Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

TANZAONE: MMEA WA ‘LOZERA’ HAUFAI KWA MATUMIZI YA BINADAMU

0
0
  Tabibu Gonzaga Marwa akiangalia baadhi ya mkopo ya Dawa jijini Dar es Salaam leo

TAASISI isiyo ya Kiserikali ya Tanzaone Herbal Clinic chini ya mradi wake wa ‘Tanzaone’ hatimaye imethibitisha pasipo shaka kuwa mmea ujulikanao kama Lozera na bidhaa zitokanazo na mmea huo hazifai kwa matumizi ya binadamu na wanyama.

Akizungumza na waandishi wa habari, sanjari na kuonyesha majibu ya vipimo vya kitaalamu kutoka Wakala wa Maabara ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikali kupitia utafiti uliofanywa chini ya mradi huo, Mratibu wa mradi.

 Tabibu Gonzaga Marwa, amesema  matokeo ya uchunguzi wa sampuli za mmea huo yameonesha una ukuvi yaani ‘fangasi’ aina ya Aspergillus ambao hutoa sumu ya Aflatoxin ambayo huweza kusababisha saratani ya maini.


Aidha, Tabibu Marwa ameiomba serikali kupitia Wizara ya Afya, na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA, kuhakikisha wanachukua hatua za haraka kunusuru afya za walaji, sambamba na kushauri wadau wa tiba asili nchini kufanya utafiti wa kina wa dawa za mitishamba na bidhaa zake kabla ya kumfikia mlaji.


Hati ya uchunguzi ya Mradi huo, namba 241/2013, uliopewa jina la ‘Tanzaone Red Tea Juice’ na kudumu kwa miaka mitatu 2010/2013, kwa kushirikisha watuamiaji wakubwa wa Lozera zaidi ya 250 nchini kote, ilichunguzwa, kuidhinishwa na kuthibitishwa na Mkemia Mkuu wa Serikali

MAZOEZI YA KUAPISHWA KUWA RAIS DK MAGUFULI YAPAMBA MOTO JIJINI DAR

0
0
 Kibanda cha kitakachotumika wakati wa kuapishwa kwa Rais Mteule, Dk John Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kesho kutwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
 Askari wa Jeshi la Wananchi akiigiza kama Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange na mwingine akiigiza kama Rais anayemaliza muda wake, Jakaya Kikwete wakati wa mazoezi ya sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange (wa pili kulia), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Maangu (wa tatu kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick wakipiga saluti ulipokuwa unaimbwa wimbo wa Taifa wakati wa mazoezi ya sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Maofisa mbalimbali  wakiwa katika kibanda cha kiapo wakipanga jinsi viongozi watakavyokaa wakati wa sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

 Kikundi cha sarakasi kikitumbuiza wakati wa maandalizi hayo
 Wasanii kutoka Zanzibar wakicheza ngoma ya kibati wakati wa mazoezi hayo
 Mtu aliyeigiza kama  Rais Jakaya Kikwete, akiwa amesimama alipokuwa akipigiwa mizinga ikiwa ni ishara ya kuagwa kwa rais huyo kabla ya kuapishwa Rais mpya wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli wakati wa mazoezi hayo.
 Viongozi mbalimbali wakiwemo wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwa Jukwaa Kuu wakati wa maandalizi hayo.
 Baadhi ya wananchi wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa na Bendi ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakati wa maandalizi hayo.
Mtu aliyeigiza kama Rais Jakaya Kikwete, akielekea kukagua gwaride la heshima la kumuaga wakati wa mazoezi hayo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

WANANCHI WATAKIWA KULINDA AMANI YA NCHI-KAMISHINA,CHAGONJA

0
0

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
 
JESHI la Polisi limewetaka wananchi kuendelea na utulivu kama walivyoonyesha wakati wa upigaji kura na hatimaye kupatikana katika siku ya uapishaji wa Rais Mteule Dk.John Pombe Magufuli.
 
Akizungumza leo na waandishi wa habari Kamishina wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi hilo,Paul Chagonja amesema kuwa jeshi la polisi limeridhishwa na utulivu uliokuwepo wakati wa upigaji kura.
 
Amesema kuwa utulivu huo umeweza kufanya uchaguzi kwenda salama na hatimaye kupelekea kupatikana kwa mshindi.Amesema katika suala la Zanzibar liko katika mazungumzo hivyo viongozi wanafanya kazi yao, hivyo maandamano hayana nafasi kutokana na taratibu wanazozitumia.
 
Chagonja amesema watu waliokamatwa katika vurugu za uchaguzi wamefikishwa mahakamani na huku wengine wakiendelea na uchunguzi,
Amesema hali ya amani ipo na wananchi wametakiwa kulinda hali hiyo na ikitokea mtu analeta uchochezi walipoti ka vyombo vya usalama ili hatua zichukuliwe.
 
Chagonja ametaka baadhi ya taarifa katika mitandao ya jamii kuupuza taarifa ambazo zinatoa taharuki kwa wananchi kutokana na hizo taarifa wanazotoa zinapotosha.

MALALAMIKO YA MAHAKAMA YA MWANZO KUTATULIWA NA KAMATI YA MAADILI–DC .MAKONDA

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
 
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni,Paul Makonda  amesema wananchi ambao hawajaweza kupata haki zao katika mahakama za mwanzo wanaweza kutumia kamati ya maadili.
 
Makonda ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Makonda amesema kuwa watu wengine wanakosa haki katika mahakama na hawajui wanaweza kupata haki sehemu gani kutokana na mwenendo wa kesi ilivyoendeshwa.
 
Makonda amesema kamati hiyo inawajibu wa kuangalia mwenendo wa maadili ya hakimu na ikibanika kamati inaweza kuchukua hatua.
 
Amesema kuna baadhi ya wananchi wanapewa hukumu za kesi lakini mwenendo wa kesi haujui na mwisho wa siku anakosa haki kutokana na baadhi ya watu kutumia mahakama vibaya.
 
Makonda amesema sheria ya Usimamizi wa Mahakama  Na.4 ya mwaka 2011 sehemu 51(1) kutakuwa na kamati ya mahakama ya wilaya  ambayo mwenyekiti wake ni Mkuu wa Wilaya.
 
