Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 684 | 685 | (Page 686) | 687 | 688 | .... | 1897 | newer

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
   WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
  JESHI LA POLISI TANZANIA.

         TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
     “PRESS RELEASE” TAREHE 12.11.2015.

  MWANAMKE MMOJA MKAZI WA HORONGO MBEYA VIJIJINI AMEKUTWA AMEUAWA NA WATU WASIOFAHAMIKA.

  MTU MMOJA AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI JIJINI MBEYA.

  MTOTO WA MWAKA MMOJA NA MIEZI SABA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA CHA MAJI.

  KATIKA TUKIO LA KWANZA:
  MWANAMKE MMOJA MKAZI WA HORONGO WILAYA YA MBEYA VIJIJINI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LUCY YESAYA [22] ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUPIGWA KITU KIZITO KICHWANI NA USONI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.

  MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA MNAMO TAREHE 11.11.2015 MAJIRA YA SAA 06:30 ASUBUHI HUKO KIJIJI CHA IZUMBWE SOKONI, KATA YA SONGWE, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.  

  CHANZO CHA KIFO CHAKE NI BAADA YA KUPIGWA KITU KIZITO SEHEMU ZA KICHWANI NA USONI. KIINI CHA TUKIO HILO BADO KINACHUNGUZWA. UPELELEZI UNAENDELEA.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.

  KATIKA TUKIO LA PILI:
  MPANDA BAISKELI MMOJA AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA LAKE, JINSI YA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA 25 – 28 ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.838 AAC AINA YA TOYOTA HIACE ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE DEO MBILINYI.

  TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 11.11.2015 MAJIRA YA SAA 16:40 JIONI HUKO ENEO LA UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO HILO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

  KATIKA TUKIO LA TATU:
  MTOTO MWENYE UMRI WA MWAKA MMOJA NA MIEZI SABA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA PROMIS DANK MKAZI WA BWAWANI WILAYA YA CHUNYA ALIFARIKI DUNIA NJIANI AKIWA ANAPELEKWA HOSPITALI BAADA YA KUTUMBUKIA KISIMANI.

  TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 11.11.2015 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO KITONGOJI CHA RAILWAY, MTAA NA KATA YA BWAWANI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.

  INADAIWA KUWA, MTOTO HUYO BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA HICHO AMBACHO KILIKUWA WAZI, ALIOKOLEWA AKIWA HAI LAKINI ALIFARIKI DUNIA AKIWA NJIANI KUELEKEA HOSPITALI TEULE YA MWAMBANI KWA MATIBABU.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI HASA KWA KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA KWA WATOTO WADOGO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.

   AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUFUNIKA VISIMA VILIVYOWAZI, KUFUKIA MASHIMO YENYE MAJI KWANI NI HATARI KWA WATOTO WADOGO HASA KATIKA MSIMU HUU WA MVUA ZA VULI.
  Imesainiwa na:
  [AHMED Z. MSANGI – SACP]
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

  0 0

  TIKETI za mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia chini Urusi mwaka 2018 kati ya Tanzania dhidi ya Algeria ziataanza kuuzwa kesho Ijumaa katika vituo 10 viliyopo jijini Dar es salaam.
  Magari maalumu yenye stika yataanza kuuza tiketi hizo za mchezo kesho saa 2 kamili asubuhi mpaka saa 12 jioni, ambapo tiketi zinauzwa kwa shilingi elfu tano (5,000) kwa viti vya rangi ya bluu na kijani na rangi ya machungwa, na elfu kumi (10,000) kwa viti vya VIP B & C.
  Vituo vitakavyotumika kuuza tiketi hizo ni ofisi za TFF – Karume, Buguruni – Oilcom, Mbagala – Darlive, Mnazi Mmoja, Luther House – Posta, Big Bone – Msimbazi, Ubungo – Oilcom, Makumbusho – Stand ya Daladala, Uwanja wa Uhuru.
  TFF inawaomba wadau, washabiki na watanzania kujitokeza kwa wingi kununua tiketi za mchezo huo katika magari maalumu yatakayokuwepo kwenye vituo vilivyotajwa, ili kuondokana na tatizo la kuuziwa tiketi zisizokuwa halali.
  Wakati huo huo Ubalozi wa Algeria nchini Tanzania, umewataka waandishi wa habari wanaotrajia kwenda kuripoti mchezo wa marudiano jijini Algiers siku ya jumanne, kuwasilisha maelezo ya chombo wanachofanyia kazi pamoja na vifaa watakavyovitumia kwenye mchezo huo (camera, vinasa sauti) kuwasilisha maelezo hayo leo Alhamsi kabla ya saa 9 mchana katika ofisi za Ubalozi huo kwa ajili ya kupatiwa Accreditation za kufanyia kazi.
  Matokeo ya mchezo wa jana  Azam Sports Federtaion Cup (ASFC), ni Mshikamano 0 - 1 Cosmopolitan

