Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 703 | 704 | (Page 705) | 706 | 707 | .... | 1898 | newer

  0 0

  HI1 
  Vifaa  vyote vya kutangazia katika Studio ya Hits FM Radio vilivyoteketea kwa moto usiku wa juzi  katika studio hiyo mara baaada ya kuvamiwa na watu wasipjuulikana  huko Migombani Mjini Zanzibar
  HI2 Waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini maelezo yanayotolewa na Mkuu wa kituo cha  Hits FM Mohammed Abdallah hayupo pichani mara baada ya kuunguzwa kituo cha  Radio hiyo.
  HI02Mwandishi  wa habari akimuhoji Mkuu wa Utawala wa Afisi kuu ya CCM FM Salum Khatibu Reja alipofika katika kituo cha Radio ya Hits FM na kujionea hali ya kituo hicho.
  HI3 
  Waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini maelezo yanayotolewa na Mkuu wa kituo cha  Hits FM Mohammed Abdallah hayupo pichani mara baada ya kuunguzwa kituo cha  Radio hiyo.
  HI4 
  Mwenyeki ti wa MCT Suleiman Seif katikati akifafanuwa  jambo  kwa waandishi wa habari kuhusiana  na kutiwa moto  Hits FM Radio  usiku wa juzi iliyopo Migombani Mjini Zanzibar. 

  0 0

   Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene akifunga Mkutano wa 10 wa  uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo jana. Tanzania imepata heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo baada  ya  kuonekana kufanya vizuri katika uhamaji wa matumizi ya mfumo wa analogia kwenda digitali kwa wakati.
   Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene (katikati) akiwaonesha jambo kupitia Kitumi chake cha Mkononi (IPAD) Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Ally Simba (kulia) na Naibu Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Bw. Fredrick Ntobi (kushoto) kabla ya kufungwa kwa Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es salaam.
   Washiriki wa Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano huo jijini Dar es salaam.
  Mada mbalimbali zikiwasilishwa kwa washiriki wakati wa  Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es salaam.Picha Aron Msigwa - MAELEZO.

  0 0

    Pichani Mbunge wa jimbo la Mafinga mji ni Cotato Chumi akimkabidhi msaada wa vitanda ,magodoro pamoja na vifaa mbalimbali kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Mafinga Dk Abdul Msuya juzi
  Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatiliwa ugawaji wa vifaa hivyo wakati wa makabidhiano
  Mbunge wa mafinga mjini Cosato Chumi akikabidhi vifaa hivyo kwa vitendo
  Baadhi ya wadau na wanachama wa chama cha mapinduzi ccm walihudhulia tukio hilo .
  …………………………………………………………………………………..
   
  TATIZO la upungufu wa vitanda katika wodi ya
  akina mama na watoto
  katika hospitali ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
  ambalo kwa muda mrefu limekuwa chanzo cha msongamano na uwalazimu
  baadhi ya wagonjwa kulala sakafuni sasa limepatiwa ufumbuzi baada ya
  uongozi wa hospitali hiyo kupokea msaada wa vitanda na vifaa tiba kutoka
  kwa mdau wa maendeleo katika sekta ya afya.

  Mbunge wa Mafinga Mjini (CCM) Cosato Chumi alisema kuwa kwa muda mrefu hospitali hiyo ilikuwa ina upungufu wa vifaa mbalimbali ikiwemo vitanda hali iliyofanya kuandika maandiko mbalimbali kwa wahisani  wa nje ya nchi ili kuweza kumsaidia kupata vifaa hivyo .
    
  Alisema kuwa umefika wakati sasa wadau mbalimbali, mifuko ya kijamii na makampuni kujenga utamaduni wa kusaidia watu wenye mahitaji mbalimbali wakiwemo watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na wagonjwa hospitalini kwani kufanya hivyo ni sehemu ya kurudisha kile wanachokitapa kwa jamii.
   
  “Unajua afya ni kila kitu katika maisha ya binadamu hivyo lazima nitekeleze ahadi zangu nilizotoa wakati wa kampeni na wanachi lazima tufanye kazi kwa kujituma ili tumuunge mkono rais wetu ambaye anania ya ya kutuletea maendeleo na kuwataka wadau mbalimbali kusaidia jamii zenye mahitaji na kuacha kutegemea serikali pekee “ alisemaChumi aliwaomba wananchi wa jimbo hilo kuunga mkono kwa kufanya kazi kwa nguvu zote ili walete maendeleo kwa pamoja maana akifanya kazi pekee yake bila wao hawezi kuleta maendeleo pekee yake.
    
  Msaada huo wa vitanda 16 na magodoro 11 na vitu
  mbalimbali umetolewa
  na taasisi binafsi inayojishughulisha na masuala ya
  afya ya nchini Astralia ijulikanayo kama “Rafiki Surgical Mission” kwa
  uratibu wa ofisi ya mbunge wa jimbo la Mafinga mjini 
  Alisema kuwa msaada huo aliopatiwa  na rafiki zao hawajatoa hata
  senti
  tano bali huwa marafiki hao wanachangishana fedha na kununua vifaa
  hivyo na kisha kuvisafirisha mpaka bandari kavu ambapo hapo ndio hutumia
  garama kusafirisha vifaa hivyo mpaka sehemu husika
  “Ndugu
  zangu nadhani kila mmoja alikuwa akifahamu machungu waliyokuwa wakipata
  mama zetu wanapokuja kujifungua kwa kukosa sehemu za
  kujifungulia lakini
  leo hii msaada huu utatusaidia sana na yoyote atakayeguswa na anaweza kuja na kuchangia chochote maana mufindi ni yetu sote na mufindi itajegwa na wanamufindi wenyewe”alisema

