Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 686 | 687 | (Page 688) | 689 | 690 | .... | 1897 | newer

  0 0

   
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Bw. Sabasaba Moshingi, (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta ya Akiba, Kenya, Bi.Anne Karanja, (Katikati), na Mkurugenzi Mtendaji Benki ya Posta Uganda, Bw. Stephene Mukweli, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa mkutano wan ne wa Bodi ya Wadhamini, ya Umoja wa Mabenki ya Afrika Mashariki, ASBEA, uliomalizika Novemba 13, 2015 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. (Habari picha na K-Vis Media/Khalfan Said)
  AFISA Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Bw. Sabasaba Moshingi, amewahimiza wananchi wa nchi za Afrika Mashariki kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba kwenye akaunti zao.

  Bw. Moshingi aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kutano wanne wa bodi ya wadhamini ya Umoja wa Mabenki ya Akiba wa Nchi za Afrika Mashariki, (ASBEA), uliomalizika Novemba 13, 2015 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

  “Lengo la Umoja huu ni kuhamasishawananchi wan chi wanachama wa ASBEA, kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba kama njia ya msingi ya kutokomeza umasikini, kimarisha uchumi na kujenga uwekezaji wenye faida katika uchumi wa mataifa yetu.” Alisema

  Afisa Mtendaji huyo ambaye alikuwa mwenyekiti wa mkutano huo uliohudhuriwa pia na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta ya Akiba ya Kenya, (KPOSB), Anne Karanja, na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta nchini Uganda, Stephene Mukweli, pamoja na wajumbe wengine, alisema Nchi za Afrika Mashariki bado zipo nyuma kwenye suala zima la uwekaji akiba na kutolea mfano Tanzania, ambapo alibainisha

  “Takriban asilimia 14 tu ya wananchi wa Tanzania ndiowanaojiwekea akiba kwenye akaunti zao, kiasi hiki ni kidogo sana ukilinganisha na asilimia 23 ambayo ndio wastani wan chi zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara.” Alisema Bw. Moshingi.

  Umoja huo wa ASBEA ulioanzanishwa mnamo mwaka 2001, unakusudia kupanua wigo wa wanachama wake ambapo uko kwenye majadiliano ili kuzishawishi nchi za Rwanda, Burundi na Sudani Kusini kujiunga na umoja huo.

  Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta ya Akiba ya Kenya,Anne Karanja alisemaukuaji wa teknolojia umeleta changamoto kubwa katika sekta ya kibenki barani Afrika na hivyo ni wajibu wa wa ASBEA kuangalia namna bora ya kuitumia teknolojia hiyo katika kuzipeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi ili kukuza uchumi wao na nchi wanachama kwa ujumla.

  Jumuiyaya ASBEA inajumla ya wateja milioni 3, wanaoweka takriban akiba ya zaidi ya dola za Kimarekani milioni 314 katika amana, wakijivunia utoaji huduma kupitia mawakala, magari ya kutolea huduma, matawi ya Benki na ATMs.
   Wajumbe wakimsikiliza mtoa mada, Mkurugeni Mtendaji wa Benki ya Posta Kenya, Bi.Anne Karanja
   Bi. Anne Karanja
   Bw. Stephene Mukweli
   Bw. Sabasaba Moshingi
   Mjumbe akizungumza
   Wajumbe wakisikiliza kwa makini
   Mjumbe kutoka Tanzania kifuatilia kwa umakini mkutano huo
   Afisa wa Benki ya Posta Tanzania, akifuatilia mad zilizokuwa zikitolewa
   Wajumbe wa bodi ya ASBEA, wakiongozwa na Bw. Moshingi, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya mwenendo wa mkutano wao na malengo yake


  0 0

   Mkurugenzi wa AUWSA, Inj. Ruth Koya akiwa anasoma gharama mpya ambapo zilipendekezwa kuongezwa na changamoto walizonazo
   mgeni rasmi wa mkutano huo ambaye ni mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda wa pili kulia  akiwa na baadhi ya viongozi  waliokaa meza kuu
   picha juu na chini wananchi waliouthuria katika mkutano huo

  mmoja wa wananchi  aliyejitambulisha kwa jina la  Ayubu
  Mshote akichangia mada
  mwananchi wa kata ya sombetini Jenifa Sumaye akiwa
  anachangia mada wakati  mkutano wa wadau na watumia
  wa maji ulioandaliwa na mamlaka ya huduma na uthibiti wa nishati na
  maji (EWURA)uliofanyika katika viwanja vya makumbusho ukiendelea

   Na Woinde Shizza,Arusha

  Wananchi wa jiji la Arusha wamekataa kupandishwa kwa gharama za maji
  kutokana na kutokuwa na kutokupatiwa huduma bora ya maji na mamlaka ya  maji safi na maji taka(AUWSA) ya jiji hili.

  Hayo waliyasema jana jiji hapa wakati wa mkutano wa wadau na watumia
  wa maji ulioandaliwa na mamlaka ya huduma na uthibiti wa nishati na
  maji (EWURA)uliofanyika katika viwanja vya makumbusho jijini hapa.

  Walisema kuwa hawawezi kukubali mamlaka ya maji safi na maji taka
  kupandisha gharama za maji wakati huduma ambazo wanazitoa sio nzuri na
  hadhikithi maitaji ya wananchi .

  Kwa upande wa mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Ayubu
  Mshote alisema kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikipata faida kila mwaka
  lakini wameshindwa kuboresha miundo mbinu yake hali inayofanya kuwepo
  kwa tatizo la maji pamoja na upotevu wa maji .

  Alisema kuwa faida wanayopata AUWSA ikitumika vyema kwa mahesabu
  inaweza kugharamia shuhuli za uendeshaji na uwekezaji  na pia
  itasaidia kuweza kubuni vyanzo vipya vya maji vitakavyosaidia
  kuboresha huduma za maji na kumfikia kila mwananchi .

  Naye Jenifa Sumaye alisema kuwa kumekuwa na tatizo kubwa sana la maji
  katika jiji hili hali ambayo inawafanya wananchi kununua maji kwa bei
  ghali ,na pia aliitupia mamlaka hiyo ya maji lawana na kusema kuwa
  wamekuwa wanakata maji kwa kipindi kirufu halafu wanakuja kusoma mita
  na kutoa bili ambayo sio ya kweli.