 Aidha amesema wengine wanaounda kamati hiyo ni Hakimu Mkazi wa Wilaya au msimamizi wa Wilaya ,Katibu wa Tawala wa Wilaya  (DAS) ambaye anakuwa Katibu wa Kamati hiyo,Kiongozi wa dini mmoja ambaye atateuliwa na Mkuu wa Wilaya ,mtu mashuhuri wa wilaya ambaye ni mwadilifu.
 
Hata hivyo amesema katika kamati hiyo maafisa wawili watateuliwa na Jaji  anayesimamia .Kamati hiyo itawajibika kupokea na kuchunguza malalamiko yaliyowasilishwa na wananchi kuhusu mahakama na kuwasilisha ripoti kwa tume..

MHUBIRI MAARUFU DUNIANI TB JOSHUA WA NIGERIA ATUA DAR ES SALAAM KUSHUHUDIA DKT MAGUFULI AKIAPISHWA

0
0
Mtume TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations nchini Nigeria  ametua jijini Dar es salaam leo  tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.
Mara tu baada ya kutua uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, TB Joshua alikwenda Ikulu moja kwa moja kumsalimia Rais Jakaya Mrisho  Kikwete  kumsabahi na kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa uhuru na amani, huku akiondoka madarakani akiwa mtu mwenye furaha. TB Joshua amepongeza Rais Kikwete pia kwa kupata Dkt Magufuli kama mrithi wake, akimtaja Rais huyo mpya mteule kama Rais wa Tanzania wa Baraka na Fanaka tele katika awamu hii mpya.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Mtume TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii. TB Joshua ametua jijini Dar es salaam  tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mtume TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii.
Picha na Freddy Maro.

 Dkt Magufuli ampokea TB Joshua Uwanja wa ndege Dar jioni hii. Mhubiri huyo aliyekuja na watu 40 kwa ndege yake mwenyewe, amekuja kushuhudia Dkt Magufuli akiapishwa

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MAALIM SHARIFF SEIF HAMAD

0
0
 Rais Jakaya Kikwete ateta na makamu wa Kwanza  wa Rais  wa Zanzibar Maalim Shariff Seif Hamad kuhusu hali ya kisiasa Visiwani leo  asubuhi  Ikulu jijini dar es Salaam
Wakiwa katika picha ya pamoja.

VYUMBA VYA KUPIMIA NGUO KABLA YA KUNUNULIWA KATIKA SOKO LA MCHIKICHINI MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM VILITUMIKA KUDHALILISHA WANAWAKE

0
0

Wawezeshaji wa Sheria katika soko la Mchikichini katika Manispaa ya Ilala, wakiwa na mabango ya mradi wa Mpe Riziki si Matusi baada ya kuzungumza na waaandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wanaotembelea masoko yaliyopo katika Manispaa hiyo kuona maendeleo ya vita ya  kupinga udhalilishaji wa kijinsia katika masoko hayo baada ya Shirika la Equality for Growth linaloendesha mradi huo kutoa mafunzo kwa Wawezeshaji wa Sheria wanaoshirikiana na wafanyabiashara katika vita hivyo.
Mwezeshaji wa Sheria, Eva Kakobe akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya ukatili wa jinsia wanavyokabiliana nayo katika soko hilo.
Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo, Charles Beatus akichangia kuhusu mwongozo wa kutoa adhabu kwa wanaobainikwa na makosa ya udhalilishaji. Kushoto ni Mtaalamu wa kujitolea wa  masuala ya kijinsia kutoka nchini Canada, Ashley Ekelund.
Mwezeshaji wa kisheria katika soko hilo, Domitila Ngwada akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mjumbe wa Bodi ya Sekta ya Kanga na Vitenge katika soko la Mchikichini Manispaa ya Ilala, Zainabu Namijojo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo asubuhi, ambao wapo katika ziara ya kutembea masoko ya Manispaa ya Ilala kuona jinsi mradi wa Mpe Riziki si Matusi ulivyowakomboa wanawake katika vita ya kupinga udhalilishaji masokoni unaoendeshwa na Shirika la Equality for Growth (EfG). Kulia ni Mwezeshai wa Sheria katika soko hilo, Nechi Omar.
Mfanyabiashara wa vitenge na magauni, Sophia Kizinga akichangia jambo kuhusu kupungua kwa ukatili wa jinsia katika soko hilo.
Mfanyabiashara, Ikram Zubery (katikati), akizungumza na waandishi wa habri kuhusu ukatili wa kijinsia katika soko hilo.
Mama Lishe katika soko hilo, Edwiga Assenga (wa pili kulia), akizungumza na wanahabari waliotembelea soko hilo.

Na Dotto Mwaibale

VYUMBA vilivyokuwa vikitumiwa kwa ajili ya kupimia nguo kabla ya kuzinunua katika soko la Mchikichini Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam vinadaiwa vilikuwa vikitumia kudhalilidha wateja hasa wanawake.

Hayo yamebainishwa na Mjumbe wa Bodi ya Sekta ya Kanga na Vitenge katika soko hilo Zainabu Namijojo Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao wanafanya ziara ya kutembea masoko ya Manispaa ya Ilala kuona jinsi mradi wa Mpe Riziki si Matusi ulivyowakomboa wanawake katika vita ya kupinga udhalilishaji masokoni unaoendeshwa na Shirika la Equality for Growth (EfG).

"Katika soko letu tulikuwa na changamoto kubwa ya udhalilishaji hasa maeneo ya wauza nguo kuu kuu (Mitumba), kwani walikuwa wakitumia vyumba vidogo vya kujaribishia nguo kuwadhalilisha wanawake kwa kuwakamata maungoni na kuwawekea kioo chini ili waweze kuona utupu wao" alisema Namijojo.

Alisema hivi sasa vitendo hivyo vimekoma baada ya shirika hilo kufanya matamasha na semina mbalimbali na kutoa mafunzo kwa baadhi yao ambao sasa ni Wawezeshaji wa Sheria katika soko hilo ambao wamekuwa karibu na wafanyabiashara kufuatilia vitendo vya udhalilishaji.

Mwezeshaji wa Sheria Domitila Ngwada alisema vitendo vya ubakaji na matusi ya nguono yalishamiri sana lakini hivi sasa hali ni nzuri kwani vitendo hivyo vimepungua kwa asilimia 70 ukilisha na hapo awali kabla ya kufikiwa na EfG.

"Tangu kuwepo na wawezeshaji wa Sheria katika soko letu vijana wengi waliokuwa na vitendo vya kudhalilisha wanawake wameingiwa na hofu kubwa hasa kupigwa faini zilizowekwa kuanzia kiwango cha sh.50,000" alisema Ngwada.