  0 0
 • 11/12/15--03:39: BEI YA MADAFU LEO

 • 0 0

   Baadhi ya Wagonja walifikishwa Hospitali hapo kwa ajili ya kupatiwa matibabu  baada ya kupata maradhi ya matumbo ya kuharisha (kipindupindu).
   Mwandishi wa Habari Rahma Suleiman akichukua maelezo kwa Mgonjwa aliyefika katika kituo hicho mara baada ya kupata hujambo.
   Naibu Waziri wa Afya  Mahmoudu Thabiti Kombo akionyesha ramani ya maeneo yanayoathiriwa zaidi na ugonjwa wa maradhi ya matumbo.
  Naibu Waziri wa  Afya  Mahmoudu Thabiti  Kombo akipata maelezo kwa Dkt. Dhamana  Fadhili Ramadhan  wakati alipotembelea wagonjwa wa maradhi ya kuharisha (kipindupindu) katika kituo cha Afya kiliopo Sheha ya Karakana. 

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Golden Fleet LTD na Golden Coach LTD Bw. Mohamed Raza Dewji (kulia) akimkabidhi Afisa Uuguzi wa Idara ya Uuguzi na Ubora wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi. Mariana Makanda msaada wa vitanda thelasini na magodoro thelasini, katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja wa hospitali hiyo Bw. Aminiel Eligaesha.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Golden Fleet LTD na Golden Coach LTD Bw. Mohamed Raza Dewji (kulia) akieleza kwa waandishi wa habari jinsi alivyoguswa na tatizo la wagonjwa kulala chini mara baada ya Rais John Magufuli alipotembea hospitali hiyo.
   Daktari akimpatia huduma mgonjwa kwa kutumia mashine ya MRI ambayo ilikuwa mbovu kwa muda mrefu ila imetengamaa mara baada ya Rais John Magufuli kufanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuagiza matengenezo ya haraka yafanyike. 
   Madaktari wakifuatilia kwa makini jinsi mashine ya MRI inavyofanyakazi mapema hii leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
  Picha zote na Eliphace Marwa - MAELEZO.

  0 0

  Katika kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri, Klabu ya Simba ilianzisha Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi wa Septemba 2015.

  Mshindi wa mwezi wa Oktoba, 2015 ni Mohamed Hussen Tshabalala ambapo alipigiwa kura nyingi na mashabiki na wapenzi wa Simba na soka la Tanzania kwa ujumla kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya Simba News.
  Akizungumza leo jijini Dar es salaam Rais wa Simba Evans Aveva alisema “Uongozi, wanachama na wapenzi wa Simba wanathamini mno mchango wa wachezaji katika kuifanya timu yetu ifanye vizuri, hivyo tumeona ni jambo la busara kuwa klabu ya kwanza Nchini Tanzania kuwa na tunzo za mchezaji wake bora.

   Tunaamini kuwa Tunzo ya Mchezaji bora wa mwezi wa Simba itaongeza ari na kujituma kwa wachezaji wetu. Sisi tukiwa kama viongozi ni kazi yetu ya msingi kuhakikisha kuwa wachezaji wetu hasa wale wanaojituma zaidi wanatambuliwa na kuenziwa’’.


