Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

MOLLEL ANATOSHA KULIONGOZA JIMBO LA ARUSHA

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha.
Mgombea ubunge wa jimbo la Arusha kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Philemon Mollel amewataka wakazi wa jiji la Arusha kumchagua kwa kura za kishindo kwani anatosha kuliongoza jimbo la Arusha na jiji hilo si sehemu ya kujinadi kwa mapambao bali kuwalete wananchi maendeleo.


Mollel ameyasema hayo wakati alipokuwa akijitambulisha na kuomba kura kwa wakazi wa kata ya Levolosi na kuwataka kuendelea kukiamini chama cha mapinduzi pamoja na yeye kwani anatosha kuliongoza jimbo la Arusha Mjini, wakati chama hicho kijiandaa kuanza kampeni zake hapo Jumamosi ijayo mgombea apita kwenye mashina kuomba kura.


Alisema kuwa anaomba kura kwa wanachama na wasiokuwa wanachama kwani maendeleo hayana itikadi za vyama vya siasa hivyo akawataka kumtuma naye awe mtumishi wa wananchi wa jimbo la Arusha mjini.


“Mnajua siendi kuganga njaa bungeni bali naenda kupeleka kero zenu na nani uchungu na maendeleo ya kinamama,wazee na vijana kwani nitaanzisha saccos kwa kila kata ilimpate mikopo ya kujikwamua na kuweza kujiletea maendeleo”alisema Mollel.


Aliwataka wakereketwa na wale wafuasi wa vyama vingine kuweka pembeni ushabiki na kumchagua yeye ilikuirudiisha Arusha kuwa Giniva ya Afrika na kuirudisha Arusha yenye amani na kuweza kurudisha sifa ya jiji hilo.


Awali akimkaribisha Mgombea kwa wanachama na wafuasi wa chama hicho sanjari na wananchi Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Arusha Dkta Soiley amewakata kuacha ushabiki wa kisiasa na kumchagua Mollel kwani anatosha kuliongoza jimbo la Arusha.


Soiley alisema kuwa pamoja na kupigwa katika uchaguzi mkuu kwa nafasi za udiwani mda umefika kwa kumchagua Philemon Mollel kuweza kuiletea maendeleo na kudumisha sifa ya jiji la Arusha ya kuwa na Amani na kivutio cha utalii kwani uchaguzi ulipita na sasa ni wakati wa kuunganisha nguvu na kumpa kura za kishindo mgombea wa chama hicho.


“Nawasihi ndugu zangu kutafuta wanachama kumi kwa kila mtu ilikuunganisha nguvu na kuipa ccm ubunge wa jimbo letu kwani nyinyi ni mashahidi wakubwa hakuna kilichofanyika katika kuwaletea wananchi maendeleo kwa mda wa mbunge aliyemaliza mda wake kwa kipindi cha miaka mitano”alisema Soiley.

MALKIA ELIZABETH II WA UINGEREZA ATUMA SALAMU ZA PONGEZI KWA RAIS JOHN POMBE JOSEF MAGUFULI

$
0
0
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SALAMU ZA PONGEZI
     RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amepokea salamu za pongezi kutoka kwa Malkia Elizabeth II wa Uingereza kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

     Katika salamu hizo Malkia wa Uingereza amemueleza Mhe. Rais Dkt. Magufuli kuwa  “Natumaini kuwa mahusiano baina ya nchi hizi mbili ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola yataendelea wakati wa utawala wako, nakutakia kheri pamoja na wananchi wa Tanzania”  amesema malkia katika salamu zake.

     Salamu pia zimetoka kwa Mfalme Akihito wa Japan ambaye amemueleza Mhe.  Rais Dkt. Magufuli “Nakutumia salamu za dhati,  mafanikio na furaha kwako Mheshimiwa Rais na watu wa nchi yako” Amesema.

     Salamu zingine kwa Mhe. Rais Dkt. Magufuli zimetoka kwa Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kiarabu  ya Saharawi, Mhe. Mohamed Abdelaziz ambaye amemtakia kheri  Mhe. Rais Dkt. Magufuli na kumueleza kuwa “Nina  imani kuwa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea vyema chini ya uongozi wako kuelekea katika kupata maendeleo  na mafanikio zaidi”.

  Amesema; na pia amekipongeza Chama Cha Mapinduzi na Watanzania kwa uchaguzi wa kidemokrasia ulioendeshwa katika mazingira ya kistaarabu chini ya usimamizi wa waangalizi kutoka kwenye kanda, bara na kimataifa na hivyo kuliletea sifa bara la Afrika.

     Mhe. Rais Dkt. Magufuli pia amepokea salamu kutoka kwa Rais wa Namibia Mhe. Hage Geingob na kumueleza Mhe. Rais Dkt. Magufuli kuwa salamu zake na zile za wananchi wa Namibia ni za dhati kwa Serikali na Watanzania kwa ujumla kwa ushindi wa kiti cha Urais.

     “Pia napenda kutoa pongezi kwa Chama Cha Mapinduzi kwa ushindi uliopatikana katika uchaguzi wa Oktoba 25, 2015”. Amesema na kuongeza kuwa  “Kwa hakika Watanzania wamezungumza na kukipa tena CCM  Mamlaka ya kuipeleka mbele Tanzania  kuelekea kwenye mafanikio zaidi”.  Ameongeza.

      Salamu zingine ni kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye amesema Tanzania kwa mara nyingine tena imedhihirisha kuwa ni nguzo ya demokrasia barani Afrika.

     Naye Rais wa Jamhuri  ya Shirikisho la Ujerumani, Joachim Gauck amemtakia Mhe. Rais Dkt. Magufuli na Watanzania kwa ujumla mafanikio  katika kuendeleza Taifa kwa ujumla.

Imetolewa na:
Premi Kibanga, 
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
16 Novemba, 2015.

ZOEZI LA USAJILI WA WABUNGE LAENDELEA MJINI DODOMA

$
0
0
Baadhi ya Wabunge wakibadilishana mawazo katika Viwanja vya Bunge wakati wa zoezi la usajili wa wabunge linaloendelea mjini Dodoma.
Mbunge wa  Jimbo la Makambako Mh Deo Sanga akifanya usajili katika zoezi la usajili wa Wabuge linaloendelea katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Baadhi ya Wabunge wakibadilishana mawazo katika Viwanja vya Bunge wakati wa zoezi la usajili wa wabunge linaloendelea mjini Dodoma. 



(Picha na Benjamin Sawe)

STARTIMES YATETA NA MAWAKALA WAKE

$
0
0

 Baadhi ya mawakala wa StarTimes Tanzania wakisoma vipeperushi wakati wa hafla iliyoandaliwa kwa madhumuni ya kutoa ufahamu zaidi wa sera na huduma mpya za kampuni hiyo. Anayeonekana mbele akifafanua jambo na kusikilizwa kwa makini ni Meneja wa Operesheni, Bw. Gaspa Ngowi. StarTimes imejiwekea utaratibu wa kukutana na mawakala wake wakubwa na wadogo mara kwa mara ili kujadili mustakabali wa huduma na bidhaa wanazozitoa kwa wateja wao.
 Meneja Masoko kitengo cha chaneli na vipindi vya StarTimes Tanzania, Bi. Paulina Kimweri (mbele) akifafanua jambo kwa mawakala waliohudhuria hafla iliyoandaliwa kwa madhumuni ya kutoa ufahamu zaidi wa sera na huduma mpya za kampuni hiyo. StarTimes imejiwekea utaratibu wa kukutana na mawakala wake wakubwa na wadogo mara kwa mara ili kujadili mustakabali wa huduma na bidhaa wanazozitoa kwa wateja wao.
 Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania, Bw. David Kisaka (mbele)  akifafanua jambo kwa mawakala waliohudhuria hafla iliyoandaliwa kwa madhumuni ya kutoa ufahamu zaidi wa sera na huduma mpya za kampuni hiyo. StarTimes imejiwekea utaratibu wa kukutana na mawakala wake wakubwa na wadogo mara kwa mara ili kujadili mustakabali wa huduma na bidhaa wanazozitoa kwa wateja wao.
Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania, Bw. David Kisaka (mbele)  akifafanua jambo kwa mawakala waliohudhuria hafla iliyoandaliwa kwa madhumuni ya kutoa ufahamu zaidi wa sera na huduma mpya za kampuni hiyo. StarTimes imejiwekea utaratibu wa kukutana na mawakala wake wakubwa na wadogo mara kwa mara ili kujadili mustakabali wa huduma na bidhaa wanazozitoa kwa wateja wao.



Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya StarTimes Tanzania mwishoni wa wiki hii waliandaa hafla fupi kwa mawakala wake wote nchini ikiwa ni utaratibu iliyojiwekea kwa lengo la kuwakutanisha kujadili juu ya huduma na bidhaa wanazozitoa kwa wateja wao.

Kampuni hiyo imesema kuwa tukio kama hilo huwa linafanyika  mara kwa mara pale wnapokuwa na sera pamoja na huduma na bidhaa mpya wanazozitarajia kuzitambulisha kwa wateja.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania, Bw. David Kisaka amesema kuwa kampuni yao kila kukicha inakuwa na hivyo inahitaji mawakala wengi zaidi ili kuweza kumfikia kila mtanzania.

“StarTimes tunayo furaha kubwa kwa kuendelea kujiongezea wateja kila kukicha ambao kwa sasa wanafika takribani milioni moja na kuzidi. Hivyo basi kutokana na idadi hiyo kubwa ni dhahiri kabisa kuwa kampuni haiwezi kuwafikia kwa jitihada zake. Mawakala wetu tunapenda kufahamu kuwa nyinyi mna nafasi kubwa sana kwetu kwani nyie ndio mnakutana na wateja moja kwa moja.” Alisema Bw. Kisaka

Aliongezea kuwa, “Na katika kuhakikisha mnawafikia vema na kuwapatia taarifa sahihi na zinazokwenda na wakati, mkutano kama huu ni muhimu. Umuhimu wake unakuja pale ambapo tunakuwa na sera pamoja na huduma na bidhaa mpya au ofa tunazotaka kuzitambulisha kwa mara ya kwanza sokoni. Tunaamini kuwa bila nyinyi kuzielewa basi itakuwa ni vigumu kwa wateja pia. Hivyo basi hafla hii fupi italenga katika Nyanja hizo pamoja na kusikiliza ushauri wenu.”

Akijibu swali la wakala Bijampora ambaye duka lake lipo Magomeni Mwembechai, aliyeuliza kuhusu kusuasua kwa huduma kwa wateja, Bw. Kisaka amefafanua kuwa StarTimes kwa sasa wamejipanga kwa hilo na tayari kitengo hicho muhimu kimekwishatanuliwa kwa kuajiri wafanyakazi wengi zaidi.

“Kitengo chetu cha huduma kwa wateja kimekuwa kikifanya kazi kwa bidii na hiyo yote inatokana na wateja kuongezeka kila kukicha. Hivyo basi kwa sasa kimeboreshwa zaidi na pia ningependa kuwataka nyinyi mawakala wetu muwe mnatoa huduma hii pia kwani ninaamini kuna maswali hata nyinyi mnaweza kuwasaidia. Ninawaomba muwe mnawapatia maelekezo mazuri zaidi ili waweze kuelewa huduma zetu.” Alihitimisha meneja huyo wa mauzo

Hafla hiyo fupi iliweza kuangazia masuala mbalimbali yahusuyo bidhaa na huduma mbalimbali zikiwemo chaneli na vipindi vinavyopatikana kwenye kisimbuzi cha StarTimes.

Kwa upande wake Meneja Masoko kitengo cha chaneli na vipindi vya StarTimes Tanzania, Bi. Paulina Kimweri alipata fursa ya kuwaelezea kwa kina mbali na kisimbuzi mawakala hao pia yawapasa kunadi na kile kilichomo ndani yake.

“Mimi kwa upande wangu ningependa kutoa wito kwenu nyinyi mawakala wetu kuwa inabidi muwe mnatoa elimu ya kutosha juu ya chaneli na vipindi vinavyopatikana kwenye visimbuzi vyetu. Kwani sio wateja wote ambao wana ufahamu na chaneli na vipindi vyetu. Wengi hununua bidhaa zetu kwa ajili ya kutazama chaneli na vipindi vya ndani tu bila ya kujua kuwa vipo vitu vingi vya kuvutia na kumfaa kila mtu ndani ya familia.” Alifafanua Bi. Kimweri

“Muwe mnawaambia wateja kuwa pia kuna chaneli nyingi tu za kuvutia ambazo zinapatikana katika vifurushi vya bei nafuu. Kwa mfano chaneli za watoto zenye vipindi vinavyofundisha, dini, filamu, tamthiliya, muziki, michezo, mitindo, makala nakadhalika,” alisema na kumalizia Bi. Kimweri, “Hivyo basi naamini kuwa mkitoka hapa mkirudi madukani mwenu mtakuwa mkivitumia vipeperushi tunavyowapatia kuwaelimisha wateja waweze kufahamu zaidi.”

StarTimes Tanzania mpaka hivi sasa ina mawakala wakubwa na wadogo zaidi ya 500 waliosambaa nchi nzima kuhukikisha inawafikia wateja kwa urahisi. Hivyo imewataka mawakala wote nchini kuwa waaminifu na pia wateja kuwatembelea kwani huduma wanazozitoa ni sawa na zile zinazotolewa katika ofisi za kampuni.

Kampuni inajivunia uwepo wa mawakala hao ambao kwa muda mrefu wamekuwa ni kiungo muhimu baina yao na wateja.  Lakini kwa upande mwingine hii ni fursa kwa watanzania kuchangamkia fursa hii kwa kujiajiri wenyewe kwani kupitia uwakala mtu anaweza kuuza bidhaa na kupata kamisheni yenye faida kubwa na kuendesha maisha yake.

WAFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB WAKISHIRIKI MICHEZO MBALIMBALI KATIKA SIKU YA FAMILIA YA CRDB

$
0
0

 Wafanyakazi wa  Benki ya CRDB mkoa wa Arusha  wakishindana kuvuta kamba katika viwanja vya Olasiti Garden leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za wateja.
Meneja wa Benki ya  CDRB  tawi la Usa River  lilipo mkoani Arusha  Jenipher  Tond akikabidhi zawadi ya tisheti kwa mtoto aliyeshinda kucheza mziki leo sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za wateja.
 Watoto wakimkimbiza kuku katika mashindano yaliyofanyika kwenye sherehe za  siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafanyakazi wa benki pamoja na familia za wateja
 Malindi band ya mkoani kilimanjaro ikitumbuiza sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafanyakazi wa benki pamoja na familia za wateja
Mfanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la USA akikabidhi zawadi kwa mtoto
 Habari picha na Woinde Shizza,Arusha
Benki ya CRDB imeendelea kukuza kipato cha familia nyingi nchini za hali ya
chini ,kati na juu kwa kuwahimiza wateja wake kufanya uwekezaji wenye tija
pamoja na kujiwekea akiba kwa maisha ya baadae.
Hayo yameelezwa Meneja wa Benki ya  CDRB  tawi la Usa lilipo mkoani
Arusha  Jenipher Tond wakati wa maadhimisho ya siku ya Familia ya CRDB iliyofanyika katikaviwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha na kuzikutanisha familiambalimbali za wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na familia za wateja wabenki hiyo waishio jijini Arusha.
Meneja huyo amesema kuwa benki hiyo inaendelea kuhamasisha uwekezaji na
kutoa mikopo kwa ajili ya kukuza mitaji na kuinua pato la mwananchi mmoja
mmoja hadi kwa taifa.Meneja wa benki hiyo tawi la Meru Leonce Mathey amesema kuwa benki hiyoimesogeza karibu huduma kwa wananchi ikiwemo boda boda ,mama ntilie pamojana wajasiriamali kwa kuanzisha matawi katika maeneo ya masoko .
Leonce amewataka wafanyakazi wa CRDB kutumia vyema siku familia  kwa kukaakaribu na familia zao na kufurahi pamoja kwani muda mwingi wanautumiakatika kufanya kazi za kuwaingizia kipato .“Kama kwenye familia mambo hayako vizuri nyumbani hata kazini mambo  hayatakua
vizuri ni vyema kuhakikisha mazingira yanakua mazuri kuanzia kwenye familiampaka kazini” Alisema Leons.
Kwa upande wake Mteja wa benki hiyo Pendo Shoo amesema kuwa benki hiyo
imemsaidia kuwalipia watoto wake ada kupitia akaunti ya Junior Acount
ambazo huwawezesha pia kupata mikopo kwa ajili ya kuwaendeleza watoto
kielimu.
Benki ya CRDB  ina matawi 8 na matawi mengine madogo madogo bado
yataendelea kuanzisha ili kusogeza huduma za kibenki karibu na wananchi.
Siku ya familia ya CRDB iliambatana na michezo   na burudani  ambazo
zilipamba siku hiyo ikiwemo mchezo wa kuvuta kamba ,kukimbia na yai mdomonipamoja na burudani ya muziki .
 Watoto wakifurahia michezo mbalimbali   katika viwanja vya Olasiti Garden
leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka
na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za
wateja.
 Wafanyakazi wa  Benki ya CRDB mkoa wa Arusha  wakishindana kuvuta kamba
katika viwanja vya Olasiti Garden leo katika sherehe za siku ya familia ya
CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi
wa benki pamoja na familia za wateja.
 Watoto wakifurahia michezo mbalimbali   katika viwanja vya Olasiti Garden
leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka
na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za
wateja


WABUNGE WA CCM WAAMUA KWA PAMOJA NAFASI YA USPIKA NI JOB NDUGAI

$
0
0
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiongea na waandishi wa habari mara baada ya Wabunge wa CCM kupitisha jisha la Spika.

Katibu wa NEC (CCM) Itikadi na Uenezi ambaye pia ni mbunge wa Mtama, Nape Nnauye alisema “Kamati ya Wabunge wote wa CCM imekamilisha kazi yake ya kwanza kuchambua na kupitisha moja kati ya majina matatu yaliyoteuliwa na Kamati Kuu.
 
“Kama tulivyoona wagombea wawili walijitoa, hivyo Job Ndugai amepitishwa kwa kauli moja kugombea nafasi ya uspika. Tunamuombea kura kwa sababu sifa zote anazo, bila shaka hakutatokea mgombea wa upinzani atakayezidi sifa zake,” alisema Nape.
Mbunge wa Jimbo la Kongwa Ndugu Job Ndugai akiongea na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa NEC baada ya jina lake kupitishwa na wabunge wa CCM.

Katibu Mkuu wa CCM akihutubia kwenye kikao maalum cha wabunge wa CCM kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
Katibu Mkuu wa CCM akipokea pongezi alizopewa na wabunge wa CCM kwa kazi nzuri iliyowapa CCM ushindi mkubwa katika uchaguzi uliofanyika oktoba 2015.
Sehemu ya wabunge wa CCM walioshiriki kwenye kikao maalum cha uchaguzi wa Spika kutoka Chama Cha Mapinduzi.
Mbunge Mteule wa Nzega mjini Hussein Bashe akizungumza na Mbunge mteule wa jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye pamoja na Jerry Slaa (katikati) kabla ya zoezi la upigaji kura kwenye ukumbi wa NEC.





KATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) ndugu ABDULRAHMAN KINANA amefungua kikao cha kamati  ya wabunge wa CCM huku akiwahimiza wabunge hao kufanya kazi ili kutekeleza kauli mbiu ya rais dr JOHN MAGUFULI ya hapa kazi tu.
Akifungua kikao hicho leo mjini Dodoma ndugu KINANA amesema ili kuendana na kauli mbiu hiyo nilazima wabunge wote wafanye kazi.
Amesema kazi waliyonayo kwa sasa ni kuwazungukia watanzania ambao wamewaamini kwa kuwa njia pekee ya kutafsiri imani hiyo ni kuwatumikia kwa nguvu zote.

Ndugu KINANA amewapongeza wabunge hao kwa kutafuta kura nyingi za rais juhudi ambayo imekiletea chama heshima kubwa na kuwahakikishia kuwa ofisi yake itaandaa siku maalum kabla ya bunge linalofuata ili kuwapa majukumu ya namna ya kuwatumikia wananchi.

Amesema kazi kubwa kwa wanasiasa ni kutekeleza ilani ya uchaguzi waliyonayo kazi ambayo ana imani kuwa wabunge hao wataitekeleza ipasavyo.

Awali akimkaribisha katibu mkuu,katibu wa wabunge wa CCM mama JENISTA MUHAGAMA amesema kikao hicho nimaalum kwa ajili ya kuchagua jina moja la atakayegombea nafasi ya uspika wa bunge la Jamhuri ya Tanzania kutoka katika majina matatu yaliyopitishwa na kamati kuu ya halmashauri ya CCM jana.

Majina hayo yaliyopitishwa ni la naibu spika mstaafu JOB NDUGAI,mbunge wa Afrika Mashariki ABDULLAH ALLY MWINYI na naibu mwanasheria mkuu wa serikali TULIA ACKSON MWASANSU ambaye ameteuliwa na rais kuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya Tanzania.

Uchaguzi huo unasimamiwa na  wajumbe wa kamati kuu ya CCM ambao ndugu WILLIAM LUKUVI,MAUA DAFTARI na JERRY SILAA ambapo jina moja litakalopatikana litapelekwa kesho bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura na wabunge wote.

SHUKRANI
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimewashukuru watanzania kwa imani kubwa waliyoionyesha  katika uchaguzi mkuu uliopita uliowezesha kuwapa  ushindi wabunge wa chama hicho kwa asilimia 74.8.

Akifungua kikao cha kamati cha wabunge wa CCM kilichofanyika ukumbi wa white house mjini Dodoma katibu mkuu wa chama hicho ndugu ABDULRAHMAN KINANA amesema kitendo hicho kimedhihirisha imani kubwa waliyonayo watanzania kwa CCM.

Amesema watanzania wametafsiri imani kwa kukipa kura CCM na kusema katika majimbo tisa yanayofanya uchaguzi mdogo tayari CCM imeshinda katika jimbo la Lulindi lililopo mkoani Tanga.

