Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

WENGI WAJITOKEZA KATIKA UZINDUZI WA MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE JIJINI DAR ES SALAAM

0
0

Maandamano yakipokelewa na Mkurugenzi wa shirika la misaada la Marekani USAID Daniel Moore, Mwakilishi wa Balozi wa Ireland nchini Maire Matthews, Mwakilishi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa Wanawake Lucy Melele, Mkurugenzi wa shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo barani Afrika - WiLDAF, Dr. Judith Odunga, pamoja na wawakilishi wa mashirika wahisani na viongozi mbalimbali.
Dr. Judith Odunga kutoka WiLDAF akiwakaribisha wageni.
Mwanaharakati mama Siwale, Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Anna Mghwira(wa kwanza kulia) ni miongoni mwa waliohudhuria maadhimisho hayo.

Wageni mbalimbali
Maigizo kuhusu uchapaji wa viboko kwa wanafunzi
Mwakilishi wa Balozi wa Ireland Maire Matthews akizungumza
Lucy Melele kutoka shirika la UN Women akizungumza

Mwalimu akitoa ushuhuda




Paulina Mkonongo(wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Akisikiliza jambo






Mgeni rasmi Bi. Paulina Mkonongo Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi akitembelea sehemu za maonyesho kutoka kwa mashirika mbalimbali.




Baadhi ya wadau wakitembelea mabanda


Wadau mbalimbali waliohudhuria maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake.


Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake leo yamefunguliwa rasmi kwa kuanza na maandamano ya amani yaliyoanzia uwanja wa Tipi Sinza darajani hadi ukumbi wa hoteli ya Blue Pearl iliyopo jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es salaam.

Maandamano hayo yalihudhuriwa na maelfu ya watu yaliongozwa na bendi ya jeshi la polisi kupitia njia za Shekilango kisha barabara ya Morogoro hadi katika jengo la Ubungo Plaza ambapo yalipokelewa na Mkurugenzi wa shirika la misaada la Marekani USAID Daniel Moore, Mwakilishi wa Balozi wa Ireland nchini Maire Matthews, Mwakilishi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa Wanawake Lucy Melele, Mkurugenzi wa shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo barani Afrika - WiLDAF, Dr. Judith Odunga, pamoja na wawakilishi wa mashirika wahisani na viongozi mbalimbali.

Akitoa neno la ukaribisho, Dr. Judith Odunga alisema kampeni ya siku 16 kwa mwaka huu imelenga zaidi kuzungumzia suala zima la usalama mashuleni. Lengo kuu ikiwa kuhamasisha umma kuhusu ukubwa wa ukatili wa kijinsia kwa vijana na watoto wetu mashuleni.

“Ni kutokana na unyeti wa tatizo la ukatili wa kijinsia mashuleni, WILDAF na wadau mbalimbali tumeona kuna umuhimu wa kushirikisha Wizara ya elimu na ufundi stadi ili kuzungumzia ukatili wa kijinsia mashuleni na kujenga mikakati ya kuzuia ukatili huo” Aliongezea.

Dr. Odunga aliitaja kauli mbiu ya mwaka huu kuwa ni FUNGUKA! CHUKUA HATUA, MLINDE MTOTO APATE ELIMU. “Kauli hii inalenga kumshawishi mtu binafsi, kuwashawishi walimu, wanafunzi, wazazi na jamii kwa ujumla, kuwalinda watoto dhidi ya ukatili wa kijinsia na kuhakikisha kwamba shule ni mahala salama. Ni vyema kutafakari kwa kina jinsi vitendo vya ukatili wa kijinsia mashuleni vinavyoathiri maendeleo ya watoto wetu kielimu.” Alisema Dr. Odunga.


Dr. Odunga alitumia nafasi hiyo kuiomba serikali kufanya yafuatayo:


1. Kufutwa kabisa kwa adhabu ya viboko mashuleni na waalimu kufundishwa au kutafuta mbinu za kutoa adhabu mbadala.


2. Kutengeneza mwongozo wa utekelezaji wa sera ya elimu ya mwaka 2014 utakaoelekeza upatikanaji wa elimu ya msingi iliyo bora na salama.

3. Kuboresha miundombinu rafiki ya elimu ikiwa ni pamoja na kuwa na madarasa ya kutosha, madawati, vyoo na sehemu za kujisitiri watoto wa kike, mabweni, uzio pamoja na kuwa na usafiri wa uhakika kwa wanafunzi.
4. Serikali kuweza kuunda na kusimamia mabaraza yatakayo kuwa yanasikiliza malalamiko ya wanafunzi mashuleni
5. Tunaomba Wizara ya elimu na ufundi stadi kushirikiana na wizara ya Katiba na Sheria na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kutunga Sheria ya Ukatili wa Majumbani sambamba na kubadilisha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 inayoruhusu ndoa kwa mtoto chini ya miaka 18.

Akifungua rasmi kampeni hizi, mgeni rasmi Paulina Mkonongo ambaye ni Mkurugenzi wa Elimu ya sekondari kutoka Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi aliyemuwakilisha Katibu mkuu wa wizara hiyo alisema, “ukatili wa kijinsia huleta athari hasi katika utoaji na upatikana wa fursa mbalimbali za kijamii ikiwemo fursa ya elimu kwa watoto wetu, hivyo kuwa ni kikwazo katika kujenga usawa wa kijinsia nchini.

