Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 694 | 695 | (Page 696) | 697 | 698 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim, Selemani Ponda (katikati) akiongea na waandishi wa habari kutangaza uuzaji wa dhamana ya kwanza ya muda mrefu nchini Tanzania yenye kuwezesha ushiriki wa wawekezaji wadogo ili kupata kiasi cha shilingi bilioni 15. Ameambatana naMeneja Benki ya Exim (uwekezaji), George Assenga (kulia), Meneja Miradi na Biashara wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, Patrick Mususa (wa pili kulia),  Mkurugenzi Mkuu wa Core Securities, George Fumbuka (wa pili kushoto) ambao ndio wenye dhamana ya uuzaji wa dhamana hizo na Mkuu wa matawi ya benki ya Exim, Agnes Kaganda.
   Mkurugenzi Mkuu wa Core Securities, George Fumbuka (wa pili kushoto) akiongea na waandishi wa habari kutangaza uuzaji wa dhamana ya kwanza ya muda mrefu ya benki ya Exim nchini Tanzania yenye kuwezesha ushiriki wa wawekezaji wadogo ili kupata kiasi cha shilingi bilioni 15. Ameambatana naMeneja Miradi na Biashara wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, Patrick Mususa (kulia),  Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim, Selemani Ponda (wa pili kulia) na Mkuu wa matawi ya benki ya Exim, Agnes Kaganda.


  Benki ya EximTanzaniaimetangaza uuzaji wa dhamana ya kwanza ya muda mrefu nchini Tanzania yenye kuwezesha ushiriki wa wawekezaji wadogo ili kupata kiasi cha shilingi bilioni 15. Benki imepanga kukusanya kiasi icho kwa ajili ya kuwekeza katika shughuli mbalimbali za ukuaji wa benki.

  Hiini dhamana ya aina yake na ya kwanza kutolewa nchini Tanzania inayowawezesha wawekezaji wenye kiasi kuanzia shilingi milioni moja kuwekeza kwenye dhamana zitakazoorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.

  Dhamana hii itawapa wawekezaji uhakika wa kupata riba ya 14% kwa mwaka isiyokuwa na makato ya kodi, itakayolipwa kila baada ya miezi 6 kwa kipindi cha miaka6. Zaidi ya hayo,Wawekezajiwanaweza kutumia dhamana zao kwa ajili ya kuombea mikopo yoyote kwa kuzingatia taratibu zilizoko katika soko la Hisa la Dar es Salaam.

  "Dhamana ya muda mrefu inayotolewa na benki ya Exim inawapatia wawekezaji wadogo na wa kati wasiokuwa na fursa za uwekezaji sawa na wawekezaji wakubwa, nafasi ya kipekee kupata gawio lisilo na kodi la asilimia 14 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka sita", Alieleza Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki hiyo,Bw. Selemani Ponda, wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana.


  "Kama ilivyo kwa mipango yetu mingi tuliyokwisha ianzisha, utoaji huu wa dhamana kwa umma unadhihirisha uvumbuzi waBenki ya Eximkatika kuendelezasoko la uwekezaji katika dhamana nchini Tanzania ili kuwezesha watanzania wote kupata huduma za kifedha,'' alisema

  "Tunayofuraha kubwa kuzindua dhamana ya kwanza ya muda mrefu kwa wawekezaji nchini Tanzania. Nina hakika kwambadhamana hii itawavutiawawekezaji wadogo, ikiwa na marejesho mazuri, uwezo wa kuuzwa katika soko la hisa la Dar es Salaam na kuweza kuitumia kama dhamana ya kupata mikopo kutoka taasisi mbalimbali huku ikitoa fursa adhimu ya kushiriki kama mdau katikaukuaji wa moja ya benki tano zinazoongoza nchini Tanzania," alisema Bw.Ponda.

  Kwa kiwango cha chini cha shilingi Milioni 1, riba ya 14%  isiyokuwa na makato ya kodi ni ya  ushindani sana ukilinganisha na  kiwango cha wastani wa 8% kwa mwaka kinachotolewa na taasisi nyingi, kwa mujibu wa Bw. Ponda.

  Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Core Securities, ambayo ndio yenye dhamana ya uuzaji wa dhamana hizo, Bw. George Fumbuka, alisema mauzo yataanza kufanyika tarehe 23 Novemba, 2015 na kufungwa tarehe 18 Disemba mwaka huu.

  “Katika kuhakikisha ushiriki wa wawekezaji wadogo ambao baadhi hawana akaunti za benki, Maombi ya ununuzi yanaweza kufanywa kupitia simu za mkononi kwa kupiga *150*36#, pia kupitia mawakala waliochaguliwa au katika matawi yote ya benki ya Exim yaliyosambaa nchi nzima. Kiwango cha chini katika uuzaji huu wa umma ni shilingi milioni moja,” alibainisha.

  Bw. Fumbuka alisema wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika dhamana hizo wanaweza kupata fomu za maombi na taarifa muhimu za uwekezaji katika matawi yote ya Benki ya Exim na mawakala waliochaguliwa.

  Bw. Fumbuka alibainisha kuwa kampuni yake kama wauzaji wakuu, iko tayari kuuza na kununua dhamana kutoka kwa wawekezaji muda wowote.


  0 0

  CH1
  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA), Bw. Dickson Mveyange (kulia) akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu tathmini ya ushiriki wa Viziwi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Taifa Tanzania Bara uliofanyika 25 Oktoba, 2015. Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Jijini Dar es Salaam 24 Novemba, 2015.
  CHA2
  Baadhi ya Waandishi wa Habari toka Vyombo mbalimbali wakifuatilia taarifa toka kwa Viongozi wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) kuhusu tathmini ya ushiriki wa Viziwi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Taifa Tanzania Bara uliofanyika 25 Oktoba, 2015. Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Jijini Dar es Salaam 24 Novemba, 2015.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO)
  ……………………………………………………………………………………………………..
  Na Zawadi Msalla
   
  Chama Cha Viziwi Tanzania (CHAVITA)   kimeeleza masikitiko yao juu ya ushiriki mbovu wa Viziwi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba  kote nchini.
   
  Akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Habari-MAELEZO leo Mshauri Mwelekezi wa Elimu ya Uraia kwa Watu wenye Ulemavu Bw. Novat Rukwago amesema kuwa, licha ya jitihada mbalimbali ambazo walijaribu kuzifanya ili kuhakikisha viziwi kote nchini wanapata haki yao ya msingi na ya kikatiba ya kupiga kura bado ushiriki wao haukuridhisha.
   
  Rukwago alizitaja changamoto mbalimbali zilizo jitokeza katika uchaguzi  huo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa wataalamu wa lugha za alama zinazotumiwa na viziwi katika kampeni mbalimbali za Vyama vya Siasa, hivyo sera na Ilani za vyama hivyo hazikuweza kujulikana kwa viziwi.“Vyama vingi vilisema ni suala la rasilimali na ukosefu wa fedha za kuweka wataalamu hao, ingawa tuonavyo sisi ni kwamba walishindwa kutoa kipaumbele na si suala la fedha,” alisema Rukwago.
   
