Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 685 | 686 | (Page 687) | 688 | 689 | .... | 1897 | newer

  0 0
 • 11/13/15--01:34: BEI YA MADAFU LEO


 • 0 0


  Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa ofisi ndogo za Bunge  jijini Dar es Salaam kuhusiana na kuachana na uongozi katika siasa.

  ALIYEKUWA Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda amejing'atua rasmi na kuachana na  uongozi katika siasa kutokana na kufanya kazi za Siasa kwa miaka 40.

  ameyasema hayo alipokua akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam leo.

  Anne amesema kuwa "Sitagombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  wala sitachukua fomu ya kugombea nafasi ya uspika wala sifikilii kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika"

  Aidha Anne amesema kuwa katika awamu yake ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kulikuwa na changamoto nyingi kutokana na kuwepo na wabunge vijana.

  Hata hivyo kuwa na changamoto nyingi ila amesema kuwa alilifurahiya sana Bunge hilo kutokana na kuwaelewa wabunge mbalimbali tabia zao hasa wakiwa Bungeni.

  Anne amepsema kuwa Spika wa sasa atakaye shinda nafasi awe si mwepesi wa kukasirika kutokana na changamoto atakazo zipata Bungeni wakati wakijadilia masuala mbalimbali ya Serikali, pia awe mtulivu na kukabiliana na changamoto zitakazo jitokeza.
   Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda leo jijini Dar es Salaam.
  Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
  Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kuzungumza nao leo katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala akizungumza nawanahabari pamoja na Waganga wakuu wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro juu ya tishio la ugonjwa hatari wa Kipindupindu.
  Baadhi ya Waganga wakuu wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Amos Makala ,( hayupo pichani).
  Baadhi ya waandishi wa habari wakiuliza maswali mbele ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala (hayupo pichani) 
  Mganga Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Hajati Dkt Mtumwa Mwako (kushoto ) akiandika mambo kadhaa ambayo yameibuliwa na waandishi wa habari katika mkutano huo.
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. John Mngodo akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Kamishna Jenerali wa Magereza alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Novemba 13, 2015.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa taarifa fupi ya Hali ya Magereza nchini kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. John Mngodo(katikati). Naibu Katibu Mkuu  yupo katika ziara ya kikazi katika Idara mbalimbali zinazounda Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi(wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Stephen Pancras.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. John Mngodo akiongea na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani). Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.

  Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakisikiliza maelekezo ya kiutendaji kazi kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. John Mngodo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi la Magereza.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akimkabidhi taarifa fupi ya Hali ya Magereza nchini Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. John Mngodo mara baada ya kufanya kikao kazi na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. John Mngodo (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Wandamizi wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo leo Novemba 13, 2015( wa tatu kutoka kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kulia) ni Kamishna wa Utawala na Fedha, Gaston Sanga.
  (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0

   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (Kushoto), akisalimiana na Maofisa  wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Braiton Manyo alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo katika mtaa wa Lumumba,jengo la Ushirika,jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,ambaye pia ni Kamishna wa Operesheni, Rogatius Kipali (kulia), akitoa maelezo mafupi kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,John Mngodo, alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo katika mtaa wa Lumumba,jengo la Ushirika,jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,ambaye pia ni Kamishna wa Operesheni, Rogatius Kipali (kulia), akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, taarifa ya ujenzi la Jengo laa  linalotarajiwa kuwa Makao Makuu ya Jeshi hilo, alipotembelea Ofisi za Jeshi hilo zilizoko TAZARA ,jijini Dar es Salaam.

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, akizungumza  na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (hawapo pichani), alipotembelea Ofisi za Jeshi hilo zilizopo TAZARA ,jijini Dar es Salaam.

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (wa tatu kutoka kulia waliokaa),akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji muda mfupi baada ya kumaliza ziara ya kutembelea makao Makuu ya Jeshi hilo na Ofisi zilizopo Tazara,jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Abubakari Akida,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
  Imeandaliwa na Kitengo Cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

   Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Mohamed Seif Khatib mara baada ya kuwasili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi,Ofisi Ndogo Lumumba.
   Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa Sekretarieti Ndugu Anamringi Macha mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za CCM Lumumba.
   Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wapenzi na wanachama wa CCM waliojitokeza kumpokea kwenye Makao Makuu ya Chama Ofisi Ndogo Lumumba.
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisani kitabu cha wageni mara baada ya kuingia kwenye ofisi yake,waliosimama ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Mohamed Seif Khatib (kulia) na Naibu Katibu Mkuu CCM (Bara) Ndugu Rajab Luhwavi.