  Alisema jambo kubwa lilokuwa likimuumiza kicha kila kukicha ni tatizo la vifaa
  katika hospital, elimu  pamoja na tatizo la maji hivyo ni
  wakati
  wawanamafinga kushikana kwa pamoja katika kusumkuma mbele gurudumu la maendeleo ili kuendana na kauli mbiu ya sasa ya HAPA NI KAZI TU.
  Akipokea msaada
  huo kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Mafinga dk Abdul Msuya alisema
  kuwa msaada wa vitanda hivyo na magodoro na  vifaa
  mbalimbali
  utakuwa umemaliza kabisa tatizo la vitanda hospitalini hapo licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kumalizika endapo kutatokea mdau mwingine kuwasaidi Kwa upande wake katibu wa ccm wilaya ya Mufindi Jimsoni Muhagamaalimpongeza
  mbunge huyo kwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo huku akimwambia kuwa
  ni wakati wa kutekeleza kazi kwa vitendo na wala si
  maneno kwani
  wananchi wanapaswa kutatuliwa kero mbalimbali zinazowakabili badala ya kupiga porojo zisizo na msingi .
  Mhagama
  alisema kuwa kila mmoja anapaswa kuwajibika ipasavyo katika nafasi yake
  kwani kasi anayokwenda nayo Rais John Magufuli si ya
  mchezo bali ni ya
  mchaka mchaka na ili nchi iweze kusimama katika mstari ulionyoka kila mmoja anapaswa kucheza wimbo wa mchaka mchaka
  ‘’Huuu si
  wakati lelemama huu sio wakati mchezo mchezo ni wakati wa uwajibikaji
  ,hakika Tanzania tumepata kiongozi mchapa kazi tazama sasa
  ni siku ya 27
  nchi inaongozwa na watu wanne lakini kila sektaa imenyoka na mimi  nasemaa Magufuli wanyooshe tu kwa kuwa watu walikuwa wakifanya kazi kwa mazoeya bila ya kuangalia madhara wanayopatawatanzania
  swengi
  Hata
  hivyo Mhgama alisema kuwa kwa kuwa kipindi cha muda mchache nchi inaongozwa
  na watu wachache na nchi imesimama haoni sababu ya kuwa na
  baraza kubwa
  la mawaziri bali Rais Magufuli achague baraza dogo kamala watu
  10 ili kupunguza mzigo kwa serekali yake ya kuwa na mawziri wengi
  wasiokuwa na tija  .

  0 0


  0 0
 • 12/04/15--05:30: Article 9


 • 0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais wa China, Xi Jinping, wakati wa Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye kitambaa cheupe) akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye kitambaa cheupe katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wakuu wa Nchi za Afrika baada ya ufunguzi wa Mkutano huo Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwa katika mazungumzo na Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi, walipokutana kwenye ufunguzi wa Mkutano huo Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Shulu Hassan, akisalimiana Mwambata wa Kijeshi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini (Defence advisor) Brig. Gen Ibrahim A. Kimario, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Olver Tambo jijini Johanesburg jana Desemba 3, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Radhia Msuya.

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Shulu Hassan, akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Radhia Msuya, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Olver Tambo jijini Johannesburg jana Desemba 3, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China.

   Baadhi ya washiriki katika Mkutano huo kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo leo jijini Johannesburg. 
  Picha na OMR.

  0 0

  Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Sayansi na Tekinolojia Priska Olomi (kushoto) , akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam leo, kuhusu kutungwa kwa kanuni za huduma za ziada kwa makampuni ya simu nchini zitakazo walinda watumiaji wa huduma hizo,kulia ni Mkuu wa kitengo cha Sheria wa Wizara hiyo,Veronika Sudayi.
  (Picha na Hassan Silayo)

  0 0

  Watendaji wa Serikali wilayani Karatu wametakiwa kutekeleza amri ya Rais kwa kusimamia masuala ya usafi katika maeneo yao.

  0 0

  LI1Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kushoto akisaini mkataba kutoka Benki ya Maendeleo Afrika kwa ajili ya Mradi wa Ujenzi ,kulia ni mwakilishi wa benki hyo Dkt. Tonia Kandiero akitia saini wakati wa makabidhiano hayo leo jijini Dar es salaam.
  LI2 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kushoto akikabidhiana hati ya makubaliano ya msaada wa fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi na mwakilishi wa benki hyo Dkt. Tonia Kandiero wakati wa makabidhiano hayo leo jijini Dar es salaam.
  LI3 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kushoto akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa makabidhiano ya fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi kulia akiwa na mwakilishi wa benki hyo Dkt. Tonia Kandiero wakati wa makabidhiano hayo leo jijini Dar es salaam.
  LI4 
  Mtendaji Mkuu wa wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale akiongea na waandishi wa habari baada ya makabidhiano ya fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
  PICHA ZOTE NA ALLY DAUD- MAELEZO

  ……………………………………………………………………………………….
  Na jacquline Mrisho-maelezoDsm
  Wizara ya Fedha na Benki ya Maendeleo Afrika(ADB) zimesaini mikataba yakuikopesha Tanzania shilingi bilioni 750 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi sekta mbili za maendeleo ya ujenzi wa barabara na viwanja vya ndege nchini.
   
  Mikataba hiyo imesainiwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt Servacius Likwelile kwa upande wa Tanzania na Mwakilishi wa Benki hiyo Dkt Tonia Kandiero.

  Akizungumza mara baada ya kusaini mikataba hiyo Dkt . Likwelile alisema kuwa katika mkopo wa kwanza utasaidia katika kuinua uchumi nchini kwa kuimarisha miundo mbinu ya barabara ya Tanzania bara na visiwani.