  Aidha, Rukwago alisema CHAVITA kwa juhudi binafsi waliweza kutembea jumla ya mikoa 17 kote nchini na kufanikiwa kutoa elimu kwa baadhi ya viziwi ambapo jumla ya viziwi 2516 walijiandikisha, idadi hiyo ikiwa na wanaume 1256 na wanawake 1260. Waliopiga kura walikuwa ni 1807.
   
  Aliongeza kwa kusema kuwa licha ya changamoto hizo pia mazingira ya kupigia kura hayakuwa rafiki kwa watu wenye uhitaji maalumu kwani hakukuwa na wataalamu wa lugha za alama  katika vituo vya kupigia kura.
   
  Waliiomba Serikali kuzingatia umuhimu wa kuyapa kipaumbele makundi mbalimbali yenye uhitaji kwa chaguzi zijazo na kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufanya mawasiliano na vyama vya watu wenye uhitaji maalum mapema ili kuweza kushirikiana katika kuondoa changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi wa mwaka huu.

  0 0

  JAL1 
  Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI) , Jumanne Sajini baada ya kuwasili kwenye Ofisi ndogo ya TAMISEMI jijini Dar es salaam kuzungumza na watumishi Novemba 24, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  JAL2 
  Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya Wakurugenzi baada ya kuwasili kwenye Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) jijini Dar es salaam kuzungumza na wafanyakazi Novemba 24, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  JAL4 
  Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akizungumza na baadhi ya watumishi wa Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) jijini Dar es salaam Novemba 24, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  JAL6 
  Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) jijini Dar es slaam baada ya kuzungumza nao Novemba 24, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum AMJAD akisalimiana na wapiga kura wake waliofika uwanja wa ndege kumpokea baadha ya kuhudhuria hafla ya kuapishwa kuwa Mbunge wao. 
  Wananchi wa Jimbo la Cumbuni Zanzibar wakimlaki Mbunge wao wakati akiwasili Zanzibar akitokea Dodoma kuhudhuria sherehe za kuapishwa zilizofanyika wiki iliopita Mjini Dodoma. 
  Viongozi wa CCM Jimbo la Chumbuni wakimlaki Mbunge wao alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akitokea Dodoma kuhudhuria sherehe za kuapishwa zilizofanyika wiki iliopita Mjini Dodoma.
  Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe, Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwasili Uwanja wa Ndege wa Kima taifa wa Abeid Amani Karume akitokea Dodoma kuhudhuria hafla ya kuapishwa iliofanyika wiki iliopita. 
  Mhe Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akitabasamu wakati akiwasili uwanja wa ndege wa Zanzibar akitokea Bungeni Dodoma.na kupokelewa na Wananchi wa Jimbo lake. 

  Mhe Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akipongezwa na Mke wakati alipofika kumpokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akitokea Dodoma kuhudhuria hafla ya kuapishwa wiki iliopita.
  Mbunge wa Jimbo la VChumbuni Zanzibar akiwa na Mgombea Uwakilishi wa Jimbo hilo Miraji akimpongeza baada ya kuwasili Zanzibar akitokea Bungeni Dodoma kuhudhuria hafla ya kuapishwa  iliofanyika wiki iliopita.
   
  Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwa na Viongozi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar waliofika kumpokea uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar akitokea Mjini Dodoma kuhudhuria sherehe za kuapishwa wiki iliopita.Imetayarishwa na OthmanMapara,Blogspot.
  Zanzinews.com

  0 0

  MWENYEKITI wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Yahya Mohamed leo amefungua semina ya mafunzo ya leseni za vilabu katika ukumbi wa mikutano wa Dar es salaam International Conference Centre (DICC) uliopo jijini Dar es salaam.

  Akiongea na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Yahya amesema imekua jambo jema kwa CAF kutupatia nafasi ya mafunzo ya leseni za vilabu hapa nyumbani, kwani viongozi wa vilabu wote wanapata nafasi ya kushiriki semina hii ya siku mbili kutoka kwa wakufunzui wa CAF.

  “Uendeshaji wa mpira wa miguu duniani umebadilika, mabadiliko haya yapo katika nyanja zote za uongozi (utawala), miundombinu, kitu ambacho kwa sisi Tanania tumeshaanza kuendana na mabadiliko hayo, na sasa kupata kwetu semina hii kutawafanya viongozi wengi kufahamu umuhimu wa leseni za vilabu na kufanyia kazi mapungufu yaliyokuwepo” alisema Yahya.

  Semina hiyo ya Leseni kwa Vilabu itakayofanyika kwa siku mbili inaedeshwa na wakufunzi watatu kutoka CAF ambao ni Dr. Bolaji Ojo Oba (Nigeria), Amanze Uchegbulanm (Nigeria) na Othman Mohamed kutoka nchini Sudan.

  Agizo la CAF ni kuwa kila klabu inayoshiriki michuano ya kimataifa (Ligi ya Mabingwa, Kombe l Shirikisho) lazima iwe imepata leseni hiyo ambayo itaipa nafasi ya kushiriki michuano inayoandaliwa na CAF, na kwa klabu ambayo haitatimiza mahitaji ya kupata leseni hiyo haitaweza kushiriki michuano ya kimataifa.

  Ili kupata leseni ya klabu, klabu inapaswa kutimiza vigezo vilvyowekwa ikiwemo masuala ya utawala, ripoti ya mapato na matumizi iliyokaguliwa, uwanja wa mazoezi nk.

  Mmiliki mmoja wa klabu hatarusiwa kumiliki timu zaidi ya moja kwenye ligi moja, kila klabu lazima iwe na program za vijana na uwanja wa mazoezi.

  0 0

  MWIMBAJI maarufu wa muziki wa Injili Tanzania, Upendo Nkone naye amejitokeza kuwa mmoja wa waimbaji watakaofikisha ujumbe wa Shukrani kwa Mungu katika Sikukuu ya Krismasi kupitia tamasha linalotarajia kufanyika Desemba 25 mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama Kamati imefanikisha makubaliano na mwimbaji huyo.Msama alisema Nkone anaungana na wenzake Rose Muhando, Ephraim Sekeleti sambamba na Kwaya ya Wakorintho wa pili.

  "Kabla ya kukubaliana na Nkone, tulikuwa tumeshamalizana na wenzake Rose Muhando, Ephraim Sekeleti ambaye ni raia wa Zambia sambamba na Kwaya ya Wakorintho wa Pili yenye maskani yake Mafinga mkoani Iringa, bado tunaendelea na mawasiliano na waimbaji wengine ili kunogesha tamasha hilo lenye malengo mawili ambayo ni Shukrani kwa Mungu sambamba na Sherehe za kuzaliwa Masiha, Yesu Kristo," alisema Msama.

  Aidha Msama alisema Kamati yake imepanga kufikisha shukrani kwa Mungu kupitia waimbaji na viongozi wa dini na wa kada mbalimbali kama ilivyokuwa kwenye Tamasha la Kuombea Amani lililofanyika Oktoba 4 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambako mgeni rasmi alikuwa ni mke wa rais wa awamu ya nne, Salma Kikwete.