Aidha Mkonongo alisema serikali imefanya juhudi za makusudi kuzuia ukatili na kuleta usawa katika kupambana na ukatili wa kijinsia kwa kuweka sera na mipango inayozingatia usawa na kupinga ukatili kwa makundi mbalimbali, katika jamii ukiwemo ukatili wa kijinsia.

Mkonongo alitoa wito kwa wananchi wote kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili na kwamba kila mtoto ana haki ya kulindwa popote anapokuwepo iwe nyumbani, shuleni, kwenye vyombo vya usafiri, michezoni na njiani wanapokwenda na kurudi shuleni pia kuwapa mbinu za kujilinda wenyewe.

Naye mwakilishi wa Balozi wa Ireland nchini Bi. Maire Matthews alisema kuwa takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa wastani wa asilimia 45 ya wanawake Tanzania wenye umri kati ya miaka 15 – 49 waliripoti kuwahi kufanyiwa ukatili wa kimwili au kingono katika maisha yao. Alisema takwimu nyingine zinakadiria kiwango hicho kuwa kati ya 41 – 56%.

Kwa upande wake Lucy Melele kutoka shirika la UN Women aliyemwakilisha Mwakilishi wa shirika hilo hapa nchini Anna Collins alisema wanawake na wasichana ulimwenguni kote wanapitia aina mbalimbali za ukatili ambayo inawanyima haki zao za msingi, ni tishio la demokrasia na ni kizuizi cha amani ya kudumu. Hata hivyo alisema shirika la umoja wa mataifa litaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na wadau wa maendeleo, serikali, mashirika mbalimbali, na jamii katika kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia pia inafanyika kikanda katika kanda ya ziwa (Mwanza, Mara na Shinyanga, kanda ya Kaskazini (Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga), kanda ya kati (Dodoma, Morogoro na Singida), kanda ya Kusini (Mtwara, Songea, Mbeya, Iringa na Lindi, Kanda ya Pwani (Dar es salaam na Pwani) zikisimamiwa na wadau mbalimbali wakiwemo mashirika ya Kivulini, CWCA, NAFGEM, Morogoro Paralegal, Mtwara paralegal, WiLDAF, TWCWC pamoja na jeshi la Polisi. 






Maelfu wajitokeza katika maandamano ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, hapa wakiendelea na matembezi ya kupinga ukatili wa Kijinsia

PAPA FRANCIS ALAKIWA NA RAIS UHURU KENYATA JIJINI NAIROBI

0
0


Papa Francis akisalimiana na Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta wakayi alipowasili nchini Kenya leo ambapo atakuwa na ziara ya siku sita katika nchi za Afrika. Kushoto ni Mke wa Rais Kenyatta, Magret Kenyatta. 
Papa Francis  amewasili jana nchini Kenya hapo jana,ambapo anatarajia kuwa na ziara ya siku sita  katia nchi za Afrika kiwemo Uganda.

 Papa Francis akizungumza jambo na Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili nchini Kenya jana ,ambapo leo atakuwa na ziara ya siku sita katika nchi za Afrika. Kushoto ni Mke wa Rais Kenyatta, Magret Kenyatta.
 Papa Francis akisaini kitabu cha wageni Ikulu,huku
Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta na Mkewe Magret wakishuhudia


 Picha ya Pamoja na Marais Wastafu wa Kenya,Mh Daniel Arap Moi na wa pili kutoka kulia ni Mwai Kibaki

WAKAZI WA MIKOA YA MANYARA,ARUSHA NA KILIMANJARO WAJITOKEZA UZINDUZI WA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA.

0
0


Maandamano hayo yakipita eneo la kituo kuu cha Mabasi cha mjini Moshi yakieekea katia viwanja vya kituo hicho ambako uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini .

Mkuu wa wilaya ya Moshi Novatus Makunga aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kujinsia kanda ya kaskazini akimsikiliza Mwenyekiti wa Mwavuli wa Vikoba wa KIVINET ,Mama Mwingira wakati alipotembelea banda la KIVINET .

Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akisikiliza malezo kutoka katika banda la shirika la NAFGEM linalopambana na vitendo vya Ukeketaji.

Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akisikiiza maelezo kutoka TAWREF ambao pia wameshiriki katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.



Afisa habari wa shirika la KWIECO ,Velonica Ollomi akitoa maelezo mbele ya mgeni rasmi katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini uliofanyika katika viwanja vya kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi,kulia kwake ni Afisa Kitengo cha elimu ya haki za binadamu na jinsia ,KWIECO ,Elizabeth Mushi.

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi,MUWSA ,pia imeshiriki katika uzinduzi huo hapa ikiwasilishwa na afisa habari wake,Florah Nguma na mfanyakazi wa mamlaka hiyo,Kisingi.

Mwenyekiti wa kamati ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini,Honorata Nasuwa akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika katika viwanja vya kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi.








