Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 683 | 684 | (Page 685) | 686 | 687 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Sali International Hospital has acquired all assets belonging to former African Medical Investment (AMI) Hospital which closed business in Dar es Salaam five months ago (May). 

  The hospital proprietors, Dr. Edward Tamale-Ssali and his wife Kate Ssali, apart from buying AMI assets, has added more modern equipments and moved to put up a state of the art international hospital at the same premise in Masaki area in Tanzania, which opened its doors for patients early October this year.

  Dr. Ssali, a consultant Obstetrician and gynaecologist with diverse experience having worked in this specialty in several hospitals in the UK and other countries, says the investment would break new grounds for healthcare in Tanzania.Briefing a section of journalists who toured the facility recently, Dr. Ssali said he had been under immerse pressure to open the facility from potential clients who were desperately in need of quality services in a good environment. 

  “A lot of potential clients ranging from local residents, business men, international and local dignitaries as well as tourists have dropped by the hospital enquiring about the services and expressed their excitement to have such a hospital in town. A lot of health services we offer here were not available since AMI closed and patients had to be flown out of the country to acquire specialized services,” said Dr Ssali.

  He said, shortly after announcing start of its operations, the hospital has been attending to an impressive number of out and in-patients, with a steady increase in the patients’ numbers.Dr. Sali said the positive response to the hospital from clients from all walks of life signals a positive business projection.  

  “The support we have been getting from the local community and uptake in patient numbers since we started has been gratifying. Our responsibility is to ensure that the trust they place in this facility and their confidence in the services we provide are upheld at all times,” said Dr. Ssali.

  He said that as patients’ numbers continue to increase, the road ahead looks promising, adding that; “There is no doubt that the excellent services at Sali International Hospital gives our health facility an upper hand in Tanzania market. It is a journey that is worth a ride.” 

  Dr. Ssali, told journalists that his hospital focuses on becoming a leading supplier of private specialist hospitals services across Tanzania, as well as East and Central Africa offering quality in and outpatient services, with plans to root its operations in Tanzania market.  

  “We are fortunate to have a number of highly respected specialists on board with extensive experience in areas such as internal medicine, gynecology, cardiology and pediatrics. They are also well versed in treating patients from different cultural backgrounds. Their skills and experience will undoubtedly be of great benefit to our patients.

  “Although we have recalled some former AMI specialists, we have also recruited specialists from local medical field with exceptional medical service records and international expatriates, with focus on racial dynamics. This gives SIH an added advantage to serve a rage of patients, thereby raising our performance and hence positively influences our balance sheet portfolio,” he said.   
   
  According to Dr. Sali, the 30-bed hospital specializes in medical and surgical disciplines and offers a delivery room, 24-hours emergency center, X-ray department, haemodialysis unit, CT-scan center, 4D ultrasound, neonatal ICU beds, well equipped Intensive Care Unit (ICU) and fully fledged theaters. 

  Dr. Sali mentioned that although the hospital opened its doors to patients early last month (October), official opening is scheduled to happen in three months time.

  0 0

  Mnamo tarehe 08/11/2015 Magazeti ya Mzalendo na Majira yaliandika habari zilizolenga  upotoshaji na taharuki kwa wananchi na hususani watumiaji wa Maji kwa mkoa wa Dar es salaam wanaohudumiwa na DAWASCO.

  Katika gazeti la Mzalendo lilikuwa na kichwa cha habari “Wengi Dar watumia maji yenye kinyesi” na upande wa gazeti la Majira lilibeba kichwa cha habari “Maji machafu yaathiri Dar”. Ndani ya habari hizo waandishi wameelezea shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) kama moja ya chanzo cha ugonjwa wa kipindupindu kwa kuwa maji hayo yameathirika na kinyesi.

   Gazeti la Majira 08/11/2015 ukurasa wa 3 inanukuliwa “Kwa kiasi kikubwa Maji ya jiji yamekuwa yameathirika na kinyesi cha binadamu”. mwisho wa kunukuu. Aidha nukuu nyingine kwenye gazeti la Majira inasomeka “Wananchi wa jiji la Dar es salaam wamekuwa wakipata Majisafi na salama kutoka mamlaka ya Majisafi na salama (DAWASCO) kwa aslimia 30 tu”.

   Ikumbukwe  pia maeneo makubwa ambayo wagonjwa wa kipindupindu wanatoka ni maeneo ambayo yameathirika na wizi wa maji kwa kiasi kikubwa na mapambano hayo bado yanaendelea kuhakikisha wizi wa maji unakwisha maeneo hayo ni pamoja na  Manzese, Buguruni ,Kigogo , Mburahati , Kinondoni mkwajuni pamoja na Tandale.Jitihada zilizofanywa na Dawasco katika kudhibiti  ugonjwa  huu hususa ni watumiaji Maji ni pamoja na Kupeleka huduma ya maji BURE kwa maeneo yaliyoathirika zaidi na mlipuko huo kupitia utarartibu wa Manispaa uliowekwa.

  ·         Kutoa Elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari , machapisho, pamoja na vikao vya pamoja na watendaji wa Mitaa, Bwana Afya kwa maeneo yaliyoadhirika.

  ·         Kuanza kwa usajili rasmi wa magari yanayofanya biashara ya maji (water bowsers) ili kulinda afya ya mtumiaji.  Zoezi lilianza tarehe 01 October 2015 na idadi ya Magari 120 yameshasajiliwa hadi sasa.Kuondoa maunganisho yasiyo halali ambayo yanafanywa na baadhi ya wananchi “vishoka” , ambayo yanapeleka huduma ya Maji kwa baadhi ya maeneo yanayoadhirika zaidi.

  Dawasco inasikitika kwa taarifa hizo za upotoshaji kwani tangu kuibuka kwa ugonjwa wa Kipindupindu jitahada mbali mbali zimefanyika kwa kushirikiana na Mamlaka husika ikiwemo Wizara ya Afya , Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha maafa ,kikosi cha kupambana na ugonjwa wa kipindupindu katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa na taaisi nyingine nyingi zenye kutetea ustawi wa Afya ya Jamii.

  Dawasco inapenda kuwakumbusha vyombo vya habari kuzingatia weledi na utashi katika kuteleza majukumu yao ya kila siku ili kuwapatia wananchi taarifa zilizo sahihi na zenye ukweli siku zote.

  Tunaamini kosa la namna hiyo halitajirudia tena ili kuepusha adha na usumbufu kwa wananchi kama ulivyojitokeza kipindi hiki.

  “Dawasco mbele kwa mbele”

  Bi Everlasting Lyaro
  Kaimu Meneja Uhusiano - Dawasco  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wa Chama chama Wananchi (CUF)wamepinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kufutwa  kutokana na mtu aliyefanya utenguzi huo ni utashi wake na sio Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

  Wajumbe 27 wa baraza hilo wamewasili jijini Dar es Salaam kuzungumza na waandishi wa habari juu ya kizungumkuti cha matokeo ya uchaguzi kufutwa huku wakiwa wenyewe hatambui hatua hiyo.