Mfanyabiashara katika soko hilo, Ikram Zuberi alisema jitihada za makusudi zinapaswa kufanyika ili kumaliza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia katika sokjo hilo ingawa kwa kiasi kikubwa vimepungua kwa msaa wa EfG.

Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo Charles Beatus alisema wale wote wanaopatika na makosa ya udhalilishaji wamekuwa wakiadhibiwa kutokana na mwongozo uliopo na kesi zote zinaanza kusikilizwa sokoni hapo na ikishindikana upelekwa ngazi nyingine ikiwemo polisi.



ONESHO LA SWAHILI FASHION WEEK LAZINDULIWA JIJINI DAR LEO

0
0
Mwanamitindo wa hapa nchini, Mustafa Assanali kulia na Katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania, Godfrey Mngereza wakifungua pazia kuzindua Onesho la Swahili Fashion Week leo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam aambalo litakuwa na mwendelezo wa kuonesha ubunifu wa mitindo kwa siku tatu mfululizo litakalokuwa likifanyika katika hoteli ya Sea Clief jijini Dar es Salaam.
Mwanamitindo wa hapa nchini, Mustafa Assanali akizunguza na waandishi wa habari leo katika mkutano na waandishi wa habar jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na uzinduzi wa onesho la Swahili Fashion week iliyozinduliwa leo ikiwa tunakaribia mwishoni mwa mwaka Mwanamitindo huyo amesema kuwa katika uzinduzi huo kutakuwa na  siku tatu mfululizo za wanamitindo mbalimbali wataonyesha mitindo, Urembo na mitindo ya maisha katika onyesho litalokuwa likifanyika katika hoteli ya Sea Clif jijini Dar es Salaam.
Pia amesema kuwa onyesho hilo la mavazi lina nia ya kusisitiza jamii kuwa mitindo ni pato linalozalisha tsinia ya ubunifu pia ni kukuza dhana ya bidhaa ya Afrika ikiwa kwa mwaka huu onesho la Swahili Fashion Week ni la nane tangu lianzishwe hapa nchini.
Kushoto ni Afisa Udhamini na matukio wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude akizungumza na waandishi wa habari leo katika mkutano wa uzinduzi wa Onesho la Swahili Fshion Week uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Maneja wa masoko wa kapuni ya magari ya Jaguar hapa nchini, Jennifer Gower.
Baadhi wa habari wakiwa katika mkutano wa uzinduzi wa Onesho la Swahili Fashion Week iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo , Globu ya jamii

DORIS MOLLEL FOUNDATION (DMF) YAANDAA TAMASHA KUBWA LA KUSAIDIA WATOTO NJITI NCHINI, NOV 8 LEADERS CLUB

0
0
DSC_0027
Mwenyekiti wa Mfuko wa Doris Mollel Foundation, Bi. Doris Mollel akiwakaribisha wageni mbalimbali na wanahabari wakati wa utambulisho maalum juu ya tamasha linalotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili Novemba 8, katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu Idara ya Afya, uzazi na watoto, Bi. Georgina Msemo na kulia kwake ni Dk. Sonal Peter ambaye ni daktari wa watoto (Pediatrician) kutoka Hospitali ya Agha Khan. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).

Na Andrew Chale, Modewjiblog
[DAR ES SALAAM] Katika kuadhimisha siku ya watoto njiti duniani, Taasisi ya Doris Mollel Foundation (DMF) imeandaa tamasha la kwanza na la aina yake kufanyika nchini siku ya Jumapili Novemba 8. 2015 kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni kuanzia majira ya asubuhi mpaka saa 12 jioni huku wasanii mbalimbali wakitarajiwa kushiriki kwa ajili ya kuchangisha fedha za kununulia vifaa vya kusaidia watoto wanaozaliwa na uzito pungufu ama watoto njiti.

Akielezea mbele ya wanahabari jijini Dar es Salaam mapema jana, dhumuni la tamasha hilo ni kuwaleta watanzania pamoja kupata uelewa na mwamko katika kuadhimisha siku hiyo muhimu kwa afya na ustakabali wa mtoto njiti ambapo kulingana na takwimu za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, takribani watoto 88,128 walizaliwa njiti au wakiwa na uzito mdogo nchini kwa kipindi cha mwaka 2014/2015 pekee.

“Lengo ni kuhakikisha kupitia Mfuko huu unasaidia watoto njiti hasa kwa vifaa vya kuwawezesha kusaidia maisha yao. Tunataka kufikisha vifaa 10 kwa kila Kanda chache za awali. Karibuni sana watanzania kwa siku ya Jumapili Novemba 8. Kwa kiingilio cha sh 2,000 pekee kama mchango ambapo utapata burudani ya kipekee kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiwemo Barnaba Classic, Mwasiti, kundi la The Voice, Miriam, Baraka De Prince, Ruby, Shilole na wengine wengi.” Amebainisha Doris Mollel.

Aidha, Doris amebainisha kuwa, Watanzania watapata fursa maalum ya kuusikia wimbo ulioimbwa na baadhi ya wasanii hao watakaoshiriki katika tamasha hilo.
DMF imeongeza kuwa, baada ya tamasha hilo, kwa kushirikiana na wadhamini pia itatoa vifaa mbalimbali ikiwemo (Suction machines, Oxygen Concentrators na Feeding tubes) hii ni kwa Hospitali za Mikoa nchini ilikuweza kusaidia watoto hao na vifaa hivyo vinatarajiwa kutolewa katika siku ya kilele cha maadhimisho ya mtoto njiti Duniani huku kwa Tanzania ikitarajiwa kufanyika Mkoani Mbeya.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu Idara ya Afya, Uzazi na Watoto, Bi. Georgina Msemo kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa wizara hiyo amezitaka jamii nchini kujitokeza kwa wingi kusaidia wamama wajawazito wakati wa kipindi chote cha ujauzito kwani kusaidia huko kutapunguza watoto wanaozaliwa kabla ya wakati ama njiti.

“Jamii iwe na huruma kwa wamama wajawazito. Kwani haya yote yanatokea kutokana na wamama wengi wanakuwa wanafanya kazi ngumu kutopatiwa huduma muhimu na hata wengine kutokwenda kliniki… hivyo ni jamii ichukue hatua ya kusaidiana na wajawazito kutatua tatizo hili” alieleza Bi Msemo katika taarifa yake hiyo aliyoitoa wakati wa hafla hiyo ya utambulisho wa tamasha la kuchangia fedha za kusaidia watoto njiti.