  Kwa upande wake kaimu mwenyekiti wa baraza la ushauri na watumiaji wa
  huduma za nishati na maji (EWURA CCC) Mubezi Lutaihwa alisema kuwa wao hawajaunga mkono upandishwaji wa bei za huduma ya maji kwani mamlakahiyo ingebana matumizi na kuongeza ufanisi  katika kutoa huduma na sio kuwapandishia wananchi gharama.

  Alisema kutokana na histori ya upatikanaji wa faida wa AUWSA baraza
  alioni kama kunasababu yeyote ya kupandisha bei ya huduma kwa sasa
  kwani faida inayopatika inatosha kugaramia shuhuli za uendeshaji n
  uwekezaji.

  Kwa upande wa mkurugenzi wa AUWSA Eng.Ruth koya alisema Wao  wameamua kupendekeza kupandishwa kwa gharama za maji ili kuweza  kutoa huduma bora na kuweza kukarabati miundo mbinu ya maji.

  “Tunapandisha gharama hizi ili kuweza kutoa huduma bora pamoja na pia
  kwa tumepandisha ili kuweza  kupata hela ya kutatua changamoto
  mbalimbali kwani kwa sasa tumeondolew msamaha wa kodi ya ongezeko la
  thamani na sasa hivi tunalipia asilimia yote mia moja na pia garama za
  umeme zimezidi hivyo tunaongeza ili tuweza kutatua matatizo
  hayo”alisema koya.


  Kwa upande wa kaimu mkurugenzi wa EWURA Nzinyangwa Nchani alisema kuwa wamepokea maoni kwa ujumla watayafanyia uchambuzi wa kina na kuona pendekezo lipi linafaa au kitu gani kifanyike na pia watapitia
  historia ya mamlaka hiyo na watatoa maamuzi ili wananchi waendelee
  kupata huduma bora.

  0 0

  Mbunge mteule wa Jimbo la Mtama, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape akisaini mkataba wa kupata vifaa vya huduma za afya mbele ya Mwambata wa Siasa wa Ubalozi wa China nchini Tanzania Mis Song Rui katika ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China.

  Mbunge Mteule wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye ameanza kazi ya kuwatumikia wakazi wa jimbo hilo baada ya kusaini mkataba maalum na Ubalozi wa China nchini wa kusaidia vifaa vya huduma ya Afya kwa jimbo la Mtama.

   Ikumbukwe katika kampeni zake Nape aliahidi kulifanya jimbo kuwa la mfano kwa kuboresha huduma mbali mbali za kijamii ikiwemo afya na elimu.

  Akiongea na mwandishi wa habari hizi Nape alisema " Wakati nimeamua kugombea ubunge nilisema nataka kuwafanyia kazi watu wa Mtama nataka niwe mbunge wa mfano na niliwaahidi nitatatua kero zao mbali mbali na leo nimeanza kwa upande wa huduma za afya ambapo vituo na zahanati kadhaa vitapata vifaa vya matibabu alivitaja baadhi ya vituo ni Mtama, Nyangamala, Chiponda, Namupa, Chiuta,Luo, Nyengedi,Kiwalala na kwengineko."


  0 0  0 0


  UTSS is sponsoring the first ever Pan - African Albinism Conference PAAC) which will take place in Dar es Salaam, Tanzania, at the Julius Nyerere Conference Centre on November 19 – 22, 2015.

  2015 PAAC theme:  Making attacks, stigma and discrimination a faint memory.

  Pan African Albinism Conference (PAAC) set to gather leading organizations of persons with albinism (PWA) and those that work with and for PWA from Africa and infamous international and local experts on albinism genetics, skin cancer, low vision and human rights and legal issues.  

  The aim of this major conference is to create a sanctuary of learning, networking and empowerment for PWA in Africa, equipping them with the best resources UTSS has managed to accumulate to date.

  The conference will be blessed with more than 200 participants from 29 African countries and 9 non-African countries in North America, Europe, Scandinavia and Japan.  PAAC sessions will be conducted in three languages:  English, French and Kiswahili.
  “PAAC is designed to equip defenders of the human rights of persons with albinism (PWA) with the necessary tools for preventing attacks, ensuring prosecution of perpetrators of attacks, monitoring the overall human rights situation of PWA including how to make credible reports, and properly advocate before their government for better responses to their plight,” says Peter Ash, Founder and CEO of Under The Same Sun.

   “UTSS hopes this will kick start other similar initiatives across continent of Africa through which concrete results will lead to practical changes in the lives of persons with albinism,” concludes Ash.

  The opening key note address will be delivered by Peter Ash, UTSS Founder / CEO.
  All PAAC attendees with albinism will benefit from free skin cancer screening and will be provided with sunscreen lotion; low vision examination and will be given vision-enhancing spectacles, low vision devises and sunglasses through experienced clinicians of Standing voice, a partner of UTSS.

  All persons with albinism will benefit from free skin cancer screening and will be provided with sunscreen lotion; low vision examination and will be given vision-enhancing spectacles, low vision devices and sunglasses.  

  There will be various visual displays of the plight of persons with albinism, such as photo-reportage by the World Bank Art Programme; hand-made craft pieces produced by UTSS’ Women’s Development Groups and a miniature of “Nithamini” (“Value Me”) Monument which depicts a protective and loving family of a child with albinism and also honours the lives of murdered and maimed PWA in Tanzania.
   
  PAAC will also form as a platform for PWA to learn about how to protect their skin; get the best out of low vision devices; how to document attacks; how to collect evidence and use it in court cases to get justice; how to engage their governments in PWA-related issues and how to promote their human rights and wellbeing. 

  It should be noted that for more than a decade there have been hundreds of PWA attacks and killings reported in 25 different African countries.  However, many victims and their families are still waiting for justice to be done.  Most of the cases do not reach the courts of law.  Further, stigma and discrimination is epidemic across the continent
  Facilitators / trainers include one of the world’s leading geneticists with decades of experience in albinism and renowned legal experts from UN and African courts and law firms.
  The four-day training programmes will incorporate interactive workshops to develop the skills of attendees on topics including:
  1. The science of albinism:  genetics of albinism, skin and skin cancer prevention, low vision and visual maximization with visual aids;
  2. How to document incidences of attacks for reporting and for preparing for prosecution;
  3. Preparing facts to assist prosecution;
  4. How to produce reports on their situation for their governments, regional bodies and international bodies;
  5. How to best advocate for PWA before the public at large, key audiences and before their government;
  6. Education system: disability rights pertaining to albinism and reasonable accommodation;
  7. National Policy on Albinism: How to advocate for and obtain one.


