Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel Catalog



Channel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 697 | 698 | (Page 699) | 700 | 701 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila akifunga Mafunzo ya siku mbili ya Waandishi wa Habari za Mahakama yaliyofanyika jijini Dar es salaam.
   Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila akitoa ufafanuzi kuhusu Kichwa cha Habari ya Mahakamani kilichoandikwa bila kuzingatia Weledi na moja ya Gazeti la Kila siku  wakati wa mafunzo ya  siku mbili ya Waandishi wa Habari za Mahakama yaliyofanyika jijini Dar es salaam. Picha/Aron Msigwa –MAELEZO.
   
   
  Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
  27/11/2015.Dar es salaam.
   
  Mahakama ya Tanzania imesema kuwa itendelea kufanya kazi na vyombo vya Habari nchini katika kuuhabarisha umma kuhusu utekelezaji wa jukumu la Kikatiba ililonalo la kutafsiri sheria mbalimbali na kuzitolea maamuzi ili kuwawezesha wananchi kujua na kupata Haki zao kwa wakati.
   
  Akifunga Mafunzo ya siku 2 ya waandishi wa Habari za Mahakama jana jijini Dar es salaam Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila aliwataka waandishi hao kutimiza wajibu wao wa kuueleza umma taarifa sahihi za mashauri mbalimbali yanayotokea mahakamani kwa kuzingatia sheria.
   
  Alisema vyombo vya habari na mahakama vinahitajiana, vinafanya kazi pamoja kwa manufaa ya umma huku akieleza kuwa mikutano ya mara kwa mara kati ya wanahabari na mahakama kunaongeza kuaminiana na kujenga mahusiano mazuri.
   
  Alifafanua kuwa kazi ya Mahakama kikatiba ni kutafsiri sheria mbalimbali na kuzitolea maamuzi kwa mujibu wa sheria kulingana na mashauri yananayowasilishwa Mahakamani na kuongeza kuwa hakuna Jaji wa Mahakama ya Tanzania anayeamua kesi bila nje ya utaratibu wa sheria zilizopo.
   
  Alisema wao kama majaji hutumia sheria zilizopo katika kutoa maamuzi hata kama haziwapendezi wahusika na kuongeza kuwa jambo wanalolifanya ni kutoa maoni na mapendekezo kwa mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi.
   
  " Sisi kama Majaji hutumia sheria zilizopo kutoa maamuzi,hatutungi sheria jukumu letu kikatiba ni kutafsiri sheria mbalimbali na kuzitolea maamuzi pia tunatumia fursa ya maamuzi tunayoyatoa  kuelimisha jamii kuhusu sheria iliyotumika kutoa haki katika kesi husika" Alisema.
   
  Aliwataka waandishi wa Habari za Mahakama kujipa muda wa kutosha pindi wanapofika Mahakamani kufuatilia mashauri yanayoendeshwa ili waweze kuwa na taarifa za kutosha pindi shauri linapofunguliwa na kutolewa hukumu ili kuwawezesha wananchi kupata taarifa za kutosha za mwenendo wa Mashauri.
   
  Aliongeza kuwa Mahakama ya Tanzania imedhamiria  kufanya kazi na waandishi wa habari nchini kwa kuzingatia kwamba wakati majaji wanapotoa hukumu mahakamani kunakuwa na idadi ndogo ya wananchi wanaoshuhudia kuliko ile iliyo nje ila vyombo vya habari kutokana na umuhimu wake huwapasha habari mamilioni ya watanzania  walio nje ya Mahakama.
   
  Alisema Mahakama itaendelea kujenga mahusiano mazuri na Vyombo vya Habari hususan waandishi wa Habari za Mahakama kwa kutenga maeneo ndani ya Mahakama yatakayotumiwa na waandishi hao kuwawezesha kufanya kazi zao bila vikwazo kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo.
   
  Pia alieleza kuwa Mahakama, itaendelea kutoa taarifa za ufafanuzi wa hukumu mbalimbali zitakazotolewa kwa vyombo vya habari pia Nakala za taarifa za Hukumu kwa waandishi wa habari ili kuwawezesha wananchi kujua ukweli wa yale yanayojili mahakamani kuondoa upotoshaji unaotokea.
   
  Aidha alisema kuwa Mahakama itaendelea kushirikiana  na Baraza la Habari Tanzania (MCT) katika kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari za Mahakama ili waweze kuandika habari zenye ukweli na uhakika.
   
  Mhe. Shaban Lila alisema kuwa Mahakama iko tayari kupokea maoni yanayohusu utendaji kazi wake ili iweze kuyafanyia kazi kwa manufaa ya vyombo vya habari na wananchi. 
   
  Awali akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo kabla ya kumkaribisha Jaji Kiongozi kufunga mafunzo hayo, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Mahakama ya Tanzania Bi. Wanyenda Kuta aliwaambia washiriki wa mafunzo hayo kuwa Mahakama inaendelea kutekeleza nguzo 3 ambazo ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na Upatikanaji wa Haki kwa Wakati, Kuongeza Imani wanachi kwa Mahakama pia kuboresha miundombinu ya Mahakama nchini.
   
  Alisema kuwa wandishi wa Habari za mahakama waliohudhuria mafunzo hayo yaliyoandalia na Mahakama ya Tanzania na Baraza la Habari Tanzania (MCT) wamejifunza masuala mbalimbali ambayo yamewajengea ufahamu waandishi wa Habari za Mahakama kuhusu lugha za kimahakama, uandishi bora wa habari za Mahakama, Uhuru wa Mahakama pamoja na kujua Haki za Washitakiwa na Watuhumiwa wanapofikishwa mahakamani.
   
  Kwa upande wake Meneja wa Maadili wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Allan Lawa  akizungumza na wanahabari hao aliwataka waandike habari za Mahakama kwa usahihi na umakini mkubwa kufuatia Mafunzo
  waliyoyapata.
   
  Bw. Lawa aliishukuru Mahakama mafunzo hayo na hatua ya uongozi wa mahakama  kuyakubali mapendekezo yaliyotolewa na Waandishi wa Habari za Mahakama ikiwemo kutenga eneo ndani ya mahakama litakalotumiwa na waandishi wa Habari za Mahakama, utoaji wa Nakala za kesi na ufafanuzi wake mara hukumu zinapotolewa, Mahakama kukubali kushawishi uanzishaji wa madawati ya Habari za Mahakama kwenye vyombo vya Habari pamoja na mahakama kukubali kuendesha mafunzo ya mara kwa mara kwa waandishi wa Habari za Mahakama na wahariri wao.

  0 0

    Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, Bw.Injinia Thomas Haule, (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa uwanja huo leo Ijumaa Novemba 27, 2015. 
   
