Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 702 | 703 | (Page 704) | 705 | 706 | .... | 1904 | newer

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadick akipanda kwenye mtambo maalum wa kuchimbia mitalo (Scaveter), wakati wa uzinduzi uliofanyika leo jijini Dar,Mtambo huo umenunuliwa na Manispaa ya Kinondoni  kwa  thamani zaidi ya Sh. Milioni 600.

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ,Mussa Natty akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadick baada ya kuzindua scaveter iliyonunuliwa na Manispaa hiyo leo  katika viwanja vya Manispaa , jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii

  0 0

    Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua bandari ya Dar es salaam  Desemba 3, 2015 ambako alikwenda kupata ukweli kuhusu makontena 2,431 yaliyopitia kwenye bandari hiyo bila kulipiwa kodi ya serikali.  
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mfumo wa kukagua makontena bandarini kwa kutumia scaner huku akipata maelzo kutoka kwa Ofisa wa forodha, January Shauri wakati alipotembelea bandari ya Dar es salaam Desemba 3, 2015  kutaka kujua ukweli wa tuhuma za makontena 2431 yaliyopita bandarini hapo bila kulipiwa kodi ya serikali.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu utoaji bili za kulipia kodi za serikali kwa watumiaji wa bandari ya Dar es salaam kutoka kwa ofisa mwandamizi wa masuala ya fedha , Bw. Sartho Mbuya wakati alipotembelea bandari hiyo  Desemba 3, 2015 kutaka kujua ukweli wa tuhuma za makontena 2431 yaliyopita bandarini hapo bila kulipiwa kodi za serikali. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwonyesha Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es salaam, Bw. Abel Mhanga (kulia) orodha ya makontena 2,431 yaliyopitia kwenye banda ya Dar es salaam bila kulipiwa kodi wakati alipofanya ziara kwenye bandari hiyo Desemba ,3, 2015. 
   Waziri Mkuu,  Kassim Majliwa  akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini TRL wakati alipotembelea stesheni ya Dar es salaam kukagua uendeshaji wa Shirika hilo Desemba 3, 2015. 
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akitembelea steheni ya reli ya Dar es salaam Desemba 3, 2015.


  WAZIRI MKUU ATINGA TENA BANDARINI NA TRL
  *Akuta makontena 2,431 yametoka bila kulipiwa ushuru
  *Ataka majina yaletwe ofisini leo saa 11 jioni
  *Atoa wiki wiki moja kwa mfumo wa malipo kubadilishwa
  *Akagua mabehewa, awaweka kiporo TRL

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara nyingine ya kushtukiza bandarini na kukagua mfumo wa upokeaji na utoaji mizigo na utozaji wa malipo baada ya kupewa taarifa kwamba kuna makontena 2,431 yametolewa bila kulipiwa ushuru.

  Waziri Mkuu alisema kwa mujibu wa taarifa ya ukaguzi wa bandari ya kuanzia Machi hadi Septemba 2014, makontena hayo yalipita bila kulipiwa kodi kupitia bandari kavu nne (ICDs) ambazo ni JEFAG, DICD, PMM na AZAM.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ni watumishi 10 tu ambao wamesimamishwa kazi kutokana na makosa hayo. “Mmeamua kuwasimamisha kazi watu wadogo na kuwaacha wakubwa wanaendelea na kazi. Hatuwezi kuendelea kuikosesha Serikali mapato namna hii,” alisema Waziri Mkuu.

  Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Meneja wa Bandari, Bw. Hebel Mhanga amletee ofisini majina ya watumishi wote waliohusika na ukwepaji kodi huo ifikapo leo saa 11 jioni. Pia amempa Meneja huyo wiki moja kuhakikisha kuwa mamlaka hiyo inabadilisha mfumo wa utozaji malipo kutoka kwenye billing system na badala yake kuweka mfumo wa malipo wa kielektroniki (e-payment).

  Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Desemba 3, 2015), wakati akikagua idara mbalimbali za mamlaka ya bandari na kuona ukaguzi wa mizigo unavyofanyika kwa kutumia scanners. Akiwa kwenye chumba cha scanner mojawapo, Waziri Mkuu alikuta manifest moja ikisema kontena limejaa diapers lakini picha ya kwenye kompyuta ya scanner ilionyesha kuwa ndani ya kontena hilo kuna vitu kama vifaa vya umeme.

  Kwa mujibu wa Kaimu Meneja Bandari upande wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Ben Usaje ambaye pia ni msimamizi wa kitengo cha scanner, inapobainika taarifa kama hiyo inapaswa itumwe kwa wenye ICDs ili wafanye ukaguzi kwa kulifungua kontena ili kuhakikisha mali zilizomo ndizo zilizoandikishwa kwenye manifest.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa amefanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi za Shirika la Reli (TRL) na kukagua mabehewa yaliyokuwepo kisha akazungumza na baadhi ya wafanyakazi waliokuwepo kwenye stesheni hiyo ambako alibaini madudu kwenye malipo ya mishahara na makato ya michango ya wafanyakazi.

  Akizungumza na Mkurugenzi Mkuu TRL, Mhandisi Elias Mshana, Waziri Mkuu alisema amefika kwenye shirika hilo ili kujifunza utendaji wao kazi lakini anazo taarifa za wao kupewa fedha na Serikali kiasi cha sh. bilioni 13.5/- ili waendeleze miundombinu ya reli lakini hawakufanya hivyo. “Nia ya kuwapa fedha hizo ilikuwa ni kuboresha miradi ili muweze kujiendesha kibiashara lakini nyie mkaamua kujilipa wenyewe,” alisema.

  “Ninazo taarifa kuwa baada ya hapo, mlikopa sh. bilioni 3 kutoka benki ya TIB ili kuendesha miradi ya shirika lakini badala ya kufanya miradi, fedha hizo mkaamua nazo kujilipa mishahara. Sasa sijui mnarudishaje huo mkopo wakati hakuna mradi wowote uliofanyika,” alihoji bila kupata majibu.

  Alipoulizwa wafanyakazi wana matatizo gani hapo TRL, Katibu wa TRAWU, Bw. Boaz Nyakeke alisema wanadai malimbikizo ya makato yao kwenye mifuko ya pensheni, malimbikizo ya makato kwenye SACCOS na malimbikizo ya kuanzia Julai – Novemba 2014.

  Waziri Mkuu kwa upande wake alimtaka Mhandisi Mshana asimamie uboreshaji huduma za usafiri wa treni katika Jiji la Dar es Salaam ili hata mabasi ya mwendo kasi yatakapoanza wananchi waweze kuwa na uhuru wa kuchagua aina ya usafiri wautakao.

  “Tunataka kujenga yadi kubwa nje ya mji ili watu wenye magari wawe wanayaacha huko na kutumia usafiri wa treni au DART kuja mjini kama njia mojawapo ya kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam,” alisema.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM
  ALHAMISI, DESEMBA 3, 2015.

  0 0

   Mwakilishi wa Kaimu Mkuruegenzi Mkuu wa NHIF, Eugen Mikongoti akifungua kikao kilichowashirikisha wenyeviti wa bodi na makatibu wa Vituo Vya Afya, Zahanati na Hospitali wa Manispaa ya Temeke juu ya mpango wa bima ya afya kwa kayo iliyofanyika leo jijni Dar es Salaam.
   Meneja wa Mkoa wa Temeke wa NHIF, Costantino Makala akitoa maada katika kikao hicho leo latika ukumbi wa Temeke jijini Dra es Salaam.wa katikati ni Mwakilishi wa Kaimu Mkuruegenzi Mkuu wa NHIF,Eugen Mikongoti Kushoto ni Mganga Mkuu wa Manispaa Temeke,Silvia Mamkwe.
  Sehemu ya Wenyeviti wa Bodi na Makatibu wa Vituo vya Afya ,Zahanati na Hospitali katika kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umesema mpango wa huduma ya afya katika kaya utasaidia upatikanaji wa huduma bora ya matibabu kwa jamii kutokana na mchango wao wa uanachama.

  Akizungumza leo Wenyekiti wa Bodi na Makatibu Afya wa Manispaa ya Temeke, Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Eugen Mikongoti amesema sharia iko tayari kwa ajili ya mpango huo kinachotakiwa ni utekelezaji kwa wananchi katika kupata huduma hiyo.

  Mikongoti amesema kuwa kila mtu mmoja katika kaya kwa Manispaa ya Temeke atachangia Sh.50000 ambapo atapata matibabu kwa mwaka mmoja katika Vituovya Afya,Zahanati na Hospitali katika Manispaa hiyo.

  Amesema fedha ambazo watachangia zitatumika katika kununua dawa na vifaa tiba katika Manispaa hiyo hivyo kila mwananchi atakayejiunga na mpango huo matibabu kwa kutambua mchango wake na dawa lazima ziwepo pamoja na vifaa tiba.

  Mikongoti amesema kuwa fedha zinazochangwa na wanachama katika mpango ho zitatumika kwa malenfo yaliyokusudiwa na serikali itachangia asilimia 50.

  Amesema NHIF itahakikisha kila mwananchi anakuwa na bima ya afya ili kuweza kupata matibabu yake wakati akifikwa na magonjwa kwani wakati mtu anaweza kuugua ugonjwa na kuweza kushindwa kupata matibabu kutokana na kutokwepo katika mapango wowote.

  “NHIF itakuwa karibu na wananchi kama tunavyofanya nia yetu ni kutaka kila mwananchi anakuwa na bima ya afya ya kumfanya maisha yake yawe  mazuri ya uhakika wa matibabu”amesema Mikongoti.

  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Viongozi na Wawakilishi wa Umoja wa Sekta Binafsi nchini (Tanzania Private Sector Foundation - TPSF) katika ukumbi wa mkutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 3, 2015. PICHA NA IKULU
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Viongozi na Wawakilishi wa Umoja wa Sekta Binafsi nchini (Tanzania Private Sector Foundation - TPSF) katika ukumbi wa mkutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 3, 2015. PICHA NA IKULU.

  0 0

  SERIKALI imewaagiza maafisa  wa  afya nchini  kuhakikisha  kila kaya inakuwa  na choo bora  ikiwa ni hatua ya kuhakikisha  jamii inaepekana  na magonjwa  yanayotokana na uchafu  mazingira , sambamba  na   suala la usafi wa mazingira  kuwa endelevu  kama ilivyoagizwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.  John Pombe Magufuli.
  Aidha Serikali imepiga marufuku ulaji wa matunda yaliyomenywa barabarani.

  Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando(Pichani),wakati wa mkutano wake na  waandishi  wa habari  uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa  wizara hiyo.

  Katibu Mkuu huyo ambaye alikuwa ameambatana na baadhi ya viongozi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Ofisi ya Waziri Mkuu, wakiwemo wa wizara yake kwa ajili ya kuzungumzia mambo matatu ambayo ni  suala la usafi  wa mazingira  katika kuadhimisha siku ya  Uhuru ,Desemba 9, mwaka 2015, ugonjwa wa kipindupindu na  polio.
  “Wakuu wa mikoa na wilaya wanatakiwa kutekeleza agizo hili kwa kujiwekea utaratibu wa kufanya usafi maeneo yao,” alisema Dkt. Mmbando.

   Dkt. Mmbando alisema  ikumbukwe kuwa ugonjwa wa kipindupindu pamoja na magonjwa mengine yanayohusiana na uchafu huenea kwa kasi kutokana na hali duni ya usafi katika maeneo tunayoishi. Hivyo takwimu zinaonesha kuwa kati ya taka ngumu zinazozalishwa ni 50% tu huzolewa na kupelekwa dampo. Kiasi cha taka kinachobaki huzagaa katika maeneo mbalimbali hususani kando kando ya barabara, katika maeneo ya kukusanyia taka (Collection points), chini ya madaraja na katika maeneo ya wazi hali inasayobabisha miji yetu kuonekana michafu. 

  “Hali kadhalika, takwimu zinaonesha kuwa ni kaya zipatazo 34% ndizo zina vyoo bora na asilimia 12% hazina vyoo kabisa. Hali hii inahatarisha afya ya jamii na kusababisha kuenea kwa urahisi kwa magonjwa ya kuambukiza.  Kwa mijini na miji midogo, mifereji ya maji taka na ile ya mvua ni michafu na mingi imeziba, hivyo hutiririsha maji ovyo na kuhatarisha afya ya jamii,” alisema .

  Aliwataka watendaji hao, kusimimia suala hilo kwa kuzingatia sheria za afya  zilizopo, huku akizitaka halimashauri na mamlaka kuweka sheria ndogo ndogo ambazo hazileti unyanyasaji kwa wananchi. Katika kutekeleza kwa vitendo agizo la Mhe. Rais .


  Kubainisha maeneo yote ya umma ambako shughuli za usafi wa mazingira zitafanyika siku hiyo,kuhamasisha jamii kwa njia mbalimbali kujitokeza kwa wingi kushiriki shughuli za usafi katika maeneo yao na sehemu za kazi au biashara, vyombo vya usafiri wa abiria na vituo vya wasafiri ili vifanyiwe usafi wa kuridhisha,kushirikisha wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafsi, vyombo vya ulinzi na usalama, taasisi za elimu, n.k. ili kufanikisha zoezi zima la ukusanyaji, usafirishaji na utupaji salama wa taka (madampo) kutoka katika maeneo ya kaya, umma na taasisi kwa siku hiyo.

  Aliongeza kwamba  wanapaswa kuhusisha au kushirikisha vyombo vya habari vya kitaifa na kijamii katika kuhamasisha jamii kushiriki zoezi la usafi,kupanga ratiba na wajumbe wa kusimamia kazi hiyo katika halmashauri kwa tarehe 9,Desemba,2015  kwenye maeneo ya kaya na ya umma na kupanga ratiba endelevu baada ya hapo,kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa kazi hizi kwa mfumo na muda ulioinishwa na Wizara.

  Pia kwa kushirikiana na wadau, halmashauri zina wajibu wa kuandaa vyombo vya usafirishaji taka ngumu na maji taka kutoka maeneo ya uzalishaji hadi maeneo yaliyoainishwa kutupwa bila kuathiri mazingira.

  Kwa upande wa wananchi  aliwataka  wafanye yafuatayo ili  kupambana na kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu kila mmoja Kuchemsha maji ya kunywa au kutibu kwa dawa maalumu (waterguard)Kuepuka kula chakula kilichopoa au kuandaliwa katika mazingira yasiyo safi na salamaKunawa mikono kwa sabuni na maji safi na salama,kabla ya kula,baada ya kutoka chooni.

  Mambo mengine ni baada ya kumnawisha mtoto aliyejisaidia,baada ya kumhudumia mgonjwa,kuosha matunda kwa maji safi kabla ya kula,Kukomesha utiririshaji wa maji kutoka chooni ,Kutoa taarifa katika kituo cha kutolea huduma za afya endapo utapatwa na ugonjwa wa kuharisha au kutapika,kutoa taarifa kwenye ofisi za serikali endapo mtu au kikundi cha watu kitafanya shughuli zenye kuashiria uchafuzi wowote wa mazingira.

  Aliongeza kwamba Serikali itaendeleza juhudi za kuwezesha wananchi kupata maji safi na salama. Napenda kusisitiza kwa wananchi wote, tuwe makini kutumia maji yanayotoka katika vyanzo visivyo salama. Hii ni muhimu kwani, kwa sehemu kubwa, ugonjwa huu huenezwa kupitia maji yasiyo salama.

  Tangu kutokea kwa ugonjwa huu kwa mara ya kwanza tarehe 15 Agosti, 2015 katika mkoa wa Dar es Salaam ugonjwa huu umeendelea kusambaa kwa kasi. Hadi tarehe 2/12/2015 Mikoa mingine 20 ya Morogoro, Iringa, Pwani, Kilimanjaro, Kigoma, Dodoma, Geita, Mwanza, Arusha, Mara, Shinyanga, Tabora, Singida, Tanga, Lindi, Rukwa, Manyara, Kagera, Katavi na Mbeya imeshaathiriwa.

   Takwimu zinaonesha kuwa hadi tarehe 2 Desemba, 2015 jumla ya watu 9,906 walipata ugonjwa  huu  na kati yao jumla ya watu 149 wameshafariki  dunia kutokana  na  ugonjwa huu. 

  Aidha, wagonjwa wengine wamepata matibabu na kuruhusiwa kurudi nyumbani ambapo hadi tarehe 2 Desemba, 2015 jumla ya wagonjwa 128 waliendelea kupatiwa matibabu katika vituo vya kutolea huduma.

  0 0

  WANAUSALAMA wa mtandao  duniani kote walikamilisha tukio muhimu sana linalofanyika kila mwezi Oktoba (Cybersecurity Awareness Month) lenye dhamira ya kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao huku ikiaminika kupitia tukio hilo uhalifu mtandao unaweza kupunguzwa kwa asilimia kubwa. Mataifa mengi yakiwa na mafanikio makubwa kutokana na hili ambapo Tanzania pia kupitia baadhi ya Makampuni ilipata kushiriki.

  Wakati bado mafanikio mbali mbali yakijadiliwa wahalifu mtandao wamegundulika kuja na uhalifu unaotafsiriwa kuwa ni wa kihistoria na uliofanyika kwa ubunifu na umahiri wa hali ya juu ambapo wahalifu mtandao wamefanikiwa kusambaza kirusi aina ya ModPOS kinacho athiri mashine zinazotumika kukamilisha miamala wakati wa manunuzi.

  Kirusi cha ModPOS, kimegundulika Nchini Marekani wakati wa sherehe za “Thanks Giving” ambapo watu wengi hufanya manunuzi. Kirusi hicho Kimekua kikifanikisha upotevu mkubwa wa pesa wakati wa miamala.
  Mara baada ya ugunduzi huo wa ModPOS, mijadala kupitia mtandao ilianza baina ya wanausalama mitandao ili kuweza kufanikisha mambo makubwa matatu. Moja ni kuweza kugundua chanzo na jinsi ilivyo fanikishwa kuwepo bila kugundulika (Inaaminika kimedumu muda – Taarifa ambazo bado zinafatiliwa) Pili, Ilikua ni kutafuta suluhu ya kirusi hicho ili kiweze kuondolewa na Tatu, ni kupanga namna ya kukuza uelewa wa namna ya kujikinga na janga hili la ModPOS.

  Hadi sasa bado hapaja patikana suluhu na inahofiwa huwenda kutokana na sherehe za mwisho wa mwaka kirusi hicho kusambaa maeneo mengine huku mataifa yakitakiwa kuchukua tahadhari. Inakadiriwa kama kitaendelea kutopatiwa suluhu; pesa nyingi zitaishia mikononi mwa wahalifu mtandao na hasara itakayopatikana ni kubwa zaidi kupata kutokea.

  Wakati hayo yakiendelea kuwa ni mjadala wa vuta nikuvute. Wahalifu wakadukua Kampuni ya VTech inayotengeneza midoli ya watoto ya kielektroniki kutumia TEHAMA ambapo walifanikiwa kuiba taarifa zaidi ya milioni tano ikiwa ni pamoja na Picha za watoto, Mawasilianao ya watoto na wazazi wao, Sauti za watoto, na taarifa za miamala wakati wa manunuzi.

  Inaaminika kutokana na umakini mkubwa wanausalama mtandao wamekua wakiweka juu ya kuwalinda watoto wawapo mtandaoni kitu ambacho kimepelekea kua na program ya kidunia maarufu kama “Child Online Protection – COP” yenye dhamira ya kuhakiki watoto wanabaki salama watumiapo TEHAMA/ Mitandao, Wahalifu walitumia udukuzi wa VTech ili kuhamisha mawazo ya kukabiliana na ModPOS na badala yake nguvu kubwa ihamie kwenye udukuzi VTech.

  Kufuatia udukuzi huo kwenye kampuni ya VTech wanausalama mtandao walishauri Kampuni hiyo kusitisha huduma zake za mtandao mara moja na kuendelea kutafuta suluhu ya tatizo. Huku kampuni hiyo ikitakiwa kuhakiki taarifa zilizo dukuliwa hazipatikani/ kusambwazwa mitandaoni. Kampuni ya VTech tayari imechukua uamuzi wa kusitisha huduma zake mtandao.

  Hayo yakijiri, Nchini Kenya nako wameshatoa Ripoti/taarifa za mwaka kuhusiana na uhalifu mtandao ambapo uhalifu mtandao umeonekana kukua zaidi. Taarifa ilifafanua uhaifu mtando umebadili taswira na kuwa sit u wa kudukua maneno ya siri bali ni taarifa zinazoweza kupelekea mabilioni ya dola kuishia kwa wahalifu mtandao. Jitihada za dhati zimeendelea nchini Kenya ili kukabiliana na uhalifu huu mtandao.

