Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

MULTICHOICE TANZANIA WAMTANGAZA RASMI DIAMOND PLATNUMZ KUWA 'OFFICIAL DSTV BRAND AMBASSADOR'

$
0
0
DSC_0168
Mwanamuiki nyota nchini Tanzania, Nassib Abdul ama Diamond Platnumz akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani). (Picha na Andrew Chale, Modewjiblog).

Na Adndrew Chale, Modewji.

KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania mapema jana imezindua ofa kabambe za msimu wa siku kuu huku ikimtambulisha rasmi Mwanamuziki Diamond Platnumz kuwa balozi maalum wa bidhaa za kampuni hiyo ikiwemo kifurushi cha DSTV BOMBA chenye chaneli zaidi ya 65 ikiwemo huduma ya vituo kadhaa vya televisheni za hapa nchini.

Akimtambulusha rasmi Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Furaha Samalu, amemtambulisha Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa balozi wa king’amuzi hicho na kutaja gharama zake kuwa ni shilingi 23,500/= kwa malipo ya mwezi na king’amuzi chenyewe kinapatikana kwa shilingi 79,000/= na kuwataka wananchi kuchangamkia huduma hiyo muhimu katika msimu huu wa ofa za sikukuu.

Meneja masoko huyo ameongeza kuwa, kifurushi hicho kimesambaa nchini mbalimbali barani Afrika hivyo wasanii wa filamu, muziki na wengineo ambao watang’aa kwenye vipindi hivyo watakuwa wakionekana pande mbalimbali barani Afrika na hivyo kuwapatia umaarufu na kuwaongezea soko la kazi zao.
DSC_0151
Mwanamuziki Diamond Platinumz akisoma kipeperushi chenye maelezo juu ya ofa mbalimbali za DStv wakati wa utambulisho wa ofa za sikukuu pamoja na kutangazwa kwa balozi huyo wa bidhaa za DSTV. Katikati Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu na kushoto ni Meneja Mwendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.
DSC_0233
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akifafanua jambo katika mkutano huo na kushoto ni Meneja Mwendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo na upande wa kulia ni msanii Diamond Platnumz balozi wa bidhaa za DSTV.
DSC_0159
Meneja mauzo wa DSTV, Bw. Salum Salum akifafanua jambo juu ya ofa hiyo mpya na mahaala wanapopatikana nchini kwa mawakala wote ambapo amewaomba watanzania kuchangamkia ofa ya kuunganishwa haraka huduma bora zaidi za chaneli za kisasa kupitia DSTV.
DSC_0174
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mkutano huo wa DSTV..

DSC_0176
Mwandishi wa gazeti la Raia Tanzania akiuliza swali juu ya bidhaa za DSTV..
DSC_0171
Mpiga picha wa Magazeti ya Habari leo, Fadhili Akida akiuliza swali katika mkutano huo wa DSTV..
DSC_0185
Ilifika wakati wa zawadi.. Diamond akisoma jina la mwandishi wa habari aliyeshinda zawadi hiyo..
DSC_0190
Diamond Platnumz akimkabidhi mwandishi wa habari, Sangu Joseph king'amuzi alichojishindia katika droo iliyochezeshwa wakati wa mkutano huo.
DSC_0196
Diamond akikabidhi zawadi ya King'amuzi cha DSTV kwa mwandishi wa habari Rajab Musa baada ya kushinda..
DSC_0204
Diamond akikabidhi zawadi ya king'amuzi kwa mwandishi wa habari, Joseph Mchekadone baada ya kushinda..
DSC_0205
Diamond Platnumz akimkabidhi king'amuzi mwanahabari wa ITV, Ester Sangai baada ya kuibuka mshindi..
DSC_0165
Meneja mauzo wa DSTV, Bw. Salum akisisitiza juu ya ofa hiyo ambapo ameeleza kuwa wateja watapa kujionea chaneli mbalimbali zenye mvuto na picha za kuvutia huku bidhaa zake zikiwa ni tofauti kabisa na zingine.

JEFF AACHIA VIDEO YA WIMBO WAKE MPYA WA "MAMA AFRIKA" UNAOTANGAZA UTALII WA TANZANIA

$
0
0
jeff
Mwanamuziki aliyewahi ishi nchini Tanzania na pia mwenye asili ya Congo, Jeff Maximum ambaye anaishi Ughaibuni katika shughuli zake za Muziki katika pozi ambapo kwa sasa ameachia video ya wimbo wake mpya wa "Mama Afrika" ambao wimbo huo unatangaza Utalii wa Tanzania.


Mwanamuziki anayefanya kazi zake nchini Marekani na Dubai, Jeff Maximum tayari ameshaachia video ya wimbo wake mpya uitwao “Mama Afrika” ambao umetayarishwa Bagamoyo Nchini Tanzania hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Jeff anaweka wazi kuwa, kuwa video hiyo iliyoachiwa Novemba 2 mwaka huu, tayari imeshaanza kuonekana katika vituo mbalimbali vya televisheni Bara la Afrika ikiwemo nchini, pia katika nchi za Nigeria, Afrika Kusini, Kongo, Ghana, Kenya na kwingineko.

Pia video hiyo inaonekana katika vituo vya televisheni vya nchini Uingereza, Dubai, Amerika na kwingineko huku ikitangaza utalii wa Tanzania kwa asilimia kubwa.Jeff anaweka wazi kuwa, aliamua kuitayarishia video hiyo nchini Tanzania kwa kuwa ni kati ya nchi nyingi anazozipenda zaidi Barani Afrika.