Kikundi cha kwaya kutoka shule ya msingi Mweleni wakitoa ujumbe kwa njia ya wimbo wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili kanda ya kaskazini.







Mkurugenzi wa shirika la Tusonge,Agnata Rutazaa akizungumza katika uzinduzi huo.







Mkurugenzi wa TAWREF,Dafrosa Itemba akitoa mada katika uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini.









Mkurugenzi wa shirika la KWIECO,Elizabeth Minde akitoa mada katika uzinduzi huo.









Mwakilishi wa mkuu wa shule ya Polisi Tanzania na Mkufunzi mkuu wa shule hiyo Graifton Mushi ,akiwa na aliyekuwa mwenyekiti wa dawati la Jinsia mkoa wa Kilimanjaro,Grace Lyimo katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.







Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akiteta jambo na mkurugenzi wa shirika la KWIECO,Elizabeth Minde.







Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga aliyekuwa mgeni trasmi katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini akitoa hotuba yake.







Baadhi ya wasiriki katika uzinduzi huo wakifutilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.










Brass Band ya Chuo cha Polisi Moshi ikiongoza maandamano ya uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini .







Wanafunzi wa kozi ya awali ya Askari Polisi kutoka shule ya Polisi Tanania wakiwa katika manda,ano ya uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kanda ya Kaskazini.








Maanda,mano ya lipita maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya kaskazini.

MUULIZE MO!: TUANDIKIE MASWALI YAKO KUMUULIZA MOHAMMED DEWJI (CEO WA METL GROUP) TUTAKUWA NA MAHOJIANO NAYE HIVI KARIBUNI

0
0
mo
Msomaji na mdau wa mtandao wako wa habari www.modewjiblog.com unakupa nafasi wewe kumuuliza maswali/swali lolote lile Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL Group, Mohammed Dewji. Maswali yote yatajibiwa na kutolewa ufafanuzi wa kina. Tutakuwa na mahojiano naye karibuni. Asanteni sana.

Utaratibu wa kumuuliza maswali ni kwa kukomenti kwenye post hii kisanduku cha maoni, Zingatia Kanuni na sheria ikiwemo kutotumia lugha zisizo rasmi.

Pia waweza kutoa maoni yako kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ukiwemo ukurasa wa Mohammed Dewji : https://www.facebook.com/mohammeddewjitz/ au Ukurasa wa Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL):https://www.facebook.com/MeTLGroup/photos

CHUKO KIKUU CHA USHIRIKA NA BIASHARA,MOSHI PAMOJA NA CHAMA CHA SOKA CHA MKOA WA KILIMANJARO VYAPIGWA JEKI

0
0

Meneja masoko wa Kampuni ya Megatrade Investment ya jijini Arusha,Edmund Rutaraka akimkabidhi hundi ya kiasi cha shilingi Milioni 1.5 ,katibu wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro ,KRFA,Mohamed Musa kwa ajili ya kusadia ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa iliyoanza hivi karibuni.

Mweka hazina wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro,Kusianga Kiata,akitizama hundi iliyotolewa na kampuni ya Megatrade Investment ya jijini Arusha.
Baadhi ya wadau wa soka waliofika kushuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo jengo la Voda House.
Meneja Masoko kanda ya Kaskazini ,Edmund Rutaraka akimkabidhi Makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Ushirika na Biashara ,Moshi,( MOCU),Profesa Faustine Bee hundi ya kiasi cha shilingi Mil 2 kusaidia maeneo mbalimbali yenye changamoto chuoni hapo.
Meneja Masoko wa kampuni ya Megatrade Investment ya jijini Arusha,Edmund Rutaraka akizungumza jambo mara baada ya kukabidhi hundi kwa mkuu huyo wa chuo.
Makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Ushirika na Bashara (MOCU) Profesa Faustine Bee akizungumza mara naada ya kukabidhiwa hundi hiyo.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

BARCLAYS YATOA HUNDI YA ASILIMIA 100 KWA MTEJA KUPITISHA MSHAHARA KATIKA BENKI HIYO

0
0



Meneja wa kitengo cha Bidhaa –Wateja wa Rejareja wa Benki ya Barclays,Valence Ruteganya akizungumza na waandishi wa habari juu ya kampeni ya wateja kupata asilimia 100 ya mshahara kwa kupita katika akaunti ya benki ya Baclays katika hafla ya kumkabidhi mteja aliyepitisha mshahara wake na kupata asilimia 10 iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam,kushoto Meneja wa Kanda ya Namba Moja,Kitumari Massawe kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa –Wateja wa Rejareja,Oscar Mwamfwagasi.
Meneja wa Kanda ya Namba Moja,Kitumari Massawe akimkabidhi mfano wa hundi kwa Julius Odinga aliyeshinda asilimia 100 baada ya kupitisha mshahara wake katika benki hiyo anayeshuhudia ni Meneja wa Tawi la Mikocheni wa Benki ya Barclays,Veronica Mcharo katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Chalila Kibuda wa Globu ya Jamii)

SHIWATA kugawa nyumba 14 Mkuranga, yampongeza Dkt. Magufuli kumteua Majaliwa Waziri Mkuu

0
0
 MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)umeandaa mkutano wa wanachama wake Jumamosi kutangaza majina ya wanachama watakaokabidhiwa nyumba 13 na misingi ya nyumba 14 katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga.

Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam jana kuwa mkutano huoutakaofanyika Ilala, Bungoni Dar es Salaam kuanzia saa 4 pia watatangazwa viongozi watakaoshika nafasi za uongozi zilizo wazi.

Nafasi za uongozi zilizo wazi ni Makamu Mwenyekiti iliyokuwa ikishikiliwa na Marehemu Kepteni John Komba,Katibu ambayo ilikuwa inashikiliwana Selemani Pembe ambaye yupo India kikazi na Mweka Hazina ambaye Flowin Nyoni ambaye ni Mhadhiri wa Chuko Kikuu cha Dodoma.

Katika hatua nyingine SHIWATA imeupongeza uongozi wa Rais John Pombe Magufuli kumteua Mkufunzi wa Mpira wa Miguu wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.

Alisema medani ya michezo inahitaji msukumo wa viongozi wanaojua michezo hivyo ni kipindi cha kujiandaa kuiletea sifa Tanzania kupitia michezo ya soka, ndondi, riadha,netiboli na mingine katika michezo ya Afrika Mashariki,Michezo ya Afrika, michezo ya madola na michezo ya dunia.

Taalib alisema ili kuonesha viongozi wetu wapya ni wapenda michezo hivi karibuni Rais Magufuli alikubali kuwa mgeni rasmi katika pambano la kuwania kucheza kombe la dunia kati ya Stars na Algeria kwenye uwanja wa Taifa ambapo alimtuma Makamu wa Rais, Suluhu Samia Hassan kumwakilisha hiyo inaonesha Tanzania imepata viongozi wapenda michezo.

Alisema wasanii na wanamichezo watapiga hatua kubwa mbele kwenye uongozi wa Dkt. Magufuli kwani kuna kila dalili kuwa kazi zao zitathaminiwa na kupewa kipaumbele.

Taalib alisema mtandao wa SHIWATA ambao unajumuisha wanamichezo, wasanii, waigizaji, waandishi wa habari na wasanii wa kazi za mikono wamemkubali Dkt. Magufuli kwa kasi aliyoanza nayo ya kufuatilia mambo hasa kuondoa kero za wanyonge ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa hawapati huduma muhimu za kijamii za elimu na afya.

Alisema wasanii wanaimani kubwa na Dkt. Magufuli kwani ni mchapakazi na mtu asiyependa wananchi wake wadhulumike wakiwemo wasanii ambao walizunguka nchi nzima kwenye kampeni zake na kujionea shida za wananchi zinazowakabili wakiomba mahitaji mbalimbali katika nchi yao yenye rasilimali lukuki.

SHIWATA yenye wanachama zaidi ya 8,000 nchini inamiliki hekari 300 za kujenga nyumba za makazi wa bei nafuu ambako nyumba 120 zimekwisha jengwa katika kijiji cha Mwanzega Mkuranga na hekari 500 zilizotengwa kwa ajili ya kilimo zimelimwa na kupanda mazao mbalimbali katika kijiji cha Ngarambe Mkuranga.

KUADHIMISHA SHEREHE 21 ZA WATOTO WA SKULI YA NASARI ISLAMIK MFENESINI ZANZIBAR.

0
0
Mgeni Rasmi Mziwanda ambae ni mlezi wa Skuli ya Nasari islamik Mfenesini katikati Diwani wa Mfenesini Msimu Seif Abdalla kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mfenesini  Kanal Masoud  Ali  wakikagua Jengo la Skuli ya Nasari katika sherehe za ishirini na moja (21)  za skuli hiyo.
Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Nasar Islamik Mfenesini Moh’d Yussuf Juma akimpatia maelezo Mgeni Rasmi Mziwanda juu ya kukwama kwa ujenzi wa Jengo lao jipya kushoto ni Diwani wa Mfenesini Msim Seif Abdalla.
Wanafunzi Sada Hassan na Arafa Hemed wakisoma utenzi katika sherehe hizo.
Mgeni Rasmi Mziwanda  ambae ni mlezi wa Skuli hiyo akizungumza na Wazazi, Wanafunzi ambao pichani hawapo kwenye Sherehe za Mahfali ya Skuli hiyo.
Baadhi ya Wanafunzi wa Skuli ya Nasari ya Islamik Mfenesini waliohudhuria katika Sherehe hizo.
Mgeni Rasmi Mziwanda akimkabidhi Sh. 500,000/ Mwalimu Rehema Sleiman kwa niaba ya Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo katikati Diwani wa Mfenesini Msim Seif Abdalla kushoto Mwalimu Mkuu Moh’d Yussuf Juma wakishuhudia. PICHA NA ABDALLA OMAR (MAELEZO ZANZIBAR).

Serikali yaweka mpango wa kutambua na kukuza watu wenye ujuzi wa chini na stadi za kazi.