  Utawala wa uwanja huo ulio chini ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA, umejipanga upya katika kuimarisha ulinzi ambapo kuanzia sasa, vifurushi na mizigo yote kutoka posta itakaguliwa kwa mara ya pili kabla ya kupakiwa ndani ya ndege, ikiwa ni hatua ya kudhibiti vifurushi na mizigo haramu kupenya kwenye ndege. Kushoto ni Kaimu Meneja Usalama wa Uwanja huo, Bw.David Ngaragi, (kushoto) na Afisa Usalama Mwandamizi wa Uwanja huo, Dorice Uhagile. (Picha na K-Vis Media/Khalfan Said).
   
  Na K-Vis Media
  UONGOZI wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere unaomilikiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA, umetangaza leo Ijumaa Novemba 27, 2015 kuwa kuanzia sasa vifurushi na mizigo mingine yote ya Shirika la Posta Tanzania, itakaguliwa kwa mara ya pili kama mizigo mingine yoyote kabla ya kupakiwa ndani ya ndege.
  Uamuzi huo umetangazwa na Mkurugenzi wa Uwanja huo, (JNIA), Injinia Thomas Haule, wakati akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa VIP ulioko uwanjani hapo.Alisema, uamuzi huo ni baada ya Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege, TAA, kutoa maonyo kadhaa, kwa Shirika la Posta, kuimarisha ukaguzi wa vifurushi na mizigo itokayo Posta kwa vile imekuwa ikikamatwa na mizigo ambayo ni tofauti na iliyokusudiwa.
  Alitaja mizigo hiyo kuwa ni pamoja nabangi, na kwamba, Uholanzi wamekuwa wakilalamika mara kadhaa kuwa wamekuwa wakikamata vifurushi vya Posta vikiwa na mizigo iliyoharamishwa.
  "Sisi Kama Mamlaka, wajibu wetu mkubwa ni kuzuia kitu au vitu vyovyote vinavyoweza kuhatarisha usalama wa abiria wawapo ndani ya ndege au ndege yenyewe haviingii ndani ya ndege." Alianza kwa kusema Injinia Haule na kuongeza kuwa, vitu vingine kama madawa ya kulevya, pembe za ndovu, na vingine vingi, , vinashughulikiwa na mamlaka nyingine ambazo zina maafisa wake hapa JNIA wakishirikiana na maafisa wetu.
  Hata hivyo makosa yafanywayo na idara Fulani ya serikali yenye afisa wake hapa JNIA, ni wazi kwamba watakaonyooshewankidole ni TAA, alisema na kubainisha kuwa Mamlaka haitavumilia tena uzembe utakaofanywa na taasisi nyingine ya serikali katika kuhakikisha zinatekeleza wajibu wake ipasavyo.
   Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, Injinia Thomas Haule, akizungumza kwenye mkutano huo
   Meneja wa Usalama wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Bw.David Ngaragi, akifafanua jambo kwenye mkutano huo na waandishi wa habari
   Waandishiw a habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, JNIA, Injinia Thomas Haule

  0 0



  0 0

  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani,DCP Mohamed Mpinga, akisalimiana na Mabalozi wa Usalama Barabarani, muda mfupi kabla ya kuzindua Operesheni ijulikanayo kwa jina la “Paza Sauti” yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani. Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo. Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga, akitoa maelekezo ndani ya moja ya basi linalofanya safari zake mkoani wakati wa kuzindua wa Operesheni Paza Sauti yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani. Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo. Wadau wanaotumia usafiri wa barabara, wakiwemo madereva na abiria wakimsikiliza Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga(hayupo pichani) alipozindua Operesheni Paza Sauti, yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani,Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo. Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo na Matukio wa Mabalozi wa Usalama Barabarani,Jackson Kalikumtima(kulia), akitoa elimu kuhusiana na Operesheni ya Paza Sauti kwa mmoja wa wadau wanaotumia usafiri wa barabara, Operesheni hii ilizinduliwa Stendi ya Mabasi yaendayo mikoani ya Ubungo, jijini Dar es Salaam leo.(Picha zote na Abubakari Akida,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

  0 0

  w2 
  Kamishna wa Bajeti kutoka Wizara Fedha Bw. John Cheyo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu kubadilishwa kwa matumizi ya Fedha za Serikali ambazo zitaelekezwa kwenye shughuli zitakazowagusa wananchi ikiwemo uboreshaji wa sekta ya elimu ambapo awali fedha hizo zilipangwa kutumika katika sherehe za Uhuru na shughuli zisizo za lazima. Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Idara ya Habari. (MAELEZO) Bw. Vicent Tiganya.
  w3 
  Kamishna msaidizi wa Bajeti Bw.Immanuel Tutuba akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu namna Serikali inavyokusanya mapato yake na kuyaingiza katika mfuko mkuu wa Serikali ili yaweze kutumika katika utekelezaji wa bajeti ya Serikali. Kulia kwake ni Kamishna wa Bajeti Bw. John Cheyo na kushoto ni msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma.
  w5 
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya Fedha na vyombo vya habari ambapo Kamishna wa Bajeti kutoka Wizara hiyo Bw. John Cheyo alitoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Serikali kulingana na mipango iliyowekwa katika kuwahudumia wananchi.

  w1 
  Kamishna wa Bajeti kutoka Wizara Fedha Bw. John Cheyo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu taarifa za upotoshaji zilizoripotiwa na vyombo vya habari hapa nchini kuwa hazina yakauka, taarifa hizo ni za upotoshaji kwani mfumo wa Serikali wa bajeti unaiwezesha Serikali kupanga vipaumbele vya matumizi kulingana na bajeti ilivyopangwa ambapo fedha zinazokusanywa kupitia mfuko mkuu wa Serikali ndizo hutumika. Kushoto ni Kamishna msaidizi wa Bajeti Bw. Immanuel Tutuba na kulia ni Mkurugenzi msaidizi Idara ya habari Maelezo Bw. Vicent Tiganya.
  w6 
  Kamishna msaidizi wa Bajeti Bw.Immanuel Tutuba akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam .Kulia nia Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma.(Picha na frank Mvungi- Maelezo)
  ……………………………………………………………………………………………………
  Na Jovina Bujulu-Maelezo
  Dar es Salaam
  Serikali imekanusha taarifa zinazosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa amekomba fedha hazina na kuiacha Serikali bila fungu lolote.
   
  Hayo yamesemwa jijini dare es salaam na Kamishina wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha Bwa. John Cheyo huku akiwataka wananchi kupuuza habari hiyo kwani hazina ukweli wowote.
   
  “Hazina inazo pesa za kutosha  na tunajivunia kufanya uchaguzi wa mwaka huu,  kununua mashine za BVR  kwa kutumia pesa za watanzania bila kutegemea msaada wowote kutoka nje ya nchi  na kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka huu” alisema Bwa. Cheyo.
   