Na kuongeza kuwa, video hiyo imetengenezwa na mwongozaji anayechipukia kutoka Tanzania Hanscana (Wanene Films), huku audio yake ikiwa imetayarishwa katika studio yake iliyopo nchini Dubai (One Vision Records).
Tazama video hiyo hapa chini.

BASATA KUWAKUTANISHA WASANII KUIJADILI SIKU YA MSANII

$
0
0

New PictureNational Arts Council BASATABaraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ijumaa hii ya tarehe 06/11/2015 linatarajia kuyakutanisha mashirikisho na vyama vya wasanii nchini kwenye Ukumbi wa BASATA ulioko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam ili kuweka mikakati ya pamoja katika kufanikisha siku ya msanii maarufu kama Msanii Day inayotarajiwa kufanyika tarehe 12/12/2015.
 Kwa mujibu wa Mratibu wa Siku ya Msanii kutoka Kampuni mwendeshaji wa siku ya Msanii (Msanii Day) Haakneel Production Tanzania (LTD) Bw. Justine Kusaga lengo la kuwakutanisha wasanii ni kuwa na mjadala wa pamoja ili kuhakikisha siku hii ya Msanii inafanyika kwa mafanikio makubwa na kuwafanya wasanii wote kuwa sehemu ya siku hii muhimu kwao.
 “Haakneel kwa kushirikiana na BASATA ambao ni wamiliki wa mradi huu wa siku ya msanii tumeamua kuwaita wasanii kupitia mashirikisho na vyama vyao ili kuhakikisha kila msanii anakuwa sehemu ya maadhimisho ya siku hii muhimu lakini pia kuifanya siku hii kuwa yenye mafanikio” alisema Kusaga
 Alizidi kueleza kwamba, mwaka huu siku ya msanii imepangwa kuwa ya tofauti ambapo shamrashamra zake zimepangwa kuanza mapema zaidi kwa kuhusisha shughuli na matukio mbalimbali ya kisanaa kabla ya kilele ambacho kinatarajiwa kupambwa na burudani mbalimbali za Wasanii.
 “Tunawaita wasanii Ijumaa hii ili kwa pamoja tujadiliane, tuweke mikakati ya pamoja na kuhakikisha kunakuwa na shamrashamra nyingi za wasanii ambazo zitawafanya waimiliki siku hii maana hakika siku hii ni yao wasanii” alisisitiza Kusaga.
 Siku ya Msanii maarufu kama Msanii Day ni mradi unaomilikiwa na BASATA ambao lengo lake ni kuenzi, kuthamini na kutambua michango mbalimbali ya wasanii nchini na kwa mara ya kwanza iliazimishwa tarehe 25 Oktoba mwaka jana wa 2014,
 IMETOLEWA NA KITENDO CHA HABARI NA MAWASILIANO, BASATA

HIVI NDIVYO HAFLA YA KUAPISHWA KWA RAIS WA AWAMU YA TANO WA TANZANIA ILIVYOFANYIKA UWANJA WA UHURU JIJINI DAR LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride maalum la Jeshi la Ulinzi lenye Umbo la Alfa, ikiwa ni ishara ya kuanza kwa Serikali mpya ya awamu ya tano, katika Sherehe za kuapishwa kwake, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo. Sherehe hizo zimehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa ndani na nje ya nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akila kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mh. Mohamed Chande Othman, katika Sherehe za kuapishwa kwake, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo.Kushoto ni Rais aliemaliza muda wake, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Makamu wake, Mh. Dkt. Mohamed Gharib Bilal. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
Rais aliemaliza muda wake, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davies Mwamunyange, wakati akiwaaga wananchi mara tu alipowasili kwenye Uwanja wa Taifa, katika Sherehe za kuapishwa Rais Mpya wa awamu ya tano, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, zilizofanyika leo jijini Dar es salaam.
Rais aliemaliza muda wake, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea salamu ya heshima ya kijeshi kabla ya kukabidhi madaraka kwa Rais Mpya wa awamu ya tano, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais Mpya wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akionyesha Mkuki na Ngao aliokabidhiwa na Wazee wa kimila ikiwa ni ishara ya Uongozi wa Kitaifa, katika Sherehe za kuapishwa kwake, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo.
 Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uwanja wa Uhuru leo.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwa amekaa na viongozi mbalimbali katika jukwaa kuu  mara baada ya kuapishwa leo hii kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
 Kadinali Policarp  Pengo na Askofu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dk. Alex Malasusa wakielekea katika eneo la kuapishia.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande na Spika wa Bunge mama Anne Makinda wakielekea katika aneo la kuapishia.
 Viongozi mbalimbali serikali na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwa katika sherehe hizo kwenye uwanja wa Uhuru.























 Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uwanja wa Uhuru leo.








SIKU YA KWANZA YA DK. MAGUFULI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na wanausalama alipowasili Ikulu mara baada ya Kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli (Katikati) Akiongozana na Mkewe Mama Janet Magufuli walipowasili Ikulu mara baada ya Kuapishwa kwenye sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na wafanyakazi wa Ikulu mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ngoma kama ishara ya kumkaribisha Ikulu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli mara baada ya kuapishwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwaongoza baadhi ya marais wa Afrika Kuimba wimbo wa Taifa, Kushoto kwake ni Rais wa Tanzania aliyemaliza muda wake Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janet Magufuli na Mke wa Rais aliyemaliza muda wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika hafla iliyofanyika mapema leo Ikulu Dar es Salaam
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ally Mohamed Shein akimueleza jambo Rais wa Kenya Uhuru Kenyata wakati wa hafla iliyofanyika leo Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya viongozi wa nchi za afrika na wawakilishi wa mataifa mengine duniani katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, Kulia ni Rais aliyemaliza muda wake Dk. Jakaya Kikwete na Kulia ni Mke wa Rais Mteule Mama Janet Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata, Raila Odinga na wake zao
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata leo Ikilu Jijini Dar es Salaam
Raila Odinga akimkumbatia Rais wa Kenya Uhuru Kenyata katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Raila Odinga, na Mama Janet Magufuli akisalimiana na Raila Odinga wakati wa Hafla iliyofanyika Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwaeleza Jambo Rais wa Kenya Uhuru Kenyata na Rais aliyemaliza Muda wake Dk. Jakaya Mrisho Kikwete leo Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa awamu ya Pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi na Rais wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu leo Jijini Dar es Salaam
(Picha na Hassan Silayo-MAELEZO)

JE MNAHITAJI SACCOS, IJUE NAMNA YA KUANZISHA.

