Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

WATU MILIONI 14 WANUFAIKA NA HUDUMA YA MATIBABU YA MABUSHA NA MATENDE TANZANA- DKT. MWELE

$
0
0

Dk. Mwele Malekela ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa NIMR akifungua Mjadala juu ya Utafiti wa udhibiti wa ugonjwa wa mabusha na matende kwa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Wilaya 94 zimefikiwa katika zoezi la unyweshaji dawa za Matende na Mabusha  na utoaji elimu linaloendeshwa chini ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti magonjwa yasiyopea kipaumbele (NTD) unaoratibiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Baadhi ya washiriki ambao ni watafiti wakifuatilia mada za mjadala huo.
Dk. Upendo Mwingira akitoa mada yake juu ya matumaini ya kutokomeza Ugonjwa wa Matende na Mabusha hasa kufuatia utafiti wake Wilayani Tandahimba.
Mmoja wa watafiti
Sehemu ya washiriki wakifuatilia majidiliano hayo juu ya ugonjwa wa matende na Mabusha.Na Mroki Mroki wa Father Kidevu Blog Arusha.


Mkurugenzi Mkuu wa NIMR Dakta Mwelecele Malecela ameyasema hayo mjini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika Kongamano la 27 la taasisi hiyo la  Sayansi la Kongamano la Pili la Afya Moja Afrika  linaloendelea mjini humo.

Dk. Malecela amesema watu milioni 14 wamenufaika na huduma ya matibabu ya mabusha na matende  katika wilaya hizo 94 ambazo zimefikiwa katika zoezi la ugawaji dawa na tiba.

Aidha alieleza kuwa katika wilaya ya pangani jumla ya watu mia mbili waliokuwa wanasumbuliwa na mabusha wamepatiwa tiba kwa njia ya upasuaji na tayari wamerejea katika hali ya kawaida na kuweza kuendelea na shughuli za maendeleo ya jamii yao.

Dk. Malecela amesema Programu ya kudhibiti Metende na Mabusha imeandaa mkakati maalum wa elimu kwa umma utakaowawezesha watanzania kupata elimu na mbinu za kuwawezesha kushiriki harakati za kitaifa za kutokomeza magonjwa hayo nchini ambayo yameleta hofu na mashaka katika jamii kufuatia imani potofu.

Mkurugenzi Mkuu huyo wa NIMR ameitaka jamii kushiriki katika zoezi la unyweshaji dawa kwa miaka mitano mfululizo bila kuchoka ili kuweza kumaliza dozi na hiyvo kuweza kujikinga na maambukizi na hatimaye kutokomeza magonjwa hayo.

Dk. Malecela amesema Wilaya ya Tandahimba, mkoani Lindi imefanikiwa  kupunguza wagonjwa wa matende na mabusha na kufikia kiwango cha chini ya asilimia moja kutokana na  jitihada za pamoja zinazoendelea za kutokomeza magonjwa hayo chini ya Mpango wa Taifa wa Kutokomeza magonjwa yasiyopewa Kipaumbele.

Pamoja mbu wa malaria aina ya Anopheles, ugonjwa wa Matende na mabusha pia huambukizwa kwa na mbu aina ya  Culex. 

Magonjwa haya  pia husababishwa na minyoo inayoishi kwenye damu na maji damu ambayo husababisha madhara makubwa kwenye miguu ,matiti, mikono na makende.

Mbu aina ya Anopholes huweka mazalia yake katika maji yaliyotuama ambapo Culex huweka mazalia yake katika maji machafu yakiwwemo yale katika mashimo ya choo na madimbwi.

Aidha Dk.Mwele amesema kuwa serikali imefanya jitihada kubwa sana kwani mfuko wa rais wa kupambana na matende na mabusha umeonyesha mafanikio makubwa na kuwezesha watu kupata matibabu kwa njia ya upasuaji.