  Tanzania nayo haijabaki salama, Baada ya uhalifu mtandao maarufu kwajina la “vikoba” ulioshika kasi kipindi kifupi cha nyuma uliosababisha waathirika kuibiwa fedha zao na wahalifu mtandao. Baadae elimu juu ya uhalifu huo ilisambaa na hatimae kupungua sasa wahalifu mtandao wamekuja na aina mpya ya uhalifu mtandao wenye dhamira ya kuiba taarifa za watu baada ya kufanikiwa kutengeneza program yenye kuwashawishi watu kuingiza taarifa za wengine kwa madhumuni ya kudukua taarifa za watu binafsi.

  Aidha, wahalifu matandao wajaomea hapo, Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni ya kiusalama mtandao ya “Symantec” imefankiwa kugundua mbinu ambayo wahalifu mtandao wamekua wakitumia mtandao wa kijamii wa “LinkedIn” ambapo wahalifu wamekua waki dhamiria zaidi kuiba taarifa zinazopatikana kwenye mtandao huo baada ya kuweka ukaribu na watumiaji mtandao huo kwa kuwaomba urafiki na baadae kutumia taarifa zilizopo huko kufanya udukuzi.

  Hili tayari Symantec kwa kushirikiana na LinkedIn imeanza opareheni funga akounti zozote zinazobainika kuwa ni za wahalifu mtandao na tunategemea kupata taarifa yake kamili hapo baadae.

  Matukio hayo na mengine yanayowea kujitokeza watai tunaelekea mwisho wa mwaka ushauri mkubwa umeendelea kutolewa ku kuhakiki panakua na mpango endelevu wa kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao (Cybersecurity awareness).

  Pamoja na hilo mataifa yana aswa kua na tabia ya kuhakiki yanatambua kwa ukaribu sana viashiria vyovyote vya kihalifu mtandao ili kuweza kuweka mataifa yao salama kimtandao. Zaidi ni pamoja na kukuza nguvu kazi watu kwenye sekta ya usalama mtandao pamoja na kua na matumizi ya watu sahihi katika kukabiliana na uhalifu mtandao.

  Natoa wito wa kutambua uhalifu mtandao upo na una madhara makubwa katika sekta zote kuanzia Kiuchumi, Kijamii, Kisiasa, nakadhaika endapo hatua kuanzia ngazi ya mtu binafsi hazitachukuliwa ili kuhakiki pana patikana usalama katika mitandao. Tujenge tabia yay a kutafakari kabla ya kutumia mitandao ili kuhakiki hatusababishi madhara kwa kuanzia kwa mtu binafsi pamoja na kwa wengine.

  0 0

  Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues akisoma hotuba mbele ya wageni waalikwa waliofika kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Mafanikio ya Mradi wa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
  (Picha zote na Geofrey Adroph wa Pamoja blog) 
  Kamishana wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini Prof, Eustella Bhalalusesa akizungumza jambo pamoja na kuwashukuru wadau ambao ni hirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) pamoja Ubalozi wa Japani nchini Tanzania ambao wamefanikisha mradi huo wakati wa uzinduzi wa ripoti ya mafanikio ya mradi wa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO. 
  Balozi wa Japani nchini Tanzania Mh. Masaharu Yoshida akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya mafanikio ya mradi wa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito uliofadhiliwa Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO Tanzania.
  Mshauri na Mwakilishi kutoka shirika la UNFPA, Anna Holmstrom akitoa ufafanuzi wa ripoti iliyofanyika katika mkoa wa Shinyanga juu ya wazazi wenye umri mdogo waliopta mimba wakiwa bado shuleni. 
  Ofisa mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta ambaye alikuwa ni msimamizi wa mradi akitolea ufafanuzi kuhusu mradi huo ikihusisha changamoto pamoja na faida za mradi huo uliofanyika Mkoani Shinyanga. 
  Baadhi ya wageni waliofika katika uzinduzi wa Ripoti ya mafanikio ya mradi wa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO. 
  Katibu Tawala wa mkoa Shinyanga, Bw. Abdul Rashid Dachi akizungumza jambo wakati wa uzinduzi huo wa ripoti hiyo.
  Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (kushoto) akitolea ufafanuzi moja ya picha zilizopigwa mkoani Shinyanga wakati kukabidhi vyeti kwa wahitimu walionufaika na mafunzo mbalimbali kupitia mradi huo.
  Subira akitoa ushuhuda kwa jinsi alivyopata ujauzito akiwa shuleni na alivyofanikiwa kutokana na Mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Japan. 
  Veronika Amosy akitoa ushuhuda na kueleza changamoto zilizomkuta mara baada ya kubeba mimba akiwa shuleni. 
  Mkufunzi Mkazi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Bw. Said Kayege kutoka mkoani Shinyanga akizungumza ni kwa namna gani wanavyotoa mafunzo hasa kwa mabinti waliopata mimba wakiwa mashuleni na kupelekea kuacha masomo yao. 
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima nchini, Dk. Fidelis Mafuniko akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa ripoti ya wazazi wenye umri mdogo walio pata mimba wakiwa shuleni. 
  Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues kwenye picha ya pamoja na wasichana waliopata mimba wakati wako masomoni ambao ni Veronika Amos (kushoto) pamoja na Subira (kulia). 
  Picha ya Pamoja

  Na Mwandisi wetu
  Shirika la Elimu, sayansi na utamaduni (UNESCO) lazindua Ripoti ya wazazi wenye umri mdogo walio pata mimba wakiwa shuleni, ambapo kama shirika waliweza kuwasaidia kwa kuwaanzishia mfumo maalumu utakao wasaidia katika kujiendeleza kielimu kwa kushirikiana na Elimu ya watu Wazima MOEVT. 

  Akiongea wakati wa uzinduzi huo mgeni rasmi Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufund (MOEVT)i nchini Prof, Eustella Bhalalusesa amesema cha kwanza ni kuishukuru serikali ya Tanzania kwa kuweka ushirikiano na shirika hili la UNESCO kwani ni jambo zuri hasa ukizingatia wote wanafanya kazi zinazo endana , cha pili nikuendelea kuungana kwa ajili ya kuweza kutoa elimu ya jinsia kwa ajili ya kuepuka mimba za utotoni kwa wanafunzi walioko mashuleni hivyo ameipongeza (UNESCO) kwa kutambua thamani ya watoto wa kike hasa wale walioshindwa kuendelea na masomo kwa kuwaanzishia njia mbadala za kuweza kuwafundisha kwa kuungana na elimu ya watu wazima kwani msingi wa watoto hao ni Elimu. 

  Naye Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues amesema wao kama shirika walianza kufanya mchakato wa kufanya tafiti kwa mikoa mbalimbali na kugundua kwamba watoto wengi wa jinsi ya kike wameweza kukatiza masomo yao kutokana na kupata mimba pindi wawapo shuleni ndipo walipoamua kuanzisha namna ya kuweza kumkomboa mtoto wa kike aweze kupata elimu inayoweza kumsaidia katika maisha yake kwa kuweza kuwasiliana na Mkurugenzi wa elimu ya watu wazima MOEVT na kuanzisha mchakato wa kuweza kuwakomboa kielimu. Vilevile Bi. Rodrigues aliongeza kwa kusema wazazi waweze kukaa na watoto na kuwafundisha elimu ya kijinsia na kuweza kuwatatulia shida mbalimbali walizonazo kwani ndio hupelekea watoto kuingia katika tamaa mbalimbali hususani wakiwa katika hatua za mabadiliko ya mwili. 

  Naye Balozi wa Japani nchini Tanzania Mh. Masaharu Yoshida amesema wazazi wenye umri mdogo Tanzania ni wengi na wanauhitaji wa kupata mafunzo ya Elimu kwa hali na mali hivyo kama ubalozi wa Japan umeamua kuanzisha mradi wa kuwasaidia wazazi hao mradi huo ambao unaratibiwa na (UNESCO) ulianza toka mwaka 2012 ambapo ulianzishwa na Bi.Zulmira Rodrigues, Mr. Min Jeong Kim na Jennifer Alima-Kotta uliogharimu kiasi dola za Kimarekani 400,653 kutoka Japanese Funds-in-Trust, Lengo kubwa ni kutaka kumkomboa mtoto wa kike ambaye amepata au alipata ujauzito akiwa shuleni, Pia alitoa shukrani kwa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kuweza kuwapa ushirikiano kuanzia walipoanza mpaka hivi leo na aliweza toa wito kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa kuomba kuendelea kupambana na mimba za wanafunzi wawapo mashuleni na kuendelea kutilia mkazo sheria zitakazo wabana watu wanao sababisha ujauzito kwa mtoto wa kike awapo shuleni. 

  Aidha Ofisa Mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta msimamizi wa mradi huo alieleza dhumuni la mradi na namna gani wameweza kufanikiwa pamoja na changamoto zake ambapo alianza kwa kueleza kuwa mradi huo sio rasmi ndio maana wameweza kushirikiana na elimu ya watu wazima kwani wanafunzi wengi wa kike huwa wanapata vishawishi mbalimbali pindi wawapo mashuleni na kuweza kuwa sababishia kuwa wazazi wadogo. 


  Kotta amesema kumekuwa na mambo mengi yanayo wakumba wanafunzi wa kike wawapo mashuleni na ndio husababisha madhara makubwa ambayo hupelekea wanafunzi hao kuwa wazazi wenye umri mdogo na bila kutegemea kwani ni ajabu na ni jambo la kusikitisha sana mtoto ana mlea mtoto mwenzake na kuwa na imani kuwa ndoto zake haziwezi timia kwa kutoendelea na masomo pindi awapo mjamzito au pindi akijifingua, ambapo aliwaomba wazazi kwani hali iliyopo kwa sasa kwa watoto wetu si nzuri sana tukumbuke kuwahimiza watoto kuhusu mila na desturi zetu na pia kuwa wafuatiliaji kwa nguvu zote kwani wazazi wengu huwa wanawadharau watoto wa kike kwa kudhani hawana msaada na ndipo yeye kama mtoto anaamua kuchukua uamuzi wake binafsi na kukuta wanaangukia katika hali ya kuwa mzazi mwenye umri mdogo vilevile aliweza kusisitiza kuhusu kuwalinda watoto wa kike hasa kipindi cha mabadiliko ya mwili ambapo ndipo changamoto mbalimbali hutokea kwa watoto hao hasa pindi wawapo mashuleni na hata mitaani. 