$
0
0
NA  BASHIR   YAKUB.
NILIWAHI  kueleza  namna ya  kuanzisha  kampuni   pamoja  na  usajili  wa  jina  la  biashara. Katika  makala  hayo  pia  nilieleza  tofauti  kati  ya   kusajili  kampuni  na  kusajili  jina  la  biashara.

  Hii  ilikwenda  sambamba  na  maelezo  ya  tofauti  za  kiuchumi   ya  vyote  viwili.  Ifahamike  kuwa  hizi  zote  ni  njia  za  kisasa  za  kujitafutia  kipato.  Makala  ya  leo  yanaeleza  namna   ya  kisheria  ya  kuanzisha   SACCOS.  

Tutaona  utaratibu  mzima  ambao   unaweza  kupitia  katika  kulifanikisha  hili.  Muhimu  ni  kujua  kuwa  SACCOS  nayo  ni  njia  kati  ya  njia  za  kisasa  za  kujipatia  na  kujiongezea kipato.  Aidha utaratibu  mzima  wa kuanzisha  na  kuendesha  SACCOS   unaongozwa  na  Sheria  namba  6  ya  2013  ya  vyama  vya  ushirika  ambayo  ndiyo  msingi  wa  makala  haya.

1.SACCOS  NI  NINI ?                                                                                                      
SACCOS   ni  kifupi  cha  neno  la  kiingereza  lijukanalo  kama  Saving  And Credit  CO-operative  Society.  Kwa  Kiswahili  kizuri  ni  chama  cha  ushirika  cha  akiba  na  mikopo.

  Kwa  faida  tu  ni  kuwa,  kwa  mara  ya  kwanza SACCOS  zilianzishwa  Ujerumani   na  mtu  aitwaye  Fredrick  Taylor.  Sura  ya  SACCOS   aliyoanzisha  Taylor  imekuwa  ikibadilika   kadri  shughuli  za  kijamii  na  kiuchumi  zinavyokua  mpaka  kufikia  aina  ya  SACCOS  zilizopo  sasa.

2.  SACCOS   KIUCHUMI.
Saccos  ni  asasi  ya  kifedha. Ni  muungano  wa  watu  ambao  lengo  lao  ni  kukusanya  fedha  na  kukopeshana  au  kufanya  biashara  moja  kwa  moja  na  kugawana  faida. Taratibu  za  kukopeshana  na  kufanya  biashara  katika  Saccos  hufanywa  na  watu   wenye  msimamo  au  fungamano  linalofanana.

 Hii  ina  maana wanaweza  kuwa  watu  wanaofanya  kazi  ya  aina  moja kwa  mfano  walimu, wafanyabiashara, wafanyakazi  katika  ofisi  fulani, vijana  wanaoishi  eneo  moja  mtaani, wanawake  walio  katika  eneo  moja,   waumini  wanaosali  katika msikiti  au  kanisa  moja, wakulima,wavuvi, wafugaji, wanakijiji na  watu  wote wa  aina  hiyo.  Watu  walio  katika  mafungamano  ya aina  hiyo  ndio  wanaweza  kuunda  Saccos.

3.  LENGO  KUU  LA  SACCOS.
Lengo  kuu  la  Saccos  ni  kuwa,  ni  ushirika  ambao  lengo  lake  ni  kuondoa  umasikini  na  kuinua  uchumi wa  wanachama  na  jamii  kwa  ujumla.  Hii  ndio  sababu  kubwa  ya  kuanzisha  Saccos.  Ni  kukuza  kipato   kwa  manufaa  ya  kiuchumi .Ni  biashara  ya  kuongeza  kipato  kama  zilivyo  biashara  nyingine  za  uanzishaji  wa  makampuni n.k.


4.  MAMBO  YA KUZINGATIA  KABLA  YA  KUANZISHA  SACCOS.
Kwanza  kabisa  ni  uwepo  wa  hiari  ya  kila  mwanachama. Ni  kosa  kumshurutisha  mtu  kuingia  katika  Saccos. Ni  lazima  kila  anayeingia   afanye  hivyo  kwa  hiari  yake.  Pili  ni  muhimu  wanaoanzisha  Saccos  wakawa  na  matatizo  ya  aina  moja.  Kama  tatizo  ni  ajira   na  Saccos  inaundwa  ili  kukabiliana  na  hilo  basi  yapasa  hilo  ndio  liwe  tatizo  la  wanachama  wote n.k. Kwa  ufupi  wanachama  wawe  ni  watu  wanaoshiriki (share) tatizo.