  "Oktoba 4, tuliandaa Tamasha la kumbea amani uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 uwanja wa Taifa, hivyo ni nafasi yetu kumshukuru Mungu baaada ya kupitisha Tanzania kwenye uchaguzi ambao ulikuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani," alisema Msama.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA), Bw. Dickson Mveyange (kulia) akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu tathmini ya ushiriki wa Viziwi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Taifa Tanzania Bara uliofanyika 25 Oktoba, 2015. Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Jijini Dar es Salaam 24 Novemba, 2015. 
  Mshauri Mwelekezi Elimu ya Uraia kwa Watu wenye Viziwi, Bw. Novath Rukwago (Kushoto) akijibu baadhi ya maswali toka kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu ushiriki wa Viziwi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Taifa Tanzania Bara uliofanyika 25 Oktoba, 2015. Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Jijini Dar es Salaam 24 Novemba, 2015.
  Baadhi ya Waandishi wa Habari toka Vyombo mbalimbali wakifuatilia taarifa toka kwa Viongozi wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) kuhusu tathmini ya ushiriki wa Viziwi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Taifa Tanzania Bara uliofanyika 25 Oktoba, 2015. Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Jijini Dar es Salaam 24 Novemba, 2015.
  (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO).

  Na Zawadi Msalla
  CHAMA Cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) kimeeleza masikitiko yao juu ya ushiriki mbovu wa Viziwi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba kote nchini.

  Akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Habari-MAELEZO leo mshauri mwelekezi wa elimu ya uraia kwa watu wenye ulemavu Novat Rukwago amesema licha ya jitihada mbalimbali ambazo walijaribu kuzifanya ili kuhakikisha viziwi kote nchini wanapata haki yao ya msingi na ya kikatiba ya kupiga kura bado ushiriki wao haukuridhisha.

  Rukwago alizitaja changamoto mbalimbali zilizo jitokeza katika uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa wataalamu wa lugha za alama zinazotumiwa na viziwi katika kampeni mbalimbali za Vyama vya Siasa, hivyo sera na Ilani za vyama hivyo hazikuweza kujulikana kwa viziwi.

  “Vyama vingi vilisema ni suala la rasilimali na ukosefu wa fedha za kuweka wataalamu hao, ingawa tuonavyo sisi ni kwamba walishindwa kutoa kipaumbele na si suala la fedha,” alisema Rukwago.

  Aidha, Rukwago alisema CHAVITA kwa juhudi binafsi waliweza kutembea jumla ya mikoa 17 kote nchini na kufanikiwa kutoa elimu kwa baadhi ya viziwi ambapo jumla ya viziwi 2516 walijiandikisha, idadi hiyo ikiwa na wanaume 1256 na wanawake 1260. Waliopiga kura walikuwa ni 1807.


  Aliongeza kwa kusema kuwa licha ya changamoto hizo pia mazingira ya kupigia kura hayakuwa rafiki kwa watu wenye uhitaji maalumu kwani hakukuwa na wataalamu wa lugha za alama katika vituo vya kupigia kura.

  Waliiomba Serikali kuzingatia umuhimu wa kuyapa kipaumbele makundi mbalimbali yenye uhitaji kwa chaguzi zijazo na kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufanya mawasiliano na vyama vya watu wenye uhitaji maalum mapema ili kuweza kushirikiana katika kuondoa changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi wa mwaka huu.

  0 0

  MAFUNDI kutoka kampuni ya Philips wanaendelea na matengenezo ya mashine za MRI na CT-SCAN katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili zilizopata hitilafu za kiufundi hivi karibuni.

  Akizungumza ofisini kwake leo hii Mkuu wa Idara ya Uhusiano Hospitali ya Taifa Muhimbili Bw. Aminiel Buberwa Aligaesha amesema mafundi wapo katika eneo la kazi wakitengeneza hizo mashine ili ziweze kurudi katika hali yake ya kawaida.

  “Tumepewa siku tatu kukamilisha ukarabati wa hizi mashine hivyo wananchi wawe na subira kwani mashine zikiwa tayari kwa matumizi tutatoa  taarifa” alisema Aligaesha.

  Ameongeza kuwa wananchi wawape muda waweze kuzitengeneza mashine hizo ili ziweze kutengemaa kwa ajili ya kutoa huduma za MRI na CT-SCAN hospitalini hapo.

  Mashine za MRI na CT-SCAN zilianza kufanya kazi  mara baada ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Joseph Magufuli kutembelea hospitali hiyo hivi karibuni na kuagiza kutengenezwa kwa mashine hizo na baadae kufanya kazi kwa muda wa siku kadhaa na kuharibika tena kutoka na hitilafu za kiufundi.

  Wakati alipotembelea Hospital ya Taifa ya Muhimbili jana Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue aliagiza mashine hizo kutengenezwa,  ndani ya siku tatu  ziwe zimekamilika kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.

  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imekuwa ni kimbilio la wananchi wengi kupata huduma za afya hivyo serikali inapamabana kwa kila hali kuhakikisha huduma za MRI na CT-SCAN zinarudi katika hali yake ya kawaida hospitalini hapo.

  0 0

       
  • Ni kupitia huduma yake ya M-Pesa
  • Sasa wateja wa Qatar kununua tiketi za kusafiri kupitia huduma hiyo

  SHIRIKA la Ndege la Qatar– Qatar Airways limeingia ubia na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kupitia huduma yake ya M-pesa kwa ajili ya kuwawezesha wateja wake kulipia tiketi zao ikiwa ni njia pekee ya kuwarahisishia wateja wao kutumia huduma hiyo kwa njia ya haraka na rahisi kwa kuwawezesha wateja wake kufanya malipo kwa njia ya simu za mkononi.

  Huduma hii inarahisisha maisha kwa wateja wanaotaka kusafiri na shirika la Qatar na wateja wa Vodacom ambapo kwa sasa hivi wanaweza kununua tiketi kupitia njia ya mtandao kupitia tovuti ya www.qatarairways.com/tz au kutembelea ofisi za shirika hilo na kulipia tiketi zao za usafiri kwa M-Pesa.

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania, Nina Pendaeli Eshum (Pichani) amesema “Tunayo furaha kubwa kuona familia ya watumiaji wa M-Pesa inazidi kuongezeka ambapo Shirika kubwa la Qatar limejiunga nasi katika huduma hii.Lengo letu siku zote ni kutoa huduma zinazoenda sambamba na mahitaji ya wateja wetu na ndio maana kupitia huduma hii tumewarahisishia maisha wateja wetu ambao wanataka kusafiri kwa kutumia ndege za shirika la Qatar kununua tiketi kwa rahisi kupitia simu zao za mkononi”.

  Eshun aliongeza kuwa huduma hii ambayo inaongoza kuwa na watumiaji wengi nchini katika kufanya mihamala ya kifedha na malipo itazidi kuboreshwa siku hadi siku ili iendane na mahitaji yao wateja na mitindo yao ya maisha katika kuwarahisishia shughuli zao kupita simu za mkononi.