  Akizungumza jinsi tunzo ya mchezaji bora itakavyoendeshwa, Mkurugenzi Mkuu wa EAG Group ambao ni washauri na watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba, Imani Kajula alisema “Wanachama na wapenzi wa Simba na wapenda michezo ndio watakao kuwa wanachagua mchezaji bora wa mwezi kwa kutuma jina la mchezaji wanayempendekeza kwenda kwenye namba 15460, Ni wale tu ambao wamejiunga na Simba News kupitia mtandao wa Voda na Tigo wataweza kupiga kura kuchagua mchezaji bora wa mwezi wa Simba’’

  Simba News ni huduma iliyoanzishwa na Simba ili kuwapa wapenzi wa Simba habari mbalimbali za Simba popote pale walipo ikiwemo matokeo, majina ya wachezaji wanaocheza mechi, usajili na habari nyingine za klabu ya Simba. 

  Kujiunga na Simba News tuma neno Simba kwenda namba 15460 ni maalum kwa Tigo na Vodacom.

  0 0

   Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa benki ya Exim Tanzania  Bw. Frederick Kanga (katikati) akimfanyia usahili mmoja wa watanzania anayeishi nchini Marekani Bw. Paul Rupiamara baada ya Mkutano wa Uajiri barani  Afrika (Career Africa Recruitment Summit 2015) uliofanyika mjini New York, Marekani hivi karibuni. Anayeshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw Dinesh Arora. Benki hiyo imeahidi kutoa fursa sawa za ajira kwa Watanzania wote wakiwemo wale wanaoishi nje ya nchi ili kuendana na  sera yake ya ajira inayoangalia zaidi uwezo wa kiutendaji.
  Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa benki ya Exim Tanzania  Bw. Frederick Kanga (katikati) akimfanyia usahili mmoja wa watanzania anayeishi nchini Marekani Bi. Pamela Mgema  mara baada ya Mkutano wa Uajiri barani  Afrika (Career Africa Recruitment Summit 2015) uliofanyika mjini New York, Marekani hivi karibuni. Anayeshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw Dinesh Arora. Benki hiyo imeahidi kutoa fursa sawa za ajira kwa Watanzania wote wakiwemo wale wanaoishi nje ya nchi ili kuendana na  sera yake ya ajira inayoangalia zaidi uwezo wa kiutendaji.

  0 0

  DSC_1572

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Yamungu Kayandabila akizungumza na wadau wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia katika mkutano maalum wa siku ya Sayansi Duniani. Kushoto kwake ni Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO- Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam Novemba 10. 2015. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
  DSC_1570
  Afisa Utawala na Fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha ambaye alimwakilisha Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa UNESCO- Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akisoma ujumbe maalum wa siku ya Sayansi Duniani wakati wa mkutano huo wa wadau wa Sayansi.
  DSC_1565
  Profesa John Kondoro Mkuu wa Chuo cha Teknolojia cha jijini Dar es Salaam – (DIT) akitoa mada katika mkutano huo wa wadau wa Sayansi wakati wa maadhimisho ya siku ya Sayansi.
  DSC_1557
  Afisa kutoka UNESCO NAT.COM, Bw. Joel Samuel akitoa mada katika mkutano huo wa wadau siku ya Sayansi Duniani.
  DSC_1580
  Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye, akifafanua jambo wakati wa mjadala huo juu ya maendeleo ya Sayansi na Teknolojia nchini katika mkutano uliowakutanisha wadau wa Sayansi katika maadhimisho ya Siku ya Sayansi Duniani.
  DSC_1584
  Wadau wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa siku ya Sayansi Duniani.  Na Andrew Chale, Modewjiblog
  [DAR ES SALAAM-TANZANIA] Tanzania kupitia wadau wa Sayansi nchini imedhamilia kupiga hatua zaidi katika kufikia malengo ya Agenda 2030 kwa kuchangamkia fursa za maendeleo katika Sayansi.

  Hayo yameelezwa jijini hapa wakati wa wadau wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, walipokutana katika majadala wa Siku ya Sayansi Duniani kwa ajili ya Amani na Maendeleo (World Science Day for Peace and Development).Akisoma neno, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Yamungu Kayandabila amelipongeza Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), katika kukuza Sayansi nchini.