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  SERIKALI imewaagiza watendaji wa Halmashauri zote za jijini Dar es Salaam kusimamia ipasavyo suala la usafi katika maeneo mbalimbali ili kusadia kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu.

  Katika agizo hilo la Serikali ametoa  wiki mbili kwa watendaji wote kuhakikisha wanaliweka jiji katika hali ya usafi na endapo halitatekelezwa hatua zitachukuliwa dhidi yao.

  Akizungumza na watendaji wa Serikali leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini, amesema kuwa utekelezaji wa malengo waliyokuwa wamejiwekea tangu  2013.

  “Mlipuko wa ugonjwa wa kipindipindu umekuwa janga, kutokana na uchafu kukithiri katika jiji na kusababisha watu kupoteza maisha na wengine kuendelea kuugua,”alisema Sagini.
  Pia amewataka watendaji wa halmashauri kuwatengea maeneo maalum ya kufanyia biashara, mama lishe na baba lishe badala ya kuwafukuza.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam(Dawasco), Mhandisi, Cyprian Luhemeja, alisema kipindupindu hakiwezi kumalizika jijini hapa kama Halmashauri hazitashirikiana na Dawassa na Dawasco.

  Alisema kutoshirikiana kwa halmashauri na mamlaka za maji, kuna sababisha ujenzi holela ambao unapita katika miundombinu ya maji taka.

  Pia alisema changamoto kubwa ambayo watu wengi hawaitambui ni kuhusu wasambazaji wa maji majumbani ambao ndio wamekuwa chanzo kikubwa cha kipindupindu.

  “Wasambazaji hawa wamekuwa wakati mwingine wanasafisha maji taka na kuyasambaza majumbani jambo ambalo linasababisha magonjwa hayo.
  Kutokana na hali hiyo sisi kama DAWASCO hatutamruhusu mtu kusambaza maji kama hana kibali maalumu kilichotoka kwetu,”alisema

  0 0

   Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
  WANANCHI wa Kata ya Saranga Manispaa ya Kinondoni wametakiwa kujitokeza kupiga kura ya Diwani Novemba 15 mwaka huu.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty amesema kuwa kufanya uchaguzi huo kunatokana na kuharibika kwa uchaguzi wa Oktoba 25 ulisababishwa na vurugu.

  Amesema wananchi wanaotakiwa kupiga kura kwa kata hiyo ni wale waliojiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura.
  Natty amesema waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura  ni 58,611 ambao ndio wataoruhusiwa kutimiza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura kwa diwani wanayemtaka kuongoza kata hiyo.

  Amesema vituo vya kupiga vitafunguliwa majira ya saa moja asubuhi na kufungwa saa 10 jioni na baada ya hapo zoezi likiwa limekamilika la uhesabiaji kura atatangazwa mshindi katika uchaguzi huo.

  Uchaguzi wa diwani katika kata hiyo ilitokana na vurugu kubwa ambazo zilianza majira ya 11:000 asubuhi ilifanywa na baadhi ya wasimamizi wa vituo na watu wasiojulikana katika cha kugawa vifaa eneo TANROAD Temboni.

  0 0

  Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa wa Mbeya Ndugu Stellah Kategile akiwasilisha maada kwa wadau wa Sekta ya Afya Mkoani Mbeya katika kikao cha kujadili juu ya kuelekea katika siku ya maadhimisho ya Ukimwi Duniani Tarehe 1 Desemba mwaka huu.
  Mratibu wa kudhibiti Ukimwi Mkoani Mbeya (RACC-Regional AIDS Control Coodinator ) Dkt Francis Philly akizungumza katika kikao hicho ambacho kimehudhuriwa na wadau mbalimbali wa masuala ya afya mkoani  katika ukumbi wa Cofee Garden jijini Mbeya.
  Mrakibu wa Polisi Mkuu  dawati la jinsi na watoto Mkoa wa mbeya Ndugu Debora Mrema akielezea masuala mbaliimbali  yanayolikumba Dawati hilo katika kupambana na ukatili wa kijinsi Mkoani humo huku akisisitiza juu ya wadau kujitokeza na kutoa michango yao ya kifedha sanjali na rasilimali nyingine ili kuweza kutoa elimu kwa jamii katika maeneo mbalimbali mkoani humo hususani maeneo ya vijijini.
  Wadau wakiendelea na majadiliano katika mkutano huo.