Aidha amesema katika kata 14 zilizofanya uchaguzi mdogo katika jimbo hilo CCM imepata kata 10 na upinzani kata 4.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

TAASISI YA DON BOSCO YAHAMASISHA WASICHANA KUPENDA KUJIUNGA NA VYUO VYAO

$
0
0
 Meneja wa mipango  wa kapeni ya Binti Thamani Rosemacy Njoki   akizungumza na waandishi wa habari  (hawapo pichani) juu ya kampeni ya  kuwahamasisha wasichana kupenda kujiunga  na vyuo vya ufundi  ili kujifunza ufundi stadi  na kujiendeleza kimaisha  ikiwa ni pamoja na kujipatia ajira endelevu, amesema hayo katika kutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushotoni Mkuu wa Chuo cha ufundi cha Don Bosco Dodoma Fromac Mulu.
 Mratibu wa kampeni ya Binti Thamani wa taasisi ya Don Bosco, Agnes Mgongo, kisisitiza jambo katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkufunzi wa Chuo cha Ufundi cha Don Bosco   Jose Kaippan.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja wa mipango  wa kapeni Binti Thamani Rosemacy Njoki.

 Wafanyakazi wa Taasisi ya Don Bosco wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa chuo cha ufundi cha Don Bosco.
Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.


TAASISI  ya kidini ya Don Bosco imeandaa kampeni ya  kuwahamasisha wasichana kupenda kujiunga  na vyuo vya ufundi  ili kujifunza ufundi stadi  na kujiendeleza kimaisha  ikiwa ni pamoja na kujipatia ajira endelevu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam  Meneja wa mipango  wa kapeni ya Binti Thamani, Rosemacy Njoki amesema wana vyuo mbalimbali hapa nchini ambavyo vinatoa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana lakini  kumekuwa na asilimia ndogo ya vijana wakike wanaojiunga na mafunzo ya ufundi stadi ukilinganisha na idadi ya vijana wa kiume kwa mwaka.

amesema baadhi ya kozi zinazotolewa  na vyuo vya Don Bosco vilivyopo Dar es Salaam Dodoma na Iringa  ni ufundi Seremala, uchongaji vipuri,  uungaji na uundaji  vyuma, umeme wa viwandani na majumbani, uhazili, ujenzi, ufundi bomba na magari, ufundi cherehani uchapishaji na kompyuta.

Kampeni ya Binti thamani ni mwendelezo wa uhamasishaji kwa wasichana kuibua na kutatua changamoto mbalimbali za vijana hususani wasichana kutambua kuwa kuna fursa ya kujiendeleza na kufanikiwa kupitia mafunzo ya ufundi baada ya kumaliza mafunzo yao.

Kampeni hiyo itasaidia kuwakumbusha kuwa wasichana nao wana uwezo wa kufanya kazi yoyote hasa anapokuwa na malengo chanya.

Kampeni hiyo leo itawakutanisha wasichana mbalimbali hasa wanafunzi wa shule za sekondari wapatao 1000 katika mikoa wa Dar es Salaam.

“Lengo la kampeni hii ni kuwakutanisha wasichana na wadau mbalimbali waliopitia mafunzo ya ufundi stadi na kuwahimiza  kuwa mabalozi wazuri katika kuhakikisha wasichana wengi Zaidi wanapenda mafunzo ya ufundi stadi.

“Tunawaomba wazazi  na walezi tusaidiane kwa pamoja katika harakati za kuwahamasisha wasichana kwani ndio tegemeo la jamii yetu,”  Rosemacy.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA DINI WA MKOA WA DODOMA.

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi wa Kamati ya Mahusiano ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, wakati alipokutana nao kwa mazungumzo kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma leo Nov 16, 2015. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa (kulia) ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, Sheikh Ahmad Said Ahmed. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,  Chiku Galawa, wakati wa mkutano na Viongozi wa Kamati ya Mahusiano ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma leo Nov 16, 2015. Picha na OMR
Baadhi ya Viongozi wa Dini wa Mkoa wa Dodoma,wakimsikiliza Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan, wakati akihutubia alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Kamati ya Mahusiano ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma, leo Nov 16, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi wa Kamati ya Mahusiano ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, wakati alipokutana nao kwa mazungumzo kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma leo Nov 16, 2015. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Chiku Gallawa (kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, Sheikh Ahmad Said Ahmed, kwa pamoja wakisimama kuomba dua wakati wa mkutano na Viongozi wa Kamati hiyo,mkoani Dodoma leo, Nov 16, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na baadhi ya Viongozi wa Kamati ya Mahusiano ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, baada ya kuzungumza nao kwenye mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo, mjini Dodoma leo Nov 16, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kamati ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, baada ya mkutano uliofanyika leo Nov 16, 2015 kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kamati ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, baada ya mkutano uliofanyika leo Nov 16, 2015 kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kamati ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, baada ya mkutano uliofanyika leo Nov 16, 2015 kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma. Picha na OMR
makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, Askofu wa Kanisa la KKKT Mkoa wa Dodoma, Kinyunyu Amon, baada ya mkutano uliofanyika leo Nov 16, 2015 kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma. Picha na OMR

SERIKALI YAANZA UTEKELEZAJI WA RUZUKU YA PEMBEJEO ZA KILIMO KWA NJIA YA VOCHA.

$
0
0
 Msemaji wa Wizara ya Kilimo cha Chakula na Ushirika,  Richard Yasini  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya pembejeo za kilimo zenye thamani zaidi ya Sh. Bilioni 78  ambazo zimesambazwa katika mikoa 24  ya  Tanzania Bara ili zitumike kufidia gharama ya mbolea na mbegu bora katika msimu wa 2015/2016.Vocha hizo zitawanufaisha wakulima 999,926 wanaojihusisha na kilimo cha mazao ya mahindi na mpunga. Mkutano huo umefanyika  leo jijini Dar es salaam kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa MAELEZO, Zamaradi Kawawa.
Baadhi ya waadnishi wa habari wakimsikiliza Msemaji wa Wizara ya Kilimo cha Chakula na Ushirika,  Richard Yasini.
                                       Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Na. Georgina Misama - MAELEZO
WAKULIMA wapatao milioni moja wameanza kunufaika na usambazaji wa vocha za pembejeo za kilimo ambazo Serikali inazitolea ruzuku kwa ajili ya wakulima katika mikoa 24 ya Tanzania bara (ukitoa mkoa wa Dar es Salaam)  ili zitumike kufidia gharama ya mbolea na mbegu bora kwa mwaka 2015/2016.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano  Serikalini kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Bw. Richard Kasuga amesema kwamba pembejeo za kilimo zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 78 zitawanufaisha wakulima wanaojishughulisha na kilimo cha mazao ya mahindi na mpunga.

“Usambazaji wa vocha hizo umeshaanza, Serikali kwa kushirikiana na makampuni 23 ya mbolea na 27 ya mbegu bora ya mahindi na mpunga yanaendelea kutoa  huduma ya usambazaji wa pembejeo katika mikoa husika” amesema Bw Kasuga.

Bw. Kasuga amesema kwamba ili kuhakikisha mbolea na pembejeo zinatumika ipasavyo, Serikali inatekeleza jukumu hilo kwa kugawa majukumu kwa ngazi mbalimbali ikianza na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Kamati ya Taifa ya Uendeshaji wa Utaratibu wa Vocha, Mikoa, Wilaya, Kata mpaka Vijiji.

Akijibu swali la mwandishi aliyetaka kujua Serikali inafanya juhudi gani katika kudhibiti ubora wa pembejeo hizo, Kaimu Mkurugenzi, Mamlaka ya udhibiti wa Ubora wa Mbolea Bw. Lazaro Kitandu amesema toka kuundwa kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Ubora wa Mbolea tatizo la ubora limepungua kwa kiasi kikubwa kwani mamlaka hiyo inasimamia zoezi zima la utengenezwaji na usambazaji wa mbolea na pia wakulima wanapewa elimu ya matumizi sahihi na namna bora ya kuhifadhi.