5.  TARATIBU  RASMI  ZA  KUANZISHA  SACCOS.
( a )  Kwanza  kabisa  hakikisha  hampungui  watu  watano. Yaani  muwe  watu  watano  na  kuendelea. Hii  ni  kwa  mujibu  wa  kifungu  cha  38(1)  cha  sheria  ya  vyama  vya  ushirika.  Hata  hivyo  idadi  hii  ni  kwa  waanzishaji  wa  awali. Hii  ni  kwakuwa  idadi  hasa  inayotakiwa  ni  kuanzia  watu  ishirini. Msajili  wa  vyama  vya  ushirika  atawapa  maelekezo  ya  idadi  kwa  namna  anavyoona  kikundi  chenu.

( b ) Baada  ya  idadi  hiyo  kutimia  mtamfuata  msajili  wa  vyama  vya  ushirika  ambaye  hupatikana  katika  kila  makao  makuu  ya  wilaya  mliyopo. Nenda  makao  makuu  ya wilaya  na  uliza  hapo  utampata. Baada  ya  kusikiliza  maelezo  yenu  msajili ataandaa  mkutao  ambao  huitwa  mkutano mkuu  wa  uanzishaji  ambao  msajili  mwenyewe  ndio  atakuwa  mwenyekiti wake.  Katika  mkutano  huo  itateuliwa kamati  ya  muda  ya  uanzishaji  ambayo  itakuwa  na  wajumbe 5 – 9 akiwemo  katibu, mwekahazina, mwenyekiti  na  wajumbe  wengine.

( c ) Baada  ya  kamati  ya  uanzishaji   kuundwa itakuwa  na  kazi  ya  kushirikiana  na  afisa  ushirika  kuandaa  katiba  za  chama, sera,miongozo, miradi  ya  kiuchumi, taratibu  za  viingilio  na  taratibu  zote  za  uanzishaji na uendeshaji.

( d ) Baada  ya  kazi  hiyo  kukamilika  basi  maombi  rasmi  ya   kuomba  kusajiliwa  yatawasilishwa  kwa  huyo afisa  ushirika  wa  wilaya  yakiambatana  na  nakala  nne  za  sera  za  chama, kidadisi  uchumi, makadirio  ya  mapato  na  matumizi, mikhutasari  ya  mikutano  miwili, na  ada  kama  itakavyoelekezwa  na  afisa  ushirika.

Tutaeleza katika makala  nyingine  umuhimu  wa  SACCOS,   tofauti  za  kiuchumi  kati  ya  SACCOS  na  kampuni na  kipi  bora kati  ya  kuanzisha  SACCOS  na  kampuni.
MWANDISHI   WA   MAKALA  HAYA   NI   MWANASHERIA  NA  MSHAURI   WA  SHERIA  KUPITIA  GAZETI  LA  SERIKALI   LA   HABARI   LEO  KILA  JUMANNE  , GAZETI  JAMHURI   KILA  JUMANNE  NA  GAZETI  NIPASHE  KILA  JUMATANO.    0784482959,        0714047241              bashiryakub@ymail.com

HAFLA YA MCHAPALO (COCKTAIL PARTY) WA KUSHEREHEHEA KUAPISHWA KWA RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI

$
0
0
 Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwasili kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Alhamisi usiku kwa ajili ya mchapalo maalum ulioandaliwa na Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli kusherehekea kupishwa kwake
 Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi 
 Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Sheim
 Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete akifuatiwa na mkewe Mama Janet Magufuli
  Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan kifuatiwa na mkewe Mama Janet Magufuli.
  Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mama Hadija Mwinyi akifuatiwa na mkewe Mama Janet Magufuli
  Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mama Sitti Mwinyi  akifuatiwa na mkewe Mama Janet Magufuli
  Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mama Salma Kikwete  akifuatiwa na mkewe Mama Janet Magufuli
  Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mama  Asha Suleiman Iddi akifuatiwa na mkewe Mama Janet Magufuli
 Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli na viongozi wengine wakiwa hema kuu
 Mama Janet Magufuli akisalimiana na Mhe Makongoro Nyerere
 Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli  akisalimiana na Mhe Makongoro Nyerere
 Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makongoro Nyerere
 Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli  akiongea na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
 Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akienda kusalimiana na wageni wake
  Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wageni wake
 Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Mtera Mteule Mhe Livingstone Lusinde
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wageni wake
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wageni wake

 Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea  kusalimiana na wageni wake
 Mama Janet Magufuli akiwa na wageni wao

 Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake

 Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
  Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake.

   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na kutaniana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana kutniana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mhe Augostino Lyatonga Mrema wakati akiendelea kusalimiana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake. Hapa akiongea na Mbunge wa Morogoro vijijini mteule Mhe Propser Mbena
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake. 
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake. Hapa akiteta jambo na kijana George Mathias Mgina
 Rais Dkt Magufuli akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Mizengo Pinda na Mzee Joseph Butiku
 Mama Janet Magufuli akiamkia na na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Mizengo pinda wakiwa Rais Dkt Magufuli na Mzee Joseph Butiku
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janet Magufuli wakiwa na kijana George Mathias Mgina
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mama Tunu Pinda akiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Mizengo pinda na wanafamilia
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa na wake wa viongozi na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Mizengo Pinda
 Mama Janet Magufuli akisalimiana na Mama Hasina Kawawa
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mhe Ole Sendeka
 Balozi wa Tanzania nchiniNigeria Mhe Njoolay akiwa na Mhe Chiligati na Mhe Profesa Jumanne Maghembe
 Wadau wakifurahia mchapalo
 Wadau wakiwa katika mchapalo huo
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe Saidi Mwambungu na Mbunge Mteule wa Nyasa
 Blogger maarufu Haki Ngowi (kushoto) na nduguye ambaye ni mbunifu wa mavazi wa mkimataifa Sheria Ngowi ndani ya nyumnba
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake. Hapa ni rafiki yake na Waziri Mkuu wa Zamani wa Kenya Mhe Raia Odinga na ujumbe wake
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
  Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mama Salma Kikwete na familia ya Rais Mstaafu
  Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimianana na Mufti Mkuu wa Tanzania 
  Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipozi na viongozi wa BAKWATA
  Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimaiana na viongozi wa dini

 Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na msanii Mrisho Mpoto

 Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wageni wake

 Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wageni wake

 Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wageni wake

 Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wageni wake

  Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana  na wageni wake
Yamoto Band ikitumbuiza. Picha zote na IKULU

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

$
0
0


Mkuu wa wilaya ya Geita awataka madiwani waliochaguliwa hivi karibuni kujenga uhusiano mwema wa kiuntandaji na watumishi wa halmashauri ili kuwaletea maendeleo wananchi. https://youtu.be/1ynKoT77ASg

Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Songea waonyesha matumaini makubwa na raisi mpya katika kubadili mfumo wa utendaji serikalini. https://youtu.be/iOHZUu4XXzU

Mapokezi makubwa yamgonja raisi Dr.Magufuli mkoani Geita huku wananchi wakiwa na amatumaini makubwa juu yake huku wengine wakitoa nasaha zao.https://youtu.be/LNnSnYYy8BU

Wakati raisi mstaafu Jakaya Kikwete ankabidhi madaraka ametoa masamaha kwa wafungwa 4160 nchini kote. https://youtu.be/_68wRnZyaLs

Taifa la Tanzania leo limepata raisi mpya wa awamu ya 5 baada ya Dr.Magufuli kuapishwa na kuanza kazi za kiserikali rasmi hii leo. https://youtu.be/ZtMxPb0k3rs

Wakazi wa Iringa watoa maoni yao juu ya mategemeo kwa raisi wa awamu ya 5 Dr.Magufuli huku wakitoa rai mbalimbali. https://youtu.be/QmUxnIAND80

Wakazi wa visiwa vya Zanzibar wametoa maoni yao kufuatia kuapishwa kwa raisi wa awamu ya 5 Dr.John Magufuli. https://youtu.be/qCFHPanLEVA

Aliwahi kuwa waziri mkuu wa Kenya na kiongozi mkuu wa upinzani wa Kenya aongea machache juu ya raisi wa awamu ya 5 Dr.Magufuli. https://youtu.be/r32j4qsgFno

Baada ya Raisi Kikwete kuhitimisha kipindi chake cha uongozi wa awamu ya 4 raisi huyo mstaafu azumgumzia malengo yake baada ya kustaafu.https://youtu.be/2BMfmtvWSHw

JEFF AACHIA VIDEO YA WIMBO WAKE MPYA WA "MAMA AFRIKA" UNAOTANGAZA UTALII WA TANZANIA

$
0
0
jeff
Mwanamuziki aliyewahi ishi nchini Tanzania na pia mwenye asili ya Congo, Jeff Maximum ambaye anaishi Ughaibuni katika shughuli zake za Muziki katika pozi ambapo kwa sasa ameachia video ya wimbo wake mpya wa "Mama Afrika" ambao wimbo huo unatangaza Utalii wa Tanzania.

Na Mwandishi Wetu
Mwanamuziki anayefanya kazi zake nchini Marekani na Dubai, Jeff Maximum tayari ameshaachia video ya wimbo wake mpya uitwao “Mama Afrika” ambao umetayarishwa Bagamoyo Nchini Tanzania hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Jeff anaweka wazi kuwa, kuwa video hiyo iliyoachiwa Novemba 2 mwaka huu, tayari imeshaanza kuonekana katika vituo mbalimbali vya televisheni Bara la Afrika ikiwemo nchini, pia katika nchi za Nigeria, Afrika Kusini, Kongo, Ghana, Kenya na kwingineko.
Pia video hiyo inaonekana katika vituo vya televisheni vya nchini Uingereza, Dubai, Amerika na kwingineko huku ikitangaza utalii wa Tanzania kwa asilimia kubwa.

Jeff anaweka wazi kuwa, aliamua kuitayarishia video hiyo nchini Tanzania kwa kuwa ni kati ya nchi nyingi anazozipenda zaidi Barani Afrika.
Na kuongeza kuwa, video hiyo imetengenezwa na mwongozaji anayechipukia kutoka Tanzania Hanscana (Wanene Films), huku audio yake ikiwa imetayarishwa katika studio yake iliyopo nchini Dubai (One Vision Records).
Tazama video hiyo hapa chini.

MKUTANO MKUU WA WANACHAMA WA MUUNGANO WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA- UTPC MJINI MOROGORO

$
0
0

Hapa ni katika ukumbi wa Flomi Hotel mjini Morogoro ambako leo Ijumaa Novemba 06,2015 kunafanyika mkutano mkuu wa wanachama wa Muungano wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania-UTPC wanakutana kujadili mambo mbali mbali ili kuboresha taaluma ya uandishi wa habari nchini Tanzania.Mkutano huo wa siku mbili unakutanisha wenyeviti wa klabu za waandishi wa habari Tanzania,makatibu na waweka hazina.Katika mkutano huo pia utafanyika uchaguzi wa rais wa UTPC na wajumbe wa bodi wa UTPC-Fuatilia picha hapa chini kinachoendelea ukumbini-Picha zote na Kadama Malunde na Shomari Binda-Malunde1 blog.

Kushoto ni mkurugenzi wa UTPC Abubakar Karsan,akifuatiwa na makamu wa rais UPC Jane Mihanji,rais wa UTPC Kenneth Simbaya na mwenyekiti wa kamati ya maadili UTPC Deo Nsogolo

Mkurugenzi wa UTPC Abubakar Karsan akiwasalimia wajumbe wa mkutano huo.