  Dkt Servacius Likwelile aliongeza kuwa,mradi huu utapunguza gharama za matengenezo ya barabara pamoja na muda usafirishaji na ukarabati wa vyombo vya usafirishaji.Naye Mwakilishi wa Benki Maendeleo ya Afrika Dkt Tonia Kandiero alisema kuwa fedha hizo zitasaidia kuimarisha miundo mbinu ya barabara kwa ajili ya kuimarisha kilimo hasa katika mikoa ya Tabora, Katavi na Ruvuma ambapo asilimia 90 ya watu wake ni wakulima.

  Maeneo ambayo mradi huu yatakayoshughulika ni barabara ya kutoka Tabora (Pangale) hadi Mpanda na nyingine kutoka Mbinga hadi Mbamba Bay kwa Tanzania Bara na kwa Zanzibar barabara itatoka Bububu hadi Mkokotoni na nyingine kutoka vijijini hadi Bitumen standadi.Mkopo mwingine unaelekezwa katika ujenzi wa viwanja vya ndege vya Msalato kwa Tanzania Bara na Pemba kwa Zanzibar.

  0 0

  KAZ1 
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza John Minja akiwasilia katiki viwanja vya Magereza Mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya hafla ya kukabishi bendera kwa watumishi 39 wa Jehi hilo wanaotarajia kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa Tanganyika kwa kupanda Mlima Kilimanjaro.
  KAZ2 
  Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja akikabidhi bendera ya Magereza kwa kiongozi wa Msafara Kamishna Msaidizi wa Magereza Alexander Mmasy leo tarehe 04/12/2015 wakiwa wanajiandaa kupanda Mlima tarehe 06/12/2015 ili ifikapo tarehe 09 siku ya Uhuru wa Tanganyika wawe kileleni
  KAZ3 
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza John Minja akitoa nasaha kwa wapanda mlima wa Jeshi la Magereza (Hawapo pichani)
  KAZ4 
  Baadhi ya wadau wa Magereza Utalii Klabu walio tayari kupanda Mlima Kilimanjaro wakisikiliza kwa makini nasaha za Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja katika hafla ya kukabidhiwa bendera ya Jeshi hilo kuipeleka katika Kilele cha Mlima huo.

  KAZ5 
  Baadhi ya wadau wa Magereza Utalii Klabu walio tayari kupanda Mlima Kilimanjaro wakiimba nyimbo za hamasa baada ya kupokea bendera kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja katika hafla ya kukabidhiwa bendera ya Jeshi hilo kuipeleka katika Kilele cha Mlima huo.
  KAZ6 
  Wapanda Mlima Kilimanjaro wa Jeshi la Magereza wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Jeshi la Magereza John Minja (Katikati),wa tatu kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Arusha SACP Hamis Nkubasi, na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro SACP Venant Kayombo, wa tatu kushoto ni Mnadhimu Mkuu wa Magereza Mkoa
  KAZ10 
  Wadau wa Magereza Utalii Klabu wakiwa katika mazoezi mbalimbali ya kukimbia na kutembea katika viunga vya mji wa Moshi ikiwa ni maandalizi ya kuelekea katika kilele cha Mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa Tanganyika sambamba na kuamasisha utalii wa ndani.
  KAZ12 
  Picha zote na Mrakibu Msaidizi wa Magereza Deodatus Kazinja na Koplo Mfaume Abdalah wa Jeshi la Magereza
  ……………………………………………………………………………………………..
  Na Deodatus KazinjaKatika kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika tarehe 9 Desemba watumishi wapatao 39 Jeshi la Magereza wakiwa katika uwiano wa wanaume 30 na wanawake 9 wataadhimisha siku hiyo kwa kupanda mlima Kilimanjaro na kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.
   Washiriki hawa wanatoka katika vituo vya Makao Makuu ya Magereza, Chuo cha Taaluma ya urekebishaji Ukonga Dar es salaam, Kikosi Maalum cha Kutuliza Gasia Magereza (KMKGM), Pwani, Dar es salaam, Iringa, Mbeya, Mara, Tabora, Tanga, Kilimanjaro na Arusha ambao kwa gharama zao wameamua kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika kwa kufanya utalii wa ndani.
   Akiongea na waandishi wa habari Kamishna Jenerali wa Magereza nchini John Casmir Minja katika hafula fupi ya kuwakabidhi bendera watumishi hao katika viwanja vya Magereza Mkoa wa Kilimanjaro amesema amefurahishwa mno na uamuzi wa askari hao kwa vile unalitangaza Jeshi la Magereza nje ya mipaka yake.Kamishna Minja alisema pia mbali na kulitangaza Jeshi la Magereza unawaweka timamu watumishi hao katika kufanya kazi zao vizuri ikiwa ni kuunga kauli mbiu ya serikali ya Awamu ya Tano ya Hapa Kazi tu.
   Aidha Kamishna huyo alitumia fursa hiyo kuishukuru serikali kwa namna ambavyo imekuwa ikijitolea kulisaidia Jeshi la Magereza ambapo alitoa taarifa kuwa tayari mikataba ya kununuliwa magari yapatayo 905 na ujenzi wa nyumba za watumishi zipatazo 9500 imesainiwa na magari yataanza kuingia mapema Januari 2016.
   Kwa upande wake mwenyekiti wa Magereza Utalii Klabu ambaye pia ni Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Magereza Ndugu Estomih Hamis mbali na kumshuruku Kamishna Minja akwa namna ambavyo amejitolea katika kufanikisha uanzishwaji wa Klabu hiyo kuelezea dhima nzima ya utalii huo.
   “ Tumeamua kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika kwa mfumo huu kwa sababu kadhaa. Mosi , ni kuunga mkono jitihada za serikali za muda mrefu za kuhamasisha utalii wa ndani ambacho ni chanzo kimojawapo cha kuongeza mapato ya ndani ya serikali”“Pili, ni kuleta mwamko kwa watumishi wa umma na watanzania kwa ujumla katika kutembelea vivutio vya utalii vya ndani kuliko ilivyo sasa ambapo sehemu kubwa ya watalii ni wageni kutoka nje ya Tanzania”
   Aidha, ndugu Hamis aliongeza kuwa zoezi la upandaji mlima Kilimanjaro ni zuri kwa kuimarisha afya za watumishi hivyo kujiepusha na magonjwa kama vile kisukari, shinikizo la damu na utimamu wa mwili na hasa kwa askari wanaotakiwa kuwa hivyo muda wote.Tukio la watumishi wa Magereza kupanda mlima Kilimanjaro litakuwa ni la pili kwa mwaka huu ambapo mara ya mwisho walipanda mlima tarehe 6 March, 2015 wakiwa ni jumla ya watumishi 20 ambapo 16 walifanikiwa kufika kileleni na wanne kurudia njiani kwa sababu mbalimbali.
   Zoezi la upandaji mlima lililopita lilifanyika kwa mafanikio makubwa kiasi cha kuibua hoja y wa unndwaji wa chombo cha pamoja kinachoweza kuratibu shughuli za utalii ndani ya Jeshi la Magereza kwa kuwaunganisha watumishi wote.
   Hoja hiyo ilifanikiwa kwa kuundwa kwa Klabu ya Utalii ya Magereza, klabu ambayo iko katika hatua za mwisho za usajili. Tayari Klabu hiyo inao viongozi wakiongozwa na Mwenyikiti ndugu Hamis, katibu wake akiwa ni Mkaguzi wa Magereza Dominick Mshana na Mweka Hazina ni Mrakibu Msaidizi wa Magereza Erasto Kipingu.Nani analipa gharama za utalii huo?
   Akijibu swali hilo katibu wa Klabu hiyo Mkaguzi Mshana alisema kwa hivi sasa watumishi hao wanapanda kwa gharama zao wenyewe kutoka katika mishahara yao ambapo karibu kila mshiriki amechanga wastani wa shilingi 300,000.Mshana amesema ni matumaini yake kuwa katika siku za mbeleni kama watapatikana wadhamini gharama hizo zinaweza kupungua sana kutoka mifukoni mwa washiri. 
   Aidha amesema gharama za kupanda mlima na kutembelea vivutio vingine kwa ujumla ni kubwa kwa mtu mmoja mmoja lakini kunakuwa na unafuu mkubwa watu wakipanda kama kikundi.

