Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46200 articles
Browse latest View live

SPEA ZA MASHINE ZA MRI NA CT-SCAN ZIMEFIKA NA MATENGENEZO YAMESHAANZA KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI

0
0
 Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete baada ya kufuatilia agizo la Rais John Pombe Magufuli ambaye awali aliagiza wagonjwa wasilale chini. Rais Magufili aliitembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) hivi karibuni na kutoa agizo hilo. Leo Balozi Sefue ameitembelea mashine ya MRI, ST-Scan na Jengo la Taasisi ya Mifupa ya MOI. Akiwa katika ofisi ambako ipo mashine ya MRI na ST-Scan Balozi Sefue amepewa taarifa ya matengenezo ya mashine hizo. 
 Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (katikati) akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ambako amefanya ziara kuangalia utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuhusu huduma bora kwa wagonjwa na kutekeleza wagonjwa kutolala chini. Wagonjwa hivi sasa wanalala kwenye vitanda na siyo chini. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi na Jamii, Dk Donan Mmbando na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa ya Moi, Othuman Wanin Kiloloma.
 Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue akihoji kutokamilika kwa mashine ya MRI kwa wakati baada ya kutembelea chumba ambako mashine hiyo imehifadhiwa. Ofisa anayesimamia utengenezaji wa mashine hiyo, Monica Joseph ameahidi kwamba mashine hiyo itakamilika Alhamisi ijayo. 
 Mmoja wa mafundi wa mshine ya ST-Scan akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue kuhusu utengenezaji wa mashine hizo. Fundi huyo ameahidi kwamba mashine hiyo itakamilika Jumatano.
Picha zote kwa hisani Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).


SERIKALI Kuendelea Kuboresha Sekta ya Afya Nchini
Katibu  Mkuu  Kiongozi  Balozi Ombeni  Sefue leo amefanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na mambo mengine amesema serikali itaendelea kuboresha sekta ya afya nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati.

Akizungumza baada ya kutembelea MNH, Balozi Sefue amesema  amekagua mashine za MRI na CT-SCAN  na kueleza kuwa spea zimeshafika na kazi ya kutengeneza mashine hizo inaendelea. Pia amesema kwamba Serikali ya Tanzania imesaini mkataba mpya na Serikali ya Uholanzi wa kununua vifaa vipya na Hospitali ya Muhimbili itapata CT-SCAN moja wakati Hospitali ya Bugando itapata mashine moja ya MRI.

Pia,  amewataka wahudumu wa afya kuwahudumia vizuri wagonjwa wanaotumia Bima ya Afya ili kuongeza mapato katika hospitali za serikali.
Akizungumzia kuhusu kudhibiti wizi wa dawa za serikali, Balozi Sefue amesema ni vema ukaimarishwa mfumo wa MSD kwa kutumia mifumo ya Tehama  na kuwa na maduka yao ya ndani.

Katika ziara hiyo, Balozi Sefue amepata fursa ya kufanya kikao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk Donan Mmbando  na  watendaji wa MNH  ili kupata sura ya matatizo yote katika hospitali hiyo.

NEWZ ALERT: RAIS MAGUFULI ATANGAZA SIKU YA UHURU KUWA SIKU YA KUFANYA KAZI

0
0
Kwa mujibu wa  Sheria ya Sikukuu za Kitaifa  (The Public Holidays Act, Cap 35) pamoja na Sheria zingine zinazompa mamlaka Rais kutangaza siku yoyote kuwa sikukuu au mapumziko,  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameamua kuwa maadhimisho ya Sherehe za Uhuru na Jamhuri zitakazofanyika tarehe 9 Desemba, 2015, yatumike  kwa kufanya kazi.  

Kwamba maadhimisho ya Uhuru ya mwaka huu  (2015) yatatumika kama kichocheo cha kujenga tabia ya kufanya kazi (Uhuru na Kazi) katika Taifa letu.  Mheshimiwa Rais ameelekeza Watanzania wote siku hiyo waitumie kwa kufanya kazi mbalimbali kama vile, mashambani, maofisini, sokoni, viwandani na usafi wa miji yao katika kutimiza dhana ya Uhuru na Kazi kwa vitendo.

Aidha, kwa kuwa Sherehe za Uhuru na Jamhuri huendana na Maandalizi mbalimbali ambayo yanatumia fedha, kwa kuzingatia kuwa siku hiyo itaadhimishwa kwa kufanya kazi,  fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hiyo sasa zitumike kwa shughuli zingine za kijamii ikiwa ni pamoja na kupambana na maradhi hasa kipindupindu, kununulia dawa za hospitali, vitanda vya hospitali n.k. kadri kamati za maandalizi zitakavyoamua.

Ieleweke kuwa sherehe za Uhuru na Jamhuri ni muhimu katika kuadhimisha kumbukumbu ya uhuru wa nchi yetu. Hivyo,   sherehe hizi zitaendelea kuadhimishwa kila mwaka kama kawaida kuanzia mwaka 2016.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

WAZIRI MKUU AKUTANA NA WATUMISHI WA OFISI YAKE

0
0

WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu watambue  jukumu walilonalo la kuwahudumia wananchi kutokana na majukumu ya ofisi hiyo ambayo yanagusa maisha ya kila siku ya Watanzania.



“Ofisi ya Waziri Mkuu ni kubwa na pana sana na inahusika na shughuli za kila siku za Watanzania. Kwa hiyo tuna kazi kubwa ya kukidhi matarajio yao,” alisema.



Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Novemba 23, 2015) wakati akizungumza na wakuu wa taasisi, wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye mkutano uliofanyika ofisini kwake, Magogoni, jijini Dar es Salaam. Leo ndiyo ameripoti kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa Ijumaa iliyopita kwenye Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.



Pamoja na kazi nyingine tunayo majukumu makubwa ambayo ni udhibiti, usimamizi na ufuatiliaji wa masuala mbalimbali humu Serikalini. Ninataraji kupata mpango kazi kutoka kwa Mkuu wa kila idara na kila taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Nitakwenda pia ofisi za TAMISEMI ili kuweka vipaumbele vyetu sawa,” alisema.