  Hata hivyo mmoja ya wazazi wadogo walioweza kuchukuliwa na kusaidiwa na Shirika la (UNESCO) Tanzania, Chausiku Subira aliweza kutoa ushuhuda namna gani wanavyokumbana na changamoto hizo mpaka hatimaye kuwa wazazi katika umri mdogo wakiwa bado ni wanafunzi. "katika safari yangu ya kimasomo mara baada ya kumaliza elimu ya msingi niliweza kuchaguliwa na kuendelea na elimu ya pili hapo ndipo ndoto zangu zilipoishia kwa kupata ujauzito ambao ulinipelekea kufukuzwa shule na hatimaye kurudishwa nyumbani jambo lililokuwa gumu kwangu kwani ujauzito huo ulikuwa sio wa kutegemea hasa ukizingatia mimi nikiwa bado mwanafunzi, nyumbani walinifukuza na kusababisha niwe na maisha magumu nisiyo ya tarajia nikizingatia nimepoteza shule pia hata ndugu hawanitaki lakini hiyo yote ni kutoka na na miundombinu ya shule tunazo soma kuwa mbali na makazi na kupelekea wanafunzi wengi kutembea kwa mguu umbali mrefu huku wakiwa na njaa na kuingia katika vishawishi mbalimbali", alisema Subira.

  Pia Subira aliweza kutoa wito kwa serikali kwa kujenga mabweni katika shule mbalimbali na kuweza kuwatengenezea mazingira ya kuweza kurejea mashuleni pindi wanapojifungua kwa ajili ya kuweza kutimiza ndoto walizo kuwanazo pia kuweka sheria ambayo itakuwa inatenda haki kwa kila mmoja kwani imekuwa ni kwa mtoto wa kike tu kufukuzwa huku aliye sababisha ujauzito mtoto wa kiume kubaki akiendelea na masomo vilevile katika upande wa shule kuweza kutoa mafunzo kwa watoto wa kike kuhusu elimu ya jinsia na ninamnagani wanaweza wakajiepusha na vishawishi wanavyo kutananavyo.

  0 0

  Dk. Nalin Nag Mshauri Mwandamizi wa madawa, aleji, upungufu wa kinga pamoja na magonjwa ya kuambukiza kutoka hospitali za Apollo; New Delhi.
  Na Mwandishi wetu.
  SIKU ya UKIMWI duniani inaadhimishwa tarehe mosi desemba kila mwaka, kutoa fursa kwa jamii kuungana ulimwenguni kupiga vita gonjwa la UKIMWI, kuwapa moyo wale wote wanaoishi na virusi vya ukimwi na kuwakumbuka wote waliokufa kwa ugonjwa huu. Siku ya ukimwi duniani iliadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1988.

  Zaidi ya miaka 30 toka ukimwi ulipoanza kusambaa nchini Tanzania, msisitizo umewekwa kwenye maendeleo ya mikakati na mbinu zaidi za kupunguza maambukizi na kuongeza huduma za matibabu. Kwa mwaka 2011, inakadiriwa watanzania milioni 1.6 walikuwa wanaaishi na virusi vya UKIMWI na miongoni mwao, milioni 1.3 ni wenye umri zaidi ya miaka 15, hiyo ni kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2012 kutoka shirika la umoja wa mataifa la kupambana na UKIMWI (UNAIDS).

   Licha maambukizi ya UKIMWI kwa Tanzania bara yamepungua kutoka asilimia 7.0 hadi 5.3 katika kipindi cha mwaka 2003/2004 mpaka 2011/2012 miongoni mwao wakiwa watu wenye umri wa miaka 15-49 na kutoka asiimia 6.3 mpaka 3.9 ambao ni wanaume katika kundi hilo, na hakuna takwimu nzuri za kuonyesha kupungua kwa maabukizi kwa upande wa wanawake.

  Kwa mujibu wa TACAIDS taarifa za mwaka 2013, kwa tanzania bara maambukizi kimikoa yanatofautiana kutoka asilimia 1.5 kwa mkoa wa Manyara hadi asilimia 14.8 kwa mkoa wa Njombe.

  “Kufikia sifuri tatu” ndio kauli mbiu iliyochaguliwa na kampeni ya siku ya ukimwi duniani kuadhamisha ya siku ya UKIMWI duniani kwa mwaka huu. Kwetu tanzania kupitia TACAIDS tunahamasisha “kufikia sifuri tatu” tukimaanisha “sifuri katika maambukizi mapya ya UKIMWI”, sifuri katika kuwanyanyapaa na kuwanyanyasa waathirika, na sifuri katika vifo vinavyohusisha UKIMWI”. 

  Maudhui hayo yalipitishwa tokea mwaka 2011 yatumike mpaka 2015, yakitafsiri yale malengo ya UNAIDS ya kufikisha kiwango cha “kufikia sifuri katika maambukizi mapya ya UKIMWI”, na sifuri katika vifo vinavyohusisha UKIMWI”. Maamuzi ya kuchagua “kufikia sifuri tatu” yalifikiwa baada ya mahojiano ya kina na watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI, wanaharakati wa afya na taasisi ya kijamii.

  Katika kuweka msisitizo katika maudhui ya mwaka huu, “kufikia sifuri tatu”, Dk. Nalin Nag mshauri mwandamizi wa madawa, aleji na upungufu wa kinga pamoja na magonjwa ya kuambukiza kutoka hospitali za Apollo; New Delhi anawaasa watanzania kuepuka maambukizi mapya ya UKIMWI, kuepuka kunyanyapa waathirika wa UKIMWI katika familia na jamii zetu na ikiwezekana kufuta kabisa vifo visababishwavyo na UKIMWI.

  ”UKIMWI ni kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wetu na tunaweza kupambana nacho kwa urahisi zaidi ya mashambulizi ya kigaidi yanayofanywa kwa kushtukizwa- “kufikia sifuri” katika maambukizi ya UKIMWI inawezekana kabisa kama wote tukidhamiria. Alisisitiza Dk. Nalin Nag
  Mtazamo chanya katika maisha, ushirikiano kutoka katika familia na marafiki, malalamishi ya ukandamizwaji kutoka kwenye jamii kwa wingi wa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI ni tatizo la muda tu. Sheria kali zinahitajika kulinda na kutunza utu wa wahanga wa janga hili. Aliongeza Dk. Nalin Nag.

  Dk. Nalin Nag anasisitiza kuwa wagonjwa UKIMWI wafanye vipimo vyote vya afya zao mara kwa mara, vipimo vya damu maabara, ufanisi wa ini, figo, kifua na tatizo la hepatitis B. magonjwa nyemelezi kama kifua kikuu, pneumonia na mengineyo yanatakiwa kudhibitiwa muda wote kabla ya kuanza kutumia dawa za ARV.

  “mlo sahihi, uongezaji wa kinga, mitindo ya maisha, na namna ya kupambana na msongo wa mawazo ni vitu vinavyojumuisha mlolongo wa kuboresha maisha bora kwa waathirika ambao kwa sasa wanatarajia kuongeza muda wa maisha yao kwa matumizi sahihi ya ARV. Alisema. 

  Dk. Nalin Nag anaelimisha jamii kuhusu umuhimu wa matumii ya dawa za ARV kwa waathirika wote wa UKIMWI. Hii imebadilisha kabisa makali ya ugonjwa na kuongeza ujasiri katika kutokomeza maambukizi mapya. Dawa tofauti za ARV zinapatikana na zinatumika zikiwa na kinga za aina 4 tofauti kwa ajili ya kudhibiti nguvu za virusi na kupunguza makali ya ugonjwa.


  “katika mazingira mengine huwa virusi havionekani kwenye damu hadi mwishoni mwa miezi sita hadi mwaka” aliongeza Dk. Nalin Nag kutoka Hospitali za Apollo Indraprastha.

  Katika kitengo cha afya ugonjwa wa UKIMWI unabaki kuwa changamoto kubwa ulimwenguni, hasa kwa wananchi wenye kipato cha chini au cha kati. Na matokeo ya hivi karibuni kuhusu upatikanaji rahisi wa ARV, kumefanya wagonjwa wa UKIMWI kuweza kuishi maish marefu zaidi yenye afya bora. Kwa kuongezea, imedhibitishwa kuwa ARV inaepusha maambukizi endelevu ya UKIMWI.

  UKIMWI umeendelea kuenea ulimwenguni, kwa mujibu wa taarifa za sasa za shirika la umoja wa mataifa la kupambana na UKIMWI (UNAIDS) takwimu za mwaka 2012, inakadiriwa watu milioni 34 wanaishi na virusi vya UKIMWI zaidi ya jinsi ilivyokuwa awali nah ii pia ni kutokana na matumizi ya dawa za ARV. Nchi zilizopo chini ya jangwa la Sahara zimebaki kuwa nchi zilizoathirika zaidi na janga hili la UKIMWI. Mwaka 2011, ilikadiriwa kuwepo kwa maambukizi mapya milioni 1.8 kwa nchi hizo; asilimia 69 ya watu wote wanaoishi na virusi vya UKIMWI wanapatikana katika nchi zilizopo chini ya jangwa la Sahara barani Afrika (UNAIDS, 2012).

  Kuhusu Hospitali za Apollo
  Hospitali ya Apollo ilifunguliwa mnamo mwaka 1983, na kutoka kipindi hicho imekuwa ikiendeshwa kwa kauli mbiu isemayo "Dhamira yetu ni kuleta huduma ya kisasa karibu kabisa na walengwa. Tunajitolea kutoa huduma bora na mafanikio katika elimu na utafiti kwa ajili ya jamii ya kibinadamu".Katika miaka 30 tokea kuanzishwa kwake, hospitali ya Apollo imeandika historia kubwa kupata kuonekana nchini India. Ni moja ya kampuni kubwa ya Afya katika bara la Asia, na pia imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya nchini india.

  Katika safari yake, imeweza kuboresha maisha ya watu wapatao milioni 39 kutoka nchi 120.Inatoa huduma maalum 52 na vitanda vya upasuaji 710.Imefanya upasuaji wa moyo wenye kufikia idadi ya watu 152,000 na panuzi 125, 000 za mishipa myembamba.Imefanya upasuaji wa wa viungo unaopita kiasi cha idadi ya watu 10,000, upasuaji wa uvimbe wa ubongo, uti wa mgongo na zaidi.Taasisi ya Apollo ni moja ya taasisi zinazoongoza nchini india, zikiwa na teknolojia za kisasa kama Novalis TX, PET MRI na Upasuaji unaotumia mashine za kiroboti.