  0 0
 • 12/04/15--06:41: MZEE DONATI KEZIRAHABI
 • This will be 10th anniversary since you left us,
  We have lived our lives with you through happiness and joy forgetting that one day you'll be gone from us and all will be gone with you. You were all that, a friend, our love, a husband, a father and grand father.
  You were our leader indeed and many followed you. Today we are here thanking your most kind and generous, open and loving heart.You are the reason behind our strengths today.  You are being missed so much and you will always be placed in a cherished part of our hearts. We will forever loving you.
   
  On 5/12/2015 this Saturday there's going to be a mass at St Imaculata, Upanga starting at 03:00pm. You arre all invited

  May his soul rest in peace Amen.

  Mama

  Hidaya Kezirahabi

  0 0

   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Mwamini Juma Malemi (katikati) akizungumza na wasanii pamoja na wadau wa filamu (hawapo pichani) wakati wa kufunguakikao cha wadau wa Filamu kujadili namna ya kuimarisha na kuboresha miundombinu katika tasnia ya filamu leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo na kulia ni Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini Bw. Simon Mwakifwamba
   Wasanii na wadau wa filamu wakisikiliza kwa makini mada zilizokua zikiendelea wakati wa kikao cha wadau wa Filamu kujadili namna ya kuimarisha na kuboresha miundombinu katika tasnia ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Mwamini Juma Malemi (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na wasanii na wadau wa filamu nchini leo jijini Dar es Salaam baada ya kufungua  kikao cha wadau wa Filamu kujadili namna ya kuimarisha na kuboresha miundombinu katika tasnia ya filamu. Wapili kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo na wapili kushoto ni Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini Bw. Simon Mwakifwamba.

   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Mwamini Juma Malemi (kushoto) akiwasili kuelekea kufungua kikao cha wadau wa Filamu kujadili namna ya kuimarisha na kuboresha miundombinu katika tasnia ya filamu leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo na kulia ni Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini Bw. Simon Mwakifwamba.

  Picha na: Genofeva Matemu - MAELEZO


  0 0

  Kaimu Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Philip Mpango akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
   Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano na 
  Kaimu Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Philip                                               Mpango jijini Dar es Salam leo.

  Na ChalilaKibuda,Globu ya Jamii
  BAADA ya Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa kufanya ziara ya kushitukiza katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kubaini upotevu wa Makontena 329, mapya yaibuka kwa Makampuni 43 kuhusika kukwepa kodi ya Sh.Bilioni 12.6 katika Bandari Kavu inayomilikiwa na Said Salim Bakh ressa.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Philip Mpango amesema kuwa kampuni hizo 43 zilipitishiwa Kontena katika Bandari Kavu ya Said Salim Bakhressa na kutaka ndani ya siku sita kuanzia leo kampuni zote ziwe zimeshalipia kodi kutokana na idadi ya kontena.

  Dk. Mpango amesema katika kampuni ambazo zilizokwepa kodi ambazo zilipitisha Kontena 329 wameshalipa zaidi ya Sh. Bilioni Tano(5) ambapo wanatakiwa kulipa kodi iliyobaki kuweza kumaliza kodi ya Sh.Bilioni 12.6 kwa kipindi alichoweka Rais Dk .John Pombe Magufuli. 