  Kwa upande wake Meneja wa Shirika la ndege la Qatar nchini Tanzania,Basel Haydar alisema “ Kujiunga kwetu na huduma hii ni kwa ajili ya kuwawezesha wateja wetu kuwa na njia mbalimbali za kufanya malipo kwa ajili ya kupata huduma zetu ambapo hivi sasa wanaweza kutumia huduma hii ya M-Pesa ambayo ni moja ya njia ya kufanya mihamala ya malipo kwa urahisi bila usumbufu wowote”.

  Alisema hivi sasa shirika hilo linatoa ofa mbalimbali kwa wateja wake na limejipanga kwa kuendelea kutoa huduma bora zinazokidhi mahitaji ya wateja katika soko la ushindani.


  Huduma ya M-Pesa ambayo inatumiwa na watu wengi duniani imeweza kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya fedha na kurahisisha maisha ya watu wengi.Ili kulipia huduma ya tiketi za usafiri kutoka Shirika la Qatar kinachotakiwa kufanyika ni kujiunga na menu ya M-Pesa kwenye simu ya mteja katika sehemu ya kufanya mihamala ya malipo ambapo atatakiwa kuandika namba 331199 ambayo ni namba ya kufanyia malipo ya shirika hilo, baada ya kuingiza namba hizo atatakiwa kuingiza namba za kumbukumbu ya booking yake na kiasi cha fedha alichotakiwa alipe wakati anashika nafasi ya tiketi (booking).Baada ya kutuma fedha mara moja atapata ujumbe mfupi wa maneno wa kumfahamisha kuwa fedha zake zimepokelewa na atapata tiketi yake kwa njia ya mtandao ambapo pia anaweza kuikuta uwanja wa ndege siku yake ya safari yake.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Uongozi wa Mtandao wa Wanawake Tanzania (WFT) wakati viongozi hao walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Nov 24, 2015 kwa mazungumzo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea baadhi ya Vipeperushi na Vitabu vya Mtandano wa Wanawake Tanzania (WFT) kutoka kwa mwenyekiti wa mtandao huo, Prof.Ruth Meena, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dares Salaam, leo Nov 24, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mtandao wa Wanawake Tanzania (WFT) baada ya mazungumzo yao yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dares Salaam, leo Nov 24, 2015. 
  Picha na OMR

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


  OFISI YA MAKAMU WA RAIS.
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na uongozi wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania (WFT) ambapo amezungumzia dhamira ya serikali katika kuyatafutia ufumbuzi matatizo mbali mbali yanayowakabili wanawake na watoto wa kike nchini.

  Katika mazungumzo hayo Makamu wa Rais aliueleza ujumbe huo kuwa wakati wa kampeni aliahidi pamoja na kazi za kumsaidia Mhe. Rais bado kama mama atafuatilia kwa karibu utekelezaji wa ahadi ya kupatikana kwa maji safi na salama, kuboresha afya ya mama na mtoto, elimu na mazingira.


  “Nilipokuwa kwenye kampeni nimejionea shida ya maji na wanawake ndiyo wanaopata tabu ya kutembea mwendo mrefu kutafuta maji. Kwa hiyo, pamoja na kazi zangu za kumsaidia Mhe. Rais nitasimamia miradi yote ya maji, alau tuhakikishe maji yanapatikana umbali wa mita 400 kutoka eneo wananchi wanakoishi au karibu zaidi”.

  Alisema kinachofurahisha zaidi suala la maji liko kwenye Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) na miradi mingi ikiwemo ya kuchimba visima virefu katika mikoa kama vile ya Singida na Dodoma iko kwenye mchakato na cha msingi ni kusimamia fedha zinatumika kuleta maji kama ilivyokusudiwa.

  Kuhusu afya ya mama na mtoto alisema kazi hiyo ataianza hivi karibuni kwa kushirikiana na Mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotetea haki za wanawake ili kupunguza vifo vinavyosababishwa na mimba za utotoni.

  “Hili tutajitahidi kulipunguza kwa kiasi kikubwa na hasa baada ya serikali ya Awamu ya Nne kusema kwamba shule ya msingi ya lazima ni kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne”, alisema na kuongeza

  “Katika kipindi hicho binti atakuwa amefikisha miaka 17, atakuwa tayari kukabiliana na mambo ya uzazi tofauti na ilivyo sasa ambapo anamaliza darasa la akiwa mdogo na matokeo yake anapata mimba katika umri mdogo. Mtusaidie kupiga debe huko nje utekelezaji uweze kufanikiwa.”

  Hata hivyo, alisisitiza kusimamia suala la kuhakikisha zahanati, vituo vya afya na hospitali nchini zinakuwa na dawa na vifaa tiba vya kutosha katika wodi za wazazi kwa ajili ya kuhudumia akina mama na wananchi kwa ujumla ambao wengi wanaonekana ni watiifu kwa serikali yao.

  Kwa upande wa elimu Mhe. Samia alisema atasimamia ujenzi wa mabweni kwa watoto wa kike na kuhakikisha mazingira yanatunzwa kwa sababu uharibifu wa mazingira ndiyo umekuwa chanzo cha upungufu wa maji nchini.

  Aidha aliuambia ujumbe huo kuwa hivi sasa tuna mpango wa kuimarisha utendaji serikalini kuanzia serikali kuu hadi serikali za mitaa ili kinachopatikana kidogo kimfikie kila mwananchi.

  “Tutaendelea kuaihirisha sherehe ili fedha hizo ziweze kutumika kwa mambo ya kijamii. Kwa msimamo huu amabao Mhe. Rais ameanza nao labda watu wote tushirikiane kwa kutatua matatizo yetu kwa gharama nafuu kwa ufanisi mkubwa.”

  Mapema akizungumza kwa niaba ya wenzake Mwenyekiti wa Mtandao huo Prof Ruth Meena alimpongeza Mhe. Samia kwa kushika nafasi ya juu ya uongozi akiwa mwanamke wa kwanza kuweka historia katika Tanzania.
  Alimweleza Mhe. Makamu wa Rais matarajio yao kwa serikali ya Awamu ya Tano kuwa itatetea misingi ya haki na usawa katika Nyanja zote.

  Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
  Dar es salaam
  24/11/2015.

  0 0

  Na Jovina Bujulu

  Uchafuzi wa mazingira katika vituo vya vivuko , utegaji wa nyavu katika njia za vivuko na kukauka kwa maji na kujaa mchanga kwenye njia za vivuko ni sababu zinazochangia kuharibika kwa vivuko nchini.

  Hayo yamesemwa leo  jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Ukodishaji mitambo na Huduma za Vivuko kutoka  wakala wa Ufundi wa umeme Tanzania Mhandisi Japhet Maselle.

  Aidha, alitaja   sababu za uharibifu wa vivuko hivyo kuwa ni pamoja na baadhi ya abiria kutofuata taratibu za vivuko na wananchi kutumia mitumbwi ambayo si salama kuvukia hasa maeneo ya magogoni Dar es salaam na  Pangani Tanga .

