Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

MAGUFULI ATINGA OFISINI KWA MAJALIWA

0
0

Rais John Magufuli akitia saini kitabu cha wageni wakati alipomtembelea Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa ofisini kwake jijini Dar es salaam Novemba 26, 2015 na kuzungumza nao kwa takribani saa moja (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Rais John Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa wakati alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam Novemba 26, 2015 na kuzungumza nae kwa takribani saa moja. Rais John Magufuli akiagana na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa wakati alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam Novemba 26, 2015 na kuzungumza nae kwa takribani saa moja. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Serikali yajidhatiti kupambana na kemikali zenye madhara maeneo ya bandari

0
0
 
Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele akifungua mafunzo ya kujiandaa kukabiliana na dharura ya kemikali zenye madhara kwa afya na mazingira kwenye maeneo ya bandari leo jijini Dar es salaam. 
Meneja wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Mashariki Bw. Daniel Ndiyo akiwakaribisha wadau wa masuala ya kemikali kutoka Mataifa mbalimbali kushiriki katika mafunzo ya kujiandaa kukabiliana na dharura ya kemikali zenye madhara kwa afya na mazingira kwenye maeneo ya bandari leo jijini Dar es salaam. 
Wadau wa masuala ya kemikali kutoka Mataifa mbalimbali wakifuatilia mafunzo ya kujiandaa kukabiliana na dharura ya kemikali zenye madhara kwa afya na mazingira kwenye maeneo ya bandari leo jijini Dar es salaam. Mwakilishi kutoka nchini Ujerumani Bibi. Stefane Deuser akichangia mada kwenye warsha ya kujiandaa kukabiliana na dharura ya kemikali zenye madhara kwa afya na mazingira kwenye maeneo ya bandari.  
Mratibu wa Kanda kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mazingira (UNEP) Bw.Patrick Mwesigye akizungumza leo jijini Dar es salaam kwenye warsha ya kujiandaa kukabiliana na dharura ya kemikali zenye madhara kwa afya na mazingira kwenye maeneo ya bandari.
Picha Zote Na Fatma Salum (MAELEZO)

JK ATINGA OFISINI KWAKE LUMUMBA

0
0

Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye mara baada ya kuwasili kwenye Makao Makuu ya Chama Ofisi Ndogo Lumumba.

Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ofisini kwake Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba .

Serikali imejipanga kukuza na kuendeleza Stadi za Kazi nchini

0
0
za1
Mkurugenzi Msaidizi Toka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi Dkt.Jonathan Mbwambo akifafanua kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mpango wa Serikali wa kuendeleza stadi za kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuongeza tija katika sekta zote nchini,kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bi. Zamaradi Kawawa.
za2Mkurugenzi Msaidizi Toka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi Dkt.Jonathan Mbwambo akiwaeleza waandishi wa Habari kuhusu faida za kuendeleza stadi za kazi ikiwemo kuongeza uzalishaji katika sekta zote nchini,kulia Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bi. Zamaradi Kawawa.
za3 
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi na vyombo vya habari leo jijini Dar eS Salaam uliolenga kueleza mpango wa Serikali kuwawezesha wananchi kupitia mpango wa kuendeleza stadi za kazi unaotarajiwa kuanza mwaka wa fedha 2016/2017.Picha Zote na Fatma Salum (MAELEZO)

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN, AKUTANA NA VIONGOZI WA MTANDAO WA ULINGO TANZANIA (UMOJA WA WANAWAKE WANASIASA).

0
0
has1 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na baadhi ya Wanawake wanaounda Umoja wa Wanawake Wanasiasa kutoka Vyama mbalimbali vya Siasa Tanzania walio katika Mtandao wa Ulingo, wakati alipokutana nao katika kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has3 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na baadhi ya Wanawake wanaounda Umoja wa Wanawake Wanasiasa kutoka Vyama mbalimbali vya Siasa Tanzania walio katika Mtandao wa Ulingo, wakati alipokutana nao katika kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has4 
Baadhi ya Wanawake Wanaulingo wakimsikiliza Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akiwahutubia kwenye katika kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has5 
Balozi Getrude Mongela, akichangia moja ya kati ya mada zilizokuwa zikizungumziwa katika kikao hicho leo. Picha na OMR
has6 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya Wanaulingo alipokuwa akipokelewa alipowasili kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria kwenye Kikao maalum kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania kwa ajili ya kumpongeza . Picha na OMR

has7 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kuimba wimbo maalum wa mshikamano kwa wanawake wakati wa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OM
has8has9 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kuimba wimbo maalum wa mshikamano kwa wanawake wakati wa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OM
has10Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi ya ‘Dua’ kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar na Katibu wa Ulingo Tanzania, Salama Aboud Talib, baada ya kumalizika kwa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has11 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi ya picha baada ya kumalizika kwa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has12 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifurahia jambo na Balozi Getrude Mongela baada ya kumalizika kwa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has13Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Mtandao wa Ulingo Tanzania, wanaounda Umoja wa wanawake Wanasiasa wa Vyama mbalimbali vya Siasa Tanzania, baada ya kumalizika kwa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has15Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Mtandao wa Ulingo Tanzania, wanaounda Umoja wa wanawake Wanasiasa wa Vyama mbalimbali vya Siasa Tanzania, baada ya kumalizika kwa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has18Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na baadhi ya Viongozi wa Mtandao wa Ulingo Tanzania, wanaounda Umoja wa wanawake Wanasiasa wa Vyama mbalimbali vya Siasa Tanzania, baada ya kumalizika kwa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR

ROSE MUHANDO KUNOGESHA TAMASHA LA KUSHUKURU DIAMOND JUBILEE

0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa matamasha ya muziki wa injili nchini Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati alipofafanua mambo mbalimbali kuhusu maandalizi ya tamasha la kushukuru baada ya kufanyika na  kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Tanzania salama salimini.

Msama amesema maandalizi yanaendelea vizuri na amemtangaza rasmi mwimbaji Rose Muhando kama mmoja wa waimbaji wa muziki wa injili watakaoshiriki katika tamasha hilo,  linalotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Desemba 25 na kushirikisha waimbaji wa kimataifa kutoka nchi za Afrika na Ulaya, ambapo ameongeza kwamba mazungumzo bado yanaendelea na waimbaji wengine kutoka nje ya nchi.

Katika picha katikati ni Mwimbaji wa muziki wa Injili Rose Muhando akishiriki katika mkutano huo na kushoto ni William Kapawaga mmoja wa waratibu wa Tamasha hilo kutoka Kampuni ya Msama Promotion.
Mwimbaji wa muziki wa Injili Rose Muhando akiwaelezea waandishi wa habari jinsi alivyojiandaa kutumbuiza katika tamasha hilo la kushukuru, Kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama.
baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion wakati alipokuwa akizungumza nao jijini Dar es salaam kuhusiana na Tamasha hilo.