  Pia aliongeza kuwa serikali imeendelea kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa bomba la gesi ambalo limekamilika hivi karibuni, vinu vya kuchakata gesi na ujenzi wa barabara nchini.
   
  Aliendelea kusema kwamba mfumo wa serikali wa bajeti unaiwezesha serikali kupanga vipaumbele vya matumizi kulingana na bajeti ilivyopangwa ambapo fedha zinazokusanywa kupitia mfuko mkuu wa serikali ndizo hutumika.Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwa kipindi cha 2015-2016 ni shilingi Trilioni 22.5 na bajeti hiyo inatengenezewa mpango wa makusanyo na matumizi kwa kulipia mishahara ya wafanyakazi na miradi mbalimbali iliyoidhinishwa.
   
  Pia katika matumizi mengine bajeti hiyo inalipia chakula cha wanafunzi, mikopo ya wanafunzi elimu ya juu, ununuzi wa dawa na vifaa tiba na chakula cha hifadhi ya taifa.

  0 0


  0 0
 • 11/27/15--08:28: Article 3


 • 0 0

  Kufuatia maagizo ya Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa hivi karibuni ya kusitisha safari za nje kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imeanza kutekeleza maagizo hayo kwa kutoa maelekezo mahsusi kwa Balozi zake nje.

  Wizara imezielekeza Balozi zote zilizopo maeneo mbalimbali duniani kujipanga ili kushiriki kikamilifu katika kuiwakilisha Serikali kwenye mikutano yote ya kimataifa na kikanda inayofanyika katika maeneo yao ya uwakilishi. Tanzania inazo Balozi 35; Balozi Ndogo tatu; Vituo viwili vya Biashara; na Konseli za Heshima 17 katika nchi mbalimbali. Hizi zote zitahusika katika kuendeleza utekelezaji wa Diplomasia yetu ya Uchumi na uwakilishi wa maslahi ya nchi yetu.

  Aidha, hadi sasa Mikutano ambayo tayari imefanyika na Balozi zetu kuwakilisha ni pamoja na Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) unaoendelea nchini Malta na Mkutano wa Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Habari wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika nchini Lesotho.

  Aidha, Wizara inatoa wito kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali kuwasilisha mapema taarifa za mikutano inayohusu sekta zao ili kutoa fursa kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuzifanyia kazi kwa wakati ili kuhakikisha ushiriki wa Tanzania unakuwa wenye tija kwa taifa.

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inaungana na wadau wengine kumpongeza Mhe. Rais Magufuli kwa hatua anazozichukua za kuleta ufanisi mkubwa wa kazi na kubana matumizi ili kuiwezesha Serikali kuwahudumia wananchi kikamilifu.

  Imetolewa na:
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
  27 Novemba, 2015

  0 0

  WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi maafisa watano na watumishi watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutokana na upotevu wa makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 80/-.

  Akizungumza na viongozi wa Mamlaka ya Bandari pamoja na viongozi wa TRA katika ziara ya kushtukiza leo mchana (Ijumaa, Novemba 27, 2015), Waziri Mkuu amewataka Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Rished Bade na Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Lusekelo Mwaseba wahahakikishe wanashirikiana na polisi kufuatilia upotevu huo na kwamba fedha hizo zinapatikana na zinarudi Serikalini.

  Akitangaza uamuzi huo baada ya kufanya kikao na baadhi ya viongozi wa Serikali bandarini hapo, Waziri Mkuu aliwataja maafisa waliosimamishwa kazi kuwa ni Kamishna wa Forodha, Bw. Tiagi Masamaki na Mkuu wa Kituo cha Huduma kwa Wateja, Bw. Habibu Mponezya.

  “Hawa wanasimamishwa kazi. IGP ninaagiza hawa watu wakamatwe na kuisaidia polisi. Hati zao za kusafiria zikamatwe na mali zao zikaguliwe kama zinaendana na utumishi wa umma,” alisema Waziri Mkuu.

  Maafisa wengine waliosimamishwa kazi ni Mkuu wa kitengo cha TEHAMA, Bw. Haruni Mpande, Bw. Hamisi Ali Omari (hakutaja ni wa idara gani), na Mkuu wa Kitengo cha Bandari Kavu (ICD In-Charge), Bw. Eliachi Mrema. “Hawa wanasimamishwa kazi hadi uchunguzi utakapokamilika na pia wawe mikononi mwa polisi,” alisema.

  Pia aliagiza watumishi watatu wa mamlaka hiyo wahamishwe kutoka Dar es Salaam na kupelekwa mikoani. Watumishi hao ni Bw. Anangisye Mtafya, Bw. Nsajigwa Mwandengele na Bw. Robert Nyoni.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemwagiza Katibu Mkuu wa Hazina, Dk. Servacius Likwelile ambaye alikuwepo kwenye kikao hicho, kuhakikisha kuwa anapeleka wataalamu kutoka Wakala wa Serikali Mtandao (e-Govt) haraka iwezekanavyo ili wakakague mifumo ya taarifa na kubaini jinsi ambavyo wizi huo unafanyika.

  “Ninataka uchunguzi uanze kufanyika mara moja, tafuteni njia ambazo zinatumika kama mianya ya wizi kutokea hapa bandarini hadi kwenye ICDs. Nataka hayo makontena yatafutwe hadi yajulikane yako wapi, na fedha hiyo ihakikishwe inarudi serikalini,” alisema.

  Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Bw. Ernest Mangu, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM, Suleiman Kova, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Bw. Awadh Massawe na viongozi mbalimbali kutoka TRA na TPA.

  Mapema akijibu maswali ya Waziri Mkuu, Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Bade alikiri kwamba kuna upotevu wa makontena ambao huwa unafanyika kati ya bandarini na ICDs na hasa ICD ya Ubungo. Akitoa ufafanuzi, alisema kwamba walifanya ukaguzi kwenye ICD moja na kukuta makontena 54 yamepotea kwa njia za wizi. “Hata hivyo, tulipoendelea na ukaguzi, namba iliongezeka na kufikia 327. Tunaendelea kufuatilia kwa kushirikiana na TAKUKURU. Mmiliki wa ICD ametakiwa kulipa faini sh. bilioni 12.6/- na ameshalipa sh. bilioni 2.4/-,” alifafanua.

  Alipoulizwa na Waziri Mkuu kama ana majina ya watumishi wanaohusika na wizi huo, Bw. Bade akakiri kwamba anayo lakini siyo kwa wakati huo labda ayapate kutoka kwa wasaidizi wake. Ndipo Waziri Mkuu akamuonyesha orodha ya makontena 349 yenye taarifa zote hadi namba za magari yaliyobeba mizigo hiyo na Bw. Bade akakiri kwamba orodha hiyo ni ya kweli.