  Mwakilishi wa Kampuni ya Mbeya Cement jijini Mbeya ambaye ni Mratibu wa Masulaa ya Afya na Jamii Grace Nyatori akichangia katika mkutano hiuo ambao unalenga kujadili na kupitisha bajeti kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani .
  Mhariri wa habari kutoka Radio Ushindi jijini Mbeya Edom Mwasamya akizungumza namna ambavyo vituo vya radio vitakavyo weza kuchangia kufanikisha zoezi hilo la siku ya Ukimwi Duniani.
  Festo Sikagonamo  kushoto Mkuu wa shirika la Elimisha  pamoja na Neema Stanton Afisa Mahusiano wa Mamlaka ya Maji safi na maji taka jijini hapa wakishirika katika mkutano huo.
  Wadau wakiendelea na majadiliano.
  Na Emanuel Madafa, JamiimojablogMbeya.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisaini kwenye Kitabu cha maombolezo ya msiba wa Mjukuu wa Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, Maryfaustna Mlyambina, aliyefariki Nov 11, 2015. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu zilifanyika leo Nov 13, 2015 Kimara jijini Dar es Salaam, na baadaye msiba huo kusafirishwa kuelekea Mkoani Mwanza kwa maziko.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais John Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimfariji Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu Maryfaustna Mlyambina zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo. Marehemu ni mjukuu wa Mhe Rais. 
  Wazazi wa marehemu wakiwa na baadhi ya wanafamilia, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu.
  Rais Dkt. John Magufuli (wa tatu kuli) Makamu wake (wa Nne kulia) Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Mke wa Rais,Mama Janeth Magufuli (kulia) na Mke wa Rais Mstaafu, Mama Salma Kikwete (kushoto) wakishiriki ibada maalum ya kumuombea marehemu wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika Kimara jijini Dar es Salaam, leo Nov 13, 2015.


  Sehemu ya wanafamilia ya wafiwa katika ibada hiyo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais John Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015.
  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015.
  Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais John Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015.
  Baadhi ya kinamama wakibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Mjukuu wa Rais Dkt. John Magufuli, baada ya shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Kimara, jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Mama mzazi wa marehemu na baadhi ya wanafamilia wafiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wakati aliposindikiza msiba wa mjukuu wa Mhe. Rais, marehemu Maryfaustna Mlyambina, leo Nov 13, 2015. 
  Picha na OMR

  0 0

  NaFrancis Dande

  WARATIBU wa Tamasha la Muziki wa injili kuombea Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, Kampuni ya Msama Promotions Ltd, wameeleza sababu za kuandaa tamasha jingine la kumshukuru Mungu kwa  kujalia  uchaguzi huo kufanyika kwa amani na utulivu.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama (pichani), mwenye uzoefu wa kuratibu matukio ya muziki wa injili tangu mwaka 2000, alisema shukrani kwa Mungu ni jambo muhimu.

  “Shukrani ni jambo muhimu sana iwe katika mambo ya kiroho hata yale ya kibinaadamu, hivyo kwa vile tulimuomba Mungu ajalie uchaguzi wetu ufanyike kwa amani na utulivu na ikawa hivyo, hatuna budi kuandaa tamasha jingine la kumshukuru,” alisema Msama.

  Msama alisema kama walivyofanya wakati wa kuombea amani na utulivu uchaguzi huo kwa kuwaleta pamoja waimbaji wa kitaifa na kimataifa, ndivyo watakavyofanya katika tamasha hilo la Novemba 25 litakaloanzia jijini Dar es Salaam kabla ya kuhamia mikoani.