  Dkt. Yamungu ameelezea kuwa, nchi yoyote ile ilikuendelea, inategemea Sayansi hivyo kwa Tanzania ni wakati wa kuchangamkia fursa ili kufikia malengo na Agenda 2030.“Tanzania tuna fursa nyingi na za kutosha. Tuna Nyuklia na hii ni uchumi tosha tutakapofanyia kazi kwa malengo tutafika mbali kwani inahitaji Sayansi ya kina.Navipongeza vyuo mbalimbali vilivyopo nchini ikiwemo DIT, Nelson Mandela cha Arusha, Chuo cha Sayansi Mbeya na vingine vingi” ameeleza Dk. Yamungu.

  Aidha, Dkt. Yamungu ametaka Sayansi kuendana na suala la ulinzi wa chakula na miundombinu mingine ikiwemo suala la maji huku akihimiza wanafunzi kuyapenda na kuyasoma masomo ya Sayansi na suala la umuhimu wa Sayansi na namna inavyoweza kuathiri maisha ya watu kila siku.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia Prof. Evelyn Mbede amepongeza wadau wa Sayansi na Teknolojia kwa kujimuika katika maadhimisho ya siku hiyo ya Sayansi Duniani ambapo ameelezea kuwa Wizara yake milango ipo wazi kwa wadau wote katika kuhakikisha wanapiga hatua katika kukuza na kuendeleza Sayansi hapa nchini.
  Kwa upande wake, Afisa Utawala na Fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha ambaye alimwakilisha Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO- Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues alipongeza juhudi za Serikali ya Tanzania katika kutilia mkazo suala la Sayansi na Teknolojia na kufanya suala hilo kuwa mtambuka kwa maendeleo ya vizazi vya sasa na baadae.
  Akisoma ujumbe maalum kutoka UNESCO, Bw. Bokosha alieleza kuwa kupitia Sayansi na Teknolojia na ubunifu, maendeleo ya Taifa endelevu, uimarishaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa maandalizi kwa ajili ya kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi na madhara yake hivyo Sayansi inahitajika kwa kiwango kikubwa juu ya hilo.
  Aidha, ameeleza kuwa, UNESCO imekuwa mstari wa mbele katika kuanzishwa kwa moduli za elimu ya Mazingira katika shule za Sekondari.

  Akinukuu ujumbe maalum kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi Irina Bokova katika ujumbe alieleza:
  “Hii ni siku ya Sayansi Duniani kwa amani na Maendeleo na imekuja miezi miwili baada ya makubaliano ya Agenda 2030 ya maendeleo endelevu.
  Hivyo Serikali zote zitambue nguvu ya Sayansi ya kutoa majibu muhimu kwa usimamizi mzuri wa maji kwa ajili ya hifadhi na matumizi endelevu ya bahari, ulinzi wa mazingira na viumbe hai, ilikukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na majanga na kuendeleza uvumbuzi na kuondokana na umasikini na kupunguza tofauti” alieleza katika nukuu hiyo.

  0 0
  0 0


  Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao Kikao Cha Kamati Kuu na Cha Halmashauri Kuu jijini Dar es salaam ambacho kimehudhuriwa kwa mara ya kwanza na Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli.PICHA NA ISSA MICHUZI WA IKULU.


  0 0

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.


  Na EmanuelMadafa,Mbeya

  Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi saba  Promis Dank mkazi wa bwawani wilaya ya chunya alifariki dunia njiani akiwa anapelekwa hospitali baada ya kutumbukia kisimani.Tukio hilo limetokea Novemba  112  majira ya saa 12 asubuhi huko kitongoji cha railway,  kata ya bwawani, wilaya ya chunya, mkoa wa mbeya. 

  Inadaiwa kuwa, mtoto huyo baada ya kutumbukia kwenye kisima hicho ambacho kilikuwa wazi, aliokolewa akiwa hai lakini alifariki dunia akiwa njiani kuelekea hospitali teule ya mwambani kwa matibabu.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya  Ahmed z. Msangi ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwa makini hasa kwa kuweka uangalizi wa kutosha kwa watoto wadogo ili kuepuka madhara yanayoweza kuepukika. 