  Overall PAAC goals include:
  • to protect the Lives of PWA by educating PWA leader-attendees on how to effectively advocate for PWA in their country, i.e. advocating for prosecution in cases of attacks and the enjoyment of their human rights; to improve the human rights, dignity and future prospects for PWA by training PWA leader-attendees on how to educate key public groups such as parents of children with albinism,  educators of students with albinism and the medical profession on the truths about albinism and how to care for and provide reasonable accommodation for PWA.

  Short term goals in detail:

  a.       Report cases of attacks in a credible and professional way
  b.      Hold government accountable for the treatment of persons with albinism by better equipping defenders of human rights of persons with albinism to document cases of attacks in a way that will inform prosecution as needed.
  c.       Understand and spread the truths about albinism including its genetic information and end myths and stereotypes that contribute to human rights violations.
  d.      Understand and replicate health models learned about in the conference to address skin and vision issues associated with albinism.
  e.       Learn effective ways to better advocate for the rights of persons with albinism.
  f.       Encourage participants to achieve the above by engaging them in a post-project contest as described above.

  For more information about the conference please visit:  Conference.TZ@underthesamesun.com
  For more material about UTSS activities and relevant documents please visit: http://www.underthesamesun.com/aboututssAND

  For media enquiries about PAAC please contact:
  Vicky A Ntetema
  Executive Director, UTSS-TZ
  Taasisi Road, Mikocheni B, Kwa Warioba
  P.O. Box 32837, Dar es Salaam, Tanzania
  Tel:  +25522278024  Ext: 102  Fax:  +255222782356
  Mob: +255756048487 / +255787600136/ ++255679448258


  -Ends-   About Under The Same Sun (UTSS) Canada & Tanzania:

  Under The Same Sun (UTSS) is passionately committed to ending the often deadly discrimination against people with albinism. UTSS promotes, via advocacy and education, the wellbeing of persons with albinism who in many parts of the world are misunderstood, marginalized, and even attacked and killed because of their genetic condition. UTSS is founded on the belief that all persons are created in God’s image and as such are worthy of love, respect and, above all, dignity. 

  While UTSS acts globally, much of our focus has been on the crisis faced by people with albinism in Tanzania. From there, UTSS is reaching across Africa and the world, to stimulate a movement that roots out discrimination and plants the seeds of empowerment for people living with albinism.

  OUR VISION:
  “I have a dream that one day people with albinism will take their rightful place throughout every level of society, and that the days of discrimination against persons with albinism will be a faint memory - EVERYWHERE!” - Peter Ash, Founder & CEO

  OUR MANDATE:
  Under The Same Sun is passionately committed to social inclusion and seeing an end to the general and sometimes deadly discrimination against persons with albinism (PWA). We exist to promote, via advocacy and education, the wellbeing of PWA who in many parts of the world are marginalized, misunderstood, abused and at times mutilated and killed because of their genetic condition.

  At UTSS we are driven by the belief that all persons have intrinsic value as each is created in God’s image. Accordingly, all persons are worthy of love, respect and, above all, dignity.

  While UTSS is active at the UN and globally, much of our current focus is on the crisis faced by PWA in Tanzania. We have developed offices there with a highly innovative and effective approach to this issue. This is beginning to bring about the societal transformation needed to stop the stigma based attacks and killings. From there, UTSS is reaching across Africa and the world to stimulate a movement that roots out stigma and discrimination by planting the seeds of empowerment for people living with albinism.

  UTSS Official Summary of Albinism:

  Albinism is a rare, non-contagious, genetically inherited difference occurring in both genders regardless of ethnicity, in all countries of the world. BOTH the father and mother must carry the gene for it to be passed on even if they do not have albinism themselves. The condition results in a lack of pigmentation in the hair, skin and eyes, causing vulnerability to sun exposure and bright light. Almost all people with albinism are visually impaired, with the majority being classified as “legally blind”.  While numbers vary widely and no comprehensive studies have been conducted, it is reported that in North America and Europe, an estimate of 1 in every 17,000 to 20,000 people have albinism. In Africa it is estimated that 1 in every 5,000 to 15,000 people have albinism with selected populations having estimates as high as 1 in 1,000. In Tanzania where UTSS is based, the prevalence of albinism is estimated to be 1 in 1,400 people being affected.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kumpongeza Nahodha wa Timu ya Taifa Stars, Nadir Haroub 'Canavaro', baada ya mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la dunia kati ya Taifa Stars na Algeria  uliochezwa jana. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao ya Stars yalifungwa na Elias Maguli na Mbwana Samatta. 
  Akizungumza na wachezaji hao baada ya mchezo huo, Mhe. Samia,aliwataka wachezaji na viongozi wa Stars kutovunjika moyo kutokana na matokeo ya mchezo huo, na kuwataka kuongeza juhudi na kujituma zaidi katika mchezo wa marudiano ili ukweza kupata matokeo mazuri zaidi.
  ''Japo mmefungwa lakini tumewaona jinsi mlivyojituma, msivunjike moyo na matokeo ya mchezo, kwani tumeowana mlivyocheza kwa kujituma, hivyo naamini hata ugenini mtaweza kupata matokeo mazuri zaidi mkiwa na moyo huo huo wa utaifa, juhudi na kujituma,
  Mtangulizeni mungu kwa kila jambo na kwa uwezo wake naamini mtaenda kufanya vizuri katika mchezo wa marudiano, na nawatakieni safari njema leo usiku kuelekea mchezo huo wa marudiano, sisi wazee wenu na Watanzania wote tupo nyuma yenu tunawaombe muweze kuwatoa waarabu hawa wenye fitina kali katika mchezo wa Soka''. alisema Mhe. Samia 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kumpongeza mchezaji wa Timu ya Taifa Stars, Thomas Ulimwengu, baada ya mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la dunia kati ya Taifa Stars na Algeria  uliochezwa jana. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao ya Stars yalifungwa na Elias Maguli na Mbwana Samatta.  Kulia ni Mbwana Samatta, akibugujikwa na machozi.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimfariji mchezaji wa Timu ya Taifa Stars, Mbwana Samatta, baada ya mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la dunia kati ya Taifa Stars na Algeria  uliochezwa jana. Baada ya mchezo huo Samatta, alionekana kubugujikwa na machozi muda wote. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao ya Stars yalifungwa na Elias Maguli na Mbwana Samatta.  Picha na www.sufianimafoto.com
  KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE


   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishangilia sambamba na baadhi ya Viongozi bao la kwanza la Taifa Stars lililofungwa na Elias Maguli, katika kipindi cha kwanza kwenye mchezo wa Kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la dunia dhidi ya Algeria uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao ya Stars yalifungwa na Elias Maguli na Mbwana Samatta. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Jamal Malinzi, wakati walipokuwa Uwanja wa Taifa katika mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la dunia kati ya Taifa Stars na Algeria  uliochezwa jana. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao ya Stars yalifungwa na Elias Maguli na Mbwana Samatta.
   Sehemu ya mashabiki waliokuwa Jukwaa kuu
   Sehemu ya mashabiki waliokuwa Jukwaa kuu
   Sehemu ya mashabiki waliohudhuria mtanange huo jana
   Sehemu ya mashabiki waliokuwa Jukwaa kuu
   Ila moja kati ya kituko ilikuwa ni hiki kiti kilichokatika mguu mmoja eti katika mchezo wa kimataifa kama huu hwakupata kiti chenye hadhi kulingana na mchezo wenyewe
   Timu zikiwa tayari kuanza mtanange huo, hapa zikipigwa nyimbo za taifa
   Mudathir Yahya, akiwachora nane waarabu....
   Mbwana Samatta, akitesa Waarabu kwa vyenga,akiwageuza atakavyo..
   Waarabu waliimarisha ulinzi zaidi kwa Mbwana Samatta.....
  Beki wa Stars, Shomari Kapombe, akiruka kwanja la mchezaji wa Algeria

  0 0

   Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ambapo ajenda kuu ilikuwa kujadili majina ya wana-CCM walioomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Uspika na Unaibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philipo Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia).
   Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kikiendelea ndani ya ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi mjini Dodoma.


   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Muhagama muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha kamati kuu mjini Dodoma.
  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza na Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Mhe. Zakhia Meghji muda mfupi kabla ya kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ambayo ilikuwa na ajenda ya kujadili majina ya wana CCM walioomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Spika na Unaibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  0 0

   Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

  Nuru inapoiangazia dunia, huwaangazia viumbe vyote vilivyo hai na visivyo na uhai, viumbe vyenye uhai, hao hufurahia nuru hiyo kwa kuruka ruka na kucheza kufurahia nuru hiyo.

  Kila ifikapo asubuhi na mapema, utasikia sauti na mili­o ya ndege wa angani, wanyama wa kufuga na waishio mwituni, milio na sauti za viumbe hao wakati mwingine kuashiria kuwa kumekucha ili waendelee kufurahia nuru inayowanaagazia kwa manufaa ya maisha yao. 

  Wanadamu nao wakiwa kama viumbe hai wengine, huanza kujiandaa asubuhi na mapema kuelekea huku na kule kutafuta riziki ya kila siku ili maisha yao yaendelee kusonga mbele baada ya nuru kuwangazia.

  Mwandishi wa makala haya anaifananisha nuru hiyo inayoiangazia dunia na Amani. Amani ni tunu adhimu, ni tunu yenye Baraka na fanaka, amani inapotamalaki duniani, binadamu na kila kiumbe chenye uhai huonesha furaha yake kwa namna kiumbe hicho kinavyoguswa na amani hiyo.

  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sheria Na.15 ibara 3 ya 1984 nayo inajali na kuzingatia amani hiyo ndiyo maana inatamka kuwa “Sisi Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani”.  0 0

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa NEC ,CCM Makao Makuu Dodoma akiwa ameshikilia kitabu cha Kanuni za Kamati ya Wabunge Wote wa Chama Cha Mapinduzi.


  Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika leo Novemba 15, 2015 mjini Dodoma imewateua wana-CCM watatu watakaopigiwa kura na wabunge wote wa CCM ili kumpata mgombea wa CCM katika nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  Walioteuliwa kugombea nafasi hiyo na Kamati Kuu iliyofanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni pamoja na Naibu Spika aliyemaliza muda wake Ndugu JOB NDUGAI, Dkt. TULIA ACKSON na Ndugu ABDULAH MWINYI.  Kwa upande wa Naibu Spika wa Bunge, mchakato wa kuchukua fomu kwa wabunge wa CCM wanaoomba ridhaa kugombea nafasi hiyo utaanza kesho Novemba 16, 2015 na kukamilika Novemba 17, 2015 saa kumi kamili jioni.  Wana-CCM hao watatu watapigiwa kura na Kikao cha Kamati ya Wabunge wote wa CCM kitakachofanyika kesho Novemba 16, 2015 saa nne asubuhi katika ofisi za Makao Makuu ya CCM Dodoma ilikuchagua jina moja kugombea nafasi hiyo katika Bunge la Jamhuri ya Muungano.
   
   Kuhusu nafasi ya Naibu Spika, alisema kulikuwa na kasoro za kutofuata kanuni za chama ambapo hadi jana ni mwanachama mmoja tu ndiye aliyekuwa amechukua fomu ya kugombea ambaye ni Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan ‘Zungu,’ lakini atatakiwa kuchukua fomu upya.
   
  “Ibara ya 57, Kanuni za kamati ya wabunge wote wa CCM toleo la 2010 toleo la nne 2011, mbunge yeyote anayetaka kugombea nafasi ya Naibu Spika atatakiwa kuchukua fomu kupitia kamati hiyo na atairudisha kisha kamati itakaa kupata jina moja,” alisema Nape.

  Kwa mujibu wa maelezo hayo mbunge wa chama hicho anayetaka kugombea Unaibu Spika, atatakiwa kuchukua fomu leo Novemba 16, kwa ada ya Sh 100,000 kisha atairudisha kesho Novemba 17, ndipo kamati itakaa kuchambua na kupitisha jina moja.


   Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye nje ya ukumbi wa NEC mjini Dodoma ambapo majina matatu yalipitishwa.  0 0

  Na Lilian Lundo
  MAELEZO
  DODOMA
  15.11.2015
   
  Mbunge Mteule wa Jimbo la Kyela,  Dkt. Harrison Mwakyembe amesema Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania  atatokana  na uteuzi utakaoidhinishwa na  Bunge na si taarifa zilizopo sasa katika mitandao ya kijamii.
   