Aliwataka watumishi hao wawe tayari kutekeleza kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ ambayo imekuwa ikisisitizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili kuweza kumudu kasi ya utendaji kazi Serikali ambayo anaihimiza hivi sasa.



Alisema ana imani kuwa watumishi hao watampa ushirikiano kama ambavyo walikuwa wakiutoa kwa mtangulizi wake, Mhe. Mizengo Pinda ambaye amestaafu hivi karibuni.



IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

2 MTAA WA MAGOGONI,

S.  L. P. 3021,

11410 DAR ES SALAAM

JUMATATU, NOVEMBA 23, 2015.

HATIMA YA MWILI WA MAREHEMU MAWAZO KUAGWA JIJINI MWANZA KUAMULIWA KESHO NA MAHAKAMA

0
0
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akitoa taarifa kwa wananchi baada ya Chadema Kufungua Kesi Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kupinga kuzuiliwa kwa mwili wa Marehemu Mawazo kuagwa Jijini Mwanza.

Mmoja wa Mawakili wa Chadema John Mallya akitoa taarifa kesi baada ya Chadema Kufungua Kesi Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kupinga kuzuiliwa kwa mwili wa Marehemu Mawazo kuagwa Jijini Mwanza.
Kesi ilisikilizwa katika Jengo la Mahakama ya Biashara lililopo katikati ya Jiji la Mwanza. Pichani ni mawakili wa Chadema wakielekea mahakamani huku kukiwa na umati wa wafuasi wa Chadema (Ukawa) pamoja na viongozi waandamizi wa Chadema
Kesi ilisikilizwa katika Jengo la Mahakama ya Biashara lililopo katikati ya Jiji la Mwanza. Pichani ni mawakili wa Chadema wakielekea mahakamani huku kukiwa na umati wa wafuasi wa Chadema (Ukawa) pamoja na viongozi waandamizi wa Chadema

Mmoja wa wafuasi wa Ukawa akilalamikia hatua ya jeshi la polisi kuwazuia kuingia Mahakamani ili kujua hatima ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Chadema hii leo
Mmoja wa wafuasi wa Ukawa akilalamikia hatua ya jeshi la polisi kuwazuia kuingia Mahakamani ili kujua hatima ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Chadema hii leo
Mmoja wa wafuasi wa Ukawa akilalamikia hatua ya jeshi la polisi kuwazuia kuingia Mahakamani ili kujua hatima ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Chadema hii leo
Mmoja wa wafuasi wa Ukawa akilalamikia hatua ya jeshi la polisi kuwazuia kuingia Mahakamani ili kujua hatima ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Chadema hii leo.

Na:George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema leo kimefungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, ili kuiomba Mahakama hiyo kutengua zuio la kuuaga mwili wa aliekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Geita Marehemu Alphonce Mawazo, lililotolewa na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kutokana na hofu ya kiusalama pamoja na uwepo wa ugonjwa wa Kipindupindu.

Katika kesi hiyo, Chadema inawakilishwa na Mawakili watatu ambao ni James Millya, John Mallya pamoja na Paul Kipeja ambapo mlalamikaji ni Charles Lugiko ambae ni baba mdogo wa Marehemu Mawazo.

Mahamaka hiyo chini ya Jaji Lameck Mlacha, imesikiliza malalamiko ya upande wa washtaki na kuahirisha kesi hiyo hadi kesho ambapo imeamuru mlalamikiwa ambae ni Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mwanza pamoja na mwanasheria Mkuu wa Serikali kupelekewa nyaraka za kesi hiyo kabla ya kusikiliza utetezi wao hapo kesho.

Mapema kabla ya kesi hiyo kusikilizwa, wafuasi wa Chadema waliokuwa wamekusanyika nje ya viunga vya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, walilalamikia hatua ya jeshi la polisi kuwazuia kuingia Mahakamani hapo ili kujua hatima ya kesi hiyo, ambapo wamesema kitendo hicho kinaondoa dhana ya Rais John Pombe Magufuli, kuwa yeye ni rais wa wananchi wote wakati wao kama Chadema wananyimwa haki zao.

Licha ya Malalamiko hayo pamoja na ulinzi mkali wa polisi uliokuwa umetanda Mahakamani hapo, bado wafuasi wa Chadema hawakuondoka katika viunga vya Mahakama hiyo hadi pale Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Freeman Mbowe alipowasihi kurejea majumbani mwao hadi kesho kesi hiyo itakaposikilizwa tena.

Ni zaidi ya siku nane sasa tangu marehemu Alphonce Mawazo auawe kikatili Mkoani Geita na watu wasiojulikana kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni chuki za kisiasa ambapo mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando.

UTT-PID yashiriki mkutano wa mwaka wa Wanahisa wa UTT-AMIS jijini Dar es Salaam!

0
0
1 (1)
Maafisa masoko wa UTT-PID, Laurence Nzuki (kushoto) na Martin Mchanjila (katikati) wakitoa maelezo kwa baadhi ya watu waliotembelea kwenye banda hilo la UTT-PID wakati wa mkutano huo wa mwaka wa Wanahisa wa UTT-AMIS uliofanyika mwishoni mwa wiki, Novemba 21-22.2015, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
AsfOxbUQv7XGaXHM7H-QB4HDmtD0NoXc-5OrHiTpRdSO
Picha ya juu na chini Afisa masoko wa UTT-PID, Mary Lugusi akielimisha wananchi juu ya miradi inayoendeshwa na taasisi hiyo kwa wananchi hao waliotembelea banda hilo.
AuISTCaTvV-iYBU-Kfj_MXe9kHuIQPYgU4bZXhQo6OXa
Wananchi wakitembelea banda hilo la UTT-PID..
AmP8BMKF9VkuKPXrXzrxLFNdWA_ZhP3KDMoYW5wunYlG
Mkuu wa Mahusiano ya Umma UTT-PID, Eugenia Simon akiwa pamoja na Mshahuri wa masuala ya uwekezaji wa UTT-Micro finance wakati wa mkutano huo mkuu wa mwaka wa wanahisa wa UTT-AMIS, uliofanyika Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

AnQqTlX1RpGgYJtjKG4oeWsJ-LyltzccztY6XmJx9t4j
Mmoja wa wananchi akipata maelezo kutoka kwa afisa masoko wa UTT-PID, Mary Lugusi.