  Akizungumza  mmoja wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Abbakari Khamisi amesema uchaguzi wao uliofutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha hawatambui na wataka waendelee kuhesabu kura hizo na sio kurudia uchaguzi.

  Amesema uchaguzi utafutwaje wakati wajumbe wa baraza la wawakilishi wamepata udhibitisho wa maandishi wa kushinda majimbo yao na kufanya uchaguzi ukirudiwa ni ukiukwaji kwa katiba.

  Khamisi amesema kuwa uchaguzi wa Zanzibar, kushinda kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) ni halali na kushinda chama kingine kati uchaguzi unaonekana batili huku wakujua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

  “Hatutaki uchaguzi urudiwe kwani kufanya hivyo ni kukiuka kwa katiba ya uchaguzi kutokana  na waangalizi walisema uchaguzi ulikuwa wa haki na huru kwa nini urudiwe wakati katiba haina tafsiri ya kufuta na matokeo na kufanya uchaguzi mwingine”amesema Khamisi.

  Nae Ismail  Jussa mshindi wa jimbo la Marindi amesema kuwa hawatambui kuendelea kwa utawala uliopo sasa kutokana na katiba ya Zanzibar.

   Aliongeza kuwa nchi ya Zanzibara haina Rais na kufanya kuendelea kwa Rais aliyemaliza muda wake ni kukiuka kwa katiba.
  Naibu katibu mkuu wa Chama Cha wananchi CUF, Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na waandishi wa habari leo katika mkutano wa waandishi wa habari leo kuhusiana na wabunge wa baraza la wawakilishi Zanzibar kumwomba rais wa jamhuri ya muungano kuwaapisha ili waanze kufanya kazi yao kwaajili ya kuwawakilisha wananchi wa majimbo yao.
  Mgombea wa baraza la wawakilishi Zanzibar, Abubakari Khamis akionyesha fomu ya  uthibitisho kuwa amechaguliwa kuwa mwakilishi wa baraza la wawakilishi Zanzibar leo katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wawakilishi waliochaguliwa kuwakilisha baraza la wawakilishi Zanzibar waliohudhilia katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
  Naibu katibu mkuu wa Chama Cha wananchi CUF, Nassor Ahmed Mazrui, akizungumza na waandihi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya wajumbe wa bunge la wawakilishi Zanzibar wakionyesha fomu zao za Ushindi wa walipohudhulia mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
  Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

  0 0

  Mwigizaji WemaSepetu  (kushoto) akifurahia jambo na mwakilishi wa  kampuni ya QWAY International inayosambaza kinywaji  cha Belvedere Vodka nchini, Tanya  Mulamula, wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu ya Spectre ya James Bond iliyofanyika Cape Town Fish Market.
   
  WATU mbalimbali walihudhuria hafla ya uzinduzi wa filamu ya Spectre ya  James Bond iliyofanyika Cape Town Fish Market chini ya udhamini wa Belvedere Vodka, Heineken, Jaguar pamoja na Land Rover.

  Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo, mwakilishi wa kampuni ya QWAY International inayosambaza  kinywaji cha Belvedere Vodka,Tanya Mulamula alisema hafla hiyo inalenga kuwakutanisha wadau na kuifurahia filamu hiyo, ikiwa siku moja kabla ya uzinduzi wake.

  Filamu ya hiyo ya Spectre iliyoigizwa na Daniel Craig kama James Bond ilizinduliwa rasmi hapa nchini Ijumaa iliyopita uzinduzi uliofana.
   
  Alisema kuwa kinywaji hicho kinatambua nafasi ya filamu katika kuwaburudisha wateja wake na ndio maana imetoa tiketi nyingi za bure kwa wateja wake wengi.
   
  " Belvedere Vodka, Heineken, Land Rover na Jaguar tumeamua kwa pamoja kuungana na watu wengine wengi katika kusherehekea uzinduzi wa filamu hii kwa kuanza na hafla hii ikiwa ni siku moja kabla ya uzinduzi wa filamu yenyewe" alisema Tanya.
   
  Pia Mkurugenzi wa mauzo wa kampuni ya CMC inayohusika na magari ya Jaguar pamoja na Land Rover, Kim Withnall alisema kuwa filamu hiyo imehusisha magari ya Jaguar na Land Rovers na ndio maana hata kwa Tanzania kampuni yake imeshiriki katika kuandaa hafla hiyo.  Bond Girls posing at the Jaguar 2
  Wadau wa Belvedere Vodka pamoja na Heineken wakishow some love
  Mchekeshaji ambae pia ni mshereheshaji Evance Bukuku akizungumza na Tanya Mulamula ambae ni mwakilishi wa  kampuni ya QWAY chini inayosambaza kinywaji cha  Belvedere Vodca pamoja na Moët-Hennessy  wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu ya Spectre ya James Bond iliyofanyika Cape Town Fish Market
  Mwakilishi wa  kampuni ya QWAY International inayosambaza kinywaji  cha Belvedere Vodka nchini, Tanya  Mulamula, kulia akiwa na Carlo wa Nyama Choma Festival wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa filamu ya Spectre ya James Bond iliyofanyika Cape Town Fish Market.
  Bond Girls posing at the Belvedere Bar
  Bond Girls posing at the Heineken DJ Booth

  Na Mwandishi Wetu

  0 0

  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa michuano ya Kombe la Shirikisho (AzamHD Federation Cup) utakaofanyika leo Jumatatu, saa 9 kamili mchana katika uwanja wa Karume ambapo timu ya Abajalo FC itacheza dhidi ya Transit Camp zote za jijini Dar es salaam.
  Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi jana kwa mchezo mmoja kuchezwa katika uwanja wa Karume uliopo mjini Musoma, ambapo Vill Squad ya jijini Dar es salaam iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3- 1 dhidi ya timu ya JKT Rwamkoma ya mkoani Kagera.
  Katika uwanja wa CCM Kirumba, Pamba FC ya jijini humo watakua wenyeji wa timu ya wachimba dhahabu kutoka mkoani Shinyanga, Bulyanhulu FC mchezo utakaoza saa 10:30 jioni.
  Jumla ya timu 64 zinashiriki  michuano hiyo kutoka Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kuwania kutwaa ubingwa, ambapo Bingwa wa michuano AzamHD Federation Cup atapata nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2017.

  0 0

  BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU


  AWAMU YA PILI YA WANAFUNZI WALIOPANGIWA MIKOPO KWA 2015/2016

  BODI  ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuutaarifu umma kuwa kuna taarifa zinazosambazwa na baadhi ya mitandao ya kijamii kuwa Bodi haitatoa mikopo kwa waombaji wapya kwa mwaka wa masomo 2015/2016. Taarifa hizo si za kweli na hivyo Bodi inauomba umma kuzipuuza. 


  Aidha, Bodi ya Mikopo inapenda kutoa taarifa kwamba hadi sasa imekwishawapangia mikopo jumla ya waombaji mikopo wenye sifa 40,836 wa mwaka wa kwanza. Katika awamu ya kwanza, Bodi ilitoa orodha yenye jumla ya waombaji 12,282 waliofanikiwa kupata mikopo na katika Awamu ya Pili iliyotolewa tarehe 9 Novemba, 2015 jumla ya waombaji 28,554 wamepangiwa mikopo.