Wagonjwa 480 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa mabusha katika mkoa wa Lindi katika mwa huu, ambapo wagonjwa 54 kati yao wamekwishafanyiwa upasuaji huo Mwezi April mwaka huu.
Watoa mada mbali mbali kutoka nchi za Afrika wakitoa mada zao juu ya Tathmini ya ugonjwa wa Mabusha na Matende katika nchi zao.

2003 Toyota Noah... FOR SALE BY OWNER

DRESS CODE:WOMEN IN BALANCE KITCHEN PART GALA

$
0
0

kitchen party gala ni tarehe 27 april jumamosi katika ukumbi uliopo jengo la golden jubelee gorofa ya tano.Jengo lipo mjini pembeni ya ppf tower.Kuanzia saa tano asubuhi mpaka saa kumi na mbili jioni kwa wanawake tu.

Tanzania yapokea shilingi bilioni 314 kutoka Benki ya Dunia

$
0
0

Waziri wa Fedha Mhe Dkt. Wiliam Mgimwa pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier wakati wa kusaini mikataba hiyo.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria Bi. Susan Mkapa pamoja na wanasheria wa Benki ya Dunia wakifuatilia kwa makini wakati Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mgimwa pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier wakitia sahii mikataba hiyo.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa wakibadilishana mkataba na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier. Picha na mdau Ingiahedi mduma.Picha na Ingiahedi Mduma na Eva Valerian - Washington DC.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yapokea shilingi bilioni 314 kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kusaidia miradi ya Umeme, Gesi, Bajeti ya Serikali pamoja na kuwajengea uwezo wa kuendesha miradi ya gesi. Mkataba huo umesainiwa leo na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt Wiliam Mgimwa Waziri wa fedha, pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier Mjini Washington DC.

Bi Kidude's State Burial in Zanzibar

AWEP TANZANIA YAZINDULIWA RASMI LEO

$
0
0
 African Women Entreprenuership Programme (AWEP) Tanzania Chapter imezinduliwa rasmi jioni hii katika hoteli ya Double Tree,mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Viwanda na Biashara ,Abdallah Kigoda ,pamoja na Balozi wa Marekani nchini  Alfonso Lenhardt
 Hii ni Ngao iliyobidhiwa rasmi na Sylvia Banda  ambaye ni balozi na mwenyekiti wa AWEP Zambia ,kudhihirisha kuwa AWEP Tanzania imezinduliwa rasmi kwa kuikabidhi kwa Mgeni rasmi wa Waziri wa Viwanda na Biashara ,Abdallah Kigoda na Balozi wa Marekani nchini ,Alfonso Lenhardt
 Madam Sylvia Banza, Balozi wa AWEP Zambia akiikabidhi ngao hii , ambayo nae alikabidhiwa na Mama Bill Clinton alipoizindua AWEP Zambia mwaka juzi
                                         Mwenyekiti wa AWEP Tanzania, Bi Flotea Masawe.
              Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt,  ambao ni wafadhili  wa AWEP  katika mkakati wake wa kuwakwamua wanawake  wajasiriamali wa Afrika
                    Waziri Abdallah Kigoda akiwasili katika hafla ilofanyika jioni hii, na kuhudhuriwa na wanachama kutoka sehemu mbalimbali nchini, ambao baadhi walikuwa katika mafunzo ya kujifunza ujasiri amali ambao unalengo la kuwafanya wawekezaji
Mama Lowasa pamoja na Balozi Maajar walihudhuria uzinduzi huu wa AWEP Tanzania
Baadhi ya wanachama wa AWEP Tanzania Chapter katika picha ya pamoja na mgeni rasmi sambamba na Balozi Alfonso
burudani ilikuwa toka kwa Makumbusho Traditional Dancers

Kinana azungumza na wakulima wa miwa Turiani Mtibwa leo

Haleluya Collection kuzinduliwa Septemba

$
0
0

KAMPUNI ya Msama Promotions inatarajia kufanya uzinduzi mkubwa wa albamu ya sita ya Haleluya, ambayo inawahusisha wanamuziki wa Injili wa nchi za Afrika Mashariki. Uzinduzi wa albamu hiyo unatarajiwa kufanyika Septemba mosi mwaka huu, ambapo kutakuwa na wanamuziki mbalimbali wa muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya nchi ambao watausindikiza uzinduzi huo.