Wajue Watoto njiti:
Watoto wanaozaliwa kabla ya muda wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kufa kutokana na magonjwa ya mfumo wa hewa, mfumo wa chakula na mfumo wa fahamu ukilinganisha na watoto waliozaliwa baada ya kutimiza wiki 37 au zaidi wakiwa tumboni mwa mama zao. Watoto njiti pia wapo katika hatari ya kupata matatizo ya kuona, kusikia, kutambua/kiakili na moyo yanayoweza kudumu maisha yao yote. Zaidi ya hapo watoto wanaozaliwa njiti katika nchi zilizo na uchumi duni wapo katika hatari ya kufa mara 10 zaidi ukilinganisha na watoto njiti wanaozaliwa katika nchi zilizoendelea
DSC_0031
Tukio hilo likiendelea.
Tunaweza kupunguza idadi ya njiti
Sababu kuu zinazosababisha hali ya hatari kwa watoto njiti nchini Tanzania na nchi nyingine zenye uchumi mdogo ni maambukizi wakati wa ujauzito, Malaria, VVU, kuzaliwa na uzito mdogo, muda mfupi kati ya uzao mmoja na mwingine na mimba za utotoni. Matunzo sahihi kabla, katikati na wakati wa ujauzito (ikiwemo uzazi wa mpango na huduma wakati wa ujauzito) ni muhimu katika kupunguza kiwango cha uzazi wa watoto njiti. Hata hivyo sehemu kubwa ya sababu zinazofanya watoto kuzaliwa njiti hazijulikani. Hivyo basi tunahitaji kufanyike tafiti zaidi ili kupata uelewa na kudhibiti visababishi vyake.
Tunaweza kupunguza vifo vya watoto wachanga wanaokufa kutokana na matatizo ya kuzaliwa njitiMtoto anayezaliwa njiti sio lazima apewe uangalizi wa karibu (intensive care) na kutumia teknolojia kubwa sana ili aishi. Huduma za gharama nafuu zinazoweza kufanyika ili kuongeza uwezekano wa mtoto mchanga kuishi na kupunguza hatari kwake ya kupata ulemavu wa 
maisha, ni pamoja na zifuatazo:
1.Antenatal steroids,hizi ni dawa ambazo hutolewa kwa akina mama wanapopata uchungu wa kujifungua kabla ya wakati, katika ngazi za afya zinazostahili, husaiidia kukuza mapafu ambayo hayajakomaa ya mtoto njiti na kuzuia matatizo kwenye mfumo wa hewa ya watoto wachanga.
2.Huduma ya Mama Kangaruu: Hii ni mbinu ya kumbeba mtoto mchanga kwenye kifua cha mama yake wakigusana ngozi kwa ngozi ili kumpa joto na kurahisisha unyonyeshaji. Ni muhimu kuwapatia joto watoto njiti kwa sababu miili yao ni midogo na hupoteza joto haraka, jambo linalowafanya kuwa kwenye hatari kubwa ya kupata magonjwa mbalimbali, maambukizi na kifo. Inakadiriwa kuwa mbinu hii ya Mama Kangaruu inaweza kuepusha vifo vya watoto 5,000 kila mwaka hapa Tanzania.
DSC_0048
Baadhi ya wasanii waliokuwapo wakati wa utambulisho huo wakifuatilia kwa makini.
3. Kusaidia watoto kupumua kwa kutumia bag na mask, ni huduma muhimu kwa watoto njiti wenye matatizo ya kupumua. Iwapo huduma hii rahisi ya kusaidia watoto wachanga kupumua inapatikana kwa asilimia 90 ya watoto wanayoihitaji, basi takribani maisha ya watoto wachanga 2,000 yangeweza kuokolewa kila mwaka. Mpango wa Kusaidia Watoto Kupumua (Helping Babies Breathe) ulizinduliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii mwaka 2009 kwa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa sekta ya afya katika ngazi zote, ukiwa na lengo la kupunguza vifo vya watoto wachanga vinavyotokana na matatizo ya kupumua. Wadau wa afya mbalimbali wameshirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika kutekeleza mpango huu.
4.Kumsaidia mama kuanza kunyonyesha mtoto ndani ya saa moja baada ya kujifungua, hii inahusisha pia kumsaidia mama kukamua maziwa kwa ajili ya mtoto na kumpa kwa kutumia kikombe pale inapo lazimu.
5.Kuzuia, kutambua mapema na kutibu maambukizi:utoaji wa huduma inayozingatia usafi wakati wa mama kujifungua (mfano kuosha mikono, uhudumiaji sahihi wa kitovu na ngozi ya mtoto mchanga) ni muhimu katika kuzuia maambukizi kwa mama na mtoto. Dawa za antibiotiki kama vile Amoxicillin zinaweza kutumiwa kutibu nimonia na Gentamicin kwa ajili ya kutibu maambukizi makubwa yanayowapata watoto wachanga.
Zaidi ya hapo, watoto wote wachanga wanahitaji kukaguliwa afya zao ndani ya masaa 24 na baada ya siku 3 ya kuzaliwa ili kuzuia matatizo yanayoweza kutokea na yale ambayo yanaweza kusababisha ulemavu katika maisha yao ya baadaye.
Huduma bora inahitajika wakati wa kujifungua na hususan kwa watoto wachanga wanaozaliwa na uzito mdogo na wale walio wagonjwa.
 