  Dkt. Mwakyembe ambaye amewahi kuwa Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya Awamu ya Nne, alisema kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi,  Waziri Mkuu anateuliwa na Rais ambaye huwasilisha jina hilo kwa Spika wa Bunge na baadaye kupigiwa kura na Wabunge.
   
   Mbunge huyo aliyasema hayo leo Jumapili  (Novemba  15, 2015) Mjini hapa wakati alipokuwa akihojiwa na vyombo vya habari kuhusu tetesi zilizopo katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii kuhusiana na jina lake kutajwa kuwa ndiye Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tano.
   
  “Mimi siwezi kuwasemea wananchi na siwezi  kusema kuna watu wengi wanasema hivi,  kwani nafasi ya Uwaziri Mkuu haiji kwa njia ya kura ya maoni, wala kwa  njia ya mitandao ya kijamii ni nafasi ya uteuzi inayoidhinishwa na bunge na ni mamlaka ya Rais wa nchi” alisema Dkt. Mwakyembe.
   
  Aidha, Mhe. Mwakyembe aliwataka Watanzania bila kujali itikadi za dini na vyama vyao wamuombee Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili aweze kuchague viongozi watakao wajibika na ambao wataendana na kasi ya Mhe. Rais.
   
  Wabunge wengine waliotajwa kuwepo kwa uwezekano wa kuteuliwa nafasi ya Uwaziri Mkuu wa Awamu ya Tano ya Mhe. Rais John Pombe Joseph Magufuli ni pamoja na Mhe. William Lukuvi, Mhe.  Prof. Sospeter Muhongo na Mhe. January Makamba.

  0 0

   Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akifafanua jambo kwa umakini mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki kuhusu maandalizi ya tamasha la kumshukuru Mungu kwa amani na utulivu wakati wa Uchaguzi Mkuu litakalofanyika Desemba 25.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki kuhusu maandalizi ya tamasha la kumshukuru Mungu kwa amani na utulivu wakati wa Uchaguzi Mkuu litakalofanyika Desemba 25.

  KAMPUNI ya Msama Promotions imeamua kuandaa Tamasha la muziki wa Injili litakalofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumshukuru Mungu nchi kuvuka salama katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama, alisema wameamua kuua ndege wawili kwa jiwe moja, kwani sasa litafanyika Desemba 25, likibeba Sikukuu ya Krismasi na shukrani hiyo ya kuvuka salama katika Uchaguzi Mkuu.


  Alisema kutokana na tamasha hilo kubeba ajenda hizo mbili kwa pamoja, kamati yake imelipa uzito mkubwa kwa upande wa suala la  maandalizi ambapo wameanza kuzungumza na waimbaji nguli wa kitaifa na kimataifa.

  Msama alisema baada ya tamasha hilo kufanyika Desemba 25 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, litahamia katika mikoa mbalimbali itakayoteuliwa na kamati yake kwa kuzingatia kigezo cha wingi wa maombi na uwezo wao kifedha.

  “Naomba ifahamike, tamasha hili la kumshukuru Mungu kuiwezesha nchi kuvuka salama katika mtihani mgumu wa Uchaguzi Mkuu uliokuwa na ushindani mkubwa, litafanyika Desemba 25 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee,” alisema Msama na kuongeza:

  “Unaweza kuona ni tamasha ambalo safari hii litakuwa na uzito mkubwa, kwani litakuwa limebeba uzito wa Krismasi itakayoambatana na shukrani maalumu kwa Mungu kutokana na kuijalia nchi kuvuka salama katika Uchaguzi Mkuu,” alisisitiza Msama.

  Kuhusu waimbaji, Msama alisema kamati yake itajitahidi kuwaleta wenye uzito na mvuto kulingana  na uzito wa tamasha hilo, akiamini litakuwa na mvuto wa tofauti na yaliyotangulia na kuwasihi wapenzi na mashabiki wa muziki wa Injili kukakaa mkao wa kupokea baraka za Mungu.

  Msama kupitia Kampuni yake ya Msama Promotions, amechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa Injili nchini kupitia ubunifu wake wa kuratibu matukio ya muziki huo kuanzia tamasha la Pasaka, Krismasi na uzinduzi wa kazi za waimbaji mbalimbali.

  Juhudi hizo za Msama ndizo zimeufanya muziki wa Injili kupata umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania kiasi cha kuwa moja ya ajira kwa vijana wenye vipaji na karama ya kumtumikia Mungu kwa njia hiyo ya uimbaji.  0 0

  CHUO Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) kimesherehekea miaka kumi (10) tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005, (2005 - 2015). Maadhimisho hayo yameenda sambamba na mahafari ya Nane katika chuo hicho(2008 - 2015) mahafari yaliyofanyika katika chuo hicho Novemba 14,2015.

  Mahafali hayo yalihudhuriwa na Mgeni rasmi,  Profesa Dkt. Fadzil Adam, Mkurugenzi wa Chuo cha Kiislam cha Morogoro na  mtafiti wa chuo kikuu cha Zanzibar (SZA),wa Nchini Malaysia Kuala Teregganu, Mkuu wa chuo hicho Hajjat Mwantum Mlale, Mkuu wa chuo kikuu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza chuo kikuu cha Kiislam cha Morogoro (MUM), Profesa Hamza Mustafa Njozi, pamoja na Mwenyekiti Baraza la chuo hicho Profesa Bakari Lembariti.

  Mahafari yalifanyika katika chuo kikuu cha Kiislam cha Morogoro (MUM) mwishoni mwa wiki Novemba 14 mwaka huu.
  CHUO Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM)kimesherehekea miaka kumi (10) tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005 - 2015, maadhimisho hayo yameenda sambamba na mahafari ya Nane ya chuo hicho,(2008 - 2015).

  Msafara wa wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) walipo wasili katika viwanja vya chuo hicho kwaajili ya Sherehe ya kuadhimisha miaka kumi ya chuo hicho pamoja na Mahafari ya wahitimu wa Kozi mbalimbali katika chuo hicho, mahafari yaliyofanyika Morogoro mwishoni mwa wiki Novemba 14,2015.
  Wageni wakiwasili katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM). 
  Mkuu wa kitengo cha masomo ya uandishi wa habari katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM), Salim Said Ali (aliyesimama) akiwakaribisha wageni katika Mahafari yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) Novemba 14,2015.
  Mkuu wa chuo hicho Hajjat Mwantum Mlale akiwa katika Mahafari ya nane ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) ambaye pia ndiye aliyokuwa akiwatunuku katika mahari hayo wanafunzi waliofuzu kozi mbalimbali katika chuo hicho.
  Mahafari hayo yalifunguliwa kwa Swala ambapo pichani ni baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wakifungua kwa swala. 
   Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

   
   
   
   Baadhi ya wanafunzi waliofunzu masomo yao na waliohudhuriwa katika mahafari ya Nane ya chuo cha Kiislam cha Morogoro, (MUM) Novemba 14, 2015.


