Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 682 | 683 | (Page 684) | 685 | 686 | .... | 1904 | newer

  0 0

  Serikali inapenda kuzitaarifu ofisi za umma  na  wananchi  kwa ujumla  kwamba  imesitisha    matumizi  ya  picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  wa Serikali ya Awamu ya Tano, Mhe.Dkt. John  Pombe Josep Magufuli mpaka hapo itakapotangazwa tena.

  Awali   majira ya saa 6: 00 mchana leo Novemba 6, mwaka huu Serikali ilitangaza kuhusu kuanza rasmi kwa matumizi ya picha ya Rais.


  Aidha,   Serikali  imesema kwamba  itazitangazia  ofisi hizo na umma wa Watanzania  kuhusu kuanza tena  kwa  matumizi ya picha  hiyo hapo baadae.

  Imetolewa na
  IDARA YA HABARI.
  Novemba 6,mwaka 2015

  0 0

  po2
  Rais Dkt.John Pombe Magufuli akimkaribisha na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chama Tawala Cha China Mhe.Zhang Ping ikulu jijini Dar es Salaam leo.Bwana Zhang alimwakilisha Rais wa China katika sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano(picha na Freddy Maro). 
  po3
  Rais Dkt.John Pombe Magufuli akipiga picha  na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chama Tawala Cha China Mhe.Zhang Ping ikulu jijini Dar es Salaam leo.Bwana Zhang alimwakilisha Rais wa China katika sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania Mh.  Lu Youqing  na kushoto ni  Mh.Balozi  Abdulrahman Shimbo Balozi wa Tanzania nchini China (picha na Freddy Maro). 
  po4

  Rais Dkt.John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chama Tawala Cha China Mhe.Zhang Ping ikulu jijini Dar es Salaam leo

  0 0

  IMG-20151104-WA0027
  To cast your vote click this link www.abryanzstyleandfashionawards.com/vote

  0 0
 • 11/06/15--12:48: MTO MSIMBAZI WASAFISHWA
 •  Mhandisi wa  Kampuni  ya Chico, David Waruma  akizungumza leo jijini Dar es Salaam juu ya kazi ya kusafisha na kuzibua daraja la Mto Msimbazi eneo la Jangwani  kuzuia na kukomesha mafuriko yanayotokea  kipindi cha mvua ambayo huleta  athari kwa jamii inayozunguka pamoja  na kulinda Kituo cha Mabasi yaendayo Haraka (BRT) cha Jangwani  (Jangwani Depot),  kisiathirike na Mafuriko endapo  yatatokea .
   Mafundi wakiendelea na  kusafisha Daraja la Mto Msimbazi wakiongonzawa na  .Mhandisi wa  Kampuni  ya Chico, David Waruma leo jijini Dar es Salaam.
   Vifaa maalum kwa aajili ya  kusafisha daraja la Mto Msimbazi jijini Dar es Salaam.
   Wananchi wakitazama  daraja la Mto Msimbazi leo jijini Dar es Salaam.
  Muonekano wa Mto Msimbazi leo jijini Dar es Salaam wakati ukiendelea kusafishwa.Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.

  0 0


   Mwenyekiti wa Jumuiko la Maliasili nchini (TNRF) ,Dr.Suma Kaare akizungumza katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
    Mkurugenzi wa Shirika la Haki kazi Catalyst Alais Moridant akifafanua jambo  katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini
  Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
  wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
    Mkurugenzi wa Shirika la AWF ,John Salehe
  akifafanua jambo  katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini
  Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
  wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
    Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini
  Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
  wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
    Viongozi mbalimbali wa jumuiko la maliasili wakiwa katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijiniArusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
  Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini
  Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
  wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel 
  Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini
  Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
  wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel 

  Mwakilishi wa Shirika la WWF ,Sware Semesi  akizungumza katika  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini
  Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
  wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel 
   Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini
  Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
  wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel.
   Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini
  Arusha wakiwa katika picha ya pamoja, ,mkutano huo ulihudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
  wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel