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho na Nyakongo Manyama -MAELEZO
  SERIKALI ya Tanzania imesaini mikataba miwili na Serikali ya Uswisi ili kuendeleza na kuimarisha huduma za kijamii nchini hasa katika Sekta ya Afya.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salam Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile amesema kuwa kupitia ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili, Serikali ya Uswisi inaendelea kusaidia kuboresha Sekta ya Afya nchini hususani kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora. 

  “Uswisi imesaidia Sekta ya Afya kwa miaka 15 na mpaka sasa imeshachangia jumla ya shilingi billion 181.7 kuanzia miradi ya afya ianzishwe nchini” alisema Likwelile.

  Aidha, Dkt. Likwelile aliongeza kuwa Serikali ya Uswisi imelenga pia kusaidia kuimarisha utoaji wa huduma katika idara ya Afya katika Serikali za Mitaa kwa kuzingatia usawa na ubora wa huduma hizo hasa kwa wanawake,watoto pamoja na makundi yaliyotengwa hasa maeneo ya vijijini. 

  Zaidi ya hayo, Dkt. Likwelile amesema kuwa Serikali ya Uswisi itarajia kuungana na Serikali ya Tanzania katika kuboresha sera za malipo kwa wafanyakazi wa Afya ili watoe huduma bora yenye tija kwa jamii.

  Kwa upande wake Balozi wa Uswisi Nchini Tanzania Bi. Florence Tinguely Mattli amesema kuwa amefurahishwa na utoaji bora wa huduma za Afya Nchini Tanzania ambazo zimekuwa zenye tija kwa wananchi wanapokuwa wanahitaji huduma hizo kwa wakati.

  Bi. Florence aliongeza kuwa Serikali ya Uswisi kupitia Mfuko wa Pamoja wa Afya mkoa wa Dodoma umekuwa wa kwanza kunufaika na mfuko huo ambapo mikoa mingine inayotarajiwa kunufaika ni pamoja na Morogoro na Shinyanga ili kuboresha afya ya wanawake, watoto, vijana wazee na watu wasiojiweza. 

  Naye Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Donan Mmbando alisema kuwa lengo la fedha hizo ni kuhakikisha huduma za Afya zinawafikia watu wote wenye mahitaji hayo kwa wakati.

  “Mchango huo wa fedha umechangia sana katika kutekeleza malengo ya Millenia kwa kupunguza vifo vya watoto kwa asilimia 4 kwa mwaka 2013 kwa kuboresha utoaji wa chanjo kwa watoto na tiba sahihi ya ugonjwa wa Malaria kwa kiasi kikubwa”. Alisema Dkt. Mmbando

  Pia Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Jumanne Sagini amesema kuwa ameishukuru Serikali ya Uswisi kwa msaada walioupata na kuahidi kuwa fedha hizo zitatumiwa katika kuboresha zaidi huduma ya Afya katika Mikoa iliyoongezwa kuanzia ngazi za Wilaya. 


  Mfuko wa pamoja wa Afya ulianzishwa nchini kwa lengo la kusaidia kuboresha huduma za Afya kwa kushirikiana na Serikali ya Uswisi pamoja na nchi zingine zilizoendelea ikiwemo Canada, Denmaki na washirika wengine wa maendeleo.

  0 0

  SIMU.TV:  Profesa Lipumba aachiwa huru. Rais Magufuli atoa siku 7 kwa waliokwepa kodi. Shule binafsi marufuku kuongeza ada;  https://youtu.be/7bO6JnD7hNA
  SIMU.TV:  Makontena 2431 yatoka TPA bila ushuru. Serikali yajipanga kuifumua TANESCO. Kito cha radio Hits FM chavamiwa, chachomwa; https://youtu.be/inH-0GdWXoo 
  SIMU.TV:  Vigogo TRA wakutwa na mamilioni nyumbani. Mama lishe akutwa akipika chakula juu ya chemba ya maji taka; https://youtu.be/6f0nyf3sqRg
  SIMU.TV:  Ngoma apewa Sh. Milioni 200. Tambwe apata gonjwa la ajabu. Straika hatari asaini miaka mitatu Simba; https://youtu.be/WddwexVxOdk 
  SIMU.TV:  Songas yatishia kuzima mitambo yake ya umeme kutokana na fedha inayoidai TANESCO. Wataka kubomoa kaburi la Mawazo. Pata habari za kina katika magazeti ya leo Disemba 2.2015; https://youtu.be/44X9CLV5XfU


  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

  ISO 9001:2008 CERTIFIED
  TAARIFA KWA UMMA
  TAHADHARI KUHUSU KUINGILIA AU KUFUATILIA MAWASILIANO YA WATU

  Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa za kuwepo kwa Programu (Application) ya simu ikijulikana kama SOFTBOX TANZANIA iliyosemekana iko kwenye Google PLAYSTORE.

  Ilidaiwa kuwa program (Application) hiyo ya SOFTBOX TANZANIA ilikuwa na uwezo wa kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya mtu binafsi.

  Kwa yeyote aliyekuwa na nia hiyo ya kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya mtu mwingine alihitajika kulipia fedha kiasi cha Tshs 35,000/= kupitia mitandao ya simu ili kupata namba ya siri kwa ajili ya kuwezesha nia hiyo.

  Mamlaka ya Mawasiliano imefanya uchunguzi kubaini kuwepo kwa programu hiyo na ukweli kuhusu uwezo wake wa kufanya kilichodaiwa, ikiwa ni pamoja na kuangalia madhara ya program hiyo na sheria inasema nini kuhusu suala hili. Baada ya kufanya uchunguzi wa kina, Mamlaka ya Mawasiliano ilibaini na imejiridhisha kuwa program (Application) hiyo haina uwezo huo wa kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya mtu binafsi kama ilivyodaiwa.

  Aidha Mamlaka imebaini kuwa watengenezaji (Developers) wa programu hiyo walikuwa na nia ya kutapeli na kujipatia fedha hiyo kiasi cha Tshs 35,000/= kwa njia ya udanganyifu wakitumia kivutio cha kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu za watu binafsi.

  Programu (Application) nyingine ya aina hiyo iliibuka tena ikiitwa SIMNET Tanzania ikiwa na maelezo kama ya awali.

  Wakati Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania pamoja na Jeshi la Polisi wakiendelea na uchunguzi zaidi, tunapenda kuuarifu umma wa Watanzania kuepuka kufanya mambo yafuatayo:

  1. Kuvutiwa na matendo yaliyo kinyume na sheria na maadili ya matumizi mazuri ya mawasiliano kama hili la kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya mtu binafsi. Kitendo hiki ni kosa la jinai kwa mujibu wa kifungu cha 6 na 10 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 na kifungu cha 123 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya Mwaka 2010. Sheria katika vifungu hivyo inakataza mtu yeyote kuingilia mawasiliano ya mtu mwingine. Adhabu kali ya makosa haya ni faini isiyopungua shilingi milioni tano au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja.

  2. Mamlaka inawatahadharisha watumiaji wa huduma za mawasiliano kutokuwa wepesi na kudanganyika kufanya malipo yoyote kwa njia ya mitandao kwa huduma wasiyokuwa na uhakika nayo au bila kujiridhisha na uwepo wa huduma hiyo. Ni vizuri kutoa taarifa kwa mtoa huduma wako au kuwasiliana na Mamlaka ya Mawasiliano kupitia barua pepe malalamiko@tcra.go.tz au kupiga simu namba 0784558270/1.
  Imetolewa na:
  Mkurugenzi Mkuu
  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania

  04/12/2015.

  0 0

  Wanyama aina ya Nyati wanane wakiwa wamekufa baada ya kugongwa na gari aina ya Fuso kwenye mbuga ya Wanyama ya Mikumi na kusababisha foleni ya magari. Tukio hili limetokea alfajiri ya leo tarehe 4 Desemba 2015.

  0 0

  WATU wawili wamefariki dunia Papo hapo baada ya Gari walilokuwa wakisafiria lililobeba Magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti kwenda mkoani mkoani Mbeya kupata ajali Eneo la Kitonga Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.


  Ajali hiyo imetokea leo alfajiri baada ya dereva wa Gari hilo kujinusuru kugongana uso kwa uso na gari jingine, hivyo kulazimika kuingia nyuma ya lori na kupelekea kifo chao.

  Kwa mujibu wa Wakala Afisa mauzo wa magazeti ya Mwananchi Mkoa wa Iringa Alex Kadea ambae alifika Eneo la tukio ameithibitisha kutokea kwa ajari hiyo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa mtandao www . Matukiodaima.co.tz kuwa waliofariki dunia wote wawili walikuwa ni madereva wa Gari hilo.

  Gari iliyokuwa ikisafirisha magazeti ya Mwananchi Communications kuelekea mkoani Mbeya na Iringa ikiwa imepata ajali Eneo la Kitonga Mkoani Iringa leo asubuhi.

  0 0


  (Pichani ni Watoto walioathirika na Polio. Picha kwa hisani ya shirika la WHO).
  Na Magreth Kinabo.
  TANZANIA imetangazwa rasmi kuwa ni mojawapo ya nchi isiyokuwa na ugonjwa wa polio katika nchi za Afrika katika mkutano wa Tume ya Afrika ya kuthibitishwa kutokomezwa kwa polio(Afrika Regional Certification Commission for Polio Eradication).

  Kutangazwa kulifanyika katika mkutano huo uliofanyika nchini Madagascar, Novemba 26, mwaka huu.

  Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu ugonjwa huo ulifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam.

  “Hii inamaanisha kuwa kwa sasa hatuna ugonjwa wa polio tena nchini kwa sababu tumeweza kuwafikia watoto wengi zaidi kwa kuwapatia chanjo ya polio na hivyo kuongeza kinga kwenye jamii.Kutokana na mafanikio hayo, tunatakiwa bado kuendelea na kutoa chanjo ya polio kwa watoto wote stahiki ili kuongeza kinga kwa jamii pamoja kuimarisha mfumo wa ufutiliaji wa mgonjwa yoyote mwenye ulemavu wa ghafla,” alisema Dkt. Mmbando.

  Katibu Mkuu huyo alifafanua kwamba mgonjwa wa mwisho wa polio alipatikana Julai mwaka 1996 hapa nchini.