  Majina ya waombaji waliofanikiwa kupata mikopo kutoka katika awamu zote mbili yanapatikana kupitia mtandao wa Bodi wa olas.heslb.go.tz na tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz). Aidha, orodha hizo pia zimetumwa vyuoni kwa ajili ya taratibu za usajili.


  Lengo la Bodi ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wenye sifa kupata mikopo katika mwaka wa masomo 2015/2016, ambao ni 50,830, wanapata mikopo.

  Aidha, Bodi inapenda kuwasihi waombaji wa mikopo kuwa watulivu wakati mchakato wa upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa unaendelea.
             

  Imetolewa na:


  MKURUGENZI MTENDAJI

  BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Donan Mmbando akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya Mlipuko wa Ugonjwa wa kipindupindu uliopo sasa ulianza mnamo 15 Agosti 2015, katika Manispaa ya Kinondoni na baadae kusambaa katika Manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam leo jijini Dar es Salaam.
    Waandishi  wa habari wakimsikiliza  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Donan Mmbando, leo jijini Dar es Salaam
  Wadau mbalimbali wakiwa katika mkutano huo leo  jijini Dar es Salaam
  (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)


  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  MLIPUKO wa Ugonjwa wa kipindupindu umesambaa katika mikoa 14  na kufikia wagonjwa 7825 na vifo 106.

  Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Donan Mmbando amesema kati ya wagonjwa wote waliougua 3746 sawa na asilimia 67 wanatoka katika mkoa wa Dar es Salaam.

  Amesema kuwa  Mikoa inayotoa taarifa ya kuwepo wagonjwa wapya ni Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Dodoma, Mwanza, Arusha, Mara, Singida na Tanga.

   Mmbando amesema kuwa  ugonjwa huo umeripotiwa katika mikoa mingine ya Tanzania ikiwa ni pamoja na Pwani, Singida, Mara, Arusha, Tanga, Mwanza, Shinyanga, Morogoro, Iringa, Kilimanjaro, Dodoma, Kigoma, Geita pamoja na Rukwa.

  Aidha amesema hadi kufikia Novemba 8,2015  idadi ya wagonjwa waliokwisha kuripotiwa tangu mlipuko uanze hapa nchini ni 7825 na vifo 106 amabo ni asilimia 1.3 ya waliougua.

  Amesema hatua walizozichukua kwa ugonjwa huo ni kutoa dawa, vifaa vya maabara na vifaa kinga kwa mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro.

  Aliongeza kuwa  Wizara imepokea maombi kutoka mikoa ya Singida, Arusha, Tanga, Mwanza, Mara na Geita kati ya Oktoba 15 mwaka huu  na yanashughukuliwa na utawala, Kupima vipimo vya maabara na kufuatilia ubora wa vipimo kutoka katika mikoa iliyofanya uchunguzi na kuthibitisha uwepo wa ugonjwa huo, Kupeleka timu za watalaam kutoka ngazi ya Mkoa na Taifa kusaidiana na timu za Wilaya husika. 

  Aidha tarehe 28 Oktoba 2015, Timu ya Kitaifa ilienda katika mikoa ya Tanga, na Singida na vilevile mkoa wa Manyara pia timu ilienda kwa ajili ya kufuatilia tarifa za kuwepo kwa ugonjwa wa kuhara na kutapika – taarifa ya timu hizi inakamilishwa na itawasilishwa.

  Mmbando amesema hatua nyingine Kutoa mafunzo kwa watumishi wa afya juu ya ufuatiliaji wa ugonjwa na utoaji wa matibabu ,Kutoa elimu ya kwa umma kupitia vyombo vya habari hususani radio na runinga. Aidha, mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini yametolewa, Kuandaa “Water safety plan” kwa kushirikisha wadau mbalimbali ikiwemo WHO, PSI, CDC, MSF, Redcross na USAID. Aidha mpango mkatati huu utajikita kwanza kwa jiji la Dar es salaam kwa kuanzia na hapo baadae itaenda katika mikoa mingine.

  Amesema changamoto katika ugonjwa huo ni,Mwitikio hafifu wa jamii juu ya kukabiliana na ugonjwa huu,Jamii kutokuzingatia kanuni za afya na mazingira,Ushiriki mdogo wa sekta nyingine katika kupambana na ugonjwa huu,Ukosefu wa pesa za kuwalipa watumishi wa afya wanaohusika katika zoezi la kukabiliana na ugonjwa huu.

  0 0


   Katibu wa soko la Tabata Muslim lililopo Manispaa ya Ilala, John Nombo (kushoto),  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu kupungua kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika soko hilo baada ya Shirika la Equality for Growth (EfG), kutoa mafunzo ya kupinga ukatili huo katika masoko sita ya Manispaa hiyo. Kulia ni Mwezeshaji wa Sheria wa Soko hilo, Aisha Juma na  Saada Ngunde.
   Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo, Saada Ngande akizungumza katika mkutano huo.
   Mwezeshaji wa Sheria, Irene Daniel (kushoto), akizungumza kuhusu kazi alizofanya za kusaidia watu kujua haki zao. Kulia ni Mwenyekiti mstaafu wa Umoja wa Wanawake katika Soko hilo, Happyness Urono.
   Mwenyekiti mstaafu wa Umoja wa Wanawake katika Soko hilo, Happyness Urono, akizungumzia changamoto walizokuwa nazo katika soko hilo.
  Mwezeshaji wa Sheria, Irene Daniel akionesha mabango yanayohamasisha masuala ya haki ya mwanamke katika soko hilo.  Na Dotto Mwaibale

  UJASIRI wa Wawezeshaji Sheria wanawake katika soko la Tabata Muslim lililopo Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam umesaidia kupunguza vitendo vya ukatili wa jinsia katika soko hilo.

  Hayo yalielezwa na Mwezeshaji wa sheria katika soko hilo, Irene Daniel wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi ambao wapo katika ziara ya kutembelea masoko ya manispaa hiyo kuona jinsi vitendo vya ukatili wa kijinsia vilivyopungua baada ya Shirika la Equality for Growth kutoa mafunzo ya kupinga ukatili huo katika masoko hayo.

  "Ujasiri tuliofundishwa sisi wawezeshaji wa sheria katika masoko na EfG wa kufuatilia matukio ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia umesaidia sana kupunguza vitendo hivyo katika soko letu" alisema Daniel.

  Akitolea mfano alisema mbali na kufuatilia masuala hayo ya ukatili katika soko hilo pia aliweza kuisaidia familia moja baada ya baba wa familia hiyo kutaka kumfanyia kitendo cha udhalilishaji mke wake ambapo alikwenda kuzungumza na baba huyo ambaye alikubali kubadilika.

  Alisema baba huyo ambaye alikuwa anashinda vijiweni baada ya kujitambua alimpatia mtaji wa fedha ambapo alianzisha biashara ya maji na sasa msuguano na mke wake umekwisha na wamefikia hatua ya kuwa na eneo lao la biashara ya mama lishe na uuzaji wa maji.