  Wasemaji Wakuu wa   mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini
  Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
  wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel 
  Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog ,Arusha.
  Mwenyekiti
  wa Jumuiko la Maliasili nchini Dr.Suma Kaare amemtaka Raisi John Pombe Magufuli
  adhibiti upotevu wa mali asili za wanyama pori na misitu uliokithiri katika
  maeneo mengi nchini ili kunusuru uhai wa maliasili.
  Suma Kaare
  amesema  hayo katika mkutano wa 7 wa
  jumuiko la maliasili  unaoendelea jijini
  Arusha,Kaare amesema kuwa jukwaa hilo litashirikiana na Rais huyo katika  kuhakikisha kuwa maliasili zinalindwa na
  kuwanufaisha Watanzania kwa kiwango stahiki.
  “Tunajua
  Rais wetu mpya ana kazi  kubwa  ya kulinda maliasili za nchi hii kama ilivyo
  kauli mbiu yake ya “kazi tu” tunaamini atazuia upotevu mkubwa wa rasilimali
  unaofanywa na watendaji wasio waaminifu” Alisema Kaare
  Mratibu wa
  Masuala ya misitu katika shirika la uhifadhi wa maliasili na Mazingira (wwf)
  ,Isaac Malungu amesema kuwa asilimia 90% ya nishati inayotumika nchini
  inatokana na kuni pamoja na mkaa hali ambayo inaathiri misitu na kutishia uhai
  wa maliasili nchini hivyo ameitaka serikali ihimize matumizi ya nishati mbadala
  ili kunusuru mazingira yanaoharibiwa kila kukicha.
  Malungu alisema
  kuwa kilimo cha kuhama hama pamoja na ukataji miti ovyo umekua ukisababisha
  uharibifu wa mazingira na hata kupelekea hecta laki 4 za misitu kupotea kila
  mwaka kutokana na shughuli hizo.
  Mkurugenzi
  wa  Shirika la AWF,John Salehe Alisema
  kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yamesababisha hali ya ukame inayowaathiri
  wanyama pamoja na mimea hivyo kuathiri uhifadhi kwa ujumla .
  Salehe
  alisema kuwa juhudi zaidi zinapaswa kuchukuliwa ikiwemo upandaji wa miti pamoja
  na kutunza misitu ili kurejesha uoto wa asili uliopotea.

  0 0

  Mwenyekiti wa Timu ya Boko Beach Veterans (BBV), Danny Ole a.k.a Aguero (wa nne toka kushoto) akimkabidhi zawadi ya mpira Mchezaji bora wa Mwezi Oktoba, Henry Horombe (wa nne toka kulia), baada ya kuonyesha kiwango kizuri kwa kipindi chote cha mwezi mwezi huo 2015. Zawadi hizo hutolewa na mdau mkubwa wa soka nchini na mmiliki wa maduka ya Zizzou Fashion, Othman Tippo Shaaban ambaye nae ni mwanachama wa timu hiyo.
  Sehemu ya wachezaji wa Timu ya Boko Beach Veterans (BBV) wakimpongeza mchezaji mwanzao aliebuka kidedea na kutwaa taji la Mchezaji bora wa Mwezi Oktoba, Henry Horombe (katikati) mara baada ya mtangango uliopigwa mapema leo asubuhu katika uwanja wa Boko.
   Timu ya Boko Beach Veterans (BBV) ikiwa imegawanyika katika mchezo wa mazoezi mapema leo asubuhi.


  0 0


   
   Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
    Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
   Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
   Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bwana Rished Bade na  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
   Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Katibu Mkuu Utumishi Mhe HAB Mkwizu  na  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
   Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
   Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
   Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
   Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
   Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju na  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
  Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  katika picha ya pamoja Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
  PICHA NA IKUL

  0 0


       Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo asubuhi katika Ikulu ya Dar es Salaam  amefanya kikao na Makatibu wakuu, Manaibu Makatibu wakuu, Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  ili kutoa uelekeo wa Serikali anayoitaka  mara baada ya  kuapishwa.
       “Nataka Serikali iendelee kwa nguvu zote na katika kutekeleza dhana ya ‘HAPA KAZI TU’ na viongozi kuzingatia na kukumbuka ahadi nilizotoa ili zianze kuonekana na kufanyiwa kazi mara moja” Rais Magufuli amesema.
       Katika Kikao chake, Rais ametoa mwongozo na kusisitizia kuwa ni lazima kila mtendaji Serikalini kuuzingatia, kufuata sheria na taratibu ili taifa lisonge mbele kwa ufanisi zaidi.
       Katika kikao hicho Rais ameelekeza mambo kadhaa ambayo watendaji hao wanapaswa kuyasimamia, kuyawekea mikakati na kuyapanga vizuri ili atakapo teua Baraza lake la Mawaziri mambo hayo yawe tayari ili Mawaziri watakaoteuliwa waweze kuyasimamia bila kukosa.
       Mambo hayo muhimu ni kama ifuatavyo:
  Kuanzia mwezi  Januari mwaka 2016, wanafunzi wote wanaoanza shule watasoma bure bila kulipa ada, Katika jambo hili, Rais amewataka watendaji kuanza kuliwekea mikakati tayari kwa utekelezaji
  Suala la mikopo ya wanafunzi nalo lifanyiwe kazi na mipango yake ikamilike kwa ajili ya utekelezaji mzuri zaidi
  Amefuta safari zote za nje ya nchi kuanzia leo hadi hapo atakapolitolea suala hilo maamuzi mengine na kueleza kuwa shughuli zote zinazotakiwa kufanywa nje ya nchi zifanywe na kusimamiwa  na mabalozi wa Tanzania  wanaowakilisha nchi  huko nje.