SERIKALI YAKANUSHA KUHUSU HAZINA KUACHWA TUPU

0
0
Na Jovina Bujulu-Maelezo

Serikali imekanusha taarifa zinazosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa amekomba fedha hazina na kuiacha Serikali bila fungu lolote.

Hayo yamesemwa jijini dare es salaam na Kamishina wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha Bwa. John Cheyo huku akiwataka wananchi kupuuza habari hiyo kwani hazina ukweli wowote.

“Hazina inazo pesa za kutosha  na tunajivunia kufanya uchaguzi wa mwaka huu,  kununua mashine za BVR  kwa kutumia pesa za watanzania bila kutegemea msaada wowote kutoka nje ya nchi  na kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka huu” alisema Bwa. Cheyo.

Pia aliongeza kuwa serikali imeendelea kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa bomba la gesi ambalo limekamilika hivi karibuni, vinu vya kuchakata gesi na ujenzi wa barabara nchini.

Aliendelea kusema kwamba mfumo wa serikali wa bajeti unaiwezesha serikali kupanga vipaumbele vya matumizi kulingana na bajeti ilivyopangwa ambapo fedha zinazokusanywa kupitia mfuko mkuu wa serikali ndizo hutumika.

Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwa kipindi cha 2015-2016 ni shilingi Trilioni 22.5 na bajeti hiyo inatengenezewa mpango wa makusanyo na matumizi kwa kulipia mishahara ya wafanyakazi na miradi mbalimbali iliyoidhinishwa.

Pia katika matumizi mengine bajeti hiyo inalipia chakula cha wanafunzi, mikopo ya wanafunzi elimu ya juu, ununuzi wa dawa na vifaa tiba na chakula cha hifadhi ya taifa.

Taasisi ya Benjamin William Mkapa yasikitishwa na udanganyifu au utapeli unaoendeshwa na baadhi ya watu wasiojulikana kupitia jina lake

0
0
Taasisi ya Benjamin William Mkapa inasikitika kuwatangazia Umma kwamba kumekuwa na udanganyifu au utapeli unaoendeshwa na baadhi ya watu wasiojulikana wakitumia jina la Taasisi hii katika kutoza fedha watu mbalimbali wakidai kusaidia kupata ajira au ufadhili wa masomo katika sekta ya afya.
Baadhi ya wadanganyifu hao wamekuwa wakitumia barua au akaunti yenye jina “Benjamini Mkapa” katika mtandao wa kijamii wa ‘facebook’ ambapo huwasiliana na watu, na kuwahadaa kuwa watawapatia ajira au ufadhili baada ya kujaza fomu na kutoa fedha katika mchakato mzima.

Taasisi ya Benjamin William Mkapa (ijulikanayo kama “Benjamin W. Mkapa HIV/AIDS Foundation”) inapenda kuwatangazia umma kuwa haihusiki na utaratibu huo wa udanganyifu au utapeli. Tunapenda kuwasisitizia wananchi kwamba hakuna fedha yoyote inayotozwa na Taasisi kwa ajili ya kupata ajira au ufadhili wa masomo chini ya miradi inayoendeshwa na Taasisi yetu.
Kwa mtu yoyote mwenye kutaka kupata habari za uhakika na kamili juu ya masuala hayo, tafadhali, awasiliane na ofisi ya makao makuu iliyopo Dar Es Salaam, na ofisi za Kanda zilizopo Mwanza, Mtwara na Iringa, au kwa kupitia email: info@mkapahivfoundation.org au facebook account: www.facebook.com/BenjaminWilliamMkapaHivAidsFoundation, namba za simu +255 22 2618556-9
Taasisi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini na hatimaye kuwatia kwenye mikono ya sheria wadanganyifu hao.

Imetolewa na:
Menejimenti ya Taasisi ya Benjamin William Mkapa 

NHIF YAKAMILISHA UJENZI WA KITUO CHA KISASA CHA UCHUNGUZI NA MATIBABU KILICHOJENGWA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA

0
0
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa NHIF, Michael Mhando akizungumza wakati wa makabidhiano ya  kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
 Mkurugenzi mtendaji kampuni ya ujenzi Tanzania Building Works Ltd, Mohamed Iqbal Moray(kushoto), akimkabidhi funguo za  kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa NHIF Michael Mhando.
 Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na uwezeshaji wa mfuko wa NHIF, Deusdedit Rutazaa akizungumza wakati wa makabidhiano ya kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma
Wafanyakazi wa mfuko wa NHIF na wa Hospitali ya rufaa ya Dodoma wakishiriki makabidhiano ya kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
 
  Jengo la ujenzi wa kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma
  Sehemu ya jengo la ujenzi wa kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma
  Sehemu ya jengo la ujenzi wa kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma


MFUKO wa Taifa wa Bima ya afya(NHIF) umekamilisha ujenzi wa kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma ambacho kitasaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali hiyo.

Akizungumza katika makabidhiano ya jengo hilo, Kaimu Mkurugenzi wa NHIF,  Michael Mhando, alisema kituo hicho kitakuwa cha kisasa na kitatoa huduma mbalimbali ikiwemo huduma za CT-Scan na kitafunguliwa kabla ya mwezi januari mwakani ili

“NHIF umelipatia ufumbuzi tatizo la msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma baada ya kukamilisha ujenzi wa jengo hili ambalo limegharimu kiasi cha sh. Bilioni sita ikiwa ni pamoja na vifaa vya matibabu na samani,”alisema Mkurugenzi huyo.

Alisema ujenzi wa huo umeanza tangu mwaka 2008 na litakuwa na uwezo wa kuchukua vitanda 34 vya
wagonjwa.

“Kituo hichi kitakuwa na vyumba vya madaktari, maabara,  upasuaji, chumba cha kutolea dawa, mapokezi,  chumba cha wagonjwa mahututi, chumba cha dharura, mfumo wa miito ya wauguzi, na vifaa tiba vya kisasa,”alisema Mhando

Alisema kitatoa huduma kwa wanachama wa mfuko huo, wananchi wa Mkoa wa Dodoma na mikoa jirani.

MWILI WA MAWAZO KUAGWA KITAIFA KATIKA UWANJA WA FURAHISHA JIJINI MWANZA

0
0
Mkutano wa Naibu Katibu Mkuu Chadema Salum Mwalimu na Wanahabari Jijini Mwanza hii leo.
Naibu Katibu Mkuu Chadema, Salum Mwalimu akionyesha kibali kilichotolewa na Manispaa ya Ilemela ili kuruhusu ibada ya kumuaga Marehemu Mawazo Kufanyika kesho katika Uwanja wa Furahisha
Mkutano wa Naibu Katibu Mkuu Chadema Salum Mwalimu na Wanahabari Jijini Mwanza hii leo (hawapo pichani).
Kushoto ni Ezekiel Wenje na Kulia ni Grace Kihwelu ambae ni Mbunge Viti Maalumu Chadema Mkoani Kilimanjaro
Singo Kigaila Benson ambae ni Mkurugenzi wa Mafunzo Chadema (Kushoto) akiwa na Peter Mekele ambae ni Mwenyekiti Chadema Kanda ya Ziwa Victoria (Kulia)

Husna Amri Said ambae ni Mwenyekiti BAWACHA Wilayani Geita
Viongozi na Makada wa Chadema
Mkutano wa kutoa ratiba za kuuaga mwili wa Marehemu Mawazo kwa wanahabari Jijini Mwanza hii leo
Wanahabari.
Na:Binagi Media Group
Mwili wa aliekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoa wa Geita Marehemu Alphonce Mawazo, kesho unatarajiwa kuagwa Jijini Mwanza kabla ya kusafirisha kwenda Mkoani humo kwa ajili ya Mazishi.

Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema Salum Mwalimu, amesema Marehemu Mawazo ataagwa Kitaifa kwa taratibu za chama hicho, katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.

Amesema ratiba hiyo itatanguliwa na ratiba ya kifamilia ya kuuaga mwili huo, ambayo itafanyika asubuhi Nyegezi Jijini Mwanza ambako ni nyumbani kwa Mchungaji Charles Lugiko ambae ni baba mdogo wa Marehemu Mawazo hiyo ikiwa ni baada ya mwili wake kutolewa katika Hospitali ya Rufaa Bugando ulikohifadhiwa.

Mwalimu amebainisha kwamba mwili huo utasafirishwa hiyo kesho kwenda Mkoani Geita kuanzia majira ya saa nane mchana ambapo wakazi wa Mkoa huo pia watapata fursa ya kuuagwa kesho kutwa jumapili.

Ameeleza kwamba kuanzia majira ya saa mbili asubuhi, shughuli za kuuaga mwili huo zitafanyika Kimkoa katika Uwanja wa Magereza Mjini Geita na baadae kusafirisha kwenda Katoro ambapo wakazi wa Jimbo lake la Busanda watapata fursa ya kuuaga mwili huo.

Mwalimu ametanabaisha kwamba, baada ya shughuli zote hizo kukamilika, mazishi ya Marehemu Mawazo yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu katika Kijiji cha Chikobe Jimbo la Busanda Mkoani Geita.

Shughuli zote hizo zinatarajiwa kuongozwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe, Viongozi waandamizi wa Chama hicho akiwemo Frederick Sumaye, aliekuwa mgombea urais wa Ukawa Edward Lowasa, wabunge pamoja na makada wa Chadema.

Ratiba za Mazishi ya Marehemu Mawazo ambae aliuawa Novemba 14 mwaka huu na watu wasiojulikana, zimejiri baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza jana kuondoa zuio la Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza, lililokuwa zinazuia mwili huo kuagwa Jijini Mwanza kutokana na hofu ya kiusalama pamoja na uwepo wa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambapo zuio hilo liliondolewa katika kesi iliyofunguliwa na baba mlezi wa Mawazo, Mchungaji Charles Lugiko baada mvutano mkali wa siku nne mahakamani hapo.

Waziri Mkuu Majaliwa azindua ununuzi wa hisa za Benki ya Walimu- MCB

0
0
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa akigonga kengelle kuashiria uzinduzi wa ununuzi wa hisa za Benki ya Walimu- MCB kwenye soko la hisa la Dar es salaam. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es salaam Novemba 27, 2015. Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua uuzaji wa hisa za Benki ya Walimu MCB kwenye soko la hisa la Dar es salaam, uliofanyika jijini Dar es salaam Novemba 27, 2015. Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akiteta na baadhi ya Viongozi wa Benki ya Walimu- MCB baada ya kuzindua uuzaji wa hisa za Benki hiyo katika soko la hisa la Dar es salaam. Uzinduzi huo uliyofanyika jijini Dar es salaam Novemba 27, 2015
Waziri Mkuu,Majaliwa Kassim Majlaiwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile baada ya kuzindua mpango wa Benki ya Walimu MCB – MCB kuanza kuuza hisa zake kwenye soko la hisa la Dar es salaam Novemba 27, 2015. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dares salaam.3065 (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KAMPENI YA ABIRIA PAZA SAUTI YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0

Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Abel Swai (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo, kuhusu kampeni ya Abiria Paza Sauti iliyozinduliwa Dar es Salaam leo asubuhi.

Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi, Mohamed Mpinga amesema kila mwananchi anawajibu kuzuia ajali za barabarani badala ya kudhani kazi hiyo ni ya polisi pekee.

Mpinga alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Abiria Paza Sauti iliyozinduliwa Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam leo asubuhi, ambao ulikwenda sanjari na mabalozi wa Usalama barabarani  (RSA) ambao walitoa elimu  kwa abiria kuhusu usalama barabarani.

"Abiria pazeni sauti pale mtakapoona dereva anaendesha gari lake ndivyo sivyo na kama mtapaza sauti itasaidia kupunguza ajali hapa nchini" alisema Kamanda Mpinga.

Mwakilishi  wa Mwenyekiti wa Usalama Barabarani ambaye ni Mratibu wa kampeni hiyo , Jackson Kalikuntima, alisema kampeni hiyo itaendelea nchini kote kwa njia ya kutoa elimu, haki na wajibu wa raia wanapokuwa safarini.

Alisema abiria wanaowajibu wa kuzuia ajali wakishirikiana na mabalozi watakao kuwa ndani ya mabasi kuhimiza abiria kupaza sauti.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Abel Swai alisema kumekuwa na changamoto kubwa kwa baadhi ya madereva kukiuka sheria na kusababisha ajali kwa makusudi.

Alisema kampeni hiyo inalengo la kutoa elimu kwa abiria waweze kujiamini na kutoa taarifa pale wanapoona dereva anakwenda kinyume na sheria kwa kutumia namba za kutoa taarifa kwa polisi na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) ambazo ni 0800110019 au 0800110020.

Swai alisema madereva wanapaswa kutii sheria bila shuruti na kuwa wana amini kila mmoja atakuwa makini na kuzingatia sheria ajali zitapungua kama sio kuisha kabisa.


Makumbusho ya Taifa yazindua maonyesho ya picha za matukio yanayohusu Albino nchini

0
0
al2Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabulla (kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Under The Same Sun Bw. Peter Ash, Mwakilishi wa Benki ya Dunia Dkt. Yutaka Yoshino wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maonyesho ya Picha za matukio ya watu wa jamii ya Albino zilizo pigwa katika kambi ya kuwahudumia Albino ya Kabanga.
al3Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabulla (kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Under The Same Sun Bw. Peter Ash, Mwakilishi wa Benki ya Dunia Dkt. Yutaka Yoshino wakipongezana mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maonyesho ya Picha za matukio ya watu wa jamii ya Albino zilizo pigwa katika kambi ya kuwahudumia Albino ya Kabanga.
al4Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabulla (kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Under The Same Sun Bw. Peter Ash, Mwakilishi wa Benki ya Dunia Dkt. Yutaka Yoshino wakifurahia mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maonyesho ya Picha za matukio ya watu wa jamii ya Albino zilizopigwa katika kambi ya kuwahudumia Albino ya Kabanga.

al1 
Mratibu wa Maonyesho ya Picha za Alibino kutoka Makumbusho ya Taifa Bibi. Flora Vicent akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa maonyesho hayo jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yanafanyika kuanzia tarehe 26 Novemba 2015 hadi tarehe 26 Januari 2016

al5 
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu akifuatilia maelekezo ya Picha wakati hafla ya uzinduzi wa mmaonyesho ya picha maonyesho ya Picha za matukio ya watu wa jamii ya Albino zilizopigwa katika kambi ya kuwahudumia Albino ya Kabanga.
al6 
Wakiwa katika picha ya pamoja.