Na Andrew Chale, Modewjiblog
Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT-PID) inafanya miradi mbalimbali ikiwemo huduma za uuzwaji wa viwanja katika maeneo tofauti nchini ikiwemo vile vya mradi wa katika miji ya Chalinze na Mapinga Bagamoyo Mkoani Pwani. Pia mradi wa viwanja vya Bunju, Tundwi songani-Kigamboni ambayo ipo Jijini Dar es Salaam. Mingine ni Kingorwila, Madaganya, Mkoani Morogoro. Lindi, Bukoba, Sengerema na kwingine kwingi hapa nchini.

UTT -PID ni miongoni mwa taasisi zinazofanya vizuri na utendaji wa kasi katika utoaji huduma za ushahuri katika maeneo ya upembuzi yakinifu wa miradi mbalimbali, Uratibu wa fedha na huduma zinazohusiana katika maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au taasisi za fedha, uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi ya zabuni na usimamizi wa majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi za usimamizi wa majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.

Balozi Sefue awaasa watumishi wa umma kuwajibika

0
0
OM1 
Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Bw Silasi David mmoja ya wagonjwa waliolazwa katika kitengo cha mifupa cha MOI.
OM2
Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue akizungumza na mmoja ya wagomjwa waliolazwa katika kitengo cha mifupa cha MOI Bw. Muhusin Hamiri.
……………………………………………………………………………………………………….
Na Beatrice Lyimo- Maelezo.
Watumishi wa umma wametakiwa kutumia muda wa kazi kuhudumia wananchi na sio kufanya kazi zao binafsi kwa kutumia ofisi na vifaa vya serikali.Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alipofanya ziara katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwa lengo la kuangalia maendeleo ya Hospitali kwa kukagua vifaa tiba na  kuongea na watendaji wakuu wa hospitali hiyo.
 
Balozi Sefue ameongeza kuwa  watumishi wa umma wanapaswa  kufanya kazi kwa kutoa huduma bora na kwa upendo kwa wananchi  kwani moja ya kanuni na taratibu za mtumishi wa umma ni kumhudumia mteja pasipo upendeleo.“kwa upande wa madaktari na watoa huduma za afya mnatakiwa kutoa huduma bora nazenye upendo  kwa wananchi ili nao wajione wanahaki ya kupatiwa huduma hiyo”.
 
“kwa watumishi wote wa umma tukijitambua kuwa sisi ni watumishi wa umma tutafanya kazi kwa bidii na kwa kujituma” alifafanua Balozi Sefue.ia muda wa kuingia na wa kutoka ofisini na pia kujipima ni nini amefanya ndani ya masaa nane katika kuhudumia wananchi.
“Hizi si nguvu za soda ni lazima kubadilika pindi tunapowahudumia wateja kwa wakati na kwa ufanisi” alisema Balozi Sefue.
 
Kadhalika katika kuhakikisha serikali inatoa huduma bora kwa wananchi Balozi sefue ameagiza katika kila ofisi itoayo huduma kuwe na dawati la msaada kwa wananchi waweze kupata huduma kwa haraka.

KATIBU MKUU KIONGOZI OMBENI SEFUE AFANYA ZIARA MUHIMBILI

0
0
SEF1
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari ambao umefanyika leo katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli kwamba wagonjwa hawapaswi kulala chini. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru. Picha zote kwa hisani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
SEF2
Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue akisaini kitabu cha wageni mara baada baada yakwasili hospitalini hapo.
SEF3
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (katikati) akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ambako amefanya ziara kuangalia utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuhusu huduma bora kwa wagonjwa na kutekeleza wagonjwa kutolala chini. Wagonjwa hivi sasa wanalala kwenye vitanda na siyo chini. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi na Jamii, Dk Donan Mmbando na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa ya Moi, Othuman Wanin Kiloloma.
SEF4
Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue akihoji kutokamilika kwa mashine ya MRI kwa wakati baada ya kutembelea chumba ambako mashine hiyo imehifadhiwa. Ofisa anayesimamia utengenezaji wa mashine hiyo, Monica ameahidi kwamba mashine hiyo itakamilika Alhamisi ijayo.
SEF5
Mmoja wa mafundi wa mshine ya ST-Scan akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue kuhusu utengenezaji wa mashine hizo. Fundi huyo ameahidi kwamba mashine hiyo itakamilika Jumatano.Picha zote kwa hisani Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
…………………………………………………………………………………
Katibu  Mkuu  Kiongozi  Balozi Ombeni  Sefue leo amefanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na mambo mengine amesema serikali itaendelea kuboresha sekta ya afya nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati.
 
Akizungumza baada ya kutembelea MNH, Balozi Sefue amesema  amekagua mashine za MRI na CT-SCAN  na kueleza kuwa spea zimeshafika na kazi ya kutengeneza mashine hizo inaendelea. Pia amesema kwamba Serikali ya Tanzania imesaini mkataba mpya na Serikali ya Uholanzi wa kununua vifaa vipya na Hospitali ya Muhimbili itapata CT-SCAN moja wakati Hospitali ya Bugando itapata mashine moja ya MRI.
 
Pia,  amewataka wahudumu wa afya kuwahudumia vizuri wagonjwa wanaotumia Bima ya Afya ili kuongeza mapato katika hospitali za serikali.Akizungumzia kuhusu kudhibiti wizi wa dawa za serikali, Balozi Sefue amesema ni vema ukaimarishwa mfumo wa MSD kwa kutumia mifumo ya Tehama  na kuwa na maduka yao ya ndani.
 
Katika ziara hiyo, Balozi Sefue amepata fursa ya kufanya kikao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk Donan Mmbando  na  watendaji wa MNH  ili kupata sura ya matatizo yote katika hospitali hiyo.