Akizungumza leo jijini Dar, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama amebainisha kuwa maandalizi ya albamu hiyo yanakwenda vizuri na wanauhakika wa kufanya mambo mazuri zaidi. “Tumeshaanza maandalizi ya Haleluya Collections, tumejipanga kutoa albamu bora iliyoshiba, itakuwa ni albamu kali ya muziki wa Injili nchini na Afrika kwa ujumla,”alisema Msama.

Alieleza kuwa uzinduzi huo utafanyika pia kwenye mikoa zaidi ya saba, ambapo utaratibu wa kuteua mikioa hiyo bado unaendelea. Alisema uzinduzi huo utakuwa ni wa CD na DVD na albamu hiyo itakuwa imebeba nyimbo zaidi ya tano.

Bendi ya Ras Inno yakamilika, kuzinduliwa mwezi ujao

$
0
0

HATIMAYE bendi ya nguli wa muziki wa reggae nchini, Ras Inno Nganyagwa imekamilika na anatarajia kuizindua rasmi mwezi ujao jijini Dar es Salaam.

Ras Inno ambaye ni mshindi wa tuzo nne za mwanamuziki bora wa reggae Tanzania, amesema bendi yake hiyo ina wanamuziki 11 na itazinduliwa katika hafla maalumu katika ukumbi utakaotangazwa hapo baadaye.

Amasema nia ya kuanzisha bendi hiyo ni kuwa na ufanisi bora zaidi wa kufanya kazi zake za muziki, kwani bendi ya kudumu na wanamuziki wa kudumu hujenga ‘patern’ ambayo ni sawa na wachezaji waliozoeana uwanjani.

“Hiyo hulinda ladha ya nyimbo husika kutobadilika kila show, pia uhakika wa kufanya kazi njema nje ya nchi. Lakini pia kuwa na bendi huhakikisha upatikanaji wa tija ya kudumu, tofauti na ukiwa ‘solo’ tu bila jina la bendi kazi huja kwa misimu kutokana na mazoea ya hapa kwetu Bongo,” amesema.

Amesema bandi hiyo ni mojawapo ya miradi iliyo chini ya usimamizi wa taasisi yake mahsusi ya kuupromoti muziki wa reggae, kwa ushirikiano na wadau wengine miongoni wa mitindo mingine kwa kuzingatia weledi.

“Taasisi inaitwa Reggae Production House ambayo itahakikisha uzalishwaji wa vipaji vipya vya vijana wanaotaka kuingia kwenye reggae, kwa kufuata njia sahihi itakayowajenga kuwa wanamuziki bora wa reggae nchini watakaoweza kufanya kazi kimataifa. 

“Dhima nzima ni kuufufua muziki wa reggae hapa nchini si kwa kuwa umekufa, la hasha, ila kuna mazingira yanayoufanya muziki huu uonekane kama haupo, lakini mahitaji yapo na mashabiki wana hamu kubwa nao.”

Aidha ameongeza kusema kwamba, ukimya wake wa muda mrefu una sababu kadhaa zikiwemo za kibinafsi kimaisha, lakini muda aliokuwa nje ya ulingo, ameyasoma vyema mazingira yanayoukabili mtindo wa reggae hivyo naamini ana dozi ya kuutibu.

“Ninayodhamiria kuyafanya kupitia taasisi yangu na vitengo vyake ikiwemo bendi, havijapata kuonekana kabla kwenye tasnia ya reggae hapa nchini. Hivyo basi naamini mwanzo huu wa mapinduzi, utaungwa mkono na wadau wote wenye mapenzi mema.”