AMANA BANK YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

0
0


Mteja wa muda mrefu wa bemki ya Amana Bw Masoud Khalfan ambaye akizindua wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Main la benki ya Amana jijini Dar ka kukata utepe. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa benki hiyo Dk Muhsin Masoud, Kulia ni mkuu wa idara ya masoko Bw Dassu Mohamed Mussa, kushoto ni mteja wa siku nyingi wa benki hiyo Bw Dossa.

Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Amana wakipata picha ya pamoja.

Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank, Dr. Muhsin Salim Masoud amesema, “Katika kipindi hiki maalum kwa benki yetu, tutashirikiana na wateja wetu wa ndani na wa nje kwa kuwapatia huduma bora zaidi. Tunaamini wateja wetu ndio muhimili wa mafanikio yetu, lengo letu kubwa ni kuwaridhisha wao hivyo tumejidhatiti kuwapa huduma bora muda wote bila kujali mahali walipo. Tunawaahidi wateja wetu huduma za kiwango cha juu kwa ajili ya mahitaji yao ya binafsi au kibiashara muda wote. 




Mkuu wa idara ya masoko Bw Dassu Mussa kushoto akiwa na mkuu wa kitengo cha fedha Bw Fahad Hamid siku ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja.

Benki ya kwanza ya kiislamu Tanzania, Amana Bank imeadhimisha miaka minne tangu kuanza rasmi kutoa huduma zake kwa wateja mnamo 24 Novemba 2011. Wakuu wa idara Mameneja na wafanyakazi siku ya jumatatu wote walikutana na wateja na kuwapatia huduma mbalimbali kupitia matawi yetu yote ya Dar es salaam, Arusha na Mwanza.


Meneja wa tawi la Main Bi Aisha Awadh akimwelekeza kitu mteja wa benki mama Sangawe.

Amana Bank ambayo kwa sasa ina wateja zaidi ya 20,000 na matawi 7 Tanzania nzima, inachukua fursa katika maadhimisho haya kuwashukuru wateja wake wote kwa kuwa wazalendo na kuichagua Amana Bank kama pendekezo lao kwa huduma za kibenki. Amana Bank inaahidi kuendelea kuwekeza na kukuza mtandao wake na kuleta bidhaa na huduma bora Zaidi na za kisasa. Amana Bank mpaka sasa ina matawi saba ambapo manne yapo jijini Dar nayo ni Tandamti, Lumumba, Nyerere na main ambapo ndipo makao makuu ya benki hiyo ya aina yake nchini.


Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Amana wakipata picha ya pamoja.

Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank, Dr. Muhsin Salim Masoud amesema, “Katika kipindi hiki maalum kwa benki yetu, tutashirikiana na wateja wetu wa ndani na wa nje kwa kuwapatia huduma bora zaidi. Tunaamini wateja wetu ndio muhimili wa mafanikio yetu, lengo letu kubwa ni kuwaridhisha wao hivyo tumejidhatiti kuwapa huduma bora muda wote bila kujali mahali walipo. Tunawaahidi wateja wetu huduma za kiwango cha juu kwa ajili ya mahitaji yao ya binafsi au kibiashara muda wote.


Mfanyakazi wa benki ya Amana (Kushoto) akiwahudumia wateja kwa viburudisho katika siku ya wiki ya huduma kwa wateja wiki hii.





Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Amana wakipata picha ya pamoja.

Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank, Dr. Muhsin Salim Masoud amesema, “Katika kipindi hiki maalum kwa benki yetu, tutashirikiana na wateja wetu wa ndani na wa nje kwa kuwapatia huduma bora zaidi. Tunaamini wateja wetu ndio muhimili wa mafanikio yetu, lengo letu kubwa ni kuwaridhisha wao hivyo tumejidhatiti kuwapa huduma bora muda wote bila kujali mahali walipo. Tunawaahidi wateja wetu huduma za kiwango cha juu kwa ajili ya mahitaji yao ya binafsi au kibiashara muda wote.


Mtoa huduma kwa wateja Bi Zainab wa tawi la Mwanza akimhudumia kwa viburudisho mteja wa benki hiyo.




Mteja huyu akijipatia huduma katika tawi la Mwanza



Huduma kwa wateja.

Maadhimisho haya yatahitimishwa ijumaa ya 27/11/2015, kwa hafla ya kuwazawadia wateja na wafanyakazi katika matawi ya Amana Bank ambapo mkurugenzi wa benki hiyo Dk Muhsin Masoud atakuwa katika tawi la jijini Mwanza mjini kukutana na wateja na kupokea maoni na ushauri wa kila aina utakaotolewa na wateja wao.


Baadhi ya wateja wakijipatia huduma katika benki ya Amana tawi la jijni Arusha.

Huduma kwa wateja zikiendelea jijini Arusha.

MAKUNDI YA JAMII ASILIA YA WAHADZABE, WABARABAIG, WAMASAI WAIOMBA SERIKALI YA TANZANIA KUWATAMBUA KAMA JAMII NYINGINE!

0
0
DSC_0928
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Mh. Idd Ramadhan Mapuri (katikati) akizindua taarifa ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu utafiti wa Hali ya Haki za watu wenye kuishi maisha asilia Tanzania. kushoto kwake ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay na (kulia) ni mmoja wa wajumbe walioshiriki kuandaa ripoti hiyo, kutoka nchini Kenya katika taasisi ya ACHPR, Dk. Naomi Kipuri.(Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
DSC_0961
Mtangazaji wa radio Deutsche Welle (DW) ya Ujerumani, George Njogopa akifanya mahojiano na Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay. Kushoto ni Mratibu wa NGONET Ngorongoro, Samweli Nangiria“Jamii zingine zinawatenga watu wa jamii ya Wamasai, tumeshuhudia lugha na matamshi kwenye mizunguko ya watu ikiwemo kwenye madaladala, mitaani huku wakimuona Mmasai kama mtu tofauti, sasa katika ripoti hii imeweza kuelezea mambo mengi sana. Ikiwemo suala la Haki ya kuishi, kufanya kazi na mambo yote kama watu wengine” alimalizia Dk. Naomi.
DSC_0953
Baadhi ya wawakilishi wa Jamii za watu asilia wakiwemo Wahadzabe, Masai, Wabarabaig na wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na wadau wengineo wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo juu ya usawa na kutambulika kama jamii asilia yenye tamaduni na desturi zake.
DSC_0944
Wadau wa haki za binadamu wakiwa katika picha ya pamoja katika mkutano huo baada ya uzinduzi wa ripoti hiyo ya kuwatambua watu wa makundi asilia. Mkutano unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Blue Pearl Ubungo jijini Dar es Salaam.