  Pengine patokee jambo la dharura sana na hata hilo lazima kibali kitolewe na Rais au Katibu Mkuu Kiongozi. Badala yake Rais amewataka watendaji hao kufanya zaidi ziara za kwenda vijijini ili kuzijua na kutatua kero za wananchi wa Tanzania.
       Katika Kikao hicho, Rais amemtaka Kamishna wa TRA, Ndugu Rished Bade kusimamia kwa makini zoezi la ukusanyaji wa mapato nchini na kuhakikisha kero ndogo ndogo kwa wananchi lianze kutekelezwa kama alivyo ahidi kwa  kufanyiwa  kazi mapema  zaidi.
       Rais ameitaka TRA kukusanya mapato hayo kutoka kwa wafanya biashara wakubwa zaidi na wale wanaokwepa kodi bila kuogopa mtu wala taasisi yoyote hapa Tanzania na kusisitiza kuwa katika Serikali hii wa kutoa maamuzi vinginevyo zaidi ya haya ni yeye Rais  ama Makamu wake.
       Rais Magufuli pia ameagiza usimamizi katika suala la manunuzi ambalo limekuwa likitumika vibaya na kuwa mwanya wa kuibia Serikali  kwa watu kuongeza bei ya vitu hata kama ni vya bei ndogo kabisa katika jamii.
       “Ikitokea suala hilo likagundulika kwa watu kuongeza bei ya vitu, watendaji watawajibishwa mara moja”. Rais amesema, na kuwataka watendaji hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo na kuzingatia maadili mema ya kazi.

  ………………………MWISHO……………………
  Imetolewa na Premi Kibanga,
  Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.

  7 Novemba, 2015

  0 0

  New PictureNational Arts Council BASATA
  Wasanii nchini wametakiwa kuwa mstari wa mbele kuhamasika na kushiriki kikamilifu kwenye maazimisho ya Siku ya Msanii maarufu kama Msanii Day ambayo yanatazamiwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu wa 2015 jijini Dar es Salaam na maeneo mbalimbali nchini.
   Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye programu maalum ya kujadili ushiriki wa wasanii kwenye siku hii muhimu kwao marais wa mashirikisho ya wasanii nchini walisema kwamba wakati umefika kwa wasanii wote nchini kuamka na kuwa mstari wa mbele kutambua maazimisho haya ya siku yao kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakitumiwa katika kuazimisha vilele vya tasnia zingine.
   “Tumekuwa tukitumika sana sisi Wasanii kung’alisha na kuzifanya kazi za wengine kuwa na mafanikio, tumekuwa tukihamasisha kazi za wengine. Hii siku ya Msanii ni yetu, tuamke, tuibebe zaidi ya tunavyofanya kwenye kazi za wengine. Tuungane tuifanye siku hii yenye tija” alisisitiza Symon Mwakifamba ambaye ni Rais wa shirikisho la Sanaa za Filamu nchini.Aliongeza kusema kwamba, Wasanii wana nguvu na mchango mkubwa katika jamii na kwamba kwa idadi yao wanatosha kabisa kuwa na uwakilishi katika maeneo mbalimbali ya maamuzi ili kuhakikisha hawaachwi nyuma.
   “Naomba wasanii wote tuitumie siku ya Msanii kuonesha nguvu yetu, tuwaoneshe na tutume ujumbe kwa viongozi kwamba kundi hili ni kubwa na muhimu katika kujenga Taifa lenye ustawi” Aliongeza Mwakifamba.
   Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Adrian Nyangamale alisema kwamba siku ya msanii ni mahsusi kwa ajili ya wasanii wote nchini na kwamba kama ilivyo kwa maadhimisho ya siku zingine kama za walemavu, wanawake, wanasheria na nyinginezo wasanii nao hawana budi kuhakikisha wanaifanya siku hii kuwa yenye kufana na mafanikio makubwa.
   “Hauwezi kuizungumzia siku ya Msanii bila kuwataja na kuwahusisha wasanii moja kwa moja. Wasanii lazima tujiunge pamoja na tushirikiane kwa dhati ili kuifanikisha siku hii” Alisisitiza Nyangamale.
   Awali viongozi wa mashirikisho ya Wasanii nchini Msule Jumanne (Sanaa za Ufundi), Samwel Mbwana (Sanaa za Muziki), Dennis Mango (Sanaa za Maonesho) na Biko wa Sanaa za Filamu walieleza namna wasanii walivyojipanga kushiriki siku hiyo na kusisitiza kwamba kila msanii nchini ajisikie furaha na heshima kushiriki siku hii muhimu kwao.
   Siku ya msanii Tanzania inatarajiwa kuanza kuazimishwa kwa shamrashamra mbalimbali yakiwemo maonesho ya kazi za wasanii, semina na makongamano ya kujadili mustakabali wa sekta hiyo nchini kuanzia tarehe 7-11 Desemba mwaka 2015 na baadaye kilele chake tarehe 12 Desemba mwaka 2015 kwenye Ukumbi wa Blue Pearl uliko jengo la Ubungo Plaza Ubungo jijini Dar es Salaam.
  IMETOLEWA NA KITENDO CHA HABARI NA MAWASILIANO, BASATA