   Baadhi ya wazazi na walezi waliohudhuria katika mahafari ya nane ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) Mkoani Morogoro Novemba 14,2015.


   Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) akivaa Kofia mara baada ya kutunukiwa kufunzu masomo yao katika mahafari ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo Novemba 14,2015.   Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) waliopata zawadi baada ya kufauru kwa kiwango cha First Class katika masomo yao katika mahafari yaliyofanyika chuoni hapo Novemba 14,2015.
   Wageni pamoja na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mafari ya nane ya chuo hicho kumalizika Novemba 14,2015.  Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa chuo hicho katika mahafari ya nane kumalizika yalifanyika chuoni hapo mkoani morogoro Novemba 14,2015..
   Watalamu wa masuala ya Kompyuta wakiwa katika picha ya pamoja katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM).

   Majengo ya mabweni ya wasichana na wafulana yaliyopo katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM)
   Jengo la masomo ya Sayansi katika chuo cha Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM). 
  Ukumbi wa mikutano kwa nje katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM).
  Ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) kwa ndani.
   Kituo cha redio pamoja na madarasa ya wanafunzi wanaosoma masomo ya uandishi wa habari katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM).
   Mwandishi na mwalimu wa somo la redio akitoa maelekezo mara baada ya kutembelewa katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM).
   Jengo la uongozi katika  Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM).

  0 0

  Kutoka kulia ni Meneja wa Kampeni Haki ya Uchumi kutoka Oxfam Eluka Kibona, Ofisa msaidizi wa Programu kutoka Forum CC Jonathan Sawaya, aliyeshiriki shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 Edna Kiogwe, na Evelina Mageni  ambaye ni Rais wa wakulima wanawake vijijini na alikuwa mshiriki wa shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015.
  Meneja wa Kampeni Haki ya Uchumi kutoka Oxfam Eluka Kibona akizungumzia juu ya mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika Novemba 20 2015 kaika Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam
   Ofisa msaidizi wa Programu kutoka Forum CC Jonathan Sawaya akizungumzia kuhusu mkutano mkubwa wa mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika Ufaransa.
   Evelina Mageni  ambaye ni Rais wa wakulima wanawake vijijini na alikuwa mshiriki wa shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 akizungumza umuhimu wa wakulima kushirikishwa katika kutunga sera, utunzaji wa ardhi kwa ajili ya kilimo.
  Kushoto aliyekuwa mshiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 Edna Kiogwe akichangia jambo wakati wa mkutano na waandishi wa Habari kuelekea mkutano mkuu wa Tabia nchi.


  0 0

  Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt Reginald Mengi akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC,Dkt Geleard Masenga wakati alipowasili katika ofisi ya Mkurugenzi  huyo mwishoni mwa wiki. 
  Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt Reginald Mengi akisalimiana na Askofu mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheria (KKKT) Tanzania ,Dkt Fredrick Shoo alipowasili katika ofisi ya Mkurugenzi wa hosptali ya rufaa ya KCMC .(kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hopstali hiyo,Dkt Gileard Masenga.
  Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt Reginald Mengi akiteta jambo na Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheria (KKKT) Tanzania ,Dkt Fredrick Shoo .
  Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt Reginald Mengi akipeana mikono na Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC ,Dkt Gileard Masenga mara baada ya kutamburishwa kuwa ndiye mtendaji mkuu wa hospitali hiyo kwa sasa.
  Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt Reginald Mengi akizungumza jambo mara baada ya utamburisho wa mkurugenzi huyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Hopstali ya Rufaa ya KCMC ,Dkt Gileard Masenga akizungumza jambo mbele ya Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt Reginald Mengi (hayupo pichani).
  Dkt Mengi akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Hosptali ya Rufaa ya KCMC.
  Mkurugenzi mkuu wa Hosptali ya Rufaa ya KCMC,Dkt Giliard Masenga akizungumza kuhusu ujenzi wa ngazi kuu za kungilia wodini katika hosptali ya Rufaa ya KCMC ambazo ujenzi wake uligharimu kiasi cha sh Mil 30 ,Fedha ambazo zilitolewa na Dkt Mengi.
  Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheria ,(KKKT) Dkt Freedrick Shoo akisoma taarifa ya Hosptali hiyo katika hafla fupi ya uzinduzi wa ngazi kuu za kuingilia wodini katika hosptali ya rufaa ya KCMC ,ujenzi uliofadhiliwa na Dkt Mengi.
  Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheria ,(KKKT) Dkt Freedrick Shoo akimkabidhi Dkt Mengi taarifa ya Hosptali hiyo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ngazi kuu za kuingilia wodini katika hosptali ya rufaa ya KCMC ,ujenzi uliofadhiliwa na Dkt Mengi.
  Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt Reginald Mengi akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya ngazi kuu za kuingilia wodini katika hospitali hiyo.
  Baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo.
  Mwenyekiti mtendaji wa Makampuni ya IPP,Dkt  Reginald Mengi akiongozana na Mkurugenzi mtendaji wa Hopstali ya Rufaa ya KCMC wakipita katika ngazi kuu zilizofanyiwa ukarabati hii karibuni.
  Dkt Mengi akitizama baadhi ya maeneo katik awodi za hospitali ya rufaa ya KCMC ambayo miundo mbinu ya maji pamona na vyoo imekuwa chakavu.
  Sehemu ya maeneo ambayo yameathirika na uchakau wa miundo mbinu ya maji.
  Dkt Mengi akisalimiana na mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika hosptali ya Rufaa ya KCMC.
  Mkurugenzi mtendaji wa Hosptali ya Rufaa ya KCMC,Dkt Giliard Masenga akimuonesha Dkt Mengi  maeneo mbali ya hosptali hiyo ambayo upanuzi umeanza kufanyika kama sehemu ya kuboresha huduma ya afya.
  Dkt Mengi akiaga mara baada ya kutembelea hospitali ya rufaa ya KCMC pamoja na kuzindua ngazi kuu za kuingilia wodini.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa tatu kulia) na Mdau wa Keki, Mama Cynthia Henjewele (wa pili kushoto), wakikata keki maalumu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Umoja wa Watengeneza keki Tanzania (TCBA), uliofanyika katika Mgahawa wa City Lounge Posta mpya Dar es Salaam jana. Kulia ni Mshehereshaji, Makena na Mdau wa Keki, Philip Mbonde.