  Katibu wa soko hilo John Nombo alisema changamoto kubwa waliyokuwa nayo katika soko hilo ni lugha za matusi, wateja kuvaa nguo fupi zilizokuwa zikionesha miili yao hivyo kuwafanya vijana kuwa na matamanio na kuanza kuwatomasa lakini hivi sasa vitendo hivyo havipo tena.

  Mwezeshaji wa sheria Saada Juma alilalamikia jeshi la polisi kituo cha Tabata kushindwa kushughulikia kesi ya mdogo wake aliye dhalilishwa na kijana mmoja katika soko hilo ambapo licha ya kijana huyo kufahamika alipo lakini polisi wameshindwa kumtia nguvuni.

  Mwenyekiti mstaafu wa Umoja wa Wanawake katika soko hilo, Happyness Urono alisema vitendo vya udhalilishaji katika soko hilo hakuna kwani mafunzo waliopatiwa na EfG yamewafanya wajitambue na kuzijua haki zao ambapo ametoa mwito kwa wanawake kuzidisha umoja wao katika kila jambo.


  0 0

  SIMU.TV:  Pata Uchambuzi toka kwa wataalumu wa mambo ya kisiasa juu ya hali ya kisiasa nchini Burundi, Ungana na SIMU.tv Hapa.
   SIMU.TV:  Pata Dondoo kuhusu Ugonjwa wa Kisukari na jinsi ya kutibu ugonjwa huo katika safari ya kuelekea sikukuu ya maadhimisho ya Kisukari Duniani. https://youtu.be/mdHmzzX7MG4
  SIMU.TV:  Pata uchambuzi kutoka kwa Mwenyekiti wa hifadhi za jamii utambue faida na Sheria mbali mbali za haki katika mifuko ya uhifadhi wa jamii. https://youtu.be/6RcGgTUt66c
  SIMU.TV:  Kutana na balozi Ally Karume kutoka Zanzibar akikujuza hali ya kisiasa Zanzibar amesema hali ya kisiasa Zanzibar ni shwari, https://youtu.be/vUaOIHrTjzk 
  SIMU.TV:  Serikali imedaiwa kutowatumia vizuri waandishi wa habari kutangaza vivutio vya utalii nchini hivyo kukosesha taifa mapato yatokanayo na sekta hiyo; https://youtu.be/71dT6sH47nE 
  SIMU.TV:  Bodi ya mikopo ya elimu ya juu yakanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao kuwa bodi hiyo haitatoa mikopo kwa waombaji wapya; https://youtu.be/D98xDcSCGks 
  SIMU.TV:  Wananchi wanaoishi mabondeni wameonesha wasiwasi wa kukumbwa na Mafuriko kutokana na taarifa iliyotolewa na mamlaka ya hali ya hewa. https://youtu.be/1DaoFINhgmk

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akipokea nyaraka za Ofisi kutoka kwa Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,leo No 9, 2015. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akisaini Kitabu cha wageni wakati alipoingia Ofisini kwake kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo Nov 9, 2015  Ikulu jijini Dar es Salaam. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia kwake), Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula na Naibu Katibu Mkuu wake, baada ya makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Nov 9,2015.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi Binafsi ya Makamu wa Rais, baada ya bakabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 9, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi yake wakati alipowasili kwenye Ofisi yake kwa mara ya kwanza leo baada ya kukabidhiwa rasmi Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Bilal. Wafanyakazi hao walijipanga kumpokea huku wakiimba, kupiga makofi na vigeregre wakati akiwasili.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi ya Maua kama ishara ya makaribisho, kutoka kwa mfanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Martha Mashuki, wakati alipowasili kwa mara ya kwanza kwenye Ofisi yake na kupokelewa na wafanyakazi wake leo, Nov 9, 2015.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ua Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan,akisalimiana na Katibu Mkuu wa Ofisi yake, Sazi Salula,wakati alipowasili kwenye Ofisi yake kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa ofisi rasmi leo, Nov 9,2015. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Eng. Angelina Madete.
   Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi Binafsi ya Makamu wa Rais, wakati akiondoka baada ya makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 9, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati alipowasili kwenye Ofisi hiyo leo Nov 9, 2015 baada ya makabidhiano. Akizungumza na wafanyakazi hao Mama Samia, aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa mashirikiano na kwa bidii ili kutimiza Kaulimbiu ya Mhe.Rais ya 'HAPA KAZI TU'
   Baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza nao leo alipowasili Ofisini kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa Ofisi rasmi.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara zilizo chini ya Ofisi ya makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) alipowasili ofisi kwake kwa mara ya kwanza leo Nov 9, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi yake baada ya kuzungumza nao alipowasili ofisi kwake kwa mara ya kwanza leo Nov 9, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wanamama wa Ofisi yake baada ya kuzungumza nao alipowasili ofisi kwake kwa mara ya kwanza leo Nov 9, 2015 kwa makabidhiano ya Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu. Picha na OMR

  0 0


  0 0


  Karibu Meru Logistics kwa huduma nzuri, safi, zenye uhakika na haraka kutuma mizigo kutoka UK kwenda Tanzania.

  Wasiliana nasi pia kama unahitaji chochote kutoka UK kama vile magari, matractor, fridge, TV, Vyombo nk. tuta kusaidia kununua na kukutumia mpaka Tanzania bila tatizo lolote na vitafika salama kabisa

  Bei za kutuma mizigo ni kama ifuatavyo:

  20' CONTAINER TO DAR /MOMBASA FROM £1,300 
  40' CONTAINER TO DAR /MOMBASA FROM £1,800
  4X4 TO DAR/MOMBASA FROM £850
  SALOON CARS TO DAR/ MOMBASA FROM £750
  AIR CARGO TO DAR £5 A KILO
  AIR CARGO TO ZNZ £4 A KILO 
  INCLUSIVE CLEARANCE
  TO COLLECT CARGO LONDON FROM £25 
  TO COLLECT CARGO OUTSIDE LONDON FROM £50
  ONCE YOU PAY HERE IN UK YOU DONT PAY ANYTHING IN TANZANIA
  (UKIISHA LIPA UK UNAKWENDA TU KUCHUKUA MZIGO WAKO)

  Address in UK: Unit 12 Manor Way Business Centre
  Marsh Way, Rainham, Essex
  RM13 8UG

  COLLECTION POINT IN DAR IS:
   DAR FREE MARKET, ALI HASSAN MWINYI ROAD
  OYSTER BAY NEAR KENYAN EMBASSY & DSTV

  Telephone: +44 (0) 1708554632
  Instagram: @merulogistics 
  Facebook: Meru Logistics

  CUSTOMER SATISFACTION GURANTEED!!!