  Aidha anatoa wito kwa jamii kufunika visima vilivyowazi, kufukia mashimo yenye maji kwani ni hatari kwa watoto wadogo hasa katika msimu huu wa mvua za vuli.

  Wakati huo 
  (JAMIIMOJABLOG MBEYA )

  0 0

   
  MAKABIDHIANO YA TAARIFA RASMI IKULU.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, leo katika Ikulu ya Dar es Salaam  amepokea taarifa rasmi ya makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

  Makabidhiano hayo yamefanyika leo mchana  na kushuhudiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue  na Maafisa wa  Ofisi Binafsi ya Rais.

  Utaratibu wa kukabidhiana Ofisi katika Ofisi Kuu hapa nchini ni jambo la kawaida na hivyo imebidi  makabidhiano hayo  kati ya Rais anayeondoka na anaye ingia madarakani kufanyika.

  Umeanza vizuri, baki na msimamo huo huo utasaidia sana wananchi” .  Mhe. Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne amemueleza Mhe. Rais Magufuli wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano.

  Mhe. Rais Mstaafu amekabidhi taarifa rasmi yenye kurasa 53, ambayo kwa ujumla inaelezea kazi zilizokwisha kufanyika, ambazo zinasubiri kukamilika na zile ambazo zinasubiri maamuzi ya utekelezaji. Mengine ni  hali halisi ya nchi katika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

  Mhe. Rais Dkt. Magufuli amemshukuru Rais Mstaafu  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  kwa muongozo wake siku zote .“Nikushukuru kwa kuiacha nchi salama na itaendelea kuwa salama, nikushukuru kwa muongozo wako, na  taarifa yamuelekeo na ninaahidi kuwa Hapa ni Kazi Tu”. 

   Mhe. Raisamesema na kumueleza Rais Mstaafu kuwa ametengeneza mazingira mazuri ambayo nchi nyingi zimeshindwa kufanya na hivyo basi kuahidi kuendelea kuchota hekima na busara kwa Marais wote wastaafu wakiwemo Mhe. Benjamin William Mkapa wa Awamu ya Tatu na Mzee Ally Hassan Mwinyi wa Awamu ya pili.

  Wakati huo huo Mhe. Rais Magufuli ameendelea kupokea salamu za pongezi kutoka Kwa  Msimamizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bibi Helen Clark.

  “Chini ya uongozi wako, tunatarajia kuzidi kuimarisha ushirikiano baina yetu, demokrasia, kushughulikia masuala ya umaskini na ajira kwa vijana , kukuza uchumi,  na kulinda na kuhifadhi mazingira, masuala ambayo Tanzania na UNDP tumekuwatukishirikianakuyaendelezanakuyatimiza” amesema Bi Clark.

  Salamu zingine ni kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Uswiss, Mhe. Simonetta Sommaruga, Rais wa Jamhuri ya Italia Mhe. Sergio Mattarella, Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Joachim Gauck na pia kutoka kwa Rais wa Finland Mhe. Sauli Niinisto.

  Pongezi zingine zimetoka kwa Rais wa Jamhuri ya Urusi, Mhe. Vladimir Putin, Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Salva Kiir Mayardit, Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Park Geun-hye na kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. XI Jinping.

  Salamu  pia zimemfikia Mhe. Rais Dkt. Magufuli kutoka kwa Rais wa  Taifa la Eritrea Mhe. Isaias Afwerki na kutoka kwa Rais wa Ufaransa Mhe. Francois Hollande.Katika ujumbe wao, viongozi hao mbali na kumpongeza Mhe. Rais Dkt.  Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  wamesisitiza kuendeleza na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi zao.

  Pia wameipongeza Tanzania kwa kudumisha demokrasia imara na Watanzania kwa ujumla kwa kuimarisha amani na utulivu wakati wa Uchaguzi Mkuu.

  Imetolewa na:
  Premi Kibanga,
  Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi.
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.