DSC_2541
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo Mhifadhi Mkuu, kutoka ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Seleman Kisimbo akichangia mada juu ya hali iliyopo sasa ikiwemo jamii hiyo ya watu asilia na changamoto za Mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo suala la ukame inayowakabili katika maisha yao ya vijijini.
DSC_0946
Dk. Naomi Kipuri wa taasisi ya ACHPR, ya nchini Kenya akijadiliana jambo na Mhadhiri wa Sheria Chuo Kikuu cha Tumaini-Makumira, Bw. Elifuraha Laltaika.
DSC_0955
Baadhi ya wawakilishi wa Jamii za watu asilia wakiwemo Wahadzabe, Masai, Wabarabaig na wengineo wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye mkutano huo.




Na Andrew Chale, Modewjiblog
[DAR ES SALAAM-TANZANIA] Jamii ya watu wa asili na makundi yao wameiomba Serikali ya Tanzania kutambua uwepo wao hapa nchini ikiwemo kuwatangaza kwa mema na kuwasaidia kwa misingi ya haki, hutu na kimaendeleo kama watu wengine wanaotambulika ndani na nje ya mipaka yao.

Hayo yameelezwa mapema leo jijini hapa wakati wa uzinduzi wa taarifa ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu utafiti wa Hali ya Haki za watu wenye kuishi maisha asilia Tanzania wakiwemo makabila ya Wa-Akiye,Wa- Hadzabe,Wa- IIparakuyio Masai na wengine wengi.

Akielezea katika uzinduzi huo mmoja wa wajumbe walioandaa taarifa ya Tume hiyo, ambaye anatoka nchini Kenya, katika taasisi ya African Commission on Human and Peoples Rights (ACHPR), Dk. Naomi Kipuri amebainisha kuwa jamii ya watu asilia wamekuwa na kilio cha muda mrefu cha kutaka kupata haki zao zao msingi na kutambulika zaidi.

“Utafiti tuliofanya jamii ya watu asilia wamekuwa katika malalamiko ya muda mrefu ikiwemo kutaka haki zao za msingi. Ikiwemo masuala ya elimu, makazi na haki zingine. Pia wameomba Serikali kuwatangaza watu hawa wa asilia ili wasionekane wageni kwani jamii nyingi bado hazijawatambua na hata kupelekea kuwavunjia hutu wao” alieleza Dk. Naomi.
Aidha, Dk. Naomi katika uwakilishi wake wa mada kwenye mkutano huo amelezea namna ya jamii inavyoendelea kuwaona watu hao ni tofauti kiasi cha kupelekea watu hao kudumaa na maisha yale yale ya asilia.

“Sie watu asilia tuna mahusiano mbalimbali na jamii zetu za kifugaji licha ya jamii zingine kutuingilia kwenye maeneo yetu na kupora ardhi yetu. Watu asilia tunahitajika kutambulika zaidi na hata kupatiwa huduma muhimu ikiwemo kujengewa shule, vyuo na mahitaji mengine ikiwemo haki na hutu kama watu wengine.” Alieleza Samweli Nangiria.

Kwa upande wake, .. ameweza kuipongeza tume ya Haki za Binadamu kwa kuweza kushughulikia suala hilo na hata kuandaa tukio hilo kwa kushirikisha wadau wengine wakiemo wao wa asilia.“Tanzania ndio nchi ya kwanza kuaandaa kikao cha Afrika kwa watu hawa wa makundi maalum wa asilia, kilichofanyika mwaka uliopita. Hili ni jambo bora sana kwani watu asilia tunaendelea kutambulika zaidi.

Ripoti hiyo iliyozinduliwa ya taarifa ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu utafiti wa Hali ya Haki za watu wenye kuishi maisha asilia Tanzania, imeweza kuangalia mambo mbalimbali ikiwemo suala la haki ya kuishi, Utawala bora na namna ya jamii hizo zinapotokea katika maeneo yao hapa nchini.

 Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Mh. Idd Ramadhan Mapuri ameeleza kuwa kupitia ofisi yake itahakikisha inashughulikia suala hilo la kuwa karibu na watu asilia na kutambua misingi ya haki zao ambapo amebainisha watu hao wa asilia kwa Tanzania wanafikia makundi zaidi ya sita.Kwa upande wao baadhi ya wawakilishi wa watu hao wa watu asilia wakielezea katika mkutano huo, waliomba na wao na wapate wawakilishi maalum ikiwemo Bungeni ama sehemu za maamuzi ikiwemo Halmashauri na maeneo mengine ya Serikali ilikutambua michakato ya Kimaendeleo kwa kina. 

 “Jambo la ardhi, ndilo linalotuumiza kwa sasa. Sie tunaporwa ardhi yetu kila siku na kesi nyingi ni za kuporwa ardhi na migogoro ya wakulima na wafugaji, ndani ya migogoro hii ina siri kubwa bila kujua kiini chake ni wakati wa kufika kule na kupata ukweli zaidi” alielezea Adam Ole MwarabuKwa upande wake, Mratibu wa NGONET Ngorongoro, Samweli Nangiria ambaye anawakilisha watu hao asilia anaeleza kuwa, wao wamekuwa wakitambuana kwa desturi ikiwemo suala la ufugaji na maisha mengine, Jamii nyingine imekuwa wakiwaona wao ni watu wa tofauti kiasi cha kupora mali zao ikiwemo ardhi, mifugo na mambo mengine ya msingi.