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Serikali la LUKEMA Community Development and Training Services baadhi ya vibao maalumu kwa ajili ya kujifunzia wanafunzi wa darasa la awali.
  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Serikali la LUKEMA Community Development and Training Services baadhi ya maboksi ya chaki kwa ajili ya kufundishia watoto wa darasa la awali ikiwa ni sehemu ya msaada kukisaidia kituo hicho. Vifaa vingine vilivyotolewa kama msaada na TTCL kwa kituo cha LUKEMA ni pamoja na maboksi ya chaki, vibao vya kuandikia, madaftari aina mbalimbali ya wanafunzi wa awali, mikeka kwa ajili ya kukalia wanafunzi. Kulia pembeni ni Ofisa Uhusiano wa TTCL Amanda 
  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (kulia) akiwagawia madaftari wanafunzi wa darasa la awali ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa kukisaidia kituo hicho. Vifaa vingine vilivyotolewa kama msaada na TTCL kwa kituo cha LUKEMA ni pamoja na maboksi ya chaki, vibao vya kuandikia, madaftari aina mbalimbali ya wanafunzi wa awali, mikeka kwa ajili ya kukalia wanafunzi.
  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (kulia) akiwagawia madaftari wanafunzi wa darasa la awali ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa kukisaidia kituo hicho. Vifaa vingine vilivyotolewa kama msaada na TTCL kwa kituo cha LUKEMA ni pamoja na maboksi ya chaki, vibao vya kuandikia, madaftari aina mbalimbali ya wanafunzi wa awali, mikeka kwa ajili ya kukalia wanafunzi.
  Wanafunzi wa darasa la awali wa kituo cha LUKEMA kinachomilikiwa na Shirika lisilokuwa la Serikali la LUKEMA Community Development and Training Services kilichopo jijini Dar es Salaam wakifurahia madaftari waliyopewa na TTCL kwa ajili ya masomo. Miongoni mwa vifaa vingine vilivyotolewa kama msaada na TTCL ni pamoja na maboksi ya chaki, vibao vya kuandikia, madaftari aina mbalimbali ya wanafunzi wa awali na mikeka kwa ajili ya kukalia wanafunzi.
  Baadhi ya maofisa wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL) na walimu na uongozi wa Shirika lisilokuwa la Serikali la LUKEMA Community Development and Training Services linalomiliki kituo cha awali wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa darasa la awali wa kituo cha LUKEMA mara baada ya kukabidhiwa misaada mbalimbali ya vifaa vya masomo. Miongoni mwa vifaa vingine vilivyotolewa kama msaada na TTCL ni pamoja na maboksi ya chaki, vibao vya kuandikia, madaftari aina mbalimbali ya wanafunzi wa awali na mikeka kwa ajili ya kukalia wanafunzi. Shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 80 inakabiliwa na changamoto mbalimbali hasa vifaa vya masomo kwa wanafunzi wake.
  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (wa pili kulia) akimkabidhi baadhi ya mikeka Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Serikali la LUKEMA Community Development and Training Services vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la awali la kituo hicho kama msaada.
  Muonekano wa darasa hilo la awali kabla ya kukabidhiwa mikeka ya kukalia, awali wanafunzi hao walikuwa wakikaa chini. 
  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (anayeandika ubaoni) akiwachemsha bongo wanafunzi wa darasa la awali wa kituo cha LUKEMA kwa maswali ya hesabu kabla ya kukabidhi misaada ya vifaa vya masomo leo shuleni hapo.
  Muonekano wa darasa hilo la awali baada ya kukabidhiwa misaada ya mikeka ya kukalia. Vifaa vingine vilivyotolewa kama msaada na TTCL kwa kituo cha LUKEMA ni pamoja na maboksi ya chaki, vibao vya kuandikia, madaftari aina mbalimbali ya wanafunzi wa awali, mikeka kwa ajili ya kukalia wanafunzi.


  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimjulia hali Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za Binadam,Bi Hellen Kijo Bisimba aliyelazwa hospital ya Agakhan mapema leo kufuatia ajali ya gari aliyoipata mwishoni mwa wiki barabara ya Al-Hassan Mwinyi jijini Dar, Dkt Magufuli pia amefanya ziara ya kushtukiza katika hopsitali ya Taifa ya Muhimbili ikiwemo pia alitembelea wodi mbalimbali za wagonjwa na kuwajulia hali zao.
   Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya Novemba 9, 2015


  Rais Dkt.john Pombe Magufuli akizungumza na kuwapa moyo wauguzi katika hospitali ya taifa Muhimbili wakati alipofanya ziara ya ghafa kujionea hali halisi.
   Rais Dkt.John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili wakati alipofanya ziara ya kushtukiza hospitalini hap oleo na kuwafariji wagonjwa.
   Rais akiagana na wauguzi na wafanyakazi wa hospitali ya taifa Muhimbili


  Rais akipungia mkono, wagonjwa na wananchi wakati alipotembelea hospitali ya taifa Muhimbili
   PICHA KWA HISANI YA K-VIS BLOG

  0 0


   
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli , leo mchana amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukutana na hali ya kumsikitisha.

  “ Rais amesikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa hususan wanaolala chini. Pia amekasirishwa na hali ya kutokujali wala kushughulikia vifaa vya kufanyia kazi ambapo amekuta mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa kama vile MRI na CT-SCAN zikiwa hazifanyi kazi kwa muda wa miezi miwili sasa, ilihali mashine kama hizo katika Hospitali za binafsi zinafanya kazi na wagonjwa wanaelekezwa kwenda kutafuta huduma huko”. 

  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema na kutoa maelekezo yafuatayo :
  Rais amevunja Bodi ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo ilishamaliza muda wake na amemteua Prof. Lawrence Mseru , kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili kuanzia kesho tarehe 10 Novemba, 2015.

  Dkt. Hussein L. Kidanto ambaye ndiye anayekaimu hivi sasa, amehamishiwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambako atapangiwa kazi nyingine.Balozi Sefue pia amesema, Rais ametoa wiki moja na kwa vyovyote si zaidi ya wiki mbili kwa uongozi mpya wa Muhimbili kuhakikisha kuwa mashine zote za uchunguzi wa magonjwa ambazo hazifanyi kazi zinafanya kazi na kuhudumia wananchi kama ipasavyo.Tayari Wizara ya Fedha imetoa shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kazi hiyo na kulipa madeni ya ukarabati wa mashine za uchunguzi wa magonjwa nchini.

  Hata hivyo Katibu Mkuu Kiongozi amesema kuanzia sasa hospitali zote nchini zinatakiwa kutenga fedha kutoka kwenye mapato yao wenyewe na kuhakikisha mashine na vifaa vyote vya kazi vinafanya kazi wakati wote (Regular Maintenance).

  Balozi Sefue pia metumia nafasi hii kuwaagiza watendaji na viongozi wote katika sehemu za kazi kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo na kazi za umma zinatekelezwa ipasavyo.

  “Hakutakuwa na huruma kwa watumishi wa Umma wasiojali wananchi na mahitaji yao” Amesisitiza Balozi Sefue.

