Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

Rais Kikwete akagua Ujenzi Nyumba za Waalimu Mboga Sekondari

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ujenzi wa nyumba za waalimu katika shule ya Sekondari ya Mboga, iliyopo kata ya Msoga wilayani Bagamoyo le0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimwelekeza  jambo Diwani wa Kata ya Msoga Bwana Mohamed Mzimba wakati Rais alipotembelea shule ya Sekondari ya Mboga,kata ya Msoga wilayani Bagamoyo leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mboga kata ya Msoga leo wakati Rais alipotembelea shule hiyo leo kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za waalimu shuleni hapo. Picha na Freddy Maro

Miss Tabata kufanyika Mei 31

$
0
0

Shindano la kumsaka mrembo wa Tabata, Miss Tabata 2013, litafanyika Mei 31 katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.

Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema kuwa shindano hilo litakuwa ni ya aina yake kulinganisha na mashindano ya miaka ya nyuma kwani mwaka huu wamemejitokeza warembo wazuri zaidi.
 
“Warembo wazuri wamejitokeza zaidi kuliko mashindano ya tuliyowahi kuyafanya nyuma. Tutakuwa na burudani nyingi kutoka nje na ndani ya nchi,” alisema mratibu huyo wa Bob Entertainment na Keen Arts.

Warembo watakaoshiriki kwenye shindano wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Da’ West Park.Warembo hao ni Pendo Judica Moshi (20), Madgalena Bhoke (21), Kabula Juma Kibogoti (20), Queen Eliakim Masha (19), Upendo Dickson Lema (22), Martha Gewe (19), Zilpha Christopher (19), Hidaya David (22), Aneth Ndumbalo (19), Amina Ally (18), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Kitereja (19),  Angela Fradius (19), Domina Soka (21), Rehema Kihinja (20), Glory Jigge (18) na Sophia Claud (21).

Wengine ni Lilian Mpakani (19), Lilian Msanchu (19), Rita Frank (20), Pasilida Mandali (21), Rafhel Mussa (19), Jasmin Damian (18), Angelina Mkinga (19), Mercy Mwakasungu (20), Tunu Hamis (19), Brath Chambia (23), Ray Issa (22), Shamim Abass (22) na Shan Abass (22). 
Kapinga aliwaomba warembo wenye sifa kuendelea kujitokeza ili waweze kupata wawakilishi bora katika shindano la Kanda ya Ilala.

"Bado milango iko wazi, mrembo yoyote anayejiamini kwamba ana vigezo anakaribishwa. Tunataka shindano la mwaka huu liwe na ushindani zaidi,” mratibu huyo aliongeza. Warembo 10 watachaguliwa kushiriki mashindano ya Miss Ilala na baadaye Miss Tanzania.

Anayeshikilia taji la Miss Tabata kwa sasa Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala. Waliyojitokeza kudhamini shindano hilo ni Fredito Entertainment, CXC Africa, Brake Point na Saluti5.
 

mwenyekiti wa chadema kata ya Kiroka morogoro vijijini ajiunga na ccm.

$
0
0
Mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Kiroka-Morogoro vijijini  alivyojiunga na CCM,wengine zaidi wahamia na kuwa wanachama wapya

MISS REDD’S ARUSHA CITY CENTRE KUFANYIKA APRIL 4 NDANI YA HOTEL YA KITALII YA SNOW

$
0
0

TOUR VISUAL PROMOTION INAWALETEA:

MISS REDD’S ARUSHA CITY CENTRE NDANI YA HOTEL YA KITALII YA SNOW

CREST HOTEL TAREHE 04/05/2013

BURUDANI:

- Mkali wa Mauno - RACHEL

- Ngoma za Asili

- Live Band

- Madancers Mbalimbali

- Live Entertaiments kutoka kwa Warembo

- Back-up DJ Music from Clouds FM – MAWINGU CLUB

KIINGILIO: V.I.P Seats = TSHS 35,000/=

Normal Seats = TSHS 25,000/=

SHINDANO ILO IMEDHAMINIWA NA:  REDD’S ORIGINAL ,SNOW CREST HOTEL,CLOUDS FM / TV AND MAWINGU CLUB - ARUSHA,MODERN DRIVING SCHOOL,DODOMA WINE,MICHUZI JUNIOR BLOG, MWANDAGO INVESTMENT,BG HORIZON LTD,SIGNATURE MINNING COMPANY, CHELSE TRAVEL LIMITED,CHELSE SOLEX LIMITED,MAMBOLEO,POINT ZONE,MEJA LINK LTD,VICTORIA SUPPORT SERVICES,LITTLE ROSES,WAKIPAMBWA NA JOE MACK FASHION.

Fanya booking yako sasa kupitia number – 0755975454 au 0713681059.

TCME: Mining sector to change Tanzania economic landscape

$
0
0
Mining industry in Tanzania will continue to face various challenges as the country witnesses a growing minerals industry albeit at a slower pace.

According to a report released by the Tanzania Chamber of Minerals and Energy (TCME) during its 18th annual general meeting, the anticipated several new major mines to be brought into production in the next five years, will change the mining sector landscape in terms of the sector’s contribution to the Tanzanian’s economy.

Releasing the report in Dar es Salaam recently, TCME Chairman Joseph Kahama said the new mines will result in a substantial increase in the number of Tanzanians employed in the sector, in government revenues, and will see improvements in the infrastructure and social services in areas related to those mines.

“Depending on fiscal policies and regulatory frameworks and mineral commodity prices it is anticipated that several new major mines will be brought into production in the next five years or so. Once they start operating Tanzania will see a major economic transformation,” he said

Mr. Kahama mentioned one of the anticipated mines to start operations soon to be the Mantra’s Mkuju River project, where he noted that there has been intense debate in the country about the development of uranium mines due to fears associated with the inherent radioactive nature of the mineral.

“It would be worth noting that globally as at November 2012, there were about 434 nuclear power reactors. According to the World Nuclear Association, there will be 650 nuclear reactors operating by 2032.
“Accordingly, yearly reactor related uranium requirements worldwide are forecast to rise to between 98,000 tonnes and 136,000 tonnes of uranium by 2035.

“This presents a great opportunity for uranium developers in the country as there will be a ready market for the concentrate (yellow cake),” said Mr Kahama.