  “Kwa utaratibu huo hatuwezi kufika, labda baadhi ya watu waondolewe kazini”. Ndipo akaanza kutaja majina ya maafisa hao waliosimamishwa kazi.
  Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na uongozi wa TRA na TPA alipofanya ziara ya kustukiza Bandarini leo asubuhi.
   Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea na viongozi wa TRA na TPA
  Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akikabidhi orodha ya makontena yaliyopotea na ambayo TRA haina taarifa nazo
  Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akiagana na viongozi wa TRA na TPA.

  0 0

  Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania, Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli amemsimamisha kazi kuanzia leo tarehe 27 Nov. 2015, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndugu Rished Bade kufuatia ziara ya kushtukiza ya Waziri Mkuu, Mh. Majaliwa Kasimu Majaliwa mapema leo asubuhi Bandarini jijini Dar es salaam.

  Hatua hiyo imekuja baada kubaini kupitishwa kwa makontena zaidi ya 300 na kusababishia hasara Serikali ya zaidi ya shilingi bilioni 80.

  Rais Magufuli pia amemteua  Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango kukaimu nafasi hiyo mpaka hapo uchuguzi utakapo kamilika.

  Taarifa hiyo iliyosomwa na Katibu Mkuu Kingozi, Balozi Ombeni Sefue Ikulu jijini Dar es salaam, imewataka maofisa wote wa TRA kutosafiri nje ya nchi mpaka pale uchunguzi dhidi yao utakapo kamilika.

  0 0


  Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro,Amosi Makala akizunumza na wakuu wa wilaya ,wakurugenzi,Wakuu wa taasisi mbalimbali za umma katika kikao cha utendaji kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa.
  Wakuu wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika kikao hicho,kutoka kuslia ni Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka, Helman Kapufi (Mkuu wa wilaya ya Same) Novautus Makunga (Mkuu wa wilaya ya Moshi) na Lembris Kipuyo (Mkuu wa wilaya ya Rombo).
  Baadhi ya wakurugenzi wakiwa katika kikao hicho.


  Watendaji wengine wa serikali wakifuatilia hotuba ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro alipokutana nao . 

  NA Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya kaskazini.

  KATIKA kutekeleza kauli mbiu ya Rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,John Magufuli ya “Hapa Kazi tu” serikali mkoani Kilimanjaro imetangaza kusitisha likizo na ruhusa zote kwa watumishi wake katika kipindi cha siku kuu za Krismasi na mwaka mpya.

  Agizo hilo linakuja wakati tayari baadhi ya watumishi wa serikali kuanza taratibu za kuomba likizo na ruhusa kwa ajili ya kwenda kushiriki siku kuu za mwisho wa mwaka za Krismasi na mwaka mpya.

  .Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makala alitangaza uamuzi huo jana wakati wa kikao cha kazi alichoitisha na wakuu wa wilaya zote za mkoa, wakurugenzi, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na watendaji wengine wa serikali.

  “Mh Rais ametoka kwenye kampeni hajapumzika,Makamau wa rais ametoka kwenye kampeni hajapumzika ,Waziri mkuu pia vivyo hivyo sasa sisi ni nani twende kwenye mapumziko ya siku kuu ya Krismasi.”alihoji Makala.

  “Kwa maana hiyo ili haya tunayotaka ya elimu bure ,kukabiliana na Kipindupindu ,kwa madaraka niliyopewa kama mkuu wa mkoa nasitisha likizo zote,kwa Wakuu wa wilaya ,Wakurugenzi na wakuu wote wa idara ili mambo haya yaweze kutekelezwa,tumesema Hapa ni kazi tu”aliongeza Makala.

  Alisema utekelezaji wa agizo la rais la kufanya usafi siku ya sikuu ya Uhuru inayofanyika Desemba 9 kila mwaka ,mapambano ya ugonjwa hatari wa Kipindupindu ambao umeendelea kusambaa sehemu kubwa ya nchi hayawezi kusubiri hadi watusmishi wa serikali watoke likizo.





  Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro,Severine Kahitwa akizungumza katika kikao hicho.
  Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Kilimanjaro.
  Baadhi ya watendaji wa taasisi za umma,kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi,Joyce Msiru.
  Badhi ya watumishi katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto) akimkabidhi kikombe mmoja wa washindi katika mchezo wa kuogelea kwenye maadhimisho ya Siku ya Familia iliyofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana.Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto) akimkabidhi kikombe mmoja wa washindi katika mchezo wa kuogelea kwenye maadhimisho ya Siku ya Familia iliyofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana.Baadhi ya washindi wa mchezo wa kuogelea wakipata picha ya kumbukumbu na viongozi waandamizi wa NMB baada ya kukabidhiwa zawadi zao kwenye maadhimisho ya Siku ya Familia yaliyofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kulia) akizungumza na wafanyakazi wa NMB pamoja na familia zao kabla ya kuzinduwa rasmi maadhimisho ya Siku ya Familia (family day) kwa wafanyakazi wa benki hiyo yaliofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni Tusherehekee pamoja mafanikio ya Miaka 10 ya NMB.Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa NMB pamoja na familia zao kabla ya kuzinduwa rasmi maadhimisho ya Siku ya Familia (family day) kwa wafanyakazi wa benki hiyo yaliofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni Tusherehekee pamoja mafanikio ya Miaka 10 ya NMB.Baadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiingia katika maadhimisho ya Siku ya Familia (Family Day) iliofanyika jana Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park Jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB wakitambuliwa kabla ya kuingia katika maadhimisho ya Siku ya Familia iliyofanyika jana Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park Jijini Dar es Salaam.Baadhi ya viongozi wa Benki ya NMB, na wanafamilia zao wakipata maelekezo kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa maadhimisho ya Siku ya Familia (family day) kwa wafanyakazi wa benki hiyo yaliofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni Tusherehekee pamoja mafanikio ya Miaka 10 ya NMBBaadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB wakipewa utaratibu kabla ya kuingia kwenye maadhimisho ya Siku ya Familia yenye kauli mbiu ya tusherehekee Miaka 10 ya mafanikio ya benki ya NMB yaliofanyika jana Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park Jijini Dar es Salaam. 
  Baadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiwa katika michezo mbalimbali na familia zao kwenye maadhimisho ya Siku ya Familia (Family Day) na iliyofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana.Baadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiwa katika michezo mbalimbali na familia zao kwenye maadhimisho ya Siku ya Familia (Family Day) iliyofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana.Baadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB wakipata huduma mbalimbali ndani ya Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park katika maadhimisho ya Siku ya Familia iliyofanyika jana Jijini Dar es SalaamMalaika Bandi wakiwaburudisha wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB katika maadhimisho ya Siku ya Familia iliyofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana.Baadhi ya huduma za kibenki za Benki hiyo pia zilipatikana.Baadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB wakifuatilia burudani anuai katika maadhimisho ya Siku ya Familia iliyofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana.Baadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB wakipata huduma mbalimbali ndani ya Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park katika maadhimisho ya Siku ya Familia na kusherehekea Miaka 10 ya benki hiyo iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (katikati) akizunguka kubadilishana mawazo na baadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki hiyo kwenye maadhimisho ya Siku ya Familia na kusherehekea Miaka 10 ya benki hiyo iliyofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam janaBaadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiwasili eneo la Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park katika maadhimisho ya Siku ya Familia iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.Mmoja wa viongozi wa NMB (kulia) akizungumza na wanafamilia na wafanyakazi wa Benki hiyo kabla ya uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Familia iliyofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker.Baadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiwa katika michezo mbalimbali na familia zao kwenye maadhimisho ya Siku ya Familia (Family Day) iliyofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana.Baadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiwa katika michezo mbalimbali na familia zao kwenye maadhimisho ya Siku ya Familia (Family Day) hafla hiyo ilifanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana.