DSC_0071
Baadhi ya waashiriki hao katika mkutano huo.
“Watoto wachanga wanahitaji kupata huduma muhimu hususan kwa wale ambao wanazaliwa kabla ya muda wao,” anasema Mwakilishi wa Unicef nchini Tanzania Dk. Jama Gulaid.
DMF imetoa pia nafasi ya wazi kwa watanzania kuchangia kiasi chochote kile kupitia M-PESA namba ya kampuni 244444 (Doris Mollel Foundation).
Jinsi ya kuchangia kwa M-Pesa: (1) Piga *150*003# chagua lipa kwa M-pesa (2) Weka namba ya kampuni ambayo ni 244444. (3) Weka kiasi (mfano: Tsh.500, 3200, 7000 na kuendelea kadri ya uwezo wa mchangiaji. (4) Weka namba ya kumbukumbu ambayo ni (2015). Kisha utaweka namba yako ya siri ya M-Pesa (PIN yako ya MPESA) na kisha utabonyeza namba moja kuthibitisha muamala wako na baadae utapokea ujumbe wa maandishi (SMS) kwamba umechangia Doris Mollel Foundation kwenye akaunti michango ya mwaka 2015. (Unaweza kuchangia kiasi chochote mara nyingi uwezavyo.
Aidha, DMF imewashukuru wadhamini mbalimbali wanaoendelea kufanikisha shughuli za kusaidia harakati hizo ikiwemo Vodacom Foundation, Clouds Media Group, Hyatt Regency, NSSF, CBA, NHIF, Coca Cola, Moments productions, Ashton Media, Expo Trading, Viva towers Easy talk, SpiceNet, MillardAyo.com, Modewjiblog na wengine wengi.
DSC_0086
Dk. Sonal Peter ambaye ni daktari wa watoto (Pediatrician) kutoka Hospitali ya Agha Khan akielezea namna ya kuchangia Mfuko huo na kuhamaisha Jamii kujitokeza kwa wingi.
DSC_0096
Wasanii wa kundi la The Voice, Barnaba Classic na wengineo wakiimba kwa hisia wimbo maalum wa kumpa matumaini Mama mjamzito na aliyejifungua mtoto njiti katika kusaidia maisha yake.DSC_0100
DSC_0107
Bi. Doris Mollel akiwapongeza wasanii hao kwa kumuunga mkono katika tukio hilo likiwemo la kuimba wimbo maalum na pia kutumbuiza siku ya Jumapili Novemba 8.2015.
DSC_0129
Mtangazaji wa Chaneli Ten, Said Makalla akiuliza swali kwa Mwenyekiti wa Doris Mollel Bi Mollel (hayupo pichani).
DSC_0144
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Idara ya Afya, Uzazi na Watoto, Bi. Georgina Msemo (kushoto) akijibu swali la Said Makalla (hayupo pichani).
DSC_0137
DSC_0090
DSC_0088
Kundi la The Voice wakiimba wimbo huo ambapo baadhi ya sehemu walizorekodia ni kwenye wodi ya watoto njiti.

KANU BALOZI MPYA WA STARTIMES BARANI AFRIKA

0
0

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes nchini Naigeria, Bw. Jack Liu (wa pili kulia) akiwa ameshikilia sare ya kampuni hiyo pamoja na mabalozi wapya Jonathan Akpoborie (wa kwanza kushoto) na Kanu Nwankwo (katikati) wakati wa hafla fupi ya kuwatambulisha mabalozi wapya wa kampuni hiyo jijini Lagos Naigeria mwishoni mwa wiki. Wakijumuika kwa pamoja katika tukio hilo ni wafanyakazi wa kampuni hiyo nchini Naijeria Bw. Maxwell Loko na Dare kafar (wa kwanza kushoto).

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes nchini Naigeria, Bw. Jack Liu (wa pili kulia) akiwa ameshikilia sare ya kampuni hiyo pamoja na mabalozi wapya Jonathan Akpoborie (wa kwanza kushoto) na Kanu Nwankwo (katikati) wakati wa hafla fupi ya kuwatambulisha mabalozi wapya wa kampuni hiyo jijini Lagos Naigeria mwishoni mwa wiki. Wakijumuika kwa pamoja katika tukio hilo ni wafanyakazi wa kampuni hiyo nchini Naijeria Bw. Maxwell Loko na Dare kafar (wa kwanza kushoto).




Na Mwandishi Wetu, Naigeria

Katika kuhakikisha huduma za dijitali zinafurahiwa na zinamfikia kila mtu, kampuni ya StarTimes imeingia makubaliano na aliyekuwa mchezaji nguli wa kimataifa wa soka wa Naijeria, Nwankwo Kanu kama balozi wa shughuli zake barani Afrika.

Akizungumzia juu ya ushirikiano huo Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes nchini Tanzania, Bw. Lanfang Liao amebainisha kuwa, “Mkataba baina yetu na Bw. Kanu ulitiwa sahihi jijini Lagos nchini Naijeria ambako Bw. Kanu alikubali kuingia mkataba kwa miaka mitatu. Hivyo basi balozi wetu huyu mpya atakuwa muwakilishi wa kampuni yetu yenye shughuli zake takribani nchi 12 barani Afrika zikiwemo Naijeria, Tanzania, Kenya, Uganda, Afrika ya Kusini, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na nyinginezo.”

Kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba huo, Kanu sasa atakuwa akishiriki katika shughuli kama vile matangazo, kuhudhuria sherehe za kampuni, matukio na kusaidia kukuza muonekano wa StarTimes barani Afrika pamoja na hamasa kwa watu kuhamia katika mfumo wa dijitali.

Kanu pia atakuwa akisaidiana na aliyekuwa mchezaji wa kimataifa wa soka wa Naijeria, Bw. Jonathan Akpoborie ambaye yeye pia ameteuliwa kuwa mtaalamu wa kupanga vipindi vya michezo na mgeni mulikwa katika uchambuzi wa vipindi vya moja kwa moja. Bw. Akpoborie atakuwa akishiriki kama mchambuzi wa kiufundi wa vipindi vya moja kwa moja vya michezo vitakavyokuwa vikirushwa katika chaneli za StarTimes vikionyesha uchambuzi na makala yakinifu.

Bw. Jonathan Akpoborie ni mchezaji wa zamani wa kimataifa kutoka nchini Naijeria ambaye alitumia muda wake mwingi kucheza soka la kulipwa nchini Ujerumani.

Akifafanua umuhimu wa kumchagua Bw. Nwankwo Kanu kama balozi wa StarTimes Afrika, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu huyo nchini Tanzania amesema kuwa StarTimes ilizingatia sana la mtu ambaye anakaubalika si tu nchini mwake bali katika bara zima la Afrika.

“Ukiachilia mbali mafanikio aliyoyapata Kanu katika medali za kimatifa, umaarufu wake haupo tu nchini kwake Naijeria bali katika bara zima la Afrika. Kanu ni hamasa ya kweli katika historia ya mafanikio ya wanasoka kutoka Afrika kwa kufikia mafanikio makubwa licha ya mazingira magumu. Ni mfano wa kuigwa ambaye kila mtu anaweza kumtazamia kufikia ndoto zake.” Alisema Bw. Liao

Aliongezea pia, “Wakati dunia tayari imekwishahama kutoka kwenye mfumo wa analogia, StarTimes inawekeza vya kutosha, kukusanya rasilimali na kuwahusisha wadau ili kuhakikisha waafrika wanaingia katika mfumo mpya wa matangazo ya luninga kwa dijitali na kuwaunganisha na ulimwengu kwa ujumla. Tunapigania kuwaunganisha watu wengi zaidi, kuwahamasisha na kuwapatia msisimko wateja wetu kote barani Afrika kuhusiana na matangazo ya dijitali.”