0
0

LEAT WATOA MIZINGA 350 KWA VIKUNDI VYA UFUGAJI NYUKI

0
0
Sehemu ya mizinga hiyo iliyokabidhiwa.
Afisa Utumishi, Allan Mwela akikabidhi moja ya mizinga kwa mwanachama wa kikundi cha wafuga nyuki kutoka kijiji cha Utosi kilichoko wilaya ya Mufindi 
Baadhi ya wafugaji nyuki wakisikiliza hotuba ya mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela. (picha na Denis Mlowe.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesera akizungumza na wafugaji mara baada ya kukabidhi mizinga ya nyuki.
Mkuu wa wilaya Richard Kasesela akikabidhi moja ya mizinga 175 kwa mfugaji nyuki kutoka Kiwele.( PICHA NA NA DENIS MLOWE, MUFINDI).


NA DENIS MLOWE, MUFINDI

TIMU ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) umetoa jumla ya mizinga ya kufugia nyuki 350, kwa vikundi 16 vya wilaya ya Mufindi na Iringa vilivyoko katika mkoa wa Iringa.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa mizinga hiyo iliyofanyika katika kata ya Sadan wilayani Mufindi juzi, Afisa mradi wa LEAT kutoka Mufindi Jamal Juma alisema lengo la mradi huo ni kuimarisha uhifadhi wa mazingira na kuongeza kipato cha jamii kwa njia ya kufuga nyuki na kupanda miti.

Alisema kuwa malengo mengine mahususi ya mradi huo ni kuleta ufanisi wa kulinda, kutunza na kutumia kwa njia endelevu rasilimali za misitu na kuongeza kipato cha mwananchi mjasiriamali mara baada ya mauzo ya asali iliyovunwa kupitia mizinga hiyo.Alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache yenye utajiri mkubwa wa rasilimali za asili mathalani misitu na wanyapori hivyo kuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Juma alisema kuwa kutokana na hali hiyo kuna changamoto mbalimbali za usimamizi na uhifadhi zikiambatana na uchomaji moto ovyo, kuchoma mkaa,ukataji miti uliokithiri na ujangiri mambo ambayo inasababisha hasara kwa taifa.Alisema kuwa kutokana na changamoto hizo husababisha umaskini, kukauka kwa vyanzo vya maji kutoweka kwa uoto wa asili na kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabia nchi.

“ Mradi huu utasaidia sana jamii ya watu wa wilaya ya Mufindi walioko katika vikundi vya ufugaji nyuki kuhakikisha unaboresha kipato kwa kuendesha mafunzo ya ufugaji nyuki na uvunaji, upandaji miti,kusaidia jamii kwa kuzipatia vitendea kazi vya ufugaji nyuki kama hivi ambavyo leat imetoa kwa kusaidiana na USAID utasaidia kuondokana na changamoto zote hizo endapo utafanyiwa kazi kwa umakini. “ alisema

Alisema kuwa awamu ya kwanza ya mradi vimenufaisha vikundi 8 vyenye watu 22 vilivyoko katika vijiji vya Lugoda, Lutali, Igombalavanu, Uhimbila, Mapogoro, Utosi, Tambalang’ombe, Kibada na Nyololo katika wilaya ya Mufindi na vikundi 8 katika wilaya ya Iringa ambapo kila kikundi kimepata mizinga 22 kama mtaji .

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mufundi,Joika Kasunga katika hotuba yake iliyosomwa na Afisa Utumishi, Allan Mwela amewaasa wananchi wanaokaa pembezoni mwa misitu kuacha kufanya shughuli za uhalibifu wa msitu ikiwemo uchomaji moto kwa ajili ya uwindaji shughuli za kilimo pamoja na uchomaji wa mkaa.

Aidha amewataka wananchi wa kuitunza vizuri misitu ili kuweza kuendelea kupata mvua kwa wingi na kuondokana na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyopo kwa sasa kwani misitu inavyoathiliwa na wananchi kwa matumizi ya kila siku na kusema kuwa chanzo cha misitu hiyo kuharibika ni kutokana na wananchi wenyewe.

“Uhifadhi wa misitu sio suala la mtu mmoja au kundi moja ila la watu wote hii inatokana na ukweli kwamba madhara yatokanayo na uaribifu wa mazingira hayana mipaka na humpata kila mtu hivyo ni wajibu wa kila mtanzania kushiriki katika kulinda maliasili” alisema .

Aliwapongeza Leat kwa kuweza kuwasadia wajasiliamali walioko katika vikundi vya kuondokana na umaskini kwa njia ya ufugaji wa nyuki.

Zoezi la Usafi wa Mazingira Kuwa Endelevu Jijini Dar es Salaam

0
0


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Said Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani) ofisini kwake leo alipokuwa akizungumzia zoezi la usafi na namna mkoa ulivyojipanga kutekeleza zoezi hilo siku ya 9 Disemba.

Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam juu ya usafi wa mazingira siku ya 9 Disemba.


Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi (Kulia) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadiki (Kushoto) alipokuwa akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu utekelezaji wa agizo la Mhe Rais la kufanya usafi wa mazingira katika maadhimisho ya sherehe za uhuru wa Tanzania Bara.
(Picha zote na Raymond Mushumbusi – Maelezo )
…………………………………………………………………………………………………………….
Na Lilian Lundo-MAELEZO
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Mhe. Said Meck Sadiki amesema zoezi la usafi wa mazingira litakalofanyika siku ya Maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Desemba, litakuwa ni endelevu kwa mkoa wa Dar es Salaam hata baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo.

Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Tano. Mhe. Dkt John Pombe Joseph Magufuli aliagiza kuwa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanzania Bara mwaka huu yatumike kwa kufanya usafi wa Mazingira kote nchini badala ya kufanya sherehe za gwaride la askari wa vikosi vya Ulinzi na Usalama.

Akiongea na vyombo vya habari leo Mhe. Sadiki alianza kwa kumpongeza Mhe. Rais kwa uamuzi aliouchukua wa kubadilisha sherehe za uhuru kuwa ni siku ya kufanya kazi badala ya kwenda uwanjani na kuangalia gwaride na halaiki mbalimbali kama ilivyokuwa ikifanyika miaka iliyopita.

“Mhe. Rais katurejesha kule tulipotoka ambako kauli mbiu ya sherehe za uhuru ilikuwa ni uhuru na kazi au uhuru ni kazi wakati watanzania walikuwa wakiungana na kufanya kazi kwa umoja na kushirikiana,” alisema, Mhe. Sadiki.

Aidha, Mhe Sadiki alisema, zoezi la usafi kwa mkoa wa Dar es Salaam litaanza rasmi tarehe 1 Disemba mwaka huu na kumalizikia 9 Disemba mwaka huu siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya uhuru na kuongeza kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu.

Mhe. Sadiki aliongeza kwa kusema kuwa, uongozi wa mkoa umewaomba wadau kujitokeza kwa kuchangia fedha au vifaa kwa ajili ya kufanikisha zoezi hilo na amewataka watendaji kushawishi wananchi wa maeneo yao kutafuta vifaa badala ya kusubiri kuletewa na Halmashauri.

Pia, Mhe Sadiki amewahimiza watendaji wa mitaa na kata kutimiza wajibu wao wa kuhakikisha maeneo wanayoyasimamia yanakuwa katika hali ya usafi muda wote ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko na pale inakapobainika eneo fulani lipo katika mazingira ya uchafu basi mtendaji wa eneo hilo atawajibishwa kwa kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa kosa la kutotimiza wajibu wake. 

Vilevile ametoa wito kwa wananchi kuzingatia usafi kwa kuacha tabia za kutupa taka ovyo hasa wanapokuwa katika vyombo vya usafiri na kutokujisaidia katika mitaro au vichaka ili kuepukana na uchafuzi wa mazingira kunakopelekea kutokea kwa magonjwa ya mlipuko

RAIS WA ZANZIBAR AKABIDHIWA TUNZO

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea Tunzo ya dhahabu iliyopewa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutoka kwa Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana na Watoto Bibi Zainab Omar Mohamed ( Gold Future Policy Award ) kwa mwaka 2015) ambayo imetolewa na Taasisi ya kimataifa ya World Future Council katika Mji wa Geneva Uswizi tarehe 20 Oktoba, 2015 baada ya Sheria ya Watoto ya Zanzibar ya Mwaka 2011 kuzishinda sheria za Nchi nyingine zaidi ya 20 kwa kukidhi vigezo vilivyoshindaniwa,hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika leo Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiiangalia Tunzo ya dhahabu iliyopewa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana na Watoto Bibi Zainab Omar Mohamed ( Gold Future Policy Award ) kwa mwaka 2015) ambayo imetolewa na Taasisi ya kimataifa ya World Future Council katika Mji wa Geneva Uswizi tarehe 20 Oktoba, 2015 baada ya Sheria ya Watoto ya Zanzibar ya Mwaka 2011 kuzishinda sheria za Nchi nyingine zaidi ya 20 kwa kukidhi vigezo vilivyoshindaniwa,hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika leo Mjini Unguja.

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA JESHI LA POLISI

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (katikati), akishiriki kuimba wimbo wa mshikamano kwa wafanyakazi wakati wa kufungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Polisi uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Polisi, Kilwa road, jijini Dar es Salaam. Washiriki wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Polisi wakishiriki kuimba wimbo wa mshikamano kwa wafanyakazi, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza hilo uliofanyika Chuo cha Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Polisi kilichofanyika Chuo cha Polisi, Kilwa Road jijini Dar es Salaam. Washiriki wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Polisi wakiwa katika mkutano Baraza hilo uliofanyika Chuo cha Polisi, Kilwa Road jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Abubakari Akida, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi) .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto), akipokelewa na Maofisa wa Jeshi la Polisi alipowasili Chuo cha Polisi Kilwa Road, kufungua Kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Jeshi hilo, jijni Dar es Salaam. 
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Muhimbili Yapokea Mashine ya kusaidia wagonjwa kupumua

0
0

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN), Profesa Lawrence Mseru akipokea mashine ya ventilator ya kusaidia wagonjwa kupumua endapo wamezidiwa baada ya kuugua. Kushoto ni Mkurugenzi Mauzo wa Mashariki ya Kati na Afrika, Qasem Sumrein akikabidhi mashine hiyo leo.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN), Profesa Lawrence Mseru akitoa ufafanuzi baada ya kupokea mashine hiyo

Daktari Bingwa wa Magonjwa Mahututi na Uzingizi, Moa Kalunga katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akiwaeleza waandishi wa habari umuhimu wa mashine hiyo kwa wagonjwa.