  12 Novemba, 2015
   


  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(wa kwanza kushoto) akiangalia mitambo ya kurushia matangazo ya Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) wakati alipofanya ziara ya kikazi katika minara ya shirika hilo leo hii  Kisarawe.Profesa Elisante amefanya ziara katika Taasisi tatu zilizo chini ya Wizara hiyo ambazo ni Baraza la Sanaa Tanzabia (BASATA),Tanzania Standard Newspapers(TSN) na Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) lengo likiwa ni kufahamiana na wafanyakazi,kuwahimiza kufanya kazi kwa bidii na kujua changamoto zinazowakabili ikiwa ni kutimiza kauli mbiu ya HAPA KAZI TU ya awamu ya Tano.Anaefuatia ni mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bw.Clement Mshana.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akiangalia tofauti ya santuri ya  zamani na flashi ya kisasa  zinavyozidiana ukubwa kwa umbo alipotembelea maktaba mojawapo katika ofisi za shirika la utangazaji Tanzania (TBC) alipofanya ziara kuongea na menejimenti ya shirika ilo leo jijini Dar es Salaam.Santuri zilitumika kipinda shirika hilo likiitwa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD).
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (waliosimama watatu kulia) akiwa katika mojawapo ya studio za kurushia matangazo ya shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wwakati alipotembelea shirika ilo leo kuongea na menejimenti yake pamoja na kuona utendaji wake.

   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (aliyekaa mwenye miwani) akipata maelekezo jinsi gazeti linavyotengenezwa kutoka kwa mtumishi wa Standard News Papers(TSN) leo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kikazi na kuangalia utendaji wa kazi.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(wa pili kulia) akiangalia moja ya kazi za vijana wanojifunza kutengeneza batiki na kuweka chapa alipotembelea ofisi za Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA) leo hii jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi akifafanua jambo wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Uhusiano wa EU, Eric Beaume. (Picha na Francis Dande)
   Balozi wa Jumuiya ya  Ulaya (EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi (kulia) akibadilishana hati na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Jumuiya ya  Ulaya (EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi (kulia) akisaini hati na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000. 

   Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla hiyo.
  Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez akizungumza katika hafla ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000.
   Na Mwandishi Wetu

  JUMUIYA ya Ulaya (EU)imetiliana saini na Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo nchini yanayofanya kazi kama shirika moja (One UN), ruzuku Euro 200,000 sawa na sh. Milioni 478.

  Utilianaji saini huo ulifanywa na Mratibu wa Mashirika ya UN nchini , Alvaro Rodriguez na Balozi wa EU, Filiberto Sebregondi.
  Sebregondi alisema Tanzania imefanikiwa kutengeneza mfano wa namna bora Mashirika ya UN yanavyoweza kufanyakazi kama taasisi moja katika kuboresha maisha ya watu.

  Naye Rodriguez, alisema fedha hizo zimelenga kusaidia miradi ya pamoja ya EU NA UN ya mawasiliano, uragibishi, uimarishaji wa ufuatiliaji na uwazi.
  Rodriguez, alisema msaada huo ni muhimu katika ufanisi wa maendeleo kwa Tanzania wakati nchi inajipanga kutekeleza malengo ya endelevu SDGs.

  “Nchi ina Rais mpya na inahitaji kuwa ya kipato cha kati sisi UN na washirika wetu ni vyema tukaunga jitihada hizi ili kusiwepo na mtanzania atakayeachwa nyuma katika mchakato wa maendeleo,” alisema.

  0 0  Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM iliyofanyika leo tarehe 12 Novemba, 2015 chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete imemteua Ndugu Deogratius Ngalawa kuwa mgombea wake wa Ubunge katika Jimbo la Ludewa mkoani Njombe.

  Ndugu Ngalawa ameteuliwa kugombea nafasi hiyo ya Ubunge baada ya kushinda kura za maoni zilizofanyika Novemba 10, 2015.