In the meantime, both Mantra and Uranex have been engaging the public in awareness campaigns on the facts of Uranium mining in the surrounding communities and far beyond. With these exciting developments, Tanzania will soon be joining the league of African Uranium producing countries.
Mantra’s Mkuju River project in southern Tanzania had an updated resource of 119.4 million pounds of uranium.
According to Mantra Tanzania's Managing Director Asa Mwaipopo, it will take a two-year period for completing construction work before they could start to produce uranium oxide, and placing Tanzania at number three in Africa in uranium production after Niger and Namibia.
In the sidline of the meeting, Mwaipopo mentioned that the project will provide direct and indirect cash flows in Tanzania in excess of $640 million and will provide foreign direct investment (FDI) in excess of $1 billion or equivalent to 4.76 percent of Tanzania's GDP.

Statistics from the TCME report shows that between 1997 and 2011 a total of USD 10.1 Billion worth of minerals were sold by Chamber members, compared to only USD 16.0 million in 1997. The minerals include gold, diamonds, silver, copper and tanzanite.

During 2011, USD 178.6 million was paid as royalties and statutory taxes to the government, while in the same year, community development initiatives amounted to USD 1.51 million compared to USD 1.96 the previous year.

Employment in the formal mines increased from 1781 in 1997 to about 15,000 in 2011 and expected to increase as potential new mines are constructed.

In 2011 TCME members spent a total of USD 441.5 million for local procurement of goods and services compared to USD 440.9 million in 2010, while salaries paid from mining operations to Tanzanian employees amounted to USD 87.3 million compared to USD 91.6 million in 2010.

The statistics provide to a large extent the tangible fiscal and social benefits that accrue to the Tanzanian economy which enables government to deliver on important development projects.

MAKALA: JAYDEE, MNAFIKI WA MIAKA 10, SHUJAA WA SIKU 30

$
0
0


MGOGORO wa kimuziki kati ya msanii Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ na kituo kimoja cha redio umezidi kuchukua kasi huku makundi mawili, kila moja likitengeneza ngome yake na kuamini linachoamini.

Kundi ambalo linamuunga mkono Jaydee na kumuona ni mkombozi, anazungumza kwa niaba yake na wasanii wengine, la pili ni lile linalobaki upande unaoshambuliwa, linatetea ngome yake.

Jaydee anashutumu kubaniwa nyimbo zake na kituo hicho ambacho kupitia mitandao kadhaa ya kijamii ameeleza wazi kuwa wanambania, wanaziponda lakini hata watangazaji wake wamekuwa wakionyesha chuki binafsi dhidi yake.

Jaydee pia aliwaponda wasanii Ben Pol na Linah anayetokea THT kwamba walishindwa kutokea kwenye uzinduzi wa video ya wimbo wake wa Joto Hasira, kwa madai walizuiwa na bosi wao.

Ujasiri huu wa Jaydee ndiyo kitu bora ambacho kimekuwa kikitakiwa kufanyika kutoka kwa wasanii, yaani wapigane kutetea muziki wa Tanzania hasa kama kuna watu au kundi la watu limejikita katika kuuangamiza.

Lakini ni tofauti kidogo, kwani wasanii wengi wamekuwa imara na kuwa tayari kujitetea wenyewe tu na si vingine. Nasisitiza mara nyingi, wao ndiyo wahusika wa kwanza na wanapaswa kuanzisha mapinduzi kuanzia kwao, mfano kusema naonewa si kitu kibaya lakini je, umewahi kupigania wanaoonewa?

Kujitetea pekee unaweza kufanya, lakini vipi utafanikiwa kama asilimia kubwa ya kundi la wanamuziki linaendelea kuonewa. Ukibaki hauonewi pekee na asilimia kubwa ya wasanii au wanamuziki inaonewa, kunaweza kuwa na mapinduzi sahihi?

Ndiyo maana nashangazwa kusikia Jaydee leo anaona ubovu wa kituo hicho, anathubutu kusema hadharani akionyesha wazi ameumia. Lakini miaka 10 au zaidi iliyopita, Jaydee alikuwa kimya na hakuwaza kusema kwamba kituo hicho kinawabania wasanii wengine na ‘kumtukuza’ yeye hata kama muziki wake haukuwa wa kiwango kilichokuwa kinazungumzwa.

Siwezi kusema muziki wa Jaydee ni mbaya, nimekuwa kati ya mashabiki wake. Lakini yoyote atanichekesha akisema nyimbo albamu zake zote alizotoa zilikuwa katika kiwango cha juu sana na ndiyo maana leo ni maarufu.

Hakuna asiyejua kwamba miaka nenda rudi, wasanii wamekuwa wanaongoza kwa unafiki, kutopendana wenyewe, kugeukana na hata kujenga makundi lukuki, ndiyo maana kila kukicha wamekuwa wakishambuliwa maana katika maisha yao hawana umoja.

Jaydee alianza kuwa mtangazaji katika kituo hicho baada ya kuacha kurap, akaamua kuachana na kurap na mwisho kuwa msanii wa nyimbo za kubembeleza, mara ya kwanza akianza kutikisa na albamu ya Machozi, Solo Thang anaweza kuhadithia vizuri kuhusu hili.

Kuanzia albamu ya Machozi, kituo hicho ndicho kilisimama kuhakikisha anakuwa bora hata kama muziki wake haukuwa ukimzidi kila mwanadada wakati huo.

 Angalia, kulikuwa wasanii kama Stara Thomas, Carola Kinasha ambao kiuwezo walikuwa juu kuliko Jaydee, lakini hawakupewa nafasi ya kutosha, badala yake Jaydee ambaye hakuthubutu kuwatetea hata kidogo akaendelea ‘kubebwa’ na watu wakaamini ni bora kuliko yoyote kwa upande wa akina dada au kina mama katika kuimba, haikuwa hivyo.

Angalia albamu ya Binti, karibu nyimbo zote zilikuwa na ujumbe mmoja, ulikuwa ukimshambulia mwaname mmoja ambaye alikuwa amemuumiza Jaydee. Takribani ujumbe wa nyimbo karibu zote ulikuwa ni mmoja, lakini ilibebwa na kuonekana ni moja ya albamu bora kabisa kuwahi kuwepo katika muziki wa Tanzania, kitu ambacho hakikuwa sahihi.