  “Utegaji wa nyavu husababisha kunasa kwenye mifumo ya kuendeshea vivuko, na takataka kuingia kwenye mitambo ya kuendeshea vivuko ambapo  husababisha athari katika mitambo hiyo” alisema ndugu Maselle.

  Katika kukabiliana na matatizo hayo, TAMESA imeendelea kutoa elimu kwa watu wanaochafua mazingira na maeneo ya vivuko kutangaza taratibu za vivuko ndani ya vivuko  na kuboresha huduma za  vivuko na kuongeza maeneo yenye uhitaji.

  Wakala wa ufundi na Umeme Tanzania (TAMESA) ilianzishwa kwa sheria ya wakala namba 30 ya mwaka 1997 ikiwa na lengo la kutoa huduma katika Nyanja za uhandisi mitambo, umeme na uendeshaji wa vivuko .
   
  Kwa sasa kuna vivuko 28 vinavyofanya kazi katika vituo 19 Nchini, baadhi ya vivuko hivyo ni Mv Msungwi,Mv sabasaba, Mv Sengerema,Mv mwanza, Mv ukara , Mv Nyerere na Mv Temesa.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Abstrat Limited Abdallah Singano kutoka klabu ya (Gymkhana) Dar es salaam akishiriki kikamilifu katika michuano ya gofu ya Waitara ambayo yalifanyika katika viwanja vya gofu vya Lugalo jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Michuano hiyo ambayo huandaliwa na kudhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti hufanyika mara moja kila mwaka kwa madhumuni ya kuenzi mchango wa kimichezo wa Mkuu wa Majeshi (Mstaafu) Jenerali George Waitara kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo golf club.
   Mshiriki wa michuano ya gofu akitokea klabu ya Gymkhana Mwanaidi Ibrahim akipiga mpira wa gofu wakati wa kushiriki katika michuano ya gofu ya Waitara ambayo yalifanyika katika viwanja vya gofu vya Lugalo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Michuano hiyo ambayo huandaliwa na kudhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti hufanyika mara moja kila mwaka kwa madhumuni ya kuenzi mchango wa kimichezo wa Mkuu wa Majeshi (Mstaafu) Jenerali George Waitara kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo golf club.
                       Katibu wa michuano ya gofu Kanali (Mstaafu) John Nyalusi akizungumza jambo wakati wa hafla ya jioni kwa washiriki wa michuano ya gofu ya Waitara ambayo iliyofanyika katika viwanja vya gofu vya Lugalo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Michuano hiyo ambayo hudhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti hufanyika mara moja kila mwaka kwa madhumuni ya kuenzi mchango wa kimichezo wa Mkuu wa Majeshi (Mstaafu) Jenerali George Waitara kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo golf club.
   Mkuu wa Majeshi (Mstaafu) Jenerali George Waitara akizungumza kwenye hafla ya jioni kwa washiriki wa michuano ya gofu ya Waitara ambayo ilifanyika katika viwanja vya gofu vya Lugalo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Michuano hiyo hudhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti ambayo hufanyika mara moja kila mwaka kwa madhumuni ya kuenzi mchango wa kimichezo wa Mkuu wa Majeshi (Mstaafu) Jenerali George Waitara kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo golf club.

   Mkuu wa Majeshi (Mstaafu) Jenerali George Waitara (Kushoto) akikabidhi zawadi ya kikombe kwa mchezaji chipukizi wa daraja A aliyecheza kwa kiwango cha juu Bw. Suleiman Kessy katika hafla ya jioni ya kuwapongeza washiriki wa michuano ya gofu ya Waitara ambayo ilifanyika katika viwanja vya gofu vya Lugalo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Michuano hiyo hudhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti na hufanyika mara moja kila mwaka kwa madhumuni ya kuenzi mchango wa kimichezo wa Mkuu wa Majeshi (Mstaafu) Jenerali George Waitara kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo golf club.
   Mshindi wa jumla wa michuano ya gofu ya Waitara George Nyakundi akionyesha zawadi yake ya kikombe mara baada ya kutangazwa rasmi kama mshindi wa jumla wa michuano hiyo iliyofanyika katika viwanja wa gofu vya Lugalo jijini Dar es salaam. (Kushoto) ni Mkuu wa majeshi (Mstaafu) George Waitara. Michuano ya gofu ya Waitara hudhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti na hufanyika mara moja kila mwaka kwa madhumuni ya kuenzi mchango wa kimichezo wa Mkuu wa Majeshi (Mstaafu) Jenerali George Waitara kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo golf club.


  MICHUANO ya gofu ya Waitara yanayodhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia pombe yake kali ya Jonnie Walker imefana na kumalizika vizuri siku ya jumamosi ambapo MCHEZAJI George Nyakundi ameibuka mshindi wa jumla wa mashindano ya kila mwaka ya Kombe la Waitara yalilofanyika kwenye Viwanja vya gofu vya Klabu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo jijini Dar es Salaam.

  Nyakundi anayecheza katika kiwango cha ubora wa mchezo wa gofu (handicap) 22 alionesha kiwango cha juu zaidi katika mashindano hayo kwa kupiga mikwaju nett 65 na kuwashinda wachezaji zaidi ya 118 waliokuwa wakiwania Kombe hilo.

  Nafasi ya pili ya jumla ilikwenda kwa Michael Obare ambaye alichuana vikali na mshindi akirejea na mikwaju nett 66.

  Akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika viwanja hivyo, Meneja Chapa wa pombe kali wa kampuni ya bia ya Serengeti Shomari Shija alisema kuwa wamedhamini mashindano hayo kwa mara ya tano sasa ili kuendelea kuenzi heshima ya muasisi wa klabu hiyo Jenerali Mstaafu George Waitara.

  Akitangaza matokeo ya washindi mbalimbali katika makundi tofauti Kapteni wa klabu ya gofu Lugalo Japhet Masai alisema katika kundi la wachezaji wa viwango vya Daraja A ambao ni wa kiwango cha juu katika mchezo huo mchezaji chipukizi Suleiman Kessy mwenye handicap 9 alishinda kwa kupiga mikwaju nett 69, Jumanne Ally handicap 8 alishika nafasi ya pili akiwa na mikwaju 70, wakati Juma Likuli mwenye handicap 8 alimaliza nafasi ya tatu akiwa na mikwaju 70 pia.

  Mchezaji Nicolaus Chatanda handicap 11 alishinda kombe kwa wachezaji wa Daraja B akiwa na mikwaju 68, akifuatiwa na nahodha wa Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam, Akhil Yusufali handicap 16 akiwa na mikwaju 71 na Priscus Nyoni handicap 12 alishika nafasi ya tatu akiwa na mikwaju 72.

  Kelvin Manuhwa handicap 19 alishinda kwa kundi la wachezaji wa Daraja C akiwa na mikwaju 72 na kufuatiwa na R. Rwiguza handicap 24 aliyepiga 74.