Aidha, Serikali imetoa rai kwa wakulima kutumia ruzuku inayotolewa ili waweze kujikomboa kiuchumi kwa kuboresha kilimo, na kuwasihi baadhi ya wakulima wanaouza vocha zao wasidanganyike kwa kupokea hela na kuuza haki yao. 

Serikali ilianzisha utaratibu wa matumizi ya vocha mwaka 2008/2009 ili kuboresha mfumo wa usambazaji mbejeo kwa wakulima. Utaratibu huu umesaidia kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula,  hivyo Taifa kufaidika na kujitosheleza  kwa chakula.

SHULE YA CATTON GROVE YA UINGEREZA YATOA MSAADA AMANI ORPHANAGE CENTRE, BAGAMOYO

$
0
0
  Mratibu wa Wafanye Watabasamu ambaye pia ni mchora vibonzo nchini, Nathan Mpangala akimkabidhi sare za shule mmoja wa malaika kituoni hapo. Aliyetupia koti ni Mwakilishi wa TNTA nchini, Bw. Mussa Mussa Zaidi kuhusu Wafanye Watabasamu tembelea: https://www.facebook.com/wafanyewatabasamu
 Rafiki wa Wafanye Watabasamu, Mussa Sango akionesha upendo.
 Watoto wakizitathmini zawadi zao.
 Watoto wakionesha furaha yao.
 Mkurugenzi wa kituo cha Amani Orphanage Centre, Bi. Margareth Mwegalawa akiwa amempakata mtoto yatima anayelelewa kituoni hapo. Mtoto huyo alitupwa Chalinze miezi ya karibuni.
 Kutoka kulia, Nathan Mpangala (Mratibu Wafanye Watabasamu), Mussa Mussa (Mwakilishi TNTA), Amani Abeid (Rafiki wa Wafanye Watabasamu) na matroni wa kituo hiko wakiangalia tenki la maji kituoni hapo. Mnara wa tenki hili umetolewa na walimu wa Shule ya Msingi ya Catoon Grove.
 Mratibu wa Wafanye Watabasamu Nathan Mpangala na Mwakilishi wa TNTA Mussa Mussa walitafakari jinsi ya kuingia jikoni kituoni hapo.

Wafanye Watabasamu haikuwaacha hivi hivi, watoto wakapata nafasi ya kucheza na rangi. Pichani rafiki wa Wafanye Watabasamu, Amani Abeid akijiachia na malaika hao.
Watoto kituo cha yatima (Amani Orphanage Centre) kilicho katika Kijiji cha Zinga, Bagamoyo wakipokea ugeni wa marafiki wa Wafanye Watabasamu uliowatembelea jana. Marafiki wa Wafanye Watabasamu kwa kushirikiana na The Tanzania Norwich Association (TNTA) walikwenda kituoni hapo kukabidhi sare za shule pea 32, mabegi ya shule 32, mikebe na madaftari vilivyotolewa na walimu wa Shule ya Msingi ya Catton Grove ya Uingereza. (Picha zote na Wafanye Watabasamu).

CHAMA CHA AFYA YA JAMII(TPHA) CHAWAOMBA WADAU KUTOA USHIRIKIANO ILI KUPAMBANA NA MATUMIZI TUMBAKU KWA VIJANA

$
0
0
Dk. Adeline l. Kimambo(kulia) kutoka Chama cha Afya ya Jamii (TPHA) akitoa muhutasari wa Madhara ya Tumbaku mbele ya waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa waliofika kujadili changamoto wanazokabiliwa nazo hasa wanapokuwa wanatoa huduma kwa jamii kuhusu matumizi ya Tumbaku na kuwaomba wadau hao kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufikia malengo waliyojiwekea.Katikati ni Dk Faustine Njau kutoka Chama cha Afya ya Jamii (TPHA).
 (Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog)
Mratibu wa Mradi wa Madhara ya Tumbaku (TPHA) Dk. Bertha T.A. Maegga(kushoto) akizungumza jambo kwenye kikao kilichowashirikisha wadau mbalimbali kutoka katika manispaa za jijii la Dar es Salaam kuhusu kushirikiana na wadau mbalimbali hasa kutoka katika manispaa za jiji hilo ili kudhibiti matumizi na madhara ya Tumbaku hapa nchini na kusisitiza kushirikiana ili kupambana na janga hili hapa nchini linalopelekea kupoteza nguvu kazi kubwa.
Dk. Faustine Njau kutoka Chama cha Afya ya Jamii (TPHA) akisisitiza wadau kujitokeza na kushirikiana nao ili kutatua tatizo la matumizi ya tumbaku pamoja na vileo hasa kwa watoto wadogo wanaoanza kutumia wakiwa wadogo na kupelekea kupata madhara udogoni.Ambapo kwa utafiti uliofanyika umeonesha asilimia 6 ya watoto 400 wa shule za msingi walianza kutumia tumbaku wakiwa hawajui madhara yake.



Mjumbe wa Chama cha Afya ya Jamii (TPHA),Dk. Mashombo Mkamba akizungumza jambo wakati wa majadiliano ni kwa namna gani wanaweza kupunguza matumizi ya Tumbaku katika jamii unayowazunguka na hata kuwaomba wadau mbalimbali kushirikiana ili kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya matumizi ya Tumbaku hasa kwa watoto wadogo ambao ni nguvu kazi ya baadae.
Dk.Tulitweni Mwinuka kutoka manispaa ya Temeke akieleza changamoto wanazozipata pale wanapokuwa wanatoa elimu ya matumizi ya Tumbaku na kusisitiza changamoto kubwa wanayoipata ni wanasiasa kutotoa ushirikiano wa kutosha kwa kuhofia kupoteza wapiga kura wao wakati wa uchaguzi.

NSSF YADHAMINI BONANZA LA MICHEZO LA CHUO CHA IFM

$
0
0
Mchezaji wa timu ya mpira wa Kikapu ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Ephraim Mlawa (kushoto) akichuana na Juvenary Shichose wakati Bonanza la michezo la wanafunzi wa Chuo hicho lililofanyika, mwishoni mwa wiki katika Kituo cha Michezo cha JMK Youth Park na kudhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kutoa vifaa vya michezo kwa timu zilizoshiriki mchezo wa soka. (Picha na Francis Dande)
Timu za mpira wa kikapu kutoka Chuo cha IFM zikichuana katika Bonanza la michezo la wanafunzi wa chuo hicho.
Kikosi cha timu ya Soka ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), BBF kikiwa katika picha ya pamoja.

Kikosi cha timu ya Soka ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), DIT kikiwa katika picha ya pamoja.

Mshauri wa wanafunzi wa Chuo cha IFM, Khamis Kihongoa akikagua timu ya DIT wakati wa Bonanza la michezo la wanafunzi wa Chuo cha IFM.
Mshauri wa wanafunzi wa Chuo cha IFM, Khamis Kihongoa akikagua timu ya DIT wakati wa Bonanza la michezo la wanafunzi wa Chuo cha IFM.
Mshambuliaji wa timu ya DIT, Shaban Juma (kushoto) akiwania mpira na mchezaji wa timu ya BBF, Yohana Galus  wakati wa bonanza la michezo la wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na kudhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. 