Wakati huo wasanii lukuki walilia kubaniwa, mmoja wao alikuwa ni Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye ndiye alimtambulisha mwanadada huyo alipomshirikisha katika wimbo wa Mambo ya Fedha, kabla ya hapo hakuwa na jina. Jaydee hakuwahi kuungana naye hata kidogo hata kwa mstari mmoja wa kumtetea au kuunga mkono kutetea muziki wa Tanzania, kuonyesha anapinga mwenendo wa wanaolazimisha kuwabagua wasanii au kufanya mambo kwa mabavu kwa kuwa wameshika mpini.

Hakuna aliyesikia kilio cha Sugu, wasanii wanaochipukia bila ya kujua wasemacho, kisa nyimbo zao zinapigwa redioni, ili kuonyesha shukrani za dhati wakaanza kutangaza Sugu anatapatapa na amekwisha kimuziki!

Ajabu, asilimia kubwa ya maneno yake ndiyo yanayozungumzwa leo, ndiyo yanatumiwa na kila msanii anayebanwa au kuhisi kaonewa. Angalia, hata Jaydee naye ameingia huko! Swali langu hapa je, Jaydee na wengine wanaolalamika, wamekwisha kisanii?

Ndiyo maana nasema, tasnia ya muziki hasa muziki wa kizazi kipya umejaza watu wavivu kufikiri, wenye mioyo ya ‘Kichina’, wasio na uwezo wa kuthubutu hata kidogo ambao wanasubiri wayumbe au kuumizwa wao ili wamtafute wa kumuangushia lawama.

Jiulize, kama Jaydee alibebwa kwa miaka 10, halafu leo analalamika atakuwa sahihi? Sitaki kumpinga kwa kuwa kuna kitu anakiona lakini ninaamini alikiona tokea mapema, akauchuna.

Bado nasisitiza, yeye na wengine wote wanaolia baada ya kuguswa wao nawaita wanafiki, wanapigana kwa ajili yao na si kwa muziki wanaoutumikia. Iwapo wangekuwa tayari kupambana kwa ajili ya muziki huo, msanii kama Jaydee asingeanza vita leo.

NARUDI KWA JAYDEE
Sijawahi kuingia naye katika malumbano zaidi ya miaka 10 tokea alipokuwa mwanahabari mwenzangu na sasa msanii. Lakini nathubutu kumueleza kuwa ni kati ya wasanii wasiojali muziki wa Tanzania na wanajiangalia wao zaidi.

Picha ya unafiki na kujiangalia mwenyewe inaonekana sasa ingawa takribani miaka mitano iliyopita nilianza kuinusa. Leo analia, anabaniwa na anauona moto unaounguza muziki wa Tanzania ulivyo mkali.

Naamini aliuona miaka kibao nyuma, lakini kwa kuwa alikuwa akitetewa hakuweza kuangalia kwamba rafiki zake, wasanii waliombeba kabla walikuwa wakiungua. Akaendelea kuwapita kwa raha zake mustarehe.

Tungeweza kumuita Jaydee ni mpambanaji kama angewakosoa hao anawakosoa sasa katika kipindi walichokuwa wamempa mbeleko yeye, basi kweli ingeonekana anapigania muziki wa Tanzania. Sasa anapigania chake tu!

Jaydee amefika mbali kimuziki, alikuwa bora jukwaani na nyimbo kadhaa na nyingi zikapewa ‘over promotion’ lakini bado ninaweza kumuita mkongwe. Ajabu alibaki chipukizi hadi leo katika suala la kutetea haki za wasanii na muziki wenyewe.

Sitaki kumkatisha tamaa kwa mapambano aliyoyaanza, ninaamini ana nafasi ya kuanza kuusaidia muziki ambao umemsaidia. Lakini ndiyo kipindi ambacho anaweza kupata machungu waliyopata wasanii wenzake kunyeshewa mvua na kuunguzwa na jua wakati akiwa kivulini kwa ‘msaada’.

Anachokifanya leo Jaydee ni nyongeza tu ya walichokifanya Sugu au Afande Sele au wasanii wachache walioamua kuwa wakweli au wale walioamua kuwa wabunifu kama Ambwene Yessaya ‘AY’, aliyekimbia vita ya redio na kuingia katika kurekodi video bora zilizoendelea kumng’arisha.

Simzuii, Jaydee kuendelea kupambana, lakini namuasa anachokifanya kama ni kwa ajili ya muziki akipozwa tena, asirudi nyuma.

Ninachomkumbusha, hata yeye amekuwa kundi moja na analowalaumu ambao angeweza kuwashauri mapema ‘ndani ya mjengo’ kama angekuwa na nia nzuri na muziki wa kizazi kipya.  Msisitizo ‘Joto Hasira’ liwe la kweli.

Airtel yatosha yatua kwa kishindo mkoani Tanga

$
0
0

 Masanii  maarufu kwa vichekesho Masele  wa kundi la vituko shoo toka
Dar es salaam akitoa burudani kwa wakazi wa Tanga  wakati wa Tamasha
maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel yatosha katika viwanja vya
Tangamano mkoani Tanga. 

 Wasanii wa kundi la Toto afrika wakionyesha umahiri wao wa kucheza na
moto jukwaani wakati wa tamasha maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya
Airtel yatosha katika viwanja vya tangamano mkoani tanga mwishoni mwa
wiki hii

 Umati wa wakazi wa Tanga wamejitokeza kushuhudia burudani na kuzindua
rasmi huduma ya Airtel yatosha mkoani Tanga katika viwanja vya
Tangamano mkoani humo


======  ======= ====== ======
Airtel yatosha yatua kwa kishindo mkoani Tanga
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea na utaratibu wake wa
kufanya matamasha ya wazi yenye lengo la kutoa burudani pamoja na
kuitambulisha huduma yake mpya ya AIRTEL YATOSHA kwa jamii ambapo
mwishoni mwa hii Airtel ilifanya tamasha katika viwanja vya Tangamano
mjini hapo.


Akizungumza wakati wa Tamasha hilo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson
Mmbando alisema "Airtel tumefurahishwa sana na umati wa wananchi
wanaojitokeza kwa ajili ya burudani lakini pia inatusaidia kuwajulisha
wote habari njema za unafuu wa gharama za mawasiliano kupitia huduma
yetu ya Airtel YATOSHA.