DC AAGIZA MUUGUZI ALIYEKAMATWA KWA WIZI WA DAWA SHINYANGA ASIMAMISHWE KAZI MARA MOJA,

0
0
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amefanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha afya Kambarage mjini Shinyanga ili kujionea hali halisi jinsi huduma zinavyotolewa kwa wananchi siku moja tu baada ya muuguzi wa kituo hicho kukamatwa kwa tuhuma ya kuiba dawa za serikali.Pichani ni mkuu wa wilaya Josephine Matiro na katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga wakiwa katika chumba cha kuhifadhia dawa wakiwa wamepigwa butwaa baada ya kuona chumba kimesheheni dawa wakati mara kwa mara wananchi wamekuwa wakiambiwa hakuna dawa badala yake wanaambiwa wakanunue kwenye maduka ya watu binafsi mtaani-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog . Hapa ni ndani ya ofisi ya mganga mkuu/msimamizi wa kituo hicho ambapo mkuu wa wilaya akiwa ameambatana na maafisa wengine wa manispaa ya Shinyanga amekutana na uongozi wa kituo hicho pamoja na wananchi waliomkamata muuguzi mkunga wa kituo hicho Joseph Nkila akituhumiwa kuiba dawa za serikali.Kulia ni Rashid Shaban akimweleza mkuu huyo wa wilaya jinsi walivyofanikisha kufichua wizi huo Wa pili kutoka kulia ni msimamizi wa kituo cha afya Kambarage Dkt Nassoro Yahya akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga kuhusu suala la upungufu wa dawa katika kituo chake ambapo alisema kituo kina upungufu wa dawa na walishatoa taarifa panapohusika siku nyingi zilizopita.Hata hivyo maelezo yake yalipingana na yale ya kaimu mganga mkuu wa manispaa ya Shinyanga Dkt Mhana Raphael(mwenye suti pichani) aliyedai kuwa mkoa wa Shinyanga hauna tatizo la upungufu wa dawa bali dawa pekee ambayo haipo ni ile ya Antibiotic Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika kituo cha afya cha Kambarage mjini Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine amemwagiza mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga kumsimamisha kazi muuguzi Joseph Nkila anayetuhumiwa kuiba dawa za serikali pamoja na msimamizi wa kituo hicho Dkt Nassoro Yahya kwa uzembe unaosababisha mwanya wa upotevu wa dawa katika kituo hicho na kusababisha wananchi kuilalamikia serikali kwa kukosa dawa wakati mkoa wa Shinyanga hauna tatizo la dawa Mfamasia/mtunza dawa wa kituo cha afya Kambarage Seleman Hamza akitoa maelezo namna anavyofanya kazi katika kituo hicho ambayo hata hivyo mkuu wa wilaya hakuridhika nayo na kumwagiza yeye na msimamizi wa kituo waandae maelezo ya kina ndani ya siku 5 Mmoja wa wasamaria wema waliomkamata muuguzi anayedaiwa kuiba dawa akisimulia jinsi wizi wa dawa unavyofanyika katika kituo hicho na jinsi walivyomkamata Joseph Nkila.Soma hapa Maelezo yake na wenzake Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akiwa katika kituo cha afya Kambarage,nyuma yake ni katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi na kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Sande Deogratius Dawa zikiwa katika chumba cha kuhifadhia dawa cha Kituo Mfamasia/mtunza dawa wa kituo cha afya Kambarage Seleman Hamza akizungumzia kuhusu tukio la wizi wa dawa katika kituo hicho na changamoto ya dawa katika kituo hicho ambapo alisisitiza kuwa kuna baadhi ya dawa hazipo katika kituo hicho Dawa zikiwa katika chumba cha kuhifadhia dawa kituo cha afya Kambarage Dawa katika kituo cha afya Kambarage Mkuu wa wilaya Josephine Matiro na katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi wakiwa katika chumba cha kuhifadhia dawa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoka kwenye kituo cha afya Kambarage Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa maelekezo kwa kaimu mganga mkuu wa manispaa ya Shinyanga Dkt Mhana Raphael(mwenye suti),kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Sande Deogratius na mfamasia wa manispaa ya Shinyanga Emmanuel Zabron Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akimpa maelekezo kaimu mganga mkuu wa manispaa ya Shinyanga Dkt Mhana-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog ******** Hapa Kazi tu ndiyo Tunaweza Kusema!! Novemba 26,2015 asubuhi..Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro anafanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha afya cha Kambarage katika manispaa ya Shinyanga ili kujionea hali halisi ya huduma zinazoendelea katika kituo hicho. 
 
Kubwa zaidi lililomfikisha hapo asubuhi asubuhi ni kuhusu sakata la muuguzi wa kituo hicho Joseph Nkina kukamatwa na wananchi akiwa na dawa za serikali ikiwemo kopo moja la dawa aina ya paracetamol na chupa mbili za dawa ya maji aina ya Erythromycin kinyume na utaratibu. 
 
Baada ya kukutana na uongozi wa kituo hicho na wananchi waliofanikisha kukamatwa kwa muuguzi mkunga wa kituo hicho Joseph Nkila amemwagiza mkurugenzi wa manispaa hiyo kumsimamisha kazi muuguzi huyo kuanzia leo Novemba 26,2015, ili kupisha uchunguzi wa tukio hilo. 
 
“Nimekuja hapa kuona uhalisia wa jambo hili,Kuna ushihidi wa wazi kabisa kuwa muuguzi huyu kweli kaiba dawa za serikali,mbaya zaidi akataka kudanganya kwa kuchukua stakabadhi kutoka kwenye duka la dawa za binadamu (pharmacy), nimekutana na msimamizi wa kituo cha afya Kambarage na mfamasia anayetunza dawa,na kinachoonekana hapa ni uzembe kwenye uongozi kwani dawa zinatoka bila kufuatiliwa kuwa dawa hizo zinafanya nini”,amefafanua Matiro. 
 
“Nitamshangaa sana hakimu atayepindisha kesi hii kwani ushahidi uko wazi kabisa kutoka kwa wananchi kwamba amekuwa akijihusisha na wizi kwa muda mrefu na kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu katika kituo hiki cha afya,wananchi wananyimwa dawa,kumbe watu wachache tu wanacheza mchezo huu mchafu wa kuiba dawa”,ameeleza Matiro. 
 
“Kila siku wananchi wanalalamika hakuna dawa,lakini tumeangalia stoo tumekuta dawa zipo za kutosha na Shinyanga hatuna tatizo la dawa,dawa moja tu ambayo ni Antibiotic ndiyo haipo,na tumeagiza iletwe”,alieleza Matiro. “Cha kusikitisha msimamizi wa kituo hiki Dkt Nassoro Yahya anasema hakuna upotevu wa dawa,huyu naye hatakiwi kuwa hapa kazi imemshinda,nimemwagiza mkurugenzi pia amsimamishe kazi kwani haiwezekani dawa zitoke kwenye kituo bila yeye kufahamu”,amesema Matiro. 
 
Katika hatua nyingine Matiro amewashukuru na kuwapongeza wananchi waliofanikisha kumkamata muuguzi huyo na kuahidi kuwapa zawadi kwa kazi nzuri waliyofanya akiwataka wananchi wengine kuendelea kuwafichua watumishi wasiofanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi zao Mkuu huyo wa wilaya ametoa onyo kwa muuguzi aliyekamatwa,ndugu na marafiki kuacha kutoa vitisho kwa wananchi waliokamata dawa hizo na kufanikisha juhudi za kukamatwa kwa muuguzi huyo kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukulia dhidi yao. Na Kadama Malunde- Malunde1 blog SOMA HAPA HABARI YA JINSI MUUGUZI HUYO ALIVYOKAMATWA

Wahamiaji haramu wakamatwa Tabata Segerea

0
0
Na Shamimu Nyaki-Maelezo

Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam limewakamata wahamiaji haramu 105 raia wa Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria wakiwa wanasafirishwa kwenda nchi nyingine za Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam  Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaamu Kamishna Suleiman Kova amesema wahamiaji hao ambao wote ni wanaume wamekamatwa kutokana na ushirikiano wa wasamaria wema wanaoshi eneo hilo la Tabata Segerea.