  Imetolewa na;
  Premi Kibanga,
  Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
  Ikulu – Dar es Salaam.
  9 Novemba, 2015

  0 0

  Kiongozi wa kampeni ya Okoa Tembo wa Tanzania,Shubert Mwarabu akizungumza na Waandishi wa habari ndani ya ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO,kuhusiana na Barua yao ya Wazi kwa Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe Magufuli juu ya mauaji ya Tembo ambayo yamekuwa yakifanyika hapa nchini kwa kiwango kikubwa.Katika barua hiyo ya wazi,uongozi wa kampeni hiyo umetoa wito kwa Serikali kutekeleza ama kufanya yafuatayo1.kuwakamata na kuwashitaki wafanyabishara wakubwa wa meno ya Tembo nchini,bila kujali Utaifa,Hadhi au Mamlaka.2.Kutumia urafiki wa kihistoria kati ya Tanzania na China kufunga masoko ya meno ya Tembo huko china.3.Kuteketeza hadharani ghala ya meno ya Tembo Tanzania-inayosadikika kuwa kubwa kuliko yote Ulimwenguni.

  Bwa.Shubert ameeleza kuwa Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika uhifadhi wa Tembo hapo kapla,anasema Mwaka 1989,Tanzania iliongoza jitihada za kupiga marufuku biashara ya mene ya Tembo Ulimwengu, "tulipochukua hatua kukomesha mauaji ya Tembo,Dunia nzima ilituunga mkono,hivyo ni lazima turejeshe upya dhamira yetu kwa ahadi tuliyojiwekea kwa hatua ya Kimataifa zaid ya miaka ishirini iliyopita,na kuleta ukomo wa biashara yote ya meno ya tembo hapa nchini'',alieleza Bwa.Shubert.
  Pichani kati ni mmoja wa Wajumbe wa kampeni ya OKOA TEMBO WA TANZANIA,Bwa.Lameck Mkubulo akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari,kwenye mkutano uliofanyika mapema leo subuhi Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar,kuhusiana na Barua yao ya Wazi waliomuandikia Rais ya kumtaka achukue hatua juu ya suala la kupungua kwa kasi idadi ya Tembo nchini,kutokana na ujangili kwa ajili ya biashara haramu ya meno ya Tembo

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Airtel , Jackson Mmbando (katikati) pamoja na Meneja  kitengo cha Airtel Money, Stephen Kimea ( kushoto) na Afisa kitengo cha Airtel Money, Aliesikia Peter kwa pamoja wakionyesha kipeperushi cha ofa mpya itakayowawezesha wateja wa Airtel kutuma pesa kiasi chochote cha pesa kupitia huduma ya Airtel Money bure.
  Meneja Uhusiano wa Airtel , Jackson Mmbando akionge na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ofa kwa wateja wake itakayowawezesha kutuma pesa kiasi chochote cha pesa kupitia huduma ya Airtel Money bure. Pichani ni Stephen Kimea Meneja kitengo cha Airtel Money ( kushoto) na Aliesikia Peter Afisa kitengo cha Airtel Money.


  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua ofa kabambe itakayowawezesha wateja wa Airtel Money kutuma pesa kwa marafiki na familia zao ndani ya mtandao wa Airtel Bure

  Ofa hii mpya ijulikanayo kama "Okoa Mapene'' ina lengo la kuinua huduma za kifedha na kuwapatia wateja njia rahisi ya kufanya miamala yao ya kila siku

  Akiongea wakati wa uzinduzi, Meneja Uhusiano wa Airtel Bwn Jackson Mmbando alisema " kwa mara nyingine tena tunadhirisha kwa vitendo dhamira yetu ya kutoa huduma za kibunifu, rahisi na zenye gharama nafuu kupitia huduma ya Airtel Money. 

   Leo tunawawezesha wateja wetu wa Airtel money nchi nzima kuokoa pesa wanapotuma pesa kwenda kwa mtumiaji wa Airtel kwani tozo za kutuma pesa ni BURE kwa kiasi chochote kitakachotumwa. Tunaamini ofa hii ya "Okoa Mapene'' itakuwa kichocheo kikubwa kwa wateja kutumia huduma ya Airtel Money kwa muda wa mienzi mitatu na zaidi"

  Aliongea kwa kusema "Okoa Mapene'' ni njia mojawapo ya kuwazawadia wateja wetu wanaotuma pesa kwa ndugu , jamaa, marafiki, familia na washirika wao wa biashara kupitia huduma ya Airtel Money. "Okoa Mapene'' pia kuwawezesha mawakala kupata kamisheni zaidi kutokana na kuwa na wateja wengi watakaofanya miamala mingi kuanzia sasa.

  Ili kupata kutuma pesa mteja anatakiwa kupiga *150*60# na kuunganishwa kwenye menu ya Airtel Money na kuanza kufanya miamala yake BURE.

  Hiv karibuni Airtel imewazawadia wateja wake kwa kuwapatia gawiwo la faida watumiaji wote wa huduma ya Airtel Money na kuwawekea gawiwo hilo moja kwa moja kwenye akaunti zao za simu.

  0 0

  Ndugu wanahabari leo hii tarehe 12 Novemba 2015 nimekuiteni hapa Kwenye ofisi zetu hapa Mlimani City kwa ajili ya mambo machache.

  Nisingependa kuwapotezea Muda wenu mwingi Maana Sasa tunaongozwa na kauli Mbiu ya Hapa Kazi Tu hivyo ni bora tukae Muda mfupi na kwenda kuchapa Kazi Tu.

  Ndugu wanahabari nimekuiteni kutoa pongezi za dhati na kuunga mkono kasi aliyoanza nayo ndugu Magufuli siyo tu ameonesha kutosha Kwenye Kiti bali amekuwa mtetezi wa wanyonge.

  Ndugu wanahabari Ziara za Ghafla za Ndugu Magufuli siyo za kubezwa Ni za kupongezwa sana. Japo kuna wenye roho mbaya na wasioitakia mema nchi yetu wanabeza maana wao walizoea kubweteka na kufurahia wanyonge wakiteseka.

  Shirikisho la Muziki Tanzania tumeona matunda ya Rais Magufuli juzi amekwenda Muhimbili na Jana tangazo limetoka kuwa mashine za MRI zimeanza Kufanya Kazi hili jambo si la kubezwa hata kidogo bila jitihada binafsi za Ndugu Magufuli leo watanzania wangeendelea kufa na kukata tamaa kwa kukosa matibabu. 

  Ndugu wanahabari haikuwa rahisi kwa wakati Kama huu ambao Ni wa Kupanga serikali mpya bado Rais ametoa Muda wa kwenda kuhakikisha wanyonge wanapata matibabu na huduma tuna pongezi sana Ndugu Magufuli.

  Wembe Ni ule ule aendelee na Ziara hizo za kushtukiza maeneo mengi yana uozo azibe mianya ya wakwepa kodi hasa Kwenye madini ambako tuna Mikatana mibovu iliyoingiwa na wasio na Huruma, wizi na usafirishaji haramu wa madini, Ni Jambo la aibu Tanzanite kwa wingi ipo Kenya na Afrika Kusini na kodi hatukupata ipasavyo na kwingine kwingi Kama Kwenye mbuga za wanyama na utalii ambapo wanyama wanauwawa kwa Faida ya wachache Jambo hili ni la kulivalia njuga na mengine mengi..
   