  0 0
 • 11/07/15--23:04: PONGEZI


 • 0 0
  0 0

  Katika juhudu zake za kuhakikisha watanzania waishio mjini na vijiji wanapata huduma bora za mawasiliano , kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua mnara wa mawasiliano katika kata ya mazinde wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga.

  Uzinduzi huo wa mnara wa mawasiliano utawahakikishia wakazi wa Mazinde na vijiji vya jirani mawasiliano ya uhakika katika kuendesha shughuli zao za kijamii na kiuchumi kila siku ikiwemo kilimo cha katani.

  Akiongea wakati wa uzinduzi, Mkuu wa wilaya ya Korogwe, Hafsa Mtasiwa alisema" tunafurahi kuwa na mnara huu wa mawasiliano kwaajili ya wakazi wa wilaya ya mazinde ambao utasaidia kukuza biashara zao na kuinua utandawazi kupitia simu zao za mkononi".

  Aliongeza kwa kusema" mawasiliano ndio chachu ya maendeleo ya uchumi wa jamii na ulimwengu kwa ujumla. na nimatumaini yetu kuwa huduma hii inayozinduliwa hapa leo itachangia kwa kiasi kikubwa endeshaji wa mashamba ya katani, kilimo, biashara mbalimbali na pia kuchagia katika kubadilisha maisha ya wengi na kwa hilo tunapenda kuwashukuru sana Airtel ".

  Kwa upande wake, Meneja mauzo wa kanda ya kaskazini, Aluta kweka amesema kampuni yake iko mstari wa mbele katika kuhakikisha inatoa huduma za mawasiliano za uhakika zitakazorahisisha ukuaji wa uchumi na pato la taifa.

  " katika ulimwengu wa leo wa sayansi na technologia watanzania wanatakiwa kuwezesha ili kupata fulsa zitokanazo na huduma bora za mawasiliano. Tunaamini mnara huu hautawahakikishia wakazi wa hapa mawasiliano ya uhakika tu bali utachangia kwa kiasi kikibwa katika kuongeza pato la taifa kwa ujumla".

  Kufatia uzinduzi huo, zaidi ya wakazi takribani 10,000 na vijiji vitatu vitafaidika na bidhaa na huduma mbalimbali ikiwemo , huduma za intaneti, Airtel money, yatosha na nyingine nyingi
  Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Hafsa Mtasiwa (wa pili kulia)) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mnara wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Kata ya Mazinde wilaya ya Korogwe mkoani Tanga. anayeshuhudia kushoto ni Meneja wa Kampuni ya Simu ya Airtel Kanda ya Kaskazini Aluta Kweka.

  0 0

   Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo imemtangaza bwana Benoit Janin kuwa Mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo.
  Bwana Janin anachukua nafasi ya Pratap Ghose ambaye ameiongoza kampuni hiyo kwa muda wa miaka mitatu.
  Uteuzi wa Janin unafatia kampuni ya Millicom kununua hisa za kampuni ya Zantel ambapo sasa itashirikiana na serikali ya Zanzibar kuhakikisha kampuni ya Zantel inakua na inaboresha huduma zake.
  Benoit, ambaye ana uzoefu wa zaidi ya miaka 16 katika sekta ya mawasiliano katika nchi za Afrika na masoko yanayokua, alikuwa Mkurugenzi wa kampuni ya Tigo nchini Chad kwa muda wa miaka mitatu, ambapo aliiwezesha kuwa kampuni namba moja nchini humo.

  Kabla ya kujiunga na Millicom, Benoit amefanya kazi na kampuni ya mawasiliano ya Vimpelcom kama Mkugenzi wa Biashara nchini Cambodia, huku pia akiwa ameshikilia nafasi mbalimbali za kiuongozi katika kampuni ya Orange.