Ujumbe wa Tanzania wawakilisha mpango wa maboresho ya maendeleo kwa Benki ya Dunia.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia katikati akifafanua jambo wakati wa majadiliano, kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier.
  Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier akifafanua jambo katika majadiliano hayo.
  Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr. Silvacius Likwelile pamoja na Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dr. Philip Mpango akiwasilisha mpango wa maboresho katika Elimu, Maji, Nishati, Usafirishaji, Rasilimali Fedha na Kilimo.
  Ujumbe wa Tanzania ukuiwasilisha mpango wa maboresho ya maendeleo kwa Benki ya Dunia. Mpango huo unahusu maendeo katika  maeneo ya Elimu, Maji, Nishati, Rasilimali Fedha, Kilimo na Usafirishaji.
 Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia katikati akifafanua jambo wakati wa majadiliano, kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier.
  Ujumbe wa Tanzania ukuiwasilisha mpango wa maboresho ya maendeleo kwa Benki ya Dunia. Mpango huo unahusu maendeo katika  maeneo ya Elimu, Maji, Nishati, Rasilimali Fedha, Kilimo na Usafirishaji.
 Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier akifafanua jambo katika majadiliano hayo.
 Ujumbe kutoka Benki ya Dunia wakifuatilia kwa makini wakati Dr. Mpango akiwasilisha mpango wa maboresho hayo.
 Kutoka kulia ni Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Dr.Mpango akijibu hoja mara baada ya kuwasilisha mpango wa maboresho. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr. Silvacius Likwelile na Kaimu Balozi  Ubalozi wa Tanzania Washington DC Bibi Lily Munanka. 
Kutoka kulia ni Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Dr.Mpango akijibu hoja mara baada ya kuwasilisha mpango wa maboresho. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr. Silvacius Likwelile na Kaimu Balozi  Ubalozi wa Tanzania Washington DC Bibi Lily Munanka. Picha zote na Bi. Ingiahedi Mduma na Bi. Eva Valerian – Washington DC

Kinana amaliza ziara yake morogoro vijijini,akagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Meneja Mradi wa mashamba ya Mfano ndani ya kijiji cha Pangawe,wilaya ya Morogoro vijijini,Bwa.Kim Sun Ho wa KOICA walipokuwa wakitembelea Shamba hilo lenye Wakaazi  wapatao 180,ambao wanasimamiwa na kupewa mafunzo ya Kilimo cha kisasa na ufugaji bora kutoka kwa shirika la Maendeleo la Korea (KOICA).

Kinana na Ujumbe wake wa chama hicho walitembelea mradi huo katika ziara yao ya kichama,Wakaazi hao wanamiliki zaidi ya hekari 150 kila mmoja ana magunia  nane ya mahindi waliyovuna mwaka jana huku wakiwa na na kiasi cha shilingi milioni 50 benki.CCM imefanya  ziara katika Wilaya ya Morogoro vijijini na kufungua mashina na matawi ya chama hicho huku akipokea wanachama wapya waliojiunga na waliotoka vyma vya upinzani.

 Sehemu ya Shamba la mfano la Mahindi.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa Meneja Mradi wa KOICA,Bwa.Kim Sun Ho wa KOICA,alipotembelea mradi wa majengo yatakayotumika katika mafunzo ya ufugaji wa kisasa katika kijiji cha Pangawe,Wilaya ya Morogoro Vijijini.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akijadili jambo na Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi CCM,Nape Nnauye walipotembelea mradi wa majengo yatakayotumika katika mafunzo ya ufugaji wa kisasa katika kijiji cha Pangawe,Wilaya ya Morogoro Vijijini.