  0 0


  Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima (katikati), Kaimu Balozi wa Palestine Derar Ghannam (kulia) pamoja na Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohammed Ali wakikata utepe kwa ajili ya maonesho ya picha za matukio mbalimbali yanayoendelea nchini Palestina hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na watu wa Palestina yaliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar.
  Kaimu Balozi wa Palestina Derar Ghannam (wa kwanza kulia) akimuonyesha picha Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima (katikati) za matukio ya mauaji ya watu nchini Palestina yanayofanywa na Waisraeli ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina yaliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar.
  Baadhi ya picha zinazoonesha matukio ya mauaji pamoja na majeruhi yanayoendelea kutokea nchini Palestina kutokana na vita inayoendelea nchini mashariki ya Kati kati ya Palestina na Israeli.
  Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi Stella Vuzo (kulia) akitazama picha za wananchi wa Palestina waliouliwa na kutokana na mapigano ya Palestina na Israel yanayosababisha vifo vya watu wengi wasiokuwa na hatia.

  Baadhi ya wageni waalikwa wakiendelea kusikiliza kwa makini wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina. Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima akisoma hotuba yake mbele ya Mabalozi, wanafunzi wa chuo cha Diplomasia pamoja na wageni waalikwa waliofika kwenye maadhimisho ya ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina yaliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar.
  Naibu Mkurugenzi wa Mipango Utawala na Fedha wa Chuo cha Diplomasia, Dk.Bernard Achiula akizungumza jambo wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika chuoni hapo.
  Prof Josephat Kanywanyi ,Chairperson Tanzania- Palestine Solidarity committee akitolea ufafanuzi kuhusu mahusiano ya Tanzania na Palestina wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina.
  Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohammed Ali akisoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na watu wa Palestina.





  Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia wakiendelea kusikiliza kwa makini kinachozungumzwa kutoka meza kuu.




  Mshauri Mwandamizi wa Utawala kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa mataifa (UNDP), Steve Lee aliyemwakilisha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza uhusiano wa Palestina na Umoja wa Mataifa katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na watu wa Palestina yaliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar.




  Baadhi ya Mabalozi waliofika kwenye maadhimisho hayo wakiendelea kufuatilia yanayojiri.








  Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya Pamoja na Viongozi mbalimbali pamoja mabalozi.




  Viongozi wakiwa kwenye picha na wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia.


  Na Mwandishi wetu

  UN Tanzania ikishirikiana na Ubalozi wa Palestina nchini waadhimisha Siku ya Kimataifa na Mshikamano na watu wa Palestina na Tanzania katika Chuo cha Diplomasia Kurasini jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma na kukutana na mabalozi wa wa nchi mbalimbali akiwepo Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima, Kaimu Balozi wa Palestina Derar Ghannam na Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohammed Ali ambapo ikiwa kuendeleza ushirikiano pamoja na mfululizo wa maonesho ya picha mbalimbali za matukio yanayoendelea huko nchini Palestina.

  Mabalozi hao ambao walikutana katika jijini Dar es salaam kwaajili ya kuadhimisha siku hiyo ya kumbukumbu za picha za mapigano ya Palestina kwa ajiri ya kudumisha upendo na mshikamano pia mabalozi hao wameuomba umoja wa mataifa kuweza kuchukua hatua za ziada zitakazo pelekea nchi hiyo kuwa huru na kuweza kuendelea kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

  Mshauri Mwandamizi wa Utawala kutoka UNDP, Steve Lee akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alisema kuwa uhusiano wa Palestina na Umoja wa Mataifa katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina alisisitiza kuwa na na umoja baina ya nchi zote mbili hususani Palestina kuweza kupata uhuru na kutambulika kuwa ni nchi nyenye mipaka yake binafsi ili kuepusha mapigano hayo yasiweze kutokea na kila mtu aweze kuishi na amani akiwa ndani ya nchi yake na kuweza kufanya maendeleo ya nchi. Na aliweza kuziomba nchi mbalimbali kulitambua taifa la Palestina kama nchi kamili tofauti na inavyotambulika kwa sasa.

  Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa siku ya maonesho ya picha Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima amesema wamefanya hivyo kwani ni hari ya kuwatakia heri Wapalestine wote kwani watu wote waparestine walipoteza uhuru na kwa sasa wanautafuta uhuru kwani nchi wanayo lakin hawako huru kwahiyo ni lazima tuwaunge mkono kwa kuweza kuadhimisha siku hii sehemu mbalimbali tunayoishi.

  Kwa upande wa Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(UNIC), Bi Stella Vuzo amesema wameamua kuwa na maadhimisho kwani ndani ya miaka 50 Palestina wamekuwa hawajatambulika kama taifa lenye mipaka yake ambapo kumekuwa na migogoro ya mda mrefu ambao unawahusu wa Palestine na wayahudi ambao upo tangu mwaka 1947,wakati katika maadhimio walio fikiana ni kuwa na mataifa mawili ndani ya eneo moja ambap mpaka sasa Israel pekee ndo iliyo pata kuwa hali ya taifa lenye mipaka yake wakati . 
   
  Kila siku Israel huwa wanaleta vita ndani ya Palestine, sasa maadhimisho haya ni kwa ajili ya kuwaunga mkono kwa vitendo vinavyo endelea huko si vizuri. Pia aliwaomba viongozi wa pande zote mbili kuweza kuketi na kuweza kuweka maadhimio mapya kwaajili ya kuepusha mapigano yanayokuwa yakitokea kila siku baina ya nchi hizo mbili. Pia katika siku hiyo waliweza kuzindua picha za matukio ya vifo pamoja na watu walioumia kutokana na vita Palestina na Israel zilizo kuwa zimeandaliwa kwa Tanzania kwa ajili ya kuonyesha dunia matukio yanayoendelea katika nchi za Mashariki ya mbali hii yote ni kwa kuwa Palestina ina ushirikiano na Tanzania na kuwaombea katika kuelekea hali ya utulivu.