  Akizungumzia majukumu yake mapya, Benoit alisema anatarajia kushirikiana na wafanyakazi wa Zantel katika kuhakikisha kampuni inakua na kufikia malengo yake.‘Nina furaha kubwa kujiunga na kampuni ya Zantel na ninatarajia kushirikiana na wafanyakazi wenzangu kuongeza idadi ya wateja, pamoja na kusimamia ukuaji wa kampuni kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato’ alisema Benoit.

  Kama sehemu ya majukumu yake mapya, Bwana Janin ataboresha huduma za mtandao za Zantel pamoja na kuzindua huduma za 4G hapo mwakani

  0 0

   Washiriki wa shindano la Bongo style kwa upande wa picha wakimsikiliza kwa makini mtaalam wao Sameer Kermalli(wa tatu kulia) akitoa maelekezo wakati wa mafunzo hayo.
   Baadhi ya washiriki kwa upande wa picha wakiwa wanasikiliza kwa makini somo
  Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa FASDO, Tedvan Chande akiwa na washiriki wa shindano la Bongo Style ambao hawapo pichani , akiwa na Mratibu wa FASDO Tanzania Joyce Msigwa alipofika kuwatembelea na kuongea nao machache.
  Baadhi ya  Washiriki kwa upande wa Ubunifu wa mavazi wakiwa wanachakalika kuandaa kazi zao mbalimbali.


  Mbunifu wa Mavazi Martini Kadinda akiwapa somo washiriki upande wa ubunifu wa mavazi.
    Washiriki  wa ubunifu wa mavazi wakiendelea na kazi
  Hawa ni washiriki kwa upande wa kupiga picha wakikamilisha moja ya mazoezi waliyopewa(Picha kwa hisani ya Washiriki upande wa wapiga picha)
   Baadhi ya Washiriki upande wa kupiga picha wakiwa mtaani wakiwa katika mazoezi waliyopewa kuyafanya na mtaalam wao Sameer Kermalli
   Baadhi ya washiriki wengine kwa upande wa Kupiga picha  na ubunifu wa  mavazi wakisikiliza kwa makini somo ambalo linatolewa na mtaalam ambaye hayupo pichani.
   Baadhi ya washiriki upande wa Ubunifu wa mavazi wakiwa wanasikiliza kwa makini maelekezo wanayopewa na Mbunifu wa Mavazi Martin Kadinda ambaye hayupo pichani
   Muda wa mapumziko 
   Muwezeshaji kutoka Wiki Loves Africa akitoa somo juu ya upigaji picha kwa washiriki ambao hawapo pichani.
   Tunukiwa Daudi (Aliyesimama) akitoa somo juu ya matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii na Faida zake
  Baadhi ya washiriki upande wa kupiga picha wakifurahia jambo

  Ikiwa ni siku ya tano tangu Washiriki 20 wa Shindano la Bongo Style linalo andaliwa na asasi isiyo ya Kiserikali ya Faru Arts and Sport   Development Organization (FASDO), ikiwahusha Wapiga picha na wabunifu wa mavazi wenye umri kati 19-25 walioingia rasmi kambini tarehe  5.11.2015,ambapo tangu tarehe hiyo  washiriki hao  wameendelea kujifua zaidi huku wakipewa kazi mbalimbali za ubunifu na masomo mengine ikiwa ni sehemu ya shindano hilo. Wakiwa kambini washiriki hao wamepata nafasi ya kujifunza mambo mapya ambayo walikuwa hawayafahamu.

  Fainali hizi zinatarajiwa kufanyika tarehe 27.11.2015 ndani ya ukumbi wa 
  Alliance Francaise Jijini  Dar es Salaam.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti washiriki wa upande wa picha wamekili kuwa walikuwa wanaona kama wanafahamu vema kupiga picha lakini baada ya kupata somo wamegundua kuwa kuna mambo mengi ambayo walikuwa hawayafahamu na mengine walikuwa wanayafanya lakini bila kujua kuwa walikuwa sahihi, Pia waliongeza kuwa wanashukuru kuwapata wataalam ambao wameweza kuwaonesha ni jinsi gani wanatakiwa kuwa wapiga picha wazuri.

  Nao washiriki wa ubunifu wa mavazi wameshukuru kupata wataalam ambao wamekuwa wakiwapa maelekezo mengi ambayo  yalikuwa ni chachu kwao kwasababu kila mmoja kwa upande wake wamejifunza mambo mapya mengi na kuona kuwa kumbe sio lazima kuwa na ubunifu wa aina moja ya mavazi lakini wanaweza wakawa na aina nyengine nyingi kulingana na mazingira waliyopo na kuishukuru Fasdo kwa kuwakutanisha.