Pichani ni Sehemu ya soko la Kisasa la Mkuyuni linalojengwa na CCM kwa gharama ya shilingi milioni 100,katika kata ya Mkuyuni,ndani ya Morogoro Vijijini.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurlhaman Kinana akiangalia kazi za ujasiliamali zinazofanywa na mkazi wa kijiji cha Makuyuni,Mkaazi huyo ameamua kujiajiri kuwa kutengeneza mafagio ya njiti na kuyauza kwa wananchi wa eneo hilo,kwa ajili ya kujiongezea kipato.

 Ndugu Kinana na ujumbe wake wa CCM wakielekea kukagua ujenzi unaoendelea wa kituo cha afya (zahanati) ya  Mkuyuni.
 Ujenzi wa jengo la kituo cha zahanati ya Mkuyuni ukiendelea  . 
 Mmoja wa Wahudumu wa kituo cha afya cha Mtamba-Matombo wilaya ya Morogoro Vijijini, kilichopandishwa hadhi na kuwa Zahanati,Bi.Lilian Peter Haule akitoa maelezo mafupi ya maendeleo ya upanuzi wa ujenzi wa  zahanati hiyo ya Mtamba kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurlhaman Kinana.

 Ndugu Kinana akikamkabidhi kadi mpya,katibu kata wa Kiroka kutoka chama cha CUF,Hadim Omary,Wilaya ya Morogoro Vijijini.
Mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Kiroka akikabidhi kadi na bendera ya chama hicho kwa Ndugu Kinana,na kuwapokea kama wananchama wapya wa chama cha CCM na kuwakabidhi kadi mpya.





 Wakazi wa Kata ya Kiroka,wakishngilia jambo walipokuwa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman alipozungumza nao mara baada ya kuzindua jiwe na la msingi la ofisi hiyo. 
 Katibu tawi la Gumba kutoka chama cha CUF,Said Almas akirejesha kadi yake ya na kupokea kadi mpya ya CCM,akijiunga kuwa mwananchama mpya kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrhman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurlhaman Kinana akipewa zana za kimila kutoka kwa Chifu Kingaru wa kabila la Waruguru .
  Wananchi wa Kata ya Mvuha-Matombo wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi wa CCM Nape Nnauye,aidha Ndugu Kinana na ujumbe wa CCM umehitimisha ziara yake ya Morogoro vijijini na leo wataunguruma Morogoro mjini ikiwemo pia kukagua  maendeleo ya miradi ya mbalimbali ya chama hicho ikiwemo na kukiimarisha chama.

Waache waendelee kusema,sisi tunaendelea kuchapa kazi-Kinana.

Kilaji cha Redd's chapambisha shindano la Redds Miss Arusha City Centre 2013.

$
0
0
 Warembo wa shindano la kumtafuta mshindi wa shindano la Redd's Miss Arusha City Centre wakiwa katika mazoezi ya pamoja kujiandaa na shindano lao ambapo jumla ya warembo ishirini na mbili wanatarajiwa kupanda ukumbini kumtafuta mshindi mmoja.

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia afanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom juu ya sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini

$
0
0
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof: Makame Mbarawa akimkaribisha ofisini kwake jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw.Rene Meza ambapo baadae viongozi hao walifanya mazungumzo juu ya masuala mbalimbali katika sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini na mipango ya Vodacom ya kushirikiana na serikali kuboresha zaidi sekta hiyo.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof: Makame Mbarawa akisalimiana na Ofisa Mkuu wa Masuala ya Sheria wa Vodacom Tanzania Bw.Walarick Nittu wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania(katikati)akiwa na ujumbe wake walipomtembelea Waziri Prof:Mbarawa na kuwa na mazungumzo juu ya masuala mbalimbali katika sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini na mipango ya Vodacom ya kushirikiana na serikali kuboresha zaidi sekta hiyo.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof: Makame Mbarawa akisalimiana na Ofisa Mkuu wa Mitandao wa Vodacom Tanzania Bw.Alec Mulugo wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania(kulia)akiwa na ujumbe wake walipomtembelea Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof: Mbarawa na kuwa na mazungumzo juu ya masuala mbalimbali katika sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini na mipango ya Vodacom ya kushirikiana na serikali kuboresha zaidi sekta hiyo.