  Amesema kuwa hatilafu za kupotea kwa makontena hayo, kazi hiyo walishakuwa wameanza kwa bahati mbaya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa Majaliwa aliwawahi wakati alipofanya ziara katika mamlaka hiyo.

  Kampuni zilizokwepa Kodi ya mapato kwa makontena 329 ni Lotai Steel Tanzania LTD yenye makontena 100,Tuff Tyres Centre Company kontena 58 Binslum Tyres Company LTD, Kontena 33, Tifo Global Mart (Tanzania) Company Limited Kontena 30,IPS Roofing Campany Ltd Kontena 20,Rashywheel Tyre Center Com.Ltd Kontena 12, Kiungani Trading Company Ltd 10 Homing International Limited Kontena 9, Red East Building Kontena Saba,Tybat Trading Co Ltd, Kontena Tano,Zing Ent Ltd,Kotena Nne,Juma Kassem Abdul, Kontena Tatu, Salum Continental Co.Kontena Mbili, Zuleha Abbas Ali Kotena Mbili na Snow Leopard Building Kontena mbili na waliobaki walikuwa na kontena moja moja.

  Hata hivyo TRA imewasimamisha kazi watu 35 wakiwemo 27 waliokamatwa katika geti namba tano ambao hadi sasa wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano na uchunguzi .


  Aidha amewataka wafanyakazi kuwasilisha mali zao ili kuweza kuangalia uwezo wake katika utumishi kama zinaendana na umiliki huo.

  0 0

  Mshitakiwa namba moja katika kesi ya kuhujumu uchumi, Tiagi Masamaki (katikati) na washitakiwa wenzake wakitoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo mchana baada ya kusomewa mashitaka yao.

  MAOFISA wanane wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akiwemo Kamishna wa Forodha wa mamlaka hiyo Tiagi Masamaki (56) wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutoa makontena 329 bandarini bila ya kulipiwa kodi na kuisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 12.7 za kitanzania.

  Ukimuondoa Masamaki maofisa wengine waliopandishwa kortini ni Habibu Mponezya (45) Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja,Bulton Mponezya (51) 

  Wakili wa Serikali Mwandamizi Christopher Msigwa akisaidiana na Peter Vitalis ameadi leo mchana mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shahidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa watuhumiwa hao wanatuhumiwa kwa makosa mawili.

  Alidai makosa mawili ya uhujumu uchumi ni kula njama ya kuidanganya Serikali na kuisababishia Serikali hasara. Kesi hiyo ni namba 35/2015 ya uhujumu uchumi. 

  Ilidaiwa katika shtaka la kwanza katika tarehe tofauti kati ya Juni 1 na Novemba 17 mwaka huu, sehemu isiyojulikana ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa pamoja walikula njama ya kuidanganya Serikali kuwa sh. bilioni 12.7 zimetolewa kwa kutoa makontena 329 katika Bandari Kavu ya Azam, baada ya kodi zote kutolewa.

  Katika shtaka la pili, washtakiwa wanatuhumiwa katika ya Juni Mosi na Novemba 17 mwaka huu ndani ya Jiji la Dar es Salaam walishindwa kutimiza majukumu yao kwa namna inavyotakiwa na kusababisha Serikali kupata hasara ya sh. bilioni 12.7.

  Baada ya washtakiwa hao kusomewa makosa yao, Hakimu Shahidi aliwaeleza kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kwa hiyo hawatakiwi kujibu chochote kama kweli au si kweli.

  Aliongeza kuwa Mahakama Kuu ndiyo inamamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kwa hiyo kama wanataka dhamana wapeleke maombi ya dhamana katika mahakama hiyo.

  "Kama mnataka dhamana pelekeni maombi Mahakama Kuu kwa sababu mahakama hii hawezi kutoa dhamana," alisema Hakimu Shahidi 

  Hata hivyo, upande wa utetezi ulidai kuwa kesi hiyo ifikishwa mahakamani hapo bila kibali na pia waliomba mshtakiwa namba nne Mrema anamtoto mchanga kwa hiyo wanaiomba mahakama imfikirie.  Wakili Msigwa alidai upelelezi bado unaendelea, wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa. Kesi hiyo itatajwa Desemba 17 mwaka huu kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika
  Watuhumiwa hao wakisindikizwa na maofisa wa polisi kuingia chumba cha Mahabusu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
  Hapa Masamaki na wenzake wakiingia ndani ya gari kuelekea gereza la Segerea.

  0 0

  BALOZI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi leo Jumamosi Desemba 5, 2015 alihudhuria mkutano wa Halmashauri ya CCM tawi la DMV ikiwa ni moja ya ziara zake anazotarajiwa kuzifanya kutembelea matawi ya vyama vya siasa nchini Marekani yenye lengo la kudumisha mshikamano na ushirikiano wa Watanzania bila kujali itikadi za vyama vyao.

  Akiongea kwenye mkutano wa Halmashauri ya CCM DMV Mhe. Wilson Masilingi amesema lengo kuu ni kuwa karibu na vyama vya siasa kwa lengo la kuleta umoja na mshikamano ndani ya Jumuiya za Watanzania nchini Marekani na pia kuvitambua kama sehemu na sura ya Diaspora na kutoa wito kwa Watanzania waishio Marekani kuelekeza nguvu katika kuwekeza nyumbani bila kujali ufuasi wa chama unachoamini au kushabikia, wote ni Watanzania.

  Mhe. Balozi Wilson Masilingi aliiomba Halmashauri hiyo ya CCM DMV kusaidia katika maendeleo ya Tanzania kwa kupanua wigo wao pamoja na kwamba lengo lao ni siasa na siasa ni sehemu ya maisha ya jamii na maendeleo ya jamii yanategemea siasa, kwa hiyo basi mnaposikia kuna muwekezaji yupo tayari kuwekeza Tanzania msisite Ubalozi upo wazi na utafanya kila liwezekanalo kuhakikisha muwekezaji huyo hapati vikwazo vyovyote.