  Aliongeza kuwa ufuatiliaji wa magonjwa yanayokingwa na chanjo uliimarishwa na kufikia viwango vinavyo kukubalika kimataifa na kuthibitisha kuwa watoto wenye umri chini ya miaka 15 waliopata ulemavu wa ghafla wanapatikana na sampuli zao kuchukuliwa mara moja. 

  Hivyo kuanzia mwaka 1997 mpaka Oktoba 2015 jumla ya sampuli 6,249 za watoto waliopata ulemavu zilipelekwa kwenye maabara za kimataifa na kuthibitishwa kuwa hakuna sampuli iliyoonesha uwepo wa ugonjwa wa polio.

  Dkt. Mmbando aliongeza kwamba wizara yake kupitia Mpango wa Taifa wa Chanjo imekuwa ikihakikisha kwamba watoto wote Tanzania wanapata chanjo zenye ubora ili kuwakinga dhidi ya magonjwa ya milipuko ikiwemo ugonjwa wa polio.

  “ Mwitikio wa wananchi kwa huduma za chanjo umeendelea kuwa mkubwa kwa takribani miaka kumi iliyopita na kufikia viwango vya zaidi ya asilimia 90 kwa kila chanjo kitaifa na wilaya zaidi ya asilimia 80 kufanya vizuri katika kutoa huduma za chanjo,” alisema Dkt. Mmbando.

  Ugonjwa wa polio ni ugonjwa wa kuambukizwa unaosababishwa na virusi vya polio, unaathiri misuli na mfumo wa fahamu hivyo kusababisha kupooza kwa viungo hasa na miguu na wakati mwingine kusababisha hata kifo .

  Alisema ulemavu huo ukishajitokeza huwa ni wa kudumu, waathirika wakuu wa ugonjwa huo ni watoto hasa waliaochini ya umri wa miaka mitano.

  Aliongeza kwamba ugonjwa huo unazuilika kwa chanjo ya polio ambayo ni salama na inatolewa bure na Serikali katika vituo vyote vya huduma ya afya.

  Dkt. Mmbando alitoa pongezi kwa wananchi wote wakiwemo viongozi na watendaji wa ngazi zote kwa ushirikiano wao ambao umeifikisha Tanzania kwenye ramani ya dunia ya kutokuwa na ugonjwa huo.

  Aidha wizara imewashukuru wajumbe wa kamati mbalimbali za kutokomeza ugonjwa huo chini ya uongozi wa Profesa Ester Mwaikambo, watendaji wa Mpango wa Taifa wa Chanjo na wadau wa chanjo, wadau wa mfuko wa pamoja wa Pamoja wa Afya , WHO, GAVI, UNICEF, CHAI, USAID,
  REDCROSS NA LIONS CLUB kwa kazi kubwa ya kuhakikisha kila mtoto mlengwa anapata chanjo.

  Tanzania ni miongoni mwa nchi nne ambazo zimepata cheti hicho mwaka huu, katika bara hilo.Pia ni nchi ya 33 kati ya nchi 47 za bara hilo ziliowahi kupata cheti hicho. 

  Katika bara hilo bado nchi 14 ambazo hazijawahi kupata cheti hicho.

  0 0

  Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo (wa nne kushoto) akisisitiza jambo katika kikao kazi kilichowakutanisha watendaji wakuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF na Business Times. Menejimenti ya PSPF ipo katika ziara ya kutembelea vyombo vya habari kwa lengo la kutolea ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali ya Mfuko na kutambulisha huduma mpya ya Bima ya Afya. (Picha zote na Abdul Njaidi).
  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu akifafanua jambo kwa Wahariri wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) alipotembelea Makao Makuu ya MCL, Tabata Relini jijini Dar es salaam, kulia ni watendaji wa PSPF.
  Meneja Mkuu wa Business Times Limited Bw. Aga Mbuguni (kushoto) akipokea machapisho mbalimbali ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF kutoka kwa Mkurugenzi mkuu wa Mfuko huo Bw. Adam Mayingu baada kikao cha watendaji wakuu wa taasisi hizo kilichofanyika Makao Makuu ya Business Times jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Bw. Francis Nanai (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugezi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, baada ya kikao kazi kati ya Wahariri wa Mwananchi na Watendaji wa PSPF, kushoto ni Bw. Daniel Mwaijega Meneja Utawala Idara ya Habari na kulia ni Bibi. Matlida Nyalu Afisa wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF.


  MKURUGENZI Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu aliongoza ujumbe wa watendaji wakuu wa PSPF kutembelea vyumba vya habari vya magazeti ya Mwananchi na Majira, ikiwa ni utaratibu wa PSPF wa kutembelea vyombo vya habari kwa lengo la kufahamiana, kutolea ufafanuzi masuala mbalimbali na kupokea ushauri wa kuboresha huduma za PSPF. 

  Katika ziara hiyo iliyofanyika Desemba 2, 2015, Mkurugenzi wa PSPF aliongozana na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Bw. Gabrilel Silayo, Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bibi Neema Muro, Mkurugenzi wa TEHAMA, Bw. Andrew Mkangaa, Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi, Bibi. Costantina Martin, Afisa kutoka Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF, Bibi. Mathilda Nyallu na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Bw. Abdul Njaidi. 

  Kituo cha kwanza cha safari hiyo ilikuwa katika ofisi za gazeti la Majira wachapishaji wa Gazeti la Majira na Business Times ambapo walikutana na watendaji wakuu wa kampuni hiyo. 

  Pia viongozi hao wa PSPF walitembelea ofisi za Mwananchi Communications zilizopo Tabata, ambapo walikutana na watendaji wakuu wa gazeti hilo. Katika maeneo yote watendaji wa PSPF walijibu maswali mbalimbali, walipokea ushauri na kutambulisha huduma ya Bima ya Afya inayotolewa na PSPF kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. 


  “Lengo la ziara hizo ni kuwatembelea wenzetu wa vyombo vya habari kwa lengo la kufahamiana, kutolea ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali ya PSPF na kujifunza kutoka kwao jinsi ya kuboresha huduma zetu, pia kwa sasa tunatangaza huduma yetu mpya ya Bima ya Afya,hivyo tupo katika mpango wa kuwaelimisha waandishi wa habari ili na wao waweze kuelimisha umma juu ya mpango huo ambao ni mkombozi kwa watanzania wengi…huu ni mwendelezo kwani tulianza ziara hizi tangu mwaka jana,” alifafanua Bw. Mayingu.

  0 0

   Rais John Magufuli ametoa siku 7 kwa wafanyabiashara waliokwepa kulipa kodi kwa kutorosha makontena  kuhakikisha wanalipa haraka.


  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe A bass Ali Hassan Mwinyi, akitembelea Kituo cha Afya cha Fuoni Zanzibar kinachotowa huduma kwa Wananchi wa Jimbo hilo na jirani wakati akitimiza ahadi yake kwa kutuo hicha, akipata maelezo kutokwa kwa mdhamini wa kituo hicho Muuguzi wa Afya ya Jamii Bi Mwaka Pandu Makame akitowa maelezo ya eneo lao la kuchomea taka za kituo hicho.
  Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Ali Hassan Mwinyi akitembelea kituo hicho cha Afya Fuoni Zanzibar akiwa katika ziara yake katika jimbo lake kujiuonea ufanisi wa kituo hicho na kukabidha Madawa na kuvifanyia mategenezo vyoo vya kituo hicho ni moja ya kero za Wananchi wanaofika kituoni hapo. 
  Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Adass Mwinyi akitembezwa katika kituo hicho na Madaktari wa Kituo hicho, akiwa katika ziara yake ya kukamilisha ahadi yake juu ya kituo hicha kikifanyia mategenezo sehemu. 
  Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Mwinyi akimsikiliza daktari wa kitengo cha kungolea meno katika Kituo hicho cha Fuoni Zainab Seif na Khadija Khamis, wakimueleza Mbunge huyo baadhi ya vifaa vinakosekana katika kitengo chao kwa ajili ya huduma ya kungolea meno Wananchi wanaofika kituoni hapo. Kituo hicho kinatowa huduma za Uzalishaji wa Kinamama kupiga Utra saund na huduma nyengine za matibabu.
  Mbunge wa Fuoni Mhe Abass Mwinyi akizungumza wa Wafanyakazi wa Kitengo cha Meno katika Kituo cha Afya Fuoni wakati wa ziara yake kutimia ahadi alizotowa kwa Wananchi wa Jimbo hilo katika kituo hicho na kufanikisha upatikanaji wa vifaa hivyo wanavohitaji katika kituo hicho kuondoa kero kwa Wananchi wake wanaofika kituoni hapo kupata huduma ya meno na nyeginezo.
  Mhe Abass Mwinyi akizungumza na Wafanyakazi wa Kituo cha Afya Fuoni Zanzibar wakati wa ziara yake kutembelea Kituo hicho na kukabidhi madawa kwa ajili ya kituo hicho, Kinachotowa huduma kwa Wananchi wa Jimbo lake na Wananchi wa jirani.ili kuboresha ufanisi wa huduma ya Afya kituoni hapo. 
  Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe. Abass Mwinyi akizungumza na wafanyakazi wa Kituo hicho na Wananchi wa Jimbo lake wakati wa ziara yake ya kwanza katika jimbo hilo na kukabidhi vifaa na Madawa kwa kituo hicho. Mhe Mbunge Abass amesema sasa Hapa Kazi Tu, ili kuwaletea maendeleo Wananchi wa Jimbo lake na kuondoa kero zote katika jimbo hilo na kuwa Jimbo la mfano katika majimbo yote ya Zanzibar. 
  Daktari Dhamana wa Kituo cha Afya Fuoni Said Fadhili Abass akizungumza wakati wa mkutano huo na Mbunge wa Jimbo la fuoni na kumshukuru kwa msaada wake huo kwa Kituo chao. na kusema dawa hizo zitatumika kwa wananchi wa Jimbo hilo wanaofika kituoni hapa kupata huduma mbalimbali za Afya. 
  Wauguzi wa Kituo cha Afya Fuoni wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Fuoni Mhe Abass Mwinyi wakati akizungumza na Wafanyakazi hao katika ziara yake kutembelea Kituo hicho na kukabidhi madawa kwa ajili ya Wananchi wanaofika kupata huduma kituoni hapo.
  Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Ali Hassaan Mwinyi akimkabidhi fedha shilingi milioni moja Dakt. Dhamani wa Kituo cha Afya Fuoni Zanzibar Said Fadhil Abass, kwa ajili ya kutatua makero zinazokikabili kituo hicho cha Afya Fuoni ili kufanya kazi zao kwa kuwahudumia Wananchi kwa ufanisi zaidi.
  Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Ali Hassaan Mwinyi akimkabidhi madawa Dakt. Dhamani wa Kituo cha Afya Fuoni Zanzibar Said Fadhil Abass, kwa ajili ya matumizi ya kituo hicho kinachotowa huduma mbalimbali kwa Wananchi wa Fuoni zikiwemo za kuzalisha kinamama na upigaji wa vipimo vya utra sound katika kituo hicho na kulaza wagonjwa. 
  Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Ali Hassaan Mwinyi akimkabidhi vifaa kwa akili ya vyoo vya kituo hicho Dakt. Dhamani wa Kituo cha Afya Fuoni Zanzibar Said Fadhil Abass na kulia Muuguzi wa Afya ya Jamii Kituoni hapo Mwaka Pandu Makame. 
  Mzee wa Jimbo la Fuoni Mzee Takrima akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi madawa na vifaa katika Kituo cha Afya Fuoni Zanzibar.
  Wananchi wa Jimbo la Fuoni wakimsikiliza Mbunge wao. 
  Wauguzi wa Kituo cha Afya Fuoni wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Fuoni Mhe Abass Mwinyi wakati akizungumza na Wafanyakazi hao katika ziara yake kutembelea Kituo hicho na kukabidhi madawa kwa ajili ya Wananchi wanaofika kupata huduma kituoni hapo.
  Mwananchi wa Jimbo la Fuoni akitowa shukrani na kumtaka Mbunge wa Jimbo hilo kukabidhiwa gari ya wagonjwa kwa ajili ya kuihudumia kutowa huduma kwa Wananchi wanaofika kituoni hapo kupata huduma gari hiyi hutumika kwa Wananchi kesi zao zinapokuwa zimeshindikana hapo na kuhamishiwa katika Hospitali ya Rafuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar. 
  Sheha wa Shehia ya Pangawe Jimbo la Fuoni akitowa shukrani kwa Mhe Mbunge Abass Mwinyi kwa msaada wake katika Kituo chao na kumtaka Mbunge huyo kufutalia ajira za Vijana wanaojitolea katika Kituo hicho sasa karibu miaka miwili hufanya kazi ya kuwahudumia wagonjwa wanaofika kituo hapo bila ya kuajiriwa amemuomba mbunge huyo kufuatilia swala hilo.
  Wauguzi wa Kituo cha Afya Fuoni na Wananchi wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Fuoni Mhe Abass Mwinyi wakati akizungumza na Wafanyakazi hao katika ziara yake kutembelea Kituo hicho na kukabidhi madawa kwa ajili ya Wananchi wanaofika kupata huduma kituoni hapo.
  Mbunge wa Jimbo la Fuoni Mhe Abass Mwinyi akiitikia dua baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya kukabidhi vifaa katika kituo cha afya fuoni Zanzibar.
  Wananchi na Waguzi wa kituo hicho wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya kukabidhi vifaa.
  Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Mwinyi akiwa na Wauguzi wa kituo hicho wakibadilisha mawazo baada ya hfla hiyo akiwa katika eneo la kituo hicho fuoni Zanzibar.