   DC Makonda akitoa hutuba ya uzinduzi.

   Mwanzilishi wa umoja huo, Stellah Rwabutaza (kushoto), akimlisha keki mgeni rasmi DC Makonda. Katikati ni mdau wa Keki Cynthia Henjewele.

  Muokaji  keki,  Roselins Sia Adhero (kulia), akimkabidhi keki DC Makonda.

  0 0

  Na Emanuel Madafa,Mbeya.

  IDADI ya vifo vya watoto wachanga imeendelea kupungua Mkoani mbeya kutoka vifo 602 kwa mwaka 2012 hadi kufikia 568 kwa mwaka 2014  ambapo ni sawa na asilimia 5.7.


  Hali hiyo inatokana timu ya uendeshaji wa huduma za afya mkoa kukaa pamoja na kutafuta ufumbuzi wa pamoja na kuweka maazimio ambayo wamekuwa wakiyatekeleza kwa pamoja.


  Akizungumza jijini Mbeya mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto mkoani humo Ndugu Prisca  Butuyuyu  amesema kutokana na usimamizi huo wameweza kufuatilia  mambo mbalimbali yakiwemo ya upatikanaji wa dawa.


  Amesema hatua nyingine iliyofanikisha zoezi hilo ni pamoja na kushughulikia  mapungufu  na changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza katika vituo vya huduma.


  Amesema  sanjali na mafanikio hayo pia wanatoa pongezi za dhati kwa shirika la UNICEF  kwa kuendelea kusaidia kutoa fedha za usimamizi  shirikishi katika eneo la huduma za afya na uzazi na mtoto.


  Butuyuyu amesema kuwa baadhi ya halimashauri  zimeweza kuendesha semina  mbalimbali kuhusu uzazi salama ambazo ni huduma baada ya kujifungua  pamoja na huduma muhimu kwa watoto wachanga.


  Hata hivyo  amesema shirika la UNICEF wakishirikiana na KOICA  wamekuja na mpango mwingine wa miaka 4 ya uboreshaji huduma za afya ya uzazi na mtoto.

   JAMIIMOJABLOG

  0 0

  Moja ya vyama muhimu katika kuleta mapinduzi ya Kilimo Nchini Tanzania ni Tanzania Agricultural Organisation (TASO). Pamoja na majukumu mengine, TASO ndio wamiliki na wasimamiaji wamaonyesho ya nanenane Nchini Tanzania. 

  Hadi sasa TASO ina viwanja vitano vya maonyesho ya nanenane kwenye kanda za Kaskazini-Arusha, kandayalati –Dodoma, Mashariki – Morogoro, NyandazaJuu –Mbeya na Kanda ya Kusini – Lindi. Mfumo wa utendaji wa TASO umeanzia kwenye Kata, Wilaya, Mkoa, Kanda naTaifa. 


  Juhudi zinafanyika kuanzisha viwanja vya maonyesho kwenye kanda ya Magharibi na kanda ya ziwa katika muda mfupi ujao. Tanzania ikiwa inatumia si zaidi ya asilia 25% ya Aridhi inayofaa kulimwa, Kilimo kinabakia kuwa msingi muhimu wa kukuza uchumi na ajira Nchini Tanzania. 

  Pia izingatiwe kuwa Tanzania ina jumla asilimia 46% ya aridhi yote ya Afrika Mashariki hivyo kuwa na fursa kubwa ya kukuza soko na kulisha nchin yingine za Afrika Mashariki na nje.

  Jumamosi yaTarehe 14 Novemba 2015 mjini Dodoma, TASO ilifanya uchaguzi wa viongozi wa Taifa ambao wataongoza taasisi hii muhimu katika kukuza kilimo kwa miaka 5. Viongozi waliochaguliwa ni Engelbert Moyo – Mwenyekiti, SharifaAbebe – Makamu Mwenyekiti, Imani Kajula – Katibu Mkuu, Daudi Mwalusyamba – Katibu Mkuu Msaidizi na Michael Lupyana – Mweka Hazina.

  Akizungumza baada ya kuchaguliw aMwenyekiti wa TASO Taifa Engelbert Moyo alisema ‘’ Huu ni mwanzo mpya wenye malengo ya kuchochea mchango wa kilimo katika Uchumi, Maisha ya Watanzania, weredi katika kilimo na ajira. Ni fursa adhimu kuwa na viongozi waTaifa wenye ujuzi katika fani mbalimbali; Kilimo, Biashara, Masoko naFedha. Naamini kuwa TASO itapiga hatua kubwa katika kuwa muda muhimu katika kutoa mchango katika sekta hii nyeti’’.

  Nae Katibu Mkuu wa TASO Imani Kajula alisema ‘’ Kilimo ni sekta yenye kuajiri watanzania wengi, lakini imekuwa na changamoto nyingi, tunatambua kazi hii tuliyopewa ni adhimu na muhimu katika kuleta mabadiliko ya kukuza soko la mazao, ubunifu watechnojia rahisi za kilimo, upatikanaji wa habariza kilimo, uvuvi, ufugaji na masoko kwa wakulima na pia kuboresha maonyesho ya Nanenane kuwa jukwaa la kuchochea ukuaji wa kilimo na ajira’’.

  0 0


  Refarii wa mchezo wa ngumi za kulipwa nchini Kondo Nassoro kulia akimnyoosha mkono juu bondia Meshack Mwankemwa baada ya kumnyuka bondia Hamisi mwakinyo katikati ni Promota wa ngumi za kulipwa Jay Msangi akimvalisha mkanda bingwa huyo mpya wa Kg 66 anaetamuliwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC kulia ni Shomari Kimbau Picha na SUPER D BOXING NEWS

  Bondia Meshack Mwankemwa kushoto akiwa na bondia Hamisi Mwakinyo na viongozi na kulia ni Shomari Kimbau wa pili kulia ni rais wa kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa na Jay Msangi.
  Bondia Asha Nzowa 'Asha Ngedere' jkulia akipambana na Joyce Awino wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa CCM Mwijuma mwananyamala Dar es salaam mpambano uho ulimalizika kwa sare.
  Refarii Kondo Nassoro katikati akiwainuwa mikono juu mabondia Asha Nzowa kushoto na Joyce Awino baada ya kutoka droo.