  Alisema ingawa bado kamati yake inaendelea na mazungumzo na waimbaji mbalimbali, lakini kwa wale wa kimataifa ni kutoka Kenya, Afrika Kusini na DR Congo na wengineo mahiri ambao wataungana na wale wa hapa nyumbani.

  Miongoni mwa waimbaji wa kimataifa ambao walipamba tamasha la Oktoba 4 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ni Ephraem Sekereti (Zambia), Sipho Makhabane na Solly Mahlangu (Afrika Kusini), Sarah Kierie wa Kenya na mwingine kutoka Uingereza.

  Msama ametumia fursa hiyo kuwashukuru wote waliojitokeza katika katika tamasha la Oktoba 4, pia kushiriki uchaguzi mkuu akiamini kila mmoja alikuwa chachu ya amani ndio maana nchi imevuka salama katika tukio hilo zito ambalo kwa nchi nyingine limekuwa chanzo cha uhasama na mifarakano.

  “Kwa kutambua nafasi ya kila mmoja katika kudumisha amani na utulivu, ndio maana sisi Msama Promotions tumeandaa tamasha hili la kutoa shukrani kwa Mungu kutuvusha salama katika tukio
  zito la uchaguzi mkuu wa Oktoba 25,” alisema Msama.

  Alisema watalitumia tukio hilo pia kuzidi kumsihi Mungu aendelee kuijalia nchi amani na utulivu wakiamini huo ndio mtaji wa maendeleo mbalimbali kwani penye mifarakano ya kijamii, ni vigumu kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo na ikafanikiwa.

  0 0

  Wakazi wa jijini Dar es Salaam wakijipatia kitoweo na mafuta ya samaki mkubwa jamii ya nyangumi aliyeonekana Novemba 13 katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Coco Beach jijini Dar es Salaam. Wakazi hao waliofika katika eneo hilo huku wakiwa na vyombo vya kubebea mafuta ya samaki huyo. Mashuhuda hao walisema kuwa mafuta yake ni dawa ya watoto, hata hivyo wataalam wa afya hawakuweza kupatikana kuelezea usalama wa nyama ya samaki huo pamoja na mafuta yake.

  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay Zefrin Lubuva alizitaka mamlaka zinazohusika na afya kufika na kuthibitisha usalama wa kitoweo hicho kwa afya za wakazi hao.  (Picha na Francis Dande)

   Wakazi wa jijini Dar es Salaam wakijipatia kitoweo na mafuta ya Samaki mkubwa jamii ya Nyangumi aliyeonekana Novemba 13 katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Coco Beach jijini Dar es Salaam.
  Wakazi wa jijini Dar es Salaam wakijipatia kitoweo na mafuta ya Samaki mkubwa jamii ya Nyangumi aliyeonekana Novemba 13 katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Coco Beach jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mratibu na Msimamizi Mkuu wa Jumuiya Ya Mama na Baba Lishe Mkoa wa Dar es Salaam, Said Said (wa pili toka kulia), akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idata Maleleo kuelezea kuhusu Uzinduzi wa Ushirika wa Mama na Baba Lishe unaotarajia kufanyika Novemba 15, 2015 ukumbi wa SabaSaba jijini Dar es Salaam. 

  Lengo la jumuiya hiyo kuunganisha kwa pamoja wadau mbalimbali, kutoa fursa kulinda haki za ajira na kuzitafutia ufumbuzi na kuondoa tatizo la ajira kupitia tasnia hii ikiwa ni kumtambua mama na baba lishe kama sehemu ya maisha ya kila mmoja wetu, kwani kila mtanzania anaufahamu umuhimu wa mama na baba lishe na takwimu zinaonyesha asilimia 50% ya wanzania waishio mijini hupata huduma ya chakula. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mama na Baba Lishe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Mhonzu akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idata Maleleo kuelezea kuhusu Uzinduzi wa Ushirika wa Mama na Baba Lishe unaotarajia kufanyika Novemba 15, 2015 ukumbi wa SabaSaba jijini Dar es Salaam.
  Mama Lishe wakiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa idata Maleleo kuelezea kuhusu Uzinduzi wa Ushirika wa Mama na Baba Lishe unaotarajia kufanyika Novemba 15, 2015 ukumbi wa SabaSaba jijini Dar es Salaam.