Tunawakumbusha kuwa YATOSHA ni huduma ya kudumu na inasaidia sana
kupunguza gharama za mawasiliano kwa wateja wetu. Kujiunga na huduma
hii ili ujipatie vifurushi vya SIKU au WIKI piga *149*99#
"Binafsi nimeshangaa na kufurahi sana sana kwa uwepo wa kifurushi cha
YATOSHA cha hadi shilingi 349" na najipatia dakika 25 kuongea bure du
kweli hii Imetosha!" alisikika akisema Hassan Juma mkazi wa chumba
geni mkoani Tanga.


mara baada ya uzinduzi huo wasanii mbalimbali wa kizazi kipya akiwemo
ney wa mitego, madii, fid q, na juma natura akiwa na kundi lake
walipanda jukwaani kutoa burudani mfululizo huku wananchi
waliojitokeza wakifuatia burudani hiyo mwanzo mwisho
kati ya vibao vilivyopigwa na wasanii hao na kuwavutia wakazi wa Tanga
ni pamoja na kile cha 'nani kwamwaga pombe yangu kilichoimbwa na madee
toka kundi la tip top connection, wakati wahudhuriaji wa tamasha hilo
wengi wao walionekana kuvutiwa zaidi na msanii wa hip hop Ney wa
mitego hasa kwa umahiri wake wa kupanga mistari na free style zake
alipoachia free style.




Airtel inaendelea  kufanya uzinduzi wa huduma ya airtel yatosha
kupitia matamasha ya burudani kwa ambapo baada ya tamasha  la Dar es
salaam, Morogoro, Chalinze na Tanga kupita  airtel yatosha jumamosi na
jumapili hii inahamia jijini Mwanza katika viwanja vya Furaisha ambapo
wasanii wa bongo flava watatoa burudani bure.

MCHEZO WA MASUMBWI ULIPO HAMASISHWA CHALINZE MKOA WA PWANI

$
0
0

Bondia Amos Thomas  kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Edrew Joseph wakati wa mpambano wa kuamasisha mchezo wa masumbwi Chalinze Mkoa wa pwani  Juzi mchezo huo ulitoka droo picha na www.superdboximgcoach.blogspot.com
Baazi ya mashabiki wakiwa na Diwani wao
Bondia Said Minyusi wa Chalinze kushoto akirusha konde ambalo alina madhala kwa Zumbe Kukwe wa Dar wakati wa mpambano wa kuamasisha masumbwi Chalinze mkoa wa Pwani juzi  Kukwe alishinda kwa TKO ya raundi ya kwanza picha na www.superdboximgcoach.blogspot.com
Baazi ya mashabiki waliojitokeza kuhamasisha mchezo wa masumbwi wakiangalia burudani hiyo
Mabondia walio itimisha mpambano huo wakati wa kuhamasisha masumbwi Chalinze
Diwani wa Kata ya Bwilingi Chalinze Ahmed Kalama Nassar akizungumza kabla ya mpambano wa mwisho kwa ajili ya kuhamasisha ngumi katika kata hiyo
Mwaite Juma wa Chalinze kushoto akimwangalia bondia Mussa Ali baada ya kupiga konde zito na kwenda chini.

======  ========
ZAIDI ya mashabiki 300 wamejitokeza kuangalia mpambano wa Masumbwi kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa ngumi Chalinze  Mkoa wa Pwani pamoja na vitongoji vyake mashindano hayo ya masumbwi yaliyoandaliwa maalumu kuhamasisha mchezo uho katika vitongoji maarufu.

Uliwakutanisha mabondia wa Dar es salaam na Chalinze na mabondia wanaotamba katika kitongoji hicho mpambano huo wa masumbwi ulioanza saa tatu ya usiku na kumalizika saa nne na nusu uliwakutanisha bondia Amos Thomas aliye toka sare na Edrew Joseph uku mpambano mwingine ukiwakutanisha Zumbe Kukwe wa Dar es salaam aliye mgalagaza bila huruma Said Minyusi wa chalinze

Mpambano mwingine ni Alex Kado wa chalinze alishindwa kuhimili mikiki mikiki ya Nassoro Khatibu na kupigwa kwa ponti

Pambano lililokuwa likisubiliwa na watu wengi zaidi ni mpambano uliowakutanisha Mwaite Juma wa Chalinze na Mussa Ali ambapo mwaite aliweza kumsambalatisha ali kwa TKO ya raundi ya kwanza na kupeleka shwangwe kwa wapenzi waliojitokeza katika mpambano huo

Baada ya kumalizika kwa mpambano huo Diwani wa Kata ya Bwilingi Chalinze Ahmed Kalama Nassar ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mpambano huo alisema yupo tayali kuwanunulia vifaa vya mchezo huo ili kuendeleza masumbwi katika kata hiyo

Ambapo ame haidi kuongeza ushirikiano wa wataalamu wa masumbwi kwa kushilikiana na viongozi ili chalinzi kiwe kitovu cha masumbwi nchini

Sensei Rumadha Fundi aka Romi (3rd Dan black belt) mtaalamu wa kujivunia

$
0
0
 Tunapozungumzia watanzania waliozaliwa na vipaji na kufanikiwa kuvipigania na kuviendeleza vipaji hivyo hadi kufikia kiwango cha kimataifa jina la Sensei Rumadha Fundi aka Romi  (pichani) hatuwezi kulikwepa. Yeye  ni Mtanzania mwenye makazi yake huko Texas, nchini Marekani. 
Kabla ya kujikita huko Romi  alikuwa moja ya wanafunzi wa karate pale Zanaki jijini Dar es salaam chini ya mwalimu wake Sensei Natambo Guru Kamara Bomani (RIP), akiwa mmoja wa vijana wadogo wateule wa mwalimu huyo aliyebuni kundi maalumu la vijana hodari wa mchezo huo, kwa jina Bomani Brigade.

Baada ya hapo Sensei Rumadha akaenda kwa mafunzo zaidi huko Okinawa nchini Japan, Sweden na Denmark. Pia akachaguliwa kwenda nchini India kwa mafunzo ya kuwa mtaalamu wa Yoga.