   Kwa kuziba mianya hiyo na kuleta maendeleo ya wote hakika hatutahitaji misaada ya wazungu.. Tupo tayari kufunga Mkanda kwa miaka hii mitano ili kuacha hazina kwa Taifa letu lenye kila aina ya utajiri.

  Jambo la kumalizia tunamtakia afya tele na tunaahidi ushirikiano kwake Kwenye haki za wanamuziki Kama alivyotuahidi pale Mlimani City vile vile Tunamuombea kwa Mungu apate Baraza la Mawaziri dogo lenye ufanisi na kupunguza mzigo kwa serikali Kama dhamira yake alivyoionesha Kwenye kuondoa safari za Nje vile vile Tunamuombea kwa Mungu asiogope vitisho vya Chura Yeye anywe Maji. Maji Ni kuwaletea maendeleo watanzania.

  Hali hii ya kasi ya Magufuli itawafanya Diasporas wote wakumbuke kuwekeza nyumbani maana Sasa wanajua hazina zao zitakua salama maana mwadilifu anaongoza nchi. Naomba nichukue nafasi hii kuwatoa hofu watanzania waishio ughaibuni kuwa nchi ipo Salama na Dereva wetu kwa Sasa ni Makini kweli kweli.

  Zaidi ya yote ninapongeza wasanii wote walioshiriki Kwenye kampeni za vyama mbali mbali Sasa kampeni zimeisha Ni Muda wa Kufanya Kazi tuwe wamoja.. Rais wetu Ni Magufuli tuvunje Makundi kwani siasa siyo uadui Ni Muda wa kujiletea maendeleo yetu wenyewe!

  Ndugu wanahabari Sasa Tunaandaa Mkutano Mkubwa wa Amani na Maandamano ya kuunga Mkono Hatua za Magufuli kwa kweli tuna Imani naye na tunaamini Mungu atamuwezesha kuyatimiza yote na kukata Kiu ya watanzania.

  Nakutakieni Kazi njema,
  Wenu 
  Addo November Mwasongwe
  Rais Shirikisho la Muziki Tanzania

  0 0


                      (Jovina Bujulu-MAELEZO)
   
  Sekta ya ardhi nchini ni ya kipekee katika uthibiti wa mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwa ndiyo sekta pekee ambapo ndipo uzalishaji na uondoaji wa kaboni hutokea.

  Mfumo wa matumizi mapana ya ardhi ambao siyo endelevu unapaswa ubadilishwe ili nafasi yake ichukuliwe na matumizi ambayo ni sahihi na endelevu zaidi tofauti na hali ilivyokuwa mwanzo. Hatua hiyo ni pamoja na kutumia vyema ardhi iliyopo kwa kupunguza uzalishaji wa gesi joto unaotokana na ardhi.

  Mnamo mwaka 2009, Ubalozi wa Ufalme wa Norway nchini Tanzania ulianza kuwa chachu ya uhifadhili wa miradi saba ya majaribio ya Mkakati wa Kupunguza Ukataji Hovyo  na Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) kwa kutoa dola za Kimarekani zipatazo milioni 100 kufadhili mradi huo.

  Fedha hizo zilipelekwa kwenye taasisi za elimu ya juu nchini ambazo zinajukumu la kuandaa wataalamu mbalimbali.
  Taasisi zilizopata fedha hizo ni pamoja na Chuo Kukuu Cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwa lengo la kuendesha mafunzo na utafiti.

  Fedha nyingine zilipelekwa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, kitivo cha Tathmini ya Rasilimali ambako huko pia waliingia mkataba na Asasi zisizo za Kiserikali (NGO’s) za hapa nchini ili kutekeleza mkakati wa MKUHUMI vijijini.

  Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt Julius Ningu hivi karibuni alibainisha kuwa MKUHUMI ni moja ya maeneo ya utekelezaji wa mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi ambao unalenga kupunguza uzalishaji wa gesi joto katika sekta ya misitu, mkataba huo uliosainiwa katika mkutano uliofanyika nchini Indonesia mwaka 2008.

  “Gesi joto ni mchanganyiko wa gesi mbali mbali zinazozalishwa kutokana na shughuli anazofanya binadamu kama vile viwanda, kilimo, sekta ya usafirishaji, magari, na mitambo inayotoa gesi mbalimbali ambayo hupanda hadi kufikia umbali wa kilometa moja hadi moja na nusu kutoka uso wa dunia na huko hutengeneza utando mzito (tabaka la gesi joto)”, alisema Dkt Ningu.

  Ongezeko la hewa ukaa unasababishwa na uharibifu wa misitu kutokana na shughuli za kilimo cha kuhama hama na upanuzi wa makazi ya watu na miji ambapo maeneo ya misitu yanabadilishwa na kuwa makazi ya watu,  ufugaji huria usio endelevu, uchomaji moto wa misitu unaofanywa kwa makusudi kutokana na mila na desturi pamoja na shughuli za viwanda zinazofanyika katika nchi zinazoendelea.

  Madhumuni ya mkakati MKUHUMI ni kushughulikia masuala ya ardhi, misitu na usimamizi wa kaboni wenye tija kwa namna mbalimbali ikiwamo ushirikishwaji mpana wa wadau katika ngazi mbalimbali.

  Aidha, mkakati huo unalenga kupunguza uzalishaji wa kaboni itokanayo na matumizi ya ardhi kwa kiwango kinachoweza kuhakikiwa na kuzisaidia kaya masikini kuainisha vyanzo mbadala vya kujipatia mapato ambavyo havitegemei  uvunaji wa misitu usio endelevu.

  Ili kuwa na maendeleo endelevu ya nchi, mradi wa MKUKUMI umeainisha malengo mengine ambayo ni kujenga utayari wa wananchi katika shughuli zake nchini, kufanya majaribio ya kisera kupata matokeo ya bora ya MKUHUMI na kuwezesha wadau mazingira kuwa na ushirikiano wenye tija.          
           
  Katika kuimarisha juhudi hizo za kuboresha mazingira na kupunguza hewa ya kaboni, zipo pia Asasi zisizo za kiserikali (NGO’S) zinazotekeleza mradi wa MKUHUMI hapa nchini.

  Asasi hizo ni pamoja na shirika la kimataifa la CARE, Taasisi ya Jane Goodall, mradi  wa kaboni wa shirika la The African Wildlife Foundation, shirika la World Wildlife Foundation na shirika la World Wildlife Fund.

  Asasi nyingine zinazojishughulisha na kupunguza hewa ya kaboni ni Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania, Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA), Shirika la Uhifadhi wa Mpingo na maendeleo na Taasisi ya Wildlife Conservation Society.

  Asasi hizo zinafanya kazi hiyo kupunguza hewa ya kaboni katika maeneo ya Kusini Magharibi mwa Tanzania, Kigoma na Uvinza, wilaya za Lindi, Kigoma, Mpwapwa, Kondoa na Zanzibar.

  Maeneo mengine ambayo miradi ya MKUHUMI inatekelezwa hapa nchini ni zile sehemu yenye aina nyingi za misitu kama vile nyanda za juu milimani, misitu ya miombo kwenye maeneo yenye ukame na maeneo ya maji maji, misitu ya ukanda wa Pwani, mapori ya acacia, na maeneo yenye misitu ya mikoko.