Meneja Mauzo barani Afrika, Gordon Blair akimalizia kufunga mashine ya ventilator ambayo imekabidhiwa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa mashine mojaya Ventilator ya kumsaidia mgonjwa kupumua yenye thamani ya Dola za Kimarekani 36,000 sawa na Shilingi milioni 80. Msaada huo umetolewa leo na Kituo cha kitabibu cha Halmiton chenye makao yake makuu nchini Switzerland . 

Akikabidhi mashine hiyo mpya na kisasa , Mkurugenzi Mauzo wa Mashariki ya Kati na Afrika kutoka Halmiton , Qasem Sumrein amesema pamoja na kutoa msaada huo wataendelea kutembela MHN ili kutoa mafunzo jinsi ya kuitumia pamoja kufanya matengenezo endapo itahitajika kwa kuwa mashine hiyo ina waranti ya miaka miwili. 

Akipokea msaada huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MHN, Profesa Lawrence Mseru ameshukuru msaada huo ambao una lenga kuboresha huduma za afya na kueleza kwamba hospitali hiyo inahitaji kutengeneza ICU nyingine ikiwamo ya mama na mtoto hivyo bado zinahitajika mashine 120 kwa sababu MHN inapokea wagonjwa wengi. 

Akielezea kuhusu mashine hiyo Daktari Bingwa wa Magonjwa Mahututi na Usingizi Moa Kalunga amesema mashine hiyo itamsaidia mgonjwa aliye mahututi kupumua na hivyo kuokoa maisha yake na mgonjwa akirejea katika hali ya kawaida mashine hiyo inaonyesha

Serikali kuendelea kushirikiana na Vijana katika kutatua changamoto zao

0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi ya ngao kutoka kwa Bibi. Dorice Assenga (katikati) kwa niaba ya Vijana kutoka Tanzania walioshiriki mkutano wa tatu wa Vijana kutoka nchi za Bonde la Mto Nile uliofanyika nchini Misri kuanzia tarehe 9 – 16 Novemba 2015 ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu kutoka nchi washiriki. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza na Vijana wa Tanzania walioshiriki mkutano wa tatu wa Vijana kutoka nchi za Bonde la Mto Nile (hawapo pichani) uliofanyika nchini Misri kuanzia tarehe 6 – 14 Novemba 2015 ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu kutoka nchi washiriki. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi

 Baadhi ya vijana wa Tanzania  walioshiriki mkutano wa tatu wa Vijana kutoka nchi za Bonde la Mto Nile uliofanyika nchini Misri kuanzia tarehe 9 – 16 Novemba 2015.Kutoka kushoto ni Baraka Chedego, Paul Simango na Rwihula Daniel
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na Vijana kutoka Tanzania walioshiriki mkutano wa tatu wa Vijana kutoka nchi za Bonde la Mto Nile uliofanyika nchini Misri kuanzia tarehe 9 – 16 Novemba 2015 ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu kutoka nchi washiriki.
Picha na Frank Shija,WHVUM.

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU UTENGENEZAJI NA UCHAPISHAJI WA KAZI ZA XMASS NA MWAKA MPYA.

0
0

VIONGOZI WA KISIASA ZANZIBAR WAKUBALIANA UCHAGUZI MKUU KURUDIWA TENA

0
0
Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi ameimbia RFI Kiswahili kuwa, viongozi wa kisiasa kutoka serikali na upinzani wamekubaliana uchaguzi Mkuu kurudiwa tena.

Hata hivyo, Makamu huyo wa pili amedokeza kuwa hadi sasa haijaafikiwa ikiwa tume ya sasa ya Uchaguzi inayoongozwa na Mwenyekiti Salim Jecha Salim aliyefuta matokeo hayo itakubaliwa kusimamia uchaguzi mpya.

Katika hatua nyingine, kiongozi huyo ameeeleza kuwa rais Ali Mohamed Shein anaendelea kuwa uongozini kikatiba.Wananchi wa Zanzibar wanasubiri uamuzi wa viongozi wa kisiasa kuhusu mvutano huu wa kisiasa katka visiwa hivyo.

Mbunge wa Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD Akiwashukuru Wapiga Kura Wake Wananchi wa Jimbo la Chumbuni

0
0

Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwasalimia Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakati wa mkutano wake wa kutowa shukrani kwa Wapiga kura wake mkutano uliofganyika katika Afisi za Jimbo Tawi la CCM Muembemakumbi Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwasalimia Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakati wa mkutano wake wa kutowa shukrani kwa Wapiga kura wake mkutano uliofganyika katika Afisi za Jimbo Tawi la CCM Muembemakumbi Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar wakati wa mkutano wake wa kutowa shukrani kwa Wananchi wa Jimbo hilo kwa kumchagua kuwa Mbunge wao na kuwataka kuwa wamoja na kujiandaa na maendekleo katika jimbo lake.
 Na kusema sasa makundi basi iliobaki ni Kazi Tu kwa maendeleo ya Wananchi wa Jimbo hilo na kusema yeye ni Mbunge wa Wananchi wa Chumbuni wote 
Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakimsikiliza Mbunge wao wakati wa hafla ya kuwashukuru 
Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakimsikiliza Mbunge wao wakati akitowa shukrani kwa wapiga kura wake katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Afisi ya Jimbo Tawi la CCM Muembemakumbi Zanzibar. 
Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakimsikiliza Mbunge wao wakati akitowa shukrani kwa wapiga kura wake katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Afisi ya Jimbo Tawi la CCM Muembemakumbi Zanzibar.