  0 0

   Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais leo Novemba 12, 2015
    Rais Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono kwa furaha na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais
    Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Obeni Sefue alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais
     Rais Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza  Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
    Rais Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza  Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakati akiongea kabla ya kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais  Ikulu jijini Dar es salaam 
   Rais Dkt John Pombe Magufuli akipokea kwa furaha hati ya makabadhiano ya Ofisi kutoka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2015

  Rais Dkt John Pombe Magufuli akipokea kwa furaha hati ya makabadhiano ya Ofisi kutoka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2015
   Rais Dkt John Pombe Magufuli akiiangalia kwa furaha hati ya makabadhiano ya Ofisi aliyoipokea kutoka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2015
   Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Makiamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Kiongozi  baada ya hafla ya makabidhiano rasmi ya Ofisi  Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi leo Novemba 12, 2015
  Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Makiamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan baada ya hafla ya makabidhiano rasmi ya Ofisi  Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi leo Novemba 12, 2015.PICHA ZOTE NA ISSA MICHUZI WA IKULU

  0 0

  Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Mbazi Msuya (wa katika) akieleza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki (wa kwanza kushoto) na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka (wa kwanza kulia) wakati wa ziara ya kukagua mtaro uliojengwa eneo la Buguruni kwa Mnyamani.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka (wa kwanza kulia mwenye miwani) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki wakiangalia hali ya daraja la Buguruni Visiwani walipofanya ziara ya maeneo yaliyoathiriwa na ugonjwa wa kipindupindu.
   (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Matthew Rycroft, Mwakilishi wa Kudumu wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa na Rais wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa,  kwa mwezi  Novemba, akizungumza na waandishi wa habari   hawapo pichani, mara baada ya  Baraza Kuu la Usalama kumaliza kikao chake kilichojadili hali ya  Burundi, kikao ambacho pia kilipitisha azimio ambalo pamoja na mambo mengine linamuunga mkono  Rais wa Uganda  Yoweri Museven ambaye aliteuliwa na  Viongozi  wenzie wa Jumuiya ya Afrika  Mashariki kuwa msimamizi na mwezeshaji wa majadiliano  kati ya pande zinazopinga  nchini Burundi.
   
  Na Mwandishi Maalum, New York
  BARAZA Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa  limelaani vikali  hali ya  kuendelea kwa matukio ya mauaji, utesaji na vitendo vingine vya  vinavyokiuka haki za binadamu nchini  Burundi.

  Pamoja na kukemea hali hiyo,  Baraza Kuu la Usalama  limeeleza  kusudio la kuchukua hatua zaidi kwa nchi hiyo ya  Burundi.  Pamoja na  kumwomba  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, katika kipindi cha siku  kumi na tano awasilishe mbele ya Baraza hilo taarifa kuhusu  uwepo wa Umoja wa Mataifa nchini  Burundi katika siku za baadaye. 

  Jana ( Alhamisi) Baraza hilo  lilikutana katika kikao chake cha 7557   ajenda  ilikuwa ni Burundi ambapo,   Baraza kwa kauli moja  lilipitisha Azimio namba 2248 (2015). Kupitia  Azimio hilo, Baraza limetoa wito kwa  pande zote nchini Burundi kujiepusha na kukataa   fujo ikiwa ni pamoja na kujiepusha na vitendo vyovyote  vinavyoweza kutishia Amani na  utulivu wa taifa hilo.

  Vile  Vile Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo kwa mwezi huu wa  Novemba  Rais wake ni Uingereza limekema vikali kauli za  uchochezi zinazotolewa na baadhi ya  watu ndani na nje ya Burundi, kauli  ambazo kwa mujibu wa Baraza hilo zinalenga katika kushawishi chuki baina ya  makundi ya watu  nchini humo.

   Kufuatia  kauli hizo za uchochezi,  Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa,  limeitaka Serikali ya Burundi kuheshimu, kulinda na kuhakikisha haki za binadamu na  misingi ya uhuru,  kuheshimu utawala wa sheria pamoja na uwajibikaji wa uwazi dhidi ya   fujo na  itoe ushirikiano kwa  Ofisi ya Kamisheni ya Haki za Binadamu.

    Kupitia  Azimio hilo  Baraza Kuu pia  limeitaka serikali ya Burundi kuwawajibisha wale wote watakaopatikana na hatia  ya ukiukwaji ya Sheria ya Kimataifa ya haki za binadamu na unyanyasajji wa haki za binadamu.