HUDUMA ZA NSSF ZAVUTIA WENGI KATIKA MAONESHO YA HUDUMA ZA HOSPITALI YA MUHIMBILI

$
0
0
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mh.UmmyMwalimu akimkabidhi cheti Ofisa Uhusiano Hudumwa kwa wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Maife Kapinga wakati wa hafla ya kufunga Maonesho ya Huduma za Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk. Merina Njelekela akisoma hotuba yake wakati wa kufunga maonesho ya Huduma za Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mh.Ummy Mwalimu akisoma hotuba yake wakati wa hafla ya kufunga Maonesho ya Huduma za Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.
Watu mbalimbali wakipata maelezo ya huduma za NSSF ikiwemo Fao la matibabu.
 Baadhi wa wadau waliojitokeza katika maonesho hayo.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mh.UmmyMwalimu akiweka sahihi katika kitabu cha wageni wakati alipotembeklea banda la NSSF. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk. Merina Njelekela.

UMOJA WA WATANZANIA UJERUMANI (UTU) NA SHEREHE ZA MIAKA 49 YA MUUNGANO WA TANZANIA

$
0
0


Mhe.Mfundo,mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania Ujerumani(UTU)
======= ======= ======
UMOJA WA WATANZANIA UJERUMANI (UTU)
Inawakabirisha  katika SHEREHE ZA MIAKA 49 YA MUUNGANO WA TANZANIA 
Mjini Koloni, Ujerumani Jumamosi 27.04 .2013

Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania nchini Ujerumani Bw. Mfundo Peter Mfundo anayofuraha kubwa kuwakaribisha watanzania na marafiki  wa Tanzania kutoka pembe mbali mbali za Dunia katika maadhimisho ya Sherehe Ya Muungano wa Tanzania Bara na Visiwani, zitakazofanyika mjini Koloni hapa ujerumani.siku ya juma mosi Tarehe 27.04.13 kuanzia saa :08:00 za mchana  hadi usiku wa manane.

Katika sherehe hio ambayo  imedhaminiwa na Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) kushirikiana na culture center ya sarakasi. Die Zirkus Fabrik,  kutakuwa na maonyesho ya bidhaa za Tanzania,  na atakayependa anaweza pia kununua bidhaa hizo. 

Ngoma za asili kutoka Tanzania, Mwanamuziki Kongwe Bi.Tabia Mwanjelwa naye atakuwepo,  Msanii wa Bongo Flava Shah Smooth mwenye maskani yake  Dublin,. Kikundi cha Sarakasi kitafanya mavitu yake Live ! na  mwisho watanzania na wageni wote watapata Fursa ya Kuduarika na midundo  kutoka Tanzania kupitia DJ Sudi Mnete wa DW.

Akihojiwa na vyanzo vyetu vya habari mwenyekiti Bw Mfundo Alisema, Madhumuni ya sherehe hiyo sio tu kusherehekea siku kuu ya muungano pekee, bali ni kutimiza moja ya maazimio ya UTU la kuwakutanisha Watanzania wanaoishi nchini humo na kutangaza utamaduni wetu wa Tanzania kwa wenyeji wetu hapa Ulaya. 

Aliendelea kufafanua kwamba moja ya Agenda ya UTU ni kuhakikisha Watanzania wanaoishi nchini Ujerumani wanakuwa pamoja kwa hali zote, wanashirikiana kwa karibu na kusaidiana. Aidha  pia kuhakikisha wasanii wanaoisha hapa ujerumani wanatangaza kazi zao hadharani na wanazitumia kazi hizo kujipatia manufaa zaidi.