WAZIRI MKU MAJALIWA AKUTANA NA WATUMISHI WA OFISI YAKE NA KUJITAMBULISHA

0
0

JA1

Waziri Mkuu, Majaliwa Kasim akipokea shada la maua kutoka kwa kaimu Mkurugenzi wa Utawala wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Savera Kazaura (kulia) Baada ya kuwasili ofisini kwake Novemba 23, 2015. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt, Florence Turuka.

JA2

Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akitia saini kitabu baada ya kuingia  ofisini kwake , Magogoni jijini Dar es salaam, Novemba 23, 2015. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Tiruka.

JA3

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa wakati alipozungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha  , Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 23, 2015.

JA4

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa wakati alipozungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha  , Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 23, 2015. .

JA5

Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akimsikiliza Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Turuka ambaye alitoa taarifa ya jumla kuhusu Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya Waziri Mkuu kuwasili Ofisini na kujitambulisha kwa watumishi wa Ofisi yake Novemba 23, 2015.

JA6

Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu katika mkutano wa kujitambulisha  alioufanya baada tu ya kuwasili ofisni Novemba 23, 2015. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

JA7

Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  na  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Turuka  wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya kuzungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha  alioufanya baada ya kuwasili ofisini kwake Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


JA8

Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu,Dkt Florence Turuka  baada ya kuwasili Ofisini Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

JA9

Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  na  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Turuka  wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya kuzungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha  alioufanya baada ya kuwasili ofisini kwake Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

…………………………………………………………………….

WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu watambue  jukumu walilonalo la kuwahudumia wananchi kutokana na majukumu ya ofisi hiyo ambayo yanagusa maisha ya kila siku ya Watanzania.


“Ofisi ya Waziri Mkuu ni kubwa na pana sana na inahusika na shughuli za kila siku za Watanzania. Kwa hiyo tuna kazi kubwa ya kukidhi matarajio yao,” alisema.


Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Novemba 23, 2015) wakati akizungumza na wakuu wa taasisi, wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye mkutano uliofanyika ofisini kwake, Magogoni, jijini Dar es Salaam. Leo ndiyo ameripoti kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa Ijumaa iliyopita kwenye Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.


Pamoja na kazi nyingine tunayo majukumu makubwa ambayo ni udhibiti, usimamizi na ufuatiliaji wa masuala mbalimbali humu Serikalini. Ninataraji kupata mpango kazi kutoka kwa Mkuu wa kila idara na kila taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Nitakwenda pia ofisi za TAMISEMI ili kuweka vipaumbele vyetu sawa,” alisema.


Aliwataka watumishi hao wawe tayari kutekeleza kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ ambayo imekuwa ikisisitizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili kuweza kumudu kasi ya utendaji kazi Serikali ambayo anaihimiza hivi sasa.Alisema ana imani kuwa watumishi hao watampa ushirikiano kama ambavyo walikuwa wakiutoa kwa mtangulizi wake, Mhe. Mizengo Pinda ambaye amestaafu hivi karibuni

NSSF YADHAMINI TAMASHA LA KUSOMA VITABU WANAFUZNI WA SHULE ZA MSINGI

0
0
 Ofisa Mwandamizi Idara ya Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abubakar Mshangama akiwaonyesha fomu ya kujiunga na uanchama wa hiari na fao la matibabu baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na NSSF wakati wa tamasha la wa kusoma vitabu wanafunzi wa shule za msingi, lililofanyika jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na NSSF. 
Ofisa Mwandamizi Idara ya Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abubakar Mshangama (kushoto) akifafanua jambo kwa wanachama wapya waliojiunga uanchama wa hiari na fao la matibabu wakati wa tamasha la kusoma vitabu wanafunzi wa Shule za Msingi lililofanyika jijini Dar es Salaam kudhaminiwa na NSSF.
 Watoto Brianna Michalis Kelly Godfrey wakisoma vitabu wakati wa tamasha la  kusoma vitabu wanafunzi wa Shule za Msingi lililofanyika jijini Dar es Salaam kudhaminiwa na NSSF.
Mtoto Baraka Ngonyani (kushoto) akisoma kitabu wakati wa tamasha la kusoma vitabu lililoandariwa na toKay&Sons na kudhaminiwa na NSSF. Katikati ni mtoto Fidelis Kennedy.

 Ofisa Mwandamizi Idara ya Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abubakar Mshangama akifafanua jambo kwa uanachama wa hiari na fao la matibabu kwa wanachama wapya waliojiunga na NSSF wakati wa tamasha la wa kusoma vitabu wanafunzi wa shule za msingi, lililofanyika jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na NSSF.
 Ofisa Mawasiliano wa tKay&Sons, Angelina Pesha akiwafundisha watoto.

UNDP YAKABIDHI MRADI WA DOLA ZA MAREKANI 150,000 WA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI KIJIJI CHA CHAMWINO

0
0
IMG_9773
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo akikata utepe kuzindua Kisima cha maji safi na salama katika kijiji cha Machali A wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma mwishoni mwa juma lililopita.

Na Modewjiblog team, Chamwino

KIJIJI cha Manchali kilichopo wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, kimekabidhiwa mradi wa dola za Marekani 150,000 wenye lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Mradi huo ulikabidhiwa kijiji hicho na Mratibu wa mashirika ya Umoja wa mataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Alvaro Rodriguez.

Mradi huo umelenga kusaidia jamii inayoishi katika kijiji hicho kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Mradi huo wa nishati ya jua umelenga kutatrua tatizo la nishati na kufanya matumizi bora ya ardhi na teknolojia ya maji.Mradi huo unasaidia familia 600.

Kwa uzoefu wa Tanzania na maeneo mengine duniani, familia maskini ndizo zinazopigika vibaya na mabadiliko hayo na ndio haizna uwezo wa kukabiliana nayo.

Kwa mradi huo wananchi wa Manchali wanatarajia kukabiliana vilivyo na mabadiliko ya Tabia nchi.

