki kwa niaba ya makatibu kata 20 wa jimbo hilo ambao wote wamewezeshwa usafiri wa pikipiki ili kurahisisha ufanisi wa kazi zao.
 Mbunge wa Jimbo la Mtama (CCM) Nape Nnauye akijaribu moja ya pikipiki kati ya 20 alizowapa makatibu kata ili ziweze kuwasaidia kufanya kazi kwa ufanisi kwenye shughuli zao za kujenga na kuimarisha Chama Cha Mapinduzi.
 Sehemu ya pikipiki zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye kwa makatibu kata 20 wa jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye akizungumza mbele ya viongozi wa CCM wilaya ya Lindi vijijini ambapo aliwaambia viongozi hao kuwa amejipanga kufanya kazi katika jimbo hilo zenye kuleta tija na kuhakikisha anatekeleza ahadi zote alizozitoa wakati wa kampeni na kuwata makatibu kata waliokabidhiwa pikipiki 20 kuzitumia katika kazi za kujenga na kuimarisha chama.

SERIKALI YA JPM KIBOKO, "UKIBEEP WANAPIGA", DKT MPANGO ATINGA TRA SAMORA BAADA YA MWANANCHI KUTUPIA UJUMBE MTANDAONI

$
0
0
KUNA ule msemo wa watu wa mjini, "Uki-beep, napiga" na kweli leo hii Desemba 8, 2015 pale Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA, barabara ya Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam, mlipa kodi mmoja alitupia ujumbe kwenye mtandao wa kijamii akiomba wataalamu wa IT wa TRA, wafike haraka kwenye ofisi zao za TRA Barabara ya Samora kwani mitambo ya ku-print Motor Vehicles License ime-collapse", na watu wamekaa tu wasijue la kufanya.
ilichukua kama dakika 15 au 20 hivi, watu wawili waliovalia suti maridhawa na dada mmoja "aliyeshiba", walitinga kwenye ofisi hizo, na kukuta walipa kodi wakiwa wamejazana kwenye mabenchi wakijipepea tu, kutokana na joto kali.
Mmoja wa watu hao waliovaia suti, alianza kuwauliza walipa kodi, "Jamani vipi huduma za hapa mnaridhika nazo."? Aliuliza mmoja wao.
Walipa kodi hao kwanza walimtazama, na mmoja "akajilipua", hapana haturidhiki nazo, hapa unapotuona tumeshakaa sana, huduma hakuna tunaambiwa mtandao haupo, tumeshindwa kuchapishiwa stika za malipo ya kodi ya barabarani.
Mwingine akasema, hata hali ya hewa humu ndani kama unavyoiona joto kali, hakuna viyoyozi, na tumekuja kulipa kodi hii ni sawa??, akahoji mlipa kodi huyo.
Baada ya majibu hayo, Mlipa kodi mmoja aliibuka na kuwaambia wenzake, jamani semeni huyo ndiye bosi mpya wa TRA, "tiririkeni" yaani semeni, na hapo malalamiko yakawa mengi, naye bosi huyo ambaye si mwingine bali ni Dkt. Philip Mpango, ambaye hivi karibuni,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, alimteua kukaimu nafasi ya Kamishna Mkuu wa TRA, akiziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Kamishna Rished Bade, akawajibu, nimeyapokea malalamiko yenu, na ndiyo maana mmeniona niko hapa, nilipokea ujumbe kutoka kwa mlipa kodi akilalamika kuwa hapa kwenye tawi letu huduma zimesimama, nikaona nfike kujua nini kimetokea. Alisema Dkt. Mpango akiwaambia walipa kodi hao ambao walionekana kufurahishwa na maneno hayo.
Wakati akiwaeleza hayo, mitambo hiyo ghafla ikaanza kufanya kazi na waliokuwa jirani na madirisha walianza kuitwa mmoja mmoja na kupatiwa huduma.Hiyo ndiyo serikali mpya ya awamu ya tano yenye kauli mbiu "Hapa Kazi Tu", hakuna kulala kila mtu anapiga kazi tu.
 "figisu figisu" ya kile wafanyakazi wa hapo waliwaambia wateja wao kuwa "system iko down", yaani kwa maana ambayo wao wamezoea kuwaambia wateja kuwa mtandao wa computer haufanyi kazi kwa hivyo walipa kodi kibao waliokuwepo kwenye ofisi hizo, walilazimika kukaa tu kwenye mabenchi wakimuomba mungu mtandao huo upone ili waweze kupata "stika" za magari yaani Motor Vehicles License .
Pichani Dkt. Mpango (kushoto), akizungumza na walipa kodi hao kwenye tawi la TRA, barabara ya Samora Desemba 8, 2015

VIINGILIO VYA KRISMASI VYATAJWA

$
0
0
 KAMPUNI ya Msama Promotions ambayo ni waandaaji wa Matamasha ya Pasaka na Krismasi, imetangaza viingilio vya juu kwenye Tamasha la Krismasi kuwa ni Shilingi 50,000 kwa viti maalum, Tamasha ambalo litafanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo linalokwenda na shukrani kwa Mungu baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 ambako kabla, Msama waliandaa tamasha la Kuombea Amani uchaguzi Mkuu lililofanyika Oktoba 4 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama VIP watachangia shilingi 10,000 na viti vya kawaida watachangia shilingi 5000.Msama alisema watoto watakaohudhuria tamasha hilo watachangia shilingi 2000, alitoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo ambalo lina lengo la kurudisha shukrani kwa Mungu baada ya kupita kwenye uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu.