Kauli mbiu ya mkutano huo ni "Tumia Klabu za waandishi wa habari kwa maendeleo ya mkoa wako"


Mkutano unaendelea

Rais wa UTPC anayemaliza muda wake Kenneth Simbaya akifungua mkutano.

Wajumbe wa mkutano wakiwa ukumbini.

Mkutano unaendelea.

Mkurugenzi wa UTPC Abubakar Karsan akizungumza ukumbini.

Mkutano unaendelea.

Rais wa UTPC Kenneth Simbaya akikabidhi hati ya usajili ya Katavi Press Club kwa mwenyekiti wa klabu hiyo Walter Mguluchuma.

Wajumbe wakiwa ukumbini.

Mkutano unaendelea.

Wajumbe wakiwa ukumbini.

Mkutano unaendelea

Tunafuatilia kinachoendelea......

Wajumbe wa mkutano wakiwa ukumbini

Mkutano unaendelea

Mkutano unaendelea.

mkutano unaendelea

Wajumbe wakiwa ukumbini

Mkutano unaendelea

Tunafuatilia kinachojiri ukumbini


Mkutano unaendelea

Mkutano unaendelea


Mkutano unaendelea

Picha zote na Kadama Malunde na Shomari Binda-Malunde1 blog

BEI YA MADAFU HII LEO

SERIKALI YATOA PICHA RASMI YA RAIS WA AWAMU YA TANO.

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene akiwaonesha waandishi wa Habari picha rasmi ya Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambayo itakuwa ikitumika katika ofisi za Serikali na Binafsi ambayo inapatikana Idara ya Habari (MAELEZO) kwa gharama ya Shilingi 15,000/

Rais Magufuli akiwa Ofisini Kwake Siku ya Kwanza

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akifanyakazi ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni siku yake ya kwanza ofisini kwake tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano.
(Picha na Freddy Maro)

KUZIONA TWIGA NA MALAWI 1,000/= TU

$
0
0
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza kiingilio cha shilingi Elfu moja (1,000)  ndio kitakachotumika kuingia kushuhudia mchezo wa kirafiki wa Kimataifa kati ya Timu ya Taifa Wanawake ‘Twiga Stars’ dhidi ya timu ya Taifa ya Wanawake Malawi utakaochezwa kesho Jumamosi, Novemba 7 katika uwanja wa Azam Chamazi.
Twiga Stars inayonelewa na kocha mzawa Rogasian Kaijage iliingia kambini wiki iliyopita ambapo imekua ikifaya mazoezi kila siku katika uwanja wa Karume kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa.
Katika mchezo huo, Twiga Stars itautumia nafasi hiyo kumuaga mshambuliaji wake wa siku nyingi Estha Chaburuma ambaye ni miongoni mwa waanzilishi wa Twiga Stars na sasa anastaafu rasmi kucheza mpira wa miguu.
Upande wa timu ya Taifa ya Malawi tayari imewasili jana jioni jijini Dar e salaam ikiwa na kikosi cha wachezaji 20 pamoja na viongozi nane ambapo leo jioni kikosi chake kitafanya mazoezi katika uwanja wa Karume saa 10 jioni.

MASHABIKI WA WASANII WAMETAKIWA KUONDOA ITIKADI ZA VYAMA ZILIZOTOKANA NA KAMPENI

$
0
0
 Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SHIRIKISHO la Wasanii nchini  wamewataka mashabiki wao kuondoa tofauti  za kiitikadi ambazo zilijitokeza  katika kampeni waendelee kuwaunga mkono.


Akizungumza na waandishi wa habari,mmoja wa msanii, Stara Thomas amesema kila watu walikuwa na itikadi katika kampeni hivyo ni wakati mwafaka wa kufanya kazi.


Stara amesema wameshiriki katika kampeni zimeisha sasa ni wakati kushiriki katika majukumu kama wasanii.


Hata hivyo amesema wanapongeza Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa na watanzania  katika kuongoza.


Nae Msanii Mkongwe, John Kitime amemtaka Rais kuwekea umuhimu wa idara ya utamaduni  kuweza kufanya wizara kutokana na kuwepo kwa changamoto nyingi kwa wasanii.


Kitime amesema idara hiyo kuhama hama kumewafanya wasanii kuwa nyuma na kufanya nchi kushindwa kupata mapato licha ya wasanii kuwa wengi.


Kwa upande Mkurugenzi wa Bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka ameshauri Rais mpya katika uteuzi wa bodi wasanii wateuliwe kutokana na uwezo wao katika kazi hiyo.


Asha amesema kuteuliwa kwa wasanii katika bodi zenye sanaa nchini zitaleta chachu na wasanii watatambuliwa na jamii kwa mchango wao.

VITI MAALUM 110 VYATANGAZWA LEO

$
0
0
Mwenyekiti  wa Tume ya Taifa ya Uchanguzi  Jaji Msitafu Damian Lubuva  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  juu ya majina ya wabunge wa Viti Maalum yatapatikana katika Vyama husika kwa mujibu wa Orodha iliyowasilishwa Tume na kila Chama ila Tume (NEC)iweze kufanya Uteuzi, kikao hicho kimefanyika leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Emmanuel Kavishe.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti  wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),  Jaji Msitafu Damian Lubuva 
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza Viti Maalum vya Wabunge 110 kwa vyama vitatu ambavyo vimevuka asilimia tano ya kura za wabunge.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu, Damian Lubuva amesema idadi ya wabunge imeongezeka kwa kufikia asilimia 40 kutokana na uamuzi wa serikali wa mwaka 2010 kwa kuongeza idadi ya viti maalum vya wanawake.