Naye kwa upande wake akiwa mwenye furaha Bw. Nwankwo Kanu aliishukuru kampuni ya StarTimes kwa kumuona anastahili kuwa balozi wa kampuni hiyo.

“Ninayo furaha kubwa sana kusaidia kukuza na kuunga mkono shughuli za StarTimes kama balozi wake barani Afrika. Lengo langu ni kuhakikisha kila mwafrika amekuwa amehamia katika matangazo ya dijitali ifikapo mwezi Juni 17, 2017 na nimefurahi kushirikiana na StarTimes katika kulifanikisha hili.” Alisema Bw. Kanu

“Ukiachana na kuwa kapteni mstaafu wa kikosi cha Super Eagles cha Naijeria, Kanu ni mchezaji wa kiafrika mwenye mafanikio lukuki yakiwemo, kushinda medali ya EUFA Kilabu Bingwa barani Ulaya, medali ya kombe la UEFA, medali tatu za washindi wa kombe la FA na tunzo mbili za mchezaji bora barani Afrika hizo zikiwa chache tu zilizoorodheshwa. Pia ni mchezaji wa kipekee kuchezea soka la ligi ya Uingereza kushinda vikombe vya EUFA Kilabu Bingwa barani Ulaya, kombe la UEFA, ligi kuu Uingereza, kombe la FA na medali ya dhahabu ya Olimpiki.” Alihitimisha Bw. Liao

Kanu pia atakuwa akishiriki kwenye uchambuzi wa kina pamoja na wapenzi wa soka kama mgeni rasmi katika matangazo ya moja kwa moja ya mechi za ligi za Bundesliga na Serie A zinazorushwa mahususi katika chaneli za StarTimes.

StarTimes kwa sasa inayo hakimiliki za kurusha moja kwa moja mechi za ligi za Bundesliga (Ujerumani), Serie A (Italia) na Ligue 1 (Ufaransa). Na kwa sasa inarusha moja kwa moja michuano ya FIFA kombe la dunia la vijana chini ya miaka 17 iliyoanza kutimua vumbi Oktoba 18 na kumalizika Novemba 8 nchini Chile.

NEWS ALERT: KESHO ALHAMISI NI SIKUKUU NA SIKU YA MAPUMZIKO

0
0

     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameamua na ameitangaza kesho, Alhamisi, Novemba 5, mwaka huu, 2015, kuwa Sikukuu na siku ya mapumziko. 

     Rais Kikwete amefanya uamuzi huo, ili kuwawezesha Watanzania kushiriki katika sherehe za kuhitimisha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne na kuingizwa madarakani Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muung ano wa Tanzania. 

     Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo Jumatano, Novemba 4, 2015 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Yohana Sefue, Rais Kikwete ametoa uamuzi huo kwa mujibu wa mamlaka aliyo nayo chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa.

 Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.


4 Novemba, 2015

RAIS KIKWETE AMWAPISHA KATIBU TAWALA MPYA WA MKOA WA LINDI

0
0
 Katibu Tawala Mpya wa Mkoa wa Lindi Bwana Ramadhani Kaswa akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
Katibu Tawala Mpya wa Mkoa wa Lindi Bwana Ramadhani Kaswaakipongezwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
(Picha na Freddy Maro)

Kipindi cha JUKWAA LANGU Nov 2, 2015 (Full Show)

0
0
Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali yaihusuyo Tanzania.Wiki hii, tumeangalia zaidi kuhusu mustakabali wa Tanzania baada ya UCHAGUZI MKUU 2015

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MAALIM SHARIFF SEIF HAMAD IKULU JIJINI DAR

0
0

MREMA ACHUKIZWA NA RAFU ZA MBATIA KATIKA JIMBO LA VUNJO

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Agustino Lyatonga Mrema amesema kuwa kushindwa kwake ubunge kulitokana na michezo mchafu uliochezwa na mshindi wa ubunge wa jimbo hilo, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NCCR-MAGEUZI, James Mbatia

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mrema amesema kuwa  mshindi wa jimbo hilo amekuwa akionywa na msimamizi  wa uchaguzi kutokana na matumizi ya vipeperushi ambavyo yeye alijipigia kura ya ubunge katika jimbo la Vunjo.

Mrema amesema matokeo ya yaliyompa ushindi Mbatia hakusaini kutokana na kufanya  hujuma nyingi ikiwa ni pamoja na  kumsema  mgombea mwenzake.

Aidha amesema kuwa  katika kipeperushi chake Mbatia sehemu ya bendera ya TLP yenye alama ya jogoo ilionekana kifaranga baada ya  kuwa na jogoo mkubwa anayewika.

Mrema katika kukutana na waandishi pia alimpongeza Rais Mteule wa CCM, Dk.John Pombe Magufuli kwa kura za kishindo na kutaka kuwa yuko naye.

Amesema kumpigia kampeni Mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli kulitokana na kazi nzuri ya kupeleka barabara katika jimbo lake akiwa Waziri wa Ujenzi.

Mrema katika mkutano wake leo aliambatana na viongozi wa juu wa chama hicho kueleza hujuma alizofanyiwa katika uchaguzi katika jimbo la Vunjo akimhutumu, James Mbatia ambaye ameibuka kidedea katika uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP),Agustino Lyatonga Mrema akizungumza leo na waandishi habari juu ya kufanyiwa rafu katika jimbo la vunjo na kusababisha kushindwa kulitwa kwa mara nyingine kushoto ni aliyekuwa Mgombea Urais wa TLP ,Maxmillian Lyimo , na Kulia  Katibu Mkuu wa TLP,Nancy Mricaria.
 Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Agustino Lyatonga Mrema akionyesha moja ya kipeperushi kilichomsababisha kukosa jimbo hilo kushoto ni aliyekuwa Mgombea Urais wa TLP, Maxmillian Lyimo , na Kulia  Katibu Mkuu wa TLP, Nancy Mricaria.
 Mwenyekiti wa Umoja Wanawake wa Vunjo,Venancia Nicholaus akizungumza na waandishi juu ya wanawake wa vunjo walivyopata pigo kuungushwa kwa mgombea wao Mrema kwa hujuma za Mbatia kulia ni Mgombea Ubunge Bunda Mjini,Dk.Lucas Webiro leo jijini Dar es Salaam.
 