Akizungumza katika kijiji hicho cha Manchali, Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Bi. Awa Dabo alisema kwamba ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi uwezeshaji wananchi kiuchumi ni muhimu sana ili kufanya familia kustawi.
IMG_9772
Kisima kilichozinduliwa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo.
“Athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa watu maskini ni kubwa na ndio wanaoathirika zaidi” alisema Mkurugenzi Mkazi UNDP Bi. Dabo.
Aidha alisema kwamba anaishukuru serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuhangaikia suluhu ya watu kukubali kuwapo kwa mabadiliko ya tabia nchi na kufanya juhudi ya kukabili hali hiyo.

“Hii imo katika malengo ya maendeleo endelevu kwani malengo manne kati ya 17 yanahusiana na mabadiliko ya tabia nchi na kuhifadhi mazingira.kwa kutumia fedha kutoka kwa wadau wa maendeleo, UNDP imefanikiwa kusaidia wananchi wa kijiji cha Manchali kufanyia kazi maeneo kadha muhimu ili kufanya uragibishi kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, kuongeza kasi ya upoandaji wa miti na matumizi ya nishati jadidifu.” alisema.

Bi Dabo amesema kwamba mradi huo wa Manchali umekamilika ni mmoja wa mradi yenye mafanikio inayosimamiwa na UNDP.

Aliwapongeza wananchi wa Manchali kwa ushiriki wao na kuufanya mradi huo kuwa wakwao hali iliyosababisha kuwepo na matunda yenye tija katika kijiji hicho.
“Sisi UNDP kutokana na mafanikio haya tunaangalia maeneo mengine ya kufanya mradi kama huu” alisema Bi Dabo.
UZINDUZI-MRADI
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja waMataifa la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), kijijini humo.


Naye Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez alisisitiza ushiriki wa wananchi katika kufaniukisha miradi na kusema kwamba mradi huo umefanikiwa kutoka na ushiriki wa wananchi na hasa kitendo chao cha kuufanya mradi huo kuwa mali yao.

Aliongeza kwamba kitendo cha kufanya mradi wao na kuwa viongozi wa maendeleo yao wao wenyewe kumefanya mradi uwe na tija kubwa kwao.

“Mradi huu umeleta maendeleo makubwa kwa wananchi wa hapa kutokana na wao kuanza kutumia nishati jadidifu, watoto wanakwenda shule na maeneo yameanza kurejewa na misitu.”
Mratibu huyo aliongeza kwamba mabadiliko ya tabia nchi ni ya kweli na wala si ya kuyafanyia mzaha, mashirika ya umoja wa mataifa na Umoja wenyewe wanatazama sana athari zake mbaya.

Alisema kijiji cha Manchali kimefanikiwa katika kuanza kukabili mabadiliko ya tabianchi kwa kubadili mambo yanayowazunguka na kurejesha uoto wa asili na kuacha kuharibu mazingira huku shughuli za maendeleo zikichukua sura mpya yenye kujali mabadiliko ya tabia nchi.
IMG_9802
Bango la mradi uliozinduliwa na Bw. Alvaro Rodriguez.
IMG_9786
Kutoka kushoto ni Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja waMataifa la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na viongozi wa kijiji wakiwakilisha wananchi ambao watanufaika na mradi huo.
IMG_9842
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja waMataifa la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum katika picha ya pamoja.

MAADHIMISHO YA SIKU YA TAKWIMU AFRIKA YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0

T1
Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha,  Prof. Adolf Mkenda akihutubia wadau mbalimbali wa takwimu katika maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya “Takwimu Bora kwa Maisha Bora”.
T2
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo ya utangulizi katika katika maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya “Takwimu Bora kwa Maisha Bora”
T3
Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano Dkt. Carina Wangwe kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) akielezea umuhimu wa kujiunga katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii wakati wa maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya “Takwimu Bora kwa Maisha Bora”.
T4
Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Prof. Innocent Ngalinda akielezea umuhimu wa takwimu rasmi katika kupanga na kutathmini programu mbalimbali za maendeleo nchini wakati wa maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya “Takwimu Bora kwa Maisha Bora”.
T5
Baadhi ya wadau mbalimbali wa takwimu wakifuatilia kwa makini matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya “Takwimu Bora kwa Maisha Bora”.
T6
Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu Prof. Milline Mbonile akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa ofisi hiyo pamoja na viongozi wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika baada ya kumaliza maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya “Takwimu Bora kwa Maisha Bora”.(PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).

……………………………………………………………………………………………..
Emmanuel Ghula Dar es Salaam
Wizara, Idara, Wakala, Taasisi za Serikali, Mashirika yasiyokuwa ya Serikali na Wadau wa Maendeleo wametakiwa kutumia takwimu zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika kupanga na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini.
 Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika leo jijini Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa matumizi ya takwimu bora ndio msingi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
 “Leo tunasherehekea Siku ya Takwimu Afrika, siku ambayo inatukumbusha umuhimu wa Takwimu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya taifa letu. Ukiwa na takwimu bora utaweza kutoa huduma zilizo bora,” amesema Prof. Mkenda.
 Prof. Mkenda amesema uwepo wa takwimu bora zinazoonesha mahitaji halisi ya wananchi ndio dira katika utaoji wa huduma muhimu za kila siku pamoja na upangaji na utekelezaji wa miradi mingine ya maendeleo ya kitaifa.
 “Maadhimisho haya leo yanazitaka Serikali zetu kuimarisha mifumo ya kitakwimu kwa kuwekeza katika teknolojia ya kisasa ya ukusanyaji, uchambuzi na usambazaji wa Takwimu. Serikali kwa upande wake itahakikisha inaiwezesha Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuwekeza katika teknolojia ya kisasa zaidi ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo ya ukusanyaji wa Takwimu bora na kwa wakati,” amesisitiza Prof. Mkenda.
 Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amesema Siku ya Takwimu Afrika kwa mwaka huu imelenga katika kuufahamisha umma kuhusu umuhimu wa Takwimu bora kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
 “Siku hii ya Takwimu Afrika ni muhimu sana kwetu sisi hasa watakwimu kwani tunaitumia kuelimisha umma juu ya umuhimu wa Takwimu katika mustakabali wa maendeleo ya Taifa,” amesema Dkt. Chuwa.Dkt. Chuwa amesema kupitia maadhimisho haya yanayoongozwa na kauli mbiu ya “Takwimu Bora kwa Maisha Bora”, itawasaidia wananchi kutambua kuwa uwepo wa takwimu bora ndio njia ya upatikanaji wa maendeleo stahiki.
 Nae Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Dkt. Carina Wangwe amesema wakiwa kama watumiaji wakubwa wa Takwimu zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika utekelezaji wa majukumu yao ndio wanathamini mchango wa takwimu rasmi katika kupanga mipango ya maendeleo.
 “Sisi ni wadau wakubwa na watumiaji wa takwimu zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, leo hii tupo hapa ili kushirikiana na ofisi hii ili kuhakikisha teknolojia ya kisasa inatumika katika uboreshaji wa Takwimu na kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma mbalimbali kwa jamii,’ amesema Dkt. Wangwe.
 Siku ya Takwimu Afrika huadhimishwa tarehe 18 Novemba, kila mwaka, Kwa hapa Tanzania maadhimisho haya yamefanyika Novemba 23, 2015 ambapo kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni “Takwimu Bora kwa Maisha Bora”.