  Mwisho Balozi Wilson Masilingi aliwashukuru Watanzania kwa kuwa mabalozi wazuri nchini Marekani na kuwaasa kuishi kwa kufuata misingi na sheria za nchi ya Marekani.

   Mhe. Balozi Wilson Masilingi akiongea jambo na mwenyekiti wa tawi CCM DMV Bwn. George Sebo kwenye mkutano wa Halmashauri ya CCM DMV siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 mkutano uliofanyika Hampton Inn, College Park, Maryland. Picha na Kwanza Production/Vijimambo Blog
  Mkutano ulianza kwa sala na kuwakumbuka wote waliotangulia mbele ya haki.

  Mwenyekiti tawi la CCM DMV Bwn. George Sebo akifungua kikao cha Halmashauri ya CCM DMV kilichofanyika siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 katika ukumbi wa Hampton Inn, College Park, Maryland.

  Mhe. Balozi Wilson Masilingi akiongea machache kwenye kikao cha Halmashauri ya CCM DMV kilichofanyika siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 katika ukumbi wa Hampton Inn, College Park, Maryland.

  Mhe. Balozi Wilson Masilingi akiongea machache kwenye kikao cha Halmashauri ya CCM DMV

  Picha ya pamoja.
  Bwn. John Mbatta katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
  Given  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
  Catherine  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
  Tino Malinda  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
  Aunty Grace Sebo  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
  Grace Mlingi  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
  Mzee Joel  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
  Dr. Secelela Malecela  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
  Katibu wa CCM DMV Bi.Jesca Mushala  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
  Mwenyekiti wa CCM DMV Bwn. George Sebo  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.  0 0

  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Jumanne Sagini wakati akizungumza na watendaji mbalimbali wa ofisi hiyo leo katika mkutano wa kikazi uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Karimjee jijini Dares Salaam , ambapo lengo kuu lilikuwa ni kutoa maelekezo ya utendaji kazi kama ilivyoagizwa na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Afya -TAMISEMI ,Dkt .Deo Mutasiwa .
  Baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) wakimsilikiza Katibu Mkuu wa ofisi ambaye hayupo pichani.

  Na Magreth Kinabo – maelezo
  SERIKALI imewataka watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha kwamba wanafanyakazi kwa uadilifu weledi wa taaluma zao na kufuata sheria zilizopo katika kusimimia suala la usafi wa mazingira, likiwemo la kudhibiti biashara holela, gereji bubu,uegeshaji wa magari holela.

  Pamoja na hayo wasimamie, upigaji holela wa muziki katika vilabu, baa na kumbi zaidi ya saa zilizopangwa na kuzuia bodaboda zinazosafirisha abiria hadi maeneo ya miji katikati, pia kuzuia ujenzi holela.

  Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Jumanne Sagini wakati akizungumza na watendaji mbalimbali wa ofisi hiyo katika mkutano wa kikazi uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Karimjee, jijini Dar es Salaam ambapo lengo kuu lilikuwa ni kutoa maelekezo ya utendaji kazi kama ilivyoagizwa na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa.

  Akizungumzia kuhusu suala la usafi wa mazingira kufuatia ziara iliyofanyika hivi karibuni imeonekana kuwa na changamoto mbalimbali alisema;
  “Kazi zetu haziendi vizuri kwa sababu hatusimamii sheria zilizopo ndio kumekuwa na malalamiko katika utendaji wa kazi zetu, mfano katika suala la gharama za usimamizi wa usafi wa mazingira ni kubwa . Lakini kinachofanyika ni kweli kinalinganishwa na gharama hizi?” alihoji Katibu Mkuu huyo.

  Akitolea mifano gharama zinazotumika katika suala hilo, kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2014/2015 alisema kwa upande wa manispaa ya Kindondoni wanatumia Sh. bilioni 2.6, Ilala ni Sh. bilioni 2.6, wakati Temeke wanatumia Sh. bilioni 1.2 .

  “Kilichobainika ni kwamba mikataba ya watu wanaojishughulisha na usimamizi wa usafi wa mazingira ni ya mwaka mmoja na wanaopewa mikataba hiyo ni watu ambao hawana uwezo wa kutosha wa kutekeleza jukumu hilo.

  “ Ama watu wasio na uwezo ama mnaofahamiana nao. Au kampuni zenye mahusiano na baadhi ya watumishi wa mamlaka za serikali za mitaa au wenye uhusiano na viongozi wenu, Jiepusheni na kuwapa watu hawa kwa sababu kutokana na hali hiyo hamtaweza kukabiliana nao. Kama kuna kiongozi ambaye mmepatia nafasi hii lazima athibitishe kuwa na uwezo. Na kama pia ni miongoni mwenu hakikisheni kuwa ni mtu mwenye uwezo. Kazi zetu haziendi vizuri kwa sababu ya nasaba au viongozi wenu,” alisisitiza Katibu Mkuu huyo, huku akisema lazima wabadilike na kuangalia kama hawana uwezo wajitoe au wafukuzwe.

  Aliongeza kwamba katika suala hilo kumekuwa na migongano ya watumishi wa halmashauri ambao wanatakiwa kufanya kazi kama timu; mfano maafisa afya, mazingira na usafishaji, lakini akasema wanaonana kama maadui.

  “ Hawa wangepaswa kufanya kazi kwa kushirikiana ,lakini ni maadui kwa sababu ya maslahi … hili ni lenu wakurugenzi kwani hata watoto wako wakisambaratika ni lazima huwaketishe chini ili mambo yaende, asiyekubali unamwajibisha,” alisema.