Motisun yaongeza uimara maradufu mabati ya Kiboko Imara

$
0
0


Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Motisun Group Subhash Patel (wapili kushoto) akiwasha mshumaa pamoja na wawakilishi wa makampuni tanzu za Motisun Group kuashiria uzinduzi wa mabati ya Kiboko Imara. Hafla ya uzinduzi ulifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar-es-salaam.
 Balozi wa mabati ya Kiboko Jacob Steven ‘JB’ akicheza ngoma ya asili na kikundi cha KP traditional dance katika uzinduzi wa mabati ya Kiboko Imara yanayotengenezwa na kampuni ya MMI STEEL. Hafla ya uzinduzi ulifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar-es-salaam.
 Mwenyekiti na mkurugenzi mtendaji wa Motisun Group Subhash Patel akimvalisha taji balozi wa mabati ya Kiboko Imara Jacob Steven ‘JB’ katika uzinduzi wa mabati ya Kiboko yanayotengenezwa na kampuni ya MMI STEEL. Hafla ya uzinduzi ulifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar-es-salaam.
Kampuni inayozalisha vifaa vya ujenzi, iitwayo Motisun imezindua teknolojia itakayoongeza ubora na kuimarisha vifaa kama mabati kwa ajili ya kuezekea paa za nyumba na majengo.

Teknolijia hiyo ilizinduliwa jijini Dar es Salaam katika Hotel ya Sea Cliff na kutangazwa kuanza kwa shughuli ya uuzaji wa mabati hayo katika maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi.

Mwenyekiti na Muasisi wa kampuni ya Motisun, Subhash Patel alisema, teknolojia hii inahusu utumiaji wa madini ya aluminiamu na zinki ambayo huongeza ubora na kuyafanya mabati kudumu zaidi.

Alisema bidhaa hii mpya itakuwa ikipatikana chini ya kampuni tanzu ya Motisun iitwayo MMI. Bidhaa zitakuwa zikiuzwa katika maduka ya rejareja hususani katika maeneo ambapo wateja hupendelea bidhaa za ubora wa hali ya juu.

“Bidhaa hii itakuwa inajulikana sokoni kwa jina la Kiboko Imara. Ili kuiunganisha na walaji, Kiboko Imara itakuwa ikitangazwa na Msanii maarufu Jakobo Stephen ambaye anafanya zivuri katika fani yake na kuwa na mvuto kwa wengi,” alisema. 

Bwana Patel anasema kuzinduliwa kwa bidhaa mpya kunaashiria juhudi za kampuni ya MMI kuongeza wigo wa bidhaa kwa kuzingatia mahitaji ya teknolojia ambayo ina manufaa mengi katika sekta ya ujenzi.

Kampuni ya MMI ni maarufu kwa uzalishaji wa bidhaa za ujenzi kama nondo ambazo zimekuwa zikiuzwa ndani na hata nchi jirani za Msumbiji, Zambia na Uganda zikiambatana na ubora.

“Tumejiandaa kikamilifu kuifanyia mauzo bidhaa hii mpya katika masoko hapa nchini na nchi   jirani ambapo pia kuna fursa ya masoko,” alisema bwana Patel.

Bidhaa za mabati zilizopakwa madini ya aluminiam na zinki zimekuwa zikikubalika sana katika masoko mengi duniani kwa ajili ya makazi ya kuishi na majumba makubwa ya biashara ambayo huweka msisitizo katika viwango vya ujenzi.

Alisema tayari kuna wimbi kubwa la asili la watu kuhamia katika matumizi ya mabati yaliyopakwa madini ya aluminiamu na zinki kutokana na kuwa na uwezo wa kudumu kwa muda mrefu.

“Ni kwa sababu hii MMI imechagua kuzalisha bidhaa hii muhimu nchini Tanzania kwa matumizi ya makazi ama miradi ya biashara,” alisema bwana Patel.

Bidhaa hii ya Kiboko Imara inatoa wigo mpana kwa matumizi mbalimbali mfano urefu, rangi na hata unene wa mabati.

 “Hii inamaanisha mapaa mbalimbali huhitaji unene na urefu tofauti wa mabati, mfano nyumba ya kuishi inahitaji mabati yenye unene wa kawaida wakati paa za majengo ya viwanda na biadhara kubwa kubwa huhitaji mabati manene zaidi,” alisema.

Kwa mujibu wa bwana Patel, utengenezaji wa bidhaa hii mpya umezingatia viwango vya kitaifa na kimataifa kwani zimejaribiwa ili kukidhi viwango vya ubora.

MSAADA WA WASAMARIA WEMA WA MATIBABU UNAHITAJIKA KWA DADA HUYU

$
0
0
Ndugu Wasamaria wema
Napenda kutumia fursa hii kukushirikisha habari ya kusikitisha kuhusu dada Joyce Mwambepo (pichani akiwa na mwanaye, na migu yake iliyopooza) mkaazi wa Sinde jijini Mbeya. Dada huyu mwenye umri wa miaka 27 anaishi na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na mwanaye mwenye umri wa miaka 4.
Kwa bahati mbaya mwezi April mwaka jana dada huyu alipata ajali ya kugongwa na gari ambayo haikusimama kumsaidia. Ila kwa msaada wa wasamaria wema alipelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa  Mbeya ambako inasemekana alikaa kwa miezi mitatu bila kupata matibabu.
Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce amevunjika miguu yote miwili,  hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa Mbeya baada ya kukosa shilingi 550,000/- za vipimo na matibabu.
Hadi nakutana naye dada huyu alikuwa amelala nyumbani kwa bibi yake (pichani kushoto) ambaye ni mlezi wake tangu akiwa na miaka minne baada ya wazazi wote wawili kufariki dunia. 
Hawezi kukaa wala kusimama na anajisaidia hapo hapo kitandani kwa msaada wa mwanaye na bibi yake. Inasikitisha.
Hivyo nimejitahidi kufuatialia ili kujua mahitaji halisi lakini sikufanikiwa kumpata daktari bingwa wa mifupa . Ili kumsaidia Joyce inatakiwa aanze process upya za matibabu kuanzia hapa Mbeya referral Hospital  hadi Muhimbili jijini Dar es salaam.
Gharama za matibabu ni kama ifuatavyo:
1. shilingi 300,000/- za kupima CT-SCAN
2. Shilingi 250,000/- za MRI
3. Usafiri wa kutoka Mbeya-Dar kwa gari maalum la kukodi 700,000/-
4. Gharama za msaidizi ambaye ni rafiki yake 300,000/-
5. Chakula 450,000/- (Endapo watakaa hospitali mwezi mzima)
6. Gharama za matibabu (CT-SCAN&MRI ni vipimo tu) 500,000/-
7. Na mahitaji mengineyo wakiendelea kupata tiba 500,000/-

Hivyo kwa kuanzia kiasi cha shilingi 3,000,000/- (milioni tatu) kinahitajika kumpunguzia mateso dada yetu huyu. Asante sana kwa moyo wako wa kujitoa na Mungu atakubariki.

Deo Kakuru Msimu
Msamaria mwema
+255769 512 420

Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal amejitolea kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba +255 754 271266 kwa jina la Ankal.