  Imetayarishwa na othmanmapara.Blogspot 

  0 0

  Afisa Uhusiano wa Airtel, Dangio Kaniki (kushoto) na Meneja uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (katikati) wakipima uzito wa kuku wa kienyeji wanaofugwa kisasa na kijana Mohamed Kigumi (kulia), anayeishi Kiluvyia jijini Dar Es Salaam baada baada ya kutembelewa nyumbani kwao na kuona maendeleo aliyoyapata baada ya kuwezeshwa na Airtel kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’ miezi sita iliyopita.
  Afisa Uhusiano wa Airtel, Dangio Kaniki (kulia) na Meneja uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (katikati) wakitazama maandalizi ya utunzaji wa kuku wa kienyeji wanaofugwa kisasa na kijana Mohamed Kigumi (kulia), anayeishi Kiluvyia jijini Dar Es Salaam baada baada ya kutembelewa nyumbani kwao na kuona maendeleo aliyoyapata baada ya kuwezeshwa na Airtel kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’ miezi sita iliyopita.
  Kijana Mohamed Kigumi anayeishi Kiluvyia jijini Dar Es Salaam akiwaelekeza meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando (katikati) na afisa Uhusiano wa Airtel, jinsi anavyoendesha ufugaji wake wa kuku baada ya kumtembelea nyumbani kwao na kuona maendeleo aliyoyapata baada ya kuwezeshwa na Airtel kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’ miezi sita iliyopita.

  VIJANA wengi wana ndoto za kujiletea maendeleo lakini wanashindwa kutimiza ndoto zao kutokana na kukosa elimu sahihi na kutokuwa na mitaji ambayo ingewawezesha kujiunga kwenye miradi ya ujasiriamali.

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa Airtel FURSA imeiona changamoto hiyo na kuamua kuwafikia vijana mbali mbali hapa nchini akiwemo kijana Mohamed Kigumi ambaye mpaka sasa ameonesha jitihada za kujikwamua na umaskini kwa kuwawezesha kupata mitaji ama vifaa vitakavyotimiza ndoto zao.

  Akiongea katika kijiji cha kiluvya, Muhamed Kigumi ambaye anajishuhulisha na ufugaji wa kuku wa kienyeji, amesema licha ya kuanza kazi hiyo kwa muda mrefu lakini sasa ameanza kuona mafanikio makubwa katika kazi yake kutokana na kujengewa mabanda ya kisasa ya kufugia kuku wake na mfuko wa Airtel FURSA tofauti na hapo awali ambapo alikuwa akifugia kukuwake kwenye mazingira magumu.

  Amesema mabanda ya kisasa aliyojengewa na mfuko wa Airtel FURSA pamoja na kupatiwa msaada wa kuku, maisha yake yamebadilika kwani sasa ameamua kujiajiri katika kazi hiyo na kumuwezesha kusaidia familia na kuuomba mfuko huo kendelea kuwasaidia vijana wengine hapa nchini.

  Akiongea katika mabanda ya kuku ya kijana huyo alipomtembelea hapo jana, meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando amesema kuwa mpango wao wa Airtel FURSA umefurahishwa na jitihada za kijana huyo ambapo wamemtembelea bila kumpa taarifa lakini wamebaini kuwa msaada waliompatia kijana Mohamed umeweza kuyabadilisha maisha yake kutokana na kuwa makini na kazi yake.


  Mmbando aliongeza kwa kusema, mpango wa kuwasaidia vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 uitwao Airtel FURSA umeanzishwa na mtandao wa simu za mikononi wa Airtel ili kuwasaidia vijana wa Tanzania wenye ndoto zao ili kuweza kuzitimiza ndoto zao kwa kuwawezesha kwa kuwapatia elimu ya biashara na nyenzo za kufanyia kazi.

  0 0

  ki7Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Dodoma Bi.Susano Chekani akiwa ameongoza na viongozi mbalimbali kutoka Manispaa ya Kinondoni katika ziara ya kuangalia hali ya usafi ya soko la magomeni kandokando ni sehemu ya kukusanyia taka za soko hilo na baadaye huchukuliwa na gari maalum la kubebea taka kwa ajili ya kupelekwa dampo kuu.
  ki8Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Dodoma Bi.Susano Chekani akiwa ameongoza na viongozi mbalimbali kutoka Manispaa ya Kinondoni katika ziara ya kuangalia hali ya usafi ya soko la magomeni kandokando ni sehemu ya kukusanyia taka za soko hilo na baadaye huchukuliwa na gari maalum la kubebea taka kwa ajili ya kupelekwa dampo kuu.
  ki9Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Dodoma Bi.Susano Chekani(Kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Soko la Tandale Mohamed Mwikya(Kushoto) wakati wa ziara ya kukagua hali ya usafi wa soko hilo
  ki10 
  Gari la Kuzoa taka kutoka katika Manispaa ya Kinondoni likiwa limebeba taka kutoka Soko la Tandale tayari kwenda kuzihifadhi katika dampo kuu, Manispaa hiyo imekuwa ikihakikisha hali ya usafi katika masoko yake kwa kupeleka magari ya kuzoa taka kila siku ili kuepukana na magonjwa ambukizi ikiwemo kipindupindu.
  ki12 
   Sehemu ya Soko lilipo kwenye kituo cha Daladala cha Simu 2000 eneo la Sinza kikiwa katika hali nzuri ya usafi huku uongozi wa eneo hilo wakiendelea kuisimamia hali hiyo kama ambavyo ilivyoagizwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kuwa siku ya sherehe ya Uhuru ambayo huadhimishwa kila Desemba 9, mwezi wa 12 kuwa ni siku ya usafi wa mazingira ili kuepukana na magonjwa amukizi kikiwemo kipindupindu.

  ki13 
  Sehemu ya Daraja la Tegeta Manispaa ya Kinondoni ikiwa imegeuzwa Dampo na wakazi wa eneo hilo kwa ambapo Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Dodoma Bi.Susano Chekani aliagiza uchafu huo kutolewa haraka kwa kuwa inahatarisha hali ya afya kwa wakazi wa maeneo hayo . 
  ki1Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Injinia, Musa Natty akieleza jambo wakati wa mkutano na wadau wa usafi wa mazingira kuhusu mkakati wa kufanya usafi katika Manispaa hiyo kufuatia agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambapo siku ya sikuu ya Uhuru, inayoadhimishwa kila Desemba 9 kuwa siku ya kufanya usafi ,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Dodoma Bi.Susano Chekani .
  ki2Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Dodoma Bi.Susano Chekani akifafanua jambo kwa wajumbe wa mkutano wa mkakati wa usafi (hawapo katika picha) namna ya kushirikiana katika kuhakikisha mazingira ya jiji la Dar es Salaam yanakuwa safi na salama ili kuepukana na magonjwa ambukizi ikiwemo kipindupindu katika kutekeleza agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kuadhimisha siku ya sikuu ya Uhuru, Desemba 9 kuwa siku ya kufanya usafi , kulia kwake ni Katibu Tawala Afya Daktari.Grace Magembe.
  ki3 
  Wajumbe wa mkutano wa usafi ambao pia ni wadau kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo Taasisi za kifedha, Mazingira,Jeshi la Magereza,Wanamazingira,Vikundi vya Usafi na Wafanyakazi wa Manispaa ya Kinondoni wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kuadhimisha siku ya sikuu ya Uhuru, Desemba 9 mwaka huu kuwa siku ya kufanya usafi .
  ki4 
  Wajumbe wa mkutano wa usafi ambao pia ni wadau kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo Taasisi za kifedha, Mazingira,Jeshi la Magereza,Wanamazingira,Vikundi vya Usafi na Wafanyakazi wa Manispaa ya Kinondoni wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kuadhimisha siku ya sikuu ya Uhuru, Desemba 9 mwaka huu kuwa siku ya kufanya usafi .
  ki5Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Dodoma Bi.Susano Chekani akikagua Soko la Magomeni lilipo Manispaa ya Kinondoni wakati ziara ya kuangalia hali ya usafi ikiwa ni kutekeleza agizo lililotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli kuadhimisha siku ya sikuu ya Uhuru, Desemba 9 kuwa siku ya kufanya usafi,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Injinia Mussa Natty.
  ki6Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Dodoma Bi.Susano Chekani akiongea na wachuuzi wa Soko la Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni katika ziara ya kuangalia hali ya usafi katika soko hilo.
   (Picha na Lorietha Laurence-Maelezo)