Kwa vipaji hivi vya Karate na Yoga, Sensei Rumadha Fundi anaiwakilisha Tanzania kuwa nchi ya wenye vipaji, akiwa  ni mwalimu wa karate na yoga mwenye utalaamu na upeo wa hali ya juu sana na mwenye nidhamu.


Sensei Rumadha ni  mmoja wa walimu wa Kitanzania wa karate ambao wanafanya vizuri katika fani hii  ughaibuni. Ni matumaini yetu wahusika katika sekta ya michezo hasa upande wa mapambano kama ngumi, kick boxing, judo na kadhalika  wataangalia uwezekano wa kupata mchango wao ambao unaweza kusaidia katika kuboresha wanamichezo wetu kufikia kiwango cha kimataifa na kuliletea sifa taifa letu.
Sensei Rumadha Fundi 'Romi' (3rd Dan black belt),  akiwajibika katika semina ya karate katika Dojo ya Sugarland, Texas, nchini Marekani katika semina ya walimu wa karate (ma-sensei)  chini ya uongozi wake Sensei Ramon Veras (7th Dan), wa Traditional Okinawan Goju Ryu Karate-Do.

diamond azua balaa morogoro...ati ooh..oohh Diamond ni freemasons..!

nitaendelea kukiimarisha na kikienzi chama cha ccm na kuulinda muungano-dkt shein

$
0
0


Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Dkt Ali Muhammed Shein amesema kuwa ataendelea kukiimarisha na kukienzi Chama Cha Mapinduzi pamoja na kuulinda Muungano wa Serikali mbili uliopo.

Kauli hiyo ameitoa leo huko katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani wakati akizindua ziara yake ya Mikoa mitano ya Zanzibar.

Dkt Shein ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amesema kuwa kuna kila sababu ya kukiimarisha chama hicho kutokana na umuhimu wake na kwamba Muungano uliopo wa Serikali mbili ndio njia bora ya kuendeleza mashirikiano ya kidugu yaliyodumu kwa muda mrefu.

Amesema kuwa lengo kuu la ziara hiyo ni kupata taarifa za matukio mbali mbali pamoja na changamoto zilizopo katika mikoa hiyo zinazohusu CCM.

Aidha amewataka viongozi wa CCM kuwa  na mashirikano mazuri katika kukiimarisha Chama na kuhakikisha kwamba kinapata ushindi katika kila uchaguzi unaokuja.

Dkt. shein amesema kuwa ana imani na Chama chake kuibuka mshindi katika chaguzi kutokana Chama hicho kuchagua uongozi makini ambao utahimili vishindo vya uchaguzi ujao.

Katika hatua nyingine Dkt Shein aliwataka Wananchi kuendelea kujishughulisha na harakati zao za kujiletea maendeleo na kuepuka kuvunja sheria za nchi.

“Serikali inataka amani na utulivu kwa Wananchi wake sambamba na kuimarisha maendeleo kama Malengo ya Mapinduzi yalivyoelekeza na kwa njia hiyo hatuna budi kuyaenzi Mapinduzi” alieleza Makamo Mwenyekiti wa CCM.


Katika ziara hiyo Makamo Mwenyekiti amezindua Tawi jipya la CCM la Vikokotoni, Kikwajuni SACCOS BANK pamoja na kutoa kadi 270 kwa wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi.


IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

Makubi Film Production and Sports Promotions yaja na mashindano ya soka la mtaani

$
0
0

Ni kampuni inayojihusisha na utafutaji, ukuzaji na kuendeleza vipaji mbalimbali vya vijana katika Nyanja za sanaa na michezo hapa nchini, kampuni tayari imefanya kazi mbalimbali za sanaa zikiwemo sinema, tamthilia zilizorushwa katika luninga mbalimbali Tanzania.

Kwa kipindi cha mwaka 2013 Makubi Film Production and Sports Promotions imekusudia kukuza vipaji vya Wachezaji wa soka walio mitaani kwa kushirikiana na kampuni au taasisi zenye lengo la ukuzaji wa soka la Vijana wa Tanzania.


Lengo la Mashindano hayo ni kuwawezesha Vijana  wanaocheza timu za mitaani kuonesha uwezo wao katika kusakata soka lakini pia mashindano haya yatatumika kuwatafutia wachezaji hawa timu kubwa zinazocheza ligi mbalimbali za kitaifa.


Mashindano  yatashirikisha jumla ya timu ishirini kutoka kata za Makurumla, Mburahati, Manzese, Mabibo na Ubungo zote za Mjini Dar es Salaam timu hizo ni zifuatazo:


Mti Pesa F.C, Dago F.C, Mburahati United, Pampona F.C, Israel Academia, Mingo,Wazulu, Mabibo Sokoni, Makutano F.C, Midizini Market, Arizona, T.C Mzozo, East Daz, Yakusela, Ranger F.C ,Umoja F.C ,Darton F.C ,Uamsho F.C , Kota Football Club na Timu ya Wanafunzi wa Chuo cha Filamu  (TFTC).


Mashindano haya yatafunguliwa rasmi tarehe 18 Mei 2013 na Mgeni Rasmi katika Uzinduzi huo ni  Mheshimiwa Nape Nnauye Katibu Siasa na Uenezi CCM Taifa  (CCM )  fainali ya mashindano haya itakuwa 11  Agost 2013.


Zawadi za Washindi, Washindi  3 wa Mashindano watapata zawadi kama ifuatavyo mshindi wa kwanza atapa jezi seti 5 na fedha taslimu shilingi laki 3, mshindi wa 2 atapata jezi seti 3 na fedha taslimu shilingi laki 3 na Mshindi wa 3 atapata jezi set 2 na fedha taslimu shilingi laki moja, zawadi hizi zitatolewa na wadhamini wa mashindano haya ambapo mazungumzo yako katika hatua za mwisho ili kukamilisha.

 

Burudani siku ya Ufunguzi, Burudani mbalimbali katika ufunguzi wa Mashindano hayo zikiwemo mechi ya hisani kati ya timu za Wanawake ya Mburahati Queens na  Sayari, Burudani ya Muziki wa kizazi Kipya toka kundi  la Tip Top Connection na Bendi ya African Stars Twangapepeta pamoja na wasanii mbalimbali wa tasnia ya filamu Tanzania, Bongo Movie , sherehe za uzinduzi zitaanza  saa  8 mchana mpka saa 11 jioni.