Ameongeza kuwa wahamiaji hao waliingia nchini ya usimamizi wa mwanamke mmoja anaeitwa Zainabu Umwiza (25) anaesemekana ni raia wa nchi ya Burundi ambae anajihusisha na biashara hiyo ya usafirishaji haramu wa binadamu ambao ni kosa la jinai tayari kuwapeleka nchi nyingine na hivyo amemuomba ajisalimishe.“ Bi Zainabu Umwiza mwenye asili ya Burundi tunamwomba ajisalimishe maana yeye ni mfanyabiashara wa usafirishaji wa binaadamu  kutoka nchi za Afrika kwenda Ulaya” kamanda Kova alisisitiza.

Aidha kamanda Kova ameeleza kuwa polisi walifanya upekuzi katika nyumba ya mwanamke huyo ndipo walipowakuta wahamiaji hao ambapo uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba, usafirishaji wa binadamu kutoka Afrika kwenda bara la Ulaya unaofanywa na mwanamke huyo, ambao hufanyika kwa malipo ya Dolla 1000 kwa mtu mmoja.

Kamanda Kova ameongeza kuwa watuhumiwa hao walipohojiwa kujua kwamba wana kibali chochote cha kuingia nchini waligunduliwa kuwa hawana na kueleza kuwa waliingia kupitia njia za panya na mbinu nyingine ambazo bado zinachunguzwa na kwamba wamewajulisha  idara ya Uhamiaji na watashirikiana nao katika upelelezi ili hatimaye sheria ichukue mkondo wake.

Hata hivyo amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kundoa na kuzuia tatizo la wahamiaji haramu ambao wamekua tishio katika usalama wa maisha ya wananchi na mali zao.
 

Tafrija ya mchapalo wa uzinduzi wa intaneti ya kasi zaidi ya Tigo 4G jijini Tanga yafana

0
0

Mkuu wa kitengo cha biashara (B2B) katika kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Rene Bascope, akihutubia hadhira iliyohudhuria uzinduzi wa mfumo wa intaneti wenye kasi zaidi (4G LTE) uliozinduliwa jana jijini Tanga.
Wadau mbalimabli wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, wakihudumiwa na watoa huduma wa kampuni hiyo sambamba na uzinduzi wa huduma ya intaneti yenye kasi zaidi (4G LTE) uliofanyika jijini Tanga jana.


Mkuu wa wilaya ya Tanga, Abdullah Lutavi akihutubia wakati wa uzinduzi huo.
Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Tanga, Nassor Sisiwaya (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na Meneja Mawasiliano ya Umma wa kampuni ya simu
Wadau mbalimbali wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mfumo wa intaneti wenye kasi zaidi wa 4G LTE, uliozinduliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, jijini Tanga jana.
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Mashariki, Goodluck Charles (wa pili kulia) akimkabidhi zawadi ya simu, James Marwa ambaye aliibuka mshindi wa kwanza wa bahati nasibu iliyochezeshwa jana sambamba na uzinduzi wa intaneti yenye kasi zaidi ya 4G LTE jijini Tanga.

Barua kwa watumishi wa umma

0
0
meiomosi-2013Nawasalimuni nyote katika jina la nchi yetu nzuri Tanzania, Jina ambalo huko nyuma sote tuliliimba “Tazama ramani utaona nchi nzuri, yenye mito na mabonde mengi ya nafaka…nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzaniaaa!” Hakika wimbo huu vijana wengi siku hizi wanashindwa kuuimba, kwa nini? Uzuri wa taifa lao haupo tena, umepotezwa na baadhi yenu watumishi wa umma wasio na uadilifu.

 Sio siri vijana wetu kwa muda mrefu wameshindwa kujivunia taifa lao, wameshindwa kuongea mbele za watu kwa sauti kubwa kwamba wao ni Watanzania, uzuri wa taifa lao na sifa nzuri ya nchi yao imeharibiwa na vitendo kama ufisadi uliokithiri ambao umesababisha wachache katika taifa kunufaika huku wengi wakiteseka. Ndugu zangu watumishi wa umma, Ni kwa kupitia jina la nchi hii ndiyo leo nawaandikieni, kuwakumbusha juu ya wajibu wenu ambao kwa muda mrefu sana umekuwa hautimizwi ipasavyo! 

Kwanza kabisa niseme wazi kwamba nayafahamu mateso yenu, nayafahamu mahangaiko yenu ya maisha magumu, ambayo wakati mwingine yamefanya uaminifu wenu kutikiswa. Pamoja na hayo yote nasema hakuna jambo hata moja linalohalalisha kwenu ninyi kupoteza vigezo vitano muhimu vya utumishi wa umma ambavyo ni; 1.UADILIFU 2.UAMINIFU 3.KUSEMA KWELI DAIMA 4.UZALENDO NA DHAMIRA 5.HOFU YA MUNGU. 

Yeyote kati yenu aliyehalalisha kuondoka kwa vitu vitano nilivyovitaja hapo juu kwa sababu ya aidha kipato kidogo anachokipata serikalini, akavunjika moyo na kuacha kuwatumikia wananchi, ama akachagua kuendeleza rushwa na kukosa uzalendo, huyu hatufai kuwa mtumishi wa umma. Kwa muda mrefu mmekuwa mkilalamikiwa, mkinung’unikiwa na wananchi kwa sababu ya utendaji mbovu unaosababishwa na kukosekana kwa mambo matano niliyoyataja hapo juu, kwa kweli ilionekana kana kwamba uadilifu katika taifa hili hauwezekani tena, vivyo hivyo uaminifu, kusema kweli, uzalendo na hofu ya Mungu vilitoweka.


 Uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, 2015 na kumwingiza madarakani rais ambaye hawezi kumaliza hotuba yake bila kusema “TUNAMTANGULIZA MUNGU MBELE” Dk. John Pombe Joseph Magufuli umerejesha tena imani ya Watanzania kwamba, kumbe utumishi wa umma uliotukuka unawezekana, yote haya yamefanyika ndani ya siku chini ya arobaini tangu aingie madarakani! Kwa matendo yake hayo, nimesikia kwa masikio yangu watu waliompinga Rais Dk. Magufuli wakati wa kampeni wakijuta na kusema: 

“Laiti ningejua ningempa kura yangu!” haya yanatokea ndani ya siku chini ya hamsini tangu rais huyu aingie madarakani, upepo umebadilika, utumishi wa umma uliowekwa madarakani na watu kwa ajili ya watu kumbe unawezekana. Ule msemo wa wazungu usemao “Once you shake the top, you have shaken the bottom” yaani ukishatikisa juu, tayari utakuwa umetikisa na chini, sasa umedhihirika kwamba ni kweli. Tanzania inakimbia mbio, kuanzia serikalini mpaka kwenye sekta binafsi, adui uvivu ameanza kupotea kwa sababu tu raia aliyeingia madarakani sio mvivu. 