  Kundi la wachezaji waandamizi wanaume kombe lilikwenda kwa Joseph Tairo handicap 13 mikwaju 73, nafasi ya pili alikuwa Jenerali Mstaafu Mirisho Sarakikya handicap 19 aliyepiga mikwaju 73 pia , wakati Edmund Mndolwa handicap 9 alipiga mikwaju 74 na kumaliza nafasi ya tatu.

  Pricilla Karobia handicap 17 alishinda kwa upande wa wachezaji wakongwe wanawake akiwa na mikwaju 82 na Lina Nkya handicap 15 alishika nafasi ya pili baada ya kurejea na mikwaju 88.

  Kwa upande wa kundi la wanawake Tayana William handicap 24 aliibuka mshindi kwa kupiga mikwaju 72, akifuatiwa na Vailet Peter handicap 13 akiwa na mikwaju 74 na Vicky Elias handicap 13 alishika nafasi ya tatu baada ya kurejea na mikwaju 76.

  Mbali na wachezaji wa ridhaa mashindano hayo pia yalihusisha kundi la wachezaji wa kulipwa ambapo Geofrey Leverian alirejea na mikwaju 75 gross na kuibuka mshindi wa kundi hilo lililohusisha wachezaji 18. Nafasi ya pili na tatu ilikwenda kwa mchezaji mkongwe Mbwana Juma na Nuru Mollel waliopiga mikwaju 76 na 77.

  Kwa upande wake muasisi wa michuano hiyo Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali George Waitara aliwashukuru washiriki wote kwa kuonyesha ni jinsi gani wameendelea kuthamini michuano hiyo na kuwataka kuendelea na moyo huo.

  Waitara pia alitumia nafasi hiyo kuishukuru Kampuni ya bia ya Serengeti na kumpongeza Mkurugenzi Mkuu (mstaafu) wa Kampuni hiyo Bw. Steve Ganon ambaye mara zote hakusita kudhamini michuano hiyo na kuomba wadau wengine kuiga mfano huo.

  Naye Mgeni rasmi wa michauano hiyo Jaji (Mstaafu) Mark Bomani alitoa changamoto ya wadau wa mchezo huo kushiriki katika kuongeza viwanja vingi zaidi vya mchezo huo huku akianisha maeneo kama Dodoma, Mwanza na Mbeya ambapo wadau hao wanaweza kuendeleza mchezo huo.

  Mashindano ya gofu ya Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali George Waitara huandaliwa na kufanyika kila mwaka kwa madhumuni ya kuenzi mchango wake wa kimichezo nchini kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo golf club. Uwanja huo ulianzishwa mwaka 2006 kwa mchango mkubwa uliotolewa na Jenerali mstaafu George Waitara kipindi alichokuwapo madarakani, pia kuendelezwa na Mkuu wa Majeshi aliyefuata na aliyeko madarakani kwa sasa Jenerali Davis Mwamunyange.

  0 0

  WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka wakurugenzi wa vitengo na wakuu wa taasisi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) wapate nakala ya hansard ya hotuba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuzindua Bunge la 11, waisome na kufanyia kazi maeneo yote aliyoyaainisha.

  “Katibu Mkuu hakikisha umepata hansard ya hotuba ya Mheshimiwa Rais wakati akizindua Bunge na uhakikishe kila mkurugenzi ana nakala na kila mmoja wenu lazima ahakikishe anafanyia maeneo ambayo Mheshimiwa Rais ameyaainisha. Ni lazima tuelewane ni nini tunapaswa tufanye,” alisema.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Novemba 24, 2015) wakati akizungumza na wakuu wa taasisi, wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) kwenye mkutano uliofanyika ofisi ndogo ya TAMISEMI, barabara ya Kivukoni, jijini Dar es Salaam.

  “Ninatamani kuona mabadiliko ya utendaji kazi Serikalini katika kipindi kifupi. Natamani kila mmoja asiridhike na uzembe unaofanywa huku chini. Ni nyote ni wataalamu, kwa hiyo mnapaswa kudhirisha elimu yenu na ujuzi mlionao,” aliwasisitizia Wakurugenzi hao.

  Alisema kila mkurugenzi na mkuu wa taasisi anapaswa kuongeza usimamizi na ufuatiliaji wa kazi kwenye sekta yake kwani hilo litasaidia kukidhi matarajio ya Watanzania ya kuona mabadiliko ya utendaji kazi kwenye Serikali ya Awamu ya Tano. “Ninyi wakurugenzi siyo desk officers bali ni field officers. Nataka muweke utaratibu wa kwenda vijijini mkasimamie watu wenu, pia mhimize uadilifu, uaminifu na weledi wa kazi,” alisisitiza.

  “Mambo ninayotaka mhimize watendaji waliopo chini yenu ni pamoja na haya yafuatayo: muda wa kuripoti kazini uzingatiwe, muda wa kukaa kazini uzingatiwe, utokaji kazini kwenda kwenye chai na chakula cha mchana udhibitiwe, na mipango na malengo ya kazi kwa siku ni lazima yafikiwe,” alisema.

  “Tunataka kujua mtumishi amefanya nini tangu alipoingia ofisini. Suala siyo kukaa tu ofisini, kwani kuna mtu anakaa ofisini, hajaenda hata kunywa chai lakini ukiuliza amefanya nini hupati jibu la kueleweka. Sisi kama vongozi wao ni lazima tujue wanafanya kazi gani wanapokuwa maofisini,” alisisitiza.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa ameitisha kikao ofisini kwake kesho saa 4 asubuhi akitaka kupatiwa taarifa ni kwa nini mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART) haujaanza kazi hadi sasa. “Kesho saa 4 asubuhi Katibu Mkuu, Mkurugenzi Mkuu DART na watendaji wako mje ofisini. Nataka kupata maelezo ni kwa nini mabasi hayajaanza kazi hadi leo, je ni lini yataanza kazi, je ni nani anakwamisha. Na hata kama ni sheria, ni kwa nini tusiziharmonise ili kuondoa hivyo vikwazo,?” alihoji Waziri Mkuu.

  “Ninataka kupata haya maelezo kwa sababu Watanzania na hasa wana-Dar es salaam, wamesubiri kwa muda kuona mradi ukianza kazi ili uondoe kero ya usafiri. Wao wanajua anayehusika ni TAMISEMI,” aliongeza.

  Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na watumishi na viongozi wa TAMISEMI, Katibu Mkuu wa OWM-TAMISEMI, Bw. Jumanne Sagini alimweleza baadhi ya mafanikio na changamoto ambazo wizara hiyo imekabiliana nazo katika utendaji wake wa kazi.

  Kuhusu ujenzi wa vyumba vya maabara kwa ajili ya kuimarisha ufundishaji wa masomo ya sayansi, Bw. Sagini alisema vyumba hivyo vimeongezeka kutoka 247 mwaka 2005/2006 na kufikia 6,161mwaka 2014/2015. Pia alisema vyumba 4,228 viko kwenye hatua za kukamilika ujenzi wake.