  0 0

  IMG_5494
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendelea na ukaguzi wa Bwawa hilo.
  IMG_5496Muonekano wa mradi wa ujenzi wa Bwawa la Charco la Nguvumoja.
  IMG_5520 
  Wananchi wakiendelea kuchimba bwawa hilo.
  IMG_5447 
  Ofisa Kilimo na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Samaluku Joseas (kushoto) akisoma taarifa ya maendeleo ya miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika mkoa wa Tabora. Pichani wa pili kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (wa tatu kushoto) wakipitia taarifa hiyo kwa pamoja kabla ya kuelekea kukagua miradi hiyo.


  IMG_5482Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa tatu kushoto) aliyeambatana na Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (wa pili kushoto) walipowasili kukagua mradi wa ujenzi wa Bwawa la Charco la Nguvumoja kwa mtindo wa utoaji wa chakula kutoka Shirika la Chakula Duniani (WFP) kwa kazi inayofanywa na mradi wa misitu ya Miyombo. Kushoto ni Ofisa Tawala msaidizi anayeshughulikia Uchumi na Tija wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Dkt. Phillips Mtiba pamoja na Ofisa Kilimo na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Samaluku Joseas (wa pili kulia).
  IMG_5486
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendelea kupata maelezo ya mradi huo.

  IMG_5532Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nguvumoja watakaonufaika na mradi wa bwawa hilo.
  IMG_5538#HapaKaziTu; ndio maneno aliyokuwa akiyasema Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakati akichimbia sehemu ya bwawa hilo alipofanya ziara ya kukagua mradi huo wa Bwawa la Charco la Nguvumoja.
  IMG_5540Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akichimba udongo na sururu huku Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan akijaza udongo unaochimbwa kwenye ndoo.
  IMG_5553#HapaKaziTu; Wanakijiji pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakishangilia kwa pamoja huku wakiunga kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya #HapaKaziTu sambamba na mabango 17 ya malengo ya maendeleo endelevu (Sustainable Development Goals-SDGs) walioyowafikia wanakijiji wa Nguvumoja. Kwa matukio zaidi bofya link hii


  Na Modewji blog team, Tabora
  MRATIBU Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Mipango ya Maendeleo la Umoja huo Bw.Alvaro Rodriguez, amesema kwamba umoja huo utaendelea kufadhili miradi ya maendeleo katika mkoa wa Tabora yenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi.
  Hayo alisema jana baada ya kuzuru miradi inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Tabora.

  Miradi hiyo ni ya ujenzi wa bwawa la nguvumoja kwamtindo wa utoaji wa chakula kwa kazi inayofanywa na mradi wa misitu ya miyombo.
  Katika ziara hiyo ambayo alikuwa na Ofisa kutoka Kitengo cha ushirikiano wa kimataifa wizara ya mambo ya nchi za nje, Bi. Maulidah Hassan Mratibu huyo aliridhishwa na mafanikio ya miradi hiyo ambayo imelenga kupiga vita umaskini na kutunza mazingira.

  Ziara ya Mratibu huyo mkoani Tabora ni moja ya ziara yake ndefu ya kutembelea miradi inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika mikoa ya Singida, Tabora na Kigoma.

  Alipotoka Singida jana asubuhi alifika katika moja ya Wilaya kame nchini, Wilaya ya Igunga na kuona mradi unaofadhiliwa na Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) wa ukarabati wa bwawa la Charco.

  Bwawa hilo ambalo litahudumia watu takribani 6,100 kutoka vijiji vya Nguvumoja, Ndembezi na Iborogelo lilijengwa awali na miradi ya TASAF lakini wakati wa mvua za Elnino tuta lake lilivurugika vibaya.

  Akizungumzia bwawa hilokaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Igunga ambaye pia ni Ofisa Kilimo na Ushirika wa Wilaya ya Igunga, Samaluku Joseas, akizungumza alisema kwenye bwawa hilo kwamba Umoja wa Mataifa kupitia WFP wanawezesha ukarabati wa bwawa hilo kwa kutoa chakula kwa wachimbaji.

  Aidha imeelezwa kuwa tuta hilo likikamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia kaya 1,200 na Ng’ombe elfu moja na kuweza kuhifadhi maji kwa mwaka mzima.Imeelezwa kuwa wajenzi wanapewa debe moja la Mahindi kwa kina cha mita moja na urefu wa mita nne na upana wa mita tatu na nusu lita ya mafuta ya kula na Njegere kilo tatu.Kumalizika kwa bwawa hilo kutasaidia kupunguza umbali wa wananchi katika kutafuta maji.

  Awali wananchi walilazimika kusafiri kilomita 30 kupata maji katika bwawa la Manzugi kuchota maji na kunywesha mifugo.Aidha imeelezwa kuwa baadae wanyama watatengewa eneo la kunywa maji.
  Aidha alitembelea kikundi cha ufugaji nyuki, utunzaji wa mazingira pamoja na usindikaji wa matunda pori cha Membo , wilayani Uyui.

  Kikundi hicho kilichopo wilayani Uyui kimeanzishwa Mei 8,2007 na Katibu wa kikundi Nasibu Baraka alisema kikundi hicho chenye wanachama 30 kimefanyakazi kubwa ya kupiga vita umaskini.Alisema ili kukabiliana na adui njaa na umaskini kikundi hicho kwa ufadhili wa UNDP kimewezesha kujiajiri wenyewe, Kusindika matunda ya asili kwa ajili ya jamu na divai,kilimo cha bustani, kilimo cha chakula na biashara, ujenzi wa majikobanifu,usagaji wa unga na kupika keki za Muhogo mbichi kwa Karanga na Asali.

  Akisoma risala kwa Mratibu wa UN Tanzania alisema kwamba wamekuwa na mafanikio makubwa kutokana na ruzuku mbalimbali za UNDP ikiwamo mafunzo.

  Aidha amesema kwamba kwa sasa wanatumia sola badala ya mafuta ya taa huku mradi wa Miyombo ukiendelea kuleta neema.Aidha ametaka umoja huo kuwasaidia kuwa na mshine za kisasa cha kusindika matunda na chakula.

  Viongozi hao walifika katika mradi huo kuangalia mafanikio ya mradi huo unaotekelezwa chini ya mpango wa miaka mitano wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa,(UNDAP).Aidha mradi huo umelenga kupunguza umaskini kutunza mazingira kwa njia ya uragibishi na na kufunza wananchi kuhusu suala la ufugaji nyuki na utunzaji wa mazingira.

  Naye Ofisa utawala msaidizi wa mkoa anayeshughulikia Uchumi na Tija Dk. Phillips Mtiba akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa Tabora, Ludovick Mwananzila ambaye hakuwepo kutokana na majukumu mengine kwenye mikutano na wananchi kuhusu miradi ya TASAF, alisema baada ya kumaliza kukagua miradi kwamba wameridhika na miradi inayofadhiliwa na UN katika mkoa huo.

  Alisema pamoja na kwamba walitembelea miradi michache lakini ni dhahiri mkoa wa Tabora umefurahishwa na misaada iliyotolewa ambayo inatia moyo na kusaidia harakati za serikali za kukomboa wananchi wake kutoka katika lindi la umaskini na ukosefu wa huduma muhimu kama za maji na hifadhi ya mazingira.

  Pamoja na kushukuru kwa misaada hiyo kwa wanatabora na maendeleo yao, alitaka UN isiwachoke kusaidia vipaumbele vya mkoa huo ambavyo ni kujitokeza kwa chakula na hifadhi ya misitu.“ Nashukuru sana kwa msaada tunaoendelea kupata kutoka UN kwa ajili ya maendeleo ya wana Tabora na Tabora kwa ujumla na niseme tu kwamba kama wana Tabora kuna vitu ambavyo tunaweza kufanya na mengine hatuwezi kuyafanya na hapo ndipo sasa tunapoweza kuona umuhimu wa nafasi ya wafadhili na wadau mbalimbali katika shughuli za maendeleo.” Alisema Dk. Phillips.

  Alisema ingawa walikuwa na muda mfupi na kutembelea miradi michache , alitamani waje kurudi kuona miradi mingi zaidi ili watambue kwamba miradi hiyo inabadilisha wana Tabora na hawachezei fedha za ufadhili.


  Alisema suala la uhakika wa chakula kwa wananchi ni muhimu kwao kutokana na ukweli kuwa wananchi wakiwa na chakula hata fedha zao zitakaa mfukoni na kufanya kazi nyingine za maendeleo. Alisema kutokana na hali hiyo wataendelea kuomba kusaidiwa katika eneo hilo.

  Aidha alitaka mkoa wa Tabora kuendelea kusaidiwa kutunza misitu ya Miyombo kwa ajili ya manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho kwa kuwa misitu ni kivuta mvua na maji ndio pembejeo namba moja katika uzalishaji wa chakula.

  Alishukuru UNDP kwa kusaidia kuhifadhi misitu hiyo ili kuwapo na uvunaji endelevu kwa kusaidia jamii kuitunza na kuismamia rasilimali hiyo na kuitumia katika fursa za kiuchumi kama ufugaji nyuki.
  Leo Mratibu huyo ataendelea na ziara yake katika mkoa wa Kigoma.

  IMG_5583

older | 1 | .... | 702 | 703 | (Page 704) | 705 | 706 | .... | 1904 | newer