Lubuva amesema kutokana na  kuwepo  majimbo ya nane ambayo hayakufanya uchaguzi kunafanya viti vitatu kutokuwepo, baada ya uchaguzi wa majimbo hayo viti vitarudi kwa vyama.

Katika mgawanyo wa viti maalumu vya wanawake katika bunge  linalotarajiwa kuanza hivi karibuni Chama cha Mapinduzi (CCM), kimepata viti 64, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) viti maalum 36 na Chama cha Wananchi (CUF)  Viti Maalum 10. 

Majina ya viti maalum yatapatikana  katika vyama husika kwa mujibu wa orodha iliyowasilishwa  Tume ya kila chama  ili tume iweze kufanya uteuzi. 

BALOZI MULAMULA AWASINDIKIZA MRAIS WA DRC NA MSUMBJIA

$
0
0
Rais wa Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo, Mhe. Joseph Kabila (wa kwanza kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakitizama Kikundi cha Ngoma kilichokuwa kikitoa Burudani kwenye Uwanja wa Ndege, Rais Kabila alikuja nchini kuhudhuria Sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli iliyofanyika hapo jana katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Rais Kabila (katikati) akielekea kwenye ndege, kulia ni Balozi Mulamula na kushoto ni Balozi wa Kongo nchini Mhe. Khalifani Mpango
Mhe. Rais Kabila akipita kwenye gwaride la heshima lililoandaliwa na Jeshi la wananchi Tanzania.
Katibu Mkuu Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) akiagana na Rais Joseph Kabila tayari kwa kuanza safari ya kuelekea nchini kwake.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (mwenye pochi mkononi) akiagana na Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi
Rais Nyusi akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mhe. Shamimu Nyanduga.
Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa ambaye anawakilisha pia nchini Algeria, Mhe. Begun Taj akimsindikiza Waziri wa Nchi anayeshughulikia masuala ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Algeria, Mhe. Ramtane Lamamra. Mhe. Lamamra alikuja nchini kwa ajili ya kuhudhiria Sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli.
Mhe. Lamamra akipanda kwenye ndege tayari kabisa kuanza safari ya kurejea nchini Algeria
Picha na Reginald Philip

Rais Magufuli afanya Ziara ya Kushtukiza Hazina.

$
0
0
 Rais Dkt.John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili katika makao makuu ya Wizara ya Fedha(HAZINA) kwa ziara ya kushtukiza leo mchana.Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Servacius Likwelile.Rais Magufuli alitembelea na kukagua ofisi zote wizarani hapo na kisha kuongea na viongozi waandamizi.
 Rais Dkt.John Pombe Magufuli akiwa na wafanyakazi wawili wa Wizara ya Fedha ambao ni walemavu Bwana Fundi Maruma na Frank Mkyama wakati Rais alipofanya ziara ya kushtukiza wizarani hapo leo.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha wakati alipofanya ziara ya kushtukiza Wizarani hapo ambapo alitoa maagizo ya kuziba mianya ya wakwepa kodi.
(Picha na Freddy Maro).

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika Ofisi za Wizara ya Fedha leo Ijumaa tarehe 6 Novemba, 2015.

Katika ziara hiyo Mhe.Rais alipata fursa ya kutembelea baadhi ya Ofisi za Wizara na baadae  kuzungumza na Viongozi wa Wizara ili kufahamu changamoto ambazo zinaikabili Wizara ya Fedha.Wakati akimkaribisha Mhe.Rais Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha        Dkt. Servacius Likwelile alimueleza kuwa Wizara ya Fedha inakabiliwa na changamoto kubwa inayotokana na makusanyo ya mapato ya ndani. 

 Miongoni mwa sababu ni misamaha ya kodi, wafanyabiashara wengi hasa wakubwa kukwepa kodi, makusanyo yasiyoridhisha ya maduhuli na kutokulipwa kwa kodi za majengo. Aidha Dkt. Likwelile alishauri ni bora kuwekwa mifumo mizuri, ikiwemo matumizi ya Tehama na EFDs.

“Pamoja na ziara yangu kuwa ni ya kustukiza nimefurahi sana kukuta Viongozi wote wapo ofisini na wanafanya kazi. Jambo hili limenipa faraja kubwa. Ziara yangu ya kuja hapa nimejifunza na kujua changamoto zipi zinazowakabili”. Alisema Mhe. Rais.

Nimesikia changomoto nyingi na ninaagiza kuwa muhakikishe walipa kodi wakubwa wanalipa kodi na kusimamia kikamilifu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili iweze kukusanya kodi kikamilifu na si kuwabana wafanya biashara wadogo wadogo.Mhe.Rais aliwataka Viongozi wa Wizara kufanya kazi kwa bidii ili kuvuka lengo.
Imetolewa na;
Msemaji wa Wizara ya Fedha
Ingiahedi C.Mduma
6.11.2015  

ENEO LA LEBANON KATIKA SOKO LA KIMATAIFA LA SAMAKI LA FERI JIJINI DAR NI HATARI KWA UCHUMI.

$
0
0

Mwenyekiti wa Kamati ya Soko la Samaki la Kimataifa la Feri, Ali Kibwana, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wanaotembelea masoko mbalimbali ya Manispaa ya Ilala kuona jinsi gani vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia umepungua katika soko hilo baada ya Shirika la Equality for Growth (EfG) kutoa mafunzo ya kupinga ukatili katika masoko hayo. Kushoto ni Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo, Bakari Said.
Mwonekano wa sehemu ya soko la Samaki la Feri.