  Waaandishi wa habari wakufuatia mkutano huo.

  0 0

  Maafisa wa Bunge wakipokea nyaraka toka kwa wabunge wateule katika zoezi lililoanza leo Mjini Dodoma.
  Wabunge wateule wakipiga picha kwa ajili ya vitambulisho vitakavyotumika kwa ajili ya matumizi ya Bunge Leo Mjini Dodoma
  Mbunge wa Jimbo la Mwanga Mkoani Kilimanjaro Mh. Jumanne Maghembe akikabidhi nyaraka zake wakati wa zoezi la usajili linaloendelea leo Mjini Dodoma.
  Mbunge wa Jimbo la Sengerema Willium Ngeleja akisajili kwa Afisa wa bunge
  Maafisa wa benki wakiwapa maelezo wabunge wakati wa zoezi la usajili linaloendelea Mjini Dodoma
  Maafisa wa Bunge wakimkabidhi nyaraka Moja ya Mbunge wakati wa Zoezi la Usajili leo Mjini Dodoma  0 0

   Afisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam General Insuarence Ndugu Manasseh Kawaloka  Akitoa Hotuba yake Kwenye halfa ya Kampuni ya NIKO Insuarence Limited Ilipobadili Jina na kuwa Sanlam General Insuarence.
  Kampuni ya Bima Niko limited Imebadili jina na kuwa Sanlam General Insuarence Limited.

  Mabadiliko hayo yanalenga Kupanua Wigo Na kuimarisha uwepo wake Nchini Tanzania na Afrika Mashariki  kwa Jumla.Sanlam General Insuarence Itaendelea Kutoa Huduma Mbalimbali za BimaKwa Wateja Binafsi na Mashirika Nchini Tanzania.Huduma za Sanlam General Insuarence  ni Pamoja na za Biashara na Binafsi kama vile Magari,Moto Na Nyinginezo.
     Sanlam General Insuarence  Yenye Makao Makuu yake Nchini Afrika KusiniInamiliki 46%ya Hisa za Niko.Kupitia Kampuni yake Tanzu ya Masoko yanayokua yaani Sanlam Emerging Markerts..
  Picha  ya Viongozo wa Kampuni ya Sanlan Pamoja na NIKO Insuarence wakiwa wameshikana mikono Mara baada ya Uzinduzi wa Sanlam General Insuarence.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam General Insuarence Ndugu Manasseh Kawaloka Alisema Kuwa Sanlam Group ni Kampuni yenye Heshima Kubwa,Hivyo Mabadiliko ya NIKO Insuarence Kuwa Sanlam General Insuarence  Utaleta Ufanisi wa Hali ya Juu Pamoja Utendaji wa Kibiashara Kwa Kampuni Hiyo.Akieleza zaidi alisema Watanzania  sasa watapata nafasi zaidi ya Kupata Aina mbalimbali za Bidhaa za Bima Zenye ubunifu kufidia Majanga Binafsinna ya Kibiashara .
  Kampuni ya Iliyobadili Jina Sanlam General Insuarence  Inatoa Huduma Mbalimbali za Bima Katika Wigo Mpana Kwa Wateja  Binafsi Pamoja na Mashirika  Nchini Tanzania .Huduma Zitolewazo na Kampuni ya Bima ya Sanlam General Insuarence  Zinalenga Biashara na Watu Binafsi Kama Magari ,Moto ,Uhandisi pamoja na Bima Maalum.Kabla ya Kubadili Jina Kampuni ya NIKO Insuarence Imekuwa Ikitoa Huduma Nchini Tangu Mwaka 2005.
  Ndugu Josep Mungai Mkurugenzi Mtendaji wa Sanlam General Insuarence Akitoa Hotuba yake wakati wa Uzinduzi huo.
  Mabadiliko ya NIKO Insuarence Limited kuwa Sanlam General Insuarence  Yanafuatia Mabadiliko ya Kampuni ya African Life Assuarence ya Tanzania na Kuwa Sanlam Life Insuarence.Sanlam General Insuarence  Inatoa utaalamu na Uzoefu wa Hali ya Juu kwa Wateja wake Pamoja na Wadua wengine wanaofanya kazi na Kampuni hiyo.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akisalimiana na wananchi alipofanya ziara katika hosptali teule ya Machame na kuzungumza na wafanyakazi.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
  HALMASHAURI ya wilaya ya Hai,mkoani Kilimanjaro, imewasimamisha kazi watumishi wake wanne kwa tuhuma za kughushi hati za mishahara na kughushi nyaraka zilizofanikisha kuchukua jumla ya kiasi cha sh Mil 73.4 zikiwemo fedha za malipo ya muda wa kazi wa ziada kwa madaktari na wauguzi wa Hospitali teule ya Machame.