MBUNGE WA UBUNGO SAID KUBENEA AWATEMBELEA WANANCHI WAKE KUWASHUKURU KUMCHAGUA NA KUJUA CHANGAMOTO ZAO

0
0

 Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Said Kubenea akiongea na wananchi Stendi ya Mabasi ya Ubungo Dar es Salaam leo, kuwashukuru kwa kumchagua na kujua changamoto zao mbalimbali. Mbunge huyo jana alitembelea Soko la Ndizi la Mabibo, Soko la Mabibo, Kituo cha Mabasi cha Mawasiliano  na kumpa pole ya sh. milioni 1.1 Diwani wa Kata ya Manzese, Ramadhani Kwangaya ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Mus’ab kilicho chomwa moto na kuunguza magodoro 30.
 Kubenea akizungumza na waandishi wa habari na wananchi katika Soko la Ndizi la Mabibo.
 Hapa akiwaunga mkono wananchi kununua mananasi katika soko la ndizi la mabibo
 Mbunge Kubenea akisalimiana na wananchi katika soko hilo.
 Wafanyabiashara katika soko la ndizi la mabibo wakimsikiliza mbunge wao Said Kubenea.
 Vijana wakiserebuka baada ya kuzungumza na mbunge wao Said Kubenea katika Soko la Mabibo.
 Mbunge Kubenea akizungumza na viongozi wa soko la Mabibo.
Hapa akiwahutubia wananchi katika soko la Mabibo.

Askofu Mkuu wa Tabora Kuongoza ujumbe wa Tanzania kumuona Papa Francis Uganda.

0
0

Na Joseph Ishengoma, MAELEZO
Askofu Mkuu wa jimbo kuu la Tabora Mhashamu Paulo Ruzoka kesho (tarehe 27.11.2015) anatarajia kuongoza ujumbe wa Tanzania kwenye ziara ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu Francis nchini Uganda.Baba Mtakatifu Francis anatarajia kuwasili nchini Uganda kesho kwa ziara ya siku mbili akitokea Kenya kabla ya kuelekea Afrika ya Kati. 

Hii ni ziara ya kwanza kwa kiongozi huyo Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani kutembelea Bara la Afrika tangu alipoliongoza Kanisa Katoliki mwaka 2013.
Katibu wa Baraza la Maaskofu (TEC) nchini Padre Raymond Saba amesema Mabaraza ya Maaskofu ya Kenya na Uganda kwa pamoja yalitoa mwaliko kwa TEC kushiriki katika ziara ya Baba Mtakatifu katika nchi hizo. 

“Tulipata mwaliko kutoka Kenya na Uganda, lakini tumeangalia nafasi yetu na jinsi ya kushiriki katika ziara hii. Hatukuweza kutuma mwakilishi Kenya, lakini Askofu Ruzoka ataiwakilisha TEC Uganda,” amesema. 

Kwa mujibu wa msemaji huyo, jana mabasi mawili ya waumini wa dini ya Kikristo yaliondoka mjini Mwanza kuelekea Namugongo, Uganda ambapo Baba Mtakatifu atakapofanyia ibada. Eneo la Namugongo ndipo Mfalme Kabaka Mwanga II alipowachoma na kuwaua mashahidi 22 wa Uganda waliofia dini katika karne ya 18. 

“Natoa wito kwa waumini wa Kanisa Katoliki nchini, wafuatilie na kusikiliza kwa makini ujumbe wa Baba Mtakatifu aliouleta katika Barani Afrika kwa sababu unagusa moja kwa moja amani na ushirikiano miongoni mwa jamii,” amesema. 

Kwa mujibu wa Padre Saba, Baba Mtakatifu hufanya ziara kufuatia mwaliko wa kanisa na serikali ya mahali husika au tukio la kimataifa linalohusiana na imani Katoliki. Amesema, “Kanisa pekee yake haliwezi kufanikisha ziara ya Baba Mtakatifu. Ndio maana alipofika Kenya alipokelewa na Rais Uhuru Kenyatta na hata alipokuwa Marekani alipokelewa na Rais Baraka Obama ingawa sio rahisi kwa kiongozi wa Marekani kumpokea mgeni uwanja wa ndege.” 

Ziara ya Baba mtakatifu nchini Marekani ilipangwa kabla hajawa kiongozi Mkuu wa kanisa Katoliki. Ziara hiyo ilitokana na kongamano la kimataifa la familia lililofanyika mjini Filadelphia. Papa Francis anatarajia kuhudhulia kongamano la vijana ulimwenguni nchini Poland mwaka 2016.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images