  Mwalimu na mtaalam wa kupiga picha Sameer Kermalli amekili kuwa tangu darasa lianze washiriki hao wamekuwa na uelewa wa haraka na yeye kupata nafasi ya  kuwaelekeza mbinu mbalimbali za kupiga picha na kanuni mbambali za upigaji picha, washiriki hao wamekuwa wasikivu na wameongeza ubunifu zaidi jambo ambalo limemtia moyo mtaalam huyo.

  Kwa upande wa Mbunifu wa mavazi Martin kadinda alisema kuwa washiriki wapo vizuri na kila mbunifu anakitu chake cha kipekee ambacho yeye anafanya mfano wapo wale ambao wanabuni nguo zao kwa kutumia kitenge tu, wengine wanatumia vitu vya asili, nguo za kisasa, nguo ambazo zipo tayari kwa ajili ya kuvaliwa na zenginezo, aliwashauri kuwa wasiegemee katika kitu kimoja tuu au aina moja ya mavazi lakini wawe na ubunifu na kubadilika kila wakati kwa sababu mitindo inakwenda ikibadirika.
    
   Mkurugenzi Mtendaji wa FASDO, Tedvan Chande  alipata nafasi ya kutembelea kambini na kujionea jinsi washiriki wanavyojituma katika kazi zao na maandalizi ya shindano hilo yanavyo kwenda " Ninachukua nafasi hii kwa niaba ya Fasdo kuwapongeza washiriki wote mliofanikiwa kuingia katika shindano hili la Bongo style ikiwa lengo ni kuwajengea uwezo zaidi wa kile ambacho mlikuwa mnafanya na sasa kipate kuwa zaidi" aliongea Chande na kuongeza kuwa kuna ushindani mkubwa na shindano linafuata vigezo vyote vya ushindani na washindi watakuwa wamekidhi vigezo hivyo.

  0 0  0 0

  DSC_1032

  Mwanamuziki nguli wa dansi kutoka DRC Congo, Papaa Wemba kushoto akiimba na kucheza sambamba na madansa wake jukwaani usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la muzuki la Karibu Music Festival msimu wa pili linaloendelea katika viwanja vya Mwanakalenge,mjini Bagamoyo. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).

  Na Andrew Chale,Modewjiblog
  [BAGAMOYO-TANZANIA] Mwanamuziki kutoka Congo mwenye makazi yake nchini Ufaransa, Papaa Wemba, ameweza kuonyesha ukomavu wake kwenye muziki wa dansi licha ya kuwa na uri wa miaka 66, kwa kupiga shoo ya aina yake usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Karibu Music Festival 2015 linaloendelea ndani ya viwanja vya Mwanakalenge, Bagamoyo-Tanzania.

  Katika shoo hiyo, Papaa Wemba aliweza kupanda jukwaani akiwa na bendi yake na kupiga nyimbo zaidi ya tano zilizokonga nyoyo mashabiki lukuki waliofurika ndani ya viwanja hivyo vya Mwanakalenge mjini hapa.

  Papaa Wemba ambaye anatamba kwa muda mrefu na wimbo wa “Show Me The Way” ameweza kuwa miongoni mwa wasanii wa muziki wa dansi kutoka DRC Congo kufika Tanzania kwa mara ya pili sasa kwa vipindi tofauti huku watanzania wengi wakionyesha kumkubali na kufuatilia muziki wake mara kwa mara.

  Baada ya shoo hiyo Papaa Wemba aliwashukuru Watanzania kwa kujitokeza kwa wingi na kumuunga mkono katika muziki wake ambapo alieleza kuwa tamasha hilo la Karibu Music Festival licha ya kuwa change kwa kufanyika mwaka wa pili, huko linakoelekea litakuwa kubwa zaidi na kuwa maarufu.

  Katika shoo hiyo, Papaa Wemba aliimba nyimbo zaidi ya nne huku akiimba pia vibao kadhaa vilivyowahi kutamba miaka ya nyuma pamoja na nyimbo mbalimbali zikiwemo mpya.