  Tuhuma hizo pia zina mtaja Mweka hazina wa Hosptali hiyo anayedaiwa kushirikiana na watumishi wa halmashauri hiyo kufanya ubadhirifu wa fedha na kwamba tayari Uongozi wa hosptali hiyo iliyo chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Kaskazini ,umekwisha  mfukuza kazi.

  Watumishi wawili kati ya wanne wamesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbili tofauti,moja ni kughushi hati za mishahara,vitambulisho na sahihi za watumishi  waliostaafu  na wengine kuacha kazi na kuchukua mikopo wa Mil 35 katika benki ya CRDB kwa majina ya watumishi walioacha kazi.
  Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akizungumza na wafanyakazi wa Hosptali teule ya Machame (hawapo pichani) .
  Baadhi ya iongozi wa Hosptali hiyo na viongozi wa serikali wa wilaya ya Hai.
  Wafanyakazi wa Hosptali teule ya Machame .
  Mkurugenzi wa Hosptali hiyo,Dkt Saitore Laizer akizungumza katika kikao hicho.
  Baadhi ya madktari wa hosptali teule ya Machame.
  Baadhi ya watumishi wa Hosptali hiyo.
  Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi katika hosptali ya Machame ,Dkt Fredrick Muro akizungumza katika kikao hicho.
  Baadhi ya wafanyakazi.
  Mkuu wa wilaya akiondoka katika hosptali hyo mara baada ya kumalizika kwa kikao na watumishi .


  0 0

  Meza Kuu , Kutoka Kushoto ni Ndugu Maumba Mgaya, Mwenyekiti wa Jumuiya, Bi Magreth Mjindo na Ndugu Andrew Katibu

  Meza Kuu , Kutoka Kushoto ni Ndugu Maumba Mgaya, Mwenyekiti wa Jumuiya, Bi Magreth Mjindo na Ndugu Andrew Katibu.

  Mnano tarehe 7/11/2015, Jumuiya ya watanzania waishio nchini Thailand ilikutana na kujadiliana mambo mbalimbali ya jinsi gani wanaweza kusaidiana katika mambo mbalimbali, TIT ilianzishwa mnano mwezi wa nne mwaka, 2015 na inahusisha watanzania mbalimbali, wanafunzi,wafanyabishara na wafanyakazi waishio na kufanya nchini Thailand. Mkutano mkuu wa Jumuiya ulifanyika katika Hoteli ya Amari Boulevard Mjini Bangkok na kuhudhuriwa na wanajumiya mbalimbali.

  Pamoja na kujadiliana mambo mbalimbali kulifanyika uchaguzi wa viongozi ambapo wafuatao walichaguliwa kuwa viongozi wa jumuiya kwa kipindi cha 
  mwaka mmoja:
  Mwenyekiti: Bwana Maumba Mgaya
  M/Kiti: Bw. Alois Ngonyani
  Katibu: Bw.Andrew Wajama
  Katibu Msaidizi: Bw. Emmanuel Mushi
  Mhazini: Bw. Adolf Kigombola
  Mhazini Msaidizi: Bi.Tumaini Kalindile
  Afisa Mawasiliano: Bw. Emmanuel Nyamageni
  Afisa Mawasiliano Msaidizi: Bw. Jordan Hossea.

  Pamoja na uchaguzi kulifanyika sherehe fupi ya kumpongeza Bi Magreth Dionis Mjindo ambaye amemaliza Shahada ya uzamili ya maendeleo ya jamii na anarejea nyumbani kulitumikia Taifa.