  0 0

   Makamu Mkuu wa Chuo cha kumbukumbu ya Hubet Kairuki Profesa, Kito Mshigeni akizugumza na wanafunzi  juu ya kutumia elimu waliyoipata  kuwasaidia, kuwainua, na kuwaletea  matumaini  mapya wote wenye uhitaji katika jamii, kwa kadri ya uwezo wao, ameyazungunza hayo katika mahafali ya 13 ya chuo kuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki Jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Chuo  Kikuu, Balozi Dk. Salim Ahmed Salim wa kwanza (kushoto) akiwa na uongozi wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki kabla ya kuanza kutunukia elimu zao wanazo hitimu  wahitimu wa elimu ya juu,  katika mahafali ya 13 ya chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki leo Jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Chuo  Kikuu, Balozi Dk. Salim Ahmed Salim akimkabidhi cheti cha shahada ya kwanza ya Uuguzi  mhitimu, Nyawawa Wawa  leo katika mahafali ya 13 ya chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuk Jijini Dar es Salaam.

  Brass Band ikiendelea kutumbuiza katika mahafali ya 13 ya chuo kikuu cha kumbukumbu cha Hubert Kairuki leo Jijini Dar es Salaam. 
  Baadhi ya wahitimu wa Kozi ya cheti cha Uuguzi wakila kiapo, leo Jijini Dar es Salaam.
  Sehemu  ya  wahitimu na wazazi waliohudhuria katika mahafali ya 13 ya chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki leo Jijini Dar es Salaam.
  (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu  ya jamii).

  0 0

  MAHAKAMA ya hakimu mkazi Morogoro imemuachia huru leo Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi baada ya mahakama kutoridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka na hivyo kuonekana hana hatia.

  ********
  Historia ya kesi ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda.

  Hati ya Mashitaka ya Kesi hiyo ilikuwa na jumla ya Mashitaka matatu  lakini Julai 22 mwaka 2015, Hakimu Mkazi Mary Moyo  alitoa  uamuzi wa kumfutia shitaka la kwanza kwasababu lilishatolewa uamuzi na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, na hivyo mahakama hiyo ya Morogoro siku hiyo ilitoa uamuzi wa kumuona ana kesi ya kujibu  katika mashitaka mawili yaliyosalia ambalo ni kosa la pili na la tatu .


  Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro  ilimfungia dhamana Sheikh Ponda baada ya kukubaliana na hati ya aliyekuwa  Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), wakati huo Dk.Eliezer Feleshi ambaye kwasasa ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam liloomba Mahakama hiyo imfungie dhamana mshitakiwa huyo chini ya Kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai ya Mwaka 2002.

  Hatua hiyo ya kufunguliwa kesi katika Mkoa wa Morogoro ilikuja ikiwa ni muda mfupi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Agosti 19 Mwaka 2013 saa Tatu asubuhi,  kumfutia kesi ya jinai  Na.144/2013 katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano baada ya DPP kudai kuwa hana nia ya kuendelea kumshitaki katika kesi hiyo No.144/2013  kwa mujibu wa kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.

  Hata hivyo baada ya hakimu Liwa kumwachilia huru,Ponda ambaye aliletwa mahakamani hapo saa 12 asubuhi na wanausalama wa polisi na magereza chini ya ulinzi mkali, alikamatwa tena na kupakizwa kwenye magari ya wanausalama hao ambapo baadhi ya wanausalama hao waliliambia gazeti hili kuwa wanampeleka Ponda mkoani Morogoro kwaajili ya kufunguliwa makosa matatu ya uchochezi, kufanya mkusanyiko haramu na kisha akarejeshwa gereza la Segerea Dar es Salaam , lakini baadae Uongozi wa Jeshi la Magereza uliamua kumuamisha Ponda kutoka Gereza la Segerea na kumuamishia Katika Gereza Moja Mkoani Morogoro.

  Sheikh Ponda alifikishwa mahakamani hapo akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi, baada ya kuwasili kwa helikopta ya Jeshi la Polisi katika uwanja wa gofu mjini Morogoro.

  Akisoma mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro, Richard Kabate, Mwanasheria Kiongozi  wa Serikali, Bernard Kongola, alidai  kuwa Agosti 10, mwaka 2013, katika eneo la Uwanja wa Ndege, Manispaa ya Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu wasikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti, kwa madai kuwa zimeundwa na BAKWATA, ambao ni vibaraka wa CCM na serikali.

  Alidai kuwa Sheikh Ponda ambaye anatetewa  na wakili wa kujitegemea Juma Nassor aliwaagiza waumini hao kuwa endapo watu hao watajitokeza kwao na kujitabulisha kwamba ni kamati za ulinzi na usalama za misikiti, wafunge milango na madirisha wawapige.

  Ilielezwa kuwa kauli hiyo ni kinyume cha agizo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyotolewa na Hakimu Victoria Nongwa Mei 9, mwaka 2010, ambayo ilimtaka Ponda ndani ya mwaka mzima kuhubiri amani na Kuwa Raia Mwema.

  Katika shitaka la pili, Kongola alidai kuwa Agosti 10, mwaka huu, katika eneo la Uwanja wa Ndege, Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu kuwa serikali ilipeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi ili kuwaua, kuwabaka na kuwatesa wananchi, kwa sababu asilimia 90 ya wakazi hao ni Waislamu.

  Kwamba, Ponda aliwaambia wafuasi wake kuwa serikali haikufanya hivyo kwa wananchi wa Loliondo walipokataa Mwarabu asipatiwe kipande cha ardhi ya uwindaji baada ya kudai ni mali yao, kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wa huko ni Wakristu.

  Shitaka la tatu ambalo linafafana na lile la pili, ambalo nalo linadaiwa kutendwa Agosti 10, mwaka huu, ambapo kauli ya Ponda inadaiwa kuumiza imani za watu wengine kinyume cha kifungu cha sheria namba 390 na kanuni ya adhabu namba 35 cha mwaka 2002.