Kwa mara ya kwanza maishani mwangu nimeanza kusikiliza taarifa za habari na kusikia habari za kamatakamata, fukuzafukuza, kila kona ya nchi. kila kiongozi, kila mtendaji sasa anajaribu kutimiza wajibu wake, yote haya kwa sababu amebadilishwa mtu mmoja tu juu ambaye kauli mbio yake ni “HAPA KAZI TU!” Ndugu zangu Watumishi wa Umma, Nawaandikieni barua hii kuwakumbusha kwamba ile kauli yenu ya kusema “huu ni moto wa mabua” naomba muiache, anayesema hivyo hamfahamu vizuri rais wetu, kwa wanaomfahamu hawawezi hata siku moja kutoa kauli hiyo, haigizi, haya ndiyo maisha yake, ni kama mapafu ambavyo kazi yake ni kupumua, ndiyo ilivyo kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli.

 Ndugu zangu, Nawasihi mfanye kazi, timizeni wajibu wenu mliopangiwa kwa faida ya taifa hili, ambaye hatayasikia maneno haya, hakika ajiandae kukumbuka ninachokisema kwani mfumo utamtema! Ni wakati wa kuchapa kazi, si wa kuchati kwenye mitandao ya jamii saa ya kazi. Tukifanya jambo hili kwa pamoja, ninawahakikishieni taifa letu litasonga mbele kutoka hapa tulipo kwenda tunakotakiwa kwenda, rais wetu ni MUADILIFU, ndivyo itakavyokuwa kwa Makamu wake wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, serikali nzima na hatimaye vijijini, vivyo hivyo katika uchapakazi, kama rais wetu si mvivu, wavivu wote watang’oka, watake wasitake. 

Matarajio yangu ni kwamba kama watumishi wa umma mtatimiza vyema wajibu wenu, mtafanya kazi kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo wa hali ya juu, lazima kipato cha taifa letu kitaongezeka na maisha yenu yataboreshwa na rais huyu huyu tuliyemweka madarakani. Lakini niwasihi msipoteze hali yenu ya kujiamini kwa kusema “Rais ni mkali mno” matokeo yake mkawa ni watu wa kutekeleza mambo kwa nidhamu ya woga, taifa la watu wenye aina hii ya nidhamu, ambao hutekeleza mambo yao kwa kutaka tu kumfurahisha mkuu huwa halisongi mbele, matokeo yake huzaa hata uonevu kwa sababu tu mtu alikuwa anataka aonekane anafanya kazi. 

Sidhani rais wetu ni mtu wa aina hii, bali ni mtu anayependa kufanya kazi na watu wanaojiamini na wachapakazi na atakuwa tayari kujenga jamii ya watu wenye kujiamini si wanaotetemeka ovyo kila wanapokutana naye wakimpa ushauri anaopenda kuusikia, si ule anaotakiwa kuusikia hata kama hautamfurahisha. Nimeyasema haya kwa sababu msipokuwa makini wale mlioko madarakani, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi nk. Mtajikuta mkionea watu au kuwatoa watu sadaka kwa sababu tu mnataka kumfurahisha mkuu au muonekane mnafanya kazi na baadaye kupanda vyeo kwa gharama za maisha ya watu wengine. Sitaki kusema mengi siku ya leo, kwa haya machache niliyoyasema nawatakieni utendaji mwema wa kazi katika Awamu hii ya tano ya HAPA KAZI TU! 

Tendeni kazi zenu kwa kujiamini na uadilifu wa hali ya juu, nawahikikisheni awamu hii ya tano itabadilisha maisha yenu, kama anavyosema mwenyewe Rais Magufuli, tumuombee kwa Mungu atimize ndoto yake yakutufikisha kwenye nchi ya ahadi. Ahsanteni. NUKUU WASALAAM Eric Shigongo James

UCHAGUZI WA MAJIMBO ARUSHA MJINI NA HANDENI MJINI KUFANYIKA DESEMBA 13 2015

0
0





  
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawakumbusha wananchi wote wa majimbo ya Arusha Mjini na Handeni Mjini kuwa Uchaguzi wa Ubunge katika majimbo hayo utafanyika kama ulivyopangwa tarehe 13/12/2015.

Aidha,Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwajulisha Wapiga Kura wa Majimbo hayo kuwa Daftari litakalotumika ni lile lililotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani wa 25 Oktoba,2015.

Hata hivyo,Tume  ya Taifa ya Uchaguzi inawataka Wananchi kupuuza taarifa zilizochapishwa na Gazeti la uhuru Ukurasa wa 5 la tarehe 26/11/2015  lenye kichwa cha habari kuwa “NEC yatakiwa kuingilia kuhujumiwa Daftari.”

Taarifa za kuwepo kwa watu waliojiandikisha zaidi ya  mara moja  na wenye Umri mdogo katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura zilipaswa kutolewa mwezi Agosti 2015 wakati zoezi la  uhakiki wa taarifa za Wapiga Kura.

 Mwezi Septemba 2015,baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki wa taarifa za wapiga kura hapa nchini,Tume ya Taifa ya Uchaguzi kupitia Mkurugenzi wa Uchaguzi ilikabidhi majina ya Wapiga Kura waliobainika kujiandikisha zaidi ya mara moja kwa Jeshi la Polisi ili hatua za kisheria ziweze kuchuliwa dhidi yao.

Kwa hali hiyo,Tume ya Taifa ya Uchaguzi haitegemei kuendelea kuwepo kwa malalamiko ya Wapiga Kura  waliojiandisha zaidi ya Mara moja au wale waliondikishwa wakiwa hawajafikisha umri wa kupiga kura.

Kuhusiana na chaguzi zitakazofanyika,taratibu zitakazotumika katika Chaguzi hizo ni zilezile zilizotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba25, 2015 ambapo Wasimamizi wa Uchaguzi watakaotumika ni wale waliokuwepo wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Vilevile Daftari la Kudumu la Wapiga Kura litatumika lile  lililotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu Oktoba 25,2015. Vituo vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni. Pia Wananchi Wanakumbushwa kuwa watakaopiga Kura ni wale tu walio kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Majina yao kuwamo kituoni na kila Mpiga kura atatakiwa kwenda na Kadi yake ya kupigia Kura.

Tume pia inawakumbusha Wagombea wa Vyama vya Siasa na Mawakala kuzingatia Sheria,Kanuni na taratibu za Uchaguzi ikiwamo kutofanya Kampeni siku ya Uchaguzi.
Ni matarajio ya Tume kuwa  watajitokeza kwa wingi katika Vituo vya kupigia Kura na kuwachagua Wabunge  wao.
 
Jaji Mstaafu Damian Z. Lubuva
MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images