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti  wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Agustino Lyatonga Mrema leo jijini Dar es Salaaam.
 Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii

NAMNA YA KISHERIA YA KUZUIA MSHAHARA WA MFANYAKAZI KULIPIA DENI LAKO.

0
0
NA  BASHIR  YAKUB - 
Unapomdai  mtu  kupitia  mahakanma  na  hukumu  ikatolewa  kuwa  ni  kweli  unamdai  na  anastahili  kukulipa basi  mtu  huyo  hustahili  kulipa.  Lakini  mara  kadhaa  hutokea  mtu  kusema  sina  hela  ya  kulipa  au  vinginevyo  ilimradi  tu  asilipe  deni.

Lakini  pia  madai  hapa  si  lazima  iwe  hela  tu  inayotokana  na  kukopeshana.  Yapo  pia  madai  ambayo  hutokana  na  mtu  kushinda  kesi. Kwa  mfano   mwanamke  alifungua  kesi  dhidi ya mme  wake  akitaka  matunzo  yake  na  ya mtoto/watoto. Au shauri  limekwisha  na  mtu  aliyeshindwa  ametakiwa  na  mahakama  kulipa  gharama. Au malipo  ya  fidia  na  mengineyo  yote  ambayo  huamuliwa  na  mahakama  kuwa  yalipwe. Haya  yote  unaweza   kuyafanya  yalipwe  kwa  kukamata  mshahara  wa  mhusika  kwa  njia  za  kisheria .

Hatua  hii imeelezwa  katika amri  ya 21  ya kanuni  ya 47  ya  sura  ya  33  ya  sheria  ya  mwenendo  wa  mashauri  ya  madai.

1.HATUA  YA  KUKAMATA  MSHAHARA  WA  MTUMISHI.

Mahakama  inapotoa  hukumu  ikimtaka  mtu  fulani  kutekeleza  jambo  fulani  au  kulipa  kiasi  fulani  kwa  mtu  fulani   amri  hiyo  hutakiwa  kutekelezwa  kwa  hiari  na  si  vinginevyo.  Yule  aliyeamrishwa  hutakiwa kutekeleza  kama  alivyoagizwa  na  ndani  ya  muda  alioelezwa.  Ikiwa  atatekeleza bila  kukosa  basi  hatua  hizi  za  kukamata  mali  zake  ikiwemo  hii  ya  kukamatwa  kwa  mshahara  wake  hazitachukuliwa.  Hii  ni  kwakuwa  atakuwa  ametekeleza  kwa  hiari.  Hatua  za  kukamata  mali  zake  ikiwemo  mshahara  wake  huchukuliwa  ikiwa  kama  njia   ya  kumlazimisha  mtu  kutekeleza  kile  alichokataa  kutekekeza  kwa  hiari .

2.  KUKAMATA  MSHAHARA  WA  MTUMISHI  WA  SERIKALI.

Watumishi  wa  serikali  huwa  na  taratibu  za malipo   ambazo  zipo  tofauti na  taasisi  binafsi.  Lakini  pia hata  ndani  ya  serikali  yenyewe  idara  na  taasisi  nazo  huwa  na taratibu tofauti katika  malipo.  Kwa  mfano wapo  watumishi   ambao  mishahara  yao  huanzia  hazina  na  wapo  ambao  utaratibu  wao  wa  mishahara  hauanzii  huko.  


Hivyo  basi  ikiwa  malipo  ya  mtumishi  huanzia  hazina  basi  mamlaka  za  hazina  zitapewa  taarifa  ya  kimahakama  itakayoeleza  kile  alichofanya  mtumishi   ikiwa  ni  pamoja  na  ile  amri  ya  kukamata  mshahara  wa  mtumishi  kulipia  deni  kwa  mujibu  wa  hukumu  na  tuzo(decree) .  Wahasibu   na  watoa  malipo(cashier)  watalazimika  kufuata  vilevile   kama  ilivyoamriwa  na  mahakama  .

3.  KUKAMATA  MSHAHARA  WA  MFANYAKAZI  ASIYE  WA  SERIKALI.

Ikiwa  mshahara  unaotakiwa  kukamatwa  kufidia  deni  ni  wa  mfanyakazi  asiye  wa  serikali  basi  taarifa  rasmi  itatolewa  kwa  mwajiri  wake  kama  ni  kampuni,  asasi   ya  kiraia  au  vinginevyo.  Mwajiri  atatoa  taarifa  hiyo  kwa  afisa  anayehusika   na  malipo   ili  kuanzia  hapo  mshahara  wa  mhusika utumike  kulipia  deni  kwa  mujibu  wa  agizo  la  mahakama.

4.  KUKAMATA  MSHAHARA  NUSU  AU WOTE.

Kwa  mujibu  wa  sheria  niliyotaja  hapo  juu mshahara  wa  mfanyakazi  unaweza  kukamatwa  wote  kwa  ujumla  wake  au  sehemu  yake  kutegemea  na  maamuzi  ya  mahakama.  Ikiwa  deni ni kubwa  sana  basi   inaweza  kuamuliwa   kuwa  kiasi  fulani  kiwe  kinakatwa  kila  mwezi   labda  kwa  kipindi  cha  miaka  miwili  au  mmoja  kutegemea  na  deni lenyewe.  Au  kama   mshahara  ni  mkubwa  na  upo  uwezekano  wa  kulipa  deni  kwa   mkupuo  mmoja(single installment)  na  likaisha  basi  inaweza kuamuliwa   mshahara  ukamatwe  wote  na  ulipie  deni  kwa  mkupuo  mmoja  ili  deni  liishe  kabisa.  

Hata  hivyo  katika  mashauri  yanayohusisha   familia  kama  matunzo  ya  watoto,  ada,  mavazi, malazi  na  matunzo  ya  mwanamke  mara  nyingi huwa inaamriwa  kiasi  fulani  kila  mwezi  kikatwe  na kiingie  katika  akaunti  ya  mwanamke   au  kipelekwe  mahakamani kwa  ajili  ya  matunzo  kwa   familia hiyo.