Hivyo katika sherehe hii (UTU) imealika wasanii mbali mbali kuja kuonyesha kazi zao. Mwenyekiti alimaliza kwa kuwashukuru wasanii na watanzania ambao tayari wameshajiandikisha kushiriki katika sherehe hiyo kubwa Mjini Koloni,
Umoja ni Nguvu!
KARIBUNI SANA MJINI KOLONI

JIUNGE TIGO RAFIKI UJISHINDIE ASCEND Y200

$
0
0


Mtaalam wa bidhaa za burudani za Tigo Pamela Makai Shelukindo akimkabidhi simu mshindi wa promosheni ya JIUNGE TIGO RAFIKI USHINDE ASCEND Y200 BW Haji Bakar Haji .

Tamasha la Exel with Grand Malt lazinduliwa jijini Dar

$
0
0

Meneja masoko wa kampuni ya bia Tanzania (TBL), Fimbo Buttala akizungumza na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya mkoa wa Dar es salaam kwenye Tamasha la uzinduzi wa kampeni ya kinywaji cha Grand Malt ya kuwashindanisha wanafundi ili kuweza kujinyakulia zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja fedha taslimu ijulikanayo kama Exel with Grand Malt, tamasha hilo lilifanyikia katika viwanja vya chuo kikuu Arthi mkoani Dar es salaam jana.
Mratibu wa tamasha la Exel With Grand Malt,Victor Ndunguru akiongoza ujumbe wa kukagua timu za mpira wa miguu za Chuo kikuu DUCE na chuo kikuu cha Dar es salaa kwenye bonanza hilo lililoshirikisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya mkoa wa Dar es salaam kwenye Tamasha ka uzinduzi wa kampeni ya kinywaji cha Grand Malt ya kuwashindanisha wanafunzi ili kuweza kujinyakulia zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja fedha taslimu ijulikanayo kama Exel with Grand Malt,Timu ya chuo kikuu Dar Es Salaam ilishinda kwa 3-1 tamasha hilo lilifanyikia katika viwanja vya chuo kikuu Arthi mkoani Dar es salaam
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Joh Makini akiwapagawisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya mkoa wa Dar es salaam kwenye Tamasha ka uzinduzi wa kampeni ya kinywaji cha grandmalt ya kuwashindanisha wanafundi ili kuweza kujinyakulia zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja fedha taslimu ijulikanayo kama Exel with grandmalt, tamasha hilo lilifanyikia katika viwanja vya chuo kikuu Arthi mkoani Dar es salaam. 

kinana ahitimisha ziara yake mkoa wa morogoro leo,azindua mradi wa visima vya maji.

$
0
0
 katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia umati wa wananchi katika Uwanja wa Uwanja wa Ndege (zamani sabasaba) mjini Morogoro leo, Aprili 21, 2013, ikiwa ni hitimisho la ziara yake ya siku nane aliyofanya katika wilaya zote, mkoani Morogoro. 


 Baadhi ya maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa CCM kwenye Uwanja wa Kiwanja cha Ndege wa mjini Morogoro, wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokuwa akizunguma Uwanjani hapo. 

Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na uenezi Nape Nnauye akizungumza katika mkutano huo uliwakutaanisha wakazi mbalimbali wa mji wa Morogoro mapema leo jioni wakati chama hicho cha CCM,kilipokuwa kikihitimisha ziara yake ya siku nane mkoani humo.


 
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ajulikanae kw jina la Abdul Nasib a.k.a Diamond akitumbuiza jukwaani jioni ya leo kwenye hitimisho la mkutano wa chama cha CCM,uliofanyika kwenye uwanja wa Ndege (zamani Sabasaba),Mkoani Morogoro.Uongozi wa Chama hicho ukiongozwa na Katibu Mkuu wake,Ndugu Abdulrahman Kinana wamefanya ziara ya kutembelea wilaya zote saba za mkoa huo kukagua uhai wa chama na maendeleo ya miradi mbalimbali.