  Sagini alisema watendaji hao , wote ni wadau wa usafi, hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa ushirikiano, hivyo aliwataka wapeane mikono katika kikao hicho, ambapo walifanya hivyo ikiwa ni hatua ya kuonesha ushirikiano.

  Pia alisema watu wanaosafirisha bidhaa za vyakula kwa kutumia majani ya migomba au matenga wasiruhusiwe kufanya hivyo wapewa muda wa wiki moja au mbili kutumia utaratibu mwingine.
  Aliwataka pia watendaji mbalimbali wa TAMISEMI kuwa na ushirikishwaji katika ngazi za chini kwenye halmashauri kwa kuwa haliko vizuri.

  Sagini alisema ni vizuri kukawekwa mfumo wa TAMISEMI wa kushirikisha ngazi za chini kama ilivyo kwa mjumbe wa nyumba kumi kwenye masuala ya vyama.

  “ Ni lazima tuingie katika mfumo huu wa kuwa na watendaji wa kaya 30 ambao watakuwa chini ya TAMISEMI . Suala hili lina faida ya ulinzi na usalama na kuwatambua wageni… tunaangalia jinsi ya kulitekeleza,” alisema.

  Aliwataka wakurugenzi wasikae maofisini kwenye madawati bali watembelee maeneo mbalimbali ili kutatua kero za wananchi na kuangalia mipangilio ya miji na majiji.

  Katika suala hilo la usafi wa mazingira alisema mtu mwenye uwezo wa kusafisha jiji liwe safi apewe nafasi huku akisisitiza suala la kushirikisha sekta binafsi ni muhimu katika mambo mbalimbali likiwemo la ujengaji wa maegesho ya magari, ambapo sasa yanahitajika kwa ajili ya mradi wa mabasi yaendayo haraka(DART).

  “ Kwenye eneo hili la DART lazima mbadilike tunataka barabara za DART ziwe nyeupe yaani watu wasifanye biashara,” alisisitiza huku akitaka kuanzia Jumatatu wiki ijayo yatekelezwe.

  Aliwataka watu wanaohusika na vyombo vya usafiri na usafirishaji kutovunja sheria, akatolea mfano boda boda.

  0 0

  Wakazi wa Mwanza na Kagera wameendelea kupata shida ya usafiri kutokana na fedha zilizotengwa na serikali kurekebisha meli ya Mv.Victoria kutumika kulipia mishahara ya wafanyakazi.


  0 0

   Bibi harusi Mary Michael Mbaya (kushoto), akimvisha pete ya ndoa mume wake Richard Mwaikenda ambaye ni mpiga picha mkuu wa gazeti la Jambo Leo na mmiliki wa Kamanda wa Matukio Blog, baada ya kubariki ndoa yao katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kivule Dar es Salaam mchana huu.

   Wanahabari wakiwa katika picha ya pamoja na maharusi hao.

  Hapa ni furaha tupu. Wa tatu kulia ni mwanahabari, Nyakasagani Masenza.
   Bwana harusi Richard Mwaikenda akiwa amepozi na mke wake Mary Michael Mbaya wakati wa ibada yao ya ndoa.
   Mchungaji wa Kanisa hilo, Naory Chuma (kushoto), akiwabariki maharusi hao.
   Baba  wadogo wa bwana harusi Richard Mwaikenda wakiwa kwenye ibada hiyo.
   Wazazi wa bibi na bwana harusi wakiwa kwenye ibada hiyo. 
   Ndugu na jamaa wa maharusi hao wakiwa katika ibada hiyo.
   Hapa ni furaha tupu kwa ndugu wa maharusi.
   Maharusi hao wakiingia kanisani.
   Baadhi ya Waandishi wanaofanyakazi na bwana harusi wakijumuika katika ibada hiyo. Kutoka kushoto ni Peter Mwenda (Majira), Anicetus Mwesa, Said Mwishehe na Peter Ambilikile wote kutoka gazeti la Jambo Leo.
   Maharusi na wapambe wao wakiwa mbele ya kanisa.
   Wanandoa hao wakionesha shahada ya ndoa yao baada ya kukabidhiwa.
   Waumini wakiwa kwenye ibada hiyo.
   Maharusi hao wakitoka kanisani na wanandoa wenzao baada ya kufunga ndoa. Ndoa 11 zilifungwa katika kanisa hilo.


  0 0

   Afisa Mwandamizi Matekelezo wa NSSF, Theopista Muheta (kushoto) akitoa maelezo kuhusu viwanja vya vinavyouzwa na NSSF vilivyopo Kiluvya A Kisarawewakati wa maonesho ya 16 ya wajasiriamali wa Sekta isiyo rasmi Afrika Mashariki yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

   Afisa Masoko na Uhusiano wa NSSF, Aisha Sango (kulia) akimuelekeza mjasiriamali, Abdulnuru Mbeo namna ya kujaza fomu ya kujiunga na uanachama wa hiari wa NSSF wakati wa maonesho ya 16 ya wajasiriamali wa Sekta isiyo rasmi Afrika Mashariki yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Afisa Masoko na Uhusiano wa NSSF, Aisha Sango (kulia) akiwaelekeza namna ya kujaza fomu ya kujiunga na NSSF wanachama wapya waliojiunga na mfuko huo wakati wa maonesho ya 16 ya wajasiriamali wa Sekta isiyo rasmi Afrika Mashariki yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 
  Afisa Masoko na Uhusiano wa NSSF, Aisha Sango (wa pili kushoto) akiwaelekeza namna ya kujaza fomu ya kujiunga na NSSF mjasiriamali, Abdulnuru Mbeo wakati wa maonesho ya 16 ya wajasiriamali wa Sekta isiyo rasmi Afrika Mashariki yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni  Afisa Matekelezo Sekta wa NSSF, Edwin Kafanabo. 