"Watanzania tujitokeze kwa wingi ili turudishe shukrani kwa Mungu baada ya kutupitisha katika uchaguzi Mkuu ambao ulikuwa tofauti na chaguzi zilizopita, hivyo ni nafasi yetu kumwambia Mungu asante baada ya kutupitisha katika tukio hilo muhimu," alisema Msama.

Aidha Msama michango inayopatikana kupitia viingilio hivyo hurudisha kwa Jamii yenye uhitaji maalum kama yatima, walemavu, wajane na wengineo wenye uhitaji kama huo.Msama alisema maandalizi ya kuelekea tamasha hilo yanakwenda vizuri, huku waimbaji kama Rose Muhando, Upendo Nkone, Ephraim Sekeleti, Rebecca Malope, Kwaya ya Wakorintho Wapili, Joshua Mlelwa na Christina Shusho wamethibitisha kushiriki tamasha hilo.

WATEJA WA AIRTEL KUONA VIDEO ZA YOUTUBE BURE WAKIJIUNGA NA YATOSHA INTANETI

$
0
0
 Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa kifurushi nafuu cha ‘Yatosha Intaneti’ na ubia kati ya kampuni hiyo na Google ambapo mteja wa Airtel ataweza kupata huduma ya kutazama video zilizopo You Tube Bure. Kulia ni Meneja wa Huduma za Intaneti wa Airtel, Erick Mshana. 
 Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) na Meneja wa Huduma za Intaneti wa Airtel, Erick Mshana wakizindua kifurushi nafuu cha ‘Yatosha Intaneti’ na ubia kati ya kampuni hiyo na Google ambapo mteja wa Airtel ataweza kupata huduma ya kutazama video zilizopo You Tube Bure katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

· Airtel waingia ubia na Google kuwezesha wateja kucheki video BURE 
· Bure kupitia vifurushi vya Yatosha intaneti 

KAMPUNI inayoongoza katika mtandao wa intaneti Tanzania, Airtel leo imeungana na Google katika kuwapatia wateja huduma yakutazama video mbalimbali zikiwemo zile za kiswahili BURE kupitia You Tube mara tu wanapojiunga na vifurushi vya Yatosha intaneti. 

Airtel imetangaza kuwapatia wateja wake ofa hiyo ya kuona video za You Tube BURE mara baada kuzindua kifurushi nafuu cha YATOSHA INTANET, Airtel imeeleza kuwa huduma hiyo ya BURE ni muendelezo wa dhamira yao ya kutoa huduma bora za intaneti kwa wateja wake zaidi ya milioni 10 nchini Tanzania ambapo wateja wa Airtel watakaojiunga na YATOSHA INTANET sasa wataweza kujipatia maudhui ya video nzuri wapendazo bila kufikiria tena gharama. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa huduma za inteneti wa Airtel Tanzania Gaurav Dhingra, alisema, "dhamira yetu siku zote ni kuendelea kuwa karibu na wateja wetu, kuelewa mahitaji yao na kuweza kuwapatia huduma bora yenye viwango vinavyohitajika.”

“Tunafahamu vizuri kwamba wimbi la uhitaji wa huduma hii ni kubwa kwa sasa, ongezeko la wanaokupakua au kuona video za aina mbali mbali zikiwemo michezo, muziki, habari za aina mbalimbali kupitia You Tube imeongezeka kwa kasi sana kutokana na wateja wetu wanavyoridhishwa na huduma zetu bora za intaneti.” Alieleza Dhingra 

Bw Dhingra akiendelea kufafanua alisema “Hata hivyo, watumiaji wa huduma hiyo ya kutazama au kupakua video hizo bado wamekuwa na kikwazo cha kufikiria swala la gharama na kutofurahia ubora wa video hizo, hivyo basi Airtel tumeamua kuwapatia wateja wetu MB’s za BURE kupitia You Tube ili waweze kufurahia kuangalia Video kupitia intaneti ya Airtel ".

Charles Murito, Meneja mwakilishi wa google nchini Tanzania, alisema ; "Tunataka kuhakikisha kwamba watumiaji wa simu za mkononi wanaongezeili na kufurahia huduma za You Tube nchini. Kwa kushirikiana na Airtel tutahakikisha kwamba wateja wote wa simu za mkononi wanaweza kutumia simu zao kwa kuangalia video kwa urahisi zaidi na kwa gharama nafuu wakiwa mahali popote. Vile vile watafurahia kutumia You Tube ikiwa na maudhui ya lugha ya Kiswahili na kuweza kufurahia mambo mbalimbali kwenye muziki, habari za biashara, burudani na elimu " .

Akielezea jinsi ya mteja kuweza kujiunga na vifurushi hivyo, Afisa huduma za intaneti wa Airtel Tanzania Erick Daniel Mshana, alisema “mteja wa Airtel wa malipo ya awali anaweza kupata huduma hii kwa kupiga *149*99# kisha kujiunga na kifurushi cha Yatosha intaneti na atafurahia huduma yetu ya Intaneti aliyojiunganayo ikiwa ni ya SIKU, WIKI, au MWEZI na zaidi ataona video za You Tube BURE. 


Airtel pia tuwakaribisha wadau mbalimbali wanaotengeneza na kusambaza video kwa njia ya mtandao kushirikiana nasi kufikisha video zako kwa jamii kupitia OFA hii. Kama wewe ni mtoa huduma wa video, unaweza kuwasiliana nasi kupitia Airtel huduma kwa wateja".
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images