RC KILIMANJARO,AMOSI MAKALA ATEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA YA MAWENZI.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro  Amos Makala akisalimiana na wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kutembelea idara mbalimbali hospitalini hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala akitia saini katika kitabu cha wageni maara baada ya kuwasili katika hosptali ya Rufaa ya Mawenzi mkaoni Kilimanjaro.
Mganga mkuu wa mkoa wa Kilimajaro Hajati, Dkt Mtumwa Mwako akifanya utamburisho wa watumishi wa hosptali hiyo katika ukumbi mdogo wa mikutano hospitalini hapo.
Baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi ya mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Novatus Makunga akizungumza jambo katika kikao cha mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Amos Makala na watumishi wa Hopstali ya rufaa ya Mawenzi.
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya Mawenzi Dkt ,Bingilaki Rwezaula (kushoto) akiwa na watumsihi wengine wa hospitali hiyo. 
Katibu wa Hosptali ya Rufaa ya Mawenzi ,Boniface Lyimo akisoma taarifa ya hospitali hiyo kwa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala (hayupo pichani)
Baadhi ya wakuu wa vitengo mbalimbali katika hospitali ya Rufaa ya Mawenzi ,mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala akizungumza na watumishi wa Hopstali ya Rufaa ya Mawenzi mara baada ya kutembelea hosptali hiyo.
Badhi ya watumishi katika hospitali hiyo.
RC Makala akizunguza na watumishi.
RC Makala akizungumza na mmoja wa wzee waliofikisha wagonjwa wao katika hospitali ya Mawenzi.
RC Makala akizungumza na mmoja wa wauguzi katika hospitali hiyo,kushoto ni mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Hajati,Dkt Mtumwa Mwako.
RC Makala akiwajulia hali wagonjwa waliofika katika hospitali hiyo kujipatia huduma ya matibabu.
Mganga Mfawidhi wa Hopstali ya Rufaa ya Mawenzi,Dkt Bingilaki Rwezaula akimuelekeza maeneo mbalimbali mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Amos Makala alipotembelea hospitalini hapo.
RC Makala akizungumza na mmoja wa wazee waliofika katika hospitali hiyo kupata matibabu.
RC Makala akitizama hali ya wagonjwa katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi.
RC Makala akitembelea kitengo kinachoshughulika na bima ya afya.
RC Makala akizungumza jambo na mkuu wa idara ya Bima ,Dkt Saganda katika hospitali hiyo.
RC Makala akizungumza na mmoja wa wagonjwa waliopo katika hospitali hiyo.
Wodi ya kina mama.
RC Makala akisalimiana na mmoja wa wauguzi wa zamu katika hospitali hiyo.
RC Makala akizungumza na mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika wodi ya kina baba.
RC Makala akizungumza na madkarai wa zamu katika hospitali ya Mawenzi.
RC Makala akimsikiliza mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika wodi ya Majeruhi katika hospitai hiyo.
RC Makala akitoa maelekezo kwa mkuu wa wilaya ya Moshi,Makunga baada ya kupata maelezo toka kwa mmoja wa wagonjwa katika hospitali hiyo namna alivyojeruhiwa .
RC Makala akitoka katika wodi ya wagonjwa wa akili hosptalini hapo.
RC Makala akiwa katika wodi ya watoto katika hospitali ya Mawenzi.
RC Makala akitembelea jengo jipya la wodi ya wazazi linalojengwa katika hospitali hiyo.
RC Makala akiondoka katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi mara baada ya kutembelea idara mbalimbali hospitalini hapo kujionea namna huduma zinavyotolewa.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

“Afya bora inaanza na kifungua kinywa bora” wito kutoka hospitali za Apollo kwenye siku ya kisukari duniani 2015

$
0
0
Dk. Bhuvaneshwari Shankar, Mkuu wa idara ya lishe kutoka hospitali za Apollo.

Novemba 14 kila mwaka tunaadhimisha siku ya kisukari duniani ili kuongeza uelewa kuhusu madhara ya kisukari, matatizo yanayoletwa na huu ugonjwa na taarifa muhimu kuhusu kisukari.

Siku hii inabeba ujumbe mahususi kwa watu wote ulimwenguni. Kauli mbiu katika siku hii tokea 2014 hadi 2016 ni maisha bora na kisukari(healthy living and diabetes) na mwaka huu kuna mtazamo zaidi katika kuzingatia mlo kamili na kuanza kila siku na kifungua kinywa bora.

Kutoka katika shirika la kisukari Africa, Tanzania ni kati ya nchi 32 katika shirikisho hilo kwa viwango vya nchi zenye viwango vya kisukari duniani. Kulikuwepo na zaidi ya kesi milioni 1.7 za kisukari hapa Tanzania kwa mwaka 2014. Shirika la afya duniani (WHO) linakadiria zaidi ya watu milioni 180 ulimwenguni wana kisukari, na hiyo takwimu inatarajiwa kuongezeka ifikapo mwaka 2030 kama hamna hatua yoyote itakayochukuliwa.

Kifungua kinywa bora na sahihi kitasaidia sana kiwango cha sukari mwilini  kutokuwa juu sana wala chini sana na kukuweka vizuri kutokea asubuhi.Katika maadhimisho ya siku ya kisukari dunia, kliniki ya sukari kutoka hospitai za Apollo imeandaa siku 2 za kupima na kuhamasisha katika kambi iliyopo hospitali za Apollo kuwaasa watu kuhusu mifumo na staili za maisha yao ili kujikinga na kisukari.

Kambi hiyo itakuwa na; vipimo vya sukari katika damu, mchanganuo wa mafuta mwilini, na namna ya kuepuka kisukari ambapo hospitali za Apollozitatoa somo kuhusu milo kamili kutoka kwenye timu yao ya wataalam wa milo. Wataalam hao watafundisha namna ya kujikinga na kisukari kwa kuzingatia milo bora, namna ya kudhibiti kiwango cha sukari mwilini na namna ya kupambana na kisukari kwa ujumla.

Kwa kuona umuhimu wa kutoa huduma hiyo ya kisukari kupitia elimu ya mlo, Dk. Bhuvaneshwari Shankar Mkuu wa idara ya lishe kutoka hospitali za Apollo, ana lengo la kuwaelimisha watanzania kuhusu mambo muhimu wanapaswa kuyajua kuhusu kisukari na mlo kamili katika siku hii ya kisukari duniani.

Kula kwa afya ni silaha bora kujikinga na kisukari. Mazoezi ya mara kwa mara na mlo kamili vinasaidia sana. Hamna chakula mahususi au mfumo mgumu wa lishe unaohitajika.
Dk Bhuvaneshwari Shankar anatutia moyo kula milo mitatu kama inavyostahili kitu ambacho watanzania wengi hatufanyi hivyo.

“muda mrefu bila chakula kunafanya sukari kushuka, na utajikuta unakula chakula kingi ambacho kitapelekea sukari katika damu kutokuwa sawa. Alisisitiza.

Ratiba nzuri ya chakula cha mtu wa kisukari kinatakiwa kiwe na mafuta kidogo, mboga mboga, katika siku ni muhimu. chakula kingi kinanafanya sukari ya mwili kutokuwa sawa. Angalizo linahitajika katika uchaguzi sahihi wa vyakula.

Katika chaguo sahihi la vyakula “Dk Shankar wa hospitali ya Apollo anasisitiza umuhimu wa watanzania kudhibiti kiwango cha sukari katika damu kwa kufuata mlo sahihi.chagua vyakula vyenye nyuzinyuzi, na kabohaidreti ndogo ni muhimu. Epuka bidhaa nyingi zilizochujwa nyuzi zake, ila chagua unga. Unga ulio na virutubisho vyote ni wa muhimu. Dhibiti kiwango cha mafuta kuingia  mwilini, na epuka mafuta yaliyotengenezwa.

Ule milo 3 kwa siku na vitafunwa hapo katikakati. Chagua milo yenye nyuzinyuzi sana zaidi ya ile yenye kabohaidrates, mbogamboga zenye stachi Epuka chokleti, barafu tamu zenye mafuta na sukari nyingi. Chagua samaki wazuri na kuku wakuchemsha sio kukaangwa na mafuta. Chagua maziwa yenye mafuta kidogo.Dumisha uzito unaopaswa kwa kufanya mazoezi kwa kutembea na kula katika muda muafaka, alisisitiza  Dk. Shankar.