   Afisa Mwandamizi Matekelezo wa NSSF, Theopista Muheta (kushoto) akitoa maelezo kuhusu viwanja vya vinavyouzwa na NSSF vilivyopo Kiluvya A Kisarawe wakati wa maonesho ya 16 ya wajasiriamali wa Sekta isiyo rasmi Afrika Mashariki yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 
   Watu mbalimbali wakipata vipeperushi vinavyoelezea miradi mbalimbali inayosimamiwa na NSSF.

  0 0


   Burudani ya ngoma kutoka kikundi cha Dhahabu ikiendelea
  Baadhi ya vijana wakiwa wanasikiliza kwa makini vijana wenzao wakielezea safari zao za mafanikio.

  Aliyekuwa nahodha wa timu ya Taifa ya wanawake 2002-2003 na kuchezea mpira timu hiyo kwa Miaka 15 mpaka anastaafu mwaka huu Esther Chabruma akielezea namna mchezo wa Mpira wa Miguu ilivyoweza msaidia mpaka hapa alipofikia na kuwasihi vijana wasikate tamaa maana kila jambo lina wakati wake,jana tarehe 4.12.2015
   Msanii wa sanaa za Maonesho Vanensia Shule, ambaye pia ni Mkufunzi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam upande wa sanaa na Filamu akielezea jinsi Sanaa inavyoweza kumkomboa kijana,na kutoa mifano ya baadhi ya wasanii walioanzia chini na sasa wanamafanikio makubwa.
   Alphonse Matata ambaye anajihusisha na kilimo pia Mjasiliamali kupitia ufugaji wa nyuki akielezea safari yake ya mafanikio ,na kuwashauri vijana wasingoje kuajiliwa bali wawe wabunifu na kujiunga katika ujasiliamali.
  MC Suhaila Thawer akiendelea kutoa utaratibu wa wazungumzaji
   Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambaye anafanya Shahada ya Sayansi katika Teknolojia ya ubunifu wa nguo mwaka watatu akitumbuiza wakati wa Kongamano hilo la Msafara
   Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo kikuu cha Dar es salaam Kitaponda Ahadi, akielezea kuhusu elimu na changamoto alizo zipata wakati wa akiwa Shule mpaka ndoto yake ilivyotimia ya kuja kusoma chuo kikuu na kuwa kiongozi, amewasihi vijana wenzake wasikate tamaa wafanye bidii katika masomo watafikia malengo.
   Major Mbuya mtaalam wa kuendesha Baiskeri na mwanzilishi wa waendesha Baiskeri Tanzania, akielezea jinsi ubunifu ulivyo msaidia mpaka sasa amefanikiwa
   Hassan ally kijana mjasiliamali akieleza namna alivyoweza kubadilisha taka na kuwa Bidhaa ambayo inaweza kutumika tena kwa matumizi mengine pia, ameelezea mpango wake wa kuanza kujenga nyumba kwa kutumia bei nafuu.
   Mjasiliamali Maarufu na Mtoa ushauri wa biashara na mambo mbalimbali James Mwang'amba, alitoa Historia ya Maisha yake na kutoa siri tatu za mafanikio ambazo ni kuwa na maono ya maisha bora ya baadae, kujifunza kwa kupitia njia mpya ya Teknolojia mfano youtube na kuwa na mtu ambaye unahisi unaweza ukajifunza kwake.
   Mwenyekiti wa Maandalizi wa Msafara James Isdore akitoa neno la Shukurani
  Baadhi ya Vijana wakiwa katika Kongamano hilo la Msafara.

  Vijana mbalimbali wamejitokeza katika kongamano la msafara kusikiliza baadhi ya vijana wenzao ambao wametoa historia zao kuhusu walipotokea mpaka wamefanikiwa kufika hapo walipofikia na kuwatia moyo vijana wengine wasikate tamaa kwa sababu mafanikio yapo.

  Msafara ambao unalenga kuibua na kurudisha ndoto za vijana katika sekta zote kwa kutambua kuwa kila eneo lina mchango mkubwa katika mafanikio na maendeleo ya vijana. Wazungumzaji tofauti tofauti walijikita katika maeneo makuu yafuatayo Sayansi na Teknolojia,Kilimo, Biashara, Sanaa na usanii, Elimu, Uongozi, Michezo, utunzaji Mazingira, haki sawa za kijinsia pamoja na harakati.

  Maeneo hayo yalikuwa ni nguzo kuu ya kufanya vijana kuwa na fursa ya kukabiliana na changamoto za kimaisha katika kufikia mafanikio na malengo yao. Katika safari hii ya Msafara matukio mbalimbali yatafanyika ikiwemo kuwaleta vijana wa rika moja wenye umri wa miaka 15-24 ili kuwaleta kwa pamoja wapate kujifunza kutoka kwa wengine waliofanikiwa, wenye fani mbalimbali/Taaruma zao, hii itawajengea ujasili wengine katika kufikia mafanikio yao.

  Programu hii inaendeshwa na muungano wa Mashirika na Makundi Matano yaliyopo hapa Tanzania ikiwa ni pamoja na DARUSO, YouthCAN, NGAO YOUTH na Young Feminist Forum na inaratibiwa na Oxfam Tanzania, msafara itakuwa ni moja ya fursa kwa vijana kutangaza na kuonesha ubunifu wao na mafanikio waliyofikia kimaisha ingawa kuna changamoto na vikwazo mbalimbali. Safari hii ya Msafara itaendelea mkoani Morogoro tarehe 12.12.2015 wilayani Ifakara.

older | 1 | .... | 703 | 704 | (Page 705) | 706 | 707 | .... | 1898 | newer