  Kuhusu utengaji wa madirisha ya kuhudumia makundi yenye msamaha kama wazee na watu wenye ulemavu hospitalini na kwenye vituo vya afya, Katibu Mkuu alisema nayo yameongezeka kutoka madirisha 5,074 mwaka 2010 na kufikia 7,903 mwaka 2014/2015 sawa na ongezeko la asilimia 55.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM
  JUMANNE, NOVEMBA 24, 2015.


  0 0

   Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI nchini Tanzania Dkt. Fatma Mrisho  akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani mwaka huu ambayo inaadhimishwa kwa  kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi  kupima afya zao na kupata elimu ya kujikinga  na maambukizi ya ugonjwa huo.
  Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa TACAIDS Dkt. Jerome Kamwela akiwaonesha waandishi wa Habari Bango lenye Takwimu za Hali ya Maambukizi ya VVU nchini Tanzania.  Na. Nyakongo Manyama- MAELEZO.
  24/11/2015. Dar es salaam.

  Wito umetolewa kwa wananchi kote nchini kuyatumia maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Desemba 1 ya kila mwaka kupima afya zao ili kudhibiti maambukizi mapya ya VVU.

  Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI nchini Tanzania Dkt. Fatma Mrisho amesema  Siku ya Ukimwi Duniani nchini itaadhimishwa kwa  kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi  kupima afya zao na kupata elimu ya kujikinga  na maambukizi ya ugonjwa huo.

  Ameeleza kuwa  maadhimisho ya mwaka huu yataambatana na shughuli mbalimbali zikiwemo za Utoaji wa Elimu ya Afya na Upimaji wa hiari wa VVU katika maeneo mbalimbali kote nchini kupitia vituo vitakavyowekwa, Kufungua kituo cha maarifa cha udhibiti UKIMWI eneo la Manyoni mkoani Singida ambayo ni njia kuu kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa na nchi za Jirani za Burundi na Rwanda.

  Ameongeza kuwa Tume kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itaendesha mikutano ya kitaalam kuhusu UKIMWI, Zoezi la upimaji wa hiari wa VVU kwa wananchi, Kupokea tamko litakalotolewa na Baraza la Watu wanaoishi na VVU pamoja na Uzinduzi wa taarifa ya tathmini ya Sheria zinazotumika  zinazohitaji kurekebishwa zinazozuia malengo ya sifuri 3.

   Aidha Tume itapokea taarifa ya hali ya maambukizi ya VVU duniani itakayotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kuhusu dunia na mapambano dhidi ya VVU.

  Dkt. Fatma amefafanua kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pamoja na mambo mengine atazindua Mfuko wa UKIMWI ambao utakuwa chachu ya kupunguza maambukizi ya VVU nchini.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa ufuatiliaji na tathmini kuhusu UKIMWI wa TACAIDS Dkt.Jerome Kamwela amesema kuwa kiwango cha maambukizi ya UKIMWI kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2011/2012 kimepungua na kufikia asilimia 5.3 huku mikoa ya nyanda za juu kusini ya Njombe, Iringa  na Mbeya ikiongoza kwa kuwa na maambukizi zaidi  na mikoa ya Manyara, Tanga na Lindi  ikiwa na maambukizi ya chini ya asilimia mbili.

  Dkt. Kamwela amesema kuwa maambukizi ya VVU ni mengi hasa kwa kundi la watu wenye umri wa miaka 19-24 huku makundi ya wanaojidunga, wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja, wanawake wanaofanya biashara ya ngono yakiendelea kuwa katika hatari ya kuathiriwa zaidi na maambukizi ya VVU.

  0 0
 • 11/24/15--05:31: Kipindupindu chapungua DAR
 • Na Jacquiline Mrisho- maelezo

  Idadi ya wagonjwa wa kipindupindu jijini Dar es salaam imepungua kufikia wagonjwa kumi na mbili (12) kwa mkoa mzima, huku wilaya ya Temeke ikiwa na wagonjwa saba,Kinondoni wagonjwa wanne na Ilala ikiwa na mgonjwa mmoja
  .
  Haya yamezungumzwa na Mratibu wa Magonjwa  ya kuambukiza wa Jiji la Dar es salaam  Bw. Alex Mkamba ofisini kwake leo akielezea jinsi gani mkoa umefanikisha kupambana na kipindupindu kwa kuzingatia usafi katika jiji.

  Ameongeza kuwa katika kufanikisha mapambano dhidi ya kipundupindu wametoa mafunzo  juu ya mbinu shirikishi ya namna ya kujikinga na kipindupindu kwa watendaji wa mitaa na pia imewahimiza kukagua maeneo yao na kuwapa kibali cha kufunga maeneo ya biashara au maeneo yatoayo huduma za chakula  yasiyozingatia usafi.

  Akielezea kuhusu huduma kwa wagonjwa wa kipindupindu jijini  Dar es salaam mratibu huyo amesema jiji lina dawa za kutosha za kuhudumia wagojwa ipasavyo  kwa kuwapatia huduma bora zaidi kuendana na kasi ya maambukizi yaliyopo.

  “ hata leo Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa dawa za kusafishia maji (Water Guard) maboksi 45 kwa kila wilaya” Mkamba alifafanua.

  Aidha alisema serikali imejipanga katika kudhibiti maambukizi mapya kwa kuwapima wagonjwa kabla na baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini  na aliwashauri wananchi kubadili tabia kwa kuhakikisha usafi unafanyika pia  kuchemsha maji na kuufanya usafi kuwa ni tabia yao ya kila siku.

  Mpaka sasa jumla ya watu 55 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa kipindupindu jijini Dar es salaam.

  0 0

  Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI nchini Tanzania Dkt. Fatma Mrisho  akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani mwaka huu ambayo inaadhimishwa kwa  kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi  kupima afya zao na kupata elimu ya kujikinga  na maambukizi ya ugonjwa huo. 
   Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa TACAIDS Dkt. Jerome Kamwela akiwaonesha waandishi wa Habari Bango lenye Takwimu za Hali ya Maambukizi ya VVU nchini Tanzania.

  Na Nyakongo Manyama- MAELEZO.
  WITO umetolewa kwa wananchi kote nchini kuyatumia maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Desemba 1 ya kila mwaka kupima afya zao ili kudhibiti maambukizi mapya ya VVU.

  Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI nchini Tanzania Dkt. Fatma Mrisho amesema  Siku ya Ukimwi Duniani nchini itaadhimishwa kwa  kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao na kupata elimu ya kujikinga  na maambukizi ya ugonjwa huo.

  Ameeleza kuwa  maadhimisho ya mwaka huu yataambatana na shughuli mbalimbali zikiwemo za Utoaji wa Elimu ya Afya na Upimaji wa hiari wa VVU katika maeneo mbalimbali kote nchini kupitia vituo vitakavyowekwa, Kufungua kituo cha maarifa cha udhibiti UKIMWI eneo la Manyoni mkoani Singida ambayo ni njia kuu kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa na nchi za Jirani za Burundi na Rwanda.