Sekeleti achomoza Tamasha la Krismasi, kushukuru

0
0
index
MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili Afrika Mashariki na Kati, Ephraim Sekeleti amethibitisha kuwa mmoja wa waimbaji watakaopanda jukwaa la Tamasha la Krismasi na kushukuru linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama Sekeleti amekubali kuwa mmoja wa waimbaji wa Kimataifa watakaopanda jukwaa la Shukrani ambalo litakuwa katika Sikukuu ya kumbukumbu ya kuzaliwa Masia, Yesu Kristo.

Msama alisema tamasha hilo ni la Shukrani baada ya kuombea amani uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, Tamasha la Maombi lilifanyika Oktoba 4 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

“Tunarudisha heshima na Shukrani kwa Mungu baada ya kuiepusha Tanzania na majaribu yaliyokuwa na mlengo wa kutaka kuvuruga amani ambayo iliasisiwa na baba wa Taifa Mwalim Julius Kambarage Nyerere,” alisema Msama.

Aidha Msama alisema kuandaa tamasha hilo inaonesha namna gani Watanzania tulivyo na shukrani ambako Watanzania tukumbuke kwamba Tukipewa, Tusisahau kushukuru.

Ujumbe mzito ambao ni kumbukizi kwa Wanadamu ni kwamba binaadam tunapobarikiwa na Mungu hatuna budi kushukuru, hivyo tamasha hilo ni shukrani baada ya Mungu kusikia vilio vya Watanzania baada ya kuisaidia Tanzania katika uchaguzi Mkuu.  

MASHAUZI CLASSIC KUZINDUA ALBAM YA “SURA SURAMBI” NOVEMBA 26 MANGO GARDEN

0
0
Hatimaye albam ya “Sura Surambi” iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa taarab, inazinduliwa Alhamisi hii Novemba 26.

Albam hiyo kutoka kwao Mashauzi Classic, itazinduliwa ndani ya ukumbi wa Mango Garden Kinondoni huku kundi kongwe la taarab East African Melody, likizindikiza tukio hilo kubwa.

Mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Mashauzi ameuambia mtandao huu kuwa albam ya “Sura Surambi” inaundwa na nyimbo sita kali.

Ni Alhamisi ya kihistoria ambayo Isha anaitaja kuwa itapambwa na ratiba iliyokwenda shule itakayomwacha mshabiki apate uhondo mwanzo mwisho.

Isha amezitaja nyimbo hizo kuwa ni pamoja na “Sura Surambi” aliouimba yeye, “Kupendwa Bahati Yangu” uimbaji wake Abdumalick Shaaban, na “Mjinga Mpe Cheo” wa Zubeida Malick.

Nyimbo nyingine alizozitaja Isha ni “Pendo la Ukakasi” wa Saida Ramadhan, “Ubaya Haulipizwi” ulioimbwa na Asia Mzinga na “Mapenzi Yamenivuruga” mwimbaji akiwa ni Naima Mohamed.

Nyimbo zote hizo sita zimetungwa na Isha Mashauzi.

Mbali na Melody, mkali wa tungo za mapenzi wa muziki wa kizazi kipya Cassim Mganga naye pia atasindikiza uzinduzi huo wa “Sura Surambi” ndani ya Mango Garden Alhamisi hii.

Kipindi cha Jukwaa Langu Nov 23 2015 (MJADALA)

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk John Magufuli akizindua Bunge la 11
Kipindi hiki hukujia kila jumatatu kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Marekani ya Mashariki kuijadili Tanzania ya sasa na ile tuitakayo.Katika kipindi hiki tumejadili (mbali na mambo mengine) muelekeo wa serikali ya Tanzania baada ya kuzinduliwa kwa Bunge la 11. Mjadala huu ambao ulifuata HABARI kutoka magazeti mbalimbali, umehusisha wadau toka Marekani, Canda na India Karibu.Waweza kutusikiliza kupitia tovuti zetu www.kwanzaproduction.com na www.vijimamboradio.com

WANAFUNZI WA UTURUKI NA BOSNIA WAFANYA ZIARA KATIKA KISIWA CHA TUMBATU ZANZIBAR.

0
0
  Wanafunzi kutoka Uturuki na Bosnia wakiwa katika Boti kuelekea katika kisiwa cha Tumbatu kwa ajili ya kuwatembelea wanafunzi wa madrasa na wananchi mbalimbali katika ziara yao ya siku mbili ili kujenga urafiki baina yao na watu wa Zanzibar.
 Wanafunzi kutoka Uturuki na Bosnia wakiwa katika Kisiwa cha Tumbatu kwa ajili ya kuwatembelea wanafunzi wa madrasa na wananchi mbalimbali katika ziara yao ya siku mbili ya kujenga urafiki baina yao na watu wa Zanzibar.
 Wanafunzi kutoka Uturuki na Bosnia wakiwasalimia wanafunzi wa madrasa na walimu waliokuja kuwa pokea katika Kisiwa cha Tumbatu katika ziara yao ya siku mbili ya kujenga urafiki baina yao na watu wa Zanzibar.