Ndugu Waandishi ni matarajio yetu kwamba mashindano yatakuwa yenye ustaarabu na amani kwa sababu yana baraka toka chama cha mpira Manispaa Kinondoni-KIFA na Jeshi la Polisi Mkoa Kinondoni kimeahakikisha ulinzi wa kutosha katika mashindano hayo aidha  kalamu zenu zitasaidia kuhamasisha Wadau kusaidia soka la mtaani ambalo ndio chimbuko kuu la Wachezaji wanaowika hivi sasa, nanyi ni mashahidi na mifano mnayo.

Nawashukuru pia tunawapongeza kwa jitihada za uenezi wa habari kwa jamii lakini tunaomba  ushirikiano katika kuripoti mashindano haya.

  

Nawatakia kazi njema


Soka ni ajira tuisimamie na tuiendeleze


WILSON  .R.  MAKUBI

MKURUGENZI

MAKUBI SPORTS  PROMOTION



MAWASILIANO: 

simu  0715 316 796,  0715 718 720.  email; Wilson.makubi@gmail.com,

Facebook : makubi sports promotion

VIKUNDI 15 VYAJITOKEZA KUFANYA MAONESHO StarLight BULE Aprili 27

$
0
0

MTANDAO WA WASANII TANZANIA (SHIWATA)

Peter Mwenda

WASANII chipukizi 300 kutoka vikundi 15 jijini Dar es Salaam wamejitokeza kushiriki maonesho ya kukuza vipaji yaliyoandaliwa na Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Jumamosi ya Aprili 27 katika ukumbi wa hoteli ya StarLight ,Mnazi Mmoja Dar es Salaam.

Vikundi ambavyo vimethibitisha kushiriki pamoja na Kaole Sanaa Group,Splendid,Uyoga Boga na vingine katika fani ya Bongo  Flava,Taarab,Maigizo,Ngoma,Mazingaombwe,Sanaa za Ufundi,Kung Fu,Sarakasi,Kusheki,Kwaya,na Ngonjera.


Maonesho kama haya yatafanyika kila mwezi na kiingilio ni bure na vikundi vingine ni Super Shine Morden Taarab,Zijiu,Edeneza Brass Band,Asili Africa,Mege Arts,Kintu,Army Kwanza,Wachapakazi,Tanhope,Tanz Arts,Mshikamano,Big House,Lutenga Boys,Kilimasta,Manuary.

Madhumuni makubwa ya tamasha hilo ni kuibua vipaji vya wasanii chipukizi ili kazi zao ziweze kupata soko hivyo mapromota, Majd,Maproducer wa filamu wasikoke kufika katika maonesho hayo ili kuona mastaa chipukizi ambao ambavyo vipaji vyao bado havijaonekana.

Vijana wa sanaa mbalimbali wanatakiwa kufika katika ofisi za SHIWATA zilizopo Bungoni Ilala ili kujisajili kwa ajili ya maonesho mengine yanayofuata .

Tanzania kuna wasanii wengi wenye vipaji lakini kazi zao hazisikiki wala kuonekana kwenye vyombo vya habari hivyo hiyo ni fursa kutumia maonesho hayo kama soko la kazi zao katika jiji la Dar es Salaam.

Wasanii mbalimbali ambao vipaji vyao vitakubalika sokoni watanufaika kupata ajira ya kuuza kazi zao pamoja na kushiriki katika matamasha mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Peter Mwenda
Ofisa Habari wa SHIWATA
0715/0752 222677

BALOZI SEIF NA WIKI YA USALAMA BARABARANI

$
0
0

   Imeelezwa kuwa ikiwa kutakuwa na  ushirikiano na uadilifu baina ya watoaji  leseni za Udereva na  Jeshi la Polisi nchini itapelekea kupunguza  ajali za Baraabarani zisizokuwa za lazima.
Hayo   yameelezwa na  Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  wakati alipokuwa akizungumza na Wananchi, Wanafunzi  pamopja na Madereva wa vyombo vya moto kwenye  uzinduzi wa wiki ya usalama barabani katika ukumbi wa Salama, Hoteli ya  Bwawani Mjini Zanzibar .
Balozi  Seif  amesisitiza Umakini katika  utoaji wa leseni na kuwataka Madereva  kufuata Sheria wakati  wanapoendesha vyombo ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika kwa wananchi wanaotembea kwa  miguu na wale wanaoendesha vyombo vidogo vidogo.
“Katika kuyafikia malengo ya mpango wa miaka kumi ya usalama barabarani natoa wito kwa madereva kutoendesha mwendo wa kasi wanapokuwa barabarani, kutii sheria, kuwajali watumiaji wengine wa barabara ikiwa ni pamoja na waenda kwa miguu, wapanda baskeli na watu wenye mahitaji maalum” Alisema Makamu wa pili wa Rais.
Ameahidi kuwa Serikali kwa upande wake  itahakikisha kuwa inasimamia kwa ukamilifu  sheria za barabarani na kuwachukulia hatua wale wote wanao kaidi kufuata sheria hizo.
Ameongeza kuwa Serikali itahakikisha kuwa barabara zinazojengwa zinakidhi viwango ikwa ni pamoja na uimara wa barabara zenyewe , upana pamoja na kuwekwa alama zote muhimu zinazohusu usalama wa  barabarani.
Miza Othman – Maelezo Zanzibar  


Nae Kamishna  wa Jeshi la Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa amesema  ni vyema kamati  ya  mawasiliano kulishirikisha  Jeshi la Polisi  wakati wanapotoa maamuzi  katika masuala ya ujenzi wa barabara ili na wao waweze kutoa mchango wao kabla ya ujenzi kuanza.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya  Dokta Ahmed Jidawi  ameshauri madereva kufanyiwa uchunguzi  wa kiafya  kabla ya kupatiwa leseni  kama vile kuchunguzwa akili na hata macho jambo ambalo litapelekea  kupata madereva  walio bora .
Mkurugenzi wa Miundo mbinu na Mawasiliano amekemea tabia mbaya inayofanywa na baadhi ya watu  kuondoa alama za barabarani na kusema kwamba serikali itawachukulia hatua watakaobainika kufanya vitendo hivyo.
 Aidha amewanasihi madereva kuwa makini na kupunguza matumizi ya simu  wakati wanapoendesha gari kwani ni miongoni mwa vichocheo vya kutokea ajili za barabarani.
 Kauli mbiu ya wiki ya usalama barabarani mwaka huu  ni ‘’KUONDOA AJALI ZA BARABARANI NI  JUKUMU LETU SOTE’’.  
IMETOLWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

taswa fc, taswa queens kucheza Kibiti Jumatano.