  Tamasha hilo ambalo leo Novemba 8.2015, linatarajiwa kufikia tamati, linaratibiwa na Karibu Cultural Promotions Organization (KCPO) na Legendary Music Entertainment and Promotions Co. Ltd, T kwa kushirikiana na kampuni ya kinywaji cha Jebel Coconut. Wadhaminiwa wengine ni pamoja na Swiss Embassy, Precision Air, Coca Cola, Mwananchi Communication, Kaya fm, Magic fm, Focus Outdoor, Jovago, Kaymu na Time tickets.
  DSC_1025
  Papaa Wemba akiimba jukwaani kwenye tamasha la Karibu Music Festival 2015, usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Mwanakalenge, mjini Bagamoyo
  DSC_1099
  Papaa Wemba akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani ) kwenye tamasha la Karibu Music Festival 2015, usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Mwanakalenge, mjini Bagamoyo
  DSC_1027
  Wanenguaji wa Papaa Wemba wakishambulia jukwaa kwa style ya aina yake ambao walikuwa kivutio katika tamasha hilo..
  DSC_1083
  Sebene likiendelea jukwaani..
  DSC_1102
  Host wa tamasha la Karibu Music Festival 2015, Mc Lulu akipata kuimbisha mashabiki waliofurika katika tamasha hilo kwa kuimba sambamba na Papaa Wemba (Hayupo pichani) kibao cha "Show Me the way"..
  DSC_1087
  Papaa Wemba katika ubora wake..
  DSC_1130
  DSC_1030
  Dansa akifanya yake jukwaani..
  DSC_1063
  DSC_1080
  Papaa Wemba..
  DSC_1090
  Mwenyekiti wa tamasha la Karibu Music Festival, Amarido Charles (kushoto) akiwa pamoja na mwanamuziki kutoka Afrika Kusini, Bodenim 'Bo' katika viunga vya tamasha hilo viwanja vya Mwanakalenge..

  0 0

  BONDIA Ibrahimu Tamba anapanda tena uringoni Novemba 22 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam kugombania mkanda wa ubingwa na bondia Baraka Mwakansope  kutoka Mbeya  kg 73 mpambano uho wa raundi kumi.

  unatalajiwa kuwa wa kisasi baada ya mara ya kwanza Tamba kumsambalatisha bondia Maisha Samsoni wa uko uko Mbeya hivyo mwakansope amekuja kwa ajili ya kulipiza kisasi cha kupigwa kwa mwenzake mpambano uliofanyika mwanzoni mwa mwaka huu

  mratibu wa mpambano uho Jaffar Ndame ameongeza kwa kusema kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mawili ya ubingwa ambapo bondia Julius Kisalawe atapambana na Ramadhani Kumbele kg 51 ubingwa wa Taifa mpambano wa raundi kumi

  mpambano mwingine utawakutanisha bondia Pius Kazaula wa Morogoro atakaepambana na Abdallah Luwanje wakati bondia chipkizi kutoka Super D Boxing Promotion Vicent Mbilinyi atakabiliana na Said Tampoo kutoka bagamoyo

  aliongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya mabondia chipkizi  mbali mbali pia kutakuwa na burudani za kutosha hivyo kawaomba wapenzi na mashabiki wa mchezo wa masumbwi kuwai ukumbini kwa michezo itanza rasmi kuanzia saa 11 jioni na kumalizika mnamo saa tano kasoro usiku.
   
  Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile.Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
  pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha.

  0 0

  DSC_0896

  Msanii nyota wa Afrika Kusini, Bo Denim "Bo" akitumbuiza jukwaani wakati wa tamasha la msimu wa pili la Karibu Music Festival..!

  Na Andrew Chale, Modewjiblog
  [BAGAMOYO-TANZANIA] Mwanamuziki nyota kutoka Afrika Kusini Bo Denim maarufu ‘Bo’ amewashukuru waandaji wa tamasha la Music Festival linalofanyika kila mwaka mjini hapa huku likihusisha vikundi na wanamuziki mbalimbali kutoka mataifaa tofauti ya Afrika nan je ya Afrikaa.

  Bo ambaye usiku wa jana Novemba 7, aliweza kupiga shoo hiyo kwa kiwango cha Kimataifa, alipata shangwe kwa mashabiki waliofurika kushuhudia tamasha hilo mjini hapa.

  Baada ya shoo hiyo Modewji ilipata kufanya naye mahojiano ambapo amepongeza muziki wa Tanzania wakiwemo wasanii wanaovuma nje ya mipaka ya Tanzania. “Wasanii wa Tanzania wanauwezo mkubwa. Nimeshuhudia kundi la Weusi wamefanya vizuri sana” ameeleza Bo.

  Tamasha hilo ambalo leo Novemba 8.2015, linatarajiwa kufikia tamati, linaratibiwa na Karibu Cultural Promotions Organization (KCPO) na Legendary Music Entertainment and Promotions Co. Ltd, T kwa kushirikiana na kampuni ya kinywaji cha Jebel Coconut. Wadhaminiwa wengine ni pamoja na Swiss Embassy, Precision Air, Coca Cola, Mwananchi Communication, Kaya fm, Magic fm, Focus Outdoor, Jovago, Kaymu na Time tickets.
  DSC_0882
  DSC_0858
  DSC_0848
  DSC_0843
  DSC_0835
  Bo akipagawisha mashabiki ...