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, nape Nnauye wakiingia katika Uwanja wa Mkutano wa hadhara wa Kiwanja cha Ndege, mjini Morogoro, leo
 Baadhi ya maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa CCM kwenye Uwanja wa Kiwanja cha Ndege wa mjini Morogoro, wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili Uwanjani hapo.

 Umati ukiwa umefurika kwenye mkutano wa CCM uliofanyika leo April 21, 2013 kwenye uwanja wa Kiwanja cha Ndege wa mjini Morogoro.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji  mkazi wa kata ya Kichangani,Bi.Fatma Said,mara baada ya kuzindua mradi huo kwenye kata hiyo,wilaya ya Morogoro mjini mapema leo mchana.Aidha Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini,Mh Mohammed Aziz Abood alisema kuwa hiyo ni sehemu ya mradi wa visima 23 vilivyochimbwa kwenye Manispaa ya mji huo na kwamba visima hivyo vya maji vimegharimu kiasi cha shilingi Milioni 365.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipewa zawadi ya dumu la sabuni ya maji,inayotengenezwa na kikundi cha akina mama wajasiliamali kiitwacho Chemchem kilichopo mtaa wa Mfungua Kinywa ndani ya kata ya Mwembesongo.Kikundi hicho kimejikita zaidi kwenye ujasiliamali wa kutengeza sabuni,Mradi wa kuweka na kukopa,biashara za mboga mboga.Ndugu Kinana alikichangia kikundi hicho kiasi cha zaidi ya shilinnigi milioni mbili.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipandisha bendera mara baada ya kulizindua shina la kikundi cha akina mama wajasiliamali kiitwacho Chemchem kilichopo mtaa wa Mfungua Kinywa ndani ya kata ya Mwembesongo. 
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikata utepe ndani ya kata ya kichangani kuashiria uzinduzi wa Visima vya maji vipavyo 23 vilivyopo ndani ya Manispaa ya Morogoro mjini,vilivyojengwa na Mbunge wa jimbo hilo Mh Mohammed Aziz Abood wa pili kulia .
Maji yanatoka safi kabisa kwa ajili ya kuwahudumia wanakijiji wa kata ya Kilongo.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na baadhi ya wakazi wa kata ya Kilongo,mara baada ya kuzindua mradi wa maji,kwenye wilaya ya Morogoro mjini mapema leo mchana.Aidha Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini,Mh Mohammed Aziz Abood alisema kuwa hiyo ni sehemu ya mradi wa visima 23 vilivyochimbwa kwenye Manispaa ya mji huo na kwamba visima hivyo vya maji vimegharimu kiasi cha shilingi Milioni 365.

SERIKALI YAPOKEA DOLA ZA KIMAREKANI BILIONI 18.42 KUSAIDIA MRADI WA MAJI MANYARA.

$
0
0
 Waziri wa Fedha Dkt. Wiliam Mgimwa akisaini mkataba wa maji ambao utawasaidia wananchi ya Manyara.
 Waziri wa Fedha Dkt Wiliam Mgimwa akipokea mkataba kutoka kwa mchumi wa Wizara ya Fedha Bw. Patrck Pima.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akibadilishana mkataba na Mkurugenzi  wa OFID kushoto ni Katibu wa Waziri wa Fedha Bw. Omar Khama akiwasikiliza wafanyakazi wa OFID.

Serikali ya Tanzania yasaini mkataba wa jumla ya dola za kimarekani milioni 16 kusaidia mradi wa maji Orkesumet mkoani Manyara. Mkataba huo umesainiwa  leo kati ya Serikali ya Tanzania na OPEC Fund For International Development (OFID) wakishirikiana na BADEA. 

OPEC wametoa milioni 8 na BADEA wametoa milioni 8. Ili kufanikisha mradi huu Serikali ya Tanzania itatoa dola za kimarekali milioni 2.42, Hivyo kufanya mradi huu kufikia jumla ya dola za Kimarekani milioni 18.42.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images