  Oktoba 18 mwaka 2012, Ponda na wenzie 49 walifikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa Mara ya kwanza   wakikabiliwa na makosa matano, kosa la kwanza ni la kula njama, kujimilikisha mali, kuingia kwa jinai katika kiwanja cha Chang'ombe  Markas,wizi wa malighafi zenye thamani ya Sh. Milioni 59 na kosa la uchochezi ambapo katika kesi hiyo Jamhuri ilikuwa ikiwakilishwa na wakili Mwandamizi wa Serikali , Tumaini Kweka .Mahakama pia iliwafunga dhamana ya Ponda na mshitakiwa wa pili tangu 0ktoba 18 Mwaka 2012 hadi siku Kesi hiyo iliyotolewa hukumu Mei 9 Mwaka 2013.

  Mei 9 mwaka 2013 Hakimu Mkazi Victoria  Nongwa akitoa hukumu yake katika kesi hiyo ya Ponda na wenzake alisema anawaachiria huru washitakiwa 49  kwasababu upande wa jamhuri  umeshindwa kuthibitisha kesi dhidi yao na kwamba anamtia hatiani Ponda kwa kosa moja tu  la kuingia kwa jinai na kwamba na anamuachiria huru katika makosa manne yaliyosalia kwasababu pia jamhuri ilishindwa kuthibitisha mashitaka hayo dhidi ya Ponda.

  Sheikh Ponda alikataa rufaa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupinga hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mei 9 mwaka 2013 ambapo alishinda rufaa yake.

  Hata hivyo siku Chache baada ya Kufungwa Kifungo hicho cha nje Mei 9 mwaka 2013, Ponda alikwenda Mkoani Morogoro na kufanya mkutano ambao alidai wa Kutenda makosa ya jinai ambao alikamtwa  Agosti Mwaka 2013 na kuwekwa chini ya ulinzi na kufunguliwa Kesi Mahakama ya Kisutu Na.144/2013 ikafutwa na DPP na ndipo akafunguliwa kesi hiyo Mkoani Morogoro ambayo imetolewa hukumu Leo na kuachiwa huru.

  0 0

    Mkurugenzi Mtendaji wa tofuti ya ajira ya Owbaz, Barbara Butter (kushoto) akimpa maua balozi mpya wa Owbaz, Abernego Damian Nyamoga ‘Belle 9’ katika hafla ya uzinduzi rasmi wa tovuti hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Cosmos,  Muhammad Owais Pardesi na Mkurugenzi Rasilimali Watu wa kampuni ya bima ya Aris, Paritosh Bajaria.
   Mkurugenzi Mtendaji wa tofuti ya ajira ya Owbaz, Barbara Butter (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa tovuti hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Cosmos,  Muhammad Owais Pardesi, balozi wa Owbaz, msanii wa muziki wa kizazi kipya Abernego Damian Nyamoga ‘Belle 9’  na Mkurugenzi Rasilimali Watu wa kampuni ya bima ya Aris, Paritosh Bajaria.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa Cosmos, na mwanzilishi wa tovuti mpya ya Owbaz, Muhammad Owais Pardes (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa tovuti hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Abernego Damian Nyamoga ‘Belle 9’ (wa tano kushoto) ambaye ni balozi wa tovuti ya Owbaz, akipozi kwa picha pamoja na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa tovuti hiyo jijini Dar esSalaam mwa wiki.

   Baadhi ya wageni waalikwa wakipiga picha ya kumbukumbu na  msanii wa muziki wa kizazi kipya, Abernego Damian Nyamoga ‘Belle 9’katika hafla ya uzinduzi wa tovuti hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  0 0
 • 11/30/15--01:42: BEI YA MADAFU HII LEO

 • 0 0

  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeandikisha wakulima wa Korosho zaidi ya 300 mkoani mtwara kwenye kampeni ijulikanayo kama NSSF Kwanza ambayo ilifanyika mahususi ili kuwafikia watu ambao wako kwenye sekta  isiyo rasmi.

  Kampeni hiyo yenye malengo ya kufikia umma wa Watanzania ambao haujafikiwa na elimu ya Hifadhi ya jamii, Kuwaandikisha kujiunga na NSSF ili kuongeza wigo wa wanachama na pia  Kupata mrejesho  wa huduma zetu kutoka kwa wanachama wa mfuko.Imemaliza mkoani Mtwara na itaendelea kwenye mikoa mingine.NSSF inaendelea kuwasihi Watanzania waendelee kujiunga na NSSF.
  Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (wa pili kulia), akiwapa maelezo kuhusu huduma zitolewazo na NSSF wakulima wa Kijiji cha Msijute, Kata ya Mayanga, mkoani Mtwara, kwenye kampeni maalumu ijulikanayo kama ‘NSSF Kwanza’, ambayo inaendelea kwa kuwafikia watu walio kwenye sekta binafsi.
   Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akiwapa maelezo wakazi wa kijiji cha Msijute jinsi ya kujiunga na Huduma ya mafao ya Matibabu bure  kwenye kampeni maalumu ya kuwaelimisha wakazi wa Mkoa wa Mtwara juu ya faida za Hifadhi ya Jamii kupitia NSSF.
  Wakazi wa Kijiji cha Msijute kata ya Mayanga Mkoani Mtwara wakijiandikisha NSSF ili kuweza kujipatia mafao bora kutoka NSSF yakiwemo mafao ya matibabu bure kwa wanachama na familia zao.

  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akifuatilia kabumbu ya wanawake iliyokua ikiendelea wakati wa tamasha la Live Your Goals kuhamasisha mpira wa miguu wa wanawake lililoandaliwa na FIFA jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Karume. Kulia ni Mkurugenzi wa Michezo Bw. Leonard Thadeo, na kushoto ni Mwenyekiti Kamati Soka la Vijana Bw. Ayoub Nyenzi.
   Baadhi ya wanasoka wanawake kutoka katika vilabu mbalimbali vya mpira wa miguu wakisakata kabumbu jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Karume wakati wa tamasha la Live Your Goals kuhamasisha mpira wa miguu wa wanawake lililoandaliwa na FIFA.
    Mabalozi walioteuliwa na FIFA kuhamasisha mpira wa miguu wa wanawake nchini wakijitambulisha kwa mgeni rasmi wakati wa tamasha la Live Your Goals lilifanyika jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume kwa mara ya pili baada ya kufanya tamasha hilo kwa mara ya kwanza Mkoani Geita mnamo mwezi Julai 2015.

   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wapili kushoto) akimwangalia mtoto Zaynab Dotto mwenye umri wa miaka 10 anavyocheza na mpira kwa umahiri jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume. Kulia ni Mratibu wa Michezo ya Vijana wadogo Bw. Raymond Gweba na kushoto ni mama mzazi wa mtoto Zaynabu Bibi. Pili Said.