  Akizungumzia suala hilo hivi karibuni jijini Dar-es-Salaam, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula alipokuwa katika mkutano wa wadau wa mazingira uliohusu utekelezaji wa miradi ya majaribio ya MKUHUMI, alisema kuwa Watanzania hawana budi kuzingatia namna bora ya kuhifadhi mazingira, upangaji wa matumizi  bora ya ardhi na utekelezaji wa mipango ili kuleta tija na maendeleo endelevu nchini.

  Naye kiongozi wa miradi ya majaribio ya MKUHUMI ndugu Merja Makela alisema kuwa taasisi yake imesifika kutokana na kutekeleza na kusimamia miradi hiyo kwa makini katika maeneo husika nchini.

  Athari zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi kwenye misitu ni pamoja na hali ya hewa kutofautiana kwa hali mbalimbali ikiwemo urefu wa msimu wa kiangazi au masika ambayo huchangia uharibifu wa uzalishaji mazao, uwepo wa njaa na upotevu wa amani ambapo baadhi ya makabila huingia kwenye mapigano ya kugombea ardhi.

  Mbali na hayo, athari nyingine inayotokana na mabadiliko ya tabia nchi ni pamoja na kuwepo kwa mvua nyingi mfano El nino ambazo husababisha mafuriko, uharibifu wa mali, upotevu wa maisha ya watu na mali zao pia ongezeko la fukuto la joto katika uso wa dunia linasababisha ongezeko la ukame unaoathiri mazingira ambayo ni mahali pao pa makazi.

  MKUHUMI katika kutekeleza majukumu yake imekuwa na faida nyingi zinazopatikana kutokana na miradi hiyo ikiwa ni pamoja na Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania kwa kushirikiana na MJUMITA kuweza kutoa kiwango cha kaboni kilichohakikiwa kwa ajili ya mauzo.

  Aidha, miradi MKUHUMI imeleta manufaa muhimu yasiyo ya kaboni yakijumuisha ongezeko la usalama wa jamii wa kufanya maamuzi juu ya usimamizi wa maliasili zao pamoja na msitu wa Masito Ugalla ulioko mkoani Kigoma wenye ekeri 93,000 uliokuwa umesambaratika ulifanikiwa kurudishwa na wanyamapori walirudi na shughuli za ufugaji ya nyuki ulianzishwa.

  Kiasi cha uzalishaji wa kaboni  kimepunguzwa kwa nchini kutoka tani 39,896  kwa mwaka mmoja kuanzia 2012 katika eneo la Lindi, na tani 27,600 zimepunguzwa kwa mwaka mmoja Kusini Mashariki mwa Tanzania katika misitu 10.

  Manufaa mengine ya mradi huo ni kuwa watu zaidi ya 50,000 nchini wamefikiwa na elimu ya mazingira katika eneo la Kusini Magharibi  mwa Tanzania kupitia mradi wa Taasisi ya Wildlife Conservation Society.

  Aidha, miradi hiyo imewanufaisha wananchi maskini kwa kuhakikisha zinaongeza ufikaji na ufanisi wa shughuli za mazingira zinawafikia kwa usawa  pia kuwepo kwa mgawanyo sawa wa faida za kifedha katika ngazi mbali mbali.

  Miradi hiyo imekuwa na manufaa makubwa ya ziada ya kaboni ikiwemo ulinzi zaidi wa haki za miliki za ardhi na misitu, uboreshaji wa usimamizi wa maliasili, vyanzo vya maji na kupunguza upotevu wa bioanuwai.

  Katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, shirika la mabadiliko ya tabia nchi kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kupitia mkutano wa kimataifa wa 21 uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam ilikubalika kuwa Afrika iwe na kauli moja  ya kuwahamasisha vijana wa jinsia zote  washiriki kutoa maoni na kuchangia  masuala ya mabadiliko ya tabia nchi.

  Katika mkutano huo, Makamu wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilali alisema kuwa  kuna kila dalili ya maeneo ya ukame kuongezeka kwa asilimia 5 hadi 8  barani  Afrika ifikapo mwaka 2080 kutokana na matumizi ya nishati ambayo husababisha joto la dunia kuongezeka kwa asilimia zaidi ya 0.74.

  Miradi ya MKUHUMI inakabiliwa na changamoto mbalimbali zilizojitokeza ikiwa ni pamoja na kiwango cha chini cha uzoefu na uelewa wa taasisi zinazotekeleza au kushughulikia masuala ya mazingira na fikra dhaifu miongoni mwa wananchi, zinazohusisha usimamizi endelevu wa uvunaji wa misitu na ufuatiliaji dhaifu wa matokeo.

  0 0

   Ndugu Julius Pawatila (kulia)akikabidhiwa fomu za kuwania nafasi ya Uspika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni,  Ndugu Mohamed Seif Khatib
    Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni,  Ndugu Mohamed Seif Khatib (kushoto)akimkabidhi fomu za kuwania nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mbunge wa Jimbo la Kongwa Ndugu Job Ndugai.
   Ndugu Simon Rubugu (kulia) akirejesha fomu za kuwania Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa  Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni,  Ndugu Mohamed Seif Khatib.
   Balozi Philip Marmo(kulia) akirejesha fomu za kuwania Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
   Balozi Philip Marmo akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kurejesha fomu ambapo aliwaambia kuwa amejipanga kuendesha bunge kisasa linaloendana na wakati na teknolojia.
  Dr.Tulia Arkson (kulia) akikabidhiwa fomu za kuwania nafasi ya Uspika wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni,  Ndugu Mohamed Seif Khatib
   Ndugu Watson Mwakalila (kulia) akikabidhiwa fomu za kuwania nafasi ya Uspika wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni,  Ndugu Mohamed Seif Khatib
   Dr. Didas Masaburi (kulia)akikabidhiwa fomu za kuwania nafasi ya Uspika wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni,  Ndugu Mohamed Seif Khatib
  Mbunge wa Jimbo la Chato Medadi Majogolo Kalemani (kulia) akikabidhiwa fomu za kuwania nafasi ya Uspika wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni,  Ndugu Mohamed Seif Khatib
   Ritta Mlaki akikabidhiwa fomu za kuwania nafasi ya Uspika wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni,  Ndugu Mohamed Seif Khatib.(Picha na Bashir Nkoromo)
   Veraikunda Urio akikabidhiwa fomu za kuwania nafasi ya Uspika wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni,  Ndugu Mohamed Seif Khatib (Picha na Bashir Nkoromo)

  Haya ndio majina ya waliochukua fomu leo;

  Ndugu Julius Pawatila
  Ndugu Job Ndugai
  Dk. Tulia Arkson
  Dk. Medadi Majogolo Kalemani
  Dk. Didas Masaburi
  Ritta Mlaki
  Veraikunda Urio

older | 1 | .... | 683 | 684 | (Page 685) | 686 | 687 | .... | 1896 | newer