Kisukari ni ugonjwa unaoathiri watu katika umri wowote ambapo mwili unashindwa kutengenzea sukari ya kutosha au kushindwa kutumia inslulini iliyotengezwa hivyo kupelekea kiwango cha sukari mwlini kutodhibitiwa. Mwili wa mwanadamu unapata sukari kutoka kwenye sehemu kuu mbili; kwanza kutoka kwenye vyakula tunavyokula, pili kutoka kwenye ini linalotengeneza pindi unapokuwa hujala chakula. Mwili unabadilisha hii sukari na wanga kwenda na kuwa nguvu kwa kutoa homoni zinazoitwa insulin zinazotengenezwa na kongosho.

Kuhusu Hospitali za Apollo
Hospitali ya Apollo ilifunguliwa mnamo mwaka 1983, na kutoka kipindi hicho imekuwa ikiendeshwa kwa kauli mbiu isemayo "Dhamira yetu ni kuleta huduma ya kisasa karibu kabisa na walengwa. Tunajitolea kutoa huduma bora na mafanikio katika elimu na  utafiti kwa ajili ya jamii  ya kibinadamu".Katika miaka 30  tokea kuanzishwa kwake, hospitali ya Apollo imeandika historia kubwa kupata kuonekana nchini India. Ni moja ya kampuni kubwa ya Afya katika bara la Asia, na pia imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya nchini india.

Katika safari yake, imeweza kuboresha maisha ya watu wapatao milioni 39 kutoka nchi 120.Inatoa huduma maalum 52 na vitanda vya upasuaji 710.Imefanya upasuaji wa moyo wenye kufikia idadi ya watu 152,000 na panuzi 125, 000 za mishipa myembamba.Imefanya upasuaji wa wa viungo unaopita kiasi cha idadi ya watu 10,000, upasuaji wa uvimbe wa ubongo, uti wa mgongo na zaidi.Taasisi ya Apollo ni moja ya taasisi zinazoongoza nchini india, zikiwa na teknolojia za kisasa kama Novalis TX, PET MRI na Upasuaji unaotumia mashine za kiroboti.

BEI YA MADAFU LEO

Watu 3 Wafikishwa Mahakamani Kwa Matumizi Mabaya Ya Mtandao Mwanza

AECF YAZINDUA AWAMU YA NNE YA DIRISHA LA UFADHILI WA KILIMO BIASHARA HAPA NCHINI.

$
0
0
Mkurugenzi wa The African Enterprise Challenge Fund (AECF), Hugh Scott akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na uzinduzi wa awamu ya nne ya dirisha la ufadhili wa kilimo cha biashara maalum kwaajili ya watanzania hapa nchini.
Afisa mkuu wa usimamizi, Sam Ng'ang'a akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kushoto ni Mkurugenzi wa The African Enterprise Challenge Fund (AECF), Hugh Scott.
Mkurugenzi wa kampuni ya Internation Tan Feed LTD, Faustine Lekule akizungumza na waandishi wa habari leo kwa jinsi kampuni yake ilivyoweza kunufaika na ruzuku inayotolewa na AECF kwa kuweza kugundua aina mbalimbalimbali za vyakula vya mifugo hapa nchini.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
MFUKO wa The African Enterprise Challenge Fund (AECF) umezindua awamu ya nne ya dirisha  la ufadhili wa kilimo cha Biashara na huduma za kifedha vijijini hapa nchini.

Ameyasema hayo Mkurugenzi wa mfuko wa The African Enterprise Challenge Fund (AECF), Hugh Scott wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Scott amesema kuwa sambambamba na kuzindua awamu ya nne kutakuwa na shindano lenye lengo la kuhamasisha watu wenye mawazo ya kilimobiashara kwaajili ya kupewa ufadhili wa waombaji watakaoshinda katika shindano hilo.

"Waombaji watakaoshinda watapewa ruzuku na mikopo isiyo na riba kati la dola za kimarekani laki moja na dola za kimarekani milioni moja", alisema Scott

Pia Scott ametoa wito kwa makampuni mbalimbali, sekta mbalimbali au vikundi yenye mawazo ya kilimobiashara kutuma maombi kwenye mtandao wa intaneti wa www.aecfafrica.org ili kuweza kuomba  na kushindania shindano.

Aidha  Scott amesema kuwa shindano hilo lipo wazi kwa makampuni yanayotengeneza faida na linahamasisha makampuni ya ndani na kampuni ya kigeni kuomba nafasi hiyo lakini mawazo yake yawe ya kilimobiashara yatakayopendekezwa katika uombaji lazima yawe yanafanyika hapa nchini.

Pia amesema kuwa shindano hili limeshaanza kuanzia leo na mwisho wa kutuma maombi ni Disemba 15 mwaka huu.

Scott alitoa wito kwa sekta binafsi kuchangamkia frusa iliyotolewa na mfuko wa AECF  hapa nchini kutokana na kuzinduliwa kwa mara ya nne na kwa ufadhili wa kilimo biashara ili waweze kuitikia na kuwa na mawazo ya biashara yenye ubunifu ambayo yataleta manufaa kwa maisha ya watanzania waishio vijijini.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.

       TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
   “PRESS RELEASE” TAREHE 17.11.2015.
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA LUSUNGO WILAYA YA RUNGWE AUAWA KWA KUKATWA PANGA.
MWANAMKE MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA ILEA WILAYA YA CHUNYA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA MTI.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA LUSUNGO WILAYANI RUNGWE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EZEKIEL MWALWEGA [34] ALIUAWA KWA KUKATWA MAPANGA KICHWANI, MGONGONI NA BEGA LA KULIA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 15.11.2015 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA KIPAPA, KATA YA LUFILYO, TARAFA YA BUSOKELO, MKOA WA MBEYA. 

INADAIWA KUWA, CHANZO CHA TUKIO HILO NI USHABIKI WA KISIASA BAINA YA KIJIJI CHA LUSUNGO NA KIJIJI CHA LUPOTO KATIKA KUGOMBEA NAFASI YA UDIWANI KATA YA LUFILYO.

WATUHUMIWA WANNE WAMEKAMATWA KUHOJIWA KUHUSIANA NA TUKIO HILI AMBAO NI 1. PAUL MWANDOMBWA [36] MKAZI WA KIFULA 2. IPYANA MWAMAKIMBULA [18] MKAZI WA KIPAPA 3. THOMAS MWASALUKUMO [58] MKAZI WA KIPAPA NA 4. BENJAMIN MWAMBUGA [17] MWANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI LUFILYO KIDATO CHA TATU, MKAZI WA MPULO.

INADAIWA KUWA WATUHUMIWA HAO WANAHUSIKA KATIKA MAUAJI YA MAREHEMU WAKATI AKIWA NA WENZAKE KWENYE GARI MBILI WAKIWA WANATOKA KIJIJI CHA LUPOTO KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI KATI YA KIJIJI CHA  LUPOTO NA KIJIJI CHAO CHA LUSUNGO.

KATIKA TUKIO LA PILI:
MWANAMKE MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA ILEA WILAYANI CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA REMMY UDODI @ JILALA [34] ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA MTI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 15.11.2015 MAJIRA YA SAA 16:20 JIONI HUKO ILEA KATI, KIJIJI CHA ILEA, KATA YA IFWENKENYA, TARAFA YA SONGWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. 

INADAIWA KUWA, MTI HUO ULIANGUKA KUTOKANA NA MVUA KUBWA ILIYOKUWA INANYESHA HUKU IKIAMBATANA NA UPEPO MKALI HALI ILIYOPELEKEA MTI KUMUANGUKIA MAREHEMU. 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA MAKINI HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA ZA VULI IKIWA NI PAMOJA NA KUEPUKA KUKAA KARIBU NA MITI MIKUBWA KWANI NI HATARI. 
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images