   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wapili kushoto) akipokea zawadi ya vifaa vya michezo kutoka FIFA vilivyokabidhiwa kwake na balozi alieteuliwa na FIFA kuhamasisha mpira wa miguu wa wanawake nchini Bibi. Ester Chabuluma jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume. Kushoto ni Mwenyekiti Kamati Soka la Vijana Bw. Ayoub Nyenzi.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (watatu kushoto) akitoa zawadi ya mpira kwa mwanasoka wakike kutoka shule ya msingi Kingugi walioshiriki katika tamasha la Live Your Goals linalo hamasisha mpira wa miguu wa wanawake jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati mwenye koti la bluu) katika picha ya pamoja na wanasoka wanawake kutoka katika shule 5 za msingi na vilabu 6 vya mpira wa miguu wa wanawake baada ya kuhitimisha tamasha la Live Your Goals lilifanyika jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (watatu kushoto) akisisitiza jambo jana alipokutana na timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 kuikabidhi bendera ya taifa kabla ya kwenda nchi mbalimbali za afrika kwa ajili ya mazoezi ya kujihimarisha kushiriki mashindano ya kufuzu mataifa ya Afrika under 17 mnamo mwaka 2017 nchini Madagasca.
    Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akikabidhi bendera ya taifa kwa naodha wa timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 Bw. Issa Abdi jana katika Viwanja vya Karume kwa ajili ya kwenda nchini Rwanda, Uganda na Kenya kupata ujuzi na mazoezi kabla ya kushiriki mashindano ya kufuzu mataifa ya Afrika under 17 mnamo mwaka 2017 nchini Madagasca.

  Picha na: Genofeva Matemu.

  0 0

   Mshiriki wa mafunzo ya Airtel Fursa mkoani Iringa Bi Fatuma Mkini (kushoto ) akipokea cheti cha ushiriki wa mafonzo hayo kutoka kwa afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki mara baada ya mafunzo ya Airtel Fursa kumalizika mkoani Iringa kwa vijana zaidi ya 200 kushiriki.
   Vijana washiriki wa mafunzo ya siku moja ya Airtel Fursa mkoani Iringa wakimsikiliza afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki (kulia) wakati wa ufungizi wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Highland mjini Iringa jana.
  Wawakilishi wa vijana zaidi ya 200 mkoani Iringa walioshiriki kupata mafunzo ya ujasiriamali kupitia mradi wa Airtel fursa wakiwa katika picha ya pamoja na afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki na wafanyakazi wengine wa Airtel mkoa wa Iringa mara baada ya kukabidhiwa  vyeti kwa niaba ya wenzao.
   (picha na mpiga picha wetu)

  BAADA ya kukata tamaa ya maisha kwa muda mrefu baadhi ya vijana mkoani Iringa wameeleza kufurahishwa na kampuni ya simu ya Airtel Tanzania kwa kuwapatia mafunzo ya jinsi ya kuanzisha na kuendesha biashara zao kwa faida kupitia mpango wa Airtel FURSA

  Wakizungumza na mara baada ya mafunzo ya siku moja ya Airtel FURSA yaliyofanyika katika ukumbi wa Highlands mjini Iringa kwa kuwashirikisha vijana zaidi ya 200,washiriki hao walisema kuwa mafunzo hayo ni ukomb0zi mkubwa kwao kwani baadhi yao walikuwa wakilazimika kushinda vijiweni kutokana na kukosa fursa ya mafunzo kama hayo .

  Washiriki wa mafunzo hayo Bi Husna Sanga na Bw Okelo Kasim wakizungumza kwa niaba ya wenzao walisema kuwa mbali ya kuwa wa hatua ya kampuni hiyo ya simu ya Airtel kutoa mafunzo hayo si tu kunawasaidia kupata elimu kuendesha biashara na miradi mingine ya kiuchumi bali ni sehemu ya ukombozi kwao na familia zinazowazunguka .

  Alisema Bi Sanga kuwa sehemu kubwa ya vijana hasa mabinti walikuwa wakirubunika na kujiingiza katika biashara zisizofaa kama za uuzaji wa miili yao kutokana na kutokuwa na elimu ya uanzishaji wa biashara ndogo ndogo ambao zingewakomboa kiuchumi hivyo kupitia mpango huo wa Airtel FURSA ni wazi kilio chao kimepata majibu.

  "Wapo baadhi ya mabinti wenzetu ambao wanalazimika kufanya biashara ya kuuza miili yao ili kupata kipato na mwisho wa siku wanapoteza maisha kwa ugonjwa wa UKIMWI , ila kwa sisi ambao tumepata elimu hii kupitia Airtel FURSA tunaweza kuwa mfano kwa wengine ambao wanafikiri kazi ni kuuza miili yao pekee"

  Huku Bw Kasim mbali ya kupongeza kampuni ya simu ya Airtel Tanzani kwa kuwakumbuka vijana bado alisema kuwa kama njia ya wao kupongeza kampuni hiyo ya simu kwa vijana wote waliopata mafunzo hayo kwenda kuonyesha mfano kwa wenzao kwa kufanya kazi ya kubuni miradi na kuendesha shughuli zao kifanisi zaidi.

  Kwa upande wake afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki kuwa Kutokana na mradi huo wa Airtel FURSA vijana wengi watanufaika zaidi na wanafaidika na mradi huo ni wale wenye miaka kati ya 18-24

  Alisema kuwa mradi huo umelenga kuwafikia vijana kote nchini na hadi sasa zaidi ya mikoa tisa wamefikiwa na mradi huo wa Airtel FURSA .

  Bi Kaniki alitaja mikoa ambayo tayari imefikiwa na mradi huo Mbeya, Arusha, Dodoma, Mtwara, Mwanza, Mtwara, Dar es Salaam , morogoro, Tanga, Tabora na Iringa kuwa hadi sasa zaidi ya vijana 1700 wamefikiwa.

  Alisema kuna njia mbili za kuwawezesha vijana njia ya kwanza kupatiwa Mafunzo ya ujasiriamali na njia ya pili kupatiwa vitendea Kazi .

  Hivyo aliwataka vijana wote nchini ambao watasikia taarifa ya kuwepo kwa Airtel Fursa katika Mkoa wao basi kuweza kuchangamkia Fursa hiyo ambao hutolewa bure.

  Alisema ili kijana aweze kufaidika au kushiriki kwenye Airtel FURSA atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:- Jina, Umri, aina ya biashara na eneo. Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara.

  Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtelwww.airteltanzania.com

  Alisema kuwa Airtel Fursa inawalenga vijana ambao wapo katika biashara na wale ambao hawana shughuli na wanataka kuanzisha shughuli pia kwao ni fursa kwao .


  Aidha alisema kuwa tayari baadhi ya vijana wamepata kunufaika na mradi huo ambao umelenga kuwainua vijana na kuongeza kuwa mradi huo ulioanza mwaka huu utakuwa ni mradi endelevu.

older | 1 | .... | 697 | 698 | (Page 699) | 700 | 701 | .... | 1898 | newer