Na Dotto Mwaibale
ENEO la Lebanon katika Soko la Kimataifa la Samaki la Feri ambalo lipo jirani na Ikulu jijini Dar es Salaam limedaiwa kuwa ni hatari kwa wafanyabiashara wa soko hilo na kuwa linadhohofisha uchumi kutokana na kukithiri kwa watu wasio rasmi.

Hayo yamebainishwa na Mwezeshaji wa Sheria wa soko hilo, Asha Malenda wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wanaotembelea masoko mbalimbali ya Manispaa ya Ilala kuona jinsi gani vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia umepungua katika soko hilo baada ya Shirika la Equality for Growth (EfG) kutoa mafunzo ya kupinga ukatili katika masoko hayo.

"Tunachangamoto kubwa sana katika soko letu la Feri tunayoipata kutoka eneo la Lebanon lenye mwingiliano wa watu wasio rasmi kutoka nje ya soko ambao ni kama wamejianzishia soko lao na wamekuwa na maamuzi yao lakini viongozi wa soko la Feri wanashindwa kuwachukulia hatua hali ambayo inatudhalilisha sisi wafanyabiashara hasa mama lishe na kuharibu uchumi wa soko letu" alisema Malenda.

Alisema wengi wa watu waliopo katika eneo hilo lisilo rasmi wamekuwa wakifanya biashara kiholela huku wakipika vyakula katika maeneo yanayoweza kuhatarisha afya ya mlaji wakati katika soko hilo kuna eneo maalumu la mama lishe na wengi wa watu hao wakienda kula eneo hilo rasmi wamekuwa hawalipi fedha na wakibanwa kulipa wanadiliki kutoa visu na silaha za jadi kuwatishia wanaodai.

"Eneo hilo la Lebanon ni hatari na kinachoshangaza linatizamana na Ikulu lakini hakuna hatua yoyote ya makusudi inayochukuliwa na viongozi wetu na linapopelekwa kwa viongozi wa kisiasa wanadai waachwe kwani ndio wapiga kura wao" alisema Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo, Bakari Said.

Said alisema katika soko hilo kuna changoto nyingi za udhalilishaji wanawake kwa kushikwa katika maungo yao lakini kupitia EfG wamejitahidi kupunguza changamoto hizo kwani wasaidizi wa sheria waliopatiwa mafunzo na shirika hilo wanajitahidi kuupenyeza ujuzi waliopata kuifikishia jamii ambayo imeanza kuelewa kuhusu vitendo hivyo.

Aliongeza kuwa uvaaji wa nguo za kubana na kuacha vifua wazi kwa upande wa wanawake pia ulikuwa ukichochea kukithiri kwa vitendo vya udhalilishaji uliokuwa ukifanywa na vijana wasio rasmi katika eneo hilo la Feri ambao hawana makazi na maisha yao yapo Feri lakini baada ya kufikiwa na mafunzo ya EfG hali hiyo imepungua kwa asilimia 80.

Mwezeshaji Fatuma Saijali alisema changamoto kubwa iliyopo hivi sasa katika soko hilo ni kuzuiliwa kupika chakula katika eneo hilo la Feri lakini wakati huo huo kuna kundi la wanawake wamekuwa wakiingiza chakula kutoka majumbano kwao na kukiuza hivyo kuharibu soko lao la chakula.

Mwenyekiti wa Kamati ya Soko hilo, Ali Kibwana alisema mafunzo waliyopata kupitia EfG yamesaidia sana kupunguza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia katika soko hilo na kila mtu anayebainika kujihusisha na vitendo hivyo amekuwa akiitwa na kukanywa na kama akiendelea kuwa mkaidi anachukuliwa hatua nyingine kwa kufuata kanuni na sheria.

Kamanda wa Ulinzi na Mazingira wa Soko hilo, Nurdin Hassan amesema hali katika soko hilo ni nzuri kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na EfG ya kufanya semina na matamasha ya uhamasishaji hivyo kuifanyajamii kuelewa kuhusu vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia.

Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa EfG, Shaban Rulimbiye alisema Shirika hilo linaendesha mradi wa miaka mitatu wa Mpe Riziki si Matusi wenye lengo la kutoa elimu ya kupinga ukatili wa vitendo vya ukatili wa kijinsia na udhalilishaji na nia zaidi mradi huo ni kuusambaza hadi katika maeneo mengine ya nchi.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.
Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo, Bakari Said akizungumza katika mkutano huo.

Mama Lishe wa soko hilo, Taus Barnabas, akichangia neno katika mkutano huo.
Mama Lishe wa soko hilo, Fatuma Saijali (katikati), akizungumza katika mkutano huo.
Mwezeshaji wa Sheria katika Soko la Kimataifa la Samaki la Feri, Asha Malenda (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wanaotembelea masoko mbalimbali ya Manispaa ya Ilala kuona jinsi gani vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia umepungua katika soko hilo baada ya Shirika la Equality for Growth (EfG) kutoa mafunzo ya kupinga ukatili katika masoko yaliyopo Manispaa ya Ilala. Kulia ni Mama Lishe wa soko hilo, Taus Barnabas na Fatuma Saijali.
Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa EfG, Shaban Rulimbiye (kulia), akizungumzia kuhusu mradi huo wa miaka mitatu wa Mpe Riziki si Matusi.
Kamanda wa Ulinzi na Mazingira wa Soko hilo, Nurdin Hassan akisisitiza jambo kuhusu wanavyo imarisha ulinzi katika soko hilo.

Rais Magufuli akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Ramtane Lamamra

$
0
0





Rais Dkt. John Pombe Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Mhe. Ramantane Lamamra Ikulu jijini Dar es Salaam leo.(Picha na Freddy Maro)
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images