  Jumuiya inapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wadhamini wao Ndugu Florean Rwehumbiza, Dada Lucy Kileo pamoja na Ndugu Kivea Mbwana (Homeboy) kwa kusimamia uchaguzi na kufanikisha kufanyika kwa mkutano huu muhimu. Shukrani za pekee ziende kwa Kampuni ya Broadhurst Pacific, kwa kusimamia, kudhamini na kufanikisha tukio hili muhimu.
  Mhazini wa Jumuiya Ndugu Adolph Kigombola akisoma taarifa ya fedha
  Mhazini wa Jumuiya Ndugu Adolph Kigombola akisoma taarifa ya fedha.
  Tunapenda kuwapongeza na kuwashukuru viongozi waasisi wa jumuiya waliomaliza muda wao ambao ni ndugu Saidi Husein Kitenge Mwenyekiti wa kwanza wa jumuiya na makamu wake Ndugu Masui Vicent Munda na ndugu Antidius Muchunguzi bila kuwasahau maafisa mawasiliano wetu akiwemo ndugu Felix Mwema na Bi Diana Richard.Mungu awabariki kwa kuitumikia vema TIT.

  Aidha Jumuiya inawakaribisha watanzania mbalimbali walioko nchini Thailand au wanaotarajia kuja nchini Thailand kushirikiana na jumuiya yetu.

  Umoja ni nguvu
  Imetolewa na Jumuiya ya Watanzania waishio nchini Thailand (TIT)
  +66947230002/+66972494819
  Mkutano Mkuu Ukiendelea
  Mkutano Mkuu ukiendelea.

  Baadhi ya Watanzania Waishio nchini Thailand
  Baadhi ya Watanzania Waishio nchini Thailand.
  Mkutanoni
  Mkutanoni.
  Timu ya Wadhamini wakisimamia Uchaguzi
  Timu ya Wadhamini wakisimamia Uchaguzi.
  Bw. Florean Akikabidhiwa keki ya kuzaliwa na Bi Lucy
  Bw. Florean Akikabidhiwa keki ya kuzaliwa na Bi Lucy.
  Ndugu Florean akimkabidhi Bi Magreth Zawadi kwa niaba ya Jumuiya
  Ndugu Florean akimkabidhi Bi Magreth Zawadi kwa niaba ya Jumuiya.
  Wanajumuiya Wakipata Chakula cha Pamoja
  Wanajumuiya Wakipata Chakula cha Pamoja.
  Watanzania Waishio Thailand wakipata chakula cha pamoja
  Watanzania Waishio Thailand wakipata chakula cha pamoja.
  Watanzania Waishio Thailand Wakiwa Katika Picha ya Pamoja
  Watanzania Waishio Thailand Wakiwa Katika Picha ya Pamoja.
  EPVI3455

  0 0


  0 0


  Dr Alok Ranjan, mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa fahamu na uti wa mgongo kutoka hospitali ya Apollo akitoa huduma kwa mtoto Zulea akiwa na mama yake Shamila Idd katika kliniki iliyofanyika siku tatu.’
  Dr Alok Ranjan, mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa fahamu na uti wa mgongo kutoka hospitali ya Apollo akiongea na waandish wa habari katika cliniki iliyoanza tarehe 11 na kuendelea mpaka tarehe 13 katika hospitali ya hindumandal.

  Bwana Hafidhi Rashid Waziri, mmoja wa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo na Dr Alok Ranjan katika hospitali ya Apollo Hyderebad akiongea na waandishi wa habari katika Klinik hiyo.
  Shamila Idd mama wa mtoto Zulea mwenye tatizo la uti wa mgongo akiongea na waandishi wa habari katika kliniki iliyoandaliwa na Dr Alok Ranjan, mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa fahamu na uti wa mgongo kutoka hospitali ya Apollo.