  Ameongeza kuwa Tume kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itaendesha mikutano ya kitaalam kuhusu UKIMWI, Zoezi la upimaji wa hiari wa VVU kwa wananchi, Kupokea tamko litakalotolewa na Baraza la Watu wanaoishi na VVU pamoja na Uzinduzi wa taarifa ya tathmini ya Sheria zinazotumika  zinazohitaji kurekebishwa zinazozuia malengo ya sifuri 3.

   Aidha Tume itapokea taarifa ya hali ya maambukizi ya VVU duniani itakayotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kuhusu dunia na mapambano dhidi ya VVU.

  Dkt. Fatma amefafanua kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pamoja na mambo mengine atazindua Mfuko wa UKIMWI ambao utakuwa chachu ya kupunguza maambukizi ya VVU nchini.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa ufuatiliaji na tathmini kuhusu UKIMWI wa TACAIDS Dkt.Jerome Kamwela amesema kuwa kiwango cha maambukizi ya UKIMWI kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2011/2012 kimepungua na kufikia asilimia 5.3 huku mikoa ya nyanda za juu kusini ya Njombe, Iringa  na Mbeya ikiongoza kwa kuwa na maambukizi zaidi  na mikoa ya Manyara, Tanga na Lindi  ikiwa na maambukizi ya chini ya asilimia mbili.

  Dkt. Kamwela amesema kuwa maambukizi ya VVU ni mengi hasa kwa kundi la watu wenye umri wa miaka 19-24 huku makundi ya wanaojidunga, wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja, wanawake wanaofanya biashara ya ngono yakiendelea kuwa katika hatari ya kuathiriwa zaidi na maambukizi ya VVU.

  0 0


  0 0


  0 0

   Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla ametembelea uwanja wa ndege Kilimanjaro(KIA) kujionea ujenzi wa ya upanuzi wa uwanja na shughuli za uwanja wa ndege Katika kikao cha menejimenti ya kampuni ya uendeshaji uwanja KADCO mkuu wa mkoa amewapongeza uongozi kwa kuongeza ndege zinazotua na kuruka, uwezo wakujiendesha kwa kuwa na mapato mazuri na uwezo wa kudhibiti vitendo haramu vya madawa ya kulevya, usafirishaji nyara za serikali na ugaidi Pamoja na pongezi hizo mkuu wa mkoa ameagiza yafuatayo yatekelezwe.
   Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla (pichani juu)akizungumza na menejimenti ya Kadco katika uwanja wa ndege kuhusiana na Uwanja huo  usiwe njia ya wapitishaji madawa ya kulevya kwani kuruhusu hilo tunapoteza nguvu kazi ya taifa ambayo ni vijana.
   Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla akitembelea Uwanja wa Kia na kuwaambia kuwa uwanja huo usiwe njia ya kutorosha nyara za taifa kwani kufanya hivyo ni kupoteza mapato ya taifa na raslimali za taifa.

  pia  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla ameagiza menejimenti kuutangaza uwanja huo kimataifa ili uvutie wageni zaidi kuja kuona vivutio vya utalii tukivyonavyo na kufanya hivyo ni kuongeza pato la taifa.
  Mkuu wa mkoa akiongea na menejimenti ya Kadco leo alipotembelea uwanja wa ndege wa Kia mkoani Kilimanjaro.

  0 0

  Katika kuelekea msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka huu, GAPCO, kampuni inayoongoza kwa uuzaji wa mafuta, imeamua kuwapa wateja wake zawadi ya kufungia mwaka. Katika kufanikisha hilo, kupitia mpango wake wa ‘GAPCO Safari Loyalty programme ‘, kampuni imelenga kunufaisha na kuimarisha uhusiano wa kudumu na wateja wake kwa kuwapa mafuta ya bure.

  Mpango huu unaoenda sambamba na promosheni ya ‘Jaza Mafuta na Ushinde’, umedhamiria kutoa lita 4,000 za petroli au dizeli za bure kwa wateja 100 watakao bahatika ndani ya wiki nne. Katika droo za kila wiki, kutakuwa na wateja 25 wanaoweza kujishindia lita 40 kila mmoja. Wateja wanaweza kujiongezea nafasi za ushindi kwa kujaza mafuta mara nyingi zaidi.

  Pia, wateja ambao hawajajiunga na mpango wa ‘GAPCO Safari Loyalty programme’ wanaweza kujiunga katika kituo chochote cha GAPCO kilichopo Dar es Salaam ili waweze kushiriki katika promosheni. Motisha zinazotolewa kupitia mpango huu, ni nje ya zawadi atakazoshida mteja katika promosheni, mteja wa GAPCO atajikusanyia pointi zitakazomwezesha kukomboa mafuta ya bure.

  “Kupitia mpango huu wa ‘GAPCO Safari Loyalty programme‘, tunataka wateja wetu wawe na furaha na waendelee kutumia bidhaa na huduma zetu. Mbali na kwamba tunatoa kadi hizi kwa mteja mmoja mmoja, pia tunaanzisha kadi kwa ajili ya makampuni na wasafirishaji. Kupitia kadi hizi, mbali na wateja kuweza kujikusanyia pointi zitakazomwezesha kupata mafuta ya bure, wateja wetu wataweza kudhibiti matumizi ya fedha zao,” alisema Meneja Masoko wa GAPCO, Caroline Kakwezi.

  Mwanzoni mwa mwaka huu, GAPCO ilifanya mabadiliko makubwa na kuamua kujikita katika kujipambanua kwa namna ya kipekee. Katika mabadiliko haya, GAPCO iliboresha muonekano na mazingira katika vituo vyake vya mafuta vilivyopo Dar es Salaam. Ahadi ya kuwa na mafuta yenye ubora na ujazo wakuaminika, mazingira mazuri na rafiki, huduma bora inayojali mteja na ya haraka ni kati ya faida mahsusi anazopata mteja anayefika katika vituo vya mafuta vya GAPCO nchini.

  “Tukiwa na mtazamo na nia ya kuwapa wateja wetu maili nyingi zaidi na tabasamu zaidi, malengo yetu ya muda mrefu ni kuweza kupanua huduma zetu na kuhakikisha tunatoa huduma za ziada ili kuwaachia wateja wetu kumbukumbu sahihi ya huduma bora na za kisasa,” aliongeza Kakwezi.
  Meneja Masoko wa Kampuni ya Mafuta ya GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (kushoto) akizungumza na wanahabari wakati wa kutangaza mpango wake wa ‘GAPCO Safari Loyalty ‘, unaolenga kuwanufaisha wateja wake kwa kuwapa mafuta ya bure, ulizindulia kwenye makao makuu ya Kampuni hiyo, Kurasini jijini Dar es salaam. Kulia ni Meneja wa Kanda ya Dar es salaam wa Kampuni ya Mafuta ya GAPCO, Jane Mwita.
  Meneja Masoko wa Kampuni ya Mafuta ya GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (kushoto) na Meneja wa Kanda ya Dar es salaam wa Kampuni ya Mafuta ya GAPCO, Jane Mwita, wakionyesha vipeperushi vya Promosheni hiyo, mara baada ya kuizindua rasmi.

older | 1 | .... | 694 | 695 | (Page 696) | 697 | 698 | .... | 1897 | newer