 -Wanafunzi kutoka Uturuki na Bosnia wakiwa katika picha ya pamoja na  wanafunzi wa madrasa na walimu  katika Kisiwa cha Tumbatu katika ziara yao ya siku mbili ya kujenga urafiki baina yao na watu wa Zanzibar.

 -Wanafunzi kutoka Uturuki na Bosnia wakipata dua kwa Mzee wa Kisiwa cha Tumbatu na kutoa msaada wa chakula ikiwa pamoja na Mchele Unga wa ngano,Sukari na Mafuta ya kupikia  katika ziara yao ya siku mbili ya kujenga urafiki baina yao na watu wa Zanzibar.
Kiongozi wa Wanafunzi Omar akimkabidhi Mzee wa kijiji cha Tumbatu Msaada wa Chakula katika ziara yao ya siku mbili ya kujenga urafiki baina yao na watu wa Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

WANAFUNZI WA UTURUKI NA BOSNIA WAFANYA ZIARA KATIKA KISIWA CHA TUMBATU ZANZIBAR.

0
0
 Wanafunzi kutoka Uturuki na Bosnia wakiwa katika Boti kuelekea katika kisiwa cha Tumbatu kwa ajili ya kuwatembelea wanafunzi wa madrasa na wananchi mbalimbali katika ziara yao ya siku mbili ili kujenga urafiki baina yao na watu wa Zanzibar.
 Wanafunzi kutoka Uturuki na Bosnia wakiwa katika Kisiwa cha Tumbatu kwa ajili ya kuwatembelea wanafunzi wa madrasa na wananchi mbalimbali katika ziara yao ya siku mbili ya kujenga urafiki baina yao na watu wa Zanzibar.
 Wanafunzi kutoka Uturuki na Bosnia wakiwasalimia wanafunzi wa madrasa na walimu waliokuja kuwa pokea katika Kisiwa cha Tumbatu katika ziara yao ya siku mbili ya kujenga urafiki baina yao na watu wa Zanzibar.
 Wanafunzi kutoka Uturuki na Bosnia wakiwa katika picha ya pamoja na  wanafunzi wa madrasa na walimu  katika Kisiwa cha Tumbatu katika ziara yao ya siku mbili ya kujenga urafiki baina yao na watu wa Zanzibar.

 Wanafunzi kutoka Uturuki na Bosnia wakipata dua kwa Mzee wa Kisiwa cha Tumbatu na kutoa msaada wa chakula ikiwa pamoja na Mchele Unga wa ngano,Sukari na Mafuta ya kupikia  katika ziara yao ya siku mbili ya kujenga urafiki baina yao na watu wa Zanzibar.
Kiongozi wa Wanafunzi Omar akimkabidhi Mzee wa kijiji cha Tumbatu Msaada wa Chakula katika ziara yao ya siku mbili ya kujenga urafiki baina yao na watu wa Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

SERIKALI YATOA UFAFANUZI JUU YA UPATIKANAJI WA VIBALI VYA KUSAFIRISHA MAZAO NJE YA NCHI

0
0
SERIKALI leo imetoa ufafanuzi kuhusu upatikanaji wa vibali vya kusafirisha mazao kwenda nje ya nchi ambapo imesisitiza kuwa vibali hivyo vinapatikana bila gharama  na hakuna urasimu wowote.


Akitoa ufafanuzi huo, Mwanasheria wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bwana George Mandepo (Pichani) alisema kuwa vibali vya kusafirisha mazao ya kilimo nje ya nchi, hutolewa bila gharama na kuongeza kuwa biashara hiyo inaweza kufanywa na mtu yeyote, kinachotakiwa ni mhusika kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.


Bwana Mandepo aliongeza kuwa, uuzaji wa mazao nje ya nchi, unasimamiwa na Sheria ya Usalama wa Chakula iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2009, inayojulikana kama Sheria ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (Serial and Other Produce Act, 2009) inayompa mamlaka Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika kutoa kibali cha kuuza mazao nje ya nchi kwa mtu mwenye vigezo.


Sheria hiyo pia, inampa mamlaka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, kukasimu madaraka ya kutoa vibali kwa Makatibu Tawala wa Mikoa wakati wa dharura kama ilivyokuwa katika msimu wa kilimo wa 2013/2014 ambapo Taifa lilikuwa na ziada ya kutosha.


Bwana Mandepo aliongeza kuwa, katika Sheria hiyo inamtaka mfanyabiashara kuainisha aina ya mazao na  kiwango ambacho anataka kusafirisha, lengo ni kuhakikisha kuwa, Serikali inakuwa na takwimu kamili za mazao yanayosafirishwa nje ya nchi.


Baadhi ya masharti nafuu ambayo mfanyabiashara anatakiwa, kuyafuata ni pamoja na kuwasilisha taarifa zake binafsi kama Jina lake kamili au Jina la Kampuni, anuani ya makazi, au eneo analotoka na uthibitisho wa mazao anayotaka kusafirisha nje ya nchi.


Aidha, Bwana Mandepo aliongeza kuwa Mfanyabiashara wa mazao kwenda nje ya nchi atapaswa kuwa na Cheti cha ubora wa mazao husika anayosafirisha, kinachojulikana kama ‘phytosanitary certificate’ kwa mujibu wa  Sheria inayosimamia ubora wa mazao (The Plant Protection Act 1997). Sheria hiyo inataka mazao yanayosafirishwa nje au kuingizwa nchini, yawe na ubora unaokubalika Kimataifa.


Bwana Mandepo alimalizia kwa kutoa wito kuwa nafasi ipo wazi kwa kila Mtanzania kuchangamkia fursa ya kusafirisha mazao nje ya nchi kwa kuwasilisha  maombi ya kibali kwa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kwa ajili ya kupata kibali hicho na kwamba Mfanyabiashara anayewasilisha maombi yake, anapaswa kuambatanisha leseni yake ya biashara, cheti cha mlipakodi na awe na idhini ya maandishi kutoka Wilaya au Mkoa ambako mazao husika yanatoka.

UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETINI

0
0
SIMU.TV: Rais Magufuli asitisha shamra za uhuru. Wasomi, wanasiasa watoa ya moyoni. CCM yashinda Ubunge Lushoto;
 SIMU.TV: Mahakama leo kuamua kuagwa ama la mwili wa mwenyekiti Mwanzo. Polisi wapiga marufuku kujichukulia sheria mkononi; https://youtu.be/LP9X-KNvLas
SIMU.TV: Ikulu yawatikisa wafanyabiashara nchini.  Taharuki CHADEMA, mtoto wa kigogo asahaulika nafasi za viti maalumu; https://youtu.be/o2GcUXkkso0  
SIMU.TV: Kili Stars, Zanzibar Heroes majaribuni leo michuano ya Chalenji. Minziro aibukia Afrika Sports. Mavungo ndani ya 18 Simba; https://youtu.be/JzJ23lyUwvg 
SIMU.TV: Familia ya Mawazo yatinga korti kuu, Waziri Mkuu awataka wafanyakazi katika ofisi yake kuwahudumia vyema wananchi; https://youtu.be/J-a7ogZRXUg

POP UP BONGO KUFANYIKA JUMAMOSI HII TRINITI OYSTERBAY DAR ES SALAAM

0
0
Na Mwandishi Wetu
WASANII mbalimbali wa muziki na maigizo pamoja na wadau wengine wa biashara watajumuika pamoja Triniti, Oyster bay katika tamasha la biashara za bidhaa mbalimbali, Pop Up Bongo. 

Tamasha hilo linalofanyika kila baada ya miezi mitatu ni la siku moja na mwaka huu litafanyika tarehe 28 likiwa chini ya udhamini wa kinywaji cha Smirnoff. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Akizungumzia kuhusiana na tamasha hilo mmoja kati ya waanzilishi wake, Natasha Stambuli alisema kuwa milango itafunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi na kuwa linatarajiwa kumalizika saa mbili usiku.

Alisema kuwa ikiwa ni kuelekea msimu wa sikukuu za Christmas na mwaka mpya tamasha hilo linawakutanisha watu mbalimbali na wamiliki wa maduka na wafanyabiashara za aina mbalimbali. 

Alikuwa inakuwa ni nafasi nzuri kwa watu mbalimbali pia kukutana na mbali na kufanyika kwa biashara kwenye eneo hilo lakini pia inakuwa ni fursa ya kuburudika kwa kuwa kutakuwa na muziki na vinwaji hivyo kuongeza furaha kwa watakaojitokeza. 

"Ni mwishoni mwa mwaka tunaelekea na kama mnavyojua kunakuwa na mambo mbalimbali wakati tukielekea kufunga mwaka vijana wanataka kujua wapi pa kununua bidhaa mbalimbali kama nguo na vinginevyo na Pop Up bongo inawapatia fursa hiyo hapo Novemba 27" alisema Natasha.

Aliongeza kuwa "kwa mwaka huu wasanii pia wapo ambao watafika kuonana nao wadau wengine wa bidhaa zinazowahusu kama nguo na nyinginezo na hakuna kiingilio kabisa.

Alisema kuwa wafanyabiashara ambao kwa mwaka huu wataonesha bidhaa zao ni pamoja na Secret Habits, KAYA African Collection, Nuya’s Essence, HIGHSUPDSM, FT boutique, Branoz Collections, ATSU, Dress Kitenge, American Nails na wengineo wengi.

Nuya Essence kushoto akimhudumia mteja.
Mwanzilishi wa Branoz Collection Bahati Abraham akiwa na wateja.
Wateja wakihudumiwa.
Mwanzilishi wa 
PSJ Brand,
 Pediah John, (aliyekaa) akiwa na wateja.

RC KILIMANJARO,AMOSI MAKALA AKUTANA NA MAOFISA WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI KUZUNGUMZIA JUU YA HOFU YA KIPINDUPINDU.

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala akiwa katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi,kuzingumza na watendaji wa Afya na Mazingira.
Baada ya agizo hilo mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga alifanya ziara katika dampo lilopo Kaloleni kujinea tatizo lililosabaisha magari ya kubeba taka kushindwa kuendelea na zoezi hilo. 
Katapila likijaribu kusawazisha takataka katika eneo hilo la dampo ili kurahisisha utupwaji wa taka katika eneo hilo. 


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala akifurahia jambo mara baada ya kukutana na watendaji wa Halmashauri kuzungumzia juu ya hofu ya Ugonjwa hatari wa Kipindupindu.kushoto kwake ni kaimu mkurugenzi wa Manispaa hiyo Jeshi Lupembe. 
Baadhi ya watendaji. 
 Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Novatus Makunga akiwa na mmoja wa maofisa wakifuatilia maelelzo yaliyokuwa yakitolewa ofisini hapo. 
 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala akizungumzia changamoto iliyojitokeza hivi karibuni ya kujaa kwa dampo la kutupa taka hali iliyosababisha mrundikano wa takataka katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi,Hapa alikuwa akitoa agizo taizo hilo kushughulikiwa mara moja. 
Wakati zoezi la kurekebisha barabara katika eneo la dampo likiendelea,mmoja wa wananchi kkatika eneo hilo alikuwa na shughuli ya kujiokotea vitu ambayo anadhani vitamsadia katika kujipatia kipato. 
Mifugo aina ya Mbuzi pia wamekuwa wakifanya eneo hilo la dampo kama sehemu ya kujipatia chakula. 
Wafanyakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakizoea taka zilizokuwa zimerundikana katika eneo la jirani kabisa na soko la Manyema mjni hapa. 
 Shughuli ya uzoaji taka ikiendelea. 
Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Novatus Makunga akizungumza namna ambavyo utekelezaji wa agizo la mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro lilivyoanza ikiwa ni njia moja wapo ya kukabiliana na Ugonjwa hatari wa Kipindu pindu. 
Hivi ndiyo hali iliyokuwa katika soko la MANYEMA. 
DC Makunga akijionea hali halisi. 
Moja ya dampo likiwa limejaa taka.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. 



Viewing all 46200 articles
Browse latest View live




Latest Images