  0 0

  Dkt. Tulia Ackson Mwansasu.

  0 0

  Kaimu mkuu wa mkoa wa Mtwara ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Mtwara Bi. Fatma Ally akikagua wodi ya watoto katika hospitali ya mkoa na rufaa ya Ligula mkoani Mtwara ambayo benki ya Ecobank Tanzania ilijitolea kukikarabati wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya Ecobank ambayo ilifanyika mkoani humo mwishoni mwa juma.
  Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Enoch Osei-Safo akitoa hotuba yake kwa wakazi wa mkoa wa mtwara katika hafla ya kuadhimisha siku ya Ecobank ambayo ilifanyika mkoani Mtwara kitaifa mwishoni mwa juma. Benki ya Eco Tanzania ilisherekea siku hii kwa kukarabati moja ya wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya Ligula mkoani Mtwara ambapo walichangia kiasi cha dola za kimarekani elfu kumi na tano.

  Kaimu mkuu wa mkoa wa Mtwara ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Mtwara Bi. Fatma Ally (katikati) akiwasili kwenye hafla ya kuadhimisha siku ya Ecobank ambayo ilifanyika mkoani Mtwara kitaifa. Katika kusherekea siku hii, wafanyakazi wa benki hii barani Afrika huhamasishwa kujitolea muda wao kwa ajili ya shughuli za kijamii zenye manufaa kwa jamii husika. Ecobank Tanzania ilisherekea siku hii kwa kukarabati moja ya wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya Ligula mkoani Mtwara.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Ecobank Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wa mkoa wa Mtwara wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya Ecobank ambayo ilifanyika mkoani Mtwara mwishoni mwa juma. Katika kusherekea siku hii, wafanyakazi hao walijitolea kufanya shughuli za kijamii ambapo walishiriki katika ukarabati wa moja ya wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya Ligula mkoani Mtwara.
  Kaimu mkuu wa mkoa wa Mtwara Bi. Fatma Ally (wa pili kulia) akipata maelezo ya utaribu mzima wa ukarabati wa wodi ya watoto katika hospitali ya Ligula kutoka kwa Meneja wa tawi la Ecobank-Mtwara Bw. Davis Minja (wa kwanza kushoto). Benki ya Ecobank Tanzania ilijitolea kukarabati wodi hiyo ya watoto wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya Ecobank ambayo ilifanyika mkoani humo mwishoni mwa juma.(katikati) ni Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo hapa nchini Bw. Enoch Osei-Safo.

  IKIWA ni sehemu ya kusherekea maadhimisho ya siku ya Ecobank ambapo wafanyakazi wa benki hii barani Afrika huhamasishwa kujitolea muda wao kwa ajili ya shughuli za kijamii zenye manufaa kwa jamii husika,

  Ecobank Tanzania ilisherekea siku hii kwa kukarabati moja ya  wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya Ligula mkoani Mtwara.

  Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika mkoani Mtwara katika hospitali ya rufaa Ligula, Mkurugenzi mtendaji wa Ecobank Tanzania, Bw. Enoch Osei-Safo alisema benki yake imekuwa ikisherekea “Siku ya ecobank” nchini Tanzania kwa takribani zaidi ya miaka mitatu sasa na kuwa ni mpango unaolenga kusherekea na kuthamini jamii inayoizunguka Ecobank.

  “Tunatambua taifa la kesho lipo mikononi mwa watoto wetu. Kwa kuhakikisha tunawapatia afya bora, watoto watakua wenye nguvu na ushupavu tayari kwa kukabiliana na Dunia”.

  Alisema kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kila Mtoto wa Afrika anastahili maisha bora ya baadaye”
  “Tungependa kusherekea na watoto wa Mtwara kwa kuwaboreshea mazingira katika wodi yao hapa hospitali ya rufaa ya Ligula. Tumejitolea muda wetu na rasilimali zetu kuweka mazingira safi na salama kwa ajili ya watoa huduma pamoja na watoto”.

  Bw. Enoch Osei-Safo aliongezea kuwa sera ya uwajibikaji kwa jamii ya Ecobank Tanzania inawaongoza kutoa ushirikiano kwa jamii mbalimbali katika sekta kadhaa ikiwemo ya afya na elimu huku afya ikichukua asilimia 60 ya miradi yote ya uwajibikaji kila mwaka.

  Akiwasilisha hotuba yake, Kaimu mkuu wa mkoa wa Mtwara ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Mtwara mjini, Bi. Fatma Ally aliyekuwa mgeni rasmi wa shughuli hiyo aliwapongeza Ecobank Tanzania kwa moyo wao mkunjufu katika kukarabati wodi ya watoto na kujitolea muda wao kukaa na watoto hao waliokuwa wamelazwa wodini hapo.

  Bi. Fatma aliihimiza benki hiyo kupanua wigo wa uhisani wao katika sekta ya Elimu, Mazingira, Kilimo na masuala mengine yanayokabili jamii moja kwa moja na akawahakikishia kuwa serikali itaendelea kuboresha huduma za afya katika hospitali mbalimbali, elimu na mazingira mkoa mzima.

  “Tumedhamiria kuendelea kufanya kazi na sekta binafsi pamoja na zile za umma ili kuhakikisha tunaboresha maisha ya mtoto wa Afrika”.

  Naye Kaimu Mganga mkuu wa hospitali hiyo Bw. Joseph Mweru aliipongeza benki hiyo kwa mchango wao na kusema ukarabati huo utasaidia kupunguza vifo vya watoto wachanga ambao hupoteza maisha yao kwa kukosa mazingira safi, salama na hewa safi.

  Takwimu zinaonyesha vifo vya watoto mkoani Mtwara mwaka 2014 vilifikia 385 kutoka 240 vya mwaka 2013. Sababu kwabwa ya ongezeko hili ni ukosefu wa hewa safi, malaria kali na maambukizo ya magonjwa mengine.

older | 1 | .... | 686 | 687 | (Page 688) | 689 | 690 | .... | 1897 | newer