$
0
0

TIMU ya soka ya waandishi wa habari za Michezo nchini (Taswa FC) na timu ya netboli (Taswa Queens) itaondoka jijini Jumatano alfajiri  kwenda Kibiti, mkoa wa Pwni kwa ajili ya mechi maalum ya kirafiki.

Mechi hiyo imepangwa kufanyika kwenye uwanja wa Samora imeandaliwa kwa ajili ya kuanzisha uhusiano wa karibu baina ya waandishi wa habari za michezo na walimu wa wilaya hiyo katika kuendeleza sekta hiyo hapa nchini.

Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary alisema kuwa mechi ya kwanza siku hiyo itakuwa kati ya Taswa Queens na kombaini ya walimu iliyopangwa kuanza saa 9.00 ambapo mechi ya pili itakuwa kati ya Taswa FC na kombaini ya walimu iliyopangwa kuanza saa 10.00 jioni.

Majuto alisema kuwa mbali ya kuanzisha uhusiano na kupromoti michezo katika wilaya hiyo, mechi hizo pia zitakuwa sehemu ya maandalizi ya Taswa FC na Taswa Queens kwa ajili ya ziara ya kimichezo mkoani Arusha na Tanga mwezi ujao.

“Maandalizi ya safari yamekamilika na tunawaomba wachezaji wazingatie muda wa kufika ili tuweze kuondoka kwa mujibu wa ratiba yetu, lengo ni kuwahi kufika na kumaliza mapema na kuendelea na ratiba nyingine kwa mujibu wa wenyeji wetu,” alisema Majuto.

Alisema kuwa timu zao zote zimejiandaa kwa ushindi katika mechi hizo ambazo zinatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na maandalizi. Taswa FC haijapoteza hata mechi moja tokea kuanza kwa mwaka huu. Timu zote mbili zilitoa vipigo kwa timu ya Kiliflora ya Arusha kwa mabao 4-1 kwa upande wa soka na mabao 28-8 kwa upande wa netiboli.

Mratibu wa mechi hiyo, mwalimu Paul Nyoni amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika na wanawasubiri kwa hamu waandishi wa habari. Nyoni alisema kuwa wamewaandaa mapokezi mazuri kwa waandishi na wanaamini mechi hizo mbili

rais wa zanzibar dkt shein asisitiza kuimarishwa kwa amani,umoja na mshikamano

$
0
0
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
   
 Zanzibar                   

                                                                           22.4.20113
  
MAKAMO Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza kuimarishwa kwa amani, umoja na mshikamano na kueleza kuwa vurugu sio utamaduni wa wananchi wa Zanzibar.

Dk. Shein aliyasema hayo leo kwa nyakati tofauti katika ziara yake ya  Chama katika Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Chama Mjini. Makamo Mwenyekiti huyo alieleza kuwa amani na utulivu ndio msingi wa mafanikio na ndio maana chama hicho cha CCM kimekuwa kikisimamia na kudumisha jambo hilo kwa kutambua umuhimu wake.

Alisisitiza kuwa tayari Zanzibar imeshajijengea sifa kubwa Kimataifa kutokana na mafanikio makubwa yaliopatikana katika kuimarisha na kuiendeleza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yenye mfumo wa Umoja wa Kitaifa, hivyo kujitokeza kwa watu wachache kutaka kuvuruga amani serikali haitowafumbia macho.

Alieleza kuwa wananchi wote wa Zanzibar wana haki sawa na ndio maana Serikali anayoiongoza chini ya chama cha Mapinduzi haimbagui mtu kwa jinsia, rangi, dini ama ukabila. Alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyo na mfumo wa  Serikali ya Umoja wa Kitaifa haitomvumilia mtu yeyote atakaevuruga amani na utulivu uliopo nchini.

Katika hotuba zake, Dk. Shein aliwasisitiza wanaCCM kuendeleza utamaduni wao wa kuimarisha amani na utulivu na kuzidisha mashirikiano kwani ndio ngao ya ushindi wa chama hicho. Aidha, Dk. Shein alisisitiza kuwa Serikali anayoiongoza itaendelea kuyalinda na kuyadumisha Mapinduzi ya Januari 12, 1964 sanjari na kuulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Mapema Dk. Shein alipokea taarifa ya kazi za Chama ya Mkoa wa Mjini na baada ya hapo alifika Kisiwandui na kwa ajili ya kuzindua rasmi Benki ya SACCOS ya Umoja wa Wajasiriamali wadogowadogo na kueleza kuwa hatua hiyo ni miongoni mwa utekelezaji wa  Ilani ya CCM. Baada ya hapo Makamu huyo wa CCM Zanzibar alikwenda Vikokotoni kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi jengo jipya la ghorofa mbili la Tawi la CCM Vikokotoni lililojengwa kwa ubia kati ya Tawi na mfanyabiashara.

Dk. Shein alimalizia ziara yake kwa Wilaya ya Mjini, Dk. Shein alitembelea maskani ya Kisonge iliyopo Michenzani na kuangalia uharibifu uliotokea baada ya kuchomwa moto kwa maskani hiyo wakati wa vurugu zilizotokezea hivi karibuni na kusababisha hasara kubwa ya zaidi ya milioni 50.

Sambamba na hayo, Dk. Shein aliwakabidhi kadi wanachama wapya  270 kutoka Jumuiya zote za CCM zikiwemo wazazi, Umoja wa Wanawake na UVCCM na baadae alisalimiana na wana CCM na kuwataka wanaCCM kuwafundisha siasa vyama vyengine ambavyo vimeonesha kutoelewa maana na umuhimu wa amani na utulivu.

Katika ziara hiyo burudani mbali mbali zilitumbuiza zikiwemo ngoma, nyimbo, mashairi, tenzi pamoja na burudani maalum iliyotolewa na   vijana wa CCM kutoka Ilala, Dar-es-Salaam waliyoitoa katika viwanja vya Kisonge mjini Zanzibar. Ziara hiyo itaendelea kesho katika Wilaya ya Amani.

 Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar.
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

wakazi wa morogoro walivyopagawishwa na diamond licha ya mvua kubwa kunyesha.

$
0
0

HUYU NDIO DIAMOND THE PLATNUMZZ....!

President Kikwete opens AU Ministerial Meeting for Peace and Security in Dar es Salaam

$
0
0
 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete delivers his speech during the opening ceremony for the Ministerial Meeting of the Peace and Security of the African Union held in Dar es Salaam this morning.
 A cross section of the delegates and dignitaries who attended the opening ceremony for the Ministerial Meeting of the Peace and Security of the African Union held in Dar es Salaam this morning.

  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete welcomes former Mozambican President and SADC mediator for Madagascar  , Joachim Chissano at Dar es Salaam Serena Hotel during the opening ceremony for the 368th Ministerial Meeting of the Peace and Security Council of the African Union.
 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete(Centre) in a group picture with some delegates who attended the opening ceremony of the Ministerial Meeting of the Peace and Security of the African Union held in Dar es Salaam this morning.(photo by Freddy Maro.).

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA WIKI YA CHANJO KITAIFA.

$
0
0
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, na  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia  mamia ya wananchi waliohudhuria kwenye sherehe za uzinduzi rasmi wa wiki ya chanjo nchini iliyofanyika kitaifa huko Mlandizi , Mkoani Pwani tarehe 22.4.2013.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpatia chanjo ya motto Haula Mlondwa ,miezi 6, kutoka katika kijiji cha Vigwaza, wilayani Kibaha, ikiwa ni uzinduzi rasmi wa wiki ya chanjo kitaifa iliyoadhimishwa huko Mlandizi tarehe 22.4.2013.


 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifurahi na mtoto Haula Mlondwa, mwenye umri wa miezi  6 ambaye aliletwa kwenye sherehe za uzinduzi wa wiki ya chanjo kitaifa huko Mlandizi, katika wilaya ya Kibaha, na baba yake mzazi Bwana Mlondwa Omar , mkazi wa Vigwaza.  Mama Salma alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo tarehe 22.4.2013.  Bwana Mlondwa Omar alikuwa ni miongozi mwa wanaume wawili tu walioweza kuwaleta watoto wadogo kwenye chanjo wakiambatana na wake zao.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na akinamama na akina baba waliowaleta watoto wao kwa ajili ya chanjo wakati wa uzinduzi rasmi wa wiki ya chanjo kitaifa iliyofanyika huko Mlandizi, wilayani Kibaha tarehe 22.4.2013.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikweteakipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa maabara wa kituo cha afya cha Mlandizi ,wilayani Kibaha katika mkoa wa Pwani, Bwana Sostenes  Nyang’olo, jinsi ya kuchukua vipimo vya damu na makohozi kutoka kwa wagonjwa wakati wa uzinduzi wa wiki ya chanjo kitaifa iliyofanyika huko Mlandizi tarehe 22.4.2013.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mheshimiwa Dr. Seif Rashid wakishiriki kuimba na kikundi cha kwaya cha Anglican Compassion kutoka Bagamoyo wakati wa uzinduzi rasmi wa chanjo kitaifa ulifanyika katika kijiji cha Mlandizi  tarehe 22.4.2013.
  Viongozi, wageni na wananchi  mbalimbali waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa wiki ya chanjo kitaifa kwa watoto wenye umri wa chini ya mwaka mmoja iliyofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Mtongani iliyoko Mlandizi katika wilaya ya Kibaha tarehe 22.4.2013. PICHA NA JOHN LUKUWI.

MAJADILIANO KATI YA UJUMBE WA TANZANIA NA BENKI YA DUNIA KUHUSU VIPAUMBELE VYA MAENDELEO YA NCHI YETU YA TANZANIA

$
0
0
 Kutoka kushoto ni Meneja wa Ubinafsishaji Sekta ya Maendeleo kanda ya Afrika Bi. Irina Astra Khan, Mkurugenzi wa Mipango na Uratibu kanda ya Afrika Bw. Jan Walliser akijibu hoja katika majadiliano hayo. Kulia ni Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier akisikiliza kwa makini.

 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu akijibu hoja kwa ujumbe wa Benki ya Dunia huku Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akimsikiliza kwa makini.
Kutoka kushoto ni Meneja wa Ubinafsishaji Sekta ya Maendeleo kanda ya Afrika Bi. Irina Astra Khan, Mkurugenzi wa Mipango na Uratibu kanda ya Afrika Bw. Jan Walliser akijibu hoja katika majadiliano hayo. Kulia ni Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier akisikiliza kwa makini.

 Wafanyakazi wa Benki ya Dunia wakifuatilia majadiliano.
 Ujumbe wa Tanzania pamoja na ujumbe wa Benki ya Dunia wakijadili namna ya kuendeleza na kuboresha sekta mbalimbali zilizopewa vipaumbele kwa Tanzania ambavyo ni pamoja na Nishati, Usafirishaji na masuala mazima ya MKUKUTA.

 Kutoka kushoto ni Mchumi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dkt. Dickson Lema, Mchumi wa BOT Bi. Haika Mbaga, Kaimu Balozi Ubalozi wa Tanzania Washington DC Bibi Lily Munanka, Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya Fedha Zanzibar Bi. Bihindi Nassor na Mchumi wa BOT Bi. Sauda Msemo wakifuatilia majadiliano hayo.
 Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akitoa ufafanuzi wa vipaumbele kwa ujumbe wa Benki ya Dunia.
 Kutoka kushoto ni Mchumi wa Wizara ya Fedha Bw. Patrick Pima, Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Prof.  Longinus Rutasitara, Afisa Mwambata anayeratibu masuala ya uchumi, biashara na uwezeshaji ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa Bw. Paul Mwafongo wakiandika majadiliano hayo.   
 Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mipango na Uratibu kanda ya Afrika Bw. Jan Walliser, Meneja wa Social Protection kanda ya Afrika Bi. Lynne D-Sherburne – Benz na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Dunia wakifuatilia majadiliano hayo.

Viewing all 46340 articles
Browse latest View live




Latest Images