  DSC_0852
  DSC_0884
  DSC_0890
  Mambo yalikuwa hivi ..
  DSC_0884
  DSC_0910
  Host wa Karibu Music Festival 2015, Jazzphaa Nassor na Lulu wakishoo love wakati wa shoo hiyo ya "Bo"..

  0 0

                                  Ndugu Dickson anayefahamika kwa wengi kama  Mr "DMK "
  Promoter "DMK" wa Kampuni ya DMK GLOBAL PROMOTIONS ashinda Tuzo ya Best Promoter USA katika zile tuzo za AFRICAN ENTERTAINMENT AWARDS USA 2015 ,Tuzo hizo zilitolewa OCTOBER 31 New York ambapo Makampuni 6 yalikuwa yakichuana kipengele hicho na DMK Global kuibuka kidedea,Pia katika Awards hizo Wasanii kutoka Tanzania Diamond alichukua Tuzo ya Hottest Male Single na Ommy Dimpoz tuzo ya People's Choice .

      Kampuni hii inafanya Shuguli zake Marekani za kuandaa Events mbali mbali za burudani kama CLUB EVENT,CONCERTS, CARNIVALS  ikiwa ni pamoja na kuleta wasanii Marekani kutoka Tanzania na Africa kwa ujumla,pia inafanya matamasha ya Burudani na wasanii wa Marekani pia.Baada ya Tuzo hizi Tulimpigia simu bwana DMK na kumpongeza kwa kuiwakilisha vyema Tanzania na East Africa kwa ujumla ambapo aliwashukuru sana waliompigia kura kote Duniani na kuongezea kuwa Tuzo hii ameipata yeye lakini angependa ijulikanekuwa shughuli hizi huwa anazifanya kwa kusaidiana na Partners wake kampuni za Safari Entertainment na J&P Ent ambazo amesema kuwa bila wao kushurikiana nao asingekuwa hapo alipo.

       Bwana DMK amesema tutegemee Mambo makubwa mengi kutoka kwake na Partners wake hivi Karibuni.

  0 0


  SU1

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akihutubia wakati wa hafla maalumu ya kuliombea Taifa Amani, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani,iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam jana Nov 7, 2015. Picha na OMR
  SU2
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Agape Television Network (ATN) Dkt. Anny Fernandes, wakati wa  hafla maalumu ya kuliombea Taifa Amani, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani,iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam jana Nov 7, 2015. Picha na OMR
  SU3
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Agape Television Network (ATN) Dkt. Anny Fernandes, wakati wa  hafla maalumu ya kuliombea Taifa Amani, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani,iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam jana Nov 7, 2015. Picha na OMR
  SU4
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik, akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jana. Picha na OMR
  SU5
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akiagana na baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla ya kuliombea Taifa amani wakati akiondoka ukumbini baada ya kuhutubia katika hafla maalumu ya kuliombea Taifa Amani, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani,iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam jana Nov 7, 2015. Picha na OMR
  SU6 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akishiriki dua ya pamoja na baadhi ya viongozi, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani Tanzania, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jana Nov 7 2015. Picha na OMR
  SU8
  Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa, akizungumza wakati wa hafla hiyo, alipokuwa akiomba dua maalumu. Picha na OMR
  SU9
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla ya kuliombea Taifa amani wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee kwa ajili ya kuhudhuria hafla maalumu ya kuliombea Taifa Amani, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani, jijini Dar es Salaam jana Nov 7, 2015. Picha na OMR
  SU10
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Kamanda Suleiman Kova, wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee kwa ajili ya kuhudhuria hafla maalumu ya kuliombea Taifa Amani, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani, jijini Dar es Salaam jana Nov 7, 2015. Picha na OMR
  SU11
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Libelata Mulamula, wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee kwa ajili ya kuhudhuria hafla maalumu ya kuliombea Taifa Amani, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani, jijini Dar es Salaam jana Nov 7, 2015. Picha na OMR
  SU12
  Baadhi ya viongozi wakiwasili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee
  SU13
  Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Taifa Bara, Philip Mangula akiteta jambo na aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha TLP, Maximillian Lymo, wakati walipokuwa kwenye hafla maalumu ya kuliombea Taifa Amani, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani, jijini Dar es Salaam jana Nov 7, 2015. Picha na OMR
  SU14
  Sheikh Alhad Mussa, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa dini ukumbini humo.

older | 1 | .... | 682 | 683 | (Page 684) | 685 | 686 | .... | 1904 | newer