  Aidha  kupitia  Azimio hilo,  Baraza Kuu la Usalama limetoa wito kwa Serikali ya  Burundi kutoa ushirikiano katika majadiliano yanayoongozwa na Jumuiya ya Afrika  Mashariki  na ambayo yameridhiwa na Umoja wa Afrika na limetaka  kuitishwa haraka majadiliano yatakayokuwa jumuishi yakiwashirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya Burundi  ili kutafuta muafaka utakaokubaliwa na pande zote.

  Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa pia kupitia Azimio hilo limesema linamuunga mkono kwa nguvu zote  mwezeshaji wa  majadiliano hayo  ambaye ni Rais Yower Museveni wa Uganda aliyeteuliwa na  Viongozi wa Jumuiya ya Afrika  Mashariki.

   Katika kusaidia  mchakato wa majadiliano hayo, Baraza Kuu la Usalama  la Umoja wa Mataifa limemkaribisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  kupeleka  timu  ya wataalam ambao kwa kushirikiana  na Serikali, Umoja wa Afrika na wadau wengine watabuni   mbinu  za  kushughulikia matatizo ya kisiasa na kiusalama.

  0 0

  SIMU.TV: Rais Magufuli akabidhiwa ofisi rasmi, kufutwa uchaguzi Zanzibar kaa la moto. Bunge la 11 kuanza leo kwa usajili wa wabunge;
   SIMU.TV: Philip Marmo, Ndungai wazidisha joto uspika, CCM yazoa viti maalum 1,021 vya udiwani, wane waimamishwa kazi halmashauri ya Hai;  https://youtu.be/FxYZqMCAsGQ

  SIMU.TV: Maduka ya dawa binafsi Muhimbili kufungwa, serikali kuanzisha maduka yake ndani ya hospitali zote za serikali; https://youtu.be/ZlfbjFp8bs8

  SIMU.TV: Pata dondoo za habari za kina za kisiasa, michezo na burudani zilizotawala magazeti ya leo;https://youtu.be/YFkLwTtiMh8 

  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (kushoto), akisalimiana na Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha), Piniel Mgonja , wakati wa  ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji,Kurasini jijini Dar es Salaam.  Wa kwanza kushoto ni Kamishna Jenerali  wa Uhamiaji, Sylvester  Ambokile.
   Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester  Ambokile (kushoto), akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, baadhi ya Ofisi za Idara ya Uhamiaji, wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara katika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye tai),akipewa maelezo alipotembelea Dawati la Mapokezi wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji,Kurasini, jijijni Dar es Salaam.
   Afisa Uhamiaji, Lilian Maleko akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye tai), jinsi  taarifa za muombaji pasi ya kusafiria zinavyohakikiwa, wakati wa ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam.

   Afisa Uhamiaji anayeshughulika na uchapaji wa hati za  kusafiria,  Amir Hassan (wa pili kushoto), akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye tai),moja ya pasi iliyokua imeshachapwa tayari kwa matumizi ya kusafiria, wakati wa ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam.
   Kamishna wa Uhamiaji (Vibali vya Ukaazi, Visa na Pasi), Victoria Lembeli (katikati), akimuonesha  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, moja ya karatasi iliyokataliwa na mfumo wa komputa baada ya kubainika kwa taarifa za uongo za muombaji wa Hati ya Ukaazi, wakati Naibu Katibu Mkuu  huyo alipotembelea Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini,jijini Dar es Salaam.
   Maafisa wa Idara ya Uhamiaji, wakimsikiliza  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (hayupo pichani), alipofanya mkutano nao wakati wa ziara aliyofanya  Makao Makuu ya Uhamiaji,Kurasini, jijini Dar es Salaam.
  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Silvester Ambokile akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, baadhi ya machapisho ya Idara ya Uhamiaji, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini Jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye tai) katika picha ya pamoja na viongozi wa Idara ya Uhamiaji wakati alipotembelea Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam.  Wapili kushoto mstari wa mbele, ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bi. Lilian Mapfa. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

older | 1 | .... | 684 | 685 | (Page 686) | 687 | 688 | .... | 1897 | newer