  Na Mwandishi Wetu,

  Tanzania ni moja ya nchi ambazo ina uhaba mkubwa wa madaktari bingwa wa mfumo wa fahamu kitendo kinachopelekea nchi kupoteza fedha nyingi kwa kuwapeleka wagonjwa wa matatizo ya aina hiyo nje ya nchi kupata matibabu na ushauri.
  Inakadiriwa kuwa watoto wachanga 1000 kati 4000 wanaozaliwa na tatizo la mfumo wa fahamu hupatiwa matibabu huku wengine 3000 wakishindwa kupatiwa matibabu.Kutokana na hali hiyo, Hospitali ya Apollo ya nchini India imemleta nchini daktari bingwa wa upasuaji wa uti wa mgongo na mfumo wa fahamu ambaye pia ni Mkuu wa idara ya upasuaji wa magonjwa ya fahamu katika hospitali hiyo DKT ALOK RANJAN ambaye atakuwa akitoa huduma na kuwaona wagonjwa wake aliowafanyia upasuaji siku za nyuma.
  Nao baadhi ya wagonjwa waliofika katika kliniki hiyo inayofanyikia katika hospitali ya hindu mandal jijini Dar es Salaam wameiomba serikali kuhakikisha kwamba inasaidia katika gharama za matibabu ya watu wanaosafiri nje ya nchi kufuata matibabu ya magonjwa mbali mbali.Wamezitaka pia kampuni za bima ya afya kuhudumia wateja wake katika hospitali za kimataifa badala ya kujikita katika hospitali za hapa nchini pekee.
  Katika mkutano huo na waandishi wa habari ulofanyika tarehe 12 katika hospitali ya hindumandali Dk.Alok Ranjan kutoka Hospitali za Apollo amewashauri watanzania kubadilisha mtindo wa maisha ili kuepukana na magonjwa ya mfumo wa fahamu na uti wa mgongo. anasema kuwa kwa watu wazima ugonjwa huu mara nying husababishwa na namna mbovu ya ukaaji ambao hudhuru uti wa mgongo, trauma, shinikizo la damu, ajali, kisukari, uzito wa kupitiliza na sababu nyinginezo.
  Tanzania kwa sasa inakadiriwa kuwa na madaktari wa mfumo wa fahamu 7 ambao wote kwa sasa ni watendaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.

  0 0

  picha ya makamu wa rais  Samia Suluhu(picha na maktaba)

  Na Woinde Shizza,Arusha

  Michuano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA), yanatarajia kuanza kutimua vumbi wiki ijayo jijini Arusha kwa kushirikisha Mikoa Yote Tanzania.


  Katibu mkuu wa SHIMMUTA Award Safari alisema kuwa hadi sasa tayari mikoa kadhaa imethibitisha ushiriki wao ikiwemo wenyeji wa mashindano hayo Mkoa wa Arusha na Mikoa mingine ni Dar es salaam, Dodoma, Morogoro, Mbeya na Tanga


  Tukiwa kama kamati tendaji ya SHIMMUTA tulifanya kikao tarehe saba mwezi huu pamoja na wajumbe wa timu shiriki ili kupeana miongozo na taratibu za michezo hasa tukiwa tunaboresha mapungufu yaliyojitokeza mwaka jana mkoani Tanga” alisema Safari.


  Takribani michezo 12 yatafanyika ikiwa pamoja na Mpira wa Miguu, Riadha, kuvuta Kamba, Mpira wa Pete, Vishale, karata, na drafti na karata.


  “Kwa mujibu wa katiba, SHIMMUTA  ipo chini ya makamu wa Raisi, hivyo mashindano ya mwaka huu tunatarajia Makamu wa Raisi Samia Suluhu atakuja kufungua mashindano hayo akiwa anachukua nafasi ya Mlezi aliyepita makamu wa Raisi Mstaafu Mohamed Ghalib Bilal” Alisema Safari.


  Mashindano ya SHIMMUTA yanatarajia kuanza Novemba 19 hadi Novemba 30 mwaka huu, hivyo timu shiriki zitaanza kuwasili kuanzia tarehe 17 wakati siku inayofuata SHIMMUTA itafanya mkutano na viongozi wa timu zote zitakazofika.


  SHIMMUTA ni moja ya mashirika manne yalioundwa na serikali kwa ajili ya kusimamia michezo makazini ikiwemo SHIMIWI ikiwa chini ya wizara ya kazi, SEMISEMISTA serikali za mitaa na MAJESHI ambalo linasimamiwa na Baraza la michezo la Majeshi.


older | 1 | .... | 685 | 686 | (Page 687) | 688 | 689 | .... | 1897 | newer