5.  MALIPO  KUFANYIKA  HATA  KAMA  MFANYAKAZI  YUKO  NJE  YA  MKOA.

Ikiwa  kesi  imefunguliwa  mkoa  fulani  na  mfanyakazi  anakofanyia  kazi  ni  mkoa  mwingine   bado  hili  halizuii  mshahara  kukamatwa.  Popote  anapofanyia  kazi   na  popote  ofisi  yake  ilipo  mshahara  utatakiwa  kukamatwa   na  kulipia  kile  anachostahili  kulipia. Yote  hayo   ni  kwa  mujibu  wa  amri  ya 21  ya kanuni  ya 47  ya  sura  ya  33  ya  sheria  ya  mwenendo  wa  mashauri  ya  madai.

MWANDISHI   WA   MAKALA  HAYA   NI   MWANASHERIA  NA  MSHAURI   WA  SHERIA  KUPITIA  GAZETI  LA  SERIKALI   LA   HABARI   LEO  KILA  JUMANNE  , GAZETI  JAMHURI   KILA  JUMANNE  NA  GAZETI  NIPASHE  KILA  JUMATANO.    0784482959,        0714047241              bashiryakub@ymail.com

                                           TANGAZO   MUHIMU                                                
VIWANJA     NA     NYUMBA          ZINAUZWA.
·         
WANASHERIA   WETU   WATAKUANDALIA   MIKATABA  YOTE  BURE  NA  KUKUSIMAMIA  MPAKA   MANUNUZI    YAKAMILIKE   BURE.
·         
UHALALI   WA  NYARAKA   NA   UMILIKI   UMETHIBITISHWA  NA                  WANASHERIA  WETU.
·         
UTAPEWA  MTU  WA  KUKUSAIDIA  KUFANYA  TRANSFER   KWA HARAKA  BURE.
·         
IKIWA   UTATOKEA   MGOGORO  NDANI   YA  MWAKA  TANGU  TAREHE  YA       MANUNUZI    UTAPEWA   WAKILI   WA   KUSIMAMIA  MGOGORO    BURE
0784482959.

NGOMA AFRICA BAND JUKWAANI MJINI BREMEN,UJERUMANI JUMAMOSI 7 NOV 2015

0
0


Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-ughaibuni yenye makao nchini Ujerumani ,itatumbuiza mjini Bremen,Ujerumani.

siku ya jumamosi 7 November 2015,katika ukumbi wa Weserterrasse, uliopo
mtaa wa Osterdeich 70b, D- 28205 Bremen kuanzia saa usiku, onyesho hilo limeandaliwa na Pan-African Org tawi la Bremen ambalo linasherekea miaka 10 ya kuanziswa kwake.

Bendi ya Ngoma Africa band kwa sasa wanatamba na CD yao mpya La Mgambo na pia song lao jipya waliloliachia juzi tu
"Mapenzi ya Pesa" nyimbo zote hizo zinapasua anga ya kimataifa
unaweza pia kusikiliza at www.ngoma-africa.com

MALALAMIKO YA MAHAKAMA YA MWANZO KUTATULIWA KAMATI MAADILI–DC MAKONDA

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (Pichani) amesema wananchi ambao hawajaweza kupata haki zao katika mahakama za mwanzo wanaweza kutumia kamati ya maadili.

Makonda ameyasema leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Makonda amesema kuwa watu wengine wanakosa haki katika mahakama na hawajui wanaweza kupata haki sehemu gani kutokana na mwenendo wa kesi ilivyoendeshwa.

Makonda amesema kamati hiyo inawajibu wa kuangalia mwenendo wa maadili ya hakimu na ikibanika kamati inaweza kuchukua hatua.

Amesema kuna baadhi ya wananchi wanapewa hukumu za kesi lakini mwenendo wa kesi haujui na mwisho wa siku anakosa haki kutokana na baadhi ya watu kutumia mahakama vibaya.
Makonda amesema sharia ya Usimamizi wa Mahakama  Na.4 ya mwaka 2011 sehemu 51(1) kutakuwa na kamati ya mahakama ya wilaya  ambayo mwenyekiti wake ni Mkuu wa Wilaya.

 Aidha amesema wengine wanaounda kamati hiyo ni Hakimu Mkazi wa Wilaya au msimamizi wa Wilaya ,Katibu wa Tawala wa Wilaya  (DAS) ambaye anakuwa Katibu wa Kamati hiyo,Kiongozi wa dini mmoja ambaye atateuliwa na Mkuu wa Wilaya ,mtu mashuhuri wa wilaya ambaye ni mwadilifu.
Hata hivyo amesema katika kamati hiyo maafisa wawili watateuliwa na Jaji  anayesimamia .
Kamati hiyo itawajibika kupokea na kuchunguza malalamiko yaliyowasilishwa na wananchi kuhusu mahakama na kuwasilisha ripoti kwa tume.

Serikali yatoa Ufafanuzi juu ya uzushi wa kifo cha Rais wa Awamu ya Tatu

0
0

Na Georgina Misama-MAELEZO
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Assah Mwambene amekanusha taarifa za uzushi zinazosambazwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kuhusu kifo cha Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Bw. Mwambene amesema kuwa Mhe. Rais Mkapa ni mzima na mwenye afya nzuri   anaendelea na shughuli zake kila siku kama kawaida.
“Mhe. Rais Benjamin William Mkapa ni mzima hajafariki, wala haumwi na si jambo jema kumzushia tukio hilo kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria na nawasihi msiendelee kusambaza ujumbe huo” alisisitiza Mwambene.
Aidha, katika mkutano huo Mwambene aliwashukuru wahariri, waandishi wa vyombo vyote vya habari na mitandao ya kijamii kwa ujumla kwa kuonyesha moyo wa uzalendo katika kipindi chote ambacho Taifa limekuwa katika mchakato wa uchaguzi na mpaka sasa ambapo serikali inaendelea na maandalizi ya sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Awamu ya Tano, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Mwambene amesema mpaka sasa maandalizi ya sherehe hizo yanaendelea vizuri, zaidi ya Marais 15 kutoka nchi mbalimbali wamealikwa baadhi wameshawasili nchini na wengine wanaendelea kuwasili.
Sherehe za kuapishwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Tano zitafanyika kesho tarehe Novemba, 5 mwaka huu katika uwanja wa Uhuru.

OMARY KIGODA AONGOZA KURA ZA MAONI JIMBO LA HANDENI MJINI

0
0
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images